Professional Documents
Culture Documents
Barua Ya Ufilisi 2
Barua Ya Ufilisi 2
Na ABL/SGF/007
Tarehe: 07.08.2020
Ndugu, walioambatana na barua hii, ni wanakikundi waliojiunga na benki ya Amana na kupata mikopo
chini ya udhamini wa kikundi.
Ndugu KHANIFA.J.DAFA amekopa mkopo wa shilingi 300,000/= mnamo tarehe 21/02/2020 chini ya
udhamini wao ambao marejesho yake ni kila wiki shilingi 12,500/=. Ndugu huyu halipi marejesho ya
mkopo wake kwa muda mrefu sasa licha ya kupelekewa taarifa mbalimbali za ukumbusho.
Hivyo tunaomba wadhamini wake waliofika katika ofisi yako uwape ushirikiano ili mdaiwa awalipe
pesa taslim shilingi 131,500/= ikiwa sehemu ya deni lililobaki. Vilevile unaombwa kuwapatia
wanakikundi ruhusa na msaada wowote utakaohitajika ikiwemo kukamata mali za mdaiwa ambazo
aliziweka kama dhamana katika kikundi na endapo hazikutosha kulipa deni basi mali nyingine ambazo
hazikuwekwa dhamana zishikiliwe ili deni lote liweze kulipika kama ilivyoanishwa katika mkataba wa
ukopeshaji.
WAKO,
Amana Bank Limited
……………………………… ………………………