You are on page 1of 12

Sauti ya Waislamu

Uvamizi na dhuluma za Israel katika mji mtakatifu wa Qudsi


Uk. 10

Katibu Mkuu Baraza Kuu Sheikh Sanze akamatwa


DPP azuiya Sheikh Ponda kupewa dhamana Wengine dhamana wazi, kutoka Novemba 5 Wadhamini watakiwa kuwasiliana na Wakili

ISSN 0856 - 3861 Na. 1043 Dhuul-Hijja 1434, IJUMAA NOVEMBA 1-7, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Watanzania sisi tutaponea wapi?

Mulugo kasoma Madrasa au Sunday School? Maaskofu KKKT waombe uchunguzi NECTA Kabla ya kuleta madai ya mateso ya Kanisa

Polisi wadaiwa kumtesa Mmemchukua yuhai mbeba mizigo Zanzibar mnamrejesha maiti?
MH. Philip Mulugo DKT. Joyce Ndalichako

KATIBU Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (Baraza Kuu), Sheikh Ramadhani Sanze.

Wamkata ngozi ya kichwa kwa kisu na kumnyoa Mwingine apigwa na Vespa yake kuvunjwa vunjwa Nusura mja mzito apate kipigo, kisa maandishi ukutani

Asema Baba wa kijana aliyeuliwa Polisi wakanusha kuhusika Uk. 12

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Habari
AN-NUUR

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA NOVEMBA 1-7 2012

AN-NUUR

Tusicheze ngoma yao


TOKA atekwe Sheikh Farid na toka akamatwe Sheikh Ponda Issa Ponda, ukisikiliza kauli za viongozi wa kisiasa, makamanda wa Polisi, viongozi wa makanisa na taarifa katika vyombo vya habari, utaona kuwa wote hao wameungana katika jambo moja: Kupiga propaganda kuwa nchi hii inakabiliwa na kitisho cha uharamia na ugaidi wa Kiislamu. Tumesikia jinsi ambavyo matukio ya kuharibiwa makanisa yanavyopigiwa zumari huku lile la kunajisiwa Quran mara mbili likionekana kana kwamba hakijatokea kitu au kama kilitokea, basi si ajabu wala hakuna kosa. Tukishajua kuwa hilo ndio lengo, busara inaelekeza kuwa tusifanye jambo lolote ambalo litawasaidia wanaopanga njama hizi. Kwa agenda yao hii, wanachotaka wao ni kuona makanisa yakiendelea kuchomwa, Waislamu kutoka mitaani kwa maandamano maana hiyo ndiyo itatoa fursa hata kutuma vijana wao wa kupanga wakachome makanisa ili wapate kuwasingizia Waislamu. Ukiwasikia wanatoa kauli za onyo, ni kama njia moja wapo ya kuwachochea Wa i s l a m u w a s e m e hatukubali. Wanawatumia pia Masheikh ambao wanajua ka kuwa hawana uso wa kusimama mbele ya Waislamu na kusema jambo wakasikilizwa. Mahesabu yao ni kuwa iwapo Masheikh hao wasiotambulika na u m m a w a Wa i s l a m u , watakataza jambo, kwa hoja yoyote ile, hata yenye mantiki, basi Waislamu na Wanaharakati watafanya kinyume chake. Kwa hiyo katika nafsi zao watakuwa wanafurahi sana wakisikia Waislamu wakihamasishana kuandamana kwa sababu watapata fursa ya kuwapiga mabomu, kuwadhalilisha wanawake wa Kiislamu, kuongeza idadi ya Waislamu rumande na kubwa zaidi kuhakikisha kuwa ghasia zinasambaa mitaani huku wakitumia vyombo vya habari kusambaza uwongo na propaganda kuwa Waislamu ni magaidi hatari wa Boko Haram. Ni jambo la kushukuru Mungu kwamba Masheikh Zanzibar, Waislamu na Wazanzibari kwa ujumla, wameigundua njama hii. Wametulizana Misikitini na majumbani mwao. Hata Mahakamani wanapanga idadi ya watu kwenda ili kuondoa wingi wa kuwapa sababu FFU. Kwa hakika busara hii ambayo inathibitisha ile kauli ya Qur an kuwa waumini ndio Ulil Albaab, yaani ndio wenye akili, ndiyo imeifanya Zanzibar mpaka sasa ipo katika salama. Na huenda ndiyo itakayoisalimisha ile hali ya maelewano baada ya kupitia katika kipindi kirefu cha tna, farka na uhasama. Katika jumla ya habari ambazo zilipewa kipaumbele na nafasi kubwa katika vyombo vya habari Tanzania, Afrika na dunia wiki hii, ni lile la kushambuliwa Kanisa kule Kaduna, Nigeria na kuuliwa watu saba. Kwa mujibu wa tarifa za vyombo vya habari ambavyo kama kawaida yao, walizipamba sana, ilidaiwa kuwa Muislamu mmoja alifanya shambulio la kujitoa muhanga akalipua Kanisa Katoliki huku waumini wa Kanisa hilo wakiwa ndani wakifanya ibada. Baadhi ya vyombo vya habari vilidai kuwa mtu huyo alindesha gari alilolijaza mabomu na kuja kuliegesha karibu na Kanisa hilo Katoliki na kulilipua. Hata hivyo kwa wanaofuatilia habari za Nigeria watakumbuka kwamba shambulio kama hilo lilidaiwa kufanyika Februari 21, 2012 nje ya Kanisa la Christ Embassy Church (CEC), Barabara ya Morocco, Suleja, Jimbo la Niger. Katika shambulio hilo ilidaiwa kuwa Waislamu Boko Haram walitega mabomu katika gari halafu wakaliegesha jirani na Kanisa hilo. Hata hivyo, haukupita muda uchunguzi wa kipolisi ukagundua kuwa gari hilo lilikuwa la mmoja wa waumini wa Kanisa hilo na ndiye aliyelipaki likiwa na milipuko akaondoka akiliacha likilipuka huku nyuma. Propaganda inayopigwa hivi sasa ni kuwa Wa i s l a m u w a n a p a n g a kulipua makanisa. Aidha, washaanza kuambiwa kuwa wana tawi la Boko Haram. Yakiwemo mazingira ya fujo na zogo litakalotokea FFU wakikabiliana na Waislamu wanaoandamana, inaweza kuwa fursa nzuri kwa wenye mipango hii miovu kulipua Makanisa na kuwasingizia Waislamu. Lakini katika hali ya utulivu, inaweza kuwa rahisi kuwaona na kuwaumbua wanaopanga kulipua makanisa yao kama walivyoumbuliwa wale waliolipua Kanisa la (CEC), Nigeria. Utulivu wa Waislamu Zanzibar umesababisha sasa laana wanayowarushia Masheikh wa Uamsho kuwarudia wao wenyewe. Ni vikosi vya SMZ sasa vinavyoonekana kubughudhi watu mitaani. Na uzuri wa mambo ni kuwa Wazanzibari wote wenye mapenzi na nchi yao wametambua kuwa vipigo vinavyotembezwa na vikosi hivyo, ni namna nyingine ya kuwachochea na kuwachokonoa wakasirike waamue kulipa kisasi. Wanazidi kuusiana na kumeza hasira na kuwa na subra. Itakuwa vyema kama Waislamu wa Tanzania Bara na hasa Dar es Salaam watakuwa na ujasiri huu wa kumeza hasira na kusubiri katika kipindi hiki kigumu.

MAONI YETU

Kukamata Masheikh sio dawa kuwadhibiti Waislamu


SASA hivi kuna zoezi linaendeshwa na vyombo vya dola la kuwakamata na kuwasweka ndani Masheikh na viongozi wa Waislamu jijini Dar es Salaam. Zoezi hili limekuwa likifanywa bila shaka kwa ajili ya kudhibiti harakati za Waislamu katika kupigania haki zao, ambazo pamoja na kuzieleza na kuzidai kwa wahusika kwa muda mrefu, lakini hakuna aliyejali wala kutaka kuwasikliliza. Maandamano na makongamano ni njia za kidemokarasia ambazo jamii y a Wa i s l a m u imeamua kuifuata katika kushinikiza wahusika kusikia kilio chao ambacho kimekosa wa kukisikiliza kwa muda mrefu. Njia hizi ndizo ambazo zimeleta hofu na propaganda chafu dhidi yao kiasi cha sasa kuwindwa na vyombo vya dola ili kudhibitiwa. Hata hivyo hatudhani kuwa suluhu ya kilio cha Waislamu hawa ni kuwadhibiti kwa

nguvu za dola. Kukamatwa Ponda, Sanze au kiongozi mwingine yeyote wa Kiislamu, hakuwezi kuwa suluhu ya matatizo. Bado Umma wa Kiislamu ambao ndio unaoathirika na kupuuzwa au kudharauliwa, utaendelea kupigania haki muda wa kuwa wanaamini kuwa hawatendewi haki. Ni vyema serikali ikatafakari kwa kina kabla ya kutumia nguvu kuzima matakwa ya Waislamu. Kuna haja ya serikali kutambua kwamba tatizo sio viongozi wa Waislamu, bali ni dhulma. Sisi tunaona kuwa jambo la ms ingi kufanyika ili kukia suluhu ya kudumu ni serikali kuacha dharau katika kusikiliza na kutatua shida za Waislamu pale zinapodhihirika kuwepo, hasa zile zinazoshabihiana na dhulma na ubaguzi. Tuache kuwakamata viongozi wao. Tuwasikilize badala ya kuwapuuzwa na kuwatisha.

Katibu Mkuu Baraza Kuu Sheikh Sanze akamatwa


Na Mwandishi wetu K AT I K A h a r a k a t i zinazoendelea za kuwakamata viongozi wa Waislamu nchini, Polisi wamemkamata Katibu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (Baraza Kuu), Sheikh Ramadhani Sanze. Sheikh Sanze alikamatwa juzi huko Mbande Mbagala akiwa na wenzake kwenye kikao cha kujadili kadhia zinazowaandamana viongozi wa Waislamu nchini. Wengine waliokamatwa pamoja na Sanze ni Ustadh Sadik Gogo, Ustadh Abdillah na Ustadh Mkadam Swaleh. Gogo ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya wanataalum wa Kiislamu, yaani Tanzania Muslim Professional Organisation (TAMPRO) Hadi sasa hazijapatikana taarifa viongozi hao wa Waislamu wamepelekwa wapi na nini kimewasibu. Hata hivyo kuna taarifa kwamba hivi sasa Jeshi la Polisi lipo katika msako mkali wa kukamata Masheikh na Maimamu wa Misikiti ambao wanaonekana kupingana na utendaji wa BAKWATA na kuhamasisha Waislamu kuwa kitu kimoja katika kutetea, kulinda na kudai haki zao. Taarifa za kuaminika zimefahamisha kwamba baadhi ya Masheikh na viongozi wanaosakwa ni wale wa taasisi za Shura ya Maimamu nchini, TAMPRO, Baraza Kuu na baadhi ya viongozi wa Misikiti jijini Dar es Salaam. Wakati huo huo, Waislamu wanaoshikiliwa katika gereza la Keko jijini pamoja na Sheikh Ponda Issa Ponda, jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Mahakama iliweka wazi dhamana za watuhumiwa wengine isipokuwa Sheikh Ponda. Taarifa kutoka kwa wakili anayewatetea watuhumiwa inasema kuwa washitakiwa wote wa kesi ya kiwanja cha Markaz, wote waliletwa Mahakamani jana na Mahakama ilikubali dhamana kwa washitakiwa 49 isipokuwa Sheikh Ponda. Aliyataja mashariti ya dhamana kuwa ni kila mshitakiwa kuwa na mdhamini mmoja. Kila mdhamini kuwa na barua ya utambulisho kama kutoka osi inayoeleweka au serikali ya mtaa. Kila mdhamini kusaini dhamana ( bo n d ) ya s h . 1,000,0000/= na kwamba washitakiwa wote watakaopata dhamana ni marufuku kuka katika eneo la kiwanja chenye mgogoro. Kuhusu Sheikh Ponda Wa k i l i a m e s e m a k u w a dhamana yake imezuiliwa kwa CERTIFICATE YA DPP. Wakili huyo amesema kuwa washitakiwa wote wamerudishwa rumande hadi tarehe 15.11.2012 kwa sababu kutokana na hali ya ulinzi pamoja na muda wa kesi kuwa asubuhi sana isivyo kawaida, wadhamini wengi walishindwa kufika mahakamani kwa wakati hivyo kushindwa kuwadhamini washitakiwa. Niliomba mahakama ikubali washitakiwa wadhaminiwe mapema kabla ya tarehe ya kesi, MAHAKAMA IMEKUBALI OMBI HILO na imesema itatoa removal order washitakiwa waletwe ili wadhaminiwe ikiwa wadhamini watapatikana, a m e s e m a Wa k i l i J u m a Nassoro. Kwa hiyo naandaa barua ya kuomba washitakiwa wafikishwe mahakamani tarehe 5 au 6 Novemba. Hivyo basi ndugu au jamaa za washitakiwa wawasilishe barua zao za utambulisho kwangu niweze kuziambatanisha kwenye barua ninayokusudia kuipeleka mahakamani KESHO INSHAALLAH! Ama kuhusu dhamana na Sheikh Ponda, Wakili Nassor amesema kuwa bado anatafakari hatua za kuchukua ili kuhakikisha kuwa naye anapata haki yake ya dhamana. Jana asubuhi helkopta ya Polisi ilikuwa ikirandaranda katika anga la jiji la Dar es Salaam ambapo imetafsiriwa kwamba helkopta hiyo ilikuwa angani muda huo kufuatia taarifa zisizothibitishwa kwamba kungekuwa na maandamano wakati Sheikh Ponda anafikishwa mahakamani. Kesi hiyo imeahirishwa kufuatia polisi kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na itatajwa tena Novemba 15 mwaka huu. Hadi tunakwenda mitamboni jana hatukuwa tumepata habari wapi anakoshikiliwa Katibu wa Baraza Kuu na wenzake na kwamba wanashikiliwa kwa tuhuma gani.

Habari

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA

NOVEMBA 1-7 2012

AN-NUUR

Polisi wadaiwa kumtesa mbeba mizigo Zanzibar


Na Mwandishi Wetu

BAADHI wa waumini wa dini ya Kiislamu walioka katika mahakama ya Kisutu kufuatilia kesi ya Sheikh Ponda na wenzie jana jijini Dar es Salaam.

MTU moja mkazi wa Mkele juzi alinusurika kuuawa katika msako wa kuwakamata watu wanaotuhumiwa kusababisha vurugu zilizotokea wiki moja iliyopita mjini Zanzibar. Vurugu hizo ziliibuka Oktoba 17 mwaka huu baada ya kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMUIKI) Sheikh Farid Ahmed Hadi kutoweka katika mazingira ya kutatanisha Oktoba 16, mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa bahari mjini hapa jana, kijana aliyenusurika kuuawa, Salum Bakari Muya alidai aliteswa kwa kukatwa ngozi kwa kisu kichwani na kisha kunyonyolewa nywele polisi ambao pia walikuwa na silaha. Alisema, kabla ya kukutwa na tukio hilo alikuwa amekaa na wenzake wakiwa wanasubiri tenda ya mizigo ya kusafirisha kwa kutumia magari ya punda. Nilikuwa nabangaya yaani kubangaiza wakatokea polisi sita, walipofika nilipokaa

wakanifunua kofia na kunikata kipande cha ngozi na nywele kichwani kwa kisu, alisema Salum. Alidai polisi waliomfanyia ukatili huo ni wa kikosi cha FFU na kwamba baada ya kitendo hicho waliamua kumpeleka Kituo cha Afya cha JKU kilichopoa Saateni kwa matibabu ya awali. Salum alidai kuwa baada ya kupata matibabu katika kituo hicho cha JKU iliamriwa kwamba apelekwe Hospitali Kuu ya Mnazimoja kwa vile alikuwa anavuja damu nyingi. Hata hivyo alisema alishangaa kabla ya kuka Mnazimoja polisi hao waliamua kumtekeleza katika eneo la kwa Abbas Hussein, kilometa chache kutoka walipomtoa hospitali ya JKU. Hawakunifikisha Manazimoja, wakaniacha na kuondoka huku wakisema Ubaya Ubaya mtakoma waambie na wenzio, alisimulia Salum akiwa na bandeji aliyofungwa wakati anapata huduma ya kwanza. Alisema baada ya kutelekezwa na Polisi

aliamua kwenda Welesi huko Kikwajuni kwa lengo la kuzungumza na waandishi wa habari juu ya mkasa uliompata. Baada ya kusimulia mkasa huo, Salum ambaye alifuatana na kaka zake walioomba wasiandikwe majina baadae alipelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi. Alipoulizwa juu ya tukio hilo, Kamishana wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema bado hajapewa taarifa na kwamba iwapo mwathirika atalalamika kituoni Polisi watachukua hatua ya kuchunguza. T u m e z o e a kulalamikiwa, kama mtu amefanyiwa ukatili kwa nini asiripoti kituo cha polisi, hapo ujue kuna jambo anacha, alisema Kamishna Mussa. Lakini baada ya kuelezwa na mwandishi wa habari hizi kwamba kijana huyo amepelekwa hospitali na kaka zake, Mussa alisema aliahidi kufuatilia tukio hilo. Kitendo cha Salum kufanyiwa ukatili na watu wanaodaiwa kuwa polisi kimetanguliwa na

Inaendelea Uk. 4

4
SIFA zote njema anastahiki Allah (S.W) Muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo. Sala na salamu zimkie kipenzi cha Umma Mtume Muhammad (S.A.W) jamaa zake, Maswahaba zake na wale wote wanaowafuata kwa wema hadi siku ya malipo. Kwa mara nyengine tena nchi yetu imetumbukia katika vitendo vya vurugu, fujo, uharamia na vitendo vya uvunjifu wa amani kuanzia tarehe 17 hadi 19 Octoba 2012 kufuatia kutoweka kwa Sheikh Farid Hadi katika mazingira ya kutatanisha. Vikundi vya Maharamia kwa kutumia kichaka cha kutekwa Sheikh Farid Hadi walitekeleza hujuma kubwa sana ambayo imepelekea maafa kadhaa ikiwemo kumwaga damu za watu, kuharibiwa mali za watu, kutia khofu kubwa wananchi, kuashiria kusambaratika kwa Umoja, kuvunja heshima za watu, na kuharibiwa kwa miundo mbinu. JUMAZA kama ilivyotangulia kusema kufuatia vurugu na fujo katika uchaguzi mdogo wa Bububu, kuwa kipo kikundi cha watu wanaotekeleza mipango yao ya kuihujumu Zanzibar kwa kupinga Serikali ya Umoja wa Kitaifa ( SUK ) ili kuwarejesha Wazanzibari

Tamko/Tangazo

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA NOVEMBA 1-7 2012


wote wasikubali kurejeshwa walikotoka pia wasiondoke katika ajenda yao ya kudai hadhi ya Zanzibar ndani na Kimataifa kwa njia ya amani na ustarabu na wajitokeze kwa wingi katika kutoa maoni bila ya woga wala khofu hivi sasa katika Mikoa ya Kaskazini Unguja na Pemba na baadae Mkoa wa Mjini Magharibi. 10. JUMAZA inawataka Maimamu wa Misikiti kuleta dua kwa wingi kwa wiki moja na kisomo maalum (kunuti) siku ya Ijumaa kuiombea kheri, amani, mshikamano na utulivu wa nchi yetu. M O L A W E T U M T U K U F U , T U N A K U O M B A UINUSURU ZANZIBAR NA WATU WAKE DHIDI YA MAADUI WA NDANI NA NJE WASIOTUTAKIA MEMA- AMIN ALI ABDALLA SHAMTE NAIBU AMIRJUMAZA

AN-NUUR

TAMKO LA JUMUIYA YA MAIMAM ZANZIBAR . TAREHE 01/11/2012 KUHUSU VURUGU, FUJO, VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI, KUNYANYASWA KUDHALILISHWA NA KUPIGWA WANANCHI WASIO NA HATIA.
katika maisha ya hasama na uadui baina yao pamoja na kupinga harakati za kupigania hadhi ya Zanzibar ndani na nje, Kimataifa. Kutokana na tatizo hili linaloendelea kukua na katika kuiangamiza Zanzibar, JUMAZA inatoa tamko lifuatalo:1. J U M A Z A inawatanabahisha wananchi w o t e k u w a Ta a s i s i z a Kiislamu Zanzibar kamwe hazihusiani na vurugu hizo kwani zenyewe zinapigania amani, utulivu mshikamano, umoja na u d u g u k a ma inavyoelekezwa katika Dini yetu tukufu ya Kiislamu. 2. JUMAZA inalaani vikali wale wote waliofanya fujo na hujuma zilizopelekea maafa katika nchi yetu kwa kutumia kichaka cha Kutekwa Sheikh Farid Hadi. 3. JUMAZA inalaani vikali vitendo vya kiharamia vilivyofanywa na makundi ya kiharamia vikiwemo vya ubaya ubaya na vinginevyo. Hivyo Serikali ipambane na makundi haya yaliyomo katika jamii na kuyafuta kabisa. 4. JUMAZA inaiomba Serikali kuunda Tume Huru ya kuchunguza kadhia ya kutekwa Sheikh Farid Hadi na ripoti yake iwasilishwe kwa uwazi kabisa kwa Wazanzibari na Jumuiya ya Kimataifa. 5. JUMAZA inaviomba vyombo vya kisheria kuwatendea haki watuhumiwa wote wa ghasia hizo wakiwemo viongozi wakuu wa Jumuiya ya Uamsho kwa mujibu wa sheria za nchi zinavyoelekeza. 6. JUMAZA inaviomba vikosi vya usalama viache kuwatesa na kuwadhalilisha na kuwapiga wananchi wasio na hatia bali iongeze juhudi za kuyasaka makundi ya kiharamia kwa kufuata taratibu za kiusalama na ulinzi wa nchi. 7. J U M A Z A inawaomba Wazanzibari wote kuwa watulivu na subra ya hali ya juu katika kipindi hiki kigumu ili kuepusha Zanzibar yetu tunayoipenda kutumbukia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na hivyo kuiangamiza kabisa. 8. J U M A Z A inawanasihi viongozi wetu wakuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutumia busara zaidi katika kutatua matatizo yaliyopo katika jamii yetu na kurudisha amani badala ya kuweka mbele matumizi ya nguvu. 9. J U M A Z A inawaomba Wazanzibar

Polisi wadaiwa kumtesa mbeba mizigo Zanzibar


Inatoka Uk. 3

KIRINJIKO ISLAMIC ENGLISH MEDIUM PRIMARY SCHOOL


P. O. Box 62 SAME Tel: 0784 833982/ 0784 435336 E-mail ipckiemps@gmail.com
Waislamu kote Nchini mnatangaziwa nafasi za darasa la kwanza katika shule ya kiislamu kirinjiko. Shule hii ni ya bweni kwa wavulana na wasichana 1. Shule hii ni ya kiislamu yenye lengo la kuwapa watoto elimu bora na kuwalea kwa malezi ya kiislami. Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 31/11/2012 2. Masomo yanayofundishwa ni haya yafuatayo:Elimu ya dini ya kiislamu, Usomaji wa Quran na mafunzo yake, Lugha ya kiarabu, English, Kiswahili, Mathematics, Science, History, Geography, Civics, Computer (ICT), Michezo(PDS) 3. Muombaji awe amemaliza elimu ya awali Fomu za maombi zinapatikana katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini. Fomu hii italipiwa Tsh.10,000/= Vifuatavyo ni vituo vya kuchukulia fomu Arusha: _ Msikiti wa Ngarenaro 0784 406 610 Kilimanjaro: _ Moshi: Msikiti wa riadha: 0755 278885 _ Same: Kirinjiko Islamic English Medium primary school 0784 833982 Tanga _ Uongofu bookshop: 0784 982525 Mawah S.S. 0784790530 Mandia Shop Lushoto: 0782257533 Mwanza - Nyasaka Islamic Secondary School: 0717417685/078441768 Osi ya IPC Mwanza Mtaa wa Ruji mkabala na Msikiti wa Sheikh Al Amini: 0714 587193/0714587193 Musoma - Osi ya IPC Musoma Mjini Mtaa wa Karume: 0714 587193 Kagera - Bukoba: Katoro Islamic S.S: 0754 523322 Shinyanga - Kahama: Osi ya AN-NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 Dar es Salaam - Ubungo Islamic High School: 0754 260241/0655 260241 Morogoro - Osi ya EKP, Msikiti wa Ijumaa 0712 689258 Dodoma - Al-Hijra Nursery School: 0716 544757/0712 325086 Singida - Osi ya Islamic Ed.panel karibu na Nuru snack Hotel-0714285465 Manyara - Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575 Kigoma - Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 - Kibondo Islamic Nursery School: 0784 442860 Lindi - Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663 Mtwara - Amana Islamic S.S: 0784 596707/0714 201146 Songea - Msamala Islamic S.S: 0717 043981 Mbeya - Rexona Video karibu na RETICO: 0713 200209 Rukwa - Sumbawanga: Twahiid Islamic S.S: Tabora - Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566 Iringa - Madrastun Najah: 0755 740762 Pemba - Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331 Unguja - Madrastul Fallah: 0777 431580 Shura ya Maendeleo ya Uislamu Zanzibar, Makao Makuu Mpendaye njia ya kaburi Kikombe: 0777 246717/0777 425412 USIKOSE NAFASI HII ADHIMU - Wahi kuchukua fomu sasa MWALIMU MKUU WABILLLAH TAWFIIQ

NAFASI ZA DARASA LA KWANZA 2013

matukio ya vijana wengine wawili kuuawa wakati wa utekelezaji wa zoezi la msako huo mjini Zanzibar mwezi Oktoba mwaka huu. Imedaiwa kuwa Hamad Ali Kaimu aliuawa Ijumaa iliyopita wakati akiwa mikononi kuwa polisi katika eneo la Magomeni na Salum Hassan Mahanju alikufa baada ya kupigwa risasi katika maeneo ya Amani Fresh na watu waliotajwa kuwa maosa ulinzi na usalama. Mbali na vijana hao, askari mmoja Koplo Said Abdulrahman aliuawa na watu wasiojulikana huko Bububu baada ya tukio la kutoweka Sheikh Farid. Wakati huo huo, kijana mtu mmoja alipigwa na Vespa yake kupondwa pondwa baada ya kukimbia kuepuka kipigo. Mtu huyo ambaje jina lake halikufahamika, alikutwa na mkasa huo akipita Michenzani ambapo alikutana na askari wakamsimamisha na kuanza kumpiga.

Alipopata upenyo alikimbia na kuacha chombo chake ambapo askari hao walikipondaponda. Katika eneo hilo hilo, mama mmoja mjamzito alinusurika kupata kipigo baada ya kuchomolewa ndani na polisi. Askari walivamia eneo hilo na kuanza kupiga watu ambao kuta za nyumba zao zilikuwa na maandishi ya kukataa muungano au msemo wa tunataka kupumua. Inaelezwa kuwa baadhi ya askari walipomwona katika hali ya uchovu wa ujauzito, ubinadamu kidogo uliwajia wakamwachia. Katika tukio jingine, kijana mmoja alikamatwa wakati anatiwa shakishaki akapita kijana mwingine akaamrishwa amnyoe alipomaliza akaulizwa tumfanyeje. Wa p a s h a h a b a r i wanasema kuwa kijana yule alisema sijui. Hujui eeh wanadaiwa kujibu askari wale, wakamkamata na kuondoka naye wakamwachia yule aliyekuwa amekamatwa mwanzo na kunyolewa.

NAIROBI KUNDI la Kutetea Haki za Binadamu la Waislamu nchini Kenya (MUHURI), limelaani vikali vitendo vinavyofanywa na jeshi la polisi la nchini humo vya kuwaua watu wawili walioshikiliwa kwa kutuhusishwa na ugaidi, ambapo limesema kwamba mauaji hayo ya kinyama hayakubaliki. Mkurugenzi Mtendaji wa kundi hilo Bw. Hussein Khalid, amesema ni jambo lililo wazi kwamba hivi sasa jeshi la polisi chini ya Wizara ya Usalama wa Ndani nchini humo limeamua kufanya ukandamizaji ambao ni uvunjaji mkubwa wa haki za kikatiba. Mkurugenzi huyo alisema jambo la kwanza ambalo wanataka serikali kufanya kufuatia mauaji hayo ya watuhumiwa, ni jeshi la polisi kuchukua hatua dhidi ya osa wake yeyote aliyehusika kwa namna moja au nyingine katika vitendo vya kutumia nguvu kupita kiasi. Kauli ya kundi la kutetea haki za binadamu la Waislamu nchini Kenya imekuja kufuatia maasa usalama wa Kenya kuwafyatulia risasi na kuwaua watu wawili wanaotuhumiwa kwa ugaidi katika mji wa Mombasa. Mauaji hayo yalifanyika Jumapili asubuhi baada ya polisi kuvamia nyumba moja katika eneo la Majengo, mjini Mombasa. Hivi karibuni Mbunge wa viti maalumu nchini Kenya, Sheikh Mohammad Dor, alitiwa mbaroni mjini Nairobi. Sheikh Mohammad Dor, alikamatwa akidaiwa kusema kuwa kama angalikuwa na uwezo angefadhili wanaharakati wa kundi la Mombasa Republican Council MRC. Sheikh Dor, ametiwa mbaroni siku chache baada ya polisi kuanzisha msako wa watu wanaounga mkono kundi la MRC katika eneo la Pwani ya Kenya. Kundi la MRC linataka eneo la pwani linalotaka kujitenge na Kenya. Katibu wa kudumu katika Wizara ya Usalama nchini Kenya, Mutea Iringo alisema kwamba, msako huo utaendelea hadi hali ya kawaida itakaporejea katika eneo hilo. Polisi nchini Kenya imesema kuwa, wanasiasa na wafanyabiashara wanaofadhili kundi la

Waislamu Kenya walaani polisi kuua watuhumiwa


MRC watatiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka. Kabla ya kadhia ya kukamatwa Sheikh Dor, hali ya wasiwasi ilitanda mjini Mombasa baada ya kuuliwa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari lake Sheikh Aboud Rogo, siku ya Jumatatu mwezi uliopita wakati akimpeleka mkewe hospitali. Kuuliwa kwa sheikh Rogo, ambaye naye alikuwa akishukiwa na kuhusishwa na ugaidi na pia alishukiwa kufadhili kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia, kulisababisha vurugu kubwa nchini Kenya, Waislamu wakipinga kiongozi wao kuhusishwa na ugaidi ili kuhalalisha kuuliwa kwake. Polisi wawili walikufa kutokana na majeraha waliyopata baada ya shambulio la guruneti katika gari lao mjini Mombasa. Hadi kufikia sasa polisi watatu wamefariki tangu kuanza kwa ghasia zilizotokea baada ya kifo Sheikh Aboud Rogo siku ya Jumatatu. Kwa siku mbili, vijana wa kiisilamu walikuwa wakipambana na polisi katika barabara za Mombasa. Watu wengine kumi na tatu walijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo. Mhubiri Aboud Rogo Mohammed, alikuwa akituhumiwa na kuhusishwa na ugaidi na pia alishukiwa kufadhili kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia. Sababu kubwa ya kushukiwa huko ni Marekani kumtaja kuwa ni mtu anayewasajili baadhi ya vijana wa Kenya kwenda kujiunga na wapiganaji wa Al Shabaab. Watu 12 walikamatwa na polisi kufuatia makabiliano

Habari za Kimataifa

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA

NOVEMBA 1-7 2012

AN-NUUR

Meli za kivita za Iran zatia nanga Sudan


KHARTOUM MELI mbili za kivita zimetia nanga nchini Sudan Jumatatu, ikiwa ni chini ya wiki moja tangu Khartoum ilipoishutumu Israel kushambulia kiwanda cha silaha jijini humo, vimeripoti vyombo vya Iran. Mpaka sasa Israel imekataa kukanusha au kukubali kuhusika na shambulio hilo. Katika shambulio hilo la ndege za Israel Jumanne huko Sudan katika kiwanda cha silaha cha Yarmouk kusini mwa jiji la Khartoum watu wawili waliuliwa. Waziri wa Habari wa Sudan, Ahmed Belal Osman, alisema kuwa ndege nne za kijeshi zilishambulia kiwanda hicho na kwamba Israel ndio mhusika mkuu. Alipohojiwa na televisheni ya Israel ya Channel Two News juu ya shutuma za Sudan, Waziri wa Ulinzi wa Israel Bw. Ehud Barak alisema, hakuna lolote analoweza kueleza juu ya hilo. Shirika la habari la Iran, IRNA lilisema meli iliyobeba helicopter inayoitwa Khark na ile ya kushambulia inayoitwa Shahid Naqdi zilibeba ujumbe wa amani na uraki kwa nchi za jirani na zinahakikisha usalama katika njia za meli dhidi ya maharamia na magaidi. Fars news agency ilieleza kuwa meli hizo zimetia nanga katika bandari ya Sudan iliyopo kwenye Bahari ya Sham na makamanda katika meli hizo wamepanga kukutana na makamanda wa kijeshi wa Sudan. Mwezi Mei mwaka jana serikali ya Sudan ilieleza kuwa mtu mmoja aliuawa baada ya gari kulipuliwa katika mji uliopo mashariki Port Sudan. Ilielezwa kuwa mlipuko huo ulisababishwa na shambulizo la kombora la Israel. Israel haikueleza chochote juu ya shambulio hilo wala lile la mwaka 2009. Iran ilieleza Juni mwaka huu kuwa ina mpango wa kuunda meli zaidi za kivita na kuongeza uwepo wake katika bahari za kimataifa, hasa kwa ajili ya kulinda meli zake za mizigo duniani kote. Maharamia katika ghuba ya Aden mwezi Januari walitka meli moja ya Iran iliyokuwa imebeba tani 30,000 za kemikali za mafuta zilizokuwa zikiepelekwa Kaskazini mwa Afrika. Katika hatua nyingine, Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA)

BAADHI ya majeruhi wa milipuko iliyotokea nchini Kenya siku za hivi karibuni

NEW YORK Kimbunga kikali kinachoitwa Sandy kimesababisha hasara na uharibifu mkubwa katika pwani ya mashariki mwa Marekani ambapo mpaka sasa kimeripotiwa kuua watu wasiopungua 38. Vifo hivyo vimetokea mapema wiki hii katika majimbo ya Marekani ya New York, North Carolina, West Virginia, New Jersey, Pennsylvania, Ottawa na Maryland. Meya wa jiji la New York, Michael Bloomberg, amesema kwamba kimbunga hicho kinaweza kuwa kikubwa zaidi kuwahi kuiathiri Marekani. Taarifa zinaeleza kuwa mbali na kusababisha vifo, kimbunga Sandy kimesababisha kuharibika miundo mbinu hasa kukatika kwa huduma ya umeme. Watu wapatao milioni 8 wameathirika ambapo katika jimbo la New Jersey, maafisa wamewatahadharisha raia kwamba kuishi bila ya umeme kwa zaidi ya wiki moja.

Kimbunga Sandy chaua 38 Marekani

kati ya polisi na vijana waliokuwa wakipinga kuuliwa kiongozi wao wa kidini Sheikh Aboud Rogo. Katika siku ya pili ya vurugu hizo, wengi ya vijana hao wamekamatwa nje ya Masjid Musa iliyo eneo la Majengo Mombasa.

limesema kuwa halikuhusika katika shambulio hilo la Israel katika kiwanda cha silaha mjini Khartoum Sudan. Gazeti la al Intiba la Sudan limeandika kuwa, mkuu wa CIA, David Petraeus aliwasiliana kwa simu na Saleh at Tayeb, naibu mkuu wa shirika la kijasusi la Sudan muda mchache tu baada ya Israel kufanya shambulio hilo na kusema kuwa Marekani haikushiriki kwa namna yeyote katika shambulizi hilo. Mamia ya wananchi wa Sudan walifanya maandamano mjini Khartoum kulaani mashambulio hayo huku wakitoa kaulimbiu dhidi ya Israel na Marekani Mauti kwa Israel na Ondoa Israel katika ramani ya dunia. Hata hivyo shambulizi hilo la kijeshi limezusha mjadala mkubwa kimataifa.

Vianzio halisi vya harakati ya Boko Haram


(Imewekwa katika mtandao Januari 23, 2012)
BOKO Haram ilianza mwaka 2002 kama kundi lililojitenga la amani la Kiislamu ambalo lilizua fikra chakaramu ya kupinga elimu ya ki-Magharibi. Kundi hilo halikujiita Boko Haram lakini likapewa jina hilo na watu wa kawaida na kupewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari vya Nigeria wakati kiongozi wa kundi hilo Muhammad Yusuf alipotangaza na kueneza kuwa Boko (vitabu, elimu ya kimagharibi) ni haram. Baadhi ya sababu alizotoa ni kuwa (elimu hiyo) inatoa nadharia ambazo ni kinyume cha kanuni za Uislamu. Mfano ni nadharia ya kubadilika maumbile (kama chanzo cha binadamu-kwamba binadamu katokana na nyani). Katika vitabu vya sayansi vya Magharibi ambavyo vinaondoa mikono ya Mungu katika kuumbwa binadamu na ulimwengu wote. Alisema nadharia hii inapingana na msingi muhimu wa Uislamu ambao unamwona Mungu kuwa ni muumba wa dunia na ulimwengu wote. Pia alitoa sababu ya kuharibika kwa maadili ya vijana ambao wanasoma shule za ki-Magharibi kwa mfano kuvaa nusu uchi, kufanya mapenzi ovyo, ulevi na utumiaji wa madawa ya kulevya. Pia aliikosoa elimu ya Magharibi kuwa haisaidii katika kuondoa tatizo la kukosa kazi miongoni mwa vijana wa Nigeria, na hivyo inawanyima muda wao wa kujifunza kuingia katika kazi za mikono. Fikra yake ilipingwa na wanazuoni wengi wa Kiislamu pamoja na waalimu wake wa zamani ambao waliiona elimu ya Magharibi kama mti wenye miiba ambao una uzuri na ubaya wake, na kuainisha kuwa Uislamu unaruhusu na kuhimiza kutafuta elimu katika mapana yake yote. Licha ya kuwa juhudi za wanazuoni hawa kumrudisha katika mstari ulionyooka zilimwelekea kiziwi, aliendelea kujitwalia wafuasi, hasa miongoni mwa vijana, ambao wamekubwa katika wimbi la umasikini na kukosa kazi. Wengi wanasemekana walikuwa wameacha shule na kuanza kufanya vibarua na umachinga. Wengi walichana vyeti vyao vya kumaliza shule licha ya kuwa katika mahojiano na BBC, Idhaa ya Kihausa, Yusuf alikanusha kuwaambia wafuasi wake wachane vyeti vya shule. Kundi hilo liliendelea kueneza kra yao na pia kutaka kuundwe dola ya Kiislamu Kaskazini ya Nigeria (itakayoweka mfumo sahihi wa elimu usio na nadharia za kudai kuwa binadamu katokana na nyani na itakayompa mtoto maadili

Makala

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA NOVEMBA 1-7 2012

AN-NUUR

Angalizo: Mada hii haina nia ya kutetea harakati ya Boko Haram ambayo mimi na Waislamu wengi wengine tunaaki ni uhalifu wa mipaka iliyowekwa na Uislamu. Mada hii ni jaribio la kuelewa chanzo cha vitendo vikubwa vya uhalifu vinavyofanywa na kundi hilo ambalo linasitisha maisha ya watu wasio na hatia kila siku, kuzuia maisha ya pamoja kwa amani na kuhatarisha usalama wote wa taifa nchini Nigeria na umoja wake.

WANAODAIWA kuwa kundi la 'Boko Haram' la Nigeria wakiwa chini ya ulinzi. mema). Waliendelea kufanya shughuli zao kama kundi la amani na kusaidiana hadi polisi walipoua wanachama wao kama 14 hivi katika msafara wa mazishi (walikuwa wakienda mazikoni polisi wakawashambulia). Polisi walitumia kisingizio kisicho na mashiko cha kutovaa koa ya kukinga ajali. Kiongozi wa kundi hilo aliandika barua kadhaa kwa Gavana wa Jimbo la Borno na Kamishna wa Polisi wa Jimbo hilo. Alitoa madai ya kulipwa dia kwa familia za waliouawa nje ya sheria na Polisi wakati wa msafara wa mazishi. Alifuatilia barua yake kwa kuwaendea Wakuu wa Polisi lakini mwito wake uliangukia viziwi. Halafu akafanya mikutano kadhaa na Inspekta Jenerali wa Polisi wakati wa utawala wa YarAdua aingilie kati, lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika kwa watuhumiwa wa mauaji hayo. Alianza kupeleka vitisho kwa serikali na polisi. Aliipinga kwa nguvu serikali ya YarAdua na kumwita YarAdua kuwa ni mkandamizaji na kuitangaza serikali yake kuwa haitendi haki. Kwa viongozi na wanazuoni wa Kiislamu ambao walipinga vitisho vyake dhidi ya serikali, aliwaita ni wanafiki na hata kuwaita baadhi yao si waumini. Yeye na wanachama wake wakaanza kujitwalia silaha huku wakiungwa mkono na wengi waliokuwa wana kinyongo dhidi ya unyangau wa usimamiaji haki miongoni mwa polisi wa Nigeria. Anasemekana kuwa alikuwa anaungwa mkono hata na wasio Waislamu ambao walimwekea dhamana mara kadhaa akiwa ameswekwa ndani na polisi kwa maelezo kuwa anahatarisha amani kutokana na vitisho vyake kwa serikali ya YarAdua. Kwa mujibu wa Dk. Aliyu Tilde, Kuwa na silaha ni jinai, kosa kubwa sana, kwani ikiwa kwa sababu yoyote ile Wanigeria wote milioni 165 wataamua kutwaa silaha, kutakuwa na umwagaji damu usioisha ambao hautamfurahisha Mungu kwa hali yoyote ile. Serikali ina wajibu kwa wananchi wengine kulidhibiti kundi hilo. Katika kudhibiti pale wanapovuka mpaka, serikali hata hivyo ilitakiwa izingatie sheria na kuheshimu haki za msingi za raia. Inaweza kuwakamata na kuwafungulia mashitaka viongozi wa BH na wanachama wake kwa uhaini, kuwa na silaha, n.k. Lakini utawala wa YarAdua haukufanya yote hayo, na badala yake ukaamua kuwaua wanachama wa kundi hilo. Kama serikali ingefuata mustakabali wa sheria na kuufuatilia kwa subira muda wote ilipokuwa inazozana na kundi hilo, mambo yasingeka yalipokia. Lakini ilitanguliza kukosea, na kosa lake lilililazimisha kundi hilo kuingia katika hatua ya mkakati wa hatari wa kufanya shughuli zake kwa kicho. Dk. Aliyu alisema pia kuwa Tusisahau amri ya kuwamaliza ambayo Rais YarAdua alitoa kwa majeshi ya usalama asubuhi ile akiondoka kwenda Brazil. Alikia kuweka muda kuwa hadi saa kumi jioni siku hiyo, kazi hiyo iwe imemalizika (yaani vijana wa Boko Haram wote wawe wameshauliwa). Mjini Maiduguri, serikali iliazimia kuteketeza kundi hilo bila kutumia mfumo wa kisheria. Dunia ilishuhudia jinsi makao yao (makuu) yalivyosambaratishwa na wanajeshi; Muhammad Yusuf, kiongozi wao aliuawa (nakala ya mahojiano yake na polisi inapatikana katika mtandao); Muhammad Foi, mwajiriwa wa zamani wa Mkuu wa Polisi wa eneo hilo, alipigwa risasi barabarani baada ya kukamatwa. Muhammad Fugu, babamkwe wa Muhammad Yusuf ambaye

hakuwahi kushiriki katika kundi hilo alitangazwa kuwa anatafutwa na polisi. Alifika mwenyewe katika kituo cha polisi na kuuawa hapo hapo bila kuhojiwa, ila tu kuwa mwanafamilia na mke wa Muhammad Yusuf. Polisi na jeshi waliendelea kuua yeyote ambaye alikuwa anafanana na wanachama wa BH kiasi kuwa watu wakaanza kunyoa ndevu wote kwa pamoja, n.k. (kwa sababu ilikuwa ukionekana una ndevu za ki-Answaar, unauliwa). Ofisa mwandamizi wa polisi akaripotiwa katika magazeti akisema kuwa hawezi kuhakikisha maisha ya mtu yeyote anayeonekana ana sharafa (ndevu mashavuni). Wengi walikamatwa pamoja na wake zao. Wamebakia jela hadi sasa bila kufikishwa mahakamani. Kuua wafuasi wa kundi hilo ndiyo mkakati halisi wa serikali katika kukabiliana na kundi hilo. Mkanda wa video wa mauaji ya Bw. Yusuf nje ya sheria ulisambazwa kila mahali, lakini hakuna mtu aliyekamatwa na kuadhibiwa kwa jinai hiyo. Wa k a t i k u n d i h i l o likiandamana katika kituo cha polisi cha Bauchi haikuwa sababu ya kuzua ulazima wa kuingia vitani moja kwa moja nao. Mjini Bauchi inakisiwa kuwa zaidi ya wanachama 70 wa kikundi hicho waliteketezwa katika maskani yao nyuma ya uwanja wa ndege. Inaelekea walikuwa hata hawana habari ya ugomvi uliozuka katika kituo cha polisi cha Dutsen Tanshi ambao ulikuwa umeanza asubuhi. Hadi kukia jioni, kamishna wa kazi maalum jimboni aliongoza kundi la mawakala wa serikali waliosambaratisha kituo hicho na matingatinga. Wasafiri katika kituo cha Yankari Park mjini Bauchi walishuhudia jinsi wanachama wanane wasio na silaha walivyokamatwa na kuuawa hapo hapo na wanajeshi wakati wakipanda basi kwenda Maiduguri. Gavana wa jimbo, Isa Yuguda, akataka kujitwalia sifa baadaye kwa jinsi serikali yake ilivyopambana kikamilifu na kundi hilo katika jimbo lake. Dunia ililaani vitendo hivyo vya kikatili vya utawala walivyoonyesha. Serikali ikaomba radhi kwa Umoja wa Mataifa baada ya kulaaniwa kwa kukiuka haki za binadamu, ikiahidi kuwa waliofanya hivyo watakishwa mbele ya sheria. Ukweli ni kuwa hawakufanya lolote. Hakuna hatua za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi ya yeyote (Polisi na wanajeshi waliouwa) hadi Boko Haram walipopiga bomu Makao Makuu ya Polisi mjini Abuja mwaka 2010. Maosa wawili wa polisi wakatangazwa kuwa

Inaendelea Uk. 6

7
Na Omar Msangi
INGEKUWA Mheshimiwa Mulugo ni Alhaj, vyombo vya habari vingekuwa vimepata karamu. Sasa hivi Waislamu wangekuwa taaban kwa kejeli na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Habari Ikulu angekuwa katika wakati mgumu akijaribu kumtetea Mheshimiwa Rais kwa mashambulizi na madongo ambayo angekuwa anatupiwa akituhumiwa kuwapa Uwaziri watu waliosoma Madrasa. Lakini maadhali Mheshimiwa Naibu Waziri Philipo Augustino Mulugo, si Muislamu, kimyaa! Utadhani hakuna kilichotokea ukiacha zile taarifa za awali ambazo hata hivyo zilitolewa na magazeti machache tu. Mnamo Oktoba 18, 2012 Maaskofu wa Kanisa la KKKT walitoa tamko kali kufuatia kile kilichoitwa uchomaji wa makanisa Mbagala ambao unahusishwa na baadhi ya Waislamu. Mengi yamesemwa katika tamko hilo lililosainiwa na Maaskofu 20 wakiongozwa na Askofu Dr. Alex G Malasusa, lakini makubwa matatu ndiyo yanayojitokeza. Kwanza kutumia tukio hilo kujenga hoja kuwa nchini hapa Wakristo wanateswa, wanatendewa vibaya na dini yao inapigwa vita. Hili limejitokeza pale tamko hilo linaposema kuwa: Kilichotokea Mbagala ni mateso ya Kimbari, yaani mateso ya Kanisa (Persecution). (na kwamba) Mateso haya ni matokeo ya mbegu ya magugu iliyopandwa katika bustani njema na sasa magugu hayo yanazaa matunda machungu. Maaskofu hao wakionyesha magugu ni yepi na nani wanaopanda magugu hayo na sasa wanawatesa Wakristo wakiwa njiani kufanya mauwaji kama yale ya Kimbari, Rwanda, wanasema kuwa: Dalili za mateso ya Kimbari kama ilivyo kwa mateso ya Kanisa, zilianza kitambo na hazikushughulikiwa na waliomrithi Baba wa Taifa. Dalili hizo ni kama hizi: (kwanza) Uchochezi wa wazi kuwa taifa hili linaendeshwa na unaoitwa Mfumokristo, na kuwa Baba wa Taifa alaaniwe kwa yote aliyotendea taifa hili. Wanachosema Maaskofu h a w a n i k u w a Wa i s l a m u wanaodai kuwa nchi hii inatawaliwa na Mfumokristo ndio wanaopanda magugu katika bustani na ndio wanaotesa Wakristo. Pengine hapa niseme jambo moja, majadala huu wa Mfumokristo na dhana nzima kuwa serikali haina dini na kwamba mambo hayaendeshwi kwa kuzingatia dini, umekuwa mjadala wa viziwi. Ameandika Padiri John Sivalon, ameandika Mohamed Said na wameandika waandishi mbalimbali jinsi Mwalimu Nyerere alivyotumiwa na Kanisa Katoliki kusimika Mfumokristo ambo ndio Waislamu wanaulalamikia hivi leo kwamba unakandamiza haki za Waislamu na kuwapendelea Wakristo. Ni kweli kama wanavyosema Maaskofu hawa

Watanzania sisi tutaponea wapi?


halionyeshi sura ya kitaifa kwa sababu toka limeundwa limekuwa kama parokia ya Kanisa hasa ukiangalia wanaozikalia zile sehemu nyeti ambazo ndio roho ya NECTA na iliyoshikilia majaaliwa ya watahiniwa wote nchini. Pili, Waislamu wanatuhumu kuwa kuna upendeleo kwa upande wa Wakristo na kwa upande mwingine Waislamu wanahujumiwa. Pamoja na mambo mengine mengi wanatoa ushahidi wakisema kuwa NECTA imeajiri Mchungaji wa kuangalia maslahi ya watoto wa Kikristo lakini mpaka sasa imegoma kuajiri mtaalamu wa kushughulikia Somo la Maarifa ya Uislamu na Lugha ya Kiarabu. Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dr. Joyce Ndalichako aliwahi kudai kuwa hajapewa idhini ya kuajiri watumishi wapya. Taarifa zilizopo ni kuwa hivi karibuni Baraza limeajiri watumishi wapya kadhaa. Je, ruhusa hiyo ya kuajiri watumishi wapya imempa maelekezo kuwa bado ni marufuku kuajiri mtaalamu wa Somo la Maarifa ya Uislamu na Lugha ya Kiarabu? Labda Maaskofu watusaidie kuuliza. Tujaaliye kuwa Dr. Joyce Ndalichako amepewa maelekezo kutoka ngazi za juu kuwa marufuku kuajiri Muislamu au anafanya tu mwenyewe kwa ukereketwa wake wa Kikristo na chuki zake binafsi dhidi ya Waislamu, je, hili Waislamu wasiliseme? Wasilalamike? Ingekuwa haya yanayofanywa na Dr. Ndalichako wanafanyiwa Wakristo, kwa maana jaaliya Ndalichako angekuwa Mchecheni, kaajiri Sheikh wa kuangalia maslaha ya vijana wa Kiislamu, lakini kagoma kuajiri mtaalamu wa somo la Divinity, Maaskofu hawa wanaosema na kuwalaumu Waislamu kuwa wanaleta mashinikizo ya kidini juu ya uteuzi wa watendaji NECTA, wangekaa kimya? Yapo pia madai kuwa kuna matatizo makubwa katika kuweka Grade Ranges ambapo wahusika ni kamati nyeti isiyofahamika kanuni na taratibu za utendaji wake wa siri. Katika jumla ya tuhuma ni kuwa mtahiniwa Muislamu akipata kwa mfano makisi 50 katika Somo la Dini ya Kiislamu anapewa D, wakati kwa makisi hizo hizo 50, mtahiniwa Mkristo katika Divinity, anapewa C!!!. Kwa utaratibu huo, Muislamu akipata kwa mfano alama 65 anapewa C, lakini kwa alama 65 hizo, Mkristo anapata B! Yapo na mengi juu ya zile shule zinazotakiwa kutesa kila mwaka na jinsi yanavyofanyika maarifa bila kujali kuwa kufanya

Makala/Tangazo

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA

NOVEMBA 1-7 2012

AN-NUUR

ASKOFU Alex Malasusa kuwa Waislamu wamekuwa wakileta madai kuwa nchi inaongozwa na mfumokristo. Ila Waislamu wanaposema hivyo, hawakusudii kuleta uchochezi. Wanachofanya ni kusema ukweli ambao umekuwa ukifukiwa miaka yote ili kuendeleza dhulma dhidi ya Waislamu. Wanachofanya ni kuwatanabahisha Watanzania kuwa ipo hatari huko mbele kama mfumo huu wa kibaguzi na uonevu hautaondolewa, Haki ikasimama. Sasa maadhali kama ninavyosema huu umekuwa ni majadala wa viziwi, kila mmoja anajifanya hamsikii mwenzake. Kwa hiyo kila mmoja akiibuka anasema lake. Katika hali hii, njia bora ni kuwa na mjadala wa pamoja. Wakae Waislamu na Wakristo kwa uwakilishi na kwa utaratibu utakaokubalika kwa pande zote mbili. Mada hii ijadiliwe. Waislamu walete hoja zao kuonyesha kuwa kuna mfumokristo na kwamba ni Nyerere aliyeusimika na kwa maana hiyo cheo hasa anachostahiki ni Baba wa Kanisa (Katoliki) lililo katika mchakato wa kumpa utakatifu. Kwa upande mwingine kama Wakristo nao wanazo hoja za kuonyesha kuwa Mwalimu Nyerere hakuwa mdini na hakuna mfumokristo, watazileta. Labda hilo niliwachie hapo nizungumzie nukta ambayo ndiyo hasa lengo la makala hii. Sehemu moja katika tamko hilo la Maaskofu wa KKKT wamesema kuwa (Waislamu) wamekuwa wakileta mashinikizo ya kidini yanayoingilia mifumo wa kitaaluma na kisheria (na pia kuleta)Mashinikizo ya kidini juu ya mfumo wa uteuzi wa watendaji wa serikali na katika osi za umma. Hivi karibuni na mpaka sasa Waislamu wanahoji utendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA). Wanasema, kwanza

hivyo kunawafanya mamia ya maelfu ya wanafunzi wa Kitanzania, kuteseka. Sasa hizi ni tuhuma na namna pekee ya kuziondoa ni kufanya uchunguzi huru na makini na kuweka matokeo yake hadharani. Kinyume cha hivyo, kutoka tuhuma itachukuliwa ni kweli ndio maana NECTA/Serikali haitaki kufanyike uchunguzi na kuweka mambo wazi. Lakini hebu tuyaache hayo kwanza, hivi karibuni tulisoma katika vyombo vya habari kuwa Naibu Waziri wetu wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Philipo Mulugo alitoa ya mwaka iliyotufedhehesha Watanzania wote. Waziri aiaibisha serikaliAsema Tanzania ni Muungano wa Zimbabwe, Pemba na Tanganyika. Limeripoti gazeti la Tanzania Daima. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amemwaibisha Rais Jakaya Kikwete na taifa kwa ujumla mbele ya jamii ya kimataifa, baada ya kuitangazia dunia kuwa Tanzania imetokana na muungano wa visiwa vya Zimbabwe na Pemba vilivyoungana na Tanganyika. Imesema taarifa hiyo ya gazeti na kuongeza kuwa, mbali na hilo, aliwaambia mamia ya wajumbe kutoka mataifa mbalimbali katika Bara la Afrika kuwa, Tanzania ilizaliwa mwaka 11964. Ili kuonyesha kuwa linasema jambo la uhakika gazeti likakariri kauli ya Naibu Waziri Mulugo akisema: Wasilisho langu litakuwa na sehemu sabaUtangulizi, Tanzania iliundwa mwaka 11964 kwa kuunganisha visiwa vya Bahari ya Hindi vya Zimbabwe na Pemba vilivyoungana na nchi ya Bara iliyokuwa ikiitwa Tanganyika. Nukuu hiyo ni tafisiri ya Kiswahili kutokana na kauli ya Naibu Waziri Mulugo kwa Kiingereza pale aliposema kwa kujiamni na bila kuonyesha dalili yoyote kuwa alikuwa amekosea, akisema: Tanzania was formed in one nineteen sixty four (11964) by unifying the Indian ocean islands of Zimbabwe and Pemba and the mainland territory formerly known as Tanganyika. (- Hon. Mulugo Philipo Augustino Deputy Minister of Education and Vocational Training.) Naibu Waziri huyo alikuwa akiwasilisha mada katika mkutano wa Viongozi na Wataalamu wa Elimu katika Bara la Afrika, ambao ulifanyika Afrika Kusini kuanzia Oktoba 5-7, mwaka huu. Baada ya kusoma habari

hizi, watu wengi walipata hamu ya kujua huyu Philipo Mulugo ni nani na historia ya kusoma kwake ikoje. Labda ingekuwa vyema Maaskofu hawa wa KKKT wanaowashutumu Waislamu wanaolalamikia uteuzi wa watendaji serikalini kuwa ni wa kibaguzi, wangefuatilia kule sekondari ya Mbeya alikosomea O Level (1990 mpaka 1993) na kule Songea Boys High School alipokuwa kidato cha tano na sita (1994 mpaka 1996), watuambie, kile Kiingereza alichosema Mulugo na kule kusema kuwa, Tanzania was formed in one nineteen sixty four (11964) by unifying the Indian ocean islands of Zimbabwe and Pemba and the mainland territory formerly known as Tanganyika; hakuwakilishi uwezo wake alipokuwa shuleni? Uwezo ambao unajidhihirisha leo na kutuletea aibu? J e , k a t i k a Wa t a n z a n i a wenye elimu, katika vijana wa Kitanzania waliosoma, hakuna wenye uwezo zaidi ambao wangeimudu nafasi hiyo na wasingetuaibisha? Je, Waislamu wakilalamikia Mawaziri na watendaji kama hawa na kulalamika kuwa huenda wameteuliwa kutokana na Ukatoliki wao kutokana na mfumokristo uliopo, watakuwa wanaleta maneno ya uchochezi? Askofu Malasusa na Maaskofu wenzake 19 wanasema kuwa Waislamu wanaleta mashinikizo ya kidini yanayoingilia mifumo wa kitaaluma na kisheria (na pia kuleta)Mashinikizo ya kidini juu ya mfumo wa uteuzi wa watendaji wa serikali na katika osi za umma. Kuna utaalamu gani uliotumika katika kuandaa hotuba hii ya Mheshimiwa Naibu wa Waziri Philipo Mulugo ? Kutokuhoji mambo haya, mimi naamini ndio kulikoifanya nchi hii, kwamba pamoja na rasilimali zote ilizonazo, tumebaki masikini miaka 51 baada ya Uhuru na wala hakuna dalili ya kuonekana mwanga mbele japo tunaimba kila siku habari ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania. Inawezekana kama Waislamu watasoma Risala mbele ya Mheshimiwa Rais wakilalamika kuwa kwa nini wao ni wachache katika Baraza la Mawaziri, katika Jopo la Makatibu, Makamishna, Wakurugenzi, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, huenda Mheshimiwa Rais atawajibu kwamba hawakuomba. Wamechelewa wakati wenzao Wakatoliki na Wakristo wengine waliomba! Tu n a c h o w a h a k i k i s h i a Maaskofu hawa wa KKKT na wengine ni kuwa hata kama itabidi Waislamu waende kupiga magoti Ikulu ili nao wapate haki katika nchi hii, lakini hawatanyanyua mikono kuwaombea nafasi za Uwaziri watu ambao ni D au C material. Wanao vijana na wazee wa kutosha wa viwango vya A na B.

8
EWE Allah ifanye historia ya maisha kuwa somo kwa viumbe. Ewe Allah utie nguvu Uislamu kwa mmoja kati ya watu wawili; Amar bin Hisham (Abu Jahl) au Umar bin Khattab. Mtume (s.a.w.) aliomba. (Bakhari na Huslim). Mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini na saba, akiwa na upanga mkononi mwake, mwenye mwili mkubwa wenye nguvu na harara ya ghadhabu, alitoka nje ya nyumba yake kuungamiza Uislamu kwa kummaliza muasisi wa Uislamu, Mtume Mtukufu (s.a.w.). Hata hivyo, haikudhamiriwa kuwa hivyo. Mtume Mtukufu (s.a.w.) aliomba mwongozo kwa mtu huyo huyo. Mtu huyo alikuwa Umar (r.a.) ambaye majaaliwa yake yalikuwa muhimu na uongozi katika kusimamisha Uislamu. Alipokuwa njiani, na upanga usio na ala mikononi mwake akitembea kwa hatua ndefu zenye nguvu, alisimamishwa na Muislamu, Noim bin Abdallah (r.a.) aliye msaili juu ya ghadhabu (hasira) yake. Baada ya kuelezwa dhamira yake, Noim (r.a.) alimshauri Umar (r.a.) badala ya kuwa na matarajio makubwa, aisafishe nyumba yake kwanza, kwani dada na shemejiye walishasilimu. Baada ya kusikia hayo, Umar (r.a.) alielekea nyumbani kwa dada yake, alipofika alisikia Qurani ikisomwa ndani. Umar alimvaa shemeji yake na akaanza kumshambulia. Dada yake aliingilia kati na alisukumwa pembeni kwa nguvu kiasi cha kujeruhiwa kichwani, na kuvuja damu nyingi. Aliinuka na kumwambia Umar bila wasiwasi, Ewe Umar fanya unyama wako. Hatuto acha Uislamu. Aliposikia hivyo, alilazimisha ayah ile ya Qurani asomewe. Aliposikia Ayah ile; Qurani, TAHA: 14, Hakika mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana Mungu ila mimi tu. Basi niabuduni Mimi, na ushike sala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi. Akili zake zilimrejea. Aliomba kumwona Mtume (s.a.w.). Aliongozana na Khabbab (r.a.) kwenda kumwona Mtume (s.a.w.) ambapo alieleza azma yake ya kusilimu. Sauti za Allahu Akbar zilishangilia maneno yale. Hili lilijiri mwaka wa sita wa Utume. Mpaka leo, Uislamu unakabiliwa na uhasama kutoka kwa Maquraish, ulikuwa na wafuasi hamsini na mmoja tu. Walikuwa bado wakichukua tahadhari kiasi cha kusali kwa kicho. Kusilimu kwa Umar kulibadili kabisa hali iliyo kuwepo. Kwa wasifu wa ujasiri wake na ushajaa wake, alitangaza hadharani kusilimu kwake, aliswali ndani ya Kaaba na alipambana na upinzani wa Maquraish. Kwa kutangaza hadharani imani yake, alipewa cheo cha FAROOQ na Mtume

Habari/Tangazo

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA NOVEMBA 1-7 2012

AN-NUUR

AMIRUL MUMINIIN SAYYIDINA UMAR AL-FAROOQ (R.A.)


(s.a.w.). Maisha yake ya Mwanzo: Katika maisha yake ya mwanzo, Umar (r.a.) alikuwa akichunga ngamia, alipo baleghe, alitumia muda wake wa mapumziko kujifunza mchezo wa mieleka, kupanda farasi, ufundi wa kushindana kwa vitara, (fencing) ufasaha wa kusema na elimu ya nasaba. Alikuwa maarufu kwa uhodari wake wa mieleka. Aidha alikuwa mpandaji hodari na farasi na aliweza kumpanda farasi bila ya kikuku (cha kupandia farasi) na bila shogi. Alikuwa mmoja wa Maquraish kumi na saba waliojua kusoma na kuandika. Katika ujana wake, Umar (r.a.) alisari sana nchini Syria na Iran kwa ajili ya biashara zake. Kwa sababu hiyo alikuwa mtu maarufu na Maquraish walimteua kuwa Balozi wao kila kulipotokea sintofahamu na makabila mengine. Nimesilimu na ninataka kuweka wazi kuwa kuanzia leo na kuendelea nguvu zangu zote zitatumika kwa ajili ya ufanifu na ushindi. (Umar(r.a.). Kusilimu mpaka Ukhalifa: Jina la Al-Farooq (anaye leta mabadiliko) linaashiria kuwa, kusilimu kwa Umar (r.a.) kulileta mabadiliko makubwa kwenye kra za Waislamu. Hata hivyo, walikuwapo watu 51 tu waliorejea na wengi wao hawakudhihirisha Uislamu wao. Kitendo cha kwanza cha Umar (r.a.) baada ya kusilimu kilikuwa kwenda na kuswali ndani ya Kaaba bila kicho, akikataa katakata kuzuiwa na yeyote. Hapana aliyethubutu. Alitangaza wazi imani yake, aliwaita Machifu wote wa Makkah na kuwaeleza mabadiliko yaliyo mpitia. Hapana aliyethubutu kusema neno, hata hivyo walikuwa na uchungu wa kumpoteza mtu hodari. Kilichofuatia ni kuwaongoza Waislamu kuingia ndani ya Kaaba na kusali jamaa. Hii ilikuwa swala ya kipekee ndani ya Kaaba: Alimshauri Mtume (s.a.w.) kuanza njia ya kuwaita waumini kwenye swala ya jamaa kwa kuadhini kwa sauti kubwa. Mtume (s.a.w.) aliridhia. Wakati wa Hijra, hakuondoka kwa kicho kama watu wengine. Alifanya Tawaaf ya Kaaba na kisha akiwambia mapagani juu ya nia yake ya kuhamia Madina, na aliwakaribisha kupambana naye kama walitaka watoto wao kuwa mayatima na wake zao kuwa wajane. Katika kutetea njia ya Uislamu, hapakuwa na mhanga uliokuwa mkubwa. Katika uhai wa Mtume (s.a.w.) alishiriki kwa ari kwenye vita vyake ambavyo Uislamu ulikabiliwa na alionyesha ushujaa wake. Zaidi ya ushiriki wake wa hali katika vita, pia alitoa mchango mkubwa wa mali yake katika vita. Masoud (r.a.) anasema, Kusilimu kwa Umar ulikuwa ushindi kwa Uislamu; kuhajiri kwake kulieneza ufanisi wake na ukhalifa wake ulikuwa ukarimu. (Al-Hadithi). Ukhalifa: Mnamo mwaka 13 A.H., Abubakar (r.a.) aliugua, na ilipofahamika kuwa maisha yake yalikaribia ukingoni, alikabiliwa na jukumu zito la kumchagua mrithi wake. Alimteua Umar (r.a.) kama kiongozi badala yake alisema: Ndugu zangu katika Imani, sijamteua yeyote miongoni mwa ndugu zangu (wa damu) au jamaa zangu kuwa Khalifa. Nimemteua mtu ambaye anafaa miongoni mwenu. Je. Mnamthibtisha? Bila shaka, ndiyo. Walipiga kelele hadhara iliyokuwepo pale. Huu ulikuwa uchaguzi wa Umar kuwa Kahalifa. Kuenea kwa Uislamu chini ya Umar Al-Farooq (r.a.): Wakati wa Mtume (s.a.w.) Uislamu ulienea sehemu za mbali ya Arabia. Kabla ya ustawi wake, Mtume (s.a.w.) alifariki dunia. Abubakar (r.a.) Khalifa wa kwanza aliimarisha dola Arabia lakini kabla ya kueneza dola iliyo madhubuti Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uajemi na sehemu ya Ulaya, naye aliondoka kukutana na Muumba wake. Hata hivyo nia ya upanuzi wa baadaye ilikuwa wazi Umar aliachiwa kumalizia utekaji wa shehemu zilizo salia. Syria ilikuwa ya kwanza kushuhudia mapambano ya k i j e s h i . Ya k i f a n y w a n a Byzantines. Hawa kufikiria kuwa mpaka sasa jeshi lisilojulikana lingeweza kuwatoa nje ya himaya yao. Chini ya uongozi wa Khalid bin Walid (r.a.), Damascus ilizingirwa na ilibidi isalimu amri baada ya kuzingirwa kwa lengo la kutawaliwa kwa miezi sita. Madhila dhidi ya Waislamu yalikuwa makubwa lakini walifanikiwa kuangusha utawala wa Damascus, baada ya hapo miji ilianza kuanguka na kisha Syria yote, Palestine na Jordan zilifuata na kuwa chini ya Waislamu. Baada ya mfululizo wa m a p a m b a n o , Wa i s l a m u wakiongozwa na Khalid bin Walid, Mothanna, Abu Abeid na mwisho Saad bin Abi Waqaas (r.a.) jeshi kubwa la Uajemi lilipigwa hapo Cadesiya, mwaka 21 (A.H.) na ardhi yote yenye rutuba ya Iraq Magharibi mwa Tigris ilikuwa chini ya Dola ya Kiislamu. Mfalme wa Uajemi na vikosi vyake walikimbia Jiji lao kuu bila mapigano na Waislamu waliingia kwa ushindi miji mikubwa ya kifalme barani Asia. Kasri nyeupe ilitwaliwa na Waislamu na utajiri wake usio fahamika ulichukuliwa. Hili lilikuwa limekwisha bashiriwa na Mtume (s.a.w.) miaka mingi iliyopita. Kikundi cha Waislamu kitateka Kasri Nyeupe ya Mfalme wa Iran. Kuelekea Kusini, kampeni mahiri ya jeshi la Waislamu chini ya Amr bin Aas (r.a.) waliiteka Misri yote. Walipoiteka

Alexandria aliendelea kwenye Pwani ya Kaskazini ya Afrika mpaka ardhi ya Barbers Tripoli. Mafanikio haya ya Waislamu na kutwaa kwa haraka ardhi (nchi) za kistratejia kutoka kwa tawala imara, yaliupa utambuzi Ulimwengu kuwa ilikuwepo nguvu inayojitokeza ya Uislamu. kuwa zingeweza kwa wakati mmoja na kwa ufanifu, nguvu mbili kubwa za dunia kwenye mipaka miwili liliushangaza Ulimwengu. Mfanikio makuu ya majeshi ya Kiislamu yalitokana na ghera yao ya kidini, imani isiyo na mipaka katika njia yao, morali wa juu ya askari Waislamu, ni ujasiri mkubwa wa Makomando, usio na kifani. Juu ya yote kiongozi alikuwa mmoja wa Washindi, aliyepanga kampeni (mashambulizi)_ na mipango thabiti. Huyu ndiye Umar Al-Farooq (r.a.) Amirul Muminin. K i l a p a h a l i Wa i s l a m u walipopateka, walianzisha mtandao kamili wa Uongozi, Mahakama na Misikiti. Hapana yeyote aliyelazimishwa kuwa Muislamu. Hata hivyo, njia ya maisha ya viongozi wa Kiislamu, kwa mujibu na mafundisho ya Mtume (s.a.w.), yaliwavutia raia ambao sio Waislamu, ambao walisilimu kwa makundi. S a y y i d i n a U m a r ( r. a . ) aliwateua magavana wenye uwezo kutawala nchi alizozitwaa.

TANZANIA MUSLIM PROFESSIONALS ASSOCIATION


P.O. BOX 72045, Dar es Salaam, TANZANIA. TEL+255 0655 654900, +255 713 731300 Email: info@tampro.org Web: www.tampro.org

Sotele Islamic Secondary School is a registered (boys & girls) boarding & day seminary with registration No.701. The school is located at Sotele Mkuranga district, Coast region. The school is inviting applications from qualied, dynamic, energetic, dedicated, experienced and performancedriven candidates from across East Africa to ll the vacancy below: 1. Headmaster(1 Vacancy) Qualications & Experience Muslim male, holding a Bachelor or Masters Degrees, preferably with Education, with proven experience of not less than 5 years in school/college leadership position. Strong communication and writing skills Ability to work independently Ability to work effectively to deadlines, in a team and sometimes under pressure Successful candidate will be result oriented, able to take lead and work without supervision. Basic working knowledge of computers will be an added advantage. Duties and Responsibilities The selected candidate will be responsible to perform all duties of a Head of the school To effectively oversee the academic and general administration of the school To ensure and take care of all matters pertaining to welfare of the school To represent the school to all outside education and legal issues Applications must include each of the following to be considered: Hand written and duly signed letter of application Current resume or curriculum vitae Photocopies of certicates and academic transcripts Letters from two referees Applicant current mailing address, contact telephone number(s), and e-mail address Interested candidates should submit their applications by hand (Head ofce), registered mail/ courier service or e-mails to: Secretary General Tanzania Muslim Professional Association (TAMPRO) P.O. Box 72045. Dar-es-Salaam E-mail: pmwinyimvua@yahoo.co.uk or suke75@yahoo.com So as to reach him by 30th November 2012. Only successful applicants will be contacted for interview.

SOTELE SECONDARY SCHOOL JOB VACANCY

Makala

Uwazi wa mambo juu ya mawasiliano kati ya Uislamu na wengine

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA

NOVEMBA 1-7 2012

AN-NUUR

Dr. Samir Mahmoud SHUKRANI zote anastahiki Mwenyezi Mungu na rehema na amani zimkie mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Ama baada ya utangulizi huu (tunasema kuwa), Uislamu umetofautisha kati ya Imani na kutendeana mambo kwa maana ya kuhudumiana. Na kwa hivyo kwa wale wasio Waislamu hapana budi kutofautisha kati ya mambo mawili haya ambayo ni muhimu. Jambo la kwanza ambalo ni Imani, yeye atakuwa na imani yake na dini yake, na mimi nina imani yangu na dini yangu. Jambo la pili ni huduma Kuhudumiana na kwa upande huu umeniruhusu mimi Muislamu kushirikiana na yule ambaye si Muislamu, bali umeniamrisha nisaidiane pamoja nae katika upeo wa wema na upole na msamaha na haya ndiyo yaliyokuja katika Qur ani tukufu na hadithi za Mtume zilizo sahihi. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu, Hakika

juu ya wale wasiokupigeni vita katika dini na wala hawakutoeni katika miji yenu, kuwafanyia wema kwao na kuwafanyia usawa wao kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao usawa (uadilifu) ama katika hadithi tunakutana na mambo mengi:1. Mtume aliishi na Mayahudi mji wa Madina

ubavu kwa ubavu na akawekeana na mikataba mbali mbali na akahimiza wafuasi wa dini hii kuheshimu ahadi hizo na kuacha kuzivunja mayahudi. 2. Kusaidiana na asiye Muislamu na pia ni mwenye kuupiga vita Uislamu; hii ilionyesha wazi katika msafara wake Mtume (S.A.W) kutoka Makka kwenda Madina,

kwani alimchagua mtu ambaye si muislamu ili awe msindikizaji wao njiani. 3. K u w a t e m b e l e a ; Uislamu umeruhusu kumtembelea asiye Muislamu na kumuona na pia kuwa na mawasiliano nae. Anasema Asmaa Bint Abubakar Swidiki (alikuja kwangu mama yangu naye akiwa si muislamu. Nikasema sitampokea hadi

nipate ruhusa kwa Mtume (S.A.W) nikasema, Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, amekuja kwangu mama yangu naye si muislamu jee nimuunge mama yangu? Kwa maana ni mpokee? Akasema ndiyo muunge mama yako ewe Asmaa. Amesema Mwenyezi Mungu, Na watakapokulazimisha katika kunishirikisha mimi na kitu ambacho hukijui usiwatii na ishi nao duniani kwa wema. 4. Umeruhusiwa kuoa mwanamke wa waliopewa kitabu na hiki ndicho kipimo kikubwa juu ya mahusiano na kuhurumiana ni pale anapomuoa muislamu mwanamke ambaye si muis lamu na akabariki katika dini yake na bila ya kulazimisha kuacha dini yake bali ataendelea na dini yake hiyo. 5. Kuuza, kununua, kuweka rehani na hudumua nyingine. Pia uislamu umeruhusu huduma nyingine kwa asiye muislamu kama vile kununua, kuuza na kuweka rahani na huduma nyingine kwa hakika amekufa Mtume (S.A.W) na kanzu yake ya chuma ipo rehani kwa myahudi mmoja. Huu ndio Uislamu unaolingania juu ya mahusiano mema na kuhurumiana na ujirani mwema kwa muislamu na kwa asiye muislamu.

Vianzio halisi vya harakati ya Boko Haram


wamefukuzwa kasi kwa mauaji ya kiongozi wa Boko Haram. Kwa vile serikali iliamua kufanya mazungumzo kwa risasi na mabomu, Boko Haram ikaingia mafichoni. Ilichukua muda kuganga majeraha yake, wakajumuika na kupanga mikakati kabla ya kuanza kulipa kisasi ya kile Imam Shekau anasema ni Utovu wa Haki dhidi yake. Ikitafuta kulipizia, Boko Haram ililenga polisi, jeshi na wanasiasa jimboni. Ilipotokeza 2010, Boko Haram ilianza kwanza kuwafyeka watu waliosaidia watawala kuwatambua. Waliouawa mapema walikuwa watawala wa jadi mitaani, wote Waislamu, wanaoitwa Lawani katika jimbo la Borno. Kati ya wanaofahamika zaidi katika wimbi hilo la mauaji ni mdogo wa Shehu wa Borno, mwenyekiti wa jimbo wa chama tawala na mgombea wake wa useneta katika uchaguzi mkuu uliopita. Baada ya kuua wachache wa kwanza, Boko Haram ikatoa onyo kuwa itawatafuta wote

Inatoka Uk. 6

waliowasaidia watawala kuwapiga vita. Hii ni pamoja na ulamaa kadhaa, watawala wa jadi, na gavana wa majimbo matatu ya Borno, Gombe na Bauchi. Ikataka kuombwa radhi na magavana wa majimbo hayo na ikaombwa radhi na wale wa Gombe la Bauchi. Mara baada ya kundi hilo kuanza mauaji ya kuchagua, Ulamaa (Viabaraka wa serikali) wakahofia usalama wao na hakuna hata mmoja aliyejaribu tena kuwalaani hadharani au kuwataja kifedheha. Wakati mmoja Boko Haram wakatoa onyo kwa yeyote ambaye atalaani hadharani vitendo vyake, ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari wasiofuata maadili kuwaandika. Siku hiyo walipoanza mauaji yao mwaka 2009, serikali ya jimbo la Bauchi ilitaka na kupata fatwa kutoka kwa Ulamaa mjini hapo ambayo ilitumika kama leseni ya kuuwa wanachama wa Boko Haram bila kufuata mkondo wa sheria. Ni Sheikh mmoja tu mwenye umri mkubwa zaidi mjini hapo aliyepinga

fatwa hiyo, akisema kuwa katika Uislamu hakuna roho inayotolewa bila hukumu ya Mahakama, Jaji. Ndiyo maana baadhi ya Ulamaa walitoroka nchini wakati Boko Haram waliporudi mwaka uliofuata. Gavana pia ameondoka katika nyumba ya serikali na kimsingi amehamishia shughuli zake Abuja tangu alipopewa taarifa za kutishiwa kifo. Serikali imeshindwa kuwalinda walioipatia habari za wanachama wa kundi hilo na wananchi wengine dhidi ya mashambulizi hayo. Hii kwa upande mmoja inaeleza kwa nini Waislamu wako kimya kuhusu Boko Haram. Kwa hali yoyote ile, hakuna chochote kinachoweza kutetea mauaji ya watu wasio na hatia yanayofanywa na Boko Haram. Kundi hilo limetoka katika mstari na kuingia katika hali ya kuona kupingwa maoni yake ni kushambuliwa. Kwa kufanya hivyo, wanaingiza hofu katika hisia za jamii na kupoteza kuungwa mkono. Kutoa rai kwa wanachama wake kuweka silaha

chini na kuzungumza na serikali watajibu kuwa Tutawezaje kuamini mazungumzo na watu ambao wanakusanya silaha kutushambulia. Jean Herkovits, Profesa wa historia katika Chuo Kikuu cha Jimbo la New York nchini Marekani anasema Badala yake, asilimia 25 ya bajeti ya Nigeria kwa 2012 inaelekezwa katika usalama, licha ya kuwa jeshi na polisi kwa kawaida wanajibu mashambulio kwa utumiaji nguvu bila mpangilio na kuua. Bila shaka, kama wanavyosema Wanigeria wengi niliozungumza nao katika eneo la Kaskazini Mashariki, jeshi linaogopeka zaidi kuliko Boko Haram. Wanigeria wenye ushawishi mkubwa mjini Maiduguri, ambako ni kitovu cha Boko Haram, waliitafadhalisha serikali ya Bw. Jonathan mwezi Juni na Julai wasiijibu Boko Haram kwa matumizi ya nguvu pake yake. Hakuna chochote, aliwahi kusema Katibu Mkuu wa Umoja

wa Mataifa baada ya kupigwa bomu Osi Kuu za Umoja wa Mataifa mjini Abuja mwaka jana, ambacho hakiwezi kutatuliwa kwa mazungumzo. Serikali ni lazima ikubali kuwajibika kikamilifu na kuanza mchakato wa kumaliza mzozo na kuingia tena miongoni mwa jamii (kwa wanachama wa Boko Haram). Jamii ya Kiislamu kwa jumla lazima iendelee kulaani mauaji haya yasiyo na msingi na kuchunguza shughulii za wana siasa kali zaidi vijana ambao hawana busara ya kuona vitu katika vivuli tofauti. Wanahitaji kuongozwa ipasavyo na viongozi wa vikundi vyao vya dini na mamlaka husika. Vinginevyo wataenndelea kutoka katika mstari unaofaa kijamii na kuingia taratibu hadi pale wanapokuwa wanaota dunia nzima ikiwa katika bahari ya damu ya binadamu. Bila shaka hii haitamfurahisha Mungu ambaye amejitambulisha kama Wa Huruma Nyingi. (Imefasiriwa katika Kiswahili na Anil Kija)

Uvamizi na dhuluma za Israel katika mji mtakatifu wa Qudsi


Hivyo basi, huo ukawa ndio mwanzo wa wavamizi hao kubadili alama za mji huo na kuweka za kwao kikamilifu kwa kujenga mamia ya makazi, huku wakifanya uovu wa kuchukua maeneo ya watu na nyumba zao zilizo karibu nao, hasa upande wa Milango Mikuu ya Mji Mkongwe. Ni wazi kabisa kwetu kinachotokea leo mjini Qudsi na katika Msikiti Mtukufu wa Aqswa, kutokana na miundo mbinu ya uharibifu kutoka kwa wavamizi, kwani Msikiti huo unashambuliwa kila siku na kufanyiwa njama ambazo hazijawahi kutokea. Mpango unaohusisha utawala wa Kizayuni na vikundi vya Kiyahudi vyenye msimamo mkali, pale wanapopanga mashambulizi dhidi ya Msikiti huo hadharani, ukiachilia mbali aina kadhaa za uharibifu wa ardhi, ikiwemo kufungua Makanisa ya Kiyahudi, kuwaingiza watalii bila ruhusa na kuzuia ukarabati wa Msikiti huo. Hakika uharibifu wa ardhi ufanywao na utawala wa Kizayuni karibu na Msikiti wa Aqswa, haulengi lingine isipokuwa ni kupotosha historia sahihi ya Mji Mtukufu na kuingiza Uyahudi wao. Jambo linalopelekea kila Mzayuni aonapo athari ya Kiislamu katika uchimbaji wake wa ardhi, hudai kuwa ipo katika eneo la hekalu la Kiyahudi. Lengo lao hasa la kufanya hivyo, ni kujaribu kuukinaisha ulimwengu kwamba athari zote za Kiislamu mjini Qudsi zipo katika eneo la Kiyahudi, jambo ambalo halipo wala halitokuwa na ukweli wowote. Vilevile wavamizi hawa wa Kizayuni, wanaendeleza mpango wao mbovu wa kugeuza alama za mitaa na maeneo mengine ili zitajwe zao hapo baadae katika historia kiudanganyifu. Pamoja na ripoti ya hivi karibuni ya wataalamu wa mambo ya kale kutoka Israel kusema kuwa, hawakugundua athari yoyote ya Kiyahudi mjini Qudsi inayothibitisha asili au uhalali wao katika ardhi hiyo ya Palestina. Hilo linatokana na uchimbaji wao katika maeneo kadhaa ya mji huo, lakini pamoja na ripoti yao hiyo, bado mtiririko wa uadui wa Kizayuni unaendelea hadi muda huu. Hakika vitendo viovu vinavyoendelea kama vile wizi na kadhalika, vinauweka ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu katika mazingatio makubwa. Huku mazingira hatarishi dhidi ya Msikiti wa Aqswa yakizidi kila siku, hali inayotilia mkazo kuwepo kwa

10

Makala

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA NOVEMBA 1-7 2012

AN-NUUR

WAVAMIZI wa Kizayuni siku zote wanajitahidi kuitumia fursa ya kitaifa na kimataifa katika kupitisha njama na amri zao mpya kwa kupotosha ukweli, kupitia uwekaji wao wa historia mpya ya mji wa Qudsi, suala la Palestina na mtazamo wa kidini wa wananchi, huku wakifumbia macho miaka elfu tatu ya historia ya Palestina. Wanafanya hivyo ili wakubalike kimataifa na hatimae kuungwa mkono katika mpango wao wa kutanua makazi ya Kiyahudi mjini Qudsi.

MJI wa Qudsi,
Qudsi, vipeperushi vinavyoitwa Mazuza, nao ni msamiati wa kidini unaomaanisha unyenyekevu kwa anayeingia, ambapo atavigusa kwa mkono kisha kuubusu huku akitamka maneno maalum. 7. Ubomoaji wa mambo ya kale uliofanywa na jeshi la Kizayuni ndani ya mwezi uliopita, eneo lililo chini ya Geti la Magharibi mjini Buraaq umesababisha mwanya mkubwa katika ukuta wa Magharibi. Si hivyo tu, bali jeshi hilo pia liliharibu njia ya Geti la Magharibi ambayo ni sehemu ya Msikiti Mtukufu mwa Aqswa. Hatua hiyo ilikiwa mnamo tarehe 9 Julai 2012. 8. Mpango wa ujenzi wa mji wa kitalii jirani na Msikiti Mtukufu wa Aqswa utaoelezea riwaya ya Kiyahudi kuhusu hekalu linalodaiwa, unalenga kutosheleza watalii milioni sita ifikapo mwaka 2020. Hatua itakayokwenda sambamba na ujenzi wa makumbusho ya Taurat kati kati ya mtaa Salwaan Kusini mwa Mji wa Kale. Hatua hiyo imekiwa mnamo tarehe 1/6/2012. 9. Ubomoaji wa nyumba nyingi za kale mjini Qudsi na maeneo yake hasa katika maeneo ya Sal-waan Kusini mwa Msikiti Mtukufu, ambapo inakadiriwa majengo hayo kuwa na umri wa miaka 100, ubomoaji huo umefanyika kwa madai yamejengwa bila ya kibali. 10. Kufuatia mpango wa kubomoa na kuhamisha watu unaotekelezwa na utawala wa Kizayuni katika maeneo ya mji wa kale na Qudsi, utawala huo unatupilia mbali ujio wa wachunguzi wa kimataifa ili kuchunguza hali hiyo nchini Palestina. 11. Jitihada endelevu za uvamizi dhidi ya wakazi wa Qudsi kwa kudanganya kununua maeneo matukufu ya kihistoria, kwa jina la mali za Kiarabu ili kubadilisha umiliki uwe wa Kiyahudi. 12. Pamoja na kuzidi kwa zoezi la ubomoaji wa Kizayuni nyumba za Wapalestina, pia kuna juhudi kubwa ya ujenzi wa makazi ya Kizayuni kwa lengo la kutanua ukoloni wao dhidi ya Wapalestina. Hatua hiyo ilishuhudiwa zaidi hivi karibuni mnamo kati ya tarehe 13/7/2012- 20/7/2012. 13. Kuzidisha kwa utawala wa Kizayuni uwekaji wa makaburi yao katika viwanja vya Msikiti wa Aqswa na Mji wa Kale, huku wakiyatoa makaburi ya kihistoria yaliyopo eneo la Maamani llah, huku wakiyapunguza makaburi ya Kiislamu yaliyopo Qudsi kwa kuyabomoa 200 mjini Maamani llah, kwa madai kwamba yapo chini ya utawala wa Kizayuni, kwa mujibu wa kanuni ya miliki ya waliopita. Hatua hiyo imekiwa tarehe 11/6/2012 14. Kugundulika kwa mpango wa Kizayuni unaolenga kutoa dola milioni 20 ili kujenga Kanisa la Kiyahudi jirani na Msikiti Mtukufu wa Aqswa, huku ukiwa mji wa Qudsi ndio wenye kipaumbele kwa Waisrael. Jambo lililowafanya watenge bajeti kubwa katika kuuboresha. Huku mpango huo ukienda sambamba na ujenzi wa makumbusho ya Kiyahudi itayogharimu mamilioni ya fedha, mji huo utaokuwa katika bustani ya Israel mjini Daawud. 15. Kuzidi kwa madai ya Kizayuni na taasisi za Kiyahudi kuhusu kubomoa Msikiti Mtukufu wa Aqswa ili kujenga Hekalu, huku mdai wa mwisho wa hilo akiwa ni mjumbe wa Kanisa Arbih ldaad, pale aliposisitiza kuwa ni lazima mpango huo utekelezwe bila kujali majibu ya kisiasa au ya kiulimwengu. Hakika uvunjifu huu wa haki za binaadamu ufanywao

RAIS Mahmoud Abbas wa Palestina


mpango maalumu wa Kizayuni wa kueneza Uyahudi katika mji mtukufu pia kuubomoa Msikiti huo. Kwani Msikiti huo, umeshuhudia na unashuhudia uvunjifu mkubwa wa athari zake za kale ufanywao na Wazayuni, jambo lililoifanya Wizara husika ya Palestina kutaja baadhi ya uvunjifu mkubwa uliofanywa tokea mwanzoni mwa mwaka huu kama ifuatavyo: 1. Ripoti ya Meya wa Qudsi kiuvamizi, kuhusu kubadili viwanja vya Msikiti Aqswa kuwa vya wazi, ili kuruhusu wakazi wa Kiyahudi na watalii kuingia muda wowote. Hatua hiyo imekiwa mnamo tarehe 01 Agosti 2012. 2. Tangazo la Yahuda Fainshtain ambae ni Mshauri wa serikali ya Kizayuni ya Israel nyanja ya sheria, kwamba eneo la Qudsi ni sehemu ya nchi yake inayojumuishwa katika mpango wa ujenzi wa makazi pia kanuni ya mambo ya kale. Hatua hiyo imekiwa mnamo tarehe 16/07/2012. 3. Utawala wa Kizayuni umebomoa majengo kadhaa ya kihistoria katika eneo la Saahatil Buraaq lililopo jirani mwa Msikiti wa Aqswa, yaliyojengwa tokea zama za Umawiya, Abbasiya na Othmaniya, kwa lengo la kuweka kituo cha Kiyahudi kikubwa chenye ghorofa tano, kitachoitwa Jengo la Asili ya Mubkaa. Hatua hiyo imefikiwa mnamo tarehe 30 Juni 2012. 4. Utawala wa Kizayuni wa Israel ulianza kutekeleza ujenzi mpya katika eneo la mbali Kusini Magharibi ya eneo la Sahatul Buraaq, kwa kumwagilia ardhi ya Baatwun, huku wakipanga kujenga vyoo na bafu 20 kwa watakaozuru eneo hilo. Hatua hiyo imekiwa mnamo tarehe 12 Julai 2012 5. Muendelezo wa uvamizi wa jeshi la Israel waliovalia rasmi kijeshi, katika viwanja vya Msikiti wa Aqswa, ambapo uvamizi wa mwisho ukifanyika tarehe 29 Julai 2012 huku wakizuia Wapalestina kuswali, hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. 6. Kutungika vipeperushi vya Kizayuni katika Milango Mikuu ya Mji Mkongwe wa

Inaendelea Uk. 11

11
Na Jean Herskovits

Makala

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA

NOVEMBA 1-7 2012

AN-NUUR

(Imewekwa kwenye mtandao: Januari 5, 2012) SERIKALI na magazeti kote duniani walielezea upigaji mabomu siku ya Krismasi (2011) wa makanisa nchini Nigeria kwa Boko Haram, kundi kivuli ambalo kila siku linasemekana ni la Waislamu wa siasa kali waliojichimbia katika ncha ya Kaskazini Mashariki ya Nigeria. Na kweli, tangu aapishwe mwezi Mei Rais Goodluck Jonathan, Mkristo kutoka jimbo la Niger Delta Kusini ya nchi hiyo, Boko Haram imelaumiwa kila kulipotokea mapigano na umwagaji damu nchini Nigeria. Lakini vyombo vya habari na wasimamizi wa sera wa Marekani wanafukuzia tishio ambalo halikamatiki na halifahamiki kiyakinifu; hakuna uthibitisho kuwa kundi lenye mfumo halisi, lenye mtazamo unaoeleweka kiitikadi linaloitwa Boko Haram kuwa lipo. Ushahidi unaoanyesha kuwa pamoja na kuwa wafuasi wa awali wa kundi hilo bado wapo katika harakati, makundi ya kiharamia yamechukua jina Boko Haram kutangaza kuhusika na mashambulizi pale inapowafaa. Marekani haitakiwi kujiingiza katika vita dhidi ya ugaidi vya Nigeria - uwe ni ugaidi kweli au udakuzi - ambao utaifanya Marekani ionekane inampendelea Rais Mkristo. Kujiingiza katika ugomvi wa kijamii unaopanuka ambao unahatarisha umoja nchini humo, kunaweza kuwageuza Waislamu nchini Nigeria dhidi ya Marekani bila kuanza kufanyika kazi hata moja kati ya matatizo makubwa yanayochochea kuvurugika utengamano na

Nigeria: Tatizo siyo Boko Haram

Uvamizi na dhuluma za Israel katika mji mtakatifu wa Qudsi


Inatoka Uk. 10 na utawala wa Kizayuni wa Israel, ni sehemu ndogo sana ya yale uyafanyayo dhidi ya mji wa Qudsi na Msikiti Mtukufu wa Aqswa. Kibaya zaidi ni ule uchimbaji wa maeneo ya Msikiti huo na yale ya jirani. Msikiti Mtukufu wa Aqswa leo upo katika hatari kubwa ya kutoweka, endapo Waislamu na Waarabu hawatosimama kidete kuuhami, watafanikiwa Wazayuni lengo lao la kuweka makazi yao. Hivyo basi, kufuatia mkakati huo Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Palestina inatilia mkazo mambo yafuatayo: 1.Yafanywayo na utawala wa Kizayuni wa Israel, yanalenga kuingiza Uyahudi na kuudhibiti mji wa Qudsi na hata ule uchimbaji wa maeneo jirani yake haulengi sekta ya kielimu bali ni ya kisiasa, ili kumdhoofisha mkazi wa Kiarabu. 2. Harakati zote hizi zifanywazo na utawala wa Kizayuni mjini Qudsi, ikiwemo kubadili alama za Kiarabu kwa kutumia gharama kubwa, hazitofaulu kufuta asili ya Kiarabu na Kiislamu mjini humo, bali vyote vitabaki kama vilivyo vikielezea asili hiyo na kuzidi kupambana na uvamizi wa Kizayuni. 3. Hakika matendo haya ya Kizayuni ni kipimo tosha cha majibu ya Kiarabu na Waislamu, vilevile ukimya uliopo kutoka kwa Waislamu kwa kutoinusuru Aqswa yao, ndio unaohamasisha utawala wa Kizayuni kuendeleza uovu wake dhidi ya Qudsi na vilivyomo. 4. Hivyo basi, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Palestina, inaziomba taasisi zote za kitaifa na kimataifa

Rais Goodluck Jonathan kukua kwa mifarakano ya matishio na taarifa zinazodai kidini nchini Nigeria. kuhusika na mashambulizi. Cha Mwezi Agosti, pale Jenerali kushangaza ni kuwa serikali ya Carter F. Ham, kamanda wa Nigeria na mashirika ya habari Vikosi vya Marekani kwa ya kimataifa vinaonekana A f r i k a , a l i p o o n y a k u w a kukubali tu anachosema. Boko Haram ina uhusiano na Mwisho wa mwezi wa makundi yanayoshabihiana Novemba, kamati ndogo na Al Qaeda, taswira ya tishio ya Kamati ya Baraza la imeongezeka. Mara baada ya Wawakilishi ya Usalama wa onyo la Jenerali Ham, Makao Ndani ilitoa taarifa ya kustusha Makuu ya Umoja wa Mataifa na kuchokoza yenye kichwa mjini Abuja yalilipuliwa, na cha habari: Boko Haram: maelezo rahisi ya kulaumu Hatari inayoinuka kwa usalama Boko Haram kwa mkasa wa ndani Marekani. Taarifa unaozidi kuongezeka wa hiyo haionyeshi kinagaubaga uslama nchini Nigeria ikawa vipi hali hiyo imekiwa, lakini jambo la kawaida. Mtu anayedai hata hivyo inatoa rai ya kuwa kuwa ni msemaji wa Boko kundi hilo liongezwe katika Haram - mwenye jina ambalo orodha ya makundi ya kigaidi hakuna anayelijua na ambaye ya nchi za nje. Idara ya Afrika hakuna aliyewahi kumfahamu ya Wizara ya Mambo ya Nje au kukutana naye - ametoa ya Marekani inapinga rai hiyo,

kusaidia kuulinda urithi huu na mji mzima wa Qudsi, kutokana na uadui pia uvunjifu wa haki za binaadamu unaofanywa na Wazayuni dhidi ya maeneo hayo na vilivyomo. 5. Wizara pia inashangazwa na ukimya wa UNESCO wakati vitendo hivi vya uadui na uvunjifu wa haki za binaadamu vikiendelea waziwazi, hivyo tunaiomba ichukue nafasi yake katika kuyahami mambo ya kale mjini Qudsi na kusitisha matendo yote ya kivamizi mjini humo. 6. Vilevile Wizara inauomba umma wa Kiarabu na Kiislamu popote walipo, kabla muda haujakwisha, kuharakisha kuuhami Msikiti Mtukufu wa Aqswa, kutokana na tamaa za kivamizi. (Habari hii imetolewa na Kituo Cha Habari cha PalestinaTanzania)

lakini shinikizo la Bunge na mamlaka kadhaa za serikali linaongezeka. Boko Haram ilianza mwaka 2002 kama kundi la amani lililojitenga. Halafu wanasiasa wakaanza kulitumia kwa maslahi yao ya uchaguzi. Lakini ni pale tu mwaka 2009 ambako Boko Haram iligeukia utumiaji nguvu, hasa baada ya kiongozi wake kijana mhubiri wa Kiislamu aitwaye Mohammed Yusuf, alipouawa akiwa ameswekwa rumande. Nakala ya mahojiano kati yake na polisi inawekwa katika mtandao, lakini hakuna aliyeshtakiwa na kuadhibiwa kwa jinai hiyo. Wakitaka kulipiza, Boko Haram iliwalenga polisi, jeshi na wanasiasa wa jimboni - wote Waislamu. Ilikuwa wazi mwaka 2009, kama ilivyo sasa, kuwa chanzo cha machafuko na hasira iwe ni Kaskazini au Kusini ya Nigeria, ni umaskini wa kutupwa na kukosa matumaini. Raia wa Nigeria wenye ushawishi mkubwa kutoka Maiduguri, ambako Boko Haram ina maskani yake, waliiomba serikali ya Bw. Jonathan mwezi Juni na Julai isifuatilie suala la Boko Haram kwa mabavu peke yake. Pia, balozi wa Marekani Terence P. McCulley amesisitiza, kipekee na matamshi ya wazi, kuwa serikali lazima itazame ufukara kijamii na kiuchumi ulio mkali zaidi maeneo ya Kaskazini. Hakuna anayeonekana kusikiliza. Wakati huo huo, Boko Haram imegeuka kuwa kampuni mwavuli yenye makundi ya kiharamia yanayojipachika jina lake. Ikionyesha hali hiyo, Idara ya Usalama wa Taifa ya Nigeria ilitoa taarifa Novemba 30 ikiorodhesha wanachama wa makundi manne ya kihalifu ambayo yanapeleka vitisho kwa njia ya simu kwa kutumia jina la Boko Haram. Wanigeria wa Kusini - siyo Waislamu wa Kaskazini - walikuwa wanaendesha vikundi vitatu kati ya hivyo vinne, ikiwa ni pamoja na kile kilichosababisha ubalozi wa Marekani na balozi nyingine za nje kutoa maonyo yaliyosomba wageni wote kutoka mahoteli ya hali ya juu Abuja. Na hivi karibuni vikosi vya usalama vilimkamata Mkristo kutoka Kusini ya Nigeria akiwa amevalia Kiislamu akiwa anawasha moto kuchoma kanisa katika eneo la Delta, miingilio ya mto Niger, Nchini Nigeria, ugaidi wa kidini una sura tatanishi. Haya yote hayaondoi lawama kwa vitendo vya Boko Haram vya kuua watu wasio na hatia. Lakini inaleta maswali kuhusu uharaka wa kutoa maamuzi ambayo yanaficha ugumu na mkanganyiko wa hali halisi nchini Nigeria.

Wanigeria wengi tayari wanaamini kuwa Marekani inaunga mkono serikali ya Bw. Jonathan bila mashariti, licha ya maeneo yake ya upotofu. Wanaamini hivi kwa sababu Washington ilisifu uchaguzi mkuu wa April ambao waangalizi wa kimataifa waliona kuwa unaaminika, lakini Wanigeria wengi, hasa wa Kaskazini, hawakuona hivyo. Pia, misaada ya Marekani kwa majeshi ya usalama ya Nigeria, licha ya vitendo ambavyo vimenakiliwa vya uvunjaji wa hali za binadamu, pia inakasirisha Waislamu Kaskazini. Vitendo vya Bw. Jonathan vya hivi karibuni havijasaidia lolote. Aliwaambia wananchi wa Nigeria majuzi kuwa Suala la kulipua ni moja ya mizigo ambayo itabidi tuikubali. Katika mkesha wa mwaka mpya, alitangaza hali ya hatari katika maeneo ya majimbo manne ya Kaskazini, iliyosababisha kuongezeka kwa shughuli za kijeshi katika eneo hilo. Na siku ya mwaka mpya, aliondoa ruzuku ya bidhaa za mafuta, hivyo kuongeza bei ya mafuta mara mbili. Katika nchi ambayo asilimia 90 ya wananchi wanaishi na kipato chini ya dola mbili za Marekani kwa siku, hasira inapanda nchini kote wakati gharama za usari na chakula zinapanda kwa kasi ya kustaajabisha. Tangu kurudi kwa Nigeria katika utawala wa kiraia mwaka 1999, wanasiasa wengi wametumia mifarakano ya kikabila na kanda, na mbaya zaidi, dini, kwa mahitaji yao binafsi. Waislamu wa Kaskazini - na hata Wanigeria wote kwa jumla - wanataka kwa hisia kali serikali ambayo itatimiza mahitaji yao ya msingi: usalama binafsi na matumaini ya kuinuliwa hali ya maisha. Wanachukizwa na sera za serikali na matumizi ya fedha ambayo yanakwamisha mahitaji yote mawili. Marekani isijiruhusu kuingizwa katika mchanga kuzama wa kuilenga Boko Haram peke yake. Watawala Marekani tayari wanaonekana n a w e n g i w a Wa i s l a m u Kaskazini -wakiwemo wale ambao kwa miaka mingi wana hisia changamfu kuhusu Marekani - kuwa wanamuunga mkono rais wa Kikristo kutoka Kusini. Marekani ni lazima ijitahidi kuondoa taswira ya unabii unaojitimiza utakaoifanya Marekani kuwa adui yao. Kuiweka Boko Haram katika orodha ya makundi ya kigaidi kutagandisha hisia kama hizo na kuwafanya Wanigeria wengi zaidi kuiogopa na kutokuiamini Marekani. (Jean Herskovits, Profesa wa historia katika Chuo K i k u u c h a N e w Yo r k , Purchase, ameandika kuhusu siasa za Nigeria kuanzia mwaka 1970. Makala hii ilichapishwa kwanza na gazeti la New York Times. Imefasiriwa na Anil Kija)

AN-NUUR
12
Na Mwandishi Wetu

Dhuul-Hijja 1433, IJUMAA NOVEMBA 1-7, 2012

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa na Jumanne


kibinadamu. Huyu kijana wetu tumemkuta ametobolewa katika sehemu ya kichwa kwa kutumia kitu chenye ncha kali, ametobolewa sehemu ya bega, ametobolewa sehemu ya ubavuni, ana uvimbe ambao una rangi nyeusi, ana uvimbe sehemu ya mgongoni, mguuni unaonyesha amepigwa kipigo kilichosababisha uvimbe ule. Majeraha hayo yanaweza kuwa sababu ya kifo chake, Polisi wametuulia halafu wanasema hakufa kwa kipigo, majeraha aliyokuwa nayo yanatosha kuwa sababu ya kifo chake, alisema mwanafamilia huyo. Akifafanua zaidi alisema kuwa viongozi wanazungumza kuwa watachukuliwa hatua kwa yeyote atakayevunja amani, kitendo walichokifanya Polisi ni cha kusikitisha na serikali imesema yeyote atakaevunja sheria atachukuliwa hatua za kisheria. Kwa kuzingatia kauli hiyo ya serikali akasema: Tunaiomba Serikali kuwachukulia hatua wale askari ambao wamefanya kitendo cha mauwaji wakamatawe kwani serikali imesema atakaevunja amani akamatwe, basi na hawa waliouwa tunataka wachukuliwe hatua za kisheria. Kitendo walichofanya askari ni kitendo cha uvunjifu wa haki za binadamu hivyo hatuna imani na jeshi la polisi. Alisema kwa masikitiko mwanafamilia huyo ambaye ameiomba serikali kuwa makini na suala la uvunjifu wa haki za binadamu kwani jeshi la polisi linahatarisha amani.

Polisi walipiga simu nikachukue maiti nikagoma kwa sababu wamemchukua mwanangu akiwa hai kwa hivyo nilitaka arejeshe hai na sio maiti, alisema Mzee Ali Kaimu. Kijana mmoja makazi wa Magomeni Unguja amefariki dunia akiwa mikononi mwa askari wa doria wanaosaka wahalifu, imeelezwa. Akizungumza na waandishi wa habari hizi baba mzazi wa kijana huyo Mzee Ali Kaimu amesema mwanawe aliondoka nyumbani kwenda kufungua ngombe ambapo alikutana na askari hao wakiwa kazini na kumchukua. Mzee Kaimu amedai kuwa alipomfuata mwanawe naye alipata kipigo kutoka kwa polisi hao wakiwa na wenziwao wa Vikosi vya SMZ. Manangu aliniomba shilingi 30,000 kwa ajili ya kununulia godoro na yeye mwenyewe alikuwa ni 20,000 kwa hivyo alikuwa ana jumla ya shiligi 50,00 ili akanunue gorogo lakini alipokamatwa nikajua wale askari watazichukua wao zile pesa na hawatazikisha kituoni kwa hivyo mimi nikazifuata ili anipe kwa kuwa aliniita baba njoo uchukue huu mzigo na nilipofika polisi wakanipiga kweli kweli, alisimuliza baba huyo wa kijana ambaye hivi sasa ni marehemu. Kijana huyo Hamadi Ali Kaimu mwenye umri wa miaka 20 mkaazi wa Magomeni alikamatwa na polisi Oktoba 26 mwaka huu majira ya saa 11 jioni na kufariki majira ya saa moja usiku . Mjomba wa marehemu anayejulikana kwa jina la Salim Mussa Omar

Mmemchukua yuhai mnamrejesha maiti?

Asema Baba wa kijana aliyeuliwa Polisi wakanusha kuhusika

Mzee Ali Kaimu baba wa Hamad (20) ambaye anadaiwa kupigwa na vyombo vya dola na kupoteza maisha mikononi mwa polisi.

amesema Hamad alikufa akiwa ndani ya vyombo vya sheria na kwamba alimuona wakati akiwa hospitalini akiwa na majeraha kichwani na michubuko sehemu mbali mbali za mwili wake. Hata hivyo, daktari mwenye dhamana ma hospitali kuu ya Mnazi moja Dakta Msafii Marijani ambae alimfanyia uchunguzi marehemu amesema katika uchuguzi wao hawakuweza kupata sababu ya kifo chake kuwa ni kipigo. Pamoja na kuwa ana michubuko mingi mwilini lakini si ambayo imesababisha kifo chake, kwa ufupi ripoti ya awali chanzo cha kifo hakijulikani maana hakuna jeraha

kubwa lililosababisha kifo kwani mara nyingi chanzo cha kifo ni kutokwa na damu nyingi...lakini huwezi kuwaridhisha wana familia maana wana familia wanasema mambo mengi lakini wataalamu wa afya ndio wenye kujua, alisema Daktari huyo. Uchunguzi wa mwisho wa daktari ni kuwa amepata michubuko katika sehemu mbali mbali za mwili wake lakini michubuko hiyo siyo iliyosababisha kifo. Kwa upande wa Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, amesema kuwa wao hawahusiki na kifo cha kijana huyo. Kamishna Mussa amedai kuwa Kijana Hamad ni kibaka na muhalfu

aliyekuwa akitafutwa na Polisi kwa kuhusika na kundi la kihalifu linaloendesha vurugu na uporaji la Ubaya Ubaya. Amesema, kipigo kilichosababisha kifo chake, alipigwa na vijana wenzake waliomtuhumu kuwa kawaibia simu na walichofanya Polisi ni kumuokoa asipigwe zaidi. Hata hivyo, baada ya kupokea tarifa kutoka kwa daktari aliyemfanyia uchunguzi, jamaa wa marehemu Mohamed Ali Idi ambaye alishiriki katika ukaguzi wa maiti hiyo alisema anasikitishwa na ripoti iliyotolea akisema kuwa japo inadaiwa kuwa ni ya kitalamu lakini si ya

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like