You are on page 1of 2

SI UMBEA...

1132H

(SPONSORED BY KENYA RURAL ROADS ASSOCIATION)

Hebu tuangalieni,sisi tumetoka mbali

Huko kwetu kijijini,twasema tena ni mbali

Tumefika tamashani,barabara nzuri kweli

Si umbea ni ukweli,barabara ziko shwaa!

Maendeleo kabambe,barabara zavutia

Wanakijiji tutambe,huduma twapata pia

Mapato shamba turambe,sokoni fikishe pia

Si umbea ni ukweli,barabara ziko shwaa!

Bidhaa zinafikishwa,na huduma teletele

Sipitali twafikishwa,twapata madawa tele

Benki pia meboreshwa, tunapata hela tele

Si umbea ni ukweli, barabara ziko shwaa!

Gari sasa hazikwami,barabara i sambamba

Umaridadi wa lami,bodaboda zinatamba

Tunaukuza uchumi,na maisha yanabamba

Si umbea ni ukweli,barabara ziko shwaa!


Ajali zimepungua,na maafa kupotea

Wa salama abiria,njiani wakitembea

Alama zi tele pia,dereva kuangalia

Si umbea ni ukweli,barabara ziko shwaa!

Mashinani kusafiri,nauli kidogo tu

Sasa ni jambo la kheri,barabara huko kwetu

Pikipiki bajaji gari,salama zabeba watu

Si umbea ni ukweli, barabara ziko shwaa!

Wageni wamefurika,kisa barabara nzuri

Kila siku wanafika,watuletea mazuri

Kwetu kumechangamka,mashinani ni kuzuri

Si umbea ni ukweli, barabara ziko shwaa!

Vyombo vya kusafiria,katu haviharibiki

Viko wima nakwambia,tairi hazitoboki

Faida twajipatia,barabara tia tiki

Si umbea ni ukweli, barabara ziko shwaa!

You might also like