You are on page 1of 1

LIGWA BUNDALA,

S.L.P 10177,
MWANZA.
27/07/2019
KATIBU MKUU,
OFISI YA RAIS,
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI),
MJI WA SERIKALI – MTUMBA,
S.L.P 1923,
DODOMA.

Ndugu,

YAH: MAOMBI YA KAZI YA TABIBU MSAIDIZI

Husika na kichwa cha habari tajwa hapo juu.

Rejea tangazo la nafasi za ajira kwa kada ya afya lililotangazwa tarehe 22/07/2019 katika tovuti ya Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (www.tamisemi.go.tz)

Mimi Ligwa Bundala mwenye umri wa miaka 28, niliyehitim mafunzo ya tabibu msaidizi (Technician
Certificate in Clinical Medicine) katika chuo Cha utabibu wasaidizi Maswa (Maswa Clinical Assistant Training
Centre) mwaka 2017, naomba nafasi ya kazi ya tabibu msaidizi katika wizara ya Afya. Ninao uzoefu mkubwa,
ujuzi, maarifa ya kutosha pamoja na mafunzo ya vitendo niliyopata wakati nipo chuoni (Maswa Clinical
Assistant Training Centre), hospitali ya wilaya ya Maswa na kituo cha afya cha Mwasai (Mwasai health centre)
kilichopo wilaya ya Maswa.

Pamoja na maelezo hapo juu, katika maombi haya, nimeambatanisha nakala za vyeti vya taaluma (kuanzia
kidato cha nne mpaka chuo), cheti cha kuzaliwa pamoja na maelezo binafsi (CV).

Nimatumaini yangu kwamba maombi yangu yatakubaliwa kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

Wako mtiifu,
……………….……….
LIGWA BUNDALA

You might also like