Professional Documents
Culture Documents
TigonaReachforChangewazinduashindanolawajasiriamalijamii
Kilamshindikupokeadolazakimarekanimilioni20,000kwaajiliyautekelezaji
wamradiwake.
Dar es Salaam, Seeptemba 25, 2015. Tigo kwa kushirikiana na taasisi ya Reach for
Change zimezindua shindano wajasiriamali jamii liitwalo Tigo Digital Changemakers lenye lengo la kuibua mawazo ya kibunifu ambayo yatasaidia kutatuta
matatizo yanayowakabili watoto na vijana nchini.
Meneja mkuu wa Tigo Diego Gutierrez leo ametangaza uzinduzi wa shindano hilo
katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo
ametoa wito kwa watu kushiriki ili wajiweke katika nafasi ya kushinda fedha taslimu
dola za kimarekani 20,000 ambazo kila mshindi atapewa azitumie katika utekelezaji
wa mawazo yao ya kibunifu.
Tigo ikishrikiana na Reach for change itatoa tuzo ya dola za kimarekani 20,000 kwa
kila mmoja kwa washindi wawili ambao watakuwa na mawazao bunifu zaidi
kiteknolojia na kidijitali yaliyo na uwezo wa kuchangia kuleta maisha bora kwa
watoto katika jamii ya kitanzania, alisema Gutierrez.
Aliongezea kwamba, Lengo letu ni kupata mawazo ya kibunifu ya kidijitali ambayo
yataleta na kutatua matatizo yanayowakabili watoto kwa kiwango kikubwa huku
tukiendelea kuwekeza katika kukuza na kuimarisha huduma zetu za mawasiliano
katika maeneo yote nchini.
Mawazo yatakayowasilishwa kupitia shindano hili yanatakiwa kuonyesha uwezo wa
kutumia simu kidijiti tekinolojia ya habari na mawasiliano kuleta ufanisi wa
utekelezaji wa mradi husika. Watakaopenda kushiriki shindano hili wanaweza kutuma
maombi kupitia mtandao wa www.tigo.co.tz/digitalchangemakers, kwa mujibu wa
Gutierrez.
Kwa upande wake, Meneja wa Tanzania wa Reach for Change, Peter Nyanda, alisema
licha ya kupata kitita cha dola 20,000 washindi pia watapewa vifaa vya kuendeleza
utekelezaji wa mawazo yao ikiwa ni pamoja na kupata ushauri kutoka kwa
wafanyakazi waandamizi kutoka Tigo na Reach for Change. Aidha wataunganishwa