0% found this document useful (0 votes)
347 views66 pages

Nipo Single

Uploaded by

Janeth Mpemba
Copyright
© © All Rights Reserved
We take content rights seriously. If you suspect this is your content, claim it here.
Available Formats
Download as PDF, TXT or read online on Scribd
0% found this document useful (0 votes)
347 views66 pages

Nipo Single

Uploaded by

Janeth Mpemba
Copyright
© © All Rights Reserved
We take content rights seriously. If you suspect this is your content, claim it here.
Available Formats
Download as PDF, TXT or read online on Scribd

NIPO

SINGLE
YALIYOMO
YALIYOMO …………………………………….……..……..…….3
TABARUKU……………………………….. ……………………4
LENGO LA KITABU…………………………………..….……5
UTANGULIZI WA USEJA(SINGLE) NI NINI ?.......…6
VITU MUHIMU VYA KUFANYA.……..…………………13
MAENEO YA KUWEKEZA ………….……………..……..20
MAJIRA YA BWANA……..…………….….…………..….. 25
NINI UFANYE UKIWA MSEJA(SINGLE)…..………..31
JINSI YA KUPINGA VISHAWISHI………………………35
UMUHIMU WA AMANI YA KRISTO…………………49
KUHUSU MWANDISHI……………………………………66
TABARUKU

NI SHAUKU YA MOYO WANGU KUKISAIDIA KIZAZI


CHANGU KWA HABARI YA UFALME WA MUNGU NA
KUWEKA NJAA NA KIU YA KUMJUA MUNGU PIA
KUINUA WATU WALIO TAYARI KWA AJILI YA
MUNGU AMBAO HAWAJAJIKINAI YAANI ASKARI
WAAMINIFU HIVYO NI MATUMAINI YANGU KUPITIA
MAARIFA HAYA KUNA JESHI KUBWA LITAINUKA NA
KUFANYA KANISA KUTAWALA NA KUMILIKI KATIKA
TAIFA NA MATAIFA KUPITIA VITABU HIVI VYA KI-
ELECTRONIKI AMBAVYO NI BURE KABISA KWA KILA
ATAKAYE.

TANZANIA, WEWE NI JIKO LA KUPIKIA MAISHA


HALISI YA WOKOVU.
Lengo la kitabu hiki ni

Lengo la Kitabu hiki ni kumsaidia kijana au mtu


yeyote anayepitia hali ya useja (Single) aweze
kujisimamia bila kuangalia upepo wa mazingira
ulivyo pia kukisaidia kizazi kinachokua na kuingia
kwenye kupevuka kujua namna ya kujitunza kwenye
majira haya Ili wasiingie mahusiano yatakayoleta
machozi kwao.
SURA YA KWANZA
UTANGULIZI
Kwenye Jamii yetu imetoa na imetupa mtazamo
kwamba kuwa Mseja (Single) ni tatizo hivyo
imepelekea vijana wengi kuwa na haraka na
mahusiano na hivyo kujipelekea maeneo ambayo
yamesababisha na kuacha maumivu makubwa
mioyoni mwao lakini kama wangeona useja ni
majira au msimu wa kiungu Kabisa basi wasifanya
mambo ya haraka na ya kuyaharibu maisha yao.

Kuna baadhi wanajaribu kuingia kwenye mahusiano


wakati hawako tayari hii yote ni kutokana na jamii
kuweka presha kwa Watu hasa vijana na siku hizi
hata vijana wa sekondari na shule ya Msingi
wamekua wahanga/watumwa wa yale
yanayotamkwa na jamii na yale wanayoyaona,
mfano jamii inasema ukiwa mkaka bila kuwa na
mahusiano basi wewe ni domo zege, au wewe ni
zoba pia jamii imetoa Nyimbo Mbalimbali
zinazoamasisha mahusiano ya kingono tena hata
Kabla ya Ndoa mfano utasikia unanitaka basi
nitongoze Nyimbo kama hii inahusisha na
kuchochea mahusiano hasaa yale yanayohusisha
ngono hata kwa watoto wadogo na hii ni hatari
lakini pia hata tamthilia nyingi hasa zile za nje ya
nchi zinachochea mahusiano na zinampa Picha
Kijana mdogo kuwa na mahusiano wewe ni
mshamba unakuta vitoto vidogo vinapigana mabusu
na vinawachumba hivyo basi vijana wanahamasika
kuingia kwenye mahusiano na hii imepelekea vijana
wengi walioingia au wanaotaka kuingia kwenye
mahusiano kuwa Watu ambao hawana maandalizi
ya kutosha ya kiukomavu yanayofaa Ili kuyamudu
mahusiano hivyo hupelekea mahusiano mengi
kuishia njiani na yakiwa yamejaa maumivu mengi
mnoo.

Useja(Single) sio jambo baya ni jambo la kutulia na


kujifunza maana ni bora uwe Mseja(Single) kuliko
kuingia kwenye mahusiano yenye maumivu makali.
Useja ni kipindi/msimu ambao mwanadamu
anapitia Kabla ya msimu wa mahusiano
yanayoelekea Ndoa.

Msimu au Majira ya useja (single) yanatofautiana


baina ya mtu na mtu kwa kadiri ya Mungu
apangavyo kutokana na Kusudi alilolibeba mtu
hivyo basi si vyema kumwambia mtu kuwa
amechelewa kuoa au kuolewa ijapokua kuna Watu
ni kweli wamechelewa lakini hii haimaanishi eti
umri fulani amechelewa kuoa au kuolewa.

Mfano Mzee kiwia alimuoa mbibi wa Miaka 60 tena


huyo Bibi alikua bado ni bikira Yaani hamjui
Mwanaume na Bwana akasema naye kuwa majira
yake ya kuolewa yamefika na akaolewa na bado
anatarajia kupata mtoto, vipi wewe Miaka 30 tu
unalazimisha kuishi na mwanamume au mwanamke
kwa sababu unaona umechelewa na kuna wengine
hadi wanabadilisha dini Yaani wanaacha wokovu Ili
wasiwe waseja tu ndio maana leo mahusiano na
Ndoa nyingi hazina amani na wengine wanaendelea
kwenye mahusiano waliyopo kwa sababu
wanaweza kutoa ngono kwa wenzi wao lakini zaidi
ya hapo hakuna upendo Yaani wakati wa ngono
wanalazimishana Kabisa usiponipa nakuacha Yaani
ni kama mnabakana tu kwa Sababu hukujua kuwa
haraka haraka haina baraka.

Useja ni wakati wa kujitafuta mpaka ujipate ni


wakati wakutambua wewe ni nani? Una Kusudi gani
la kuumbwa kwako? Je kama wewe ni mwanamke
unajua unaenda kumsaidia nini huyo mwanamume?
Lazima ufikie hapa katika Uwezo wa kujitathimini na
ukifikia hapa hauwezi kuoa au kuolewa na yeyote
yule kama wengi wanavyosema kuwa mi yeyote tu
yule akija yaani inamaanisha hujui unachokihitaji na
mtu wa namna hii ni lazima akosee mtu wa kuoa au
kuolewa naye.
Je, wewe hujaoa, lakini hupendi msimu wa
useja(Single) uliomo? Iwe hujawahi kuolewa hapo
awali, au wewe ni mseja hivi karibuni baada ya
kuvunjika, talaka, au kifo, unaweza kujifunza
madokezo ya kuwa mseja na kuipenda. Hapa kuna
vidokezo saba vya kutia moyo kwako.
Tumia vidokezo hivi ili upate kuridhika zaidi katika
useja wako, haijalishi majira haya ya useja
yanachukua muda gani.
Ona useja kuwa fursa badala ya kuwa mzigo.

Kwa wale ambao hawajaoa au kuolewa na wajane


nasema kwamba ni heri wakae kama mimi nilivyo.
— 1 Wakorintho 7:8

Vidokezo 7 vya Kusitawi Katika Biblia inathibitisha


useja na ndoa pia. Lakini inasema kwamba ndoa
ni ngumu zaidi kuliko kuwa mseja.

useja hukupa fursa ambazo ndoa haina.


Unapokuwa huna furaha katika useja wako, ni
rahisi kuyaona majira ya useja kuwa kama mzigo.
Hata hivyo, unaweza kukumbatia uhuru wa kuwa
na maamuzi yako mwenyewe kuhusu mambo ya
kufanya na maisha yako ukiwa mseja. Ukiwa mtu
mzima anayewajibika, huhitaji kushauriana na
mtu mwingine yeyote kabla ya kufanya maamuzi.
Unapochagua kutazama useja kwa njia hii, macho
yako yatafunguliwa kwa fursa nyingi zilizo mbele
yako.

Omba ili Mungu akusaidie kuona fursa za useja


badala ya kukazia fikira kuwa mzigo. Atakuinua ili
upate pumziko ndani yake (Mt. 11:28-30).

Kuwa single Sio dhambi au laana bali ni majira


ambayo MUNGU amemuwekea mtu wake apitie
ambayo yanasimama kama majira ya maandalizi
kwa ajili ya familia yake atakayoianzisha.

Ni vyema kujua kutokana na biblia mbali na maneno


ya watu wa mitaani ambao wanasema single ni
laana, Kuwa single ni mikosi na Kukosa baraka hivyo
unatakiwa ujue kuwa hakuna mtu atakayebaki
single maisha yake yote kwa sababu neno linasema
Isaya 34:16
[16]Tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome;
hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo,
hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa
maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake
imewakusanya.

Na hilo andiko linasema ni jukumu la Roho wa


MUNGU kuwakusanya watu au watakaooana
SURA YA PILI
VITU MUHIMU VYA KUFANYA UNAPOPEVUKA NA
KUINGIA KWENYE MAJIRA YA USEJA.
1 Wathesolonike 4:4
[4]Kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake
katika utakatifu na heshima;

Ni Kazi Yako kuhakikisha unajitunza na kuuweza


mwili wako kwa Utakatifu na usafi, vifuatavyo ni
vitu vitajavyokusaidia kujitunza na kutoingia katika
mahusiano ya hovyo hovyo yanayohusisha ngono.

✓ Hakikisha unakua na Maisha ya Maombi.


Maombi sio tu kupeleka hoja bali hutumika kwa ajili
ya kujijenga nafsi zetu Ili tuwe Watu bora na
tunaoweza kuitawala miili yetu.
Luka 22:40,46
[40]Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni
kwamba msiingie majaribuni.
[46]Akawaambia, Mbona mmelala usingizi?
Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni.
Kusalitiwa na Kukamatwa kwa Yesu

Mathayo 26:40
[40]Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala,
akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha
pamoja nami hata saa moja?

Yesu anawauliza mmeshindwa kukesha nami walau


lisaa limoja akimaanisha mtu mvivu walau aombe
lisaa limoja.

Mathayo 26:41
[41]Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni;
roho I radhi, lakini mwili ni dhaifu.
Kwa hiyo Maombi yanasaidia kukupa Uwezo wa
kuutiisha mwili hasa pale unapoomba juu ya lisaa
limoja hivyo chini ya lisaa limoja mwili utakusumbua
hivyo omba bila kukoma.

✓ Jaa Neno.
Unataka uishinde tamaa ya mwili ni lazima ujae
Neno kwa sababu neno linakukamilisha kuwa mtu
kamili na linakupa njia sahihi ya kushinda tamaa za
useja.

Zaburi 119:105
[105]Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga
wa njia yangu.

2 Timotheo 3:16-17
[16]Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa
mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao,
na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika
haki;
[17]Ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa
apate kutenda kila tendo jema.

Wakolosai 3:16
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika
hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa
zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku
mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

Jaa Neno kwa kulisoma Neno au vitabu vya


watumishi wa Mungu Mbalimbali.

✓ Hakikisha unajaa Roho Mtakatifu kwa


uendelevu na kunena kwa lugha.
Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni siku moja lakini ujazo
ni suala endelevu hivyo basi hakikisha umejaa Roho
Mtakatifu kila iitwapo leo
Matendo ya mitume 1:8
[8]Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu
yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi
wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote,
na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Kwa hiyo kila unaponena kwa lugha unapokea


Nguvu Zaidi ya kushinda Dhambi na kila tamaa za
duniani kitabu cha yuda anatuonesha vizuri kuwa
kila tunapojaa Roho Mtakatifu na Nguvu zake basi
tunaongezeka zaidi katika roho zetu.

Yuda 1:20
[20]Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu
iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho
Mtakatifu,

Mitume wenyewe hawakuishia siku Moja tu kujaa


bali ilikua endelevu.
Matendo ya mitume 2:4
[4]Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza
kusema kwa lugha nyingine, kama Roho
alivyowajalia kutamka.

Matendo ya mitume 4:31


[31]Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali
pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa
Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa
ujasiri. Waumini Washiriki Mali zao pamoja

✓ Hakikisha unatafuta maarifa kwa juhudi kubwa.


Mimi nimesoma vitabu zaidi ya 500 kwa sababu
nilitamani kuwa bora maana unapokua bora utakua
na uwezo wa kupita kwenye kipindi cha useja
salama.

Mithali 19:2
[2]Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa; Naye
afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi.

Mithali 12:1
[1]Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali
yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama.

Mithali 8:10,15-16
[10]Pokea mafundisho yangu, wala si fedha, Na
maarifa kuliko dhahabu safi.
[15]Kwa msaada wangu wafalme humiliki, Na
wakuu wanahukumu haki.
[16]Kwa msaada wangu wakuu hutawala, Na
waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia.

Vitu hivi vitakusaidia kuwa bora katika majira ya


useja
SURA YA TATU
MAENEO YA KUWEKEZA KABLA YA MAHUSIANO.
01.Wekeza mda wako kwa MUNGU.
Mungu hawezi kukusaliti, kuna mtu anamsaliti
Mungu Ili ampate mwanaume au mwanamke Aisee
huyu mtu atakusaliti tu hivyo wekeza muda wako
kwa MUNGU.
Ukiwa karibu sana na Mungu itafanya mwenzi wako
aje kwa haraka maana Mungu atamvuta mtu sahihi
kwa wakati sahihi kwako.
Ukiwekeza kwa Mungu inakua rahisi kwa mtu
ambaye amekusudiwa na Mungu kwa ajili Yako
kukupata kiurahisi, yaani ukiwekeza kwa Mungu
utampata aliyewekeza na Mungu, kaa vikao na
Mungu nawe utazidishiwa

Mathayo 6:33
[33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki
yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Mahusiano ni mazidisho yaani hata kama mtu yupo
na mahusiano na mtu mwingine kama Mungu
amepanga umuoe au uolewe nae basi hayo
yatavunjwa na Mungu mwenyewe na atakuja
kwako.
Wekeza kumjua MUNGU, soma vitabu vya kuhusu
kumjua MUNGU, sikiliza audio zitakazokufanya uwe
karibu na Mungu ukiwa karibu naye utapata mtu
sahihi kwa ajili ya maisha Yako.
Nenda kwenye mikesha, nenda kwenye kwenye
Ibada za Maombi.

2.Wekeza katika mahusiano ya kindugu usiwe na


mtazamo wa kimahusiano ya kimapenzi tu.
Kuna wakaka au Wadada wakiona mtu kawa karibu
naye tu anachokiwaza ni kuwa ninaweza kuwa na
mahusiano naye au ananipenda nini hebu hama
huku na kuwa na marafiki wa kawaida bila kuwaza
mapenzi, marafiki kanisani, marafiki kazini na hata
darasani usiwaze mapenzi tu.
3.Wekeza kwenye ujuzi wa Fedha.
Fedha haina likizo ndugu yangu utaihitaji kila
iitwapo leo, hivyo wekeza kwenye maarifa kuhusu
fedha na upatikanaji wake.
Mapenzi hayaleti fedha hivyo basi anza kufanya
Kazi, tafuta fedha, hivyo wekeza kwenye maarifa
kuhusu fedha, soma vitabu kama RICH DAD POOR
DAD, MILLIONAIRE MINDSETS, na MONEY
FORMULA cha joel nanauka na vitabu vinginevyo
vinavyohusu uchumi.

4.Wekeza katika kufahamiana na watu tofauti na


maeneo tofauti.
Kwanini uwekeze kwenye kufahamiana na watu
kwa sababu itapanua ufahamu wako.
Watu hao wanaokuzunguka asilimia wanaamua
uolewe na mtu wa namna gani hivyo jitahidi
usipoteze kuhusiana na watu fulani fulani.

05.Wekeza katika vitu unavyovipenda na ujuzi wa


maisha.
Wekeza kwenye kujua kupika na kadhalika kuna
siku ROHO MTAKATIFU alinipa neno la maarifa
kuwa kuna binti yupo form six na hajui kupika hivyo
akajifunze kupika baada ya Ibada akaja mtu
akasema neno Hili ni langu kabisa mimi sijui kupika
na Huwa naogopa kwenda kwa ndugu kwa sababu
sijui kupika na akaniahidi akienda likizo atajifunza
kupika.

06.Wekeza kwenye Kusudi uliloumbiwa.


Wekeza hapa maana ndoa sio kila kitu bali Kusudi
ndio kila kitu sikia ndoa ni kwa ajili ya Kusudi.
Tafuta na uwekeze kwenye eneo la Kusudi lako
soma vitabu kuhusu Kusudi la aina hiyo na
kadhalika.

07.Wekeza kwako mwenyewe.


Jiendeleze mwenyewe katika maisha yako, jifunze
vitu Mbalimbali, soma kozi fupi fupi mfano mimi
nimesoma kozi fupi fupi zote zinazotolewa
mtandaoni na USA, soma kozi za bure za
mtandaoni, unakuta binti au mkaka hana cha ziada
zaidi ya kuwaza ngono na ndoa tu ndio maana
hakuna wanaoendelea, soma vitabu vya mahusiano,
soma vitabu vya uchumi, soma vitabu vya familia na
kadhalika.

Ukiwekeza kwenye haya mambo na ukawa


unatumia muda wako mwingi kwenye haya maeneo
basi utakua bora hii ndio inaongeza Uwezo wako wa
kufikiri na kiakili, leo hii unakuta binti hana cha
kufanya anawaza mapenzi tu na hela ndo wengine
wanapost Picha za uchi.

Mithali 11:22
[22]Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe,
Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili.
SURA YA NNE
MAJIRA YA BWANA NI MIAKA MINGAPI?
Kibiblia hakuna miaka kamili iliyotajwa moja kwa
moja ya majira ya Bwana ya kuingia kwenye
mahusiano yanayoelekea kwenye ndoa ila biblia
inatuonesha dalili au ishara inayomfanya mtu aingie
huko na dalili yenyewe ukomavu.

Ukomavu ni dalili ya kujua majira ya Bwana ya


kuingia kwenye mahusiano yanayoelekea ndoa
ambapo yatakua Mapenzi yataona vema yenyewe,
ila ukomavu ni Zaidi ya watu wanavyoona kwa
kawaida kwa sababu ukomavu umegawanyika
makundi makuu matatu nayo ni

UKOMAVU WA KIMWILI.
Huu ni ukomavu ulio katika maumbile ya jinsia
fulani ambayo yanaonesha tayari Upo tayari kwa
ajili ya familia na Ndoa.
1 wakorintho 7:25
Kwa habari za wanawali sina amri ya Bwana, lakini
natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za
Bwana kuwa mwaminifu.

Hilo andiko linatuonesha kwa habari ya


mwanamwali na Maana halisi ya hili neno toka
kwenye kamusi ni

1. Msichana aliyekwisha kubalehe lakini bado


hajaolewa.
2. Msichana ambaye bado hajapoteza ubikira
wake

Kutoka kwenye maana hizo tunaona kuwa


mwanamwali ni mtu aliyefikisha umri wa kupevuka
lakini bado hajaolewa, hii inatuonesha kuwa
inampasa kwanza awe amekomaa kama ishara
kuwa anastahili kuolewa
UKOMAVU WA KIROHO
Huu ni aina ya ukomavu unaotuhakikishia kutembea
SawaSawa na Neno la Mungu mfano Neno la
Mungu linasema usiibe na usizini yaani mtu
aliyekomaa kiroho pamoja na hisia zake kuwa ni
kubwa lakini sharti awe anaweza kuishi Sawasawa
na Neno la Mungu pasipo kuyumba wala kusita sita

Mfano yusufu alisha komaa kiroho hivyo Ilimfanya


aweze kuwaza kumuacha kwa siri lakini malaika
wakamtokea kwenye ndoto na kumwambia kuwa
asimuache huyo Maria hii inaonesha kuwa
amekomaa kiroho

Mathayo 1:19
Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa
haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa
siri.
Mfano mwingine ni yusufu pale ambapo amepewa
fursa ya kulala na mke wa potifa lakini yeye
anagoma wakati angeweza kumkubalia na kulala
naye bila hata potifa kufahamu lakini yusufu
alisimama na Mungu wake na kukataa kulala nae na
kupelekea kufungwa gerezani Ili mradi tu asimtende
Mungu dhambi

Mwanzo 39:9
Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala
hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa
wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa
nikamkose Mungu?

UKOMAVU WA KIAKILI
Ukomavu wa kiakili umegawanyika katika aina kuu
tatu nazo ni Uwezo wa kutatua mambo,Uwezo wa
kusimamia jambo au mambo uliyoyakubali, Uwezo
wako wa kiuchumi.
✓Uwezo wa kutatua mambo
Mtu yeyote yule ni lazima awe na Uwezo wa
kutatua mambo na sio tu kutatua bali inabidi awe
jawabu kwa mambo yanayokuja mbeleni ni hatari
kukuta haswa Mwanamume hana jawabu kwa vitu
vinavyowakumba, mtu akikosa hii atapata wakati
mgumu Sana.

✓Uwezo wa kusimamia jambo ulilolikubali.


Watu wengi hupata tabu Katika hili eneo na kama
mtu hawezi kusimamia anachokiamini ujue hawezi
kulinda anachokipenda yaani inabidi uwe na
maamuzi na uyasimamie usiwe mtu wa
kuendeshwa ndo utasikia mama kaniambia nisioe
waluguru au wachaga au nisioe aliyenizidi umri au
utasikia rafiki yangu ameniambia hunifai yaani
vituko ni vingi sasa mtu ambaye kila maamuzi
mpaka aulize mtu huyo bado hajakomaa, Mtu wa
hivi je anaweza kukutetea kwa wazazi na Ndugu
zake pale watakaposema hatumtaki huyo
✓ Uwezo wa kiuchumi
Hasa mwanaume ni lazima awe nao Ili kufanya
mahusiano yawe na nguvu, bila fedha mahusiano
magumu ijapokua mahusiano sio fedha ila fedha ni
muhimu sana
SURA YA TANO
NINI UFANYE UKIWA SINGLE NA UNASUBIRI
MWENZI WAKO.

✓Weka Mkazo kwanza kwenye ukuaji wa Maisha


yako Binafsi.
1 wakorintho 7:32,34-35
[32]Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye
asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana,
ampendezeje Bwana;
[34]Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali.
Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya
Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini
yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya
dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
[35]Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee
tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate
kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo
mengine.
Mtume Paulo anakazia kuwa haujaolewa usiwe na
haraka Wewe mpendeze Bwana Yesu tu na
mtumikie Mungu na hakikisha mahusiano yako na
Bwana yanakua sawa sawa yaani ndio Muda wa
kusoma vitabu vingi, kuwa na mikesha yako binafsi
na kadhalika.

✓Usiwaze kuingia mahusiano na mtu Ambaye


hajaokoka kwa Sababu ni chukizo mbele za
MUNGU.

2 Wakorintho 6:14
[14]Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa
jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani
kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya
nuru na giza?

Ni lazima utambue uliyeokoka sio sawa kuwa mtu


na ambaye hajaokoka na Mungu hataki kabisa
✓Weka mipango endelevu ya kujitunza.
1 Wakorintho 6:16,18-20
[16]Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba
ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili
watakuwa mwili mmoja.
[18Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo
mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye
zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake
mwenyewe.
[19]Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la
Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na
Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
[20]Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi,
mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

✓Tazama tabia za kiungu zaidi kwa mtu.


Wagalatia 5:19-21
[19]Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya,
uasherati, uchafu, ufisadi,
[20Ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu,
hasira, fitina, faraka, uzushi,
[21]Husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana
na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama
nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu
watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme
wa Mungu.

Tafuta tabia za kiungu ambazo ni tunda la Roho


Mtakatifu.
Wagalatia 5:22-23
[22]Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani,
uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
[23]Upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna
sheria.

✓Kuwa mtu mwenye Hekima na wala sio ukiroho


uliokosa Hekima ya Mungu.
SURA YA SITA
JINSI YA KUPINGA VISHAWISHI
“Wakati mwingine wasichana huniomba namba ya
simu na kutaka tuwe wapenzi. Mimi hukataa na
kuondoka. Lakini akilini, mimi huendelea kujiuliza,
‘Ingekuwaje kama ningempa namba yangu?’ Kwa
kweli, baadhi ya wasichana hao ni warembo sana.
Ni rahisi kujiambia, ‘Afadhali ningekubali.’”—Kijana
Carlos mwenye miaka 16 akielezea kishawishi
chake.

Je, wewe hukabiliana na vishawishi kama Carlos?


Ikiwa ndivyo, unaweza kushinda vita hivyo.

UNACHOPASWA KUJUA
Mtu yeyote anaweza kushawishiwa—hata watu
wazima. Kuna vishawishi vya aina mbalimbali.
Mtume Paulo hakuwa kijana alipoandika: “Kwa
kweli naipenda sheria ya Mungu . . . , lakini mimi
naona ndani ya viungo vyangu sheria nyingine
ikipigana na sheria ya akili yangu na kunichukua
mateka kwa sheria ya dhambi.” (Waroma 7:22, 23)
Licha ya mkazo huo, Paulo hakushawishika, nawe
pia unaweza kubaki imara! Usikubali kuwa mtumwa
wa tamaa zako. (1 Wakorintho 9:27) Kujifunza
kushinda vishawishi unapokuwa kijana kutakusaidia
uepuke mahangaiko sasa, na utakapokuwa mtu
mzima utahitaji sana ustadi wa kupinga vishawishi.

Vyombo vya habari huchochea vishawishi. Biblia


inataja “tamaa zinazotukia ujanani,” ambazo zina
nguvu kwelikweli.

(2 Timotheo 2:22) Lakini sinema, televisheni, muziki,


na vitabu kwa ajili ya vijana mara nyingi huchochea
tamaa hizo kwa kuonyesha kwamba ni jambo la
kawaida kukubali kushawishiwa. Kwa mfano, watu
wawili katika sinema ‘wanapopendana,’ ni kawaida
kwao kufanya ngono. Hata hivyo, Biblia inaonyesha
kwamba katika maisha halisi wanaume na
wanawake wana uwezo wa kuendelea “kujiepusha
na tamaa za kimwili.” (1 Petro 2:11) Hilo
linamaanisha kwamba unaweza kupinga vishawishi.
Inawezekanaje?

UNACHOWEZA KUFANYA
Tambua udhaifu wako. Usipoziba ufa, utajenga
ukuta. Vivyo hivyo, azimio lako la kutenda mema
huenda likavunjwa na udhaifu wako. Ni mambo gani
ambayo unahitaji kuzingatia?—Kanuni ya Biblia:
Yakobo 1:14
[14]Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake
mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

Wazia vishawishi utakavyokabili. Wazia hali ambazo


huenda zikaleta vishawishi. Jitayarishe kiakili jinsi
utakavyopinga vishawishi hivyo vitakapotokea.—
Kanuni ya Biblia:
Mithali 22:3
[3]Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha;
Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.

Uwe na msimamo thabiti. Biblia inasema kwamba


Yusufu aliposhawishiwa afanye ngono alisema:
“Ninawezaje kufanya ubaya huu mkubwa na kwa
kweli nimtendee Mungu dhambi?” (Mwanzo 39:9)
Neno “ninawezaje” linaonyesha kwamba Yosefu
alikuwa na msimamo thabiti kuhusu mema na
mabaya. Je, wewe una msimamo kama huo?

Tafuta marafiki watakaokusaidia. Unaweza kuepuka


vishawishi vingi ikiwa utachagua marafiki ambao
wana msimamo kama wako kuhusu maadili. Biblia
inasema: “Anayetembea na watu wenye hekima
atakuwa na hekima.”—Methali 13:20.

Epuka hali zinazochochea vishawishi. Kwa mfano:


Usijiruhusu kuwa peke yako na mtu wa jinsia
tofauti.

Epuka kutumia Intaneti wakati au mahali ambapo


utashawishiwa kutazama ponografia.

Epuka watu ambao tabia na maneno yao yanafanya


uovu uonekane kuwa jambo zuri.

Unaweza kujiwekea kanuni gani ili uepuke


vishawishi?—Kanuni ya Biblia: 2 Timotheo 2:22.

Mwombe Mungu akusaidie. Yesu aliwaambia


wanafunzi wake hivi: “Endeleeni . . . kusali sikuzote,
ili msiingie katika jaribu.” (Mathayo 26:41) Ukweli ni
kwamba Yehova Mungu anataka ushinde
vishawishi, na anaweza kukusaidia kufanya hivyo.
Biblia inasema: “Hatawaacha ninyi mjaribiwe kupita
mnavyoweza kuhimili, bali pamoja na hilo jaribu
ataifanya pia njia ya kutokea kusudi mweze
kulivumilia.”—1 Wakorintho 10:13.

UNAWEZA KUPINGA KISHAWISHI!


“Sikupanga kutazama ponografia. Lakini
nilipofungua Intaneti tangazo lilitokea. Nikaamua
kulifungua, hata sijui ni kwa nini.”—CODY. *

“Nilipokuwa kazini msichana mrembo alianza


kunitongoza. Siku moja aliniomba twende hotelini
‘tukajifurahishe.’ Nilijua alichotaka.”—DYLAN.

“N INAWEZA kupinga jambo lolote isipokuwa


kishawishi.” Maneno hayo yanafafanua vizuri jinsi
baadhi ya watu wanavyohisi kuhusu vishawishi, kwa
kweli moyoni wanavifurahia. Hata hivyo, wengine
wanaona kishawishi kama adui ambaye
wangependa kumshinda. Wewe unaonaje?
Unaposhawishiwa, unapaswa kukubali au kukataa?
Bila shaka, si vishawishi vyote vinavyosababisha
matatizo makubwa. Kwa mfano, kula biskuti moja
zaidi hakuwezi kuharibu afya yako. Lakini kukubali
vishawishi vingine—hasa vile ambavyo vinaongoza
kwenye ukosefu wa maadili katika ngono—
kunaweza kusababisha matokeo mabaya. Biblia
inaonya hivi: “Yeyote anayefanya uzinzi . . .
amepungukiwa moyoni; yule anayefanya hivyo
anaiangamiza nafsi yake mwenyewe.”—Methali
6:32, 33.

Ukishawishiwa kufanya uasherati, unapaswa


kutendaje? Biblia inajibu hivi: “Haya ndiyo mapenzi
ya Mungu, kwamba mtakaswe, kwamba mjiepushe
na uasherati; kwamba kila mmoja wenu ajue jinsi ya
kukiweza chombo chake mwenyewe katika utakaso
na heshima.” (1 Wathesalonike 4:3, 4) Unawezaje
kusitawisha ujasiri huo? Fikiria hatua tatu zifuatazo.

Hatua ya 1: LINDA MACHO YAKO


Kutazama picha zinazoamsha hamu ya ngono
kutachochea tu tamaa mbaya. Yesu alieleza
uhusiano kati ya kuona na kutamani aliposema hivi:
“Kila mtu ambaye anaendelea kumtazama
mwanamke na kumtamani tayari amefanya uzinzi
pamoja naye moyoni mwake.” Kisha akakazia hivi:
“Ikiwa, sasa, hilo jicho lako la kuume linakufanya
ukwazike, ling’oe ulitupilie mbali nawe.” (Mathayo
5:28, 29) Alimaanisha nini? Ili tupinge vishawishi
tunapaswa kuepuka kutazama picha zinazoamsha
hamu ya ngono.

Kijana akiwa kwenye duka la kuuza sinema anajizuia


kutazama picha chafu
Unapoona picha zinazoamsha hamu ya ngono
tazama kando

Kwa mfano: Wazia unaona mwanga wa kifaa cha


kuchomelea vyuma. Je, utaendelea kuutazama? La
hasha! Utaangalia kwingine au kuyakinga macho
yako ili yasiharibike. Vivyo hivyo, ukiona picha
inayoamsha hamu ya ngono—kwenye vitabu,
Intaneti, video, au mtu akiwa uchi—tazama kando
mara moja. Linda akili yako isichafuliwe. Juan
aliyezoea kutazama ponografia anasema:
“Ninapoona mwanamke mrembo, ninashawishiwa
kumtazama kwa mara ya pili na hata ya tatu. Hivyo
ninajilazimisha kutazama kando, na kujiambia: ‘Sali
kwa Yehova! Kwa kweli unahitaji kusali sasa hivi!’
Baada ya kusali, tamaa isiyofaa hupotea.”—
Mathayo 6:9, 13; 1 Wakorintho 10:13.

Fikiria maneno ya Ayubu, aliyesema hivi:


“Nimefanya agano pamoja na macho yangu. Basi
nawezaje kukaza fikira kwa bikira?” (Ayubu 31:1)
Kwa nini usiazimie kufanya hivyo pia?

Jaribu kufanya hivi: Ukiona picha inayoamsha hamu


ya ngono, tazama kando haraka. Iga mfano wa
mwandikaji wa Biblia aliyesali hivi: “Uyafanye
macho yangu yapite ili yasione jambo lisilofaa.”—
Zaburi 119:37.
Hatua ya 2: LINDA MAWAZO YAKO
Kwa sababu hatujakamilika, wakati mwingine
tunaweza kupambana na tamaa mbaya. Biblia
inasema hivi: “Kila mtu hujaribiwa kwa kuvutwa na
kushawishiwa na tamaa yake mwenyewe. Kisha
tamaa, wakati imetunga mimba, huzaa dhambi.”
(Yakobo 1:14, 15) Unawezaje kuepuka kunaswa na
hali hiyo?

Mwanamume kwenye duka la kuuza nguo


anapatwa na mawazo mabaya kisha anasali
Unapoanza kufikiria mambo yasiyofaa, acha mara
moja na usali

Unapokabili tamaa zisizofaa, kumbuka kwamba


unaweza kuamua jinsi ya kukabiliana na kishawishi
hicho. Unapaswa kupinga tamaa hizo mbaya. Ondoa
kabisa mawazo yasiyofaa akilini. Kataa kuendelea
kufikiria mawazo machafu. Mwanamume anayeitwa
Troy, aliyezoea kutazama ponografia kwenye
Intaneti anasema hivi: “Nilipambana ili kuondoa
mawazo yasiyofaa kwa kufikiria mambo yanayofaa.
Haikuwa rahisi. Wakati mwingine nilishindwa.
Hatimaye nilifanikiwa kudhibiti mawazo yangu.”
Mwanamke anayeitwa Elsa, aliyepambana na
kishawishi cha kufanya ngono alipokuwa tineja
anasema: “Kwa kuendelea kuwa na shughuli nyingi
na kusali kwa Yehova, nilifaulu kushinda mawazo
mabaya.”

Jaribu kufanya hivi: Unapoanza kufikiria mambo


yasiyofaa, acha mara moja na usali. Pambana na
mawazo mabaya kwa kujaza akili yako “mambo
yoyote yaliyo ya kweli, mambo yoyote yaliyo ya
hangaiko zito, mambo yoyote yaliyo ya uadilifu,
mambo yoyote yaliyo safi kiadili, mambo yoyote
yaliyo ya kupendeka, mambo yoyote yanayosemwa
vema, wema wa adili wowote ulioko na jambo
lolote la kustahili sifa.”—Wafilipi 4:8.
Hatua ya 3: LINDA HATUA ZAKO
Tamaa mbaya, kishawishi, na fursa zinapokutana, ni
rahisi kutumbukia kwenye dhambi. (Methali 7:6-23)
Unawezaje kuepuka hatari hiyo?

Mwanamume anatumia kompyuta yake mahali


penye watu nyumbani
“Ninatumia Intaneti wakati tu wengine
wanapokuwa nyumbani”

Biblia inatoa ushauri huu wenye busara: “Mtu


mwerevu ni yule ambaye ameona msiba na
kujificha, lakini wasio na uzoefu wameendelea
mbele nao lazima waumie.” (Methali 22:3) Kwa
hiyo, linda hatua zako. Jaribu kuwazia hali ambazo
zinaweza kukuletea matatizo na uziepuke. (Methali
7:25) Mwanamume anayeitwa Filipe, aliyefanikiwa
kushinda tabia ya kutazama ponografia anasema:
“Ninaweka kompyuta mahali ambapo mtu yeyote
anaweza kuiona na nimeweka programu ya kuchuja
taarifa zisizofaa kwenye Intaneti. Ninatumia Intaneti
wakati tu wengine wanapokuwa nyumbani.” Pia,
Troy aliyetajwa mapema anashauri hivi: “Ninaepuka
kutazama video zinazoamsha hamu ya ngono na
ninajitenga na watu wanaopenda mizaha michafu
kuhusu ngono. Sitaki kujihatarisha.”

Jaribu kufanya hivi: Kwa unyoofu changanua


udhaifu wako, kisha panga jinsi unavyoweza
kuepuka hali ambazo zinaweza kukuongoza kwenye
kishawishi.—Mathayo 6:13.

USIKATE TAMAA!
Utafanyaje ikiwa baada ya kujitahidi unatumbukia
tena kwenye vishawishi? Usikate tamaa na kuacha
kupambana. Biblia inasema hivi: “Huenda mwadilifu
akaanguka hata mara saba, naye hakika
atasimama.” (Methali 24:16) Kwa kweli, Baba yetu
wa mbinguni anataka ‘tusimame.’ Je, utakubali
msaada wake? Basi, usichoke kusali na kumwomba
msaada. Imarisha imani yako kwa kusoma Neno
lake. Imarisha azimio lako kwa kuhudhuria
mikutano yenye Nguvu za Mungu. Kumbuka ahadi
hii ya Mungu:
“Nitakutia nguvu. Nitakusaidia kwelikweli.”—Isaya
41:10.

Kijana mmoja anayeitwa Cody alisema maneno


haya:
“Nilipambana sana ili kushinda tabia ya kutazama
ponografia. Nilirudia kutazama mara kadhaa,
hatimaye kwa msaada wa Mungu nilifanikiwa
kuacha kabisa.” Dylan, ambaye pia alitajwa mapema
anasimulia hivi: “Ingekuwa rahisi kufanya ngono na
mfanyakazi mwenzangu. Hata hivyo, nilisimama
imara na kumwambia ‘Hapana!’ Inapendeza sana
kuwa na dhamiri safi. Jambo muhimu hata zaidi
ninajua kwamba nilimfurahisha YESU.”
Unaposimama imara na kupinga kishawishi, uwe na
hakika kwamba utamfurahisha Mungu!—Methali
27:11.
SURA YA SABA
UMUHIMU WA AMANI YA KRISTO KWENYE
MAAMUZI YA KUOA NA KUOLEWA.
Kuna Single (waseja) wa aina mbili moja ni wale
ambao majira yao ya useja ndo kwanza yanachangia
na wengine majira ya useja ndo yameisha au
yanaishia na wanasubiri mtu rasmi wa kuoa au
kuolewa naye hivyo ni muhimu kujifunza kuhusu
amani ya Moyo.
Wakolosai 3:15
Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo
mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa
shukrani.

Kuanzia mahusiano yenye malengo ya kufikia hatua


ya ndoa ni jambo la Busara na lenye kupendeza
machoni pa BWANA,pale tu muhusika atakapokuwa
na Utayari wa kumpa BWANA nafasi ya kuhusika
kwenye haya Majira ya huitaji wake.
Kwasababu msingi wa Ndoa upo Kwa BWANA,Ndio
mana sikila nafsi yafaa kujiunganisha nayo ,na kwa
kuwa MUNGU aliliona jambo hili akaona aweke
kiashiria ndani ya nafsi ya muhitaji kiitwacho”
AMANI YA KRISTO”
Akiwa na maana kitumike Kwa jicho la mizani ya
kupima ajae mbele yake ametoka kwake au la?

Amani ya Kristo ni kiashiria muhimu Sana


kinachotumiwa na Roho Mtakatifu kutujulisha
usahihi au kutokua Sahihi kwenye maamuzi Yetu ya
kukubaliana na au kukataa kuingia kwenye
mahusiano ya kuelekea Ndoa takatifu.

Mtume Paulo anawaambia kolosai ” Na Amani ya


Kristo iamue mioyoni mwenu”

Tupo kwenye nyakati ambazo ndoa nyingi Sana


walengwa Wanataka kuachana, wengine wamesha
tengana, lakini wapo ambao wanasubiri hati ya
talaka mahakamani, Katika vitu ambavyo
vinamshangaza hata MUNGU ni Kwamba ni kiashiria
gani awali kilikupelekea ufanye maamuzi ya kusema
Ndio Kwa kinywa na vitendo (yani kupiga hatua ya
kukiri mbele ya madhabahu Kuwa huyo ndiye) na
kiashiria gani muda huu kinakupigia kelele
kukwambia huyu si Mke au Mume wako?

Pindi namuuliza Roho Mtakatifu Kwanini jambo hili


Kwasababu Kuna mazingira ambayo Ufalme wa
Mungu unashindwa kukaa kwenye familia.

Kitu nilicho tambua ni hiki tulio wengi tumefanya


Maamuzi pasipo kujipima na kiashiria hiki cha
AMANI YA KRISTO.

Wapo waliotegemea marafiki, wazazi, wachungaji


wao Leo Hii wanapita mahali pa gumu sana.
Sasa Sina maana ya kudharau watu wa karibu Yako
lahasha!

Anachokihitaji Roho Mtakatifu kutukumbusha leo

Usifanye maamuzi kijana kuoa Binti au Binti


kuolewa na kijana kwasababu marafiki,
familia,Mchungaji Wana Amani nae.

Isipokuwa rudini magotini pa BWANA tafuteni


kiashiria hiki cha AMANI YA KRISTO ndani ya nafsi
zetu ambako Roho Mtakatifu yupo kuwaonesha
matokeo yajayo mwishoni mwanzoni mwake
kufuatana na kile kinachofuniliwa ndani ya nafsi
zenu.

Ndoa ni sekta yenye usimamizi wa Kiagano,Kwa


misingi hiyo tafuta kujua Bwana wa hilo Agano, na
nini anasema nawe Kwa habari ya huyo aliye kuja
kukuchumbia au unayetaka kumchumbia.
Tuna ambiwa Amani ya Kristo iamue mioyoni
mwenu. Kwa hiyo Kuna nguvu ya maamuzi ya
Kiungu imefichwa ndani ya Amani ya Kristo ambayo
imebeba uthibitisho wa mtu kama katoka Kwa
Bwana Sawa Sawa na Mithali 18:22 au la Kitendo
Cha kumuuliza rafiki, ndugu, familia eti
mnamuonaje huyu Binti au kijana anafaa kuwa
shemeji au wifi yenu haitoshi kwasababu wao
hawajui kusudi la Mungu kwenye Maisha Yako ya
ndoa na hawawezi kukujulisha mambo yajayo
mwishoni mwanzoni mwake. Isipo Roho Mtakatifu
pekeake kupitia Neno linalotoka kinywani mwa
BWANA. Ndio mana alisema atatupasha habari Kwa
kila alionalo Ni maombi yangu Kwa Mungu sana
kwamba nafsi zote zenye kiu ya kuingia kwenye
ndoa zipate utulivu binafsi nafsini ambao
utawasaidia kutafuta Uso wa BWANA hadi
wahakikishe utu wao wa andani Kuna Amani ya
Kristo mana katika hiyo Amani Yapo maamuzi
sahihi.
Usikubali mtu tu akuunganishie kwasababu ya umri
acha njia za kupata mume au mke Kwa michongo,
mwambie BWANA atoe yeye hana kona wala
hafanyi madili Bali anasimama kwenye kusudi lake
na uthibitisho wa Kila kitu ndani yako ameuficha
kwenye

Wakolosai 3:15, AMANI YA KRISTO.

Unaweza jiuliza kwanini Amani ya kristo ifanye


maamuzi ndani yako Wakati wewe umesubiri miaka
mingi uitwe mke au Mume wa mtu? Kwani
ukiendelea na michakato Kuna shida gani?

Sikia Neno la BWANA, yafaa ni kwako kuwa na


furaha masaa 12 na kupitia uchungu wa Maisha?
Kufuatana na maandiko yanatuambia Amani ya
Kristo inapofanya maamuzi ndani yako na ndani ya
mwenzi Kuna uwepo wa umoja wa roho lakini pia
mioyo inajawa na shukrani Kwa BWANA, Ambacho
natamani Roho Mtakatifu akufunulie upate
kusaidika kungali mapema ni hiki.
Amani ya Kristo huwa ni endelevu ndani ya nafsi za
wahusika au inaondoka mara baada ya kutangaza
uchumba au kuingia kwenye Agano la ndoa?
Mioyo ya shukrani Kwa BWANA huwa inapotekeaga
wapi baaada ya Ndoa?

Haya ni maswali muhimu Sana Kwasababu wapo


Watu wanakwambia awali walikua na Amani ila
baada ya kutangaza uchumba au kufunga Ndoa tu
Amani imepotea.

Yohana 14:27
Amani nawaachieni; amani yangu nawapa;
niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo.
Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.

Kufuatana na Yohana 14:27 tunaona namna


ambavyo Amani ya Kristo inapo achiliwa ndani ya
Mtu ,hufanya matuo milele ndani ya nafsi,na uwepo
wa hiyo Amani kunaondoa fadhaa mioyoni. Kwa
misingi hiyo lazima turudi kutafuta ni nani aliyekupa
Amani ya kitambo Kwa habari ya huyo binti au
kijana alafu ikaondolewa Baada ya Siku, wiki,
miezi,ya uchumba kutangazwa , au Baada ya
kufunga ndoa mkachukiana ghafla. Mana Amani
atupayo BWANA haina ubabaishaji kabisa. Na Ndio
mana watumishi huwa wanauliza watu nafsini ipo
Amani juu ya jambo unalolifanyia maamuzi au ni
shinikizo la mtu ?

Sasa hapo ndipo watu wanapo lazimisha kutoa


Majibu yaliyo Kosa uhalisia, kwasababu nafsi huwa
zinapiga kelele ya kukataa Kwa baadhi yetu, lakini
vinywa vyetu Kwa jinsi ya Mwili vinajitia moyo Kwa
Bwana,na kutamka Pepo shindwa alafu unajibu
Mtumishi ninayo Amani ,ila Roho Mtakatifu ndani
anasema nawe kwamba Amani ya Kristo juu ya
huyo kijana,Binti haipoo. Haitoshi anakuinuliwa na
watu wanakwambia” Kaa magotini pa BWANA
usikimbilie hili jambo ” lakini huelewi, Na vijana na
Mabinti wengi kipigo kilianzia hapo kutaka
kutembea Kwa mihemko yetu badala ya kutembea
pamoja na BWANA, kwasababu tumewekwa wazi
“Hatua zetu zitaongozwa na BWANA”

Sasa kwanini mambo haya yanatokea na kufika


mahali pasipo stahili?

Isaya 6:9-10
Naye akaniambia, Enenda, ukawaambie watu hawa,
Fulizeni kusikia, lakini msifahamu; fulizeni
kutazama, lakini msione.
Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito
masikio yao, ukayafumbe macho yao; wasije
wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio
yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na
kuponywa.

Kufuatana na Isaya 6:9-10 utagundua Kuna maeneo


muhimu sana ambayo yamefungwa Kwa watu
wengi na adui huwa anatumia Zaidi lango hili la
ndoa kuhakikisha anadaka nafsi za watu
waliobebeshwa Agano la Mungu kwenye Maisha
Yao.

Unaweza jiona upo sawa Lakini ukawa nashida Kwa


mtu wako wa ndani ambao ni muhimu sana kuwa
active nyakati zote,mana hapo ndipo kwenye kitovu
Cha makutano yako na Mungu.

Kwahiyo Roho Mtakatifu anaweza kukupigia kelele


juu ya maamuzi unayotakiwa kufanya lakini kama
huna ufahamu ndani ,huna jicho la kuona mambo
mwishoni mwanzoni mwake , lazima utapita
kwenye shida Kwasababu adui anakufunga Kwa
Majira pale anapo fanikiwa kukuingiza kwenye tukio
Ndio anafumbua macho, na kukupa ufahamu wa
kuona ulipo Sio Sahihi.

Kiu ya Roho Mtakatifu anahitaji kuongea nawe mtu


wa MUNGU, yamkini upo kwenye hatua ya
uchumba,au Kuna vijana au Mabinti Wanakuja
kudai kuingia kwenye mahusiano ya kuelekea Ndoa.

Rai kutoka kwa BWANA hebu kaa pata utulivu wa


kutafuta uso wa BWANA,na Katika vitu muhimu
ambavyo unatakiwa kujiombea wewe unaefuatwa
kuchumbiwa au unae enda kuchumbia ni Masikio
yako, Macho ya moyo na roho ya ufahamu.

Kwanini ni muhimu kujiombea Masikio?


Mwanzo 35:2-4
Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na
wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu
migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo
zenu.
Tuondoke, tupande kwenda Betheli, nami
nitamfanyia Mungu madhabahu huko; yeye
aliyenisikia siku ya shida yangu, akawa pamoja nami
katika njia yote niliyoiendea.
Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote
iliyokuwa mikononi mwao, na pete zilizokuwa
masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya
mwaloni ulioko Shekemu.

Kutoka 32:1-4
Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia
kushuka katika mlima, wakakusanyana
wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya!
Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu,
kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya
Misri hatujui yaliyompata.
Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu
zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu,
na binti zenu, mkaniletee
Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo
katika masikio yao, wakamletea Haruni.

Ambacho nataka uone uhusiano uliopo. Kati ya sikio


lako na Mungu au miungu kwamba Kuna mazingira
ambayo sikio linaweza Kuwa Chini ya mamlaka ya
miungu mingine usitarajie kumsikia MUNGU aliye
Katika Kristo, na Ndio mana Yakobo alijiongeza
akawaambia Watu wanyumbani mwake wampe
miungu mingine mana anataka kwenda kumwabudu
Mungu wake,tunaona Watu wakivua Pete za
masikioni(hereni) . Lakini Haruni naye anataka
kutengeneza miungu mingine anawaambia Watu
walete Pete za masikioni za wake na Binti zao,
inamana Kuna uhusiano mkubwa kati ya sikio lako
na Mungu au miungu.
Kumbuka eneo la mahusiano lina hitaji usikivu zaidi
kutoka utu wako wa ndani kuliko Chochote
kwasababu utu wako wa ndani Ndio unaopokea
connection ya mtu sahihi au kinyume chake na
kukusikilizisha.

Kwanini uombee Macho Yako?


Waefeso 1:18
Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la
mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa
urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;

Kwa hiyo Kuna umuhimu wa wewe unayetarajia


kuchumbia au kuchumbiwa Macho Yako ya ndani
uhakikishe yanaona sawa sawa,yana toa Nuru
inayokujulisha Tumaini la mwito wa Ndoa
unayotaka kuingia jinsi ulivyo.

mwanzo 2: 21-23
Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito,
naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja,
akafunika nyama mahali pake,
Na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana
Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa
Adamu.
Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa
yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa
mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika
mwanamume.

Ukisoma mstari wa 23 utagundua baada ya Macho


ya moyo wa Adamu kutoa uhakika wa kilicho onwa,
ndipo Adamu anasema ” Sasa huyu ni mfupa Katika
mifupa yangu,na nyama Katika nyama yangu” Hii
kauli ya Adamu inamana walikuwepo Mabinti
wengine lakini jicho halikuona ule mwito ndani ya
hao wengine, isipokuwa kwa Binti aliyetoka Kwa
BWANA.
Utaona namna ambavyo Kuna umuhimu wa
kuombea Macho ya moyo wako yaone yule
anayetoka Kwa BWANA.
Lakini pia upo umuhimu wa kumuomba Roho
Mtakatifu akupe Roho ya ufahamu , Kwasababu
kusikia na kuona pekeake hakutoshi lazima
ufahamu ulicho kisikia na kukiona Kwa usahihi wake
Ili ujue Nini unatakiwa kufanya kufuatana na hatua
za MUNGU.
Kitendo Cha wewe kufanya bidii kutafuta uso wa
BWANA ndivyo unavyo toa uhalali wa Roho
Mtakatifu kutumia kiashiria Cha AMANI YA KRISTO
ndani yako.
Sijui umepoteza watarajiwa wangapi na
imekuuumiza Kwa kiwango Gani? Ninacho sikia
kukwambia Rudi magotini kwanza jiombee binafsi
Kuna kitu Roho Mtakatifu atakufandisha na
kukuweka mahali pa zuri pa kukusaidia kutumia hiki
kiashiria Cha AMANI YA KRISTO kama silaha ya
kuzuia maumivu ya Mara Kwa Mara.
MUNGU akusaidie uwe na kiu ya kujiombea
KUHUSU MWANDISHI
Naitwa Paulo Evarist Koba nimeokoka na nampenda
sana YESU, Muhitimu wa ngazi ya astashahada pale
kwenye chuo cha ufundi cha DIT.
Niliokoka Mwaka 2014 nikiwa kidato cha tatu huko
shuleni nilipokua nasoma elimu ya sekondari, tangu
hapo Maisha yangu yamebadilika kabisa.
Ninaabudu kanisa la Gilgal Revival Church pia ni
mtoto wa kiroho wa mchungaji Paulo Israel Shaban.
Haya maarifa nimejifunza Kupitia kwa Baba yangu
wa kiroho Askofu Paul Israel Shaban.
Kama umeguswa na huduma hii na una ushuhuda
kuhusu hiki kitabu basi karibu kwa namba za hapo
chini pia unaweza kutoa sadaka Yako Ili kutoa sapoti
karibu kwa mawasiliano ya hapo chini pia kwa
ushauri na msaada wa kiroho karibu sana kupitia
Email ifuatayo paulokoba395@gmail.com na
mawasiliano ya 0783428460 au mitandao ya kijamii
nitafute kama Evarist Koba.
Vitabu vinginevyo vilivyoandikwa na mwandishi.
✓USICHOCHEE MAPENZI
✓KIJANA ALIYEOKOKA NDANI YA BABILONI
✓MAHALI PA SIRI PA MUNGU
✓UELEWE ULIMWENGU WA ROHO
✓USIMZIMISHE ROHO MTAKATIFU
✓SAFARI YA MTUMISHI WA MUNGU
✓RAFIKI YANGU ROHO MTAKATIFU
✓SIRI YA KUNENA KWA LUGHA
✓KUHUSU MALAIKA
✓SIRI YA MUZIKI
✓TUNDA LA ROHO
✓ROHO SABA ZA MUNGU
✓KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU
✓MIMI NI MWANAMKE

You might also like