You are on page 1of 115

Page | 1

YALIYOMO:
 Utangulizi.......................................................................3
SEHEMU YA KWANZA:
 FAIDA ZA SURA MBALIMBALI ZA QUR’AN TUKUFU
Faida ya Surat FAATIHA..............................................4
Faida ya Surat IKHLASWI............................................16
Faida ya Surat NNAS..................................................24
Faida ya Surat NASR..................................................29
Faida ya Surat HADIDY..............................................31
Faida ya Surat YASIIN.................................................36
SEHEMU YA PILI:
 MASAAA YA KAZI ZA DUA NA TIBA MBALIMBALI
Siku ya Jumapili Shamsi......................................42
Siku ya Jumatatu Qamar....................................45
Siku ya Jumanne Mirihi........................................47
Siku ya Jumatano Atwarid/Utawarid...............49
Siku ya Alkhamis Mushtara..............................51
Siku ya Ijumaa Zuhurat........................................53
Siku ya Jumamosi Zohar.......................................55

SEHEMU YA TATU:
 Majina 28 ya BARHATIH
Utukufu wa Majina 28 ya BARHATIH.........................58
Faida ya kuyasoma majina 28 ya BARHATIHI.........61
Utaratibu wa kuyasoma majina 28 ya BARHATIH...63
Matumizi ya majina ya BARHATIH.............................65
Kombe la majina ya BARHATIH.................................72
Ruqya ya majini ya Barhatihi....................................80
Faida za jina moja moja la Barhatih........................82
Page | 2
UTANGULIZI:
Kitabu hiki kimeandikwa na:-
Bashir Hussein Lugamba
Simu: +255 757 455 646
+255782 010 104
+255 672 410 104
+255 628 289 078
E-mail: ustadhbashir31@gmail.com/bashirustadh@gmail.com

Kikiwa ni kitabu cha nne katika vitabu alivyoviandika Bashiri


Hussen Lugamba. Kama bado haujazipata nakala za vitabu
hivyo unaweza kuwasiliana nane kwa mawasiliano hayo
yaliyopo hapo juu.
Ndugu Msomaji kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu
aliyeniwezesha kukuandikia kitabu hiki kilicho kusanya tiba
kupitia Qur’an tukufu na maji 28 ya BARHATIH zenye kufaa
dhidi ya uchawi, majini na maradhi mbalimbali
yanayosababishwa na uchawi na majini.
Lengo ni kukufahamisha wewe ndugu yangu msomaji
uweze kuzitumia tiba hizi ili uweze kuepukana na shida na
maradhi mbalimbali yaliyokithiri katika jamii na hasa Marathi
yatokanayo na uchawi na majini.
Nitafutahi sana kama utasoma kitabu hiki na ukaamua
kuyafanyia kazi yaliyomo humu na sio kusifia tu.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu ajaalie kila atakaye soma
kitabu hiki akielewe na ayafanyie kazi yaliyomo humu. Na
popote utakapokwama nitakusaidia kupitia anuani yangu
iliyopo hapo juu.

Nakutakia usomaji mwema wa Kitabi hiki

Bashiri Hussen Lugamba/ Ustadhi Bashiri

Page | 3
SEHEMU YA KWANZA
FAIDA YA SURA MBALIMBALI ZA QU’RAN TUKUFU.
FAIDA YA SURATUL FAATIHA
(SURA YA 1)

Suratul FAATIHA ndio Sura ya kwanza katika


mpangilio wa Sura zilizomo ndani ya kitabu kitukufu
cha Qur’an. Sura hii inafaida nyingi sana katika
ulimwengu wa tiba kupitia kitabu kitukufu cha
Qur’an.

Sura hii inatibu maradhi zaidi ya 70 na kuondosha


shida mbalimbali katika maisha ya mwanadamu.
Tuangalie baadhi ya faida za sura hii katika kutibu
maradhi na kuondosha shida mbalimbali.

Page | 4
1. NI KINGA YA MARADHI YOTE.

Ifikapo siku ya Ijumaa baada ya swala ya Ijumaa


soma surat FAATIHA x 7, Surat NNAS x 7 na Surat
FALAQ x 7.

Kisha tia nia yako juu ya kisomo hicho kuwa


unahitaji ALLAH (S.W) akukinge kutokana na
maradhi yote. Maradhi ya Kibailojia, maradhi ya
Kijini na maradhi ya kichawi na Hasidi zote za majini
na binaadamu. Hakika utakingwa na maradhi
hayo kwa muda wa wiki nzima.

Amali hii unaweza kuifanya kila siku ya Ijumaa,


ikawa ndio uradi wako.

2. KUPOOZA MAUMIVU YA VIUNGO KATIKA MWILI.


Iwapo kama unasumbuliwa na maumivu ya aina
yoyote katika viungo, basi utasoma Suratul Fatiha
kwa idadi ya mara 14, kwa nia ya kuyaondosha
maumivu hayo, ukiwa umeshika eneo hilo lenye
maumivu. Hakika maumivu hayo yatakwisha
kabisa kwa uwezo wa M/Mungu.

3. KUVUTA MVUA SEHEMU YENYE UKAME.


Iwapo kama katika eneo lenu mmekumbwa na
ukame mvua hazinyeshi eneo hilo, nawe ukahitaji
kumuomba ALLAH (S.W) akuleteeni mvua zenye
Baraka kwa ajili ya mazao.

Page | 5
Basi utachukua maji katika chombo, kisha utaweka
katika kiganja chako huku ukiwa unaweka nia
yako ya kuhitaji M/Mungu akuleteeni mvua katika
eneo hilo. Kisha utaanza kusoma Surat FAATIHA
kwa kuirudia rudia hali ya kuwa yale maji yanavuja
kutoka katika kiganja chako cha mkono.

INSHAALLAH haitopita wiki moja mvua itanyesha


katika eneo hilo.

4. KUTULIZA MVUA YENYE MADHARA IACHE


KUNYESHA.
Iwapo kama unataka kuituliza mvua yenye imeleta
madhara katika kunyesha kwake basi utachukua
mchanga mkavu, kisha utausomea Surat FAATIHA
mara 313 kwa nia ya kuhitaji mvua hiyo iache
kunyesha katika eneo hilo.

Kisha baada ya kumaliza kusoma Surat FAATIHA


kwa idadi hiyo utautupia ule mchanga katika eneo
ambalo mvua inanyesha. Hakika hayatopita
masaa mawili kwa uwezo wa M/Mungu mvua hiyo
itaacha kunyesha. INSHAALLAH.

5. KUSAFISHA NYUMBA AU CHOMBO CHAKO CHA


KAZI KUTOKANA NA NUKSI.
Iwapo Kama unahitaji kuisafisha nyumba yako au
chomco chako cha kazi (mfano Mtumbwi, gari,
pikipiki n.k) kutokana na Nuksi na Mikosi basi
Page | 6
utaiandika Suratul FAATIHA katika chombo au
karatasi kwa wino wa dhafarani kisha utayaosha
hayo maandishi kwa maji yaliyosafi.

Kisha maji hayo utatumia kusafishia hiyo nyumba


yako kwa kudekia dekia ndani au katika hicho
chombo chako cha kazi. Hakika Nuksi na Mikosi
itakwisha kabisa katika chombo au nyumba hiyo
kwa uwezo wa M/Mungu. Dua hii mujarrabu sana.

6. KUFUNGUA RIZIQI NA MAMBO YALIYOFUNGWA.


Kama unahitaji kufungua Riziq zako au mambo
yako yaliyofungwa basi utafanya yafuatayo:-
Utachukua nafaka aina 9 (mfano, mahindi,
mtama, mpunga, ulenzi, ufuta n.k) kisha
utazisomea nafaka hizo Suratul FAATIHA kwa idadi
ya mara 99. Kisha nenda kawape ndege wale zile
nafaka (Mfano, kuku, njiwa, nk) wakati unawapa
ndege utakuwa unatia nia yako ya kuhitaji
M/Mungu akufungulie mambo yako au Riziqi zako
zilizofungwa kwa uwezo wa M/Mungu INSHAALLAH
mambo yako yatafunguka.

7. KUTIBU MARADHI AINA MBALIMBALI MWILINI.


Iwapo kama unahitaji kutibu maradhi aina
mbalimbali katika mwili wako, (mfano maradhi ya
Kibailojia, maradhi ya Kijini, maradhi ya kichawi),
basi utaiandika Surat FAATIHA kwa kutumia wino
wa dhafarani, kisha utayaosha hayo maandishi
kwa maji yaliyo safi au maji ya mvua. Maji hayo
Page | 7
utatumia kwa kunywa grasi moja asubuhi na grasi
moja jioni. Fanya hivyo kwa muda wa siku saba
mfululizo. ISHAALLAAH maradhi hayo yatakwisha.

8. KUONDOA MIKOSI NA NUKSI SUGU KATIKA MWILI.


Utasomea katika maji yaliyosafi Surat FAATIHA kwa
idadi ya mara 40. Kisha maji hayo atamwagiwa
kichwani mtu mwenye matatizo ya NUKSI na
MIKOSI katika mwili wake. INSHAALLAH
ataondokana na mataizo hayo.

9. KUKIDHIWA HAJA YA JAMBO LAKO LOLOTE.


Iwapo kama unahaja ya jambo lako lolote nawe
unahitaji M/Mungu akujibu basi utafunga swaumu
ya sunna katika siku saba mfululizo ndani ya
swaumu hiyo utakuwa unasoma Surat FAATIHA
mara 111 na unamswalia Mtume (s.a.w) mara
111wakati wa kufuturu, jiepushe na kula mboga au
vitu vyenye roho (mfano, samaki, kuku, mbuzi n.k).
Baada ya kufuturu utamuomba M/Mungu haja ya
jambo lako hapo. Dua hii ni Mujarrabu sana.

10. KUKUBALIWA HAJA AU DUA YA JAMBO LAKO


LOLOTE.
Iwapo kama unahitaji kukubaliwa haja au Dua
yako yoyote utasoma Suratul Faatiha kwa
utaratibu ufuatao.

Page | 8
Utasoma Suratul Faatiha mara 21 kila baada ya
swalatil Fajri, kisha utasoma mara 22 Suratul Faatih
kila baada ya swalat Dhuhuri, kisha utasoma
Suratul Faatiha mara 33 kila baada ya Swalati
Raasir, kisha utasoma mara 24 kila baada ya
swalati Magharibi, kisha utasoma suratil Faatiha
mara 10 kila baada ya swalati Raishai.

Utaratibu huo utaufanya kila siku kwa muda wa


siku 40 mfululizo ISHAALLAHH haja ya jambo lako
litatimia.

11. KUACHWA HURU KUTOKA MAHABUSU AU


GEREZANI.
Iwapo kama umefungwa au umekamatwa kwa
uonevu nawe ukahitaji kutoka mahabusu au
gerezani, basi utasoma Suratul Faatiha kwa idadi
ya mara 111 kila siku kwa muda wa siku saba
mpaka 14. INSHAALLAH utaachiwa huru na
kutolewa, mahabusu au gerezani.

12. KUPATA RIZIQ KWA WEPESI KATIKA NJIA


USIZOZITEGEMEA.
Utasoma Suratul Faatiha kwa idadi ya mara 41
mwisho wa usiku kuanzia (saa 9 – 11) usiku
INSHAALLAH utafungukiwa na Riziq mbalimbali
katika njia uzisozitegemea.

Page | 9
13. KUSAFISHA NYUMBA KUTOKANA NA UCHAWI.
Utasomea katika maji Suratul Faatiha mara saba,
Ayatul Qursiyyu mara saba na Aya tano za
mwanzo za Suratu Jinni mara saba.

Kisha maji hayo utatumia kudekia dekia ndani ya


nyumba yako na kumwagia nje ya uwanja wako.
Hakika kama eneo hilo kuna uchawi utabatilika
na hautofanya kazi tena wala kukudhuru.

14. KUUFANYA MTI USIOTOA MATUNDA UTOE


MATUNDA YAKE.
Iwapo kama umepanda mti wa matunda kisha
mti huo baada ya muda ukaacha kutoa
matunda kwa sababu zisizojulikana, basi
utaiandika Suratul Faatiha yote katika chombo au
katarasi kwa kutumia wino wa dhafarani.

Kisha chini ya sura hiyo baada ya kuiandika


utaiandika ile aya namba nne (4) mara saba kwa
kushuka chini “MMALIKI YAA UMIDINI”. Utaandika
aya hiyo kwa lugha ya kiarabu kisha maandishi
hayo utayaosha kwa maji safi, kisha maji hayo,
utatumia kuumwagilia mtu huo asubuhi na jioni
kwa siku saba mfululizo. INSHAALLAH mti huo
utaanza kutoa matunda kwa uwezo wa
M/Mungu.

Page | 10
15. UKITAKA KUYAONA MAAJABU MBALIMBALI YA
M/MUNGU
Iwapo kama unahitaji kuyaona maajabu
mbalimbali ya M/Mungu na miujiza yake, basi
utasoma Suratul Faatiha kwa idadi ya mara 800
katika kikao kimoja kwa muda wa siku saba zenye
kufuatana, kisha unatia nia ya jambo lako hilo
unalohitaji. Hakika M/Mungu atakuonyesha
maajabu na miujiza yake katika dunia hii.

16. KUJIBIWA DUA YA JAMBO LAKO LOLOTE.


Kama unahaja ya jambo lako nawe unahitaji
ALLAH (S.W) akujibu au akutimizie basi utafanya
yafuatayo;

Baada ya kuswali Swalatil Magharibi, utaswali


swalatul Hajjah yenye rakaa mbili kisha utataja
haja ya jambo lako hapo. Kisha utasoma Suratul
Faatiha kwa idadi ya mara 40 bila kunyanyuka
katika eneo hilo, kisha utaomba dua zako hapo.
INSHAALLAH mwenyezi Mungu atakutimizia haja
hiyo.

17. KUONDOA HUSDA ZA MAJINI, WACHAWI NA


KUCHUKIWA NA WATU BILA SABABU.
Utachukua chombo kisafi kisha tia maji ndani
yake. kisha maji hayo yasomee Suratul FAATIHA
mara 41, AYATUL QURSIYYU mara 7, LAA ILAAHA
ILA ANTA SUBHAANAKA IN KUNTUMINA
Page | 11
DHWALIMIIN X41, Suratul FALAQ x 7 na SURAT
NNAS x 7.

Kisha maji hayo utatumia kwa kuoga asubuhi na


jioni kwa siku saba zenye kufuatana. INSHAALLAH
utaondokana na changamoto hiyo

18. KUPATA HIFADHI YA MASOMO, HADITHI AU JAMBO


LOLOTE UTAKALO LIONA NA KUHADHITHIWA.
Iwapo kama unahitaji kuwa na hifadhi nzuri katika
masomo au jambo lolote unaloliona au kusikia au
kuhadithiwa, basi utasoma Suratul Faatiha kwa
utaratibu ufuatao.
Utasoma suratul Faaatiha katika maji kwa idadi ya
mara 70 kila siku, kwa muda wa siku saba
mfululizo. Kisha maji hayo siku ya saba utakunywa
kwa nia ya kupata hifadhi ya masomo au hadithi
au jambo lolote unaloliona au kuhadithiwa.

Inshaalla utakuwa na hifadhi kubwa ya masomo


na hadithi wala hautosahau kila jambo
ulalofundishwa INSHAALLAH.

19. KUPATA CHOCHOTE UNACHOKIHITAJI KATIKA


DUNIA HII AU AKHERA.
Katika Suratul FAATIHA kuna herufi saba ambazo
hazipatikani katika sura hiyo nazo ni:-
1. FE 2. JIIM 3. SHIN 4. THE 5. DHWE 6. KHE 7. ZE.

Page | 12
Katika herufi hizo zilizokosekana katika Suratul
Faatiha, kila herufi moja inasimama kuwakilisha
jina la M/Mungu.

1. F = FAARIDUN
2. J = JABBARUN
3. SHIN = SHUKURUN
4. THE = THAMITUN
5. DHW = DHWAHIRUN
6. KHE = KHABIRUN
7. ZE = ZAKIYYUN

Sasa iwapo kama mtu atadumu, kuyatamka


majina hayo ya M/Mungu kwa idadi ya mara
1000 kila siku, kwa kila siku anatamka jina moja

Jumapili YAA FAAARIDUN X 1000


Juma tatu YAA JABBARUN x 1000
Jumanne YAA SHUKURUN x 1000
Juma tano YAA THAMITUN x 1000
Alkhamisi YAA DHWAHIRUN x 1000
Ijumaa YAA KHABIYRUN x 1000
Jumamos YAA ZAKIYYUN x 1000

Kisha baada ya kutamka jina hilo la siku husika


utamuomba M/Mungu haja ya jambo lako lolote
liwe la kidunia au Akhera. INSHAALLAH ALLAH
(S.W) atakutimizia jambo hilo.
Page | 13
20. KUPATA MAKHADIMU (WATUMISHI/ MALAIKA WA
SURATUL FAATIHA).
Ukihitaji kuwapata Makhadimu (watumishi
wanaoitumikia Surat Faatiha na uweze kufanya
nao kazi, (mfano kukukufanyia jambo lolote
ulitakalo, kuponyesha mgonjwa wako maradhi ,
kukupa habari kupitia ndoto, kukufundisha elimu
za aina mbalimbali i.e elimu za tiban.k) au dua
zako unataka ziwe ni zenye kukubalika na mambo
mengine mengi.

Utafanya mambo yafuatayo:-


Utakaa (RIADHA) utajitenga sehemu ya pekee
yako ndani au katika chumba chenye utulivu na
utahitajika uwe umefunga swaumu ya Sunna hali
ya kuwa umevaa nguo zilizo safi na twahara
zenye rangi nyeupe zilizotokana na chumu la
halali katika mali yako.

Amali hiyo utaianza siku ya jumapili utaanza


kusoma kama ifuatavyo.

Juma pili utasoma AYATUL QURSIYYU mara


313, kisha utasoma na BISMILLAH
RRAHMAAN RRAHIIM x 582, ambayo
ni aya ya kwanza katika Suratul
FAATIHA.

Page | 14
Jumatatu Utasoma Aya ya pili katika Suratul
Faatiha mara 618.

Jumanne utasoma aya ya tatu katika Suratul


Faatiha mara 242.

Jumatano Utasoma aya ya nne katika Suratul


Faatiha mara 236.

Alkhamisi Utasoma Aya ya tano katika Suratul


Faatiha mara 1037.

Ijumaa Utasoma aya ya sita katika Suratul


Faatiha mara 807.

Jumamosi Utasoma Suratul Faatiha aya ya


mwisho mara 1034.

Baada ya kila unapomaliza kisomo chako


utakuwa unaamrisha makhadimu wa suratul
Faatiha kwa kusema
“Nimewaiteni enyi watumishi wa suratul faatiha,
nahitaji nifanye kazi na nyie” (Kisha utataja haja
zako hapo).

Baada ya kumaliza amali hiyo siku ya saba


wanaweza kukujia katika ndoto, au ukaona dalili
ya maumivu ya kichwa kiasi kwa muda basi hiyo
ni dalili ya kufahamu kuwa hao Makhadimu teari
wameshakuja na wapoteari kukutumikia. Na
Page | 15
wakati wa kufuturu jioni kipindi unafanya amali
hiyo, jiepushe kufuturu vyakula au mboga zenye
asili ya kuwa na roho (mfano, nyama, samaki n.k)
bali ule vyakula vyenye asili ya matunda n.k).

FAIDA YA SURATUL IKHILASWI


(SURA YA 112)

Suratul Ikhilaswi ni Sura ya 112 katika mpangilio wa


Sura zilizomo ndani ya kitabu kitukufu cha Qur’an.
Sura hii ni miongoni mwa zile sura tano zilizotelemka
kwa AMRI. Zinajulikana kama sura za Amri, ambazo ni
Surat Jinn, Surat Qafiruun, surat Falaq, Surat Ikhilaswi
na Surat Nnas.

Sura hii ilishushwa kwa ajili ya kumtakasa M/Mungu


kutoka na shirki za aina zote alizozushiwa na makafiri
enzi za Mtume. Ikiwa ni pamoja na kuambia
Mwenyezi Mungu ana watoto, M/Mungu anafanana

Page | 16
na kitu Fulani, M/Mungu alizaliwa n.k. yote hayo
Mwenyezimungu alikuja kuyakanusha kupitia sura hii.

Sura hii pindi mtu aisomapo hupata faida nyingi sana


ikiwemo, thawabu, kuponyeshwa maradhi katika
mwili wake na kuondolewa shida na matatizo
mbalimbali. Tuangalie baadhi ya faida za sura hii.

1. KUPATA KINGA DHIDI YA MAJINI NA KUBATILISHA


HUKUMU/KESI.
Mwenye kusema neno YAA SWAMADU (neno hili
lipo katika aya ya pili katika sura hii)kwa idadi ya
mara 134 katika kikao kimoja, hupata kinga ya
kuingiwa na kuzuliwa na kila aina ya shetani na
kijini wala wa kibinadamu.

Pia neno hilo ukilitamka mara 134 kwa nia ya


kuzima kesi au kubadilisha hukumu basi M/Mungu
hukutimiza haja hiyo INSHAALLAH.

2. KUTEKELEZEWA JAMBO LAKO LOLOTE UTAKALO


MUOMBA M/MUNGU.
Mwenye kusoma Surat Ikhilaswi kwa Idadi ya mara
1001 katika kikao kimoja, Mwenyezi Mungu
atamtekelezea haja yake yoyote atakayoiomba
baada ya A’amali hiyo INSHAALLAH.

Page | 17
3. KUSAMEHEWA MADHAMBI YA MIAKA 100.
Mwenye kusoma Surat Ikhilaswi mara 101 katika
kikao kimoja M/Mungu atamsamehe madhambi
yake mtu huyo ya miaka 100.

4. KUWEKWA MBALI NA MOTO WA JAHANNAM.


Mwenye kuisoma Suratul Ikhilaswi kwa idadi ya
mara 100 M/Mungu atamuweka mbali na moto wa
Jahannam mtu huyo, kwa rehema zake.

5. KUSAMEHEWA MADHAMBI YAKO NA KUEPUSHWA


NA MADHAMBI YAJAYO.
Mwenye kusoma Surat Ikhilaswi kwa idadi ya mara
51 M/Mungu atamsamehe madhambi yake na pia
atamuepusha na madhambi yajayo mtu huyo.

6. KUJENGEWA KASRI KATIKA PEPO YAKO.


Mwenye kusoma Suratul Ikhilaswi kwa idadi ya
mara 21 katika kikao kimoja M/Mungu atamjengea
Kasri katika pepo yake mtu huyo (Kasri ni mji wa
kifalme peponi).

7. KUJENGEWA JUMBA LA KIFAHARI KATIKA PEPO


YAKO.
Mwenye kusoma Suratul Ikhilaswi kwa idadi ya
mara 10 katika kikao kimoja M/Mungu
atamjembea jumba la kifahari katika pepo yake
mtu huyo.
Page | 18
8. KUKIDHIWA HAJA ZA MAOMBI YAKO.
Mwenye kusoma Surat Ikhilaswi kwa idadi ya mara
10 pindi jua linapochomoza katika siku ya Jumapili,
Mwenyezi Mungu atamkidhia haja yake yoyote
atakayo muomba M/Mungu.

9. KUONESHWA WATU WANAOKUFANYIA UBAYA/


WANAOKULOGA/ MAADUI ZAKO.
Iwapo kama unahitaji uonyeshwe watu
wanaokufanyia ubaya au wanaokuloga au
maadui zako basi utasoma Suratul Ikhilaswi mara
10 na Suratul Qafinuni mara 10. Pindi
unapokwenda kulala kisha utatia nia ya jambo
lako unalotaka M/Mungu akuonyeshe.
INSHAALLAHH utaliona jambo hilo katika ndoto.

10. KUKUBALIKA DUA ZAKO AU HAJA YA JAMBO LAKO.


Mwenye kutekeleza amali hii kupitia Surat Ikhilaswi
kwa muda wa siku 41 mfululizo Mwenye Mungu
atamtekelezea haja yake yoyote atakayoiomba
hata iwe kubwa kiasi gani.

Utakuwa unaswali Rakaa nne za Swalatul Hajjah


kila siku, kwa muda wa siku 41 mfululizo. Katika
Rakaa ya kwanza utakuwa unasoma Surat
Faatiha mara moja na Suratul Ikhilaswi mara 10,
katika Rakaa ya pili utasoma suratul Faatiha mara
moja na Surat Ikhilaswi mara 20. Katika Rakaa ya
Page | 19
tatu utasoma surat Faatiha mara moja na Surat
Ikhilaswi mara 30 katika Rakaa ya nne utasoma
Surat Faatiha mara 1 na Surat Ikhilaswi mara 40 .

Baada ya hapo utafanya Istighafari mara 100,


utamsalia mtume (s.a.w) 100, na utasoma neno
“HASBUNALLAHU WA NAIMAL WA KIILI” mara 100.

11. KUFUKUZA MASHETANI NA MAJINI WABAYA NDANI


NYUMBA YAKO.
Iwapo kama unataka kufukuza majini na
mashetani wabaya katika nyumba yako,
utatafuta ubani shari (mfano halititi, miatusaila,
uban mashitaka, na mruturutu) vyote
utachanganya pamoja kisha utakuwa unachoma
mafusho hayo pindi unasoma dua yako.

Utasoma Suratul Ikhilaswi kwa nia ya kufukuza


viumbe wabaya ndani ya nyumba yako kwa
idadi ya mara 1001.

12. KUFUNULIWA SIRI MBALIMBALI ZA M/MUNGU.


Kama unahitaji M/Mungu akufunulie siri zake
mbalimbali, ambazo wanadamu wengine
hawazifahamu, wala hawajawahi kuziona basi
utasoma Surat Ikhilaswi kwa idadi ya mara 3226
katika kikao kimoja. INSHAALLAH utaona maajabu
ya M/Mungu kwa dua hiyo.

Page | 20
13. KUTIBU MARADHI YA PRESHA, MOYO NA MARADHI
YA INI.
Utaiandika Suratul Ikhilaswi mara tatu Suratul
Faatiha mara tatu, Surat Falaq mara tatu na
Suratul Nnas mara tatu katika karatasi nyeupe
kwa wino wa dhafarani. Kisha utayaosha
maandishi hayo kwa maji safi. Kisha ndani ya maji
hayo utaweka na maji ya waridi (woter rose)
chupa mbili.

Kisha utatumia mchanganyiko huo wa maji kwa


kunywa kutwa mara tatu grasi moja kwa siku saba
mfululizo. INSHAALLAH utapona maradhi hayo.

14. KUTIBU MARADHI SUGU KATIKA MWILI.


Kama unasumbuliwa na maradhi sugu katika
mwili, ambayo umeambiwa kuwa maradhi hayo
hayana tiba. Au umetumia dawa aina mbalimbali
bila mafanikio basi utatumia tiba hii na Mwenyezi
Mungu atakuponyesha kwa rehema zake.

Utaiandika Suratul Faatiha mara tatu, Suratul


Ikhilaswi mara tatu, Suratul Falaq mara tatu,
Suratul Nnas mara tatu na Ayatul qursiyyu mara
tatu, katika karatasi nyeupe kwa wino wa
dhafarani.

Kisha maandishi hayo utayaosha kwa maji safi,


kisha ndani yake utaweka halititi kidogo na
chumvi ya mawe halafu maji hayo utayatumia
Page | 21
kwa kunywa gras moja kutwa mara tatu, na maji
mengine utakuwa unaoga kwa mfumo wa
kijupakaa mwili mzima. Hakika utapona maradhi
hayo INSHAALLAH.

15. KUFUNGULIWA MAMBO YAKO YALIYOFUNGWA.


Utaswali sunatul Hajjah Rakaa mbili, rakaa ya
kwanza utasoma Suratul Faatiha na Surat Qafirun,
Rakaa ya pili utasoma Suratul Fatiha na Surat
Ikhilaswi, kisha baada ya kutoa salaam, utafanya
Isitaghafari mara 100 na utamswalimu Mtume
(s.a.w) mara 100.

Kisha utasoma Surat Ikhilaswi mara 1000, na kila


ukifika idadi ya mia moja (100) utakuwa unatia nia
yako hapo, kisha unaendelea na kisomo chako
mpaka umalize.

16. KUWAREHEMU MAREHEMU.


Kama unataka kumuombea dua marehemu
wako M/mungu amsamehe na kumrehemu basi
utaswali Rakaa mbili za Sunatul Hajjah, katika
rakaa ya kwanza utasoma Surat Faatiha mara
moja na Surat Ikhilaswi x 11 na suratul Takathur
mara 11 na katika rakaa ya pili utafanya hivyo
hivyo kama ulivyofanya katika rakaa ya kwanza.

Kisha ukimaliza swala yako hiyo utafanya


istighafari kwa niaba ya marehemu huyo mara
100, kisha utamswalia mtume mara 100.
Page | 22
INSHAALLAH ukitekeleza A’amali hiyo Mwenyezi
Mungu atampelekea Malaika elfu 1000 huyo
marehemu katika kaburi lake kwa ajili ya
kumuombea msamaha na watamkinga na
adhabu za kaburi, na watakaa nae katika kaburi
lake wakimliwaza mpaka siku ya kufufuliwa mtu
huyo.

17. KUONDOSHA MIKOSI NA NUKSI KATIKA MWILI.


Utaiandika Suratul Ikhilaswi katika karatasi nyeupe
kwa wino wa dhafarani kwa idadi ya mara 11.
Kisha utayaosha maandishi hayo kwa maji safi.
Kisha ndani yake utaweka chumvi ya mawe
kidogo na karafuu maiti madonge mawili. Kisha
maji hayo utayasomea Surat Ikhilaswi mara 11.

Kisha maji hayo utatumia kwa kuoga asubuhi na


jioni kwa muda wa siku tatu mpaka saba.
INSHAALLAH Nuksi na Mikosi katika mwili
itaondoka na utakuwa na Nuru kali sana na
mvuto.

18. KUBATILISHA UCHAWI MWILINI.


Iwapo kama mtu ana uchawi katika mwili wake
nawe ukataka uchawi huo uuwe au uuvunje
nguvu zake, basi utaiandika Surat Ikhilaswi mara 3,
Surat Falaq mara tatu, Surat Nnas mara tatu
katika karatasi nyeupe kwa wino wa dhafarani.
Kisha utayaosha maandishi hayo kwa maji safi
Page | 23
kisha mgonjwa mwenye uchawi katika mwili wake
atatumia maji hayo kwa kunywa grasi moja kutwa
mara tatu na maji mengine atumie kwa kuoga
asubuhi na jioni. INSHAALLAH uchawi huo
utabatilika.

FAIDA YA SURAT NNAS


(SURA YA 114)

Suratul Nnas ni sura ya 114 katika mpangilio wa sura


zilizopo katika kitabu kitukufu cha Qur’an. Sura hii ni
miongoni mwa zile sura tano zilizoshuka kwa AMRI
ambazo ni Surat Jinn, Surat kafiruuni, Surat Ikhilaswi,
Surat Faraq na Suratul Nnas.

Sura hii iliteremshwa baada ya Mtume (s.a.w)


kufanyiwa uchawi wa kurogwa. Pindi Mwenyez
Page | 24
Mungu alipotaka kumponyesha maradhi hayo basi
ndipo aliposhusha sura mbili (Surat Nnas na Surat
Faraq) malengo ya kushushwa sura hizi ilikuwa kama
ponyo ya maradhi yatokanayo na uchawi au majini.
Sura hii inafaida nyingi sana katika ulimwengu wa
tiba kupitia Qur’an tukkufu. Miongoni mwa faida hizo
ni pamoja na:-

1. KUTIBU MARADHI YA WASIWASI YATOKANAYO NA


MAJINI AU UCHAWI.
Kama mtu anasumbuliwa na maradhi ya wasiwasi
basi ataiandika Surat Nnas kwa kutumia wino wa
dhafarani. Kisha mwishowa sura hii kwa chini
ataandika aya ya Qur’an inayosema “WALLAHU
KHAYRUN HAFIDWIIN” ataandika kwa maandishi ya
kiarabu kama ulivyoiandika sura yenyewe.

Kisha karatasi hiyo wakati wa usiku utakuwa


unaiweka katika mchegemeo wako wa kulalia. Na
wakati wa mchana utakluwa unatembea nayo
umeiweka katika mfuko wako wa nguo, au pochi
au wallet yako. kwa uwezo wa M/Mungu maradhi
hayo ya wasiwasi yatakuondoka .INSHAALLAH.

2. NGOME YA KUJIKINGA NA HUSDA ZA WASHIRIKINA.


Mwenye kukithirisha kuisoma sura hii (Surat Nnas)
mara kwa mara, kila baada ya swala ya faradhi,
Mwenyezi Mungu atamjaalia mtu huyo kuwa na
ngome madhubuti dhidi ya washrikina na majini
wabaya (hawezi kurogeka mtu huyo).
Page | 25
3. KUTIBU MARADHI MBALIMBALI YATOKANAYO NA
UCHAWI NA MAJINI
Utaiandika surat Nnas katka karasi kwa wino wa
dhafarani kwa idadi ya mara saba (7) kisha
utayaosha maandishi hayo kwa maji safi. Kisha
utayasomea maji hayo Surat Nnas mara 70 surat
falaq mara 70 surat Nnas mara 70 na Ayatul
qursiyyu mara 70. Kisha ndani maji hayo utaweka
kidogo na halititi. Kisha maji hayo atatumia
mgonjwa mwenye maradhi yatokanayo na
uchawi na majini atatumia kwa kunywa kiasi cha
kikombe cha kahawa kutwa mara moja. Na maji
mengine atatumia kwa kuoga kwa mfumo wa
kujipaka mwili mzima, kwa siku saba mfululizo.
INSHAALLAH maradhi hayo yatakwisha.

4. KUVUNJA NGUVU ZA UCHAWI KATIKA MWILI.


Utaiandika surat IKhilaswi mara tatu, surat Falaq
mara tatu, surat Nnasi mara tatu kaktika chombo
au karatasi nyeupe kwa wino wa dhafarani. Kisha
utayaosha maandishi hayo kwaji safi. Kisha
mgonjwa atatumia kwa kunywa maji hayo kutwa
mara tatu kwa siku saba zenye kufatana
INSHAALLAH nguvu za kichawi zitakwisha katika
mwili wa mgonjwa huyo.

Page | 26
5. KUMVUTA MTU ALIOKO MBALI.
utachukua ubani maka, ubani dhukra kisha
utauchanganya pamoja, kisha utatia nia yako ya
kuhitaji kumvuta mtu uliyemkusudia baada ya
hapo utaupuliza ubani huo.

Kisha utasoma Surat Nnas kwa idadi ya mara 500,


na pindi unaposoma dua utakuwa unachoma
ubani huo na kila ukifika idadi ya 100 utakuwa
unatia nia, kisha unandelea tena kusoma mpaka
utakapomaliza kwa kutimiza idadi ya 500.
INSHAALLAH mtu huyo atakuja kwako haraka sana.

6. ANAYETAKA KUPENDWA NA JAMII AU KATIKA


BIASHARA.
Utasoma Surat NNas kwa idadi ya mara 500 na
sura waqiah mara saba (7) kisha utatia nia yako ya
jambo lako hapo. Hakika utapendwa sana na
watu au kupata mvuto katika biashara yako. au
unaweza kusoma surat Nnas mara 500 na
BISMILLAH RRAHMAN RRAHIIM mara 786 badala ya
kusoma suratul Waqiah

7. KURUDISHA KITU KILICHOIBIWA.


Utatafuta ubani shari (mfano, Halititi, miatus,
karafuu maiti, mruturutu, manemane n.k) kisha
utachanganya pamoja, halafu utakuwa
unachoma pindi unasoma dua yako.

Page | 27
Kisha utasoma Surat nnasi kwa idadi ya mara 500.
Na kila ukifika mara 100, utakuwa unatia nia yako
hapo mpaka unamaliza kusoma kwa idadi ya
mara 500. Dua hii utaifanya mara tatu kwa siku tatu
tofauti tofauti. INSHAALLAH kitu chako kitarajeshwa
haraka sana.

8. KUMPATA KHADIMU WA SURAT NNAS.


Iwapo kama unahitaji kuwaita MAKHUDAMU wa
Surat NNAS na uwaagize jambo lolote wakufanyie
basi utafanya kama ifuatavyo;
Tafuta muda wa kutosha kisha jitenge peke yako,
kisha utasoma Surat nnas mara 1000 katika kikao
kimoja, na kila ukifika idadi ya mara 100 utakuwa
unatia nia yako hapo. Kwa lugha yoyote
unayoifahamu ya kuwaamrisha wakufanyie jambo
lako lolote unalilihitaji (mfano, waende
wakamponyeshe mgonjwa wako maradhi Fulani,
wakufanyie jambo lako Fulani unalolitaka, waende
wakamuadhibu adui yako nk.)

Chochote utakachowaamrisha hakika


watakufanyia haraka sana. Sharti lake ni wewe
utekeleze kisomo hicho kwa idadi ya mara 1000
katika kikao kimoja.

Page | 28
FAIDA YA SURAS NASRI
(SURA YA 110)

Surat NASRI ni sura ya 110 katika kitabu kitukufu cha


Qur’an, sura hii inafaida nyingi sana. Kwa mtu
atakayeisoma sura hii mara 1 huandikiwa katika
kitabu chake cha A’ama sawa na ameisoma robo
ya Qur’an nzima.

Katika ulimwengu wa tiba kupitia Qur’an sura hii


inaweza kutumia kama siraha kali sana dhidi ya wezi,
majini, wanga au wachawi. Sura hii ina uwezo wa
kuwadhibiti watu hao wasiweze kuingia katika eneo
lako la nyumba, shamba au sehemu ya biashara.

Na atakaye lazimisha kuingia eneo hilo basi kwa


uwezo wa M/Mungu mtu huyo atanasa katika eneo
hilo mpaka wewe uliyetengeneza mtego huo
Page | 29
umruhusu ndipo atakapo ondoka eneo hilo mtu
huyo.

JINSI YA KUFUNGA NYUMBA DHIDI YA WEZI, MAJINI,


WANGA NA WACHAWI KUPITIA SURAT NASRI.
Iwapo kama unahitaji kumkamata mwizi anekuja
kukuibia eneo lako, iwe shambani, au nyumbani
kwako au sehemu ya biashara yako. Au kama
unahitaji kufunga nyumba yako wasiweze kuchezea
eneo hilo majini wabaya na wachawi basi utafanya
yafuatayo;
1) Tafuta mzizi wa mti wa mbono kaburi kisha
utaukata vipande ishirini (20).

2) Tafuta na yai la kuku zima (ambalo


halijaharibika). Kisha yai hilo utaliandika Surat
NASRI yote katika yai hilo kwa kutumia kalamu ya
wino nyekundu. Kisha mwisho wa sura hiyo kwa
chini utaandika maneno yafuatayo kwa lugha
ya kiarabu “WALAHAULA WALAQUATA ILA BILLAH
LA’ALIYUL ADHWIIM”.

3) Kisha utatafuta na uzi mweuzi wa kushonea


nguo. Kisha utaifunga miziz hiyo kwa kuzigawa
vipande vya mizizi vine vine na utavigawa katika
mafungu matano. Katika hayo mafungu matano
ya mizizi fungu moja utalifunga pamoja na yai lile
la kuku uliloliandika Surat NASRI.

Page | 30
Kisha mafungu hayo ya mizizi utakwenda kufukia
katika pembe nne za eneo unalotaka kulifunga
ima shamba, nyumba ua eneo lako la biashara
dhidi ya wezi au majini au wanga au wachawi.

Na pindi unapofukia mizizi hizo katika hizo


pembe, hapo ndipo utakuwa unatia nia ya
jambo lako vile unavyotaka iwe dhidi ya mtu
atakayeingia eneo hilo.

Fungu moja la hiyo mizizi lile lililofungwa pamoja


na yai utalifukia katikati ya eneo lako la uwanja
au shamba lako. Hapo kazi yako itakuwa
imekwisha.

Akija mtu katika eneo hilo kisha akanasa


kutokana na vile ulivyokusudia, basi kumzingua
kwake ni wewe kumsemesha na kumruhusu
aondoke eneo hilo. Usipomruhusu mtu huyo
hawezi kuondoka wala kuondolewa na mtu
yoyote tofauti na wewe uliyeweka mtego huo.

FAIDA YA SURAT HADIDY


(SURA YA 57)

Page | 31
Surat HADIDY ni sura ya 57 katika kitabu kitukufu cha
Qur’an sura hii ni miongoni mwa sura tukufu sana
katika kutibu maradhi yatokanayo na uchawi na
majini. Pia sura hii kama mtu ataitumia katika kuweza
kinga katika mwili wake basi mtu huyo atakuwa na
kinga ya mwili mithiri ya chuma. Kama sura hii
itatumika kwa ajili ya kuweka kinga ya nyumba au
sehemu ya biashara au shamba lako, basi eneo hilo
haliwezi kuchezewa na jinni, mchawi au mwanga
yoyote na patakuwa na kinga madhubuti sana eneo
hilo, tuangalie baadhi ya faida za sura hii katika tiba.

1. KINGA YA KUINGIWA NA JINI YOYOTE KATIKA MWILI


AU UCHAWI.
Utasoma Surat HADIDY aya nne za mwanzo ukiwa
umekusanya viganya vya mikono yako miwili kisha
utajipulizia hewa katika viganja hivyo, kisha
utajipangusa katika mwili wako kuanzia kichwani,
usoni, kifuani, tumboni na mgongoni. Isipokuwa
katika tupu yako ya mbele na tupu ya nyuma, na
katika chini ya nyayo za miguu yako. Dua hii
unaweza kuifanya asubuhi au jioni.

2. KINGA YA MWILI MADHUBUTI MITHILI YA CHUMA


DHIDI YA UCHAWI NA MAJINI.
Utachukua maji ya mvua (maji ya kutegwa) kisha
utatia nia yako ya kuhitaji kinga. Kisha utayasomea
maji hayo Aya nne za mwanzo za Surat HADIDY
Page | 32
kwa kuanza na BISMILLAH RRAHMAAN RRAHIIM.
Utasoma aya hizo kwa kuzirudia rudia kwa idadi ya
mara (7). Baada ya kumaliza kisomo hicho
utapuliza katika maji hayo mara saba kisha
utakunywa maji hayo. Hakika utakuwa na kinga
madhubuti katika mwili wako mithiri ya chuma.

3. KONDOSHA MARADHI YA NGOZI.


Iwapo kama mtu anasumbuliwa na maradhi ya
ngozi, mfano, upele, n.k basi utaziandika hizo aya
nne za mwanzo katika Surat HADIDY kwa wino wa
dhafarani katika karatasi nyeupe.

kisha utayaosha maandishi hayo kwa maji safi.


kisha mgonjwa anayesumbuliwa na maradhi hayo
ya ngozi atatumia maji hayo kwa kuoga asubuhi
na jioni, kwa muda wa siku tatu mfululizo.
INSHAALLAH atapona Marathi hayo.

4. KUWAADHIBU MAJINI WALIOPANDA KICHWANI:


Iwapo kama unahitaji kuwaadhibu majini
waliopanda kichwani kwa mgonjwa, basi
utamsomea mgonjwa huyo Surat HADIDY kwa
kuanza na AUDHUBILLAHI MINA SHETWAN RAJIIM
utasoma mara kumi a moja (11) kisha utaanza
kusoma Surat HADIDY kuanzia aya ya kwanza
mpaka aya ya nne kwa kuzirudia rudia aya hizo
mara kadhaa hakika mgonjwa huyo utamsikia
akipiga kelele sana kwa maumivu na uchungu
anaoupata kutokana na aya hizo.
Page | 33
5. KUZIMA KESI MAHAKAMANI INAYOKUSUMBUA.
Utaswali Sunatil Hajjah rakaa mbili, kisha utataja
haja yako hapo, kisha utakaa chini na kusoma au
kumsomea mtu mwenye kesi, utasoma aya nne za
mwanzo za Surat HADIDY utazisoma kwa idadi ya
mara 11. INSHAALLAH kesi hiyo itakwenda
kuvunjika haraka sana kwa uwezo wa M/Mungu.

6. KINGA YA NYUMBA DHIDI YA MAJINI NA WACHAWI


MADHUBUTI SANA.
Utaziandika hizo aya nne (4) za mwanzo katika
Surat HADIDY katika karatasi kwa kuanza na
BISMILLAH RRAHMAAN RRAHIIM. Utatumia kalamu
nyeusi ya wino. Utaiandika katika karatasi tano
tofauti tofauti, kisha chini ya hizo aya nne
utaandika na Aya ya 41 inayopatikana katika Surat
FATWIR (sura ya 35). Kisha utatia nia yako ya
kuhitaji kinga.

Kisha utakwenda kuzifukia katarasi hizo katika


pembe za nyumba yako au uwanja wako kwa
manuizi ya kuweka kinga eneo hilo, na karatasi
nyingine utaifukia katikati ya nyumba au uwanja
wako. Hakika eneo hilo litakuwa na kinga
madhubuti sana mithiri ya chuma dhidi ya majini
na washirikina.

Page | 34
7. KUONDOA NUKSI NA MABALAA KATIKA MWILI.
Utaziandika hizo aya nne za mwanzo za Surat
Hadidy katika karatasi kwa wino wa dhafarani
iliyochanganywa na marashi ya miski. Kisha
utayaosha maandishi hayo kwa maji ya zamzam
au maji ya mvua ya kutegwa. Kisha maji hayo
utayaweka juani kutwa nzima yapigwe na jua.

Kisha mgonjwa mwenye tatizo la Nuksi, Mikosi na


Mabalaa katika mwili wake atatumia maji hayo
kwa kuoga kutwa mara mbili, asubuhi na jioni kwa
siku saba mfululizo.

8. KUPATA USHUJAA VITANI AU KATIKA MASHINDANO


YOYOTE.
Utaiandika Surat Hadidy aya nne za mwanzo
katika karatasi kwa kalamu ya kawaida, kisha
karatasi hiyo utaivaa katika mwili wako sehemu
yoyote ile katika nguo. Hakika hautopata madhara
yoyote katika uwanja wa vita au katika
mashindano yoyoye.

9. KUPATA USHINDI DHID YA MAADUI ZAKO.


Utaziandika hizo aya nne za mwanzo kwa kutumia
wino wa dhafarani na Miski, kisha utayaosha
maandishi hayo kwa maji safi kisha maji hayo
utayalaza nje usiku mzima kisha ifikapo asubuhi
utakwenda kuyaoga maji hayo kwa manuizi ya
kuhitaji kupata ushindi dhidi ya maadui zako, kisha
Page | 35
utakwenda kuonana na maadui hao. (mfano, kesi,
mijadalani n.k).

FAIDA YA SURAT YASIIN


(SURA YA 36)

Surat Yasiin ni sura ya 36 katika kitabu kitukufu cha


Qur’an. Sura hii inafaida nyingi sana kwa mtu
atakayeisoma ikiwa ni pamoja na kuandikiwa
thawabu katika kitabu chake cha A’amal sawa na
amesoma Qur’an nzima mara 10, kwa kuisoma Surat
YASIIN mara 1 tu.

Sura hii ndio moyo wa Qur’an tukufu. Faida nyingi za


Surat Yasiin nimezieleza katika kitabu change
kinachoitwa “MAAJABU YA QUR’AN TUKUFU KATIKA
KUTIBU MARADHI NA KUONDOSHA SHIDA
MBALIMBALI”

Page | 36
Kama bado hujakipata kitabu hicho unaweza
ukawasiliana na mimi kupitia anuani au namba ya
simu iliyopo mwanzoni mwa kitabu hiki.

Hapa nataka tangalie baadhi ya faida za surat


YASIIN katika kumfunga adui yako anayekusumbua,
au kufunga kesi, au kumfunga mke au mume asitoke
nje ya ndoa au kumfunga mtoto yoyote kutokana na
tabia yake mbaya yoyote ambayo wewe huipendi.
Pia tutaangalia jinsi ya kuitumia Surat YASIIN ili
kumfanya mtu awe maarufu aweze kupendwa,
kukubalika, na kujulikana, mahali popote pale
aendapo.

1. JINSI YA KUMFUNGA ADUI YAKO AU KESI


MUME/MKE N.K.
Iwapo kama kuna mtu anakusumbua au
mnafanya nae kesi nawe ukataka kuifunga kesi
hiyo au kumfunga adui huyo. Au kumfunga mke au
mume asitoke nje ya ndoa. Au kumfunga binti
yako au kijana wako asiweze kufanya mambo ya
hovyo hovyo basi utafanya mambo yafuatayo
utaandaa karatasi vipande saba vidogo vidogo
kisha utaviandika majina ya mtu huyo unaetaka
kumfunga utaandika majina yake mawili au
matatu na nia ya jambo lako.

Kisha utaandaa na vipande vidogo vidogo vya mti


wa ndulehe au mtulatula. Halafu tafuta na
vipande saba vya kitambaa cheusi cha kuokota
Page | 37
jalalani au njiani. (usitoe kitamba ndani ya nyumba
yako au kuchana katika nguo yako).

Baada ya kukusanya vitu vyote hivyo, hapo


utaanza kusoma Surat YAASIN kuanzia aya ya
kwanza mpaka aya ya tisa. Aya hizi ndio
zinazoitwa aya za (Qurtub) zikiwa na maana aya
zenye kuficha mambo au kufunga mambo.

Kama umezihifadhi aya hizi kichwani, (unaweza


kusoma bila kuangalia kwenye kitabu), basi
utazisoma aya hizo hali ya kuwa umefumba
macho mpaka utakapofika aya ya tisa, kisha
utachukua kipande cha ule mti wa ndulele au
mtulatula kisha utakikunja vizuri katika karatasi
yako, ile ulioiandika majina ya huyo mtu unayetaka
kumfunga. Kisha uvifunge pamoja katika kile
kitambaa chako cheusi huku ukiwa unatia nia
yako. hali ya kuwa umefumba macho.

Kama haujazihifadhi aya hizo kichwani, (huwezi


kuzisoma bila kuangalia katika kitabu), basi
utazisoma hali ya kuwa unaangalia katika kitabu
mpaka utakapofika aya ya tisa. Ukifika aya hizo
utafumba macho yako kisha utaanza kufunga
kama tulivyoeleza katika maelekezo ya hapo juu
utafanya hivyo kwa kila karatasi mpaka karatasi
zote saba ziishe.

Page | 38
i.e kila utakapotaka kufunga karatasi moja basi
utaanza tena kusoma surat Yasiin kuanzia aya ya
kwanza mpaka aya ya tisa.

Baada ya kumaliza zoezi la kufunga zile karatasi


zote, basi hapo kuna njia mbili za kuhifadhi vile
vitambaa ulivyovifunga.

1) Kama mtu uliyemfunga ni mtu wa ndani mfano,


mke au mume au mtoto au mtu yoyote wa
ndani ya nyumba yako, basi vitambaa vile
utavihifadhi katika kopo jeusi lenye mfuniko. Au
kopo lolote lisiloonesha kilichomo ndani yake.
Kisha kopo hilo utalihifadhi sehemu salama
unayoijua wewe mwenyewe kama utalichimbia
hilo kopo chini kisha ufukie au utalihifadhi katika
begi lako vyote ni sawa.

NB: Kama kopo hilo litafunguliwa na mtu yoyote basi


kifungo hicho kitakuwa kimefunguka. Na muda
wote ambao kopo, lile litakuwa limefungwa basi
kifungo hicho kitakuwa kinafanya kazi.

2) Kama mtu uliyemfunga ni adui yako au


umefunga kesi inayokusumbua, basi vitambaa
hivyo utakwenda kuvifukia katika lalo la zamani
(kaburi) kwa nia ya kumfunga adui huyo au kesi
hiyo.

Page | 39
Hakika jambo lako litakuwa kama utafanya zoezi hilo
kwa usahihi bali kukosea sehemu au hatua yoyote
katika hizo nilizozitaja hapo juu.

2. DUA YA KUMFANYA MTU YOYOTE AWE MAARUFU


AKUBALIKE NA KUPENDWA SEHEMU YOYOTE
ATAKAYOKWENDA, KUPITIA SURAT YASIIN.
Iwapo kama mtu anahitaji kuwa maarufu,
kupendwa na kukubalika katika jamii sehemu
yoyote atakayokwenda basi ataisoma surat Yasiin
kwa utaratibu ufuatao:-

Utasoma Surat Yasiin kuanzia aya ya kwanza


mpaka aya ya 58, ukifika hapo utaacha kusoma
kisha utarudia tena mwanzo, kwa idadi ya mara
tatu.

Mara ya tatu utakapofika aya ya 58, basi aya hiyo


utairudia kwa idadi ya mara 816. Na kama
unamsomea mtu dua hii ili awe maarufu,
kupendwa na kukubalika, basi ataka mbele yako,
pia utaweka na mqji pembeno na kila unapotimiza
kusoma mara moja kuanzia aya ya kwanza mpaka
aya ya 58, hapo utakuwa unatia nia yako, kisha
unapouliza mara moja ndani ya yale maji na
ukimaliza kisomo chako, basi utapuliza ndani ya
yale maji mara saba (7) na maji mazuri kwa ajili ya
dua hii ni maji ya mvua ya kutengwa (utege
chombo chako katikati ya uwanja ili matone ya

Page | 40
mvua yatoke mawinguni yaingie moja kwa moja
katika chombo hicho.

Kisha maji hayo yatumike kwa kuoga kutwa mara


moja kwa siku saba mfululizo. Pindi unaposoma
dua hii utakuwa unachoma ubani kandari ndio
Bukhuri yake.

Dua hii unaweza kuisoma siku yoyote ila uchague


muda mzuri wa kufanya dua. Kama haufahamu
muda mzuri wa kuifanya dua nenda ukasome
kipendele cha saa za kazi katika kufanya dua.

SEHEMU YA PILI
SAA ZA KAZI KATIKA KAZI ZA DUA NA TIBA
MBALIMBALI
Saa za kazi katika kazi za dua na tiba mbalimbali ni
saa maalumu zenye kutawaliwa na watumishi wa
siku maalumu. Iwapo kama unahitaji kufanya dua na
unataka dua hiyo ikujibu haraka sana au unataka
kumfanyia mtu tiba Fulani, mfano, kumuondoshea
uchawi katika mwili wake, au kufunga kesi, au
kumuhamisha mtu kutoka sehemu moja kwenda
nyingine au kufarakarisha watu n.k. basi ni vizuri
ukazingatia kufanya jambo hilo ulilokusudia kwa
kufuata saa maalumu ya kufanya tukio hilo.

Kila saa katika siku lina mtumishi wake ambaye


hushughurika na mambo Fulani katika muda wa

Page | 41
utawala wake katika siku au saa maalumu
analokuwa analitawala katika siku hiyo.

Katika siku nzima yenye masaa 24 kuna wawala


takribani saba wanaotawala katika hayo masaa 24
ya siku nzima. Na kila mtawala wa saa Fulani
anapoingia kazini (kutawala katika saa yake
maalumu) basi muda huo kuna mambo ambayo
yeye hushughulika nayo. Hivyo ni vyema kufahamu
kuwa saa Fulani, mtawala wake ni nani na mtawala
huyo anapoingia kazini katika saa hiyo basi
hushughulika na mambo gani?

Katika kurasa zijazo utajifunga aina za watawala wa


siku na katika saa na siku za kazi zao
wanazoshughulika nazo, hivyo ni vema ukatambua
saa Fulani atatawala mtawala Fulani na nini jambo
au mambo anayoshughulika nayo mtawala huyo. Hii
itakusaidia kufanya kazi zako za dua na tiba kuwa
nyepesi zenye matokeo ya haraka katika jambo
unalolihitaji. Yafuatayo ni majina ya watawala wa
siku saa na saa za kazi wanazoshughulika nazo katika
utawala wao.

(1) SHAMSI - Juma pili


 Shamsi ni mtawala wa siku ya jumapili katika
wiki. Utawala wa Shamsi unapoingia katika siku
huwa ana shughulika na mambo yafuatayo:-
i) Kumfanya mtu atoe kitu furani mfano, kudai
madeni, kushawishi mtu akupende,
akukubali n.k
Page | 42
ii) Kumfanya mtu ashinde katika jambo Fulani,
au ashindwe katika jambo Fulani.

iii)Kumfanya mtu apate utukufu, cheo au


heshima Fulani.

iv) Kumfanya mtu akubalike katika jambo


fulani mfano, kazini katika biashara au
katika jamii.

v) Kumfanya mtu apate utukufu au uongozi


au kushindwa jambo Fulani n.k

Kwa hiyo unapoingia wakati wa SHAMSI (yaani


saa ya Shamsi) katika siku yoyote basi unaweza
kufanya shughuli za mambo hayo tulioyataja
nawe utapata majibu ya haraka. Kwa hiyo kama
unataka kumfanyia mtu dua au kumfanyia mtu
tiba, na tiba hiyo ikahusiana na mambo hayo
tulioyataja hapo juu, basi fanya shughuli hiyo
katika saa ya SHAMSI au siku ya SHAMSI ambayo
ni Juma pili katika siku saba za wiki.

Tuangalie utawala wa siku ya jumapili katika


masaa ishirini na nne na watawala wa masaa
hayo.

Page | 43
 SHAMSI:
- Saa moja asubuhi - Shamsi
- Saa mbili asubuhi - Zuhurat
- Saa tatu asubuhi - Atwarid /Utwaridi
- Saa nne asubuhi - Qamari
- Saa tano asubuhi - Zohari
- Saa sita mchana - Mustara
- Saa saba mchana - Mirihi
- Saa nane mchana - Shamsi
- Saa tisa mchana - Zuhurat
- Saa kumi jioni - atwarid
- Saa kumi na moja jioni - Qamar
- Saa kumbi na mbili jioni - Zohari
- Saa moja jioni - Mustara
- Saa mbili usiku - Mirihi
- Saa tatu usiku - Shamsi
- Saa nne usiku - Zuhurat
- Saa tano usiku - Atwarid /Utwaridi
- Saa sita usiku - Qamari
- Saa saba usiku - Zohari
- Saa nane - Mustara
- Saa tisa usiku - Mirihi
- Saa kumi usiku - Shamsi
- Saa kumi na moja alfajiri - Zuhurat
- Saa kumi na mbili Alfajiri - Atwaridi

Kwa hiyo katika siku ya jumapili mtawala wa siku hiyo


hutawala katika masaa manne. Masaa mawili ya
mchana; ambayo ni saa moja asubuhi na saa nane
mchana. Na masaa mawili ya usiku ambayo ni saa
tatu usiku na saa kumi usiku. Hivyo katika masaa
Page | 44
hayo manne basi unaweza kufanya shughuli au dua
zinazohusiana na uatawala wa SHAMSI.

2) QAMAR – Jumatatu
Qamari ni mtawala wa siku ya Jumatatu katika
wiki. Utawala wa Qamari unapoingia katika siku,
hua anashughulika na mambo yafuatayo;

i) Kumfanya mtu akutii au akunyenyekee, au


kumnyenyekeza kwa mtu Fulani.

ii) Kufanya dawa au dua za mvuto.

iii) Kufunga ndimi za watu wanaokusema vibaya,

iv) Kumfungua mtu vifungo mbalimbali, katika


mwili au kufanya dawa au dua za kumtoa mtu
mahabusu au magereza, na kazi zingine
zinazofanana na hizo tulizozitaja hapa.

Hivyo unapoingia wakati wa saa ya Qamar katika


siku yoyote ya wiki basi unaweza kufanya shughuli
za mambo hayo tuliyoyataja hapo juu au
zinazofanana na mambo hayo. Hakika jambo
lako litakubalika na utapata majibu ya haraka
sana . INSHALLAH.

Kwa hiyo kama unataka kumfanyia mtu dua au


kumfanyia mtu tiba na tiba hiyo ikahusiana na
shughuli hiyo katika saa ya QAMAR au siku ya

Page | 45
Qamari ambayo ni Jumatatu katika zile siku saba
za wiki.

Tuangalie utawala wa siku ya jumatatu katika


masaa 24 na watawala wa msaa hayo.

 QAMAR .
 Saa moja asubuhi - Qamar
 Saa mbili asubuhi - Zohari
 Saa tatu asubuhi - Mushtara
 Saa nne asubuhi - Mirihi
 Saa tano asubuhi - Shamsi
 Saa sita mchana - Zuhurat
 Saa saba mchana - Atwarid/Utwarid
 Saa nane mchana - Qamar
 Saa tisa mchana - Zohar
 Saa kumi jioni - Mustara
 Saa kumi na moja jioni - Mirihi
 Saa kumbi na mbili jioni - Shamsi
 Saa moja jioni - Zuhurat
 Saa mbili usiku - Atwarid
 Saa tatu usiku - Qamar
 Saa nne usiku - Zohari
 Saa tano usiku - Mushtara
 Saa sita usiku - Mirihi
 Saa saba usiku - Shamsi
 Saa nane - Zuhurat
 Saa tisa usiku - Atwarid
 Saa kumi usiku - Qamari
 Saa kumi na moja alfajiri - Zohari
 Saa kumi na mbili Alfajiri - Mushtara
Page | 46
Kwa hiyo katika siku ya Jumatatu Mtawala wa
siku hiyo ambaye ni Qamari hutawala masaa
manne katika masaa ishirini na nne, masaa
mawili ya mchana ambayo ni saa moja asubuhi
na saa nane mchana.

Na masaa mawili ya usiku ambayo ni saa tatu


usiku na saa kumi usiku.

Hivyo katika hayo masaa manne katika hiyo siku


unaweza kufanya shughuli za dua au tiba
zinazoendana na utawala wa QAMAR.

3) MIRIHI – Jumanne
Mirihi ni mtawala wa siku ya jumanne katika wiki
utawala wa mirihi unapoingia katika siku, mirihi
huwa anashughulika na mambo yafuatayo;

i) Kutengeneza uadui baina ya mtu na mtu.


ii) Kumtia mtu chuki ya hali ya juu.
iii)Kumtoa mtu katika mji, kumuhamisha mtu
kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
iv) Kumtia mtu maradhi Fulani.
v) Kumuangusha mtu katika utawala,
kumuangamiza mtu.

Page | 47
vi) Kumvuta mtu alioko mbali na mambo
mengine yanayofanana na hayo tuliyoyataja
hapa.
Hivyo unapoingia wakati wa Mirihi au saa ya mirihi
katika siku yoyote ya wiki, basi unaweza kufanya
shughuli za mambo hayo tuliyotaja hapo juu au
shughuli zinazofanana na mambo hayo hakika
jambo lako litakubalika na utapata majibu ya haraka
sana.

Tuangalie utawala wa siku ya Jumanne katika masaa


24 na watawala wa masaa hayo.

 MIRIHI
o Saa moja asubuhi - Mirihi
o Saa mbili asubuhi - Shamsi
o Saa tatu asubuhi - zuhurat
o Saa nne asubuhi - Atwarid/Utwarid
o Saa tano asubuhi - Qamari
o Saa sita mchana - Zohari
o Saa saba mchana - Mushtara
o Saa nane mchana - Mirihi
o Saa tisa mchana - shamsi
o Saa kumi jioni - Zuhurat
o Saa kumi na moja jioni - Atwarid
o Saa kumbi na mbili jioni - Qamari
o Saa moja jioni - Zohari
o Saa mbili usiku - Mushtara
Page | 48
o Saa tatu usiku - Mirihi
o Saa nne usiku - Shamsi
o Saa tano usiku - Zuhurat
o Saa sita usiku - Atwarid
o Saa saba usiku - Qamari
o Saa nane - Zohari
o Saa tisa usiku - Mushtara
o Saa kumi usiku - Mihiri
o Saa kumi na moja alfajiri - Shamsi
o Saa kumi na mbili Alfajiri - Zuhurati

Katika siku ya Jumanne mtawala wa siku hiyo


hutawala mara nne katika masaa ishirini na nne
msaaa mawili ya mchana ambayo ni saa moja
asubuhi na saa nane mchana.

Na masaa mawili ya usiku ambayo ni saa tatu usiku


na saa kumi usiku.

Hivyo katika mAsaa hayo manne, unaweza kufanya


shughuli au dua zinazoendana na utawala wa
MIRIHI.

4) ATWARIDI – Siku ya Jumatano


Atwarid ni mtawala anayetawala siku ya
Jumatano katika wiki. Utawala wa Atwarid
unapoingia katika siku, atwarid huwa
anashughulika na mambo yafuatayo;
i) Kutoa kitu kilichozikwa chini, mfano, uchawi,
madini n.k.

Page | 49
ii) Kuulainisha moyo wa mtu kwako.Kumfanya
mtu akupende kwa lazima au ampende mtu
mwingine

iii)Kumtoa mtu maradhi.

iv) Kufunga ndimi za watu wanaokusema vibaya


na mambo mengine yanayofanana na hayo.

Hivyo katika siku ya jumatano unapoingia wakato


au utawala wa Atwarid, basi unaweza kufanya
mambo hayo tuliyoyafanya hapo juu na mfano
wa mambo yanayofanana na hayo

Tuangalie utawala wa Atwarid katika siku ya


jumatano, katika masaa 24 na watawala wake
ndani ya masaa hayo

 Saa moja asubuhi - atwarid


 Saa mbili asubuhi - Qamari
 Saa tatu asubuhi - Zohari
 Saa nne asubuhi - Mushtara
 Saa tano asubuhi - Mirihi
 Saa sita mchana - Shamsi
 Saa saba mchana - Zuhurat
 Saa nane mchana - Atwarid
 Saa tisa mchana - Qamari
 Saa kumi jioni - Zohari
 Saa kumi na moja jioni - Mustara
 Saa kumbi na mbili jioni - Mirihi
 Saa moja jioni - Shamsi
Page | 50
 Saa mbili usiku - Zuhurat
 Saa tatu usiku - Atwarid
 Saa nne usiku - Qamar
 Saa tano usiku - Zohari
 Saa sita usiku - Mushtara
 Saa saba usiku - Mirihi
 Saa nane - Shamsi
 Saa tisa usiku - Zuhurat
 Saa kumi usiku - Atwarid
 Saa kumi na moja alfajiri - Qamari
 Saa kumi na mbili Alfajiri - Zohari

5) MUSHTARA – Siku ya Alkhamisi:

MUSHTARA ni, mtawala anaetawala siku ya


Alkhamisi akisaidiwa na watawala wengine wa
siku zingine. Utawala wa Mushtrata unapoingia
katika siku, Mushtara huwa anashughulika na
mambo yafuatayo;

i) Kupatanisha watu waliogombana.

ii) Kupamba mtu awe na mvuto wa mwili, au


kufanya dawa za mvuto wa mwili n.k

iii) Kumfungua mtu vifungo vya kichaw na kijini


katika mwili wake.

iv) Kung’arisha nyota ya mtu au kuoga dawa za


mvuto wa mwili na mambo mengine
yanayofanana na hayo tuliyoyataja hapo juu.
Page | 51
Hivyo unapoingia wakati wa MUSHTARA katika
siku yoyote, basi unaweza kufanya shuguli za
mambo hayo tuliyoyataja hapo juu au shughuli
zinazofanana na mambo hayo katika tiba au
dua.

Tuangalie utawala wa siku ya alkhamis


ambayo mtawala wake ni MUSHTARA katika
msaa 24 na watawala wa masaa hayo.

 MUSHTARA
o Saa moja asubuhi - Mushtara
o Saa mbili asubuhi - Mirihi
o Saa tatu asubuhi - Shamsi
o Saa nne asubuhi - zuhurat
o Saa tano asubuhi - atwarid
o Saa sita mchana - Qamar
o Saa saba mchana - Zohari
o Saa nane mchana - Mushtara
o Saa tisa mchana - Mihiri
o Saa kumi jioni - shamsi
o Saa kumi na moja jioni - Zuhurat
o Saa kumbi na mbili jioni - Atwarid
o Saa moja jioni - Qamar
o Saa mbili usiku - Zohari
o Saa tatu usiku - Mushtara
o Saa nne usiku - Mirihi
o Saa tano usiku - Shamsi
o Saa sita usiku - Zuhurat
o Saa saba usiku - Atwarid
Page | 52
o Saa nane - Qamar
o Saa tisa usiku - Zohar
o Saa kumi usiku - Mushtara
o Saa kumi na moja alfajiri - Mirihi
o Saa kumi na mbili Alfajiri - Shamsi

Hivyo katika siku ya Alkhamis, Mushtara


anapoingia kutawala katika yale masaa yake
manne basi ni vyema mtu akafanya shughuli
zinazoendana na utawala wa MUSHTARA, ili
aweze kupata amatokeo ya haraka katika
jambo lake INSHAALLAH

6) ZUHURAT – Ijumaa.
Zuhurat ni mtawala wa siku ya Ijumaa katika wiki
akisaidiwa na watawala wengine sita ila yeye
ndiye mtawala mkuu katika siku ya Ijumaa.

Zuhurat anapoingia katika utawala wake basi


hushughulika na mambo yafuatayo katika
shughuli za dua na tiba mbalimbali;
i) Kumdhalilisha mtu, au kumuangusha mtu
katika cheo au madaraka yake.

ii) Kumvuta mtu katika mapenzi au kumvuta


mtu aliyoko mbali.

iii)Kuwaunganisha watu waliofarakana au


kutengana.

Page | 53
iv) Kufanya shughuli za kuoa au kuanzisha
mapenzi au mahusiano na Fulani.

v) Kuunga udugu baina ya mtu na mtu na


shughuli zingine zinazofanana na hizo
tulizotaja hapo juu.

Kwa hiyo unapoingia utawala wa ZUHURAT


katika siku ya Ijumaa au siku yoyote basi ni vema
kufanya shughuli zinazoendana na utawala wa
Zuhurati ili uweze kupata majibu ya haraka katika
shughuli hizo.

Tuangalie utawala wa Zuhurat katika siku ya


Ijumaa ndani ya masaa 24 na wasaidizi wake,
katika siku hiyo.

 ZUHURAT
o Saa moja asubuhi - Zuhurat
o Saa mbili asubuhi - Atwarid
o Saa tatu asubuhi - Qamar
o Saa nne asubuhi - Zohari
o Saa tano asubuhi - Mushtara
o Saa sita mchana - Mirihi
o Saa saba mchana - Shamsi
o Saa nane mchana - Zuhurat
o Saa tisa mchana - Atwarid
o Saa kumi jioni - Qamar
o Saa kumi na moja jioni - Zohari
o Saa kumbi na mbili jioni - Mushtara
o Saa moja jioni - Mirihi
Page | 54
o Saa mbili usiku - Shamsi
o Saa tatu usiku - Zuhurat
o Saa nne usiku - Atwarid
o Saa tano usiku - Qamar
o Saa sita usiku - Zohar
o Saa saba usiku - Mushtara
o Saa nane - Mirihi
o Saa tisa usiku - Shamsi
o Saa kumi usiku - Zuhurat
o Saa kumi na moja alfajiri - Atwarid
o Saa kumi na mbili Alfajiri - Qamar

Hivyo katika siku ya Ijumaa ZUHURAT anatawala


katika masaa manne ndani ya masaa 24 masaa
mawili ya mchana ambayo ni saa moja asubuhi
na saa nane mchana.

Masaa mawili ya usiku ambayo ni saa tatu usiku


na saa kumi usiku.

7) ZOHARI – Jumamosi
Zohari ni Mtawala wa siku ya Jumamosi katika
wiki akisaidiwa na watawala wa siku zingine,
lakini yeye ndiye mtawala mkuu wa siku ya
jumamosi.

Utawala wa Zohari unapoingia katika siku ya


Jumamosi au katika masiku mengine, basi yeye
hushughulia a mambo yafuatayo;
i) Kufarakanisha watu.

Page | 55
ii) Kumfuka mtu au kumuhamisha mtu eneo lako

iii)Kuondosha vitu vibaya au uchawi katika mwili


au nyumba.

iv) Kumfanya mtu achukiwe au kumtia mtu Nuksi.

v) Kufunga matamanio ya mtu au kumfunga mtu


usingizi na vitu vingine vinavyofanana na
hivyo.

Hivyo unapoingia wakati wa ZOHARI katika siku


yoyote basi ni vema kufanya shughuli za
mambo kama hayo tulioyataja hapo juu.
Ukizingatia utaratibu huo basi mambo yako
yatakuwa na majibu.

Tuangalie utawala wa zohari katika siku ya


Jumamosi na wasaidizi wake katika masaa 24.

 Saa moja asubuhi - Zohari


 Saa mbili asubuhi - Mushtara
 Saa tatu asubuhi - Mirihi
 Saa nne asubuhi - Shamsi
 Saa tano asubuhi - Zuhurat
 Saa sita mchana - Atwarid
 Saa saba mchana - Qamar
 Saa nane mchana - Zohari
 Saa tisa mchana - Mushtara
 Saa kumi jioni - Mirihi
 Saa kumi na moja jioni - Shamsi
Page | 56
 Saa kumbi na mbili jioni - Zuhurat
 Saa moja jioni - Atwarid
 Saa mbili usiku - Qamari
 Saa tatu usiku - Zohari
 Saa nne usiku - Mushtara
 Saa tano usiku - Mirihi
 Saa sita usiku - Shamsi
 Saa saba usiku - Zuhurat
 Saa nane - Atwarid
 Saa tisa usiku - Qamar
 Saa kumi usiku - Zohar
 Saa kumi na moja alfajiri - Mushtara
 Saa kumi na mbili Alfajiri - Mirihi

Kwa hiyo katika siku ya Jumamosi ZOHARI


anatawala katika msaa manne. Masaa mawili
ya mchana, ambayo ni saa moja asubuhi na
saa nane mchana.

Na masaa mawili ya usiku ni saa tatu usiku na


saa kumi usiku. Hivyo zohari anapoingia katika
utawala wa siku ya Ijumaa ni vyema mtu
akafanya shughuli au kazi za dua
zinazoendana na utawala wa Zohari katika siku
hiyo ili aweze kupata matokeo kwa haraka
zaidi

NB: Unapotaka kufanya shughuli yoyote ya dua,


ili kupata matokeo ya haraka dhidi ya
dua hiyo ni vyema ukazingatia utaratibu
huu wa kutumia masaa ya kazi. Au pindi
Page | 57
unapotaka kufanya kazi za tiba kupitia
mitishamba napo ni vyema, ukazingita
utaratibu huu ili uweze kupata majibu na
matokeo ya haraka katika jambo hilo

SEHEMU YA TATU
UTUKUFU WA MAJINA YA BARHATIHI

BARHATIHI NI NINI?

Barhatihi ni majina matukufu sana ya Mwenyezi


Mungu na yenye uwezo wa kipekee tena yenye
uwezo wa kutoa majibu ya haraka.

Haya ni majini ya Mwenyezi Mungu yaliyotajwa kwa


lugha ya KI – ISRANIYYA (Kiebrania). Lugha tukufu
miongoni mwa lugha ya watu wa Nabii Musa (a.s).
Majina ya BARHATIHI yamebeba siri nzito mno na
utukufu mkubwa sana.

Majina haya yapo majina 28, ingawa kuna riwaya


inasema majina yapo 30, kama imamu Ghazali
amekubali kuwepo kwa majina hayo mengine. Cha
kuzingatia, wana chuoni wengi wamekubali majina
ya Barhatih yapo ishirini na nane (28).

Majina haya kila jina moja lina faida nyingi vile vile
kila jina lina MAKHUDAMU (watumishi) wengi sana
zaidi ya elfu hamsini (50,000) unaweza ukalitumia jina
Page | 58
lolote katika majini hayo ishirini na nane na ukapata
MAKHUDAMU wa kukufanyia jambo lako lolote
unalolitaka.

Majina ya Barhatihi unaweza kuyatumia kwa


kuomba jambo lako lolote unalolitaka cha kuzingatia
ni muda na Bukhuri zako. Kama kazi yako ni nzuri basi
utatumia BUKHURI nzuri, na kama kazi yako sio nzuri
tumia BUKHURI mbaya mbaya .

Majina haya unaweza kutibu mgonjwa, kukinga


nyumba, shamba, kuomba kitu, kuita mtu, kufungua
vifungo, kuondoa Nuksi, kubatilisha uchawi, Kuita
MAKHUDAMU (watumishi), kuadhibu maadui na
unaweza tengeneza jambo au kuharibu jambo.

Majina haya unaweza kuyatumia katika dua yako


yoyote au katika kazi yako yoyote ya dua.
Unaposoma dua yako yoyote mwisho ukisoma haya
majina ya BARHATIHI inasaidia kuipandisha dua yako
kwa haraka sana.

Majina ya BARHATIHI yana faida nyingi sana kwa


maisha yako yote katika elimu ya uganga na
mambo mengine, pendelea kuyasoma usiku mara
nyingi, utapata urafiki na majini wema. Na watu
watakuogopa sana na utashangaa kila unachokiota
katika ndoto inakuwa ni kweli.

Page | 59
MAJINA YENYEWE NI HAYA

MAJINA 28 YA BARHATIHI

Page | 60
Majina ya Barhatih ndio mama wa uganga kwa
sababu, kila jambo unaweza lifanya na likatimia na
vile vile sehemu yoyote Barhatihi inakubali Mujarrabu
sana.

FAIDA ZA PAMOJA ZA KUSOMA MAJINA YA


BARHATIHI.
Hizi ni baadhi tu ya faida unazoweza kuzipata kwa
kusoma majina hayo ya BARHATIHI.

1. KUMUANGAMIZA JINI AU SHETANI ALIYEKATIKA


MWILI WA BINADAMU AU NYUMBA.

2. UKITAKA KUMUONA MCHAWI (Kumjua ni nani


mchawi na nani sio mchawi).

3. UNAWEZA KUBAINI KITU AMBACHO UNA MASHAKA


NACHO.

4. UNAWEZA KUMUHAMISHA ADUI YAKO AENDE MBALI

5. KUMTIA ADABU ADUI YAKO KWA NAMNA YOYOTE


UITAKAYO.

6. INAUA UCHAWI WA AINA YOYOTE KWENYE MWILI


AU KWENYE NYUMBA.

7. INAFUKUZA MASHETANI AU MAJINI KATIKA NYUMBA.

Page | 61
8. INABATILISHA UCHAWI.

9. IUNAFUNGUA RIZIQI ZILIZOFUNGWA

10. INAUWEZO WA KUMKATA MWIZI.

11. NI KINGA YA MWILI WAKO, SHAMBA LAKO AU MALI


YAKO.

12. KUOMBA UPATE KAZI.

13. KUVUTA MAHABA KATIKA NDOA

14. KUMUACHISHA MTU UZINIFU AU TABIA YAKE MBAYA


YOYOTE

15. KUPATA MAKHUDAMU (WASAIDIZI) WA KUFANYA


NAO KAZI (MALAIKA/MAJINI)

16. KUPATA UTAJIRI WA HALALI.

17. KUSAFISHA MWILI AU NYOTA ILIYOCHAFULIWA.

18. KUFUNGUA UFAHAMU KWA MTOTO.

19. KUPATA NGUVU YA KINGA KWA MATABIBU.

20. KUMRUDISHA MKE/MUME/MPENZI ALIOKIMBIA.

Page | 62
UTARATIBU WA KUYASOMA MAJINA YA BARAHATIHI.
Kabla ya kuanza kuyasoma majina ya barhatihi
kwanza utachukua udhuu ule wa swala kamili kisha
utaelekea qibra na kuswali Rakaa mbili za Sunatul
Hajja. Hali ya kuwa mwili, nguo na mahali pa
kuswalia pawe pasafi na twahara.

Swali rakaa mbili za Sunatul Hajjah, na katika rakaa


ya kwanza utasoma suratul FAATIHA NA KISHA
UTASOMA IKHLASWI MARA 10.

(FAATIHA + IKHLASWI x 10)

Raakaa ya pili utasoma Suratul FAATIHA na kisha


utasoma SURATUL QADRI MARA 10.
(FAATIHA + IKHLASWI x 10).

Kisha utapokuwa katika Sijda ya mwisho katika rakaa


ya pili utasoma neno (YAA WADUWDU MARA 7)

Kisha ndipo utataja haja yako hapo. Kisha utatoa


salamu kulia na kushoto

 Baada ya hapo utamswalia mtume (s.a.w) kwa


idadi ya mara 100.
 Kisha utafanya Istighafar (kuomba msamaha)
mara 100.
 Utasema YAA LATWIFU mara 129.
Page | 63
Kisha ndipo utaanza kusoma hayo majina ya
Barhatihi. Majina ya BARHATIHI utaratibu wake wa
kuyasoma ni kila jina moja unalisoma mara mbili

Mfano; BARHATIHI = MARHATIHI x 2

Yaani utasoma BARHATIHI , BARHATIHI.

Hapo ndio itahesabika idadi ya moja, kisha ndipo


unakwenda jina lingine, mpaka unayamaliza majina
yote 28.

Kwa hiyo unapoambiwa soma jina hili au majina


haya mara kadhaa, basi kila jina moja utalisoma kwa
idadi ya mara mbili mbili kama tulivyoelekeza hapo
juu.

Na ukiambiwa liandike jina hili au majina haya mara


kadhaa, basi kila jina moja huandikwa mara moja
moja tu.

Majina haya unaweza kuyasoma kwa idadi ya mara


7, 11 au 21, au mara 45. Pia jina moja linaweza
kusomwa kwa idadi nyingi kulingana na mizani yake
mpaka kufikia mara 1000 au zaidi. Ila mizani ya
majina yote ya Barhatihi ni mara 45 au 47 Riwaya
nyingi ndio zimependekeza idadi hiyo na sio zaidi ya
hiyo.

Page | 64
MATUMIZI MBALIMBALI YA MAJINA YA BARHATIHI

1. KUMUANGAMIZI JINI AU SHETANI ALIYE KATIKA


MWILI WA BINADAMU/KATIKA NYUMBA.
Kama unahitaji kumuangamiza jinni au shetani
aliye katika kiwili wili au katika nyumba yako basi
fanya yafuatayo:

Utaandika majina yote ya BARHATIHI katika


lugha yake (kiarabu) kwa kutumia wino wa
dhafarani katika karatasi nyeupe.Utayaandika
majina yote kwa idadi ya mara tatu (mwanzo
mpaka mwisho katika karatasi tatu tofauti. Kisha
zile karatasi ulizoziandika majina hayo utaziweka
katika chombo halafu tia ndani yake na maji safi.
Kisha somea maji hayo majina yota ya BARHATIHI
kwa idadi ya mara saba.

Baada ya hapo mpe mgonjwa anayesumbuliwa


na majini au mashetani katika mwili wake anywe
maji hayo kikombe kimoja kutwa mara tatu. Kwa
muda wa siku saba na maji mengine atatumia
kwa kuoga kwa mfumo wa kujipakaa mwili
mzima. Asubuhi na jioni.

Au utatumia maji hayo kumwagia mwagia ndani


ya nyumba yako au kupigia deki ndani maji
hayo. Hakika kama jinni au shetani
atang’ang’ania kuka katika mwili wa huyo
mgonjwa au katika nyumba hiyo iliyotumiwa maji
hayo, hakika atapoteza maisha kabisa.
Page | 65
2. KUPATA URAFIKI NA MAKHUDAMU (WATUMISHI)
Kwa mwenye kutaka kuwa na urafiki na
Makhudamu (watumishi wanaoyatumikia majina
hayo) ili wakusaidie katika kazi zako mbalimbali za
dua na tiba basi utatumia kusoma majina hayo
yote kila siku kwa idadi ya mara moja. Utasoma
kila siku asubuhi majina hayo yote mara moja
huku ukiwa umewasha (Sandari udi). Kisha baada
ya kuyamaliza kuyasoma majina hayo, omba
“Enyi watumishi wa majina haya ya Barhatihi
kuanzia sasa naomba mnifanyie kadhaa wa
kadhaa (utataja haja yako hapo).

Ukitumia vizuri majina hayo utaona maajabu yake


ni Mujarabu sana. Ukimsomea mtu Ruqya (mtu
mwenye mashetani) basi atapiga kelele sana kwa
uchungu na maumivu makali kutokana na wewe
kuwa na hao MAKHUDAMU na wanaweza
kukufanyia chochote ukitakacho.

Pia unaweza kumuamrisha pepo alipanda katika


kichwa cha mgonjwa jambo lolote naye akakutii
bila usumbufu wowote, kama utaakuwa ni
mwenye kutekeleza A’amali hii kila siku asubuhi.
INSHAALLAH.

3. KUMZINDUA ALIYEZIMIA.
Ikiwa kama kuna mgonjwa amezimia kwa jinni au
kifafa au kurogwa na kila akiamshwa hajibu kitu
chochote, basi unaweza kutumia njia hii na
Page | 66
akazinduka haraka sana, bila mlolongo mrefu na
ukitekeleza amal hii ni tiba tosha ya mgonjwa
wako.

Utachukua maji safi, ndani yake weka halititi


kidogo na chumvi ya mawe. Kisha yasomee Surat
YASIIN mara tatu na kama huwezi kusoma Surat
YASIIN soma BISMILLAH RRAHMAN RRAHIIM mara
40, kisha somea maji hayo majina ya BARHATIHI
mara 21 (soma majina yote kwa kurudia rudia).
Baada ya hapo puliza umo katika maji hayo mara
tatu.

Kisha maji hayo utamwagia kifuani mgonjwa


huyo, na atazinduka hapo hapo. Kama alishikwa
na jinni basi jinni huyo atapanda kichwani, kwani
dawa hiyo inachoma sana mashetani na majini
wabaya walioko katika mwili.

4. KUONDOA NUKSI MWILINI.


Barhatihi ni miongoni mwa dawa nzuri sana za
kuondoa NUKSI na MIKOSI katika mwili. Ili kuondoa
NUKSI na MIKOSI katika mwili, basi utayaandika
majina ya BARHATIHI yote mara tatu katika
karatasi kwa kutumia wino wa dhafarani. Kisha
utazitia zile karatasi katika chombo kisafi, halafu
ndani yake utatia maji ya bahari, maji ya marasi,
chumvi ya mawe na unga wa Habati Nuksi.
Baada ya kuvichanganya vitu vyote hivyo
pamoja. Utasomea majina ya Barhatihi yote kwa
idadi ya mara 21.
Page | 67
Baada ya kisomo hicho mgonjwa mwenye nuksi
atatumia kuoga maji hayo kutwa mara mbili kwa
mtindo wa kujipakaza katika mwili, ataoga kwa
muda wa siku saba mfululizo.

Hakika utaondokana na kila aina ya uchafu na


NUKSI katika mwili wako. Dawa hii ni Mujarabu
sana.

5. KUWAFUNGA MAPEPO WACHAFU WASIRUDI TENA


KATIKA MWILI WA MGONJWA.
Iwapo kama umemfanyia mgonjwa kisomo cha
Ruqya na jinni akakubali kutoka , fahamu
kwamba jinni huyo ataondoka kwa sababu ya
kuzidiwa na visomo au madawa yako tu. Ila jinni
ataendelea kumfata fata mgonjwa huyo mpaka
siku 40.

Na kuanzia siku ya saba asipopata mafaanikio


ya kumkalia tena ndipo anapoanza kukata
tamaa ya kurudi tena katika mwili wake.

Ili kumfunga jinni huyo asirudi tena katika mwili


wa mgonjwa utafanya yafuatayo;
Utachukua karatasi nyeupe kisha utaandika
Majina yote 28 ya BARHATIHI, kisha utatia karatasi
hiyo katika maji (utaandika kwa kutumia wino wa
dhafarani). Kisha baada ya kutia karatasi hiyo
katika maji. Utayasomea majina yote ya Barhatihi
Page | 68
kwa idadi ya mara saba katika maji hayo. Kisha
mgonjwa atatumia kunywa maji hayo kutwa
mara mbili, na atakunywa kwa muda wa siku
saba mfululizo. Ndani ya maji utaweka na Halititi
kidogo. Hakika jinni huyo hatarudi tena katika
mwili wa huyo mgonjwa, dawa hii ni mujarabu
sana.

6. KUFUNGUA MAMBO YALIYOFUNGWA KICHAWI.


Iwapo kama mambo yako yamefungwa
kichawi, kila ulifanyalo linakuwa halifanikiwi na
hata kama linafanikiwa basi inakuwa ni kwa
shida sana ili kujifungua katika vifungo hivyo
utatumia njia hii.

Njia hii pia ni nzuri hata kwa wale waliofungwa


vifungo vya kijini na mikosi ya mizimu na
mashetani. Chakufanya utaandika Surat
BAYYINAH yote (sura ya 98 katika kitabu cha
Qur’an tukufu)

Kisha chini yake andika na majina yote 28 ya


BARHATIH utaandika kwa kutumia wino wa
dhafarani utayaandika mara moja tu. Kisha
utailoweka karatsi hiyo katika maji. Halafu maji
hayo utayasomea majina yote ya BARHATIH kwa
idadi ya mara kumi na moja (11)

Mgonjwa atatumia maji hayo kwa kuoga, kwa


mfumo wa kujipaka mwili mzima. Kutwa mara 2
kwa muda wa siku saba mfululizo. Dawa hii ni
Page | 69
mujarrabu sana itakusaidia kufungua mwili wako
kusafisha mwili kutokana na mikosi mbalimbali.

7. KUVUNJA KILA AINA YA UCHAWI MWILINI.


Kama katika mwili wako una maradhi
yatokanayo na uchawi. Nawe umehangaika
hospitali mbali mbali bila kupona, pengine
wanasema “hatuoni ugonjwa”. Basi tumia njia hii
itakusaidia sana.

Utayaandika majina yote ya Barjatihi mara tatu


katika karatasi kwa wino wa dhafarani. Kisha
utailoweka ile karatasi yako katika maji, halafu
ndani ya maji hayo utaweka na halititi kidogo na
unga wa kitunguu swaumu. Kisha utayasomea
maji hayo majina ya BARHATIH kwa idadi ya
mara 21.

Kisha mgonjwa atakuwa anakunywa grasi moja


kutwa mara tatu kwa muda wa siku saba. Na
maji mengine atatumia kupakaa mwili mzima
asubuhi na jioni. Inshaallah ataondokana na
changamoto hiyo.

8. KUSAFISHA NYOTA.
Nyota ndio mfumo mzima wa maisha, nyota
inapochafuliwa, basi utaona mambo yako
yanakuendea hovyo. Kila unalolipanga
halifanikiwi au linaishia njiani n.k.

Page | 70
Ukitaka kusafisha nyota yako fanya yafuatayo
utayaandika majina yote ya BARHATIHI katika
karatasi kwa kutumia wino wa dhafarani kisha
utatia karatasi hizo katika maji. Kisha ndani ya
maji hayo utaweka na;
i) Maji ya waridi (water rose)
ii) Habati Nuksi
iii)Dawa inayoitwa Kasera bala
iv) Sukari ya mawe

Kisha utasomea Surat BAYYINAH mara 21 katika


maji hayp na majina ya Barhatihi utayasomea
mara 21 ndani ya hayo maji, kisha utasomea na
Surat QADRI, mara 100. Kisha maji hayo
yatatumika kwa kuoga asubuhi na jioni kwa
muda wa siku saba. INSHALLAH mambo yako
yatafunguka na yataanza kwenda vizuri.

9. KINGA YA MWILI WAKO USIROGEKE.


Kuna njia nyingi sana za kuweka kinga ya mwili
miongoni mwa njia hizo ni kutumia majina ya
Barhatihi. Iwapo kama unataka kuweka kinga ya
mwili wako kwa kutumia majina ya BARHATIHI
utafanya hivi,

Tafuta ubani mashtaka na ubani maka, kisha


weka nia yako kuhusu kisomo hicho ni kwa ajili ya
kinga ya mwili wako, kisha utasoma Surat YASIIN
yote mara 11, na majina ya BARHATIHI yote mara
45, na kila unapofika idadi ya 11, pindi unasoma
majina ya BARHATIHI utakuwa unatia nia yako.
Page | 71
Na pindi unaposoma utakuwa unachoma huo
ubani wako. Njia hii ni mujarrabu sana, hata kama
utahitaji atakae kuroga basi afe mwenyewe
INSHALLAH itakuwa kwa uwezo wa Mwenyezi
Mungu.

Dua hii unaweza kuifanya mara moja tu kwa wiki


na unaweza kuifanya kama uradi wako. Dua hii ni
vizuri ukaifanya usiku wa Ijumaa kuamkia
jumamosi.

KOMBE LA MAJINA YA BARHATIHI


FAIDA MBALIMBALI ZA KOMBE LA MAJINA YA
BARHATIHI.
Kombe ni nini?
Kombe ni mfumo wa kumfanyia mgonjwa dua
kwa kutumia maandishi. Maandisha hayo
yanaweza kuwa ni Aya za Qur’an au majina
matukufu ya Mwenyezi Mungu au majina
matukufu ya Barhatihi. Huandikwa maandishi
hayo ambayo ni aya za Qur’an au majina ya
Mwenyezi Mungu kwa kutumia wino wa dhafarani
kisha maandishi hayo huoshwa kwa maji safi, kisha
mgonjwa hutumia maji hayo kwa kunywa au
kuoga. Njia hii ni nzuri sana na wagonjwa wengi
hupona.

Katika utaratibu wa kusoma majina ya Barhatihi


na uandishi wa majina hayo ni tofauti,
Page | 72
 Ukiambiwa soma majina ya Barhatihi mara 11
au 21 au zaidi, basi fahamu hapo kila jina
moja utalitamka mara mbili.

 Ukiambiwa andika majina yote mara moja


basi utaandika kila jina mara moja moja tu,
hapo teari imeshakidhi

1. KUONDOA NUKSI SUGU.


Mwenye kusumbuliwa na NUKSI SUGU za
kurogwa atumie tiba hii ni Mujarrabu sana,
Utaandika majina yote katika karatasi mara 3
kisha karatasi hizo utaziweka ndani ya maji, ili
kuyaosha yale maandishi yayayuke, kisha ndani
yake utatia kidogo na unga wa Habati Nuksi na
maji ya marashi (water rose) chupa moja.

Kisha maji hayo utayasomea majina ya


BARHATIHI yote mara tatu. Kisha mgonjwa
atatumia maji hayo kwa kuoga kutwa mara mbili
kwa muda wa siku saba mfululizo.

2. KUFUNGUA VIFUNGO VYA KICHAWI KATIKA


MWILI.
Mtu yoyote mwenye kuwa na vifungo katika
mwili wake huwa ni jambo gumu sana
kufanikiwa katika mambo yake, na hata ikitokea
amefanikiwa huwa amepitia tabu na misukosuko
mingi sana katika utafutaji wake. Vifungo

Page | 73
huwekwa na wachawi na majini ili kukukwamisha
katika mambo yako mbali mbali.

Ukitaka kujifungua vifungo vyote katika mwili


wako tumia njia hii ni mujarrabu sana. Utachukua
nazi nne kisha utazitoboa tundu halafu ndani
yake utaweka vitu vilivyotoka katika mwili wako
(nywele zako kidogo, mate yako, mchanga wa
kivuli chako, mchanga wa nyayo zako, kucha
zako na nyuzi ya nguo ya ndani) kisha baada ya
kuweka vitu hivyo ndani ya nazi utaziba tundu
hilo kwa mshumaa au nta.

Kisha kila nazi utaziandika jina la kwanza la


Barhatih mpaka jina la nne. Kisha kila nazi moja
utaisomea majina yote ya Barhatih mara saba.
Kisha utampa mgonjwa huyo hizo nazi baada ya
kuzifanyia kisomo aziweke ndani ya maji ya
kuoga kwa nia ya “Najiongezea vifungo katika
mwili wangu mpaka pale nitakapojifungua
vifungo hivyo kwa kuzivunja nazi hizi” kisha
ataoga maji hayo.

Baada ya mgonjwa kuoga maji hayo, mgonjwa


ataenda kuvunja hizo nazi maeneo yafutayo;

Nazi moja atakwenda kuvunja njia panda kwa


nia ya kujifungua vifungo, nazi ya pili atakwenda
kuvunjia jalalani, na nazi nyingine atakwenda
kuivunja katika mti mkubwa, na nazi nyingine
ataivunja katika mlango wake wa nyumba kwa
Page | 74
nia ya kujifungua vifungo vilivyo katika mwili
wake. Atakuwa anasema kwati wa kuvunja hizo
nazi;

“Najifungua kila aina ya vifungo katika mwili


wangu, nafungua nyota zangu, riziki zangu,
kipato chagu, baati zangu, mvuto wangu nipate
ndoa nipate kazi, n.k kwa nguvu za Mwenyezi
Mungu.”

3. KUTIBU MATATIZO YA NGUVU ZA KIUME.


Mwenye shida ya matatizo ya nguvu za kiume
atatumia tiba hii ni mujarrabu sana. Hurudisha
haraka nguvu za kiume.

Utachukua karatasi kisha utayaandika majina


yote ya barhatihi mara tatu (3) kisha utayaosha
yale maandishi katika maji yenye ujazo wa lita
mbili. Kisha utaweka asali kiasi cha nusu lita ndani
yake, kisha utatia na sukari ya mawe kiasi cha
kiganja cha mkono, kisha utaweka ndani yake
unga wa kungu manga kiasi cha vijiko vitano vya
chakula, na unga wa karafuu maiti kidonge
kimoja.

Kisha mchanganyiko huo utausomea majina


yote ya Barhatih kwa idadi ya mara 21.

Baada ya kisomo hicho mgonjwa atatumia kula


vijiko viwili kutwa mara tatu. Hakika

Page | 75
ataondokana na changamoto hiyo ya kutokuwa
na nguvu za kiume haraka sana.

4. KUTIBU MARADHI YA TUMBO.


Mtu anayesumbuliwa na maradhi ya tumbo ya
aina yoyote, mfano, mchafuko wa tumbo,
uvimbe tumboni, vidonda vya tumbo n.k
maradhi yote ya tumbo tiba hii inafaa sana.

Utayaandika maji yote ya Barhatih mara tatu


katika karatasi, kwa kutumia wino wa dhafarani,
kisha maandishi hayo utayaosha kwa maji safi.
Kisha maji hayo utaweka ndani yake na dawa
inayoitwa mvuje kidogo.

Kisha mgonjwa atatumia kunywa nusu kikombe


cha dawa hiyo kutwa mara tatu kwa muda wa
siku saba. Dawa hii ni mujarrabu sana.

5. KUTIBU MARADHI YA MACHO.


Ugonjwa wa macho ni miongoni mwa maradhi
yanayosumbua na kutesa watu wengi sana.

Kwa mwenye kusumbuliwa na maradhi hayo


atumie njia hii ni Mujarrabu sana kwa maradhi
yote ya macho.

Utaandika majina yote ya Barhatihi mara tatu (3)


kwa kutumia wino wa dhafarani, katika karatasi

Page | 76
au chombo kilichokisafi. Kisha utayaosha
maandishi hayo kwa maji yaliyosafi.

Kisha utatia ndani yake na asali kidogo, kisha


utaweka na maji yaliyokamuliwa katika majani
ya kivumbasi kidogo. Kisha utakuwa unaoshea
macho yako asubuhi na jioni macho hayo.
Fanya hivyo mpaka utakapokuwa vizuri. Tiba hii
ni nzuri sana kwa maradhi ya macho.

6. KUWATESA MAJINI WALIO KATIKA KIWILIWILI.


Kama mtu anasumbuliwa sana na majini katika
mwili wake, basi atatumia njia hii ina uwezo wa
kumuua jinni mkolofi atakaeng’ang’ania
kuendelea kukaa katika mwili wa mgonjwa.

Utachukua karatasi nyeupe kisha utayaandika


majina yote ya BARHATIH kwa idadi ya mara
saba. Kisha utayaosha maandishi hayo kwa maji
yaliyosafi. Kisha ndani yake utaweka na maji ya
BAHARI yaliyochotwa kwa nia ya jambo hilo, pia
utakamulia na maji ya ndimu ndani yake, halafu
utaweka na Halititi kidogo.

Kisha maji hayo utayasomea majina yote ya


Barhatih kwa idadi ya mara 45. Kisha mgonjwa
atatumia maji hayo kunywa nusu kikombe kutwa
mara tatu, kwa muda wa siku saba zenye
kufuatana. Na maji mengine atatumia kujipakaa
mara mbili kwa siku, atajipakaa mwili mzima
asubuhi na jioni.
Page | 77
7. KUBATILISHA UCHAWI.
Mtu mwenye maradhi ya kijini na uchawi katika
mwili wake, ukitaka kumbatilishia huo uchawi
katika mwili wake, basi utafanya yafuatayo;
Utakwenda mpaka kwenye mti wa mbaazi ukiwa
na SANDARI UDI (ni udi huo) kisha ukifika hapo
utawasha udi wako hapo kisha utatia nia kuwa
unahitaji kuchukua dawa katika mti huo iende
ikakusaidie kutibu maradhi yatokanayo na majini
na uchawi.

Kisha utakuwa unauzunguka mti huo huku ukiwa


unasoma majina yote ya BARHATIHI kwa idadi ya
mara saba. Kisha ukimaliza, utachuma majani
mengi ya mti wa mbaazi. Kisha utarudi nayo
nyumbani, na utayatwanga upate unga wake.
Unga huo utausomea majina yote ya Barhatihi,
ukiwa umeuchanganya na unga wa karafuu
maiti.

Kisha mgonjwa atakuwa anachukua unga kiasi


kidogo anachemsha katika maji yenye ujazo wa
grasi tatu. Kisha atatumia kunywa grasi moja
kutwa mara tatu kwa siku, na kwa muda wa siku
saba.

Dawa hi inatibu maradhi mbalimbali yatokanayo


na uchawi majini katika mwili.

Page | 78
8. KUBATILISHA UCHAWI MWILINI.
Hii ni njia nyingine inayotumika kubatilisha uchawi
mwilini na kutibu maradhi yatokanayo na uchawi
na majini.

Utakwenda katika mti wa mbaazi ukiwa na udi


wako wa metro milani. Ukifika katika mti huo
utawasha udi wako, kisha utaanza kusoma
majina yote ya Barhatihi kwa idadi ya mara
saba, ukiwa umetia nia yako ya kutaka kuhitaji
kuuchukua mti huo uende ukakusaidie kutibu
maradhi ya kijini na uchawi, na maradhi hayo
unaweza ukawa hauyafahamu ni maradhi gani,
ila yanatokana na uchawi au majini. Baada ya
kumaliza kuuzungu mti wa mbaazi kwa idadi hiyo
utachuma majani yake ya kutosha. Kisha
utakwenda kuyatwanga upate unga wake.

Kisha utayaandika na majina ya BARHATIH katika


karatasi. Kisha karatasi hiyo utaiunguza, kisha
uisage upate majivu yake. Majivu hayo
utachanganya na unga wa majani ya mbaazi,
halafu utaongezea na unga wa halititi kiasi. Kisha
mchanganyiko huo atakuwa anatumia
kuchanganya katika maji ya moto grasi moja,
kisha atakunywa, anywe grasi moja kutwa mara
tatu kwa siku saba mfululizo. Ni dawa mujarabu
sana ya kutibu maradhi ya uchawi na majini
katika mwili.

Page | 79
RUQYA YA MAJINA YA BARHATIHI.
Miongoni mwa dua nzito sana na yeye matokeo
mazuri na ya haraka ni hii Ruqya ya majini ya
BARHATIH. Kisomo hichi cha majina ya BARHATIH ni
moto mkali sana dhidi ya majini na uchawi.

Ruqya hii inasomwa kwa mtu mwenye majini na


uchawi katika mwili wake.

Kabla ya mgonjwa kusomewa Ruqya hii, anatakiwa


mgonjwa apewa masharti na utaratibu utakaofanya
kisomo hicho kiwe ni chenye kukubalika na kuleta
matokeo mazuri.

Masharti hayo ni yale yale anayopewa mgonjwa


anayefanyiwa kisomo cha Ruqya za Aya za Qur’an
tukufu. Miongoni mwa taratibu na mamsharti hayo ni
pamoja na;
i) Mgonjwa anatakiwa kuambiwa awe msafi wa
mwili na mavazi (asiwe na janaba wala najisi
kubwa au ndogo).

ii) Mgonjwa aambiwe ajirazimishe kuweka mwili


katika stara nzuri ya kukubalika katika jamii na
Mwenyezi Mungu mwenyewe n.k.

Ruqya hii ni kimbilio la mashekh wengi sana pindi


wanapoletewa wagonjwa wenye mapepo wabaya
na mazito sana katika miili yao.
Page | 80
Pia sehemu panapofanyiwa kisomo cha Ruqya
haopatakiwi kuwa na makelele wala mapicha picha
ya masanamu ya viumbe hai, mfano, picha za
binadamu, wanyama au ndege, pia pasiwe na
matunguli eneo hilo. Pia msomaji anatakiwa awe na
udhu kamili, na afanye dua za kinga dhidi ya
mashetani kabla ya kuanza kisomo cha dua hiyo.
Kikubwa anatakiwa kujitoa kwa nafsi yote kwa niaba
ya watu wengine.

Ruqya hii inasaidia sana kwa mgonjwa mwenye


mapepo wachafu kwani hukimbia haraka sana pindi
kinaposomwa kisomo hicho cha RUQYA ya majina ya
BARHATIH.

UTARATIBU WA KUISOMA RUQYA HII:


Utamwambia mgonjwa akae chini kisha wewe
utakaa upande wake wa sikio la kulia kisha
utamsomea majina yote ya Barhatih.

Utamsomea majina ya BARHATIH, na kila jina moja


utalitamka kwa idadi ya mara 100 ndipo uende jina
linguine, na utamsomea majina yote ishirini na nane
(28).

Bukhuri yake ya kuchoma pindi unaposoma dua hiyo


ni:- (i) Halititi, (ii) Miatusaila na (iii) Karafuu maiti.

Page | 81
Zote utazichanganya pamoja kisha utakuwa
unachoma wakati wote unapofanya dua. Hakika
mgonjwa anaweza kudondoka chini au mashetani
kupanda kichwani na kupiga kelele za uchungu wa
maumivu. Au wanaweza kujidhihilisha hapo na
kukimbia mbali sana.

Kisomo hichi afanyiwapo mgonjwa mwenye


matatizo ya mashetani na uchawi katika mwili wake
basi mgonjwa huyo hupona kabisa, maradhi hayo.

FAIDA YA JINA MOJA MOJA LA BARHATIHI:


Hapo katika kipengele hiki utajifunza faida na
matumizi ya jina moja moja la BARHATIH.

Majina haya kumbuka yanashikiliwa (na


makhudamu) kwa kila jina moja linashikiliwa na
Makhudamu zaidi ya elfu hamsini (50,000). Kwa hiyo
unaweza kujifunza baadhi ya matumizi ya majina
haya yakakustaajabisha katika ulimwengu wa tiba.
Wewe usiwe na mashaka juu ya faida hizo zilizotajwa
katika jina husika, bali wewe unapaswa uamini na
ufanye kwa vitendo. Hapo ndipo utakapoona
matokeo kwa macho yako, na imani itazidi juu ya
utukufu wa majina haya ya Mwenyezi Mungu
(majina ya Barhatih)

Page | 82
1. BARHATIH

Jina hili ndio jina la kwanza katika majina 28 ya


Barhatih na ndio jina kiongozi. Ndio maana majina
haya yote yameitwa majina ya BARHATIH kwa
sababu ya jina hili la kwanza linaitwa BARHATIH

Jina hili ndio jina tukufu sana katika majina ya


BARHATIH. Kupitia jina hili unaweza kufanya
mambo mengi sana katika shughuli za tiba na
ukapata majibu makubwa sana katika shughuli za
tiba. Jina hili ni miongoni mwa majina ya BARHATIH
yenye kufanya kazi zake kwa haraka sana na
ukapata matokeo unayoyahitaji. Tuangalie
baadhi ya faida za jina hili la kwanza la BARHATIHI

 KUFUNGUA MILANGO YA RIZIQ


Iwapo kama umekubwa na dhiki ya kupata riziki
mbalimbali, utafutaji kwako umekuwa mgumu
sana. Na umetumia njia nyingi bila mafanikio
yoyote, basi tumia jina hili la kwanza la Barhatih,
utakuwa unalitamka jina hil, kwa utaratibu wa
Page | 83
kusoma majina ya Barhatih kama tulivyojifunza
kule mwanzo; utalitamka jina hili kwa idadi ya
mara 1000 kila siku usiku ukiwa unachoma
Bukhuri ya udi Sandar.

Basi hazitopita siku 40, Mwenyezi Mungu


atakufungulia riziki zako kwa njia ya ajabu sana
na ya haraka, dua hii ni Mujarrabu sana.

 KUPATA URAHISI WA MWANAMKE KUJIFUNGUA.


Kama kumekuwa na ugumu wa mwanamke
kujifungua basi utaliandika jina hili la Barhatih
katika chombo cha udongo au karatasi iliyosafi
kisha maandishi hayo utayaosha kwa maji safi,
kisha atapewa mama mwenye tatizo hilo
atumie maji hayo kwa kunywa kidogo kidogo
kutwa mara tatu, hakika haitopita muda mama
huyo atajifungua kwa wepesi na salama.

 KUPATA KIZAZI KWA MWANAMKE.


Endapo kama umekuwa na ugumu wa
mwanamke kupata kizazi basi utaliandika jina
hili kwa wino wa dhafarani kwa idadi ya mara
35 kisha utaosha maaandishi hayo kwa maji safi,
ndani yake utachanganya na asili kidogo.

Mama mwenye tatizo hilo atatumia kunywa


maji hayo grasi moja asubuhi na jioni kwa muda
wa siku saba. INSHAALLAH uzazi utafunguka
kwa uwezo wa M/Mungu.
Page | 84
 KUPATA HIFADHI YA MASOMO NA HADITHI
MBALIMBALI.
Utaliandika jina hili la BARHATIHI mara 7 katika
kiganja cha mkono wa kulia, kwa wino wa
dhafarani kisha utatia na asali katika kiganja
hicho. Kisha utaramba maandishi hayo mpaka
yote yafutike. Hakika utapata hifadhi kubwa
sana ya masomo na hadithi mbalimbali za
masomo. Dua hii mujarrabu sana.

 KUKIDHIWA HAJA YAKO YOYOTE UTAKAYO.


Iwapo kama unahaja kwa Mwenyezi Mungu
nawe unahitaji haja hiyo akutimizie au akujibu
basi utalitamka jina hili kwa idadi ya mara 662.
Na kila unapotimiza idadi ya 100 utataja haja
yako hapo, kisha utendelea na utaja huo huo
mpaka umalize au utimize idadi ya 662.
INSHAALLAH haja hiyo itajibiwa haraka sana.

 KUBATILISHA UCHAWI NA KUMUUNGUZA JINI


KATIKA MWILI.
Iwapo kama mtu anasumbuliwa na maradhi ya
uchawi au jinni katika mwili wake, basi
utaliandika jina hili la BARHATHI kwa wino wa
dhafarani katika karatasi iliyosafi mara 111.
Kisha utayaosha maandishi hayo kwa maji maji,
halafu ndani yake utatia na HALITITI kidogo na
Page | 85
unga wa kitunguu swaumu na chumvi ya
mawe.

Kisha maji hayo utayasomea jina la Barhatih


kwa idadi ya mara 313.

Kisha maji hayo atapewa mtu mwenye tatizo


hilo atumie maji hayo kwa kunywa kidogo
kutwa mara tatu na maji mengine atumie kwa
kuoga asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba
mfululizo, INSHAALLAH ataondokana na
changamoto hiyo.

2. KARIRY

Kariry ni jina la pili katika majina ishirini na nane 28


ya BARHATIH. Jina hili linafaida nyingi na miujiza
mingi endapo kama mtu atatambua siri
iliyojifisha katika jina hili.

Miongoni mwa siri kubwa zilizojifisha katika jina hili


ni pamoja na mwenye kutaka urafiki na majini
wema, basi akilitumia jina hili anaweza kuwa
naurafiki na majini hao na akafanya nao kazi
Page | 86
mbalimbali ikiwemo kazi za tiba, kuwaadhibu
majini waovu wanaokaa katika miili ya watu, basi
mtu anaweza akawatumia majini hao wema
wakaweza kuwaadhibi majini waovu, na
wanaokaa katika miili ya watu, basi mtu
anaweza akawatumia majini hao wema
wakaweza kuwaadhibi majini waovu, na
kuwatoa katika miili ya wagonjwa na kwenda
nao katika miji ya majini wema. Pia jina hili
unaweza kulitumia katika kuzuia mali zako
zisiweza kuibiwa na kiumbe yoyote, jinni au
binadamu. Pia faida nyingine kupitia jina hili la pili
unaweza kulitumia katika kumtia mtu mapenzi
makubwa juu yako. jina hili linaweza kutumika
katika kufungua nyota au biashara iliyofungwa
n.k.

Tuangalie baadhi ya faida za kulitumia jina hili la


pili katika majina 28 ya BARHATIHI.

 ANAYETAKA KUNYENYEKEWA NA VIUMBE WA


M/MUNGU (Majina, binadamu, wanyama n.k).
Iwapo kama unahitaji viumbe wa ALLAH (s.w.)
wakunyenyekee kila utakapo kwenda, majini,
watu, wanyama, ndege n.k. basi utalisoma jina
hili la KARIRY kwa idadi ya mara 100 kila siku
usiku, na kila unapofikisha idadi ya mara mia
moja utakuwa unatia nia yako hapo ya haja ya
kuhitaji kunyenyekewa na viumbe wa ALLAH

Page | 87
(s.w). Hakika utanyenyekewa na kila kiumbe wa
ALLAH (s.w) katika mgongo huu wa ardhi.

 KUFUNGUA NYOTA AU BIASHARA ILIYOFUNGWA


KICHAWI.
Iwapo kama nyota ya mtu imefungwa au
imechafuliwa au biashara ya mtu imefungwa
kishirikina basi utaliandika jina hili la pili, KARIRY
kwa kiarabu, katika karatasi nyeupe kwa
kutumia wino wa dhafarani. Kisha utayaosha
hayo maandishi kwa maji safi, kisha maji hayo
utachanganya ndani yake na marashi rose
(Rose Flavour) na maji ya marashi/maji ya waridi
(water rose).

Kisha maji hayo utatumia kwa kuoga asubuhi


na jioni kwa muda wa siku tatu mpaka saba. Na
wakati wa kuoga utakuwa unatia nia ya
kuhitaji kujifungua nyota yako.

Au katika biashara utatumia maji hayo kwa


kudekia sehemu ya biashara yako na maji
mengine utatumia kumwagia mwagia eneo la
nje katika biashara yako INSHAALLAH nyota
yako itafunguka na kung’aa na mambo yako
yatakwendea vizuri pia biashara itafunguka na
utapata wateja wa kutosha katika biashara
hiyo.

Page | 88
 KUPENDWA, KUKUBALIKA NA KUSIKILIZWA
KOKOTE UENDAKO DUNIANI.
Mwenye kuhitaji kupendwa, kukubalika na
kusikilizwa na watu na majini kokote aendako
duniani basi ataliandika jina hili la pili kwa
kiarabu katika karatasi kwa kalamu ya wino
mwekundu. Kisha karatasi hiyo hiyo utaisomea
jina hilo la la KARIRY mara 21, huku ukiwa
unaivukiza karatasi hiyo pindi unaisomea ubani
KANDARI.

Baada ya kuisomea karatasi hiyo utaitia


mfukoni au katika pochi au wallet yako
ambayo huwa unatembea nayo; kisha nenda
kokote duniani utapendwa, utasikilizwa na
utakubalika na kila mtu akutazamaa.

 KUTIBU MATATIZO YOTE YA MACHO.


Mwenye anasumbuliwa na matatizo yoyote ya
macho na akawa ametumia tiba mbalimbali
bila mafanikio yoyote basi atumie tiba hii ni
Mujarrabu sana kwa matatzo yote ya macho.

Utaliandika jina hili la pili katika chombo cha


udongo au katika karatasi nyeupe kwa wino
wa dhafarani. Kisha maandishi hayo
utayaosha kwa maji ya mvua au maji ya kisima
kisichokauka msimu mzima wa mwaka. Kisha
utatumia maji hayo kunawia usoni asubuhi na
jioni kwa muda wa siku saba mfullizo.
Page | 89
INSHAALLAH TATIZO HILO LA MACHAO
LITAKWISHA. Hii ni kwa maradhi yote ya macho.

 KUZUIA KITU CHAKO AU MALI YAKO YOYOTE


KUIBIWA.
Iwapo kama unahitaji kuazuia usiibiwe kitu
chako chochote au mali yako kuibiwa katika
eneo lako kutokana na wezi, majambazi,
vibaka n.k basi utaliandika jina hili la pili kwa
maandishi ya kiarabu katika karatasi, kwa
kutumia karamu ya wino mwekundu, kisha
karatasi hiyo utakwenda kuifukia kwa manuizi
ya kuweka kinga katika eneo lako. Basi
sehemu hiyo itazungukwa na malaika wengi
sana na hata kama utaacha mlango wazi na
wewe ukaondoka mwizi/wezi hawezi kuiba
eneo hilo.

 MWENYE KUTAKA URAFIKI NA MAJINI WEMA.


Iwapo kama unataka urafiki na majini wema
wakukusanyikie na wawe rafiki zako. Na
unaweza kuwaagiza chochote wakakufanyie
kwa idhini ya M/Mungu. Basi utasoma jina la
pili kila siku usiku kwa idadi ya mara 1000.

Na kila ukifika idadi ya 100 utakuwa unatia nia


ya haja yako, na endelea kusoma. Wakati
unasoma utakuwa unachoma SANDAR UDI.

Page | 90
 KUMFANYA MTU AKUPENDE SANA.
Miongoni mwa faida za kushangaza za jina hili
ni kumtia mtu mapenzi ya kukupenda sana
mithiri ya kichaa. Mtu huyo atakuwa haambiwi
neno lolote baya kuhusu wewe akalisikilza
wala kuliamini kutokana na mapenzi yake
makubwa kwako.

Iwapo kama unahitaji kumfanya mtu yoyote


akupende kupita kiasi, mpenzi, mke, mume,
bosi wako au mtu yeyote basi utafanya hivi,

Utaandika katika karatasi “BISMILLAH


RRAHMAAN RRAHIIM” kwa kiarabu kisha
utaandika kwa chini yake na majina mawili ya
BARHATIH jina la kwanza na jina la pili kwa
kiarabu (BARHATIH, KARIRY)

Kisha baada ya kuandika majina hayo mawili,


chini ya majina hayo utaandika na nia yako
kwa lugha yoyote unayoifahamu. Maandishi
hayo yote utatumia wino wa dhafarani
kuandika.

Kisha maandishi hayo utayaosha kwa maji safi


halafu ndani yake utachanganya na athari ya
mate yako kidogo.

Maji hayo utatumia kupikia chakula


atakachokula mtu huyo au utamuwekea maji
hayo kidogo katika kinywaji chake atakacho
Page | 91
kunywa. hakika mtu huyo atakupenda sana
kupita kiasi. Tiba hii ni mujarrabu sana.

3. TATILIHI

Hili ni jina la tatu katika ile idadi ya maji 28 ya


BARHATIH. Jina hili limebeba siri nyingi sana. Jina
hili linauwezo wa kuvuta au kuhamisha kitu kuleta
maelewano baina ya wanancdoa, kuvuta utajiri
wa halali kutoka kwa M/Mungu, kuondoa mauza
uza ndani ya nyumba n.k.

Tuangalia baadhi ya faida za jina hili

 KUMUHAMISHA MTU DHWALIMU/ADUI YAKO


KATIKA NYUMBA YAKO.
Iwapo kama katika nyumba yako kuna mtu
unahitaji ahame eneo hilo bila kupenda. Au
unahitaji kufukuza vitu vibaya katika eneo hilo,
mfano majini wabaya, misukule, vibwengo n.k,
basi utafanya yafuatayo;

Page | 92
Utaliandika jina hili la TATILIHI kwa kiarabu katika
kitu kigumu (mfano ubao) kwa idadi ya mara
13. kisha utalisomea jina hilo hilo kwa idadi ya
mara 13. Kisha utafukia katika eneo la nyumba
yako kwa manuizi yako unayohitaji kama ni
kumuhamisha mtu au kufukuza vitu vibaya
katika nyumba yako n.k.

INSHALLAH haja yako itakubalika haraka sana


dua hii ni mujarrabu sana, na ina matokeo ya
haraka sana.

 KUPATA UTAJIRI WA HALALI NA MAISHA YENYE


KURIDHISHA.
Kama unahitaji utajiri wa halali na maisha yenye
kuridhisha basi utasoma jina hili kwa idadi ya
mara 70 kila siku usiku au baada ya swala ya
Alfajri kwa muda wa siku 40 mfululizo. INSHALLAH
M/Mungu atakuruzuqu utajiri wa halali na
maisha yenye kuridhisha kabla mtu huyo
hajafikwa na mauti.

 KUONDOSHA MIGOGORO BAINA YA


WANANDOA.
Iwapo kama wanandoa wamekosa
maelewano mpaka ikifikia hatua ya mmoja
kudai taraka kisha mmoja wao akahitaji
ipatikane suluhu baina yao basi ataliandika jina
la tatu katika karatasi kwa karamu ya kawaida
kwa idadi ya mara 70 kisha karatasi hiyo
Page | 93
atapewa mmoja kati ya wana ndoa hao
aibebe kichwani kwa nia ya kuleta maelewano
kati yao.

Kama ni mwanamke atatia juu ya kichwa kisha


atavalia ushungi au kofia au kilemba juu yake,
na mwanaume ataweka juu ya kichwa kisha
atavalia kilemba au kofia juu yake kisha
karatasi hiyo atashinda nayo siku nzima. Hakika
maelewano yatapatikana na wataelewana
na kupendana sana.

 KUONDOA MAUZA UZA NDANI YA NYUMBA.


Kama ndani ya nyumba yako kuna mauzauza
au vitu vya kutisha tisha visivyojulikana, nawe
ukahitaji kuviondoa vitu hivyo basi utasoma
jina la kwanza, la pili na la tatu la BARHATIH
kwa idadi ya mara 100 huku ukiwa unachoma
Bukhuri shari au chumvi ya mawe (utasoma
BARHATIH, KARIRY na TATILIH x100).

INSHAALLAH mauza uza hayo yataondoka


katika nyumba hiyo na kutakuwa na Amani
kabisa eneo hilo la nyumba

Page | 94
4. TWURAN

Hili ni jina la nne katika majina 28 ya BARHATIH,


jina hili ni miongoni mwa majina matukufu, katika
majina ishirini na nane ya BARHATIH.

hili ni lenye uwezo wa kumfanya mtu apate


uwezo wa kutiiwa na watu au majini pia jina hili
linaweza likasababisha mtu atoke magereza
(kifungoni), kuondosha mashetan na kubatilisha
uchawi katika mwili na kumfanya mtu akubalike
na kutekelezewa haja yako kutoka kwa watu.

Tuangalie baadhi ya faida hizo kwa kina zaidi;

 MWENYE KUTAKA KUTIIWA NA WATU NA MAJINI:


Iwapo kama unahitaji majini na watu wakutii
kwa chochote utakacho waamrisha
wakufanyie na usipingwe na mtu yeyote basi,
utariandika jina hili la nne katika karatasi
nyeupe kwa karamu ya kawaida kwa idadi ya
mara tano (5) kisha chini yake utaandika na zile
aya nne za mwisho za Surat HASHRI (21 – 24).
Page | 95
Kisha baada ya kuziandika aya nne hizo za
mwisho, chini yake utaandika na herufi HAMZA
(hii ni miongoni mwa irabu katika herufi za
Qur’an) utaiandika herufi hiyo ya Hamza mara
saba. Kisha utaivukiza karatasi hiyo kwa ubani
sandarusi. Utachoma ubani Sandarus kisha
utakuwa unatia nia yako huku ile karatasi
unaipitisha pitisha katika ule moshi wa ubani
uliochoma. Kisha karatasi hiyo utakuwa
unatembea nayo mfukoni au katika pochi au
wallet yako. INSHAALLAH utatiiwa na watu,
viongozi na majini wote, pia M/Mungu
atakufungulia katika shughuli zako zote
unazozifanya.

 KUTEKELEZEWA HAJA YAKO BAADA YA


KUDHULUMIWA.
Iwapo kam umedhulumiwa mali yako au
umekimbiwa na mke/mme wako nawe ukahitaji
mkeo au mme arejee /mali yako irejeshwe
kwako.

Basi utasoma jina hili kwa idadi ya mara 1000,


na kila unapofika 100 utakuwa unatia nia ya
haja yako hapo kisha unaendelea. Kipindi
unasoma dua hii utakuwa uchoma ubani
Mashitaka au udi Sandar fanya hivyo kila siku
usiku kwa muda wa siku saba mfululizo,
INSHAALLAH hazitopita siku tatu kitu chako
Page | 96
kitalejeshwa au kama ni mke au mume atarejea
nyumbani haraka sana.

 KUMTOA MTU KIFUNGONI.


Iwapo kama unahitaji kumtoa mtu kifungoni
aliyefungwa basi utaliandika jina hili la nne
katika karatasi au nguo kisha apewe mtu huyo
awe anatembea nayo hiyo karatasi au nguo
hiyo. Au unaweza kuliandika jina hili katika
chakula kisha akapewa mtu huyo akala kile
chakula INSHAALLAH atatolewa mtu huyo
kifungoni haraka sana kwa uwezo wa
M/Mungu.

 KUONDOA MASHETANI NA KUBATILISHA


UCHAWI KATIKA MWILI.
Iwapo kama mtu anasumbuliwa na mashetani
katika mwili wake au ametupiwa uchawi katika
mwili nawe ukahitaji uchawi huo ubatilike au
mashetani hayo yaondoke. Basi utayaandika
majina hayo manne kuanzia jina la kwanza
mpaka la nne (BARHATIH, KARIRY, TATILIHI na
TWURAN, kwa kiarabu) utaandika katika
chungu cha udongo.

Kisha ndani yake utatia na maji. Utaandika


kwa kutumia wino wa dhafarani.
Kisha maji hayo atapewa mtu mwenye
amefanyiwa uchawi katika mwili wake au
mwenye matatizo ya majini. Atumie maji hayo
Page | 97
kwa kunywa kidogo kidogo, kutwa mara tatu
na maji mengine atatumia kuchanganya
katika maji yake ya kuoga. Atatumia kuoga
kwa muda wa siku saba mfululizo.

Hakika atapiga kelele sana kama mtu huyo


ana mashetani katika mwili wake. Na uchawi
huo ubatilika.

 KUPENDWA NA KUKUBALIKA KATIKA JAMII.


Kama unahitaji kupendwa na kukubalika
katika jamii basi utaliandika jina la kwanza
mpaka jina la nne katika karatasi. Kwa karamu
ya kawaida. Kisha karatasi hiyo utaipakaa
mafuta uzuri (Miski) ukiwa unatia nia yako
hapo ya kuhitaji kupendwa na kukubalika
katika jamii.

Kisha karatasi hiyo utakuwa unatembea nayo


mfukoni au katika pochi au wallet yako.
INSHAALLAH utapendwa na utakubalika sana
katika jamii inayokuzunguka na kila mahali
unapokwenda.

Page | 98
5. MAZJAR

Hili ni jina la tano katika majina 28 ya Barhatih ni


miongoni mwa majina matukufu yenye uwezo wa
kufanya mambo mengi katika ulimwengu wa tiba.

Miongoni mwa faida za jina hili kwa atakaelitumia


ni pamoja na kurahisisha mwanamke kupata
kizazi, kupata vitu vizuri vya kidunia, kusamehewa
madhambi kwa mtamkaji wa jina hili kuepushwa
na adhabu za kaburi, kumuona mtume (s.a.w)
kupitia ndoto n.k.

 KURAHISISHA MWANAMKE KUPATA KIZAZI.


Kama kuna shida ya mwanamke kupata kizazi
nae akawa ni mwenye uhitaji wa kupata watoto
basi utaliandika jina hili la MAZJAR (kwa kiarabu)
kwa idadi ya mara (7) katika sahani ya kaole
(sahani ya udongo) au katika karatasi nyeupe,
kwa wino wa dhafarani.

Kisha chini ya maandishi haya ya jina hilo,


utaandika na jina hili (ALTWAHAA TWILY) Huyu ni
khudamu – mtumishi anayelitumikia jina hili, nalo
Page | 99
utaliandika kwa kiarabu kwa idadi ya mara nane
(8).

Kisha utayaosha maandishi hayo kwa maji safi.


Kisha maji hayo atapewa mwanamke huyo maji
anywe kidogo kidogo kwa muda wa siku saba.
Pindi anapomaliza siku zake za mwezi (hedhi)
INSHAALLAH M/Mungu atamjaalia kupata kizazi
kwa wepesi hata kama alikuwa amefungwa
kichawi.

 KUPATA VITU VINGI VIZURI VYA KIDUNIA.


Iwapo kama unahitaji M/Mungu akupe vitu
vizuri vizuri vya kidumia, basi utalisoma jina hili
kwa idadi ya mara 50 kila siku usiku. Fanya
kama uradi wako kulitamka jina hili kisha
ukimaliza utakuwa unatia nia yako ya haja hiyo.

 KUSAMEHEWA MADHAMBI YA MTU.


Endapo kama unahitaji Mwenyezi Mungu
akusamehe madhambo yako, basi utalitamka
jina hili kwa idadi ya mara 1000 usiku kisha
muombe msamaha M/Mungu INSHAALLAH
m/Mungu atakusamehe madhambi yango.

 KUEPUSHWA NA ADHABU ZA KABURI.


Mwenye kupendelea kulitamka jina hili mara
kwa mara usiku katika uhai wake, Mwenyezi
Mungu atamuepusha na adhabu za kaburi
baada ya kufa kwake.
Page | 100
 KUMUONA MTUME (S.A.W) KATIKA NDOTO.
Iwapo kama unahitaji kumuona Mtume (s.a.w)
katika ndoto basi utalitamka jina hili, kwa idadi
ya mara 100 kila siku usiku, kwa muda wa siku
saba. Na pindi unapokwenda kulala katika siku
hizo saba utakuwa unalala ukiwa na udhu
uliokamilika, pia utalala na nguo zenye kusitiri
mwili wako hasa hasa tupu yako pia katika siku
hizo ulale ukiwa haujajifunika nguo yoyote
INSHAALLAH M/Mungu atakukutanisha na Mtu
(s.a.w) katika ndoto.

6. BAZIJAL:

Bazijal ni miongoni mwa majina ya Balhatih


katika majina 28 ya BARHATIH. Hili ni jina la sita
katika majina ya Barhatih. Miongoni mwa faida
unazoweza kuzipata kupitia jina hili ni pamoja na
kuweza kupata chochote ukitakacho kutoka
kwa ALLAH (S.W), kubatilisha uchawi na kuondoa
uchawi katika mwili au nyumba.

Page | 101
 KUPATA KITU CHOCHOTE UKITAKACHO KUTOKA
KWA MWENYEZI MUNGU.
Kama unahitaji jambo lolote kutoka katika
hazina za Mwenyezi Mungu basi utaliandika
jina hili la BAZJAL kwa kiarabu katika karatasi
nyekundu kwa idadi ya mara moja.

Utaandika alfajiri ya siku ya ALKHAMISI kabla


hujaongea na mtu yeyote na jua
halijachomoza kisha kwa chini ya jina hilo
utaandika na manuizi ya haja yako kwa lugha
yoyote ile. Kisha karatasi hiyo utakwenda
kuitupa Baharini. Hakika M/Mungu
atakutekelezea haja yako haraka sana.

 KUBATILISHA UCHAWI NA KUONDOA UCHAWI


KATIKA MWILI AU KATIKA NYUMBA.
Kama unahitaji kuuwa uchawi ulio katika
nyumba yako au katika mwili wako basi
utachukua chumvi ya mawe kisha utaweka
katika maji yako kiasi cha lita 10, chumvi iwe
kiasi chagao la mkono mmoja. Kisha
utayasomea haya majina mawili ya BARHATIH.
Jina la tano na jina la sita (MAZJAL, BAZJAL)
kwa idadi ya mara 66 kisha maji hayo atatumia
kuoga mtu mwenye uchawi katika kiwili wili au
yatatumika kudekia dekia ndani ya nyumba
yako. hakika uchawi wote katika mwili au

Page | 102
nyumba utabatilika kabisa dua hii mujarabu
sana.
7. TARQAB.

TARQAB ni jina la saba katika majina 28 ya


BARHATIH. Jina hili ni miongoni mwa majina
matukufu sana katika majina ya BARHATIH.

Iwapo kama unahitaji mvuto wa wateja katika


biashara yako au katika kazi yako, basi
utaliandika jina hili katika karatasi nyeupe kwa
wino wa dhafarani mara saba. Kisha maandishi
hayo utayaosha kwa maji yaliyosafi. Kisha maji
hayo utayasomea jina hilo hilo kwa idadi ya
mara 70 kisha utatia nia yako ya kuhitaji mvuto
katika biashara au shughuli yako yoyote.

Maji hayo utatumia kudekia dekia na kumwagia


mwagia kwa nje katika biashara yako au eneo
lako la kazi.

Pia jina hili unaweza kulisoma kwa idadi ya mara


70 ukiwa katika biashara kwa nia ya kuvuta

Page | 103
wateja eneo hilo, dua hii ni mujarrabu sana
katika mvuto wa wateja katika eneo lako la kazi.

8. BARHASHI.

Hili ni jina la nane katika majina 28 ya BARHATIH


jina hili ni miongoni mwa majina matukufu sana
katika majina ya Barhatih. Jina hili hutumika sana
katika shughuli za kuvuta mtu alioko mbali au
aliekukimbia aweze kurudi haraka sana kwako.
Humvuta mtu yoyote alioko mbali, ndugu,
mpenzi, mke au mume au yeyote unaehitaji
akuijie kwako haraka basi unaweza kutumia jina
hili.

Utaratibu wake;
Ufikapo usiku wa kuanzia majira ya saa sita
mpaka saa 11 alfajiri, utaswali Rakaa mbili za
sunatil Hajja kisha baada ya salam utataja shida
yako hapo. Kisha utafanya Istighafari mara 100,
utamswalia mtume mara 100, na utasema YAA
LATWIFU mara 129.

Page | 104
Kisha baada ya hapo utaanza kulisoma jina hili
kwa idadi ya mara 1209. Na kila ukifika idadi ya
100, utakuwa unatia nia yako hapo, kisha
unaendelea tena mpaka utakapotimiza idadi
hiyo.

Pia ni vizuri wakati unafanya dua hiyo basi


inapendeza uwe unachoma udi Sandari au
ubani dhukra au ubani mashtaka. Ufafanya
hivyo ndani ya siku tatu mfululizo. Hakika mtu
huyo atakuja haraka sana.

9. GHARMASH.

Hili ni jina la tisa katika majina 28 ya BARHATIH jina


hili ni maarufu sana kwa sifa yake ya kuita
Makhudamu (watumishi wa jina hili).

Jina hili unaweza ukalitumia katika kuita


makhudamu wanao litumikia jina hilo na
ukaweza kufanya nao kazi. Kazi za makhudamu

Page | 105
( Watumishi) zipo nyingi sana ambazo unaweza
ukafanya nao hao Makhudamu.

Miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na


kukufundisha elimu mbalimbali, kukupa ndoto na
tafasiri ya mambo yajayo, kuwaadhibu majini
wakolofi, kukufundisha uganga n.k.
Kazi zote hizo na zile utakazozihitaji unaweza
kumuamrisha khudamu huyo baada ya kumuita
na akakufanyia kwa idhini ya Mwenyezi
Mungu.iwapo kama utahitaji kumuita khudamu
(mtumishi wa jina hili ili akufanyie jambo lako
loloteulitakalo, basi utalisoma jina hili kwa idadi
ya mara 300 kila siku usiku kwa muda wa siku
saba zenye kufuatana na kila unapofika idadi ya
100 utakuwa unatia nia ya jambo lako ambalo
unataka huyo khudamu akufanyie. Utatia nia
hiyo kwa lugha yoyote unayoifahamu.

Masharti yake;
i. Pindi unapofanya A’amali hiyo unatakiwa uwe
(RIADHA) umejitengta na mambo yafuatayo.

ii. Usifanye mapenzi katika siku hizo saba na mtu


yoyote usitumie kilevi chochote, uwe katika
swaumu ya Sunna siku zote saba, na wakati
wa kufuturu jioni usifuturu mboga yenye roho
katika chakula chako (kuku, samaki, nyama)
pia uwe katika mavazi twahara wakati wa
amali hiyo.

Page | 106
10. KHUTWIR.

Hili ni jina la kumi katika majina 28 ya Bartihi, jina


hili ni miongoni mwa majina matukufu ya
Barhatihi na lenye matumizi mengi katika
ulimwengu wa tiba. Miongoni mwa faida
zipatkanazo kupitia jina hili ni pamoja na;

Kumkinga mtoto asiweze kuchezewe kichawi na


majini au washirikina, jina hili pia hili unaweza
ukalitumia mtu akupende sana katika moyo
wako, kumuokoa mtu kutokana na balaa au
tatizo lililompata n.k.

Tuangalie baadhi ya faida za jina hili kwa


ufafanuzi;

 KUMKINGA MTOTO ASICHEZEWE NA MAJINI NA


UCHAWI.
Kama unataka mtoto kumkinga kutokana na
kuchezewa kichawi kutokana na majini na
washilikina basi utaliandika jina hili katika
karatasi nyeupe kwa kalamu nyeusi kwa idadi
Page | 107
ya mara saba. Kisha chini yake katika karatasi
hiyo utaiandika Surat TWAARIQ yote. Kisha
karatasi hiyo utamfungia mtoto katika
kitambaa cheusi kisha utamvisha katika mkono
wake. Hakika mtoto huyo hawezi kuchezewa
na wachawi wala majini. Pia ataepukana na
maradhi mengi yale ya kitoto, pia jina hilo
linaweza kuandikwa katika karatasi kwa idadi
hiyo hiyo kisha ikaandikwa na hiyo sura chini
yako kwa wino wa dhafarani kisha maandishi
hayo yakaoshwa kwa maji safi kisha akapewa
mtoto huyo akawa anakunywa kidogo kidogo
na maji mengine yatumike kwa kumuogeshea.

 KUWA NA UWEZO WA KUHIFADHI ELIMU MBALI


MBALI NA KUPATA HEKINA.
Kama unahitaji uwe na uwezo wa kulifadhi
elimu mbalimbali unazojifunza au kusoma
katika vitabu mbalimbali au kuwa na hekima
katika maneno yako na matendo yako, basi
utalisoma jina hili kwa idadi ya mara 70 katika
kikao kimoja. Utasoma kila siku kwa muda wa
siku saba au zaidi INSHAALLAH M/Mungu
atakujalia kuwa na elimu mbalimbali na
zitaweza kuhifadhika katika akili yako, pia
mwenyezi Mungu atakupa hekima katika
maneno yako na matendo yako.

Page | 108
 KINGA DHIDI YA UCHAWI NA KUBATILISHA
UCHAWI KATIKA MWILI.
Utaliandika jina hili mara 21 katika chombo au
karatasi nyeupe kwa wino wa dhafarani kisha
utayaosha maandishi hayo kwa maji safi kisha
maji hayo utayatumia kwa kunnywa kwa
muda wa siku saba mfululizo. INSHAALLAH mwili
wako utakuwa na kinga dhidi ya uchawi wa
aina yoyote utakaologwa au kutupiwa katika
mwili wako. Pia kama ndani ya mwili wako
kuna uchawi basi utakwenda kubatilika na
utakuwa salama kutokana na uchawi huo.

 KUMFANYA MTU AKUPENDE SANA.


Iwapo kama unahitaji mtu Fulani akupende
sana kwa moyo wake wote, basi utalisomea
tunda tamu au chakula kitamu jina hili kwa
idadi ya mara saba kisha utatia nia yako juu ya
mtu huyo, halafu utalipuliza tunda hilo. Kisha
tunda hilo au chakula hicho utampa mtu huyo
uliomkusudia akupende ale tunda hilo au
chakula hicho.

Hakika mtu huyo atakupenda sana kwa moyo


wake wote atake au asitake atakupendwa
sana. Dua hii ni mujarrabu sana isitumike kwa
majaribio, bali ufanye kwa mtu ulie na
malengo nae.

Page | 109
 KUTIIWA NA KUPENDWA NA WATU.
Kama unahitaji watu wakutii na kukupenda
popote uendapo, basi utaliandika jina hili
katika chombo au kitu utakuwa unatembea
nacho kitu hicho, basi watu watakupenda
sana na kukutii sana utaandika kwa kutuimia
wino wowote wa kalamu.

 KUMUOKOA MTU NA TATIZO AU BALAA.


Utaliandika jina la KHUTWIR na KHUTWISH
(khadimu na jina hili) kwa maandishi ya kiarabu
katika kiganja cha mkono utaandika kwa
maka pen nyekundu.
Kisha utamnyoshea mtu huyo kiganja chako
hicho huyo mtu mwenye tatizo au balaa
lililompata au unaweza kwenda kumshika mtu
mwenye mashetani kipindi una msomea dua
hakika mtu huyo atapiga kelele sana. Na pia
kama utamnyoshea kinganja hicho mtu
mwenye balaa huku unatia nia ya kumuokoa
hakika atakuwa salama.

 KUTIBA MARADHI YA KISHETANI.


Iwapo kama unahitaji kumtibu mtu mwenye
maradhi ya kishetani, basi utaliandika jina hili la
KHUTWIR kwa kiarabu katika karatasi kwa
kutumia wino wa dhafarani kwa idadi ya mara
99. Kisha utaosha maandish hayo kwa maji safi.
Kisha maji hayo utayasomea Surat FATIL na
AYATUL QURSIYYU zote kwa idadi ya mara 75.
Page | 110
Kisha maji hayo atapewa mtu huyo mwenye
maradhi ya mashetani atumie kwa kunywa
grasi moja kutwa mara tatu na maji mengine
atumie kwa kuoga asubuhi na jioni afanye
hivyo kwa muda wa siku saba mfululizo.
INSHAALLAH atakwenda kupona maradhi
hayo ya kishetani, katika mwili wake.

 UKITAKA KUMPATA KHUDAMU (MTUMISHI)WA


JINA HILI LA KHUTWIR NA UMUAGIZA
CHOCHOTE AKUFANYIE.
Utasoma jina hili kwa idadi ya mara 70 kila siku
usiku ukiwa katika mavazi meupe na yaliyo safi,
huku ukiwa unachoma ubani Kandani na kila
unapomaliza kulitamka jina hilo kwa idadi hiyo
ya mara 70 utakuwa unatia nia yako juu ya
kumuhitaji huyo Khudamu akufanyie au
umuagize kile unachokihitaji utafanya hivyo
kwa muda wa siku 40 mfululizo, INSHAALLAH
jambo lako litakuwa kama unavyotaka.

Page | 111
11. QALNAHUWD:

Hili ni jina la kumi na moja katika majina 28 ya


Barhatih jina hili ni miongoni mwa majina
matukufu ya Barhatih, jina hili ni maarufu sana
hasa katika mambo ya kuvunja nguvu za
uchawi na kufurusha mashetani katika nyumba
au mwili wa mgonjwa. Tuangalie baadhi ya
faida za jina hili

 KUBATILISHA/KUVUNJA NGUVU ZA UCHAWI.


Iwapo kama unahitaji kubatilisha uchawi katika
mwili, basi utaliandika jina hili kwa lugha ya
kiarabu katika karatasi nyeupe kwa wino wa
dhafarani mara 21. Kisha utayaosha maandishi
hayo kwa maji yaliyosafi. Kisha ndani ya maji
hayo utaweka na halititi kidogo na chumvi ya
mawe.

Kisha maji hayo atapewa mgonjwa mwenye


maradhi ya kijini au aliyesibiwa na uchawi
katika mwili wake atumie maji hayo kwa kuoga
na kupaka kichwani asubuhi na jioni kwa siku
Page | 112
saba mfululizo. Kwa uwezo wa M/Mungu
uchawi huo au kama anamashetani katika
mwili wake yataondoka, na uchawi utabatilika
INSHAALLAH.

 KUFURUSHA MAJINI KATIKA MWILI.


Iwapo kama mtu anasumbuliwa sana na
majini katika mwili wake, basi utamsomea mtu
huyo jina hili mara 60 hali ya kuwa amejifunika
shuka na ukiwa unachoma au unamfusha kwa
kuchoma ubani maka, ubani kandari , ubani
jawi na ambali. Hakika majini hao wataondoka
haraka sana tena muda huo huo.

Pia jina hili linaweza kuandikwa katika karatasi


kwa wino wa dharafani mara 99, kisha
ukayaosha maandishi hayo kwa maji safi na
ndani yake ukaweka karafuu maiti, unga wa
karafuu tunda, Halititi, kisha utayasomea maji
hayo majina yote ya BARHATIH kwa idadi ya
mara 7, kisha mgonjwa atatumia maji hayo
kwa kuoga asubuhi na jioni na maji mengine
atatumia kwa kunywa kidogo kidogo kutwa
mara tatu kwa muda wa siku saba,
INSHAALLAH kama katika mwili wake kuna jini
wa aina yoyote basi jini huyo ataondoka
haraka sana katika mwili wa mgonjwa huyo.

Page | 113
 KUMZUIA JINI ASIRUDI TENA KATIKA KICHWA
CHA MGONJWA.
Kama unawasiwasi wa jinni aliyetoka katika
mwili wa mgonjwa wako anaweza kurudi tena
katika siku za mbele, basi ukitaka jinni huyo au
majini wa aina yoyote wasirudi tena basi
utaliandika jina hili katika karatasi kwa kalamu
ya kawaida kisha utampa mgonjwa abebe
jina hilo katika kichwa chake kwa siku nzima
(kama anavaa kofia, kilemba au ushungi basi
karatasi hiyo ataiweka kichwani kisha atavaa
ushungi au kilemba au kofia wa siku nzima).
Hakika jinni huyo hatorudi tena katika kichwa
cha mgonjwa milele. Inshallah

Page | 114
HITIMISHO:
Naamini kitabu hiki baada ya kukisoma vizuri na kukielewa,
kitakuwa kimekusaidia sana katika kujifunza elimu ya tiba
kupitia Qur’an tukufu na majina 28 ya Barlhatih.
Ninakusihi ufanyie kazi yale uliyojifunza kwa bidii ili uweze
kupata matokeo makubwa zaidi.
Ndugu msomaji wa kitabu hiki, katika kitabu hiki nimejaribu
kueleza mambo mengi na kufafanua kwa kina zaidi, lakini
na kusihi usikikose kusoma kitabu cha pili cha
“UTUKUFU WA MAJINA 28 YA BARHATIH”
Pindi kitakapotoka Inshaallah,
Pia unaweza kujipatia Nakala za vitabu vilivyopo vya Bashiri
Hussein Lugamba kwa kuwasiliana nae kwa namba
zifuatazo;-
+255 757 455 646
+255 782 010 104
+255 672 410 104
eBooks/softcopy (Nakala laini)
1. Maajabu ya miti shamba katika kutibu maradhi ya Kijiji
na uchawi No. 1
2. Maajabu ya miti shamba katika kutibu maradhi ya kijini
na uchawi no. 2.
3. Maajabu ya Qur’an tukufu katika kutibu maradhi na
kuondosha shida mbalimbali
TEMBELEA MITANDANO YA KIJAMII YA BASHIRI
YOUTUBE: Tiba Facts Oline TV (utapata video nyingi za
kukufundisha mambo mbalimbali yanayohusu tiba
kupitia Qur’an na miti shamba.
FACEBOOK: (a) Tiba Facts
(b) Qur’an and Herbals medicine
INSTAGRAM: Tiba Facts/Ustadh. Bashiri.
Page | 115

You might also like