You are on page 1of 5

BARAKA NA UTOSHELEVU WA KI-MUNGU (ABUNDANCE)

Zaburi 86:5

Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu
wote wakuitao.

(NLT)
O Lord, you are so good, so ready to forgive, so full of unfailing love for all who ask for your help

AMP
For You, O Lord, are good, and ready to forgive [our sins, sending them away, completely letting them go
forever and ever]; and abundant in lovingkindness and overflowing in mercy to all those who call upon
you

NIV
You, Lord, are forgiving and good, abounding in love to all who call to you.

Mithali 21:5

Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji.

AMP
The plans of the diligent lead surely to abundance and advantage, But everyone who acts in
haste comes surely to poverty.
NIV
The plans of the diligent lead to profit as surely as haste leads to poverty.
NLT
Good planning and hard work lead to prosperity, but hasty shortcuts lead to poverty.

Mithali 28:19

Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa
kumtosha.

AMP
He who cultivates his land will have plenty of bread, But he who follows worthless people and
frivolous pursuits will have plenty of poverty.
NIV
Those who work their land will have abundant food, but those who chase fantasies will have
their fill of poverty.
NLT
A hard worker has plenty of food, but a person who chases fantasies ends up in poverty.

Isaya 8:8
naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hata shingoni; na kule
kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.

AMP
“Then it will sweep on into Judah; it will overflow and pass through [the hills], Reaching even
to the neck [of which Jerusalem is the head], And its outstretched wings (the armies of Assyria)
will fill the width of Your land, O Immanuel.
NLT
and sweep into Judah until it is chin deep. It will spread its wings, submerging your land from
one end to the other, O Immanuel.
NIV
and sweep on into Judah, swirling over it, passing through it and reaching up to the neck. Its
outspread wings will cover the breadth of your land, Immanuel!”

Isaya 11:9

Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua
BWANA, kama vile maji yanavyoifunika bahari.

AMP
They will not hurt or destroy in all my holy mountain, for the earth will be full of the knowledge
of the Lord As the waters cover the sea.
NIV
They will neither harm nor destroy on all my holy mountain, for the earth will be filled with the
knowledge of the Lord as the waters cover the sea.
NLT
Nothing will hurt or destroy in all my holy mountain, for as the waters fill the sea, so the earth
will be filled with people who know the Lord.

Isaya 30:23

Naye atatoa mvua juu ya mbegu zako, upate kuipanda nchi hii; na mkate wa mazao ya nchi, nayo
itasitawi na kuzaa tele; katika siku hiyo ng’ombe zako watakula katika malisho mapana.

Mambo ya Walawi 26:5

Tena kupura nafaka kwenu kutaendelea hata wakati wa kuvuna zabibu, na kuvuna zabibu kutaendelea
hata wakati wa kupanda mbegu; nanyi mtakula chakula chenu na kushiba, na kuketi katika nchi yenu
salama.

Kumbukumbu la Torati 30:9

Na BWANA, Mungu wako, atakufanya uwe na wingi wa uheri katika kazi yote ya mkono wako, katika
uzao wa tumbo lako, na katika uzao wa ng’ombe wako, na katika uzao wa nchi yako; kwa kuwa BWANA
atafurahi tena juu yako kwa wema, kama alivyofurahi juu ya baba zako;
Zaburi 16:11

Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna
mema ya milele.

Yeremia 2:7

Nami nikawatia katika nchi ya shibe, mpate kula matunda yake na mema yake; lakini ninyi mlipoingia
katika nchi ile, mliitia unajisi nchi yangu, na urithi wangu mliufanya kuwa chukizo.

Yeremia 33:6

Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli.

Amosi 9:13

Angalieni, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo huyo alimaye atamfikilia avunaye, na yeye akanyagaye
zabibu atamfikilia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka.

Mathayo 6:34

Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

Mathayo 12:34-35

Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena
yaujazayo moyo wake.

Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.

Mathayo 13:12

Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile
alicho nacho atanyang’anywa.

Luka 6:38
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata
kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho
mtakachopimiwa.

Yohana 10:10

Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Warumi 5:20

Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;

Isaya 58:11

Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu
mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake
hayapungui.

Warumi 5:8

Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu,
tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Warumi 10:12

Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri
kwa wote wamwitao;

Mathayo 6:33

Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Warumi 15:13

Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa
na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.

Yeremia 29:11
Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya,
kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Warumi 12:2

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika
mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

You might also like