You are on page 1of 3

1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 19/05/2014.
Ndugu waandishi wa habari, Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora
linaendelea na Operesheni katika wilaya zote za mkoa wa Tabora.
Ambapo kufuatia operesheni hiyo tumefanikiwa kukamata
watuhumiwa wa makosa mbali mbali kama ifuatavyo:-
KUPATIKANA NA RISASI: Mnamo tarehe 18/05/2014 huko eneo la
barabara ya Sikonge kata ya Ngambo Manispaa ya Tabora
alikamatwa BARANABA s/o JOSEPH, 36yrs, Mkonongo, mkazi wa
Inyonga wilaya ya Mlele mkoa a Katavi akiwa na risasi 307 za
SMG/SAR, mtuhumiwa amekiri kujihusisha uchuuzi wa risasi na
matukio mbalimbali ya unyangaanyi wa kutumia silaha. Baada ya
mahojiano alieleza kuwa risasi hizo ameuziwa na CHRISTINA D/O
PILIPILI, 42YRS, muha, mkazi wa mataa wa Hali ya hewa, kigoma
mjini ambaye naye amekiri kuwa ni muuzaji wa risasi na huzitoa
maeneo ya kigoma na kuja kuuzia hapa mkoani Tabora na mikoa
mingine ya jirani . Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara
baada baada ya upelelezi kukamilika.
KUPATIKANA NA SARE ZA JESHI: tarehe 18/05/2014 huko eneo la
Isike jirani na NBC Bank manispaa ya Tabora alikamatwa KARIMU
S/O ALLY, 25yrs, Muhurudu mkazi wa Mirambo, akiwa na sare za
Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Mtuhumiwa amekuwa akitishia na


2

-kulaghai wanachi kuwa ni askari wa jeshi hilo kwa nia ya
kujipatia fedha na huduma mbalimbali. Mtuhumiwa atafikishwa
mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
KUPATIKANA NA SILAHA: katika eneo la Ndono wilaya ya Uyui
alikamatwa, RAJABU S/O HUSSEIN, 65yrs, Mnyamwezi, mkulima
mkazi wa Kidatu manispaa ya Tabora akiwa na silaha aina ya
Shortgun iliyotengenezwa kienyeji kinyume na sheria, kisu kimoja
kikiwa ndani ya ala, tochi moja na Risasi tatu za Short gun.
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa aliwataja watu wawili
wanaomuuzia risasi ambao ni:- NOEL S/O VITALI, 40yrs,
mkulima, na ADREA S/O JOSEPH, 50yrs, Mnyamwezi, wote ni
wakazi wa Ukumbisiganga wilaya ya Kaliua, wameshakamatwa
tarehe 15/05/2014.upelelezi unaendelea na watuhumiwa
watafikishwa mahakamani.
Pia huko eneo la usoke mjini kata na Tarafa ya usoke wilaya ya
urambo walikamatwa HIRALY S/O RASHIDI @ BAKARI 40YRS ABDALAH
S/O RASHID @BAKARI 35YRS, MOSHI S/O RASHID @BAKARI 38YRS NA
ALADIN S/O RASHIDI @BAKARI 22YRS wote wakazi wa Usoke mjini
wakiwa na bunduki aina ya RIFFLE na risasi tano ambayo
wanamiliki kinyume na sheria. Upelelezi unaendelea na
watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
AJALI YA GARI KUGONGA PIKIPIKI NA KUSABABISHA KIFO: Mnamo
tarehe 16/05/2014 huko barabara ya Jamhuri maeneo ya
mahakama ya wilaya ya Tabora gari T.516 ALA Toyota Rav 4
aligonga pikipiki T. 458 ACC Sanlg na T.295 CPF SANLG na
kusababisha kifo cha RICHARD S/O ALOYCE na majeruhi
wawili.majeruhi hao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya
mkoa kitete. chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa
gari.Ambapo baada ya ajali dereva aliyefahamika kwa jina
STUMAI D/O TAMBWE, mkulima, mkazi wa chem chem manispaa


3

ya tabora la alipimwa na kupatikana ametumia kilevi.mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani.
AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA NA KUSABABISHA VIFO:
huko kijiji cha Bulyangombe barabara kuu ya Igunga Nzega gari
lenye namba za usajili T.677 AGJ Scania bus mali ya ZUGA s/o
AUGOSTINO @RICHARD wa Mwanza ikiendeshwa na PIUS s/o?
iligonga gari T.968 AJX Iveco iliyokuwa imeegeshwa pembeni
mwa barabara na dereva JUMA s/o BUNDALA, 41yrs, msukuma,
mkazi wa Shinyanga na kusababisha vifo vya watu 2 na
majeruhiwa 14 wamelazwa katika hospitali ya (w) Igunga .
chanzo ni uzembe wa dereva.
Jeshi la Polisi (M) Tabora linatoa shukurani kwa wote wanaolipatia
taaarifa tunazidi wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na
Jeshi lao ili kukomesha na kutokomeza vitendo vyote vya uhalifu
na kuwafichua wahalifu, pia watumiaji wa barabara wafuate
sheria za usalama barabarani ili kupunguza matukio ya ajali
Operesheni za kukamata wahalifu na makosaya baarabarani
zinaendelea ili kuhakikisha mkoa unakuwa na amani,utulivu na
usalama wa raia na mali zao.
Imetolewa na :-
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA TABORA.

You might also like