You are on page 1of 4

PRESS RELEASE

Siku ya Mtoto Njiti Duniani: Huduma za gharama nafuu zenye ufanisi katika kuzuia vifo vya watoto njiti
Tanzania, inasema UNICEF na wadau wengine

Dar es Salaam, 17 Novemba 2014 Nchini Tanzania, kila mwaka, watoto takribani 213,000 huzaliwa mapema
sana kabla ya muda wao (watoto njiti) na zaidi ya 9,000 miongoni mwao hufariki kutokana na matatizo
yanayohusiana na kuzaliwa mapema mno. Idadi hii ni takribani robo ya watoto wachanga 40,000 wanaofariki kila
mwaka hapa nchini. Vifo kutokana na matatizo yanayohusiana na kuzaliwa kabla ya muda kutimia ni sababu
kubwa ya pili inayosababisha vifo vya watoto wachanga hapa Tanzania.
Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupunguza vifo vya watoto. Vifo
vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua kutoka 166 kati ya 1,000 waliozaliwa hai mwaka 1990 hadi kufikia
vifo 54 kati ya kila 1,000 waliozaliwa hai mwaka 2012. Hata hivyo kasi ya kupunguza vifo vya watoto walio chini
ya umri wa mwezi mmoja imekuwa ndogo, kutoka watoto 43 kati ya 1,000 waliozaliwa hai mwaka 1990 hadi
watoto 21 kati ya 1,000 waliozaliwa hai mwaka 2012. Pia kasi ya kupunguza vifo vya watoto wachanga
vinavyotokana na matatizo ya kuzaliwa njiti ni ndogo sana na hivyo basi vinaendelea kuchangia asilimia kubwa ya
vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Kila siku zaidi ya watoto wachanga 100 hufariki nchini Tanzania, kutokana na maambukizi, matatizo
yanayojitokeza wakati wa kuzaliwa kama vile kupumua kwa shida na matatizo yanayotokana na kuzaliwa kabla ya
muda (watoto njiti). Nchini Tanzania, vifo vya watoto wachanga vinachangia hadi asilimia 40 ya vifo vyote vya
watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Kimsingi, vingi kati ya vifo hivi vya watoto wachanga vinaweza
kuepukika kwa kutumia huduma za gharama nafuu zenye ufanisi. Takwimu hizi zinaonesha haja ya kuwa makini
zaidi
na
kuchukua
hatua
madhubuti
kwa
ajili
ya watoto wachanga na mama zao. Kwa mujibu wa Mpango Kazi wa Kila Mtoto Mchanga (Every Newborn Action
Plan) ambao ni mpango kazi wa kimataifa wa kutokomeza vifo vinavyoweza kuepukika, kipindi muhimu cha
kuokoa maisha ya maelfu ya akina mama na watoto wachanga ni wakati wa kuzaliwa na ndani ya masaa 24 ya
kwanza ya maisha ya mtoto mchanga, kwani kipindi hicho ndipo asilimia 40 ya watoto wanazaliwa wakiwa
wameshafariki (uzazimfu) na vifo vya watoto wachanga; na asilimia 48 ya vifo vya akina mama vinavyotokana na
uzazi hutokea.
Mwaka huu 2014, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ikiwa imeungwa mkono na na wadau mbalimbali,
imeanzisha mpango mkakati (Sharpened One Plan) wa Kuharakisha zaidi Kupunguza Vifo vya akina Mama
vinavyotakana na uzazi, pamoja na vifo Watoto Wachanga na vya Watoto wenye umri Chini ya miaka mitano,
Tanzania mwaka 2014-15. Mpango huu umeweka kipaumbele dhamira ya kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya
watoto wachanga na vya akina mama vinavyotokana na uzazi hususan kufatilia kwa kina suala la uzazi wa
mpango, huduma za afya wakati wa kujifungua na uwepo wa dawa muhimu ili kupunguza vifo vinavyoweza
kuepukika. Iwapo mpango huu ukitekelezwa nchi nzima, tutaweza kuokoa maisha ya akina mama 1,400, watoto
wachanga 9,400 na kupunguza vifo 2500 vya watoto wanaozaliwa wakiwa wamefariki (uzazimfu) ifikapo mwaka
2015.

Watoto njiti wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kufariki na kupata ulemavu

Watoto wanaozaliwa kabla ya muda wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kufa kutokana na magonjwa ya mfumo
wa hewa, mfumo wa chakula na mfumo wa fahamu ukilinganisha na watoto waliozaliwa baada ya kutimiza wiki
37 au zaidi wakiwa tumboni mwa mama zao. Watoto njiti pia wapo katika hatari ya kupata matatizo ya kuona,
kusikia, kutambua/kiakili na moyo yanayoweza kudumu maisha yao yote. Zaidi ya hapo watoto wanaozaliwa njiti
katika nchi zilizo na uchumi duni wapo katika hatari ya kufa mara 10 zaidi ukilinganisha na watoto njiti
wanaozaliwa katika nchi zilizoendelea.
Tunaweza kupunguza idadi ya njiti
Sababu kuu zinazosababisha hali ya hatari kwa watoto njiti nchini Tanzania na nchi nyingine zenye uchumi mdogo
ni maambukizi wakati wa ujauzito, malaria, VVU, kuzaliwa na uzito mdogo, muda mfupi kati ya uzao mmoja na
mwingine na mimba za utotoni. Matunzo sahihi kabla, katikati na wakati wa ujauzito (ikiwemo uzazi wa mpango
na huduma wakati wa ujauzito) ni muhimu katika kupunguza kiwango cha uzazi wa watoto njiti. Hata hivyo
sehemu kubwa ya sababu zinazofanya watoto kuzaliwa njiti hazijulikani. Hivyo basi tunahitaji kufanyike tafiti zaidi
ili kupata uelewa na kudhibiti visababishi vyake.
Tunaweza kupunguza vifo vya watoto wachanga wanaokufa kutokana na matatizo ya kuzaliwa njiti
Mtoto anayezaliwa njiti sio lazima apewe uangalizi wa karibu (intensive care) na kutumia teknolojia kubwa sana
ili aishi. Huduma za gharama nafuu zinazoweza kufanyika ili kuongeza uwezekano wa mtoto mchanga kuishi na
kupunguza hatari kwake ya kupata ulemavu wa maisha, ni pamoja na zifuatazo:
1. Antenatal steroids, hizi ni dawa ambazo hutolewa kwa akina mama wanapopata uchungu wa kujifungua
kabla ya wakati, katika ngazi za afya zinazostahili, husaiidia kukuza mapafu ambayo hayajakomaa ya
mtoto njiti na kuzuia matatizo kwenye mfumo wa hewa ya watoto wachanga.
2. Huduma ya Mama Kangaruu: Hii ni mbinu ya kumbeba mtoto mchanga kwenye kifua cha mama yake
wakigusana ngozi kwa ngozi ili kumpa joto na kurahisisha unyonyeshaji. Ni muhimu kuwapatia joto
watoto njiti kwa sababu miili yao ni midogo na hupoteza joto haraka, jambo linalowafanya kuwa kwenye
hatari kubwa ya kupata magonjwa mbalimbali, maambukizi na kifo. Inakadiriwa kuwa mbinu hii ya Mama
Kangaruu inaweza kuepusha vifo vya watoto 5,000 kila mwaka hapa Tanzania.
3. Kusaidia watoto kupumua kwa kutumia bag na mask ni huduma muhimu kwa watoto njiti wenye
matatizo ya kupumua. Iwapo huduma hii rahisi ya kusaidia watoto wachanga kupumua inapatikana kwa
asilimia 90 ya watoto wanayoihitaji, basi takribani maisha ya watoto wachanga 2,000 yangeweza
kuokolewa kila mwaka. Mpango wa Kusaidia Watoto Kupumua (Helping Babies Breathe) ulizinduliwa na
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mwaka 2009 kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa sekta ya afya
katika ngazi zote, ukiwa na lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga vinavyotokana na matatizo ya
kupumua. Wadau wa afya mbalimbali wameshirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika
kutekeleza mpango huu.
4. Kumsaidia mama kuanza kunyonyesha mtoto ndani ya saa moja baada ya kujifungua, hii inahusisha pia
kumsaidia mama kukamua maziwa kwa ajili ya mtoto na kumpa kwa kutumia kikombe pale inapo lazimu.
5. Kuzuia, kutambua mapema na kutibu maambukizi: utoaji wa huduma inayozingatia usafi wakati wa
mama kujifungua (mfano kuosha mikono, uhudumiaji sahihi wa kitovu na ngozi ya mtoto mchanga) ni
muhimu katika kuzuia maambukizi kwa mama na mtoto. Dawa za antibiotiki kama vile Amoxicillin
zinaweza kutumiwa kutibu nimonia na Gentamicin kwa ajili ya kutibu maambukizi makubwa
yanayowapata watoto wachanga.

Zaidi ya hapo, watoto wote wachanga wanahitaji kukaguliwa afya zao ndani ya masaa 24 na baada ya siku 3 ya
kuzaliwa ili kuzuia matatizo yanayoweza kutokea na yale ambayo yanaweza kusababisha ulemavu katika maisha
yao ya baadaye.
Huduma bora inahitajika wakati wa kujifungua na hususan kwa watoto wachanga wanaozaliwa na uzito
mdogo na wale walio wagonjwa.
Watoto wachanga wanahitaji kupata huduma muhimu hususan kwa wale ambao wanazaliwa kabla ya muda
wao, anasema Mwakilishi wa Unicef nchini Tanzania Dk. Jama Gulaid. Hii inajumuisha kuwakausha, kuwapa
joto na kuwaweka safi, kuwaanzisha kunyonya ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa na kuhakikisha kwamba
watoto wanaopata shida kupumua wanapata huduma na uangalizi wa haraka. Dakika ya kwanza baada ya
kuzaliwa ni dakika ya dhahabu (golden minute) kwa kila mtoto mchanga.
Kuna ushahidi wa uhakika kwamba utolewaji wa huduma muhimu wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua na
baada ya kujifungua bila ya kutumia gharama kubwa na uangalizi wa karibu (intensive care) unaohitaji teknolojia
ya juu, unaweza kuokoa maisha ya watoto wengi wanaozaliwa kabla ya muda na wengi wao wakaweza kukua na
kuwa na afya nzuri bila ya ulemavu wa kudumu.
Kama ilivyoainishwa katika Mpango Kazi wa Kila Mtoto Mchanga (Every Newborn Action Plan) na Mpango
mkakakati wa kuharakisha zaidi kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi, pamoja na vifo vya
watoto wachanga na vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano (Sharpened One Plan) tunahitaji kuimarisha
na kuwekeza zaidi kwenye huduma wakati wa kujifungua na katika wiki ya kwanza ya maisha ya mtoto.
Uboreshaji huduma za akina mama wajawazito na watoto wachanga zinazotolewa katika vituo vya afya na katika
jamii, vitapunguza tofauti na kuleta usawa katika jamii kwa kuhakikisha kila mama na mtoto mchanga wanafikiwa
na huduma; kutumia nguvu za wazazi, familia na jamii; na kumhesabu kila mtoto mchanga kwa kutumia vipimo
maalumu, uwepo wa mipango ya ufuatiliaji wa programu na uwajibikaji, duniani kote pamoja na Tanzania. Kila
mwananchi ana mchango wake katika kudai huduma bora na kuwekeza kwenye afya.
Jambo moja muhimu, tunahitaji kuwaongezea mafunzo na kuwaunga mkono wale wote wanaotoa huduma za
kuzalisha na huduma kwa watoto wachanga kuanzia madaktari bingwa wa akina mama, madaktari bingwa wa
watoto, madaktari, wakunga na wauguzi, anasema Dk. Jama Gulaid.
Wadau mbalimbali pamoja na UNICEF wanaunga mkono juhudi za Wizara za Afya katika kutathmini hali ya
watoto wachanga, kuainisha changamoto na njia kuu za kuzikabili ili kuboresha afya ya mtoto mchanga Tanzania
bara na visiwani. Wadau wapo tayari kuisaidia serikali kuwajengea uwezo watoa huduma za afya ili watoe
huduma bora kwa akina mama wajawazito, watoto wachanga na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano
ikiwemo Kusaidia watoto wachanga kupumua, huduma ya Mama Kangaroo, huduma za Dharura wakati wa
Ujauzito, huduma Muhimu kwa Watoto Wachanga, pamoja na kutoa vifaa na zana muhimu na kujenga uelewa na
hamasa katika jamii ya kudai na kutumia huduma bora za afya za mama na mtoto.
Wadau wamekuja pamoja kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani na kurudia ahadi waliyotoa ya kutokomeza
vifo vya watoto ambavyo vinaepukika. Kuboresha afya ya watoto wachanga pamoja na kuzuia watoto kuzaliwa
njiti na kuhakikisha utolewaji wa huduma bora kwa mtoto mchanga ni sehemu muhimu ya harakati hii.
###
Kwa mawasiliano zaidi, yakiwemo mahojiano wasiliana na:
Sandra Bisin, UNICEF Tanzania, Simu: +255 787 600079, sbisin@unicef.org
Jacqueline Namfua, UNICEF Tanzania, Simu: +255 754 711073, jnamfua@unicef.org

You might also like