Professional Documents
Culture Documents
Kuku Ni Dhahabu
Kuku Ni Dhahabu
1. UCHUMI
Uchumi ni namna (maarifa) ya mtu kutumia rasilimali zilizopo kwa madhumuni ya kutimiza
mahitaji na matakwa yake kwa njia nafuu /bora zaidi.
T6
Mahitaji
Matakwa
1
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
2
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
For the purpose of spending and saving money wisely, every person must know the difference
between needs and wants.
B. MATAKWA: ni yale mambo yote yanapokosekana hayakwamishi maisha ya
mwanadumu kuendelea.
2. MAENDELEO.
Maendeleo ni hali ya mtu kutoka katika kiwango cha maisha duni na kupiga hatua
kuishi katika kiwango cha maisha bora zaidi.
SWALI:
1. Kwa mtazamo wako umeelewa nini kuhusu uchumi?
2. Kwa mtazamo wako umeelewa nini kuhusu Maendeleo?
3
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
2 Wakorintho 9:8-13
Mwanzo 1:24-31
2 wakorintho 9:8-13 hapa kuna maswali matatu muhimu sana ya kujiuliza
1. Kwa nini hatuna Neema hizi kwa wingi.
2. Kwa nini hatuna Riziki za kila namna sikuzote
3. Kwa nini hatuzidi sana katika kila tendo jema
Tuangalie suala la “Mkiwa na Riziki za kila namna siku zote”
Mahitaji ya lazima kwa mwanadamu yanatazamwa kwa namna mbili kuu
1. Ki-dunia ( kama inavyoelezwa hapo juu kwenyemchoro wa pembe tatu)
2. Ki-biblia ( kama inavyoelezwa kwenye 1 Timotheo 6:8)
Tunapataje Riziki
Kuna namna nyingi za halali na zisizo za halali za mtu kujipatia Riziki. Mungu amempa
mwanadamu rasilimali nyingi tena za kutosha ili zimsaidie kujipatia riziki kwa njia za halali tu.
Mwanadamu anaweza kupata riziki ya kila namna kutoka katika vyanzo vilivyotajwa hapa
chini ingawa ni baadhi tu vyanzo hivyo:-
1. Kilimo
2. Ufugaji
3. Viwandani
4. Uchimbaji madini
5. Uvuvi
6. biashara
Muda haututoshi kuzitazama zote. Muda huu kutazama namna mojawapo ya njia ya
kujipatia Riziki ambayo ni:-
1. Njia ya asili ambayo ilibuniwa na Mungu mwenyewe
Mwanzo 1:24
Biblia inatoa ushahidi wa kutosha ya kwamba katika UFUGAJI mtu aliyesoma na asiyesoma
wote wanaweza kuwa na maisha yanayofanana yaani ya kuwa na Riziki za kila namna siku
zote kama Mungu alivyopanga hata kabla ya mwanadamu kuwepo
Mithali 27:23
Kufanya bidi kuijua hali ya makundi yako
Hapa Mungu anamaanisha kuwa kazi ya ufugaji inahitahi usimamizi
madhubuti/makini/tumaanishe/usimamizi bora/imara kama ilivyo katika usimamiaji wa
shughuli zingine kama za miradi ya kijamiin n.k.
4
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
Sababu ya kufanya bidii ya kujua hali ya makundi yako ni mali huwa si ya milele
Kwa kuwa mpango huu ni mwema sana kwa Mungu, wakati mwingine mwanadamu
anakosea kama ilivyokuwa kwa wakati wa Nuhu, utaona kuwa mwanadamu muovu
aliangamizwa cha ajabu kila aliyepata Neema machoni pa Mungu alipewa nafasi ya
kuendelea kufuga mwanzo 9:10
Familia za wakirsto waishio kwenye umasikini zimeonesha bidii kubwa katika kuombea
hali ya uchumi wa familia zao, maombi ambayo kwa sehemu kubwa yamekosa tija kwa
kuwa familia hizi hazijawa tayari kutawala mazingira, wakati Fulani maombi yao yanadai
uchumi huu utoke mbinguni aliko Mungu, jambo ambalo si sawa. Kwani katika siku 5 wa
kwanza za uumbaji zilifanya mambo mengi pamoja na uchumi wa mwanadamu.
Tunahitaji akili tu kutambua na kuchukua hatua.
Kuishi bila hawa wanyama ni kuishi nje ya mpango na kusudi la Mungu. Tangu
mwanzo Mungu alikusudia mahali popote atakapokuwa mwandamu aishi akiwa
amezungukwa na wanyama. Ukiwakataa au kuwafukuza usidhani watakwenda porini,
watapotelea mtaani.
5
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
Ni muhimu kuwajengea kuku banda bora ili wapate kujikinga na mvua, baridi, wezi
na wanyama. Banda la kuku linaweza likajengwa kando kando au nyuma ya nyumba
ya kuishi. Banda la kuku linaweza kujengwa kwa kutumia raslimali za misitu
zinazopatikana kwa urahisi kwenye eneo husika.
N.B. Jua ni muhimu katika kuhakikisha vitamini A na D zinatumika vizuri
mwilini, kwahiyo banda ni lazima lijengwe kwa mtindo ambao
unaruhusu mwanga kupita hasa nyakati za asubuhi na jioni.
6
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
v. Maji.
Mwili wa Ndege/Kuku umebeba 70% ya maji na yai lake lina 65%. Kuku
anahitaji maji ya kutosha kwa muda wote. Kuku anahitaji maji safi na salama
ili yamwezeshe kumeng’enya chakula, kuondoa taka mwilini na kurekebisha
hali ya joto mwilini. Ukosefu na upungufu maji kwa kuku huchangia kwa kiasi
kikubwa kudumaa na kuathilika vibaya mfuko wake wa chakula hatimaye
hufa.
7
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
8
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
9
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
Typhoid.
Kuzuia Kideri.
Kuhara.
Mafua.
Vidonda.
Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba)
Ndui.
Kuhara damu (Coccidiosis)
10
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
v. MLONGE
Ina vitamini A na C. Chukua majani ujazo wa mikono miwili (gao mbili). Kisha yapondeponde na
kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12-16, chuja na wape kuku. Isiyotumika
mwaga na tengeneza nyingine.
Mlonge hutibu :
Mafua.
Kideri – inyweshwe kabla kwa kukinga
Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).
Homa ya matumbo
Ini.
vi. NDULELE.
Majani hutibu Minyoo.
Matunda hutibu Vidonda
.
vii. MAJANI YA MPAPAI
Chemsha magao mawili ndani ya maji lita 6 hadi ubakie na lita 1. Poza kisha chuja.
Hutibu: Minyoo
Kuandaa Pata jani moja bichi la Mpapai na uliponde ponde lilainike kiasi. Kisha changanya na
maji kiasi cha lita mbili na nusu.
Kutumia (kwa tiba) – Kuku wapewe maji hayo wanywe, wasipewe maji mengine kwa ajili ya
kunywa kwa siku angalau nne au zaidi.
– Inafaa zaidi kila siku kuwaandalia dawa mpya ili dawa isiharibike.
Kutumia (kama kinga) – Hata kama kuku hawaharishi, wakizoeshwa kunywa maji yenye majani
ya mpapai yaliyopondwa angalau mara tatu kwa wiki watakingwa magonjwa mengi.
Kuandaa na Kutumia – Chukua majani ya Mpapai uyatwange upate kisamvu chake kiasi cha lita
1.
– Waweza kuongezea maji kidogo na kuwapatia kuku wanaoumwa watumie chakula hicho hadi
wapone.
11
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
Kama kuku ni wachache, andaa chakula wanachoweza kumaliza kwa siku moja ili kisibakie na
kuharibika kabla hawajakimaliza.
Mwembe hutibu:
Homa ya matumbo.
Mafua.
Kinga ya Kideri/Mdondo.
x. KITUNGUU SWAUMU:
Jinsi ya kutumia Unakitwanga kisha uchanganye kwenye maji chuja kwa chujio ili kuondoa nyuzi
na uchafu.
Kiwango cha kuwapa kitategemeana na idadi ya kuku. Huu ni ushuhuda wa mfugaji aliewahi
kutumia kitunguu swaumu kwa kuku wake
TEKNOLOGIA
5. Faida za kuku
a) Ufugaji hauhitaji mtaji mkubwa kuuanzisha.
b) Ni rahisi kuusimamia.
c) Faida inapatikana mapema.
12
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
13
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
Pesa ni kitu chenye nguvu sana , kama mtu hana pesa anaweza kudhalilika n ahata kupoteza
UTU wake
Mf :-
1. wanawake walioajiliwa kwenye bandi za mziki
2. kufanya Ngono na Mbwa
3. Kufanya ngono ya jinsia moja kwa lengo la kupata ufadhili wa masomo
4. vyombo vya habari vya hapa nchi viliwahi kuripo matukio ya kutweza UTU wa
WATU chuo kikuu kimoja wanafunzi wake waanza kufanya rekodinging za
ngono na kusambaza kwenye mitandao na tovuti
suala la kuwa uchi wa mnyama pekee liliwashinda ADAMU na EVA baada ya
kukosa/kuasi kiasi kwamba walihangaika kushona majani majani kama nguo
14
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
zao ili tu kutunza UTU wao. Je, kufanya ngono na kusambaza dunia nzima
kwa video na picha kisa unasaka tonge/pesa.
5. Migogoro ya familia za wakristo MAHALI FLANI (KIGOMA) baraza la wazee
tukakutana ili kugawana majukum
6.
Namna hii inawashushia heshima, wanadhalilika, kwa sababu hawana ULINZI/USALAMA
Unayeniskia mahali hapa au mahali pengene kamwe usijaribu kufanya hayo wakati wowote
kwenye maisha yako ama kwa kuisifu kwa sababu ya PESA
UMASIKINI ni nini?
Ni ukosefu au upungufu wa rasilimali vitu au Pesa.
Katika dunia hii MATAJIRI ndio huweka mipango na MASIKINI ndio huikamilisha mipango hiyo.
Mtu akitaka kutawaliwa basi akose fedha.
Mf:-
1. Delila na Samson
Delila alikuwa mwanamke mzuri kwa sura na kwa umbo, Delila
hakuwa mwanamke mbaya. Ubaya wa Delila unajitokeza kwenye
umaskini wa Nyumbani kwao, kama si Pesa asingemsalti Samsoni
mpenzi wake ambaye naye alikuwa mwenye mvuto mkubwa kwa sura
na umbo.
Wafiliti walikuwa tayari kufadhili masomo yake na kuwasaidia wazazi
wake kama tu angewasaidia kujua asili ya nguvu za SAMSONI
2. YESU alipokuwa kwenye chakula cha usiku na wanafunzi wake
aliwaambia mmoja wenu atanisaliti
Wote walikana Je, ni mimi bwana ! mimi kweli! Kamwe
haitawezekana hata Yuda Mwanzoni alikana.
Lakini pamoja na shetani lakini pesa ndiyo ilimuua Yesu baada ya
Yuda kushirikishwa na wakuu wa makuhani, baada ya usaliti huu
aliujutia na kuchukua hatua za yeye kujiua
Kuna watu wanatenda mabaya si kwa kupenda, wengine wapo hapa
ni wanandoa kwa sababu ya umasikini wanasalti ndoa zao.
3. Wakuuu wa makuhani wale wale waliotoa pesa kwa Yuda amsaliti
Yesu hao hao walitoa pesa tena kuufuta ukweli wa tukio la kufufuka
kwa Yesu. MATHAYO 28:11-15
4. Shetani anatumia fedha katika kuwalaghai na kuwaaminisha watu
kuwa fedha ni mali yake LUKA 4: 5-7 Jambo ambalo si kweli.
15
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
BARAKA ZA BWANA
Mungu anazo Baraka kwa ajili ya watu wake,Baraka hizi si vitu vinavyoshikika
MITHALI 10:22 Baraka za Bwana hutajirisha wala hachanganyi huzuni nayo
Kubarikiwa na Bwana haina maana ya moja kwa moja kwamba una MALI na wala si lazima
uipime kwa kuwa na PESA
Lakini Baraka ya Bwana ina uwezo wa kufanya/kuwezesha kuwa
tajiri
Baraka ya Bwana ni kama nyenzo inayokuwezesha wewe kuwa
tajiri
Unaweza kuwa umeberikiwa na Bwana lakina maisha yako
yakaendelea kuwa ya umaskini.
Leo tuzungumie kidogo kuhusu UKUBWA WA ENEO ambalo Baraka za Bwana zinachukua
Baraka za Bwana zinaweza kuenea kwa umbali gani yaani zinachukua eneo kubwa kiasi gani
KUMBU 28:1-8 hapa tunaona utajiri wa Baraka za Bwana, unaziona kwa urefu wake upana na
kimo chake vizuri.
1. Eneo la Kwanza:
Baraka za Bwana zimeenea maeneo ya mjini na vijijini hii inamaana kuwa hazina mipaka.
Katika mazingira halisi yanaweza kuonesha kasoro Fulani Fulani hasa katika maeneo ya
vijijini ila katika mpango wa Mungu hakuna eneo lisilokuwa na Baraka za Bwana.
16
KUKU NI DHAHABU-EV PETER KILEZU
Kwenye UCHUMI wa Mungu hakuna eneo hata moja lisilokuwa na Baraka za Mungu.
Kama ni Africa au Ulaya Baraka za Bwana zi kila mahali kwa utimilifu.
2. Eneo la Pili:
Baraka za Bwana zimeenea kwenye UZAO wote wanaotoka kwenye viuno/tumbo lako
lakini pia hata wale unaoishi nao wanauhusiano na wewe kwa namna moja au nyingine.
Aina hii ya Baraka ni ya vizazi vyote, Baraka ya ajabu maana inawagusa hata wale
wasiokuwa kwenye agano moja na wewe
Mf: ibrahimu ni mtu aliyebarikiwa na Bwana lakini Luthu mpwae hakuwa kwenye
agano lakini alibarikiwa kwa sababu ya Baraka ya mjomba wake Ibrahimu.
3. Eneo la Tatu:
Baraka zimeenea kwenye maeneo ya uzalishaji kwenye vitu tunavyolima na kuzalisha
4. Eneo la Nne:
Baraka za Bwana zimeenea kwenye safari zote za ndani ya nchi, nje ya nchi, ukiamua
kubaki hapa nchini utabarikiwa ukisafiri kwenda nje ya nchi utabariki kwa sababu Eneo
halitazuia Baraka za bwana. 2 SAMWEL 8:14, 2 SAMWEL 19:2
Mf: Yusufu alibarikiwa alipokuwa nyumbani kwa babaye, alipoenda kwa potifa,
gerezani n ahata ikulu alibarikiwa.
Ukiwa na usafiri wako utabarikiwa.
5. Eneo la Tano:
Baraka za Bwana zimeenea kwenye eneo la VITA chochote kitakachokuja kinyume chako
Baraka hii itakiondoa. Masha ya mtu yamezungukwa na vita kama huna vita basi, wewe
si kiumbe hai. Vita kama magonjwa n.k yatakuja juu yako yakiwa yamejipanga
yataondolewa mbele yako bila utaratibu. Mungu anapigana kwa ajili yako. 2 NYAKATI
23:6
6. Eneo la Sita:
Kwenye eneo la STOO YA CHAKULA CHA NYUMBANI KWAKO Hautakusanya na
usivitumiwe mwenyewe wala havitapeperushwa. Ukivuna au Benki na uwekezaji Baraka
za bwana zitafika huko.
Hii ni package kubwa sana ya Baraka za Bwana hii inatosheleza maeneo yote ya maisha
ya mtu
Chini ya Baraka za Bwana umebarikiwa popote utakapokuwa
17