You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA

TELEGRAMS: POLISI,
TELEPHONE: 2500712
Fax: 2502310
E-mail: mwapol@yahoo.com
rpc.mwanza@tpf.go.tz

OFISI YA
KAMANDA WA POLISI,
MKOA WA MWANZA,
S.L.P. 120,
MWANZA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA


VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 10.01.2016

MWANAMKE MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA


KUTUPA MTOTO BAADA YA KUJIFUNGUA.

KWAMBA TAREHE 09.01.2016 MAJIRA YA SAA 16:00HRS JIONI KATIKA ENEO LA


BUTUJA A KATA YA PASIANSI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA,
MWANAMKE MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA EVELINE JOHN MIAKA 24,
MKURYA, MKAZI WA BUTUJA, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA
KUMTUPA MTOTO WAKE MCHANGA KATIKA ZIWA VICTORIA MWENYE JINSIA YA
KIUME, UMRI WA SIKU MOJA MARA BAADA YA KUJIFUNGUA KITENDO AMBACHO
NI KOSA LA JINAI.
KICHANGA HUYO ALIOKOTWA NA WANANCHI KATIKA ZIWA VICTOIRIA AKIWA
AMEFARIKI DUNIA, WANANCHI WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO
HILO NDIPO ASKARI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUFANYA UPELELEZI NA
KUFANIKIWA KUMKAMATA MWANAMKE TAJWA HAPO JUU AMBAYE ALIKIRI
KUHUSIKA KATIKA TUKIO HILO, AIDHA CHANZO CHA UKATILI HUO WA KUTUPA
MTOTO ULIOPEKEA HADI KUFARIKI DUNIA BADO HAKIJA FAHAMIKA.
JESHI LA POLISI LIPO KATIKA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA, PINDI UCHUNGUZI
UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA KICHANGA HICHO
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE KWA AJILI YA
UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA
MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED
MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA
AKIWATAKA KUWA KARIBU NA WA MAMA WAJAWAZITO PINDI WANAPOKUWA
WANAHITAJI KUSAIDIWA ILI KUWEZA KUEPUSHA MATATIZO AMBAYO YANAWEZA
KUEPUKIKA, AIDHA ALIONGEZA KUWA ENDAPO IKIBAINIKA MTU ANATENDA
TUKIO LA AINA KAMA HII KWA NIA OVU HATUA STAHIKI ZA KISHERIA
ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

You might also like