Professional Documents
Culture Documents
Kitabu Cha Sala 5
Kitabu Cha Sala 5
(1) Mtu akitaka kufanya jambo kubwa au dogo ni bora aombe rukhsa kwa Mungu. Na akihitaji
kitu akitamani amuombe Mungu. Tunatakiwa tumuombe Mungu hata chumvi ya kupikia mara
moja.
(2) Nimemsikia shekhe akisema kuwa ukishakusali sala hii si lazima uambiwe kuwa fanya au
usifanye. Mwenyewe utajua kwa kulitaka lile ulilokusudia au kulikataa yaani utaraghibika
kulifanya au utaona si jema, yaani utahisi. Kuna watu wawili waaminifu kwa nijuavyo mimi
wamesali sala hii na wamepata uwamuzi sahihi, wamefurahi.
(3) Wengine wameona bora kuifundisha sala ya kuomba haja peke yake na sala ya kutaka rukhsa
iwe mbali. Mimi nafupisha kwa maelezo haya haya wewe nuilia lile ulilokusudia.
(4) Ikiwa umekusudia kufanya jambo zuri muombe Mungu akuwafikishe uweze kulifanya
akutilie barka na kheri nyingi ndani yake. Ikiwa jambo hilo halina kheri na wewe akuepushe nalo
asikujaalie kulitenda na akuongoze kwenye jema.
(5) Mtu humuomba Mungu wakati wowote lakini kuna nyakati nyengine nzuri zaidi tutazitaja
baadaye na ni bora kwanza kusali sala hii ikiwa unataka uwe karibu zaidi na kutakabaliwa.
(6) Ni sala ya rakaa mbili. Husaliwa wakati wowote usiokatazwa kusali lakini bora usiku na ni
bora kuisali siku tatu mfululizo.
(7) Ukishamaliza kusali soma dua. Tutaitia hapa aliyotufundisha Mtume S. A. W. tuliyoipata
vitabuni.
(8) Wala si lazima kuitamka hiyo haja yako kwa kiarabu. Mola anajua haja yako kuliko
unavyoijua wewe mwenyewe. Iseme moyoni au kwa kuitamka kwa lugha ujuwayo baada ya dua.
(9) Huu mfano tu, omba utakavyo wala usipange kuwa ntasema nini ntaomba vipi, omba kama
unamuona Mungu mbele yako, yuko mbele yako kweli na kama humuoni yeye anakuona
anakusikia.Taja haja yako kama kuolewa, kuoa, kusafiri, kuuza shamba na kama hayo. Kama haja
yako ni kuolewa na Abdulla.
" Ewe Mola wangu mimi nataka kuolewa na Abdulla basi ikwa ndoa hii ina kheri na mimi
nakuomba unijaalie aniowe ututilie kheri nyingi na barka ndani yake. Na kama haina kheri na
mimi nakuomba isiwe na uniepushe nayo kwa salama na unipe lililonakheri na mimi tena
uridhike nalo Mola wangu". kisha utamsalia Mtume S. A. W. kama tulivyoelekeza.
(10) Umewahipo kuisali sala hii, au hata umefikiripo kuisali. Tia nia ya kuisali usijiweke mbali na
dini yako.
(11) Ukitaka kutamka nia:-
Kuomba dua
Hapa ni pazuri kutaja kidogo yahusuyo dua. Tazama kitabu changu kiitwacho Hivi Ndio
Kuabudu cha 1995 ukurasa wa 53 kuna maelezo ya namna ya kuomba dua. Kama huna
nikuletee chako lakini omba dua zako kama kawaida yako usingoje kitabu huenda kikachelewa
kukufika au kisikufike.
* wakati nzuri wa kuomba dua
(1) laylatulqadir (2) usiku wa nusu ya Shaabani
(3) siku ya Arafa (Arafa) (4) laylatiljumaa
(5) kila siku usiku (6) kabla na baada ya sala
(7) baada ya adhana (8) kabla ya iqama
(9) akifuturu ( mfungaji) (10) Mwezi wa Ramadhani
(11) baada ya mawaidha ya dini.
* pahala pazuri
(1) Msikitini Makka (2) Msikitini Madina
(3) Safa na Marwa (4) Msikiti (Beitl Maqdis)
(5) Msikiti wowote (6) Arafa na Muzdalifa
(7) Muna baada ya kupiga mawe .
* wakati mzuri
(1) ndani ya kusujudu (2) ndani ya kufunga
(3) Unapoamka (4) safarini
(6) inaponyesha mvua (6)) unapokunywa maji ya zamzam
Nakumbusha kuwa unaweza kuomba dua wakati wowote pahala popote na katika kitendo
chochote chema. Humu nilimotaja ni afadhali na uwezekano wa kutakabaliwa ni mkubwa zaidi.
Sala ya Maiti
(1) Kuna thawabu nyingi sana katika kumsalia maiti. Inasikitisha sana kuwa wengi wetu ingawa
tunakwenda kuzika lakini wachache tunaomsalia. Mashekhe wengi wanasema hii ni faridha
kwani maiti asiposaliwa watu hupata dhambi.
(2) Sala hii tumeifundisha katika vitabu vitatu vyengine kwa hivyo hapa tuaitia kwa ufupi. Vitabu
hivyo ni kiitwacho Sala ya Maiti na chengine Huduma za Maiti na Kitabu cha Hijja na Umra.
Tafadhali visome.
(3) Husaliwa jamaa au hata mtu peke yake. Ina takbiri ya kuhirimia na nyengine tatu. Zote ni nne.
Haina kurukuu wala kusujudu. Ni kusimama tu kwa wanaoweza.
(4) Haina kusoma Qur-an baada ya alhamdu.
(5) Anza sala yako kama kawaida kwa tawjihi na nia. Imamu akileta takbiri ya kuhirimia nawe
ilete. Na hii ndio ya mwanzo.
(6) Soma alhamdu, ukisha msubiri imamu.
(7) Akileta imamu takbiri ya pili nawe ilete, usimtangulie imamu katika takbiri zote.
(8) Baada ya takbiri ya pili (i) Msalie Mtume S A W au (ii) soma alhamdu ya pili. Khiari yako.
Wa zamani wakisoma alhamdu ya pili.
(9) Msubiri imamu akileta takbiri nawe ilete, hii ni ya tatu.
(10) Soma dua. Tutakutilia dua fupi, ukitaka refu utaipata pahala pengine.
kama umesoma alhamdu mbili msalie Mtume S.A.W. katika hii dua. Tutakutilia hapa dua ya
kumsalia Mtume S. A. W. pia kwa ufupi.
(11) Msubiri imamu akileta takbiri ya nne nawe ilete.
(12) Msubiri imamu akitowa salamu nawe maliza sala yako kwa salamu pia. Kasha omba
maghfira na kushukuru, ukiwa na hakika kuwa nawe siku yako haiko mbali.
(mwanamme)
mwanamke)
*
* *
(13) Ikiwa ulisoma alhamdu mbili, hapa,mwisho wa dua msalie Mtume S. A. W..
(14) Kila ukitaka kumsalia Mtume S.A.W. soma hii au kama hii.