You are on page 1of 1

Hatua za kufuata katika upimaji

Kiwanja/shamba

1.UKAGUZI WA KIWANJA/SHAMBA

a) Kuchukua alama (Coordinates) za eneo husika kwa kutumia kifaa maalum kiitwacho GPS (Global
Positioning System).

b) Alama (Coordinates) za kiwanja zikishachukuliwa hupelekwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo


ya Makazi au Halimashauri husika katika idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kwa ajili ya kupatiwa
Mchoro wa Mipanngo Miji wa eneo huaika.

c) Kwa kutumia mchoro wa Mipango Miji utabaini eneo unalotaka kupima limepangiwa Matumizi gani.
Linaweza kua limepangwa kwa ajili ya Makazi, Viwanda, Biashara, Huduma za jamii, Hifadhi au eneo
hatarishi, hivyo sasa ni muhimu kujua.

2. KIBALI CHA UPIMAJI

Mmiliki halali wa eneo husika ataandika barua Halmashauri husika akiambatanisha vithibitisho kua eneo
ni lake ili apatiwe kibali cha Upimaji.

3. UPIMAJI

a) Kama eneo halina Mchoro wa Mipango Miji (TP- Drawing), Mchoro huandaliwa kwanza kwani upimaji
hauwezi kufanyika bila kuwepo Mchoro wa Mipango Miji.

b) Kama eneo lina Mchoro wa Mipango Miji Upimaji huanza mara moja na Mpima (Land Surveyor) kwa
kushirikiana na Mtaalam wa Mipango Miji (Town Planner) Kwa kutumia vifaa Maalum kama Total
Station au RTK.

c) Baada ya uupimaji kukamilika na Mawe (Bicons) kupandwa kwenye kiwanja husika faili huandaliwa na
Kupelekwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi kwa ajili ya ukaguzi na kisha kurudishwa
kwa Mteja kwa ajili ya kufuatilia hati (Tittle deed)

Kwa Maswali, Maoni au Ushauri tuwasiliane kupitia

You might also like