Professional Documents
Culture Documents
MAMBO YA KUZINGATIA
1. Mwanahisa atahudhuria mkutano huu kwa gharamia yake mwenyewe, na anatakiwa aje na
nakala za Depository Certificate, pamoja na kitambulisho cha uraia, kadi ya mpiga kura,
leseni ya udereva au hati ya kusafiria kwa kumtambulisha.
2. Mwanahisa anayestahili kuhudhuria mkutano na kupiga kura ana haki ya kuteua mwakilishi
ahudhurie kwa niaba yake, iwapo yeye atashindwa kufanya hivyo, kwa kuzingatia
vipengele vya katiba ya kampuni.
3. Nakala za fomu za uwakilishi zinapatikana kwenye ofisi za NICOL zilizopo Na.11 Barabara
ya Serengeti, Mikocheni "B'; Dar es Salaam, au kuziomba kwa barua pepe kupitia
invest@nicoltz.com. Fomu za uwakilishi zirudishwe kwenye ofisi za kampuni sio chini ya
masaa 48 kutoka saa ya mkutano.
4. Nakala za Taarifa ya Mwaka zitapatika kuanzia tarehe 23 Oktoba 2019, maombi yatumwe
kwa barua pepe kwa irene@nicoltz.com.
Benjamin S Mwakagamba
Katibu wa Kampuni
28 Septemba 2019