You are on page 1of 36

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/ J/01 24 Agosti 2017

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri katika
Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi za Umma mbalimbali Serikalini, Sekretarieti
za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 789 kama inavyooneshwa
hapa chini.

1.1.1 MSAJILI MSAIDIZI WA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA WA WILAYA-


NAFASI 1
1.1.2 KAZI/MAJUKUMU YA MSAJILI MSAIDIZI WA BARAZA LA ARDHI NA
NYUMBA WILAYA
Msajili Msaidizi wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Wilaya atakuwa na Majukumu
yafuatayo:
i. Kusimamia utekelezaji wa sheria Na. 2 ya mwaka 2002;
ii. Kuelimisha Umma kuhusu mfumo mpya wa utatuzi wa migogoro ya Ardhi na
Nyumba;
iii. Kushirikiana wa Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya kuhakikisha kuwa Mabaraza
ya Ardhi ya Vijiji yanaundwa na Mabaraza ya Kata yanafufuliwa na yote
yanafanya kazi kwa mujibu wa sheria husika;
iv. Kuhakikisha kuwa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya yanakuwa na
mazingira mazuri ya kufanyia kazi; Pale ambapo hakuna ofisi, kuwasiliana na
viongozi wa Mkoa/Wilaya kuhakikisha kuwa ofisi zinapatikana/Majengo
yanapatikana.
v. Kuhakikisha kuwa kila Baraza lina wajumbe kulingana na matakwa ya Sheria na
kama kuna upungufu kuwasiliana na Mkuu wa Mkoa ili atume mapendekezo kwa
Mheshimiwa Waziri;
vi. Kuhakikisha kuwa Mabaraza yana vitendea kazi vya kutosha;
vii. Kuratibu vikao vya Mabaraza kwa ushirikiano na Wenyeviti;
viii. Kuhakikisha kuwa Taarifa ya utekelezaji (Return) ya kila mwezi inaandaliwa kwa
usahihi na kutumwa kwa Msajili;
ix. Kusimamia utayarishaji wa nyaraka mbalimbali zinazohusiana na marejeo, rufaa,
nk na kuhakikisha kuwa zinapelekwa Mahakama Kuu- Kitengo cha Ardhi kwa
wakati;
x. Kusimamia utendaji kazi wa Madalali wa Baraza;
xi. Kuhakikisha kuwa fedha zinazokusanywa katika Mabaraza kutokana na ada
mbalimbali katika Mabaraza zinapelekwa Benki kwa wakati na kuwa fedha za
matumizi zinatumwa katika Mabaraza kama ilivyokusudiwa;
xii. Kuhakikisha kuwa taarifa za makusanyo na matumizi (uthibitisho wa jinsi fedha
zilivyotumika) zitumwe kwa Katibu Mkuu kila mwezi.
xiii. Kuhakikisha kuwa Watumishi wanapata haki zao;
xiv. Kusikiliza malalamiko ya wananchi;
xv. Kufanya kazi zingine kama utakavyoelekezwa na Mkuu wako wa kazi.

1.1.3 SIFA ZA MWOMBAJI


Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali na awe
amemaliza mafunzo ya kazini internship/Externship au mafunzo ya Shule ya
Sheria (Law School), uzoefu wa miaka mitano (5) na kuendelea katika masuala
ya Sheria, awe mwadilifu na asiye na historia ya makosa ya jinai na awe na umri
usiopungua miaka thelathini na tano (35)

1.1.4 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS I.

1.2 AFISA ARDHI MSAIDIZI (ASSISTANT LAND OFFICER) NAFASI 3


1.2.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuingiza kumbukumbu katika kompyuta;
ii. Kutoa ushauri kwa wateja;
iii. Kupokea, kukagua na kusambaza majalada kwa maafisa kwa utekelezaji.
iv. Kusaidia Maafisa Ardhi katika ukaguzi na kuchukua kumbukumbu, picha taarifa,
vipimo vya majumba na michoro;
v. Kujumuisha na kuandaa taarifa za ukaguzi;
vi. Kuandaa rasimu za Hati na uingizaji wa plani ya Hati (deed plan);
vii. Kuagiza plani za Hati (Deed Plan).

1.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au cha Sita, waliofuzu mafunzo ya miaka
miwili ya Umiliki Ardhi na Uthamini kutoka Vyuo vya Ardhi au Vyuo Vikuu vingine
vinavyotambuliwa na Serikali.

1.2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C .

1.3 MPIMA ARDHI DARAJA LA II (LAND SURVEYOR GRADE II) NAFASI 2


1.3.1 MAJUKUMU YA KAZI
Sehemu ya Upimaji Milki (Cadastral Survey)
- Kuingiza taarifa za Upimaji (alpha numeric data) kwenye
kompyuta.

Sehemu ya Topographic na Geodetic Surveys


- Kukagua kazi za upimaji na kuingiza taarifa za kazi
zilizothibitishwa kwenye komputa.

Sehemu ya Ramani
- Kufanya upimaji picha (aerial triangulation and block adjustment);
- Kuandaa vikosi kwa ajili ya kuhuisha ramani (map revision)
- Kutunza kumbukumbu za picha za anga.

Sehemu ya Hydrographic Surveys


-Kusimamia na kuchukua vipimo vya tide gauges.

Mpima Ardhi katika Serikali za Mitaa

- Kufanya kazi za nje ya Ofisi (field survey operations) chini ya


usimamizi wa mpima aliyesajiliwa.

1.3.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi katika fani za Geomatics au Land
Surveying kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi katika fani ya Upimaji Ardhi au Taasisi
yoyote inayotambuliwa na National Council of Professional Surveyors (NCPS).
Au
Kuajiriwa wenye cheti cha East African Land Survey (EALSC) au National
Council of Professional Surveyors Certificate (NCPSC) katika fani ya upimaji
ardhi.

1.3.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS E..

1.4 AFISA ARDHI DARAJA LA II NAFASI 4


1.4.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kusimamia uingizaji wa kumbukumbu katika kompyuta.
ii. Kushughulikia utayarishaji wa nyaraka za kisheria.
iii. Kufanya ukaguzi wa viwanja.
iv. Kutoa notisi na kupendekeza ubatilishaji wa miliki kwa visivyoendelezwa kwa
mujibu wa sheria.
v. Kuwasiliana na wateja kuhusu Hati zilizotayarishwa na kuwakabidhi.

1.4.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika mojawapo ya fani ya
Bachelor of Science in land Management and valuation, Bachelor of Science in
property and facilities Management``, Bachelor of Science in Real Estate and
Finance Management, au Shahada ya Sheria kutoka Vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali.

1.4.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.E.

1.5 MTHAMINI DARAJA LA II (VALUER GRADE II) NAFASI 2


1.5.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kukusanya taarifa za utafiti na mwenendo wa soko la ardhi;
ii. Kuhakiki kumbukumbu za utafiti na kuziingiza kwenye kompyuta.

1.5.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika fani ya Land management
and Valuation kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi au Taasisi nyingine zinazotambuliwa
na Serikali katika fani za Usimamizi Ardhi na Uthamini. Au
Kuajiriwa wenye cheti cha NCPS katika fani ya Usimamizi Ardhi na Uthamini.

1.5.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS E.

1.6 AFISA MIPANGO MIJI DARAJA LA II (TOWN PLANNER) NAFASI 1


1.6.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa mipango ya maeneo yaliyoendelezwa kiholela;
ii. Kuandaa michoro ya Mipangomiji;
iii. Kupokea michoro ya Mipangomiji na taarifa za maeneo ya ardhi
yanayopendekezwa kuiva kwa ajili ya uendelezaji kimji;
iv. Kuchambua takwimu na taarifa kwa ajili ya maandalizi ya mipango mipya ya
makazi;
v. Kupokea na kuweka kumbukumbu za maombi ya mabadiliko ya matumizi ya
ardhi na umegaji wa viwanja;
vi. Kuhakikisha kuwa mabadiliko ya matumizi ya ardhi yanaingizwa katika michoro.

1.6.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa mwenye Shahada katika moja ya fani za Mipangomiji, ``Bachelor of
Science in Housing Infrastructure Planning``, na ``Bachelor of Science in
Regional Development Planning`` kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi au Vyuo Vikuu
au Taasisi nyingine zinazotambuliwa na Serikali.

1.6.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E.

1.7 AFISA USAJILI MSAIDIZI DARAJA LA II (REGISTRATION ASSISTANT II)


NAFASI 2
1.7.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kupokea na kuingiza kumbukumbu za hati katika kompyuta;
ii. Kufungua majalada ya hati mpya;
iii. Kupokea maombi na kutayarisha taarifa za uchunguzi wa hati (search report);
iv. Kufunga hati zilizokamilika (binding) na kuziwasilisha masjala.

1.7.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye astashahada ya Sheria (certificate in law), cheti cha Uthamini na
Usimamizi wa Ardhi kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

1.7.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.C.

1.8 FUNDI SANIFU DARAJA II- URASIMU RAMANI (CARTOGRAPHY) NAFASI 2


1.8.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya maandalizi ya uchoraji wa ramani za miji kadiri ya uwiano unaohitajika;
ii. Kutunza kumbukumbu za ramani na plani;
iii. Kuchora plani za hati miliki, upimaji, mashamba na vijiji;
iv. Kutoa nakala za plani za hati za viwanja, mashamba na vijiji.

1.8.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya
ufundi ya miaka miwili katika fani ya Urasimu Ramani (Cartography) kutoka
kwenye vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

1.8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C .

1.9 MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) - NAFASI 25


1.9.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandika na kutunza register zinazohusu shughuli za uhasibu;
ii. Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha;
iii. Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu;
iv. Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki;
v. Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.

1.9.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au Foundation Level kinachotolewa na
NBAA.

1.9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B.

1.10 AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS)


NAFASI 46
1.10.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio;
ii. Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio;
iii. Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora;
iv. Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti;
v. Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo, matumizi ya mbolea na madawa,
pembejeo za kilimo;
vi. Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei kwa wiki mwezi, robo na
mwaka ngazi ya halmashauri;
vii. Kukusanya takwimu za mvua;
viii. Kushiriki katika savei za kilimo;
ix. Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu matatizo na teknolojia sahihi za
kutumia;
x. Kupanga mipango ya uzalishaji;
xi. Kupima uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi;
xii. Kuwatambua wasambazaji wa pembejeo;
xiii. Kutoa mafunzo ya lishe kwa wakulima;
xiv. Kufanya vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu;
xv. Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea;
xvi. Kusimamia shughuli za kila siku za majaribio ya kilimo;
xvii. Kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji;
xviii. Kutoa ushauri wa kilimo mseto;
xix. Kuandaa sheria ndogo za hifadhi ya mazingira na;
xx. Kutoa taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo.

1.10.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha nne (IV) au Sita (VI) wenye stashahada
(Diploma) ya kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

1.10.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C.

1.11 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - MAJI - (TECHNICIAN GRADE II - WATER)


NAFASI 1
1.11.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Ukusanyaji na ukaguaji wa takwimu za maji
ii. Kutunza takwimu za maji
iii. Kuingiza takwimu za maji kwenye fomu Na: H: 12 tayari kwa kutumiwa kwenye
michoro
iv. Kuchora hydrograph za maji
v. Utengenezaji visima vya rekoda, stendi za winchi, sinia za maji cable way post
n.k.
vi. Kufanya matengenezo ya vifaa vyote vya kupimia maji na hali ya hewa
vii. Kuingiza takwimu kwenye kompyuta
viii. Kufundisha wasoma vipimo

1.11.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao
wana cheti cha ufundi (FTC) au Stashahada ya Rasilimali za Maji na wenye ujuzi
wa kutumia kompyuta.

1.11.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C.

1.12 AFISA MAENDELEO YA JAMII DARAJA II (COMMUNITY DEVELOPMENT


OFFICER GRADE II) NAFASI 17
1.12.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa na kupendekeza mipango na mikakakati ya kubadili fikra za watu ili
waweze kuwa na mawazo ya maendeleo sawia na Sera za Serikali na wakati
uliopo
ii. Kupitia mbinu shirikishi kuwezesha jamii kuanzisha miradi ya kijamii kama vile:-
- Usafi wa mazingira
- Ujenzi wa nyumba bora
- Ujenzi wa shule
- Ujenzi wa zahanati
- Kuchimba au kuzifanyia matengenezo barabara hasa za vijijini
- Ujenzi wa majosho
- Uchimbaji wa visima vifupi
- Utengenezaji wa malambo
iii. Kuhamasisha matumizi endelevu ya mazingira
iv. Kusambaza na kuhamasisha matumizi ya teknolojia sahihi kama vile uvunaji wa
maji ya mvua, majiko sanifu, matumizi ya mikokoteni
v. Kuhamasisha watu kutumia huduma za mafunzo ya Vyuo vya Maendeleo ya
Wananchi
vi. Kuwasadia wanachi vijijini kuandaa maandiko (Project Write ups) ya kuombea
fedha za kuendesha miradi yao
vii. Kuhamasisha, kuandaa na kutoa elimu kwa umma kuhusu uraia na Utawala bora
viii. Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kusambaza takwimu na kumbukumbu muhimu
kwa ajili ya matumizi ya jamii
ix. Kuwezesha wananchi kupambana na mila zenye madhara kwa afya za wanchi
hasa wanawake na watoto wa kike, kuenea kwa virusi vya UKIMWI na magonjwa
ya mlipuko.
x. Kuelimisha viongozi wa Serikali za Vijiji, Dini na Mashirika yasiyo ya Kiserikali
kuhusu Sera mbalimbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na
kutumia Sera hizo
xi. Kutoa taarifa za hali ya jamii kwa ngazi mbalimbali

1.12.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa Shahada au Stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii
kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliojiimarisha katika moja ya fani
zifuatazo:- Maendeleo ya Jamii (Community Development), Elimu ya Jamii
(Sociology), Masomo ya Maendeleo (Development Studies), Mipango na
Usimamizi wa Miradi na Menejimenti (Project Planning and Management) au
Jinsia na Maendeleo (Gender and Development).

1.12.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D.

1.13 AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI II (ASSISTANT COMMUNITY


DEVELOPMENT OFFICER GRADE II) NAFASI 18
1.13.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuratibu shughuli zote za maendeleo ya jamii katika Kijiji zikiwemo za wanawake
na watoto na zikizingatia jinsia;
ii. Kuwezesha jamii kushiriki katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia,
kutathmini mipango/miradi ya maendeleo;
iii. Kuhamasisha na kuwawezesha wanachi kupanga na kutekeleza kazi za
maendeleo ambazo ni pamoja na usafi wa mazingira, ujenzi wa nyumba bora
vijijini, ujenzi wa shule, zahanati, majosho, barabara za vijijini (Feeder Roads),
uchimbaji wa visima vifupi na uchimbaji wa marambo;
iv. Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga mbinu za kutatua vikwazo
vya maendeleo hasa vya maji na nishati kwa kuwa na miradi ya uvunaji wa maji
ya mvua, majiko sanifu na matumizi ya mikokoteni;
v. Kutoa na kuwezesha upatikanaji wa mafunzo kwa viongozi wa kijiji na vikundi
mbalimbali vya maendeleo kijijini kuhusu:-
- Utawala bora na Uongozi
- Ujasiriamali
- Mbinu shirikishi jamii na kazi za kujitegemea
- Chakula bora na lishe
- Utunzani na malezi bora ya watoto
vi. Kuwa kiungo kati ya wanakijiji (Afisa Mtendaji wa Kata) na watumishi wengine wa
Serikali katika kutekeleza shughuli za maendeleo;
vii. Kuwawezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za kujitegemea;
viii. Kuwawezesha wananchi kubaini na kuratibu rasilimali zilizopo na kuzitumia
katika miradi ya kujitegemea;
ix. Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kuwasaidia wananchi kutumia takwimu na
kumbukumbu mbalimbali za kijiji;
x. Kuwawezesha viongozi wa vijiji kutumia mbinu shirikishi jamii kuandaa ratiba za
kazi na mipango ya utekelezaji;
xi. Kuandaa na kutoa taarifa za kazi za maendeleo ya jamii kila mwezi kwa uongozi
wa kijiji na kwa Afisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya kata;
xii. Kuhamasisha na kuwezesha jamii kuona umuhimu wa kuthamini mazingira kwa
kutumia mazingira kwa njia endelevu na hasa kulinda na kuhifadhi vyanzo vya
maji kwa matumizi ya vizazi vya sasa na vya baadae;
xiii. Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na vya kimaendeleo;
xiv. Kuratibu shughuli za Mashirika na Asasi zisizo za Kiserikali na za kijamii;
xv. Kuratibu shughuli za kupambana na UKIMWI.

1.13.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye Stashahada ya


Maendeleo ya Jamii kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (Buhare au
Rungemba) au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

1.13.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C.

1.14 MKUTUBI DARAJA LA II (LIBRARIAN II) - NAFASI 1


1.14.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandikisha wasomaji;
ii. Kupanga vitabu katika rafu (Shelves);
iii. Kuazimisha na kupokea vitabu vinavyoazimwa;
iv. Kukarabati vitabu vilivyochakaa;
v. Kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wa kituo.

1.14.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza katika fani ya ukutubi au sifa inayolingana
na hiyo kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

1.14.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D.

1.15 MTENDAJI WA KATA DARAJA LA III (WARD EXECUTIVE GRADE III)


NAFASI 69
1.15.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika
Kata na atashughulikia masuala yote ya Kata;
ii. Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji,
mali, kuondoa njaa na Umasikini;
iii. Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya Kata;
iv. Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya Kata, Vijiji na
vitongoji;
v. Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata
yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika
Kata;
vi. Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo
lake;
vii. Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katika ngazi ya
Kata;
viii. Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi na
nakala kwa Katibu Tarafa;
ix. Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa
Vijiji, na NGOS katika Kata yake;
x. Atakuwa Msimamizi na Mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika Vijiji,
vitongoji, na Kata yake.

1.15.2 SIFA ZA MWOMBAJI.


Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne au Sita na kuhudhuria mafunzo ya
Stashahada yenye mwelekeo wa Utawala (Public Administration and Local
Gorvernment) au Sheria kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

1.15.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C

1.16 KATIBU WA KAMATI DARAJA LA II (COMMITTEE CLERK GRADE II)


NAFASI 3
1.16.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa ratiba ya vikao vyote vya Halmashauri na kamati zote kwa
kushauriana na Mkurugenzi Mtendaji;
ii. Kuandika Mihutasari ya vikao vya Halmashauri;
iii. Kuweka Kumbukumbu za vikao vya Halmashauri na kamati zake;
iv. Kutunza Vifaa vyote vinavyohusiana na mikutano;
v. Kuhifadhi orordha ya mahudhurio ya Madiwani na Wataalamu;
vi. Kutoa ratiba ya ufuatiliaji na utekelezaji wa maazimio;
vii. Kutunza Kanuni za Mikutano;
viii. Kusimamia cutting za mihutasari.

1.16.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Shahada /Stashahada ya Juu ya Sheria/Sanaa/ Utawala kutoka
vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

1.16.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D

1.17 MPISHI DARAJA LA II (COOK GRADE II) NAFASI 5


1.17.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kusafisha jiko
ii. Kupika chakula cha kawaida

1.17.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliofuzu mafunzo ya cheti yasiyopungua
mwaka mmoja katika fani ya Food Production yanayotolewa na Vyuo vya
Forodhani (Dar es Salaam), Masoka (Moshi), Arusha Hotel, Y.M.C.A (Moshi),
VETA (Mikumi) na Vision Hotel (Dar es Salaam) au vyeti vingine
vitakavyotambuliwa na Serikali.
1.17.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C

1.18 AFISA WA SHERIA DARAJA LA II (LEGAL OFFICER GRADE II) NAFASI 6


1.18.1 MAJUKUMU YA KAZI
Hili ni daraja la mafunzo katika kazi, hivyo Maafisa wa Sheria katika daraja hili
watafanya kazi za kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria Waandamizi ikiwa ni
pamoja na:
i. Kutoa ushauri na kufanya utafiti wa kisheria pale anapohitajika kulingana
na Wizara, Idara ya Serikali ama sehemu aliko;
ii. Kufanya mawasiliano na ofisi nyingine kuhusu masuala ya kisheria kwa
maelekezo ya Maafisa wa Sheria walio katika ngazi za juu.

1.18.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ya Sheria kutoka vyuo vinavyotambuliwa
na Serikali na waliomaliza mafunzo ya uwakili yanayotambuliwa na Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

1.18.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E

1.19 AFISA USTAWI WA JAMII DARAJA LA II NAFASI 2


1.19.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuendesha Usaili wa wahudumiwa (watu wenye ulemavu, wazee, familia zenye
matatizo, watoto na vijana wenye matatizo mbalimbali);
ii. Kufanya ukaguzi wa mazingira wanayoishi wahudumiwa ili kupata taarifa zao
kamili;
iii. Kuandaa taarifa za usaili na ukaguzi wa mazingira ya wahudumiwa;
iv. Kupokea na kukusanya taarifa za Ustawi wa Jamii kutoka kwa wadau na vituo
mbalimbali vya Ustawi wa Jamii;
v. Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za watu wenye ulemavu,
wazee, malezi ya watoto na familia zenye matatizo;
vi. Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya uandikishaji vituo vya
kulelea watoto wadogo mchana, malezi ya kambo (foster care) na vituo vya
walezi wa watoto wadogo mchana;
vii. Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya msaada wa Rais kutoka
kwa akina mama, waliojifungua watoto watatu au zaidi kwa mara moja;
viii. Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya watoto yatima au
wanaohitaji misaada mbalimbali;
ix. Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali toka kwenye
familia za watu wenye dhiki;
x. Kuhoji na kuandaa taarifa za washitakiwa;
xi. Kusimamia wahudumiwa katika makazi, vyuo vya mafunzo ya Ufundi Stadi vya
watu wenye ulemavu, Mahabusu za watoto na shule za maadilisho;
xii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
elimu, uzoefu na ujuzi wake.

1.19.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa katika fani ya Social Works au Sociology
au Stashahada ya juu katika Social Works kutoka Chuo cha elimu ya juu
kinachotambuliwa na Serikali

1.19.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D .

1.20 AFISA BIASHARA DARAJA LA II (TRADE OFFICER GRADE II) NAFASI 4


1.20.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuwasiliana na Wizara nyingine ambazo zinafanya biashara, kupata takwimu
ambazo zitatumika katika kutathimini mwenendo wa biashara na masuala
mengine ya kibiashara;
ii. Kusambaza taarifa za kibiashara kwa wafanyabiashara;
iii. Kutathmini mwenendo wa biashara kwa kuangalia hali ya masoko katika nchi
mbalimbali ambazo bidhaa zetu zinauzwa;
iv. Kuandaa grafu na chart ambazo zinaonyesha, mwenendo wa bidhaa
zinazoingizwa nchini na zile ziendazo nje kwa kila nchi ambazo hufanya biashara
na Tanzania.

1.20.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa mwenye Shahada/Stashahada ya Juu ya Biashara waliojiimarisha
katika fani ya Uchumi, Masoko, Uendeshaji Biashara au inayolingana nayo
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salam au chuo kingine chochote
kinachotambuliwa na Serikali na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka
mitatu.

1.20.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D .

1.21 AFISA BIASHARA MSAIDIZI- NAFASI 5


1.21.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa takwimu za mahitaji kutokana na bidhaa zinazozalishwa hapa nchini;
ii. Kuandaa takwimu zinazoonyesha tofauti kati ya mahitaji na uzalishaji;
iii. Kukusanya na kuunganisha nyaraka za sera za biashara na sheria za biashara;
iv. Kuandaa sifa za biashara na huduma ambazo zinauzwa nchi za nje kwa kila
sekta kama vile kilimo, madini, nguo na kadharika, na kuandaa sifa za kampuni
zinazouza nje;
v. Kukusanya takwimu za biashara kutoka kila wilaya, kuzichambua na kutathmini
mwenendo wa biashara kwa kila wilaya;
vi. Kukusanya takwimu kutoka kwa wafanya biashara ambao wanauza na kununua
kutoka masoko ya nje kama vile SADC, EAC, EU, U.S.A

1.21.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Stashahada ya Biashara kutoka vyuo vinavyotambuliwa na
serikali au sifa inayolingana na hiyo

1.21.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya mshahara TGS.C

1.22 MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II (WARD EXECUTIVE GRADE II)


NAFASI 28
1.22.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika
kata na atashughulikia masuala yote ya Kata;
ii. Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji,
mali, kuondoa njaa na Umasikini;
iii. Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya Kata;
iv. Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya Kata, Vijiji na
Mtaa;
v. Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata yake;
vi. Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika
Kata;
vii. Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo
lake;
viii. Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katikangazi ya
Kata;
ix. Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na
nakala kwa Katibu Tarafa;
x. Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa
vjiji, na NGOS katika kata yake;
xi. Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika Vijiji,
Vitongoji, na Kata yake.

1.22.2 SIFA ZA MWOMBAJI.


Kuajiriwa wenye Shahada yenye mwelekeo wa Utawala, (Public Administration
and Local Gorvernment) au Sheria kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali.

1.22.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D. .

1.23 AFISA MAENDELEO YA VIJANA DARAJA LA II (YOUTH DEVELOPMENT


OFFICER GRADE II) NAFASI 1
1.23.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuratibu na kisimamia utekelezaji wa Sera ya Vijana;
ii. Kuratibu shughuli za mikopo/mifuko ya Vijana;
iii. Kuhamasisha vijana ili kufufua moyo wa kujitolea nchini;
iv. Kupanga na kuendesha mafunzo yanayohusu stadi za maisha, stadi za kazi na
Afya ya Vijana;
v. Kuanzisha vituo vya ushauri nasaha, Ajira kwa Vijana na Elimu ya Familia kwa
kushirikiana na vyama visivyo vya kiserikali (NGO);
vi. Kukusanya takwimu mbalimbali zinazohusu Vijana;
vii. Kuratibu shughuli mbalimbali za NGO zinazoshughulikia masuala ya Vijana;
viii. Kuandaa mipango ya kuboresha malezi ya Vijana;
ix. Kuwahamasisha Waajiri na Wafadhili mbalimbali wachangie mfuko wa mikopo
nafuu kwa Vijana katika maeneo mbalimbali;
x. Kukuza na kuendeleza vipaji mbalimbali walivyonavyo Vijana ili kuwawezesha
kujiajiri;
xi. Kuandaa mipango ya kuwahamasisha Vijana ili kuanzisha miradi midogomidogo
ya kujiajiri

1.23.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya Maendeleo ya Vijana kutoka
chuo kinachotambuliwa na Serikali.

1.23.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D .

1.24 AFISA MIFUGO MSAIDIZI DARAJA LA II (LIVESTOCK FIELD OFFICER II)


NAFASI 35
1.24.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Atafanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa wafugaji wa eneo lake;
ii. Kwa kushirikiana na wakaguzi wa afya, atakagua nyama na usafi wa machinjio
mara kwa mara;
iii. Atakusanya takwimu za nyama na mazao yatokanayo na mifugo kama ngozi na
kuandika ripoti;
iv. Atatibu magonjwa ya mifugo chini ya usimamizi wa Daktari wa mifugo na
kushauri wafugaji jinsi ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa;
v. Atatembelea wafugaji mara kwa mara na kuwapa ushauri fasaha wa kitaalam
katika eneo lake la kazi;
vi. Atakusanya takwimu zote za maendeleo ya mifugo katika eneo lake;
vii. Atashauri na kusimamia ujenzi wa majosho, machinjio, vibanio na miundo mbinu
inayohusiana na ufugaji bora;
viii. Atahusika na uhamilishaji (Artificail Insemination) na uzalishaji (breeding) wa
mifugo kwa ujumla;
ix. Atashauri wafugaji kuhusu mbinu bora za kuzalisha maziwa na utunzaji wa
ndama;
x. Atafanya kazi nyingine za fani yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa
kazi.

1.24.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha VI waliofuzu mafunzo ya Stashahada
(Diploma) ya mifugo kutoka chuo cha Kilimo na Mifugo (MATI au LITI) au chuo
kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali.

1.24.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C

1.25 AFISA UVUVI DARAJA LA II (FISHERIES OFFICER GRADE II) NAFASI 1


1.25.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutekeleza Sera ya Uvuvi;
ii. Uhifadhi wa samaki na viumbe wengine wa majini na mazingira yao;
iii. Kuratibu na kusimamia uhifadhi wa mazingira;
iv. Kuendeleza uvunaji endelevu wa samaki na viumbe wengine wa baharini,
maziwa, mito, mabwawa na malambo;
v. Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu Uvuvi bora, utengenezaji na udhifadhi bora
wa Samaki na mazao ya uvuvi, Biashara na Masoko ya Samaki pamoja na
Ufugaji wa Samaki na viumbe wengine wa majini;
vi. Kutoa leseni za uvuvi;
vii. Kuendesha mafunzo ya taaluma ya uvuvi;
viii. Kusimamia na kutekeleza Sheria za Uvuvi (k.m. kuzuia uvuvi haramu);
ix. Kusimamia ukusanyaji wa takwimu za uvuvi pamoja na maduhuli;
x. Kuratibu shughuli za utafiti wa uvuvi;
xi. Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi
endelevu ya rasilimali ya uvuvi;
xii. Kukagua ubora wa Samaki na mazao ya uvuvi na kuweka viwango vya kitaifa.
1.25.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza katika fani za Sayansi ya Uvuvi (Fisheries
Science/Management, Zoology, Microbiology, Marine Biology, Food Science and
Aquaculture).

1.25.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D.

1.26 AFISA MIFUGO DARAJA LA II (LIVE STOCK OFFICER II) NAFASI 3


1.26.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuratibu mipango ya uzalishaji mifugo wilayani;
ii. Kuratibu uzalishaji wa mifugo katika mashamba makubwa ya mifugo;
iii. Kusaidia kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani;
iv. Kuratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo
kwa wataam wa mifugo na wafugaji;
v. Kufanya mapitio na marekebisho ya miundo ya masoko ya mifugo wilayani
kwake na mkoani;
vi. Kubuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani;
vii. Kufanya soroveya ya rasilimali (resource survey) kama vile mifugo, vyakula vya
mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi;
viii. Kuendesha mafunzo kwa Mawakala, wauzaji na wataalam juu ya njia salama
katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo;
ix. Kutafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali ;
x. Kufanya utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya;
xi. Kushiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa
malisho;
xii. Kuandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo;
xiii. Kufuatilia, kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo;
xiv. Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na fani yake kama atakavyoelekezwa na
mkuu wake wa kazi.

1.26.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Mifugo (Animal Science)
kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali au sifa inayolingana nayo.

1.26.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D

1.27 AFISA UTAMADUNI II (CULTURAL OFFICER GRRADE II) NAFASI 3


1.27.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutafiti masuala ya Lugha, Sanaa, Mila na Desturi katika ngazi ya Wilaya;
ii. Kufundisha fani mbalimbali za utamaduni katika Vyuo na Vituo vya Elimu na
mafunzo ya utamaduni;
iii. Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa kituo.

1.27.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye shahada au stashahada ya juu katika Sanaa au Lugha kutoka


vyuo vinavyotambulika na Serikali

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D

1.28 AFISA TARAFA NAFASI 7


1.28.1 MAJUKUMU YA KAZI
(i) Kwenye Mamlaka ya Serikali Kuu
i. Kumwakilisha na kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za
Serikali Kuu katika Tarafa;
ii. Kuandaa na kuratibu taarifa na ripoti zinazohusu masuala ya ulinzi na usalama
ya kata kwenye tarafa yake na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya;
iii. Kuhamasisha na kuhimiza wananchi kushiriki kwenye shughuli za maendeleo
kwenye Tarafa;
iv. Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Wananchi kwenye Tarafa;
v. Kuwa mlinzi wa amani katika eneo lake;
vi. Kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa sera za Serikali katika eneo lake na
kuhakikisha kuwa zinatekelezwa ipasavyo;
vii. Kuratibu shughuli zote za maafa na dharura mbalimbali katika eneo lake;
viii. Kuandaa taarifa zote zinazohusu masuala ya Serikali Kuu kuhusu utendaji wa
kazi za maafisa Watendaji wa kata wa eneo lake na kuziwasilisha kwa Mkuu wa
Wilaya;
ix. Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa katika eneo lake;
x. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Wilaya.

(ii) Kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa


i. Kuwasaidia Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa katika shughuli za Maendeleo
katika eneo lake;
ii. Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Vijiji, Kata na Mitaa;
iii. Kushiriki na kutoa ushauri katika upangaji wa mipango ya Maendeleo katika
eneo lake;
iv. Kuhudhuria vikao vya kamati za Halmashauri na Baraza la madiwani na kutoa
ushauri;
v. Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa
kutoka kwa Watendaji wa Kata;
vi. Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Wilaya, Miji,
Manispaa au Jiji.

1.28.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za Sheria,
Menejimenti, Utawala, Kilimo, Mifugo, Ushirika, Mazingira, au Maji kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.

1.28.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D

1.29 AFISA USHIRIKA DARAJA LA II (COOPERATIVE OFFICER GRADE II)


NAFASI 2
1.29.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kukagua vyama vya Ushirika vya Msingi vinavyoendesha miradi ya pamoja
(Jointy Venture );
ii. Kuhamasisha uanzishaji wa vyama vya Ushirika vya Msingi;
iii. Kukusanya na kuchambua takwimu zinazohusu Masoko katika Mkoa;
iv. Kutoa ushauri juu ya uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi;
v. Kuratibu/kushiriki katika Elimu ya Ushirika Shirikishi katika Vyama vya Ushirika
vya Msingi.

1.29.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza au Stashahada ya Juu (Advanced
Diploma) katika fani ya Ushirika kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali.

1.29.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D.

1.30 MKADIRIAJI UJENZI DARAJA LA II (QUANTITY SURVEYOR GRADE II)


NAFASI 1
1.30.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya kazi chini ya uangalizi wa Mkadiriaji Ujenzi aliyesajiliwa na bodi ya usajili
husika kama Proffesional Quantity Surveyor;
ii. Kufanya kazi kwa vitendo katika fani zinazomhusu ili kumwezesha mkadiriaji
ujenzi kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Ujenzi inayohusu;
iii. Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu miradi mbalimbali kuhusu bei za vifaa vya
ujenzi vya Majengo ndani na nje ya nchi;
iv. Kupitia mapendekezo ya miradi (project proposals) mbalimbali ya Majengo
yanayowasilishwa Wizarani na kutoa ushauri unaotakiwa.
1.30.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Shahada/Stashahada ya juu ya Uhandisi kutoka vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali katika fani inayohusiana na Ukadiriaji Ujenzi
(quantity Surveryor).

1.30.3 MSHAHARA.

Kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya Serikali TGS E

1.31 MTAKWIMU DARAJA LA II (STATISTICIAN GRADE II) NAFASI 1


1.31.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kubuni na kuendeleza mfumo wa kitaifa wa kukusanya na kuratibu takwimu;
ii. Kutengeneza utaratibu wa kukusanya takwimu pamoja na ule wa kuchukua
takwimu za mfano/vielelezo (Sampling);
iii. Kukusanya, Kuchambua na kuwasilisha takwimu ngazi za juu.

1.31.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza katika fani ya Takwimu au Hisabati kutoka
Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia Kompyuta.

1.31.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D.

1.32 MVUVI MSAIDIZI DARAJA LA II (FISHERIES ASSISTANT II) NAFASI 2


1.32.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutengeneza, Kushona, Kutunza na Kukarabati zana za uvuvi;
ii. Kutunza na kuangalia mabwawa ya samaki;
iii. Kutega mitego Ziwani au Baharini;
iv. Kutengeneza nyavu ndogo ndogo;
v. Kuwapa chakula samaki katika mabwawa;
vi. Kuvua samaki katika mabwawa;
vii. Kutoa ushauri kwa wavuvi kuhusu mbinu mbalimbali za uvuvi;
viii. Kukusanya takwimu za uvuvi kutoka kwenye vituo vya kupokelea samaki;
ix. Kutoa ushauri juu ya uhifadhi wa samaki na mbinu za usambazaji na uuzaji wa
mazao yatokanayo na samaki;
x. Kuwaelimisha wananchi juu ya ufugaji wa samaki na mambo muhimu ya
kuzingatia.

1.32.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye stashahada (Diploma)
ya Uvuvi au Uhifadhi wa Samaki na Masoko (Fish Processing & Marketing)
kutoka vyuo vya uvuvi vya Mbegani, Kunduchi au vyuo vingine vinavyotambuliwa
na Serikali.

1.33 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C

1.34 MPOKEZI (RECEPTIONIST) NAFASI 1


1.34.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kupokea wageni na kuwasaili shida zao;
ii. Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni wanaoingia
ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni;
iii. Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani;
iv. Kutunza na kudumisha usafi wa Switchboard na ofisi zake;
v. Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma;
vi. Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani wana miadi (Appointment) au
wamepata idhni ya maafisa husika;
vii. Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa mbalimbali ofisini;
viii. Kupokea simu kutoka Extension za ndani na kupiga nje ya ofisi;
ix. Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa
kwenda nje.

1.34.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili
na Hisabati na kufuzu mafunzo ya Mapokezi (front desk operation) au Upokeaji
Simu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

1.34.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B

1.35 MWANDAZI DARAJA LA II (WAITER GRADE II) - NAFASI 1


1.35.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa meza ya kulia chakula;
ii. Kupamba meza ya kulia chakula;
iii. Kupanga vifaa vya kulia chakula mezani;
iv. Kuondoa vyombo baada ya kula chakula

1.35.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV na kufuzu mafunzo ya
mwaka mmoja katika fani ya Food and Bevarages yatolewayo na vyuo vya
Forodhani Dar es Salaam. Masoka Moshi, Arusha Hotel na Y.M.C.A ya Moshi
na Vyuo vingine vinavyolingana ambavyo vinavyotambuliwa na Serikali.

1.35.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B

1.36 MTUNZA BUSTANI DARAJA LA II - (GARDNER II) NAFASI 3


1.36.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kupanda mboga, matunda, n.k. katika bustani;
ii. Kupalilia mazao katika bustani;
iii. Kupanda maua katika maeneo yanayohusika;
iv. Kupanda na kukata majani na kumwagilia maji;
v. Kufanya kazi zingine zitakazoelekezwa na Viongozi wa Kitengo chao.

1.36.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Cheti katika fani ya utunzaji bustani za maua, mboga na
upandaji majani kutoka chuo cha Maendeleo ya Wananchi, VETA, au JKT au
Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

1.36.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A

1.37 MHANDISI KILIMO DARAJA LA II (AGRO ENGINEERS) NAFASI 1


1.37.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo;
ii. Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana;
iii. Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za umwagiliaji;
iv. Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji;
v. Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafunindisha wakulima uendeshaji wa skimu
za umwagiliaji;
vi. Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji;
vii. Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji
pamoja na matumizi ya maji;
viii. Kuandaa mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za za kilimo;
ix. Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na
wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta;
x. Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora na
xi. Kushughulikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji
ipasavyo.
1.37.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye


mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo cha umwagiliaji au cha Zana za Kilimo
kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.

1.37.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS E

1.38 WAKILI WA SERIKALI DARAJA LA II - NAFASI 51


1.38.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Hili ni Daraja la Mafunzo katika kazi, hivyo Wakili wa Serikali katika daraja hili
atafanya kazi za kisheria kwa maelekezo ya Mawakili wa Serikali walio na
Uzoefu kazini, pamoja na ;
ii. Kuendesha mashauri mepesi Mahakamani;
iii. Kuendesha kesi za mahakama kuu;
iv. Kutoa Ushauri wa Kisheria kwa Serikali chini ya usimamiziwa Mawakili
Waandamizi;
v. Kushughulikia kesi za vizazi, vifo, ndoa, na kesi zinazotokana na mirathi
mahakamani;
vi. Kusimamia utayarishaji wa takwimu zinazohusu ndoa, talaka, mabadiliko na
mabatilisho ya ndoa;
vii. Kutayarisha maandishi juu ya Sheria ambazo Serikali/Tume ya kurekebisha
Sheria inataka zifanyiwe utafiti na kurekebishwa;
viii. Kufanya utafiti wa Sheria;
ix. Kuelimisha Umma kuhusu mambo ya Katiba na Haki za Binadamu.

1.38.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Mwenye Shahada ya Sheria (LLB) Kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na
Serikali na kumaliza vizuri mafunzo katika kazi (Internship) ya mwaka mmoja
katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

1.38.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia mishahara ya Serikali yaani TGS E.

1.39 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II NAFASI 1


1.39.1 MAJUKUMU YA KAZI
i.Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi na mbuga za wanyamapori;
ii.Kusimamia utekelezaji wa taratibu za uwindaji na utalii;
iii.Kutekeleza kazi za maendeleo katika Mapori ya Akiba;
iv.Kuhakiki ulinzi wa nyara za Serikali;
v.Kuhakiki vifaa vya doria;
vi.Kudhibiti usafirishaji wa wanyamapori na nyara nje na ndani ya nchi;
vii.Kudhibiti matumizi ya magari ya doria;
viii.Kuratibu uingiaji wa wageni katika Mapori ya Akiba;
ix.Kusimamia uwindaji wa kitalii;
x.Kudhibiti na kusimamia umilikaji wa nyara;
xi.Kuweka mikakati ya kudhibiti moto mkali;
xii.Kukusanya takwimu za wanyamapori na mimea.

1.39.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au Kidato cha VI, wenye stashahada ya


Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

1.39.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C.

1.40 AFISA UTALII DARAJA LA II NAFASI 1


1.40.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kukusanya taarifa za maeneo mapya yenye vivutio vya utalii kwa kushirikiana na
wadau wote;
ii. Kutoa Leseni za utalii kwa mahoteli na wakala wa utalii;
iii. Kukusanya na kuweka takwimu za watalii na safari za kitalii;
iv. Kutafuta na kupanga nafasi za masomo ya utalii ndani na nje ya nchi;
v. Kujibu malalamiko kutoka kwa watalii;
vi. Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wadau katika uendeshaji wa Biashara ya utalii.
vii. Kuandaa kaguzi mbalimbali za Wakala wa utalii;
viii. Kuchambua miradi ya wakala wa utalii na hoteli;
ix. Kukagua hoteli, loji na migahawa;
x. Kujibu na kufatilia malalamiko yanayoletwa na watalii;
xi. Kutoa ushauri wa kiutaalam kwa wakala wa utalii;
xii. Kukusanya taarifa za maeneo mapya yenye vivutio vya utalii kwa kushirikiana na
Washika dau wote;
xiii. Kukusanya takwimu za watalii kwenye sehemu/vituo nchini vya kuingilia/kutoa
wageni;
xiv. Kutunza kumbukumbu za vitabu/majalada ya Maktaba ya Utalii;
xv. Kutayarisha taarifa ya kila mwezi ya takwimu za watalii waliongia nchini na
mapato yaliyopatikana;
xvi. Kufanya tafiti ngo Survey kwenye Hifadhi za Taifa na maeneo tengefu ili kupata
idadi kamili ya Hoteli au Loji zinazotoa huduma kwa watalii;
xvii. Kufuatilia kwa karibu na kushirikiana na VETA juu ya maendeleo ya vyuo
vinavyotoa mafunzo ya utalii nchini;
xviii. Kuratibu miradi yote inayohusiana na utoaji wa mafunzo ya utalii;
xix. Kutayarisha ripoti za mwezi, robo mwaka, na za mwaka mzima;
xx. Kufuatilia kwa karibu maendeleo ya Sekta kwa kufanya survey;
xxi. Kuitisha mikutano ya Tourism Facilitation Committee;
xxii. Kutayarisha ripoti na kusambaza kwa wajumbe na kukufuatilia utekelezaji wa
maazimio;
xxiii. Kupitia miongozo inayohusu Tourism Facilitation Committee;
xxiv. Kuratibu shughuli za kubuni vivutio vya utalii na mienendo mipya ya kuendeleza
utalii;
xxv. Kutayarisha kuhakiki vivutio vya utalii nchini;
xxvi. Kuitisha mikutano/semina za uhamasishaji kuhusu uendelezaji utalii;
xxvii. Kushiriki katika kupitia ripoti za tathmini ya athari za kimazingira (EIA) kuhusu
miradi ya utalii;
xxviii. Kushirikiana na Mashirika/taasisi mbalimali za mazingira katika shughuli
zihusuzo utalii na mazingira;
xxix. Kukusanya rasilimali za uendeshaji katika vyanzo vya ndani na nje.

1.40.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada/stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za Utalii


au Hoteli kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

1.40.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D.

1.41 AFISA KUMBUKUMBU DARAJA LA II NAFASI 1


1.41.1 MAJUKUMU YA KAZI
Hili ni daraja la mafunzo katika kazi hivyo atafanya kazi kwa maelekezo ya Maafisa
Kumbukumbu walio juu yake kwa cheo. Kazi atakazojifunza na kufanya ni zile
zifanywazo na Afisa Kumbukumbu Daraja la I:-
i. Kudhibiti mifumo ya kumbukumbu, kutunza, na kusimamia matumizi ya
kumbukumbu za Wizara, Idara zinazojitegemea, Vituo vya kutunzia
kumbukumbu, Mikoa, Manispaa, Halmashauri za Wilaya, Nyaraka za Taifa na
Mashirika ya Umma kulingana na mahali alipo;
ii. Kutambua na kutafuta kumbukumbu katika masjala za Wizara, Mikoa, Idara
zinazojitegemea, Manispaa, Halmashauri za Wilaya, Vituo vya kuhifadhia
kumbukumbu na Nyaraka za Taifa;
iii. Kudhibiti mfumo wa kumbukumbu zinazozalishwa na kompyuta, kutunza na
kusimamia matumizi yake katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Asasi na
Serikali za Mitaa kulingana na mahali alipo;

1.41.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada ya Kwanza katika fani ya Utunzaji na Uhifadhi wa


Kumbukumbu (Records management & Archieves), Upimaji na Ramani na sifa
nyingine zinazolingana nayo kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na
Serikali. Aidha wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

1.41.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D.


1.42 AFISA USAFIRISHAJI DARAJA LA II (TRANSPORT OFFICER GRADE II )
NAFASI 1
1.42.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutayarisha gharama za uendeshaji wa usafiri kwa ajili ya kusaidia kutoa
maamuzi;
ii. Kuhakikisha kuwa takwimu na kumbukumbu zinazohusu vyombo vya usafiri
pamoja na mitandao yake zinatunzwa vyema na kwa usahihi. Kuandaa takwimu
zinazohusu maendeleo ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji, na kuwasilisha kwa
watumiaji ndani na nje ya nchi;
iii. Kukusanya takwimu za usafirishaji nchini;
iv. Kukadiria na kushauri juu ya utendaji wa miradi mbalimnbali ya sekta ya
usafirishaji;
v. Kutekeleza majukumu mengine yanayohusu sekta ya usafirishaji

1.42.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada/ Stashahada ya juu katika fani ya Usafirishaji kutoka


Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

1.43 FUNDI SANIFU (HAIDROLOJIA) DARAJA LA II (TECHNICIAN GRADE II


HYDROLOGY) NAFASI 9
1.43.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Ukusanyaji na ukaguaji wa takwimu za maji;
ii. Kutunza takwimu za maji;
iii. Kuingiza takwimu za maji kwenye fomu Na: H: 12 tayari kwa kutumiwa kwenye
michoro;
iv. Kuchora hydrograph za maji;
v. Utengenezaji visima vya rekoda, stendi za winchi, sinia za maji cable way post
n.k;
vi. Kufanya matengenezo ya vifaa vyote vya kupimia maji na hali ya hewa;
vii. Kuingiza takwimu kwenye kompyuta;
viii. Kufundisha wasoma vipimo.

1.43.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao
wana cheti cha ufundi ( FTC- Hydrology) au Stashahada ya Rasilimali za Maji na
wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

1.43.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C


1.44 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - HAIDROJIOLOJIA (TECHNICIAN GRADE II -
HYDROGEOLOGIST) NAFASI 12
1.44.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuhakiki uwezo wa kisima kutoa maji (Pump test);
ii. Kuchora ramani za awali za kiufundi;
iii. Kuhifadhi taarifa za kikazi (Field Data) zipatikanazo wakati wa utafiti wa maji
chini ya ardhi.

1.44.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao
wana cheti cha ufundi (FTC HYDROGEOLOGY) au Stashahada ya Kawaida ya
Rasilimali za Maji na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

1.44.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C

1.45 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - MAABARA YA MAJI (LABORATORY


TECHNICIAN WATER II) NAFASI 31
1.45.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya mchanganuo (analysis) kikemikali ili kuthibitisha/kutathmini vielelezo
(samples) vinavyohusika kwenye maabara;
ii. Kutunza vyombo vya maabara;
iii. Kutayarisha vitendea kazi vya maabala kwenye masomo ya sayansi kwa vitendo
iv. Kutambua, Kuthibitisha na kuweka kumbukumbu za takwimu za vielelezo
mbalimbali;
v. Kusaidia kazi za watafiti.

1.45.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita (vi) waliofuzu mojawapo ya mafunzo ya


miaka miwili (2) ya Stashahada (Diploma) ya ufundi sanifu wa Maabara ya maji
au sifa zinazolingana na hizo kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

1.45.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi ya Mshahara wa Serikali TGS C

1.46 MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) WATER RESOURCE ENGINEER


NAFASI 20
1.46.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya
miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji na kushiriki shughuli za
upembuzi yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu
mikubwa ya ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira;
ii. Kufanya mapitio ya taarifa za upembuzi yakinifu na sanifu za ujenzi wa
miundombinu ya miradi ya usambazaji maji na usafi wa mazingira;
iii. Kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na utengenezaji wa
miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya
kupata ubora unaokusudiwa;
iv. Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi na kupitia mapendekezo ya miradi
(project proposal) ya usambazaji maji na usafi wa mazingira;
v. Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa miundombinu au ajali zinazojitokeza
wakati wa utekelezaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira;
vi. Kutayarisha bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji;
vii. Kusimamia, kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na
mategenezo ya miundombinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
viii. Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za sekta
ya maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya
Wahandisi.

1.46.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water Resource


Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

1.46.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E.

1.47 MFUGAJI NYUKI MSAIDIZI II (NAFASI 2)


1.47.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kusimamia manzuki;
ii. Kutunza hifadhi za nyuki;
iii. Kukusanya takwimu za ufugaji nyuki;
iv. Kutunza kumbukumbu za kazi za utafiti;
v. Kuondoa nyuki wanaodhuru binadamu na mifugo;
vi. Kutoa leseni za biashara ya mazao ya nyuki;
vii. Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wananchi juu ya ufugaji endelevu wa nyuki na
matumizi bora ya mazao ya nyuki;
viii. Kutunza makundi ya nyuki wanaouma na wasiouma.

1.47.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye Astashahada (Cheti) au
Stashahada (Diploma) ya Ufugaji Nyuki kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na
Serikali.

1.47.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B/C.

1.48 AFISA WANYAMAPORI DARAJA LA II NAFASI 1


1.48.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutekeleza Kazi za Ushirikishaji Wadau Katika Uhifadhi;
ii. Kudhibiti Utoaji wa Leseni za Biashara Za Nyara na Vibari vya Kukamata
Wanyama Hai;
iii. Kushiriki Katika Kusuluhisha Migogoro ya Matumizi ya Wanyamapori
iv. Kudhibiti Matumizi Haramu ya Leseni za Uwindaji na Kuhahakikisha Kufuatwa
Kwa Maadili Katika Kutumia Wanyamapori;
v. Kuthibiti Matumizi Haramu ya Wanyamapori;
vi. Kufuatilia Utekelezaji wa Miongozo Mbalimbali ya Uhifadhi Wanyamapori;
vii. Kuhakiki Viwango vya Kukamata Wanyama Hai Kwa Ajili ya Biashara na Ufugaji.
viii. Kufanya Kazi za Kuzuia Ujangili;
ix. Kukusanya Taarifa, na Takwimu za Uhifadhi;
x. Kutekeleza Kazi za Uhifadhi Katika Mapori ya Akiba.

1.48.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa Wenye Shahada ya Sayansi ya Wanyamapori Kutoka Chuo Kikuu
Kinachotambuliwa na Serikali.

1.48.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D.

1.49 AFISA MICHEZO DARAJA LA II (GAMES AND SPORTS OFFICER GRADE II)
NAFASI 1
1.49.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa Walimu wa Vyuo, Shule, na Vituo
vya Elimu na Mafunzo;
ii. Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa walimu, Makocha, viongozi wa
vyama na vilabu vya michezo;
iii. Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa Timu za Michezo mbalimbali.

1.49.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa mwenye Shahada au Stashahada ya Juu ya Elimu ya Michezo
(Physical Education) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.49.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D.

1.50 FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UJENZI) - (CIVIL TECHNICIAN GRADE II)


NAFASI 2
1.50.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya kazi za ujenzi wa kuta za nyumba na kupaka rangi na kufunga
mabomba;
ii. Kuchonga vifaa vya nyumba za serikali ikiwa ni pamoja na samani furniture;
iii. Kufanya kazi za upimaji (survey) wa barabara, majengo na mifereji kama
atakavyoelekezwa;
iv. Kuwapangia kazi Mafundi sanifu wasaidizi na kuhakikisha wanamaliza kama
ilivyopangwa.

1.50.2 SIFA ZA MWOMBAJI


i. Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili
kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani za fundi ujenzi;
ii. Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu
kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika fani za
fundi ujenzi;
iii. Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I ( ujenzi) kutoka Chuo
cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali;
iv. Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za fundi ujenzi kutoka
Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

1.50.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C .

1.51 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III NAFASI 2


1.51.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi;
ii. Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi;
iii. Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha;
iv. Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori;
v. Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali;
vi. Kufanya usafi na ulinzi wa kambi;
vii. Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi;
viii. Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani;
ix. Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na
kukusanya takwimu zao;
x. Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya
Nchi;
xi. Kudhibiti wanyamapori waharibifu;
xii. Kudhibiti moto kwenye hifadhi;
xiii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake.

1.51.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au kidato cha sita wenye Astashahada ya
Uhifadhi Wanyamapori (Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka
Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa
na Serikali.

1.51.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B2.

1.52 FUNDI SANIFU DARAJA LA II (MIPANGOMIJI)- NAFASI 2


1.52.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kumsaidia Afisa Mipangomiji katika kukusanya kumbukumbu za shughuli za
mipangomiji;
ii. Kumsaidia kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa mipango ya matumizi ya
ardhi ya vijiji na kata;
iii. Kumsaidia Afisa Mipangomiji katika kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi na
kata.

1.52.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya
ufundi ya miaka miwili katika fani ya Mipangomiji

1.52.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C.

1.53 FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UPIMAJI ARDHI) NAFASI 2


1.53.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kupanga na kuandaa mahitaji ya kambi za upimaji, vifaa vya upimaji na mahitaji
ya jumla;
ii. Kufanya upimaji wa awali na kusimika ardhini alama za upimaji;
iii. Kufanya upimaji na kukusanya taarifa na takwimu zote za upimaji;
iv. Kuchora sketch ya mchoro wa upimaji;
v. Kufanya mahesabu ya upimaji.
1.53.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya
ufundi ya miaka miwili katika fani ya Upimaji Ardhi.

1.53.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C

1.54 FUNDI SANIFU DARAJA LA II (PHOTOGRAMMETRY)- NAFASI 2


1.54.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuianisha picha za anga na ramani na kutayarisha photo index;
ii. Kutunza kumbukumbu za picha za anga na ramani za photogrammetria;
iii. Kuhudumia wateja wa picha za anga na ramani za photgrametria;
iv. Kutunza kumbukumbu za uchoraji wa ramani;
v. Kuchora ramani ktika uwiano mbalimbili.

1.54.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya
ufundi ya miaka miwili katika fani ya Upimaji Picha (Photogrammetry)

1.54.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C.

1.55 MSAIDIZI WA MAKTABA (LIBRARY ASSISTANT) - NAFASI 3


1.55.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandikisha wasomaji;
ii. Kupanga vitabu katika rafu (Shelves);
iii. Kuazimisha na kupokea vitabu vinavyoazimwa;
iv. Kukarabati vitabu vilivyochakaa;
v. Kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wa kituo.

1.55.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa waliohitimu cheti cha Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne ambao
wamefaulu mafunzo ya Wasaidizi wa Maktaba (National Library Assistants
Certificate Course) yatolewayo na Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania au
wenye cheti kinacholingana na hicho.

1.55.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS. B.
1.56 OPERATA WA KOMPYUTA MSAIDIZI (ASSISTANT COMPUTER
OPERATOR) - NAFASI 3
1.56.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuhifadhi data;
ii. Kutunza kumbukumbu za shughuli za kila siku;
iii. Kugundua na kusahihisha makosa yanayotokea katika data;
iv. Kufanya kazi za Kompyuta;
v. Kuchapa orodha ya makossa;
vi. Kufanya programu ya matumizi;
vii. Kuchapa taarifa za mwisho;
viii. Kufanya kazi chini ya usimamizi wa Opereta wa Kompyuta Daraja la II.

1.56.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiliwa waliomaliza kidato cha nne au cha sita wenye Astashahada ya mwaka
mmoja ya masomo ya awali ya Kompyuta yanayojumuisha Uendeshaji wa
Kompyuta wa Msingi (Basic computer operations), Progam Endeshi (Operating
system), na Program Tumizi (Application Programs) au Fundi Sanifu wa
Kompyuta kutoka Kwenye Taasisi/Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

1.56.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B

1.57 MSAIDIZI WA MTENDAJI MKUU DARAJA LA II (ASSISTANT EXECUTIVE


SECRETARY) NAFASI 2
1.57.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida;
ii. Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu
wanapoweza kushughulikiwa;
iii. Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi na wageni, tarehe za
vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa;
iv. Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majadala, nyaraka au kitu chochote
kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini;
v. Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia
kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao;
vi. Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo,
na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika;
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali mahali alipo;
viii. Kutoa taarifa na kufuatiliapanapohusika kuhusu matengenezo yam ashine za
kazi;
ix. Kuandika muhtasari wa vikao vinavyohusika sehemu alipo na kufuatilia
utekelezaji wa maamuzi ya vikao hivyo;
x. Kuandika barua zinazotoa taarifa ya ratiba ya shughuli au safari za mkuu wake
na kuitisha vikao;
xi. Kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya mkuu wake sehemu mbalimbali.

1.57.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye stashahada ya kawaida ya Uhazili itolewayo na chuo cha
Utumishi wa Umma (TPSC) au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali
ambao wamehudhuria mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za'' Window,
Microstoft Office, Internet, E-mail na Publisher''. Pia wawe na uzoefu wa kazi
usiopungua miaka kumi na mbili. Aidha wawe wamehudhuria na kufaulu mtihani
wa mafunzo ya menejimenti kwa ajili ya wasaidizi wa watendaji wakuu kutoka
chuo cha utumishi wa Umma (TPSC) au vyuo vingine vinavyotambuliwa na
serikali.

1.57.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS F

1.58 AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA III (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS)


NAFASI 53
1.58.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kushirikiana na wakulima kuendesha mashamba ya majaribio na mashamba
darasa;
ii. Kutembelea wakulima/vikundi vya wakulima katika mashamba yao na kutoa
ushauri wa kitaalamu juu ya mbinu bora na za kisasa za kilimo cha kibiashara;
iii. Kufundisha na kuelekeza wakulima juu ya matumizi bora ya mbolea, madawa na
zana za kilimo;
iv. Kukusanya na kutunza takwimu za hali ya kilimo katika Kijiji;
v. Kubuni na kuandaa vihenge vya kisasa vya hifadhi ya mazao na kutoa elimu ya
matumizi sahihi ya mazao;
vi. Kutoa taarifa juu ya dalili za kuwepo visumbufu vya mimea na mazao;
vii. Kuandaa na kutumia daftari la kilimo katika kutekeleza majukumu yake ya kila
siku;
viii. Kushiriki katika mchakato wa kuibua fursa na vikwazo vya maendeleo
(Opportunities and Obstacles for Development (O & OD) na kuandaa mpango wa
maendeleo ya kilimo wa kijiji (Village Agricultural Development Plan (VADP), na
ix. Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya kila mwezi kuiwasilisha kwa Afisa Ugani wa
Kata na nakala kuiwasilisha kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji.

1.58.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne wenye Astashahada (Certificate) ya Kilimo
kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

1.58.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B

1.59 MSAIDIZI MIFUGO (LIVESTOCK FIELD ASSISTANTS) NAFASI 3


1.59.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kutoa huduma za ugani katika uendelezaji mifugo na mazao yake;
Kutibu mifugo na kutoa taarifa za magonjwa, tiba na chakula;
Kusimamia utendaji kazi wa wahudumu mifugo;
Kutunza takwimu na taarifa mbalimbali za mifugo;
Kukaguo ubora wa mazao ya mifugo;
Kusimamia ustawi wa wanyama;
Kufanya kaza nyingine atakazo pangiwa na msimamizi wake wa kazi
zinazohusiana na fani yake.

1.59.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV ambao wamepata mafunzo ya mifugo ya
muda wa miaka miwili na kutunukiwa Astashahada (certificate) ya uzalishaji na
afya ya mifugo kutoka vyuo vya mafunzo ya mifugo. (Livestock Training Institute
LITI) au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

1.59.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B

MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.


i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja Passport size ya hivi karibuni.
vi. Testmonials, Provisional Results, Statement of results, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 8 SEPTEMBA, 2017.
xii. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA

xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa


Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya
Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa Recruitment
Portal)

MUHIMU: KUMBUKA KUAMBATISHA BARUA YAKO YA MAOMBI YA


KAZI ILIYOSAINIWA PAMOJA NA VYETI VYA ELIMU. ANUANI YA
BARUA HIYO IELEKEZWE KWA KATIBU, OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA S.L.P 63100
DAR ES SALAAM.

You might also like