You are on page 1of 2

26 alphabets zimejaza library za dunia mzima na vitabu, knowledge ya binadamu origin ya taabu, fear of

God ikiwa ndio beginning ya wisdom, rainbow ya ideas mvua ya fikra ukibrainstorm, verse moja ya Biblia
ni nzito kuliko uzani wa dunia, dhambi ikiendelea kuongeza uzito wa dunia, dhambi ikichafua uzito wa
dunia, dhambi ikipunguza miaka ya binadamu na dunia, mwili ya binadamu ni vumbi, hupeperushwa na
upepo wa dhambi, uzuie upepo wa dhambi kukublow off kama foundation yako ni rock of ages, miaka
unataka kuishi iko embedded kwa rock of ages, wengi hawaelewi kuwa born again, ni muhimu kuliko
kuzaliwa ndani ya maternity, sasa naishi ndani ya hizi words kuepuka jela ya reality.

Kwake Yesu unafaa kusimama hata kama huna cha kutumaini, kuja ukuwe mwana wake, Christ atakupea
maji ya uzima, usiende kwa Club kuCHROME kwa KREST unaZIMA. Atakujaza na Holy Spirit wengine
wakijaza tumbo zao na WHISKEY na SPIRITS, yeye ndiye mwamBAR….so sijui ni nini unafanya kwa BAR.

Kumbuka Paulo na Sila walitoa LOCK bila WINES and SPIRITS but na HOLY SPIRIT, kazi ya kukata maji
wachia MOWASCO. Sisi wote tunajua Christ ni BABA YAO, yeye ndiye alitoa Ugandans kutoka kwa brutal
reign ya Idi Amin Dada, situation yako sio kitu, mnona hauAmini dada?... Ati ukimbelieve, maovu yako
anayaita past, cheki John 15:14, God anadai atakuwa beshte yako if you do as He commands you to do,
anadai hakuna kitu umenyimwa, all you have to do is ask, na atadeal na the elephant in your room,
kwake hakuna a hard task. …..Kwa hii life nimelearn that friends ni muhimu kuliko benefits, nimelearn
hata kama hakuna vacant room, there is still room for improvement, nimelearn that, hata kama
hukuenda shule, bado uko na class, fullness and happiness hutoka heaven, na hauhitaji capital kumind
your own business, juu sio biashara zote huturn out kuwa business, learn to love the people God has
rented you, because He will need them someday, na 1st time yako, inaweza kuwa ndio last time ya
mwingine.

Dear junior youth, when our parents were growing up STD only meant STANDADRD, AID(s) was simply
help, but hii time tunalelewa ni tricky sana, coz saa hii tunabelieve ati sex ni kitu essential but wao
waliijua kama tabia mbaya, Sugar-mummy ilikuwa ile time unatandikwa na mamako juu ya kukula
sukari, soap operas zilikuwa zinakam pas our bed times, na hizo enzi watu hawakuwa wanableach, balck
women walikuwa bold, wakiclaim wako beautiful, na ni hard kuwapea advice sometimes wakati wengine
wetu tuko caught up in the vice, but sisi tumelelewa na maadili mema, wacha tukuwe different na
tujiamini, ati hata kwa peer pressure tunaweza kupinpoint service we can trust. Nilikuwa yule kifaranga
mwewe hangeguza hata kama ningeshinda outdoors all day, but believe it or not, with the help of God,
my mom moved mountains for me, na influence yake ndio reason mimi hucheki obstacles kama mole
hills, hakuwa mwaashi but alinizibia nyufa ndio nisilive kama ruins, no medical training but hakuna
wounds alishindwa kuheal, STRENGTH OF A WOMAN.

In Mathew 6:33 Biblia inakukumbusha, “But seek first His Kingdom and His righteousness, and all these
things will be given to you as well.” Jaribuni kuguza moyo wa Mungu mwenyezi, muone miujiza na
baraka zitakavyo wakujia, yeye alisema mjaribuni muone kama hatafungua Baraka zenu, mbona
mfanane na watu wawekao kwenye mifuko iliotoboka? Mtoleeni Mungu kadri ya mnavyopata, ni tabia
ya Mungu na hicho ndicho chanzo chz Baraka, toeni mali zenu, saidieni maskini, na hata wahitaji na
mtaleta utukufu kwa jina la baba, kama vile Cornelius alisaidia maskini na kuleta utukufu mbele za
Mungu. Digitalization ingekam kumaliza racism coz back then screens zote zilikuwa BLACK & WHITE, but
then kukawa na more colors na kila race ikataka kuwa superior, tukasahau ati yule anaown the supreme
CROWN alitu PAINT differently with a purpose, na inside tuko all the same, nje ni rangi tu design ya
mabuyu, God anakupenda hata bila make up, you are a beauty from heaven, and that’s not a thing I
made up, imeandikwa kwa Bible ati uliundwa na image ya Mwenye-Enzi, alichagua fine soil for your
build up, you are not perfect, kuna cracks hapa kule, that explains how Jesus The Light gets in you, so
shetani akingoja tubishane nay eye mwambie uko busy na map, safarini to Brighter days. In the Name Of
The Father, The Son and the Holy Spirit. Amen.

You might also like