Professional Documents
Culture Documents
Kitabu Cha Sala 2
Kitabu Cha Sala 2
Haya ni baadhi ya masharti ya lazima katika hali ya kawaida kwa sala zote.
(1) Kuwa Muisalmu.
(2) Kuwa na nia ya kutaka kusali sala ile.
(3) Kuwa tohara mwili, kivazi na pahali pakusalia.
(4) Kuvalia kivazi cha kufaa kwa sala.
(5) Pahala pakufaa kusali.
(6) Kusali ndani ya wakati wake.
(7) Kuelekea kibla.
Sala za Faridha
(1) Sala ya adhuhuri husaliwa rakaa nne kwa kusoma ndani yake alhamdu tu katika rakaa zote
nne. Siku ya Ijumaa husaliwa sala ya Ijumaa rakaa mbili badala ya adhuhuri.
(2) Sala ya laasiri husaliwa rakaa nne kwa kusoma ndani yake alhamdu tu katika rakaa zote nne.
(3) Sala ya magharibi husaliwa rakaa tatu kwa kusoma ndani yake alhamdu na sura au aya za
Qur-an katika rakaa mbili za mwanzo na kusoma alhamdu tu katika rakaa ya tatu, ya mwisho.
(4) Sala ya isha husaliwa rakaa nne kwa kusoma ndani yake alhamdu na sura au aya za Qur-an
katika rakaa mbili za mwanzo na alhamdu tu katika rakaa mbili za mwisho.
(5) Sala ya alfajiri husaliwa rakaa mbili kwa kusoma ndani yake alhamdu na sura au aya za
Qur-an katika rakaa zote mbili..
(6) Wengine wanasema sala ya maiti ni faridha na sala ya witri ni sunna ya wajib. Mtu akiwa
hakusali sala ya witri lazima ailipe. Na Mola Anajua zaidi.
(7) Sunna ya alfajiri mtu akiikosa anaweza kuilipa baada ya faridha ya alfajiri au baada ya kutoka
jua.
Nguzo za sala
Ni zile ambazo mtu akiziacha bila sababu hata kwa kusahau basi sala huharibika. Nazo ni pamoja
na:-
(1) Nia (2) Kusimama
(3) Takbir ya kuhirimia (4) Alhamdu
(5) Kurukuu (6) Kusujudu
(7) Kukaa kwa tahiyatu (8) Tahiyatu
(9) Salamu.
Nyakati za sala
(1) Adhuhuri huanza mchana pale kivuli chako kinapoanza kurefuka kwani jua lilipokuwa juu ya
utosi wako kilikuwa kifupi umekikanyaga.. Mwisho wa wakati ni pale kitakapokuwa sawa na
wewe mwenyewe.
(2) Hapo huanza laasiri na kuendelea mpaka kutua jua.
(3) Hapo hapo huanza magharibi na kuendele mpaka yaanze kutoweka mawingu mekundu.
(4)Hapo huanza wakati wa isha mpaka thuluthi ya usiku. Maulamaa wengine wanasema mpaka
nusu ya usiku.
(5) Alfajiri huanza kwa kutoka alfajiri na humaliza kwa kuchomoza jua.
Namna ya Kusali
Sala ya mtu peke yake ya rakaa nne
Sala ya adhuhuri au laasiri au isha..
(1) Simama uelekee kibla usiache nafasi kubwa baina ya miguu. Iwe nafasi kiasi ya urefu wa
unyayo wako. Elekea kibla kwa kifua chako utazame pahala pakusujudia. Fanya hivi kwa sala
zote. Sala za sunna unaweza kusali umekaa lakini thawabu zinapunguwa.
(2) Soma adhana kama haijasomwa hapo. Mwanamke hasomi adhana.
(3) Soma iqama. Mwanamke hasomi iqama.
(4) Soma tawjihi. Madhehebu yetu sala zote zinayo tawjihi hata ya maiti tawjihi ni hii:-
(ii) Ya laasiri:-
(iii) Ya isha:-
(iv) Ya magharibi:-
(v) Ya alfajiri
Rakaa ya pili
(1) Rakaa zote nyengine usisome adhana wala iqama wala audhu wala tawjih. Anza na
bismillahi na alhamdu. Ikiwa ni isha au magharibi au alfajiri basi utasoma sura au aya za Qur-an
baada ya alhamdu.
(2) Rukuu kisha usujudu kama rakaa ya mwanzo ila usisimame utakaa kusoma tahiyatu ya
mwanzo. Ukimaliza ndio usimame kwa ajili ya rakaa ya tatu. Kila ukisujudu au ukisimama lete
takbir.
Rakaa ya tatu
(1) Simama uanze rakaa ya tatu. Umeshajua kuwa rakaa huanza kwa bismillahi ya alhamdu na
humaliza rakaa kwa kumaliza sijda.
(2) Katika sala ya rakaa nne, rakaa ya tatu haina tahiyatu. Simama kwa ajili ya rakaa ya nne.
(3) Kumbuka katika sala ya isha rakaa mbili za mwanzo utasoma sura au aya za Qur-an baada ya
alhamdu.
Rakaa ya nne
(1) Kumbuka kuwa haina kusoma sura baada ya alhamdu lakini inayo tahiyatu. Soma tahiyatu ya
mwisho wenye kujua ile tahiyatu ya zamani wataona tafauti kidogo. Zote zinafaa hii ni nyepesi
na ina dua ndani yake.
Sala ya Jamaa
(1) Unaposali na imamu nuilia kusali na jamaa na kuwa ni amri unaitekeleza.
(2) Usimpite imamu kwa chochote ikiwa kisomo au kitendo, usimtangulie wala usiwe nyuma
sana. Unaweza kujua spidi yake kutoka rakaa ya mwanzo. Ikiwa atasujudu na wewe hujamaliza
kusoma alhamdu basi ana spidi kubwa na wewe itabidi uongeze kidogo. Ikiwa wewe utamgonja
sana hajasujudu baada ya kumaliza alhamdu basi ana spidi ndogo na wewe itakubidi upunguze
spidi.
(3) Wewe utaanza kwa tawjihi na nia kisha utaanza rakaa ya mwanzo na kuendelea kama
unayesali peke yako.
(4) Usisome sura wala aya baada ya alhamdu mote. Msikilize imamu na uzingatie maana ya yote
unayomsikia khasa maana ya Qur-an.
(5) Mfuate imamu vitendo vyote. Usisome samiallahu wewe soma rabbanaa
mote.
(6) Ikiwa imamu ni msafiri akasali rakaa mbili katika sala ya rakaa nne basi wewe kamilisha nne
kama sala ya mtu peke yake. Ama ikiwa nyote ni wasafiri mutamaliza pamoja rakaa mbili
zinatosha.
(7) Ikiwa wewe ni msafiri unasali rakaa mbili katika sala ya rakaa nne ukamuwahi imamu
anayesali rakaa nne katika rakaa mbili za mwisho basi itakubidi usitowe salamu naye, uzisali
rakaa mbili za mwanzo za mtu peke yake ndio utowe salam, utakuwa na wewe umesali nne.
(8) Si makosa kutamka nia kabla ya kuhirimia. Matamko ya nia ni:-
(i) Ya adhuhuri:-
(ii) Ya laasiri:-
(iii) Ya isha
(iv) Ya magharibi:-
(v) Ya alfajiri
This document was created with Win2PDF available at http://www.daneprairie.com.
The unregistered version of Win2PDF is for evaluation or non-commercial use only.