You are on page 1of 2

Watumiaji wengi wa barua pepe (e-mail) wanapoingia kwenye uwanja wa kutuma ujumbe katika akaunti

zao ama iwe Gmail, Yahoo, Microsoft Outlook, Live Mail, na Mozilla Thunderbird, kuna sehemu
inayoonesha CC na BCC.

Lakini wapo baadhi ambao wamekuwa hawaelewi nini maana ya hizo herufi na nini matumizi yake
kuwepo hapo.

Maana ya CC na BCC

CCing inasimama badala ya ‘Carbon Copying‘ na BCCing inasimama badala ya ‘Blind Carbon Copying‘.
Zote mbili, CC na BCC zinakuwezesha kuwatumia watu wengi kwa wakati mmoja ujumbe au mafaili
unayokusudia kuwapelekea.

Kuona na kutumia CC au BCC ni pale unapofungua uwanja wa kutuma barua pepe yako sehemu ya
kuandika barua pepe kwa unayemtumia ndipo utapoona hizo CC na BCC.
Yaani unaweza kuwatumia ujumbe kwa njia ya barua pepe watu 20 au zaidi kwa wakati mmoja bila ya
kupata taabu ya kumtumia mtu mmoja mmoja; ni kitendo cha kuweka barua pepe zao kwenye kipengele
cha BCC/CC na kuwatumia mara moja.

Pamoja na kufanana kwa kazi ya kuwatumia watu wengi kwa wakati mmoja, lakini kuna tofauti ndogo
baina ya CC na BCC:-
Unapotumia njia ya ‘CC’ kuwatumia watu wengi ujumbe, ni kwamba kila mmoja ataweza kuona orodha
kamili ya wapokeaji wengine waliotumiwa ujumbe huo; kila aliyetumiwa ataona na barua pepe za
wengine waliotumiwa ujumbe kama wake.

Kama utahitaji kuwatumia watu wengi ujumbe wa aina moja na kila mmoja asijue mwingine aliyetumiwa
basi matumizi ya ‘BCC’ yatakuhusu. Kupitia kipengele cha BCC kwenye barua pepe utaweza kuwatumia
watu wengi lakini kila mmoja ataona ujumbe wake bila ya kujua kama kuna mwingine ametumiwa kama
huo.

You might also like