You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA.
RPC.
Namba ya simu 2502572
Fax - +255252503734
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz
tanpol.mbeya@gmail.com

Ofisi ya Kamanda wa Polisi,


Mkoa wa Mbeya,
S. L. P. 260,
MBEYA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA


HABARI PRESS RELEASE TAREHE 05.12.2014.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU


WAWILI KWA TUHUMA TOFAUTI.
KATIKA MSAKO WA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MELANIA
RICHARD (60) MKAZI KIJIJI CHA KAMFICHENI ANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA
MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 05.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.12.2014
MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
KAMFICHENI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI
NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MRISHO
RAMADHAN (22) MKAZI AIRPORT ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KETE 01 SAWA NA UZITO WA
GRAM 05.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.12.2014
MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA MANGA,
KATA YA MANGA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA,
TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE YA MOSHI/BHANGI KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
[AHMED Z. MSANGI SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

You might also like