You are on page 1of 52

Hija na Umrah

Namna ya Kuhiji na Kufanya Umrah

Ghalib Yusuf Tamim Baalawy


HIJA NA UMRA – HATUA KWA HATUA

‘… Na kwa ajili ya Mwenye-ezi-Mngu imewajibikia watu


wahiji kwenye Nyumba hiyo (Kaaba), kwa mwenye kuiweza
njia ya kwendea….Surat Al’Imran 3:97.

‘Na timizeni Hija na Umra kwa ajili ya Mwenye-ezi-Mngu…’


Surat Al-Baqara 2:196.

‘Hija ni miezi maalumu. Anaekusudia kufanya Hija katika


miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu, wala asifanye
vitendo vichafu wala asibishane (asishindane wala
kugombana) katika Hija…..Surat Al-Baqara 2:197.

Imepokewa kwa Abu Huraira kuwa Mtume (S.A.W.)


amesema: ‘Mwenye kuitimiza Hija ikawa ndani ya Hija hiyo,
akakatazika na kujizuia na uchafu na matusi, basi hujaji huyo
hurudi kwao hali amesafishifika kana kwamba amezaliwa
upya na mamake siku hiyo.’

Hija ni safari ya mara moja tu katika umri wa Waislamu


wengi. Hija ni nguzo ya tano katika Nguzo Za Uislam. Kwa
vile Hija ni ibada, ni lazima itimizwe kwa njia ya amani na
kwa dhati ya moyo wako wote. Kuna mambo mengi mepesi
na njia nyingi za sahali, zinazoweza kukutayarisha wewe
kimawazo, na kukutia katika hali ya kuweza kuikamilisha
amali hii ya kipekee vile inavyotakiwa.

Kwanza kabisa: Niya yako ni lazima iwe ni kuitimiza amali


hiyo ya Hija kwa ajili ya Mwenye-ezi-Mngu peke Yake.

 Gharama zako za Hija, zote ni lazima ziwe ni pesa za


halali.
Madeni yako yote yalipwe kabla ya kuingia safarini,
na kila jukumu lako linalohitajia fedha ni lazima

1
ulikamilishe kwanza kabla ya kuanza safari yako ya


Hija.
Ni lazima ujitahidi kwa dhati ya moyo wako
kupatana na kila ulokuwa na utesi nae. Na uwatake
msamaha wale ulowakosea na kuudhiana nao kwa


njia yoyote ile.
Kumbuka kuwa safari hii huwenda ikawa ni safari
yako ya mwisho. Kwa hivyo matayarisho yako
nikujisafisha na kujitayarisha kuonana na Mola wako,
hali yakuwa Yeye yuradhi na wewe, na wewe uradhi
na Mola wako (lau utapatikana na ajali ya mauti yako
ukiwa ndani ya Hajj).

Kijitabu hiki ni jaribio la kumtayarisha hujaji katika amali


yake hii ya kipekee. Ningependa kushirikiana na
kukugawanyia kile nilicho kipata katika Kitabu cha ‘Fiqh –us
– Sunnah (Fiqh 5.125)’ katika CD ya Alim, na ‘Hatua kumi
na tano za kuitimiza amali ya Hija’ zilochapishwa na
Musisitul Waqf Islamiyah (alelmyah@waqf.com) pamoja na
kitabu cha ‘Amali za Hijja’ cha Sheikh Al-Amin bin Ali
Mazrui.

Bibi mmoja alimuomba Sh. Al-Amin amuandikie amali hiyo


kwa njia nyepesi. Sheikh Muhammad Kassim Mazrui ambaye
ndie aliyekuwa mwanafunzi mkubwa wa Sh. Al-Amin
akaipiga chapa ili kiwafae wengine.

Chanzo cha kajitabu hiki ni matayarisho tulokuwa


tukiyafanya mimi na mke wangu Maryam kwa amali yetu ya
Hija. Tukiwa katika hali hiyo ya matayarisho swahibu yangu
mmoja akaniomba nimpe na yeye shuhudiani hiyo, kwani na
yeye pia ameazimia safari hiyo ya Hija. Katika hali hiyo ya
matayarisho nikiyapitia na kuyarudia makala nilokuwa nayo,
tukapitiwa na fikira na kujiuliza kwa nini tusingechapisha

2
makala hayo kama kijitabu ili kiwanufaishe mahujaji
wengine?

Hili ni jaribio tu la kukugawanyia na wewe faida ya kijitabu


hiki, Insha-Allah. Kinaweza kutumika kama kiongozi chako
katika kila amali inayohitajika wakati wa Hija na Umra yako.

Ilitubainikia kuwa ni vigumu sana kwa mtu, kuweza


kukumbuka kila kinacho hitajiwa katika kuitekeleza amali
hizi, pamoja na dua mbali mbali zilizopendekezwa. Tafadhali
kitumie kitabu hiki, uwe nacho mkononi kila mara ili
kikusahilishie katika njia na amali mbali mbali zinazohitajika.
Kikusaidie wakati unapotoka kutoka kwenye amali moja, na
huku ukenda katika amali nyengine katika amali za Hija na
Umra.

Ni wajibu wako ujitayarishe vilivyo kabla hujaianza safari


yako hii. Njia ya pekee ni kujitayarisha vilivyo: kiimani,
kiafya na kinadharia/ kimawazo, ndipo utakapo weza
kutosheka kikweli katika safari hii ya Hija. Namuomba
Mwenye-ezi-Mngu akutakabalie amali yako ya Hija na Umra.
Mwenye-ezi-Mngu akutimizie, yawe ni mapitio ya
kukuridhisha katika maisha yako. Amin, Ya Rabbal Alameen!

Usitusahau na sisi katika dua zako – Insha’Allah.

Ghalib Yusuf Tamim,


20th November, 2006

3
Orodha na mpangilio wa Kitabu

1. Hajj na Umra kwa ufupi– Hatua Kumi na Tano..5


2. Aya zinazohusika na Hijja ……..….………….6
3. Mpangilio wa Hija na Umrah – Mtizamo .............9
4. Kuingia katika hali ya Ihram ..……….………….11
5. Ukisha ingia katika hali ya Ihram.…….………...13
6. Unapokingia Makka…………………….……….13
7. Unapoiona Alkaaba.………………….………….14
8. Ukiwa ndani ya Msikiti Mtukufu wa Makka…..16
9. Kufanya Tawaf na dua zilizopendekezwa..…….16
10. Sa’yi…………….………………………….........23
11. Hajj – Tarehe 8 Dhul Hijja……………….…........27
12. Jua linapochomoza - tarehe 9 Dhul Hijja.……...29
13. Arafah.................................................................. 30
14. Tarehe 10 Dhul Hijja……...…………………… 33
15. Linapo pinduka jua tarehe 11 Dhul Hijja.……....39
16. Tarehe 12 Dhul Hijja……..………….…………...40
17. Kafara unapokosea amali za Hija na Umra……...41
18. Namna ya kuvaa Ihram…………………………..44
19. Ziara ya Madina………………………………….45
20. Talbiya…………………………………………...48

4
15 14 13 12 11
Tarehe 13 Tarehe 12 Tarehe 11 Tarehe 11, 12,
Hatua 15 Dhul Hijja Dhul Hijja Dhul Hijja 13 Dhul Hijja
Za Tawaful * Kupiga * Kupiga * Mutalala
Kuitimiza Widai * Hii ni Siku mawe - mawe, Mina siku
(Tawaf ya ya mwisho ya (wakati ukitumia mbili au tatu
Amali Za
kuaga). kupiga mawe. unaoruhusiwa vijiwe za Siku za
Hija na
ni baina ya ulivyookota Tashriq yaani
Umrah * Dhuhr na Muzdalifah. tarehe 11, 12
Mutaondoka Maghrib). * Utapiga na 13.
Mina na * Waweza vijiwe saba:
kurudi zenu kuondoka - Jamratul * Ibada ilio
Makkah. ukimaliza Sughra - 7, bakia Mina ni
siku ya pili, - Jamratu kupiga
na kurudi lWusta – 7, mawe.tu.
Makkah. na -
Jamratul
Kubra -7.
1 10
*Ingia Nguzo za Hja Yanayo mlazimu Hujjaj Tarehe 10
katika Dhul Hijja
Ihram 1. Ihram 1. Awe Muislamu. 2.
mukifika Tawaful Mwenya akili * Mtakwenda
Ifadhah. 3. Aliye Baleghe. 4. Aliye Makkah
Miqat:
2. Sa’yi (baina ya huru – si mtumwa kufanya
*Vaa nguo Tawaful
Swafa na 5. Mwenye uweza 6.
zako za Marwa). Mwanamke afuatane na Ifadha na
Ihram. 3. Kusimama Mahrim. Sa’yi.
*Tia niya Arafah
ya Hija au . * Ukimaliza
Umrah. Namna tatu za Hija: umetoka
* Anzeni Tamattu Qiran Ifrad katika Ihram.
kusoma - Sasa uko
Kufanya Umrah Kufanya Hija na Kufanya amali huru hata wa
Talbiya - kuingiliana na
nyote kwa kwanza Umrah pamoja ya Hija peke
yake. mkeo au
pamoja, mumeo.
mukirudia Nia – Labbayka Nia - Labbayka Nia - Labbayka
Umrah Hajj-wal-Umrah Hajj
mara kwa * (Tahallul ya
Uingiye tena Kuchinja ni Hakuna kuchinja
mara mwisho).
Ihram na Uhiji lazima
Kuchinja ni * Utarudi na
lazima kulala Mina.
2 9
* Yalio Wajibu katika Hija Tarehe 10
Utakapofika 1. Kuingia katika 2. Kusimama Arafah Tarehe 9 Dhul Hijja
Masjidil Ihram kwenye Miqat D/Hijja - (Qiyamul Arafah)
Haram: 3. Kulala 4. Kupiga mawe Jamrah 3 siku za * Baada ya
* Muzdalifah siku ya Tashriq (Tarehe 11, 12 na 13) kuchinja
Hamusomi Arafah umetoka
tena Talbiya katika Ihram
5. Kunyoa au 6. Kulala Mina siku za Tashriq.
* Fanya (Tahallul ya
kupunguza nyele
Tawaf kwanza).
Qudum
Suna za Hija
* Sa’yi * Sasa una
baina ya 1. Kuoga kabla ya kuingia 2. Kusoma Talbiaya - uhuru wa
Swafa na katika Ihram wanaume wakiinua sauti kuyafanya yale
Marwah. 3. Kulala Mina tarehe 8 4. Ittiba’a - kuliacha wazi uliokatazwa
* Nyoa au D/Hijja bega la kulia katika Tawaf ukiwa katika
punguza 5. Ramal – kwenda mititi 5
6. Kulibusu Jiwe Jeusi Ihram,
nyele. yaani haraka haraka kwa (Hajaril Aswad) - isipokuwa
* Huu ndio wanaume katika ikiwezekana. Usipigane na kuingiliana na
6
2:197 Hija ni miezi maalumu. Anaekusudia kufanya Hija
katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala
asifanye vitendo vichafu, wala asibishane (asifanye
utesi) katika Hija. Na kheri yoyote mutakayo ifanya
Mwenye-ezi-Mngu anaijua. Na chukueni masurufu (na
mjiandalie). Na bora ya masurufu (na maandalio) ni
kujihifadhi na kumcha Mwenyez-ezi-Mngu. Basi nicheni
(muniogope) Mimi, enyi mulio na akili.

Ayah 198 Si vibaya kwenu kutafuta fadhila za Mola


wenu (na kufanya biashara zenu). Basi mutakapo rudi
kutoka Arafah mtajeni Mwenye-ezi-Mngu katika Mash-
aril-Haram (huko Muzdalifah), mkumbukeni (Mwenye-
ezi-Mngu) kwa ajili ya kuwaongoa. Na hakika kabla ya
kuwaongoa mulikuwa ni miongoni mwa wale walio
potea.

Ayah 199 Kisha ondokeni kutoka pale wanapomiminika


watu (Arafah), mumuombe Mwenye-ezi-Mngu maghfira
(msamaha). Hakika Mwenye-ezi-Mngu ni mwingi wa
kusamehe, Mwenye kurehemu.

Ayah 200 Na mukisha maliza kutekeleza ibada zenu (za


Hija), basi mtajeni Mwenye-ezi-Mngu kama mlivyokuwa
mukiwataja baba zenu, bali mtajeni zaidi Mwenye-ezi-

7
Mngu. Na miongoni mwa watu, kuna wale wanaosema
“Mola wetu tupe (mema) katika dunia”, wala hana fungu
lolote huko Akhera.

Ayah 201 Na miongoni mwao, wapo wanao sema “Ewe


Mola wetu tupe mema hapa duniani, na utupe mema
huko Akhera. Na utuhifadhi na adhabu ya Moto.”

Ayah 202 Hao ndio watakao pata fungu lao katika yale
walio yachuma. Na Mwenye-ezi-Mngu ni mwepesi wa
kuhisabu.

Ayah 203 Na mtajeni Mwenye-ezi-Mngu katika zile


siku zilizo hisabiwa (Siku za Tashriq – tarehe 11, 12
na 13 Dhul Hijja). Basi anae fanya haraka (kuondoka
Mina) katika siku mbili (hizo), hana madhambi. Na
mwenye kukawia (akaondoka siku ya tatu) pia hana
madhambi, kwa ajili ya kumcha Mwenye-ezi-Mngu.
Basi mcheni Mwenye-ezi-Mngu, na mujuwe kuwa nyinyi
mutakusanywa Kwake (Yeye Mwenye-ezi-Mngu).

8
9
10
Kuingia katika Ihram (Kuhirimia)

Utakapo fika katika Miqat (Pale mahali maalum palipo


wekwa kwa ajili ya Kuhirimia) wewe kama Hujaji watakiwa

 Upunguze masharubu yako


ufanye mambo yafuatayo:

 Upunguze nyele
 Ukate kucha
 Uoge na/au utawadhe
 Ujitie manukato
 Kisha uvae nguo zako za Ihram
 Kisha uswali rakaa mbili (sunnatul Ihram)
 Kisha utie niya ya kuhiji au kufanya Umrah au Hija
na Umrah (kama ulivyo kusudia).

Hija ya Tamattu ni bora zaidi kwetu sisi watu wa Afrika


Mashariki kwa sababu ya wepesi wa kutokuwa katika hali ya
Ihram kwa muda mrefu. Utahirimia kufanya Umrah, kisha
utoke katika hali hiyo ya Ihram. Siku ya Hija itakapo fika
(tarehe 8 Dhul Hijja, utahirimia tena kwa sababu ya Hija.

Niya ya Umra na Hija:

1. Natia niya ya (Nawaitul


kufanya Umrah, Umrata wa- ‫ن يت لع‬
na naingia katika
hali ya Ihram,
ahramtu biha,
Lillahi Taala)
‫أح مت ب ه‬
kwa ajili ya ‫تع ل‬
Mwenye-ezi-
Mngu, Aliye
Mtukufu.

11
2. Natia niya ya (Nawaitul
Hija, na naingia Hajja wa- ‫ن يت لحج‬
katika hali ya
Ihram, kwa ajili
ahramtu biha,
Lillahi Taala)
‫أح مت ب ه‬
ya Mwenye-ezi- ‫تع ل‬
Mngu, Alie
Mtukufu.

Kuvaa nguo za Ihram (kwa mwanamume) na kutia niya ni


wajibu wa Hija na Umrah. Wala Hija na Umrah hazitotimia
bila ya kufanya hivyo.

Si lazima kutaja namna ya Hija ulokusudia – ikiwa ni Ifrad


(kufanya amali ya Hija peke yake), Tamattu ' (kufanya amali
ya Umrah kwanza, baadae ukafanya amali ya Hija) au Qiran
(ukafanya amali ya Hija na Umrah kwa pamoja bila ya kutoka
katika Ihram). Yeyote anae tia niya ya Hija bila ya kuitaja
Hija aliyo ikusudia, kuhirimia kwake kumekamilika. Mtu
aweza akafanya aina yoyote ya Hija, katika namna tatu za
Hija, kama tulivyo zitaja hapo juu.

Mtu akisha ingia katika hali ya Ihram, basi inamlazimu aanze


kusoma Talbiyah (wanaume wanatakiwa waisome kwa kutoa
sauti). Vile vile inatakiwa isomwe kila munapo panda na
kushuka milima, munapo kutana na wenzenu, wakati wa
asubuhi na baada ya swala za faradhi – almuradi muisome
Talbiyya katika kila hali na kila wakati.

12
(Labbeika Allahuma Labbeik, Labbeika La-sharika laka
Labbeik. Innal Hamdah, wa-nne’mata Laka wal-Mulk. La’
shariika Laka).

‘Labbeika! Ewe Mwenye-ezi-Mngu (Nipo chini ya Twaa


Yako), Labbeika! Huna mshirika, Labbeika! Hakika sifa
njema zote, na neema zote ni Zako Wewe. Na Ufalme wote ni
Wako! Huna mshirika!

Ukisha Ingia Katika Hali Ya Ihram:

 Ujiepushe na kufanya mapenzi, na uhakikishe


umejiepusha na kila litakalo kupelekea kufanya


mapenzi.
Jiepushe na utesi wowote, na vile vile jitahadhari na


matusi na kulalama na kulaumu wengine.
Huna ruhusa kufunga ndoa wala kuhudhuria harusi
yoyote – huu sio wakati wa ndoa wala harusi ni


wakati wa ibada.
Hujaji mwanamume hana ruhusa kuvaa nguo zilizo
shonwa, wala kuvaa viatu vya kufinika kisigino –


utavaa champali au makubadhi.


Hujaji mwanamke hana ruhusa kufinika uso wake.


Mwanamume hana ruhusa kufinika kichwa.


Huna ruhusa kutumia manukato.


Usikate nyele wala usikate kucha.


Huna ruhusa kuwinda wanyama.
Huna ruhusa kukata miti wala majani wala nyasi
katika maeneo ya Haram ya Makkah – haya ni
maeneo matukufu.

2. Unapoingia Makkah

Soma dua ifuatayo, hii ni moja katika dua zilizo pendekezwa:

13
‘Ewe Mwenye-ezi- (Allahumma
Mngu! Hii ni
Haram Yako na
haadha
Hara’muka, wa-
‫ل م ه ح مك‬
Amani Yako, basi Amnuka. ‫أم ك فح لح‬
iharimishe nyama Faharrim ‫م شع‬
yangu, damu Lahmiy, wa . ‫بش ع ل‬
yangu, nyele zangu damiy, wa
na ngozi yangu na shaariy, ‫ل م ه لح‬
Moto wa waBashariy ala- ‫ح مك ل ب‬
Jahannam. nNar. Allahumma ‫أمن أم ك‬
‘Ewe Mwenye-ezi- hadhal – ‫لع ج ت من‬
Mngu! Haram hii Hara’mu
ni Haram Yako. Hara’muka, wal- ‫با بعي‬
Na mji huu ni mji baladu baladuka, ‫ب ن كتي‬
Wako. Na Amani Wal-Amnu ، ‫أع ل لسي‬
ya mji huu ni
Amani Yako. Na
Amnuka. Wal-
abdu jiitu min
‫أسألك أ‬
Mja (mimi Bila’di bai’din, ‫ب حض‬ ‫تست‬
nilokuja kuhiji) ni bidhunubi ‫ع‬
mja Wako. kathiratin, wa- ‫أ ت خ فسيح‬
Nimetoka miji ya amali Sayyiatin.
mbali nikiwa na As-aluka an- ‫ج تك‬
madhambi mengi tastaqbilaniy bi-
na amali mbaya – mahdhi
nakuomba Af-wika, wa-
unipokee kwa antudkhilaniy
Msamaha Wako. fasiha Jannatika.)
Na unitie katika
Pepo Yako.

 Ni vizuri kwa mwenye kuhiji aingie Makkah kwa


upande wake wa juu.

14
 Ikiwezekena ni vizuri kuoga kabla hujaingia Makkah
kwenye kisima cha Dhi Tuwaa, mahali panapoitwa


Zahir.
Kisha uwende moja kwa moja mpaka kwenye Al-
Kaaba, uingie Msikiti Mtukufu wa Makkah. Ni vizuri
kiingia kwa mlango unaitwa Babu-s-Salaam, na huku
ukisoma dua ya kuingia msikitini. Uingie kwa
heshima kubwa na kwa taqwa. Kumbuka kuwa kabla
ya hapo ulikuwa bado ukisoma Talbiyya. Ukisha
ingia Msikiti Mtukufu hapo Talbiyya haisomwi tena.

Unapo-iona Al-Kaaba Unapo-iona Al-Kaaba, inua mikono


yako na umuombe Mwenye-ezi-Mngu kwa khushui dua
ifuatayo:

‘Hapana Mola mwenye (La ilaha illa


haki ya kuabudiwa,
isipokuwa Mwenye-
Llahu wa-Llahu
akbar.
‫اإله إاّه ه‬
ezi-Mngu peke Yake.
Allahumma anta ‫أك ل م أنت‬
Mwenye-ezi-Mngu
ndiye Mkubwa kuliko sSalaam, wa- ‫لسا م ك‬
kila kitu. Ewe Mwenye- minka sSalaam. ‫لسا حي ب‬
ezi-Mngu! Wewe ndiye HayyinaRabbana
Amani, na Kwako bi sSalaam. ‫ب لسا ل م ه‬
ndiko itokako Amani. Allahumma ‫بيتك فز تش ي‬
‫تعظي م ب‬
Tuhuishe, Ewe Mola
wetu kwa amani. Ewe
hadha Baituka,
Mwenye-ezi-Mngu! Hii fazid-hu ‫من حجه‬
tashreefan, wa-
‫عت تش ي‬
ndiyo Nyumba Yako.
Basi izidishie heshima, taadhiman, wa-
utukufu na utisho. Na mahabattan. Wa- ‫ت ي م ب‬
umzidishie mwenye
kuikusudia kwa Hija
zid man hajja-hu ‫ب‬
na Umrah, heshima,
wa-atamarahu
utukufu, utisho na tashreefan, wa-
wema - Amin. takrimman, wa-
mahabattan wa-
birran).

15
 Ukisha ingia ndani ya Msikiti Mtukufu, nenda moja
kwa moja mpaka Hajaril Aswad, ulibusu


ikiwezekana.
Na ukishindwa kwa sababu ya wingi wa watu, basi
liashirie kwa mkono wako wa kulia, kisha uubusu
mkono wako. Usipiganie kulibusu ukaharibu Hija
yako! Kuliashiria yatosha na yakubalika.

Ukiwa ndani ya Haram – Msikiti Mtukufu wa Makkah

Baada ya kulibusu Hajaril Aswad, utaanza Tawaf kama


ifuatavyo:

 Simama kwenye mraba wa kuonyesha mwanzo wa


Tawaf. Elekea upande wa Hajaril Aswad na ukiinue
kiganja chako cha mkono wa kulia, ukikielekeza
upande wa Hajaril Aswad na kutamka maneno
yafuatayo:

‘Kwa Jina la (Bismi-Llahi, wa-


Mwenye-ezi-Mngu,
Mwenye-ezi-Mngu ni
Llahu akbar.
Allahumma
‫بسم ه ه أك‬
Mkubwa kuliko kila
i’manan bika, wa- ‫ل م إي ن بك‬
kitu.Ewe Mwenye-ezi-
Mngu, (nafanya haya) tasdiqqan ‫تص ي ب ت بك‬
kwa kukuamini Wewe bi-kita’bika, ‫ف ء بع‬
na kukisadiki Kitabu wawafan bi-
Chako, Na kwa ahdika wa- ‫ت ع‬ ‫ع‬
kuitekeleza ahadi waadika. ‫لس ن يك مح‬
‫ص ه ع يه‬
Yako na waadi Wako,
na kufuata Suna ya
Wattibaan li-
Mtume Wako sunnati Nabiyyika ‫سم‬
Muhammad (Rehema Muhammadan
na Amani za Allah Swalla Llahu
zimshukie). Alaihi wa sallam).

16
Katika mizunguko mitatu ya mwanzo ni suna kwa wanaume
kwenda mititi (kwenda haraka haraka). Vile vile wanaume

 Mizunguko mine iliobaki utatembea kwa hatua za


wanatakiwa kuliwacha wazi bega lao la mkono wa kulia.

 Ni suna katika kila mzunguko kuishika Ruknul


kawaida.

Yamani na kulibusu Hajaril Aswad ikiwezekana.


Ikiwa haiwezekani kwa sababu ya wingi wa watu,
basi usijikalifishe ukaanza kusukumana na watu na
kuiharibu Tawafu yako. Yatosha kuiashiria kwa
mkono wako wa kulia kisha ukaubusu mkono wako.

17
Dua zilizo chagulia utakazo omba ukifika pembe mbali mbali
za Al-Kaaba:

1. Hajaril Aswad (Jiwe Jeusi – mahali pa kuanzia na


kumalizia Tawaf), utasema:

Kwa Jina la Mwenye-


‫بسمه ه أك‬
ezi-Mngu, Mwenye-
(Bismi Llahi Allahu
Akbar. Allahumma
‫ل م إي ن بك‬
ezi-Mngu ni Mkubwa imanan-bika, wa-
kuliko kila kitu.
Ewe Mwenye-ezi-
tasdiqan bikitabika, ‫تص ق ب ت بك‬
wawafaan bi-ahdika
Mngu (nafanya haya)
wawaadika, ‫ف ء بع‬
kwa kukuamini Wewe,
na kukisadiki Kitabu wattibaan lisunnati
Chako na kuitekeleza Nabiyyika
Muhammadin,
‫ت ع‬ ‫ع‬
‫لس ن يك مح‬
ahadi Yako na waadi
Wako, na kufuata swalla Llahu alaihi
suna ya Mtume Wako wassallam). ‫ص ه ع يه‬
‫سم‬
Muhammad (S.A.W.).

2. Ukiwa mkabala wa Mlango wa Kaaba:

Ewe Mwenye-ezi- (Allahumma


Mngu! Nyumba hii hadhal baitu, ‫ل م ه ل يت بيتك‬
ni Nyumba Yako. baituka.
Na Haram hii ni Wahadhal
‫ه لح ح مك‬
Haram Yako. Na H’aramu, ‫ه م‬
hapa ndipo mahali H’aramuka. ‫لع ء بك من ل‬
pa mwenye Wahadha
kujilinda Kwako maqamul
na Moto. aidhubika mina
nnar).

18
3. Ukifika mkabala wa Ruknul Iraqi:

Ewe Mwenye-ezi- (Allahumma


Mngu! Nilinde na aidhnii mina ‫ل م أع ن من‬
shirki na unilinde ‘shirki, wal-
na kukufanyia ishrak, wal-kufri
‫إش‬ ‫لش‬
ushirika. Unilinde wannifaq, wa-suil
na kufuru na akhlaq, wa-suil ‫ل‬ ‫ل‬
unafiki, tabia muntadhwiri fil ‫س ء أخا‬
mbovu na unilinde ahli, wal-mali,
na macho maovu wal-waladi) ‫س ء ل تظ ف‬
(ya wivu) juu ya
watu wangu, mali ‫ل ل‬ ‫أهل ل‬
yangu na watoto
wangu.

4. Utakapofika mkabala wa kopo la maji ya mvua la


Al-Kaaba (Mizab al-Rahma):

Ewe Mwenye-ezi- (Allahumma


Mngu nifinike adhwillinii tahta ‫تحت‬ ‫ل مأ‬
chini ya uvuli wa
Arshi Yako Siku
dhwillu Ar-
shuka, yauma la
‫ل ع شك‬
hiyo ambapo dhwilli illa ّ
‫ي ا ل إا ل‬
hapatakuwa na dhwilluka).
kivuli isipokuwa
kivuli Chako.

5. Utakapofika mkabala wa Ruknu Shaamy:

Ewe Mwenye-ezi- (Allahummaj-


Mngu ijaalie (Hija
yangu hii) ni Hija
alhu hajjan
mabrura, wa-
‫ل م جع ه حج‬
yenye kukubaliwa, sa’yyan mash- ‫سعي‬ ‫م‬

19
na (amali yangu) kura, wa-dhanban ‫ن‬ ‫مش‬
ni amali yenye
kushukuriwa, na
maghfura, wa-
tijaratan lan
‫لن‬ ‫تج‬ ‫مغ‬
(madhambi yangu) tabura). . ‫ت‬
ni madhambi
yenye
kusamehewa, na
iwe ni biashara
isiokuwa na
hasara..

6. Utakapofika mkabala wa Ruknul Yamny - uishike


pembe hiyo ya Al-Kaaba ikiwezekana, (au uashirie
kwa mkono wako wa kulia) kisha uubusu mkono
wako:

Ewe Mwenye-ezi- (Allahumma


Rabbana a’tina fi
Mngu, Bwana
wetu! Tupe mema dduniya hasanatan,
‫ل ني‬ ‫ل م ب آت ف‬
ulimwenguni, na wa-fil a’khirati ‫حس‬
utupe mema hasanatan, wa-qina ‫ق‬ ‫ف أخ حس‬
Akhera. Na adhaba nnar). ‫ل‬ ‫ع‬
utulinde na
adhabu ya Moto.

 Baada ya kumaliza mizunguko saba ya Tawaf,


utakwenda Maqamu Ibrahim kama tulivyo amrishwa
katika Qur’an : "Na pafanyeni Maqamu Ibrahim ni
mahali pa kuswalia.” (Baqarah 2:125)

20
2:125 Na (Waidh-
kumbukeni kuwa jaalnal baita
tuliifanya (Al- mathabattan
Kaaba) ni linnasi wa-
Nyumba amna.
wanapokusanyika Wattakhadhu
watu (kwa min maqami
ibada), na mahali Ibrahi’ma
pa amani. Na muswalla…)
pafanyeni
Maqamu Ibrahim
ni mahali pa
kuswalia…

 Hapo Maqamu Ibrahim, utaswali rakaa mbili.


Rakaa ya kwanza utasoma Qul- ya ayyuhal kafiruun,
baada ya Alhamdu. Na katika rakaa ya pili utasoma
Qul huwa Llahu.

Ukimaliza rakaa zako mbili za hapo Maqamu Ibrahim,


utaomba dua uitakayo. Dua ifuatayo ni katika dua
zilochaguliwa:

Ewe Mwenye-ezi- (Allahumma


Mngu nisahilishie
njia nyepesi, na
yassirlil yusra,
wajannibi usra.
‫ل م يس ل‬
uniepushe na njia Waghfirlii fil- ‫ج‬ ‫ل يس‬
nzito. Nighufirie akhira’ti wal- ‫غ ل‬ ‫لعس‬
katika Akhera na uula. Allahumma ‫ف آخ‬
katika dunia. Ewe aidhnii min
Mwenye-ezi- mudhwillatil ‫ ل م‬، ‫أ ل‬
Mngu! Nilinde na fitani, waaidhnii ‫أع ن من م‬
fitina yenye min juhdil balai, ‫ أع ن من‬،‫ل تن‬
kupoteza, na Wadarka shika’i, ،‫ج ل اء‬
21
unilinde na wa-suil qadhwa’i, ‫لش ء س ء‬
maonjo ya
kuchosha na
wa-shamaitil
a’adai.
‫ ش ئ‬،‫ل ء‬
mateso ya Birahmatika Ya ‫أع ء ب ح تك ي‬
kudidimiza (au Ar’hamma .‫أ حم ل ح ين‬
mateso yenye rRa’himiin).
kufuatana) na
hukumu ya
(kufikiliwa) ni
maovu, na furaha
za maadui, kwa
Rehma Yako, Ewe
Mbora wa wenye
kurehemu.

 Kisha uende ukanywe maji ya Zamzam, shibe yako.


Maji ya Zamzam ni dawa, kwa hivyo unapoyanywa
ukusudie iwe dawa ya magonjwa uliyonayo, yoyote
yale yawayo. Moja katika dua za kunywiwa maji ya
Zamzam ni:

(Allahumma inni
Ewe Mwenye-ezi-
Mngu, nakuomba
as-aluka ilman
na’fia, wa-rizqan
‫ل م إن أسألك‬
unipe elimu yenye wa’sia’, wa- ‫ق‬ ‫ع ن فع‬
manufaa, na riziki shifaan min kulli ‫سع ش ء من‬
kundufu na dawa da’in. Ya Ar- ‫كل ء ب ح تك ي‬
ya kila ugonjwa. hama rRa’himin).
Ewe Mbora wa .‫أ حم ل ح ين‬
wenye kurehemu.

22
Baadae uende Multazam (Kikuta cha Kaaba baina ya Hajaril
Aswad na Mlango wa Kaaba) – ikiwezekana- usimame hapo
na uombe dua zako kwa unyenyekevu, ujiombee wewe na
Islamu wenzio, kheri za dunia na akhera. Katika jumla ya dua
utakazoomba, pia jiombee dua hii:

Ewe Mwenye-ezi- (Allahumma Ya


Rabbal baitil a’tiq.
Mngu, Bwana wa
Nyumba hii ya Aatiq raqbatii
‫ل يت‬ ‫ل مي‬
kale! Iache huru minan nNar. Wa- ‫لعتيق أعتق ق ت‬
shingo yangu na aidhnii min kulli ‫أع ن‬ ‫من ل‬
Moto, na suin). . ‫من كل س ء‬
uniepushe na kila
ovu.

 Baadae uende kwenye Hajaril Aswad na ikiwezekana


– ulibusu.

Sa’yi

Ukisha maliza amali ya Tawaf, utakwenda kwenye kilima cha


Swafa ili ufanye amali ya Sa’yi, kama tulivyo amrishwa na
Mwenye-ezi-Mngu katika aya ya Al-Baqarah 2:158.

23
2:158 Kwa (Inna
hakika! Swafa’ wal-
Swafa na Marwata
Marwa ni min shaaril
katika Ishara
Llahi.
za
kuadhimisha Faman
dini ya Hajjal
Mwenye-ezi- baita,
Mngu. Basi awiitamara,
anayehiji fala’
kwenye junaha
Nyumba hiyo alaihi an
au kufanya yatwawwafa
Umrah, si bihima’)….
kosa kwake
kuvizunguka
(vilima hivyo)
viwili; na
anaefanya
wema
(atalipwa)
kwani
Mwenye-ezi-
Mngu ni
Mwenye
shukrani na
Mjuzi (wa
kila jambo).

 Kipande Kilima cha Swafa, uelekee Al-Kaa'bah, na


uombe dua kama ilivyopokewa kutoka kwa Mtume
(S.A.W.):

24
Allah ndiye (Allahu Akbar,
Mkubwa kabisa!
Allah ndiye
Allahu Akbar,
Allahu Akbar. La
‫ه أك ه أك‬
Mkubwa kabisa! ilha illa Llahu, ‫ه أك اإله إاه‬
Allah ndiye wahdahuu, La ‫ح اش ي ه له‬
Mkubwa kabisa! sharika-lahu. ‫له لح‬ ‫ل‬
Hapana mwenye Lahul Mulku, wa-
kuabudiwa Lahul Hamdu, ‫ه ع كل شيء‬
isipokuwa Allah wahuwa ala’ kulli ‫قي‬
Peke Yake. Hana sha-in Qadir).
mshirika! Ufalme
ni Wake Yeye. Na
Yeye ndiye
mwenye kusifiwa.
Na Yeye ndiye
muweza wa kila
kitu.

 Hapo tena teremka Kilima cha Swafa na uanze kutembea


ukielekea Kilima cha Marwah. Hii ndiyo itakayo kuwa
safari yako ya kwanza katika mizunguko yako saba baina
ya vilima viwili hivi. Katika kutembea kwako utakuwa
ukileta adhkari mbali mbali katika kumbuka Allah, na
huku ukiomba dua ifuatayo, katika dua zilizo pokewa:

Ewe Mola! Rehemu na (Rabbighfir war- ‫حم‬ ‫غ‬


Usamehe, na Ujazi ha’m, wa-tajawaz
yale Unayo yaelewa.
amma’ ta’alam.
‫تج ع تع م‬
Kwani Wewe ni
Innaka antal ‫إنك أنت أعز‬
Mwenye Nguvu,
Mwenye Kutukuka . aazzul akram. ‫أك‬

 Utakapofikia maeneo yalio wakishwa taa mbili


za kijani, hapo mahujaji wa kiume watakwenda
haraka haraka. Huku ni kukumbuka mbio

25
alizokwenda Bibi Hajara wakati akishuka kilima
kimoja na kukimbilia kilima cha pili katika hali
ya kumtafutia mwanawe, Ismail maji ya
kunywa.

 Ukisha ifikia taa ya pili ya kijani, hapo utarudi


mwendo wako wa kawaida, mpaka utakapo kifikia
kilima cha Marwah. Utakipanda kilima cha Marwah
uelekee Kibla, ukiulekeza mwili wako Al-Kaa'bah.
Inua mikono yako, uombe dua kama ile uloomba
ukiwa Swafa.

 Huu utakuwa ndio mzunguko wako wa kwanza,


katika mizunguko saba baina ya Swafa na Marwa.

 Utaanza mzunguko wa pili, baina ya Marwa na


Swafa. Watatu ni Swafa na Marwa, mpaka utakapo
maliza mzunguko wa saba, ukimalizia Marwa.

 Sa'yi ni katika mambo ya wajibu (ya lazima) katika


Hajj. Hujaji yoyote atakae wacha Sa’yi, au
akashindwa kuimaliza mizunguko saba ya Sa’yi,
basi itambidi atoe kafara ya kuchinja mnyama.

Utakapo maliza ibada ya Sa’yi ikiwa ni mwenye kufanya Hija


ya Tamattu' utamaliza Umrah yako kwa kunyoa au kupunguza
nyele. Ukiteremka tu, kutokea mlango wa Marwa utakuta
vinyozi, wako tayari kukufanyia kazi hiyo ya kunyowa.
Silazima kwenda kwa kinyozi, waweza kujinyoa mwenyewe.
Wanawake wanatakiwa kupunguza tu kidogo, kiasi ya ada.
Wao hawaruhusiwi kunyoa nyele zote, kwani nywele ni
katika mapambo ya kike.
Ukisha nyowa au kupunguza nyele, hapo utakuwa
umekamilisha amali ya Umrah kwa wale mahujaji wa
Tamattu’. Hapo utakuwa huru na vikwazo ulivyo wekewa vya

26
Ihram. Uko huru sasa kurudia mavazi yako ya kawaida na
maisha ya kawaida. Una uhuru wa kustarehe na mumeo au
mkeo. Utaendelea na ibada za kawaida, mpaka Siku ya tarehe
nane Dhul Hijja, utakapoingia tena katika hali ya Ihram, ili
uanze amali ya Hijja.

Ama wale walokusudia Hajj Ifrad (Hija peke yake) au


Hajj Qiran (Hija na Umrah pamoja bila ya kusita), hao
wataendelea kuwa katika hali ya Ihram. Huu ndio uzito
wa Hija aina mbili hizi.

Hajj

4. Tarehe Nane (8) ya Dhul-Hijjah

Baada ya Swala ya Al – Fajiri ya tarehe nane - (Siku Ya


Hija, Yaumu nNahar)

Wale walokusudia Hajj Tamattu', wataingia tena katika hali


ya Ihram. Wataoga na kuvaa tena vazi lao la Ihram kama
walivyofanya mwanzo wa safari yao ya Hija walipotoka
mijini mwao. Tafauti ya mara hii ni kuwa utaingia katika hali
hii ya Ihram, katika makazi yenu ya Makkah. Hapo nyumbani
Makkah ndipo patakapo kuwa Miiqat ya Hija.

(ANGALIA: “Kuingia katika hali ya Ihram” – kurasa za


mwanzo). Mukisha ingia katika hali ya Ihram, mutatia niya
ya Hija. Hapo tena mutaanza safari ya kwenda Mina.
Mahujaji wote – wa Tamattu’, Ifrad na Qiran, watajumuika
pamoja katika safari hii ya kwenda Mina. Huu ndio mwanzo
wa Hajj. Mahujaji wote watalala Mina, hii tarehe nane Dhul
Hijja.

27
Niya ya Hajj:

Ninakusudia Nawaitul Hajja,


kufanya amali ya
Hija, na ninaingia
wa-ahramtu
biha’, Lillahi
‫ن يت لحج‬
katika hali ya Taala. ‫أح مت به ه‬
Ihram kwa ajili ya . ‫تع ل‬
Mwenye-ezi-Mngu
aliyetukuka.

Katika safari yenu hii ya kwenda Mina, mahujaji nyote


mutasoma Talbiyya kwa umoja wenu, wanaume wakisoma
kwa sauti, na wanawake wakisoma kwa pamoja kimoyoni.
Vile vile, mutasoma Swalatu ala nNabii. Huu ndio umoja na
nguvu za mahujaji!

Mutakapo iona Mina, utaomba dua ifuatayo. Hii ni miongoni


mwa dua zilopendekezwa:

Ewe Mola wangu! Hii (Allahumma


ni Mina! Nimeifikia! ha’dhihii Mina’,
Alhamdu Lillahi!
qad atai-taha’.
‫ل مه م ق‬
Nakushukuru Mola
Alhamdu Lillahi ‫أتيت لح ه‬
wangu, ulo niwezesha
kuifikia kwa salama, balaghani’ha ‫ل بغي سل‬
nikiwa katika hali ya sa’liman mua’fii. ‫ ل م إن‬. ‫مع ف‬
afya. Ewe Mola Allahumma inni
wangu! Najilinda audhubika minal ‫أع بك من‬
Kwako kutokana na hirmani, wal- ‫ل صي‬ ‫لح م‬
‫ني ي‬ ‫ف ي‬
mitihani na misiba
katika dini yangu, na
muswibatii fi-dinii,
duniya yangu. Ewe wa-duya’ya. Ya . ‫أ حم ل ح ين‬
Mwingi wa Ar-hama
kurehemu. rRahimiin).

28
Mahujaji wataswali swala ya Adhuhuri na Alasiri
watakapofika Mina kwa nyakati zake. Swala zitapunguzwa,
za rakaa nne, zitaswaliwa rakaa mbili mbili kama, swala ya
safari. Swala ya Magharibi haipunguzwi; swala ya Isha
itaswaliwa rakaa mbili kwa wakati wake. Ni vizuri swala zote
ziswaliwe kwa jamaa. Hapa muko safarini, kwa hivyo hakuna
swala za sunna. Hakuna kablia wala baadia, ndio maana swala
zikapunguzwa.

Mahujaji wote watalala Mina. Ndiyo Sunna ya Mtume


(S.A.W.).

5. Jua Linapo chomoza – Tarehe Tisa (9) ya Dhul-Hijjah


(Yaumul Arafah!)

Baada ya Mahujaji kuswali Swalatul Fajr ya tarehe tisa, na


baada tu ya jua kuchomoza, mutaondoka Mina na kwenda
Arafah. Mukifika Arafah, mutafikilia katika mahema yenu
yalokitwa katika kiwanda cha Arafah, karibu na Msikiti
Namira.

Mukiwa safarini kwenda Arafah kutoka Mina, mutakuwa


mukisoma dhikri mbali mbali. Moja katika dua zilizo pokewa
ni:

29
Ewe Mola wangu!
Kwako Wewe
(Allahumma Ilaika ‫ل م إليك ع‬
‫إليك ت ج ت‬
adawatan, wa-Ilaika
najiegemeza, na tawajjahtu wa-Waj-
Kwako Wewe
nauelekeza uso
hika arad-tu. Faj- ‫ف‬ ‫ج كأ‬
‫جع م ن ت ه‬
alnii mimman tubahi
wangu.Uso Wako
bihi yaumal
‫به لي مائ تك‬
Mtukufu ndio ninao
upendelea. Nijaalie Malaikatika.
mimi niwe miongoni Allahumma inni
audhubika ‫ل م إن أع‬
mwa wale Utakao
wakumbatia, Siku biridhwaka min ‫ب ض من س ك‬
utakayo jisifu mbele ya
Malaika Wako. Ewe
sakhatwika, wa-
biafwika min
‫من‬ ‫بع‬
Mola wangu! Najilinda uqubatika). .‫ع بتك‬
Kwako, kwa Idhini
Yako, na hasira
Zako.Nihifadhi kwa
mapenzi Yako
kutokana na adhabu
Yako. Amin.

Arafah:

 Munatarajiwa kufika Arafah milango ya saa sita


mchana. Ni Sunnah kuoga mutakapofika. Mutaswali
swala ya Adhuhuri na Alasiri kwa pamoja, kama
swala ya safari, wakati wa adhuhuri. Kutaadhiniwa,
kukimimiwe na muswali Adhuhuri, rakaa mbili.
Mukimaliza swala ya Adhuhuri, kutakimiwa na hapo
hapo muswali swala ya Alasiri, rakaa mbili. Ni bora


kuswali jamaa.
Ikiwa haikuwezekana kuswali jamaa, basi vile vile,
utaswali ukiwa peke yako, swala ya kisafari. Uadhini,
ukimu na kuswali kama tulivyo eleza katika swala ya
jamaa hapo juu.

30
 Mkusanyiko wa Mahujaji katika kiwanja cha Arafah
unaanza baada ya kupinduka jua wakati wa mchana –
saa sita mchana.

 Wakati huu, kila Hujaji atakiwa awepo katika kiwanja


cha Arafah, karibu na majabali ya Arafah. Shughuli


zako zote ziwepo hapa katika uwanja huu.
Kusimama Arafah ndiyo Hajj yenyewe. USIJE
UKAIKOSA!

 Usijitie uhodari wa kupanda Jabali Rahma.Usione


watu wafanya na wewe ukafuata. Sunna ni kusimama
kiwanja cha Arafah. Kulipanda Jabali Rahma
hakutakiwi, sunna ni kufuata aloyafanya Mtume,
usifuate hawaa za watu.

 Kipindi chote mutakapo kuwa Arafah,


jishughulishe na ibada. Elekea Qibla, uingie katika
kumkumbuka Mola wako. Urafiki, usuhuba,
ujirani kwa sasa usahau. Kumbuka na
ujikumbushe kuwa sasa ni wewe na Mola wako tu!

KUMBUKA!

Mtume (S.A.W.) amesema: ‘Hajj ni Arafah’.

USIIKOSE ARAFAH kwa sababu yoyote! Ukikosa


QIYAMUL ARAFAH – Kusimama Kiwanja cha Arafah,
umeikosa Hija. Safari yako yote utaiharibu, ukisahau

 Masaa yako sita au saba utakayo kuwepo hapa


kusudio lako la kuwepo katika kiwanja hiki!!!!

ndio Hija yako yote!

Ewe NDUGU YANGU nakuusia!

31
USAHAU ulimwengu,
WASAHAU ulofuatana nao,
KUMBUKA kusimama hapa ni kama kusimama Siku Ya
Kufufuliwa!!!!

Hapa ndipo mahali pa Rabbi Rabbi Nafsi!

Kusimama Arafah kumefananizwa na Mkusanyiko wa


Malaika mbele ya Mola wao, kumefananizwa na Siku ya
Qiyama.

 Kusimama kwako hapa Arafah, ndipo kusimama


kwako kwa karibu zaidi mbele ya Mola wako.

 Hapa ndipo panapo hitajia khushui yako yote.


Uchaji Mngu wako wote ulete hapa!

 Hapa ndipo khaswa pa kumlilia Mola wako!

 Usijishughulishe na mambo ya kilimwengu.


Usitafute mzunguzaji. Usitafute rafiki, wala ndugu
wala jamaa. Ni wewe na Mola wako tu!

 JISHUGHULISHE na Talbiyya, Istighfar, Tasbih,


Tahlil, kusoma Qur’an, Swalatu-ala nNabii.
Omba dua utakazo katika kufanikiwa kwako
katika maisha yako ya kidunia na Akhera.
Waombee wazee wako, ndugu zako na jamaa
zako. Waombee waIslamu wenzako waliohai na
wale waliotangulia mbele ya haki.

Moja katika uradi wako mkubwa, uwe uradi huu ulopokewa


kutoka kwa Mtume (S.A.W.)

32
Hapana afaae (La Ilaha illa
kuabudiwa kwa
haki, isipokuwa
Llahu, wahdahu,
la sharika-lahu,
‫اإله إاه ح‬
Mwenye-ezi- Lahul-Mulku, ‫اش ي ه له ل‬
Mangu Peke Yake. walahul-Hamdu, ‫له لح ه‬
Hana mshirika! wahuwa ala kulli ‫ع كل شيء ق ي‬
Ufalme ni Wake shain qadir).
Yeye Peke Yake.
Na ni Zake Yeye
Sifa njema zote.
Na Yeye Peke Yake
ndiye Muweza wa
kila kitu.

6. Tarehe 10 Dhul Hijja

Linapotuwa jua Yaumul Arafah

Baada ya kutuwa jua Siku ya Arafah, tarehe tisa Dhul Hijja,


mahujaji huondoka katika kiwanja cha Arafah bila ya kuswali
Magharibi. Watakwenda Muzdalifah.

 Mahujaji watakapo fika Muzdalifah, wataswali swala


ya Magharibi na Isha kisafari. Kutaadhiniwa,
kukimiwe na kuswali swala ya Magharibi rakaa tatu.
Mukitoa salamu kutakimiwa na muswali swala ya
Isha, rakaa mbili peke yake. Baadae mutalala hapo
Muzdalifah.

7. Tarehe 10 Dhul Hijja


Alfajiri ya tarehe kumi Dhul Hijja, baada ya swala, Mahujaji
watasogea mpaka Mash'ar al Haram (Maeneo matukufu
yaliyo tajwa ndani ya Qur’an), hapo wataleta dhikri za
kumkumbuka Allah, mpaka litakapo chomoza jua. Surat Al-
Baqarah 2:198 Allah anasema:

33
Ayah 198: Laisa
Si vibaya kwenu alaikum
kutafuta fadhila junah’un an
za Mola wenu tabtaghuu
(na kufanya fadhlan min
biashara zenu).
Rabbikum.
Basi mutakapo
rudi kutoka Faidha
Arafah mtajeni afadhtum
Mwenye-ezi- min
Mngu katika Arafa’tin,
Mash-aril- fadhkuru
Haram (huko
Llaha indal
Muzdalifah),
mkumbukeni Masha’aril
(Mwenye-ezi- H’aram.
Mngu) kwa ajili Wadhkuru
ya kuwaongoa. Llaha kama
Na hakika kabla hada’kum,
ya kuwaongoa wa-inkuntum
mulikuwa ni
miongoni mwa
min qablihi
wale walio lamina
potea. dhwa’lin.

Ayah 199: Thumma


Kisha ondokeni afidhu min
kutoka pale h’aithu
wanapomiminika afadha
watu (Arafah), nnasu,
mumuombe wastaghfiru
Mwenye-ezi-
Mngu maghfira Llaha.
(msamaha). Inna Llaha
Hakika Mwenye- ghafurun
ezi-Mngu ni Rah’im.
mwingi wa
kusamehe,
Mwenye
kurehemu.

34
Ayah 200
Na mukisha Faidha
maliza qadhwaitum
kutekeleza ibada manasikaku
zenu (za Hija), m fadhkuru
basi mtajeni Llaha
Mwenye-ezi- kadhikrikum
Mngu kama
mlivyokuwa
abaakum au
mukiwataja ashadda-
baba zenu, bali dhikra,
mtajeni zaidi famina nnasi
Mwenye-ezi- man yaqulu
Mngu. Na Rabbana
miongoni mwa
a’tina fi-
watu, kuna wale
wanaosema ddunya
“Mola wetu tupe wamalahu fil
(mema) katika akhirati min
dunia”, wala khalaq.
hana fungu
lolote huko
Akhera.

 Kusimama Masha-aril Haram ni wajib, (ni


lazima), na yeyote atakae wacha kusimama hapo,
basi itambidi achinje kama kafara.

Mahujaji wanatakiwa waokote vijiwe kupiga majabali matatu.


Utaokota vijiwe kisivyo pungua sabiini (70). Kila jabali
hupigwa vijiwe saba kwa siku mbili (tarehe 11 na 12) au tatu
(tarehe 11, 12 na 13). Na jabali la kwanza hupigwa vijiwe
saba, siku ya tarehe kumi. [vijiwe 7 kupiga majabali x3 =
vijiwe 21 kwa siku x3 = vijiwe 63 ukiongeza vijiwe vya siku
ya kwanza +7 = vijiwe 70].

35
8. Tarehe 10 Dhul Hijja

Baada Ya Kuchomoza Jua, tarehe kumi ya Dhul Hijja

Hujaji anatakiwa akarushe vijiwe saba katika Jamarah Al-


Aqabah huko Mina. Kila atakapo tupa kijiwe kimoja,
atasema:

Mwenye-ezi-Mngu Allahu Akbar!


ni Mkubwa kabisa,
Mwenye-ezi-Mngu
Allahu Akbar!
Allahu Akbar!
‫ه أك ه أك‬
ni Mkubwa kabisa, WaliLlahil hamd! . ‫ه أك ه لح‬
Mwenye-ezi-Mngu
ni Mkubwa kabisa!
Na sifa njema
nzote ni za
Mwenye-ezi-Mngu.

 Ukisha maliza ibada ya kutupa vijiwe, utachinja


mnyama wako, kisha unyoe au kupunguza nyele
zako. Mwanamke haruhusiwi kuzinyoa nyele zake.
Linalo takiwa kwake ni kupunguza tu nyele zake
kidogo, kiasi ya kutimiza ada. Hii ni kwa sababu,
nyele ni katika pambo la mwanamke. Kwa hivyo
linahifadhiwa pambo la mwanamke.

9. Tarehe 10 Dhul Hijja

 Tahallul ya kwanza. Baada ya kuchinja na


kunyoa/kupunguza nyele, hapo utatoka katika baadhi
ya hali ya Ihram. Hii inajulikana kama Tahallul ya
kwanza. Hapo unaruhusiwa kufanya mambo yote
ulokuwa umekatazwa ukiwa katika hali ya Ihram,
isipokuwa kulala na kustarehe na mkeo/mumeo.

36
10. Tarehe 10 Dhul Hijja

 Utakapo maliza ibada ya kutupa vijiwe, kuchinja na


kunyoa, hapo tena utakwenda Makka ili ukafanye
ibada ya Tawaf Al-Ifadah, hii ni yajulikana pia kama
Tawaf Az-Ziyarah. Tawaf hii ni moja katika nguzo
za Hija.

 Tawaf hii utaifanya kama ulivyo tangulia kufanya

Tawaf Al-Qudum
Mwanzo ulipofika Makkah, (angalia kurasa za mwanzo).
Utaomba dua ifuatayo miongoni mwa dua zilizo
pendekezwa:

Ewe Mola wangu! Allahumma in- ‫ل م إ ك ت ضيت‬


Ikiwa umeridhika
name (katika ibada
kunta radhwita
anni, fazid anni
‫ض‬ ‫ع فز ع‬
yangu hii ya Hija na ridhwa! Wa-illa, ‫إا ف ن ع‬
Umrah), basi famunna alayya ‫ ل مه‬، ‫ب ض‬
nakuomba uendelee
kuwa radhi na mimi.
biridhwaka.
Allahumma hadha
‫إ ص ف إ‬ ‫أ‬
La ikiwa awawana-nswirafi ‫أ نت ل غي‬
hukuridhika na inadhanta-lii ghaira ‫مست بك ا ب يتك‬
mimi, basi naiomba mustabdilin bina ‫ ل م فص ح‬،
Ihsani Yako, unipe wala bibaitika.
radhi Yako. Ewe Allahumma ‫لع في ف جس ي‬
Mola wangu, wakati faswahibni ‫لعص ف ي‬
umewadia wa mimi a’fiyattan fii jismi, ‫أحسن م‬
kurudi kwetu, ikiwa
utaniruhusu.
wa-ismatan fii dinii,
wa-ahsin
‫عتك‬ ‫ق‬
Msimamo wangu munqalabii, ‫ج ع ل بين‬
uko thabiti Kwako warzuqnii twaatika, ‫ل ني آخ‬ ‫خي‬
Wewe na kwa
Nyumba Yako. Ewe
waj-maalii baina
khairi ddunya wal-
‫إنك ع كل شيء‬
Mola wangu! akhira. Innaka ala . ‫قي‬
Nakuomba kulli sha-in Qadir.

37
unibarikie afya
njema katika mwili
wangu, na uniruzuku
imani thabiti.
Kujaalie kurudi
kwangu kuwe ni
kwenye
kumebarikiwa.
Ithibitishe vyema,
imani yangu Kwako.
Yajumuishe mema
ya duniya na ya
Akhera. Kwani
Wewe ni Muweza wa
kila kitu.

Ikiwa ni mwenye kufanya Hajj Tamattu', basi hapo


unapomaliza ibada ya Tawaf, utaendelea na ibada ya Sa'yi
baada ya Tawaf Al-Ifadhah.

Kwa Mahujaji wa Hajj Qiran au Ifrad, Sa’yi hii ya mara ya


pili si lazima. Kwani pale ulipo wasili Makkah ulitanguliya
kufanya Sa'yi baada ya Tawaf Al-Qudum.

Tarehe 10 Dhul Hijja

Baada ya kuitimiza Tawaf Al-Ifadhah

Baada ya kuimaliza Tawaful Ifadhah, Mahujaji sasa


wameingia katika Tahallul ya pili. Sasa umeshatoka katika
hali ya Ihram, na uhuru kamili hata wa kulala na kustarehe na
mkeo/mumeo.

38
Mahujaji sasa wanatakiwa warudi Mina. Mutalala Mina siku
zinazo fuata. Kulala Mina usiku wa tarehe kumi ni wajibu.
Usipolala usiku huo, itakubidi uchinje na kutoa kafara
kwa kuwacha jambo la wajibu.

11. Tarehe 11, 12 na 13 Dhul Hijja

 Kukaa Mina siku mbili au tatu katika siku zinazo itwa


Yaumu – Tashriq.

Tarehe 11 Dhul Hijja

12. Baada ya kupinduka Jua siku ya tarehe 11 ya Dhul-


Hijja,
Kila Hujaji anatakiwa afanye ibada ya kutupa vijiwe,
kuyapiga majabali matatu ya Jamarah. Utaanza kwa lile jabali
lililo upande wa Mina na kulitupia vijiwe saba. Kisha
utalipiga lile la kati kati pia kwa vijiwe saba. Hapo tena
utasita kwa muda na kuomba dua kabla ya kuliendea jabali la
mwisho - Jamratul Sughra, JamratulWusta na Jamratul Kubra.

 Utalipiga jabali la mwisho kwa vijiwe saba. Ukisha


lipiga, onoka mahali hapo bila ya kuangalia nyuma.
Hii ndio sunna ya Nabii Ibrahim, kama alivyo
tufundisha Mtume (S.A.W.). Ibada hii inatakiwa
imalizwe kabla ya kukutwa jua.

39
Kubra Wusta Sughra

13. Tarehe 12 Dhul-Hijja

 Utairudia tena ibada ya kutupa vijiwe kama vile


ulivyo fanya jana.
Unapo maliza ibada hii ya kutupa vijiwe kwa siku ya
pili, waruhusiwa kuondoka na kurudi Makkah kabla
ya kutwa jua. Ukipenda, waweza kuirudia tena ibada
hii kwa siku ya tatu ya tarehe 13 Dhul Hijja, hii ina
maana kuwa utalala Mina tarehe 12 na kuitimiza
ibada hii kwa siku ya tatu.

14. Bakia Mina tarehe 13 ya Dhul-Hijjah na kutimiza ibada


ya kutupa vijiwe kwa siku tatu.

Ibada ya kutupa vijiwe ni wajibu wa Hija. Ikiwa


hukuifanya itakubidi uchije na kutoa kafara kwa kukosa
kutimiza wajibu.

15. Ukisha maliza ibada ya kutupa vijiwe, utarudi zako


Makkah. Ikiwa uko tayari kurudi nchini kwenu, au kuondoka
Makkah na kwenda ziara ya Madina, basi utfanya Tawaf-al-
Wida' yaani Twawaf ya kuiaga Makkah. Tawaf ya kuaga

40
pia ni wajibu. Hii ndiyo inayo takiwa iwe ibada yako ya
mwisho kabla ya kuondoka mji wa Makkah. Na ikiwa
utaiwacha, basi itakubidi urudi tena kabla ya kuivuka Miiqat,
uchinje na uilipe.

Ibada ya Hija na Umrah kwa ufupi:



Kuvaa Ihram katika Miqat,


Tawaf,


Sa'yi,
Kunyoa au kupunguza nyele.

Unapo timiza amali nne hizo, utakuwa umeshatimiza ibada ya


Umrah.

Ama kutekeleza ibada ya Hija, unatakiwa ufanye ibada zaidi.


Nazo ni:

 Kusimama katika kiwanja cha Arafah, Siku hiyo ya


Arafah,


Kupiga mawe katika Jamarah,


Tawaf Al-lfadhah,


Kukaa Mina,


Kuchinja,
Kunyoa au kupunguza nyele.

Huu ndio mukhtasari wa ibada ya Hija na Umrah.

KAFARA ZINAZO KULAZIMU UNAPOWACHA


MAMBO YA LAZIMA KATIKA HAJJ NA UMRAH

Kafara inayo kulazimu kutowa unapo wacha jambo la lazima,


au kufanya jambo ulilo katazwa wakati wa Hija na Umrah, ni
kuchinja au kufunga siku tatu katika siku za Hija, na kufunga
siku nyengine saba utakapo rudi kwenu. Hiyo ikiwa ni kafara

41
kama kufunga siku kumi, kama zilivyo tajwa katika Qur’ani
au kulisha maskini.

Yafuatayo ndiyo mambo yanayo lazimu kutolewa kafara kwa


kiwango kilicho wekwa, na kwa mpango ulowekwa:



Ukikosa kusima kiwanja cha Arafah (Qiyamul Arafa).


Usipopiga vijiwe katka Jamarat.
Usipokaa Mina katika siku za Tashriq (Tarehe 11, 12


na 13 Dhul Hijja).


Usipo lala Muzdalifah usiku wa Arafah.


Ukikosa kuingia katika hali ya Ihram katika Miqat.


Ukivunja kiapo ulicho jiwekea.
Usipo fanya Tawaful Widai.

Kundi hili la makosa, una uhuru wa kuchagua kafara utakayo


towa, kulingana na aina tatu za kafara zilizowekwa. Nazo ni
kuchinja, kufunga au kulisha maskini sita katika maeneo ya
Makkah, kila mmoja akipewa kilo moja ya nganu:



Kuzikata nyele zaidi ya tatu kwa mara moja.


Kukata kucha zaidi ya tatu
Mwanamume atakapo vaa nguo zenye mshono,


au kufinika kichwa akiwa katika hali ya Ihram.


Kujipaka mafuta ukiwa katika hali ya Ihram.


Kutumia manukato ukiwa katika hali ya Ihram.
Kucheza cheza na mkeo/mumeo kwa njia ya


mapenzi ukiwa katika hali ya Ihram.
Kurudia kufanya mapenzi na mkeo/mumeo
baada ya kuwa mumeshatozwa kafara mara ya


kwanza.
Removing 3 or more of your hairs at the same
time.

42
 Kufanya mapenzi na mumeo/mkeo ukiwa katika
Tahallul ya kwanza, baada ya kupewa ruhusa ya


kwanza ya hali ya Ihram.
Kuuwa mnyama katika Haram ya Makkah, kwanu


huruhusiwi kuinda.
Kukata mti katika Haram ya Makkah.

Jitahadhari kuingia katika starehe na mkeo/mumeo mukiwa


katika amali ya Hija au Umrah. Huu ni wakati wa Ibada, si wa
starehe, juu ya kuwa ni halali yako.

Utakapo iharibu ibada yako ya Hija au Umrah, itakubidi:

 Kwanza lazima uitimize ibada hiyo ya Hija au


Umrah.
Lazima ulipe kafara kama ilivyo wajibika. Kafara


yake ni kuchinja ngamia!
Lazima uilipe Hija hiyo au Umrah.

Hii ndiyo athari ya kuifanyia mchezo ibada hii ya mara


moja katika maisha yako!

Kumbuka kuwa lililo kupeleka Hija au Umrah ni kuonana na


Mola wako, sio starehe yako. Mkeo/mumeo uko nae siku zote.
Kusudio lenu liwe ni kuonana na Allah. Musiiharibu ibada
yenu, kwa starehehe ulio hlalishiwa wakati ufaao!
Ihifadhi Hija na Umrah yako! Kumbuka ibada hii ni kipimo
cha hali ya juu ya kumuogopa kwako Mwenye-ezi-Mngu.
Hapa inapimwa uzito wa imani yako na taqwa yako na subira
yako katika mipaka aliyo kuwekeya Mwenye-ezi-Mngu.

{NAKUOMBEA MWENYE-EZI-MNGU AITAKABALI


HIJA NA UMRAH YAKO – AMIN.}

43
{EWE NDUGU YANGU WA DHATI TUKUMBUKE NA
SISI WAKATI WA HAJI NA UMRAH YAKO –
INSHA’ALLAH!}

NAMNA YA KUVAA IHRAM

44
ZIARA YA MADINA

 Baada ya kuikamilisha amali ya Hija na Umrah, ni


vizuri sana kuichukuwa fursa hii na kuutembelea mji
wa Madina. Ukazuru Msikiti na kaburi la Mtume
(S.A.W.). Hii ni nafasi muwafaka wa ziara, kwani
huna uhakika kama utaipata nafasi nyengine tena
kama hii ya kwenda Makkah kuhiji na kufanya
Umrah. Kwa hivyo ni jambo la muhimu sana
kuitimiza amali yako ya Hija pamoja na kuiandamiza
na ziara.

 Utakapo wasili mji wa Madina, fuliza moja kwa moja


mpaka Msikiti wa Mtume (S.A.W.). Uingiapo
msikitini, utaswali rakaa mbili za Tah’iyyatul masjid.
Swala moja katika Msikiti wa Mtume una thawabu
mara alfu moja zaidi kuliko msikiti mwengine
wowote

 Ikiwezekana jitahidi uswali katika Raudha (hili ni


eneo la msikititi liliopo baina ya Mimbar ya Mtume
na kaburi lake). Mtume (S.A.W.) ameisifu hii Raudha
na kusema kuwa ni bustani katika mabustani ya
Peponi.

 Utakapo maliza swala yako ya Tahiyyatul Masjid,


basi omba dua utakayo katika haja zako za halali
katika haja zako za kidunia, na kujiombea kheri za
Akhera.

 Hapo tena utainuka na kwenda kulizuru kaburi la


Mtume (S.A.W.) pamoja na makaburi ya maswahaba
zake wawili, Sayidna Abubakar na Sayidna Omar –
Mola awe radhi nao. Makaburi yote matatu yamo
katika chumba kilicho kuwa cha Bibi Aisha, mke wa

45
Mtume (S.A.W.) – Mwenye-ezi-Mngu awe radhi nae.
Chumba hicho kimefungwa ili kuepusha shirki zinazo
patikana lau kingewachwa wazi. Chumba hicho
kimekuwa ni sehemu ya msikiti.

 Hii ndio salamu ilopendekezwa za kumsalimia


Mtume (S.A.W.):

Amani iwe juu yako, (Assalamu alaika ‫لسا ع يك ي ن ي‬


ewe Mjumbe wa Ya Rasula Llah!
Mwenye-ezi-Mngu! Assalamu alaika Ya ‫ه لسا ع يك ي‬
Amani iwe juu yako Khaira Khalqi ، ‫خي خ ق ه‬
ewe mbora wa
viumbe vya Allah!
Llah! Assalamu
alaika Ya Sayyidal
‫لسا ع يك ي سي‬
Amani iwe juu yako, Mursaleen, wa- ، ‫ل س ين‬
ewe mbora wa Imamal muttaqeen.
Mitume wa Allah, na
Imam wa wamchao Ash-hadu annaka
، ‫إم ل ت ين‬
Allah! Mimi ballaghta rrisalat, ‫أش أنك ب غت‬
nashuhudia kuwa
wewe umeufikisha
wa-naswahtul ‫ل س ل نصحت‬
ujumbe na ummata, wa- ‫أم ج هجت ف‬
ukaunaswihi Ummah. jahadtu fi Llahi . ‫ه حق ج‬
Na ukapigana jihadi haqqa jihadihi
kwa ajili ya Allah,
upeo wa kupigana
jihadi.

Ewe Mola wangu! Allahumma swalli, ‫ل مص سم‬


Mrehemu, umpe wa-ssallim,wa-barik
ala hadha nNabiyyil
‫ب ع ه‬
amani na umbariki
Mjumbe Wako huyu kareem, wa-rrasulil ، ‫ل ي ل يم‬
mtukufu. Mtume Amin, Sayyidil ، ‫ل س أمين‬
muaminifu, mbora wa
Mitume na Imamu wa
Mursaleen, wa-
Immal Muttaqeen.
‫سي ل س ين إم‬
wacha-Mngu. ‫ل ت ين‬

46
Ewe Mola wangu!
Mrehemu na mpe
Allahumma swalli,
wa-ssallim, wa-
‫ل مص سم‬
amani, na umbariki barik ala’ Sayyidina ‫ب ع سي ن‬
Bwana wetu Muhammad, wa- ‫مح ع آ‬
Muhammad pamja na ala’ a’li Sayyidina
A’li zake. Na tujaalie Muhammad, waj-
، ‫سي ن مح‬
sisi tuwe miongoni alna minal-ladhina ‫جع من ل ين‬
mwa wale ulio
waneemeshwa
an-amta alaihim, ‫أنع ت ع ي م من‬
miongoni mwa Nabii,
minan nNabbiyyina, ‫ل يين لص ي ين‬
wa-swiddiqina, wa-
na wakweli na
shuhadai, wa- ‫لش ء‬
‫لص لحين حسن‬
mashahidi natuwe
miongoni mwa watu swalih’ina. Wa-
wema. Hao ndio ha’suna ulaika ‫أآئك في جع‬
marafiki wema. (Ewe rafeeqa. Waj-alna
minal faizeen.
‫من ل ئزين‬
Mola wetu!) Tujaalie
tuwe miongoni mwa Amin.
wenye kufaulu.
Amin.

 Hapo tena utasogea kwenye makaburi ya maswahaba


zake wawili, uwatolee salamu na kuwaombea Mngu.

 Kila swala za faradhi utakazo ziswali katika msikiti


wa Mtume, utazidisha thawabu zako. Kwa hivyo
jitahidi kwa upeo wa jitihadi yako, kuswali swala
zako zote katika Msikiti wa Mtume. Tumia wakati
wako mwingi katika Msikiti hii mtukufu, uswali na
kukaa Itikafu. Uzidi kumswalia Mtume, na kila la


kheri.
Maji ya Zamzam yapatikana katika Msikiti huu wa
Mtume. Maji hayo yamevutwa kutoka Makkah hadi


Madina kwa mabomba.
Jitahidi sana kunywa maji ya zamzam kama
uwezavyo. Kwani maji haya matukufu ni dawa ya
kila magonjwa kama ilivyo pokewa kutoka kwa

47
Mtume (S.A.W.). Utakapo yanywa maji hayo, basi
yakusudie kuwa ni dawa uihitajiao.

Ewe Mola Allahumma inni


nakuomba unipe as-aluka ilman ‫ل م إن أسألك‬
na’fia warizqan
elimu yenye
manufaa, na riziki wa’sia washifaan
‫ق‬ ‫ع ن فع‬
yenye min kulli da’in ‫سع ش ء من‬
kunitosheleza, na ‫كل ء ي أ حم‬
dawa ya kila .‫ل ح ين‬
maradhi – Ewe
Mwenye
kuwarehemu
wanaorehemewa.

 Kwa kumalizia, tafuta wakati wa kuyazuru

 Haya ndiyo makaburi ya maswahaba


makaburi ya Baqii.

watukufu wa Mtume (S.A.W.)

48
49
50
51

You might also like