Professional Documents
Culture Documents
Hali Ya Watetezi Wa Haki Za Binadamu
Hali Ya Watetezi Wa Haki Za Binadamu
1 Taarifa katika picha ni jeshi la polisi wakitumia nguvu dhidi ya wanafunzi wa Chuo Kikuucha Dar es
salaam waliokuwa wakiandamana kuelekea Ikulu ili kumuomba Mh Raisi, Jakaya Mrisho Kikwete na
serikali yake iwadhamini wanafunzi wa mwaka wa kwanza walionyimwa mikopo, Mnamo tarehe 11 no-
vemba 2011, eneo la geti maji jijini Dar es Salaam, Tanzania
Shukrani zangu 9
Historia ya Mwandishi 10
Malengo ya Kitabu 11
Sura ya Kwanza 13
Sura ya Pili 24
Sura ya tatu 30
Sura ya nne 38
Sura ya Sita 48
Sura ya Saba 52
Kwa namna ya pekee, shukrani pia ziwaendee watu wote walioshiriki katika kuandika
na kushauri wakiwemo watetezi wenzangu wafuatao: Evarist Ambrose, Francis
Ndunguru, Elius Mwambapa, Wilfred Rolland, Bob Wangwe, Hellen Mushi, Hatari
Chacha, Mabirika Mawazo, Monance Baraka, Gervas Shayo, Godbless Charles,
Charles Jackson, Laizer Yonas, lema Tumsifu, Kalabamu Joseph. Wengine ni Ado
Joseph, Joel Ntile. Raymomd Abuya, Bashari Shonza, Daniel Mswelo, Michael Legan.
Pia wamo Daiel Naftal, Garubindi Gaston Odillon na wengine wengi ambao wote
ninathamini mchango wao maridhawa.
Ni matumaini yangu kuwa, kitabu hiki kitakuwa na manufaa makubwa kwa watumiaji
na kitawezesha jamii ya Kitanzania na wadau wa mbalimbali kupata zana muhimu ya
kutambua umuhimu wa watetezi wa haki za binadamu; lakini vile vile, wanafunzi wa
vyuo vikuu watapata ari mpya na hamasa ya kuendelea kutetea haki zao na za taifa
kwa ujumla wake, kwa kufuata hatua halali za kisheria.
Alphonce Lusako M. Alias Emekha Ikhe, ni kijana aliyezaliwa katika kijiji cha Ipagika,
Tukuyu, Mkoani Mbeya nchini Tanzania mnamo tarehe25-11-1988, na alijiunga na
Shule ya Msingi Manga na baadaye akiwa darasa la nne kuhamia shule ya Msingi
Mapambano mkoani Mbeya kati ya mwaka 1996-2002. Alisoma katika Shule ya
Sekondari ya Samora Machel kuanzia mwaka 2003-2006 hukohuko mkoani Mbeya;
na hatimaye kidato cha tano na sita alisomea katika shule ya sekondari Sangu High
School kuanzia mwaka 2007-2009.
Baada ya hapo alijiunga na Chuo Kikuu cha Taifa University of Dar es Salaam 2009
ambako alifukuzwa chuo kwa sababu ya harakati zake za utetezi wa wanyonge.
Mnamo tarehe 14/11/2011 akiwa mwaka wa tatu alifukuzwa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam kwa tuhuma za kuratibu maandamano tarehe 11/11/2011 ya kuwatetea
wanafunzi wa mwaka wa kwanza ambao hawakudhaminiwa mikopo nchini.
Malengo ya kitabu
Malengo ya kitabu hiki ni kuibua ukiukwaji mkubwa wa haki za watetezi wa haki za
binadamu uliotokea, unaotokea na unaoendelea kutokea ndani ya vyuo vikuu nchini,
ambapo kama taifa tukiendelea kufumbia macho suala hili, ni hatari kwa ustawi wa
amani ya nchi yetu. Hivyo kitabu hiki kina lengo la kuibua ukiukwaji husika ili jamii ya
Kitanzania wakiwemo viongozi tuliowapa dhamana, AZAKI (Asasi za Kiraia) na jamii
kwa ujumla wake, waweze kutambua ukiukwaji husika na kuchukua hatua stahiki ili
kuleta maendeleo endelevu nchini.
Lengo jingine ni kuamsha ari na hamasa ya wanavyuo katika kutetea haki zao na za taifa
kwa ujumla wake, bila kutetereka kwa njia halali za kisheria, ikiwemo maandamano na
migomo ya amani katika kushinikiza upatikanaji wa haki.
Lakini kwa upande mwingine, kupitia katika kitabu hiki, tunaoneshwa harakati za
kukandamiza uhuru wa kujieleza na kutoa maoni vyuoni. Hizi ni harakati zinazofanywa
na vyombo vya dola kwa kupitia viongozi wa Vyuo Vikuu nchini .
Katika kitabu hiki, tutagusia kidogo historia ya migogoro ya wanafunzi wa vyuo vikuu
ambao wamekwishawahi kusiamishwa na kufukuzwa kwa kuwa watetezi wa haki
za binadamu vyuoni.Yapo majina ya viongozi mashuhuri ambao walisimamishwa au
walifukuzwa kutokana na migogoro hiyo vyuoni, mathalani Mh. Samweli Sita, Mh.
Wilfred Mwabulambo, Mh. Chacha Zakayo Wangwe, Mh. John Mnyika, Mh. Zitto
Zuberi Kabwe, Mh. James Mbatia, Mh. Julius Mtatiro, Mh. David Silinde na Wengine
wengi ambao tunatambua na kuthamini harakati zao.
Pia kitabu hiki kimeeleza kwa undani jinsi watetezi wa haki za binadamu wa vyuo
vikuu nchini wanavyodhulumiwa haki zao za kikatiba, wanavyokosa utetezi katika
jamii kutokana na taarifa potofu zinazotolewa na watawala wa vyuo vikuu wakati
wanawafukuza vyuoni na kutokulindwa na vyombo vya dola, kwani bado serikali
yetu imekuwa na dhana potofu dhidi ya watetezi wa haki za binadamu.Hivyo hutumia
vyombo vya dola kuwakamata na kuwapiga ili kukomesha harakati za utetezi ndani
ya vyuo vikuu nchini.
6 Gazeti la Mwananchi, TANGAZO ukurasa 14. Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kufukuzwa kwa
Wanafunzi wachache Vinara wa uhalifu katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, kama ilivyosomwa na
Profesa Yunus D. Mgaya, Naibu Makamu Mkuu Chuo-Utawala
Historia hii ya timua timua imechambuliwa kwa kina katika Ripoti ya Tume ya
Uchunguzi wa Migogoro ya Wanafunzi Vyuo Vikuu Tanzania iliyoongozwa na Dr. Hawa
Sinare ya mwaka 2004.
Historia ya timua timua Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 1960s 1970s
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kifupisho chake UDSM kutoka Kiingereza University
of Dar es Salaam) ni Chuo Kikuu cha kwanza nchini Tanzania kilichoanzishwa mwaka
1961 baada ya uhuru wa Tanganyika, kama Chuo Kikuu Kishiriki cha Afrika Mashariki.
Kiko katika jiji la Dar es Salaam. Kilianza kuwa Chuo Kikuu mwaka wa 1970 baada ya
kutengwa kwa Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki katika vyuo vikuu vitatu: Chuo Kikuu
cha Makerere, Uganda na Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya. Kwa ujumla, chuo hiki ni
chuo kikongwe chenye hadhi ya kitaifa na kimataifa ambacho kina historia kubwa
katika harakati za ukombozi wa kifikra; na mazao ya chuo hiki hayapo ndani ya nchi
tu bali yapo hata nje ya nchi katika tasnia mbali mbali.
Mnamo tarehe 22 oktoba 1966, wakati huo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kikiwa ni
Chuo Kikuu kishiriki cha Afrika Mashariki. Mh. Samweli sita akiwa kiongozi wa Serikali
ya Wanafunzi UDSM na Wanafunzi wengine waliamua kugoma na kuandamana
kupinga ulazima wa wao kujiunga na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) na kukatwa
mishahara yao baada ya JKT. Walihoji kwanini vigogo wa Serikali na wanasiasa
wanalipwa mishahara minono na marupurupu makubwa?. Baada ya shinikizo hilo la
Wanafunzi, Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliamua kupunguza mshahara wake wa
Tsh. 4000 bila kodi na akaagiza mishahara ya mawaziri ipunguzwe kwa asilimia mbili.
Miezi miwili baadae, Mwalimu akatangaza Azimio la Arusha (Februari 5, 1967) kuyapa
uzito malalamiko ya wanafunzi hao.
Watetezi wawili waliotolewa kafara ni Mh. Samweli Sitta na Mh. Wilfred Mwabulambo
kwa sababu walitoa maneno makali kwa Mwl. J.K.Nyerere kwamba ni heri wakati
wa Ukoloni kuliko utawala wa Mwalimu.
Mh. Samweli Sitta amesomea Shahada yake ya Sheria kwa takribani miaka saba
(7) tangu kufukuzwa kwake mwaka 1966 na ameshika nyazifa mbali mbali serikalini
ikiwemo kuwa Spika wa Jamhurui ya Muungano wa Tanzania.
Mh. Wilfred Mwabulambo na Mh. Jaji, Joseph Wariba ni watetezi walioingia katika
historia ya kuchapwa viboko baada ya mgomo wa Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam(UDSM) wa kupinga tamko la walowezi-Waingereza la mwaka 1965 la
kujitangazia uhuru Unilateral Decleration of independence wa kuongoza Rhodesia
ya Kusini(Zimbabwe). Mgomo huo uliongozwa na Mh. Jaji Joseph Warioba, Wilfred
Mwabulambo na wanafunzi wengine ambapo walitapakaa mtaani na kuvamia Ubalozi
wa Uingereza na kufanya Vurugu kubwa kuonyesha hasira zao. Mwl. J.K. Nyerere
aliwaita Ikulu na kuwaomba waombe radhi ubalozi wa Uingereza kwa niaba yake,
lakini wao walikataa. Mwalimu akaamuru wachapwe viboko7. Ndugu Wilfred amewahi
kushika nafasi mbali mbali za kiserikali ikiwepo Ukatibu Mkuu kiongozi Ikulu.
Mh. Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye ambaye kashika nafasi mbali serikalini, kwa
mwaka 2014 alikuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya
Katiba Mpya Tanzania, na ameshawahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri
Mkuu na Makamu wa Rais serikalini.
7 Simulizi hii ilitolewa na kuandikwa na Jaji Joseph Sinde Warioba kuhusu vuguvugu la wanafunzi nchini
kuupinga utawala wa kimabavu nchini Rhodesia ya Kusini (Sasa Zimbabwe). Maprofesa Omary na Mihyo
wanaongezea kwamba Mwalimu na Serikali yake walisukumwa kuwadhibiti wanafunzi kutokana na hali
halisi ya wakati husika. Wanayasema hayo kwenye kitabu chao kinachoitwa The Roots of Students Unrest
in African Universities (Tafsiri ni yetu):
Mnamo Machi 1978, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walifanya mgomo
mkubwa wa kupinga nyongeza za posho kwa mawaziri, wabunge na maafisa wa
serikali. Watawala waliamua kuwasimamisha watetezi na wanafunzi wote waliogoma
kwa muda wa miezi tisa na kuwaacha wanafunzi wasiogoma kuendelea na masomo.
Lakini pia ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza, watawala wa chuo hiki waliamua
kufuta serikali ya wanafunzi DUSO na ikawekwa chini ya uangalizi wa Kamati ya
Umoja wa vijana wa TANU ujulikanao kama TANU Youth League
Pichani kushoto ni Mh. James Mbatia ambaye miaka 1990s yeye na wenzake mathalani
Anton Kom na wengine walifukuzwa UDSM kwa kupinga sera ya kuwashirikisha wazazi
kuchangia elimu ya juu.Amekuwa Mbunge wa kuteuliwa 2010-2015 na Mbunge wa
Kuchaguliwa 2015-2020 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na Ni Mwenyekiti wa
Chama Cha NCCR. lakini vile vile alikuwa ni Mbunge wa Kuteuliwa mwaka 2010 2015,
hakufanikisha kumalizia shahada yake ya uinjinia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
UDSM. Alienda nje ya nchi baada ya nchi.
Hawa ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Mlimani wakiwa nje
na mizigo yao, wakiwa hawajui waelekee wapi baada ya chuo hicho kufungwa ghafla
mwaka 2008.
11 Waraka wa Wanafunzi wa Elimu ya juu kwa Serikali kuhusu migomo na maandamano ya mara kwa mara
vyuoni.
Ulioandikwa na viongozi wa serikali za wanafunzi vyuo vikuu Tanzania baadhi yao ni Debora Gabriel-Rais wa
Chuo Kikuucha Dododoma Dodoma, Musa Ndile (Waziri Mkuu Serikali yaWanafunzi Chuo Kikuucha IFM
Mboya James Katibu katika serikali ya wanafunzi Chuo Kikuucha IFM, Daniel Naftal Waziri wa mikopo Chuo
KikuuCha Dar es Salaam Mruta Julius aliyekuwa Waziri wa Elimu Chuo Kikuucha Dar esSalaam mwaka
2009/10, Lusapi Yudah-Mwakilishi kamati ya mikopo Chuo Kikuucha Arusha, Mr. Paul Makuli aliyekuwa
Waziri Mkuu mstaafu Serikali yawanafunzi Chuo Kikuucha Dar es Salaam, Rwezaula Robert-waziri mkuu
serikali ya wanafunzi Chuo Kikuucha st.John Tawi la Dar es Salaam. Nk
Pichani, kushoto ni Mh. Julius Mtatiro ambaye kwa sasa ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama
Cha CUF taifa, Mh. David Silinde ni Mbunge wa Mbozi Magharibi kwa tiketi ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA. Mh. Steven Owawa kwa sasa ni mwajiriwa
serikalini.
Pichani kushoto ni Mtetezi Godbless Charles aliyefukuzwa MUHAS mwaka 2008, aliamua
kufungua kesi dhidi ya chuo ambayo alishinda kesi yake ya rufaa Mahakama kuu mwaka
2014 iliyosimamiwa na wakili Msomi, Prof. Abdallah Safari.
Mnamo tarehe 11/11/2011, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa niaba
ya Vyuo Vikuu vya umma nchini, tulifanya mgomo mzito dhidi ya serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, ili kuishinikiza serikali kupitia bodi ya mikopo (HESLB)
iwadhamini wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vya umma waliotelekezwa
kudhaminiwa mikopo. Watetezi walihoji uwepo wa mikopo hewa iliyokithiri ndani ya vyuo
Vikuu vya umma na kuiomba serikali kuelekeza mikopo husika kwa wanafunzi halisi na
kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika katika ubadhirifu wa Fedha za umma.
12 Taarifa hizi zilitolewa na Baraka Monance mmoja wa watetezi walioshiriki kikamilifu katika maandamano
husika ndami ya Chuo Kikuucha Dar es Salaam wakati wa mahojiano baina yangu na yeye tarehe 20 julai
2012.
13 MUCCOBS-Moshi University College of Co-operative and Business studies.
14 CBE- College of Business Education
15 IMTU-International Medical and Technology University
16 IFM-Institute of Finance Management
17 TIA-Tanzania Institute of Accountacy
Pichani ni mtetezi jasiri wa kike, Hellen P Mushi akiwahutubia wanazuoni wa Chuo kikuu
cha Dar es salaam, umuhimu wa kupinga wanafunzi wa mwaka wa kwanza kurudishwa
nyumbani kwa hoja hafifu ya bajeti haitoshi huku kukiwa na mikopo hewa lukuki Vyuoni.
Mpaka leo hii hajafanikiwa kumaliza shahada yake
18 kama Gazeti la Majira, ISSN 5086. Na. 6580. Vol 11/4590. Jumatano. Januari 11.2012 lenye kichwa cha
habari Wanafunzi 99 UDSM nao wafukuzwa Chuo. Uk. 4.
Hitimisho
Tathmini nzima ya historia ya timua timua Watetezi wa haki za binadamu Vyuo vikuu
Tanzania inaonyesha namna vyuo vikuu vinavyopoteza dira katika harakati za utetezi.
Watetezi wa huko Nyuma walitumia taasisi ya Chuo kikuu kupigania mambo ambayo
yanamaslahi mapana na taifa na kimataifa mathalani kupinga mishahara minono kwa
vigogo wa kiserikali, kutetea uhuru wa nchi ya Zimbabwe kinyume na sasa ambapo
watetezi wengi wamejikita katika kutetea maslahi binafsi ya wanafunzi na sio jamii
kwa upana wake Selfish Activism. Kwa sasa Watetezi Vyuoni huongoza harakati za
kutetea matumbo yao mathalani Boom likichelewa, kuongezewa fedha za kujikimu
na huoni wakijishughulisha kutetea wanyonge nje ya uanafunzi wao. Tunamfano hai,
Mchakato wa katiba Umekwama, taasisi za vyuo vikuu zilizotegemewa kusiama na
kudai katiba mpya kwa masalahi mapana ya taifa zipo kimya, hii ni hari ya hatari katika
taifa hili. Jamii inashindwa kuelewa wasomi wa sasa na hatimaye kutotuunga mkono
katika madai mbali mbali tunayoyadai. Watetezi Vyuo vikuu wanapaswa kujielekeza
katika kutetea masuala yenye maslahi mapana na wanyonge wa taifa hili.
19 Taarifa ya Mh. Philipo Mulugo bungeni aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu katika Gazeti la Uhuru ISSN
0876-21494 Ijumaa Mei 3, 2013 Uk. 4.
- Matatizo ya Mikopo na Usiri wa vigezo vya kutoa mikopo ndani ya Bodi ya Mikopo
- Sera mbovu za elimu.
- Ubovu wa miundombinu vyuoni
- Watetezi kuwekwa kizuizini
- Mabavu ya watawala dhidi ya wanafunzi wa vyuo vikuu
- Wanavyuo kupinga madhaifu ya kisheria ya mfumo mzima wa kuwapata watawala
wa vyuo vikuu
Hawa ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi ya Mlimani wakiandamana
kuelekea Ikulu tarehe 4/02/2011 ili kushinikiza Serikali kuongeza pesa ya kujikimu, kutoka
5000/= hadi 10,000/= kwa siku. Faida ya mgomo huu ni kwamba, serikali iliongeza bumu
mpaka ikawa 7,500/=.
20 The report of the probe team on students crises in higher education institutions in Tanzaniam May 2004.
Ni tume iliyoongozwa na Dr. Hawa Sinare kama Mwenyekiti, Mrs. N.E. Ligate kama Makamu Mwenyekiti
na Profesa Tolly. S. A. Mbwette kama katibu mkuu wa tume husika kwa ajili ya kufanya tafiti za vyanzo vya
migogoro ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kuja na suluhu ya kuisaidia serikali kutatua migogoro ya vyuo vikuu
Tanzania. Kubadilisha utawala wa vyuo vikuu vya umma ili kuweka mazingira mazuri ya kitaaluma ndani ya
vyuo vikuu Tanzania
21 Gazeti la Majira ISSN 0856. Na 6580. Vol. 11/4590, Jumatano Januari 11, 2012
22 35 [1] The Chancellor of the Public University shall be appointed by the respective President.
23 Taarifa hizi alizitoa aliyekuwa Rais wa serikali ya wanafunzi MUHASO, ndugu Gervas Shayo ndani ya
Chuo Kikuucha Muhimbili mnamo tarehe 12 novemba 2012 wakati wa mahojiano naye. Yeye kama mte-
tezi ndiye aliyesimama kuwaongoza wanafunzi kupinga sheria husika kwani alikiri kwamba serikali inaingilia
uhuru wa serikali za wanafunzi ili zisitekeleze wajibu wake kwa maslahi mapana ya wanafunzi na taifa kwa
ujumla wake.
- Lakini vile vile mnamo mwaka 1978, Serikali ya Wanafunzi DUSO ilifutwa na
kuwekwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Vijana wa TANU ulioitwa TANU YOUTH
LEAGUE TYL. Binafsi naamini hizi ni mbinu za watawala kutaka kuingilia uhuru
wa serikali za wanafunzi na kuua sauti za wasomi wa vyuo vikuu kwa kutengeneza
mifumo itakayowalinda watawala na serikali.
Tuhuma ambazo zimekuwa ni sumu kuliko tuhuma zote ni hii ya kutumiwa na wanasiasa
hasa wa upinzani, kama ilivyoonekana katika Gazeti la Mtanzania lenye kichwa cha
habari VURUGU UDSM24. Uongozi wa chuo kikuu ulidai kuwa, waliofukuzwa ni
wanasiasa, na pia habari kama hiyo ilichapishwa katika Gazeti la Uhuru25, nalo Gazeti
la Mzalendo la Jumapili tarehe 15 Januari 2012, katika makala ya 7 lilikua na habari
kama hizo.
2.3 Hitimisho
Katika sura hii, tumedondoa sababu mbalimbali ambazo zinawafanya au zimewafanya
wanafunzi wa vyuo vikuu kugoma. Ni matumaini yangu kuwa, msomaji atakayesoma
sura hii, atapata picha ya ukweli kuhusu madai ya wanavyuo ambayo yanawafanya
wagome; tofauti na taarifa potofu ambazo zimekuwa zikitolewa mbele ya jamii. Kwa
kusoma sura hii ya pili, ndugu msomaji utaanza kuelewa ukiona wanafunzi wanagoma,
kwa kuwa hutakuwa msikilizaji tu wa sababu zinazotolewa na upande wa watawala;
bali pia utapata shauku ya kusikiliza madai ya wanafunzi wanaogoma.
24 Gazeti la mtanzania ISSN 0856 - 5678 toleo namba na5842 Jumapili Januari 15, 2012 makala ya13
25 Gazeti hili liliandikwa: vurugu za UDSM: chama cha CHADEMA cha shukiwa kuwa nyuma ya mgomo
ukweli wabainika.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idriss Kikula alithibitisha kufukuzwa kwa
wanachuo hao na kusema kuwa, suala la kuwarejesha litatokana na utaratibu
watakaoupanga baadaye27.
27 Taarifa hizi ziliripotiwa na Gazeti la Majira la tarehe 15 juni 2011. Kufukuzwa huko kulikuja siku mbili
baada ya kuanzisha maandamano yaliyoshinikiza kujiuzulu kwa viongozi waandamizi wa Serikali, Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kwa madai kwamba wamewadanganya kuhusu malipo yao ya masomo
kwa vitendo kama vyuo vingine wasomavyo.
Maandamano ya
mtetezi wa haki za
binadamu UDSM
Ndugu, Richard Mwita.
28 Taarifa hizi zilitolewa na ndugu Baraka Monance, mtetezi wa haki za binadamu aliyefukuzwa na kufutwa
katika mfumo wa Elimu Tanzania katika mahojiano baina yangu nay eye mnamo tarehe 20 novemba 2012.
29 Rejea sura ya pili inayoeleza kwa kina vyanzo vya migogoro ikiwemo sababu ya serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuingilia serikali za wanafunzi Tanzania.
Pichani Kushoto ni Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makumira wakiwa katika maandamano,
wakilalamikia suala la ucheleweshwaji wa mikopo yao. Jeshi la Polisi lililazimika kutumia
mabomu kuwatawanya, baada ya kuzuia barabara ya Arusha na Moshi.
Pichani kulia ni wanafunzi wa Chuo Kikuu Tumaini Tawi la Dar es Salaam, wakiwa katika
mgomo tarehe 3/01/2012. Mgomo huu ni baada ya pesa yao yakujikimu kucheleweshwa,
kufuatia utaratibu mpya wa pesa hiyo kutolewa vyuoni badala ya Bodi ya Mikopo (HELSB).
Pichani kushoto ni Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha IFM wakimsikiliza mtetezi wao (Waziri
Mkuu, ndugu. Mussa Ndile), kufuatilia mgogoro wa wanafunzi na utawala wa chuo hicho.
Mwaka 2011, wanafunzi hawa waligoma kwa ajili ya kupinga utawala kuingilia chaguzi za
serikali za wanafunzi.
Pichani kulia ni Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha IMTU wakifanya mgomo kwa niaba ya vyuo
vikuu vingine vya binafsi kuhoji uhalali wa chuo hicho kutoza ada wanafunzi kwa Dola ya
Kimarekani lakini vile vile kupandishwa kwa ada za wanafunzi kiholela holela hasa katikati
ya muhula wa masomo na hivyo wakiitaka serikali iingilie kati suala husika.
3.6 Hitimisho
Katika sura hii tumekugusia migomo iliyotokea katika vyuo vikuu mbalimbali nchini na
sababu za kutokea kwake. Kwa hakika sababu nyingi zinashabihiana na nizamsingi.
Ni ukweli usiofichika kuwa panaweza kuwepo na nchi ambazo serikali zinatoa tishio
la kijumla dhidi ya kazi zote zinazohusiana na utetezi wa haki za binadamu. Lakini
pia nchi yetu imekuwa na shughuli za kutishia watetezi wa haki za binadamu kupitia
matamko mbali mbali kwa mfano kauli ya Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Peter Pinda
aliyoitoa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mnamo tarehe 27 Juni
2012, kwamba, Serikali itatoa tamko la hatua itakazochukua kuhusiana na mgomo
wa madaktari nchini na litakalokuwa na liwe31. Huu ulikuwa ni wakati wa mgomo
wa madaktari ulioongozwa na Dr. Steven Ulimboka. Hii ina maana kwamba, watetezi
wote wanaweza kukabiliwa na hatari.
Lakini najua pia kwamba, watetezi wengine wanakabiliwa zaidi na hatari kuliko wengine
kwa sababu ya misimamo yao. Tunaweza kusema kuwa, timua timua ya watetezi
wa haki za binadamu ndani ya vyuo vikuu ni jambo la kawaida, lakini pia linaweza
kushangaza tunapofanya uchunguzi wa sababu zinazopelekea kuwepo kwa hali
kama hii ili tuwe na ufahamu bora na hata kuyashughulikia matatizo yanayowakabili
watetezi. Kiwango cha hatari kinacholikabili kundi la watetezi wa haki za binadamu
vyuo vikuu kinaongezeka kulingana na vitisho wanavyovipokea, uwezekano wao wa
kudhuriwa, na pia uwezo wao wa kukabiliana na vitisho mbali mbali.
31 kama ilivyoripotiwa na Gazeti la nipashe la 28 juni 2012 katika Mgomo wa Madaktari ulioongozwa na
Steven Ulimboka.
- Vitisho ni nini?
Maana kamili ya vitisho ni uwezekano kwamba mtu fulani atamdhuru mtu mwingine
kimwili, au kimaadili ama kimali kupitia kwa fujo za kimakusudi, na za kila mara32.
Tathmini ya hatari au matishio ndani ya vyuo vikuu nchini imezidi kukithiri kwani
watetezi wengi wamekuwa wakidhuriwa na watawala wa vyuo vikuu nchini na baadhi
ya viongozi katika sekta ya elimu. Kuwadhuru huku ni kwa kuwachafua watetezi hao
mbele ya vyombo vya habari na hivyo kuchafua sura yao na maadili yao kwa umma.
Katika mazingira kama haya, watetezi huanza kujihami na watetezi chipukizi huogopa
kuendelea kudai haki za binadamu wenzao. Watetezi pia wanaweza kukumbana na
matishio mbalimbali katika hali ya mgogoro. Kwa mfano mwaka 2011 utawala wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, ulitoa tamko dhidi ya watetezi kuwa, wamefutwa
katika mfumo wa elimu nchini na kuwatishia waliobaki kwamba, watakaojihusisha na
harakati za utetezi (ambazo wao wanazibatiza kuwa ni vurugu) watafukuzwa mara
moja33.
Sababu ya tatu ni pale ambapo watetezi wa haki za binadamu wanarudishwa kwa amri
ya mahakama baada ya wao kwenda kudai haki zao katika mhimili wa mahakama.
Kwa mfano, wanafunzi wa UDSM waliofukuzwa chuoni mwaka 2011 walirudishwa
masomoni kwa amri ya mahakama36.
35 Taarifa hizi zilitolewa na Wilfred Mwalusanya mtetezi aliyefukuzwa UDSM mwaka 2011 ambaye alirud-
ishwa na chuo kwa kukubaliana na masharti ya watawala tumepewa masharti kadhaa kama kutafuta cheti
cha hati ya tabia nzuri kutoka kwa wakuu wetu wa wilaya-Certicificate of clean character. Barua za kututisha
endapo tutarudia tena harakati za utetezi
36 CRIMINAL CASE NO. 270/2011, REPUBLIC VERSUS MWAMBAPA ELIUS & 49 OTHERS-ACCUSED,
iliyoamuliwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu mnamo tarehe 30/08/2012 na kuamuru wanafunzi
wote kurudishwa chuo.
39 THE RESIDENT MAGISTRATES COURT OF DSM AT KISUTU CRIMINAL CASE NO. 270 OF 2011
REPUBLIC VERSUS MWAMBAPA ELIUS & 48 OTHERS- ACCUSED.
4.9 Hitimisho:
- Kuzika vyuo vikuu visiwe visima vya fikra huru think tank of the nation.
Kupitia timua timua ya watetezi wa haki za binadamu, ni dhahiri kuwa imeua ari ya
wanafunzi wa vyuo vikuu kulitumikia taifa lao kufa na kupona, kwa kukemea kwa
vitendo serikali yao, na kuikosoa na kuishauri inapokosea. Watawala wa vyuo vikuu
wanataka wanafunzi wa vyuo vikuu wasihoji, wasishauri na wasiikosoe serikali au
mamlaka ya chuo pale inapobidi.
Nitadadavua hasara ilipayo taifa kwa kumfukuza mwanachuo kwa kutumia wastani
wa wa mwanafunzi mmoja kwa mwaka 2011.
41 Taarifa hizi zinapatikana kwa kina katika Gazeti la Mtanzania ISSN 0856-5678. Toleo Na. 7308. Jumatano
mei 6, 2013. UK.3
42 Taarifa hizi zilitolewa na mwenyekiti wa chama cha watetezi waliofukuzwa vyuo vikuu Tanzania-UEUST
Nasema haya kwa niaba ya watetezi walio wengi ambao tumeteswa, tumenyanyaswa,
tumebezwa, tumepuuzwa, tumeshutumiwa, tumesingiziwa, tumetukanwa vya kutosha
kama utafiti wa kitabu hiki unavyojitanabaisha.
5.I Hitimisho:
Mambo ambayo yanatendeka ya uvunjwaji wa haki za kibinadamu kwa watetezi wa
wanyonge vyuoni, hayana budi kukomeshwa kwani yakiachwa yaendelee kwani
kuna hatari kubwa huko mbele ya safari tunakokwenda. Itafika sehemu wanyonge
hatutaona thamani ya sheria za nchi yetu, kwa sababu sheria si msumeno na
zinawalenga tabaka la wavujajasho, hivyo hatutaona thamani ya kuishi na hivyo
kukubali kupambana kwa ajili ya vizazi vijavyo! Wanyonge hatutathamini uhai wetu
zaidi ya mapambano na tutakuwa tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya faida ya vizazi
vijavyo. Wanyonge tutaamua kuweka historia yetu kwenye taifa letu kwa mapambano
dhidi ya waliotuonea kwa muda mrefu.
43 Taarifa hizi alizitoa mtetezi aliyefukuzwa UDOM mwaka 2011, ndugu Lema Tumsifu alipo nipigia simu
juu ya kutafuta namna ya kutatua tatizo la mtetezi Philipo Mwakibinga aliyekuwa anatakiwa alipe ada yote
1500,000 mara baada ya kurudishwa chuo UDOM mwaka 2014.
- Mikopo itolewe kwa asilimia mia moja (100%) kwa kila mwanafunzi anayepata
fursa ya kuchaguliwa kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu.
- Mikataba kati ya Bodi ya Mikopo na mwanafunzi uwe wazi katika vigezo vya
mwanafunzi mwenye sifa ya kudhaminiwa mikopo, kwa sababu, kuna usiri
mkubwa sana wa utoaji mikopo kwa wanavyuo. Hakuna kanuni formular
maalumu inayoweza kutuwezesha sisi waombaji mikopo kutambua ni kiasi gani
tutalipa kulingana na hali halisi ya mwombaji.
- Serikali ifungue akaunti maalum ya Bodi ya Mikopo kwa ajili ya wanafunzi wa elimu
ya juu ili kuondoa ukiritimba wa ucheleweshaji wa pesa kutoka Hazina kwenda
Bodi ya Mikopo. Pia Bodi ya Mikopo iingie mkataba na benki nyingine kama NBC,
NMB kuliko kutegemea kupitisha pesa kwenye Benki moja tu ya CRDB pekee;
na hao CRDB kusambaza fedha taratibu kwenye benki nyingine. Kitendo hiki
kinachosha na hufanya wanafunzi wenye akauti tofauti na CRDB kuchelewa zaidi
ya siku 4 ili kupata pesa zao wakati wenzao waliomo kwenye akaunti ya CRDB
wakiwa wameshapata na hivyo kuleta vurugu kwa wenzao.
- Suluhu ya migogoro ya vyuo vikuu sio nguvu ya vyombo vya dola: mabomu na
risasi, virungu; lakini vile vile sio kuwasimamisha na kuwafukuza watetezi vyuo
vikuu, ila suluhu ni kutatua matatizo yanayowakabili au mambo wanayoyadai kwa
wakati sahihi.
6.2 Hitimisho:
Kama tulivyojitahidi kuelezea katika sura hii, tumetoa mapendekezo kadha wa kadha
ambayo serikali, Bodi ya Mikopo, na watawala katika vyuo vikuu nchini hawana budi
kuyazingatia, ili kujenga jamii bora ya vijana wasomi kwa manufaa ya kizazi cha leo
na kesho.
6.3 Wito
6.3.1 Utangulizi:
Katika sehemu hii, nitatoa wito wangu kwa makundi mbalimbali yaliyopo katika jamii,
ili kila mmojawao ajue wajibu wake na majukumu yake katika mazingira ya kutetea
haki za watu wanyonge wa taifa hili. Wito ni kama ufuatavyo:
Ninasisitiza na kuomba kuwa, AZAKI mbali mbali kama vile: Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu Legal Human Rights Center (LHRC); THRDC44, TGNP45; TLS46;
TAMWA47; TAWLA48; JUKATA49 na FORDIA kuendelea kujitolea kuwatetea watetezi wa
haki za binadamu.
Pichani, Picha Mbili kulia ni mawakili waliojitolea kutetea haki za wanafunzi watetezi
waliofukuzwa Vyuoni tangu 2011-2017. Picha moja kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo Cha
Sheria na Haki za Binadamu-LHRC , Mh. Hellen Kijobisimba ambaye alisaidia sana kutoa
msaada wa kisheria kwa watetezi tuliofukuzwa vyuo.
6.4 Wito
Napenda kutoa wito jumuishi kwa makundi mbalimbali ambayo wakati wa mapito
yetu watetezi tumepata kuyafikia ili kuomba kuingilia kati uonevu tuliofanyiwa
mathalani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jeshi la polisi, watawala wa
Vyuo Vikuu Tanzania, Serikali za Wanafunzi Vyuoni, Jumuiya ya Wanafunzi TAHLISO,
taasisi za kidini, Vyama vya Siasa, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
watu binafsi na jamii kwa ujumla wake. Kutokuwa na mitazamo hasi dhidi ya Watetezi
wa haki za binadamu. Watetezi ni nguzo pekee kati ya watawala na watawaliwa na
dhamira yao kuu ni kusaidia kuwasemea walioonewa.
6.9 Hitimisho.
Mwandishi anahitimisha sura hii kwa kusisitiza kwamba, elimu juu ya haki za
binadamu haina budi kutolewa kwa kila mtu ili tujenge jamii ya watu wanaozilinda
na kuzitetea. Nashauri Azaki zote zinazojihusisha na masuala ya utetezi wa haki za
binadamu zifanye harakati shirikishi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ili ziwekeze kikamilifu katika kutoa elimu juu ya haki za binadamu.
Pichani kushoto ni Alphonce Lusako akitafakari uonezi dhidi ya haki yake ya kupata Elimu
kwa takribani miaka sita sasa, pichani kushoto akiondoka ndani ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam baada ya kufukuzwa kwake
Pichani ni Mtetezi Alphonce Lusako alipoamua kuwaeleza watanzania kupitia vyombo vya
habari uonezi unaomkabili katika harakati za kupata elimu ndani ya Nchi yake. Alisema :
Kihistoria(Hatua Tulizozichukua)
Watetezi tuliofukuzwa kwa sababu ya mgomo tuliouratibu wa kupinga kuwarudisha
wanafunzi wa mwaka wa kwanza nyumbani kwa hoja hafifu kwamba bajeti haitoshi
huku kukiwa na mikopo hewa lukuki, tulianza kufanya hatua za ndani ya Chuo,
tukakata rufaa dhidi ya maamuzi ya kutufukuza na kutufuta katika mfumo wa elimu,
Tukaomba baraza la Chuo (UDSM) Lirejee maamuzi husika yenye lengo la kupoka haki
yetu ya kusoma katika vyuo vya umma nchini. Baraza la chuo lilikataa maombi yetu.
Tukaanza njia za kidiplomasia tena, tulizunguka nchi hii kwa kila kiongozi mwenye
mamlaka na sekta ya Elimu, tukiomba huruma yao ya kuturudisha Chuoni tumalize
shahada zetu. Tuliandika barua kwa Mkurugenzi wa Vyuo vikuu, Waziri wa Elimu, Mh.
Shukuru Kawambwa kwa wakati huo, Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda, Waziri wa
Mambo ya Ndani, Mh. Nahodha vuai kwa wakati huo ambaye tulimuomba atusaidie
suala letu la kesi mahakamani. Tuliomba Tume ya Utawala bora na haki za Binadamu
iingilie kati, Tuliomba Bunge La jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kamati
maalumu iliyokuwa inaongozwa na Mh. Magreth Sitta, kuingilia kati. Hatua zote hizi
hazikuleta suluhisho.
Baada ya hatua zote hizo kushindikana, tuliona kutafuta haki yetu Mahakamani ndio
njia pekee. Tuliomba msaada katika taasisi zinazotoa msaada wa kisheria, Kituo cha
Sheria na haki za binadamu (LHRC) na Tanganyika Law Sociaty (TLS), tukapatiwa
mawakili ambao wamepambana miaka yote kututea (takribani miaka 5) mahakamani
ili tupate haki yetu ya kusoma bila mafanikio, tulianza Mahakama ya Hakimu Mkazi
kisutu, tukakata rufaa mahakama kuu, tukakata rufaa mahakama ya Rufaa (Appeal
Court of Tanzania). Ilipofika mwaka 2016, nikaona niachane na masuala ya kesi kwani
ni muda mrefu nipo mahakamani. Nikatoa faili langu mahakamani.
Mnamo tar 12. 02. 2016, TCU waliwaandikia barua rasmi Chuo (UDSM) kwamba kwa
mujibu wa sheria ya vyuo vikuu [Universities reguration 43(1) GN 226 ya mwaka 2013,
Mwanafunzi aliyefukuzwa Chuo kwa masuala ya kinidhamu anaruhusiwa kuomba
Chuo kwa mara nyingine tena baada ya miaka miwili kupita, katika chuo hicho hicho
au vyuo vingine tangu kufukuzwa kwake (Barua imeambatanishwa), hivyo akakiomba
Chuo kitupe Ushirikiano.
Kutokana na Ushauri husika, mwaka 2016 nikaomba udahili katika Vyuo vikuu vitatu
ikiwemo UDSM. TCU wakanichagua nisome UDSM shahada ya Uchumi (Economics)
kipaumbele changu cha pili baada ya Sheria, kwa kuwa ndoto yangu ni kusoma
shahada ya Sheria, nikaanza hatua za kubadilisha kozi kuelekea Shahada ya Sheria,
Utawala wa UDSM, Ulinipa Ushirikiano kwa kugonga mihuri ya kukubali kubadilisha
kozi yangu, hadi DVC Undergraduate UDSM, alithibitisha uhamisho wangu.
Baada ya miezi minne kupita tangu aanze masomo yake, katika hali ya sintofahamu
mnamo tar 30.01.2017akiwa katika ratiba yake ya mtihani akapewa barua ya
kusimamishwa uanafunzi wake kwa kile kinachodaiwa kwamba alidahiliwa kimakosa
na hivyo kusimamishwa rasmi masomo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Sio siri, nilishtushwa na niliumizwa sana kibinadamu ni masuala magumu sana ila
namuachia Mungu anitetee alisema Lusako
Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ni chuo kikuu cha umma, ni chuo kilichojengwa
na kodi za watanzania, ni chuo kilichojengwa na jasho la kila mtanzania. Hivyo kila
mtanzania mwenye sifa kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria, anapaswa kusoma
katika chuo hiki bila kubaguliwa. Natamani kuona nchi hii inaongozwa kwa mujibu wa
katiba na sheria . Tukiendelea kuongoza vyuo vikuu , kwa visasi, kwa chuki binafsi,
neno la mtu likawa sheria, watawala wa vyuo vikuu wakawa juu ya sheria, tutaliingiza
taifa hili katika gharama za machafuko.