You are on page 1of 34

Jarida la

NCHI YETU
TANZANIA

Toleo la 228

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

KA

55

MIA

RU

U
UH

Desemba, 2016

Miaka 55 ya Amani, Umoja na Kazi

www.tanzania.go.tz

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Bodi ya Uhariri
Mwenyekiti
Hassan Abbas
Wajumbe
Zamaradi Kawawa
Tiganya Vicent
John Lukuwi
Jonas Kamaleki
Casmir Ndambalilo
Patrick Kipangula
Elias Malima
Wasanifu Jarida
Benedict Liwenga
Hassan Silayo
Huduma tunazotoa
Tunauza picha za Viongozi wa Taifa na matukio
muhimu ya Serikali,
Tunasajili Magazeti na Majarida,
Ukumbi kwa ajili ya Mikutano na
Waandishi wa habari,
Rejea ya Magazeti na picha za zamani,
Tunapokea kero mbalimbali za Wananchi
Jarida hili hutolewa na:

Idara ya Habari (MAELEZO)


S.L.P 8031
Dar es Salaam
Simu: 022-2122771
Faksi: 2113814
Baruapepe: maelezo@habari.go.tz
Tovuti: www.habari.go.tz

Jarida la Nchi Yetu 2016

ii

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

TUONAVYO SISI
Hongera Rais Magufuli kwa kusaini Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016
Hivi karibuni RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
alisaini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 iliyopitishwa na Bunge la 11 la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa tano Mjini Dodoma.
Hatua hiyo ya Rais Magufuli ilitokana na kazi nzuri ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania baada ya kuujadili Muswada huo kifungu kwa kifungu na kuunga mkono.
Mara baada ya kusaini Muswada huo na kuwa Sheria, Rais Magufuli aliwapongeza wadau
mbalimbali waliofanikisha shughuli hiyo na kusema kuwa anamini kuwa Sheria hiyo itasaidia
kuboresha sekta ya habari kwa manufaa ya wanataaluma wenyewe na Taifa.
Mnamo Novemba 04, mwaka huu, wakati Rais Magufuli akizungumza na Wahariri wa vyombo
vya habari, aliahidi kuusaini Muswada huo mara moja utakapomfikia huku akiusifia kuwa ni Sheria
nzuri inayolenga kulinda maslahi ya Waandishi wa habari na kuweka heshima katika tasnia hiyo.
Awali akiongea na Waandishi wa habari mara baada ya kupitishwa kwa Muswada huo, Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye aliwashukuru wadau wote walioshiriki
katika kutoa maoni juu ya Muswada huo kwani ndiyo yamepelekea kukamilisha mchakato mzima
wa Muswada huo.
Kwa niaba ya Serikali napenda kuwashukuru wadau wote walioshiriki kwa namna moja au
nyingine katika kuhakikisha tunatimiza malengo ya takribani miaka 20 iliyopita ya kuifanya
taaluma hii ya habari kuheshimika kama zilivyo taaluma zingine, alisema Waziri Nape.
Waziri Nape aliongeza kuwa, kwa sasa Muswada huo umeshapitishwa hivyo kilichobaki ni
utungaji wa Kanuni ambapo aliomba wadau wa tasnia ya habari kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya
kutoa maoni yatakayopelekea kuwa na Kanuni zenye tija kwa wanahabari na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Mhe. Nape aliwaasa wadau wa habari kuunganisha nguvu kwa pamoja hasa katika kipindi
hiki ambacho Muswada huo umepitishwa na kuwataka wadau hao kutoruhusu mgawanyiko
utokee kati yao, bali washirikiane na Serikali katika kutekeleza wajibu wao wa kihabari kwa jamii.
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju alisema kuwa, Muswada
wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ni mwanzo mpya wa tasnia ya habari nchini
ambapo aliwaasa wadau wa habari wakiwemo Waandishi wa habari kutambua kuwa haki mara
zote huendana na wajibu, hivyo hakuna haki isiyo na wajibu.
Baadhi ya mambo muhimu yaliyomo kwenye Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016
ambayo imefuta rasmi Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 ni pamoja na kuanzishwa kwa Bodi
ya Ithibati itakayoainisha viwango vya taaluma kwa wanahabari na kutoa vitambulisho vya
wanahabari, Baraza Huru la Habari ambalo pamoja na majukumu mengine litasaidia kutatua
migogoro na kuandaa Kanuni za Maadili kwa wanahabari.
Jambo jingine ni kuwepo kwa kipengele cha kuwakatia Bima Waandishi wa habari kufanya kazi
katika mazingira hatarishi na kuanzishwa kwa Mfuko wa Mafunzo kwa Waandishi wa habari
ambao utakuwa unatoa mafunzo ya muda mfupi ya kitaaluma.
Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 iliyosainiwa na Mhe. Rais Magufuli itasaidia kujenga
upya taaluma ya Uandishi wa habari iliyokuwa imevamiwa na baadhi ya watu mbalimbali kama
vile Makanjanja na hivyo kuhatarisha usalama wa jamii kwa kuandika matukio yasiyozingatia
maadili na yaliyojaa uchochezi.

Jarida la Nchi Yetu 2016

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

TAHARIRI

Miaka 55 ya Amani, Umoja na Kazi


Tanzania Bara ambayo awali ilijulikana kama Tanganyika imetimiza miaka 55 ya
ujenzi wa amani, utulivu na maendeleo. Tangu Awamu ya Kwanza, Pili, Tatu, Nne
na sasa ya Tano, kama kuna jambo limesisitizwa sana kwa Watanzania kwa ujumla
basi ni kazi.
Kwa upande wake tangu aingie madarakani Rais wa Awamu ya Tano, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli amekuwa akisisitiza umuhimu wa wananchi kufanya kazi kwa
bidii na maarifa huku wakimtanguliza Mwenyezi Mungu.
Msisitizo huo wa Rais Magufuli unalenga kuifanya Tanzania kuwa nchi ya wachapakazi
na sio ya watu wanaoshinda vijiweni wakipiga soga bila
kufanya kazi.
Katika kuwahamasisha wananchi, Rais Magufuli amekuwa akihimiza watu wafanye
kazi kupitia falsafa yake ya HAPA KAZI TU ambayo kimsingi inaamsha ari na kutoa
msukumo wa kipekee kwa wananchi kushiriki katika kujenga uchumi wa viwanda.
Sisi tunaunga mkono hatua hizi na tunatumia fursa hii kuwakumbusha Watanzania
kuwa nchi yetu imetoka mbali na bado ina safari ndefu hivyo tuendelee kuchapa kazi
ipasavyo.
Tunaiona kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru mwaka huu isemayo
Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi wa
Viwanda kwa Maendeleo Yetu. Kuwa namna inayosadifu umuhimu wa kuendeleza
mapambano ya kuijenga nchi yetu.
Kauli mbiu hii inaunga mkono nia ya dhati ya Mhe. Rais Dkt. Magufuli ya kuwaletea
wananchi maendeleo kwa kujenga mazingira rafiki yasiyo na rushwa wala ufisadi ili
kila mwananchi aweze kushiriki kujenga uchumi kwa kufanya kazi halali.
Ni katika dhamira safi ya Mhe. Rais tunaiona Tanzania mpya yenye uchumi imara
na misingi madhubuti inayowafanya wananchi wa kizazi hiki na kizazi kijacho kuonja
matunda ya falsafa hii ya HAPA KAZI TU.
Dhamira hii ya kuhamasisha wananchi washiriki katika uzalishaji mashambani na
viwandani inaonyesha kuwa nchi hii sasa inaendelea kuwa katika mwelekeo mzuri
wa kimapinduzi katika kujenga uchumi wake.
Jambo la muhimu ni kwa kila Mtanzania kujitoa na kumuunga mkono Mhe. Rais kwa
kutimiza wajibu wake ipasavyo kwa wakati muafaka ili hatimaye sote tuonje matunda
ya kazi nzuri ambayo Serikali ya Awamu ya Tano inafanya.
Viongozi wote katika ngazi mbalimbali wameonyesha kwa dhati nia na dhamira ya
dhati kuwahamasisha na kushirikiana na wananchi katika maeneo yao ili kujenga
Tanzania mpya kwa kutumia mvua za masika kulima mazao yanayostawi kwa muda
mfupi.
Tunapojenga uchumi wa viwanda wananchi wanalo jukumu la kuongeza nguvu katika
kufanya kazi na kutumia vyema rasilimali za Taifa letu ikiwemo misitu,ardhi,madini na
vivutio vilivyopo katika Taifa letu ili tuweze kuyafikia maendeleo ya kweli na endelevu.
Hongereni Watanzania kwa kuadhimisha miaka 55!

Jarida la Nchi Yetu 2016

Jarida la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo


Yaliyomo

iv

Uk. 1

JPM: Miaka 55 na Misingi Mitano ya Kuivusha Tanzania

Uk. 3

Awamu ya Tano Yaanza Kuigeuza Tanzania kuwa Nchi ya


Viwanda

Uk. 5

Sekta ya Mawasiliano Nguzo Muhimu ya Ukuaji wa


Uchumi

Uk. 7

Hongera Rais Magufuli kwa Kukienzi Kiswahili

Uk. 8

Amani, Utulivu, Uvumilivu Misingi ya kukua kwa Uhuru wa


Habari

Uk. 10

TRA yavuka Lengo la Makusanyo ya Mapato yakusanya


Wastani wa Trilioni 1.1 kila Mwezi

Uk. 17

Matukio Mbalimbali Katika Picha

Uk. 21

JPM Atimiza Ahadi ya Kuanzisha Mahakama ya Mafisadi

Uk. 27

Uhakiki wa Taarifa za Watumishi wa Umma ni Kazi


Endelevu
Jarida la Nchi Yetu 2016

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

JPM: Miaka 55 na Misingi Mitano


ya Kuivusha Tanzania

Na Hassan Abbas-MAELEZO

esemba 9 miaka 55 iliyopita,


bila shaka Rais Dkt John
Pombe Magufuli (JPM), alikuwa
miongoni mwa vijana wadogo
kabisa wa Afrika waliokuja kupata
fursa adhimu ya kukua wakiiona
kivitendo safari yenye changamoto
nyingi ya kutimiza ndoto ya Uhuru.
Leo miaka 55 baadaye, na akiwa
ameishi, amesoma na kufanya kazi
katika miongo hii mitano ya uhuru,
Dkt. Magufuli amepata fursa adhimu
ya kupokea kijiti kutoka kwa wazee
wengine wa kukumbukwa wa nchi
hii na Afrika kwa ujumla ili naye
aendeleze jahazi hili la maendeleo.
Ni

kwa

sababu

hii

basi

leo

ningeweza
kufanya
uchambuzi
kuhusu mengi ya uhuru na mengi
yaliyofanywa na viongozi wetu.
Ningeweza pia kufanya uchambuzi wa
nini kifanyike pale penye changamoto
kama alivyopata kutuasa Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere
kuwa: kujikosoa ni kujisahihisha.
Lakini jambo moja, huenda la sadfa tu,
ni kuwa maadhimisho ya miaka 55 ya
mwaka huu yamekuja wakati ambapo
tupo katika mwaka mmoja wa Serikali ya
Awamu ya Tano, Serikali yenye jukumu
muhimu la kutufikisha katika matarajio
ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025.
Ni kwa sababu hii basi nimeona leo
nifanye tafakuri; wenzangu humu
wameangalia masuala kama ya

kisekta kama vile kuimarika kwa


utumishi wa umma, uhuru wa habari,
elimu na mengineyo, basi nimeona
nijikite katika mada pana na misingi
muhimu inayowekwa na JPM katika
kuivusha Tanzania yetu kwa ujumla.
#1 Dira
Nimepata kusoma maoni ya baadhi
ya wachambuzi wakiwemo baadhi
ya Maprofesa ambapo pamoja
na mambo mengine wamegusia
dhana kwamba katika mwaka
pamoja na mazuri mengi, Rais
Magufuli hajaonesha wazi Dira yake.
Kwangu, labda kama tunazungumzia
Tanzania mbili tofauti katika kipindi
cha mwaka mmoja kama kuna msingi
muhimu ambao Rais amekuwa wazi
moyoni, machoni na hata kwa lugha ya
Inaendelea Uk. 2

Jarida la Nchi Yetu 2016

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 1

kauli ya ulimi na lugha ya picha ya mwili


wake basi ni juu ya Tanzania aitakayo.
Katika mwaka mmoja huu wa miaka
55 ya Uhuru, sijui baadhi ya wasomi na
wanasiasa wetu wanataka nini zaidi, dira
ya Rais na ambayo inatafsirika kivitendo
katika kuifikia Dira ya Taifa iko
wazi, anataka Tanzania yenye uchumi
imara utakaosaidia nchi kujitegemea.
Na katika kufikia msingi huu
tumeuona mwaka mmoja wa msisitizo
katika masuala mengi ikiwemo
uwekezaji katika viwanda, uzalishaji
wa umeme, utoaji wa huduma za jamii
ikiwemo ujenzi wa miundombinu.
Huu
ni
msingi
wa
kwanza
unaobeba misingi mingine yote.
#2 Hapa Kazi Tu
Hii ilikuwa kaulimbiu yake katika
kampeni na wakati wengi wakidhani
itabaki tu kuwa mbwembwe za Uchaguzi,
Rais Magufuli ameonesha kuwa huu ni
msingi wake mwingine mkuu wa kutaka
tuifikie Tanzania yenye kujitegemea.
Katika siku hizi 366 za awamu yake
ndani ya miaka 55 ya Uhuru, ameienzi
kivitendo falsafa ya Mwalimu Nyerere
kuwa Kazi Ndio Kipimo cha Utu na
tumeona, tumesikia na tumeshuhudia
akiwa mkali na kuhamasisha watu
kufanyakazi kwa bidii na ubunifu.
Ameishi kwa dhana hii akijifungia
kuchapa kazi iwe siku ya kazi, wikiendi
au sikukuu, amekuwa mtu wa maneno
machache huku vitendo vikiongea zaidi,
na hata pale alipoongea kabla ya vitendo
alitimiza alichoongea kivitendo katika
kuonesha hataki mchezo katika kazi.
Nimeona katika siku hizi 366 Mawaziri,
watendaji wa taasisi na watumishi
wa umma wameanza kubadilika na
kwenda na mwendo wa Kazi Tu.
Wananchi kwa sasa wanafuatwa
kutatuliwa kero zao badala ya wao
kuhaha kwenda maofisini na kushinda
muda mrefu. Viongozi wanajitokeza
katika vyombo vya habari kujibu kero
na kufafanua utekelezaji wa kazi zao.

Kama alivyoasa mtunga shairi


mashuhuri la Karudi Baba Mmoja
kwamba kama vijana wanataka mali
watayapata shambani, Rais amesema
na ameonesha kivitendo kuwa
kama tunataka Tanzania ya ndoto
yetu basi sote tujitume katika kazi;
nafahamu vijana wengi tena wasomi
wamehamasika na sasa wameingia
katika kazi ya kilimo cha kisasa.
Na tumeona hata sisi viongozi vijana
tuliopewa majukumu ya kumsaidia Rais
katika azma yake hii moto unawaka
katika kila maeneo walikopewa wajibu
wa kuutimiza. Kwangu hii ni kasi
yenye haki ndani yake na ambayo sote
tunapaswa kwenda nayo sambamba.
#3 Ufisadi na Mali ya Umma
Katika kuifikia visheni yake mbali
ya kazi, Rais Dkt Magufuli amejenga
msingi mwingine muhimu kwamba
hatutaweza kufika huko tunakotaka
kama viongozi hasa wenye dhamana
katika utumishi wa umma watafuja mali
za umma na nchi kumezwa na mafisadi.
Inafahamika kuwa moja ya vikwazo
vinavyozuia maendeleo ni keki ya Taifa
kufaidisha wachache. Nikiwa kiongozi
kijana, na ambaye nimekua nikiishi na
kuyaona mengi katika miongo mitatu hii
ya pili ya uhuru wetu ninapomuona Rais
akiwa mkali katika haya namwelewa.
Hakika kama kuna tatizo ambalo
linawanyima wananchi haki ya
kupata maendeleo basi ni hili la fedha
kutofika katika miradi husika na
badala yake kutumika isivyopaswa.
Akifafanua mzunguko huu wa kifisadi
unaokwamisha maendeleo Afrika,
Prof. Robert White, Mmarekani na
mwalimu wa wengi katika masuala
ya mawasiliano kwa umma katika
nadharia yake ya Systems Awareness
anaeleza jambo adhimu kulitafakari.
Anasema wafanyakazi wengi wa umma
katika Afrika wanafuja mali za umma
au kufanya ufisadi bila kujua kadiri
wanavyofanya hivyo mduara wa
athari za matendo yao unazunguka

na kuwaathiri pia jamaa zao wenyewe


na hata kuwarudia wao wenyewe.
Unapofuja dawa hospitalini, anasema
Prof. White, unaondoka ukifurahia
vijipesa vya muda lakini hujui ni
wiki moja tu baadaye ndugu yako,
jamaa yako, jirani yako na hata wewe
mwenyewe
unaweza
kufikishwa
hapo hapo hospitali ukiwa hoi na
kupata matatizo kwa kukosa dawa.
Rais JPM amebomoa ukuta na kujenga
msingi imara wa si tu kuwakataa
wanaoendekeza
haya
bali
pia
kuwakatisha tamaa hata wanaowaza
kuja kurithi jambo hili. Mahakama
ya Mafisadi imeanza kazi, wenye
ugonjwa mbaya wa majipu ya udokozi
wanatumbuliwa, tena bila ganzi na leo
unaposoma makala haya kila mmoja
anajua Serikali hii si ya kujaribiwa!
#4 Kodi Tu
Nimegusia ufujaji na nimegusia ufisadi,
basi kama tunapambana na hayo lazima
pia, anaonesha Rais katika siku hizi 366
za miaka 55 ya Uhuru, kuwa yatupaswa
tupambane na suala la kukusanya
kodi na kuwabana wakwepa kodi.
Ujumbe wa Rais Magufuli unasadifu
kauli za Baba wa Taifa miaka ya
1960 kuwa uhuru ni kujitegemea
hivyo tunapaswa kuhakikisha kuwa
nchi yetu, pamoja na kusaidiana na
marafiki wema, lazima ijenge msingi
wa kuondoa utegemezi usio na tija.
Katika hilo la kodi nampongeza Rais
kwa namna mbili. Mosi, kuwa kwake
muwazi kwa kila mtu juu ya wajibu
wa kulipa kodi. Pili, kuanza kuwabana
wanaokwepa wajibu wao huo wa
kulipa kodi. Katika hili, hata kabla
ya kubadilisha sheria na sera zozote,
tumeshuhudia mapato ya mwezi
yakipanda hadi zaidi ya Sh. trilioni moja.
Mimi sio mchumi lakini nimejifunza
kupitia nchi nyingi zilizoendelea
kuwa kama kuna pato muhimu na
la uhakika katika kuendeleza nchi
ni kodi na si misaada. Rais Magufuli
ameturejesha katika kuuelewa na
Inaendelea Uk. 3

Jarida la Nchi Yetu 2016

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

3
Inatoka Uk. 2

kuuzingatia msingi huu ambao hata


wachumi wabobezi kama Prof. Joseph
Stiglitz aliyepata kufanyakazi Benki
ya Dunia wamepata kuipigia kelele.
Si kukusanya kodi tu, Rais pia
amesimamia vyema matumizi. Hii ni
kwa sababu unaweza kuzuia upotevu
wa mapato, unaweza kuzuia rushwa na
unaweza kuhakikisha watu wanalipa
kodi stahiki na ukapata fedha nyingi
lakini bado malengo yanaweza
yasifikiwe iwapo fedha zinafujwa.
Katika
siku
hizi
366
Rais
ameshadidisha azma ya kujiongezea
mapato kwa kuuimarisha msingi
huo kwa kusimamia matumizi sahihi
ya fedha husika-aliagiza taasisi za
umma kuachana na matumizi yasiyo
na maana kama vikao mahotelini,
safari za nje zisizo na tija, maposho
kochokocho kila kikao na amepunguza
ukubwa wa Serikali. Ametekeleza.
#5 Anasema anatenda
Ni siku 366 katika miaka 55 ya Uhuru
zilizosheheni maajabu. Labda nianze
hivi, kuna rafiki yangu mmoja yeye siku

zote huamini kuwa wazungu wanatuzidi


vitu vichache sana-smartness. Neno
hili linaweza kubeba maana nyingi.
Lakini moja kubwa na linalosadifu
hoja yangu leo ni uuangwana wa
kusema na kutenda. Wakati Rais
akiwania nafasi hii wapo waliosema
si
mwanasiasa-kumbe
tumezoea
wanasiasa! Sasa kama hilo ni la kweli
basi sasa tunafurahia ladha tofauti
ya kuongozwa na asiye mwanasiasa.
Rais katika kutekeleza Ilani na ahadi
zake ameweka msingi mmoja mujarabu
sana katika masuala ya kuwaletea watu
maendeleo-anaahidi na anatenda,
asicho na uhakika nacho hakiahidi!
Alipoahidi kuunda Serikali ndogo
alitimiza hilo; alipoahidi kuwa ataleta
ndege na kulifufua Shirika la Ndege,
kila mmoja leo anajua habari kubwa
mijini na vijijini ni Bombardier Q400;
alipoahidi kupunguza matumizi yasiyo
ya lazima na uhifadhi usio na usalama
wa fedha za umma kila mmoja leo
anajua kinachowakuta wapiga dili.
Katika uongozi na kama anavyoshauri
Waziri Mkuu wa zamani wa

Uingereza, Tony Blair katika kitabu


The Art and Science of Delivery
kutekeleza mipango, mikakati na sera
ndio sifa kubwa inayomtofautisha
kiongozi wa kawaida na kiongozi
wa
kimageuzi
(transformational
leader).
Hitimisho, kama kuna kitu nikiulizwa
niwaambie watanzania wenzangu
na ambacho siwezi kukisahau
popote niendapo basi ni hii; kwa
azma na misingi hii ya Rais, hatuna
chaguo jingine bora zaidi zaidi ya
kumuunga kwa kuungana naye katika
treni hii ya mabadiliko, ikitokea
umeshindwa kuungana nasi sasa
basi haraka wahi kituo kinachofuata.
Kila la kheri Tanzania Bara katika
miaka 55 ya uwepo wako!
*Mwandishi wa makala haya ni
Mkurugenzi wa Idara ya HabariMAELEZO na Msemaji Mkuu wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.

Awamu ya Tano yaanza Kuigeuza Tanzania kuwa


Nchi ya Viwanda

Na May Simba-MAELEZO

ekta ya viwanda nchini ina jukumu


kubwa la kuleta mabadiliko ya
uchumi wa Taifa kutoka kuwa nchi
maskini hadi kufikia uchumi wa kati
wa viwanda unaoendana na kilimo
cha kisasa cha kibiashara chenye tija.
Kwa kuzingatia umuhimu wa viwanda
kwa ajili ya maendeleo , Serikali ya
Awamu ya Tano imeanza mkakati
wa kuweka mazingira mazuri ya
ujenzi wa viwanda vipya na ufufuaji
viwanda
vilivyokuwa
vimekufa.
Jitihada hizo za Serikali ya Rais Magufuli
zinaungwa mkono na Kaulimbiu
ya Maadhimisho ya mwaka huu ya
miaka 55 ya uhuru ambayo ni Tuunge
Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa

na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi


wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu.
Kwa mujibu wa taarifa ya mafanikio ya
Serikali ya Awamu ya Tano iliyotolewa
na Wizara ya Viwanda na Biashara , sekta
hii ya viwanda imekua kwa asilimia 9.1
katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka
2016 ikilinganishwa na robo ya pili ya
mwaka 2015, ukuaji huu kwa ujumla
umechangiwa na ongezeko la uzalishaji
wa bidhaa mbalimbali za viwanda.
Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Taifa
ya Takwimu unaonyesha kuwa
kuanzia Novemba 2015 mpaka
Oktoba mwaka huu jumla ya viwanda
vipya 1,843 vilianzishwa na kufanya
nchi kufikisha viwanda 54,422.

viwanda itaongezeka sana kutokana


na juhudi kubwa zinazofanywa
na Serikali ya Awamu ya Tano.
Wizara kupitia Idara na Taasisi zake
imehamasisha kwa kiasi kikubwa
ongezeko la uzalishaji wa viwanda
hivyo kufanya baadhi ya viwanda
nchini kama kiwanda cha Saruji
Mbeya
kuongeza uzalishaji wake
kutoka tani 350,000 na kufikia tani
1,050,000, sambamba na kiwanda
cha Saruji Tanga kutoka tani 750,000
hadi tani 1,250,00 kwa mwaka.
Kiwanda kingine cha Mavazi cha
Touku
Germent
kinategemea
kuongeza uzalishaji na hvyo kuongeza
ajira kutoka 1600 za sasa hadi 6000.

Hatua hii inaonyesha kuwa idadi ya


Inaendelea Uk. 4
Jarida la Nchi Yetu 2016

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 3

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa
Tanzania, Mhe,
Dkt. John Pombe
Magufuli akipokea
maelezo kutoka
kwa Wafanyakazi
wa Kiwanda cha
Matunda cha Azam
kilichopo Mkoani
Pwani wakati wa
Uzinduzi wa Kiwanda
hicho.

Aidha ,Wizara imeendelea kuhamasisha


uwekezaji katika viwanda vipya
ambapo jumla ya miradi 19 ya viwanda
inaendelea kujengwa mkoani Pwani.
Kati ya viwanda hivyo, kuna kiwanda
cha Nondo cha Kilua Steel ambacho
kitazalisha tani 1000 za nondo kwa siku
pamoja na kiwanda cha kutengeneza
vigae
cha
GoodWill
Tanzania
Ceramics Co.Ltd kilichopo Mkuranga.
Viwanda vingine vilivyo katika
mradi huu ni pamoja na Global
Packing cha kutengeneza vifungashio.
Mbali na hayo katika kipindi cha
kuanzia Novemba, 2015 hadi Machi,
2016 kituo cha uwekezaji Tanzania
(TIC) kilisajili jumla ya miradi 60
ya uwekezaji ambayo inatazamiwa
kuingiza mtaji wa dola za Kimarekani
1,184.86 millioni katika uchumi
na kuajiri Watanzania 14,777.
Miradi hiyo iliyosajiliwa inalenga
kuwekeza katika sekta mbalimbali
ikiwemo sekta ya viwanda 28, Utalii
10,Majengo ya biashara 10,Kilimo
4, Usafirishaji 4, Taasisi za fedha 2,
Nishati 1 na huduma za biashara 1.
Katika kusimamia ukuaji na uwekezaji
wa viwanda nchini, Wizara inaendelea
kubainisha maeneo ya Viwanda

katika Mikoa yote kwa kushirikiana


na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Halmashauri zote za Jiji, Manispaa,Miji
na Wilaya kwa ajili ya kutenga
maeneo ya shughuli za viwanda.

Wizara pia imekamilisha mgawanyo


wa eneo la viwanda la TAMCO Kibaha,
ambapo viwanda vya nguo vimetengewa
ekari 95, viwanda vya magari ekari 64,
na eneo lingine limetengwa kwa ajili
ya ujenzi wa viwanda vya madawa.

Halikadhalika, Wizara hiyo kwa


kushirikiana na Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
inahakikisha maeneo ya viwanda
yanaendelea
kuhuishwa
katika
mipango miji, ambapo jumla ya
viwanja 240 vya kujenga viwanda
katika eneo la Pemba Mnazi Kigamboni
vimepimwa na kutangazwa kwa ajili
ya uwekezaji na hadi kufikia mwezi
Septemba, 2016, jumla ya maombi
150
yamewasilishwa
Wizarani.

Wizara imebainisha kuwa kuna baadhi


ya wawekezaji waliokwishajitokeza
kuwekeza ambao wako katika
majadiliano ni pamoja na kampuni
ya magari ya TATA, BENBROS ya
kuunganisha mabasi aina ya YUTONG.

Mbali na hilo eneo la Mkulanzi ambalo


lina ukubwa wa hekta takribani elfu
20 limekabidhiwa kwenye Mifuko
ya Hifadhi ya Jamii hasa NSSF na
PSPF kwaajili ya kuwekeza katika
kilimo na kiwanda cha sukari.
Vile vile Wizara inamiliki hekta 107
katika eneo la Zuzu mkoani Dodoma
kwa ajili ya uanzishwaji wa kijiji
cha viwanda vya ngozi na bidhaa za
ngozi, ambapo wawekezaji wadogo
(wajasiriamali) watatumia kutengeneza
bidhaa
mbalimbali
za
ngozi.

Jarida la Nchi Yetu 2016

Hivi karibuni Tanzania ilipokea ujio wa


Marais kutoka Nchi mbalimbali ambao
wameonesha nia kubwa ya kushirikiana
na
Tanzania
katika
uwekezaji
hususani katika sekta ya Viwanda
Baadhi ya Nchi hizo ni pamoja na
Morocco, India, Cuba na China nchi
zote hizi zimeonyesha dhamira kubwa
katika kushirikiana na Tanzania
katika uchumi wa Viwanda Nchini.

Tuunge Mkono Jitihada


za Kupinga Rushwa na
Ufisadi na Tuimarishe
Uchumi wa Viwanda kwa
Maendeleo Yetu

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Sekta ya Mawasiliano Nguzo


Muhimu ya Ukuaji wa Uchumi

Moja ya Mitambo ya Simu iliyokuwa ikitumika mara baada ya


Uhuru wa Tanzania Bara.

Na Benjamin Sawe-MAELEZO moja kwa moja na kwa kupitia sekta

i miaka 55 ya Uhuru ambapo


Tanzania inashuhudia ukuaji
mkubwa wa Sekta ya Mawasiliano
na kuwa moja ya nguzo muhimu
ya kukuza uchumi kwa Taifa.
Ukuaji huo ni ule wa kutoka kaya chache
sana kuwa na mawasiliano ya simu
wakati wa Uhuru na kufikia mwaka 2016
ambapo sasa laini za simu za mkononi
zimefikia takribani 39,808,419, kwa
upande wa mawasiliano ya simu.
Sekta hii inachangia katika uchumi

ya elimu, afya, kilimo, biashara,


ajira, benki, utalii, uwekezaji na
sekta nyingine zote kama nyenzo ya
uwezeshaji katika kuongeza ufanisi
wa utendaji kupitia jamii habari.
Takwimu zinaonesha kuwa laini za simu
zinazotumika zimeongezeka kutoka
34,251,801 mwaka 2014 hadi kufikia
laini 39,808,419 mwaka 2016 na idadi
ya watumiaji wa intaneti waliongezeka
kutoka 14,217,311 kwa mwaka 2014 hadi
kufikia 17,263,523 kwa mwaka 2015.
Aidha, zaidi ya asilimia 64 ya kaya
nchini zinamiliki simu za mikononi.

Pia ukuaji huu umeongezeka hadi


kwenye vituo vya kurusha matangazo.
Vituo vya kurusha matangazo ya redio
vimeongezeka kutoka vituo 91 mwaka
2014 hadi kufikia vituo 116 mwaka 2015.
Wakati Tanganyika inapata uhuru
mwaka 1961 kulikuwepo na kituo kimoja
cha redio (RTD) kwa sasa ni zaidi ya 140
Kwa upande wa vituo vya luninga wakati
wa Uhuru hakikuwepo hata kimoja
lakini miaka 55 baadae vipo zaidi ya 25
na vinaendelea kutoa taarifa za habari,
matukio na burudani kwa wananchi.

Inaendelea Uk. 6
Jarida
ya Habari
Jarida la
laWizara
Nchi Yetu
2016

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 5

Mafanikio hayo yamewezesha kukua


kwa kasi kwa sekta ya mawasiliano
kutoka asilimia 8.0 mwaka 2014 hadi
kufikia asilimia 12.1 mwaka 2015 na
hivyo kuwa sekta ya kwanza katika
sekta za huduma na kuwa ya pili kwa
sekta zote katika ukuaji hapa nchini.
Sekta hii imechangia katika pato
ghafi la Taifa kwa asilimia 3.6 mwaka
2015. Matokeo haya ya ukuaji
na mchango katika teknolojia ya
habari na mawasiliano kwa sehemu
kubwa yametokana na kuongezeka
kwa matumizi ya huduma za
mawasiliano zikiwemo zile za muda
wa maongezi kwa simu za viganjani
na mezani, intaneti na utangazaji.
Pia, ufanisi huu umechangiwa na
kukua kwa matumizi ya miamala ya
kielektroniki ambayo ni pamoja na
uuzaji na ununuzi wa bidhaa na utoaji wa
huduma kwa njia za kielektroniki kama
vile kutuma na kupokea pesa, kulipia
ankara za maji, umeme, ada, leseni
za magari na usajili wa makampuni.
Utafiti kupitia tathmini ya Global
Microscope
umebaini
kuwa
Tanzania imeshika nafasi ya sita kati
ya nchi 55 duniani na inaongoza
katika Bara la Afrika kwa kuwa na
mazingira mazuri ya huduma za

kifedha kupitia simu za kiganjani.


Vilevile, kwa mujibu wa ripoti ya
Fiscope Survey ya mwaka 2015,
huduma za kifedha zimewafikia
Watanzania kwa asilimia 76 kutoka
asilimia 44 mwaka 2009 ikiwa
imechangiwa kwa kiasi kikubwa na
uwepo wa Mawakala wa Kibenki.
Hii pia inachangiwa na huduma
za kifedha kupitia makampuni
ya simu kiasi cha kufikia akauti
za miamala ya kifedha (mobile
money
accounts)
takribani
17,639,349 hadi Desemba 2015.
Zaidi ya hapo, takwimu zinaonesha
kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza
duniani kwa kampuni za simu
za viganjani kuwa na utayari na
makubaliano
ya
kuunganisha
miamala ya huduma ya fedha.
Hii imewezesha kupunguza gharama
za kutuma fedha kutoka mtandao
mmoja kwenda mitandao mingine.
Jambo hili limewezesha Tanzania
kuongoza duniani katika kutumia
huduma ya Mobile Money Banking
kwa kiasi cha fedha zinazozunguka
kwenye mtandao kwa wastani wa
Shilingi trilioni 4.5 kwa mwezi.
Ukuaji imara na
wa kasi wa sekta
ya
mawasiliano
nchini ni sehemu
ya
mafanikio
yaliyotokana
na
Sera za Serikali.
Sera hizo
za
Serikali
na
kufunguliwa
kwa soko huria
zimewezesha
kuongezeka kwa
wawekezaji
na
hivyo
kuwapa
watumiaji fursa ya
kuchagua huduma
bora wanayohitaji
kwa
gharama
wanazomudu.
Jarida la Nchi Yetu 2016

Katika kukabiliana na changamoto ya


idadi ndogo ya wananchi wanaotumia
huduma za simu, Serikali zote
tangu Uhuru zimeendelea kupanua
wigo ikiwemo kujenga Mkongo wa
Taifa unaotarajiwa kufikia Mikoa
yote ili wananchi wote wapate
kiurahisi
huduma
za
intaneti.
Ni kwa sababu hii ndio maana Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.
Makame Mbarawa anasema wakati
Serikali inaanza ujenzi wa mkongo huo
ulikuwa umejengwa kiasi cha kilometa
700 tu lakini hadi leo tayari ujenzi wake
umefikia takribani kilometa 18,000.
Nina uhakika baada ya miaka miwili
utakuwa umefikia zaidi ya kilometa
25,000, anasema Prof. Mbarawa.
Anaeleza zaidi kuwa Serikali inatambua
umuhimu wa matumizi hayo ya simu
nchini na ndio maana imeanzisha
huduma za kilimo mtandao, afya
mtandao na elimu mtandao ili wananchi
na wao waweze kufaidika zaidi.
Aidha, maendeleo ya mkongo wa
Taifa nchini Tanzania yamesababisha
kuongezeka kwa ukuaji wa uchumi,
kupunguza gharama za mawasiliano
kutoka dola 20,000 za Kimarekani
kwa mwezi hadi dola 160 kwa mwezi,
hilo likiwa ni punguzo la asilimia 99.
Pia imepunguza gharama kwa
watumiaji wa mwisho kutoka dola
0.06 kwa dakika mwaka 2009 hadi 0.03
dola kwa dakika mwaka 2013 na pia
kupunguza gharama za intaneti kutoka
dola 16.45 kwa gigabyte moja mwaka
2009 hadi dola 4.11 mwaka 2013.
Ni ukweli usiopingika kuwa sekta
ya mawasiliano imekuwa kwa kasi
katika kipindi cha miaka 55 ya Uhuru
wa Tanganyika (sasa Tanzania Bara)
ambapo inakadria kukua zaidi ifikapo
2025 ukuajia wa sekta hii utasaidia zaidi
azma ya Dira ya Maendeleo ya Taifa.

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Hongera Rais Magufuli kwa


Kukienzi Kiswahili
Na Immaculate Makilika-MAELEZO

angu uongozi wa Awamu ya Tano


uingie madarakani mwishoni
mwa mwaka jana umeweka mkazo
mkubwa katika kuimarisha lugha
ya Kiswahili ili iwe kiunganishi
kikubwa
cha
mawasiliano
ya
Watanzania na mataifa mbalimbali
katika shughuli za maendeleo.
Hatua hiyo inafuatia Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli kuonyesha kwa
vitendo matumzi ya lugha ya Kiswahili
katika shughuli za kitaifa na kimataifa.
Rais Magufuli amekuwa akitumia
lugha ya Kiswahili katika mikutano
mbalimbali ya kimataifa iliyofanyika
hapa
nchini
hivi
karibuni
alipokutana na viongozi mbalimbali
waliomtembelea
hapa
nchini.
Jitihada hizo za Rais Magufuli zinatokana
na lugha hiyo kuwa miongoni mwa
lugha 10 inayozungumzwa na watu
wengi duniani na Afrika ikikadiriwa
kuwa na wazungumzaji
milioni
zaidi ya 100 ulimwenguni kote.

Hatua hiyo ya Rais Magufuli inaunga


mkono na kuenzi juhudi za Baba wa
Taifa,
Julius Kambarage
eko Mwalimu Wizara
ya
Habari,Utamaduni,Sanaa
na
Nyerere za kutumia lugha katika
Michezo
kusimamia
wa
njia ya kwa
mawasilano
kwa ujenzi
wapigani
mageti ya kielektroniki katika kuboresha
uhuru ndani na nje ya Tanzania.
makusanyo yatokanayo na michezo

iinayofanyika

Uwanja

wa

Taifa.

Lugha hii sasa huzungumzwa katika


Hizo
zilizokuwana
zikitolewa
kwa
nchi ni
zapongezi
Afrika Mashariki
hasa katika
uongozi wa Wizara kutoka kwa wadau
nchi za Tanzania, Kenya, Uganda,
wa michezo hivi karibuni mara baada ya
Jamhuri ya kwa
Kidemokrasia
Kongo,
kuzinduliwa
mfumo wa ya
kisasa
wa
na katika
za Rwanda,
mageti
ya nchi
kieletroniki
ambayoBurundi,
hutumia
kadi
maalumu
ambazo
ndiyonahuruhusu
Msumbiji,
Zambia,
Comoro
Malawi.
mageti
kufunguka
na
mtu
kupita.
Nje ya Afrika lugha ya Kiswahili
Hivyo basi namna hiyo ya mageti hayo
huzungumzwa katika nchi za Uarabuni
yanavyofanya kazi ndiyo huleta tafsiri
kamamfumo
Dubai,waYemeni
wa
ya
mageti na
ya Umoja
kieletroniki.
nchi za kiarabu na hata mashirika
Akizungumza
katika kama
makabidhiano
ya
makubwa ya habari
BBC, VOA
mageti hayo ya kieletroniki yaliyoko katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

na nchi nyingine kama Ufaransa


wameanzisha Idhaa za Kiswahili.
Lugha hii ya Kiswahili imetoa
mchango mkubwa katika harakati
za kupigania uhuru na hata baada
ya uhuru, kiasi ambacho sasa dunia
nayo inashawishika kutumia Kiswahili
katika masuala ya siasa, elimu,
diplomasia, uchumi na biashara.
Baada ya kupata Uhuru mwaka
1961, Kiswahili kiliendelea kuwa
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
lugha
ya mawasiliano kwa kada za
Michezo, Mhe.Nape Moses Nnauye
chini
za
utawala,
serikali
za mitaa,
alisema kwa
kufanikisha
hilo kumeifanya
utamadunikuwa
wanchimijini,
viwandani,
Tanzania
ya kwanza
kuwa na
mageti
ya kisasa
katika ukanda
huu wa
mashamba
makubwa,
elimu
ya
Afrika
Na hii
sehemu
nzuri.
msingiMashariki.
hadi darasa
la ni
sita,
mahakama
za mwanzo,
kadhalika.
Kukamilika
kwanaujenzi
wa magetiKatika
hayo
vyombo vya na
habari
maeneo
ya
kunafuatiwa
agizo na
la Waziri
Mkuu
Mhe.Kassim
Majaliwa
alipofanya
ziara
starehe Kiswahili
kilikuwa
kikitumika
ya
kikazi uwanjani
hapo ya
mnamo
Februari
sanjari
na lugha
kiingereza.
17,2016 na kumwagiza Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mnamo
tarehe
10ujenzi
Desemba
1962, Rais
kuhakikisha
kuwa
huo unakamilika
wa
Tanganyika
Baba
wa
Taifa,
kwa haraka kwa kuwa ni Mwalimu
sehemu
ya
mkataba
wa ujenzi
wa uwanja.
Julius
Kambarage
Nyerere
katika

hotuba yake, kwa Kiswahili, alisisitiza


Pamoja na hayo Waziri Nnauye alieleza
matumizi
ya lugha
kama lugha
kuwa mfumo
huo hiyo
umeandaliwa
na
asilia ambayo
wa Tanganyika
wakati
Kampuni
ya raia
kizalendo
ya SELCOM

huo walipaswa kuitumia ili kuelewana


ifaavyo, na kuondoa uwezekano
wowote wa mafarakano yanayohusiana
na mitafaruku ya kimatamshi.
Utamu wa lugha hii umeenea sana tangu
Mwalimu alipoitangaza rasmi kuwa
lugha ya kuwaunganisha wananchi.
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume
ya Umoja wa Afrika, Alpha Omar
Konare, Rais wa Jamhuri ya Mali alipata
kusema: Wakati umefika kwa bara letu
kujipatia mbinu za kuzifanya lugha za
Kiafrika kuwa lugha za mawasiliano
katika nyanja zote za maisha ya jamii.
Harakati hizo za ngazi ya Bara
kuunga mkono juhudi za Serikali
zinajidhihirisha baada ya Tanzania
kuridhia itifaki ya kuanzishwa kwa
Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki
ambapo
Makao Makuu yapo Zanzibar.
Hivi karibuni, Wabunge wa Bunge la
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA)
kwa pamoja wametoa mapendekezo
ya kutumia lugha ya Kiswahili
katika shughuli za Bunge hilo.
Inaendelea Uk. 8

Jarida
la Tume
ya Taifa
Uchaguzi
Jarida
la Nchi
Yetu ya
2016

8
Inatoka Uk. 7

Matumizi ya Kiswahili ndani ya


Bunge hilo yataongeza msukumo
wa lugha ya Kiswahili kutambuliwa
na kupewa uzito kimataifa, hatua
ambayo licha ya kuharakisha masuala
ya uchumi yataongeza fursa za ajira
kwa wananchi wa jumuiya yetu.

kikongwe nchini na Afrika, Chuo


Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
kimeendelea
kukienzi
Kiswahili
kwa kuamua mikutano yake yote
ya kiutawala ya ndani iendeshwe
kwa Kiswahili na pia mikhtasari ya
vikao nayo iandaliwe kwa Kiswahili.

Itakumbukwa kuwa Viongozi wastaafu


wetu wote ambao ni Mzee Ally Hassan
Mwinyi, Benjamin Mkapa na Dkt. Jakaya
Kikwete kwa nyakati zao walikipigania
sana Kiswahili na hata nao kuzungumza
kwa kutumia lugha hiyo katika baadhi
ya mikutano ya ndani na nje ya nchi.

Wakati tunampa kongole Mheshimiwa


Rais Magufuli na viongozi wote
mashuhuri nchini waliopita huko
nyuma
kwa
kuenzi
Kiswahili,
kila Mtanzania ana budi kwa
upande wake kutumia miaka hii
55 kutafakari namna bora zaidi ya
kukienzi Kiswahili popote alipo.

Hamasa
kutoka
kwa
viongozi
imeendelea kuchochea hata taasisi
nazo kuanza kukienzi Kiswahili kwa
karibu zaidi. Kwa mfano, Chuo Kikuu

Gwiji wa Lugha ya Kiswahili


Marehemu Shaaban Robert.

Amani, Utulivu, Uvumilivu Misingi


ya Kukua kwa Uhuru wa Habari
Na Ismail Ngayonga-MAELEZO

atika kipindi cha miaka 55


ya Uhuru wa nchi yetu, sekta
ya habari na utangazaji imekua
na kupanuka kwa kiasi kikubwa
kutokana na maendeleo ya teknolojia
ya habari na mawasiliano ambavyo
vimerahisisha upataji na utoaji habari.
Kubwa pia linaloifanya Tanzania
kuwa tofauti na nchi nyingine
duniani na Afrika ni kuwepo kwa
uvumilivu wa kisiasa, Amani na
utulivu vitu ambavyo vimeipa fursa
sekta ya habari kukua kwa kasi.
Nafahamu zipo namna nyingi za
kupima kiwango cha uhuru wa habari;
wapo wanaangalia wingi wa magazeti
na vyombo vingine vinavyosajiliwa
na kupewa fursa ya kufanyakazi yao
kwa mapana. Wapo pia wanaotumia
vigezo kama vile uhuru wa kukusanya,

kuhariri na kusambaza habari hizo.


Miaka 55 leo, Tanzania inajipambanua
katika Afrika katika uhuru wa habari
kwa vigezo vyovyote mtu anavyoweza
kuvitumia kupimma huku ikiwa ya
kwanza katika Afrika Mashariki kwa
uhuru kwa mujibu wa Ripoti ya 2016 ya
Reporters Without Borders (Tanzania
ya 71 duniani; Kenya 95; Uganda 102;
DRC 152; Rwanda 161 na Burundi 156)).
Ripoti hiyo ni kiashiria kuwa
Tanzania imefanya mengi katika
miaka 55 ya uhuru kwa sekta ya
habari. Tukianza na idadi ya vyombo
vya habari: imeongezeka kutoka
vyombo
vichache
vilivyokuwepo
wakati wa uhuru hadi utitiri wa
vyombo vya habari uliopo hivi sasa.
Kwa mfano mwaka 1961 kulikuwa
na kituo kimoja tu cha redio
(Redio Tanzania Dar es SalaamRTD), na leo hii Tanzania inavyo
vituo vya redio vipatavyo 126.

Aidha
magazeti
na
majarida
yameongezeka
kutoka
manne
(4) yaliyokuwepo mwaka 1961
hadi kufikia 477 mwaka huu
2016. Kati ya hayo magazeti 12
yanatoka kila siku na 30 kila wiki.
Uhuru wa habari pia unaweza
kupimwa kwa namna Serikali
ilivyoweka sera, sharia na mifumo ya
kitaasisi ili kuhakikisha kuwa vyombo
vya habari vinatekeleza haki yao
lakini pia vikitimiza wajibu husika.
Kwa mfano, mwaka 1970 Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere alitoa sera mpya ya
vyombo vya habari kupitia gazeti la
The Standard ambalo lilibadilishwa
jina na kuitwa The Daily News.
Sera hiyo iliyokuwa ikiongozwa
na mfumo wa siasa ya Ujamaa na
kujitegemea ilivitaka vyombo vya
Inaendelea Uk. 9

Jarida la Nchi Yetu 2016

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 8

habari kuwa ni taasisi za kutoa huduma


kwa umma badala ya biashara ya
kutafuta faida na falsafa ya sekta
ya habari na mawasiliano ilikuwa:
Mawasiliano kwa ajili ya maendeleo.
Lakini
pia
Mwalimu
alisema
vyombo hivyo lazima vikusanye,
kuhariri na kutangaza habari za
kweli, zenye usahihi na zaidi viwe
na uhuru wa kukosoa pale baadhi ya
watendaji wa Serikali wanapokwenda
kinyume na mtazamo wa Serikali.
Kutoka
tamko
la
Mwalimu
hadi miaka ya karibuni Serikali
imefanya mengi ikiwemo kuanzisha
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
ambayo inaratibu vyombo vya
habari vya redio na televisheni.
Kwa upande wa magazeti, Idara ya
Habari-MAELEZO nayo ilihusishwa
na kupewa majukumu baada ya Uhuru
kuwa Mratibu wa masuala ya vyombo
vya habari kwa upana wake lakini
Idara hiyo ikisajili zaidi magazeti.
Hatua za hivi karibuni za kutunga
Sheria mpya mbili; Sheria ya Haki ya
Kupata Taarifa na Sheria ya Huduma za
Habari zote za mwaka 2016 zimekuwa
mkombozi mkubwa kwa tasnia hiyo.
Wakati Sheria ya Haki ya Kupata Habari
ikilenga kuwahakikishia wananchi na
wanahabari kwa upande wao uhakika
wa kupata taarifa muhimu kwa
maendeleo yao kutoka ofisi za umma,
Sheria ya Huduma za Habari ni muhimu
kwa sababu inakwenda kuongeza
weledi kwa tasnia ili itumie vyema jamii
Mkurugenzi wa Idara ya HabariMAELEZO, ambaye pia ndiye Msemaji
Mkuu wa Serikali, Bw. Hassan Abbas
anasema uhuru wa vyombo vya habari
umeimarika kwa kiwango cha juu
hapa nchini hasa ikizingatiwa historia
ya Amani, utulivu na uvumilivu.
Uhuru uliopo sio kwamba umeibuka
tu; umejengwa katika misingi
mikubwa iliyotokana na waasisi
wa uhuru wetu kuweka sera na

utamaduni wa kuvipa vyombo vya


habari nafasi ya kushiriki katika
ujenzi wa Taifa, anasema Bw. Abbasi.
Katika miaka hii nchi yetu pia
imepiga hatua kubwa katika kusajili
na kuendesha vyuo vya taaluma ya
habari. Wakati baada ya uhuru uhitaji
wa wanataaluma ya habari ukiwa juu
sana, hivi sasa kuna vyuo vinavyotoa
mafunzo ya taaluma ya habari na
baadhi yake vinaendesha mafunzo
hayo kwenye ngazi ya Chuo Kikuu.
Baadhi ya vyuo hivyo ni Shule Kuu ya
Uandishi wa Habari na Mawasiliano
ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (SJMC), Chuo Kikuu cha
Tumaini, Chuo Kikuu cha Waislamu
Morogoro(MUM) na Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Augustino cha Jijini Mwanza
(chenye kampasi kadhaa sehemu
nyingine nchini) (SAUT) na Chuo
Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).
Vyuo vingine ni Chuo cha Uandishi wa
Habari cha Dar es Salaam (DSJ), Chuo
cha Uandishi- TIMES (TSJ), Chuo cha
Uandishi wa Habari cha Royal na Taasisi
ya Elimu ya Jamii na Habari na Chuo cha
Upigaji Picha vyote vya Dar es Salaam.
Vipo pia vyuo vya uandishi wa
habari huko mikoani, ikiwa ni
pamoja na MSJ, AJTC, Taasisi ya
Mafunzo ya Afrika Mashariki Arusha
na Chuo cha Habari- Zanzibar.
Awali pia miaka ya 1970 Serikali kwa
kutambua umuhimu wa taaluma
ya habari katika kuleta maendeleo,
ilianzisha Chuo cha Uandishi wa Habari
cha Tanzania (TSJ) na ndicho mwaka
2003 kilibadilishwa jina na kuwa sehemu
ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Anaongeza kuwa Serikali pia ilitoa
mwongozo wa uanzishaji Vitengo
vya Habari, Elimu na Mawasiliano
katika ofisi za umma ikiwemo
Wizara, Idara, Taasisi, Wakala na
Mamlaka ya Serikali za Mitaa, hatua
iliyolenga kurahisisha utoaji na
upatikanaji wa taarifa za Serikali kwa
umma kupitia vyombo vya habari.

Jarida la Nchi Yetu 2016

Dhumuni la kuanzisha vitengo


hivyo ni bkuhakikisha kuwa Serikali
inakuwa na wasemaji wake ambapo
wanajitokeza mara kwa mara katika
vyombo vya habari kwa ajili ya
kuzungumzia sera, mipango, mikakati
na utekelezaji wa ahadi mbalimbali
zinazotolewa
kwa
wananchi.
Mpaka sasa kuna takribani Maafisa
Habari 406 katika Wizara, Idara,
Taasisi, Wakala na Mamlaka ya Serikali
za Mitaa, ambapo MAELEZO inaratibu
vitengo hivyo kwa kuwajengea uwezo
na weledi katika kuisemea Serikali.
Akizungumzia kuhusu miaka 55 ya
uhuru na wajibu wa vyombo vya habari,
Mkurugenzi Abbasi anasema vyombo
vya habari vya Tanzania vinaendelea
kufanya kazi vizuri zaidi ingawa kuna
baadhi ya changamoto ambazo anasema
Idara yake itaendelea kushirikiana
na wanahabari wenyewe kuzitatua.
Wakati wanahabari wengi wakitimiza
wajibu wao kwa kuchangia katika
maendeleo ya Taifa wapo wachache
wanaodhani uandishi wa habari ni
kuamka asubuhi na kumwandika
mtu mwingine bila kufuata misingi
ya kisera na kisheria iliyopo, alisema.
Anaongeza kuwa dhana kwamba
uhuru wa habari hauna ukomo ni
ubatilifu kwa sasa hata mikataba
ya kimataifa kuna masuala imezuia
vyombo vya habari kuyasema au
kuyatangaza na kuyachapisha ili
kulinda uhuru wa watu wengine.
Katika sharia inazotunga, sera na
usimamizi wa habari, Bw. Abbas
anasema
Serikali
ya
Tanzania
imekuwa na itaendelea kuheshimu
haki za wanahabari lakini pia
itaendelea kuwakumbusha kuenzi
wajibu wao kwa watu wengine.

10

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

TRA yavuka Lengo la Makusanyo


ya Mapato, yakusanya Wastani wa
Trilioni 1.1 kila Mwezi

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kushoto) akiongea na Waandishi wa
habari Jijini Dar es Salaam kuhusu Mamlaka hiyo kuvuka lengo kwa kukusanya zaidi ya Shilingi
Trilioni moja kila mwezi.

Na Jovina Bujulu-MAELEZO

angu uongozi wa Rais wa Jamhuri


ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli ulipoingia
madarakani, mwaka mmoja uliopita,
Watanzania wameshuhudia mafanikio
makubwa katika sekta ya ukusanyaji kodi
kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato.
Hatua hii inatokana na Rais Magufuli
alipoingia
madarakani
amekuwa
mstari wa mbele kuhakikisha hakuna
mfanyabiashara anayekwepa ulipaji
kodi na kuwahimiza wananchi
kuhakikisha wanadai risiti kwa kila
bidhaa au huduma wanayolipia.

Juhudi hizi za Rais Magufuli za


kuongeza mapato na kudhibiti
upotevu wa mapato ya Serikali
zimejionyesha
katika
mikutano
yake mingi ambapo mara nyingi
amekuwa akisema Ukinunua bidhaa
dai risiti na ukiuza bidhaa toa risiti.
Hapa nchini, Mamlaka ya Mapato
(TRA) ndicho chombo chenye
jukumu la kusimamia ukusanyaji wa
mapato ya Taifa na imekuwa ikitimiza
lengo hilo kwa kutekeleza mikakati
mbalimbali kama ilivyoainishwa katika
mpango mkuu wa miaka mitano.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi,
Bw. Richard Kayombo, katika kipindi

cha mwaka mmoja wa utawala wa


Rais Magufuli
kumekuwepo na
ongezeko la makusanyo ya mapato
ya Serikali yatokanayo na kodi.
Anasema katika kipindi hiki, TRA
inakusanya wastani wa trillion
1.1 kila mwezi kuanzia mwezi
Novemba, 2015 hadi Septemba 2016.
Hili ni ongezeko la asilimia 28.1
kutoka kwenye kukusanya wastani wa
shilingi bilioni 867 kwa mwezi katika
kipindi cha mwezi Novemba, 2014 hadi
Septemba 2015, anasema Bw. Kayombo.
Makusanyo ya mapato katika kipindi
cha utawala wa Rais Magufuli kuanzia
mwezi Novemba 2015 yamekuwa
yakiongezeka ikilinganishwa na miaka
Inaendelea Uk. 11

Jarida la Nchi Yetu 2016

11

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 10

iliyotangulia kwa mfano mwaka wa fedha


2015/2016 mapato yaliyokusanywa
yalikuwa shillingi trilioni 12.5 ikiwa
ni ongezeko la asilimia 26.4 ya
makusanyo ya mwaka 2014/2015.
Aidha TRA imekwisha kusanya
kodi kiasi cha shilingi trilioni 3.5
kufikia mwezi Septemba 2016,
ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.4
ikilinganishwa na kipindi kama
hiki cha robo mwaka 2015/16.
Bw. Kayombo anaongeza kuwa kwa sasa
TRA inatekeleza mpango mkakati wa
nne wa ukusanyaji kodi wenye dhamira
ya kuongeza makusanyo ya kodi za ndani
kwa kuongezea ulipaji kodi wa hiari.
Jitihada mojawapo zinazofanywa
na TRA ni pamoja na kuboresha
mifumo ya makusanyo inayoendana
na mazingira ya sasa ya ukuaji na
teknolojia ili kuhakikisha walipa
kodi wanalipa kwa urahisi kama
ilivyo dhamira yake ya kurahisisha
ulipaji kodi na kufanya mazingira
yawe bora anasema Bw. Kayombo.
Katika kipindi cha mwaka mmoja
ambao Rais Magufuli amekuwa
madarakani,
juhudi
mbalimbali
zimefanyika
ili
kuhakikisha
matarajio ya Rais ya kuimarisha
makusanyo ya kodi na kudhibiti
mianya ya rushwa yanafanikiwa.

Mafanikio
hayo
yatamuwezesha,
Rais Magufuli kutimiza ahadi
zake alizozitoa wakati wa kampeni
zikiwemo kuboresha afya, upatikanaji
wa maji, umeme, kutoa elimu bure,
ujenzi wa miundombinu kama vile
viwanja vya ndege, reli na barabara.
Aidha makusanyo hayo yatawezesha
uwekezaji katika ujenzi wa viwanda
ambavyo vitatoa ajira kwa wananchi
na Serikali kuweza kujitegemea
na hivyo kupunguza utegemezi
wa misaada kutoka kwa wafadhili.
Bw. Kayombo anataja kiini cha ongezeko
la kukusanya kodi kuwa ni matumizi
ya mashine za kielectroniki (EFD)
ambazo zinatumika zaidi badala ya
stakabadhi zinazoandikwa kwa mkono.
Matumizi
ya
stakabadhi
zinazoandikwa
kwa
mkono
hayajakuwa na ubora mzuri wa
kukusanya na kuongeza mapato
na
kutunza
kumbukumbu
sahihi ambayo yaliifanya serikali
ipoteze mapato mengi aliongeza.
Katika hatua nyingine TRA ilitoa
mashine za EFDs 130 bure kwa
makatibu wakuu wa Wizara mbai
mbali kwa ajili ya taasisi za Serikali
ambazo
zinakusanya
maduhuli
ya Serikali kwa nia ya kudhibiti
upotevu wa mapato ya Serikali.

Katika kuhakikisha makusanyo ya


kodi yanaongezeka TRA imeenndelea
kudhibiti mianya ya kwepaji kodi,
kufichua wakwepa kodi, kupambana
na rushwa na kupanua wigo wa
kodi kwa kusajili wafanyabiashara
ambao hawajasajiliwa sambamba na
kuendesha zoezi la kuhakiki namba
ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN)
linaloendelea jijini Dar es Salaam kwa
sasa ili kuboresha daftari la walipa kodi.
Pamoja na mafanikio hayo Kayombo
alizitaja changamoto wanazokutana
nazo katika ukusanyaji kodi kuwa
ni pamoja na taarifa za kodi
kutowafikia wananchi wote ili
kujenga uhiari wa kulipa kodi na
uwepo wa ukanda mrefu wa Pwani
unaosababisha kuwepo mianya mingi
ya ukwepaji kodi ambapo bidhaa
huingizwa nchini kwa njia za panya.
Pamoja na changamoto hizo, TRA
imeendelea kubuni mikakati mbali
mbali ya kuongeza ukusanyaji wa mapato
ili kuendana na kauli mbiu ya serikali
ya awamu ya tano isemayo HAPA
KAZI TU ili kutimiza na kuvuka lengo
la kukusanya shilingi trilioni 15.1 kwa
kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17.

Ukinunua bidhaa dai


risiti na ukiuza bidhaa
toa risiti

Jarida la Nchi Yetu 2016

12

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Miaka 55 ya Uhuru,
Tanzania Kuanza Kutumia
Anwani za Makazi
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

erikali ya Tanzania kupitia Sera


ya Taifa ya Posta ya mwaka
2003,
imedhamiria
kuanzisha
mfumo wa anwani zinazoendana
na majina ya mitaa ambapo watu
binafsi na maeneo ya biashara
yatatambulishwa kwa kutumia majina
ya maeneo yaliyopo na postikodi.
Sera hiyo imejikita katika kuchangia
utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo
ya mwaka
2025 yenye lengo la
kuwaondoa watanzania kutoka kwenye
umaskini na kuinua ubora wa maisha.
Hivi karibuni Serikali ya Tanzania
imezindua mwongozo wa mfumo wa
anwani za makazi na postikodi ukiwa
na lengo la kutekeleza na kuwezesha
Wizara,
Idara
zinazojitegemea,
Wakala wa Serikali na wadau wa
Sekta ya Posta namna ya kutimiza
wajibu katika kusimamia masuala
ya anwani za makazi kwa kuzingatia
Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.
Katika Mwongozo huo Serikali
imezitaka
Taasisi
zake
katika
Sekta ya Posta kuhakikisha kuwa
zinaanzisha na kutumia vema mfumo
wa anwani za makazi hapa nchini.
Aidha, wadau wa mpango huo ikiwa
ni pamoja na Wizara zinazohusika
na utekelezaji, watoaji na watumiaji
wa huduma za posta, wananchi
na waendelezaji wa makazi nchini
wanahimizwa
kushirikiana
kikamilifu katika utekelezaji wa

Balozi wa Anwani za Makazi Duniani, Prof. Anna Tibaijuka akimkabidhi Waziri


Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa moja ya
anwani ya makazi wakati wa Uzinduzi wa Mwongozo wa Mfumo wa Anwani
za Makazi Bungeni Mjini Dodoma.

mfumo huo. Anuani hizi na katika


miaka hii 55 ni muhimu sana katika
kuwafikishia
wananchi
huduma.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi
Mwongozo wa Mfumo wa Anwani
za Makazi na Postikodi Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa amesema kuwa
Mfumo wa Anwani za Makazi na
Postikodi mbali na faida zake ikiwemo
kuinua ummoja wa utaifa katika nchi
pia utarahisisha ukusanyaji wa mapato
kutoka vyanzo mbalimbali nchini.

kodi stahiki na hili ni jambo muhimu la


Utawala bora alifafanua Waziri Mkuu.
Aidha, alisema Mfumo huo wa
Anwani za Makazi utaiwezesha
Serikali kuwahudumia wananchi
wake kirahisi ikiwa ni pamoja na
kutoa ulinzi, kurahisisha mawasiliano
miongoni mwa wananchi na Serikali.

Mhe. Majaliwa alisema kuwa Mfumo


huo utawezesha ukusanyaji wa kodi
mbalimbali kwa urahisi na kwa
wakati ambapo itawezesha kutambua
mali na kaya katika eneo fulani.

Vile vile, mfumo huo utasaidia


kurahisisha na kuongeza ufanisi
katika utoaji huduma za kijamii,
huduma za kibiashara, huduma za
dharura na uokoaji, kurahisisha
sensa, kuboresha daftari la wapiga
kura, kuboresha huduma za posta na
kuwezesha utoaji wa biashara mtandao.

Kama kila mlipa kodi tutamfahamu


kwa uhakika anaishi wapi, tutamtoza

Waziri Mkuu aliongeza kuwa katika


nchi nyingi za viwanda na nchi
Inaendelea Uk. 13

Jarida
Nchi
Yetu
2016
Jarida
la la
Nchi
Yetu
2016

13

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 12

zilizoendelea suala la miundombinu


ikiwemo Mfumo wa Anwani za Makazi
na Postikodi ni muhimu na linaeleweka
kwa kila mtu katika kuanzisha, kukuza
na kuendeleza uchumi wa viwanda.
Kwa kutumia mfumo huu, viwanda
viwe vikubwa au vidogo vinatambulika
viko wapi kwa anwani zao za makazi na
hivyo kuweza kupima kirahisi ukuaji
wa viwanda alifafanua Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alisisitiza taasisi zote za
umma na zile za binafsi zianze kutumia
anwani za makazi na postikodi ili
kuchochea kasi ya maendeleo ya
nchi ikiwa ni pamoja na kutumia
katika makusanyo ya mapato.
Waziri Mkuu Majaliwa alisisistiza
wadau wote nchini kuzingatia kuwa

na anwani ni haki ya kila mtu na pia


kupata huduma za msingi kupitia
mfumo huo ni haki ya kila mtu.
Aidha, dhana ya kuwa dunia ni kijiji
inapaswa kuwa chachu ya kupata
huduma zote mahali ulipo, inahitaji
juhudi za makusudi za kuhakikisha
Tanzania imekuwa sehemu ya kijiji
hicho na inakuwa ni moja ya mataifa
kinara wa kutoa huduma mbalimbali
kwa ufanisi kwa kutumia Mfumo
wa Anwani za Makazi na Postikodi.
Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof Makame Mbarawa
alisema kuwa azma na lengo la Serikali
ni kuhakikisha kunakuwepo na
anwani za kitaifa ambazo zitaainisha
makazi na mahali pa kazi au biashara.
Mfumo za anwani za makazi na

Postikodi
utawezesha
kufikiwa
kwa lengo la Serikali la kuwa na
anwani mahususi za kitaifa kwa ajili
ya kufikisha huduma mbalimbali
za uchumi, jamii na biashara kwa
walengwa, alisisitiza Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Balozi wa Anwani za
Makazi Duniani Prof. Anna Tibaijuka
alisema kuwa anajivunia mradi huo
kutekelezwa nchini ambao utasaidia
kuonesha watu mahali wanapoishi
ambapo Tanzania imefanikiwa kuwa
na anwani za makazi nchi nzima
licha ya changamoto ya kuwa na
miji mingi ambayo haijapangwa.

Nuru ya Umeme Vijijini Yabadili


Ndoto na Maisha ya Watu

na mara nyingi kulazimika kuwasha


moto wa kuni ili kupata mwanga.
Tangu Serikali ilipoanzisha Wakala
wa Umeme Vijijini (REA), ndoto za
Bibi Joyce na wakazi wengi wa vijijini
kuwa maisha yao yangebaki yaleyale
ya unyonge linapoingia kazi ghafla
zimeyeyuka. Sasa ni furaha na amani tele.

Miradi ya Umeme imechochea maendeleo maeneo ya vijijini nchini.

Na Daudi Manongi-MAELEZO

aisha ya Bibi Joyce John


wa
kijiji
cha
Msolwa
mkoani Morogoro yalikuwa kama
maisha ya wakazi wengine wa
vijijini hapa nchini: kuishi gizani,
usiku kuwa wa taabu kwa kukosa nishati

Kupitia REA, Serikali imefanya


maajabu vijijini kwa kiwango cha vijana
pia kuanza kuhama kutoka mijini
kwenda vijijini. Ukweli huu unatokana
na takwimu kuonesha kuwa vijiji 4,395
kati ya vijiji 12,268 vya Tanzania Bara
sawa na asilimia 36 vimeshaunganishwa
na huduma ya umeme.
Utekelezaji wa Mradi Kabambe wa
Awamu ya Tatu wa kusambaza nishati
vijijini utakaojumuisha vijiji 7,873 katika
wilaya na mikoa yote ya Tanzania Bara
ambao utatekelezwa kwa kipindi cha
miaka mitano (5) kuanzia mwaka huu
Inaendelea Uk. 14

Jarida la Nchi Yetu 2016

14

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 13

wa fedha 2016/17 ni mwendelezo huo


wa kuwaletea wananchi maendeleo.
Kati ya vijiji hivyo, vijiji 7,697
vitapelekewa umeme wa gridi na vijiji
176 umeme wa nje ya gridi (off-grid)
kutokana na nishati jadidifu kwa kuwa
ndiyo njia pekee ya kuvipelekea umeme
kwa gharama nafuu kwa sasa. Hadi
kufikia sasa jumla ya vijiji 4,395 kati ya
vijiji 12,268 ambayo ni sawa asilimia 36
vimeunganishwa na huduma ya umeme.
Wakati akiahirisha Mkutano wa Tano
wa Bunge la 11 Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe.Kassim Majaliwa alisema vijiji
7,873 vilivyoko katika wilaya na mikoa
yote ya Tanzania Bara vitafikiwa katika
mwaka huu wa fedha wa 2016/17.
Kati ya vijiji hivyo vijiji 7,697
vitapelekewa umeme wa gridi na
vijiji 176 umeme wa nje ya gridi
kutoka na nishati jadidifu (Off-grid)
na Wakala wa Umeme Vijijini-REA.
Akifafanua kuhusu usambazaji wa
umeme wa Gridi ya Taifa, Waziri Mkuu
anasema mradi huo mkubwa chini
ya REA utahusisha kufikisha umeme
katika vijiji ambavyo havijafikiwa na
miundombinu ya umeme wa gridi ili
kuongeza wigo wa usambazaji umeme.
Inakadiriwa kuwa miradi ya kusambaza
umeme wa gridi itagharimu takribani
Shilingi Bilioni 7,000. Kati ya fedha
hizo kiasi cha Shilingi Bilioni 4,000
ni kwa ajili ya kufikisha umeme
kwenye vijiji ambavyo havijafikishiwa
umeme katika mikoa na wilaya zote;
na kiasi cha Shilingi Bilioni 3,000 kwa
ajili ya kusambaza umeme kwenye
maeneo
ambayo
yameshafikiwa
na
miundombinu
ya
umeme.
Utekelezaji wa miradi ya nishati
jadidifu kwa vijiji 176 vilivyo mbali na
gridi utaanza katika Mwaka wa Fedha
2016/17 na itatekelezwa na sekta binafsi
kwa ruzuku kutoka Serikalini kwa
kushirikiana na wabia wa maendeleo.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati


na Madini, Profesa Sospeter anasema
kuwa Serikali imeweka mikakati ya
kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka
2020 kila mwananchi anapata
umeme wa uhakika na kupelekea
uchumi wa nchi kukua kwa kasi.
Na kwa kutambua mchango wa
nishati ya umeme katika ukuaji wa
viwanda nchini Serikali imeweka
mkakati wa kuhakikisha kuwa kasi
ya usambazaji wa umeme vijijini
inaongezek ili ifikapo mwaka 2020
mgawo wa umeme uwe ni historia.
Profesa
Muhongo
aliongeza
kuwa kupitia REA Awamu ya
Pili
wakandarasi
wakitanzania
wameonyesha uwezo mkubwa katika
kusambaza umeme vijijini huku
akiwataka wakandarasi zaidi wenye
vigezo wajitokeze na kuchangamkia
fursa ya kusambaza umeme vijijini
kupita REA Awamu ya Tatu.
Alisema wakati Serikali kupitia REA
ikiendelea na kasi yake ya kusambaza
umeme nchi nzima, TANESCO
inatakiwa kuhakikisha nishati ya
uhakika inapatikana ikiwa ni pamoja na
ubunifu wa vyanzo vipya vya umeme.
Takwimu za REA zinaonesha kuwa
mpaka sasa Serikali imeshatumia
shilingi bilioni 881 katika mradi wa
REA Awamu ya Pili ambayo ni sawa
asilimia 92.1 huku wateja wapya
waliounganishwa waliounganishiwa
umeme kati ya Oktoba, 2015 na
Oktoba, 2016 wakifikia 110,597.
Jumla ya taasisi za elimu 995 (shule
za msingi na sekondari, vyuo vya
elimu) zimeunganishiwa umeme,
Zahanati na Vituo vya Afya 364
vimeunganishiwa umeme, Pampu
za maji 68 ziliunganishiwa umeme
na Jumla ya maeneo ya biashara
915
yameunganishiwa
umeme.
Katika mwaka 2016/17 kupitia Wizara
ya Nishati na Madini Serikali imetenga
Shilingi bilioni 952.25 sawa na asilimia
Jarida la Nchi Yetu 2016

90 ya bajeti yote ya maendeleo


na zilielekezwa katika miradi ya
kimkakati ya nishati, Miradi hiyo ni
pamoja na kupeleka umeme vijijini.
Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea
na jitihada za kuhakikisha upatikanaji
wa umeme kwa maeneo mbalimbali
nchini. Kufuatia jitihada hizo,
kiwango cha upatikanaji wa huduma
ya umeme kimeongezeka kutoka
asilimia 36 mwezi Oktoba, 2015
hadi asilimia 51 mwezi Oktoba,
2016. Ongezeko hilo limetokana
na juhudi za Serikali za kusambaza
umeme nchini kupitia Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) na Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO).
Aidha, jumla ya wateja wapya
234,383 waliunganishiwa umeme
kwa kipindi cha kuanzia Oktoba,
2015 hadi Septemba, 2016 sawa
na ongezeko la asilimia 14.68.
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ni
Taasisi ya Serikali ambayo ilianzishwa
kwa Sheria ya Bunge Na. 8 ya Mwaka 2005
chini ya Wizara ya Nishati na Madini.
Wakala inaratibu shughuli za Mfuko wa
Nishati Vijijini (Rural Energy Fund
REF) chini ya usimamizi wa Bodi ya
Nishati Vijijini (Rural Energy Board
REB). Oktoba 2007 Wakala ilianza
kutekeleza majukumu ya kerasmikama
yalivyoainishwa na Sheria ya Nishati
Vijijini na Majukumu ya Wakala
na Mfuko wa Nishati Vijijini ni
kuwezesha upatikanaji na kuhamasisha
matumizi ya nishati bora vijijini.

15

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Baadhi ya Mafanikio ya Awamu


Tano za Uongozi wa Tanzania
Tangu Uhuru

Na Tiganya Vincent-MAELEZO

Nyerere yalikuwa ni kujenga umoja


wa kitaifa kati ya watu wa makabila
na dini tofauti, na hivyo kudumisha
amani ya muda mrefu tofauti na
hali ya nchi jirani, ari iliyofanya
Tanzania iitwe kisiwa cha amani.

Katika kipindi hicho chote Tanzania


imeongozwa na Marais watano ambao
wamesaidia kuleta mafanikio makubwa
kwenye nyanja za maendeleo ya kijamii,
kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.

Katika kuuhakikishia ulimwengu kuwa


Tanzania inaongozwa kwa utawala
kidemokrasia
wa
kubadilishana
madaraka toka kiongozi mmoja
kwenda mwingine Mwalimu Nyerere
alimkabidhi nchi kwa Mhe. Ali Hassan
Mwinyi kama Rais wa Awamu ya Pili
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
baada ya uchaguzi wa mwaka 1985.

esemba 9, mwaka huu Tanzania


bara inaadhimisha miaka 55 ya
Uhuru ambao ulipatikana mwaka
1961, chini ya uongozi wa Hayati Baba
wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere.

Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya


uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere ilidumu
kwa miaka 24 kuanzia 1961 hadi 1985.
Historia inakiri kwamba enzi za
Mwalimu Nyerere zilikuwa za
kuimarisha uhai wa Taifa la Tanganyika
na baadae Tanzania , kulinda uhuru
wa nchi ambao ulikuwa mchanga
na kuhimiza wananchi kufanya kazi
kwa juhudi na maarifa kwa ajili ya
maendeleo yao na Taifa lao kwa ujumla.
Kazi nyingine kubwa iliyofanywa
na uongozi huu ni kuhakikisha
inasaidia nchini nyingine kudai
Uhuru, kupambana na ukandamizaji
pamoja na ubaguzi wa rangi ulikuwa
ukifanywa
na
wachache
hasa
katika Nchi za Kusini Mwa Afrika.
Mafanikio mengine ya Mwalimu

Chini ya Utawala wa Rais Mstaafu


Mwinyi alifanyia marekebisho misingi
ya itikadi ya Ujamaa na Azimio la Arusha
ili iweze kuendana na mageuzi ya kisiasa
na kiuchumi yaliyokuwa yanakuja
kwa kasi na nguvu kubwa duniani.
Awamu hii ilipokea mageuzi hayo
ya kuanza kuyaweka katika mkakati
wa utekelezaji na hivyo kuongoza
mabadiliko hayo kwa amani na
utulivu kinyume na hofu ya baadhi
ya watu waliodhani kuwa amani na
utulivu wa Tanzania ungevurugika.
Awamu hii ilifungua milango ili kila
anayeweza kuzalisha basi asaidie kazi
ya serikali ya uzalishaji ili chakula na

bidhaa ziwafikie watu wa Taifa letu.


Kidogo kidogo marekebisho ya mfumo
wa uchumi wa nchi hii kutoka uchumi
inaoshikiliwa na dola kwenda kwenye
uchumi huria ambao watu na wadau
mbalimbali ni washiriki katika kufanya
shughuli za uzalishaji na kutoa huduma.
Ni kipindi hiki taifa lilianza kuona
huduma za kijamii zikianza kutolewa
na mashirika yasiyo ya kiserikali,
huduma za ughani katika kilimo,
mifugo na uzalishaji mdogo mdogo
na kipindi ndipo asasi mbalimbali
zilianzishwa na kusajiliwa ili ziisaidie
serikali
katika
kujenga
Taifa.
Hatimaye uongozi wa Awamu ya
Tatu uliokuwa chini ya Rais Mstaafu
Benjamini William Mkapa uliingia
madarakani kuanzia mwaka 1995 hadi
mwaka 2005 ambapo kazi moja kubwa
ilikuwa kuimarisha misingi ya hatua
zilizopigwa na awamu ya pili hasa katika
kuendelea kuupanga na kuuimarisha
uchumi wetu katika mfumo mpya
na kuanza kujibu hoja hizo juu.
Kipindi chake kilikuwa na kazi kubwa
ya marekebisho ya kimfumo na
kitaasisi, wengi wenu mtakumbuka
Tume maarufu ya Parastatal Sector
Reform
Commission
(PSRC)
ambayo ilianzishwa kwa sheria ya
Inaendelea Uk. 16

Jarida la Nchi Yetu 2016

16

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 15

Mashirika ya Umma ya mwaka


1992 na kazi kubwa ilikuwa kufanya
ubinafsishwaji wa mashirika ya umma.
Uongozi wa Awamu hii ulijitadi kuweka
nguvu katika maeneo yafuatayo:
Kuhakikisha kuwa Tanzania inatekeleza
ushauri wa mashirika ya fedha ya
kimataifa kuhusu kufufua uchumi
wa Tanzania uliokuwa umezorota.
Kuweka mikakati madhubuti ya
kuongeza mapato ya Serikali ikiwemo
kuanzisha Kodi ya ongezeko la
thamani (VAT).
Kubinafsisha mashirika ya umma
yaliyokuwa yaendeshwa kwa hasara.
Kuimarisha miundombinu ikiwemo
ujenzi wa barabara mbalimbali hapa
nchini.
Kuvutia wawekezaji katika sekta ya
madini, utalii, kilimo na viwanda.
Kufanyia mabadiliko katika utendaji
Serikalini na uboreshaji wa maslahi ya
watumishi wa umma.
Kuimarisha huduma za afya, maji na
elimu.
Kuimarisha utawala bora na haki za
binadamu hapa nchini.
Mwisho wa Awamu ya Tatu ukawa
mwanzo wa uongozi wa Awamu ya
Nne ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania chini ya Rais Mstaafu Jakaya
Mrisho Kikwete chini ya kauli mbiu ya
ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya
alifanikiwa kuweka msingi imara katika
kutekeleza Mkakati wa Maendeleo
wa Mwaka 2025, ambao unalenga
kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye
uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025.
Uongozi huu uliendelea kuliweka
Taifa katika hali ya Umoja licha ya
changamoto zilizopo na umetoa
mchango mkubwa katika harakati
za kisiasa zilizopelekea vyama
Viwili kutiliana saini maridhiano

na kupata muafaka Mwaka 2010.


Chini ya uongozi wake ulisaidia
kuwepo makubaliano yalipelekea
Zanzibar kufanya uchaguzi kwa amani
na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa
baina ya vyama vya CCM na CUF.
Mafanikio yaliyopatina ni pamoja na
ujenzi wa bomba la gesi kutoka mkoani
Mtwara hadi jijini Dar es salaam, ujenzi
wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
pamoja na Chuo Kikuu cha Afya cha
Muhimbili Kampasi ya Mloganzila
(MUHAS) ambacho ni chuo Kikubwa
cha kuelimisha Madaktari hapa nchini.
Wakati
unaondoka
madarakani
mwaka jana ,Tanzania ilikuwa kati ya
nchi 10 Afrika zinazokua kiuchumi
ambapo katika kipindi cha miaka
kumi pato la taifa limekuwa kwa
asilimia 7 kutokana na sera za uchumi
zinazogusa wananchi wa kawaida.
Pato ghafi la Taifa limeongeza mara tatu
toka trilion 14 .1 mwaka 2005 hadi trilion
79 huku pato la wastani la mwananchi
wa kawaida kwa mwaka limeongozeka
toka shilingi 444,030 hadi 1,724,000.
Awamu ya nne ilikuwa na jukumu la
kuendelea kujitahidi kugawa keki ya
Taifa kama vile ujenzi zaidi wa barabara,
uwekezaji zaidi katika elimu na kilimo.
Kwa upande wa Uongozi wa
Awamu ya Tano ,tangu ulipoingia
madarakani Novemba mwaka jana
chini ya Rais John Pombe Magufuli
umeleta
mafanikio
mengine
ambayo yamegusa nyanja za kisiasa,
kiuchumi, kijamii na kitamaduni.
Maeneo yaliyoanza kushugulikiwa ni:
Kuhakikisha elimu inatolewa bure
kuanzia Shule ya Awali hadi Kidato
cha Nne.
Kudhibiti makusanyo ili kuongeza
mapato ya Serikali.
Kuendelea kuimarisha miundo
mbinu.
Jarida la Nchi Yetu 2016

Kuongeza uwajibikaji kwa watumishi


umma.
Kuanzisha Mahakama ya Mafisadi.
Kuhakiki taarifa za Watumishi wa
umma.
Kuendelea kuimarisha Huduma
za Afya katika Hospitali ya Taifa na
Hospitali nyingine.
Ununuzi wa ndege mbili.
Kila mtu mwenye uwezo wa kufanya
kazi.
Maeneo ili ni pamoja na kuhakikisha
wananfunzi wenye umri wa kuanza
shule za Awali na wale waliochaguliwa
kujiunga na Kidato cha kwanza
wanajiunga kwa gharama za Serikali.
Hali hiyo imesaidia kuwepo na ongezeko
kubwa na wanafunzi wa Shule ya Awali
na Kidato cha Kwanza, jambo lilizalisha
changamoto nyingine ya upungufu wa
madawati ambayo pia Serikali kwa
kushirikiana na wadau wamezitatua.
Kwa upande wabadhirifu , Uongozi
wa Awamu hii umeanza zoezi la
kuwachukuliwa
hatua
ikiwemo
kufukuza kazi na kuwachukulia
hatua wale wote wenye kufanya
kazi kwa mazoea na kutowajibika
ipasavyo maeneo yao ya kazi.
Halikadhalika Serikali hii imejitadi
kuhakikisha
inaongeza
mapato
kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania
ambapo makusanyo ya TRA yamevuka
lengo ambapo kwa sasa inakusanya
wastani wa trilioni 1.1 kwa Mwezi.
Huduma katika sekta ya afya
zimeboreshwa
kutoka
chini
hadi Hospitali ya Taifa ambapo
kumekuwepo na upatikanaji wa dawa.
Suala la usafi limekuwa ajenda ya
kuduma katika maeneo mbalimbali
hapa nchini , hatua iliyosaidia kuamsha
moyo wa wananchi kufanya kazi
katika maeneo yanayowazunguka.

17

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Miaka 55 ya Ujenzi wa

Rais wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akimsikiliza Mtaalam wa mitambo
katika moja ya ziara za kukagua uzalishaji viwandani wakati wa uongozi wake.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi akipata ufafanuzi juu ya namna ya uzalishaji
picha toka kwa aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Raphael Hokororo
(kulia) wakati alipotembelea Idara hiyo wakati wa utawala wake.

Jarida la Nchi Yetu 2016

18

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Tanzania Tunayoitaka

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa (kulia) akiongea na Waandishi wa
habari wakati wa utawala wake.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiwasikiliza mapacha
walioungana wakati wa ziara yake Mkoani Iringa.

Jarida la Nchi Yetu 2016

19

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Miaka 55 ya Ujenzi wa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki zoezi la usafi
eneo la Kivukoni karibu na Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 54
ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Pastoralism and Climate Change
Jijini Dar es Salaam.

Jarida la Nchi Yetu 2016

20

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Tanzania Tunayoitaka

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akiongea na
baadhi ya Watendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake
ya kushtukiza mapema mwaka huu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa pamoja na Watendaji wa Bandari
alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam Septemba 26, 2016.

Jarida la Nchi Yetu 2016

21

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

JPM Atimiza Ahadi ya Kuanzisha


Mahakama ya Mafisadi

Na Eliphace Marwa-MAELEZO

i mwaka mmoja tangu Serikali


ya Awamu ya Tano iingie
madarakani na kutekeleza kwa
vitendo moja ya ahadi alizozitoa
mgombea urais wakati ule, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli ya kuanzisha
Mahakama ya Rushwa na Mafisadi.
Mahakama ambayo imeanza miezi
michache iliyopita inaleta matumaini
kwa Watanzania hasa wanaoipenda
nchi yao wakiwa na uzalendo na fikira
za kiutaifa. Katika ahadi za TANU kabla
na baada ya Uhuru, na baadae kurithiwa
na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
imetamkwa wazi kuwa Rushwa ni adui
wa Haki, Sitapokea wala Kutoa Rushwa.
Rais Magufuli anatekeleza kwa
vitendo anachokiahidi. Leo naomba
nizungumzie utekelezaji wa ahadi
yake ya kuanzishwa kwa mahakama

maalum ya kushughulikia mafisadi


na wahujumu uchumi wa nchi yetu.
Ni dhahiri kuwa Dkt. Magufuli
anafuata nyayo za muasisi wa Taifa
letu, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere ambaye
alithubutu kukemea na kuwaadhibu
viongozi
wote
wala
rushwa.
Mwalimu Nyerere alichukia sana
rushwa na alichukua hatua kali sana kwa
wala rushwa wote bila kujali nyadhifa
zao au uwezo wao wa kifedha kwani
nakumbuka kuna waziri wake mmoja
alihukumiwa kifungo na viboko baada
ya kupatikana na hatia ya kula rushwa .

kupanda farasi wawili kwa wakati mmoja


na alikuwa sahihi kabisa. Kitendo cha
kuruhusu wafanyabiashara kuingia
kwenye siasa, na viongozi kuruhusiwa
kufanya biashara ndio chanzo cha wizi
na ufisadi wa mali na fedha za umma.
Katika hotuba ya kufungua Bunge la
11 mjini Dodoma Novemba 20,2015,
Rais Magufuli jambo moja alilolisitiza
na kulisemea kwa nguvu ni juu ya
ahadi yake wakati wa kampeni ya
mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

Watumishi wa umma, waliohusika


na ufisadi walichukuliwa hatua kali
ikiwa ni pamoja na kufungwa jela na
kufilisiwa mali zao na hiyo ilipunguza
sana rushwa na ufisadi serikalini.

Sikufanya hivyo (kuahidi kupambana


vikali na rushwa) kwasababu nilitaka
tu kuwarubuni wananchi ili wanipe
kura zao na kunifanya kuwa Rais
wao. Nililiongea jambo hili kwa
dhati kabisa, na nilichokisema na
kuwaahidi wananchi ndicho hasa
nilichokikusudia,
alisema
Dkt.
Magufuli.

Mwalimu aliamini kwamba mtu hawezi

Ni kweli kuwa wananchi wanachukia


Inaendelea Uk. 22

Jarida la Nchi Yetu 2016

22

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 21

sana
rushwa
na
ufisadi,
na
wamechoshwa na vitendo hivyo na hata
yeye pia anachukia rushwa na ufisadi
na wala hafurahishwi kabisa na vitendo
vya rushwa na ufisadi vinavyoendelea
hapa nchini kwani vitendo hivyo
vinawanyima haki wananchi na kuitia
hasara serikali kwa mamilioni ya fedha
ambazo zingeweza kutumika kwa
ajili ya kujenga miradi ya maendeleo.
Rais Magufuli aliongeza kuwa chama
chake, CCM, kimejengwa katika
misingi ya kukataa rushwa na ufisadi
na ndiyo maana moja ya imani kuu za
CCM ni ile isemayo, Rushwa ni adui
wa haki, sitatoa wala kupokea rushwa
na hivyo Mtanzania mwaminifu kwa
imani yake hatakuwa na kigugumizi
katika kuwa mstari wa mbele katika
kupambana na rushwa na ufisadi.
Rais Magufuli alimnukuu Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
kuwa aliwahi kuifananisha rushwa na
ufisadi Kama Adui Mkubwa wa Watu.
Akiongea Bungeni Mei 1960, Mwalimu
Nyerere alisema yafuatayo kuhusu
rushwa, Rushwa [na ufisadi] havina
budi kushughulikiwa bila huruma
kwa sababu naamini wakati wa amani
rushwa na ufisadi ni adui mkubwa
kwa ustawi wa watu kuliko vita.
Haya ni maneno makali ya mtu na
kiongozi aliyeichukia na kuikemea
rushwa katika maisha yake yote ya
uongozi. Ni maneno yanayotukumbusha
tu nini kinaweza kikatutokea kama
taifa endapo tutaendekeza rushwa
na ufisadi. Chuki za wananchi dhidi
ya rushwa na ufisadi ni dhahiri.
Akidhamiria vikali kuendeleza ahadi
ya Mwalimu na kuendeleza pale
walipoishia watangulizi wake, Rais
Magufuli aliliambia Bunge katika
hotuba yake ya ufunguzi akisisitiza:
Nimewaahidi wananchi, na nataka
niirejee ahadi yangu kwao mbele
ya Bunge lako tukufu, kwamba
nitapambana na rushwa na ufisadi bila
kigugumizi na bila haya yoyote na dawa

ya jipu ni kulitumbua, na mimi nimejipa


kazi ya kuwa mtumbua majipu.
Najua
kutumbua
jipu
kuna
maumivu lakini bahati mbaya halina
dawa nyingine, hivyo ninaomba
Waheshimiwa Wabunge na Watanzania
wote mniombee na mniunge mkono
wakati natumbua majipu haya.
Aidha, katika siku ya kilele cha Wiki ya
Mwaka Mpya wa Mahakama Jijini Dar
es Salaam mapema mwaka huu, Rais
Magufuli alimtakia Jaji Mkuu, Othman
Chande kutosubiri Bunge kupitisha
Sheria ya Uanzishwaji wa Mahakama ya
Mafisadi, badala yake mahakama hiyo
ianze kufanya kazi haraka iwezekanavyo.
Alisema kuchelewesha kuanza kwa
mahakama hiyo kunatoa mwanya
kwa mafisadi kuendelea kuangamiza
nchi na kuifanya kuwa masikini
wakati ina rasilimali za kutosha
ambazo zinaweza kuiendesha nchi
bila kutegemea fedha za wafadhili.
Rais Magufuli
wa uanzishwaji
ambayo alitaka
ya mahakama
Mahakama za

alisisitiza umuhimu
wa mahakama hiyo
ifanye kazi ndani
kuu kama zilivyo
Ardhi na Biashara.

Hatimaye
ahadi
hii
imekuwa
kweli, tamko la kuanza kazi kwa
Mahakama hiyo lilitolewa bungeni
na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
wakati akiwasilisha makadirio ya
mapato na matumizi ya Ofisi yake.
Kuhusu
ahadi
ya
kuanzisha
Mahakama Maalum ya Ufisadi napenda
kuliarifu Bunge lako kwamba, Serikali
imeanzisha Divisheni ya Mahakama ya
Rushwa na Ufisadi katika Mahakama
Kuu itakayoanza kufanya kazi
mwezi Julai 2016, alisema Majaliwa.
Aidha,
Waziri
Mkuu
alisema
pia Serikali itaimarisha Ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashtaka na Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili
kwa pamoja ziweze kuharakisha utoaji
wa haki kwa kesi zitakazofikishwa
kwenye
mahakama
hiyo.

Aidha, ahadi hiyo nayo imetimia


ambapo Juni, 24, 2016 Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania lilipitisha
kwa kauli moja Sheria ya Marekebisho
Mbalimbali, ambayo pamoja na mambo
mengine, yamempa Jaji Mkuu mamlaka
ya kuanzisha Divisheni ya Rushwa na
Uhujumu Uchumi ya Mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa muswada huo
uliowasilishwa
na
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, George Masaju,
adhabu kwa watakaokutwa na hatia
zimeongezwa,
huku
mahakama
hiyo ikiwekewa mazingira wezeshi
ili iendeshe kesi hizo kwa haraka.
Divisheni Maalumu ya Mahakama Kuu,
itakuwa na majaji pamoja na watumishi
wengine, ambao wanahusika moja kwa
moja na kesi za rushwa na uhujumu
uchumi tu, hatua hii itawezesha kesi
za makosa ya rushwa na uhujumu
uchumi kusikilizwa kwa urahisi,
ufanisi na kwa haraka, alisema Masaju
wakati alipokuwa akisoma muswada
huo kabla ya kupitishwa na Bunge.
Hatua hiyo ya kuwa na majaji maalumu
na wafanyakazi wake, Masaju alisema
imelenga kuondoa udhaifu uliojitokeza
wakati wa kushughulikia kesi za
rushwa na uhujumu uchumi, kwa
kuwa majaji waliokuwa wakisikiliza
mashauri hayo, walikuwa hao hao
wanaosikiliza
mashauri
mengine
ya jinai, madai, katiba na mengine
yanayofunguliwa Mahakama Kuu.
Aidha
Masaju
aliongeza
kuwaMazingira mengine wezeshi
yanayotengenezwa na sheria hiyo
kwa divisheni hiyo, ni thamani ya
fedha inayohusishwa na makosa
hayo, kuwa inaanzia Sh bilioni moja.
Inapendekezwa kuwa pale makosa
ya rushwa na uhujumu uchumi
yanapohusisha thamani ya fedha, basi
makosa yatakayofunguliwa katika
Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa
na Uhujumu Uchumi, yawe ni yale
ambayo thamani yake haipungui
Inaendelea Uk. 23

Jarida la Nchi Yetu 2016

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

23
Inatoka Uk. 22

Muonekano wa sehemu ya jengo la Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Sh bilioni moja, alisema Masaju.


Lengo la kuweka thamani hiyo ya
fedha, limeelezwa kuwa ni kuiwezesha
divisheni hiyo kujikita kusikiliza
makosa makubwa ya rushwa na
uhujumu uchumi, ili makosa madogo
yasiyofikia thamani hiyo, yasikilizwe
na mahakama za wilaya, mahakama
za hakimu mkazi na Mahakama Kuu.
Hata hivyo, divisheni hiyo pia kwa
mujibu wa sheria hiyo itasikiliza
makosa mengine ya rushwa na
uhujumu uchumi bila kujali thamani
ya fedha, kutokana na namna makosa
hayo yalivyotendeka, asili yake na
ugumu wa kuyawekea thamani ya fedha.
Marekebisho
mengine
yaliyopendekezwa ni pamoja na
makosa ya rushwa na uhujumu uchumi
chini ya sheria hii iwe ni kifungo cha
gerezani, kisichopungua miaka 20
na kisichozidi miaka 30 au vyote kwa
pamoja na hatua nyingine za kijinai,
ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali
zilizopatikana kutokana na makosa
hayo.
Kifungo
hicho
kimeongezwa
kutoka katika sheria ya sasa ambayo
ndiyo
inayorekebishwa,
ambayo

ilitaka kifungo kisizidi miaka 15.


Kwa mujibu wa Masaju, maneno hayo
kifungo kisichozidi miaka 15, yaliipa
Mahakama mamlaka ya kutoa adhabu
ndogo zaidi, ilimradi tu adhabu hiyo
haizidi miaka 15, jambo lililoonekana
kuwa baadhi ya adhabu zilikuwa
ndogo kuliko uzito wa makosa.
Katika kutaifisha mali za waliokutwa
na hatia, sheria hiyo imeweka
masharti ya kuzuia kutumika kwa
sheria zinazohusu ufilisi au uamuzi
wa kufilisi kampuni, kwa mali
ambayo inachunguzwa chini ya Sheria
ya Makosa ya Uhujumu Uchumi.
Marekebisho
hayo
yanalenga
kukabili vitendo vya watu au kampuni
kujifilisisha
wakati
uchunguzi
unapoanza dhidi yao na pia kuhakikisha
kuwa mali zote zinazohusika na kosa
linalochunguzwa, au linaloendelea
mahakamani, inaendelea kuwepo
hadi uchunguzi au kesi husika
itakapohitimishwa, alisema Masaju.
Aliongeza: Kwa ujumla hatua hii ni njia
mojawapo ya kuwafanya watu waogope
kutenda makosa ya rushwa na uhujumu
uchumi na pia kuhakikisha kuwa
mhalifu, hanufaiki na uhalifu alioutenda
Jarida la Nchi Yetu 2016

kwa kutaifisha mali zilizopatikana


kwa njia ya rushwa, ufisadi na
uhujumu uchumi, alisema Masaju.
Mahakama hiyo hatimaye imeshaanza
kazi kwa kuanza kusikiliza kesi
ikitumia eneo tulivu lililotengwa
kwenye majengo ya Shule Kuu ya
Sheria (LaW School) ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaa. Mahakama hii ni
mwendelezo wa kasi ya aina yake kwa
Serikali kutekeleza ambayo iliyaahidi.

Najua kutumbua
jipu kuna maumivu
lakini bahati mbaya
halina dawa nyingine,
hivyo ninaomba
Waheshimiwa
Wabunge na
Watanzania wote
mniombee na
mniunge mkono
wakati natumbua
majipu haya.
-JPM-

24

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Miaka 55 ya Uhuru; Ubora wa


Elimu Nyerere hadi Magufuli
Na Judith Mhina-MAELEZO

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Buhigwe katika Halmashauri ya Buhigwe Kigoma wakipalilia shamba la Kahawa
katika kutekeleza elimu ya kujitegemea.

akati
Watanzania
wakiadhimisha
miaka
55
ya Uhuru, Rais wa Awamu ya
Tano, Dkt. John Pombe Magufuli
ameweka juhudi katika Kuinua
ubora na usawa wa elimu Tanzania.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Kassim Majaliwa katika kutekeleza
Sera za Kuinua Elimu na kutambua
jukumu la kuhakikisha kila raia wa
Tanzania anapata elimu ambayo ni
haki ya kikatiba Serikali imetenga
bilioni 137 kama ruzuku kwa shule
za Serikali za Msingi na Sekondari.

Ruzuku hii ni kwa ajili ya uendeshaji


wa shule ambapo kila mwanafunzi
anapatiwa shilingi 10,000 kwa
shule za msingi na Sh 25,000 kwa
shule za sekondari kwa mwaka.
Pia, itatoa Sh 1,500 kwa siku
kwa mwanafunzi kwa shule za
Msingi na Sekondari kwa ajili ya
chakula kwa wanafunzi wanaokaa
bweni,
anasema
Simbachawene.
Fedha
hizo
zimegawanywa
kwenye Shule za Serikali za
Msingi 16,394 na Sekondari 3682
kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu na fedha hizo zimeanza

kutumika

kuanzia

Januari

2016.

Aidha, ili kutekeleza Sera ya Kuinua


elimu, Serikali imetoa ruzuku ya
shilingi bilioni 36 kwa mwaka maalum
kwa Shule za Msingi, chini ya Mpango
wa Kuinua Elimu Tanzania, EQUIP-T
katika Halmashauri 53 za Mikoa
7 Dodoma, Lindi, Kigoma, Mara,
Simiyu, Shinyanga na Tabora yenye
jumla ya shule 5430 walimu 20,000 na
wanafunzi 2.3 milioni wa madarasa
ya awali mpaka darasa la tatu.
Serikali imechukua uamuzi huo
baada ya kuona kiwango cha elimu
kinazidi kudidimia zaidi katika Mikoa
Inaendelea Uk. 25

Jarida la Nchi Yetu 2016

25

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Inatoka Uk. 24

7 iliyopata wastani usioridhisha na


kushika mkia mfulululizo tangu mwaka
2000 hadi Mpango ulipoanzishwa 2014.
Juhudi hizi za Rais wa Awamu ya
Tano, katika kumuunga mkono Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
ambae elimu aliyoitoa ilikuwa inakidhi
haja ya mazingira ya Kitanzania
na ubora ulitolewa kwa usawa kwa
wanafunzi wote bila kubagua kipato,
kabila, rangi au sehemu anayotoka.
Pia, kwa kutambua mawazo ya
Mwalimu Nyerere, mdau wa elimu
EQUIPT ameona ni sahihi kujenga
msingi mzuri wa kuinua ubora wa elimu
na ni vyema kuanza na Shule za Msingi.
Kupitia mradi wa EQUIP ili kufikia
lengo la elimu ya kujitegemea kila
shule katika Mikoa iliyochaguliwa
imeandaa mchanganuo wa biashara
(Business Plan) wa Elimu ya
Kujitegemea na ile itakayoonekana
inakidhi vigezo, kati ya shule 4,530
nusu ya hizo shule ambapo ni 2,715
zitapewa ruzuku ya shilingi milioni
1.5, ikiwa ni miradi inayoanza au ile
ya elimu ya Kujitegemea inayoendelea.
Tayari
hali
hii
imeshaonesha
matunda mbapo miradi ya Elimu ya
Kujitegemea inatekelezwa vema katika
Shule za Msingi 88 za Serikali zilizopo
Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe
ambayo imejikita katika miradi ya
kilimo, mifugo, misitu. mazingira,
utengenezaji wa matofali na uchomaji
na maduka ya vifaa vya elimu.
Pamoja na masuala ya Elimu
ya
Kujitegemea,
Mpango
wa
EQUIP-T umetoa vitini 13 vya
mafunzo ya kuboresha ufundishaji,
vitabu vya hadithi vya darasa la
awali hadi darasa la tatu 25,000,
vitabu vya ziada na kiada 417,852.
Kuwapatia Waratibu Elimu Kata
pikipiki 1,000 za kurahisisha ukaguzi
wa shule, vishikwambi (Ipad) 5,853
ambazo zitaboresha mifumo ya
ukusanyaji, utumiaji na utoaji wa taarifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe


Magufuli akiwa na baadhi ya Wanafunzi wa shule za Msingi wakati wa
sherehe ya kukabidhiwa madawati kutoka Ofisi ya Bunge
Jijini Dar es Salaam

za sekta ya elimu kuanzia ngazi ya kijiji,


shule kata, Tarafa, Wilaya mpaka Taifa.
Ili kuboresha utoaji wa taarifa
EQUIP-T imetoa mbao za matangazo
katika shule 4,000 ili wazazi na jamii
wapate matangazo mbalimbali ya shule
hususani mapato na matumizi ya fedha
na kuweka matokeo ya darasa la 4 na la 7.
Vilevile,
kuweka
vipaumbele
vya shule, matukio, taarifa na
shughuli za wanafunzi. Mpango
huu pia kupitia Halmashauri hizo
53 ambazo zilipokea ruzuku ya
ushirikiano wa wazazi na walimu ya
shilingi bilioni 2.5 katika Mikoa 7.
Mpango pia umewatambua vijana
waliomaliza shule za Sekondari na wapo
vijijini kwa kuwahusisha katika kuandaa
na kufundisha madarasa ya utayari
takribani 234 katika Mikoa 7 ambayo
ni nje ya utaratibu wa shule za Msingi.
walimu
wakujitolea
wamepatiwa
simu za mkononi na kulipwa posho
kidogo ya muda wa maongezi.
Katika kutekeleza majukumu yao,
Wadau wa EQUIP wamezingatia falsafa
ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.
Nyerere ya kuwa na usawa na ubora
wa Elimu aliojengwa katika jamii.
Kwa kuzingatia umuhimu wa elimu
katika jamii, EQUIP Tanzania
Jarida la Nchi Yetu 2016

wamekuja na mpango wa ushirikiano


wa Wazazi na Waalimu-UWW ili
kurudisha moyo wa jamii katika
kutumikia shule zinazowazunguka
kuona ni sehemu ya maisha yao kwani
wanafunzi wanapata malezi mema
kutoka kwa wazazi na walimu husika.
Kipindi cha Mwalimu Nyerere, shule
zilipokea idadi ndogo ya wanafunzi
waliotakiwa kujiunga na shule, japo
changamoto zilikuwa nyingi kutokana
na uchache wa shule, umbali na
dhana nzima ya elimu kutopewa
kipaumbele na wazazi wa enzi hizo.
Mwalimu alitoa fursa ya elimu kwa
rika zote, jinsia zote, kabila zote
pamoja na dini zote katika kutekeleza
falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea
iliyoasisiwa na Azimio la Arusha.
Kwa
kuzingatia
umuhimu
wa
elimu, Serikali ya Awamu ya
Tano imeamua kurejesha kuamua
kurejesha ruzuku ili kuinua kiwango
cha elimu na usawa katika shule
za serikali za msingi na Sekondari.
Pamoja na mafanikio hayo, bado
ziko
changamoto
zinazoikabili
sekta ya elimu Tanzania, hivyo
rai inatolewa kwa wadau wote wa
elimu kuunga mkono juhudi za Rais
Dkt. John Pombe Magufuli katika
kufufua ubora wa elimu nchini.

26

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Jeshi la Magereza Laanzisha Shirika la


Uzalishaji Mali.
Naamini uwekezaji huu wa Kiwanda
kipya cha Viatu cha Karanga ni ishara
tosha ya kuunga mkono dhamira ya
dhati ya Rais wetu Dkt. John Pombe
Magufuli ya kutaka Tanzania mpya ya
Viwanda inawezekana, hivyo kutimiza
malengo na Dira ya Taifa ya Uchumi
wa Viwanda ifikapo mwaka 2025.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi


Hamad Masauni akiangalia moja kiatu kinachotengenezwa na Jeshi la
Magereza katika Gereza Karanga Mkoani Kilimanjaro.

Na Eliphace Marwa-MAELEZO

angu Jeshi la Magereza lianzishwe


nchini mwaka 1962 watu wengi
wanaamini
kwamba,
wafungwa
wanapokuwa gerezani hutumikishwa
kwa kazi nyingi na ngumu ili
wanaporudi nyumbani baada ya
kutumikia kifungo wajutie makosa
waliyofanya na hivyo kutorudia.
Kwa mujibu wa aliyekuwa Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini John Minja,
jukumu la msingi la Jeshi la Magereza
ni kuwapokea na kuwahifadhi gerezani
watu wote wanaopelekwa kwa mujibu
wa sheria za nchi baada ya kupatikana na
makosa mbalimbali. Wakiwa gerezani
wafungwa hao kufanya kazi mbalimbali
kulingana na utaratibu uliowekwa kwa
lengo la kuwajengea uwezo ili hatimaye
watoke gerezani wakiwa raia wema.
Ili kuboresha utendaji wake wa kazi,
mwaka 1983 Jeshi la Magereza kwa
Sheria ya Bunge namba 23 ya mwaka
1974 (the Corporation Sole Act No.
23/1974) chini ya kifungu cha 3(1) na
kanuni zake za mwaka 1983 lilianzisha
Shirika (Shirika la Magereza) kwa
lengo la kuwajengea uwezo wafungwa
kwa kuwapa elimu ya ujuzi mbalimbali

ili
wakitoka
wakautumie
kwa
manufaa yao na Taifa kwa ujumla.
Kwa kuwatumia Wataalamu wake
ambao ni askari walioajiriwa wakiwa
na ujuzi katika fani mbalimbali,
Shirika la Magereza limeweza kupata
mafanikio makubwa sio tu katika
kuwafundisha wafungwa ujuzi huo
bali pia limekuwa likifanya kazi
mbalimbali za mikataba za wateja wake.
Katika kuunga mkono dhamira ya
Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya
nchi ya viwanda, Jeshi la Magereza
kupitia Shirika lake limeingia Mkataba
wa Uwekezaji na Mfuko wa Pensheni
wa Mashirika ya Umma (PPF) katika
Mradi wa kiwanda cha viatu cha
Gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na Maafisa Waandamizi
wa Jeshi la Magereza pamoja na
Wanahabari,
Kamishna
Jenerali
John Minja amesema Mkataba huo
utaliwezesha Jeshi la Magerezeza
kuimarika zaidi kiutendaji wa shughuli
za kibiashara sio tu na PPf bali pia na
Taasisi nyingine za Serikali, Umma na
watu binafsi. Vile vile, hiyo ni nafasi pekee
kwa Jeshi hilo kuweza kuchangamkia
fursa mbalimbali za kibiashara.
Jarida la Nchi Yetu 2016

Alisema Kamanda Minja. Amesema,


hadi sasa Shirika la Magereza lina
jumla ya Miradi 23, kati ya hiyo
miradi 15 ni ya kilimo na mifugo na
8 ni ya viwanda vidogo vidogo. Pia
zipo shughuli za miradi ya Kikosi cha
Ujenzi inayosimamiwa na Shirika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko wa Jamii wa PPF, Bw. William
Erio amesema kuwa PPF ipo tayari
kushirikiana na Shirika la Magereza
katika mradi huo wa ujenzi wa Kiwanda
cha Viatu kwani yapo mahitaji makubwa
ya bidhaa hiyo ya ngozi hapa nchini.
Makubaliano haya yanahusisha ujenzi
wa Kiwanda kipya cha viatu pamoja
na uwekezaji wa mashine za kisasa
za kutengenezea bidhaa mbalimbali
za ngozi. Aidha, uwekezaji huo
utawezesha vyombo vyote vya Ulinzi
na Usalama nchini kununua sare za
viatu na vifaa vingine vya bidhaa
za ngozi zitakazozalishwa katika
Kiwanda hicho badala ya kuagiza nje
ya nchi. Alisema Kamanda. Erio.
Ili kuleta ufanisi wa kiwanda hicho
Kamanda Erio ameeleza kuwa tayari
Jeshi la Magereza limewapeleka
wataalamu wake nchini China kwa
ajili ya kufanya upembuzi wa mashine
za kisasa zitakazotumika kuongeza
uwezo wa viwanda vyake vya
kutengeneza bidhaa mbalimbali nchini.

27

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Uhakiki wa Taarifa za Watumishi


wa Umma ni Kazi Endelevu.
Na Florence Lawrence-Utumishi

oezi la kusafisha taarifa za


kiutumishi na kuondoa wale
wasiostahili kuwepo katika orodha
ya malipo ya Serikali-payroll, ni kazi
endelevu kwa kila mwajiri hapa nchini.
Kuanzia mwezi Machi, 2016 hadi
mwezi Septemba,
2016 jumla
ya Watumishi wa Umma 17,667
walioondolewa katika orodha ya malipo
ya mshahara ya Watumishi wa Umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya RaisMenejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Mhe. Angellah
J. Kairuki, Mb, alisema hayo hivi
karibuni ambapo jumla ya shilingi
17,573,720,033/= ziliokolewa endapo
watumishi
hao
walioondolewa
wangeendelea kuwepo katika mfumo
wa malipo ya mshahara Serikalini.
Waziri Kairuki aliainisha kuwa, hadi
kufikia tarehe 20 Agosti, 2016 jumla
ya watumishi 839 walifikishwa Jeshi la
Polisi na TAKUKURU ili kutoa maelezo
na uchunguzi unaendelea hatimaye
hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa
kulingana wa ushahidi utakaopatikana
kwa
waliozembea
katika
kazi.
Lengo la Serikali ni kuhakikisha
kwamba fedha zote zilizolipwa kwa
watumishi wasiostahili zinarejeshwa
Serikalini, alisema Mhe. Kairuki.
Aliongeza
kuwa
tatizo
hilo
limesababishwa na kukosekana kwa
uwajibikaji kwa baadhi ya Waajiri
katika usimamizi wa malipo ya
mshahara ambako kumesababisha
maafisa wazembe na wasio waadilifu
kutotimiza wajibu wao ipasavyo.
Kutowajibika huko ni pamoja na
kutokusafisha (kufanya mabadiliko

na takwimu) ya Taarifa za
Kiutumishi za watumishi
kwa wakati kushindwa
kuwaondoa
kwenye
mfumo watumishi ambao
utumishi wao umekoma;
kubadilisha
akaunti
za
Benki za watumishi ambao
utumishi wao umekoma na
kuelekeza mishahara hiyo
iende kwenye akaunti za
Maafisa
Utumishi/Tawala
ambao wanatumia mfumo.
Mambo mengine ni baadhi
ya waajiri kuelekeza Benki
kusimamisha mishahara ya
watumishi ambao utumishi
wao
umekoma
badala
ya
kuwaondoa
kwenye
mfumo na mtumishi kuwa na zaidi
ya cheki namba moja kutokana na
kudanganya majina yake au tarehe za
kuzaliwa au kwa watumishi wawili
kutumia cheti kimoja na hatimaye
kupewa
cheki
namba
tofauti.
Wakati huo huo Katibu Mkuu, Ofisi
ya Rais-Menejimenti ya Utumishi
wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro
alisema toka Serikali ilipoelekeza
kuondoa watumishi wasiostahili katika
orodha ya malipo mweiz Machi, 2016
zimekuwepo hatua mbalimbali za
kuhakiki Watumishi wa Umma kwa
madhumuni ya kubaini watumishi hewa
na kuimarisha usimamizi na wajibikaji.
Dkt. Ndumbaro alisema lengo la
Serikali kufanya zoezi hilo ni kupata
idadi ya Watumishi ambao wanalipwa
mshahara ili kutoa huduma kwa
wananchi, kukuza uwajibikaji katika
eneo la usimamizi wa malipo ya
mshahara,
kuwaondoa
kwenye
Mfumo wa Malipo ya Mshahara
watumishi wasiostahili na kukusanya

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti


ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Angellah Kairuki

ushahidi wa kuwachukulia hatua wale


wote watakaobainika kusababisha
kuwepo kwa watumishi hewa.
Mtumishi hewa maana yake ni nini?
Mtumishi hewa ni yule ambaye
utumishi wake umekoma tarehe
fulani kutokana sababu mbalimbali
mfano; kustaafu, kufariki, kuacha kazi,
kuachishwa kazi, kufukuzwa kazi,
au kuwa kwenye likizo bila malipo,
lakini mwajiri kuendelea kumwacha
mtumishi huyo kwenye orodha ya
mshahara ya Watumishi wa Umma
(payroll) hivyo kupokea mshahara
ambao haufanyii kazi na hastahili.
Kila Mwajiri hapa nchini anaowajibu
wa kumwondoa mara moja Mtumishi
asiyestahili kuwepo katika orodha ya
malipo. Mfumo wa Taarifa Shirikishi
za Kiutumishi na Mshahara (HCMIS)
umefungwa kwa kila mwajiri, pia mwajiri
ndiye anayetunza kumbukumbu za
Inaendelea Uk. 28

Jarida la Nchi Yetu 2016

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na


Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

28
Inatoka Uk. 27

kiutumishi na mshahara za Watumishi


walio chini yake, hivyo jambo hili
linampa wajibu wa kumwondoa
kwenye mfumo mara moja mtumishi
ambaye utumishi wake umekoma.
Kwa maana nyingine ni kwamba
kazi ya kuwaondoa kwenye mfumo
watumishi ambao utumishi wao
umekoma lipo mikononi mwa
waajiri na sio mahali pengine.
Malipo ya mshahara ya Watumishi
wa Umma hulipwa kupitia Mfumo
Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na
Mshahara (HCMIS). Hivyo, Mfumo
huu umepelekwa kwa waajiri wote
ambao ni Wizara, Idara za Serikali
zinazojitegemea,
Sekretarieti
za
Mikoa, Halmashauri za Serikali za
Mitaa, Wakala za Serikali, Taasisi za
Umma, Hospitali za Mashirika ya Hiari
(VAH) ambapo jumla ya Waajiri 409
wameunganishwa kwenye mfumo huo.
Mfumo

wa

HCMIS

unatumika

kuimarisha taarifa za kiutumishi kwa


waajiri kuwa na taarifa sahihi kuhusu
Watumishi, namna wanavyolipwa
mshahara na wakati huohuo kutumia
taarifa hizo katika kupanga mipango
ya sasa na baadaye ya matumizi bora
ya Rasilimali watu na mshahara.
Pamoja na hilo, HCIMS hutumika
kukuza uwajibikaji katika eneo
la usimamizi wa rasilimali watu
na malipo ya mshahara ikiwemo;
Watumishi wapya kuingizwa kwenye
orodha ya malipo ya mshahara ya
Serikali kwa wakati, kuhakikisha
wanalipwa mshahara sahihi kulingana
na vyeo vyao na kuhakikisha
wanaondolewa kwenye orodha ya
malipo ya mshahara kwa wakati
pindi utumishi wao utakapokoma
kutokana na sababu mbalimbali.
Kazi
nyingine
ni
kuharakisha
utekelezaji wa maamuzi mbalimbali
ya
kiutumishi
pale
mtumishi
anapopandishwa cheo kuhamishwa,

kusimamishwa kazi au kupewa likizo


bila malipo, kufukuzwa kazi au kufariki.
Hatua hii inalenga pia kuipunguzia
Serikali mzigo mkubwa wa madai ya
malimbikizo ya mshahara ya muda
mrefu na ambayo yalikuwa yanazua
malalamiko mengi na kupunguza
gharama za uendeshaji wa shughuli
za Serikali kwa kuwa fedha ambazo
zingetumika kwa ajili ya safari
kama mafuta ya magari, posho za
maafisa na gharama za vifaa vya
uchapishaji sasa zitatumiwa katika
shughuli nyingine za maendeleo.
Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala
Bora miongoni mwa majukumu
yake ni kuandaa na kusimamia
utekelezaji wa Sera za Usimamizi wa
Rasilimaliwatu katika Utumishi wa
Umma; Taratibu, Miundo na Mifumo
ya Utoaji Huduma; na Uendelezaji
Rasilimaliwatu. Ofisi hii pia husimamia
maadili ya Watumishi wa Umma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati), Makamu wa Rais, Mhe. Samia
Suluhu Hassan (kushoto), Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Viongozi wengine wa Serikali wakiwa
katika sherehe za Mei Mosi Kitaifa Mkoani Dodoma mwaka 2016.

Jarida la Nchi Yetu 2016

Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi


na Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo Yetu

Baba wa Taifa akienzi utamaduni kwa kupiga ngoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Waziri
Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi wakipiga ngoma wakati wa ukaribisho Ikulu Jijini Dar es Salaam.

@TZ_MsemajiMkuu

Msemaji Mkuu wa Serikali

www.tanzania.go.tz

Tanzania Official Blog

You might also like