Professional Documents
Culture Documents
ISSN 0856 - 3861 Na. 1044 Dhuul-Hijja 1434, IJUMAA NOVEMBA 9 - 15, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Shari iliyokusudiwa ni kubwa mno, lakini. Wanaotamani kuona vurugu wataumbuka Sheikh Mataka, haya ya Askofu hujasikia? Uk. 6
Hakuna Kanisa lililochomwa Yombo Mishale, mikuki wanamwandalia nani? Labda somo la Rwanda bado halijaeleweka
HAYA ni Makanisa yaliyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa yamechomwa moto huko Yombo Dovya jijini Dar. Picha ya juu ni Kanisa la Faraja International lililopo mtaa wa Uwazi, Yomnbo Dovya. Picha chini ni Kanisa la Walokole lililopo katika mtaa wa Njia Panda kwa Kombo, Yombo Dovya.
kuwa taarifa hizo ni urongo na uzushi mtupu. Awali Maaskofu chini ya Umoja wao unaojulikana kama Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT) walitoa taarifa wakisema kuwa wamegundua mpango Inaendelea Uk. 4
2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
Tahariri/Habari
AN-NUUR
AN-NUUR
MAONI YETU
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste nchini Ta n z a n i a ( P C T ) , Askofu David Mwasota amewataka Wakristo kujihami kwa visu, mishale na mikuki ili kupambana na Waislamu. Askofu Mwasota amedai kuwa wana habari kuwa Waislamu wana mpango wa kuchoma makanisa nchi nzima na kwamba tayari kikosi kimoja kimetua Mbeya kwa kazi hiyo. Baadhi ya vyombo vya habari baada ya kusherehesha habari hiyo ya Askofu David Mwasota vikasema kuwa katika kutekeleza mkakati huo jijini Dar es Salaam, Waislamu walikuwa wameliteketeza kwa moto Kanisa la Kipentekoste la Faraja International Yombo Dovya, huku jingine la KKKT Yombo Dovya nalo likinusurika kuteketezwa na watu wanaojiita wanaharakati wa Kiislamu. (na kwamba) Mlinzi wa Kanisa hilo aliripotiwa kujeruhiwa. Ufuatiliaji wa karibu wa madai haya umebaini kuwa hakuna Kanisa lililochomwa moto Yombo kama ilivyodaiwa. Ni habari za kuzua. Kutokana na habari hizi za urongo, Wakristo wameambiwa na Askofu wao wajihami kwa visu, mishale, mikuki na silaha nyingine. Jaaliya katika mazingira haya anatokea kichaa tu anarusha kijinga cha moto kanisani au inatokea hitilafu ya umeme na kanisa linateketea kabisa, hali itakuwaje mitaani? Si jambo gumu kujua
hatari itakayotokana na uchochezi huu. Lakini maadhali wanaoleta uchochezi huu ni maaskofu, hilo hutasikia likisemwa. Maadhali wanaochochea chuki hizi za hatari za kidini ni Maaskofu, hutamsikia Mkuu wa Mkoa, Kamanda Kova na viongozi wa ngazi za juu wa kisiasa wakiwakemea maaskofu h a w a . Wa t a j i f a n y a hawajasikia. Lakini kwa bahati mbaya kabisa, hata Masheikh wetu wanaoona kuwa usheikh wao hauwezi kukamilika bila ya kuwashutumu mara kwa mara Waislamu wenzao ili waonekane na serikali/ maaskofu, kuwa wao ni waungwana; hutawasikia wakilani uchochezi , chuki na uhasama huu unazopandikizwa!!! Jambo moja Waislamu watie akilini: Maadhali maaskofu hawa wapo tayari kusema uwongo kuwasingizia Waislamu kuwa wana mpango wa kuchoma makanisa, hawataona vibaya pia kufanya lolote ili ile kauli yao kuwa makanisa yanateketea Yombo na Mbeya ionekane kuwa ni ya kweli. Ndio pale tukasema kuwa, wakipewa fursa kama ile ya maandamano na vurugu mitaani, wanaweza kuitumia kuchoma makanisa yao weneywe na kuwasingizia Waislamu. Ni katika mazingira haya yaliyopo hivi sasa, bado tunazidi kuwasisitiza Waislamu kutulizana na kujisaidia katika hali hii kwa Swala na Subra. Hautapita muda, wataumbuka waovu na uovu wao.
kuwavunja moyo wananchi ili wachukie serikali yao. Maalim Seif alisema kwa kuwa yeye ni kiongozi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa hangependa kumsema Rais wake hadharani, lakini kwa kuwa amefanya jitihada za kuwasiliana na kiongozi wake na kumueleza juu ya vitendo wanavyofanyiwa raia, lakini jambo la kusikitisha Dk. Shein hajachukua hatua yoyote ya kusimamisha vitendo hivyo. Kwamba bado wananchi wanaendelea kupigwa na kufuatwa majumbani kwa kisingizio cha kutafutwa wahalifu. Leo naongea kwa masikitiko makubwa, nina huzuni kubwa kwa mambo yanayofanyika hapa nchini kwetu na niseme ni mambo ya kishenzi kabisa wanaofanyiwa raia, alisema Maalim Seif. Rais wangu Dk. Shein unatungusha kwa kuwa wewe ndiye mwenye jukumu kubwa zaidi la kulinda amani ya Zanzibar. Alisema. Katika kumkumbusha Dk. Shein ahadi yake aliyoitoa siku ambayo anatangazwa mshindi na Tume ya Uchaguzi miaka miwili iliyopita, Maalim Seif alisema Dk Shein alichukua ahadi kwa Wazanzibari wote kwamba atawalinda rai wote bila ya ubaguzi na akachukua hadi kwa Mwenye enzi Mungu kwamba atailinda Zanzibar, basi namuomba Rais wangu mpenzi akumbuke ahadi yeke. Katika mkutano huo, Maalim Seif pia alisema mbali ya lengo la kuivuruga Serikali ya Umoja wa Kitaifa, lakini wahadhina wanafanya juu shini ili kuuharibu mshikamano wa Wazanzibari ambao kwa kiasi fulani ulikuwa umeonesha nia njema. Akizungumzia lengo la tatu la wahafidhina hao alisema ni kuogopa mchakato wa katiba ambao unaonesha dhahiri kwamba Wazanzibari wanapigania mamlaka kamili ya Zanzibar na kutaka Muungano wa Mkataba jambo ambalo ni mwiba kwa baadhi wana CCM na wahadhina. Katika hatua nyengine Maalim Seif aliitupia lawama Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kushindwa kuheshimu mawazo ya wananchi juu ya aina ya Muungano wanaotaka na kusema kwamba tume hiyo imekuwa ikiwalazimisha wananchi waseme kile ambacho wao wanakiamini. Maalim Seif alimshauri Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Warioba kuhakikisha kuwa Tume yake inaheshimu mawazo ya makundi yote, yakiwemo yanayotaka mabadiliko katika mfumo wa sasa wa Muungano. Awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho Salim Bimani alisema Wazanzibari wamechoshwa na vitendo wanavyofanyiwa vya kudhalilishwa na kupigwa bila ya hatia. Bimani alisema ni jambo la kusikitisha kuona hakuna hatua zinazochukuliwa licha ya vitendo hivyo kuripotiwa na kuonekana hadharani.
Habari
AN-NUUR
Baada ya hapo, inadaiwa kuwa Mkuu wa Shule alianza kuwakejeli Wanafunzi hao akisema maandamano yao hayakuwa na tija kwa kuwa hawakufika walipotarajia na kuwa wamejisumbua. Oktoba, 22, Mkuu huyo inadaiwa kusimama mstarini na kusema, anawashangaa wale ambao hawamtaki, huku akidai siku zote bosi huwa sahihi na atabaki kuwa sahihi, huku akiwalaumu kwa kitendo cha Wanafunzi wa Kiislamu kulalamika kwa Asa Elimu. Akiwa mstarini hapo, Mkuu huyo alinukuliwa akisema, kuwa suala hilo, ama zake ama zao, na kwamba atahakikisha ama anaondoka yeye ama hao wanaomlalamikia. Oktoba 23, ilikuwa ni siku ya kuapishwa viongozi wapya kama alivyopanga Mkuu wa Shule, ambapo Waislamu waligoma kufanyika kwa zoezi hilo kwa kuwa hawautambui uchaguzi huo, kwa kuwa ulipandikizwa chuki miongoni mwa wanafunzi. Mkuu huyo, alipuuza rai ya Waislamu, ambapo aliendelea na utaratibu wake na ilipoka wakati wa kuwaapisha washindi, mmoja wa wanafunzi wa Kiislamu aliipora karatasi ya kulia kiapo kutoka kwa mwanafunzi mwenzake na kuichana, na kuzua zogo. Baada ya tukio hilo, alika Asa Elimu (D.E.O), kiongozi wa Bakwata, Bagamoyo, kengele iligongwa ambapo Waislamu wote waligoma kwenda mstarini wakisema wanamtaka Mkuu wa Wilaya na si D. E. O, kwa madai aliwapuuza na hawajamuona toka alipoahidi kushughulikia tatizo hilo. Walisema, kufuatia msimamo huo, Mkuu wa Wilaya, Bw. Ahmed Kipozi, alika Shuleni hapo na kufanya kikao cha pamoja, ambapo Amir wa wanafunzi Shuleni hapo Abubakar Yusuph, akiongea kwa niaba ya wenzake, alisema wamechoshwa na mwenendo wa Mkuu wa Shule kwa kupandikiza chuki za kidini miongoni mwa wanafunzi kwa kuwahusisha na Alqaida. Alisema, Mwanafunzi Somji, aliweka wazi kuwa Mkuu huyo wa Shule ameshamtamkia mara kwa mara kuwa hampendi na hatompenda kwa vile ni Al Qaidah. Wanafunzi wa Kiislamu walitanabaisha kuwa hawana ugomvi na wenzao Wakristo Shuleni hapo kama inavyo vumishwa bali ni chuki tu zinazopandizwa na Mkuu wao na kuvuruga mwenendo wa upendo na umoja uliokuwapo kabla ya ujio wake. Kwa upande wa wanafunzi Wakristo miongoni mwao
Inaendelea Uk. 4
Habari
AN-NUUR
WAT U H U M I WA 3 7 waliokuwa wakishikiliwa mahabusu katika gareza la Segerea wameachiwa huru Jumatano mchana baada ya hakimu katika mahakama ya Kisutu Bi. R. M Nongwa kukubali dhamana kwa watuhumiwa. Watuhumiwa waliopewa dhamana baada ya kutimiza masharti ya udhamini ni Kuluthumu Mfaume, Zainabu Mohamed, Adam Ramadhani, Selemani Abdurahaman, Salum Mzee Juma, Halima Abbas, Maua Omar Mdumila, Fatihia Habibu Abdulrahman, Hussein Ally Hussein, Shabani Ramadhani Kondo, Rashid Ramadhani, Yusuf Athumani Penza, Alawi Mussa Alawi, Ramadhani Rashid Mlali, Omary Ismail, Salma Abdullatif, Said Rashid, Feiswari Abubakar, Issa Abdulwahabu, Ally Mohamed Mussa na Abdallah Haule . Wengine ni Juma Hassani, MwanaOmary Omari Makuka, Omar Bakari, Rashidi Omar Ndimbo, Hamza Ramadhani, Maulid Namdeke, Swalehe Maulid, Jumanne Mussa Msumi, Salum Abdallah Mohamed, Hamisi Halid Mfiyome, Dite Bilali Waikela, Amiri Said Idd, Juma Yasin Ally, Thumani Rashid Selemani, Abubakar Shabani na Ally Shabani Salehe. Hata hivyo mtuhumiwa namba moja ambaye ni Sheikh Ponda Issa Ponda bado yupo mahabusu kufuatia dhamana yake bado imefungwa. Aw a l i w a k i l i w a watuhumiwa Juma Nassoro aliiomba mahakama kuwapatia dhamana watuhumiwa kabla ya kutajwa tena hapo Novemba 15 baada ya kukamilika barua za wadhamini wa watuhumiwa hao. Kesi ya jinai namba 245 ya mwaka 2012 inayomkabili Ponda na wenzake itatajwa tena hapo
Novemba 15 mwaka huu. Sheikh Ponda na Wa i s l a m u w e n g i n e walikamatwa na Polisi baada ya kupinga kuuzwa kiwanja cha Bakwata kwa mtu binafsi cha Markaz Changombe jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Mara baada ya kupewa dhamana, Bi. Detention Bilal Waikella, ambaye ni mtoto wa mwanasiasa veteran maarufu mkoani Ta b o r a M z e e B i l a l Waikela, alidai kuwa
pamoja na kufunguliwa kesi na kuwekwa ndani, ataendela kudai haki stahiki za Waislamu dhidi ya madhalimu na kwamba anafauata nyayo za baba yake, ambaye naye aliwahi kuwekwa ndani kwa sababu ya kutetea maslahi ya umma tangu enzi za TANU. Alisema hata jina la Ditention, alipewa wakati baba yake akiwa amewekwa ndani na serikali ya Nyerere kwa sababu za kisiasa.
Inatoka Uk. 1
kuchomwa tunayafahamu, si kweli kwamba kuna kanisa lililochomwa na ni vyema umekuja mwandishi ukayaona. Alisema Bw. Shamte Mwegiro mkazi wa Yombo Dovya. Alisema kuwa baada ya kusikika habari za kuchomwa makanisa hayo hapo Dovya, taarifa ziliwafikia Wenyeviti wa Serikali za Mitaa minne ya Yombo Dovya ambayo ni mitaa ya Uwazi, Makangarawe, Dovya na Msalakala. Baada ya kupata taarifa hizo viongozi hao waliwafuata viongozi wa makanisa yaliyotangazwa kuchomwa moto pamoja na kutizama hali ya makanisa yenyewe. Taarifa zinabainisha kuwa baada ya kufika mtaa wa Uwazi lilipo kanisa la Faraja International, walikuta lipo salama. Walipomhoji muhusika juu ya kuripotiwa kuchomwa moto kanisa hilo, alijibu kuwa kanisa hilo halijaungua bali inaonekana kulikuwa na dalili za kuwepo hitilafu ya umeme. Viongozi hao walikwenda katika Kanisa la Walokole lililopo mtaa wa Njia Panda kwa Kombo, ambalo nalo liliripotiwa kuchomwa moto. Kanisa hilo lililojengwa kwa mabati na kuzungushiwa pazia, nako walilikuta ni salama. Walipohoji kulikoni kuenea habari za kuchomwa kanisa hilo, majibu yalikuwa ni moto uliokuwa umewashwa kuchoma taka zilizokuwa jirani na kanisa hilo, uliruka na kuchoma moja ya pazia la kanisa lakini uliwahiwa na kuzimwa na haukuleta madhara kanisani. Kufuatia uzushi huo, tayari viongozi wa misikiti Yombo Dovya hususan Masjid Swabrina, wametoa tahadhari kwa Waislamu kuwa makini kufuatia kuwepo propaganda za kuwapaka matope Waislamu kwa kuwazulia uhalifu.
Hata hivyo imefahamishwa kwamba yaliyotokea nchini Rwanda ndio yamekuwa m w a l i m u w a Wa i s l a m u kujihadhari na uzushi dhidi yao. Ila inavyoonekana ni kuwa wapo baadhi ya viongozi wa Makanisa, ambao bado somo la mauwaji ya Kimbari halijawaingia ndio maana wanaendesha propaganda za kuchochea chuki baina ya Waislamu na Wakristo. Uchochezi na uzushi uliofanywa na viongozi wa kanisa nchini humo ulisababisha maelfu ya raia wa Rwanda kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwa mtindo huo huo vyombo vya habari vya Kikristo, nanyo vimenogewa na staili ya Maaskofu wa Rwanda ya kueneza propaganda za uongo na uzushi ili kusababisha athari kubwa kwa watu wa imani nyingine kwa sababu ya chuki. Hivi karibuni Redio ya Kikristo ya Wapo na gazeti la Kikristo la Msema Kweli, viliripoti kwamba makanisa mawili huko Yombo Dovya yamechomwa moto na wanaodaiwa kufanya hujuma hiyo ni Waislamu. Huko nyuma iliwahi kuripotiwa kwamba kuna kiwanda cha majambia huko Mbagala, ambayo yalisadikiwa kuwa yatatumika kuleta vurugu wakati wa uchaguzi mkuu. Aidha vyombo hivi viliwahi kuripoti kwamba kuna kontena la silaha la CUF limeingia bandarini Dar es Salaam, na ilikuwa ni kipidi cha harakati za uchaguzi mkuu. Hadi leo hakijaonekana kiwanda hicho cha majambia wala kontena la silaha la CUF. Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste, Jean Uwinkindi, ni mmoja wa viongozi saba wa dini walioshitakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya
Kimbari ya Rwanda (ICTR) kwa kuongoza vitendo vya mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994. We n g i n e n i p a m o j a n a Askofu wa kanisa la Anglikana, mchungaji wa kanisa la Wasabato na Mapandre wanne wa Kanisa katoliki. Ni mmoja tu kati ya viongozi hao wa dini ndiye aliyeachiwa huru huku mwingine mmoja akifa kabla kesi yake haijaanza kusikilizwa. Uwinkindi alizaliwa katika wilaya ya Rutsiro, Magharibi ya Rwanda. Baada ya kuwa mwalimu wa dini nyumbani kwao alikozaliwa, alipandishwa hadhi na kuwa Mchungaji kwa kutoa huduma za kiroho katika mikoa ya Bugesera na Kibungo huko Rwanda. Wakati wa mauaji ya kimbari mwaka 1994, alikuwa Mchungaji Kiongozi katika parokia ya Kayenzi. ICTR inamshita kwa mauaji ya kimbari na uteketezaji kizazi kwa madai ya kusimamia au yeye mwenyewe kushiriki katika mauaji dhidi ya Watutsi. Alhamisi Aprili 19, mwaka huu, akawa ni mshitakiwa wa kwanza wa ICTR kuhamishiwa nchini Rwanda ambako kesi yake ndiko itakaposikilizwa. Askofu wa Kanisa la Anglikana, Samuel Musabyimana ni kiongozi wa ngazi ya juu kabisa wa kanisa kuwahi kushtakiwa na ICTR, lakini alikufa Januari 2003 kabla hata kesi yake haijaanza kusikilizwa. Alikana mashitaka yaliyokuwa yanamkabili ya mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu aliyodaiwa kufanya katika dayosisi yake ya Shongwe. Askofu huyo alitiwa mbaroni nchini Kenya, mwaka 2001. Naye Mchungaji wa Kanisa
Inaendelea Uk. 5
Haki itasimama tu
Habari
AN-NUUR
SHEIKH Farid Had akiwa katika karandinga la Polisi akirejeshwa rumande. Na Alghaithiyyah
SHEIKH Farid Hadi Ahmed amesema hakuna namna, lazima haki itasimama tu. Sheikh Farid alipaza sauti wakati akiingia katika karandika akisema kuwa, pamoja na vikwazo wanavyowekewa katika kupata dhamana, lakini haki lazima itasimama kwa sababu si katika maumbile kuchwa na ikachika. Amesema, maadhali wanasimama katika haki na maadhali wanapigania haki, batili haiwezi kushinda. Farid na viongozi wenzake saba wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar wanaokabiliwa na kosa uchochezi, juzi walipewa masharti magumu ya dhamana n a M a h a k a m a y a Wi l a y a ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja. Ni kutokana na mashariti hayo na madai mengine ya kunyimwa haki za msingi kwa mujibu wa katiba na sheria, Farid amesema kuwa yote hayo yanafanyika ili kuzima nuru ya haki, lakini juhudi hizo hazitafanikiwa. Hakimu wa mahakama hiyo alisema kuwa baada ya mahakama kupitia maelezo ya pande zote mbili imeamuwa kutoa masharti magumu kwa watuhumiwa hao wakitakiwa kuwasilisha kiasi cha shilingi 1,000,000 taslim kila mshitakiwa, pamoja na kudhaminiwa na wadhamini watatu kila mmoja wadhamini ambao kila mmoja ametakiwa kuwasilisha kiwango kama hicho cha fedha taslimu. Sambamba na masharti hayo, wadhamini hao pamoja na washitakiwa wenyewe wametakiwa kuwasilisha vivuli vya hati zao za kusaria (pass port) au vitambulisho vya Mzanzibar Mkaazi. Kwa mujibu wa mahakama, wadhamini hao lazima wawe ni wafanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) wawe na vitambulisho vya kazi pamoja na barua za Sheha wa Shehia wanazoishi. Wa s h i t a k i w a w o t e wamerejeshwa rumande chini ya ulinzi mkali wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuwa hata kama wangeweza kukamilisha masharti hayo ya dhamana, bado wangeendelea kuwepo rumande, kutokana na kukabiliwa na kesi nyengine katika mahakama ya Mrajis wa Mahakama Kuu Vuga, ambayo dhamana zao zimefungwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Ibrahim Mzee Ibrahim. Kesi ya Sheikh Farid na wenzake saba ilianza kutajwa Oktoba 19 mwaka huu, ambapo juzi ilikuwa ni siku ya kutoa mamuzi juu ya dhamana za watuhumiwa hao ambao wanadaiwa kutenda kosa hilo Agasti 17 mwaka huu, huko katika maeneo ya Magogoni Msumbiji wilaya ya Magharibi Unguja. Wa t u h u m i w a w e n g i n e wanaokabiliwa na shitaka hilo ni Sheikh Farid Hadi Ahmed (41) Mkaazi wa Mbuyuni, Msellem Ali Msellem (52) Kwamtipura, Mussa Juma Issa (37) Makadara, Azzan Khalid Hamdan (43) Mfenesini, Suleiman Juma Suleiman (66), Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) Mwanakwerekwe na Hassan Bakari Suleiman (39) Tomondo. Watuhumiwa hao wote kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 45 (1)(a) na (b) sheria namba 6 ya mwaka 2004 sheria ya Zanzibar. Imeelezwa mahakamani hapo kuwa, Agosti 17 mwaka huu, majira ya saa 11:00 za jioni huko Magogoni Msumbiji wilaya ya Magharibi Unguja, wakiwa ni wahadhiri toka Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu, walitoa matamko ya uchochezi yanayoashiria uvunjifu wa amani na kusababisha fujo, maafa mbali mbali na mtafaruku kwa Serikali ya Mapinduzi ya
l a Wa s a b a t o , E l i z a p h a n e Ntakirutimana, naye pia alikufa akiwa na umri wa miaka 83, Januari 2007, muda mfupi baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake ya kifungo cha miaka 10 jela. Kwa mujibu wa jamaa zake, alikuwa anaugua kansa kwa muda kwa miaka mingi. Alitiwa hatiani pamoja na mtoto wake wa kiume na daktari wa magonjwa ya binadamu, Gerard Ntakirutimana ambaye bado anatumikia adhabu yake jela, kwa kuhusika kwake na mauaji dhidi ya Watutsi katika eneo la kanisa lake la Mgonero, Magharibi ya Rwanda. Padre Athanase Seromba, ni mmoja wa Mapandre ambao wamewahi kushitakiwa na ICTR. Yeye anatumikia kifungo cha maisha jela nchini Benin kwa kuamuru tingatinga kubomoa kanisa lake la Nyange, Magharibi ya Rwanda katikati ya Aprili, 1994 ambapo wakimbizi
6
Na Omar Msangi NI kweli yawezekana aliyewaroga Watanzania huenda hayupo katika sayari hii kama kilivyosema kibozo cha gazeti la Majira la Jumamosi Novemba 3, 2012. Katika kibonzo hicho, msanii anaonyesha Tanzania ikilia njaa, ikinyosha mkono wa saidia masikini, huku imekalia madini, gesi na utajiri mwingine. Baada ya mamia ya maelfu, kama si mamilioni, ya tani za mchanga wenye madini kusombwa kwa miaka mingi tu kupelekwa nchi za nje, wiki hii ndio Waziri mwenye dhamana na madini anasema kuwa wapo katika mkakati wa kuandaa mchakato wa kuweka utaratibu wa kufanya uchunguzi kuona mchanga huo una madini aina gani ya thamani!!! (Rejea kipindi Dakika 45 kinachorushwa na ITV). Laiti ile hasira wangekuwa wanashushiwa wahujumu uchumi na mafisadi walafi wanaoifisidi nchi hii na kuibakisha masikini huku wao wakinenepeana. Laiti hiki kinachoonekana kuwa ni umakini wa vyombo vya dola ingekuwa unaelekezwa katika kuwatizama wanaoitwa wawekezaji wanaokuja kuwekeza katika madini na miradi mingine pakawa na mikataba mizuri ya kuifaidisha nchi! Laiti nguvu na hasira hizi za dola zingekuwa zinawashukia waliopewa madaraka ambao huwapa wawekezaji leseni na vibali vya kupora nchi bila kujali maangamizi wanayowasababishia Watanzania. Lakini kwa bahati mbaya kabisa, hasira hizi anashushiwa adui wa kubuni. Nguvu zilizopita kiasi zinazotumia rasilimia kubwa ya nchi, hufujwa kupambana na adui asiyekuwepo. Unajitisha mwenyewe unatishika, unapambana. Sawa na yule mtu anayejitekenya mwenyewe na kucheka. Yupo mzee mmoja alikuwa amejipumzisha mchana wa jua kali baada ya uchovu wa kazi. Sasa kila akitaka kulala, watoto waliokuwa wakicheza nje chini ya dirisha la chumba alimokuwa amelala, wanamghasi kwa makelele. Kila akiwafukuza, mara wamerejea tena. Yule mzee akabuni mbinu. Akatoka
Makala
AN-NUUR
7
Inatoka Uk. 6 kuwa Maosa wa usalama kikiwemo Kikosi cha Ulinzi c h a J e s h i l a Wa n a n c h i Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi na askari kanzu walionekana wakivinjari katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam. Nalo gazeti la Mtanzania likieleza hali ilivyokuwa mbaya likasema: JWTZ waingia mitaani..(kwamba) kutokana na vurugu (za Waislamu), Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), lililazimika kuingia mitaani huku askari wake wakiwa wamevalia kiraia. Kama askari hao walikuwa wamevalia kiraia, mwandishi wa Mtanzani aliwajuaje kuwa ni JWTZ? Anaeleza akisema kuwa: Mtanzania (gazeti) iliwashuhudia askari hao, huku mmoja wao akijikuta katika hali ngumu baada ya kitambulisho chake cha kazi kudondoka kutokana na vurugu hizo. Sijui kitambulisho changu kimedondoka wapi, ni cha jeshi maana duh sasa hii imeshakuwa kazi, ahaaa kumbe kipo katika soksi nimekibana. Alisikika askari huyo wa JWTZ akimwambia mwenzake. Akionyesha jinsi askari wa JWTZ walivyofanya kazi kubwa Mtanzania likashangaa na kuwasifu likisema kuwa: Katika hali ya kushangaza, askari wa JWTZ waliweza kufanya kazi ya ziada huku wakilazimika kutimua mbio kukimbizana na waandamanaji hao na kufanikiwa kuwatia mbaroni baadhi yao. Kwa waliokuwa Dar es Salaam Ijumaa iliyopita wanajua kuwa hapakuwa na maandamano ya Waislamu wala mabomu yaliyorindima. Hata taarifa ya Kamanda Kova inasema kuwa hao vijana 19 wanaodaiwa kukamatwa, walikamatwa wakiwa nje ya Msikiti wa Idrisa, sio wakiandamana. Na mabomu mawili matatu yaliyopigwa, hawakupigwa watu waliokuwa wakiandamana. Yalirushwa eneo la Msikiti wa Idrisa askari wakitaka waumini watawanyike haraka mara baada ya swala. Na waumini waliondoka. Tulipewa taarifa kuna vijana nje ya Msikiti wa Idrisa, nasi tuliwamrisha kuondoka, wakakaidi nasi tukawakamata. Hiyo ndiyo taarifa ya Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es
Makala
AN-NUUR
MAGARI ya jeshi yakiwa yamebeba askari wa jeshi hilo wakipita mitaa ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam Salaam, Suleiman Kova. Sasa hizi taarifa nyingine kwamba polisi walitumia mabomu ya machozi na risasi za moto kutawanya Waislamu waliokuwa wakiandamana zinatoka wapi? Lakini Waswahili wana msemo wao, njia ya mwongo fupi. Hata hao walioibuka na vichwa vya habari kuwa risasi za moto zilirindima kutawanya maandamano ya Waislamu, bado katika maelezo yao ukisoma wanasema kuwa, baada ya kikundi cha watu wa dini ya Kiislamu waliokuwa katika Msikiti wa Idris kuonyesha dalili ya kutaka kuanzisha maandamano ndipo Askari wa Jeshi la Polisi walipolazimika kufyatua mabomu ya machozi.
8
Inatoka Uk. 7 mkononi wakati akiendesha ibada bila kushtukiwa na waumini. Katika maelezo yake Padiri Buhembo hakueleza iwapo anajua Kiarabu kwa hiyo aliposoma, alifahamu kilichoandikwa au alikwenda kutafuta mkalimani baadae baada ya kumaliza Misa. Ila anachosema ni kuwa walimkamata na kumhoji lakini wakamuacha akaondoka bila ya kumdhuru! Kama hiyo haitoshi, uongozi huo wa Kanisa Katoliki Mwanza ukadai tena kuwa walikuja mabinti wawili waliovalia Hijabu na kutaka kuingia kanisani lakini wakazuiwa. Labda niulize tena, Masheikh wetu ambao kawaida yao imekuwa ni kushutumu tu Waislamu, taarifa hii ya Padiri Andreas, hawajaipata? Je, wanakubaliana na madai yake kuwa kuna Waislamu wamempelekea ujumbe wa kumtangazia kifo? Kama nilivyotangulia kusema, upo utamaduni mzuri tu ambapo Masheikh hukaa katika vikao pamoja na Maaskofu kuzungumzia masuala ya kinchi. Je, wameshakaa na kiongozi mwenzao huyu wa kidini na kumtaka atoe ushahidi wa madai yake haya? Au kimya chao kieleweke kuwa nao wanakubaliana na Padiri huyo kuwa kuna wasichana wa Kiislamu wanavamia Makanisa na hijabu zao (kufanya nini? Kuyalipua?) na kuwatumia ujumbe wa kifo mapadiri? Kwa maana hiyo tusubiri kuwasikia wakiibuka na kauli za kuwashutumu Waislamu kuwa waache kuwatisha mapadiri?!!! Ukitizama yale madai ya Askofu David Mwasota na haya ya Padiri Andreas Buhembo, kubwa wanachofanya ni kupiga propaganda ya kuwapakazia uovu Waislamu na hasa kujaribu kuisimika ikae na ikubalike kuwa nchini kuna kitisho cha Boko Haram kama ilivyokwisha kutajwa katika baadhi ya magazeti. Ukijua kuwa mengi ya makanisa haya ni yale yaliyoanzia Marekani au kufadhiliwa na taasisi za Kimarekani, matamshi ya Maaskofu hawa hayakupi shida sana. Lakini niseme yafuatayo, ili kupitisha sheria ya Patriot Act, ilibidi kitumike kitisho cha kweli cha shambulio la kimeta (Anthrax Terror Attack), wakafa watu saba wasio na hatia. Kitisho cha Al Qaida na Usam Bin Laden, kimeonekana kweli baada ya
Makala
AN-NUUR
MMOJA wa askari wakimkatama mama mmoja katika kamatakamata ya Polisi iliyofanyika Kariakoo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Septemba 11 ambapo watu sio kama kweli waliopiga u c h a w i w e n y e w e k w a takriban 4,000 walikufa. Kampla walikuwa Al Shabab wenyewe. Lakini wakati huo Uganda ilikuwa hivyo au la. Ila tu tusisahau kuwa walilokusudia lishatimia. Sasa labda kwa wale hivyo. Watu kama 70 hivi k a t i k a A n t h a x Te r r o r Watanzania wenye hamu ya walikufa ili kitisho cha Al A t t a c k w a l i t u a m b i a Shabab kionekane kuwa ni kuwa ni Al Qaidah, lakini kuona kitisho cha Waislamu real, cha kweli. Hapa hoja haukupita muda wakashikana kinakuwa real, cha kweli,
9
Said Rajab
NI vyema Serikali ikatambua wazi kwamba kukamata viongozi wa Waislamu kwa lengo la kuwafanya wasalimu amri, haitasaidia kuzima jitihada za Waislamu wa Tanzania kudai haki zao. Kwa kifupi hiyo inazidisha tu imani ya Waislamu na kuwafanya wawe madhubuti zaidi kupigania haki zao. Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na haya wanayofanya madhalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku ambayo macho yao yatakodoka (yatoke nje kwa hofu). Wawe wanakwenda mbio, vichwa juu, na macho yao hayapepesi, na nyoyo zao tupu Qur ( 14:42:43). Mfumo na muundo wenyewe wa dini ya Kiislamu ndiyo unaowafanya Waislamu wasikubali kudhulumiwa. Kama dhulma dhidi ya Waislamu itaendelea katika jamii yoyote ile, lazima atapatikana kiongozi madhubuti, aliye tayari kujitoa muhanga, ili kukomesha dhulma hiyo. Hilo ni jambo la kimaumbile tu. Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye aliyeumba maisha haya na akayewekea mfumo maalumu ambao hauwezi kubadilishwa hata kidogo, kama mwenyewe alivyobainisha ndani ya kitabu chake: Hii ni kawaida ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa kwa wale waliopita zamani; wala hutapata mabadiliko katika kawaida ya Mwenyezi Mungu Qur(33:62). Mahali pengine Mwenyezi Mungu anasema: Wala hutapata mabadiliko katika desturi yetu. Qur (17:77). Sehemu ya mfumo huu wa Mwenyezi Mungu ni mapambano baina ya Haki na Dhulma. Haitakuja kutokea duniani Haki ikavumilia Dhulma, wala Dhulma ikakubali Haki. Mapambano baina ya Haki na Dhulma yataendelea tu mpaka siku ya Kiyama, na yanaweza kuchukua sura mbalimbali kisiasa, kidini, kiutamaduni na hata mapigano. Ndipo wanapokuja watu madhubuti kama Sheikh Ponda Issa Ponda. Sheikh Ponda, mara zote amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za Waislamu Tanzania. Amepata misukosuko mingi sana kutoka serikalini kwa sababu ya msimamo wake usiyoyumba wa kupigania haki za Waislamu zinazodhulumiwa. Kuna baadhi ya watu, wengine ni ndugu zetu, wanamuona Ponda ni mtu hatari, anayepanga kuleta vurugu katika nchi. Wao ni vipaza sauti vya propaganda za madhalimu. Uhodari wao uko katika kukosoa tu harakati zinazofanywa na Ponda, lakini siyo wao kupanga harakati hizo! Waislamu wa Tanzania wanahitaji viongozi kama Sheikh Ponda Issa Ponda katika mazingira yaliyopo sasa. Yaani viongozi wakweli, waadilifu, wanaoweza kujitoa muhanga na walioungana kihisia
Makala
AN-NUUR
10
Makala
AN-NUUR
Na Khalid S Mtwangi
K U M E K U WA na malalamiko ya muda mrefu sana kuwa maendeleo makubwa ya Uislamu yamekuwemo katika miji mikubwa tu. Ni jambo la kusikitisha kuwa hata vile vijiji ama miji midogo iliyokaribu na miji hiyo mikubwa, nao wamesahauliwa. Huko nyuma katika gazeti hili kulitolewa mfano wa ustadh mmoja aliyetembelea kijiji kilichoko karibu ya Tabora ambako alishindwa kuendelea na swala ya L J u m a a k w a s a b a b u alivyokuwa akiboronga yule Imam ambaye ndiye alikuwa khatib pia. Hakika Tabora pamekuwa ni mji wa mashina ya Uislamu kwa muda mrefu sana na wapo Alim wengi tu hapo mjini. Shida ni kwamba hawa Alim wanajishughulisha na malumbano mijini na kujigamba nani kasoma zaidi ya mwenzake. Hali kama hiyo ya kusikitisha nayo inapatikana vitongoji vinavyizunguka Ujiji na Kigoma yote kwa jumla. Hakuna asiyefahamu sifa ya Ujiji katika nyanja ya ilm ya dini ya Kiislamu. Kwa sababu hiyo ni sawa kabisa kutegemea kuwa takriban mkoa wote wa Kigoma ungekuwa nao ni ngome ya Uislamu. Huko nyuma kulikuwepo wamishionari wa Kikristo kama aliyekuwa akijulikana kama Padri Yusufu wa pale misheni Kagera. Huyu alikuwa ni raki wa kila mtu pale Ujiji. Lilikuwa ni jambo la kawaida kabisa kumkuta kijiweni katika kundi la waSwahili naye akinywa nao kahawa na akipiga domo. Alikuwa akiijuwa lugha ya Kiha kuliko hata wale watu wa mjiji Ujiji. Alipofariki takriban mji mzima wa Ujiji ulihudhuria mazishi yake ingawa yalikuwa ndiyo yale ya Kikatoliki. Ni jambo la kujivunia kuwa mpaka alipofariki hakuwahi kumrubuni hata mtu mmoja, awe kijana ama mzee, aliyekubali kupotea
Hawa waislamu wa Uvinza wanahitaji misaada sana kwa sababu uwezo wa Waislamu na wenyeji wote kwa jumla ni duni sana. Wengi hujikimu kwa kufanya vibiashara vidogo vidogo tu ambavyo husaidia kupata chakula tu. Huko nyuma Uvinza palikuwa ni mapanda njia ya mizigo na watu kwenda Mpanda kulikokuwa na migodi ya dhahabu na madini nyingine. Kweli wakati huo uchumi wa Uvinza ulikuwa mzuri lakini hivi sasa wenyeji hujishughulisha sana na vibiashara vidogovidogo tu Kweli pana kiwanda cha chumvi ambacho kimekuwepo kikizalisha chumvi tangu wakati wa Utawala wa Kidachi (Jeremani) na hata wakati wa WaArabu. Lakini uzalishaji wa kiwanda hicho na ajira inayopatikana kutoka kiwanda hicho haikidhi kabisa kuendesha maisha bora ya wenyeji. Wameshindwa hata kuendeleza msikiti mdogo ulio Kibaoni ambaho ni kitongoji cha mji huo. Hali ya kimsikiti hicho ni aibu sana kwa vile jirani yake pana kituo kikubwa tu cha Kanisa Katoliki ambacho maendeleo yake ndiyo yanaaibisha nguvu ya Waislamu. Waislamu wa Uvinza wamejaribu sana kuomba misaada kurekebisha hali hii ya aibu. Maombi yamepelekwa kwa taasisi za Kiislamu nchini na nje ya nchi kujaribu kuuhami Uislamu. Ni jambo la kusikitisha sana kuwa taasisi hizo zimekuwa kimya. Wakati huo huo Kanisa Katoliki na hata makanisa mengine wamo mbioni kuwaghilibu vijana wa Kiislamu na wasio Waislamu kujiunga na dini ya Kikristo. Waislamu wa Tanzania tunawezaji kuuokoa Uislamu??
Msikiti wa KIBUTA- Kitondwe B Munga- Kisarawe Wanaomba Msaada wa Kuchimbwa KISIMA cha Maji. Kwa Mawasiliano Piga No. 0656 092 436 au 0685 171 221
11
(Imewekwa kwenye mtandao Februari 27, 2012) NI kweli maajabu hayaishi, hasa nchini Nigeria. Kuna usemi wa siku nyingi kuwa ni rahisi zaidi kumshawishi mtu achome nyumba yake kuliko kumshawishi aache upendeleo wake wa asili. Sikudhani hata siku moja kuwa usemi huo ungekuwa kweli kama ulivyo, hadi niliposoma kuwa wapiga mabomu tisa, wanaoaminika k u w a n i Wa k r i s t o , walikamatwa wakijaribu kulipua Kanisa la Kristo la Nigeria (COCIN) lililoko Miya Barkate, kilomita 20 katika barabara ya JoshBauchi jimbo la Bauchi. Watuhumiwa wa ulipuaji ni Lamba Goma, Filibus Danasa, Joshua Ali, Danjuma Sabo, Joseph Audu, Simon Gabriel, Bulus Haruna, Yohanna Ishaya na Daniel Ayuba (aliyekuwa Katibu wa PDP chama kilichoko madarakani, Peoples Democratic Party cha Rais Dk. Goodluck Jonathan) katika kata ya Tilden Fulani, wilaya ya Toro, jimbo la Bauchi. Wa t u h u m i w a h a o n i wanachama wa kanisa hilo la COCIN eneo al Unguwar Rimi, makazi madogo mapya ya Wakristo kati ya Tilden Fulani na vilima vya Shere. Watuhumiwa hao ambao walipigwa vibaya na wananchi waliokolewa na polisi na halafu kufungiwa katika kituo cha polisi cha tarafa ya Toro kabla ya kuhamishiwa kituo kikuu cha polisi jimbo la Bauchi. Wakati huo huo katika jimbo la karibu la Plateau, mlipuko wa bomu uliripotiwa katika makao makuu ya kanisa hilo la COCIN katika ibada ya Jumapili. Mchungaji wa kanisa lililolengwa la COCIN katika eneo la Bauchi ni Ishaya Izam, ambaye alianza kazi katika kituo hicho kutoka makao makuu ya COCIN mjini Jos, ambako bomu lililipuka (asubuhi hii). Hakuna uhakika kama milipuko hiyo ya mabomu inahusiana. Taarifa kuhusu tukio hilo katika jimbo la Bauchi ilikuwa haijatolewa na polisi. Kwa mujibui wa Shirika la Habari la Ufaransa, AFP, watu watatu waliripotiwa kuuawa katika mlipuko wa Jos. Shambulio hilo lilisababisha vurugu zilizofanywa na vijana wa Kikristo ambao walianza kuua watu ovyo. Waislamu takriban wawili waliuawa na kundi hilo la vijana wa Kikristo. Watu hao walivutwa kutoka kwenye pikipiki zao baada ya kusimamishwa
Makala
AN-NUUR
mashambulio mengine dhidi ya makanisa, likiwemo lile la Jos, yalifanywa kutokana na migongano katika jumuia ya Kikristo? Vyombo vya habari vya
Kikwete, kupitia wasaidizi wake ili amfahamishe mantiki na sababu ya hatua alizochukua ili na yeye atumie uwezo wake alionao ili Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake waachiliwe, kwa mustakabali wa Taifa, hata hivyo alisema hakuweza kumpata, Rais (Jakaya) kwa wakati muafaka. Alisema, katika kuhangaika zaidi ili viongozi hao waachiliwe, siku ya Ijumaa (iliyopita) alipata fursa ya kuzungumza na IGP na kumfahamisha sababu
hawajaachiwa. Niliwasiliana na RCO na nikabaini kuwa suala hilo haliko tena chini ya uamuzi wake na litakamilishwa siku ijayo, (Ijumaa). Alisema. Alisema, juhudi zake hazikuishia hapo kwani siku hiyo hiyo usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa (wiki iliyopita) alijaribu kuwasiliana na Rais
ya juhudi alizochukua na mategemeo kuwa Sheikh Sanze na wenzake wangeachiwa toka siku ya Alhamisi. Ninakiri kuwa katika mazungumzo ya simu, IGP Mwema alikuwa msikivu na mkarimu sana katika kauli yake. Alinishukuru kwa kauli niliyoitoa katika vituo vya televisheni na kuwa atafuatilia suala nililomueleza. Hatimaye Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake waliachiwa siku ya Ijumaa. Alisema. Prof. Lipumba alisema, baada ya mlolongo wote huo na juhudi zake za kusimama kati ya Waislamu na Jeshi la Polisi, anaamini kuwa Waislamu wengi na wananchi kwa ujumla walipokea vizuri wito wake na hawakushiriki katika maandamano, japo kwamba wapo waliohoji hatua yake hiyo.
AN-NUUR
12
Na Bakari Mwakangwale
WAKATI wanasiasa na wakuu wa vyombo vya dola na hata baadhi ya Masheikh wakitoa kauli za vitisho na kejeli kwa Waislamu, Profesa Ibrahim Lipumba, wiki iliyopita alifanya juhudi kubwa kuepusha shari ambayo ingewasibu Waislamu na wananchi wa Dar es Salaam. Katika jitihada zake, Prof. Kipumba alisimama kati kama msuluhishi wa Polisi na Waislamu huku akipigania kupewa dhamana viongozi waliokuwa wamekamatwa. Hata hivyo, baadhi ya watu wamemshutumu Lipumba hali ambayo imempelekea kutoa ufafanuzi akisema kuwa ndani ya Tanzania kuna Watanzania wengi, miongoni mwao ni Waislamu ambao nao pia wanastahiki kutendewa haki na kusikilizwa. Profesa Lipumba, aliye Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Taifa, ametoa kauli hiyo mbele ya waandishi wa habari mwishoni mwa wiki hii, akijibu wale waliohoji sababu za yeye kuingilia kati mvutano baina ya Waislamu na Jeshi la Polisi nchini. Katika majibu ya hoja hizo, Prof. Lipumba, alisema kwamba CUF inasimamia Haki Sawa kwa Wananchi Wote, kwani miongoni mwa Watanzania wamo Waislamu, ambao nao wanastahiki kupata haki katika nchi yao. Kuna Watanzania wengi ambao miongoni mwao ni Waislam na wao pia wanastahiki kutendewa haki katika nchi yao. Amesema Prof. Lipumba. Ama kuhusu hoja kwamba katika mikutano ya CUF, hujaa balaghashia na hijabu, utadhani kuna mawaidha, Prof. Lipumba, alisema ni vyema wanaohoji suala hilo wakasoma historia ya nchi hii ambayo hata picha zinaonyesha umati wa watu waliokuwa katika mikutano ya kupigania Uhuru, iliyokuwa ikihutubiwa na Mwalimu Nyerere, wengi wao walikuwa wamevaa balaghashia na baibui, hivyo haoni kama ni tatizo. Kuhusu balaghashia na baibui ni vyema vijana wakatazama histori, zipo picha za umati wa watu ukihutubiwa na Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania Uhuru wa nchi hii. Picha hizo zinaonyesha waliokuwa wakipigania Uhuru wengi walikuwa wavaa balaghashia na baibui, hata Mwalim Nyerere alipewa zawadi nyingi za balaghashia na akaamua kuwa anazivaa. Alibainisha Prof. Lipumba. Prof. Lipumba, alitanabahisha kwamba, kushamiri kwa demokrasia ya kweli mahala
saa 12 jioni. Alisema Alisema, baada ya hapo, alifanya juhudi ya kuwasiliana na vyombo vya habari (Televisheni) kwa lengo la kuongea na Waislamu na akiwasihi wasiandamane baada ya sala ya Ijumaa, na kuwaahidi kuwa atalishughulikia suala hilo na viongozi wao wataachiwa. Hata hivyo, alisema, mambo hayakwenda kama alivyokuwa amekubaliana na Makamanda hao wa Polisi, kwani alidai baada ya kutoa taarifa katika vituo vya Televisheni na Radio Iman, kuwa Sheikh Ramadhan Sanze na wenzake wataachiliwa lakini hawakuachiliwa. Baada ya kuwasihi Wa i s l a m u w a s i s h i r i k i maandamano baada ya sala ya Ijumaa nilimpigia simu Abdul Kambaya kuulizia kama naweza kuzungumza na Sheikh Ramadhan Sanze. Kambaya akanieleza mambo yamebadilika na Inaendelea Uk. 11
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.