You are on page 1of 16

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Mlinzi, fundi ujenzi watoa ushahidi kesi ya Ponda


Uk. 14

Tusiishie kwenye mabucha tu


Tusitesane wengine wakitesa Kila watu wawe na NECTA yao Kero za MoU, OIC, udini zitaisha

ISSN 0856 - 3861 Na. 1056 RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1-7, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Uamsho: Farasi keshatoka mkifunga mlango kazi bure

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akiwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Idd Seif.

Yaliyomkuta mzee Jumbe Maalim ni gharama stahiki


Ndio maana Karume, Salmin wanafuata nyayo Wameachana na zile siasa muisi za Kisonge
WANAOIJUWA athari ya gesi ya Mtwara kwenda Dar es Salaam na kuwaacha watu wa Mtwara wakiendelea kuwa masiki ni watu wa Mtwara. Wa j u w a o a t h a r i y a Zanzibar kumezwa huku Wazanzibari wakibakia wanyonge hawana maamuzi, hawana heshma ya nchi yao, hawana mamlaka ya nchi yao na uchumi wao ukizidi kufa ni Wazanzibari. Adhabu ya kaburi aijuae ni maiti. Wazanzibari wamechoka kunyanyasika na wataendelea kupambana kuliko walivyowahi kupambana mpaka watakapoyatia mikononi mwao mamlaka kamili ya nchi yao. Jamhuri ya watu wa Zanzibar Kwanza! (Soma Uk. 10)

WAZIRI katika osi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Abood.

Si Sheikh Farid pekee, ni Wazanzibari Kama mabavu sawa, lakini mpaka lini? Ilishindwa KGB ya USSR. Hamjifunzi tu?

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Habari
AN-NUUR
tusilalamikiane habari za MoU, OIC, Mahakama ya Kadhi na kuwa na Wakuu wa Mikoa/ Wilaya, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, Makamishana na Mawaziri ambao wakikaa vikao kufanya maamuzi ya kinchi, wanajiona kama wapo katika kikao cha Diyosisi kutokana na jinsi walivyo wengi ikilinganishwa na watu wa dini nyingine. Ufupi wa maneno tuseme kuwa kama ni lawama, basi wa kulaumiwa ni Waislamu ambao pamoja na dhulma za wazi ambazo wamekuwa wakifanyiwa kwa muda mrefu, wameshindwa kuwa na kauli thabiti na kuchukua hatua madhubuti za kukomesha dhulma na uonevu huo. Hivi kuna dhulma iliyozidi

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013


mtoto wa Kiislamu kufaulu na kukatwa akachukuliwa mtoto wa Kikristo mwenye alama za chini au mtoto wa Kikristo akapewa jina la mtoto wa Kiislamu akasoma sekondari huku huyu Muislamu akiambiwa kuwa hakuchaguliwa? Hivi kuna udini uliozidi huu wa kuunda Tume/Kamati ya kuchagua watoto wa kwenda kidacho cha tano, Kamati ambayo huficha majina ya watoto Waislamu waliofaulu vizuri ili wasichaguliwe. Na hili hufanywa na Mwenyekiti wa Jopo kwa kujiamini kabisa akijua kuwa anao waongoza ni Wakristo watupu kama alivyowahi kufichua Mzee Bori Lilla? Haya yote na mengine mazito wamefanyiwa Waislamu katika nchi hii na ushahidi wanao, lakini wapo wapo tu mpaka imeka mahali sasa wanaowadhulumu wameota jeuri sasa wanataka kuwalisha vibudu na kwamba eti wakawachinjie nguruwe wao kule Sengerema na Bunda! Hapa ndipo walipofika Waislamu wa Tanzania kwa kutokufuata kwao Amri ya Quran kwamba wasikubali kudhulumiwa. Sasa maadhali Wakristo wenyewe wamekuja na hoja kuwa watu wagawane mabucha (na kwa maana hiyo mitaa ya kuishi), basi hapana shaka itakuwa busara kwao kuwaunga mkono.

AN-NUUR

MAONI YETU

KAMA ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari, wapo baadhi ya Wakristo wamekuja na madai wakitaka Wakristo nao waruhusiwe kuchinja, isiwe ni haki ya Waislamu pekee kuchinja na wengine wale. Madai hayo yanakwenda mbali zaidi. Kwamba kama Waislamu watakataa Wakristo kuchinja, basi kila watu wachinje na kuwa na mabucha yao. Serikali inakataa madai ya Wakristo na hoja zake zinaeleweka na za msingi kabisa. Kwanza ni hoja ya kidini. Kwamba Wakristo hawajawahi kuwa na tatizo na uchinjaji wa Waislamu. Kwamba hawana kanuni maalum za uchinjaji za kidini ambazo wanahofia kuwa Waislamu watazikiuka na hivyo kuwalisha nyama isiyostahiki kuliwa kwa misingi ya dini yao. Hiyo ni kinyume na Waislamu. Wao wana kanuni za uchinjaji na zikikiukwa, nyama inakuwa haramu kuliwa. Na kwamba imekuwa kama sheria isiyoandikwa kuwa wachinjaji ni Waislamu toka zama na Wakristo hawajakuwa na tatizo. Kwa hiyo kuleta madai hayo sasa, ni kuleta vurugu tu zisio na msingi. Hilo moja. Hoja ya pili ni kuwa u k i s e m a Wa k r i s t o n a o wachinje, itabidi wawe na mabucha yao na Waislamu mabucha yao. Lakini huwezi kuweka bucha la Wakristo kwenye eneo la Waislamu wengi au la Waislamu katika ya Wakristo wengi. Itabidi sasa kugawana mitaa na maeneo. Ukifika hapo hakuna tena Tanzania tunayoizungumzia hivi leo. Hata hivyo, sisi tunadhani kuwa yapo mambo makubwa zaidi ya hili la kuchinja wanyama ambayo tungeyazungumzia kwanza uwezekano wake wa kugawana kila watu wakaenda kivyao. Ni hivi karibuni tu, Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) litatangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana. Ambapo kama ada yao, watatungazia wale

Tusiishie kwenye mabucha tu

ambao imekuwa ni kawaida yao kupewa upendeleo wa kutesa huku wengine w a k i t e s e k a . N E C TA watatangaza matokeo hayo bila kujali kuwa kuna madai mazito ya Waislamu ya muda mrefu, madai ambayo yanawafanya kutokuwa na imani na Baraza hilo. Ukiacha yale madai ya jumla kwamba toka Baraza hilo limeundwa limekuwa kama Parokia kutokana na sehemu zote muhimu katika utendaji na uongozi kuwa miliki ya Wakristo, lakini yanatajwa madai na kutolewa mifano hai jinsi Baraza lisivyotenda haki. Si nia ya safu hii kukariri madai yote kwani yalishawasilishwa rasmi serikalini, lakini tugusie tu hili la Kamati ya Kutunuku ambayo inatuhumiwa kufanya upendeleo katika kuamua nani watese na nani wateseke. Na hii hufanyika kutokana na kutokuwa na kanuni maalum iliyo wazi ya kuamua viwango vya ufaulu na madaraja kwa masomo mbalimbali. Wakati baadhi wakifanyiwa ugumu kufaulu kwa kuwekewa alama za juu katika kupata daraja la juu, wengine hufanyiwa wepesi na kulazimishwa kufaulu hata wakipata maksi za chini. Sasa haya ni madai mazito na katika baadhi ya nyaraka za kiserikali zinakubaliana na mudai haya ya muda mrefu ya Waislamu. Hata hivyo hakuna hatua zozote zinazochukuliwa bali kauli za hadaa na kuwatarajia Wa i s l a m u w a e n d e l e a kuliamini Baraza hilo. Sisi tunadhani kama ni kugawana, tuanze na mambo ya msingi kama hili. Kama serikali inaona haiwezi kuyatizama madai ya Waislamu kujua ukweli wake na kuchukua hatua, basi uandaliwe utaratibu ambapo kila watu watakuwa na NECTA yao. Na maadhali yanayolalamikiwa katika NECTA ndio hayo hayo yanayolalamikiwa katika taasisi nyingine, basi nako utaratibu uwe huo huo. Tufike mahali

Uamsho: Farasi keshatoka mkifunga mlango kazi bure


Na Omar Msangi

NILIBAHATIKA kuwepo Zanzibar katika wiki moja ya heka heka ambapo ilikuwa kipigo mtindo mmoja. Polisi wakipiga watu bila ya sababu inayoeleweka na wengine kuwakamata na kuwatia ndani. Ilikuwa vikosi wakipita mahali wakiona maandishi ya hatuutaki, Je, mnautaka? Tunataka muungano wa mkataba, au maneno yoyote yenye kuashiria kuwa watu wanahoji muungano, mtakaokutwa hapo, haijalishi kama miliandika nyinyi au mnapita njia tu. Mtapigwa virungu, bakora, mateke na kusombwa katika karandinga. Ilikuwa patembezwa mkongoto ikabidi watu wawe wanajihami kwa kufuta maandishi yaliyokuwa katika kuta za nyumba zao au kupaka rangi ili kupata salama. Na kweli ukipita katika mitaa ya Unguja hukuti tena maandishi yenye ujumbe wa kuhoji muungano kama ambavyo itakuwa vigumu sana kukuta bendera ya Uamsho ikipepea mahali. Pengine tafsiri ya harakaharaka inayoweza kutolewa ni kuwa harakati ile ya vikosi na polisi, ilikuwa jitihada za serikali kuzima wimbi la wananchi wanaohoji muundo wa sasa wa muungano wakitaka mabadiliko. Ilikuwa pengine pia mbinu za kusambaratisha umoja wa Wazanzibari katika suala hilo na walivyolipachika Uamsho ionekane kuwa hiyo ni agenda

SHEIKH Farid Had ya Uamsho na ukitaka shida, hiki cha kukusanya maoni ukitaka yakukute, basi shika Zanzibar juu ya katiba mpya, mambo ya Uamsho. Kwa utaona kuwa suala la kuhoji vipigo vile na kwa kuwa muungano, kukataa muundo baadhi ya Masheikh wa wa sasa wa muungano huo Uamsho walikuwa ndani na na kutaka Zanzibar iwe na wamezuiliwa dhamana, basi mamlaka yake kamili kama huenda ingewafanya watu nchi na kama Dola, sio suala hata katika kutoa maoni yao la Uamsho, Masheikh au juu ya suala la Katiba Mpya, wanasiasa wachache. wasiguse hoja zilizodhaniwa Kwa yale ambayo za ki-Uamsho. yashasemwa juu ya maoni Hata hivyo, kama utafuatilia ya wananchi wa kawaida vizuri taarifa za vyombo vya pamoja na viongozi wa habari katika kipindi chote Inaendelea Uk. 7

3
wa Maaskofu. A l i s e m a , Wa k r i s t o wanaopinga adhabu ya kifo MAALIM Ally Bassaleh hoja zao wanazitoa katika a m e t i l i a s h a k a m a o n i Biblia, akitolea mfano wa yaliyotolewa na Waziri Mkuu kisa cha Kaini na Abeli, huku Mstaafu Mh. Edward Lowasa, akinukuu maandiko kutoka aliyetaka hukumu ya kifo katika Biblia, yanayoonyesha nchini ifutwe, bila kuzingatia kupinga adhabu ya kifo. Sasa anapojitokeza Mh. umuhimu wa sheria hiyo katika jamii akidai maoni Lowasa, akapinga waziwazi hukumu ya kifo, jambo ambalo hayo, yana harufu ya udini. M a a l i m B a s s a l e h linapigiwa debe na Maaskofu ameyasema hayo akiongea na na si tu kwamba adhabu hiyo Waislamu mara baada ya ibada ipo kulingana na maumbile ya swala ya Ijumaa katika lakini pia ni sehemu ya ibada Msikiti wa Idrisa, Kariakoo, kwa Waislamu, anataka Jijini Dar es Salaam, Ijumaa tumfikirie vipi Waislamu. Alisema Maalim Bassaleh. ya wiki iliyopita. Alisema, sheria hiyo ipo Maalim Bassaleh amesema, kulingana na maumbile ya ukifuatilia kwa makini nyendo za Mh. Lowassa, tokea huko mwanaandamu kwani huzuia nyuma akiwa madarakani, mauaji na pia inalinda uhai utabaini kwamba ni wazi kwa sababu mtu asiyejali uhai ameelemea zaidi upande wa wa mtu akaamua kuutoa uhai dini yake ya Ukristo katika wa mwenzake, uwepo wa sheria ya kifo utamuhosha kufanya siasa. Akasema kuwa ni hatari kwamba na uhai wake pia kuwa na kiongozi kama utatolewa kwa mujibu wa huyo na kuongeza kuwa, sheria. Kwa maana hiyo, alisema suala la kutaka hukumu ya kifo ifutwe humu nchini, mtu atatakae muuwa mwenzake ni jambo lililoanza kitambo pindi akielewa kwamba huko nyuma na limekuwa akiuwa na yeye atauwawa mauaji ya hovyo hovyo katika likijirudia rudia. Alibainisha kwamba wengi jamii hayatokuwepo. Maalim Bassaleh, wanaotoa maoni hayo tokea akionyesha kushangazwa na huko nyuma na hata hivi sasa ni Wakristo, kwa msukumo maoni hayo ya Waziri Mkuu Na Bakari Mwakangwale Na Mwandishi Wetu

Habari

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

Bassaleh apingana na Lowassa


huyo wa zamani aliyejiuzulu, alisema sababu alizozitoa hazikuzingatia kulinda amani katika jamii, bali zina harufu ya udini zaidi. Alisema, Waislamu bado wanaumia na kitendo cha Mh. Lowasa, kuidhinisha Serikali kutoa mabilioni ya fedha za walipa kodi Waislamu kupewa Makanisa, kwa ajili ya miradi yao na kuwabagua Waislamu, akiwa kiongozi wa umma. Waislamu siyo huyu Lowasa, katika ile MoU, baina ya Serikali na Makanisa nchini, akatia saini yake, kwamba Serikali itoe mabilioni ya fedha zikiwemo kodi za Waislamu zitumike katika miradi ya Makanisa na Waislamu hawana lao, ndio huyu leo anaibuka akiwaunga mkono Maaskofu, akitaka adhabu ya kifo iondolewe. Alisema Maalim Bassaleh. Alisema kwa kuwa kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni yake katika Tume ya Katiba, basi Bw. Lowasa, alitumia fursa yake hiyo kama Mtanzania mwingine yoyote kutoa maoni yake. Alisema, kwa kuzingatia hilo, Lowasa kabla ya kutoa maoni yake hayo, alitakiwa azingatie kwa makini hilo analotakiwa kulipendekeza

Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowasa. kwani akitoa maoni ambayo yataonekana yana dalili ya kutolinda amani katika jamii itakuwa ni tatizo kwake. Kufutwa kwa adhabu ya kifo, amini nawaambia Polisi watazidisha mauwaji, wanajeshi watakuuwa, mgambo watauwa kwa sababu watajua kwamba, hata akikuuwa hafanywi kitu na muathirika wa kwanza utakuwa ni wewe Muislamu. Alisema Maalim. Alisema, mtu anapouwa mwenzeke ukataka asiuliwe ni wazi kwamba hali hiyo itachochea watu wauane kwa chuki ndogondogo tu, jambo ambalo litaweza kuvuruga amani katika jamii.

MGENI rasmi katika mahafali ya wanafunzi Waislamu wa kidato cha sita Minaki Sekondari Ustadhi Nurdin Kishik, amewataka wanafunzi hao kutambua kwamba kuhitimu kidato cha sita ndio kwanza safari yao ya elimu inazidi kushika kasi. Akisheresha aya za Quran, Kishki amesema kuwa Mwenyezi Mungu anasema, kwamba watu wa aina mbili ndio atawapandisha daraja, kwanza wale walioamini a m b a o n i Wa i s l a m u walioingia katika imani ya Uislamu kamili kamili na wale waliopewa elimu. Alisema, Mitume waliacha elimu, na dunia ya sasa inataka kusoma elimu zote, Qur an haipo nyuma bali ipo mbele zaidi ya wakati uliopo. Akaongeza kuwa, Qur an, ndio kitabu pekee cha dini kilicho ipa elimu kipaumbele kwani sura ya

Kishki atoa nasaha kwa wahitimu kidato cha sita


kwanza kabisa imehimiza kusoma, kwa jina la Mola aliyeumba. Alisema, elimu waliyoipata ni amana na kesho siku ya malipo wataulizwa juu ya amana hiyo, kwani elimu ni kati ya mambo manne ambayo mtu ataulizwa aeleze aliitumiaje. Aliwataka wahitimu hao, pindi watakapofanya mtihani na kurejea makwao, wasije wakajifananisha na vijana wa mitaani ambao hawajajaaliwa kupata elimu waliyo ipata wao. Alisema, muhitimu wa kidato cha sita anasifa mbili ambazo zinamtofautisha na vijana wa mtaani, kwanza ni Muislam na pili ni msomi, ambaye ukifanya jambo sawa na yule wa mtaani la kwako litakuwa ni kubwa kuliko la yule wa mtaani. Unaweza hata nyumbani kwenu, ukafungua darasa kwa wiki mara tatu kuwasaidia vijana wa kidato cha kwanza, pili tatu na nne, pasi ya kuwatoza hata shilingi moja ukasema huu ni mchango wangu katika Uislamu. Alisema. Wanafunzi wa kidato cha sita kote nchini wanatarajia kufanya mitihani yao ya Taifa ya kuhitimu masomo yao February 11, mwaka huu. Wakati huo huo imeelezwa kuwa ratiba za masomo katika shule za Sekondari nchini, unawanyima Uhuru wa kuabudu wanafunzi wa Kiislamu. Hayo yamebainishwa na wahitimu wa Kiislamu wa kidato cha sita wa Sekondari ya Minaki, iliyopo Kisarawe Mkoani Pwani, katika mahafali yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki iliyopita. Akianisha changamoto walizokumbana nazo wakiwa shuleni hapo, mwanafunzi ambaye ni muhitumu Ramadhani Athumani, alisema pamoja na kwamba Serikali haina dini lakini wananchi wake wana dini, hivyo ilikuwa ni vyema Serikali kuzingatia hilo katika mipango yake ya kusimamia huduma kwa watu wake. Alisema, moja ya tatizo kubwa linalowasumbua wanafunzi wa Kiislamu wakiwa shuleni ni juu

ya ratiba ya vipindi kutokwenda na mfumo wa ibada ya Uislamu. Hali hii husababisha tushindwe kufanya ibada zetu kwa muda muafaka, huku akitolea mfano wa swala za Dhuhuri, ambayo hutukuta tupo madarasani. Alisema mwanafunzi Ramadhan. Alisema, changamoto ingine ni kukosa sapoti ya wasomi na viongozi wa Kiislamu ambao wapo Serikalini, kutowajibika au kuwatembelea wanafunzi wa Kiislamu mashuleni hata pale wanafunzi hao wanapowaomba kuwatembelea na kuishia kutoa ahadi bila kutekeleza. Alisema, mbali na changamoto hizo lakini pia kwa muda waliokuwepo shuleni hapo wakishirikiana na wanajumuiya wengine, wameweza kudumisha na kuendeleza madrasa kwa watoto wa Kiislamu wanao zunguka katika eneo la Shule yao.

4
Na Pendo Masasa NDOA ya mke zaidi ya mmoja inapigwa vita na baadhi ya watu, hasa wale wanaodai kuwa ni watetezi wa haki za wanawake. Mwanamume kuoa mke zaidi ya mmoja inaonekana kwa wapinzani wa ndoa ya mke zaidi ya mmoja kama ni jambo la kumfanya mwanamke duni. Fikra hizo zimeenea hata kwa baadhi ya Waislamu ambao wanaziunga mkono kibubusa hoja za wapinzani huku wakiacha mafundisho ya Mwenyezi Mungu. Wamechagua wakishikamana na maelekezo ya watu ambao wanaonekana kama ndio watetezi wao wakubwa. Kwa bahati mbaya watetezi hao wakiwa ni viumbe tu wa Mwenyezi Mungu na hawana wanalojua juu ya binadamu kuliko aliyetuumba Allah (s.w), ambaye ndiye mjuzi wa tulivyo wanadamu. Ndiyo maana akatuwekea utaratimu wa kuishi kwa kufuata sheria na mipaka kwa ajili ya kutimiza lengo la kuumbwa kwetu na kutuleta hapa duniani, na si lingine ni kumwabudu Mwenyezi Mungu. Wanawake tena wasomi, nao wanapinga uke wenza kama vile hawajui agizo hilo limetoka kwa nani na nini hukumu yake. Binafsi nimejaribu kuzungumza na wanawake wengi wasomi katika madrasa mbalimbali na wengine walimu wa madrasa. Wengi wameonekana kupinga suala hili la uke wenza moja kwa moja. Wengine walithubutu iwapo mume ataoa mke mwingine lazima atamwacha. Sababu ni kwamba wengi wana wivu hivyo hawapendi kuchangia mume na mke mwingine. Wengine wanahisi kuwa mume akioa atashindwa kufanya uadilifu, atampenda zaidi mke mdogo. Walio wengi wanaogopa uke wenza kwa kuhoa vita baina yao. We n g i n e wanatoa sababu za kukataa uke wenza kwa roho mbaya tu, hawataki wanawake wenzao wasitirike, wanataka wabaki wakihangaika mitaani. Hata hivyo wengi wana hofu ya mali zaidi. Hawa wanahisi mali za mumewe zitapungua kwa kuwa akioa mke mwingine, lazima awape wote haki sawa katika misingi ya kufanya uadilifu. Hakutakuwa na tofauti ya Bi. Mkubwa na Bi. Mdogo. Kwamba mkubwa anaona kuwa yeye anastahili zaidi kwa kuwa alitangulia na kuchangia kwa kiasi fulani

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013


ndogo. Lakini kwa kuwa kwao hakuna kuachana, basi wanaposhindwana mke na mume husema wanatengana na si kuachana. Katika kipindi cha kutengana kwao, hakuna anayeweza kujizuia. Kibaya zaidi ni kwamba hata ukomo wa muda wa utengano wao haufahamiki. Matokeo yake ni kila mmoja kwa wakati wake anakuwa huru zaidi kuzini atakavyo. Wa t e t e z i w a h a k i za wanawake haya hawayazungumzi. Zaidi wamewafanya wanawake wengi kuharibu ndoa zao. Kisa mume anataka kuoa hivyo wakatangaza vita bora kuachika. Kibaya zaidi ni kwamba mtu anaachika kwa ajili ya kupinga ruksa aliyotoa mmiliki wa vilivyoko ardhini na mbinguni Allah (s.w). Kwa hili tungoje kwenda kuadhibiwa. Kwa nini wanawake wenzangu tupate adhabu kwa ajili ya mafundisho yanayotokana na matamanio ya viumbe? Hebu tuchukue hatua kwa kufanyia kazi vile alivyotuagiza Mola wetu na Bw. Mtume (s.a.w), ili tuishi kwa amani na kwa upendo miongoni mwetu hapa duniani. Ngoja niwape siri ya mafanikio ya uke wenza. Siri ya kwanza ya mafanikio hata kama mumeo hajaoa mke mwingine au hajawahi kukutamkia kuoa mke mwingine, usichukie uke wenza kabla au baada ya mumeo kuoa, ukawa na kra za uke wenza kuwa ni vita. Siri nyingine siku zote amini kuwa sheria iliyo mkomboa mwanamke wa Kiislamu ni hii ya Kiislamu, inayomruhusu mwanaume mmoja kuoa mke zaidi ya mmoja lakini wasiozidi wanne. Si tija kufuata sheria za watetezi wa usawa wa wanawake wanaoshikilia nadharia ya mume mmoja mke mmoja, kiasi tukaona uke wenza ni vita. Tukumbuke tu kuwa wanaharakati mantiki zao zimeegemea zaidi matakwa ya nafsi za wanadamu. Lakini hoja za Allah (sw) zimeegemea zaidi katika sheria na maumbile ya mwanadamu. Kama katika Qur an ameuliza Allah (s.w), Je, wao wanaotaka hukumu za kijahili? Na nani aliye mwema zaidi katika hukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini? (5:50).

AN-NUUR

Ukewenza sio vita

katika kuchuma mali na mume. Hebu mwanamke wa Kiislamu uliyepewa kra za watetezi wa haki wanawake, tambua kuwa hoja zote zinazotolewa na hao watetezi wa wanawake, zimeegemea zaidi katika matamanio ya kibinadamu kuliko mafundisho na mwongozo wa Mwenyezi Mungu kwa binadamu katika maisha ya ndoa. Kufuata nafsi na matamanio ni dalili tosha kwamba hujaelimika. Iwapo mwanamke wa Kiislamu angekuwa anasoma vizuri Quran na hadithi za Mtume (s.a.w), basi asingekwazika na suala hili la uke wenza pale inapobidi kuwepo. Sasa kupiti gazeti hili la An nuur, natumia nafasi hii kukumbushana kuwa, aliyetoa ruksa ya wanaume kuoa mke zaidi ya mmoja ni Allah (SWT) na sababu zimewekwa bayana. Kuna taratibu kadhaa zinazodhihirisha namna mume anavyoweza kuoa mke mwingine. Mfano ni mwanamke kuwa tasa, maradhi kwa mke kiasi cha kushindwa kabisa kutimiza majukumu yake ya ndoa, basi mume anaweza kuoa mke mwingine. Lakini katika hali hizi mume analazimika kuendelea na wajibu wake wa kumtunza mkewe kwa mahaba yote kama ilivyokuwa kabla ya kuoa. Wa k a t i m w i n g i n e n a katika baadhi ya sehemu,

idadi ya wanawake inaweza kupindukia ya wanaume. Kuna wanawake wajane waliowa na waume zao na bado wanastahili kupata stara ya mume. Hali inaweza kuwa mbaya iwapo hali hii itaachwa kwa staili ya kila mume na mke mmoja tu. Iwapo wanawake hawa watakosa stara, basi bila shaka katika hali hii itarajie zinaa kubwa, zao la nje ya ndoa, chokoraa, wahalifu, mimba kutolewa na vichanga kutupwa hovyo nk. Iwapo hali hiyo itatokea mahali, bila shaka wale wanaoonekana wameelimika na kuona uke wenza ni kumkanda miza mwanamke, wakashinikiza wanawake kukataza waume zao kuoa panapo haja, basi hao watakuwa hatiani. Ukitizama kwa kina mifano hii kwa mtu mwenye kutumia akili zao vizuri walizojaaliwa na Allah bila kutawaliwa na ubinafsi, watafahamu mara moja kweli. Kwamba kupinga amri ya aliyetuumba ni kuleta madhara makubwa katika jamii. Kwa hakika zipo faida kubwa za uke wenza pale inapobidi kuwepo. Hata hivyo wengi wanaoongea juu ya kuukataa uke wenza, hata hawajawahi kuingia katika ndoa adilifu ya uke wenza. Kwanza mwanamke huyo aliyeridhia ndoa adilifu ya uke wenza, atakuwa hajapingana na Mwenyezi Mungu, kwa hiyo utapata radhi za Mwenyezi Mungu

kwa kukubali kwa moyo mmoja mumewe kuoa mke mwingine. Pia wakati mwingine mke anakuwa na mapenzi na mume kutokana na kiasi cha wasaa anachomkosa na akiwa na hakika ya kuwa na muwewe kitambo kidogo. Hali inampa fursa na wasaa mke katika majukumu yake ya ndoa. Lakini pia ningependa kuwaambia kuwa katika utati nilioufanya kuhusu wanaume, baadhi ya wasio na mke zaidi ya mmoja wanafanya zinaa. Na hufanya hivyo wake zao wanapokuwa na udhuru. Wengine wanafanya hivyo baada ya kukataliwa na wake zao kuowa mke mwingine, hali ya kuwa wana uwezo. Mwanawake mwingine anaona bora akatae mumewe kuoa mke mwingine licha ya kutambua mafundisho kutoka kwa Allah (s.w) juu ya suala hilo. Mume anaamua kumtii mke kwa kufanya zinaa nje ya ndoa. Tambueni wazi wanawake kuwa mnapowakataza waume zenu kuoa mke mwingine pindi anapokujulisha juu ya hilo, kaeni mkijua kuwa mmefungulia uwanja wa shetani. Kwa wenzetu ambao inadaiwa kuwa kwa mujibu wa imani yao ni sharti kuwa na mke mmoja, licha ya kuwa na mke mmoja lakini inaonekana wengi wao wameshindwa kumudu sharti hilo. Wengi wamekuwa mahodari wa nyumba

Habari za Kimataifa/Tangazo

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

Total Sumsung kununua mafuta ya Iran


TEHRAN Shirika la Mafuta la U f a r a n s a n a K o re a Kusini lijulikanalo kama Samsung Total, limeanza tena kununua mafuta gha ya petroli ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hatua ya shirika hilo imekuja baada ya kupata hasara kubwa iliyotokana na vikwazo vya upande mmoja vya nchi za Magharibi hasa Marekani dhidi ya Iran. Ripoti hiyo imeongeza kwa mashirika hayo yalipata hasara baada ya kuzuiwa kununua mafuta ya Iran. Hasara hiyo inakadiriwa kufikia kiasi cha zaidi ya dola milioni 6.5, hali iliyoyalazimu shirika hilo kuachana na shinikizo la Marekani na nchi za Magharibi hivyo kuanza tena shughuli za ununuzi wa mafuta ya nchi Iran. Hatua hiyo inahesabiwa kuwa moja ya hatua za kususia vikwazo dhidi ya mafuta ya Iran kwa wateja wa mafuta hayo, sambamba na kuendelea mbinyo wa Wamagharibi kwa wateja wa Tehran. Baada ya kusimamishwa bidhaa ya mafuta ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwenda kwa wateja wake kama vile Japan na Korea Kusini, wateja mbalimbali wa bidhaa hiyo muhimu wameanza kufuatilia njia za ununuzi wa mafuta ya Iran mbali na vikwazo hivyo vya maadui wa Tehran.

Jumuiya na Taasisi za Kiislamu ( T) pamoja na shura ya Maimamu (T)


Inawaalika Waislamu wote kuhudhuria katika Kongamano litakalo fanyika Siku: Jumapili tarehe 3/2/2013 Muda: kuanzia saa 8 Mchana Mahali: Kiwanja cha Nuuru Yaqiin ( Uwanja wa pumba karibu na uwanja wa Mwembe Yanga- Temeke jijini Dar es salaam). Mada: Tamko la Waislamu kutolewa dhidi ya kauli ya Maaskofu kwa Serikali. Msimamo wa Waislamu katika Gesi ya Mtwara na mwenendo wa kesi katika kiwanja cha Markaz Chang'ombe jijini Dar es salaam.

Kongamano

BALOZI wa Jordan nchini Marekani amesema kuwa, kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi huko katika ardhi ya Palestina inazokaliwa kwa mabavu, kunazuia kuundwa kwa taifa huru la Palestina. Mwana Mfalme Zaid bin Raad, aliyasema hayo jana katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya Bloomberg na kusisitiza kuwa, kuendelea kwa ujenzi huo wa

Vitongoji vya walowezi vinazuia kuundwa taifa la Palestina


vitongoji vya walowezi wa Kizayuni, kunalifanya suala la kuundwa taifa la Palestina kuwa lisilowezekana. Amesema, kuongezeka nafasi ya haki ya taifa la Palestina katika Umoja wa Mataifa, kunaonyesha mustakbali mzuri kwa Wapalestina na kwamba, kwa hatua hiyo Wapalestina wataweza kuiweka Israel katika shinikizo. Aidha kiongozi huyo wa Jordan amesema kuwa, Wapalestina sasa wanaweza kuuburuza utawala bandia wa Kizayuni katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC. Hivi karibuni Mjumbe mwandamizi wa wanaharakati wa Palestina Fath, anayeshughulikia masuala ya utungaji sharia, alikosoa vikali hatua ya kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kuitaka Kamisheni ya Siasa za Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya kuitisha kikao mwezi Machi kujadili kwa kina suala hilo.

RAIS wa Iran, Ahmadnajad

Nyote mnakaribishwa

Marekani inafikiria juu ya mpango wa kupeleka ndege zisizo na rubani huko Kaskazini Magharibi mwa Afrika. Viongozi wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani wamesema kuwa, wanachunguza mahala pa kuwekwa kambi ya ndege hizo katika eneo hilo. Hata hivyo viongozi hao

Marekani kutuma ndege zisizo na rubani Afrika


Imeelezwa kuwa, iwapo mpango huo utatekelezwa, Wa s h i n g t o n i t a t u m a wanajeshi wasiopungua 300 kwenye kambi hiyo.
wamebainisha kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwa ndege hizo kuwekwa nchini Niger, nchi jirani na Mali. Viongozi hao wa Pentagon wamedai kuwa, lengo la

mapigano yaliyotokea siku ya Jumapili katika mji wa Gao, Kaskazini mwa Mali.

al Qaeda. Wakati huo huo, jeshi la Ufaransa limetangaza kuwa, waasi wasiopungua 25 wameuaw a kwenye

kuwekwa ndege hizo zisizo na rubani ni kukabiliana na makundi ya kigaidi kama

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

Umaarufu wa Mwalimu wa kutengenezwa


Je, Nyerere ni kikwazo cha katiba ya umma?-4
alitokea Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi alipoka Makanya Same wanafunzi wa shule za msingi walilala barabarani wakimzuia asipite na aliposimama na kuuliza kuna tatizo gani walimuonyesha nguo zao za shule zilivyokuwa zimechafuka, zilikuwa hazijafuliwa kwa siku nyingi kwa vile hakuna sabuni! Akina mama walitoka nje ya ndoa kisa mwenye duka anampendelea kumuuzia robo kilo (250 grms) ya sukari! Kila kitu kuanzia Unga, sukari, mafuta, maharage, mchele, mabati, bia, sigara, cement n.k., ulikuwa huwezi kuvipata mpaka upate kibali toka wizarani au Ikulu; na kibali hakitoki hivi hivi mpaka utoe kitu kidogo au uwe unajuana na wakubwa wakupe kimemo! Hapa ndipo Ugonjwa wa Rushwa na Usadi Ulipoanzia! J a m a n i ! Wa t a n z a n i a wenzangu! Mbona hatuna kumbukumbu? Tukumbuke hata kungatuka madarakani kwa Nyerere ilikuwa siyo matakwa yake, bali maji yalimka shingoni! Alikuwa hana ujanja zaidi ya kuondoka. Nchi ilikuwa imemshinda kabisa, akawa hawezi kwenda nchi za Magharibi kuomba misaada kwa vile alikuwa anawatukana kwamba ni wanyonyaji na mabepari! Hivyo suluhu yake ikawa ni yeye kuondoka na kutafuta mtu mwingine atayeenda kuongea na mabepari. Kweli Watanzania hatuna kumbukumbu kabisa, au kama zipo bas i s is i ni Wanaki wakubwa, na kwa mwendo huu hatutoki hata siku moja, na tutaendelea kulalama tu hadi mwisho wa dunia hii! Simtukani Nyerere bali najitahidi sana kusema ukweli, ni tabia yangu ndivyo nilivyo sikuzoea unaki wala kusema uongo, hivyo kama Watanzania au Wanamtandao wowote ule utakaoamua kuniangamiza kwa kusema ukweli au watakaoamua kuniadhibu kwa namna yoyote ile kwa kusema ukweli, basi sawa tu. Watanzania tumezoea kupindapinda mambo siku zote na hii ndiyo sababu ya kufika hapa tulipo hivi leo. Nyerere simchukii, bali nampenda sana kama vile alivyokuwa Mtanzania mwenzangu, lakini Nyerere kama kiongozi wa nchi alishindwa na kama system bado ataendelea kushindwa, alifanya majaribio mengi na kwa bahati mbaya sana yote yalishindwa (he never won). Na suala la kushindwa ni jambo la kawaida siyo kitu cha ajabu, marais wengi duniani wanashindwa kabisa na wengine hutolewa kwa maandamano, migomo au wao wenyewe kujiuzulu, hivyo tusipate kigugumizi kusema Nyerere alishindwa na bado ataendelea kushindwa, na kushindwa kwa Nyerere ndiyo sababu ya kuka hapa tulipo leo hii. Tumeka hapa kwa misingi DHAIFU aliyoijenga N y e r e r e . Tu s i m u o n e e Nyerere huruma kusema alishindwa, kwani kufanya hivyo tutakuwa tunajiumiza sisi wenyewe. Wale wanaomshabikia Nyerere kwamba aliweza, tunaomba watueleze au watuonyeshe aliweza nini, au ametuachia nini raia wa kawaida wa nchi hii! Je, kwani Nyerere ni Bora kuliko Umma wa Watanzania!? Je, Nyerere ni Bora kuliko vizazi vijavyo!? Nyerere asihurumiwe, bali avune alichokipanda. Tusiendelee kuwa wajinga, hata kama tuliweza kutawaliwa kwa katiba mbaya kuliko zote duniani kwa miaka 52, lakini tusiendelee kushabikia ujinga wetu. Miaka 52 ya ujinga inatutosha sana, tusikubali tena kuendelea kufanywa mateka ndani ya nchi yetu. Kwa mfano Rais George Bush (baba) pamoja na kwamba alikuwa Veterani wa vita vya Vietnam, na aliwahi pia kuwa Mkurugenzi Mkuu wa CIA kwa miaka 15, Makamu wa Rais wa Marekani kwa miaka 8 chini rais Ronald Reagan, lakini akiwa kama Rais wa 41 wa Marekani alishindwa kuboresha uchumi wa Marekani, na hata katika harakati zake za kuinusuru nafasi yake ya urais kwa kipindi cha pili alienda Japan kuomba serikali ya nchi hiyo inunue magari laki mbili (200,000) ya kutoka Marekani ili anusuru kiwango kikubwa cha watu wasiokuwa na kazi, Wajapan walipokataa kununua magari hayo alianguka jukwaani na kuzimia kwa kupata kihwehwe kwenye mkutano wa hadhara mjini Tokyo, na kutokana na hali hiyo Wamarekani walimuambia umeshindwa, na hivyo Wamarekani wakamtoa na kumuweka Rais Bill Clinton

Na Dr. Noordin Jella MZEE Edwin Mtei alijiuzulu Ugavana wa Bank Kuu baada ya kushindwa kumshauri Nyerere. Leo hii jina la Nyerere limekuwa suluhisho la kila tatizo. Ili uonekane mwanasiasa mpevu lazima ukipanda jukwaani umsie Nyerere hata kwa yale ambayo hakuwahi kuyasimamia au kuyatetea, imekuwa ni kama desturi au kaugonjwa fulani kwa Watanzania ili watu wakuone una busara na unaongea point, basi lazima umtaje Nyerere kwamba alisema hivi, au alifanya vile, au alinena lipi, ili mradi tu umesema hata kama hakuwahi kufanya hivyo au kutenda hivyo! Huu umaarufu wa Nyerere wa kutengenezwa, umaarufu wa kuchakachuliwa unatoka wapi jamani!? Tu m e s a h a u k w a m b a Nyerere baada ya vita vya Uganda umaarufu wake ulipotea kabisa na aliyumba kupita kiasi? Baada ya vita ya Uganda Waziri Mkuu wa wakati huo Edward Moringe Sokoine alikuwa mashuhuri na wananchi walikuwa wanampenda kuliko Nyerere. Na kama Watanzania wangekuwa na desturi na tabia ya migomo na maandamano, basi Nyerere angetolewa madarakani kwa maandamano. Tukumbuke jamani machungu ya Kaya, watu wamefulia nguo na majani ya mapapai! Wanaume wazima walihonga wanawake vipande vya sabuni za Mbuni au dawa za Meno au Viberiti au Sabuni za Kuogea za Rexona! Ukikuta watu wamejipanga foleni, na wewe unajipanga tu bila hata ya kuuliza, bali ukimfikia mwenye duka ndipo utajua nini kinauzwa! Mtu akikuta kuna foleni mahali na alikuwa na shughuli zake zingine, basi huchukuwa jiwe na kuliweka katika foleni ikiwa kama ishara kwamba yupo kwenye foleni, na wale waliopo kwenye foleni ile husogeza jiwe lile kadri foleni inavyosogea mbele! Wasichana wa shule za secondary walipewa ujauzito kwa kuhongwa pipi za Big G au Bazoka toka Kenya! Watu walifulia majani ya Mapapai kama mbadala wa Sabuni! Wakati mmoja Nyerere

HAYATI Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa rais wa 42 wa nchi hiyo. Mawaziri Wakuu wa Israel na Japan wanashindwa mara kwa mara na kujiuzulu, kwa vile wenzetu wana ustaarabu wa kujiuzulu. Ukiona huwezi kuwakisha wananchi pale wanapokusudia, basi inabidi ujiuzulu ili aje mtu mwingine atekeleze yale ambayo yamekushinda. Sisi hatuna ustaarabu huo, hata kama umeshindwa utalazimisha unaweza na waliopo karibu yako ambao wamekusaidia kushindwa, wanashabikia kwamba unafanya vizuri sana, ili mradi tu wewe na wao mambo yenu yawe swa kabisa! Licha ya kwamba umma unapata taabu na upo hoi bin taaban! Kwa nini Watanzania mnaona Kigugumizi kumtaja Sokoine katika harakati zake za kweli za kupambana na Ufisadi na kinyume chake wanamsingizia Nyerere kwamba alikuwa anachukia U f i s a d i ! ? Wa t a n z a n i a wanaishi chini ya wingu zito la vitisho lililotengenezwa na Nyerere. Mimi najiuliza hivi Nyerere alifanya nini kibaya nchi hii mpaka jina lake linalindwa kwa mtutu wa bunduki!? Kama ni kushindwa, ni kitu cha kawaida kwa binadamu kushindwa! Kwenye maisha siku zote kuna kushindwa na kusinda! Kwani aliwatendea Watanzania ubaya gani zaidi ya kushindwa kuongoza? M b o n a Wa t a n z a n i a hawatakiwi kumjadili Kiongozi wao, Mwasisi wa Taifa hili!? Kwani kuna ubaya gani raia wa nchi wakimjadili kiongozi wao aliyewahi kuwatawala!? Hivi jina la Nyerere litaendelea kulindwa kwa mtutu wa bunduki hadi lini!? Je, Watanzania wapo tayari kuendelea kugharamia kulinda jina na falsafa za mtu ambaye hayupo na hata kama falsafa hizo hazina manufaa kwa raia wake wanaoendelea kuishi na watakaozaliwa miaka ijayo!? Nyerere aliishi karne ya 20 na Watanzania wanaishi karne ya 21 sasa, tutaendelea kuabudu mizimu mpaka lini!? Mwaka 2000 Magazeti ya Generali Ulimwengu (Habari Corporation) yalianzisha mjadala kwamba mtu yeyote anayejua madhambi ya Nyerere ayaorodheshe na kuyapeleka Osi za Habari Corporation pale Sinza, watu wengi sana wakajitokeza na kuanza kuandika, ghaa mjadala huo ukasitishwa mara moja! Inaendelea Uk. 11

7
Inatoka Uk. 2

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013


na bado ndio kwanza zinaongezeka? Tume hii mpya anayopendekeza Mheshimiwa Waziri Mkuu, itakuwa na tofauti gani na zilizopita? Kwa nini tuendelee kuzungumzia kero badala ya kuondoa chanzo? Na chanzo kinajulikana kama wanavyosema Wazanzibari wenyewe kwamba ni ulaghai katika muungano, moja ikiwa ni Tanganyika kujivika Tanzania na Rais wa nchi, Zanzibar, kupachikwa cheo cha Waziri katika kebineti, mambo ambayo hayakuwa ya muungano kuingizwa kinyemela n.k. Kama hakuna sababu ya malumbano, basi itumike demokrasia ya kweli na huru, waulizwe Wazanzibari kivyao na Watanganyika kivyao kuwa wanataka muungano wa namna gani. Kinyume cha hivyo, ni kutaka malumbano yasiyokwisha ambayo yatazaa utumiaji wa nguvu na kuzaa vurugu. Hivi sasa kuna zogo linaendelea juu ya gesi Mtwara na tayari watu kadhaa washapoteza maisha na nyumba za baadhi ya wabunge kuchomwa moto. Inawezekana serikali ina hoja nzuri katika uamuzi wake wa kusarisha gesi hadi Dar es Salaam ili kuzalisha umeme wa kuingiza katika gridi ya taifa. Lakini maadhali wananchi wa Mtwara hawajazielewa hoja hizo za serikali na kuzikubali, suala hili halitakwisha kwa salama. Sasa sidhani kwamba itakuwa busara kwa serikali kusubiri kutumia mabavu na watu kuchomeana nyumba kama ilivyotokea Masasi, ndio ione mantiki ya kuwasikiliza wananchi, hasa wa Zanzibar juu ya suala la muungano.

AN-NUUR

kisiasa walio madarakani na wastaafu, utaona kuwa wote wanaungana katika kudai Zanzibar huru yenye Rais wake mwenye madaraka kamili. Wanaungana kudai Dola ya Zanzibar yenye kiti chake Umoja wa Mataifa. Wanaungana kutaka ile nchi inayoitwa Tanganyika iliyojivisha joho la Tanzania, ivue joho hilo ndio ikae meza moja na Zanzibar wapange wanashirikiana vipi katika hicho kinachoitwa muungano. Lakini wapo pia wanaosema kuwa ili kuwe na heshma, basi Zanzibar na Tanganyika wakutane katika Shirikisho la Afrika Mashariki na katika Umoja wa Afrika kama wanavyokutana na Uganda na Kenya. Sasa kama haya ndiyo maoni ya ujumla ya wananchi wa Zanzibar wa kada zote, mtu utajiuliza, wale vikosi waliokuwa wakipiga watu ovyo waliokuwa na mabango yanayouliza watu kama wanautaka, walikuwa wakimfanyia nani kazi? Wale vikosi na polisi waliokuwa wakipiga watu na kuwalazimisha kupaka rangi kuta zenye mabango ya kutaka mabadiliko katika muungano, walitumwa na nani na kwa masilahi ya nani? Mbona Wazanzibari walio wengi wanadai kuwa masilahi yao yapo katika mabadiliko? Haya, mabango ndio yashangolewa na kuta zishapakwa rangi. Je, ndio wamefuta pia yaliyo ndani ya nafsi za watu? Mbona ndio kwanza wanasema waziwazi mbele ya Tume ya Jaji Warioba kwamba muundo huu wa muungano hawautaki? Iliyokuwa Urusi ya zama zile, ilizishikilia nchi 15zilizounda iliyoitwa The Union of Soviet Socialist Republics (USSR) kwa mabavu na kwa mkono wa chuma kwa zaidi ya miaka 69. Lakini mwisho wake nini? Leo USSR ipo wapi? Yale mabavu yaliyoasisiwa na Joseph Vissarionovich Stalin na KBG yaliyokuwa yakiishikila USSR, yaliishia wapi? Leo wenye masilahi na mfumo wa sasa wa muungano (mfumokristo?) wanaweza kutumia vikosi, polisi hata jeshi kuhakikisha kuwa muungano unabaki kuwa wa serikali mbili hata kama hautakiwi na walio wengi katika Wazanzibari (Tanganyika? Sina hakika), Swali ni je, mabavu hayo yatafanya kazi mpaka lini? Kama hao wenye mabavu ya kuushikilia muungano huu,

Uamsho: Farasi keshatoka mkifunga mlango kazi bure

DKT. Emmanuel Nchimbi hawaoni busara ya kusikiliza maoni na kujali matakwa ya wananchi, je hizi ngonjera za demokrasia wanamwimbia nani? Wanachotaka nini, iwapo hawataki kuwasikiliza wananchi na kuleta mabadiliko kwa njia za mazungumzo na amani? Je, wanasubiri litokee la kutokea ndio watafute wachawi wakati wachawi ni wao wenyewe? Kama wakongwe wa mapinduzi na muungano, wanahoji na wanataka mabadiliko, kama Marais Wa s t a a f u w a Z a n z i b a r wanahoji na wanataka mabadiliko wakisema kuwa kukaa kwao madarakani wameona mengi jinsi Zanzibar inavyosidiwa kupitia mfumo huu wa muungano, kama wafanyabiashara, wachumi na wasomi wanataka muundo huu wa muungano ufe, kama Masheikh, viongozi wa taasisi za kijamii na wananchi kwa ujumla wanataka Zanzibar yao, huyo aliyebaki anayetaka mfumo wa sasa wa serikali mbili, lije jua au mvua, anamwakilisha nani? Aliwahi kusema Sheikh mmoja kuwa mfumo wa sasa wa muungano upo kwa ajili ya kuunufaisha mfumokristo na kwamba ukitaka kujua nguvu ya kanisa katika nchi hii, basi gusa muungano. Je, tuseme hawa vikosi na wanasiasa walio madarakani hivi sasa wanaotetea serikali mbili, ni katika watumishi wa mfumokristo ambao hawasikii la mwananchi wa Kiboje wala Chwaka, ila lile wanaloagizwa na

IGP Said Mwema mfumokristo? Je, nao wanasubiri wakistaafu ndio waseme yale wanayosema leo Dr. Amani Abeid Karume na Dr. Salmin Amour? Kwa nini wasioneshe uzalendo wao na ujasiri wao wakingali madarakani kwa kusimama katika yale yaliyo na masilahi na wananchi wao? Ilikuja miafaka hapa ya CCM Vs CUF, tukatamba sana nayo, lakini ikawa inakufa na kuwaacha Wazanzibari wakirudi kule kule katika chuki, magomvi na uhasama. Mheshimiwa Amani Abeid Karume akiwa madarakani akatanabahi akajisemea, huu ujinga. Akatizama Uzanzibari wake na kuwatizama Wazanzibari. Hakuhofia kelele za wahafidhina wala kuhofia yaliyowakuta watangulizi wake kama Mzee Aboud Jumbe. Leo Zanzibar ipo shwari. Yule Sheikh wetu anasema kuwa Dr. Karume na Maalim Seif walifanikiwa kwa sababu walikwepa zile taratibu za kimfumokristo. Wamesimama na wananchi na mfumokristo haukuweza kuwafanya lolote. Je, hili halitoshi kwenu mlio madarakani kuwa ni somo? Kama upo na wananchi wako, unachohofia nini? Kama umesimama katika haki, cha kuhoa nini? Ukiwa katika haki, upo katika ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Lakini ukiwa katika batili, hata hiyo nguvu ya mfumo unayoihoa, haitaweza kukusaidia kitu zaidi ya kukutia utumwani

IGP Said Mwema wakati u-kiumbe huru. Kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, katika maoni yake juu ya Katiba Mpya, Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda amependekeza kuwa kuwe na Tume itakayoshughulikia kero na mambo mengine ya muungano akisisitiza kuwa hakuna sababu ya kulumbana ila kinachotakiwa ni kutatua kero zilizopo ili kwa pamoja tuendelee kuuenzi na kuudumisha (muungano) kwa faida ya Watanzania wote. Swali hapa ni je, Tume na Kamati ngapi zishaundwa kutatua kero za muungano

Kongamano
Mahala: Msikiti wa Tungi Temeke Siku: Jumamosi Tarehe 2.2.2013

Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu Tanzania linawaalika wanawake wote wa Kiislamu kuhudhuria katika kongamano kubwa la aina yake litakalofanyika Inshaalah.

Saa: Kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni. Mada: Nafasi ya mwanamke wa Kiislamu katika harakati za Kiislam. Mhadhiri: Ahmad Ayoub kidege kutoka Tanga. Kila atakayesikia tangazo hili amwaarifu na mwenzie. Naibu Katibu Taifa Ukhut Mayasa Sadallah

8
WANANCHI wa Israel walipiga kuna mnamo 22 Januari 2013. Kati ya makundi 34 yaliyogombea kura, walioshinda ni vyama vya mrengo wa kulia vinavyopigania upanuzi wa makazi haramu ya Wayahudi katika maneo ya Palestina yaliyovamiwa na Israel. Matokeo ya uchaguzi huu unaonyesha kupungua kwa nguvu za kisiasa za Netanyahu. Ingawa inawezekana akaendelea k u w a Wa z i r i M k u u . Hata hivyo uwezo wake wa kuendelea na ubabe utapungua, hasa kwa vile chama cha msimamo wa wastani, Yesh Atid, kimejitokeza na huenda kikajiunga na serikali mpya ya mseto kwa kuweka masharti yake yenyewe. Yesh Atid kimeshinda viti 19 na kimekishinda chama cha Labor Party, ambacho kimepata viti 17. Wakati huohuo chama cha mrengo wa kushoto cha Meretz kimeongeza maradufu viti vyake na kukia sita badala ya vitatu ilivyokuwa navyo hapo zamani. Licha ya aibu hii aliyopata Netanyahu, haimaanishi kuwa sera kali za Israel zitatulia. Inamaanisha tu kuwa sera hizo za kivamizi zitakuwa zikitekelezwa kwa uangalifu badala ya kwa jeuri. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Israel, suala la amani halikupewa umuhimu sana katika ya kampeni. Hii haistaajabishi, kwani kura ya maoni iliyoendeshwa na asasi ya Israel Democracy na Chuo Kikuu cha Tel Aviv, ilidhihirisha kuwa asilimia 67 ya wananchi wa Israel waliunga mkono mbinu ya serikali yao ya kuchelewesha mchakato wa amani. Kwa kweli, matokeo ya kura za maoni zilizoendeshwa tangu mwaka jana imeonyesha kuwa raia wengi wa Israel wanapendelea hali iliyopo iendelee kuliko kuleta maelewano kati yao na Wapalestina. Aidha, serikali zote zilizoundwa na vyama tofauti mpaka sasa zimekuwa zikipigia

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013 H i v y o Wa p a l e s t i n a hawakuwa na matumaini sana. Viongozi wa chama cha Fatah walikuwa na mashaka kuhusu uwezo wa serikali mpya ya Israel kujihusisha na mazungumzo ya amani yenye tiba. Yasser Abed Rabbo, msaidizi mwandamizi wa Rais wa Palestina Bw Mahmoud Abbas, alisema, Ni dhahiri kuwa Israel haitapata serikali yenye uwezo wa kuendelea na mazungumzo ya amani. Naye Rais Mahmoud Abbas alinena kuwa serikali yoyote itakayotawala Israel, italazimika kuendelea na mazungumzo ya amani, pamoja na kutimiza majukumu yake ya kimataifa. Kutawala kwa serikali ya mrengo wa kulia hakutushitui hata kidogo, aliliambia gazeti ya Itali liitwalo La Repubblica. Na Waziri Mkuu wake Salam Fayyad aliwaambia waandishi kuwa Israel ni lazima itekeleze wajibu wake wa kimataifa. Tuonavyo sisi, matarajio ya ulimwengu kwa Israel ni sawa na ya kwetu, alisema said. Iwapo atamuingiza Lapid katika serikali yake, basi Netanyahu atakuwa anajifagilia mbele ya ulimwengu. Hata hivyo jambo hilo halitamzuia kuendelea kupanua makazi haramu, hasa katika Jerusalem (Al Quds) Mashariki, alisema Mohammed Ishtayeh, mshauri mwandamizi wa Rais Abbas. Msemaji wa chama cha Fatah Bw Ahmed Assaf alisema: Wapalestina ndio watakaoachwa nyuma katika mvutano huu miongoni mwa vyama vya mrengo wa kulia. Kwani jambo hilo litapelekea kukwama kwa mchakato wa amani na kuwavunja moyo Wapalestina. Wakati huo huo raia wa Israeli nao watadhurika kwa sababu hawatakuwa na usalama na amani iwapo Wapalestina watanyimwa haki zao kama taifa. Ndio maana Wapalestina hawana matumaini kuwa amani itapatikana baada ya uchaguzi.
Inaendelea Uk. 15

AN-NUUR

Matokeo ya uchaguzi wa Israel yalivyopokewa na Wapalestina

WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

debe upanuzi wa makazi haramu. Katika kura ya maoni ya Chuo Kikuu cha Tel Aviv, raia wa Israeli waliulizwa nani ni bora zaidi katika kuongoza masuala ya jamii na uchumi. Asilimia 45 walisema ni chama cha Labour kinachoongozwa na Shelly Ya c h i m o v i c h , w a k a t i asilimia 36 walimtaja kiongozi wa Likud, Benjamin Netanyahu. Netanyahu amekuwa akitumia sana ukaburu wa Israeli, akiiga staili ya rais wa zamani George W Bush aliyekuwa akitumia mbinu ya tishio kutoka nje. Matokeo yake ni kuwa Netanyahu amefanikiwa kupoteza lengo kwa kuwachanganya wapiga kura. Matokeo yake uwoga wa kigeni ulitawala kampeni badala ya kutumia hoja yakinifu. Yaani Waziri Mkuu Netanyahu alikuwa akisisitiza sana tishio la Iran badala ya kuzungumzia makazi ya Wayahudi ambayo ndiyo yanayotishia usalama wa dunia. Inakumbusha zaidi ya miaka 20 iliyopita

wakati Waziri Mkuu wa Israeli, Yitzhak Shamir alimwambia rais George Bush kwamba Iraq ni tishio kubwa la amani na kwa hiyo lazima ishughulikiwe kabla ya kuzungumzia amani na Wapalestina. Labda miaka kumi ijayo, kiongozi mwengine wa Israeli atajitokeza na kubuni tishio lingine ili kuepukana na lawama ya kuivamia of Palestina. Inasikitisha kuwa ulimwengu unaendelea kudharau ukweli kuwa tishio kubwa la amani duniani ni uvamizi na udhalimu wa Israel nchini Palestina na wala si haya matishio bandia yanayobuniwa na Israel. Hivi karibuni hata Rais Barack Obama alinukuliwa akisema katika mazungumzo ya siri: Israel haielewi maslahi yake. Hata Waziri Mkuu wa zamani wa Israeli, Ehud Olmert, aliiambia Channel 7 nchini Israel kuwa serikali ya sasa ya Israel haina hamu kabisa na amani wala haina lengo la kukia makubaliano na wananchi wa Palestina. Sasa baada ya matokeo kutangazwa Israel

itaendelea kuongozwa na Waziri Mkuu ambaye alijitapa kwa faghari mwaka 2001 kuwa azma yake ni kukomesha mchakato wa kuleta amani. Ukweli ni kuwa tangu kuchaguliwa kwake mnamo 2009, sera ya Netanyahu ya kujenga makazi haramu imevuruga kabisa uwezekano wa kuunda taifa huru la Palestina. Netanyahu anasema yeye anakubaliana na lengo la kumaliza mgogoro kwa kuunda mataifa mawili. Lakini wakati huohuo, anaendelea kupanua makazi haramu katika maeneo ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi. Jambo hili limewafanya wengi waamini kuwa yeye hana azma yoyote ya kuleta amani. Kabla ya uchaguzi Wapalestina walionesha wasiwasi wao kuhusu uchaguzi huu usivyotabirika. Wengi wao walihofu kuwa ushindi utakwenda kwa vyama vya mrengo wa kulia vyenye siasa kali. Wao wakishinda, basi matokeo yake ni kudidimia kwa mchakato wa amani unaoyumba.

Uingiliaji kijeshi Mali na ugawaji upya wa Afrika: Mkondo mpya wa uharamia


Na Ben Schreiner January 15, 2013 (Mtandao wa kupashana habari) UINGILIAJI kijeshi wa Ufaransa nchini Mali hivi karibuni -mara ya pili Ufaransa imefanya hivyo ndani ya miaka miwili kwa nchi iliyokuwa koloni lake zamani - ulitangazwa kuwa umeungwa mkono na Marekani. Hii haiwezi kuwa ni habari ya kushangaza, ukizingatia jinsi Pentagon (makao makuu ya Jeshi la Marekani) inavyopenyeza makucha kwa ndani katika Afrika. Kwa mujibu wa Kamandi Maalum ya Afrika (AFRICOM), Pentagon inatazamia kupeleka vikosi katika nchi 35 za Afrika mwaka wa 2013. Mtandao mmoja wa habari, NPR unaarifu kuwa zaidi ya askari 4,000 wa Marekani watashiriki katika mazoezi ya kijeshi kutoa mafunzo kwa askari wa Afrika kuhusiana na nyanja tofauti, kama kubeba vifaa, kulenga shabaha na huduma za tiba. (Osa wa kijeshi wa Mali aliyehusika na kupindua serikali mwezi Machi mwaka jana imetokea kuwa alikuwa vile vile amepata mafunzo hayo ya kijeshi ya Marekani). Bila shaka, Jeshi la Marekani tayari lina uwepo katika maeneo mengi Afrika. Kwa mfano, kituo chenye shughuli nyingi zaidi za ndege za mawindo zisizo na rubani (drone) nje ya eneo la vita la Afghanistan, kikiwa na miruko 16 ya drone kwa siku, kiko Camp Lemonnier nchini Djibouti. Hata hivyo kama gazeti la kijeshi la Army Times linavyoeleza, eneo hili kwa sehemu kuwa ni ukanda usiojulikana kwa majeshi la Marekani. Hivyo, ili Marekani itiishe dunia kwa j u mla, h ak u n a maen eo yasiyotiishwa ambayo mipaka yake haitaondolewa. Hivyo, kama taarifa ya mwezi Juni mwaka jana katika gazeti la Washington Post ilivyosema, vianzio kuhusu ugaidi kokote? Kama Rais Francois Hollande wa Ufaransa alivyosema akitangaza hatua hizo, magaidi inabidi wajue kuwa Ufaransa wakati wote itakuwepo wakati haki za watu, hao wa Mali ambao wanataka kuishi kwa uhuru na katika demokrasia, zinapohatarishwa. Fikra ya wakati wetu, hasa inapokuja katika kuhalalisha vita, anaandika Jean Bricmont katika kitabu chake, Ubeberu wa Kiutu, ni aina fulani ya msisitizo kuhusu haki za binadamu na demokrasia. Na, tunaweza kuongeza, utumiaji kijanja wa dhana ya kupambana na ugaidi. Ni wazi, kwa maana hiyo, kuwa dhana kuwa shauku mpya ya nchi za Magharibi kuhusu Afrika inatokana na nia ya dhati ya kusaidia nchi za Afrika kupambana na ugaidi ni kichekesho. Ilikuwa ni ushirika wa NATO, ikiwa itaanza kusahaulika, ambao ulifungamana kwa dhati na wapiganaji wa ki-Salafi (wanaharakati wa mrengo wa Kisaudia) kumpindua Muammar Gaddafi nchini Libya. Isitoshe, ni ushirika huo huo wa kijeshi ambao hivi sasa unawashangilia wapiganaji wa ki-Salafi nchini Syria, wakati inawapiga mabomu katika eneo la Afghanistan na Pakistan, Somalia, Yemen na sasa Mali. Ni wazi kuwa ni wale tu wenye uwezo wa undumila kuwili kifikra watafaulu kuelewa mkakati unaobadilika kila siku wa vita dhidi ya ugaidi ya Magharibi. Ndiyo maana, pale mitandio ya kulinda demokrasia na kupigana na ugaidi inapoinuliwa, uso halisi wa uharamia unachuliwa. Hivyo, suala la msingi linalosimika shauku mpya ya Magharibi kwa Afrika, kama Conn Hallinan anavyosaidia kueleza, ni mbio za kukamata utajiri mkubwa wa Bara hili. Marekani hivi sasa inapata asilimia 18 ya mahitaji yake ya nishati kutoka Afrika, kiwango ambacho kinatazamiwa kupanda na kufikia asilimia 25 hadi mwaka 2015, Hallinan anaandika. Afrika pia inatoa kiasi cha theluthi moja ya mahitaji ya nishati ya China, pamoja na shaba, platinum, mbao na chuma. Zaidi ya hayo, kama Maximilian Forte anavyoainisha katika Msukumo Kuelekea Sirte, maslahi ya China yanaonekana kushindana na nchi za Magharibi katika kupata raslimali na ushawishi wa kisiasa. AFRICOM na mikakati mingine ya serikali ya Marekani ina nia ya kukabiliana na hali hiyo. Na hii inaeleza kwa nini NATO ikajitosa Libya mwaka 2011, akaondolewa kiongozi mbishi wa kizalendo barani Afrika ambaye alikuwa tishio la juhudi za kupanua AFRICOM katika eneo la mwisho ambalo Jeshi la Marekani halijalidhibiti. Na pia inaeleza uingiliaji huu unaoongozwa na Ufaransa na kuungwa mkono na Marekani nchini Mali, ambao unaainisha kusimika kwa nguvu maslahi ya nchi za Magharibi katika Afrika. Uingiliaji, kama tunavyoona, unazaa uingiliaji. Na kama Nick Turse alivyoonya mwezi Julai (mwaka jana), Mali inaweza kuwa ndiyo mwanzo tu na huwezi kujua hali hiyo itakia wapi. Kinachoonekana kiko bayana ni kuongezeka kwa mkondo wa uharamia, kwa jinsi kugawana upya Afrika kunavyopamba moto. (Ben ni mwandishi wa kujitegemea anayeandika kuhusu Marekani na siasa za kimataifa. Ana shahada moja ya taaluma ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Willamette cha Salem, jimbo la Oregon nchini Marekani na hivi sasa anasomea shahada ya uzamili katika uandishi wa habari kutoka Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, Anapatikana kupitia anuani ya bnschreiner@gmail. com. http://www.workingleft. blogspot.com)

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

vya uwepo wa jeshi la Marekani tayari vimejikita maeneo mengi Afrika. Kama lilivyosema gazeti hilo, ndege za upelelezi za Marekani zinaendesha shughuli zake katika makambi yasiyo rasmi katika nchi za Burkina Faso, Mauritania, Uganda, Ethiopia, Djibouti na Kenya, na mipango inaendelea kuweka kambi nyingine Sudan Kusini. Post iliripoti zaidi kuwa Pentagon inatumia dola milioni 8.1 kuboresha kambi ya kukaribiana na medani (za vita) na uwanja mdogo wa ndege nchini Mauritania, katika ncha ya magharibi ya jangwa la Sahara. Kambi hiyo iko karibu na nchi yenye machafuko ya Mali. Inapokuwa na amana kama hizo zimewekwa tayari, Pentagon ilikuwa na nafasi siyo tu ya kuunga mkono uingiliaji kijeshi wa Ufaransa, lakini kama gazeti la New York Times lilivyosema, Marekani iliweza kupima njia tofauti za kusaidia juhudi za Ufaransa, ikiwa ni pamoja na ushirikiano wa karibu zaidi wa kupeana taarifa za upelelezi na kuongezea vifaa. Akifafanua nini msaada wa Marekani unaweza

kuwa nchini Mali, J. Peter Pham, Mkurugenzi wa Kituo cha Afrika cha Baraza la Atlantiki (la NATO) ambaye pia ni mshauri mwandamizi wa AFRICOM, alisema: Mashambilizi ya ndege zisizo na rubani hayatarudisha umoja wa nchi au kuwashinda wanaharakati wa Kiislamu, lakini ndiyo njia pekee rahidi zaidi. Ni ishara ya mambo magumu baadaye, ikifahamika kuwa njia hiyo rahisi zaidi imeshasababisha vifo vya mamia ya watu wasio na hatia katika kampeni ya mashambulizi ya drone. Bila shaka, kama ilivyo katika kampeni ya kutumia ndege hizo zisizo na rubani, kuingia kwa Pentagon katika Afrika kunakuja ndani ya kifurushi chenye anuani kuwa ni mwendelezo wa vita dhidi ya ugaidi. Kama taarifa ya Army Times ya mwezi wa Juni inavyoeleza, Afrika, zaidi, imeibuka kuwa eneo muhimu kwa serikali ya Marekani kwa sababu vikundi vya kigaidi eneo hilo vimekuwa tishio linaloongezeka kwa Marekani na usalama wa ukanda huo. Kwani ni uingiliaji upi kijeshi ambao haujahalalishwa kwa kutumia mojawapo au nyingine ya wasiwasi

Ipi zaidi, kupambana kukomboa gesi au nchi?


Na Ahmed Omar Khamis

10

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

WAHENGA walisema adhabu ya kaburi aijuae ni maiti. Dunia imewahi kuishuhudia Tanzania ikipambana vikali na Uganda katika mwaka 1979 kwa madai ya kuvamiwa na sehemu ya nchi yake katika Mkoa wa Kagera kukaliwa kwa mabavu na Iddi Amin. Halikadhalika dunia imewahi kushuhudia mara kadhaa Tanzania ikikwaruzana na jirani yake mwengine, Malawi, kwa madai kwamba eneo lake la ziwa Nyasa linatala kuvamiwa na nchi hiyo. Tumewahi kushuhudia pia jamii mbali mbali za Watanzania wakiuwana na kuchinjana kwa kugombania raslimali kadhaa, kila mmoja akidai kudhulumiwa. Hili limejitokeza wazi katika mapambano kadhaa ya kugomania raslimali ya ardhi, raslimali za madini nk. Hivi sasa mapambano yamepamba moto katika raslimali ya gesi iliyoko katika Mkoa wa Mtwara. Somo lililopo katika utangulizi hapo juu ni kwamba kumbe kila mmoja anathamini kitu chake na kukiona ni bora kuliko cha mwenzake, na bila shaka yuko tayari kwa lolote lakini kitu chake hicho kisimtoke mikononi mwake. Hii ndio maana Tanzania iliingia vitani na Uganda kuipigania Kagera, hii ndio maana Tanzania imekua ikitishia mara kadhaa ikilazimika itaingia vitani na Malawi kulinusuru ziwa Nyasa. Halikadhalika hii ndio maana Watanzania wa jamii mbali mbali wamekua wakipigana wenyewe kwa wenyewe kama vile jamii za wafugaji dhidi ya wakulima. Wamekua wakipigana na wawekezaji katika maeneo yao kama vile mapambano ya wanavijiji dhidi wamiliki wa migodi. Hakadhalika wananchi wamekua wakipambana na serikali yao kukataa maamuzi ambayo kwa mtazamo wa wananchi wa maeneo hayo

ni kuibiwa raslimali zao na badala yake ni kwenda kuwanufaisha wengine. Mfano wa haya ndio kama yanayojiri hivi sasa katika Mkoa wa Mtwara. Wananchi wa Mtwara wanaendelea kupambana na serikali huku watu kadhaa wakipoteza roho zao alimradi tu wanahakikisha raslimali yao ya gesi haitoki ndani ya Mtwara na badala yake inabaki Mtwara na inatumika kwa ajili ya maslahi na maendeleo ya watu wa Mtwara kwanza. Maelezo yote hapo juu yanaonyesha j i n s i Wa t a n g a n y i k a walivyokua mashujaa kupambana na mataifa jirani ili kulinda maeneo ya nchi yasivamiwe. Pia maelezo hayo yanaonyesha j i n s i Wa t a n g a n y i k a wenyewe kwa wenyewe (jamii moja na nyengine) wanavyopambana kwa ushujaa ili kulinda maslahi ya sehemu zao, ardhi zao au raslimali za jamii zao husika zisichukuliwe na wengine. Sasa basi, iweje iwe ni jambo dogo linaloonekana halina maana kwa Wazanzibari kusimama kidete, kujaza munkari, mori na hamasa kupigania nchi yao iliyomezwa na kupokonywa mamlaka yake yote ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutawala? Hivi ni mtu gani mwenye akili yake asiyefahamu kama

gesi haina thamani mbele ya nchi nzima? Mbele ya utamaduni wa taifa zima? Mbele thamani ya watu wa taifa zima? Alipopambana Mzee Aboud Jumbe wakati ule wa Mwalimu Nyerere, yaliitwa ni machafuko tu ya hali ya hewa Zanzibar yaliyolengwa kuuhatarisha Muungano. Machafuko ambayo yalihitaji kudhibitiwa kwa kufukuzwa Mzee Jumbe katika kiti cha urais wa Zanzibar. Alipopambana Maalim Seif na wenzake wakati ule wa Nyerere ulionekana ni uchochezi uliolengwa kuigawa CCM na kuuhatarisha Muungano, uchochezi ambao ulihitaji kudhibitiwa kwa kufukuzwa Maalim Seif na wenzake katika chama na katika nyadhifa za serikali. W a n a C U F walipoandamana mwaka 2001, pale Unguja na Pemba enzi ya Mheshimiwa Benjamin William Mkapa kudai pamoja na mambo mengine mabadiliko ya katiba ya Tanzania ili kutoa fursa ya muungano wa haki na usawa baina ya Tanganyika na Zanzibar, walifanywa kama wahalifu tu na hivyo kuvamiwa na vikosi vyote vya ulinzi na usalama na kumiminiwa risasi za moto na kusababisha vifo

vya watu wasiopungua 50, walemavu, wajane, mayatima na maelfu ya wakimbizi. Halikadhalika Wazanzibari walipopambana na vyombo vya dola mara kadhaa katika mwaka wa 2011/2012 chini ya harakati za taasisi za Kiislamu kudai Muungano wa haki, hadhi na heshma ya Zanzibar kurejeshwa, waliitwa wahuni, magaidi, Alshababb, Alqaida nk. Walivamiwa na polisi kupigwa, kuumizwa, kuwekwa vizuizini na kufunguliwa kesi wao na viongozi wao wa harakati hizo. Hapa ndipo pale penye lengo la makala yangu hii. Lengo ni kuwauliza watawala wa Jamhuri ya Muungano na wale walioko Zanzibar, kama Wazanzibari wanaopigania nchi yao nzima ni wahuni, magaidi, Alshabab na Alqaida, jee hawa wanaopigania gesi tu isichukuliwe tena na serikali yao wenyewe tuwaite vipi? Kati ya hawa Wazanzibari waliopigana kujibu na kupinga maonevu ya vyombo vya dola dhidi ya harakati zao, na wale waliojipanga wenyewe kuanzisha harakati za mapambano ya kupinga gesi yao isitoke nje ya Mtwara, ni nani gaidi zaidi? Alkaida zaidi? Muhuni zaidi? Au Alshabab zaidi? Wazanzibari tunasema

kama ambavyo wana Mtwara wanayo sababu ya kupambana kulinda gesi yao isichukuliwe kwenda kuimarisha Dar es Salaam, Dodoma na Arusha; basi Wazanzibari wanazo zaidi sababu za kupigania nchi yao na hatimae kuirejesha katika mikono yao hata kama wataendelea kuitwa magaidi, alshabab, alqaida, wahuni nk. Wataendelea na mapambano ya kuimezua nchi yao hata kama makombora yote makubwa ya Tanganyika yataelekezwa Zanzibar. Kama wana Mtwara wanayo sababu ya kuipigania gesi yao ambayo bado imo katika matayarisho ya kuchukuliwa Dar es Salaam, basi Wazanzibari wanazo zaidi sababu za kupigania nchi yao iliyomezwa miaka 49 iliyopita na raslimali zake kadhaa kuibiwa na watu wake kuachwa maskini tokea miaka hiyo hadi leo. Wanaoijuwa athari ya gesi ya Mtwara kwenda Dar es Salaam na kuwaacha watu wa Mtwara waki endelea kuwa masiki ni watu wa Mtwara. Halkadhalika, waijuwao athari ya Zanzibar kumezwa na Tanganyika h u k u Wa z a n z i b a r i wakibakia wanyonge hawana maamuzi, hawana heshma ya nchi yao, hawana mamlaka ya nchi yao na uchumi wao ukizidi kufa ni Wazanzibari. Adhabu ya kaburi aijuae ni maiti. Wazanzibari wamechoka kunyanyasika na wataendelea kupambana kuliko walivyowahi kupambana mpaka watakapoyatia mikononi mwao mamlaka kamili ya nchi yao. Jamhuri ya watu wa Zanzibar Kwanza! Wala isidhaniwe kuwa yale yaliyowakuta Mzee Aboud Jumbe na Maalim Seif Shariff Hamad yatawakatisha tamaa Wazanzibar. Tunasema kuwa hiyo ni gharama stahiki ya kuipata Zanzibar yetu. Ndio maana tunawasikia Mzee Moyo, Waheshimiwa Dr. Amani Karume na Dr. Salmin Amour wakiachana na siasa muflisi za Kisonge na kusimama na Wazanzibari kuipigania Zanzibar.

Umaarufu wa Mwalimu wa kutengenezwa


Inatoka Uk. 6 Wa t a n z a n i a h a t u n a utamaduni wa kuwajadili viongozi waliotangulia, akimaliza muda wake tunampa heshima zote na tunasema Mwacheni Mzee Apumzike na hili limechangia sana kurudisha maendeleo ya nchi nyuma. Viongozi hawaogopi kuwajibishwa wanajua watalindwa kama wenzao walivyolindwa. Hivyo lazima turudi nyuma tuangalie tumejikwaa wapi ili tukingoe hicho kisiki mwingine akija apite kwa usalama zaidi. Mimi bado naamini kwamba kama hatutataka kuweka wazi mazuri na maovu ya Nyerere, basi hata tufanyeje hatuwezi kufika huko tunakotarajia, tutaendelea kumtafuta mchawi mpaka Millennium hii ipinduke, na hata kikaja chama kingine kama kisipochambua matatizo ya nchi tangu ilipopata uhuru, basi hakiwezi kufika huko kinakotarajia. Tukimchambua Nyerere tutakuwa tumevunja mwiko wa kulindana hivyo hakuna atakayepona tena, na kila mtu atachambuliwa na kupewa haki yake. Kumjadili mtu si vibaya na wala siyo hukumu, bali kumjadili mtu ni kuweka wazi mazuri na mabaya aliyoyatenda; na kama mazuri yatakuwa yamezidi mabaya basi, atapewa haki yake, kwa vile hakuna binadamu asiyekuwa na kasoro. Ndugu zangu wa Vyama vya Upinzani huwa wananikera sana pale wanapopanda majukwaani na kuanza kushindana kumsia Nyerere! Huo upinzani gani? Au ni upinzani wa kubadili sura za watu tu lakini system ni ile ile? Wapinzani msiwadhihaki Watanzania; kama mnaipenda system ya Nyerere rudini CCM ili mumuenzi Mwalimu vizuri. Watanzania wanataka mabadiliko ya kweli, na mabadiliko ya kweli hayawezi kutokea bila ya kumchambua Nyerere na System yake yote, kinyume na hivyo itakuwa ni danganya toto! Watanzania wengi wamekuwa wakitaka Mzee Benjamin Mkapa ajadiliwe na hata ashitakiwe na kukishwa mahakamani, lakini kwa nini tuanze na Mkapa? Wakati Nyerere tumeshamtawaza siku nyingi kuwa Nabii wa nchi hii? Na nasikia minongono kwamba eti Kanisa la Katoliki linataka kumtangaza Nyerere kuwa Mtakatifu; kama hiyo ikitokea, basi Nyerere atakuwa amevunja rekodi ya dunia
kwa vile haijapata kutokea kiongozi wa nchi, mwanasiasa kutawazwa kuwa Mtakatifu, na ukizingatia ni kiongozi wa nchi ya siasa za Kijamaa, siasa za ugandamizaji, siasa za usiri, kila kitu ni siri, siasa za kudhulumiana. Siasa za matabaka ya watawala na watawaliwa, siasa za vitisho, mateso na kuuwawa kimya kimya kwa raia wasiokuwa na hatia, siasa za mitandao ya uhalifu wa kupangwa (Mob of Organized Crimes)! Huwezi kuwa Rais wa nchi ya Kijamaa halafu mwisho wa siku uwe Mwenyekheri, haiwezekani kabisa, kwa vile siasa ni mchezo mchafu sana: unadanganya wananchi kwa kutoa ahadi za uongo zisizotekelezeka, wakigundua kwamba unawadanyanya wakiamua kuandamana unatuma polisi wawavunje miguu na hata kuuwawa; unawaibia wananchi wakilalamika unawaangamiza kimya kimya chini kwa chini bila ya kujulikana; unafanyika uchaguzi wananchi wanaamua wasikupigie kura, unashindwa, lakini hutaki kukubali unalazimisha umeshinda uchaguzi na upo tayari nchi iende vitani potelea mbali. Suala muhimu wewe uendelee kuwa rais wapende wasipende. Wakati mwingine waweza toa amri baadhi ya watu wafungwe gerezani, au uwaweke vizuizini. Watawala wa siasa za Kijamaa, wakimkataa mtu hata kama watakuwa wamemkataa kwa uonevu au kumuonea, basi wao wanaamini kwamba dunia nzima nayo lazima imkatae, kwa vile hawatataka akubalike popote pale duniani, watahakikisha wanatumia pesa nyingi sana huku wakishirikiana na mitandao mingine ya nchi uliyohamia au nchi ambayo au ambazo ana maslahi nako, ili mradi tu wahakikishe kwamba na huko nako hukubaliki; hizi ni mila na desturi za kijinga na hazitofautiani na mila za Kichawi (Witch hunting), kwa vile ukiwakosea wachawi wa kijiji kimoja na ukakimbilia kijiji kingine, usidhani umepona, hapana, watatafuta mawasiliano na wachawi wa kijiji ulichohamia ili mradi tu wahakikishe wamekula nyama yako! Katika utawala wa Nyerere M z e e K a s a n g a Tu m b o aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, serikali ilimfukuza kazi Kasanga Tumbo na kumrudisha nyumbani na kumuweka kizuizini kwa vile alizungumza na Oscar Kambona; Oscar Kambona wakati Nyerere anatangaza Azimio la Arusha, Kambona alipinga Azimio la Arusha hivyo Nyerere akamfukuza kazi na aliondoka nchini na kuhamia Uingereza kama mkimbizi wa kisiasa; wazee wa zamani wanasema Tumbo na Kambona walikuwa marafiki hata kabla nchi haijapata uhuru na walikuwa ni miongoni mwa wale waliokuwa mustari wa mbele katika kupigania uhuru wa nchi hii! Baadhi ya Marais wa zamani wa taifa la Marekani kama vile George Washington, Abraham Lincoln, Ronald Reagan na Bill Clinton ni miongoni mwa maraisi ambao wamefanya mambo makubwa sana katika taifa lao, na hadi leo hii Dollar ya Marekani inaheshimika kila kona ya dunia, na Marekani ni Mother of Technology, Marekani ina uchumi mkubwa kuliko nchi yoyote ile duniani (US $ 13 Trillion), lakini pamoja na miujiza yote hii Wamarekani hawajafikiria na wala haitakuja wakirie kuwatawaza Marais hawa wa zamani kuwa Watakatifu! Sasa najiuliza Nyerere anapewa Utakatifu kwa lipi!? Au Utakatifu umegeuka wadhifa wa Kisiasa ambao unashabikiwa na Mitandao ya chini kwa chini ya wanakitengo? Huwezi kuwa Mwanasiasa na mwisho wa siku uwe Mtakatifu, labda kama Makanisa ya siku hizi yanaongozwa na Wanasiasa na Mitandao yao ya Usalama wa Taifa! Tusicheze na Mungu. Mungu hapendi na wala hataki kufanyiwa Dhihaka! Dr. Mohamed Mahathari alikuwa Waziri Mkuu wa Malaysia, huyu bwana alitawala wakati mmoja na Nyerere, miaka ya sitini mwanzoni ikumbukwe Tanzania ilikuwa na vitega uchumi vingi kuliko Malaysia na ilikuwa imeendelea zaidi katika sekta mbali mbali ukilinganisha na Malaysia. Baada ya kutawala Malaysia kwa miaka 20 tu, Dr. Mahathari alistaafu na kukabidhi nchi kwa Wamalaysia lakini amekabidhi nchi ikiw a imetoka kwenye dunia ya tatu na kuingia kwenye dunia ya kwanza. Ameikabidi nchi ikiwa kinara kwa kutengeneza computer na vifaa mbali mbali vya electronics duniani; ameikabidhi nchi ikiwa ni moja kati ya nchi 21 zinazouza bidhaa nyingi nchi za nje duniani; ameikabidhi nchi ikiwa imetoka kwenye nchi masikini na kuwa nchi tajiri duniani; ameikabidhi nchi ikiwa imetoka kutegemea kilimo cha ujima na sasa ni nchi ya viwanda duniani; ameikabidhi nchi ambayo ilikuwa tegemezi wa misaada toka kwa nchi zilizoendelea na hivi sasa haihitaji msaada wowote toka nje, bali nchi yenyewe imekuwa ikiwekeza kwenye miradi mbali mbali

11

Makala/Tangazo

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

MWALIMU Julius Kambarage Nyerere duniani (Potential Investor). hawajawahi kukiria kumuita Dr. Mahadhari alisimamia Baba wa Taifa lao. Anaweza na kutengeza Katiba nzuri akawa amefuzu kuitwa hivyo, ya nchi hiyo ambayo hasa lakini wakawa hawataki kwa ndiyo iliyoweza kusimamia vile siku zote na popote pale mafanikio ya nchi hiyo, Siasa ni Mchezo Mchafu. Katiba inayolinda maslahi (Makala hii imeandikwa na ya umma na wala siyo Katiba inayolinda maslahi ya mtu Dr. Noordin Jella (Ph.D. in Economics) mmoja. Malaysia ilikuwa haina F o r m e r L e c t u re r o f t e c h n o l o j i a l a k i n i s a s a Mzumbe, Open & KIU inatengeneza kila kitu kuanzia D a r, U n i v e r s i t i e s . sindano hadi ndege, hivi Currently: Freelance karibuni inatarajia kupeleka Journalist & Seasonal Rocket kwenye Orbit. Email: Pamoja na miujiza yote hii Political Analyst ya mafanikio yaliyofanywa norjella@yahoo.com Mobile: +255 782 000 na Dr. Mohamed Mahathari, lakini bado Malaysia wala 131)

Inapenda kutoa shukran zake za Dhati kwa mahujaji wote waliosari na Ahlul-daawa. Pia inatangaza kua imeandaa safari ya Umra Mfungo wa Saba ni sawa na machi 11 2013 kwa Gharama ya Dola 1450 tu. Inaendelea kuandikisha mahujaji kwa Mwaka 2013. Wale watakao jiandikisha na kufanya malipo mapema watapata punguzo maalumu la bei. Usisahau Ahlu Daawa Hajj kwa Bei nafuu na huduma bora. Kwa mawsiliano piga simu zifuatazo. Dar es salaam: 0773 724444, 0715 786101 na kwa Zanzibar 0777 417736, 0777484982.

AHLU-DAAWA HAJJ

12
Mnataka Mwembechai nyingine
Salamu alaykumu, Islamu Tanzania, Nyakati lamuhujumu , Shekhe Ilunga kuua , Gazeti limetuhumu , na picha kubwa kutoa, Ilunga si muuaji, Mhariri kakosea. Wala Ilunga hatishi , mzushi kamzushia , Shekhe wetu ni mcheshi, yu karibu na raia, Na wala sio mbishi, kwa dini apigania, Ilunga si muuaji, mhariri kakosea. Kanipa kichefuchefu, gazeti kuangalia , Maneno yake machafu, amani yanatishia, Labda hana uzoefu, kazi anajifunzia, Ilunga si muuaji, mhariri kakosea. Ilunga kaua nani, mbona hakutuambia, Hayo ni yenu maoni, kanisani mlikaa, Ya kwenu hamuyaoni, Lwambano alivyoua, Ilunga si muuaji, mhariri kakosea. Nyie tumeshawajua, Serikali kuburuza, Lwambano twakumbukia, kauli alitangaza, Mwembe chai wakaua, na damu kuisambaza, Ilunga si muuaji, mhariri kakosea. Wanafanya mikakati, kukamatiwa Ilunga, Kije kizungumkuti, serikali kumfunga , Ilunga ni madhubuti, hana mambo ya kutunga, Ilunga si muuaji, mhariri kakosea. Viziwi mnajidai, vipofu mlobobea, Mabubu hamsemei, mfumo kukumbatia, Kutuona hatufai, Islamu Tanzania, Ilunga si muuaji, mhariri kakosea. Tumevumilia sana, tangu uhuru sikia, Serikali kutubana, madhila yametujaa, Na hatutofungamana , njuga tutaivalia, Ilunga si muuaji, mhariri kakosea. Mwisho ninatoa wito, Islamu Tanzania, Nyakati ni la kitoto, muda lawapotezea, Soma kisha choma moto, mikakati endelea, Ilunga si muuaji, mhariri kakosea. Mwl. Zabibu I Ngonda - Mwanza

Barua/Shairi

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

Viwanja vilivyopimwa vinauzwa Kongowe Kibaha


1118 sqm - 4 Milion, 1261 sqm 5 milion, 1348 sqm 5.5 milion, 674 sqm 3 milion, 848 sqm - 3.4 milion, 510sqm - 1.5 milion, 516sqm - 2 milion, 522sqm - 2 milion, 523sqm - 2 milion, 646sqm - 2.6 milion, 656sqm - 2.6 milion, 474sqm 1.8 milion, 456 sqm 1.8 milion, 538 sqm 1.8 milion, 469sqm 1.9 milion, 406 sqm 1.6 milion, 356sqm 1.5 milion, 399sqm 1.6 milion, 359sqm 1.5 milion, 612sqm 3 milion. Vipo Barabara ya Kongowe-Soga Kilomita moja toka barabara ya Morogoro. Simu No.0755 090 754/0715 090 754.

KWA waumini wa dini na imani zote zile duniani, sina shaka wanatambuwa umuhimu wa kutenda wema, na kuwatendea wema wengine. Wema kwa mtazamo wa kiimani, ni kufanya yote ambayo Mola anaridhia ikiwa ni pamoja na kusaidia wanaokulazimu na hata jirani zako. Wema ni kuishi na watu vizuri na kuwatendea haki watu wote hasa wale unaowasimamia au wanaokutegemea. Haya ndio mafunzo ya dini na imani yasemavyo. Lakini pamoja na mafunzo hayo, tumeonywa sana kutofanya wema uliopindukia uwezo wetu. Yaani kwa lugha nyepesi, tunasema wema usizidi uwezo. Pia tunatanabahishwa kwamba, pamoja na kuwa ni wema mkubwa kumkirimu mgeni na jirani yako, ni bora zaidi kujikirimu wewe mwenyewe na wanaokuzunguka au kukutegemea kwanza, kabla ya kutazama upande wa takirima hiyo kuwafanyia wengine. Tanzania, bahati mbaya au nzuri, ni moja kati ya nchi masikini siki ambayo kiuchumi na kimaendeleo iko nyuma sana hata ukilinganisha na nchi nyengine duni za Afrika, na sio angalau za Ulaya, Latino Amerika, Marekani na Asia. Baya zaidi ni ukweli kwamba, umasikini wa Tanzania, kwa kiasi kikubwa naweza kusema na hata kuthibitisha kuwa ni wa kujitakia wenyewe. Lakini kwa vile mada yangu haitalenga sana kwenye uchumi, nitatosheka kwa kusema kuwa tunajitakia wenyewe kwa sababu tu ya kutotazama letu. Kwamba hatushuhuliki na yale ya kwetu bali, ama tunashulika na maslahi ya mtu binafsi au mataifa jirani na wahisani. Tabia hii ambayo bila shaka tumeirithi kutoka katika hekaya za Nyani asieona lake, ndio iliyotukisha pabaya leo. Pamoja na kuwa Tanzania ina rasilimali ya madini, mbuga za wanyama, maumbile ya kijograa yenye kuvutia, gesi , mafuta na hata vivutio lukuki vya Utalii, inashangaza kuwa faida ya vitu vyote hivi haionekani. Tunashindwa na jirani zetu Kenya ambao hawatimizi hata nusu ya Rasilimali tulizonazo. Nasema faida ya utajiri tulionao haionekani kwa sababu kama iko tungeona kuboreka kukubwa kwa huduma za jamii ndani ya miaka hii 50 ya Uhuru. Miaka ambayo Serikali imeshuhulika zaidi na kuboresha maslahi ya sehemu fulani na kusahau ya pengine. Miaka ambayo viongozi huangalia zaidi kujishuhulisha na kazi na amali zitazowapatia umaarufu wa bure (cheap popularity) kuliko umaarufu enedelevu (sustainable popularity) kwa

Ajabu ya Tanzania: La Zanzibar tunaliacha tunakimbilia Bukini!


wananchi wao. Kwa mfano, viongozi wetu hujisia zaidi kuweka mawe ya msingi, kufungua na kuzindua miradi ya watu binafsi na ya wahisani, na hata kufungua mashina na matawi ya vyama, badala ya kujenga miundo mbinu, kudhibiti na kuzitumia rasilimali zetu kwa ufanisi wa taifa na kuboresha huduma za jamii. Tanzania ikiwa mtu mzima wa miaka 50, ndio kwanza inapapatua kujenga barabara zenye kiwango cha lami huku kukiwa na maeneo kadhaa ambayo hayajawahi hata kuotewa kupatiwa barabara. Pamoja na utajiri mkubwa tulionao wa gesi na wataalamu Tanzania hatuna umeme wa uhakika, hatuna Hospitali za uhakika wala madawa, shule zetu hazina viwango wala vitendea kazi. Umasikini wa mtu kwa mtu, kila kukicha afadhali ya jana. Katika miaka hii 50 ya Uhuru, tunaona kuwa tunashindwa na hata huduma za uhakika za gari za kusarishia wagonjwa, gari za zima moto, na hata za kufanyia patrol ya polisi kwa sababu tu hakuna pesa ama za kuyakarabati, kununua mapya, na la aibu zaidi hata za kuyatia mafuta magari hayo. Hili tumeliona na lipo, tusikasirike wala kutaka ushahidi kwani upo wa dhahiri na wa picha. Wakati nchi yetu ikiwa na matatizo makubwa ya uchumi, na hata katika mgogoro wetu wa mipaka ya ziwa Nyasa, bado tunakimbilia kupeleka marundo na makundi ya majeshi Sudan, Comoro, Congo huku tukiacha kulijenga jeshi letu kiuzalishaji zaidi na hata kiulinzi wa ndani. Tafauti na wenzetu wa Magahribi, wao hupeleka majeshi pale tu wanapoona kuna maslahi yao, na mara nyingi huwa wao ndio wanaonzisha fujo na machafuko hayo. Yakishawashinda mambo yao, huwaita Tanzania wakalinde usalama na amani. Kwa lipi? Nchi yetu hivi sasa imejaa vilio vya wananchi kuhusu katiba na nafasi ya Zanzibar katika Muungano. Kilio hichi chenye ukali wa kwiki na maombwe ya uchungu wa kuchoshwa na madhila na uonevu unaosababishwa na unyonyaji wa upande mmoja wa Muungano dhidi ya mwengine, ulipaswa uwe kipaumbele kwa Serikali ya Muungano hivi sasa. Lakini kama ilivyo kawaida yetu, lakini tumekuwa kama wauguzi au manesi. Kawaida, muuguzi hakerwi na kilio cha mwanawe na wala hakimzuii kulala. Hivi ndivyo tulivyo. Laiti kama Serikali yetu inatazama lake kwanza na kujali, basi suala la vilio vya wananchi

wa Zanzibar lingekwishapatiwa ufumbuzi ambao haukuwa na haja hata ya kuundiwa tume. Kwa ufupi, suala la Zanzibar lilikuwa lirudishwe kwa wananchi moja kwa moja walipigie kura bila vitisho wala ushawishi. Na maamuzi yao yalikuwa yawe ya mwisho. Lakini hili halikufanyika wala halifanyiki. Cha ajabu, wakati mgogoro wa Muungano kwa upande wa Zanzibar ukiachwa na jeraha bichi, bila kupatiwa tiba ya kudumu, Tanzania imejikita kutatua migogoro ya Madascar (Bukini). Hii ni ajabu kweli. Inakuwaje nyumba yako inavuja, ukaezeke ya jirani? Suala la Rais Kikwete, kwa mfano, kumtaka Rais Rajoelina wa Bukini aache kugombea Urais muhula ujao, lilituhusu nini? Tena hasa kwa wakati huu ambao hata viongozi wetu wanapaswa waletewe washauri wa kimataifa kuwashauri angalau wafanye uchaguzi wa huru na haki, iwapo hawawezi kuachia madaraka wanayoyapata kwa mazingaombwe na nguvu za kiza? Tanzania, tufike pahala tuamke na tuseme basi. Ike pahali tuseme basi kwa vitendo vya rushwa na kuuza Rasilimali zetu kwa ubinafsi na kwa kutaka kuyaridhisha mataifa makubwa na wahisani. Tujenge nchi yetu. Mwenyezi Mungu ametubarikia kila aina ya utajiri ambao kwa udumavu wetu, tunashindwa hata kuutumia na kwa maana hio tunawavutia wenzetu waje wautumie, huku sisi tukifa njaa na shida, kwa kutazama yasiyototuhusu. Nionavyo, ifike pahala tujitambue na tukiri makosa yetu. Tukae na wananchi na tule viapo vya haki na ukweli vya kuwatumikia wao tu na sio mtu mwengine. Kwani nchi zote duniani, hasa za Ulaya na Marekani ziko tayari kuuwa na kuvunja taifa jengine zima alimradi maslahi yao na ya wananchi wao yaende mbele. Na kwa mantiki hii ndio ukaona wao wako mbali mno kimaendeleo, kwani hakuna anaeshuhulika na tatizo la mwenziwe. Hakuna anayeshulika na tatizo la mtu licha ya kuona kuwa wanajitia kutoa misaada na kujiita wahisani. Misaada inayotolewa na hao wanaojiita wahisani yote, ni chambo cha kutudhibiti ili wapata yale wayatakayo kwa urahisi tu. Na ndio hivi, wakati sisi tumelala, madini yetu wanayamiliki wao na kufaidisha nchi zao. Ardhi yetu, bahari na fukwe zetu zinawafadisha wao, na zaidi ya yote misitu na mbuga zetu pia. Haya yote ni matokea ya uhisani wao kwetu. Tumesahau kuwa Mtaka nyingi nasaba, hupata mwingi msiba Natoa hoja. Mwananchi, Zanzibar

13

MAKALA

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013


vya zinaa vinavyosababishwa na mavazi. Mipaka ya maeneo ya uchi kwa mwanaume katika maadili ya Kiislamu ni sehemu yote iliyo kati ya kitovu na magoti. Na mipaka ya sitara ya mwanamke kutokana na umbile lake ni pana zaidi kuliko ile ya mwanaume. Mwanamke ni mwili mzima isipokuwa uso na vitanga vya mikono kama Quran inavyosema: Na waambie Waislamu wanawake wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao na wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika (uso na vitanga vya mikono) na waangushe shungi zao (mitandio yao) mpaka vifuani mwao (24:31). Pia katika hadithi Bi. Aisha, mke w a Mtume (s .a.w ) ameeleza kuw a alipokea mbele ya mpwa wake Abdullah bin ALTufail, akiwa amejipamba Mtume (s.a.w) hakupendezwa akasema Ewe Mtume wa Allah ni mpwa wangu. Mtume (s.a.w) akasema, mwanamke baleghe si halali kwake kuacha wazi sehemu yoyote ya mwili wake ila uso wake na hapa(akashika sehemu ungio la kiganja cha mkono kiasi cha kuacha sehemu ndogo kati ya hapo aliposhika na mwanzo wa kiganja). Va z i l i n a l o o n y e s h a (transparent) hata kama linafunika mwili mzima mpaka kwenye mipaka iliyowekwa, pia limeharamishwa katika Uislamu kama tunavyojifunza katika hadidhi ifuatayo. Asmaa binti Abu Bakar (r.a), shemeji yake Mtume (S.a.w) alikwenda kwa Mtume akiwa amevalia nguo nyepesi iliyoonyesha mwili wake. Mtume (s.a.w) aliangalia kando na akasema; ewe Asmaa, mwanamke anapokia baleghe si halali sehemu yake yeyote ya mwili wake kuonekana ila hapa, (kisha akaonyesha uso wake na vitanga vya mkono). Mtume (s.a.w) amesema Allah (sw) amewalaaani wanawake wanaovaa nguo laini bado wamevaa uchi. Kwa mifano michache ya haya na hadidhi, naamini kuwa mwanamke wa Kiislamu utakuwa umepata ukumbusho wa jinsi Uislamu ulivyokuelekeza kusitiri umbile lako zuri alilokuumba nalo Mwenyezi Mungu, kwani kukumbushana ni kwetu Waislamu kwa ajili ya kukia lengo la kuubwa kwetu sisi wanadamu. Pamoja na kwamba namna ya kujistiri si taratibu za wanadamu bali zilizowekwa na Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa kitabu, na kwa heshina ya mwanamke, lakini wanaharakati wa hakia za wanawake wamekuwa wakipikia kelele hili, wakidai kuwa Uislamu umemnyima haki mwanamke kwa kujifunika funika! Ajabu wanawake hao wanaitwa ni wasomi na tunaelezwa kuwa na wao wana dini, na majina yao yametokana na imani za dini, na wakiolewa au kuzikwa ni kwa dini zao, lakini hao hao wanapingana na taratibu za mwenye dini (Mwenyezi Mungu) katika kujisitiri kwao, kwa sababu tu ya kutaka kutimiza matamanio ya nafsi zao, na si kwa ajili ya heshima na usalama wa mwanamke mwenyewe. Ajabu zaidi, wapo wanawake wa Kiislamu pamoja na kuzifahamu taratibu za dini zao katika kujihifadhi na faida zake, bado wako radhi kuasi taratibu hizo sahihi za Mwenyezi Mungu, wakaona ni vyema kwao kufuata matamanio ya nafsi zao, na kuunga mkono kampeni za wanaharakati za kuwavua hijabu na kufuata mavazi ya yanayoakisi tama za zinaa. Jambo la msingi kwa kina mama ni kuzingatia kwa makini kwamba, aliyeweka mipaka ya strara ya mwanamke na mwanaume ni Allah [s.w], mjuzi mwenye hekima na mwenye kujitosheleza na aliyemkamilifu ambaye hana sababu ya kumpendelea au kumwonea yeyote kati ya mwanamke na mwanaume. Ambaye ameweka mipaka ya stara kulingana na umbile la mwanamke na mwanaume. H iv y o u n ap o tek eleza amri hii ya kujisitiri, fahamu wazi unatekeleza agizo la Allah [s.w] na si la binadamu mwenzako. Ukiwa na msimamo huu utakuwa na nguvu ya kutekeleza agizo hili hata kama mawazo ya jamii inayokuzunguka yatapingana na wewe. Wanaotembea uchi kwa kuvaa kaboka, mini-skirt, waachwe na wakati wao. Wenye hekina na kufuata utaratibu wa maisha alioweka Mwenyezi Mungu, ndio waliosalimika zaidi. Muislamu wa kweli hana hiari katika kutekeleza amri ya Allah [s.w] kama tunavyokumbushwa katika Quran. Haiwi kwa mwanaume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wanapokata shauri wawe na hiari katika shauri lao na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi [33] (36].

AN-NUUR

Kwa nini stara yatakiwa zaidi kwa mwanamke


Na Pendo Masasa KADIRI siku zinavyosonga mbele, binti au mwanamke akipita kavaa nguo ya kubana, fupi au inayoonyesha sehemu kubwa ya maungo yake, anaonekana anakwenda na wakati. Akifunika kichwa kwa nywele bandia, au akaziweka rangi na kemikali za namna kwa mamna, akafanana na mwanamke wa bara Ulaya, basi huyo kadhalika anatafsiriwa kuwa kaendelea na kwenda sambamba na wakati. Sehemu kubwa kubwa ya jamii, hasa wanaopiga vita Uislamu, huwaona wanawake waliojisitiri miili yao kwa mavazi sahihi kama wamepitwa na wakati. Wengine wanadiriki kutoa maneno ya kejeli kwamba stara za wanawake hao ni kujizeesha. Kwa jinsi ilivyo na bila shaka ndio mantiki yenyewe, mwanamke kuvaa kihasara, yaani kuonyesha sehemu za mwili kama matiti, kifua, mapaja, kiuno, kichwa wazi, kuvaa nguo za kubana zinazothihirisha umbo la mwili wake au hata kuonyesha mwili (transparent), lengo kubwa ni kuvutia tamaa za uzinzi. Ili mtu aonekane kapendeza, basi kupendeza kwenyewe ni lazima kulete mvuto wa kimatamanio ya kimapenzi kwa watu wa jinsia ya kiume. Kila utakapopita mbele yao w a k a k u o n a , basi mtu ana hakika atawatamanisha na atawavuta kimapenzi. Hii ndio tafsiri ya baadhi ya wanawake, hususan mabinti kuvaa mavazi haya ya kihasara. Kupendeza bila kukidhi vigezo hivyo kuna maana kwao. Huwa mara nyingi najuliza, kwenda na wakati na mavazi kuna uhusiano gani hasa. Kwamba wakati huu kunastahili kuvaa mavazi haya. Muongo, karne, mwaka vina uhusiano gani hasa na mavazi? Hii ni ndio dhana ya wanawake wanaoishi kwa kufuata matamanio ya nafsi zao katika maisha yao ya kila siku, ambao hawafahamu lengo la kuumbwa kwao, wala mipaka waliyowekewa na Mwenyezi Mungu katika kujihifadhi na kujistiri. Bila shaka mwanamke asiyejistiri ni wa kuonea huruma kwa kujiweka katika madhara yeye mwenyewe na Mwenyezi Mungu anamsubiri kwa ajili ya kumuadhibu. Lakini madhara haya ni vigumu kumpata mwanamke kama unajitambua lengo la kuubwa kwako na mipaka yake aliyokuwekea Mwenyezi Mungu s.w ,hata kama watu watatumia njia zote kama ilivyo sasa kumekuwa mitindi mipya ya nguo kiasi cha

kuweza kukufanya uvue hijabu lazima utawapuuza kwa kuwa unajitambua lengo la kuubwa kwako. Hata ukitizama katika matangazo ya biashara ya Televisheni, wanawake ndiyo wamekuwa kivutio cha biashara kwa kuwaonyesha wakiwa nusu uchi au uchi kabisa tofauti na wanaume ambao mara nyingi hutolewa wakiwa wamevaa nadhifu. Siku hizi ni rahisi kupita njiani na kukutana na dada kavaa nguo fupi, akawa anahangaika kuivutavuta ishuke chini kila anapotembea, au kavaa kisuruali cha kubana kinacholazimu kuacha kuino wazi na akikutana na watu huhangaika kuivuta kuilazimisha kupanda juu, anakaa au kutembea kwa wasi wasi kwa mavazi aliyovaa mwenyewe na akiwa na hakika hayamfai. Inashangaza binadamu licha ya kujaaliwa akili na Mwenyezi Mungu, lakini tumefikia kuwa kama wanyama kwa kushindwa kutumia akili tuliyopewa vizuri. Kwa jinsi Mwenyezi Mungu alivyotuumba, umbile la mwanamke na mwanaume linatofautiana. Ndio maana Mwenyezi Mungu ameweka mipaka ya sehemu za uchi kwa mwanamke na mwanaume. Akaelekeza namna bora ya kujistiri ili kuondoa vishawishi vyote

14
Na Shaban Rajab

KESI ya jinai Namba 245 iliyofunguliwa na Jamhuri inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake, jana ilinguruma katika mahakama ya Kisutu, kwa Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Vi c t o r i a N o n g w a , kuendelea kusikiliza mashahidi wa upande wa mashitaka. Safari hii wakili wa serikali Bw. Tumaini Kweka, alileta mashahidi wawili wa upande wa mashitaka ambao ni Bw. Hamisi Mkangama, ambaye ni fundi mwashi na Bw. Wiliam Milanzi, ambaye alikuwa mlinzi wa eneo lenye kesi. Akiwasilisha ushahidi wake mbele ya hakimu Nongwa, Bw. Hamisi alidai kuwa yeye na wenzake, walipewa kazi ya kujenga uzio wa kulitenga eneo la Markaz Changombe na eneo aliloliita kuwa ni la Bw. Suleiman. Alisema, wakati wakiwa ndio kwanza wamemaliza kuchimba msingi wa uzio huo, alikuja Sheikh Ponda majira ya saa kumi jioni na kuwauliza ni nani aliyewapa idhini ya kujenga ukuta huo. Alisema kuwa walimjibu Sheikh Ponda kuwa aliyewapa idhini ni bosi wao Bw. Suleiman. Shahidi huyo alisema baada ya majibu hayo, Sheikh Ponda aliwataka kusimamisha ujenzi wa uzio huo kwa kuwaeleza kuwa eneo hilo lina mgogoro. Hata hivyo wao walimjibu kuwa hawawezi kusimamisha ujenzi huo mpaka atakapokuja bosi wao. Bw. Hamis aliongeza kuwa baadae Sheikh Ponda alipiga picha eneo hilo na kuondoka. Shahidi huyo alisema baadae jioni

Mlinzi, fundi ujenzi watoa ushahidi kesi ya Ponda


Shahidi asema Ponda ni kiongozi wake wa dini

Habari

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

SHEIKH Ponda Issa Ponda akifunguliwa pingu na askari katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kuwasili mahakamani hapo.

SHEIKH Ponda Issa Ponda (kulia) na Ustadh Saleh Mkadamu wakiwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam kusikiliza kesi inayowakabili. Wote wawili dhamana zao bado zimezuiwa na DPP. Bw. Hamis alijibu Wakili wa utetezi bosi wao alikuja na kumweleza yaliyotokea, Bw. Kweka, alimuuliza kuwa anamfahamu vizuri n a y e a k a w a a m b i a shahidi huyo iwapo Sheikh Ponda kwa kuwa wasimamishe ujenzi alikuwa akimfahamu ni kiongozi wake wa w a k a t i a k i e n d e l e a S h e i k h P o n d a h a p o dini. kuchukua hatua zaidi. Shahidi mwingine, kabla?

tena, kwa kuendelea kusikila mashahidi wa upande wa mashtaka.

Bw. William Milanzi, ambaye alidai alikuwa mlinzi wa eneo hilo, alisema alikuwa akifanya kazi hiyo udhamini wa mtu aliyemtaja kwa jina la Bw. Seif. Yeye alisema siku hiyo Oktoba 12, 2012 alikuwa eneo la kazi lililopakana na Markaz Changombe tangu saa 1:00 asubuhi. Alisema baada ya swala ya Ijumaa, majira ya saa 7:00, aliona umati mkubwa wa watu unaka katika eneo hilo. Aliongeza kuwa akiwa katika eneo hilo, walikuja watu sita na kumsalimia na baada ya hapo wakamweleza kuwa wao ni Waislamu na wamekuja kuhami eneo lao. W a i s l a m u walimweleza kuwa aliyeuziwa kiwanja hicho, basi amfuate yule aliyemuuzia ili kurejeshewa fedha zake kwani eneo hilo ni mali ya Waislamu. Alisema kuwa Waislamu waliendelea kukaa eneo hilo usiku na mchana kwa siku kadhaa hadi walipokamatwa na polisi. Alipoulizwa iwapo anajua uhusiano wa eneo analolilinda na lile la Markaz, Bw. William alisema hajui kama kuna uhusiano huo na kuongeza kuwa hapakuwa na uzio wa kutenga eneo la Markaz na eneo la mgogoro. K e s i h i y o imeahirishwa hadi Februari 14 itakapotajwa tena kwa watuhumiwa wawili tu, yaani Ponda na mwenzake. Februari 18, 25, 27, 28 kesi hiyo itasikilizwa

Mfumo wa Benki za Matokeo ya uchaguzi wa Israel Kiislamu wafafanuliwa yalivyopokewa na Wapalestina


Akitoa mfano akasema mtu kapeleka Benki Milioni kumi, ikiwa moja kwa moja utamwekea masharti ya kumkata kiasi fulani cha pesa utakuwa tayari ushamuingizia riba, umemdhulumu. Lakini alisema pesa hiyo, inaweza kuzalisha zaidi ya pesa iliyowekwa, na mwenye nayo akapata kiasi kidogo sana, hapo alisema tayari utakuwa umemdhulumu mwenye pesa, aliyetoa pesa nyingi na kupata kidogo. Lakini, kwa upande mwingine alisema, mwenye pesa anaweza kudhulumu pale ambapo ameweka pesa hiyo lakini Benki ilipoifanyia biashara, badala ya faida ikapata hasara, lakini wewe utahitaji pesa yako kamili kwa hali hiyo, utakuwa umeidhulumu Benki. Kwa hiyo katika mfumo wa Kiislamu wewe hudhulumiwi na ile benki nayo haidhulumiki kwa kuwa inafuata mfumo na misingi ya Kiislamu inayopinga dhulma kwa kila mtu. Alisema Akielezea huduma zitolewazo na Benki hiyo, Shkh. Machano, alisema ni huduma zote zitolewazo katika benki zingine kwa ujumla. A l i s e m a , unapozungumzia suala la kuweka amana (Deposit) katika Benki zingine na Benki ya Kiislamu ya PBZ, nayo ni hivyo hivyo lakini wao wana amana za aina mbili. Akifafanua alisema, katika njia ya amana, kwa maana kwamba mteja unaweka kitu na siku akikitaka hurejeshewa kama kilivyo, lakini kinaweza kutumika kwa dhamana ya muwekaji mwenyewe. Aina nyingine ya amana inafahamika kama njia ya uwekezaji (Almudhwaraba), yaani mteja anakwenda Benki na pesa yake kuweka kisha anairuhusu ifanyiwe kazi
Inatoka Uk. 16

15

Makala/Habari

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013

AN-NUUR

ambapo mteja huhitaji kununua kitu lakini pesa ya kununulia hana, hivyo mteja ataenda Benki na kujieleza kisha benki itaenda kununua kitu hicho, na kumpatia mteja wake ambaye atalipa kwa kadiri watakavyopatana. Kuna mkopo mwingine unajulikana kama Al-Muajal, ambao hauna tofauti kubwa na Murabah, kwa maana benki inakuwa na hitajio la mteja wake na yeye anachagua anachokitaka katika vilivyopo. Pia kuna njia zingine pia za kutoa mikopo kama vile Al-hijara, ambapo mteja huka Benki, akiwa anahitaji kununua mathalani Trekta, lakini pesa hana, hivyo Benki hununu kisha linakuwa lao kisha mteja an akodishwa

lakini faida itakayopatikana hugawana. Mbali ya huduma hizo, alisema, pia Benki ya Kiislamu ya PBZ, hutoa huduma ya mikopo, kwa mtindo huo huo wa kuzingatia Sharia za Kiislamu bila riba. Alisema, mikopo hiyo inafanyika katika njia ya Al-mu rabaha, (Cost plus)

Inatoka Uk. 8

kwa makubaliano ya kuilipa Benki kulipa kidogokidogo, bila riba. Akijibu swali kwamba ni nguvu gani inasaidi Benki za Kiislamu kutotetereka pamoja na mtikisiko wa Kiuchumi duniani, alisema, mwaka 2008, Uchumi wa Ulaya kwa ujumla ulitetereka, mabenki yalifilisika na mengine yalipata hasara; lakini katika kipindi hichohicho nchi ambazo zilikuwa zikifuata mfumo wa benki za Kiislamu hazikutetereka hata kidogo kutokana na mfumo wa Benki hizo kuendeshwa katika misingi ya mali halisi zenyewe na sio kwenye vitu kama hisa, zenye mrorongo mrefu namba tu bila mali. Ufupi wa maneno ni kuwa katika mfumo wa riba watu hutengeneza fedha na utajiri kupitia namba zisizowakilisha mali halisi wakati kitu hicho hakipo katika mfumo wa Kiislamu.

Kwa kweli hali yetu itazidi kuwa mbaya kuliko zamani kwani makazi haramu yalijengwa wakati wa Netanyahu huyu huyu, Mpalestina mmoja wa Ukingo wa Magharibi alinena. Gazeti la Mamlaka ya Palestina, Al-Hayat AlJadida liliandika: Kimsingi hakuna kitakachobadilika, kila kitu kitaendelea kama ilivyokuwa, makazi haramu, mauaji na ubomoaji. Tunatazamia kuwa sera za Israel zitaendelea kama ilivyo, mashambulizi ya Gaza, ujenzi wa makazi haramu katika Ukingo wa Magharibi na ubomoaji wa nyumba za Wapalestina katika Jerusalem (Al Quds), lilisema gazeti hilo. Magazeti mengine ya Kiarabu yaliwalaumu wapiga kura wa Israel kwa kuendelea kuvichagua vyama vya mrengo wa kulia. Yawezekanaje kwa jamii ya Israel inayodai inataka amani kumchagua kwa kura nyingi fashishti kama Avigdor Lieberman, na kwa hivyo kumtunukia uwezekano wa siku moja kuwa Waziri Mkuu wa Israel? lilisema gazeti la Al-Ahram linalomilikiwa na serikali. Kwa wale wasiomjua vilivyo, Benjamin Netanyahu ana mawazo kuwa Waarabu hawaelewi kitu isipokuwa tu lugha ya mabavu, lilisema gazeti la Misri liitwalo AlGomhuriya. Kwa kifupi, iwapo mchakato wa amani hivi sasa umekwama basi kwa kuchaguliwa tena Netanyahu ndio utadidimia zaidi. Kwa kweli, wakati wa uongozi wake kama Waziri Mkuu mnamo 1996 hadi 1999, Netanyahu alifanya kila jitihada kukwamisha amani kwa kuamrisha upanuzi

YASSER Arafat, kiongozi wa zamani wa Palestina mkubwa wa makazi haramu ya Wayahudi. Sasa inatumainiwa k u w a Wa a r a b u t i s a waliochaguliwa katika bunge la Knesset , wataweza kuunganisha jitihada zao ili kuhakikisha kuwa ubaguzi dhidi yao sio tu unapunguzwa bali unatokomezwa. Baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa, Binyamin Netanyahu amelazimika kuwasiliana na chama kipya cha msimamo wastani baada ya chama chake cha mrengo wa kulia kupoteza viti kumi na moja katika uchaguzi, na kwa hiyo kushinda viti 31 tu kati ya jumla ya viti 120 katika Knesset. Matokeo haya ni kinyume cha ilivyotabiriwa kuwa serikali ijayo ya Israel itakuwa ya mrengo wa kulia wakati nchi hiyo inakabiliwa na upinzani mkali ulimwenguni pamoja na matatizo ya kiuchumi na vurumai za mashariki ya kati. Ndani ya nchi, Israel inakabiliwa na nakisi kubwa katika bajeti inayofikia dola 10.5 bilioni. Mnamo Oktoba mwaka jana Netanyahu alishindwa kupitisha bajeti katika bunge na ndipo akalazimika kuvunja serikali yake na kuitisha uchaguzi mwengine. Mnamo mwaka 2012 nakisi ya bajeti ya Israel iliongezeka kwa asilimia 4.2 ya uchumi mzima wa nchi na hii ni mara dufu ya makisio. Kwa hivi sasa, Lapid atakuwa na kazi ya kuiuza Israel katika uwanja wa kimataifa. Kazi hii ataifanya wakati umaarufu wa Israel umeporomoka hivi karibuni, na maraki zake kama Uingereza na Marekani zikikosoa sera ya Israel ya kuendelea kupanua makazi haramu na kukataa kupokea ushauri. Mara ya mwisho waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw William Hague aliionya Israel kuwa ilikuwa inapoteza maraki wa kimataifa kwa vile Israel ilikuwa inapanua makazi haramu na kwa hiyo kuvuruga uwezekano wa kuunda mataifa mawili ili kumaliza mgogoro wa Israel na Palestina. (Habari hii ni kwa hisani ya Kituo cha Habari cha Palestina (Tanzania), 30 Januari 2013.)

16

AN-NUUR
16
kwa ajili ya vijana wa Kiislamu. Alisema, jambo hilo limeaamrishwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe pale aliposema, Soma na wala hakuifunga aliicha hivyo na akaendelea kwa kusema, soma kwa jina la Mola wako. Kwa maana hiyo ni jambo la maana sana mlilolifanya kwa hakika mna ujira mkubwa kwa Mwenyezi Mungu. Alisema Sheikh Matata. Matata, alisema Uislamu si sawa na kabila, kwamba unaweza kuwa Mnyamwezi na hata kama usipofanya yale ya Kinyamwezi, unaweza kubaki kuwa Mnyamwezi, bali katika Uislamu ni kinyume chake. Alisema, haitoshi tu kuzaliwa Muislamu na ukapewa jina zuri kama Abdallah, ikatosha bali ukiwa Muislamu ni lazima uujue Uislamu katika misingi yake kisha uufuate kwa matendo. Alisema, huwezi kuwa Muislamu wa kweli kama hujasoma na baada ya kuusoma unatakiwa kuutekeleza kwa matendo. Akisherehesha mafundisho ya Uislamu kuhusu msingi wa Uislamu Sheikh Matata, alisema Uislamu ni kunyenyekea na kufuata aliyokuja nayo Mtume Muhammad (s a w), na huwezi kuyafanya hayo kama hukusoma. Matata amesema Mwenyezi Mungu ameamrisha kuingia katika Uislamu wote na si kwa mafungu, kwa hiyo aliwataka Waislamu kuzinduka kwani hapa duniani ni pakupita tu. Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasimi, Katibu wa Masjid Muumin, aliwataka Waislamu kupigania dini ya Mwenyezi Mungu kwa hali na mali wakiwa ndani ya mwamvuli wa umoja na mshikamano. Akielezea mafanikio ya kituo hicho cha Kiislamu (Muumin Islamic Center) Kimara alisema, taasisi hiyo toka kuanzishwa kwake mwaka 2000, imepata mafaniko kadhaa ikiwemo

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA FEBRUARI 1 - 7, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa

AN-NUUR

Waislamu wahimizwa umoja


Na Bakari Mwakangwale WITO umetolewa kwa Waislamu kupigania Dini ya Allah (SWT) wakiwa katika mwamvuli wa umoja na mshikanao, ili kuweza kufikia malengo kupitia katika Misikiti yao. Wito huo umetolewa na Katibu wa Al-Masjid Muumin Islamic Center, Kimara, akiongea katika uzinduzi wa Shule ya Awali iliyopo chini ya Msikiti huo, iliyoanzishwa kwa umoja na mshikanao wa Waumini wa eneo hilo. Katibu huyo amesema, umoja na kuepuka mifarakano katika Uislamu ndiyo njia pekee itakayo weza kuwaletea mafanikio Waislamu. Alisema, kwa umoja na mshikamano wa waumini wa Al-Masjid Muumin, wameweza kupata mafanikio mengi tokea kuanzishwa kwa kituo hicho, mwaka 2000, ikiweo kuanzishwa kwa shule ya Kiislamu ya awali katika Msikiti wao. Akitaja changamoto wanayokabiliana nayo hivi sasa, akasema kuwa ni uhaba wa vitendea kazi vya shule ambayo wanaizindua hivi sasa kama vile madawati, meza, viti pamoja na vitabu. Aidha, alisema, anatoa wito kwa wadau kuwasaidia kupatika kwa kisima cha maji katika kituo hicho, kwani kilichopo kwa sasa hakikidhi haja. Tunahitaji msaada wa kupatiwa kisima cha maji, kama mnavyojua Uislamu unajengwa na usafi na maji ndio kiungo kikubwa cha ukamilifu wa usafi. Katika Taasisi yetu tuna tatizo kubwa la ukosefu wa maji. Alisema katibu huyo, akiomba msaada huo kwa wadau. Akiongea katika uzinduzi huo, mgeni rasmi Sheikh Othman Matata, alisema amefarijika kuona Waislamu wa eneo hilo wamepata muamko katika sekta ya elimu kwa kuanzisha kitua cha elimu kwa kuanzia na shule ya awali ya Kiislamu kuendesha madrasa ya kinamama yenye wanafunzi 45 na ya watoto yenye wanafunzi 150, sambamba na kufanya Sensa ya Waislamu wanaozunguuka kituo hicho. Pamoja na mafanikio hayo, alisema, pia kituo kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maji, kutokana na kisima kilichokuwepo awali kupata itilafu. Katibu huyo pia alisema, pamoja na kufanikiwa kuanzsisha shule ya awali, lakini pia wanakabiliwa na upungufu wa vitendea kazi kwa ajili ya uendeshaji wa shule, kama alivyoainisha awali. Taasisi ya Al-Masjid Muumin Islamic Center, iliyopo Kimara, imezindua rasmi shule ya awali ya Kiislamu (Nursary School) Januari, 13, 2013, na kuanza masomo siku ya Januari, 14, 2013, ambapo watoto wa eneo hilo na wale wa jirani, watapata fulsa ya kupata elimu, kupitia kituo hicho.

Mfumo wa Benki za Kiislamu wafafanuliwa


Na Bakari Mwakangwale

SHEIKH Ponda Issa Ponda (katikati) akifunguliwa pingu wakati akiwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana.

MFUMO wa Benki za Kiislamu kote Duniani hulinda haki za wateja wake huku ikilinda pia haki za wenye benki huku ikitoa huduma zote zitolewazo na Mabenki mengine. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Benki ya Kiislamu ya PBZ, Sheikh Shamim Hamisi Machano, akiongea katika kipindi Jenerali on Monday kinachorushwa na Televisheni ya Channel Ten, Jumatatu wiki hii. Sheikh Machano

aliyekuwa sambamba na kiongozi mwenzie katika Benki hiyo, Sheikh Said Mohammed Said, walikuwa wakifafanua huduma zitolewazo na benki ya PBZ na mfumo kwa ujumla wa benki za Kiislamu. Machano alisema kwa ujumla riba imeharamishwa katika dini zote, Ukristo, Uislamu na hata Uyahudi kwa sababu ni ni dhulma. Akasema, Mtume Muhammad (s.a.w) alifundisha kwamba Mwenyezi Mungu kahalalisha biashara na kuharamisha riba,

kutokana na huko nyuma kabla yake kushamiri biashara iliyoambatana na riba. Alisema, Mwenyezi Mungu ameeleza katika Qur an kwamba, wasidhulumiwe wale wanaoweka pesa kwa watu na wala wasidhulumu wale wanaotunza pesa. Akafafanua akisema kuwa, katika mfumo wa Benki za Kiislamu kwa yule anayekwenda kuweka pesa zake asiwadhulumu wale wenyewe Benki na yule mwenye benki asimdhulum mteja wake.
Inaendelea Uk. 15

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like