S.L.P BUNDA YAH: PIKIPIKI NAMBA T.213 CDF Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu, pikipiki yenye namba hapo juu ina tuhuma ya kumpakia raia wa Ethiopia siku ya tarehe 06/11/2013. Tukiwa eneo la darajani rubana kwenye doria zetu dereva wa pikipiki hiyo alipita akiwa amempakia raia huyo wa Ethiopia na aliposimamishwa hakusimama. Ndipo tukaomba msaada wa gari binafsi na kumfuatilia na kwa ujanja wake akapita njia za panya. Lakini kwa kushirikiana na askari wa kizuizi wa upande wa Lamadi mtuhumiwa alipita kwa mbali na kukimbizwa na pikipiki nyingine hadi akamshusha raia huyo wa Ethiopia na kukimbia zake. Na bahati nzuri namba za pikipiki zilijulikana. Hivyo tunaomba ushirikiano na ofisi yako namna ya kumpata mmiliki wa chombo hicho ili kukomesha biashara hiyo kwa sheria kuchukuliwa dhidi ya mhusika. Nswima O.S Kny; Afisa Uhamiaji Wilaya BUNDA NAKALA; AFISA UHAMIAJI (M) S.L.P 369 MUSOMA OC CID WILAYA S.L.P 50 BUNDA