Professional Documents
Culture Documents
2022 Joining Irugwa Sekondari-1
2022 Joining Irugwa Sekondari-1
MZAZI/MLEZI WA ………………………………………..................
…………………………………………………….
KUFUNGUA SHULE
Shule itafunguliwa tarehe 17/01/2022 na masomo yataanza mara moja na mwisho wa
kuripoti ni tarehe 30/01/2022 iwapo hutaripoti hadi tarehe hiyo utahesabiwa kuwa umekataa
nafasi uliyopewa, hivyo nafasi itahesabiwa kuwa wazi na itajazwa na mtu mwingine..
MAELEKEZO MUHIMU
Siku ya kuripoti unatakiwa kuja/kukamilisha maelekezo yafuatayo;
A. SARE ZA SHULE
i. Sketi mbili za za rangi ya blue iliyokolea (dark Blue) isiyo na michirizi ndefu hadi kiwiko cha
mguu kwa wasichana na suruali mbili blue iliyokolea (dark Blue) isiwe modal kwa wavulana.
ii. Shati mbili nyeupe za mikono mifupi za tetron
iii.Tai moja (dark Blue)
iv.Viatu vyeusi vya ngozi vya kufunga na kamba , visiwe na visigino virefu
v. Soksi nyeupe jozi mbili
vi. T-shirt moja rangi ya blue ya kola (wanafunzi wote )
Vii.Wavulana T-shirt moja rangi ya damu ya mzee (inapatikana shuleni) na suruali ya kijivu
iliyokolea kwa ajili ya shughuli za nje
viii. Wasichana gauni mbili za kijivu iliyokolea mshono wa solo ndefu kwa ajili ya shughuli za
nje
ix. Sweta moja Blue iliyokolea (dark blue) kwa wanafunzi wote
x. Raba za michezo jozi moja
xi. Track suit moja rangi nyeusi na bukta moja rangi nyeusi kwa ajili ya michezo
xii) Raba za michezo
N.B mahitaji haya ni muhimu mwanafunzi afike nayo siku ya kureport shuleni, nguo za
nyumbani haziruhusiwi. Mwanafunzi hatapokelewa asipo kamilisha mahitaji haya