You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MATOKEO YA


OPERESHENI MAALUM ILIYOFANYIKA MJINI MAGHARIBI-
ZANZIBAR, KUANZIA TAREHE 14 – 21.03.2018

Ndugu Wanahabari,

1. UTANGULIZI ;
Zipo taarifa kuwa baadhi ya wananchi Mkoa wa Mjini
Magharibi wanatumia, wanashiriki, wanafadhili au kusaidia
biashara ya madawa ya kulevya kama ilivyo kwenye maeneo
mengine nchini.

Hata hivyo Serikali ipo kwenye vita kali ya kupambana na


mtandao wa madawa ya kulevya na Inspekta Jenerali wa
Polisi kwa kushirikiana na Kamisheni ya Polisi Zanzibar
waliunda timu kutoka Kitengo cha Operesheni Maalum za
Polisi Makao Makuu Dar es salaam kuja kuongeza nguvu
katika ufuatiliaji wa kero hii kama ilivyo kwenye maeneo
mengine ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2. MATOKEO YA OPERESHENI ;
S/N MAFANIKIO MATOKEO
/ IDADI
TAARIFA ZA INTELIJENSIA

1. Kupatikana kwa taarifa za watuhumiwa 105


wanaojihusisha na mtandao wa madawa
ya kulevya (kutumia, kuuza, kufadhili au
kusaidia)
JUMLA KUU 105

1
WATUHUMIWA WALIOPATIKA NA HATUA

1. Watuhumiwa waliofikishwa Mahakamani 26

2. Watuhumiwa waliopo chini ya Upelelezi 16

3. Watuhumiwa waliopo chini ya uangalizi 16


wa Polisi (Police Supervisee)
JUMLA KUU 58

VIELELEZO
1. Heroin Kete 1293
na Vifuko 3
sawa na
Gramu
74.385
2. Banghi (Vifurushi) 373

3. Banghi (Vifuko) 3

3. WITO :
Natoa wito na tahadhari kwa wananchi wote wanaohusika
kwenye mtandao huu kuacha mara moja kwa kuwa vita hii
imeshaanza na inaendelea kwa lengo la kuhakikisha usalama
wa vizazi vilivyopo na vizazi vijavyo maana madawa haya
yanaathiri zaidi vijana ambao ndiyo muhimili na nguvu kazi
ya Taifa.

Aidha nawapongeza wananchi wote waliotoa ushirikiano wa


kutoa taarifa za uhalifu huu bila ya kuona muhali. Niwaombe
2
wananchi wote kuendelea na ushirikiano huu wa kutoa
taarifa.

Mwisho natuma salamu kwa watuhumiwa wote waliotoroka


kule walipo wajue kuwa wanatafutwa na watakamatwa ili
wahojiwe na hatimae kufikishwa Mahakamani.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza

Liberatus Sabas – DCP


Mkuu Wa Uperesheni Maalum za Polisi Tanzania
21.03.2018

You might also like