You are on page 1of 1

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA


MTIHANI WA MOCK KIDATO CHA NNE 2016
SHULE YA SEKONDARI NYAMWEZI
SOMO: KISWAHILI
CHANGAMOTO ZILIZOBAINIKA KATIKA MTIHANI WA UTIMILIFU KISWAHILI
KIDATO CHA NNE, NI KAMA IFUATAVYO;

a) Maelekezo ya mtihani hayakuwa sahihi, kwani yalikinzana kutoka sehemu moja hadi
nyingine
b) Mtihani haukuwa na kipengele cha ufupisho katika sehemu ya kwanza kwenye swali la
UFAHAMU.
c) Vilevile mtihani huu haukutoa muda wa kutosha kwa wanafunzi wa maandalizi hivyo ni
changamoto kwa wanafunzi.
d) Mtihani huu haukutoa mwongozo wa usahihishaji hivyo ilileta ugumu sana katika
kuandaa mwongozo huo pamoja na usahihishaji.
e) Mtihani huu pia haukuandaa posho kwa wasimamizi, wasahihishaji hivyo kupelekea
kushindwa kukamilisha zoezi hilo kwa wakati uliotolewa.

MAPENDEKEZO YA UBORESHAJI WA MTIHANI HUO

a) Muda au wakati wa kufanyika mtihani huu uzingatiwe ili kuwapa wanafunzi muda
mwingi wa kujiandaa.
b) Mtihani huu lazima uhakikiwe vizuri ili kuepuka mkanganyiko wa maswali yaliotolewa
kwa kufuata maelekezo.
c) Vilevile mwongozo wa usahihishaji lazima utolewe ili kurahihisisha zoezi la usahihishaji
kwa muda uliotolewa.
d) Waandaji wa mtihani huu waakikishe wanawapa vipaumbele wanaohusika na shughuli
zote za usimamizi na usahihishaji ili kuwapa moyo katika kufanya kazi kwa juhudi.

IMEANDALIWA NA:

_______________________

PASKAL A. KALINGA

MWALIMU WA SOMO

You might also like