You are on page 1of 2

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF TRANSPORT

TANZANIA AIRPORTS AUTHORITY


Tel: +255.22.2842402/3
Fax: +255.22.2844495
E-mail: info@airports.go.tz
Website: www.taa.go.tz

P. O. BOX 18000
DAR-ES-SALAAM
20 Novemba 2014
PRESS RELEASE

Serikali yatoa bilioni 4/- kuongeza kasi upanuzi kiwanja cha ndege Mwanza
Serikali imetoa sh. Bilioni 4 kwa ajili ya kumlipa mkandarasi anayepanua kiwanja cha ndege
cha Mwanza, Kampuni ya Beijing Construction and Engineering Group (BCEG) ya China na
hivyo kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara ya kurukia ndege, jengo la
kuongozea ndege na ghala la mizigo. Kiasi hicho kinafanya fedha ambazo Serikali imeshampa
Mkandarasi kufikia shilingi bilioni 13 baada ya awali kumlipa shilingi bilioni 9.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Esther Madale amesema kazi ya upanuzi wa
kiwanja hicho inaendelea vyema na kwa kasi na tayari mkandarasi ameanza kujenga tabaka la
pili (la kokoto) kabla ya kuweka lami kwenye barabara ya kurukia ndege na pia kujenga kuata
zinazogawa vyumba jengo la kuongozea ndege.
Katika jengo la kuongozea ndege mafundi wameanza kujenga kuta. Hadi kufikia Januari
mwakani tutakuwa tunazungumza mambo mengine labda mvua ndio ituharibie. Upanuzi wa
njia ya kuruka na kuua ndege unakwenda vizuri. Itakwisha lini itategemea na upatikanaji wa
fedha na hali ya hewa. Mvua ikiendelea inaweza kutuchelewesha, Esther amesema kuhusu
maendeleo ya upanuzi huo mkubwa wa kiwanja hicho cha ndege.
Meneja huyo amesema, ziara ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyofanya kukagua maendeleo
ya ujenzi huo Agosti 2014 imezaa matunda kwani tayari Serikali imetoa sh. Bilioni 4 za
kumlipa mkandarasi ili kazi isisimame baada ya kuwa ametishia kusimamisha ujenzi kutokana
na kutolipwa zaidi ya sh. Bilioni 5.
Amesema, hata sehemu ya mizigo ambako mkandarasi alikuwa amesimamisha kabisa ujenzi,
nako kazi imeanza tena baada ya kulipwa fedha hizo. Upanuzi huo unafanywa na BCEG kwa
gharama y ash. Bilioni 105 zikiwa ni mkopo kutoka Benki ya BADEA iliyotoa sh bilioni 10 na
pia OFID iliyotoa sh bilioni 10. Serikali ya Tanzania imetoa sh bilioni 85 ili kukamilisha mradi
huo unaohusisha ujenzi wa jengo jipya la abiria.
Pia amesema, kituo cha kufua umeme (power house) ambacho wakati Waziri Mkuu, Pinda
anazuru ujenzi huo kilikuwa hakijaanza kazi ujenzi wake unaenda kwa kasi ambapo tayari
nguzo zimeshajengwa. Pia Meneja Esther alisema maegesho ya ndege za abiria yako mbioni
kupanuliwa ili ndege ndogo zihamishwe kutoka zinapoegesha sasa.

Meneja Esther alisema kazi zilizobaki nyingi zinahusiana na ujenzi wa jengo jipya la abiria
utakaohusisha ujenzi wa maegesho ya magari ya abiria, mfumo wa maji safi na taka kutoka
kwenye jengo hilo litakalochukua miaka 2 kukamilika. Amewataka wakazi wa Kanda ya Ziwa
kuwa na subira kuhusu ujenzi huo.
Kwa mujibu wa Meneja huyo, mkandarasi amesema anafanya kazi kwa kasi zaidi ili amalize
ndani ya mwaka mmoja. Mradi huo umepangwa kukamilika Oktoba 2015 kama hakutakuwa
na tatizo la fedha na hali ya hewa.
Kuhusu usalama, Meneja huyo amesema, hali ya usalama ya kiwanja cha ndege cha Mwanza
ni nzuri hadi sasa na kwamba Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) inazidi
kuimarisha usalama huo kwa kuongeza kamera zaidi za usalama (CCTV). Jana wajumbe wa
Bodi ya Ushauri ya TAA walikagua maendeleo ya ujenzi huo.
Upanuzi huo mkubwa ni ahadi ya Rais Jakaya Kikwete kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya
Ziwa ambao wanategemea kiwanja hicho kwa usafiri wa anga kutoka Mwanza kwenda maeneo
mengine ya nchi. Upanuzi huo ukikamilika utaiunganisha Kanda ya Ziwa na nchi za Ulaya,
Asia na Marekani kuanzia hapo.
Hiyo inafuatia upanuzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege kuwa na uwezo wa kupokea
ndege kubwa kama Boeing 747 za abiria na mizigo na ambazo zinaweza kuruka kutoka hapo
hadi viwanja vya Ulaya. Tayari ndege za nchi jirani kama Rwandair zimeanza safari huku
Precision Air ikienda Nairobi, Kenya.
Imetolewa na Kitengo cha Sheria na Uhusiano TAA

You might also like