You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu: 255-22-2114512, 2116898 OFISI YA RAIS,


IKULU,
E-mail: press@ikulu.go.tz
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
Tovuti : www.ikulu.go.tz 11400 DAR ES SALAAM.
Faksi: 255-22-2113425 Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mazungumzo kati ya Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli na Kampuni ya Bharti Airtel inayomiliki hisa katika
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania yameanza
rasmi leo tarehe 12 Machi, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo kamati iliyoundwa na Mhe. Rais


Magufuli inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
Palamagamba Kabudi na timu ya Bharti Airtel inaongozwa na
Mwanasheria Mkuu wake Bw. Mukesh Bhavnani.

Mazungumzo hayo yanalengo la kufikia makubaliano


yatakayokuwa na tija kwa pande zote mbili (Serikali ya
Tanzania na Bharti Airtel) na kuimarisha sekta ya
mawasiliano nchini Tanzania.

Kampuni ya Bharti Airtel iliomba kufanyika kwa


mazaungumzo hayo baada ya kamati iliyofanya uchunguzi
kuhusu umiliki wa kampuni ya Airtel Tanzania kuwasilisha
ripoti yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
12 Machi, 2018

You might also like