You are on page 1of 4

HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOMBERO

(Barua zote zitumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya)

TANGAZO

Kumb.Na.KDC/E.40/4/Vol.V/39 18/08/2017

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero anatangaza


nafasi za kazi za wasaidizi wa Hesabu, Dereva Daraja la II, Katibu Muhtasi
Daraja la III na Watendaji wa Vijiji Daraja la III watakaofanya kazi katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

A.MSAIDIZI WA HESABU (NAFASI 1)

1.SIFA ZA MWOMBAJI:

i. Awe na cheti cha kufaulu cha mtihani wa kidato cha nne (IV)
ii. Awe na cheti cha ATEC Level II au Foundation Level kinachotolewa
na NBAA
iii. Awe na uzoefu wa kazi Zaidi ya mwaka mmoja (1) katika fani hiyo.

2.KAZI ZA KUFANYA:

i. Kuandika na kutunza Register zinazohusu shughuli za Uhasibu.


ii. Kuandika hati za malipo na Hati za mapokezi ya Fedha.
iii. Kutunza majalada yenye Kumbukumbu za Hesabu.
iv. Kupeleka barua /nyaraka za Uhasibu Benki.
v. Kufanya usuluhisho wa masurufu,Karadha,Hesabu za Benki na Amana.

3.MSHAHARA:

Utakuwa katika ngazi ya TGS B,kima cha kuanzia ni Tshs.390,000/=


B.DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 1)

1. SIFA ZA MWOMBAJI:
i. Awe amehitimu kidato cha nne (iv), mwenye leseni daraja la C ya
uendeshaji.
ii. Awe na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka
mitatu bila kusababisha ajali.
iii. Awe na cheti cha majaribio ya ufundi daraja II.

2. KAZI ZA KUFANYA:
i. Ataendesha magari ya abiria (watumishi) au malori.
ii. Atahakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote
na kufanya uchunguzi kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu
unaohitaji matengenezo.
iii. Atafanya matengenezo madogo madogo katika gari na
iv. Atatunza na kuandika daftari la safari log-book kwa safari zote.

3.MSHAHARA:
Utakuwa katika ngazi ya TGOS A, kima cha kuanzia ni Tshs. 300,000/=

C.KATIBU MUHTASI DARAJA III (NAFASI 1)

1. SIFA ZA MWOMBAJI:
i. Awe amehudhuria mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu
ii. Awe amefaulu somo la hatimkato ya Kiswahili na kiingereza maneno 80 kwa
dakika moja
iii. Awe amepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote
kinachotambulika na Serikali na kupata cheti katika program za Windows,
Microsoft Office, Internet, E-Mail na Publisher.

2. KAZI ZA KUFANYA:
i. Atachapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
ii. Atapokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu
wanapoweza kushughulikiwa
iii. Atasaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada, nyaraka au kitu
chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini
iv. Atafikisha maelekezo ya mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na
kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.

3.MSHAHARA:
Utakuwa katika ngazi ya TGS B, kima cha kuanzia ni Tshs. 390,000/=
D.MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III (NAFASI 3)

1. SIFA ZA MWOMBAJI:
i. Awe mwenye elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo
ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani yoyote:

2. KAZI ZA KUFANYA:
i. Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
ii. Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na
Msimamizi wa Utawala Bora katika kijiji
iii. Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo
ya Kijiji
iv. Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
v. Kutasfiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
vi. Kuandaa taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha
wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini
na kuongeza uzalishaji mali
vii. Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya kitaalam katika kijijiKusimamia,
kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za kijiji
viii. Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu waliopo katika kijiji
ix. Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
x. Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji; na
xi. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

3.MSHAHARA:
Utakuwa katika ngazi ya TGS B, kima cha kuanzia ni Tshs. 390,000/=

4. MASHARTI MENGINE:
i. Awe Raia wa Tanzania
ii. Awe mkazi wa Wilaya ya Kilombero
iii. Awe na umri kati ya miaka 18-45
iv. Maombi yaambatanishwe na nakala za Vyeti vya Shule,Chuo,maelezo
binafsi (CV) na nyaraka zote muhimu pamoja na picha (passport size)
(2) zilizopigwa hivi karibuni.
v. Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza na
yatumwe kwa njia ya posta kwa anwani ifuatayo: -
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOMBERO,
S.L.P 263,
IFAKARA /KILOMBERO.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 04/09/2017 saa 09:30 Alasiri.

You might also like