You are on page 1of 1

HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA

SHULE YA SEKONDARI LUPA


S.L.P 36,
CHUNYA
8/9/2022
MWL . FARAJI KATENGA
SHULE YA SEKONDARI LUPA
S.L.P 36
CHUNYA
YAH; UTORO MUDA WA KAZI
Mada tajwa hapo juu yahusika na;
Umekuwa mtoro muda wa kazi, kwa karibu wiki mbili sasa, muda wa kazi unakuwa kunywa Pombe
vilabuni na kila siku asubuhi unakuwa na harufu ya pombe nimekuonya juu ya tabia yako hii mbaya
kwa mtumishi kama wewe lakini bado hutaki kubadilika.
1.Tarehe 29/08/2022 siku ambayo tulifungua shule rasmi kama walimu kwa ajili ya maandalizi ya
mhula wa pili 2022 hukuwepo
2.Tarehe 05/9/2022 ulifika shuleni na kusaini tu lakini hukuwepo kazini
3.Tarehe 07/09/2022 nilikuonya juu ya tabia yako ya ulevi muda wa kazi
4.Tarehe 08/09/2022 leo umefika asubuhi na kusaini kisha kutoweka.
Tabia yako unayoifanya ina;
1.Aibisha kada ya ualimu mitaani kwani muda wote unaonekana mitaani
2. Unaiibia serikali muda na fedha kama mtumishi wa umma kwani unalipwa mshahara pasipo
kutekeleza wajibu wako
3. Unajishushia hadhi kama mtumishi wa umma kuwa mitaani muda wa kazi
4. Ni aibu kwa mtumishi mzoefu unawafundisha nini watumishi vijana
Kwa barua hii nataka ufanye yafuatayo.
Fika ukiwa ofisini kwangu tarehe 9/9/2022 saa 2.00 asubuhi ukiwa na
(a) Barua ya maelezo kwanini usiadhibiwe.
(b) Scheme of work’, Andalio la somo. Bank of questions na Mark list za vidato unavyofundisha.

……………………………………………………
Kilasi, E. A
Nakala
Afisa elimu (W) ( kwa taarifa)
Chunya
Afisa elimu kata (Kwa Taarifa)
Kata ya Lupa

You might also like