You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA.

RPC.
Namba ya simu 2502572
Fax - +255252503734
E-mail:- rp.cmbeya@tpf.go.tz

Ofisi ya Kamanda wa Polisi,


Mkoa wa Mbeya,
S. L. P. 260,
MBEYA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA


HABARI PRESS RELEASE TAREHE 28.04.2015.

WATU WATATU WASIOFAHAMIKA WANYANGANYA GARI [W]


MBALIZI NA KISHA KUSABABISHA AJALI YA WATU WAWILI
KUFARIKI WILAYA YA MBEYA.

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA GARI NA


PIKIPIKI WILAYA YA MBALIZI.

WATU WANNE WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MAKOSA YA


KUPATIKATIKANA NA POMBE YA MOSHI WILAYA YA MBEYA NA
CHUNYA.

JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU 13 RAIA


WA NCHINI BURUNDI WILAYA YA ILEJE.

TUKIO LA KWANZA.
WATU WATATU WASIOFAHAMIKA WALINYANGANYA GARI T.640 CDE AINA YA
TOYOTA IPSUM MALI YA NICHOLAUS MASHAKA [26], MKAZI WA MBALIZI II,
LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA TAXI DRIVER FRANK STAFORD [23], MKAZI WA
NDOLA-MBALIZI.
TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 27.04.2015 SAA 21:00HRS USIKU HUKO KATIKA
ENEO LA ST MARY MBALIZI, KATA YA SONGWE,TARAFA YA USONGWE BAADA
YA WATU HAO KUMKODI DEREVA ILI AWAPELEKE KIJIJI CHA IWALA KUCHUKUA
MGONJWA NA NJIANI KUMFUNGA KAMBA, KUMTUPA VICHAKANI KISHA
KUONDOKA NA GARI HILO. MAJIRA YA SAA 23:30HRS WATU HAO WAKIWA NA
GARI HILO ENEO LA UYOLE WAKIWA KATIKA MWENDO KASI WALIWAGONGA
WANAWAKE WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI 1. TELEZA JACKSON [38] NA 2.
SNARA HENRY [36], WAKAZI WA UYOLE NA KUSABABISHA VIFO VYAO. BAADA
YA AJALI HIYO WATU HAO WALIKIMBIA NA KULITELEKEZA GARI ENEO HILO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI
WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAENDESHAJI WA MAGARI
YA BIASHARA AMBAYO HAYAJASAJILIWA KUFANYA BIASHARA (TAXI BUBU
)NA PIKIPIKI @ BODABODA WAKASAJILI ILI KUWEZA KUBAINI HATA IKIIBIWA NA
VILEVILE
KUTOWEKA
TINTED
ILI
KUWEKA
TAHADHALI
PINDI
WANAPOSAFIRISHA ABIRIA WASIOWAFAHAMU HASA USIKU. AIDHA ANATOA RAI
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATU HAO AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE MARA MOJA
DHIDI YAO.
TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA GARI NA PIKIPIKI
WILAYA YA MBALIZI.
MWENDESHA PIKIPIKI T. 990 AAJ AINA YA SKY MARK AITWAE ANTHONY
MWESENGA [28], MKAZI WA MBALIZI ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA
NA GARI T.296 BGE AINA YA M/CANTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA
DEREVA NURU NICKSON [34],MKAZI WA MBALIZI.
TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 27.04.2015 MAJIRA YA SAA11:30 JIONI
HUKO KATIKA KIJIJI CHA KESALIA, KATA YA UMALILA,TARAFA YA ISANGATI
WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA,
BARABARA YA
UMALILA/MBALIZI.
CHANZO CHA AJLI HIYO BADO KINACHUNGUZWA.
MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI
WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATEMBEA
KWA MIGUU KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA
KATIKA MISAKO
WATU WATANO WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MAKOSA YA
KUPATIKATIKANA NA POMBE YA MOSHI WILAYA YA MBEYA NA CHUNYA.

TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA CHRISTINA MBANGA [47], MKAZI WA MAKUNGULU, ALIKAMATWA
AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 5.

TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 27.03.2015 MAJIRA YA SAA 12:15HRS HUKO


KATIKA EENO LA JUAKALI, KATA YA MAANGA, TARAFA YA IYUNGA JIJINI
MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI.
TUKIO LA PILI
AIDHA KATIKA TUKIO LA PILI. WATU WATATU IKUPA ALLY {26},MKAZI WA
MAKUNGULU, EMANUEL RAPHAEL [29],MKAZI WA MWANJELWA NA GEOFREY
JEREMIA [31],MKAZI WA ISYESYE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA
YA KUKAMATWA WAKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 5.
TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 27.04.2015 MAJIRA YA SAA 13:10HRS HUKO
KATIKA ENEO LA JUAKALI, KATA YA MAANGA,TARAFA YA IYUNGA JIJINI
MBEYA.TARATIBU
ZINAFANYWA
ILI
WATUHUMIWA
WAFIKISHWE
MAHAKAMANI.
TUKIO LA TATU:
MTU MMOJA YELA MWASILE [45], MKAZI WA UPENDO, ALIKAMATWA AKIWA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA 5.
TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 27.04.2015 MAJIRA YA SAA 19:00HRS HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MAJENGO, KIJIJI NA KATA YA TARAFA YA KIWANJA,
WILAYA YA CHUHNYA MKOANI MBEYA.
TUKIO LA NNE:

JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU 13 RAIA WA


NCHINI BURUNDI WILAYA YA ILEJE.
WAHAMIAJI HARAMU
13 RAIA NA WAKAZI WA NCHINI BURUNDI
WAMEKAMATWA KATIKA KIJIJI CHA ISONGOLE,KATA YA ISONGOLE,TARAFA YA
BULAMBYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 27.04.2015 SAA 21:30HRS KIJIJINI HAPO JIRANI
NA MPAKA WA TANZANIA NA MALAWI WAKIWA WAMETOKEA NCHINI MALAWI.
WAHAMIAJI HARAMU HAO NI 1. RUTON JOSEPH [71], 2. KWINZEYA JEREMIA [27]
3. FREDY SHUTINAMAGAGARA [29] 4. ENDAKUMANA LEWANCE [24] 5.
NIYONZURU ALBER [30] 6. ATANGAMANA ELISA [25] 7. NIYOKUSENGA
SHARIOT [ 5], 8. HAFASHIMANA ADELINE [10], 9. NIMPAYE FAINES [7]
10.NIYONZIMA CHANINE [27] 11. MOGISHA FRANK [1] 12. SABUSHIMIKE
ANISETI [33] NA 13. SABUSHI MIKEME [12]. TARATIBU ZINAFANYWA ILI
WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI
WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA
TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA
SHAKA IKIWEMO RAIA WA KIGENI ILI HATUA/UCHUNGUZI DHIDI YAO UFANYIKE.

Imesainiwa na
[AHMED Z. MSANGI SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

You might also like