KUCHAPA

You might also like

You are on page 1of 6

HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA

SHULE YA SEKONDARI
LUPA
S.L.P 36,
CHUNYA
22/01/2023
KUMB: NA: LSS/CDC/NIDHAMU/2023/01

MWL. ANNETH MWAMAKULA

SHULE YA SEKONDARI LUPA

S.L.P. 36,

CHUNYA

YAH; MAELEZO JUU YA KWA NINI MWANAFUNZI BENSON CHARLES RONGWE KIDATO CHA SITA
HGL KUADHIBIWA PASIPO KUFUATA TARATIBU ZA UTOAJI ADHABU KISHERIA

Tafadhari husika na mada tajwa hapo juu, nataka nipate maelezo ya kina kutoka kwako juu ya tukio
la kuadhibiwa kwa mwanafunzi Benson Charles Rongwe.

Aidha kwa kuwa ulishuhudia na ulikuwepo katika tukio hilo, wakati mwanafunzi huyu akipewa
adhabu hiyo ya viboko na Mwalimu Joram Umbuli, kwa nini hukuzuia tukio hilo lisifanyike?

Wewe kama Mwalimu unafahamu sheria, kanuni na taratibu za utoaji wa adhabu kwa wanafunzi wa
kiume na wanafunzi wa kike (wanafunzi wa kiume kuchapwa katika makalio viboko visivyo zidi vitatu
na wanafunzi wa kike viboko visivyozidi vitatu na Mwalimu wa kike ndiye anayemwadhibu
mwanafunzi wa kike) na mwanafunzi anaye pewa adhabu akili kosa kwa kusaini katika daftari la
makosa (Reward and Punishment book). Adhabu kwa wanafunzi na ruhusa/idhini ya kumchapa
viboko ni lazima itolewe na mkuu wa shule.

Hivyo kwa barua hii nakutaka utoe maelezo kwa kina ya kwa nini hilo halikufanyika ? na badala yake
mwanafunzi huyu aliadhibiwa kwa kuchapwa viboko vinne katika mwili wake na si katika makalio
yake. Na ukiri kuwa utafuata na utasimamia kama Mwalimu taratibu zote za utoaji adhabu kwa
wanafunzi.

Nataka unipe maelezo haya ndani ya siku moja.

Nakutakia maelezo mema.

……………………………………………..

Erasto A. Kilasi

Mkuu wa shule
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA

SHULE YA SEKONDARI
LUPA
S.L.P 36,
CHUNYA
22/01/2023
KUMB: NA: LSS/CDC/NIDHAMU/2023/02

MWL. GODLOVE KIHINDO

SHULE YA SEKONDARI LUPA

S.L.P 36,

CHUNYA

YAH; MAELEZO JUU YA KWANINI MWANAFUNZI BENSON CHARLES RONGWE KIDATO CHA SITA
HGL KUADHIBIWA PASIPO KUFUATA TARATIBU ZA UTOAJI ADHABU KISHERIA

Tafadhari husika na mada tajwa hapo juu, nataka nipate maelezo ya kina kutoka kwako juu ya tukio
la kuadhibiwa kwa mwanafunzi Benson Charles Rongwe.

Aidha kwa kuwa ulishuhudia na ulikuwepo katika tukio hilo, wakati mwanafunzi huyu akipewa
adhabu hiyo ya viboko na Mwalimu Joram Umbuli, kwa nini hukuzuia tukio hilo lisifanyike?

Wewe kama Mwalimu unafahamu sheria, kanuni na taratibu za utoaji wa adhabu kwa wanafunzi wa
kiume na wanafunzi wa kike (wanafunzi wa kiume kuchapwa katika makalio viboko visivyo zidi vitatu
na wanafunzi wa kike viboko visivyozidi vitatu na Mwalimu wa kike ndiye anayemwadhibu
mwanafunzi wa kike) na mwanafunzi anaye pewa adhabu akili kosa kwa kusaini katika daftari la
makosa (Reward and Punishment book). Adhabu kwa wanafunzi na ruhusa/idhini ya kumchapa
viboko ni lazima itolewe na mkuu wa shule.

Hivyo kwa barua hii nakutaka utoe maelezo ya kina ya kwa nini hilo halikufanyika ? na badala yake
mwanafunzi huyu aliadhibiwa kwa kuchapwa viboko vinne katika mwili wake na si katika makalio
yake. Na ukiri kuwa suala kama hilo halitajirudia tena kwa siku za usoni

Nataka unipe maelezo haya ndani ya siku moja.

Nakutakia maelezo mema.

……………………………………………..

Erasto A. Kilasi
Mkuu wa shule

HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA

SHULE YA SEKONDARI
LUPA
S.L.P 36,
CHUNYA
22/01/2023
KUMB: NA: LSS/CDC/NIDHAMU/2023/03

MWL. JORAMU UMBULI

SHULE YA SEKONDARI LUPA

S.L.P 36,

CHUNYA

YAH; MAELEZO JUU YA KWA NINI MWANAFUNZI BENSON CHARLES RONGWE KIDATO CHA SITA
HGL KUADHIBIWA PASIPO KUFUATA TARATIBU ZA UTOAJI ADHABU KISHERIA

Tafadhari husika na mada tajwa hapo juu, nataka nipate maelezo ya kina kutoka kwako juu ya tukio
la kuadhibiwa kwa mwanafunzi Benson Charles Rongwe.

Wewe kama Mwalimu unafahamu sheria, kanuni na taratibu za utoaji wa adhabu kwa wanafunzi wa
kiume na wanafunzi wa kike (wanafunzi wa kiume kuchapwa katika makalio viboko visivyo zidi vitatu
na wanafunzi wa kike viboko visivyozidi vitatu na Mwalimu wa kike ndiye anayemwadhibu
mwanafunzi wa kike) na mwanafunzi anaye pewa adhabu akili kosa kwa kusaini katika daftari la
makosa (Reward and Punishment book).

Aidha adhabu kwa wanafunzi na ruhusa/idhini ya kumchapa viboko ni lazima itolewe na mkuu wa
shule.

Hivyo kwa barua hii nakutaka utoe maelezo ya kina ya kwa nini hilo halikufanyika ? na badala yake
ulimwadhibu mwanafunzi huyu kwa kumchapwa viboko vinne katika mwili wake na si katika makalio
yake. Ulivunja sheria, Kanuni na taratibu za utoaji adhabu kwa wanafunzi

Nataka unipe maelezo haya ndani ya siku moja.

Nakutakia maelezo mema.

……………………………………………..

Erasto A. Kilasi

Mkuu wa shule
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA

SHULE YA SEKONDARI
LUPA

S.L.P 36,

CHUNYA

21/01/2023

LSS/CDC/ADM/2023/01

MWL. JORAMU UMBULI

SHULE YA SEKONDARI LUPA

S.L.P 36,

CHUNYA

YAH; ONYO LA KUMPIGA MWANAFUNZI BENSON CHARLES RONGWE KIDATO CHA SITA HGL-
2022/2023

Husika na mada tajwa hapo juu, Rejea barua yako ya kukiri juu ya kumpiga mwanafunzi mtajwa
hapo juu yenye kumb. Na. LSS/CDC/NIDHAMU/2023/03/01 ya tarehe 22/01/2023, kwa mamlaka
niliyopewa na msaidizi wa R.A.S- Mkoa (Afisa elimu Mkoa) Nakuonya kwa kitendo cha kukiuka
taratibu za utoaji wa adhabu kwa wanafunzi, kwa kumchapa mgongoni na kumsababishia maumivu
mwanafunzi Benson Charles Rongwe kidato cha sita (HGL) Rejea mwenendo wa makosa ya
kinidhamu kwa Mwalimu kanuni ya 13 (1) (2)(4)

Mimi kama msimamizi wako wa kazi katika kituo hiki ninayo mamlaka ya kukupa onyo juu ya
mwenendo wako wa makosa uliyofanya na kukupa adhabu juu ya kosa ulilolitenda, kwa kitendo cha
kutoa adhabu ya viboko kwa mwanafunzi kinyume na maagizo ya wizara ya elimu na mafunzo ya
ufundi juu ya utoaji wa adhabu hiyo kwa mwanafunzi.

Aidha idhini/ruhusa ya utoaji wa adhabu ya viboko kwa mwanafunzi inatolewa na mkuu wa shule
kwa maandishi (mwanafunzi wa kiume kupigwa katika makalio na mwanafunzi wa kike anapigwa
katika viganja vya mikono na anayemwadhibu ni Mwalimu wa kike baada ya mwanafunzi huyu kukiri
kosa lake kwa maaandishi na anaadhibiwa viboko vitatu tu) wewe hukuzingatia hilo, hivyo ulifanya
kinyume na maagizo ya wizara juu ya utoaji adhabu kwa mwanafunzi

Kwa barua hii nakupa onyo la utoaji wa adhabu za Viboko kiholela pasipo kuzingatia Sheria, Kanuni
na Taratibu za utoaji adhabu kwa wanafunzi na ninakutaka uache mara moja tabia hiyo.

Aidha kutozingatia hilo mimi kama mkuu wako wa kituo cha kazi nitafanya moja wapo ya yafuatayo

1. Kukusimamishia daraja la mshahara/cheo,

2. Kukusimamishia nyongeza ya mishahara yako
3. Kukupunguzia mshahara kuanzia asilimia 20 hadi 50.

Nakutakia utekelezaji mwema wa miongozo ya utoaji wa adhamu kwa wanafunzi

…………………………………..

Erasto A. Kilasi

Mkuu wa shule

NAKALA

AFISA ELIMU (W)

IDARA YA SEKONDARI

S.L.P 73,

CHUNYA

AFISA ELIMU (K)

KATA YA LUPA

S.L.P 66,

CHUNYA
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA

SHULE YA SEKONDARI
LUPA

S.L.P 36,

CHUNYA

21/01/2023

LSS/CDC/ADM/2023/01

MWL. JORAMU UMBULI

SHULE YA SEKONDARI LUPA

S.L.P 36,

CHUNYA

YAH: KUSITISHA UTEUZI WAKO KUWA MWALIMU MWANDAMIZI NIDHAMU

Husika na mada tajwa hapo juu, Rejea barua yako ya kukiri juu ya kumpiga mwanafunzi mtajwa
hapo juu yenye kumb. Na. LSS/CDC/NIDHAMU/2023/03/01

Mimi kama msimamizi wako wa kazi katika kituo hiki, nasitisha rasmi uteuzi wako wa kuwa
Mwalimu mwandamizi wa nidhamu katika shule hii, kumbuka kuwa. Adhabu ya viboko kwa
mwanafunzi hutolewa baada ya mkuu wa shule kutoa idhini/ruhusa ya utoaji wa adhabu hiyo kwa
maandishi na mwanafunzi wa kiume kupigwa katika makalio na mwanafunzi wa kike anapigwa
katika viganja vya mikono na anayemwadhibu ni Mwalimu wa kike baada ya mwanafunzi huyu kukiri
kosa lake kwa maaandishi na anaadhibiwa viboko vitatu tu) wewe hukuzingatia hilo, hivyo ulifanya
kinyume na maagizo ya wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi juu ya utoaji adhabu kwa mwanafunzi

Nakutakia kazi njema ya ualimu yenye kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za kiutumishi katika kada
hii ya Ualimu

…………………………………..

Erasto A. Kilasi

Mkuu wa shule

You might also like