Professional Documents
Culture Documents
02/05/2022
Ndugu wanahabari, nimewaita leo hapa, kwa ajili ya kutoa taarifa mbili
za ukamataji wa wahalifu.
TUKIO LA KWANZA.
Mnamo tarehe 12/04/2022 majira ya saa 10:00 hrs hapa Uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jengo la abiria namba tatu eneo
la kuondokea abiria sehemu ya ukaguzi wa mizigo alikamatwa abiria
mmoja Raia wa CHINA, DONG WEIJUN, mwenye umri wa miaka 44,
aliyekuwa akisafiri kwa ndege ya QATAR mruko namba QR 1499 majira
ya saa 10:00 hrs kwenda BANGKOK, THAILAND akiwa na vidani 10
na bangili moja vilivyo tengenezwa kwa meno ya tembo vyenye uzito wa
gram 110, pia alikutwa na bangili nyingine moja iliyotengenezwa kwa
manyoya ya mkia wa tembo (singa) vyote vikiwa na thamani ya tembo
mzima.
Mtuhumiwa tayari amefikishwa Mahakamani kwa hatua za kisheria.
TUKIO LA PILI,
Mnamo tarehe 29/04/2022 majira ya saa 20:30 hrs hapa uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal three eneo la ukaguzi wa
mizigo ya abiria wanaosafiri kwenda nje ya Nchi alikamatwa abiria
mmoja Raia wa India mwenye umri wa miaka 23, akiwa na madawa ya
kulevya aina ya HEROIN yenye uzito wa Kg 17.40
Jeshi la polisi Viwanja vya ndege Tanzania linatoa onyo kali kwa watu
wote wanaojihusisha na kusafirisha madawa ya kulevya na nyara za
Serikali kwani watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Polisi Viwanja vya Ndege kwa kushirikiana na vyombo vya vingine vya
ulinzi na usalama vimejipanga vizuri kuhakikisha hakuna aina yoyote ya
uhalifu utakaofanyika katika Uwanja wowote wa Ndege Nchini Tanzania.
IMETOLEWA NA:
JEREMIA N. SHILA ACP
KAMANDA WA POLISI VIWANJA VYA NDEGE ‘T’
DAR ES SALAAM.