You are on page 1of 3

Barua ya wazi kwa Afrika

Sanduku la barua Afrika

Africa.

YAH: KUPOKEA UGENI NDANI YA JAMII YA AFRIKA UVIKO-19.

Husika na kichwa cha habari, Apo awali taifa la Afrika lilipata fursa isio adhimu ya kupokea
wageni tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya waandaaji shughuli iyo isio adhimu kwa Afrika ya
kuletewa wageni hao bila mwaliko kutoka Afrika ila tu kwa matakwa ya waandaaji wa wageni hao,

Hapo awali tulishapokea wageni kama Polio, Kifua kikuu, Pepopunda, Dondakoo, Kifaduro, Homa ya
ini, Homa ya uti wa mgongo, Surua, Nimonia na Rotavirus izo ni chanjo ambazo zipo ndani ya mwili wa
Afrika ila zote amezibeba tangu apo awali na anaishi nazo wala hazikupotea katika mgongo wa Afrika
na hakuna media wala wanasiasa waliovalia njuga kuhoji ujio wa ugeni huu na uwepo wake huu ni wa
muda gani.

Tukapokea wageni wengine ndani ya jamii wakiwemo wakina malale, ugonjwa wa vikope unaoathiri
macho, kichocho, upofu na matende,kipindupindu, hawa wageni wanagalimu sana maisha ya Afrika
kwa ukubwa sana lakini hakuna anayesimama adharani kuwasema wageni hawa kwa sauti ya
kuchukizwa nao sio media,wala wanasiasa wote kimya ambapo tungepatiwa chanjo ya maambukizi
haya tungeona ni msaada mkubwa kuliko kukaa kimya kana kwamba si tatizo sugu kwa Afrika na jamii
yake na kabla hatujatua mzigo huo sasa tumempokea uviko-19.

ila Afrika tumebeba wageni hawa kimya maisha yanaendelea apa mgeni maarufu na
mashuhuri ni uyo Malale na njaa hawa kwenye orodha ya kuchukua maisha ya wana Afrika kwa kasi
wana kasi kuliko wageni wote ambao tumewahi kuwapokea mpaka sasa wakifatiwa na ila uyu Mgeni
njaa ambae nae si maarufu na mashuhuri kwa media na wanasiasa ila kwa jamii ya Afrika
tunamtambua kama namba moja kwa kuchukua maisha ya wana wa Afrika kuliko mgeni yeyote yule
uyu njaa yeye upitia njia ya vita ya wenyewe kwa wenyewe kama inavyoitwa ila hao wenyewe kwa
wenyewe hawana ata technolojia ya kutengeneza izo siraha za kivita ila wanazo mmmh Afrika pole
kwa majukumu.

Pia kuna uyu Mgeni Ebola,uyu uja kila anapojisikia bila kugonga hodi pia hanaga mwaliko pia upenda
kutembelea maeneo yenye rasilimali nyingi sana kwenye mgongo wa Afrika, basi atakaa apo mpaka
mauti ziwakute wana wa Afrika wa kutosha ndipo mwenye kumleta mgeni uyo atapojisika kumtoa
mgeni wake uja na madege makubwa na askari wakakamavu na kuzoa hazina ya mali lukuki na
kupakia na kuondoka na mgeni uyo Ebola na uku nyuma akiacha ivyo vita vya wenyewe kwa
wenyewe vikiendelea na mgeni njaa akitawala na kuchukua maisha ya wana wa Afrika.ila mgeni Ebola
hanaga kupotea yeye uludi mala kwa mala kwa mtindo ule ule na kuja kuchukuliwa kwa gharama
kubwa aswa.
Kuna uyu mgeni mrembo UKIMWI mashalaah kimwali uyu ni maarufu yeye amefanikiwa kudhuru
mataifa mbalimbali ulimwenguni ila walimdhibiti ila apa kwetu Afrika amepata umaarufu sana kuliko
ata uyu anayepigiwa chapuo kwa sasa Uviko-19.

Kwa uyu mgeni Ukimwi apa kwetu kuna babu yetu alishawahi kusema”mgeni uyu amekaa mahali
pabaya” yani kwa sisi Afrika alituonea kuja kwetu kwani aliingia mpaka chumbani ingawa wageni karibu
yao huwa sebuleni lakini yeye alipitiliza mpaka kwa chumba yani aliingia Ikulu ya Afrika mmmh mgeni
uyu pambee lakini kwetu Afrika mgeni uyu tuliishi naye ingawa alichukua wana wa Afrika wengi sana
mpaka leo anaendelea kupukutisha jamii ya wana wa Afrika mpaka akawekewa na mifuko ya kumuifadhi
kwa yule anayeshindwa kumvumilia kumuepuka mgeni uyu japo haikuwa ngome ya kumzuia mgeni uyu
ingawa sasa umaarufu wake sio kiivyo sana kama ilivyo kwa mgeni uyu anayevuma ulimwenguni kote
alimaarufu uviko-19

Uyu uviko-19 ni mgeni mashuhuri aswaah mgeni ambaye ni maarufu kuliko wageni wa awali
ambao tuliowahi kuwapata sasa uyu ni wa tofauti sana kwani yeye wale waliomleta wamemleta kwa
shuruti aswah bila ridhaa ndani ya Afrika uku wakimtangaza kila kona ya ulimwengu huu kuwa ni lazima
tumpokee mgeni uyu UVIKO-19 maarufu kweli kweli kuliko umaarufu wenyewe.

Ila Afrika wenyewe walimpuuzia uyo uviko-19 kwani uyo uviko-19 ni Virusi vya korona yani jamii
kubwa ya virusi vinavyojulikana kusababisha magonjwa yanayoanzia homa ya kawaida hadi homa kali
kama vile Homa Kali ya Upumuaji ya Mashariki ya Kati (MERS) na Homa Kali ya Mfumo wa Upumuaji
(SARS). Sasa Afrika iyo homa ya upumuaji sio ajabu kwani Afrika imeishi na homa ya aina iyo kwa kipindi
kirefu na hakuna cha ajabu katika homa iyo, ila kwa kuwa mgeni uyo amekuwa tatizo kwao wao
wanaotawala ulimwengu sasa wameamua liwe janga letu pia Afrika ili watupandikizie chanzo yao tena si
kwa hiali ila kwa shurti kwenye mgongo wa Afrika.

Lakini Afrika kama wangetuuliza kwamba tunahitaji chanjo ya aina gani sisi jamii ya Afrika
tungependekeza chanjo ya Malaria,chanjo ya ukimwi,na ata chanjo ya njaa na vita ya wenyewe kwa
wenyewe,ila kutokana na unyonge wetu sisi uwa tunatupiwa tu kila uchwao,na sasa imekuwa tofauti na
zama za hapo hawali ambapo wageni walikuwa wakiingia kimya kimya na kujikuta wameshafika mpaka
sebuleni kwetu na tukaishi nao kama ilivyo kwa ukimwi ila sasa tumeshulutishwa kumpokea mgeni uyu
uviko-19 kwa shuruti na vitisho na matangazo lukuki kwenye vyombo vya habari,

Uku tukitakiwa kutoa takwimu za mgeni uyu uviko-19 kwamba kaingia kwa raia wangapi na
kachukua maisha ya raia wangapi ili tu azidi kuleta taaruki na hofu kwenye jamii zetu, ila cha kushangaza
pamoja na jitihada zote za kumpandisha chati uyo uviko-19 bado kitakwimu hajafikia kasi ya njaa
ambayo kwa Afrika ndio mpaka sasa anaongoza kuchukua maisha ya raia wetu kwa kasi ya juu ila
hakuna anayedai takwimu wala kuweka juudi za kumzuia au kumpunguza kasi ya kuchukua maisha ndani
ya jamii zetu za Afrika.

Hao ni wageni wachache kati ya wengi ambao Afrika imewapokea tangu kuumbwa kwa Taifa la Afrika
lakini Afrika bado ni Afrika na Afrika ni Afrika taifa la Mungu.

KARIBU KWETU,KARIBU AFRIKA.


Theostell1986@gmail.com

Theostell1956196119841986@Africa.home

You might also like