You are on page 1of 103

SHAIRI : SHEMU LAKE

Alitaka niwe wake, alinivuruga bwana

Kwa hivi vituko vyake, limvumilia sana

Nipoze ashki yake, lengo lake niliona

Samahani shemu lake, ila kwa hili hapana.

Kanifanyia vioja, nikaepuka mitego

Tasikia shemu ngoja, chumbani fata mzigo

Yungali na kanga moja, lawama hizi si ndogo

Samahani shemu lake, ila kwa hili hapana.

Kaka aliposafiri, hapo kazidi ukali

Vazi lake la hariri, ananiwinda rijali

Shemeji hajistiri, anataka mema kweli

Samahani shemu lake, ila kwa hili hapana.

Nia anidhoofishe, nguo fupi zimbane

Na kisha ajipitishe, nyuma palivyo panene

Maumbile atingishe, limradi nimuone

Samahani shemu lake, ila kwa hili hapana.

Nimeona niondoke, kuyaepuka majanga

Aheri nieleweke, ndugu yangu namtenga

Kuliko siku ifike, aje niua kwa panga

Samahani shemu lake, ila kwa hili hapana.


HONGERA

Naanza kwa shukrani, zile ziso na kifani

Kwa jina lake manani, shairi natia shani

Mbora ni subiani, muumba vya duniani

Vya mbingu na aridhini, na viumbe baharini.

Hayawi hayawi kuwa, wengi wameyaongea

Leo ameruzukiwa, mola amemtengea

Mwenzetu kajaaliwa, polepole ajongea

Dada leo kaolewa, watabaki kuongea.

Kijana kadhamiria, kumfata dada yetu

Maneno akamwambia, yanomsibu mwenzetu

Kuwa anamzimia, ataka kuposa kwetu

Nasi tumemridhia, aje kuwa mkwe wetu.

Kamwambia mahamumu, niweke moyoni mwako

Mahaba yako matamu, nami ni liwazo lako

Vile ukitabasamu, nafarijika mwenzako

Kinonizidisha hamu, ni huo urembo wako.

Mungu kaumba wazuri, wakila aina wako

Tena wengi mashuhuri, ila huko mie siko

Kila nitafakuri, hakuna mithili yako

Hakuna ilo nakiri, Kisura kaliba yako.


Kukupenda naahidi, nawe naomba ridhia

Takutunza uwaridi, hutikifu kunukia

Ndoa ndio langu sudi, si muhuni nakwambia

Leo wameitakidi, ndoa wamejifungia.

Mume zidisha mapenzi, mdumu miaka mia

Mke wewe ndo mjenzi, kuboresha familia

Yangu zawadi ya tenzi, Soma kujikumbushia

Pendaneni na muenzi, Wazazi wao usia.

SHAIRI- KINYOZI

Simpi kwa masihara, namshughulisha kweli

Kwa upole sipapara, yanini kuwa mkali

Hudai yangu bakora, humponya yake hali

Nami nayala mapera, kama samata na goli.

Zangu kukurukakara, hajaiona mithili

Hunionyesha ishara, ninyoe kwa maadili

Kinyozi wangu kipara, hupenya kwenye jabali

Amenuna na kafura, kama muwa wa pingili.

Marimba yangu sungura, sipigi kwa ukatili

Japo ninampurura, zangu mpya staili

Hukiri bila subira, kinyozi kweli rijali

Sitaki waje nipora, nakuomba tafadhali.


Vinyozi wengi wakora, najua tangu awali

Pungufu zao busara, hawana stahamili

Hufanya ukadorora, na wengi ni majahili

Ujuzi wao hukera, hawanyoi kwa kamili.

Nikamwambia kisura, poza moyo tua tuli

Nasema sitakukera, nakupa yangu kauli

Nishazoea mapera, sitaki mastafeli

Utamu wako ni bora, unavyo vitu asili.

Mtoto kapewa sura, tabia njema adili

Kapewa shepu na chura, hekima nazo akili

Kazipinga nyingi sera, zao wezi mafedhuli

Kwangu mpera mpera, ninashida na msuli.

SHAIRI - NENO MOJA

Ungalifanya lolote, mwenzio nilikungoja

Machozi yangu ufute, nideke kwenye mapaja

Umenifanya nijute, nimegeuka kioja

Umekufa moyo wangu, kuninyima neno moja.

Mwenzio ninateseka, ghadhabu naungulika

Leo nadharaulika, fedheha imenishika

Ipo siku itafika, nawe utanikumbuka

Umekufa moyo Wangu, kuninyima neno moja


Hukuwahi niamini, tuliishi kwa mashaka

Kujali na kuthamini, kwako nilikuwa taka

Yamenifika shingoni, mwenzako ninaondoka

Umekufa moyo Wangu, kuninyima neno moja.

Nilibaki gugumia, bila kosa ni kipigo

Usiku ukifikia, uligeuza kisogo

Hukutaka nisikia, mwenzangu likuwa mbogo

Umekufa moyo wangu, kuninyima neno moja.

Sisemi ninajutia, sijinyongi sijiui

Siwezi kukurudia, sitosema sikujui

Ila yatakufikia, kesho yako huijui

Umekufa moyo wangu, kuninyima neno moja.

SHAIRI - MJA.

Mungu hakupi kilema, akakukosesha mwendo

Madhali bado wahema, hebu zidisha upendo

Usijitie nakama, uchunguze wako mwendo

Tuache kusukuana, sote watumwa wa tumbo.

Ubayani watusema, tukifanya kila jambo

Unatutia lawama, watuteta kwa mafumbo

Watuzushia tuhuma, watuimbia na nyimbo


Tusiishi kwa salama, kiuzibe kila jambo.

Mja weye mja gani, kila siku sekeseke

Wataka tuwe shidani, wenzako tudhalilike

Waibua tafarani, udugu ufadhaike

Tumekufanyia nini, taka tuparanganyike.

Wayasambaza maneno, asubuhi na Jioni

Watunanga minong'ono, kipita barabarani

Hufai kuwa mfano, si rafiki si jirani

Weye mnafiki mno, Uwe mgeni wa nani.

Watu wamechoka visa, unafiki lokithiri

Jamii itakususa, kose pa kukustiri

Ndugu ushakuwa sasa, hebu keti ufikiri

Siseme sijakuasa, tabia zako si nzuri.

SHAIRI - MAHABA

Makosa hutia doa, natambua mahbuba

Ila unanizuzua, mana sili nikashiba

Japo nimekukosea, ila usiwe ngariba

Penzi langu kulingoa, mawazo yakanikaba

Jua nakusabilia, nimekupa kubwa huba

Mwengine sitamgea, kumpa yako mahaba

Nisamehe malkia, kwako ninaomba toba


Usije kunisemea, kusema kwa wangu baba

Penzi nitakupatia, pomoni si habahaba

Kwako pweke tabakia, sitofata makahaba

Fahamu zimenijia, siku nitaitwa baba

Nisamehe mardhia, maradhi yangu we tiba

Gonjwa linonizuzua, si lingine ni mahaba

SHAIRI- KWANINI

Kwanini hivi kwanini, baadae ujutie

Tulikwambia jamani, tahadhari uchukue

Sasa hili tafrani, wajatulaumu sie

Hivi weye mja gani, usosemwa usikie

Mja usiye na soni, sikio na lisikie

Nosengenya buldani, Habari zikufikie

Kwanini hivi kwanini, baadae ujutie.

Ulijionea shani, uongo ujitungie

Gombanisha majirani, tusiishi vyema sie

Aftiri na shetani, Mal'uuni tusikie

Nyoo wajiliza nini, nyamaza situchulie

Kuteta tete na nani, huruma tuone sie

Hatutoona hisani, limbukeni jitambue

Kwanini hivi kwanini, baadae ujutie.

Ulipokuja kwa goto, kujivuna kila kaya

Kujikweza kwa kipato, hukuhisi ni vibaya


Mbele ya wetu watoto, ukatuita malaya

Ulijipalia moto, kwa yako tabia mbaya

Umekumbwa na msoto, leo waja kama yaya

Unaleta zako fito,,msamaha! huna haya?

Kwanini hivi kwanini, leo hii ujutie

Ulivyovitegemea, leo vimekutoroka

Mali uzojivunia, sasa umefilisika

Afya ya kujigambia, magonjwa yamekufika

Marafiki wale pia, shida hawakuzitaka

Wamekwacha na udhia, pweke unasulubika

Unabaki kujutia, dunia imekushika

SHAIRI - SHILOLE

Ninakupenda shilole, yanini wapata tabu

Uwe waimba malele, hata kama taarabu

Achana na kina wale, njoo kwangu mahbibu

Nitakuponya kipele, kwa mahaba taratibu.

Walia nini shilole, pole kwayo masahibu

Si chozi wala kelele, kwangu sitokupa tabu

Nitakupenda milele, nakutimiza wajibu

Nisikilize shilole, huba hili wewe jibu.

Usishangae shilole, mapenzi yaniadhibu

Nitazame ndo nilale, picha yako niratibu


Nikikuona na wale, kwangu ni kubwa adhabu

Wavizia kwa machale, hapo kati pa dhahabu.

Ninateseka shilole, na wewe ndio sababu

Kucha napiga misele, nikuone kwa karibu

Memtuma bob tale, barnaba na nasibu

Hadithi zao za kale, sijapata zuri jibu.

Natamatisha shilole, sisongi mbele sababu

Usije kumbuka kule, kwao wale wenye gubu

Nimekuwa msukule, huba lako mujarabu

Nitue kwako nilale, unidekeze muhibu.

SHAIRI- ETI

Eti nakupagawisha, mahabuba laazizi

Moyo wako naukosha, wapi mejifunza kozi

Penzi langu dawa tosha, ya kukupa usingizi

Mwengine nisimfate, umenipa moyo wako.

Umenipa moyo wako, wapagawa na makeke

Napoza ashiki yako, kitandani sichomoke

Tunu yenye huba lako, wanipa niteseke

Penzi nalokupatia, Nizidishe mara saba.

Penzi nalokupatia, niongeze mara saba

Eti umedumbukia, langu dimbwi la mahaba


Navyo kushughulikia, chururu habahaba

Eti ninakuzuzua, Nilete posa kwa baba.

Kikutazama usoni, huwa ninatabasamu

Ninakushika shavuni, ndimizo ninazichumu

Unalala kifuani, kupa maneno adhimu

Unayenipenda mimi, ndio wako muadhamu.

Unarembua machoni, wanong'ona kwa karibu

Nyongo mkalia ini, mpenzi wangu muhibu

Hebu papasa kwa chini, polepole taratibu

Nisiibiwe jamani, hapo utaniadhibu.

SHAIRI :PENDO LANGU

Pendo langu ni kilema, lachechemea mtoni

Chubwi chubwi lilizama, dimbwi la yule fulani,

Nilimpenda kinoma, yeye hakunithamini

Hanitaki alisema, fedha Sina mfukoni

Mithili mekula kungu, jicho lake teketeke

Lilia nafsi yangu, wale kunizidi kete

Litamani awe wangu, tubaki chanda na Pete

Nifanyeje walimwengu, nami hali yangu tete

Yalinifika marudi, nashidwa kujieleza

Nikipeleka zawadi, lisema kwa kunibeza


Na sonyo la makusudi, eeh! babu toniweza

Hapa njoo na Audi, ferrari na altezza.

Nikimkumbusha enzi, akumbuke angalau

Pindi namwimbia tenzi, linijibu kwa dharau

Kwenye penzi Lile penzi!?, hanipi moyo walau

Pesa hununua penzi, jidai kanisahau.

Leo niliyoletewa, nimeumia moyoni

Eti ameshatumiwa, amechoka taabani

Ukimwi amepatiwa, kafariki masikini

Roho ye mechukuliwa, sasa yupo kaburini.

SHAIRI :EWE MOYO

Limeniathiri pendo, pendo la fulani

Kitembea wake mwendo, mie hoi taabani

Heshima yake matendo, staha na ihsani

Ewe moyo wangu moyo, unaogopa kwanini?.

Naungulika kwa ndani, hisia zinalalama

Sauti yake laini, na vile kinitazama

Huwa nafungwa lisani, ninakosa la kusema

Ewe moyo wangu moyo, unaogopa kwanini?.

Nikiwa nae karibu, kwa uwoga natetema

Sijui nini sababu, mapigo yaenda hima


Mwenzie napata tabu, hivi hanioni jama

Ewe moyo wangu moyo, unaogopa kwanini?.

Ona ona kanifata, nimwambie lile jambo

Ila najing'atang'ata, nahisi ugua tumbo

Maneno yagotagota, jambo halikuwi jambo

Ewe moyo wangu moyo, unaogopa kwanini?.

Mbona ninadhoofika, kinishika mabegani

Vipi ninaweweseka, sipomtia machoni

Ila Kwangu akifika, siwezi sema kwanini

Ewe moyo wangu moyo, unaogopa kwanini?

SHAIRI - NIKUHONGE?

Nikuhonge kipi hasa, faida gani nipate?

Sio kwa yako mikasa, inifanyayo nijute

Nikuhonge wanitesa!, kwa viporo na mkate

Eti nikuhonge pesa, sitokuhonga chochote.

Nikuhonge unipende, kwani penzi nanunua?

Nikuhonge ndo ulinde, mi ndo wananifunua?

Nikuhonge usiende, utaacha nisumbua

Kama hivyo bora wende, usije ukaniua.

Nikuhonge wewe nani?, utamu wamechachua

Si tende halua yani, umeisha kama bua


Ngozi ya paka yanini, watisha kujichubua

Nikuhonge huna soni , mwili umeupurua.

Nikuhonge ndo udumu, makubwa mie nacheka

Kufua kudeki ngumu, tena hujui kupika

Nihonge kipi kitamu, nihonge nafadhaika

Nihonge nijilaumu, kama umechoka toka.

Lile tendo maujudi, visababu wanambia

Unagawa makusudi, kisa? sijakuchumbia

Nikuhonge sifaidi, ubaki kunitambia?

Eti nikuhonge kodi, mi ndo nimekupangia?.

Nikuhonge unichune, kwa wenzako uniseme

Dume bwege nijione, nifulie uniteme

Nihonge nisitafune, unibanie uhame

Sikuhongi hata tone, swaga hizo unikome.

SHAIRI- SIKU YANGU YA HARUSI

Kiukweli ninawivu, nawaza sina majibu

Japo hili sio povu, wifi na shemeji gubu

Jambo hili ni tulivu, ndo mana napata tabu

Hivi vipi itakuwa, siku ya harusi yangu.

Nimechoka kuongopa, nikienda za wenzangu

Eti lofa naogopa, wananipiga majungu


Mi sitaki jike shupa, kajutia ulimwengu

Ila vipi itakuwa, siku ya harusi yangu.

Wapi nitaifungia?, itakuwa ya fahari?

Watu wahudhuria?, walokuwa mashuhuri

Nani atanipambia?, kitu kiwe ng'aring'ari

Nawaza itavyokuwa, siku ya harusi yangu.

Nichague ipi yani, vikindu nimezipanga

Tuanze uzaramuni, segere la mkuranga

Baikoko nayo ndani, labda nianze za tanga

Ngoma ipi itakuwa, siku ya harusi yangu.

Mwanetu usitutenge, samehe yetu madoa

Jiepushe na magenge, hayo yanavunja ndoa

Familia kaijenge, huba lisije kupoa

Nasaha zipi tapewa, siku ya harusi yangu.

Wapi nikalile tunda?, kisu changu nikakate

Nchi gani nitakwenda?, zile saba za fungate

Na yule ninompenda, pita wanawake wote

Vipi kwako itakuwa, siku yako ya harusi.

SHAIRI :RIDHIKA

Hali yangu idhlali kujikweza sitoweza

Siwezi kuwa mithili, wenye fedha tanibeza


Watanifanya dhalili, kama mjane ajuza

Ridhika mpenzi wangu, kwenye bahari ya huba.

Si unakula halali, wavaa unapendeza

Na ninakupa kamili, pamoto nakupooza

Ninakukanda na mwili, huwazi mauzauza

Ridhika mpenzi wangu, kwenye bahari ya huba.

Mpenzi stahamili, hatuna cha kujikweza

Ila penzi letu hili, waosha ninasuuza

Tunapendana wawili, nimekufa nikaoza

Ridhika mpenzi wangu, kwenye bahari ya huba.

Yalishasemwa anzali, penzi nuru kwenye kiza

Staha ni mhimili, mahaba kujituliza

Kwake metulia tuli, najilia na kusaza

Ridhika mpenzi wangu, kwenye bahari ya huba.

Nawaona majangili, mbugani wajipitiza

Mlinzi nipo kamili, wigo nimeutandaza

Halindi mbwa mkali, bali simba nawajuza

Ridhika mpenzi wangu, kwenye bahari ya huba.

SHAIRI- ZA MWIZI AROBAINI

Hadithi hadithi huwa, tamu ila hii chungu

Paukwa kisha pakawa, yalinifika wenzangu


Zamwizi chache mwajuwa, sikia mkasa wangu

Fedheha ile jamani, mpemba alinipata.

Mi tajiri mtaani, kijana mwenye mvuto

Mke watoto nyumbani, kwema hatuna msoto

Barubaru hasa yani, hujipitisha vitoto

Huwaga tabia yangu, kuonja hapa na pale.

Nyumba ya tatu jirani, kajaza mama masudi

Mume Kienda sokoni, naenda kupiga hodi

Najilia kilaini, kujilamba sina budi

Za mwizi arobaini, sina hili wala lile.

Jembe naweka shimoni, utamu wamzidia

Ooh ohh wewe yani, nini unanifanyia?

Bado mapema jamani, nipe tena nakwambia

Tukanogewa na fani, kumbe tunachuliwa.

Hamadi! mlango pu!, mpemba katangulia

Ile nichomoke tu, si kitu kikanasia

Hata sijasema su, mke wangu kaingia

Mjumbe mshenga duh!, baba mkwe ndugu pia.

Mpemba akanishika, kafura kakasirika

Mke wangu kacharuka, talaka anachotaka


Ma masudi kadhalika, machozi yanamtoka

Aibu imetufika, sote tumefedheheka.

Haramu huwa vitamu, ila vinatia doa

Doa linozidi damu, limevunja yangu ndoa

Fedha fedheha ni sumu, familia imebomoa

Jifunzeni wanadamu, heshimuni zenu ndoa.

SHAIRI - NA NIKIWA SINA HELA

Na nikiwa sina hela,

Asubuhi ni mawazo, wapi nikabangaize

Tumbo lipate ujazo, akili niitulize

Nafanya yuhudi nazo, shida sinieleleze

Njaa haina likizo, sitaki niidekeze.

Na nikiwa sina hela,

Sijui neno subira, kila kitu nalalama

Sitaki mi masihara,nakunja sura kinoma

Napiga sana mikwara, siku haikwishi vyema

Nakumbuka ukapera, ila ndo sirudi nyuma.

Na nikiwa sina hela,

Nafura najinamia, nanuna ninachukia

Amri ninatumia, siombi ninavamia

Njiani spidi mia, salamu hutosikia

Nguvu nyingi natumia, na kujisikitikia.


Na nikiwa sina hela,

Vitu vingi nasahau, kichwa kina mambo mengi

Nashindia kaukau, kama shule ya msingi

Mambo yangu jaujau, ninageuka mdingi

Si walau angalau, sina moja sina vingi.

Na nikiwa sina hela,

Jua linakuwa Kali, mishe nazo zinabana

Nawa dhooful hali, afueni mie sina

Afya madeni muhali, majanga kila namna

Kashumbari na ugali, kwangu mlo wa maana.

Na nikiwa sina hela.

Siambiwi ninapendwa, chumbani nakaa zangu

Mahaba kukandwa kandwa, hakuna tena wenzangu

Hizi nyimbo za kutendwa, naimba imba kivyangu

Zile huduma nashindwa, nabaki kuomba mungu.

Na nikiwa sina hela,

Hutosikia misemo, ngebe wala minong'ono

Ghadhabu nabwaja domo, mlevi sina mfano

Nyumbani ka lomolomo, ninatembeza kibano

Majukumu mimi simo, pesa likwisha kasino.


Na nikiwa sina hela,

Na nikiwa sina hela, hakinipendi kwa sana

Hakinitaki msela, huniona sina mana

Kanataka zangu hela, eti kaje kunichuna

Nakiamshia tela, misonyo chagunaguna

Na nikiwa sina hela,

Usilete udananda, ishia huko uliko

Swaga za pete na chanda, ziishie huko huko

Usije niganda ganda, pambana na hali yako

Eti ooh wanipenda, penda kwanza ndugu zako.

Na nikiwa sina hela,

Nawa mtu tofauti, sifa zangu nyingi mbaya

Natenda vitu sijuti, sijali sioni haya

Nauza utu kwa noti, nikawe mbwa ulaya!

Tujichunguze kwa dhati, hatutendi mambo haya.

SHAIRI- NAKULAMBA

Nakulamba kwelikweli, kama chai ya kisosi

Mtamu zidi ya sali, tende halua na ngisi

Nakulamba wakubali, eti kwangu ndio basi

Nami ninatakabali, tendea haki nafasi.

Nakulamba unaguna, kelele na minong'ong'ono

Dole gumba nakukuna, si tatu wataka tano


Watamba hujajibana, kama feni kokiuno

Nakulamba wajivuna, shababi sina mfano.

Nakulamba unahema, utamu uso kifani

Wanigamba ninazama, hadi kule upenuni

Panda shusha unasema, nenda juu shuka chini

Nikiacha ni lawama, wasema sikuthamini

Nakulamba pole pole, taratibu kwa salama

Yani vile kilokole, kwa adabu na heshima

Nishakuwa msukule, we nitumikishe mama

Achana na kina wale, hawatoacha kusema.

Nakulamba napapasa, zinakutoka fahamu

Kwa stadi natomasa, nje ndani zamu zamu

Nawe wapata hamasa, kwa yangu mashamsham

Kelele nikikugusa, unasema tamutamu.

Nalamba sijakupiga, ila chozi lakutoka

Si kwa ndumba sijaroga, ila unaweweseka

Nakulamba wanipiga, mayowe warukaruka

Yule mzungu wa niga, nami ninampachika.

SHAIRI- ACHA

Nabaki kuwa na wivu, nawatazama kwa mbali

Nagumia maumivu, na sipati afadhali


Mie mbona mtulivu, bibie nitakujali

Usiende kwakwe huyo, utaumiza mtima.

Utaumiza mtima, nisije nikawa chizi

Hebu ona nalalama, naumia laazizi

Huu wivu si lawama, nikwonapo na mchizi

Juwa nakupenda sana, nami Najua mapenzi.

Nami Najua mapenzi, yale ya nje na ndani

Takupeti takuenzi, nitakukanda mwilini

Kwa nyimbo na nyingi tenzi, yangu mahaba ya pwani

Najua unateseka, yanini ung'ang'anie.

Yanini ung'ang'anie, kitandani huyo ziro

Naomba ufikirie, hujachoka zake kero

Hebu njoo kwangu mie, hutoshindia viporo

Njoo upokee dozi, acha kujibanabana.

Acha kujibanabana, njoo upate utamu

Ukiwashwa takukuna, kwa yangu mashamshamu

Nami ukitaka tena, tutakipiga chandimu

Hutosema bora Jana, kila siku tamu tamu.

Kila siku tamu tamu, maana nitakuchua

Nitagusa kwa awamu, na huku ninasugua


Nasoma yangu kalamu, kitabu nakifunua

Limao chachandu ndimu, raha mate kukujia.

KWANINI

Mume wangu, mfariji wangu,

Tabibu wa moyo wangu, kipenzi changu,

Baba watoto wangu... wangu... wangu,

Japo maneno haya ni matamu mtu ukijasikia,

Ila kwangu kila neno ni ishara ya kujutia,

Hatua nilizozipitia,

Ni mithili ya kumchuna mbuzi ngozi ilhali hajajifia,

Kwanini.

Kwanini ile,

Nitakujali, nitakuheshimu, nitakusikiliza,

Nitakutunza, nitakulinda, nitakupenda,

Nita... nita ... nita.. nita...,

Ahadi zako zilizoniliza zilizoniumiza,

Hivi kwanini ulibadilika hukutaka hata kunisikiliza,

Mwangaza uliosawijika ukawa kiza,

Ulinipuuza badala ya kuniliwaza,

Kwanini.

Nanyi familia kwanini,

Nilimfulia huyu, nilimpikia huyu, nilimlelea huyu,

Hata nilipougua nilimtimizia haki zake huyu,


Anataka nini huyu, ….huyu... huyu….huyu,

Leo mnaniambia sina adabu,

Mwaja na vibwebwe mawifi kwa zenu gubu,

Kwani nanyi si wanawake kama mimi mnanipa majaribu,

Tena mbona hamna hata chembe ya aibu,

Kwanini lakini.

Nikiuliza kwanini,

Mnasema fyata mdomo wako,

Unatuaibisha wazazi wako,

Huyu ni mume wako, lazima awe juu yako,

Ni halali yake kufanya chochote kwenye mwili wako,

We kuwa kiburi ipo jikoni dawa yako,

We ni nani unayehoji mila zilizowekwa na mababu zako,

Ila nisihoji kwanini.

Mnaniona mimi tu kwanini,

Malaya Mimi, sijiheshimu mimi,

Jeuri Mimi, kiburi mimi,

Mpumbavu mimi, mhuni mimi,

Au kisa yeye hamumfumi,

Nimevumilia amenidhalilisha sana mimi,

Mbona yeye kubadilisha wanawake hakomi,

Kitandani ananifanya bila ridhaa sisemi,

Akilewa nyumbani ananishushia mangumi,


Nikisema nimepigwa haiwaumi haiwachomi,

Mnakaa vikao maamuzi hamnihusishi mimi,

Kwanini lakini.

Sina nia mbaya kuuliza kwanini,

Wapo mnasema ni mila au dini,

Eti ameshapanga manani,

Muone mama fulani,

Kakubali mitara wewe usikubali unanini,

Nini... Nini... Nini…

Ni kweli mnasema ni mila na dini,

Mitara ni haki kwake sipingi lakini,

Mbona huduma kwa familia sizioni,

Hawa watoto wake mnataka wale nini,

Hajali majukumu yake kazi zote nafanya mimi hamuoni,

Mie mmoja amenishidwa wapili atamuwezaje jamani,

KICHEKESHO

Leo mnasema nisihoji kwanini,

Ila kwanini lakini.


SHAIRI- SAUTI YA SAUTI YANGU

Sauti yangu kwanini unanisaliti?,

Sauti ya sauti yangu kwanini haunidhibiti?,

Sauti yangu yanini kuwaza suti wakati,

Sauti ya sauti yangu haumiliki hata shati.


Sauti yangu hivi kweli wakumbuka?,

Sauti ya sauti yangu mbona kama washtuka?,

Sauti yangu makubwa nayakukufika hakika,

Sauti ya sauti yangu mbona hupendi kuridhika?.

Sauti yangu mbona watamani nisivyoviweza,

Sauti ya sauti yangu nayo yanieleleza,

Sauti yangu hii tamaa kama moto waikoza,

Sauti ya sauti yangu ona inakudekeza.

Sauti yangu wajua hakukupenda yule,

Sauti ya sauti yangu bado yamtaka yule,

Sauti yangu wataka vya pupa ule kwa vile,

Sauti ya sauti yangu imeng'ang'ana mulemule.

Sauti yangu wanambia nenda,

Sauti ya sauti yangu inashiriki kutenda,

Sauti yangu inasema nakupenda,

Sauti ya sauti yangu inajua nitatendwa.

Sauti yangu ulizoea kuuliza mbona sasa wanyamaza,

Sauti ya sauti yangu wang'ata na kupuliza unaniumiza,

Sauti yangu ushanidumaza ulinipuuza,

Sauti ya sauti yangu umenitatiza ushanimaliza.


Sauti yangu umenipa penzi la mauzauza,

Sauti ya sauti yangu kunidumbukuza dibwi kiza,

Sauti yangu ulitega viza nini ungekuza,

Sauti ya sauti yangu ushaniunguza kuniteketeza.

SHAIRI- TABASAMU

MWANAMME

Ili langu litimie, linakuhitaji wewe

Kwako nijitazamie, mana Wanipa kiwewe

Nipe usinibanie, nipe nichanganyikiwe

Nakupenda nisikie, tabasamu nipatie.

MWANAMKE

Utakacho we chukua, tabasamu ulipate

Nataka kukuzuzua, univalishe na pete,

Tabasamu kuchanua, kwangu ni tuishi wote,

Mahaba nayajulia, nitakupatia vyote.

MWANAMME

Naogopa kuibiwa, maana we ni mrembo

Fedha ikakuchukuwa, nikachezea kikumbo

Nataka kikuchukuwa, nikufiche kwetu chimbo

Nakupenda Laazizi, wasiwasi wanitesa.

MWANAMKE

Wasiwasi nakutoa, wewe wangu mahabuba,


Nipose uje nioa, tugandane kama ruba,

Hakika wanichengua, penzi lako lanikaba,

Mie kwako nishatua, yani nimekuwa zoba

MWANAMME

Shukrani waubani, moyo umesuuzika

Nilikuwa taabani, wasiwasi na mashaka

Wangu moyo bur'dani, ila waeza ridhika

Kipato changu ni duni, usije kufadhaika.

MWANAMKE

Fadhaiko kukukosa, katika yangu maisha

Nitavumilia hasa, dhiki mola tatuvusha

Tukipata tukikosa, matatizo yatakwisha

Nalotaka penzi lako, wewe peke wanitosha.

MWANAMME

Zuri lako tabasamu, na langu yakikutana

Nawa muendawazimu, kwa huba lako mwanana

Unaniamsha hamu, ndimi zetu kipeana

Nakupenda mahmumu, mwenzako nimeshazama.

MWANAMKE

Ufundi wako nahama, nawaza ile mipindo

Huwa wanifanya kama, simba kwa yake mawindo


Jua ndo limeshazama, njoo nikupe upendo

Kitanda kiwe uwanja, mashabiki ni miguno.

SHAIRI- UNANICHOKOZA

MWANAMKE

Nikipi nikufanyie, moyo hasa uridhike,

Utachokosa nambie,wala usiyapayuke

Na kazi niyafanyie, mradi usinitoke,

Moyoni nikuingie, ukuondoke upweke.

MWANAMME

Nipende na unienzi, kwa babu fanya zindiko

Yani unipe mapenzi, nisiwe na fadhaiko

Nipige nyundo mjenzi, uitike miitiko

Nitue kwako mpenzi, nisende kwa michepuko

MWANAMKE

Michepuko sio dili, wanakugeuza buzi

Njoo kwangu we rijali, ninyonye na hiyo ndizi,

Tuponyane zetu hali, tuoneshane ujuzi

Twende kote huko mbali, tukashushe na pumzi

MWANAMME

Tutaizunguka pwani, yupate ule upepo

Kisha twende na mbugani, mito bahari zilipo

Usiku mle chumbani, tuchombezane na ndipo

Nizame humo kunani, na nigande hapo hapo

MWANAMKE

Huwa ninasisimka, kwa hiki kifua chako,


Sindano ukipachika, dawa hufika kunako

Nazungusha kwa mizuka, ka ngoma ya mdundiko

Ukinipa Karateka, mie nakupa mdako

MWANAMME

Nawe unanijulia, lako halichachi bando

Vile unakichafua, kama tupo kwenye Ndondo

Wanipa hujabania, nakujaza kwenye lango

Chini juu warukia, misamba na taikondo

MWANAMKE

Aah mpenzi muhibu, mbona unichokoza,

Haraka kwa tararibu, kidonda wakipooza,

Dozi yako mujarabu, na sauti naipaza,

Ooh ohoo mahibu, shindilia Jaza Jaza

MWANAMME

Sauti ukiitoa, mie nawa hai hai

Yani mambo sio poa, kichwa kinataka tai

Kikizama kitapoa, tena bila kukinai

Sime langu nimenoa, na mori ya kimasai

MWANAMKE

Wanaleta pekepeke, nia yao niachike,

Kisha wote wanicheke, nyoyo zao ziridhike,

Ninadumu kuwa mke, bora nisitetereke

Wanafiki waumbuke, ya kwetu yasitirike

MWANAMME

Nitakupenda daima, cha msingi watupishe


Tumeshapendana jama, vipi mtuachanishe

Mtaja kufa na homa, nongwa iwaaibishe

Njoo udeke nasema, waja sikubabaishe.

SHAIRI- LAITI

Laiti ungelijua namna akili yangu ilivyokufikiria,

Taswira yako katika mboni zangu haikuwahi kauka wangu dia,

Uliuteka moyo wangu kwa penzi lako n'singeweza kujinasua,

Nilikupenda pweke peke yako katika hii dunia,

Ila laiti ungelijua.

Laiti ungelijua ni shida gani na mateso mwenzako nilipitia,

Nilikimbizwa na mbwa koko nilipokuja kwenu kukuchungulia,

Nilimwagiwa maji ya makoko mfanyakazi wenu alinichukia,

Na nilijifanya nauza piko ilimradi kwenu nipate ingia,

Nilikuwa jela ya huba lako mfugwa mwenye hatia,

Ila laiti ungelijua.

Laiti ungelijua ni mimi tu katika wote ndo nilikuwa na nia njema,

Sikupenda ufadhaike na kuvunjiwa heshima,

Nilitetea kwa nguvu zote na kukupamba kwa sifa njema,

Nilikulinda popote sikujali watu wanayosema,

Nilikuwa radhi nisote ila wewe uwe salama,

Ila laiti ungelijua.

Laiti ungelijua nilikupa vyote ulivyohitaji,


Nilitoa bila ya malalamiko na kuhoji,

Ulivaa ukanawiri ukajilia na makulaji,

Hukuridhika ukaniadhiri kwa kujifanya mjuaji,

Ulitangatanga ona leo watapatapa mfamaji,

Ila laiti ungelijua.

Laiti ungelijua mimi sikuwa kikwazo,

Nilinyamaza ulipoongea kuiepusha mizozo,

Uliponipuuza nilivumilia ukaniona hamnazo,

Makosa ya kwako nikikuambia unaniletea maigizo

Penzi hili kujifia jua wewe ndo tatizo,

Ila laiti ungelijua.

SHAIRI- JANADUME

Mi ni chovya chovya yani lambalamba,

Vitoto hivi vya mjini navitia kamba,

Mi ni bonga bonga ninasombasomba,

Nawatafuna kilaini naenda nao sambamba.

Vipi unataka gari mama ntakuhonga,

Mradi wangu msumari dirisha nshaligonga,

Muongo zaidi ya serikali siku zinasonga,

Vitoto vya geti gali navi dunga dunga.

Binti chunga chunga ukinipa zaga,

Pilipili na upupu mi nnamwaga mwaga,


Mimba yako mimi simo mwenyewe ulitega,

Toa au kuwa kuku uende tu kutaga.

Nashika simu halo mpenzi nimekucheki DM,

Njoo getto nitakupa yale mambo adimu,

Mtoto kaelewa somo najilia mautamu,

Ukiondoka nafuta namba ninageuka mzimu.

Sina nyumba sina gari mi ni mdananda,

Ila huwa nanawiri mwenyewe utapenda,

Ukinichekea tu binti umeshakwenda,

Kosa lako kuamini kuwa nakupenda.

Maarufu wastarabu hata na machangu,

Wote wanasujudia la kipepe rungu,

Mimba idadi washatoa anajua mungu,

Sitaki kujisumbua najilia vyangu.

Nimekataa hadi watoto semeni mkalale,

Natembeza mkong'oto ninatibu ngale,

Wake za watu shobo nyingi kwanini nsiwale,

Umeolewa na mdingi njo nkusolole.

Masheykhati wapagani hadi walokole,

Walokubuhu mijimama husema polepole,


Nakuza bila kujali vitoto vya shule,

Shoo wangu wanalewa zaidi masele.

Wanapenda nikosoa vyongozi wa dini,

Jamii yanichukia sijui kwanini?

Ila mnotenda nyie huwa hamuoni?

Tena nyuma ya pazia huko madhabauni.

Wanajamii mbona huwa mnachukiana,

Mnasemana mwarogana pia mnauana,

Mwatukana hadharani kweupe twaona,

Pambaneni na hali zenu ndo mje kwangu bwana.

Mi ndo mwanamme kidume wa enzi hizi,

Yani janadume likali la hizi kazi,

Mi ndo paka shume nkufume sina makuzi,

Niundie tume na bado natoa dozi.

WA AKILI ZA USIKU

Wa akili za usiku,

Sisi ni watu wa tuvituvitu

Kichwani tuna viduku, na hatutoacha hili katu

Tupo watembea peku, hilo si tatizo kwetu

Tupo sie wa vikuku, mtuache tuna yetu.

Wa akili za usiku,
Mbona mwatuwekea sana vikwazo,

Njiani kule na huku, tukivaa milegezo,

Nanywa chai mwanzo wa siku, kisha mswaki kuna tatizo,

Mrembo ale chipsi kuku, mi ntakula mihogo bila likizo.

Mi sipitwi na fasheni bwana, wataisoma mi ndo sikitu,

Navaa nguo ya gharama sana, nyumbani sina kitanda ni godoro tu,

Tupo wenye magari ya gharama sana, Mwanamme bila gari we si bwege tu,

Sisi huwa nyumba hatuna, tunapanga kitaeleweka tu.

Nitakuchamba ntakutukana mchana, usiku nitete ndo maisha yetu,

Nitakuchekea nitakuibia bwana, we mroge tumuite mume wetu,

Nitakunyanyasa kisa si wangu mwana, kirudi babio nakuita mwanetu,

Ulipokuwa hai sikukusifu ona, utakapokufa ntakupamba wa watu.

Tupo sie tusokubali kwakweli, tungali wazee ila hutukosi viwanja,

Tupo tunoikana asili, tukija mjini sisi ndo wajanja,

Ila mbona mwasema hatuna akili, nyumba si urithi hakuna haja ya kuivunja,

Tuboreshe hapana kwakweli, tuuze tu yanini kujipunjapunja.

Raha ya mapenzi upate danga, ulichune kama mkorogo,

Tunavaaga nguo ya ndani na kanga, barabarani twatembea kwa mikogo,

Jimama nalipigisha vanga, linanihudumia vipi kwenu iwe zogo

Tupo sie uzazi twapanga, nasie twajizalia kitu mpigo mpigo.


Wa akili za usiku, aeza kuwa wewe mimi au Fulani,

Tuishio sote kila siku, tuvumiliane tu hapa mjini,

Mitazamo juu ya vitu hivi huku, vina ukakasi tusipigane mangumi usoni

Tutulizane kama mboga ya chukuchuku, hujui huu mchuzi au maji yenye vitunguu ndani.

SHAIRI - KIBAMIA KIMENIPONZA

Jogoo huwa lawika, kelele zinasikika,

Banda huwa naliteka, tetea wote patashika,

Ila ninacho kasirika, pale nguo zikinitoka,

Hubaki ananicheka, ghadhabu inanifika,

Kibamia kimeniponza.

Situmii hata pweza, naamini ninaweza,

Najua kubembeleza, utamu kuukoleza,

Ila kinoniumiza, kila muda ninawaza,

Yeye anapo jikaza, kibamia chateleza,

Kibamia kimeniponza

Anasema amechoka, yeye kazoea nyoka

Mbwembwe zangu ni paka, hata robo sijafika

Eti shombo nampaka, napati anachotaka

Kibamia ateseka, hamu haijamtoka

Kibamia kimeniponza.

Nilijisifu ufundi, mchezoni mi sigandi

Hata waje kwa makundi, majaribu mi sipendi


Kwake nimekuwa bundi, kibamia hanipendi

Eti hafiki stendi, nabaki na zangu gundi

Kibamia kimeniponza.

Wanasifiwa wengine, eti mwaume mashine

La yule jogoo nene, la huyu refu muone

Ataka kwenda kwengine, mshono akaushone

Akachezeshwe sebene, simkuni hata tone

Kibamia kimeniponza.

Ninatafuta mganga, ili niweze kujijenga

Nami nianze kuringa, najiona ka mjinga

Changu kisu yeye tenga, anakwenda kwa madanga

Naona ananitenga, jogoo wapi tapanda?


Kibamia kimeniponza.

Mganga anipe tango, nivunje hadi viungo

Nipitilize ukingo, mabao mengi kwa lango

Fujo nyingi kwa ulingo, au nipate mpingo

Nikabe kila kitengo, niwaundie mipango

Niwakomoe maringo, dozi yangu songombingo

Niwavunje na migondo,

Ila mpaka sasa, kibamia kimeniponza.

Shairi : KAMPA KAMPA TENA

Kampa kampa tena, si juzi kampa bwana

Kampa akajichana, kweupe pee mchana,


Kampa akatafuna, tunda tamu lilonona

Si nusu kampa nzima, na tena kampa sana.

Juzi kampa mkaka, wakati u safarini

Kampa bila mipaka, yule mangi wa dukani

Kampa nazi na mbata, kajilia kilaini

Kampa yani mizuka, kama anamaruhani.

Hakumpea uani, wala si kichochoroni

Hajampea porini, au chumba cha wageni

Haikuwa varandani, stoo wala jikoni

Bila ya haya usoni, kaja kumpa chumbani.

Kampa ye kisirani, kwani utafanya nini

Kakuweka kiganjani, hufurukuti kwapani

Alopewa limbukeni, anatamba mitaani

Katwambia maskani, shemeji haumkuni.

Kampa Kwa ustadi, sijui ni lake danga

Chumba kafukiza udi, marashi ya zenji tanga

Shemu anamakusudi, hupitapita na kanga

Mangi kala kafaidi, sema simpige panga

Kampa haikutosha, ikawa ni israfu

Akaenda muogesha, na huku anamsifu


Mkwezi kapagawisha, kuangulisha madafu

Eti wewe wamchosha, shemu amekukashifu.

Kampa kwa utulivu, taratibu si haraka

Kajituma si kivivu, kutomasa na kushika

Kupapasa palokavu, hadi pakaloanika

Nshazali na ubavu, kampa akachomeka.

Kampa vyote Kwa kina, faradhi wala si sunna

Mipindo kila aina, kelele ligunaguna

Mh mh tamu sana, kesho takuita tena

Kampa hata kikana, chabo watu waliona.

SHAIRI : NAKUPENDA

Nakupenda wewe na kila kilichopo ndani yako,

Napenda kila kilichomo ndani yako,

Napenda kila kilichomo ya ndani ya kilichomo ndani yako,

Napenda kila vilivyomo ndani yako,

Napenda kila vilivyomo ndani ya vilivyomo yako,

Nakupenda wewe na naomba uniridhie ndani ya moyo wako,

Sijakupendea sababu nawe usinipendee sababu,

Maana ikiniondoka hiyo sababu,

Kwangu itakuwa kubwa adhabu,

Nipende unihifadhi kama ua nienziwe,

Kwa siha hata maradhi sitaki tengana nawe,

Kwangu unakubwa hadhi useme nini upewe,


Ama nizidishe mapenzi ujirambe unogewe.

SHAIRI : HERI YA KUZALIWA

Sio tabasamu sio cheko lako,

Sio kwa salamu sio mwendo wako,

Sio kwa mashamshamu au kwa urembo wako,

Hatukutazama vyote hivyo sisi kuwa rafiki zako.

Sio kwa upweke sio kwa faraja,

Sio kwa makeke sio kwa tafrija,

Sio kwa sekeseke sio kwa zetu tija,

Hatujafata hivyo vyote katika maisha yako.

Sio kwa vilio sio kwa vicheko,

Sio uwe kimbilio sio kwa madeko,

Sio kwa mashambulio sio kwa ujiko,

Hatujaamua kwa hilo kuja kwenye sherehe yako.

Ujio wetu wewe ndio jibu,

Mana kukupenda kwetu sisi ni wajibu,

Tunakuahidi kuwa nawe kwa karibu,

Tutakupenda kwa raha shida misukosuko na tabu.

Sisi ni ndugu jamaa na marafiki,

Sisi tulokuwa nawe ukiwa na madhila na dhiki,

Sisi tunakula nawe siku ya leo hii keki,


Ni sisi tukuombeao heri baraka za dhati

Heri ya siku ya kuzaliwa rafiki.

SHAIRI : NDOTO PEVU

Natazama sina wasiwasi,

Mawio hadi jua kuzama sitapoza yangu kasi,

Sitalalama sitoruhusu hisia hasi,

Chuki ya moyo inapovuma huo ni udhaifu wa nafsi,

Napambana.

Napambana na wangu ubinadamu,

Ubini usio na damu ubini haramu,

Ubini waliouona mtamu,

Siku nikipatikana wataniita mwanaramu,

Ubini wangu hukata salamu,

Ubini ugombanishao ndoa na ndugu wa damu,

Sina nao hamu,

Na makosa sina.

Makosa sina ila mateso nabeba mimi,

Hata waswahili husema kichwa huponzwa na ulimi,

Nilowathamini wamekuwa ndumi,

Wameniteta kwa zao ndimi,

Leo nami nawa na umimi,

Amani na faraja kwamwe sijinyimi,

Najithamini mimi kama ua.


Ninachanua Ua ang'avu,

Ua yekundu lililo tulivu,

Ua sikuvu ua vumilivu,

Ua limeumizwa na mabavu,

Ua linosumbua wapumbavu.

Ua lenye dira ua la taswira,

Ua la akili na sio hasira,

Ua lachefua matahira,

Ua la ndoto ndoto ya busara.

Ndoto ya busara inajongea, Kuyatafuta mafanikio,

Watabaki tu kungea, hawayajui yangu mapitio,

Vyangu vilio, Chache salio,

Pindi sikuwa na kimbilio,

Mafanikio, hujengwa nasisi akina dada au sio?,

Akina dada wa ndoto pevu.

SHAIRI : HAWARA HANA SHUKRANI

Utampenda kwa mahaba hadi shetani atayaogopa,

Pete na chanda si haba kwa madeni yani utakopa,

Hawara hana nasaba ni fisi kwenye mifupa

Mchepuko ni kama maktaba siri zako usije ukampa.

Utamficha ficha akufiche kwa lake joto,

Utamsifu licha unawako mama watoto,


Atakupa cha ukucha uwe teja penzi la mpito,

Yakianza mapicha picha utabaki na tumbo joto.

Atakusahaulisha mkeo na familia,

Utamdhalilisha mumeo kwa ofa za bia,

Atawafitinisha marafiki na ndugu pia,

Ila mwisho jua ye ni mwizi achezeaye hisia.

Atakuonyesha dunia utatembea unapotaka,

Atakugharamikia kwa fedha isiyo na mipaka,

Takwita laazizi dia mahabuba wangu malaika,

Shamba unojilimia utachovuna ni talaka.

Hawara usimweke bondi hafai kwenye madeni,

Atakufaa kwa kipindi usithubutu kumwamini,

Awe hodari na fundi haimanishi atakuthamini,

Hawara chanzo cha ndondi fedheha uswahilini.

Kibenteni hata umlee umpe pesa mamilioni,

Chakula nguo umgee atambe jeuri mjini,

Jumba kasri umjengee hatoridhika moyoni,

Atakuacha peupe pee na atakuona chanini.

Mchepuko maji ya bahari hayawezi kata kiu,

Usiione fahari kisa ngono kauli mbiu,


Mchepuko ukiuajiri ndoa yako hatoki tasa,

Mchepuko hatunzi siri ukionja tu umenasa.

Hawara ni watulivu wanawinda vya kudaka,

Wale vyao kavukavu kisha ugeuke takataka,

Michepuko ni wasikivu mama ndoani utatoka,

Mchepuko hana mabavu lakini anamadaraka.

Hawara atakupeti uhisi upo peponi,

Tena unajua eti haukumwonaga zamani,

Anakupenda kwa dhati hutomwacha abadani,

Kaa kumbuka hii beti hawara hana shukrani.

SHAIRI : BARUA KWAKO

Barua kwako mwanamke au mwanamme wa ndoto zangu.

Naomba unielewe nakupenda zaidi ya nilivyokupenda jana,

Nakupenda kiasi kwamba mfano wake sijaona,

Yangu mashaka huu ukakasasi naomba uweke bayana,

Mahusiano yanayodumuyo siku zote siri hayana.

Lengo la barua ni kukwambia kuwa naogopa,

Mapenzi yale siyaoni yale mahaba ulokuwa ukinipa,

Naona ukungu nuru mwangaza na shani ya penzi inasepa,

Nahofia machungu wasije kula nyama wakaniachia mifupa.

Mpenzi,
Unajua wazi raha ya upendo upokee na kutoa,

Kujulikana kwa wazazi haimaanishi tayari ni ndoa,

Mapenzi nayo ni kazi ubaya ni hisia kuwa mshahara wako wengine wanaopoa,

Nachotaka ni laazizi na si mama au baba ambaye kila jambo anakosoa.

Unajua mpenzi,

Mapenzi hayana bima moyo upendapo hauna breki,

Kwa miguu miwili maji ya mto huwezi yapima utazama upotee punje isibaki,

Nitoe hofu ninachokilima je wenzangu hawaking'oi kwa reki?,

Laiti wangejua yani dunia nzima kukosa mahaba nako pia dhiki.

Unajua,

Ulouteka moyo wangu ni wewe pweke peke yako,

Ila haimaanishi duniani hakuna warembo au marijali zaidi yako,

Mboni zangu zimechagua wewe kuridhika na kutazama uwaridi lako,

Tafadhali sitaki zione pengine wengine nikapoteza wajihi wako.

Mpenzi

Penzi lako silitii walakini ila wasiwasi ndio akili,

Ninamawazo ujazo wa kitini napata fadhaa kulala muhali,

Jua napata mingi mitihani ukitazamia niko nawe mbali,

Nachoomba nifanyie hisani nibainishie matendo si kauli.

Nionyeshe kuwa kweli wanipenda,

Nidhihirishie kwa mwingine hutokwenda,


Nibainishie huba nideke kama kinda,

Keti na ujue kila siku kuwa mimi nakupenda

Wako,

Mpenzi mwenye wasiwasi.

SHAIRI: MPENZI ZUHURA

Mpenzi zuhura,

Hii ndio barua ya mahari,

Mapenzi yangu kwako ni zaidi ya mjane akisubiri,

Au adui apendavyo shari,

Au malaika na mungu wajadilivyo za binaadamu siri,

Penzi lako limenikaba nakiri.

Unalijua uwaridi?

Ni ua adhimu ila linamiba,

Watu wanaduwaa vile midomo tumewaziba,

Walisema nakuhadaa penzi letu wao wawe ngariba,

Hatambui,

Kama ni mti basi ni mizizi ya mbuyu,

Tumeshabihiana kama mtungi wa maji na kibuyu

Tunaliwazana hatujali maneno ya yule wala huyu.

Mpenzi Zuhura,

Hivi unawajua wanafki,

Walivyo ni kama ajali na mwendokasi,

Mhalifu na risasi,
Waganga na nuksi,

Dini na wafuasi,

Vita na majasusi,

Dhambi na ibilisi,

Watataka tufarikiane,

Nami sitaki wahadithiane.

Sitaki tuwe kichekecho cha mtaa,

Waseme tulijua penzi lile liaishia kwenye mataa,

Waone walivyochakaa,

Eti sie tumefubaa,

Tumekomaa zaidi ya wazazi wetu waliotuzaa.

Kuna hekima moja katika maneno,

Ukisifiwa kwa sifa njema ni raha isiyo na mfano,

Ikiwa fedheha au tuhuma ni zaidi kung'atwa meno,

Maumivu yake hayana salama afueni bali kibano.

Usihuzunike,

Nipo wako jemedari,

Wewe ni kama chakula na mimi ni achari,

Wewe ni maji kadhalika mimi ni anjari,

Unapokuwa mbao mimi nawa msumari,

Nagongelea,

Taratibu kwa tahadhari,


Usibabaike,

Maana hakuna jipya kwenye sayari.

Madhali ardhi na miti bado vya salimiana,

Ila vinajua mafuriko hayawezi viacha vikinong'onezana,

Ila vinashikamana,

Tena vinang'ang'ana huku vikiambiana,

Wewe ni wangu mimi ni wako mpaka dunia inasimama.

Nakupenda

Kwangu penzi sio kikohozi,

Umenikumbata kwa huba lako mahabuba laazizi,

Umenikamata kwa mapenzi yako wapi umepata ujuzi,

Unavyorembua na sauti yako pale n'kikupa dozi,

Unanichengua nakwisha mwenzako kama wali na tui la nazi.

Unanituliza...Naaa nashukuru hujanipuuza.

Mpenzi zuhura

Penzi langu sio mtaala,

Tumeshibana mimi wakwako kama msalani na ndala,

Niridhie n'takuwa wako ndoa tufunge inshallah,

Nivike pingu ya penzi lako moyoni mwako ndo pawe jela.

Mpenzi zuhura,

Nakupenda,

Mpenzi zuhura.
SHAIRI- KAMA MAPENZI

Kama mapenzi ng'alawa toboa jahazi nataka kuzama,

Kama mapenzi mabawa basi n'tapaa dunia nzima,

Kama mapenzi kipawa mola hebu nipe usije ninyima,

Na kama mapenzi ni dawa we ndo daktari njoo hima jama.

Kama mapenzi wakati ohhh sitaki mi kufa mapema,

Kama mapenzi mauti ninaomba nife bila kulalama,

Kama mapenzi ithbati nitashudia mpaka kiama,

Kama mapenzi ardhi na samawati nitayachunguza nipate hekima.

Kama mapenzi huwa yana Siri naweka dhahiri sitaki kuficha,

Kama mapenzi kukunana shwari nitakusugua Kwa usiku kucha,

Kama mapenzi huwa yaathiri mie teja lako nipe chaukucha,

Kama mapenzi ni dirisha zuri sianzi miguu napenyesha kichwa.

Kama mapenzi adhabu nipe tena bila huruma,

Kama mapenzi jawabu naomba maswali yaje himahima,

Kama mapenzi hesabu narudi msingi nianze kusoma,

Kama mapenzi wetu ukaribu niwe donda ndugu siponi nasema.

Kama mapenzi ni umasikini n'takuwa fukara dhooful hali,

Kama mapenzi nyota mawinguni n'takuwa kimondo nisikae mbali,

Kama mapenzi matamu jamani yazidi halua tende na asali,

Kama mapenzi Ngoma mizimuni We cheza segere ukatike kweli.


Kama mapenzi ndo nipe popote nitakupakata na udeke sana,

Kama mapenzi ni chanda na Pete nitakukumbata usiku mwanana,

Kama mapenzi vuta 'n' kuvute nizame ninate hiyo ndio sunnah.

Kama mapenzi ni kupanga kete ninakupa bao nazi kuikuna.

Kama mapenzi yangekuwa rangi ningezichanganya zote nijuazo,

Kama mapenzi yangekuwa bangi ningevuta hadi niwe hamnazo,

Kama mapenzi yangekuwa tungi chibuku chang'aa mbona chache hizo,

Kama mapenzi kisiki kigingi mikito ngingingi sikupi likizo.

SHAIRI - NINAKUMBUKA

Ninakumbuka uwepo wako,

Hakuna siku ipitayo nisitaje jina lako,

Ulivyo mithili marashi ya uaridi ni nzuri harufu yako,

Sikaidi zako pingu na jela ya huba lako,

Nakumbuka makusudi na vile vituko vyako,

Vya kudeka kwa stadi tabasamu na vicheko,

Kwako ndipo nafaidi na kupata pumziko.

Nakumbuka pendo lako mana haliishi bando,

Ukiringa hata twiga hafikii wako mwendo,

Zigo la kuvunja chaga iweje nikae kando,

Uvyonipa hilo zaga hodari yako mitindo,

Yani mambo gagaga kwichi kwichi mdundo mdundo,

Nginda nginda ngenga ngenga nikipachika mpingo.


Nakumbuka visauti vya kutoka kwenye pua,

Nizama na ambakati vyote ninavitegua,

Nakipenya hapo kati hubani unatanua,

Ninatandika mashuti nyavu nazisalimia,

Mi mzizi na mbolea wewe uwa wachanua,

Nakupa joto la jua kisha maji namwagia,

Unahisi burudani..... nayakumbuka wasema nakujulia,

Si robo wala si nusu kilo ninakutilia,

Ukisema shika huku nami nashughulikia,

Nakuponya wanisifu nakuchomeka sawia,

Wajaangua madafu mkwezi kwa kukawia,

Rungu langu la lufufu wala sio kibamia,

Nakujuliaaaa.

SHAIRI - WAONGO

Waongo hao waongo hawajawahi kupenda,

Wataka walipe chongo penzi letu lije vunda,

Nipende tu kwa maringo niridhie mwananyonda,

Mi mchele wewe ungo nidekeze kama kinda.

Waongo wataropoka ila mwisho watachoka,

Gubi umenifunika nami sitaki chomoka,

Waongo hao goroka nguo sofaa viraka,

Nitomase pasi shaka tekenya unapotaka.


Waongo wanaumia twawakera mapoyoyo,

Vile unanipatia faraja yangu ya moyo,

Vile unaniachia hunibanii kichoyo,

Vile ninadidimia nikune kwa mahabayo.

Waongo watuonea donge tukiongozana,

Chuki wanatuwekea Kisa sie twaendana,

Sie tunaendelea tuwachefue na tena,

Utamu unakolea nipe zaidi ya jana.

Waongo huja na ari ukiwa na mimi mbali,

Wenye fedha na magari maneno matamu ya asali,

Zawadi na nguo za hariri wateke yako akili,

Nakuomba jistiri mie ndo nakupenda kweli.

Mpenzi,

Penzi letu linaamani sinitende ajizi,

Kipimo cha umri ni hisani unazonipa lazizi,

Raha yako kwangu deni ninakupa kwa ujuzi,

Tulia pata bur'dani waongo ni wapuuzi

Maana waongo hawajapata kupenda wala kupendwa

SHAIRI- NIPE TENA

Nipe tena pendo lako, kila mara nahitaji

Kiu ya penzi mwezako, yazidi kiu ya maji

Nisihadaike huko, nawe upo mponyaji


Nipe tena niwe wako, nijilie makulaji

Nipe tena.

Nipe tena popote napotaka,

Nipe tena nami nikukune fika,

Nipe tena niweke wese gari halitozimika,

Nipe tena uwe shwari mubashara huna shaka,

Nipe tena.

Nipe tena sio tamaa useme swadakta,

Nipe tena kwa kila saa cheza kibao kata,

Nipe tukitazamana tete nimekupakata

Nipe tena uwe wazimu nikupigishe kwata,

Nipe tena.

Nipe tena kama chandimu peku chini kibukta,

Nipe tena chachandu ndimu nataka kunata,

Nipe tena uwe wazimu utamu utaopata,

Nipe tena sitalaumu kifinya hata kung'ata,

Nipe tena.

SHAIRI- JIPENDE

Jipende ujithamini, usiiweke mipaka

Jilinde ujiamini, kushukuru kuridhika

Jitulize burdani, moyo ukasuuzika

Jiongoe mitihani, yakuondoke mashaka.


Jipoze jipe faraja, na furaha ikibidi

Jikuze panapo haja, kwa elimu na stadi

Jiulize nyingi hoja, sifanye ilimradi

Jipambe na wema waja, sio wale wakaidi.

Jiongoze kwa kauli, za adabu na heshima

Jikoze stahamili, kwa busara na hekima

Jichunguze maadili, yasijeenda mrama

Jiliwaze kila hali, daima uwe salama.

Jionye usirejee, kamwe usirudi nyuma

Jiponye usiongee, yanoumiza mtima

Jikanye usiwalee, watu wengine si wema

Jifanye jipendelee, usikae nyuma nyuma.

Jikumbushe jikosoe, jijaribu jisumbue

Jiepushe jiokoe, jipejibu jifumbue

Jishushe jikokotoe, jihesabu jitumbue

Jivushe jifurahie, tabasamu jitambue.

SHAIRI – MUNGU NA MUSA WA KARNE YA 21

MUSA
Umesema vipaji vya roho mbalimbali lakini roho ni mmoja,

Huduma ni mbalimbali lakini bwana ni mmoja,

Matendo ni mbalimbali lakini mungu ni mmoja,

Kama usemacho ni ukweli hebu jibu zangu hoja.


Tunagombana kisa wewe unajifanya hauoni,

Tunauana kuchinjana chanzo imani za dini,

Ufukara kila kona tunakufa masikini,

Tunakunyenyekea sana ila unatuona cha nini.

Kwani juma yule mwanao anafata neno lako,

Lile neno ulisema shika maagizo ya baba yako,

Usitupe mafundisho ya mama yako,

Yaimarishe siku zote moyoni mwako,

Uyavae yasitoke shingoni pako.

Ulisema ,

Yatamlinda yatamuongoza,

Ila mbona anaona giza,

Maisha yake ni mauzauza,

Afya yake ni ya kutatiza,

Maombi yake unayapuuza,

Kwanini?.

Mbona Samwel alifika kwako,

Kutaka fadhili zako,

Ndani ya hekalu akasujudu kwa ajili yako,

Apate utakatifu wako.

Si we ulisema kichwa cha mvi ni taji la utukufu,


Maajabu nimeamini huna aibu,

Sasa mbona umemuacha na maisha yake ya tabu,

Umechuka kila alicho nacho ibada imekuwa adhabu,

Huoni yanayomsibu?.

Ila si ulisema amkianeni kwa busu la upendo,

Mbona maneno yako hayafanani na matendo,

Ulichofanya kwa dada pendo,

Amekuabudu sana na bado umemuweka kando.

Maishaye umeyatia doa,

Umeharibu yake ndoa,

Mimbaye umeiondoa,

Unayumba mwamba unaboa,

Eti hatupaswi kukukosoa?,

Nashangaa!!.

Ulisema,

Ampendae mungu ampende na ndugu yake,

Mbona umempa uchungu na bado usiridhike,

Umechukua wazazi wake,

Hukumlinda nyumbani pake,

Kawa mtoto wa mtaani umeharibu maisha yake,

Sasa ni hivi….,
Baki na ufalme wako,

Utukufu wako,

Ulimwengu wako,

Kosa moja sikosei

Kupiga magoti nikuombe ujinga huo sirejei.

Nishajua umnafiki,

Mbinafsi huridhiki,

Tena wala si rafiki,

Unachosambaza chuki,

Kwako tena sitishiki,

Am done kukuita mungu am done.

MUNGU

Hongera,

Wewe unayehoji ufalme wa bwana mungu wako,

Muumbaji wa maisha yako,

Ajuae upatacho na kila cha muhimu kwako,

Hivi unajua mimi siabudiwi kwa kejeli,

Kwahiyo mwambie samweli,

Kimfaacho mja ni kile apatacho kwa halali,

Mi bado namjali,

Ila yeye alinitupilia mbali,

Alipokuwa hana mimi nilimpa afadhali,

Alipopata kanisahau akathamini zake mali,


Na neno linasema,

Hakuna awezaye kuabudia mabwana wawili,

Aidha amuache wa kwanza na kumpenda wapili,

Au wapili amuone funza na wakwanza amjali,

Yani mungu na fedha havipikiki ndani ya moja bakuli.

Mi sihusiki na imani zenu ama yenu mawindo,

Mi sikushusha dini ila mwema mwenendo,

Mnapoikosa amani sababu vyenu vitendo.

Mnasema mnaimani yangu,

Mnaonyesha imani isiyo na ujumbe wangu,

Badala muonyeshe imani katika matendo yangu,

Mwambie juma napokea msamaha na asirudie tena.

Aniamini mimi na sio ushirikina,

Chuki huamsha fitina,

Alifanya ndugu wakagombana,

Alisahau mi ni bwana.

Bwana niliye juu,

Bwana ni mimi tuu,

Sina mshirika bwana nisiye na makuu,

Bwana ndo jungu kuu.

Asifuate njia ya waovu hii barabara ya wabaya,


Atubu awe mwoko aombe msamaha kwa haya,

Akajutie maumivu kwa watu alowatenda ubaya.

Mwambie Pendo,

Sitokumbuka makosa ya ujana wake nitamkumbuka kadiri ya upendo wangu,

Hekima ni kutubu hizo dhambi zake kutoa mimba haikuwa mafunzo yangu,

Akipata aheshimu na ndoa yake aliivunja mwenyewe asinilaumu mungu,

Ajifunze kushukuru kwa kidogo aridhike rizki yangu huwa naitoa kwa mafungu.

Mwambie mtoto asikate tama,

Naona amefubaa na kuchakaa,

Analala njaa kila saa,

Anavyosumbuka na mitaa,

Ila kwangu ye ni nuru anang'aa.

Mwambie sijamsahau,

Ila kitu naondoa katika nafsi yake ni dharau,

Kipindi yupo na wazazi wake wakubwa aliwadharau,

Alijisahau.

Namkumbusha,

Kwamba akikuwa athamini kila mtu kwenye maisha,

Najua qadari yake mwambie haya yatakwisha.

Mi ni mungu wa izraeli mungu wa mataifa yote,

Si dini taifa na rangi mimi ni mungu wa wote,


Fanye yalo ya msingi duniani siku zote,

Kwenye raha na vigingi nikumbuke siku zote.

Usichoke,

Ukiacha kuniabudu,

Umeweka mkataba wa kuishi maisha ya tabu.

Fata yote nnayosema hata chembe usisite,

Bora ufike mbinguni alafu kweli usinikute,

Kuliko unikane duniani alafu huko uje ujute.

SHAIRI : NINAMPENDA

Moyo kasi wanidunda, pindi nisipomuona

Ninajihisi hukonda, dawa yeye nitapona

Kwake mie nawa kinda, mahaba yanisonona

Ukweli ninampenda, mwingine sijamuona

Kinipatia salamu, ninajihisi salama

Shauku yangu na hamu, akili huwa zahama

Naona najidhulumu, moyo wangu walalama

Nahisi kujituhumu, uoga wanisakama.

Mdomo unajifumba, maneno nashindwa sema

Mawazo yananikumba, fikira zangu kilema

Asiniveshe kilemba, ye ndo wangu chanda chema

Niunyake kama temba, mana sitaki kudema.


Nikamfata taratibu nimpe maneno adhimu,

Yale maneno yatayofanya ubachela nikahitimu,

Maneno ya ukarimu,

Maneno yasemayo moyo na ubongo ukaheshimu.

Kiukweli ilikuwa vigumu sikujua vipi angechukulia,

Mie nae tunanidhamu sasa vipi atanifikiria,

Vipi njiani ataniangalia,

Hivi atanikubalia, au baharini kunichinjia,

Mtaani atanitangazia nionekane sina njema tabia,

Au atanichunia chuki kuipalilia.

Siku niloyokuwa nasema nae naikumbuka,

Maana usoni nilikuwa natabasamu ila mwili unatetemeka,

Nilikaza nikaweka ngumu ila miguu nilihisi nataka kuanguka,

Kupinduka,

Kimoyomoyo nilikuwa naomba mtu mzima nisije kuumbuka.

Narusha sarafu kama kamari nikakaa kimya na kukausha,

Hisia ni kama zigo zito la misumari alafu kisha nimelishusha,

Hakuniangusha ,

Hakutaka siri leo mi ndo faraja ya yake maisha.

SHAIRI : SOULMATE

Mpenzi uwepo wako nifaraja maishani,

Wewe ni wakipekee hakuna mwingine duniani,


Nidekeze ninyenyekee kama mtoto kifuani,

Nipulize unipepee nijihisi burdani.

Soulmate

Natamani utambue ninavyokufikiria,

Yalaiti ung'amue ulivyonishika dia,

Vile ulivyonikamatia ulivyoning’ang’ania,

Mpaka chini unanishughulikia,


Mi sitaki nije kulia,

Chozi langu liwe la raha ila lisiwe la kujutia.

Soulmate,

Macho yako vile husema na mimi yani,

Tabasamu lako hufanya nashidwa kujiamini,

Ukiwa karibu nami nati kichwani zinaachia,

Nacheka sijui kwanini vile nashidwa kujizuia.

Sauti yako nzito huashiria kidume rijali,

Nami nataka halali,

Njoo uniponye name niipate afadhali,

Mi sijali,

Iwe kwa shida na raha maradhi na zote hali,

Wasiyojua mapenzi ndo tasikia wanasifia asali.

Soulmate

Jua lazama zima taa niweke gizani,


Kitandani sita kwa sita iwe varangati si utani,

Nikunje nipe mahaba utamu wa kisogoni,

Nikune vyote si haba tuwenyewe hakuna jirani.

Soulmate

Nakupenda wewe tu wewe pweke hakuna mwingine,

Nishike sitaki kwenda sitaki ona pengine,

Nitomase mwanayonda niongeze round nyingine,

Jimwae cheza kandanda kama hakuna mechi nyingine.

Napata mawazo ukiwa mbali nikiwa sijui uhali gani,

Wivu sina njema hali nawa na hofu sina amani,

Napiga simu baby tafadhali baba watoto wahi nyumbani,

Nafikiria hao mafedhuli wanakunyapiavyo huko mitaani.

Soulmate

Sitaki kutangatanga sitaki weka rehani,

Penzi letu mola kupanga atujaalie ndoa salmini,

Najiheshimu sivai kanga kisha n'jipitize barabarani,

Umenifunza stara ni anga niwe wazi n'kiwa chumbani.

We ndo sumaku ya moyo wangu unauvuta kila masaa,

Weye mafuta mie kandili wangu kimuli cha mshumaa,

Laazizi tulia ya ulimwengu yasikuhadae ukazubaa,

Takupenda hadi kufa kwangu pepo twende sote kunapong'aa


Kunapotufaa.

Soulmate

Moyoni nimeridhia, penzi letu linafanana,

Habibi umetulia, furaha tukionana,

Umeniponya maradhia, huba lako mithili halina

Naapa sitokimbia, yani tufe na kuzikana.

SOULMATE.

SHAIRI : MWAMBIE

Mwambie naja anihurumie, japo nimechelewa asikasirike

Mwambie naja nimhudumie, huku nafanya haraka asikarahike

Mwambie naja anisubirie, ni hizi foleni tu chonde asifadhaike

Akiwa na mashaka huwa sina amani mie, naja laazizi asighadhibike.

Mpenzi naja sitaki kukutatiza, mana mapenzi yanaumiza nitelezapo tafadhali nikumbuke

Nikuponye haja, sintokuacha kwenye kiza, sintokupa mauzauza unichoropoke,

Nitakupa faraja, nitakudekeza, kukubembeleza unigande polepole na udeke

Wasiyempenda kaja, mahaba nitayajaza, nitayaongeza wanafki watusonye na mijicho iwatoke.

Mwambie ndani ya moyo nimemdhamiria,

Nafsini mwangu twasira yake yeye pweke imetulia,

Halitamtoka chozi bali la raha ya mahaba nitayompatia,

Maisha yake daima ni neno furaha atasikia,

Ulimwengu wake ni amani itamtamalakia,

Usoni pake lake tabasamu halitokuja kufifia.


Mwambie yeye ni awali yangu ananitosha

Yeye ni tafsiri ya maana ya neno maisha,

Yeye ni wangu msiri na kiukweli nakiri huba lake lanikosha,

Amejua kunistiri naomba anisubiri naeka nadhiri sitomuangusha.

Mwambie wanaume tupo wengi wa kila rika na tabaka,

Mwambie kuna wengi hajawaona na wengine wazaliwa na kufika,

Wa nyadhifa na madaraka,

Wa kibri cha fedha cheo na mahoka,

Ila,

Mwambie mimi nitabadilika,

Mwambie kwangu hatadhalilika, hatakasirika,

Mwambie kwangu aliwazika, ataburudika,

Nafsi yake itatulizika,

Atathaminika, ataheshimika hadi umauti unatufika.

Mwambie naja anisuburie,

Moyoni anifikirie, akilini aniwazie,

Akinikumbuka anipigie, salamu anijulie,

Utani wa mahaba anitanie, kiona kimya aulizie,

Maombi na dua akakazie,

Magumu avumilie hakika nimpendae ni mie,

Mwambie hilo alitambuenimpendae ni mie na naomba anisubirie.


SHAIRI- MUDA

Inashangaza namna huwa tunafikiri kuwa tuna muda?

Ila no,

Ni taswira tu zinatudanganya na kutufanya tuhisi kuwa tupo incontrol.

Inashangaza vile tunafanya maamuzi yetu,

Like hii moment tuiskip tutaspend another time like time ni yetu,

Vile tunasogeza ratiba nyingi mbele au kufanya kwa haraka tukiamini kila kitu ni chetu,

Hivi ni vyetu, hapa ni petu, yule ni mwana mwanetu,

Like huyu hatotuacha akifanikiwa damu yetu,

Tunaandaa majibu ya maswali ilhali muda haupo nasi na muda haupo kwetu,

Muda haupo na sisi kwani muda hauendi kwa ridhaa yetu.

Muda unatabia mbaya sana,

Muda unakuaminisha na kisha unakukana,

Unakuthaminisha kisha unakutukana,

Muda unaweza kukuboresha na kukudororesha ukafubaa kijana.

Muda si rafiki wa kumtegemea,

Muda si ukuta wa kuegemea,

Muda usije ukaulealea,

Ukaselelea, ukaudekea,

Muda utakuonjesha asali na usijue wapi umepotelea.

Muda ni kama m'bea asiye jasiri siku zote hafichi siri,


Muda hautokusubiri usithubutu kuutabiri,

Muda unawafanya wengi kuwa dhalili unawalisha pilipili na shubiri,

Muda ndo kile kitendawili ambacho werevu wameshindwa kukibashiri.

Muda ni kama maji usipoyaoga utayanywa,

Muda ndio bora mtaji utakufunda kama hukukanywa,

Walioudharau muda wanajua kitu walichofanywa,

Muda mithili ya kutu unakukakasi usije ukachanganywa.

Muda ni kitu pekee kitachobaki dunia ikisimama,

Muda ndo hufanya masheikh na mapadri wakumbushe toba na kuungama,

Muda si lele mama, muda si kitu salama,

Muda ni zigo la lawama, muda ni kitu cha kutazama.

Muda wa mja ni pale tu anapohema,

Sikia yangu ninayosema,

Tumia muda vyema, kisha jipambe kwa yaliyomema,

Usibebe kila waja wanachosema,

Na ujitunze uwe chanda chema.

Kumbuka kuwa, kuna muda wa furaha,

Kuna muda wa karaha, maumivu na majeraha,

Muuda wa wosia utulivu na nasaha,

Tamaa starehe na raha,

Ndugu tambua, kuja tumia muda kwa staha.


Maishani kuna muda wa maradhi na uzima,

Utoto ujana na utu uzima,

Dhiki faraja kuanguka na kusimama,

Kuteleza kukosea na kutupiwa lawama.

Ukitaka kujua thamani ya ulichonacho,

Muulize asiyenacho,

Muulize yule akitamaniacho,

Wewe ulichonacho,

Muulize akitoleaye macho hicho wewe ukidharaucho.

SHAIRI – HONGERA
Kati ya milioni wa kwanza alitokea,

Kati ya milioni mwenye mbio alikimbia,

Kati ya milioni ushindi kujishindia,

Kati ya milioni dunia kuisogolea.

Aliandika rabuka mimba utaiingia,

Aliandika rabuka duniani utaingia,

Aliandika rabuka siku hii kuifikia,

Inshaallah rabuka umri mrefu kukupatia.

Siha njema nakuombea, furaha na amani pia,

yenye kheri kukushukia, shida na shari kukukimbia,

Allah kukutangulia, kwenye kila hatua ukisogea,


Mafanikio kuyafikia, yenye rehma na baraka pia,

Kheri ya kuzaliwa kaka.

SHAIRI- NJIWA MWEUPE

Hadithi hadithi....

Hadithi njoo uongo njoo utamu kolea,

Hadithi naiweka mbolea,

Ipate unyevunyevu mvua na maji kunyeshea,

Iongezeke shina ipate kujongea.

Hadithi yangu nawaletea,

Ni Hadithi ya njiwa mweupe..

Njiwa alipoijua dunia mashababi wakamuwinda,

Akaonja mbegu yungali kinda,

Akampata wake alodhani atakuwa pete na chanda,

Huba likapepea kujenga kibanda,

Mapenzi yakastawi kama melody za kinanda.

Vile kijana kala matunda ya uzima,

Mara ya kwanza mara ya pili ikawa desturi shamba kulima,

Njiwa kazama wake mtima,

Miguu miwili mwili mzima,

Masikini njiwa kasahau sheria usiingie mtoni pasi kina kwanza kupima.

Baada ya tendo likaja fukuto,

Ni kweli kuvunja uschana ni wito,

Ila ukivunja kwa asiye sahihi kinachofata ni majuto.


Kijana katafuta mwengine njiwa moyo ukajaa fadhaa na msuto,

Njiwa kajihisi kuwa si kito bali ni puto,

Japo si kweli njiwa ni uwaridi lililokuwa na mvuto.

Njiwa liweka matarajio na shule kwelikweli,

Kweli kapata vigezo babae akawa bahili,

Mzee kagoma kumsomesha kichwa kikajawa na ujahili,

Unanambia habari za chuo hivi we mtoto unaakili!?.

Njiwa kahisi kuonewa hasira zikamjaa,

Kabembeleza sana mwishowe maoni yake hayakufaa,

Maisha kwenda kaja kidume kuleta barua ikawa balaa,

Familia ikasema atoswe ila njiwa akakataa,

Kalazimisha hae hae na kwa bwana kenda kukaa.

Maisha yakaenda na bwana kabadilika,

Japo bwana alimpenda akaishia kudhalilika,

Akiwa na mimba bwana kamtenda tena na rafiki yake mshirika,

Kwa wazazi hatoweza kwenda ukizingatia wamekasirika.

Muda si muda mwezi wa kenda haukukawia nao ukafika.

Ilikuwa siku yenye mvua,

Uchungu ukamfika bila kung'amua,

Akiwahi hospitali faraja yake ipate kutua,

Hayupo bwana hana na habari yeye vitamu anavitumbua,

Njiwa aomba tena anasali salama apate kujifungua.


Muda ukapita mjukuu wakampokea,

Kusamehe hawakusita hawakumtenga kumzomea,

Muda ukenda ukijongea,

Moyo ukapona maumivu japo makovu hayakupotea.

Njiwa akapata kijana aliyemsahaulisha ya nyuma,

Alimnogesha vile mapenzi mithili anataaluma,

Alomtunza na kumuenzi ukili wa huba wakaanza fuma,

Njiwa akasema Usiniache mpenzi moyo wangu utajaniuma,

Njoo nyumbani uone wazazi sirudii kosa na dhambi kuchuma.

Njiwa kazama kwa ahadi hewa na mapenzi yalojaa hamu,

Hizo raha azopata pewa kwenye hili huba kawa chakaramu,

Kijana akajafikiwa na majanga yalomlazimu,

Kumuacha njiwa pasi kuchelewa ikawa ugomvi mambo fumufumu.

Njiwa ameachwa kwenye bumbuwazi,

Upweke na hamu vyampa uchizi,

Mithili mnazi uso na mkwezi,

Hakuna sababu ilowekwa wazi,

Kaanza kuwaza hana usingizi,

Au pa mahaba hanaga ujuzi,

Yani muda wote kawa mpuuzi,

Kafata hekima makungwi wajuzi,


Wakamwambia sipate simanzi,

Si rizq yako usijipe kazi,

Mwisho akaona afunike kombe,

Hakuwa mkweli yule sombesombe,

Sio mashindano kusema ni kombe,

Mapenzi yalevya kuizidi pombe,

Muhimu subira mola nimuombe,

Na sisi tupo kama njiwa,

Kuna baadhi ya vitu vipo nje ya uwezo wetu si vyote utafanikiwa,

Vitu kama kukosa, kuondokewa na kufiwa,

Vitu kama kuacha, kuachika na kupungukiwa,

Vitu kama ukiamini ukasalitiwa ukishikuru ukadharauliwa,

Muhimu ni kujipenda na kujikaza kwa mazito ukifikiwa,

Yaliyotokea sio majuto bali mafunzo umepitia,

Unayothamani bado ni kito haijalishi vipi watu wanakufikiria,

Ishi mana kuna maisha zaidi ya vile akili zetu zinafikiria,

Kama wewe unamatatizo wapo wanayo zaidi na bado wanavumilia,

Kumbuka huwezi walazimisha watu wakupende hicho ni kitu watu moyoni hujiamulia,

Ukikosa au kukosea juwa yupo bora anayekusubiria,

Tambua mapenzi si kila kitu kwenye dunia.

SHAIRI - NILINDE NAO

Ni weledi wa kusema, kuyananga ya wenzao


Kwao hakuna la wema, lawama kila uchao

Hata ukifanya jema, itakuwa shari kwao

Ndimi zao sio njema, kuwili kauli zao

Watakusifu umwema, ukiwa sambamba nao

Wakupambe chanda chema, ili fungamane nao

Ila siku ukidema, tang'amua rangi zao

Hata mate watatema, kwonyeshe dharau zao

Watanena we nyangema, kiko wapi bwege lao

Ulitamba uko vyema, kibushuti zombie kwao

Natambua sio mwema, ila sipo kama wao

Mungu naomba rehema, yarabi nilinde nao

Nipe tohara mtima, pate cheza kwa matao

Wasinigeuze kima, nikawa hadithi yao

Vile wapo himahima, ni hodari waja hao

Mazuri yako kuzima, yakasikika ya kwao

Wapo radhi kutwa nzima, wakuundie vikao

Wanyeshee na kulima, chuki na fitina zao

Wakeshe giningi wima, waroge husda zao

Sitoshe mji mzima, sambaze uongo wao

Eeh!!! mola nipe hekima, sinipe kalbi zao

Niwe mja wa kupima, kileta habari yao

Natambua si msafi, ila sipo kama wao

Mungu nipe moyo safi, yarabi nilinde nao


Fadhali wanyama pori, ila sio waja hao

Hasidi waja wa n'nari, zi kutu nafsi zao

Duniani mashuhuri, watu na makamo yao

Wenye fedha utajiri, cheo nyadhifa zikwao

Mali nyumba za fahari, matajiri hadhi zao

Ila kinowaathiri, ni kile kiburi chao

Kwenye jema ama zuri, woni msaada wao

Waje vyombo vya habari, ndo wayatoe mafao

Wamekosa tafakuri, katika mibichwa yao

Unyenyekevu ndo siri, si sifa na ria zao

Napiga goti nakiri, niepushe waje hao

Mola Wangu nistiri, yarabi nilinde nao

Marafiki wazandiki, wakunigeuza ngao

Wanipende kinafiki, wakiwa Na shida zao

Mambo yao yakitiki, taona waenda zao

Wewe upatapo dhiki, hutoona sura zao

Wale kweli mashabiki, ni wachache wafaao

Wataponda husikiki, na matusi kazi yao

Mapenzi hayashikiki, ka umeme wa mgao

Wapendwa hawaridhiki, mithili wacheza bao

Chozi limetamalaki, keti sawia mkao

Mahusiano ni kiki, wajinga ndo waliwao

Moyo wangu mi mdogo, siwezi harija zao

Niepushe hili zogo, yarabi nilinde nao.


SHAIRI - KIUNO CHAKO

Kiuno chako kinanivutia, jinsi unavyokikata

Chenda kushoto kulia, mithili kia la bata

Kinanipa maradhia, vile kilivyomatata

Siku n'kikikamatia, utajasema swadakta

Uno Siri ya mahaba, mautundu na bashasha

Kwikwi ya Huba imenikaba, uno lanipa mshawasha

Nistiri mi jibaba, siniue kwa presha

Nionje japo si haba, kimoko sitokuchosha

Hivi.....,

Uliumbwa muda gani, mana napata majibu tasa

Vile umenona yani, kama mbao lopitiwa msasa

Uno lako ngapi disaini, mana umeubwa kuumbika hasa

Nipe niweshe mia ishirini, kama drafti iwe tutusa

Uno mejawa urembo, cheni michoro na shanga

Kicheza ngoma ndo tuseme wimbo, kibao kata baikoko ya tanga

Niruhusu niiweke nembo, nikuchumbie twende msanga

Nikuoe nikufiche chimbo, mi si guberi sitaki kutanga

Hiko kiuno kikiwa mali yangu, itakuwa fisi kapewa bucha

Vile natambua hii mori yangu, uunge singeli vanga wachukucha

Nikubalie maombi yangu, ulewe mahaba teja la ukucha


Utambe useme wenzangu, napata dozi usiku kucha.

SHAIRI - KIZUKA

Hiviii nawe unanini hasa,

Kujifanya haihai kama pindo la sambusa,

Ulivyo ka koroboi unajifanya baunsa,

Mkononi haujai wala punje kuinusa,

Ujue sikukohoi ole wako nakuasa,

Uji utaita chai siku utayonigusa.

Teeenaaa,

Majungu wako mtaji vipi umeshakulipa?,

Shoga umegombana na maji mana wanuka kikwapa,

Umbea chako kipaji kwangu utatoka kapa,

Kujitia mjuaji drafti umepigwa supa,

Ndo mana mwili hauji umebakia mifupa.

Ndugu watia huruma,

Hizo fito hazipoi ni umbea waeneza,

Waenda ka pangaboi sioni kinachocheza,

Kujibinua ka toi vipi wajieleleza,

Hapo mbele ndio hoi nyuma ni mauzauza,

Hata hunichokonoi mwenzo nimejituliza.

Mja unopenda sifa,

Namungu kakupatia maishani kakunyuka,


Milango kakufungia husda unaumbuka,

Mie anipigania mola wangu mtukuka,

Mitaani nasikia jina wamekupachika,

Roho mbaya chafu nia wanakuita kizuka.

Kizukaaaaaaa....,

Vile umekongoroka kama spea za gari,

Nguvu huna waropoka jifanya wapenda shari,

Mikwara wapapatika jidai mepanda mori,

Leo pyee limekushuka hasidi mja wa n'nari,

We zimwi umefufuka utanitisha kaburi.

Halooo halo ya mgambo,

Shoga wakodi vijora mawigi unaazima,

Mefubaa wadorora puyanga mji mzima,

We chakula ya wakora wametibua kisima,

Mabwana metia fora skendo zako zavuma,

Gumegume we kombora shangingi mchamba wima.

SHAIRI - USI

Usifadhaike unapohisi hakuna msaada,

Usifanye israfu weka akiba upatapo ziada,

Usimsahau mungu kwa toba sala na ibada,

Usidharau ndoa kisa penzi la kimada.

Iwe futa ama chatu wote nyoka niskize kwa makini,


Usiwaridhishe watu jipende hutojuta maishani,

Usiuze utu kwa pesa tamaa ni sukari ya shetani,

Usiige maisha uhuru upate furaha na amani.

Usilee chuki na vinyongo chuki si ya kuikimbilia bali kuikimbia,

Aliyekusaidi kukutoa tongotongo akianguka mshike mkono si kumvimbia,

Rafiki mamluki na muongo upatapo shida ndo wa kwanza kukukimbia,

Chunga kauli epuka longolongo si lazima kila mtu habari zako kumwambia.

Usijikweze roho safi haikai kwenye kifua cha mwenye kiburi,

Usijieleleze hizi nafsi zimeumbwa kwa matamanio na dosari,

Usijitweze mtaka nyingi nasaba misiba ndo yake safari,

Usijilalamikize kauli njema kwenye haba humuepusha mja na Shari.

Usisahau hisani akutendae ubaya mlipe wema wenye thamani,

Usivunje heshima ya mwandani mjali kama anavyokupenda mwake moyoni,

Usikufuru penye mitihani matatizo huletwa kupima imani,

Usijifunze kisirani tizama chini usitamani cha jirani.

Usinitukane usinidharau,

Usinikane ukipanda dau,

Usigombane jishushe angalau,

Usinichene mimi ni ukumbusho wa maisha ukanisahau,

Usi tafadhali usi.


SHAIRI - MAPENZI

Mapenzi ni bahati nasibu, waeza pata nazi au koroma lililowehuka

Mapenzi ndio bingwa wa kuharibu, aliyehongwa na nyoka ni desturi kushtuka

Mapenzi siwezi yake majaribu, sipo radhi kuwa mtumwa nikasumbuka

Mapenzi hawawezi kunitibu, moyo wangu unavidonda visivyokauka.

Mapenzi hayakawii kukusulubu, uliyempenda atakapompenda mwengine

Mapenzi fedheha utakuwa bubu, chakula chako ukijua wanakula na wengine

Mapenzi ni moto yaingiapo gubu, nyumba haikaliki umpendae hamsikilizani pengine

Mapenzi ni jela ya kuhutubu, ukitendwa furaha ya penzi kwako takuwa stori nyingine.

Mapenzi ni kitunguu maji, nafsi yangu dhaifu nami sitaki kulia

Mapenzi hapa mjini mtaji, watakudanga ufilisike na kufulia

Mapenzi kwa wengine kipaji, hili jumba la sinema kwangu bado halijanivutia

Mapenzi si kitu cha kutaraji, “expectations always hurt” usijesema sikuwahi kukwambia.

Mapenzi yatakugombanisha na marafiki, ndugu jamaa washkaji na wana

Kisa mapenzi dada zetu hawashikiki, wanadharau wazazi kwa sababu ya vibwana

Kwenye mitandao pamejaa mapenzi mapenzi ya kiki, drama za usaliti hakuna jambo La maana

Mapenzi yanatuumiza sisi tu wenye dhiki, malalamiko ya mapenzi yanazidi laana

Maana, wahanga wa kujiua kwa vitanzi wengi wao ni vijana.

Tambua,

Mapenzi hayana m'babe, hayana mtemi jemedari wala shujaa

Mapenzi usiombe yakukabe, utakuwa uhemi waona mikosi na balaa


Mapenzi kofi yasikuzabe, utakuwa husemi tunaona unakonda tu na kufubaa

Mapenzi ukimpata kinabe, atakujaza madeni unyooshewe vidole kwa huruma na fadhaa.

Mapenzi ni chungu tamu yani sumu tamu, ni kama panya yanang'ata na kupuliza

Mapenzi yamekosa nidhamu, hayana mwalimu wala refa kusema ukizidiwa kipenga atapuliza

Mapenzi ni jehanamu, kuna watu wanaishi ila mioyo yao inavisasi vya kulipiza

Mapenzi sintofahamu, yameharibu maisha na ndoto za mengi yamekatiza.

Mapenzi yamenikifu, sioni jipya nadiriki kusema nimeyakinai

Mapenzi ni udhaifu, unayemuwekea mahesabu yupo njiani na kwako anapita

Mapenzi ni ubabaifu, utafanya kila kitu sawa ila bado atakuona hufai

Mapenzi hayana uadilifu, maana siku atayoondoka

He or she won't bother to tell you why.

SHAIRI : MAMA

Mama yangu mama,

Ni wewe pweke uliye kwenye mtima,

Ulonifunza kujitunza na kujituma,

Ulonipa moyo wa kujiamini nikasimama.

Uliniasa nisiwe kungwi na sikupinga,

Nikaenda Shule niwe mwerevu na si mjinga,

Ukasema nianze chini ndipo nivuke anga,

Tamaa na Ulimbukeni usiwe kichwani nikatangatanga.


Ulivumilia na kujinyima mradi mimi kunigea,

Kunikanya nia kunirekebisha nilipokosea,

Kunisaidia hisi za upweke zisije ninyemelea

Ulinikosea ukaniboresha yangu kuninyookea.

Lau kungalikuwepo wastahiki nishani,

Yasingetosha malipo kwa kubwa yako hisani,

Linisamehe ambapo nilikuwa kisirani,

Cha kululipa hakipo nakiri toka moyoni.

Wewe waizidi nuru fedha vito vinagota,

Maramaru mwezi lulu jua sayari na nyota,

Si lamborghini subaru thamaniyo havijakamata,

Kwako nikakua huru mwangaza mmea ukiota

Unajua,

Wewe kwangu ni zaidi ya rafiki,

Upo nami katika shida raha madhila na dhiki,

Wewe ni mfano bora hilo nalisadiki,

Nakupenda mama yangu,

Upendo wangu kwako haumithiliki.

Wewe jemedari langu katika mikikimiki,

Wewe ni faraja yangu kwa wengi heshima unastahiki,

Wewe ni chuma cha kukomesha wazandiki,

Wewe haupaswi kurudi nyuma kuabishwa kwa hizi kiki.


Nashukuru haukunitoa kabla sijazaliwa,

Leo nimekuwa kijana mi ni ile zawadi ulozawadiwa,

Wewe ni mama mama wa ulimwengu mzima,

Wewe ni mama wa masudi ally na juma,

Wewe ni mama wa sikitu gift na fatuma,

Ulipowarekebisha leo umeboresha dunia nzima,

Wewe unaheshima si lazima wengine waje kusema.

Wewe unaheshima sababu wewe ni mama.

SHAIRI- NIKUONAPO

N'sipokuona machoni, taabuni waniweka

Lile busu la shavuni, bado ninalikumbuka

Nakuwaza akilini, roho yangu yasumbuka

Hisia hizi kwanini, nikwonapo naridhika.

Umbali wako jamani, nakosa ile furaha

Huwa sipati amani, nateseka sina raha

Unanijia ndotoni, upweke kwangu karaha

Njoo wangu waubani, uniponye majeraha.

Tabasamu la usoni, lako lanipa wazimu

Nacheka mi taabani, maneno yako matamu

Nyongo mkaliaini, mahbuba mahmumu

Kukwambia natamani, ninaishia salamu.

Ukisema unitege, kwa mapambo na mavazi


Kungu jicho legelege, uirahisishe kazi

Juu natazama ndege, mawingu na mbalamwezi

Nageuka domo zege, napata kigugumizi.

Nakuwa muoga kwani, waeza ukajigamba

Majirani barazani, wakaniita mshamba

Rafikizo maskani, mje nyote kunichamba

Kichekesho mtaani, ninuke shombo vumba.

Nakupenda si utani, mahaba yananikaba

Ila n'kikueka ndani, masharo watakuiba

Kipato changu ni duni, nashidwa weka akiba

Usijenifanya kuni, nikakaba na kuiba.

Ninaungilika nafsi, hivi niwe jemedari?

Ninaipenda nafasi, ila waeza subiri?

Tusiwe paku na pusi, nyumba kila siku shari

Zuri likawa nuksi, tamu ikawa shubiri.

Nakuhitaji lazizi, ninaogopa machungu

We ganda mi utelezi, mi mfungwa we ndo pingu

Penzi lako kikohozi, nikwonapo nawa pungu

Nachohofia machozi, na visa vya walimwengu.


ASANTE

Sina nitalolitenda, kuusadifu upendo, wa jalia

Kaumba miti matunda, waja wa kila mwenendo, walotimia

Na bado anatupenda, kwa zuri na baya tendo, kutendea

Yumkini atulinda, mola mwingi wa upendo, jalia.

Nami ukaniruzuku, nisije patamajuto, ya dunia

Ukanipa wa usiku, wakunipa lile joto, mardhia

Na mie siku ya siku, ndoa ile motomoto, kanigea

Kwa soda wali na kuku, ilivyoada na wito, furahia.

Mola kanipa rijali, anaejua kuenzi, kwa murua

Mume anaenijali, na anajua mapenzi, nawambia

Anafanya kwa kamili, habakishi lote penzi, hunigea

Naye ndie mhimili, kuimarisha ujenzi, familia.

Leo nimepata shani, mola nami kaniona, mlimwengu

Mwenza anonithamini, mahaba yanayofana, si machungu

Karuzuku rahmani, usiku kwake napona, tamu yangu

Furaha isokifani, nimekosa cha kunena, kwake mungu.

Nachosema shukrani, mola ndie unojua, kesho yangu

Ninakuomba amani, riziki kutusushia, lake fungu

Kuondoa tafrani, Mabaya kuepushia, ndoa yangu.


SHAIRI - UA

Ua langu la thamani, sichoki kulangalia

Sitazami kwa jirani, ni kwangu nalifungia

Chumbani ndipo mtini, matunda najichumia

Ua lisoisha hamu, dawamu linanukia.

Ua langu zuri sana, yakini nalisifia

Ua lingali kijana, kila siku lachanua

Ua harija halina, hanjamu janipatia

Ua lisoisha hamu, dawamu linanukia.

Ua ni sanjari yake, heshima kujipatia

Hung’ara kwa rangi yake, mithili ya malkia

Sitoliacha lipweke, ua langu mardhia

Ua lisoisha hamu, dawamu linanukia.

Burkata na jioni, ua nalihudumia

Jukumu langu jamani, kulipa maji mbolea

Ling’are kiwa mtini, lizidi mengi maua

Ua lisoisha hamu, dawamu linanukia.

Staharaki kwa dhiki, shida zikitufikia

Staharaki lukuki, maneno akasikia

Hataki kujialiki, hodari kuvumilia

Ua lisoisha hamu, dawamu linanukia.


Magwiji wenye ujuzi, walienda kwa halani

Wenye pesa nyingi kozi, uhaini hadharani

Yakawatoka machozi, aftiri wenye fini

Ua lisoisha hamu, dawamu linanukia.

Harashi waso na soni, ua walinyemelea

Nia yao walihini, yangu kuniharibia

Ila ua yumkini, anasa jiepushia

Ua lisoisha hamu, dawamu linanukia.

Upendo kwa ua langu, siwezi kumithilia

Fuadi mnasiri yangu, nadhiri kukusudia

Niwe wake awe wangu, ndoa mjejifungia

Ua lisoisha hamu, dawamu linanukia.

Nawambia watunzaji, nyote mliobakia

Matunzo ya ua maji, samadi kulichochea

Yakini huo mtaji, ua lako kupatia

Ua lisoisha hamu, dawamu linanukia

Nakushuku rahmani, subira kutupatia

Magumu yote njiani, tuliweza vumilia

Furaha iso kifani, leo ndoa jifungia

Takutunza duniani, paka siku najifia.


SHAIRI - NINALIA

Enyi waja wa dunia, mbona huruma hamna

Hisani imepotea , juu yetu waschana

Maovu mwatufanyia, hilaki kila namna

Kigori ninauliza, mbona hamtendi haki.

Waschana tunalia, machozi kwa yetu haki

Mbona mwajipendelea, hamjali itfaki

Tena mnatubagua, hamtaki tushiriki

Kigori ninauliza, mbona hamtendi haki.

Kupika na kupakua, kudeki napo kufua

Mifugo kuhudumia, shambani kulima pia

Kuosha masufuria, kazi tunawafanyia

Kigori ninauliza, mbona hamtendi haki.

Tena mnafanya hila, mwachagua na wachumba

Mwasema eti ni mila, kwa goto tena mwatamba

Mila za kimakabila, mwatumia kama kamba

Kigori ninauliza, mbona hamtendi haki.

Toa ngono pata kazi, kauli ya huyu bosi

Kukeketwa ndo malezi, bila hivyo we nuksi

Naonewa waziwazi, jamii sina nafasi

Kigori ninauliza, mbona hamtendi haki.


Hivi nini kosa letu, hadharani mtamke

Kosa jinsia yetu, tumeumbwa wanawake

Kwa dhambi ipi wenzetu, hata tusiheshimike

Kigori ninauliza, mbona hamtendi haki.

SHAIRI : DHAIFU

Dhaifu mie mwilini, mawazo yanipa tabu

Taharuki akilini, ukimya kwangu adhabu

Nawaza nifanye nini, iniondoke adhabu

Mimi nimefanya nini, mbona silipati jibu

Nakesha usiku yani, na wewe ndio sababu

Mja usiye na soni, usiyejua adabu

Unanitia tabuni, tabia yako ya gubu

Uhuru sina jamani, kama sura ya nikabu

Nambie mekosa nini, nipatie basi jibu

Naomba uniamini, mie mstaarabu

Niliyofunzwa nyumbani, kwa mama bibi na babu

Nimefanya tathmini, iniepuke ikabu

Kuwa nawe najihini, wanizidishia tabu

Wewe mwanamme gani, kauli zako ni subu

Nakuacha mal'uuni, nitatafuta tabibu

Atakayenithamini, kunitunza kwa adabu

Atayenipa auni, kwa mapenzi taratibu

SHAIRI : AMKA

Amka mwanajamii, burkata imetimu


Kawika na hakawii, jogoo katusalimu

Nimetunga tungo hii, kwa dabiri zojihimu

Cha shuka mwanajamiii, kafanye mambo muhimu

Amka ndugu amka, uijenge kesho yako.

Amka kiharakati, tupiganie amani

Pia tuwashike shati, wanochochea udini

Tuepuke mahuluti, unyanyasaji nchini

Tuhoji kwa ithbati, wahujumu wahaini

Amka ndugu amka, uijenge kesho yako.

Amka mama fatuma, kuwa mjane si mwisho

Tena usikate tama, kulidai lako jasho

Na kwako dada mwajuma, heri uuze korosho

Uguberi sio mwema, utakufa kichekesho

Amka ndugu amka, uijenge kesho yako.

Amka we mwanafunzi, kiakili na ujuzi

Mawazo yako ujenzi, tafakuri tunduizi

Epuka utumwa kwenzi, wa bwana utandawazi

Shule sifanye mapenzi, si sambamba hizi kazi

Amka ndugu amka, uijenge kesho yako.

SHAIRI : CHANGU

Nijuzeni walimwengu, yakini pia wasifu

Fikira pata ukungu, dabiri zangu pungufu


Taharaki hizi kwangu, mvuvi kwa maji mafu

Ipi maana ya changu, ninapata hitilafu.

Changu ni huyu samaki, wa ziwa na baharini

Kutwa apata hilaki, za wavuvi wahaini

Hawiliwa baramaki, pelekwa ughaibuni

Wananchi wenye dhiki, faida hatuioni.

Au change ni guberi, lijiuzalo usiku

Changu yule aftiri, ndoa za watu wereku

Azitiaye dosari, harija kama kasuku

Pate timiza nadhiri, talaka fuo ya siku.

Au changu kiso chako, chako kile ulonacho

Kijali kile cha kwako, nakugwaza uwe macho

Harubu weye kwa hicho, mja ukidharaucho

Usiwe wa changu chako, chako pweke upatacho.

Beti tano ninagota, jibu mnipe malenga

Changu anipa utata, ndoa kujivisha kunga

Funzo kichwani menata, ninawajuza wajinga

Lugha hadhi inapanda, kwa tungo zetu malenga.

SHAIRI : MAWIMBI YA MAUTI

Kifo kitu lothabiti,

Lazima kujizatiti,
Amali ndio feleti,

Jahanamu si bahati,

Kama kuvaa bushuti,

Rangiye chanikiwiti.

Mauti huja fajaa,

Dunia hii hadaa,

Maovu yana fazaa,

Sakaratu pata dhaa,

Kwa yule aso kiraa,

Nafsie huchakaa.

Roho luja tachenyeta,

Wachawi na masalata,

Mioyo haita tuta,

Bali itanyongorota,

Miili itafukuta,

Majasho yatatokota.

Waja wake rahmani,

Fuadi duli lisani,

Wataipata auni,

Roho zenye ihsani,

Fanana zao thamani,

Nafasi ya daharani.
Roho yangu jidhibiti,

Uyakwepe mahuluti,

Ibada kwa ithbati,

Jahanamu yake hati,

Nimefikia tamati,

Hili wimbi la mauti.

SHAIRI : CHANGAMOTO ZA MAISHA

Maisha jama maisha,

Yazidi kunidatisha,

Kichwa ninafikirisha,

Hali yazidi nitisha,

Changamoto za maisha.

Kila nikishughulika,

Maishani kujengeka,

Ninanyonywa na tabaka,

Lile lisowajibika,

Nabaki kulalamika.

Nimeshafanya juhudi,

Kulima kwa makusudi,

Biashara na miradi,

Vipawa zangu staidi,

Wakubwa ndo wafaidi.


Kidogo changu kipato,

Pale niuzapo sato,

Mbogamboga na tomato,

Na mnada wa kipeto,

Kodi abeba pilato.

Mama chanja anibana,

Taka doti ewe bwana,

Sivyo nitafumukana,

Pweke uwalee wana,

Mfukoni pesa sina.

Kazini hawanitaki,

Wawekwa sostahiki,

Rushwa imetamalaki,

Kwa masikini hilaki,

Yatunyima zetu haki.

Maisha ni changamoto,

Boka katika mseto,

Siku niliota ndoto,

Mkononi nina kito,

Kuamka shika mto.

HAWATAKI

Waswahili niambia, jasiri hachi asili


Fumbo hili nafumbua, muweke kwenye akili

Rabana kakadiria, wa moja hawi wa mbili

Na huo ndio ukweli.

Kasumba zimeingia, za kuwaiga wazungu

Tunaona wavutia, twafata yao mizungu

Tamaduni puuzia, bila kuona uchungu

Mzungu mekuwa mungu.

Twaana jikurubisha, kwa kufata mila

Twaona ndio maisha, vijana wengi wa leo

Rangi kujibadilisha,zifanane na za kwao

Msiba uso vilio.

Wamkuta mwanadada, rangi haieleweki

Usoni kama kishada, mgongo kama kaniki

Visigino ni blada, kakonda hajala wiki

Kisa ni kufanya dayati.

Wayasemayo wahenga, katika busara zao

Kila mchuma majanga, atalia na wakwao

Kucha za ndege kipanga, kuku hana kimbilio

Kutwa ni mashambulio.

Ninakusudi kuasa, nyote jibadilishao


Msisahau kansa, ya ngozi iso tibio

Kemikali zinatesa, zikianza shambulio

Nanyamaza chambilecho.

Nilifanya tafakuri, niutatue mzozo

Ili niweke dhahiri, mlitambue tatizo

Ila ni chao kiburi, kimekuwa ni kikwazo

Hawataki badilika.

SHAIRI : NINAWAKUMBUSHA

Kwanini mnihukumu,

Wengine mwanishutumu,

Mwaniona chakaramu,

Nisemayo sifahamu,

Umasikini dawamu,

Viongozi madhalimu,

Hawafanzi majukumu,

Chelele tangu dawamu,

Utajiri wa haramu,

Mwawaona maasumu,

Hamuwezi washutumu,

Katiba haihukumu,

Ulanguzi kwao chumu,

Mali ghafi za kaumu,

Bakaa wanadhulumu,

Mapadri na maimamu,
Ashuhudia kaumu,

Maadili ndi ghamu,

Wazazi nawalaumu,

Subu baleghe kitimu,

Wana wenda jahanamu,

Hata wale mahmumu,

Usaliti ndio sumu,

Ninasema mfahamu,

Naziakhiri nudumu,

Kugota yanilazimu,

Huu wangu ufahamu,

Ninawakumbusha.

SHAIRI : RAFIKI

Ni nani huyu rafiki,

Abadani haridhiki,

Kwangu bakaa la chuki,

Daima halifutiki.

Kanitenda mtimani,

Kosale ni ufitini,

Kuficha la fuadini,

Loniumiza moyoni.

Daima limpashani,

Kumuona wa thamani,
Kilonisibu jamani ,

Kwake kuwa hadharani.

Nilimwomba ushauri,

Kila pokata shauri,

Katika baya na zuri,

Nikapata ujasiri.

Sasa ameshanitenda,

Japo kuwa limpenda,

Moyoni kaweka donda,

Mahabangu weka inda.

Kwangu si mwema rafiki,

Si furaha si kwa dhiki,


Rafiki yu mnafiki,

Samaha hastahiki.

SHAIRI : MTUKUFU DHAMBINI

Yaliyomo duniani, yamenisakama mimi

Bul’dani limwenguni, wananichukia sipimi

Wanasema nawahini, madhila kucha sihemi

Atibu buka moyoni.

Ninonena kwa lisani, kwa ithbati makini

Kuwaonya wanandani, duizo la budharani


Naonekana shetani, kuwalumba wafulani

Duala langu pomoni.

Niking’gamua madhila, yanayokumba hadhira

Walanguzi wala hela, faida wala chotara

Mama n’tilie jela, kwa mfumo uso bora

Dabu za dariji sera.

Nikiwaasa vijana, turudi kwenda kulima

Chaki kushirikiana, kipato kukuza hima

Anasa na waschana, hata kukwepa lukuma

Subu zao nadatama.

Pombe na hizo sigara, acheni zina madhara

Elimu ni taathira, dabiri zenu fikira

Uasherati ishara, Ugonjwa vifo madhara

Wanasema nawakera.

Waheshimu wazazi, walimu na viongozi

Juhudi kufanya kazi, ya uvuvi na viazi

Hata tukafuge mbuzi, tukageme na minazi

Wanisekua mi duzi.

Naonekana shubiri, Mlumbaji kisirani

Jamii kuistiri, Kuifanya daharani


Hata wangu muajiri, Aninyonya taabani

Mtukufu yu dhambini.

SHAIRI - NAONDOKA

Hali yangu taabani,

Joto nizidi mwilini,

Mapigo nayo moyoni,

Kiza metanda machoni,

Sioni kitu jamani.

Juma asha sogeeni,

Omari na athumani,

Niwape ya mtimani,

Hapahapa kitandani,

Myaweke akilini.

Naondoka buriani,

Wosia ninawapeni,

Elimu kito thamani,

Kinojuzu maishani,

Msiache abadani.

Nawausia heshima,

Tabasuri na hekima,

Maadili yalo mema,

Tamaduni mila nzima,


Na dini kufata hima.

Nayo mambo ya ujana,

Ya kugwea vischana,

Uguberi uso mana,

Anasa kufanya sana,

Hiyo si yetu dafina.

Malaika kashafika,

Roho inapukutika,

Pumzi zinazimika,

Dhima imeshanitoka,

Wosia ninaondoka.

SHAIRI : SIKU NIKIFANIKIWA

Siku nikifanikiwa, swali hili nitatiza

Kweli nitashukuriwa, na watu wasojiweza

Yatima walofiliwa, nitawapa mwangaza

Au taharibikiwa, kwa kuanza kujikweza.

Watu nitawaibia, nifanikiwe kwa shari

Dhulma tawafanyia, kwa jeuri na kiburi

Uchawi nitatumia, urozi tanga dahari

Freemason taingia, nikawe hata kafiri.

Au nitashughulika, fanikiwe kwa halali


Maharage taridhika, mchunga huku ugali

Ninazoa takataka, kazi yangu ni dhalili

Koradhi kusulubika, kipato kiwe halali.

Nitawapa sikitiko, ndugu pia Marafiki

Tulogombea makoko, kipindi nanuka dhiki

Kutokumbuka miiko, kuwaona watubaki

Lopata misukosuko, na kusoma kwa hilaki.

Nitaheshimu wazazi, au nitawadharau

Nitakumbuka malezi, au nitayasahau

Nitamfata mwenyezi, dini na chake kirau

Nitakuwa sijiwezi, kwa anasa na vidau

Nitafanya ihsani, au tatenda machafu

Nitakuwa kama nani, lingana wake wasifu

Nami hapa duniani, nitakuwa maarufu

Maswali mengi kichwani, fikira zangu kifipo

Tamati nimefikia, ila jibu sijatoa

Kazi ninawapatia, malenga mlobakia

Mdabiri na kujua, kisha mtaniambia

Tahadhari ninatoa, muhimu kujitambua.

SHAIRI : UPENDO WANGU

Ewe mahmumu wangu,


Mi bukheri afya yangu,

Utenzi watoka kwangu,

Samehe ile mizungu,

Nilotenda japo chungu.

Dini ni yako sabili,

Mtoto uso batili,

Ukanipata batuli,

Nikakufunza fisuli,

Hukujuta bilikulikuli.

Jua nakusabilia,

Pendo nitakupatia,

Kukukosa tajutia,

Hadi mwisho wa dunia,

Japo sijafikiria.

Iwe watokea tanga,

Dodoma ama Msanga,

Dariji nilizopanga,

Tukaishi mkuranga,

Kwa kula ama kufunga.

Nawajuza machambenga,

Juu limbo wanotega,


Na fanaka wanopika,

Wapate wangu kinega,

Ni juhudi za kisaga.

Nakadimu tenzi zangu,

Kuwajuza walimwengu,

Mapenzi kwa mwenzi wangu,

Ni kama taka na pungu,

Huu ni upendo wangu.

SHAIRI : ULIMI

Ulimi nyama laini, yasifika kwa lisani,

Zitokazo akilini, za uzembe na makini,

Zanena ya fikirani, mabaya au ya shani,

Kauli ni tathmini, tuzichunge kwa makini.

Kauli ni tathmini, busurizao bayani

Wanojua duniani, kuna watu na shetani

Tunu za hawa fanani, kazisifu bur’hani

Vitabu vya rahmani, bilikuli havidhani.

Ulimi wake shetani, husema kwa dalihini

Kwa hii yake fanani, mola haupi auni

Hupotosha buldani, kwa chambilecho pomoni

Bui walo wanandani, bur’kata na jioni


Ulimi weza tamani, ufujaji budharani

Wasemaji buharini, kunena uongo fani

Wakifika majimboni, porojo zi midomoni

Mepenya mahakamani, atapata haki nani?

Ulimi kule shambani, umeleta mtihani

Hali zao taabani, pembejeo hawaoni

Na wavuvi baharini, kigugumizi nyoyoni

Fazaa umasikini, chuku zake sultani.

Ulimi hauthamini, subu tele mdomoni

Banati sasa ni duni, ulimi unawahini

Swali chonyota kichwani, nikifanya tathmini

Mwenendo huu jamani, wazazi hamuuoni.

Ulimi wangu jamani, wosia huu ni deni

Usimseme Fulani , kumsengenya Fulani

Kiumeni na kikeni, kwa asiya za kudhani

Ithbati ndo thamani, ya kuniponya moyoni.

Tambua ukinihini, utawekwa na dayani

Siku ya mwisho motoni, kwa dhambi za duniani

Some vitabu vya dini, ujue wake undani

Ikuponye maishani, pate ingia peponi.

You might also like