You are on page 1of 37

Development also is a source of climate change because of high industrial growth that

lead to the occurance of global warming due to the most of the old and advanced machinery that
work twenty four hours a day and various transport medium for instance buses or motorcycle
produce Green House Gases like methane or carbon dioxide Co 2 which brings a substantial or
potential threat to our surroundings. Climate change is likely to push millions further into
poverty and limit the opportunities for development. Through the effects of global warming on
the earth surface like rising temperature threaten development because of negative effects on
economic growth in developing countries. The social impact of climate change will be further
affected by society’s efforts to prepare and adapt. For instance the aspect of global warming in
climatic change in most of poor and developing countries, particularly least developed countries,
will be among those most adversely affected and least able to cope with the anticipated stocks to
their social, economic and natural systems.

Development play a great role in climate change through the reduction of environmental
destruction that help to protect the problem of climate change. Through development there is a
emerge of introduce of new tools and equipment’s that has facilitated the reduction of
decompose waste. For example the introduction of electrical cookers facilitated in the slow
reduction of decompose waste that are not be friendly and sustainable in the development
process. Nevertheless development can cause facilitation in the reduction of the environmental
destruction, in turn, environmental destruction can undermine development.

SIMULIZI: SITOSAHAU - SEHEMU YA 01

MWANDISHI: SHAABAN HIJA

SIMU: 0786 056307

Mvua za masika ziliendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam nakusababisha maeneo
mbalimbali kushindikana kupitika kutokana nakujaa maji. Ilikua ni mwezi wa nne mwishoni
nikiwa katika likizo ndefu iliyosababishwa na ugonjwa wa Corona, mida ya saa kumi jioni wakati
nimelala chumbani nilisikia sauti ya mama ikiniita. Peter, Peter, ww Peter mbona unapenda
kulala hivyo mwanangu.Naam mama nakuja, niliitika uku nikiwa bado nausingizi.Taratibu
nilinyanyuka kitandani nakuelekea sebuleni alipokuwepo mama. Ehee, sasa hivi nimetoka
kuongea na bibi yako anasema uende Tabora ukamsaidie Tito kazi za shambani maana mara hii
wamepata mpunga si mchezo. Aliniambia mama mara tu baada yakufika pale sebuleni
hakungoja ata nikae. Waoooh, nilifurahi sana kusikia hivyo maana nilikua nishachoka kukaa
nyumbani ata kutembea ilikua ngumu kuhofia Corona. Sawa mama, sasa lini nitaenda?,
nilimuuliza mama kwashauku kubwa. Kama upo tayari ata kesho unaweza kwenda Tabora,
alinijibu huku akinikazia macho kunitizama. Wewe tu mama nanauli yako, nilimjibu kwa utani
uku nikijikuna kichwani japo sikua ata nikiwashwa. Ata usijali, ngoja nimpigie baba yako ampigie
rafiki yake yule wa Ubungo akuandalie tiketi kabisa kesho mapema tu usafiri
mwanangu.Alinijibu uku akichukua simu mezani namimi sikutaka kuchelewa nilirudi mbio
chumbani kupanga nguo zangu.

Nililichukua begi langu nakuanza kupanga nguo zilizokua kabatini, chache tu ndio zilikua
chafu ila nyingi zilikua safi kwani sikua na kawaida yakuvaa nguo nyingi bila kufua mara kwa
mara. Niliacha nguo zakuvaa tu kesho wakati wa safari nabuti yangu air max niliyokua
nikiipenda hatari. Usiku mida ya saa mbili baba alirudi kutoka Mwenge alipokua kafungua duka
na sisi tulikua tukiishi Tegeta kwa jeshi. Tukiwa menzani tukila chakula, mama alimuuliza baba
kama tayari ameisha ongea narafiki yake kuhusu kunikatia tiketi, baba alimjibu kua tayari
ameisha ongea nae hivyo nijiandae tu kesho safari. Nilifurahi sana baada yakusikia hivyo ndipo
mawazo mbalimbali yalianza kuniijia, nilitamani sana kuona misitu iliyopo kando ya barabara,
nyumba za vijijini pamoja namilima ya Morogoro vyote nilipenda sana kuvitizama wakati wa
safari. Mawazo hayo yalinifanya nitabasamu pekeangu nikiwa nimeshika kijiko bila kuendelea
kula. Ww Peter, sauti ya baba ilinishtua kutoka katika dimbwi la mawazo hadi kijiko
kikaniponyoka nakudondoka chini. Dada Eliza alicheka kwa nguvu hadi furaha niliyokuanayo
ikapotea. Muone vile, mtoto mdogo unamawazo mengi kama babu wamiaka sabini, alinitania
Eliza uku akinyanyuka kuelekea kabatini kuniletea kijiko kingine. Mda wote nilikua kimya
nikimtizama dada Eliza maana nijana tu tuligombana sababu yakutaniana.

Unawaza nini mwanangu?, aliniuliza baba uku akimimina maji ya kunywa katika glasi.
Nikiwa nawaza nijibu nini mama alidakia, "mwanao anawaza safari ya kesho maana toka
nimuambie ile mchana amekua nafuraha kweli". Hivi bado unapakumbuka vizuri uko kijijini
kwabibi yako?, aliniuliza baba uku akinitupia jicho. Aaah baba, nitapakumbuka tu japo ni miaka
mitatu imepita tangu niende nilipomaliza darasa la saba.Kijijini hapabadiliki labda mashamba
yaongezeke tu. Nilitania na wote wakacheka, ww leta ujuaji tu, ufike uko umuige Tito ufate
watoto wawatu watakuozesha uko uko. Alisema dada Eliza, aaah ushaanza dada. Nilimjibu uku
nikiendelea Kula. Baada ya maongezi marefu ulifika muda wa kwenda kulala, tuliagana nikaingia
chumbani kwangu kulala. Nilijitupa kitandani uku usingizi ukigoma kabisa, mawazo yote yalikua
katika safari ya kesho. Baada ya kuwaza muda mrefu nilipata usingizi miada ya saa nane. Niliota
nipo kijijini kwa bibi Ipole, nimesimama na binti niliyekua nikimpenda sana sehemu iliyokua na
nyasi nyingi. Wakati tukiongea mara ghafla alitokea ndege mkubwa, ndege yule alikuja
tulipokua tumekaa kisha akatuzunguka mara tatu kisha akapaa juu sana. Tukiwa katika taharuki,
ndege yule alishuka kwakasi nakunikamata kwa nguvu kwa kucha zake katika bega langu
lakushoto kisha akaanza kupaa namimi angani.Baadae ndege wengi walitokea angani wakawa
wanazunguka wakiwa wameniweka katikati yao.Walikua wakipiga kelele nyingi wakinibeba
kwakupokezana kuelekea juu zaidi. Kilichonishangaza ndege wale walikua wakininyenyua
kwakutumia bega langu la kushoto tu.

Nililia sana uku nikijitahidi kujinasua kutoka katika ndege hao lakini ilishindikana. Nikiwa
nimekata tamaa, mara ghafla ulivuma upepo mkubwa kule angani hali iliyopelekea ndege
aliyekua kanikamata kuniachia kisha nikaanza kurudi chini kwa kasi kubwa. Nilipiga kelele nyingi
kutokana na hofu yakudondoka chini, lakini kabla sijafika chini nilishtuka kutoka katika ndoto.
Mara baada yakuamka nilijikuta na jasho jingi pale kitandani, mmmh! hii ndoto vipi mbona
inatisha hivi. Nilijisemea uku nikishukuru kua ilikua ni ndoto tu lakini hofu juu ya ndoto ile bado
nilikua nayo. Ilikua vigumu kupata tena usingizi hivyo niliamua kuchukua simu nakuanza
kucheza gemu. Haukupita mda mrefu sana, nilisikia mlango wangu wachumbani ukigongwa.
Peter, Peter..... Ilikua ni sauti ya mama ikiniita. Naam mama, niliitika uku nikisitisha gemu ya
gari niliyokua nikicheza. Amka ujiandae baba yako akuwahishe stendi, aliniambia mama kisha
akaenda jikoni kuandaa chai. Niliangalia saa katika simu yangu, ilikua ni saa kumi na nusu.
Nilinyanyuka nakuelekea chooni kujiandaa. Chumba changu kilikua nachoo humo humo hivyo
sikutoka nje. Baada ya dakika kadhaa nilitoka chumbani nikiwa tayari nimeshajiandaa. Nilimkuta
baba mezani akinisubiri tunywe chai, nilimsalimia kisha tukaanza kunywa chai. Baadae
nilimuona mama akija kutoka chumbani kwake akiwa kashika kibegi kidogo, nilimsalimia kisha
akaniambia hilo begi linazawadi za bibi, mamamdogo na Tito hivyo nitaenda nalo.Pia alinipa laki
mbili za kutumia nikiwa njiani na nyingine nikampe bibi. Tulipomaliza kunywa chai baba
aliniambia niitoe pikipiki nje ili tuondoke kuelekea stendi. Muda wote dada Eliza alikua kalala
kwani alikua pono hatari. Baada yakuitoa pikipiki nilimuaga mama kisha tukaondoka.
Hatukuchukua mda mrefu sana tukawa tushafika stendi ya Ubungo sehemu ambayo mabasi ya
mikoani yanapoondokea. Tulipofika nje ya geti tulisimama kisha baba akampigia rafiki yake
ambae ni ajenti katika mabasi kampuni ya Colour Star yaendayo mikoa tofauti tofauti. Alikuja
akanichukua kisha baba akamlipa pesa ya tiketi Kisha tukaagana na baba nakuongozana na
rafiki yake kuingia ndani ya stendi. Mara nyingi hua sina story na baba hivyo hatukuchukua mda
mrefu kuagana. Muda wa basi kuondoka pale stendi ulikua tayari ushafika hivyo hakupoteza
muda alinionesha basi ninalotakiwa kupanda kisha akanikabidhi tiketi yangu.

Niliingia ndani ya basi baada yakunawishwa mikono kwa kutumia sanitizer dawa ya kuua
virusi vya Corona kisha nikampa konda begi kubwa aliloliweka katika buti, mimi niliingia na begi
dogo nikiwa nimeva barakoa (mask) usoni.Nilitafuta siti ambayo haikua namtu kisha nikakaa
upande wa dirishani. Baada ya kama dakika tano basi lilianza safari kuelekea mkoani
Tabora.Hakukua na abiria wengi hivyo siti kadhaa zilikua wazi. Tulipofika Mbezi kituo cha
mwisho Dar es salaam, basi liliingia stendi ambapo abiria kadhaa waliingia ndani ya basi. Katika
siti ya pembeni yangu alikuja jamaa akakaa. Baada ya kama dakika tano basi liliondoka. Ulikua
ni mwendo wa dakika kadhaa tukawa tushafika kituo chamabasi Kibaha mkoa wa Pwani.
Mabasi mengi tuliyakuta pale stendi yaendayo mikoa tofauti tofauti lakini namengine tuliyaacha
nyuma.Tulipofika pale kituoni abiria kama saba wali walipanda nakufanya basi kua level seat
nasafari ikaendelea. Baada yakushangaa shangaa maeneo kadhaa nilipata usingizi, baadae
alikuja konda aliyenikurupua usingizini kutaka nimuoneshe tiketi yangu. Pembeni yake alikua
kasimama mmama aliyekua na mtoto mdogo. Dogo, hii siti sio ya kwako. Siti yako ile pale mbele
namba kumi na tano kulia kwa yule dada, hii siti ya huyu mama. Aliniambia konda kisha
nikanyanyuka na kuchukua begi langu nilikua nimelipachika juu kisha nikaenda katika siti
aliyoniambia. Sikuipenda ile siti kwani haikua ya dirishani, upande wa dirishani alikua amekaa
msichana ambaye kiumri tupo sawa. Alikua bize kuangalia muvi iliyokua ikioneshwa katika basi
hilo hivyo ata sikumsalimia, nilipachika juu begi langu kisha nikaa.

Niliamua kulala kwani bado nilikua na usingizi maana jana yake sikupata usingizi
wakutosha. Wala sikuchelewa kupata usingizi na mara hii niliota ndoto yakutisha sana hali
iliyopelekea kelele ndani ya basi. Niliota nipo chini ya Mbuyu mkubwa uku giza likiwa
limetawala pande zote. Pembeni kulikua na moto ukiwaka unazunguka ule Mbuyu.Tulikua kama
watu nane tukiwa katika mstari mmoja kuuzunguka Mbuyu.Tulikua tumepakwa unga mweupe
kichwani, usoni, tumboni, mikononi, mgongoni na miguuni. Pembeni nilimuona msichana akilia
uku akisema "Bibi muacheni huyu". Kidole chake alikielekeza kwangu kumaanisha ni mimi lakini
chaajabu sikumuona yule aliyekua akiambiwa aniache isipokua sauti tu za ajabu ajabu zilitawala
juu ya Mbuyu ule. Ghafla alitokea ndege aliyefanana na bundi nakuja kutua chini yashina la
Mbuyu. Kufumba nakufumbua ndege yule aligeuka nakua mtu. Mtu yule sikuweza kumuangalia
usoni kwani macho yake yalikua makali yaliyotoa cheche za moto. Mara zile sauti za ajabu
zilizokua zikisikika zilikoma kusikika. Baadae walitokea ndege wengi ambao walikuja wakatua
kama atua kumi kutoka katika Mbuyu ule. Haukupita mda mrefu nawao waligeuka watu uku
mmoja wao akiwa kashika mkuki. Walikua ni wengi na wote walikua uchi wamejifunga
vitambaa vyeupe na vyekundu kichwani na mikononi.

Yule mtu aliyekua akitoa cheche za moto machoni alimuamuru aliyekua kashika mkuki
kufanya jambo, sikufahamu kamuambia nini kwani sikuelewa hiyo lugha aliyotumia. Yule mtu
mwenye mkuki alikuja karibu yetu na kuanza kumkodolea macho kila mmoja kwazamu.
Alimkamata mkono mmoja wetu na kumuweka pembeni. Aliamrishwa kulala chali kisha
akachomwa mkuki wa moyo. Damu ziliruka juu kisha yeye akaanza kuweweseka pale chini.
Alikuja bibi kizee nakata mkononi nakuanza kuikinga ile damu na baada yakumaliza aliipeleka
kwa mkubwa wao. Yule mtu Mwenye mkuki alitufata tena na kuanza kutuangalia kwazamu
kama mwanzo. Alikuja hadi niliposimama akanishika mkono nakuniweka pembeni. Duuh! zamu
yangu imefika, nilijisema uku machozi yakianza kunitoka nilijikuta nikiishiwa nguvu kwa hofu
nanilifata kila alichokua akiniamuru kufanya. Nililala chali kama alivyoniamrisha lakini mara yule
binti aliyekua akilia mwanzo akitaka Mimi niachwe alianza kulia tena nakuja nilipokua nimelala.
Niliona akimwagiwa unga mweupe na mmoja wawale wachawi kisha akanyamaza kimya.
Kulitokea kama marumbano hivi kati yao muda wa dakika moja hadi mkuu wao alivyoingilia kati
na kuamrisha kitu.Nikiwa bado nimelala pale chini nilimuona bibi kizee akija nakumchukua yule
binti. Alienda nae pembeni kisha wakapotea.

Mkuki ukanyenyuliwa juu ili kunichoma kifuani, nilipiga kelele nyingi hadi nikaamka
kutoka ndotoni najikuta watu wote ndani ya basi wakicheka uku wakinitazama. Dogo fala kweli,
anapiga makelele kama toto vile. Muvi yenyewe hata haitishi. Ilisikika sauti ya mwanaume
nyuma ya siti niliyokua nimekaa. Alizani zile kelele nilizopiga zilitokana na muvi iliyokua
ikioneshwa ndani ya basi lile. Hamna sio muvi jamani, alikua kalala toka tulipovuka
kibaha.Sasahivi tunakaribia Morogoro mjini ndio huyo kaamka na makelele hayo. Yule binti
niliyekua nimekaa nae alizungumza. Mara nilisikia sauti kutoka nyuma ya mwanamke, "atakua
kaota anabakwa huyo". Kauli ile iliamsha vicheko upya kwaabiria wengine lakini kwaupande
wangu nilikereka sana. Nilikua kimya ata sikuweza kunyenyua sura yangu kumtizama yeyote
sababu ya aibu niliyokua nayo mda huo.

ITAENDELEA.......

SIMULIZI: SITOSAHAU - SEHEMU YA 02

MWANDISHI: SHAABAN HIJA

SIMU: 0786 056307

Mida ya saa tano asubuhi tulikua tushafika stendi ya morogoro mjini. Abiria tulipewa
dakika kumi za kunywa chai pamoja nakwenda msalani ili baadae safari iendelee. Abiria wengi
tulishuka pamoja na yule dada niliyekua nimekaa nae karibu ambae ata jina sikumfahamu.
Haraka haraka nilishuka kwenda msalani. Dogo, kuingia toi shilingi mia tatu, jamaa aliyekua
pembeni ya mlango wakuingia chooni aliniambia. Nilitoa noti ya elfu mbili kisha nikampa yule
jamaa na akanirudishia chenji na kunipa kikaratasi kidogo mfano wa tiketi. Wabongo bwana,
kuingia tu toi hadi tiketi. Nilijisemea uku nikielekea katika moja ya mlango wa choo japo kulikua
na watu kadhaa pembeni waliokua wakisubiri pia. Niliusukuma mlango lakini haukufunguka.
"Dogo kuna foleni au hutuoni". Alisema mmoja wao lakini baada ya kumuangalia vizuri nilimjua,
alikua ni jamaa aliyenipakazia ndani ya basi. Ahaa, ngoja nikuoneshe sasa zamu yako bro.
Nilijisemea mwenyewe. Jamaa aliyekua chooni alitoka na mimi fasta sikuchelewa nikaingia
nakufunga mlango. Nje nilisikia makelele yule jamaa akiongea kwa jazba uku akigonga mlango
"Fanya fasta bichwa wewe". Mdogo mdogo ata sikua na haraka nilitaka nimkomeshe ikibidi
ajikojolee pale nje mlangoni. Mara mlango ukagongwa tena kwa nguvu na watu kama watatu
ikabidi nifungue tu maana mda mrefu nilikua nishamaliza. Nilipotoka tu jamaa mwingine
akaingia haraka hivyo yule jamaa akaendelea kusubiria. Nilipita karibu yake kisha
nikajikoholesha, jamaa alikasirika Ile mbaya. "Acha ufala dogo, unazingua njia pana hivyo hadi
uniguse", ata sikumjibu nikasepa zangu kibabe mdogo mdogo.

Nilitoka na kuanza kutembea tembea maeneo ya stendi, nilihakikisha siendi mbali ili basi
lisije likaniacha. Pale stendi palikua na mabasi mengi yaendayo sehemu tofauti tofauti uku haisi
za mjini Morogoro zikiingia na kutoka katika stendi hiyo. Nilimfata mmoja kati ya
wafanyabiashara wa stendi hiyo waliokua wamebeba vikapu begani wakiuza maji, soda, juis,
mahindi na vitu vingine. Nilinunua juis na kuanza kurudi kulifuata basi nililokua nimepanda.
Sikununua chakula maana mama aliniandalia usiku hivyo kilikuwepo katika kifuko kidogo ndani
ya begi langu. Nilifika katika basi kisha nikapanda na kukaa katika siti. Hawakuwepo abiria wengi
kwani mda wakuondoka ulikua bado japo si sana lakini kilichonishangaza nikwamba abiria
waliokua wamekaa katika siti ya nyuma hawakuwa wale niliowaona mwanzo. Mwanzo
alikuwepo mmama wamakamo na yule jamaa aliyenipakazia eti naogopa muvi baada
yakushtuka katika ile ndoto. Lakini mda ule niliwaona madada wawili wamekaa wakila ndizi.
Baadae alikuja bibi nakukaa mbele ya siti niliyokua nimekaa akiwa kashika kifuko chenye
mkate. Mmmh! Mbona anakaa siti sio yake, nilijiuliza sana maana mwanzo walikua wamekaa
madada wawili waliokua wakiogea sana mda wote. Itakua wameshuka njiani, nilijisemea uku
nikifungua juis yangu nakuanza kunywa. Mara nikakumbuka mkate wangu wa mayai
alionitengenezea mama, nikanyanyuka ili kuuchuku katika begi. Mmmh! Mbona begi langu
halipo naniliweka hapa hapa juu. Nilijiuliza pasipokupata jibu. Mda huo abiria karibu wote
walikua wameisharudi ndani ya basi lakini baadae walikuja wanaume wawili wakati nikiendelea
kupapasa pale juu kuangalia begi langu nikizani kua huenda limekandamizwa na mabegi
mengine uku gari likipiga honi ya mwisho tayari kwa kuondoka. Dogo unatafuta nini katika
mabegi yetu, aliniuliza mmoja kati ya wale vijana. Naangalia begi langu, niliweka hapa lakini
silioni. Niliwajibu uku nikiendelea kunyanyua baadhi ya mabegi yaliyokuwepo sehemu hiyo.
Dogo kwanini usiweke katika siti yako unakuja kuweka uku, jamaa mwingine aliniuliza. Hii ndio
siti yangu, niliwajibu huku nikijiamini. Wakati huo gari likianza kuondoka. Aah, hebu pisha tukae
hii siti sio yako tulikua tumekaa sisi toka tumetoka Arusha hadi hapa, jamaa alidakia. Bro vipi,
basi hili limetoka Dar sio Arusha bhana isitoshe hii siti nilikua nimekaa na mdada hivi nyinyi
hamkua katika siti hii. Niliwajibu uku nikionesha wasiwasi usoni. Hahahahaaa, abiria waliokua
wakifatilia maongezi yetu walicheka baada ya mimi kuwajibu hivyo. "Dogo ashapanda gari
sio,kua makini ushaachwa na basi lako", sauti ya mtu pembeni ilisikika ikiniambia mimi.

Nilihisi kuchanganyikiwa kwakweli maana basi nililokua nimepanda mwanzo linafanana


kila kitu na basi nililopanda sasa hivi. Baada ya abiria kuona hali yasitofahamu niliyokua nayo
walimwita konda wabasi lile. Konda njoo, kunadogo huku kapanda ila sio basi aliotakiwa
kupanda. Mmoja kati ya abiria alimuita konda. Konda alikuja uku kakunja uso. "Dogo vipi, basi
gani ulikua umepanda na unatoka wapi unaenda wapi?". Aliniuliza konda baada yakufika.
Linaitwa Colour star, natoka Dar naenda Tabora linafanana nahisi hadi jina,nilimjibu konda.
Duuh, mabasi yanafanana haya yote nikampuni moja tena yapo zaidi ya hamsini lakini hili bas
limetoka Arusha linaenda Dar, ukishuka unatakiwa kukariri plet namba ya basi ulilopanda dogo.
Alinijibu konda. Inamaana narudi tena Dar na je mizigo yangu nitaipataje, nilijiuliza tena kwa
sauti hali iliyosababisha konda kumuambia dereva asimamishe basi. "Oya Oswad simamisha
tumshushe dogo kakosea basi anaenda Tabora". Konda alimwambia dereva uku akinivuta
mkono kuelekea mlangoni kunishusha.

Basi lilisimama nanikashushwa nisijue la kufanya, sikua mbali sana na stendi hivyo
niliamua kurudi stendi uku nikikimbia nikizani huenda nitalikuta basi nililokua nimetokanalo
Dar. Ilinichukua kama dakika tano kufika pale stendi lakini sikujua sehemu lilipokua limepaki lile
basi kutokana na stendi kujaa mabasi hivyo bila kupoteza mda nilienda moja kwamoja
kwamfungua geti wapale stendi kumuuliza kama basi kampuni ya Colour star liendalo Tabora
kama limeisha toka. Nilijua fika atakua anayajua mabasi vizuri maana ndo kazi yake. Bro
shikamoo, nilifika nakumsalimia yule jamaa mfungua geti. Marhabaa, nambie dogo. Alinijibu
uku akiandika andika kitu katika note book aliyokua kaishika. Bro naomba kuuliza, eti basi la
Colour star litokalo Dar kwenda Tabora limeondoka, nilimuuliza uku nikitamani anijibu kua bado
halijatoka lakini si rahisi maana dakika kumi tulizokuwa tumepewa zakushuka kunywa chai
nakwenda msalani zilikua zishapita. "Lishaondoka kama dakika nane hivi, kwani vipi dogo
umeachwa?". Yule jamaa alinijibu uku akiniachia swali zito. Nilitikisa tu kichwa kuashiria
kukubali maana ata kuongea nilishindwa.

Uzembe huo dogo, acha kuchelewa chukua bodaboda kama unapesa uliwahi basi maana
halijafika mbali sana siunajua hawaruhusiwi kukimbiza ata mji halijavuka. Aliniambia yule jamaa
nami sikuona sababu yakuendelea kusimama pasipo kuchukua hatua. Nilitoka nje ya stendi
kuangalia bodaboda maana niliziona wakati narudi stendi baada ya kushushwa katika lile basi.
Hazikua mbali zilikua nje ya stendi tu. "Bro naomba nisaidie, natoka Dar naenda Singida ila
nimeachwa na basi la Colour Star niliyokua nimepanda imeondoka stendi kama dakika 11
zilizopita hivyo naomba uniwahishe katika hilo basi" .Nilimwambia mmoja kati ya madereva
bodaboda watatu waliokua wamekaa pamoja. "Dogo unashingapi fasta nikuvushe?", Alijibu
mmoja wao. Elfu tano, niliwajibu uku nikionesha sura ya huzuni. "Aaah unazingua dogo, basi
lipo mbali sasahivi, kwakukusaidia fanya elfu ishirini na tano mda unaenda". Jamaa aliongea uku
akinikazia macho usoni. Nilikubali kisha nikapewa helmeti nilikaa katika pikipiki natukaanza
safari kulifata basi. Tuliondoka kwaspidi kubwa lakini sikujali ilikua muhimu nilifikie tu lile basi.

Tuliyapita mabasi kadhaa pasipo kuliona basi la Colour star hali iliyosababisha kunitia hofu
zaidi. "Dogo shikilia vizuri inabidi tuongeze spidi basi lipo mbali", alizungumza yule bodaboda
uku akizidisha kasi. Ata sikujibu kwani nilikua nikitizama mbele tu kuangalia lile basi. Ilituchukua
kama dakika kumi, kwambali tuliliona basi lenye rangi ya basi la Colour star. Nilihisi furaha
moyoni natabasamu taratiibu likarejea usoni. Tulilisogelea basi karibu kabisa na hivyo tukapata
uhakika ndo lenyewe lakini tulitakiwa kulipita ili twende mbele tulipige mkono lisimame. Ilikua
vigumu maana basi lilikua lishaupita mji wa Morogoro mjini hivyo liliongeza spidi. Bahati gani
mbaya hii jamani, nilijisemea huku nikionesha tena kukata tamaa. Mungu si asumani
tulifanikiwa kuliovatake na kwenda kusimama mbele ili kulisimamisha.Tulilipiga mkono kisha
likasimama, nilimpa dereva bodaboda pesa yake baada yakuamini kua ndo lile lile basi nililotoka
nalo Dar.

Niliingia ndani ya basi nakumwambia konda kua mimi niabiria walile basi niliachwa stendi
ya Morogoro. "Tiketi ikowapi", aliniuliza konda. Nilimuonesha baada yakuitoa katika mfuko
washati. Nilielekea katika siti yangu nakumkuta yule msichana niliekua nimekaa nae tangu
nilipohamishiwa katika siti ya pembeni yake kule Kibaha. Mara minong'ono ndani ya basi
ikaanza "Kubwa jinga hili sinilikuambia Dogo kaachwa stendi". Ilisikika sauti ya yule jamaa
niliyemzingua kule chooni stendi ata sikumjibu nikakaa katika siti.. "Ww mkaka unachekesha
kweli, hahahaa". Aliniambia yule msichana uku akimalizia nakicheko kilichonikasirisha. "Sasa
ww mtoto mjinga uliachwa vipi nabasi", aliniuliza yule mdada.

ITAENDELEA..................

SIMULIZI: SITOSAHAU - SEHEMU YA 03

MWANDISHI: SHAABAN HIJA

SIMU: 0786 056307

Sasa wee mtoto mjinga uliachwa vipi na basi?, aliniuliza yule mdada kimasihara uku akiwa
nashauku yakutaka kujua kilichonipata. Aaaah kawaida tu. Nilimjibu uku nikiwa nimeinama
sikutaka ata kumtizama usoni niliona kama ananichoresha tu ndani ya basi. Ona ulivyochafua
shati mgongoni, mmmh jamani nacheka lakini ata si yakucheka. Aliongea yule mdada nakufanya
abiria wa siti yaupande wa pili sawa natulipokaa kuanza kunitizama sana uku wakicheka. Haraka
nikageuka nyuma kujiangalia nilivyochafuka lakini sikuweza kuona, hivyo yule dada alishika
shati langu kwa nyuma kisha akaivuta ile sehemu iliyochafuka ili nione. Duuuh! Ilikua ni hatari.
Nilikua nimechafuka sana nikakumbuka nilidondoka wakati nikirudi mbio pale stendi baada
yakushushwa katika basi nililopanda likitoka Arusha kwenda Dar. Hii kweli dhahma. Nilijisemea
uku nikisimama kuchukua shati lingine. Nilivuta begi langu nililokua nimelipachika kwa juu
nikatoa tisheti kisha nikavaa baada ya kuvua lile shati lililokua limechafuka. Nilirudisha begi pale
juu lakini wakati wote nikiendelea napirika zakubadirisha shati abiria karibu nusu kati ya abiria
wote waliokuwemo humo walikua wakinitizama. Mtoto anabalaa huyu. Ilisikika sauti ya
mwanamke siti za nyuma. Itakuwa hajawahi kusafiri, huwezi jua. Mtu mwingine pia nilimsikia
akisema hivyo lakini ata sikua na mda wakumtizama mtu. Hiyo aibu niliyokuwanayo ata
haielezeki.

Sikua nastori na mtu japo aibu nilikuanayo lakini nilijikaza. Suruali yako pia imechafuka
balaa. Aliniambia tena yule dada niliyekua nimekaa nae, ikabidi nianze kujikagua. Sasa hii si
balaa, ujinga ngani huu, hii siivui bhana. Nilijisemea uku nikijiangalia lakini sikuona
nilipochafuka. mmmh nimechafuka wapi, mbona sioni?. Nilimuuliza yule dada aliyekua kainama
akicheka mda wote. Nakutania bhana, umezubaa mno na wewe. Mdada aliniambia bila ata
kujali watu waliokua wakitutizama mda wote. Ikabidi nipige kimya maana kanichoresha vya
kutosha. Mara simu yangu iliita, alikua ni mama aliyepiga. Halloo mama. Niliongea baada ya
kupokea simu. Mwanangu umefika wapi sasa hivi?. Aliniuliza mama. Tumefikaa.. tumefikaaa.
Dah! Kiukweli nilikua ata sijui tumefika wapi maana sikua mwenyeji, ikabidi nimuulize yule
dada. Eti hapa ni wapi?. Nilimuuliza wakati simu ikiwa bado ipo hewani, aliniambia kisha
nikamjulisha mama. Tuliongea kwa mda kidogo kisha tukaagana.

Ehee hebu niambie ilikuaje maana hadi basi linaanza kuondoka pale stendi sikukuona
nikajua ushashuka Morogoro ndo safari yako inapoishia. Aliniambia yule msichana huku
akinigeukia kunitizama. Hapana bado sijafika safari yangu inaishia Tabora ila basi liliniacha tu
pale stendi. Nilimjibu yule msichana uku nikimtizama usoni kwa kuibiaibia. Sikuweza kumkazia
macho maana toka nilipokaa nae pale sikuwahi kumuangalia machoni nazani nikutokana na
aibu iliyotokana na mikasa iliyokua imenitokea. Kumbe ni msichana mdogo tu ndo ananisumbua
mda wote huo, tena ata hajaniacha miaka. Nilijisemea baada ya kumuangalia vizuri yule mdada.
Sasa ilikuaje tukakuacha?. Aliniuliza tena uku akionesha shaauku ya kutaka kujua kilichonitokea.
Ilibidi nimpe stori yote ilivyokua hadi kufanikiwa kulipata tena hilo basi. "Mmmmh! Pole sana
aisee”, alinipa pole baada ya kuvuta pumzi ndefu kutokana na kustaajabishwa na kuachwa
kwangu pamoja na gharama niliyotumia kulifatilia basi. Asante nishapoa. Kwa muda ule mfupi
tulijikuta tukizoeana hivyo kwakiasi fulani, hali yakujiamini ilirejea tofauti na mwanzo. Baada ya
stori nyingi aliniambia anaitwa Farida anaelekea Tabora. Waooo! Jina zuri kama wewe vile.
Niliamua kujitutumua japo kiukweli nilikua mwoga hatari kupiga stori na wanawake. OK, "ww
unaitwa nani?”. Aliniuliza uku akichukua ndizi mbili katika kifuko kidogo kisha akanipa moja.
Naitwa Peter Wakitaa. Nilimjibu kimasihara uku nikimenya ndizi aliyonipa na kuanza kula.
Hahahaaa, Jina lako nikama la mtu mjanja mjanja ata halifanani na vituko unavyovifanya, mara
kupiga kelele katika basi, mara kuachwa na basi stendi. Sijui kama linaendana na wewe hilo jina,
Alinijibu uku akionesha mdhaha zaidi. “Ah,nilipewa hilo jina na jirani yetu ata kwenyeukoo wetu
halipo". Nilimjibu kisha sote tukacheka.

Eti Peter Wakitaa, ilikuaje ukapiga makelele yale baada yakuamka ndotoni?. Aliniuliza swali
lile uku akinitizama usoni na hivyo macho yetu yaligongana. Tulitazamana kwasekunde kadhaa
huku nikionesha wazi kustaajabishwa na uzuri wa Farida. Tulitazamana kwakukaziana macho
uku tukitoleana tabasamu usoni. Kiukweli hapo ndipo nilipogundua kua nilikua nikipiga stori na
msichana mrembo sana. Sikulijua hilo nazani sikupata nafasi yakumtizama vizuri. Alikua nasura
nzuri yaduara nangozi yarangi yamaji yakunde, macho mazuri namwanya mdogo niliouona
kutokana na tabasamu dogo aliloliachia usoni. Alikua nachuchu ndogo zilizosimama, hakua
mwembamba wala mnene. Lipsi nyembamba zilizonishawishi kila nilipozitizana ata sikutamani
kufumba macho nisimuone. Zilipita sekunde kadhaa kama sio dakika bado macho yangu yalikua
yakipiga kona katika mwili wake. Mara ghafla alitizama pembeni ili kukwepa macho yangu
nakushindwa kuniangali. "Mbona hunijibu swali langu?”. Alinializa akiwa kainama. Oooh
kunakitu nilikua najaribu kukumbuka. Ilibidi nizuge kidogo kama hakijatokea chochote kisha
nikamuhadithia jinsi ile ndoto mbaya ilivyokua hadi kusababisha kuamka na makelele yale ndani
ya basi. Heee, kumbe ulikua sahihi kupiga yale makelele baada yakuamka maana mmh ndoto
yako inatisha sana, "sitaki tena unisimulie”. Aliniambia uku tukiendelea kula ndizi taratibu.

Baada ya stori nyingi zautani, alitoa simu yake kubwa aina ya Samsung Galax kisha
akaanza kucheza gemu ya gari. Alicheza kwa muda kisha akanipa na mimi nicheze. Peter
unaweza kucheza gemu hii, ningumu kila nikicheza huwa sifiki mwisho, "ningumu balaa”.
Aliniambia uku akinipa simu yake. Waooo!. Ilikua nigemu ambayo hua naipenda sana lakini kila
nikijaribu ku-download katika simu yangu ilikua inakataa. Nilianza kuicheza uku akinitizama
navoicheza, nilifanikiwa kufika mwisho nakupata point nyingi. Farida alishangaa hali
iliyopelekea kunisogelea karibu kabisa ili aone nacheza vipi. Aliniambia nimfundishe hivyo
nilipitisha mkono wangu wakulia mgongoni kwake ukatokea kwambele namkono wakushoto
niliupitisha kwambele nikaikamata simu nakuanza kumuelekeza. Baada yamuda kidogo wakati
nikimuelekeza alilalia begani kwangu uku akionesha kusinzia. Ule mtikisiko wa gari ulizidi
kuniweka matatani kwani alipoegemea siti alikua kaubana mkono wangu wakulia hivyo nikawa
kama nimemkumbatia nakufanya mapigo yangu ya moyo kwenda mbio.

ITAENDELEA..................

SIMULIZI: SITOSAHAU - SEHEMU YA 04

MWANDISHI: SHAABAN HIJA

SIMU: 0786 056307

Baada ya muda kidogo wakati nikimuelekeza jinsi ya kucheza gemu, alilalia begani kwangu
uku akionesha kusinzia. Ule mtikisiko wa gari ulizidi kuniweka matatani kwani alipoegemea siti
alikua kaubana mkono wangu wa kulia, nilikua kama nimemkumbatia nakufanya mapigo yangu
ya moyo kwenda mbio. Safari iliendelea uku tukivipita vijiji mbalimbali vya Morogoro ambavyo
ata kwa majina sikuvijua zaidi ya Dumila sehemu ambayo basi ilisimama na akapanda abiria
mmoja. Niliendelea kucheza gemu katika simu ya Farida lakini ghafla nilipata wazo lakujipiga
picha kupitia simu yake kwani simu yangu ilikua haitoi picha vizuri.

Nilibofya sehemu ya camera nakujipiga picha wakati huo Farida akiwa bado kalala tena akiwa
kaniegemea. “Waoooo! Picha kali balaa”, Farida alitoka vizuri japo alikua kalala lakini uzuri
wake haukujificha kabisa. Niliipenda sana ile picha hivyo nikairusha katika simu yangu kwa njia
ya Bluetooth. Ni kama nilinogewa hivi, nikaamua kupiga picha nyingine tena, nikanyoosha
mkono kisha nikamuegemea Farida aliekua bado kalala. Wakati nikijiandaa kupiga picha mara
simu yake ikaanza kuita. “Duuuh hii noma sasa”. Nilijisemea uku nikimtazama Farida aliyekua
tayari ameshaamka kwa sababu ya mlio wa simu yake. “Vipi nani kapiga?”. Aliniuliza uku
akifikicha macho yake. Ata sikumjibu nilimpa simu yake aangalie mwenyewe atamjua aliyepiga
wakati akipokea.

Aliipokea na kuanza kuongea, alitumia dakika kadhaa kuongea na simu lakini mabishano
ndio yaliyotawala zaidi. Baadae alikata simu baada ya kusonya kisha akanigeukia mimi. “Watu
wengine sijui wakoje, wasumbufu hatari. Nishamwambia simtaki bado tu ananilazimisha”.
Aliongea Farida uku akionesha kukasirishwa na mtu aliyetoka kuongeanae katika simu muda
mfupi uliopita. “Ukiona hivyo ujue kweli anakupenda, kama hajakupenda hawezi kupoteza
muda wake siku zote kukuambia nakukusisitiza umkubalie”. Nilimwambia uku nikionesha uoga
maana sikufikilia kama Farida atakua ni mkali kiasi hicho maana alikua akimfokea sana yule mtu
aliyempigia na kumsisitiza kua asimpigie tena simu. “Kupenda sio kosa lakini umpende mtu
anaekupenda, upendo mwingine nikaraha kwawengine maana nawao wanahaki yakuwapenda
watu wengine. Ukiona hakujali ujue yupo anaempenda, inabidi ujiongeze ili usipoteze mda
wako bure”. Farida alizungumza uku akionesha msisitizo wakile anachozungumza nakunifanya
niamini kua tayari Farida anamtu anaempenda hivyo mimi nimechelewa.

Ukimya ulitawala kwa muda nikiwa nimezama katika dimbwi la mawazo nikiamini kua ata
mimi sina nafasi kwa Farida. “We Peter mbona huongei au ndio umekasirika nilivyokua
nikimjibu yule aliyepiga simu”. Alinishitua Farida kwa kuniuliza swali, wakati nikitafakari jinsi ya
kumjibu mara sauti ya konda wa basi ikasikika. “Abiria wa Dodoma wajiandae, tunaelekea
stendi sasa hivi”. Mazungumzo pamoja na pirika za watu kuandaa mizigo yao vilitawala ndani ya
basi hivyo mazungumzo yetu hayakuendelea. Niliangalia muda ilikua ni saa tisa na dakika
hamsini, muda huo tulikua tukivuka Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania tukielekea
stendi ya mabasi ya mkoani Dodoma. Haukupita muda mrefu tukawa tushafika stendi ya mabasi
Dodoma ambapo abiria kadhaa walishuka na wengine walipanda. Haukupita muda mrefu, basi
lilianza kuondoka pale stendi.

Tulielekea kituo kingine cha Dodoma mjini, sehemu ambayo kunavyoo kwaajili ya wasafiri
pamoja na vyakula. “Abiria tunawapa dakika kumi na tano kwenda msalani na kula chakula”.
Ilisikika sauti ya konda mara baada ya kufika katika kituo hicho ambapo bila kuchelewa abiria
walianza kushuka haraka ili wawahi msalani pamoja na kula chakula. “Hapa kama mtu
hajapotea tena, ha ha ha haaa nakula kandala mimi”. Alisema Farida akinilenga mimi. “Acha
zako, mimi sikupotea Morogoro. Nilitaka kutembeatembea kidogo nikawaacha mtangulie tu”.
Nilimwambia uku nikinyanyuka kwenye siti. “Ha ha haaa Peter bhana, hebu twende kwanza
tukale maana hii njaa niliyonayo sio poa”.

Kiukweli mwanzo sikua nikiifurahia sana safari yangu ila kwa muda mfupi niliozoeana na
Farida nilijikuta nikifurahia zaidi uwepo wake katika siti yangu. Nilijikuta nikijisemea moyoni,
"nakupenda Farida". Lakini haikusaidia kitu maana hakusikia nilichokua nikiwaza juu yake.
Tulienda sehemu wanayouza chakula tukakaa uku viti vyetu vikitizamana. “Niletee wali nyama
na juisi ya parachichi”. Aliagiza Farida mara baada ya kufika muhudumu wa pale. “Umepata
dada, ehee vipi wewe nikuletee chakula gani?”. Aliniuliza muhudumu yule. “Mmmmh! Kama
alivyoagiza malkia wangu”. Nilijibu uku nikimtizana Farida nakumshika mikono aliyokua
ameiweka juu ya meza uku nikitikisa miguu yangu kwa chini. “Nikweli wapendanao hula chakula
cha aina moja”. Alijibu muhudumu na kuondoka, wakati huo Farida alikua akinitizama tena
akicheka na kufanya dimpozi zilizokua katika mashavu yake kuonekana na kufanya urembo
wake kutawala machoni mwangu.

“Weee muhudumuuu, hebu tuambie shingapi tusije tukashindwa kulipa mkatuoshesha


vyombo hapa”. Farida alimuuliza muhudumu aliyekua tayari kashafika mbali kidogo akifata
chakula. “Sahani moja ya wali ni elfu mbili, juisi glasi shilingi miatano tu”. Alijibu muhudumu
yule. “Haya poa”. Tulimjibu kisha tukaendelea na stori. “Farida labda hujalijua hili, uwepo wako
umefanya niifurahie safari yangu licha ya matukio niliyopitia uko nyuma ambayo yalifanya
niichukie safari hii”. Nilimwambia Farida wakati chakula kikiwekwa mezani na muhudumu. “Mh!
Kwa nini Peter?”, Aliniuliza Farida wakati muhudumu akitunawisha mikono. “Ukiachana na
uzuri ulionao, wewe nimchangamfu sana. Yaani kila ulitajapo jina langu kwa sauti yako nzuri na
nyororo natamani safari yetu iendelee, ata sitamani tufike haraka tuendako maana mmoja
wetu akifika hatutokua pamoja tena.

Nilianza kutupia ndogo ndogo lakini ule uchangamfu wake aliokuanao mwanzo mara
ghafla ulipungua. “Duuh nimeyakoroga”. Nilijisemea mara baada yakumuuliza maswali mara
kadhaa akawa ananijibu kwa mkato tu. Nilipata hofu tutakaporudi tena ndani ya basi itakuaje.
“Peter ulikua unasema mimi ni mzuri, mbona mimi ata siuoni huo uzuri jamani?”. Aliniuliza
Farida uku akipeleka mdomoni glass ya juis. Aisee nilihisi kupata nguvu upya maana nilikua
nishakata tamaa nilihisi kua hakuzipenda stori nilizokua nikimpa. Acha nianze kuropoka sasa
nikiamini kua nimepata nafasi nyingine tena. “Farida, hakika wewe ni mzuri huenda ikawa
nitofauti katika macho ya wengine lakini kwangu wewe nizaidi ya mrembo.

ITAENDELEA..................

USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU ZINAZOFUATA.

SIMULIZI: SITOSAHA - SEHEMU YA 05

MWANDISHI: SHAABAN HIJA

SIMU: 0786 056307

“Farida, hakika wewe ni mzuri huenda ikawa nitofauti katika macho ya wengine lakini
kwangu wewe ni zaidi ya mrembo na kama.......”. Kabla sijamaliza alidakia, “Peter acha
kuniongopea mwenzio nikavimba bichwa bure kumbe ata sitofautiani na sanamu la uhuru”.
Ilibidi nicheke sana maana Farida alikua nikama comedian vile, muda mwingi alikua akiongea
utani tu. Muda huo tulikua ndio tunamaliza kula, haukupita muda muhudumu alikuja tukamlipa
kisha tukanawa na kuondoka. “Naenda chooni nikukute hapa maana nilikuambia utangulie
unaweza ukapanda tena basi lingine". Alinitania Farida mara baada ya kutoka nje. “Poa lakini
ata mie naenda chooni nikapunguze maji, atakaewahi kutoka amsubiri mwenzie hapa”.
Nilimjibu kisha tukaachana kwenda msalani maana vyoo vya wanaume na wanawake havikua
sehemu moja.

Baada yakumaliza nilitoka nakurudi sehemu tuliyo ahidiana kukutana kabla ya kuingia
kwenye basi. Nilimkuta akinisubiri, tabasamu mwanana aliliachia mara baada ya kukutanisha
macho yetu. “Daah! Dogo mkali huyu, kama konda asingenihamishia kwenye siti yake wala
nisingejuana nae. Kweli viruri huja kwa njia usiyodhani kabisa”. Niliendelea kuwaza uku
nikimsogelea taratibu, ghafla kuna mtu alipita akikimbia akanigonga begani nikawa kama
nadondoka chini. Ata sikutegemea, nilimuona Farida akija haraka nakunishika mkono. “Pole
Peter, yaani jamaa anapita mbio pasipo ata kuangalia. Kakuumiza ata haombi samahani
anaendelea na safari zake”. Alizungumza Farida uku akionesha kukasirika, sikumjibu maana
nilihisi aibu kidogo.

Wakati tukiwa bado tumesimama pale pasipo kuongea chochote tulisikia tangazo
likitangazwa kwa njia ya kipaza sauti kilichokuwepo katika stendi hiyo. “Abiria wa basi la Colour
Star No. 2 rudini ndani ya basi kuendelea na safari”. Baada ya kusikia hivyo tu, Farida alinivuta
mkono kuniharakisha kwenda kupanda basi. Tulikua tukikimbia kuelekea lilipo basi lakini kabla
hatujafika katika basi mara tukaona ajali ya bodaboda na basi kampuni ya Mohamed Trans
liendalo Msoma kupitia Shinyanga. Niajali ambayo niliishuhudia kwa macho yangu, nilimuona
dereva bodaboda na abiria wake mwanamke wakirushwa juu mara baada ya kugongana uso
kwa uso na basi lililokua likitoka pale stendi. “Mungu wangu”. Nilimsikia Farida akizungumza
uku akiniachia mkono nakushika kichwa chake.

Farida alikua kama kaishiwa nguvu vile, alikua akitetemeka hivyo sikuchelewa nikamvutia
kwangu kisha nikamkumbatia na kumziba usoni asiendelee kutazama ajali ile. Aisee, dogo alikua
na joto zuri hatari, chuchu zake zilinichoma kifuani kwa sekunde kadhaa na kunifanya nisahau
kwa muda kua tunatakiwa kuwahi kupanda basi. Nilikuja kushtuka baada ya kusikia honi ya basi
lingine lililokua likirudi nyuma usawa na pale tulipokua tumesimama ili kutoka pale stendi. “He!,
twenzetu basi litatuacha”. Nilimwambia Farida wakati nikimtoa kifuani kwangu kisha
nikamshika mkono kwenda kupanda basi ambalo halikua mbali natulipokua tumesimama.

Tulipanda nakukaa katika siti zetu nakuacha watu kibao wakitazama ile ajali. Basi lilianza
kuondoka pale stendi kwa mwendo wa taratibu kutokana na kuwepo kwa foleni
iliyosababishwa na ajali ile. Trafiki walikua wameshafika hivyo uangalizi zaidi ulichukuliwa.
Muda wote Farida alikua kainama tu akionesha kua hakua sawa kabisa. “Vipi mbona kimya?”.
Nilimuuliza wakati tukiwa bado hatujavuka eneo la ajali. “Mmmh! Ww acha tu, sitamani ata
kuangalia nje. Hivi watapona kweli wale?”. Alimaliza kwa kuniachia swali uku akinitazama usoni,
alionesha dhahri kua ile ajali imemgusa sana. “Daah! Sijui itakuaje, mimi na wewe hatujui ila
hiyo ajali si ya kitoto”. Nilimjibu uku nikisimama kuchugulia nje kupitia dirishani, ata sikuona
vizuri kinachoendelea sababu ya wingi wa watu waliokua wamezunguka pale kuwasaidia
majeruhi na wengine wakifatilia tukio lile.

Baada yakuvuka pale foleni iliisha hivyo basi liliongeza kasi uku minong’ono mingi
ikitawala ndani ya basi. Kila mmoja aliizungumza kwa namna yake ile ajali, wapo waliosema
dereva bodaboda ndiye mwenye makosa wengine walimlaumu dereva wa basi lile. Safari
iliendelea na baada ya masaa kadhaa tulifika Manyoni stendi ikiwa ni saa kumi na mbili na nusu
jioni. Walishuka abiria watatu na baada ya muda kidogo basi liliondoka, wakati huo Farida
alikua kalala nadhani ni kwa sababu ya mchoko wa safari. Nilitoa simu mfukoni ili nimpigie bibi
kumjulisha kua nimefika Manyoni lakini simu yake ilikua haipatikani nikaamua kumtumia Tito
meseji kumjulisha.

Mida ya saa tatu usiku tulikua ndio tunaingia Tabora mjini hivyo nilianza kuandaa vitu
vyangu kwa ajili yakushuka. Nilimwamsha Farida aliyekua bado kalala. “Hee! Tumefika?”.
Aliniuliza uku akikaa vizuri kutazama nje. “Kumbe kweli, tupo Checkline hapa sasa hivi tutafika
stendi". Aliongea Farida mara baada ya kutazama nje kwa muda kidogo, aliuchukua mkoba
wake kisha akatoa simu kutazama muda. “Kuna Miss call kibao za mama kanipigia mara nane
nilipokua nimelala, atakua ana wasiwasi sana uko. Itabidi nimpigie”. Alizungumza uku akipiga
simu nakuanza kuongea mara baada ya simu kupokelewa upande wa pili. Baada ya dakika
kadhaa basi lilikatisha na kuingia stendi. “Haya abiria tumefika”. Alisema konda wa basi na
abiria wakaanza kushuka. Tulitazamana kwa sekunde kadhaa pasipo kuongea chochote uku
abiria wakiendelea kushuka. “Acha nimwambie ukweli kua nampenda ata akikataa poa tu si
hatutoonana tena”. Nilijisemea uku nikitaka kuupeleka mkono wangu kumshika Farida aliyekua
bado kakaa akinisubiri ninyanyuke.

“Faridaa, Faridaa…..”. Ilisikika sauti ya mwanamke ikiita nje karibu na mlango wa basi.
“Mmmh! Mama huyo, twende tushuke ananisubiri”. Alizungumza Farida kisha akasimama, ata
sikua najinsi ikadi nisimame tu nakuanza kutembea taratibu kuelekea mlangoni. "Kirahisi rahisi
tu, haiwezekani ngoja nifanye kitu muda bado ninao wakumueleza". Niliwaza haraka
chakufanya Kisha nikaamua!!!!!

ITAENDELEA..................

SIMULIZI: SITOSAHAU - SEHEMU YA 06

MWANDISHI: SHAABAN HIJA

SIMU: 0786 056307

“Kirahisi rahisi tu, haiwezekani ngoja nifanye kitu muda ninao wakumueleza”. Niliwaza
haraka chakufanya kisha nikaamua kumvuta mkono Farida aliyekua mbele yangu akiukaribia
mlango wa basi ili kushuka. Ooooh! nilikua na wakati mgumu sana pale Farida alipo simama
baada kumvuta mkono. “Vipi Peter?”. Aliniuliza baada ya kusimama kwa sekunde kadhaa
pasipo kumuambia chochote. Nilipata kigugumuzi, sikujua nianze vipi kumuambia kua
nampenda. Alipoona siongei chochote alitabasamu na kuanza kupiga hatua tena kuuelekea
mlangoni, taratiibu na mimi nilianza kupiga hatua kuelekea mlangoni uku nikijilaumu kua
nimeshindwa kuitumia nafasi yangu ya mwisho. Baada ya kushuka nilimuona mama yake Farida
akimpokea mwanae, alikua ameongozana na msichana mwingine ambae kwa kumtizama alikua
ni mkubwa zaidi ya Farida. Nilienda hadi kwenye buti (sehemu ambayo huwekwa mabegi
makubwa ubavuni kwa basi kwa nje) ili kuchukua begi langu ambapo nilikuta abiria kadhaa
wakitolewa mabegi yao na Konda wa basi na kuondoka zao.

Farida na mama yake pamoja na yule msichana mwingine walikuja na kusimama karibu
na mimi wakisubiri kuchukua begi. Walipofika tu niliona begi langu likitolewa kwenye buti
hivyo nilienda kulichukua na kuanza kuondoka kuelekea nje ya stendi. Wakati nikitembea
kuelekea nje niliwaza mengi sana kuhusu Farida pasipo kupata majibu. Niliwaza ni lini nitaonana
nae tena ili nimuambie hisia zangu kwake. Sikua ata na namba yake ya simu zaidi ya ile picha
niliyompiga akiwa kalala, kiukweli nilikata tamaa kabisa ya kuonana nae tena na hivyo nilianza
kuangalia usafiri wa bodaboda kunipeleka gesti. Ilikua ni lazima nilale ili kesho yake niendelee
na safari ya kwenda kijijini kwa bibi Ipole. Niliwaona dereva bodaboda wengi pale nje ya stendi
hivyo niliamua kumfata mmoja wao lakini kabla sijawafikia nilisikia sauti ikiniita. “Peter Peter
simama”. Alikua ni Farida akiniita, nilimjua baada ya kumuangalia vizuri wakati akija akikimbia.
Kulikua na kiza kidogo lakini haikua kazi kumtambua binti niliyempenda safarini.

Nilihisi furaha sana kumuona tena japo sikujua ni kipi kilichomfanya anikimbilie. Alikuja na
kusimama karibu yangu uku akipumua kwa kasi akionesha kua si mtu wa mazoezi. “Farida
kukimbia hapo na hapa tu unahema hivyo duuuh!”. Nilimtania uku nikiangalia nyuma kutizama
kama mama yake anakuja. “Safari imenichosha tu, hua na kimbia hadi chozi zinanitoka kwa
kupigwa na upepo usoni kwa sababu ya kasi niliyo nayo, yaani ni noma au tujaribu
kushindana?”. Alinijibu Farida hali iliyonifanya ni cheke sana. “Aisee takuacha mbali, gari ya Fid
Fosi ishawahi kunikimbiza hadi ikapata pancha. Nilimjibu kwa utani zaidi. Akaniuliza “Lakini si
walikukamata”. Nikamjibu “Mmmh mimi au mwingine? Wanipate wapi, gari yao imepata
pancha na kwambio hawaniwezi, niliwasumbua siku hiyo”. Nilivyomwambia hivyo alicheka hadi
akaniegemea. “Kweli wewe kiboko. Unajua nini, nimekumbuka kua sijakupa namba yangu best.
Nipe simu yako nikuandikie fasta coz mama na dada wananisubiri”. Aliongea akionesha kua
anaharaka sana hivyo nilimpa simu bila kuwaza nisije nikakosa ata namba yake. Alichukua
nakuanza kuandika kisha akawa anapiga na kukata katika simu yangu kama mara mbili hivi kisha
akanirejeshea simu yangu. “Isipopatikana hiyo ya tigo nicheki katika hiyo nyingine ya voda
muda wote ipo hewani”. Aliongea uku akisogea kunikumbatia ili kuniaga.

Alikuja na kunikumbatia, nilihisi msisimko wa ajabu kwa mara nyingine tena lakini mara hii
ilikua ni zaidi. Pasipo kutarajia niliachia begi nililokua nimelishika likadondoka chini tiiii,
nilipeleka mikono yangu mgongoni kwake na kuanza kumpapasa. Kutokana na kuwepo na hali
ya baridi mda ule, tulikumbatiana kwa muda kidogo uku Farida akipumua kwakasi. Alikua
akiniita kwa sauti ya chini sana. “Basi P… P…Peeter kwa heri tutawasilia.. a..an..a, nasubiriwa
uuuko nitachelewa”. Alizungumza kwa shida kidogo lakini cha ajabu aliendelea kunikumbatia
zaidi. “Wee Faa hebu twende tunachelewa. Mama anatusubiri kwenye gari uko, unafanya
ujinga gani huo”. Dah! Nilishtukaa kusikia hivyo, fasta nikamuachia isije kua msala. Ile kuangalia
nyuma namuona yule msichana aliekuja kumpokea kakasirika ile mbaya. “Ngoja nisepe zangu
nisije nikalala selo bure”. Nilijisemea uku nikiinama kuchukua begi langu. Farida hakuonekana
kua na wasiwasi badala yake alinikonyeza nakuniambia “Baiii Peter”. Wee ata sikujibu
chochote, nikanyanyua begi nikaanza kutembea mbele nikiwa na wasiwasi sana. Baada ya
kupiga hatua kadhaa niligeuka nyuma nikamuona Farida aliongozana na yule msichana hadi
kwenye gari ndogo ambayo ilikua mbali na sehemu tuliyokua tumesimama. Haukupita mda
mrefu, walipoingia tu gari lile liliondoka.

Ilibidi nisimame nibaki nikiitazama ile gari hadi ilipopotea machoni mwangu. Nilihisi
kuchoka ghafla, nikalikalia begi langu na kubaki nimeshika kichwa nikijilaumu kua peke yangu
muda ule bila Farida. Zilipita dakika kadhaa nikiwa bado nimekaa juu ya begi, mara meseji
ikaingia katika simu yangu iliyonipa nguvu ya kunyanyuka nikiwa na furaha sana.

ITAENDELEA..................

SIMULIZI: SITOSAHAU - SEHEMU YA 07

MWANDISHI: SHAABAN HIJA

SIMU: 0786 056307

Zilipita dakika kadhaa nikiwa bado nimekaa juu ya begi, mara meseji ikaingia katika simu
yangu iliyonipa nguvu ya kunyanyuka nikiwa nafuraha sana. Ilikua ni namba ngeni na meseji
iliandikwa hivi “Usijali Peter, tutaonana kesho. Mwambie dereva bodaboda akupeleke Victoria
Gest house maana sio mbali na hapa home, utamlipa elfu nne tu. Ukifika nijulishe”. Meseji yake
ilimalizikia hivyo. “Waooooh”. Nilijisemea kwa sauti uku nikitamani kumjibu lakini niliacha
baada ya kuona kua muda umeenda sana. Ilikua ni saa nne na dakika mbili usiku. “Daah! time
imeenda hiyo, ngoja nifanye fasta nisije nikakuta vyumba vimejaa”. Nilijisemea uku
nikinyanyuka na kuelekea sehemu ambayo kulikua na dereva bodaboda, hawakua mbali sana
nanilipokua nimekaa.

“Vipi dogo wapi hiyo nikupeleke fasta” (Dereva bodaboda :1), “Oya man njoo nikupeleke
chap” (Dereva bodaboda :2), “Mwache mwanangu, kichwa changu hicho” (Dereva bodaboda :
3). Zilikua ni sauti za madereva bodaboda ambazo zilinichanganya kiasi kwamba sikujua ata
nimfate yupi. Alikuja mmoja wao na kunipokonya begi langu kubwa kisha akaliweka mbele
katika uskani wa bodaboda. Sikufurahishwa jinsi begi langu lilipochukuliwa pasipo ridhaa
yangu. “Twenzetu dogo acha kushangaa, huoni time ishaenda”. Alisema dereva bodaboda uku
akinisogelea akiwa kashika helment mkononi na kunipa nivae. Sikua na jinsi ilibidi nipande
maana nilitaka niwahi kufika ili nichati na Farida. Tukiwa tupo njiani kuelekea gesti, mama
alinipigia simu nikamjulisha kua ndio naelekea gesti kuchukua chumba nilale hadi kesho yake.
Tuliagana baada ya mazungumzo machache.

Baada ya kuelewana bei tulianza safari kuelekea Victoria gest house ambayo ilikua mbali
kidogo kutoka stendi. Baada ya kufika fasta nilifanya mchakato wa chumba na nilifanikiwa
kupata, maana vyumba kadhaa vilikua vitupu. Niliweka vizuri vitu vyangu kisha bila kuchelewa
nikamtext Farida kumjulisha kua nipo katika gest aliyoniambia. Nilisubiri kwa muda bila kujibiwa
nikaamua kuiacha simu kitandani nikaenda kuoga. Kile chumba kilikua na choo mule mule hivyo
nilivua nguo nikabaki na boksa nikaingia kuoga. Nilijipaka sabuni kichwani na kufungua kok
taratibu maji yalianza kutiririka kichwani kwangu na kusababisha sabuni niliyopaka kuanza
kutapakaa mwili mzima.

Hapo ndipo matukio yote niliyopitia nikiwa safarini yalianza kupita kichwani mwangu moja
baada ya jingine. Nikakumbuka jinsi nilivyohamishiwa katika siti iliyokua pembeni ya siti ya
Farida hadi kuzoeana nae. Nilicheka kidogo baada ya kukumbuka jinsi nilivyoachwa na basi pale
Morogoro mjini. “Mmh! Peter acha uzembe”. Nilijiambia mwenyewe huku nikijifuta maji usoni
ili kufumbua macho. Nilitabasamu baada ya kukumbuka jinsi nilivyokua nikimshika mikono
Farida mezani wakati tukisubiri kuletewa chakula na muhudumu pale stendi ya Dodoma.
Nilikumbuka pia jinsi tulivyo kumbatiana wakati nikitoka nje ya stendi baada ya kushuka katika
basi. “Uuuhuuuu! Nilivuta pumzi ndefu na kuachia kwa nguvu uku maji yakiendelea kumiminika
kichwani kwangu.

“Oooooh! Kumbe sabuni imeisha kichwani”. Nilijisemea uku nikinyoosha mkono kuchukua
sabuni na kujipaka tena. Wakati sabuni ikiendelea kutapakaa usoni na sehemu zingine nilisikia
simu yangu ikiita pale kitandani. “Atakua Farida huyo, babe beibeee”. Nilijikuta nikisema kwa
sauti nikiwa na furaha hatari, fasta nikatoka mbio na mapovu yangu kwenda kupokea simu.
Sikua nikiona vizuri kutokana na mapovu kuniingia machoni hivyo nilienda mbio nikiwa
nimefumba macho. Nilipofika sehemu nilipoiweka nikaanza kupapasa mara ghafla nikaisukuma
ikadondoka chini pwaaaa!. “Duuuh! Mambo gani haya sasa”. Nilijisemea wakati nikiinama
kuichukua ikiwa bado inaita.

“Hallo Queen, mambo”. Nilipokea fasta na kuanza kuongea nikiwa na tabasamu kinoma
yani. “Mmmh! Pumbavu wewe. Mimi Queen wako eeeh?”. Niliisikia sauti ya upande wa pili
ikijibu na kufanya nishtuke, nilifikicha na kujaribu kufumbua macho kwa tabu kutizama ni nani
aliyepiga japo sauti ilikua kama ni ya mama. “We Peter mbona huongei”. Aliongea tena wakati
nikiwa bado sijaona vizuri katika kioo cha simu. “Aaah! Shikamoo mama”. Baada ya kujua ni
mama nilimjibu uku nikijikuna kichwa nakung’ata meno yangu nikijilaumu. “Vipi umepata
chumba uko ulikoenda?”. Aliniuliza mama, nikashukuru ile mada ya kumuita Queen imeisha.
“Ndio, nishapata na nipo chumbani sasa hivi”. Nilimjibu huku nikijichekesha chekesha. “Haya,
naona upon na Queen wako sasa hivi” Aliirudisha ile mada tena. “Hamna mama nimepitiwa tu”,
nilijitetea hadi alipoamua kukata simu akionyesha kukereka sana.

Baada ya kukata simu niliona meseji kama mbili hivi za Farida. Ya mwanzo alikua akijibu
meseji yangu niliyomtumia. “Ok upo room ngapi nije nikucheki mara moja coz kwetu ni nyumba
ya pili nyuma ya hiyo gesti”. Baada ya kuisoma hiyo meseji moyo ulilipuka paaah!. Nikaendelea
kusoma meseji nyingine aliyotuma akisema, “P nishafika nipo hapa nje ya gesti, toka basi my”.
Hapo sasa ndo ilikua balaa mtu wangu. Fasta nikatoa taulo kwenye begi nikajifuta yale mapovu,
nikaenda chooni kunawa uso kisha nikarudi kuvaa nguo. Wakati nikivaa nguo meseji nyingine
ikaingia katika simu ikisema “Basi mimi narudi home maana nimekupigia nikajibiwa kua simu
yako inatumika, utanishtua kesho nikusindikize. Usiku mwema”. Wee niliona muda unaenda
kuandika meseji, chap nikafunga mkanda wangu wa suruali na kuchomoka mbio bila ata
kufunga mlango ili kumuwahi Farida.

ITAENDELEA..................

SIMULIZI: SITOSAHAU - SEHEMU YA 08


MWANDISHI: SHAABAN HIJA

SIMU: 0786 056307

Wakati nikivaa nguo meseji nyingine ikaingia katika simu ikisema “Basi mimi narudi home
maana nimekupigia nikajibiwa kua simu yako inatumika, utanishtua kesho nikusindikize. Usiku
mwema”. Wee niliona muda unaenda kuandika meseji, chap nikafunga mkanda wangu wa
suruali na kuchomoka mbio bila ata kufunga mlango ili kumuwahi Farida.

Nilipita kwenye korido spidi kubwa kuelekea mlangoni, ile naukaribia mlango tu ghafla mtu
aliekua nje akausukuma mlango ili kuingia ndani. Aisee mlango ulinipiga kwenye paji lauso hadi
nikaona marue rue. Nikaegemea ukutani kusikilizia maumivu nikiwa nimejikamata katika paji la
uso. Nikamuona jamaa akiingia akiwa kalewa katoka kunywa bia katika baa iliyokuwepo hapo
hapo gesti. Akaanza kufoka hovyo akiwa kasimama pale katikati ya mlango. “Nani huyo anazuia
mlango nisiingie? Nani huyo nauliza? shuwainii”. Aliongea kwa sauti yake ya kilevi huku akiwa
kasimama akiyumbayumba pale mlangoni nachupa yake ya bia mkononi. “Daaah! Boya huyu,
kaniumiza kishenzi bado anazingua tu”. Nilijisemea nikiwa bado nimesimama pembeni kusubiri
apite ili na mimi nitoke.

“Wewe ni nani hadi uzuie mlango, pumbavu wewe! Hivi unanijua vizuri mimi………”. Aliendelea
kuongea akiwa bado kasimama mlangoni akinitazama. Nilitamani kumzingua lakini nilikua
mwoga hatari kupigwa ata hivyo nilikua sitaki kuendelea kupoteza muda tena. Nilipopata
upenyo nikapita mbio nikamuacha yule jamaa akiendelea kutukana pale mlangoni. Nilienda
moja kwamoja hadi kwenye geti la kutokea nikafungua fasta nikiamini nitamkuta Farida. Aisee
ata sikumuona, walikuwepo tu madereva bodaboda waliokua pale nje. Wakaanza mambo yao
tena wakinigombania wakijua nataka usafiri. “Oya mimi siendi popote bhana”. Niliwajibu ndipo
waliponipotezea.

Nikaenda mbio kuchungulia katika chochoro ya upande wa kulia ata sikuona mtu, nikaenda
chochoro ya kushoto pia sikumuona. Niliita jina lake mara kadhaa kwanguvu lakini ata
sikuitikiwa. Haraka nikatoa simu yangu ili kumpigia, nikabonyeza sehemu ya kupiga baada ya
kuipata namba yake kisha nikaweka sikioni. “Samahani hauna salio la kupiga simu hii,
tafadhali...………” Ata sikusubiri nikaikata simu nikiwa na hasira. “Dah! Kweli nimekumbuka,
nilikua sina salio”. Kudadadeki yule mlevi kanichelewesha kishenzi yaani”.

Nilijisemea huku nikirudi ndani taratibu nikiwa nimejishika usoni sehemu niliyoumia. Niliingia
chumbani nakujitupa kitandani sikutamani ata kwenda kuoga tena. Sikua na usingizi sababu ya
kumuwaza sana Farida, niliamini kua lazima atakua amekasirika sana jinsi alivyokuja na
kushindwa kuonana na mimi. Baada ya kuwaza sana nilipata usingizi, niliota nipo na Farida mule
chumbani. Alikua kajifunga kanga kifuani kakaa kitandani akijikata kucha za mikononi, wakati
huo mimi nilikua nakunja nguo zangu.

Alipo maliza kukata kucha za mikononi aliupandisha mguu wake mmoja wa kulia kitandani
nakuanza kukata kucha za mguuni. Lahaula! Nilistaajabu nilipotupia jicho nakuona mapaja yake
meupe baada ya ile kanga kuachana pale kati. Nikajikuta naacha kukunja nguo na kumsogelea.
Nilifika na kukaa karibu yake kisha nikaupeleka mkono wangu wa kulia mapajani kwake,
nilipeleka kwa woga nikiamini labda Farida hatopenda. Niliyapapasa mapaja yake kwa muda
akiwa bado katulia tu bila kunizuia. Ata sikuchelewa, fasta nikamsukuma akadondoka chali pale
kitandani nakubaki akiwa mtupu baada ya kanga aliyokua kajifunga kufunguka.

Aisee ilikua noma sana, chuchu zilikua simesimama balaa. Nikapeleka ulimi wangu nakuanza
kuzichezea chuchu zake uku mkono wangu ukishuka chini kuelekea maeneo. Nilimchezea kwa
muda nikiwa na papara kibao nikiamini kua bahati haiji mara mbili. Haraka nikavua suruali
nikairusha pembeni kisha nikamlalia tena kwajuu. Mara ghafla nikashtuka kutoka ndotoni
nakujikuta nipo pekeangu pale kitandani baada ya kuamshwa na mlio wa simu. Daaah!
Nililaumu sana, kwanini aliyepiga hakusubiri ndoto yangu iishe ndio apige. “Watu wengine
bhana basi tu, amenikatisha uhondo hivi hivi”. Nilijisemea huku nikipeleka mkono kuichukua
simu ili kupokea. “Kumbe Farida, weweee”. Nilijikuta nikisema kwa sauti baada ya kusoma jina
lake katika kioo cha simu.

Nikanyanyuka nikakaa kisha nikakohoa kidogo kuweka sauti vizuri ndio nikapokea simu. Si
unajua tena sauti nikishawishi moja wapo kati ya mambo yanayo mvutia mtu kimapenzi. Hivyo
nilihakikisha namvutia kwakila namna. “Halloo! Love, mambo”. Niliongea baada ya kupokea.
“Poa tu, vipi bado umelala”. Aliitikia nakuniuliza, kabla sijamjibu niligeuka nakutizama dirishani.
Jua lilikua limeisha chomoza namwanga ulikua mkali. Mwanzo sikuweza kutambua maana
nililala bila kuzima taa. “Hapana nimeamka kitambo kidogo ila nilienda msalani ndio maana
nimechelewa kupokea simu”. Nilimjibu huku nikitoa simu sikioni nakuangalia muda kisha
nikaenda mwayo. Kumbe ilikua ni saa tatu na nusu asubuhi. “Ok, umekunywa chai?”. Aliniuliza
Farida nadhani alisikia nilipoenda mwayo. “Bado ndo nataka nitoke nikaangalie chochote hapo
nje”.

Nilimjibu nikiwa kweli nahisi njaa. “Basi subiri humo humo chumbani, taingia hapo gesti
kwandani tachukua supu na chapati kisha nikuletee”. Aliniambia Farida nakufanya mapigo ya
moyo wangu kuanza kwenda mbio kwa hofu. Kiukweli sikua nikijiamini sana maana nilikua
sijawahi kua katika mahusiano ya kimapenzi hivyo sikua nahali ya kujiamini sana. “Sasa mbona
hunijibu Peter?”. Nilishtuka baada ya kusikia akiniuliza, mawazo yangu yalikua katika ile ndoto
niliyoota. “Kumbe sijamjibu”. Nilijisemea huku nikiwa bado sijajua nimjibu nini. “Sa.. sawa, nipo
room 14 ukifika utaingia tu mlango utakua wazi”. Nilimjibu huku nikijikuna kichwa japo sikua
ata nikiwashwa. “Poa, basi baadae mi ndo natoka ata sikawii takua nishafika” Alinijibu kisha
akakata simu baada ya kuagana.

ITAENDELEA..................

SIMULIZI: SITOSAHAU- SEHEMU YA 09

MWANDISHI: SHAABAN HIJA

SIMU: 0786 0563 07

“Sa … sawa, nipo room 14 ukifika utaingia tu mlango utakua wazi”. Nilimjibu huku nikijikuna
kichwa japo sikua ata nikiwashwa. “Poa, basi baaade mi ndo natoka ata sikawii takua nishafika”.
Alinijibu akakata simu baada ya kuagana.

Nilibaki nikiwa kama nimezubaa hivi pale kitandani nikiwa siamini kile kinachoenda kutokea
muda mfupi ujao. “Hivi ni kweli Farida anakuja humu chumbani? mmmh hii itakua ndoto bado
naota mimi”. Niliendelea kuwaza pale kitandani huku nikijipiga makofi shavuni ili kama naota
basi niamke. “Sasa akishafika sijui itakuaje jamani”. Niliendelea kuwaza hadi nilipoamua
kunyanyuka kitandani nakuanza kutembea mule chumbani huku na kule kwa hofu. Kwa jinsi
nilivyokua naogapa nilihisi kutetemeka mwili mzima. Mara mlio wa simu yangu ukasikika pale
kitandani, ilikua imeanza kuita muda kidogo ila sikuisikia kabisa kutokana na kuwaza sana ujio
wa Farida.

“Duuh! Sasa hivi tu Farida ameishafika? eheee leo kasheshe”. Nilijikuta nikiongea kwa sauti uku
nikiwa na hofu kuifata simu ili kupokea. Taratibu nilipiga hatua nakuifata simu pale kitandani.
“Uuu….huuu! Afadhali, kume ni bibi”. Nilijisemea huku nikivuta na kushusha pumzi kisha
nikapokea haraka. “Bibi shikamoo”. Nilisalimia mara tu baada ya kuipokea. “Unazingua
mwanangu aaah, mimi bibi yako vipi dogo?”. Alizungumza Tito mtoto wa mama mdogo hali
iliyonifanya niangue kicheko balaa. “Aaah, umezidi kukaa sana na simu ya bibi dogo hadi
mmeanza kufanana sauti”. Nilimtania, ikabidi acheke tu kwa sababu hua tunataniana sana
maana kwa umri tupo sawa.

“Ehee nambie dogo, muda gani utakua ushatimba kitaa ili nisogee stendi kukupokea?”.
Aliniuliza baada ya kupeana salam, nilipata kigugumizi kidogo kumjibu maana sikujua Farida
atakapo kuja atachukua mda gani hadi kuondoka. “Sikiliza mwamba, kwani gari ya mwisho
kuondoka hapa town kuja huko ni saa ngapi maana kunavitu tapita dukani kununua”. Niliamua
kumdanganya asijue kinachoniweka Tabora mjini maana sipo kwa ndugu. “ Ahaa, gari ya
mwisho ni saa tisa ambayo huku inafika saa kumi namoja na nusu”. Alinijibu kisha tukaagana
baada ya kukubaliana kua saa kumi na moja na nusu anipokee huko takua nishafika.

Haraka nikaenda kufungua mlango kwakutoa loki ili akifika Farida asukume tu kisha nikaingia
chooni ili kupiga mswaki na kuoga. “Sijui nipige paspoti saizi tu”. Niliwaza niishie kunawa tu
baada ya kumaliza kupiga mswaki maana kulikua na baridi sio poa, lakini baadae niliamua
kuoga. “Ayaa!” Nilishindwa kujizuia nikajikuta nimeongea kwa sauti huku nikiibana mikono
yangu katikati ya mapaja kwa sababu ya baridi kali. Maji yalikua ya baridi sana nazani hali ya
hewa pia ilichangia ya Tabora kwa mwezi huo. “We Peter huko chooni vipi? Kelele zote hizo
unaogopa maji ya baridi au?”.

Hee nilishtuka kusikia hivyo, ilikua ni sauti ya Farida akiwa yupo chumbani. “Mmmh! Kafika mda
gani huyu?”. Nilijiuliza huku nikiwa nimepigwa na butwaa mule chooni. “Hapana siogopi bhana,
nimekumbuka tu kua nimesahau kuchukua taulo”. Nilimjibu kisha nikajiziba mdomoni kwa
mkono wangu wa kulia huku nikitoa macho kusubiri atanijibu nini. “Ok nimeliona nakuletea”.
Wee asikuambie mtu, nilishtuka kusikia kauli hiyo. “Ha… ha… hapana, usijali takuja kujifuta tu
huko huko”. Nilimjibu huku nikiuegemea mlango wa chooni maana nilihisi kua anaweza akaja.

Kiukweli nilikua nampenda sana Farida na si kwamba sikupenda yeye kuja chooni kuniletea
taulo. La hasha, nilitamani sana lakini tatizo nikwamba nilikua namuonea haya sana. Sikuwahi
kua katika mahusiano hivyo nilistahili kabisa kua katika hali hiyo maana wengi tu hupitia hiyo
hali si wanamke wala si wanaume. “Mh! Haya”. Alinijibu kisha nikaendelea kuoga hadi
nilipomaliza na kutoka. Nilimkuta kakaa kitandani akichezea simu yake, nilichukua taulo
nakuanza kujifuta. “Vipi ukopoa?”. Nilimsalimia huku nikimtizama usoni pasipo yeye kujua. “She
is so beautiful jamani”. Niliwaza huku nikiinama kufungua zipu ya begi na kutoa nguo za kuvaa.

“Poa tu”. Alinijibu nakuniachia tabasamu usoni. Tulipiga stori nyingi sana hadi akaniambia kua
anamjomba wake uko Ipole na akipata nafasi ataenda. Ni sehemu ambayo ndiyo ninayoenda,
aisee nilipata furaha sana. Wakati tukiendelea kupiga stori alilala chali pale kitandani huku
akichezea simu yake. “Peter unaikumbuka hii gemu?”. Aliniuliza Farida. “Gemu gani?”.
Nilimuuliza huku nikilala kiubavu ili kuangalia. Alikua akicheza ile gemu ya gari tuliokua
tukicheza ndani ya basi tulipokua safarini. Duuh! Ikabidi nilale chali na mimi ili nione vizuri
anavyocheza, kwahyo tukawa sote tumelala chali huku tukiwa tumekaribiana kabisa.

Wakati akiendelea kucheza gemu, nilianza kutupia macho ya wizi katika kifua chake pamoja na
sehemu zingine. Oooh! Nilishtuka kidogo baada ya kuona mapaja yake meupe yaliyo onekana
kutokana na sketi aliyokua kavaa kuvutika kwaju. Taratibu nilianza kupata matamanio
nakusababisha mjeshi wangu ndani kupiga saluti mara kadhaa. Ilikua nishida kiukweli, hadi
nikaamua kuweka mkono juu ya zipu ya suruali ili asije akanishtukia Farida.

Niliendelea kukaa kwa tabu pale bila ata kufatilia anavyocheza gemu. “Ngoja nijaribu kuweka
mkono kifuani kwake, nione kama atazingua”. Nilijishauli na kuamua kunyanyua mkono liwalo
na liwe. Hee ile kunyenyua mkono tu Farida si akauona, akaupiga mkono wangu huko. “Ehee
nimeumbuka chalii yangu”. Nilijisemea moyoni nakuanza kukata tamaa kabisa. Nikajua kua
kumbe hata hanipendi, nikatulia kimyaa. “Aa leo sitaki unielekeze, nataka nicheze mwenyewe”.
Aliniambia Farida huku akigeuka kunipa mgongo nakuelekea upande mwingine. “Dogo mpuuzi
huyu, yaani alijua napeleka mkono ili kumuelekeza”. Niliwaza kwafuraha kisha nikamwambia
“Poa ukishinda nakupa zawadi”.

Nililala kwa ubavu kama alivyokua amelala yeye hivyo nikawa nimembana kwa mgongoni.
Nilijidai kama nachungulia kuona anavyocheza gemu kumbe nipo mbali kihisia. Mara kadhaa
nilinyanyua mkono wangu ili kumshika lakini nilikua nikishusha kutokana na kushindwa
kujiamini. “Mimi boya kweli yani, hivi naogopa nini?”. Nilijiuliza huku nikijilaumu lakini kila
nikitaka kumshika narudisha mkono. “Weweeee nimeshindaaaa”. Aligeuka Farida huku
akishangilia na kunikumbatia kwanguvu.

“Ehee kama nilikusikia ukisema kua nikishinda unanipa zawadi, si ndio Peter?”. Nilibaki kimya
kidogo maana niliropoka tu pasipo kujua tampa zawadi gani kama atashinda. “Mbona hunijibu,
nataka zawadi yangu”. Aliniambia Farida huku akinitikisa na nyuso zetu zikiwa zimekaribiana
kabisa tukitazamana. “Nimwambie zawadi gani sasa?”. Niliendelea kuwaza kisha nikamwambia
afumbe macho japo bado sikujua nampa nini. Ata hakubisha, akafumba macho huku akisubiri
nini nitampa. Wakati nikiendelea kuitizama sura yake kwa uhuru zaidi haraka nikapata wazo.
“Ehee yes, ngoja nijaribu nione itakuaje”. Nilijisemea huku nikivuta pumzi kisha…….

SIMULIZI: SITOSAHAU - SEHEMU YA 10

MWANDISHI: SHAABAN HIJA

SIMU: 0786 056307

“Nimwambie zawadi gani sasa?”. Niliendelea kuwaza kisha nikamwambia afumbe macho
japo bado sikujua nampa nini. Ata hakubisha, akafumba macho huku akisubiri nini nitampa.
Wakati nikiendelea kuitizama sura yake kwa uhuru zaidi haraka nikapata wazo. “Ehee yes, ngoja
nijaribu nione itakuaje”. Nilijisemea huku nikivuta pumzi kisha nikanyanyuka nikakaa vizuri.
Mara nikamuona mtu kapita kama mshale mule chumbani. Aisee nilichanganyikiwa si kidogo na
ilikua ngumu kuamini kile nilichokiona. “Hivi nimeona mtu au maruerue tu, na kama ni mtu
kaingilia wapi na katokea wapi?”. Nilibaki nikijiuliza huku Farida akiwa bado kafumba macho
yake akisubiria zawadi. Haraka nikapeleka mikono yangu machoni kufikicha nilifikilia huenda
machoni kuna vumbi iliyosababisha nione hivyo. Wakati nikiendelea kufikicha macho nikahisi
kuguswa begani kama mara mbili hivi kama ishara ya mtu kunitaka nigeuke. “Peter bado tu
jamani”. Alizungumza Farida aliyekua bado kafumba macho yake, yaani ata sikumjibu haraka
nikageuka kuangalia ni nini kilichonigusa begani lakini cha ajabu sikuona kitu.

Wakati nikirudisha kichwa hivi nikamuona paka mweusi akinitazama kisha akaanza
kutembea haraka kuelekea chooni. Alipoukaribia tu mlango wa chooni akapotea, haikujulikana
ata kaelekea wapi. “Mungu wangu, ni nini hiki”. Nilijisemea huku nikinyanyuka pale kitandani
na kuanza kuangalia huku na kule. Wakati nikiendelea kushangaa ile miujiza uzalendo
ulimshinda Farida akaamua kufumbua macho. “Nishafumbua sasa, muda wote nakuuliza hata
hunijibu”. Aliniambia Farida huku akionesha kukasirika. Kiukweli nilishindwa kuzungumza,
nilibaki nikimtazama tu. Nilikua kama bubu, kila nilipojaribu kuzungumza nilishindwa. Niliamua
kunyoosha kidole upande wa chooni ili kumfahamisha kua kuna kitu kimeingia humo.Jamani
nilipata tabu kumuelewesha, Farida alikua hata haelewi nilichokimaanisha. “Nini sasa, kwahiyo
hiyo zawadi ndio ipo huko chooni?”. Aliniuliza akiwa tayari ameshasimama na kuanza kunisogea
nilipokua nimesimama. “Hebu ongea basi, kwani hunisikii”. Alizungumza kwa sauti kubwa huku
mkono mmoja akiwa kajishika kiunoni. Nilimuwekea kidole mdomoni kumnyamazisha aache
makelele yake maana nilikua naogopa hata kuongea kwa sauti ya chini. “Si ipo huko chooni?.
Basi naifata wee kaa kimya tu hivyo hivyo”. Alizungumza nakuanza kupiga hatua kuelekea
chooni kule nilikomuona paka wa ajabu.

Haraka nikamvuta mkono kisha nikamwambia kwa sauti ya chinii tena ya uwoga “Farida
kuna kitu humu ndani hebu tulia”. Hee ilikua bado kiza kinene kwa Farida, hakuelewa kabisa.
“Hebu niachie kwanza. Kituu kituu, si unipe sasa lakini kama hutaki basi”. Aliniambia Farida
huku akiuvuta mkono wake na kunisukuma kwa nguvu hadi nikadondoka chini. Nilibaki
nimetulia pale chini nikimtazama Farida aliyekua ananikodolea macho kwa hasira. Farida alikua
kasimama kaupa mgongo mlango wa chooni, mara ghafla nikamuona mtu kasimama nyuma
yake kajifunika shuka jeusi akinitazama huku akitabasamu. “Farida mtu huyo nyuma yakoo”.
Ilinitoka tena kwa sauti kubwa huku nikipeleka mikono haraka sana usoni kujiziba nisimuone.
“We Peter mbona sikuelewi, hebu acha utani bhana”. Nilimsikia Farida akizungumza huku
akinisukuma kichwani. “Angalia nyuma yako, mtuuuuu”. Niliongea tena nikiwa bado nimeinama
kujiziba uso nisimuone. “Mbona hakuna kitu, hahahahaa ushaanza mambo yako ya kupiga
makelele kama ya kwenye basi ile jana”. Alizungumza Farida huku akicheka na kunifanya
ninyanyue kichwa ili kuhakikisha kama kweli hakuna mtu.

Baada ya kufumbua macho yangu ambayo nilijiziba kwa mikono sikumuona tena yule mtu,
haraka nikanyanyuka na kumvuta mkono Farida ili tutoke nje. Nikamvuta mkono kisha
nikafungua mlango tukatoka kisha nikaubana kwa nje. “Mh! Hivi kweli umemuona mtu humo
chumbani?. Aliniuliza huku akionesha kushangazwa sana na hali niliyokua nayo ya wasiwasi.
“Sio mtu tu, pia nimemuona paka mweusi kaenda chooni huko”. Nilimjibu tena kwa msisitizo
kumaanisha ninachokiongea sio masihara ata kidogo. Dogo mjinga yule, alicheka hadi akaa chini
na kufanya watu waliokua wanapita katika korido hiyo kutushangaa. “Ndo umetoa macho hivyo
kwa woga, dah! Peter we umezidi bhana….”. Alizungumza kwa tabu maana alikua anacheka sio
poa pale chini. Nilibaki kutazama tu pasipo kufanya chochote mara jamaa mmoja aliyekua
akifanya usafi karibu na tulipokua tumesimama akaja tulipo simama. “Oya vipi kuna usalama
kweli maana nimewasikia kama mnasema kua kuna kitu mmekiona sijui ni chumbani?”. Jamaa
alituuliza huku Farida akinyanyuka pale chini na kujizuia kucheka kwa kuweka mkono mdomoni
huku akinitazama. “Bro, nimeona mtu na paka humo chumbani ila kila nikimuambia huyu
haniamini”.

Nilimwambia yule jamaa hali iliyofanya Farida kuangua tena kicheko kwa mara nyingine
tena. “Hakuna chochote mbona mimi sijaona, huyu mwoga tu”. Alizungumza Farida na
kunifanya nikasirike lakini nilijizuia nisiioneshe hiyo hali kwake. “Huenda kweli kaona, hebu
fungueni tukaangalie”. Alizungumza yule jamaa lakini nilikataa kwenda ndani nikamwacha
aende yeye mwenyewe. Baada ya kuingia mule chumbani aliangalia sehemu zote lakini
hakuona kitu kisha akatoka. “Mh! Mbona hakuna kitu chochote”. Alizungumza huku
akitabasamu, alionesha dhahiri kua anataka kunicheka lakini alijikaza tu. “Chooni pia
umeenda?”. Nilimuuliza huku nikimkazia macho usoni. “Ndio, kote hadi uvunguni”. Alinijibu
huku akicheka kidogo hali iliyonifanya nibaki nimeduwaa pale mlangoni. “Si nilikuambia hakuna
chochote, Peter labda unaumwa malaria”. Alizungumza Farida huku akiniangalia kwa jicho la
huruma, alikua hacheki tena. “Yaa inabidi ukacheki, huenda unamalaria bro”. Aliniambia yule
jamaa na kuanza kuondoka huku akicheka. Nilibaki kimya kwa muda nikitafakari ushauri wao
wa kwenda hospitali. Nilitikisa kichwa kukataa maana niliamini nilichokiona ni kweli wala sio
ugonjwa. “Toka lini mimi naumwa malaria, na itakuaje inianze ghafla hivi. Hapana mimi siumwi
bhana”. Yalikua ni mawazo niliyokuwa nikiwaza pale nje pembeni ya mlangoni.

“Hiyo sio hali ya kawaida Peter, bora twende hospital ukapime. Malaria itakua ipo juu
sana”. Aliniambia kisha nikatikisa kichwa kukataa. “Twende tuwahi, sio mbali ni mtaa wa mbele
hapo”. Kabla ata sijaamua chochote, mara nikaisikia simu yangu ikiita pale kitandani. Wee nani
aende, nilibaki nikiisikiliza tu huku nikiwa nimeinamisha kichwa changu. “Kachukue simu yako
inaita”. Aliniambia Farida huku akinikazia macho nazani alimaanisha kua nilivyoviona mule
chumbani sio vitu vya kweli hivyo sina haja ya kuendelea kuogopa. Nikaufungua mlango
kuchungulia chumbani kisha nikafunga haraka. Nilihisi kama kuna kitu kinakuja spidi mlangoni.
Aisee ilikua shida sana kwangu, Farida kuona hivyo akaingia chumbani na kuniletea simu. Ilikua
inaelekea kukata, haraka nikaipokea baada ya kusoma katika kioo na kuona kua ni mama ndiye
aliyenipigia. “Hallo mama, shikamoo”. Niliongea kwa sauti ya kutetemeka kidogo. “Marhabaa,
za uko mwanangu?”. Alizungumza mama upande wa pili. Nilibaki kimya kidogo pasipo kuongea
chochote, niliwaza nimjibu nini. Nimjibu ni salama au si salama. Ilikua ni vigumu kumjibu maana
bado sikua na uhakika wa kutosha takua naumwa malaria au nilichokiona kweli ni sahihi.

“We Peter si nakuuliza, mbona hunijibu?”.

Alizungumza mama na kunigutusha kwenye dimbwi la mawazo. “Ah sa.. salama tu”.
Nilimjibu huku nikimtazama usoni Farida aliyekua pembeni yangu akisikiliza. “Haya, vipi
umeishafika uko Ipole”. Aliniuliza tena mama lakini kabla sijamjibu nilimuona tena yule mtu
niliyemuona chumbani kapita kwa mbele shwaaa, kisha akapotea. Nilibaki nimeyatoa macho
kwa kupigwa na bumbu wazi, niliiachia simu ikadondoka chini pwaaa. “Peter vipi, kuna nini?”.
Aliniuliza Farida huku akiinama kuiokota simu ambapo betri na mfuniko vyote vilitawanyika.
Nilijishika kichwani kisha nikashusha mikono na kuanza kuangaza huku na kule. “Vipi kichwa
kinakuuma? Nimekuambia twende hospitali lakini bado tu umesimama tu hapo”. Alizungumza
Farida pasipo ata kujua kama nimemuona tena yule mtu niliye muhuhadithia. Yeye alivyo ona
nimeshika kichwa aliamini kua kichwa kinaniuma. Daah! Ilibidi nikubali kwenda hospitali ili
kupata uhakika ni kweli naumwa au ni kweli macho yangu hayanidanganyi.
SIMULIZI: SITOSAHAU - SEHEMU YA 11

MWANDISHI: SHAABAN HIJA

SIMU: 0786 056307

“Vipi kichwa kinakuuma? Nimekuambia twende hospitali lakini bado tu umesimama tu


hapo”. Alizungumza Farida pasipo ata kujua kama nimemuona tena yule mtu niliye
muhuhadithia. Yeye alivyo ona nimeshika kichwa aliamini kua kichwa kinaniuma. Daah! Ilibidi
nikubali kwenda hospitali ili kupata uhakika ni kweli naumwa au ni kweli macho yangu
hayanidanganyi. “Sawa itabidi twende”. Nilimwambia Farida huku nikitabasamu ingali sikua ata
nafuraha ata kidogo. “Kachukue viatu basi twende”. Aliniambia Farida nakuniacha njia panda,
ilikua ni vigumu kuamua kua niende chumbani au nimtume akanichukulie yeye. Kiukweli nilikua
naogopa kwenda humo chumbani lakini pia nilikua naogopa kubaki pale pekeangu. Baada ya
kuwaza sana niliamua kumtuma afate mimi nimsubiri pale. “Kanichukulie wewe, kachukue na
pesa katika mfuko mdogo wa begi lile kubwa”. Nilimwambia huku nikiegemea ukutani huku
nikiwa na hofu kiasi. “ Mh! Haya sawa naona bado unaogopa tu”. Aliniambia kisha akafungua
mlango kuingia chumbani na kuniacha pale nje mlangoni.

Wakati nikiendelea kumsubiri pale mlangoni mara nikahisi kuguswa mgongoni.


“Mamaaaa”. Nilipiga kelele huku nikikimbia bila kuangalia nyuma, nikafungua mlango mkubwa
kisha nikatoka nduki tena. Nilipofika sehemu ya baa nilipiga mieleka kama miwili hivi ya adabu.
Wakati nataka kunyanyuka niendelee kukimbia nikasikia sauti ya mwanamke “Wee kaka vipi,
mbona unanikimbia”. Ikabidi nigeuke huku watu kadhaa waliokuwepo pale wakinishangaa
nawengine wakicheka, ilikua ni aibu balaa maana lile picha lilikua si lakitoto. Kumbe alikua
mdada wa usafi kashika mop akinitazama pale mlangoni. Ikabidi nirudi mdogo mdogo nikiwa na
aibu za kutosha. “Kaka vipi mbona nilivyokugusa tu ili usogee nideki ukakimbia?”. Aliniuliza
huku akicheka cheka baada ya mimi kufika pale nikijikung’uta kung’uta vumbi. “Aah hamna
kitu”. Nilimjibu huku nikiingiza mikono katika mifuko ya suruali nakuanza kurudi hadi kwenye
mlango wa chumba nilipokua nimesimama nikimsubiri Farida. “Samahani kaka, wewe ndio wa
chumba hiki?”. Aliniuliza yule mdada baada ya kuja na kusimama pembeni yangu. “Yaa ni
mimi”. Nilimjibu huku nikiinamisha kichwa maana nilikua na aibu kidogo. “Nataka kufanya usafi,
vipi naweza nikaingia?”. Aliniuliza na baada ya kumkubalia aliingia kufanya usafi. Niliendelea
kumsubiri Farida hadi nikachoka ikabidi nifungue mlango kidogo kisha nikachungulia
kumuambia yule mdada amwambie Farida awahi. “Mbona hamna mtu humu”. Alinijibu hali
iliyonifanya nishangae sana, hayupo vipi wakati kaingia kaniacha pale nje. “Atakua yupo chooni,
mgongee”. Nilimwambia huku nikiamini kua lazima atakua kaenda chooni maana bila hivyo
angekua ameisha toka zamani. “Huku chooni hakuna mtu”. Alinijibu yule mdada wa usafi
nakunifanya nishangae sana ikabidi nimwite kwa nguvu maana sikuamini anachoniambia yule
mdada. “Faridaaaa”. Niliita lakini ata sikuitikiwa ikabidi nijikaze, nikaingia ili kuhakikisha.
Aisee sikumuona kabisa, niliangalia kila sehemu. Chooni, uvunguni hadi nikatoa shuka zote
lakini ata sikumuona. Nilichanganyikiwa si kidogo, nilimtafuta hadi kwenye mifuko ya suruali.
Nilifungua hadi mabegi yangu lakini ilikua kazi bure. “Farida njoo basi, hebu twende
tunachelewa”. Niliongea kwa sauti kubwa ili popote alipo anisikie huku machozi yakinitoka.
Niliamua kukaa chini huku woga wote ukiwa tayari umeniisha, kiukweli nilikua tayari kwa lolote
litakalo tokea.

“Kwani kaka unauhakika kua huyo Farida aliingia humu?”. Aliniuliza yule mdada huku akisogea
taratibu pale nilipokua nimekaa. Hayo maswali yake nikama yalinizidishia maumivu niliyokua
nayo, nikaamua kukaa kimya tu nakuanza kuwaza Farida atakua wapi. Taratibu nikaanza
kuamini kua ata siumwi malaria, vitu vyote nilivyoviona vya ajabu vilikua ni vya kweli hivyo
niligundua kua nipo sehem ya hatari. Haraka nikakusanya vitu vyangu nakutoka navyo ili
kuelekea stendi kwenda kijijini kwa bibi. Ata sikukumbuka kwenda kukabidhisha funguo pale
kaunta, nikatoka nje nakumwacha yule dada akiendelea nausafi mule chumbani.

Baada ya kutoka nje nilipokelewa na madereva bodaboda waliokua wakinigombania wakitaka


kunipeleka ninakoenda. “Oya wapi nikupeleke? (dereva wa 1), Panda twenzetu mwanangu
(dereva wa 2), twenzetu takufanyia bei ya kishkaji (dereva wa 3) …... Zilikua ni sauti za
madereva wa bodaboda ambazo zilizidi kunichanganya tu, haraka nikapanda katika bodaboda
iliyopo karibu yangu kisha nikamwambia anipeleke stendi ya mkoa. Wakati tunatoka pale gest
kwenda stendi ilikua imetimia saa saba kama na robo hivi. Tulifika nikashushwa pale kwa nje
kisha nikamlipa nakuanza kuingia mule ndani.

“Ni jana tu nilikua nimesimama hapa na Farida tukiagana”. Nilizungumza kwa sauti ya huzuni
baada ya kufika sehemu tuliyokua tumesimama jana yake usiku tukiagana tulipo shuka kwenye
basi. Kiukweli niliamini kabisa kua Farida kachukulia na yule mtu niliyemuona mule chumbani
wala sikua na sababu ya kutokuamini hivyo. Nilitembea taratibu kiunyonge sana kuelekea
sehemu ambayo kulikua na mabasi madogo (costa) na kukutana na lundo la wapiga debe
waliokuja na kunizonga kila mmoja akitaka kunikatia tiketi.

Baada ya kusumbuana nao sana nilifanikiwa kukata tiketi na kupanda katika basi (costa)
iendayo Ipole. Niliingia na mizigo yangu yato na kukaa katika siti ya nyuma kabisa maana siti za
mbele zilikua zimeisha jaa abiria kisha nikamtumia meseji Tito kua nishapanda gari. Nilitulia
zangu kimya huku nikiwa namawozo tele maana ata sikujua tumeondoka muda gani pale
stendi, nilikuja kushtuka tumefika Pangale sehemu ambayo basi lilisimama katika geti na
kukaguliwa kisha tukaendelea na safari. Wakati safari ikiendelea ghafla nikamuona Farida kaka
siti kule mbele akinitazama. “Mh! Farida kafikaje huku?”. Wakati nikiendelea kuwaza nilimuona
akigeuka tena kunitazama kisha akatabasamu na baadae akageukia mbele.

Haraka nikanyanyuka kumfata nikiamini ni Farida, nilipita kwa shida kidogo hadi nilipomfikia
maana kulikua na mabegi pamoja na abiria waliokua wamesimama katika njia ya kati.
Nikanyoosha mkono kumgusa mgongoni nikiwa natabasam tele usoni. Mh! Si akageuka bhana
kuniangalia, aisee nilipigwa na butwaa sana. Kumbe hakua Farida, nilimfananisha tu. “Naam
nakusikiliza, unasemaje?”. Aliniambia yule dada baada ya kuona namtazama tu ata siongei
chochote nikiwa nimejiziba mdomoni kwa kiganja cha mkono. “Samahani dada,
nimekufananisha”. Niliongea huku nikianza kuondoka pale kurudi nyuma tena.

Kiukweli nilihisi dalili za kuanza kuchanganyikiwa kabisa na nilipofika katika siti yangu nilikuta
tayari mtu mwingine ameisha kaa “Dah! Ujinga gani huu, lakini poa tasimama tu”. Nilijisemea
huku nikinyoosha mkono kukamata bomba la juu. Mara simu yangu ikaita, alikua ni mama
akinipigia. Niliikata kisha nikamtumia meseji kua nipo kwenye basi naenda Ipole. Sikutaka
kupokea maana kulikua na kelele hivyo tusinge elewana vizuri. Safari iliendelea hadi tulipofika
Ipole sehemu ambayo basi hilo lilikua likiishia hapo. Nilichukua mabegi yangu na kushuka,
nilimkuta Tito mlangoni akinisubiri nadhani alikua nashauku sana ya kuniona. Alinipokea begi
moja kubwa kisha tukaanza kutembea kuelekea nyumbani.

Tito alikua anaongea sana njia nzima kiasi kwamba nilichoka kumsikiliza, mawazo nyangu yote
yalikua kwa Farida binti ambaye nimepotezana nae katika mazingira ya kutatanisha. “Oya Peter
vipi mbona kama haupo poa hivi?”. Aliniuliza Tito tukiwa tunakaribia kufika nyumbani kwa bibi.
“Daah! Ni balaa ndugu yangu, nikitulia takuhadithia yaliyonikuta”. Nilimjibu huku tukipishana
na madada wawili hivi waliomsimamisha Tito na kuanza kuongea. Mmoja wao alinisalimia
“Peter mambo?”. Hee nilishtuka kidogo, “huyu demu kanijuaje”. Nilijiseme huku nikimuangalia
kwa kumkazia macho kama taweza kumkumbuka. Wakati nataka kumjibu mara simu yangu
ikaita.

Nilibaki kukodoa macho tu baada ya kuona jina la Farida. “He!”. Nilijikuta nikishangaa tena kwa
sauti na kubaki nikijiuliza kua nipokee au niache.

ITAENDELEA……………………………………….

USIKOSE KUFUATILIA SIMULIZI HII

Asante 🙏 sana kwa upendo 💞 na ukarimu wenu. Naombeni mashabiki wangu mnaopenda
simulizi hii ya SITOSAHAU inayo andikwa na mm mwandishi wenu Diaspora Tz mchango wako
wa elfu 1000/= kupata muendelezo wa simulizi hii kwanzia sehemu ya kwanza hadi sehemu ya
kumi kwa njia ya SMS (Message) au kwa njia ya WhatsApp. Ukiwa upo tayari nitext au nipigie
katika namba hii 0786 056307

Amani ikae pamoja nanyi mashabiki wangu na sito acha kuwaletea simulizi kali ambazo
zinaburudisha, kuelimisha na kusisimua. 🤗

Kwanza niombe🤲 radhi kwa kutoipost simulizi kwa kipindi kirefu ila hii ilitokana na sababu zilizo
njee ya uwezo wangu but tusonge pamoja sasa.

You might also like