niwajulishe wote kuwa kuanzia sasa askari wote wa uhamiaji wenye rank ya kuanzia konstebo hadi sajini meja mtakuwa mnafanya gwaride (Parade) kuanzia saa moja na nusu hadi saa mbili kasoro robo kabla ya kuanza kazi. Gwaride hilo kwa kuanzia litafanyika kwa siku za jumanne na alhamisi na baadae tutarekebisha kulingana siku zitakavyokuwa zinaenda. Afisa Uhamiaji Wilaya atakagua gwaride hilo wiki ya mwisho wa kila mwezi. Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya sheria ya Jeshi la Polisi na Idara za Uhamiaji na Magereza namba 38 ya mwaka 2015 na notisi ya Serikali ya namba 438 iliyotolewa tarehe 2/10/2015 kifungu cha 23 (d), (n) na (t). Yeyote ambaye hatotii kanuni hii atachukuliwa hatua kali za kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 27 cha kanuni iliyotajwa hapo juu. Shughuli hii itafanyika nje ya lango kuu la kuingilia ndani ya ofisi hii. Nawatakia utekelezaji mwema wa kanuni hii.