You are on page 1of 113

Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

UCHUMBA NA MAISHA
YA NDOA
KATIKA MISINGI YA
KIKRISTO

FRANK P. KAROLI

Frank Philemon Karoli


1
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Mwandishi: Frank P. Karoli


S.L.P. 116,
Liwale-Lindi,
Tanzania.
Simu: +255762426746/+255683114202.
Barua Pepe: naxfra@gmail.com/naxfra@yahoo.com

Mhariri: Suleiman Mange.


Wasarufi: Melkior Patrick.

Kimechapwa Na: Naxfra Mixed Education Enrichment


S.L.P. 116,
Liwale-Lindi,
Tanzania.

Toleo la Biblia lililotumika: Swahili Union Bible (Toleo la mwaka 1952)

© 2018

Haki zote zimehifadhiwa, hivyo hairuhusiwi mtu ye yote kunakili, kurudufisha au


kuhifadhi kwa njia ya kielekitroniki au njia yo yote kitabu chote au sehemu ya kitabu
hiki bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa mwandishi wa kitabu hiki.

Haki-miliki © 2018

Frank Philemon Karoli


2
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

SHUKRANI

N
amshukuru sana Mungu na najinyenyekeza mbele Zake, kwani amenitia nguvu na
uwezo wa ajabu katika kutafiti na hadi kuikamilisha kazi yote ya kitabu hiki. Ni
kwa jinsi ya ajabu, Roho wa Mungu kanishuhudia, nami nikaona, sina budi ya
kuwashuhudia wengine kile ambacho Roho wa BWANA amekuwa akinishuhudia
kwa muda mrefu.
Sanjali na kumshukuru Mungu, napenda pia kuishukuru familia yangu ambayo kwa
sehemu kubwa nimeitumia kama sehemu ya utafiti katika kujiridhisha na kile ninachopaswa
kushiriki na Wakristo wenzangu ili niandike yaliyowazi ambayo yanawapasa Wakristo wote
na wasio Wakristo kuyafuata, kuyatenda na kuyaishi katika urafiki, uchumba, ndoa na malezi
ya vijana na watoto wao.
Shukrani za pekee ni kwa mke wangu kipenzi wa ndoa, Mariam Lucas na Mtoto
wangu Kevin Frank ambao kwao, ni sehemu ya kazi hii kutokana na maombi yao na yale
niliyojifunza kutoka kwao; hasa kwa kunivumilia na kukubali kuwa wapweke kwa wakati
nilipokuwa nikitumia muda mwingi ili kukamilisha kazi ya kitabu hiki. Siwezi kumsahau
kumpa shukrani zangu za pekee shujaa wangu miongoni mwa wanawake mashujaa
ulimwenguni; mama yangu mpendwa Koretha Karol ambaye amenilea kwa kujitoa kwa
upendo katika hali na mali hadi nilipofikia hatua ya kujitegemea katika maisha yangu.
Shukrani za pekee pia zimwendee Mchungaji Suleiman Mange aliyekuwa mlezi
wangu kipindi nilipokuwa Chuo Kikuu cha Dodoma (2009-2012). Naikumbuka kauli mbiyu
yake aliyoitumia kwa vijana wa vyuo vikuu kanda ya Dodoma iliyosema “It is not good for
man to stay alone” ikimanisha, “Si vyema mtu huyu akae peke yake”. Vivyo hivyo,
namshukuru sana Mchungaji Fransis Katengu, Mchungaji aliyenibatiza (Novemba 2011) pale
kwenye kanisa la Dodoma kati na kuniweka wakfu ili niweze kumtumikia Mungu katika
maisha yangu ya hapa duniani.
Kwa jinsi ya pekee pia, shukrani zangu zimwendee kaka yangu Japhet Ngh‟abi
ambaye aliniongoza juu ya misingi mizuri ya kumjua Mungu. Kwa namna ya pekee,
nalishukuru sana kanisa la Waadventista wa Sabato la Liwale kwa kunilea kiroho na
kunisaidia mambo mengi kwani hata mpaka nakikamilisha kitabu hiki, nilikuwa bado
mshiriki wake. Shukrani zangu za dhati zinamhusu pia Mwinjilisti Fredrick Jonathan
Sogoseye pamoja na mke wake. Namshukuru sana Mchungaji Israel Kagya kwa mafundisho
yake mazuri yaliyonijenga kiroho, na baadhi ya mafundisho yake yamo katika kitabu hiki.
Aidha, ni wengi wa kuwashukuru katika ufanikishaji wa kazi ya kitabu hiki; kwa
kuwataja baadhi ni; bwana na bibi Shamsi Kashoro, bwana na bibi Wilson Nyamanga, bwana
na bibi Paul Enock Jangu, bwana na bibi Ephraim Mmbaga, bwana na bibi Elly J. Moses,
bwana na bibi Ephraim Mwandendi, bwana na bibi Mwalimu Mbwambo, bwana na bibi
Daibrin Kibamba pamoja na Neema Erasto, ASSA-Liwale sekondari, Samson Balele, Elisha
Magoma, Graceana Makota, na wengine wengi ambao sikuwataja, natambua mchango weo,
hivyo, BWANA awabariki sana.

Frank Philemon Karoli


3
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

DIBAJI

M
iaka ya hivi karibuni, ulimwengu umekuwa ukishuhudia mabadiliko makubwa
ya ajabu katika ndoa na familia za wanadamu. Mabadiriko hayo yanachagizwa
na sababu nyingi ambazo zimepelekea familia baadhi kuyumba na kusababisha
aidha kuvunjika kwa ndoa, kuwa na migogoro isiyokoma, watoto kutokuwa na
maadili mema, usaliti kwa wanandoa, uzinzi, ngono zembe kwa vijana, magonjwa ya
kisaikolojia yatokanayo na changamoto za kifamilia au vifo miongoni mwa wanafamilia kwa
sababu ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Nishauku yangu kumwona kijana au mwanandoa akiziepuka changamoto zote hizo
kwa kuzingatia na kuyafuata yale yaliyomo ndani ya kitabu hiki huku akimruhusu Mungu
atawale maisha yake yote. Kitabu hiki ni kazi iliyochukua muda wa miaka sita, hivyo
yaliyomo yote ni kweli isiyokuwa na mashaka maana hata Biblia inayashuhudia kwa
kuyaeleza katika utimilifu wake. Kitabu hiki ni kitabu lulu kwa wale wote walio katika ndoa,
uchumba, na vijana wote wasiokuwa katika mahusiano ya uchumba, kwani, kinamashauri juu
yao pia (vijana) ili waweze kuuelekea mwelekeo sahihi juu ya mahusiano na ndoa zao.
Ndani ya kitabu, pia pameandikwa mashauri juu ya malezi ya watoto na changamoto
zinazowakabili katika makuzi na malezi yao, na jinsi ya kuwaepusha ili waiepuke njia ile
pana ielekeayo katika upotevu. Unapokisoma kitabu hiki, yathibitishe mafungu yaliyomo
kwa kusoma Biblia yako huku ukimruhusu Roho Mtakatifu awe sehemu ya mabadiliko kwa
yale yote yaliyoelekezwa ndani ya kitabu. Kwa kuwa mwandishi wa kitabu hiki ni mwalimu
kwa taaluma na mwinjilisti, hivyo, kitabu hiki kimeandikwa kwa mtililiko na mpangilio
mzuri, unaovutia, wenye lugha rahisi, ili kumfanya msomaji aelewe kirahisi na kutochoka
pia.
Kitabu hiki chenye jina la Uchumba na Maisha ya Ndoa Katika Misingi ya Kikristo
ni kitabu ambacho kimekusudiwa kutoa elimu, ufahamu, ujuzi na maarifa katika Nyanja
zifuatazo: 1. Jinsi ya kujenga urafiki na mahusiano bora, 2. kuuelewa uchumba wa kweli na
hatua zake katika misingi ya Kibiblia; 3. Madhara ya kushiriki tendo la ndoa kabla ya ndoa
na jinsi ya kuacha au kuepuka kushiriki tendo la ndoa kabla ya ndoa; 3. Kanuni za Kibiblia
katika kujipatia mchumba anayepaswa kuwa mwenzi wa maisha; 4. Mambo ya kuzingatia
kabla ya kufanya maamuzi ya kuingia katika ndoa; 5. Utakatifu wa ndoa na makusudi ya
Mungu kuasisi ndoa kwa wanadamu; 6. Vyanzo vya migogoro katika ndoa na namna ya
kufanya ili ndoa kuwa na ustawi mzuri; 7. Jinsi ya kuwa mke au mume mwema katika ndoa
na familia; 8. Jinsi ya kuifanya familia kuwa ya kiroho na yenye furaha na amani; 9. Malezi
sahihi ya watoto katika misingi ya Kibiblia; 10. Kiasi na uwakili katika familia. Na hayo ni
kwa kutaja baadhi.
Mwandishi wa kitabu hiki ni mwalimu (wa sekondari na vyuo vya ualimu) kwa
taaluma, mwinjilisti na mwalimu wa Biblia anayemtumikia Mungu. Uzoefu alioupitia katika
makuzi, kazi, malezi, uchumba, ndoa, tafiti na maisha yake binafsi, ni miongoni mwa vionjo
alivyovitumia katika kitabu hiki, ili kushiriki na ulimwengu wote wa Wakristo na wasio
Wakristo katika kuijua hatima yao na nini wafanye ama kufuata katika “Uchumba na Maisha
ya Ndoa katika Misingi ya Kikristo”.

Frank Philemon Karoli


4
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

YALIYOMO
SHUKRANI:………………………………....................................................……..…...………………...............…… 3

DIBAJI: …..…………………………….....................................................…..……….….....…………....................… 4

UTANGULIZI: ………………………..................................................……..............……….….....…...…………….. 7

SURA YA O1:
MAMBO YA KUFAHAMU KWA VIJANA: …........................................................................…….....….…. 8

SURA YA 02:
MAMBO YA KUZINGATIA KWA MCHUMBA ILI AWE MWENZI WA MAISHA: ..........................15

SURA YA 03:
HATIMA YA UCHUMBA NA MAAMUZI YA KUOA AU KUOLEWA: ……..…................................… 28

SURA YA 04:
MPANGO NA MAKUSUDI YA MUNGU KUASISI NDOA: ……………………...........................…..….… 33

SURA YA 05:
UASI KATIKA NDOA NA FAMILIA YA KWANZA: ……………………..…........................…..........…….. 38

SURA YA 06:
CHANGAMOTO KATIKA FAMILIA ZA KIKRISTO:.........................................................................… 45

SURA YA 07:
JINSI YA KUWA MKE AU MUME MWEMA KATIKA NDOA NA FAMILIA: .................................. 53

SURA YA 08:
FUNZO KUTOKA MITHALI 31:11-31 KWA WANAWAKE-WANANDOA: ........ ...... ...................57

SURA YA 09:
UFAHAMU NA MAARIFA JUU YA NDOA YA KIKRISTO: …………....…........................................… 65

SURA YA 10:
FAMILIA YA KIROHO YENYE FURAHA: …….……............................................................................. 70

SURA YA 11:
MALEZI BORA YA KIKRISTO KWA WATOTO: .…......................................................................… 76

SURA YA 12:
SAIKOLOJIA YA TABIA NA HISIA ZA MAKUNDI YA WATU: ……….....….......................……...… 87

SURA YA 13:
TOFAUTI ILIYOPO KATI YA MWANAMKE NA MWANAMUME: .................................. 94
SURA YA 14:
UMUHIMU WA KUSAMEHEANA KWA WANANDOA: …….....…........….......................…………..... 100

SURA YA 15:
UWAKILI WA MUDA KATIKA NDOA NA FAMILIA: ……………….…........................…...………...... 104

Frank Philemon Karoli


5
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

HITIMISHO: …………………………………………....................………..................................………....…....... 110

REJEA: ………….…...............................……................................................................................................ 112

Frank Philemon Karoli


6
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

UTANGULIZI

M
wenzi wako si mkamilifu, na wewe pia, na wote wawili hamuwezi kuwa
wakamilifu, lakini kama anaweza kukufanya ufurahi, umfikirie mara mbili na
zaidi na anakiri kuwa yeye ni binadamu anaweza akatenda makosa, basi,
mshikilie yeye na mpende kwa kadiri uwezavyo, maana, ni mtu sahihi kwako.
Anaweza kuwa hakufikirii kila sekunde katika siku, lakini anatumia sehemu ya maisha yake
kwa ajili yako. Usimbadilishe, na usitegemee makubwa zaidi ya yale awezayo kukutendea au
yale anayoyamudu. Tabasamu pale akufurahishapo, mwambie pale anapokukasirisha, na
umkumbuke (um-miss) pale anapokuwa hayupo karibu nawe. Hapo utakuwa na furaha ya
kweli katika ndoa yako.
Kwa mwanamke na mwanamume kuwa na furaha katika ndoa kunahitajika upate mtu
mnayependana, mtu atakayejali sana furaha yako kuliko hata yake, mtu atakayekuwa wa
mwisho kukufanya ulie, mtu ambaye atakupa kila unachostahili, atakayejitolea muda wa
maisha yake kuishi na wewe kama mke au mume; ambaye ni mkweli, mwaminifu, mtu asiye
na tamaa, mtu makini katika kufikiri na ajuaye anachohitaji mwenzi wake, mtu pekee ambaye
atajisikia fahari kuwa na wewe po pote na kulitetea penzi lenu kwa namna yo yote ile na
kudumisha uaminifu.
Mwanamume au mwanamke atakayekupenda kuliko wewe utakavyompenda
hapatikani kirahisi, ila tu ni kama wewe nawe utakuwa unavigezo uvitakavyo huku
ukimkabidhi Mungu atende miujiza juu yako ambapo ukiwa sehemu kubwa ya matarajio
uyatakayo. Hakuna haja ya kukata tamaa na kujiona kuwa huna thamani katika maisha yako
kwakuwa tu kila uchumba unaouanzisha hauwi na mwisho mzuri au ulioutarajia. Maisha ya
uchumba ni maisha yasiyotoa uhakika wa muda sahihi wa uwepo wa ndoa bali ni matazamio
katika kufanyiana tathimini kama mtaendana.
Ukimpata yule umpendaye kwa dhati kama lilivyokuwa tarajio lako toka ndani ya
moyo wako, mhakikishie kumpenda siku zote. Pale muda utakapowadia na utakaporuhusu
nywele zake nyeusi ziwe nyeupe, zidi kumpenda. Pale ngozi yake laini ya ujana
itakapokaliwa na ngozi iliyojikunja ya uzee, bado hitaji lako la kumkumbatia lisipotee daima.
Tena mhakikishie kuwa “pale sura yake itakapokuwa na makunyanzi anapotabasamu, bado
utampenda”.
Kwa kuyathibitisha hayo yote; kama wote, (yaani mimi na wewe msomaji) tungejua
kuwa kila mtu katika ndoa zetu anahitaji faraja na upendo, tungesema kuwa sote tupo tayari
kuwapenda wenzi wetu wa maisha kama tujipendavyo sisi wenyewe na tukavaa viatu vyao
vya magumu yote wayapitiayo katika maisha ya ndoa. Tukinuia na kuweka nadhiri kuwa siku
zote, miaka yote tutawapenda wenzi wetu, na hiyo ni kwa kuwa tu kuwapenda kwetu kwa
dhati ni amani ya mioyo yetu na ustawi wa familia zetu.
Pangekuwepo na upendo wa dhati kwa wanandoa, pasingekuwepo na matatizo ya
kifamilia kama; kesi nyingi za familia mahakamani au ustawi wa jamii, ugomvi uletao
majeraha katika mwili au vifo, usaliti, malezi mabovu ya watoto, uwepo watoto wa mitaani,
maambukizi ya magonjwa ya zinaa, migogoro ya watoto, kutengana na kuwepo kwa
magonjwa ya kisaikolojia yatokanayo na matatizo ya kifamilia. Natumaini bila hayo yote
yanayosababisha matatizo ya ndoa na familia, dunia ingekuwa mbingu ndogo.

Frank Philemon Karoli


7
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 01=

MAMBO YA KUFAHAMU KWA VIJANA AMBAO HAWAJAOA AU


KUOLEWA

“Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini,


Msiyachokoze mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”
Wimbo Ulio Bora 2:7

Kijana wa kike au wa kiume, yampasa kuwa mwangalifu sana katika kuchagua


marafiki ambao watakuwa msaada na watu wakaribu katika kushirikiana kwa mambo
mbalimbali. Ukiwa kijana, siyo tu lazima uwe na rafiki mwanasheria, daktari, kiongozi ndani
ya serikali na kanisani bali kuwa na marafiki walio wema wengi kadri iwezekanavyo. Katika
maisha yetu ya kila siku binadamu anahitaji kuhusiana sana kunakotengeneza marafiki
ambao, kwa sehemu kubwa huwa kimbilio letu katika kupata msaada na ushauri. Uhusiano
wa kirafiki kulingana na sosholojia yaani “sociology” ambayo ni elimu inayohusu mahusiano
ya wanadamu inapambanua aina zifuatazo za mahusiano katika urafiki:

1. Aliyekataliwa (Rejectee).
Aina hii ya urafiki, unakuta kundi zima, mmoja au baadhi katika kundi zima
hakubariki kwa sababu ya tabia au kutoendana na kundi zima. Utakuta kundi zima
linamtenga lakini mtu huyo anazidi kujishikamanisha katika kundi hilo bila yeye kujitambua.
Aina hii ya urafiki katika kundi hili unaitwa urafiki wa kulazimisha au kujipendekeza, na
hivyo mtu huyo atakuwa mtumwa wa kundi.

2. Anayejitenga (Isolatee).
Ni aina ya uhusiano au urafiki ambapo mtu mmoja au watu baadhi wanakuwa
wamejitenga na hawashirikishi mambo yao wengine katika kundi zima, japo ni sehemu ya
kundi hilo. Marafiki wanamna hii hunufaika na kundi, bali wao hawalinufaishi kundi maana
ni wasiri juu ya masuala yao.
3. Aliyekataa (Neglectee).
Aina hii ya uhusiano, unakuta kundi zima la marafiki linamuhitaji mtu mmoja au zaidi
lakini mtu huyo hataki kuwa sehemu na mshiriki wa kundi, hivyo hujitenga kwa sehemu
kubwa na hashirikiani na wenzie katika mambo mbalimbali ya kundi aidha, kwa sababu
mbalimbali au yeye kutotaka kwa hiali.

4. Nyota (Star).
Miongoni mwa kundi nzima yupo mtu mmoja ambaye ni maarufu, mtu mwenye
mvuto na mwenye ushawishi mkubwa sana kwa watu wengine. Katika aina hii ya uhusiano

Frank Philemon Karoli


8
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

watu wengi hujikuta wamevutwa kwa sababu ya umaarufu na ushawishi wa mtu mmoja
hivyo kila mtu anajitahidi kujenga urafiki na huyo mtu na kuwa kiungo pekee cha wengine
kufahamina.
Faida za Urafiki wa Kweli
Yampasa kijana (au mtu ye yote) kutambua kuwa urafiki wa kweli haujali jinsia.
Japokuwa yapo mabaya mengi yanayosababishwa na urafiki, lakini, yapo mengi pia yaliyo
mazuri katika urafiki wa kweli na baadhi ya faida miongoni mwa nyingi ni zifuatazo:
Kufurahishana: Urafiki wa kweli ni kuleteana furaha iliyo ya kweli miongoni mwa
marafiki na siyo kuumizana au kuleteana huzuni kwa kutendeana mabaya na usaliti.
Kukubaliana: Marafiki wenye urafiki wa kweli hukubaliana na siyo kushurutishana ili
kutekeleza jambo fulani kutoka upande mmoja wa urafiki.
Kuheshimiana: Marafiki walio na urafiki wa kweli ni lazima waoneshe hali ya juu ya
kuheshimiana na si vinginevyo. Kuheshimiana kunaleta usikivu katika kushauliana miongoni
mwa marafiki.
Kusaidiana: Kusaidiana ni jambo moja la msingi katika urafiki ulio wa kweli.
Marafiki wenye urafiki wa kushibana ulio wa kweli husaidiana katika namna mbalimbali iwe
kwenye raha au changamoto mbalimbali.
Kushiriki hisia kwa pamoja: Kushiriki hisia kwa marafiki ni kielelezo cha urafiki wa
kweli. Rafiki wa kweli ni yule anayekufaa katika huzuni na raha na kwa mazingira au muda
wo wote.
Kujuana au kuelewana mapungufu: Marafiki walio na urafiki wa kweli wanajuana
mapungufu yao, hivyo wanajua jinsi ya kuishi na kurekebishana kulingana na mapungufu yao
wao kwa wao. Kujuana mapungufu na madhaifu kunasaidia kujua jinsi ya kuishi bila
kukwazana au kuumizana.
Kuaminiana: Marafiki walio wa kweli hawana haja ya kutiliana mashaka maana kila
mmoja humwamini mwenzake. Kuaminiana kunajenga ustawi mzuri wa urafiki endapo kila
mmoja atakuwa mwaminifu kwa mwenzake.
Uwazi na uhuru wa kuelezana: Kuelezana ukweli bila kufichana ni jambo la msingi
kwa marafiki maana hujenga uaminifu miongoni mwao. Mambo au masuala yakiwekwa wazi
miongoni mwa marafiki inakuwa rahisi kusaidiana au kushauriana.

Dhana ya Urafiki na Uchumba


Urafiki ni hatua inayohusisha hali ya watu wawili au zaidi wasiokuwa ndugu wa
damu wanaofahamiana au kupendana na kushiriki mambo mbalimbali bila kisia za kimapenzi
kwa jinsia au jinsi mbili tofauti. Uchumba ni hatua kutoka hatua ya urafiki inayohusisha hisia
za kimapenzi baina ya watu wawili wenye jinsi au jinsia tofauti. Hivyo basi, kabla ya
uchumba lazima paanze na urafiki, na kabla ya ndoa lazima paanze na uchumba.
Ili Mkristo ye yote aweze kuifikia ndoa lazima aanze na hatua mama mbili, ambazo
ni urafiki na uchumba. Bila hatua hizo mama, itakuwa ni ndoa iliyotokana na utashi wa
watu wengine nje na wale wawili (wachumba) wanaotazamia au waliooana. Ndoa
inayopatikana bila urafiki na uchumba, ni ndoa iliyofanikishwa na watu wengine bila adhima
ya wawili (mke na mume) kukubaliana kisha kuridhiana wao kwa wao.
Urafiki na uchumba ndiyo barabara sahihi inayompeleka mtu katika ndoa. Tambua
kuwa, kukosekana kwa furaha katika ndoa si kwa sababu ya ukosefu wa upendo miongoni

Frank Philemon Karoli


9
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

mwa wanandoa, bali ni kukosekana kwa urafiki miongoni mwa wenzi katika ndoa. Kurukwa
kwa hatua ya urafiki husababisha wanandoa kutokuwa na mazingira mazuri ya urafiki. Katika
Wimbo Ulio Bora 5:16, Sulemani akiwa anamsifia mwenzi wake kwa binti za Yerusalemu
anasema “.... Ni huyu mpendwa wangu, ni huyu rafiki yangiu .....”
Hatua ya urafiki na uchumba huwa ni hatua nyeti sana kwa Mkristo anayejiandaa
kuingia katika ndoa hapo baadaye. Ni hatua ambayo haihitaji uzembe katika kuomba au
kumshirikisha Mungu; ni hatua inayotoa hatima ya aina gani ya ndoa au familia
itakavyokuwa. Itambulike kuwa: Uchumba siyo ndoa, hivyo waweza ukavunjwa au
kuvunjika na kukosea katika uchaguzi wa mchumba husababisha majuto na migogoro
isiyokoma katika ndoa na familia na hupelekea kutengana kwa wanandoa.

Kuuelewa Upendo wa Kweli.


Wengi wao hasa vijana wamekuwa wakikutwa na changamoto katika maisha yao ya
uchumba na wakati mwingine ndoa, hii ni kutokana na kutokujua ni nini upendo wa kweli.
Neno upendo (kwa lugha ya Kiyunani, yaani Kigiriki) lipo katika makundi makuu matatu:
Upendo aina ya “Agape” ni upendo wa Mungu kwa wanadamu, upendo aina ya “Eros” ni
upendo wa wanandoa hususani jinsia mbili tofauti na upendo aina ya “Philia” ni upendo
baina ya ndugu wa damu au marafiki. Jinsi upendo wa „eros‟ unavyopatikana kati ya
mwanamke na mwanamume (Mithali 30:18 - 19) ni siri ya Mungu pekee juu ya mvutano
uliopo.
Upendo wa „eros‟.
Upendo wa eros kati ya mwanamke na mwanamume hujitokeza katika njia zifuatazo:
Njia ya kwanza ni pale siku ya kwanza tu mwanamke na mwanamume kuonana na njia ya
pili huja kwa kufahamiana kwa muda mrefu kati ya mwanamke na mwanamume, aidha
walisoma pamoja, au wananasali pamoja katika kanisa moja. Hivyo basi, upendo waweza
kuja kwa ghafla au polepole.
Jambo la kuzingatia, upendo baina ya mwanamke na mwanamume ni maamuzi na
siyo hisia pekee. Upendo huangalia utayari wa kujitoa kwa yule anayependwa. Pia upendo
huhusisha kujitoa kikamilifu kwa mwingine na upendo usio wa kweli ni ubinafsi. Upendo wa
kweli hauhusishi rushwa ya vitu au pesa kwa kusema kuwa “kama unanipenda ni nipatie au
ninunulie kitu fulani”.
Kumjua Anayekupenda.
Alama ya upendo wa kweli ni uvumilivu, kwa maana pendo la kweli huangalia
baadaye (ndoa) na siyo hapohapo (tamaa). Ni jambo gumu kumjua moja kwa moja
anayekupenda kwa dhati kwa mtazamo wa kibinadamu. Kwa kuunga hoja za William Fagal,
ili kumjua mtu anayekupenda, atajibainisha katika nyanja zifuatazo:

 Kwa asilimia kubwa atapendezwa na kuvutiwa na kile unachokifanya na kukisema,


 Fikra, utashi, na mwitikio wako na wake unafanana na kuendana bila ushurutishi,
 Anaridhika na kukukubali jinsi ulivyo,
 Mnapokuwa pamoja anajihisi kuwa na kila kitu bila ukinai wa mazungumzo na
uwepo wako,
 Anajisikia amani ama furaha na kuridhika anapokuwa pamoja na wewe, na

Frank Philemon Karoli


10
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

 Uwepo wa mvuto na uhitaji wa kuingia nawe katika ndoa tofauti na anapokuwa na


marafiki wengine wa jinsia tofauti.

Jinsi ya Kumtambua Mwenzi wa Maisha


Mungu huwapatia wenzi wa kufanana nao wale wote wamkabidhio haja zao. Kwa
sababu, kumbukumbu na haja zao wale wamtumainio Mungu zipo dhahiri maana ameziweka
kwenye viganja (vitanga) vyake (Isaya 49:16) hivyo, Mungu huwajibu kwa haraka wale
wamtumainio kadri ya waombavyo sawasawa na mapenzi Yake. Hivyo basi, jinsi ya
kutambua mchumba ambaye atakuwa mwenzi wa maisha huhusisha mambo yafuatayo:

(a) Kabla ya Kumpata Mchumba


1. Mungu atakuongoza: Kama jambo la kupata mwenzi litakuwa limemuhusisha
Mungu kwa kufanya maombi mengi na kufunga. Mungu kwa kutumia njia mbalimbali
atamuongoza kwa mkono wake ulio hodari naye atamuonesha yeye aliye mwaminifu
(Mwanzo 2:18-23; Mwanzo 24:1-27; 62-67). Wakati mwingine Roho Mtakatifu anaweza
akashuhudia na kuthibitisha katika nafsi ya mtu kuwa, “huyu ndiye au siye” (Warumi 9:1;
Wafilipi 4:7).
2. Uthibitisho wa watu wengine: Patakuwepo na ushuhuda wa watu wengine juu ya
yule ambaye Roho amekushuhudia. Endapo Roho wa Mungu amekushuhudia kuwa ndiye,
watu wa Mungu na wale wanaomfahamu fika, nao watakushuhudia kua anafaa kuwa mwenzi
wa maisha kutokana na matendo yake mema na tabia (Mithali 15:22).

(b) Baada ya Kuingia Naye Uchumba


1. Kutakuwepo na upendo wa kweli utokanao na Mungu (Zaburi 121:1-2; 1Petro 4:8):
Upendo wa kweli ni ule tu uliojikita mizizi katika Bwana ambaye Yeye ndiye aliye Pendo.
2. Kutakuwepo na kuvumiliana katika kila hali na nyakati zote (1Wakor 13:4): Upendo
wa kweli ni ule wenye hali ya kuvumiliana miongoni mwa wachumba kwa yale yaliyochini
ya uwezo wao.
3. Kuheshimiana (1Wakor 13:4-8, 1Sam 20:17): Mwenye kupenda kwa dhati
atamheshimu yule ampendaye; hivyo, wachumba wote kwa pamoja wataheshimiana.
4. Amani ya Kristo itatawala miongoni mwa wachumba (Wkolosai 3:15): Uchumba
wenye muelekeo mzuri utatawaliwa na utulivu na amani bila kutokea magonvi mara kwa
mara.
Sababu za Kujipatia Mwenzi wa Maisha:
1. Kujipatia mwenzi wa maisha ni mpango wa Mungu (Mwanzo 2:18).
2. Kujipatia mwenzi wa maisha huleta furaha katika maisha (1Wakorintho 7:9).
3. Kujipatia mwenzi wa maisha ni kujipatia mlinzi wa maisha (Yeremia 31:22).
4. Kujipatia mwenzi wa maisha ni kwa makusudi ya kuendeleza uzao (Mwanzo 1:18-25).
5. Kujipatia mwenzi wa maisha kunakidhi hitaji la mhemko wa mwili (1Wakor 7:8).
6. Kujipatia mwenzi wa maisha kunasaidia kujijengea heshima kwa jamii (Isaya 4:1).

Frank Philemon Karoli


11
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Wakati Unaofaa Kuoa au Kuolewa:


1. Ni pale tu umri unaporuhusu kuoa au kuolewa, hasa baada ya kupevuka na kukomaa
kwa via vya uzazi. Inashauliwa kuanzia miaka 18 na kuendelea.
2. Wakati mtu anapokuwa amekomaa kiakili anaweza akaoa au kuolewa maana anaweza
kuyamudu vyema majukumu ya familia katika ndoa.
3. Kunapokuwa na kazi au chanzo sahihi na salama cha kuingiza kipato, mtu anaweza
akaoa au kuolewa.
4. Kunapokuwa na utayari toka ndani ya moyo, mtu anaweza kuoa au kuolewa
sambamba na maelezo ya vipengele vya namba 1, 2, na 3.

Jinsi ya Kuepuka Uzinzi Kabla ya Ndoa.


Kitu cho chote alicho kikataza Mungu anamalengo ya kutuepusha na madhara yake.
Ni vyema vijana wakahakikisha kutunza usafi wa miili yao na kuheshimu utukufu na usafi
wa tendo la ndoa. Yampasa kijana wa kike au wa kiume aliye Mkristo ajiepushe kushiriki
ngono kabla ya ndoa. Vijana wa kike na wa kiume wafanye mambo yafuatayo ili kuepuka
kujamiiana kabla ya ndoa:
 Waepuke kuwa katika mazingira hatarishi yanayoshawishi kufanya zinaa, mfano
sinema na sehemu zingine za starehe.
 Waepuke marafiki wabaya katika kundi rika ambao wanamatendo mabaya.
 Waepuke utembeaji wa usiku bila sababu zo zote katika mazingira yasiyo salama
kwao.
 Waepuke kuangalia au kusoma vitu vinavyohusu mapenzi na ngono ili wasiziamshe
hisia zao.
 Waoe haraka kama umri umefika ili kuiepuka zinaa.
 Wajihusishe na programu za kanisa juu ya ibada na kumtumikia Mungu ili muda wote
waufikirie utukufu wa Bwana.
 Wapende kusoma na kulitafakari neno la Mungu ili Roho wa Mungu akae ndani ya
maisha yao.
 Wajue kufanya ngono kabla ya ndoa ni dhambi na wanavunja amri ya saba ya Mungu
inayokataza kufanya uzinzi.
 Wajiheshimu katika mavazi, mazungumzo na mienendo mizima ya maisha yao ili
wasimpe nafasi Shetani.
 Wapende kufanya mazoezi hususani ya viungo vya mwili ili kuondoa hisia na
mawazo mabaya katika fikra zao.

Faida za Kujilinda Bila Kutenda Ngono Hadi Wakati wa Ndoa


Kujitunza na kujilinda bila kutenda tendo la ndoa kwa vijana wa kike na wakiume
kunafaida zifuatazo:
 Kuwa mwenzi unayefaa katika ndoa.

Frank Philemon Karoli


12
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

 Huamsha ari na hisia za kujithamini.


 Ni kipimo kizuri cha uwezo wa kuzuia au kuzimudu hisia.
 Hujenga uwezo wa uvumilivu wa kihisia.
 Hutoa nafasi ya kujikita katika mambo na malengo ya msingi ya maisha bila
kuingiliwa na tamaa za mapenzi kabla ya ndoa.
 Hujenga taswira na msingi wa uaminifu kwa kijana.
 Huepusha maumivu ya mapenzi kwa vijana kabla ya ndoa.
 Husaidia kutunza via vya uzazi mpaka vikomae ili kuwa tayari kwa ajiri ya kushiriki
tendo la ndoa na kuzaa pindi kijana awapo ndani ya ndoa.
 Huepusha kuharibu hisia na ubongo katika kufikiria mapenzi kabla ya ndoa.
 Huepusha utumwa wa ngono kabla ya ndoa kwa vijana.
 Huepusha utoaji wa mimba zitokanazo na kushiriki tendo la ndoa bila malengo ya
kuzaa.
 Huondoa hofu kwa vijana juu ya kuhisi maambukizi ya magonjwa ya zinaa na Virusi
Vya Ukimwi kwa kushiriki ngono kabla ya kuoa au kuolewa.
 Huwaepusha vijana dhidi ya kupata mimba katika umri mdogo.

Nini cha Kufanya Endapo Kijana Ameshiriki Uzinzi (ngono) Kabla ya Ndoa?
Endapo kijana wa kike au kiume atakuwa ameshiriki ngono aidha kwa makusudi au
bahati mbaya (ni mara chache sana bahati mbaya hujitokeza) yampasa afanye mambo
yafuatayo ili awe safi mbele za Mungu na kujipanga kwa ajili ya kushiriki awapo ndani ya
ndoa tu:
 Afanye toba ya dhati kwa Mungu kisha aache kabisa.
 Abadilishe mienendo na mitindo yake yote ya maisha kwa kuacha yale yote yaliyokuwa
yakimvuta kufanya uzinzi.
 Aepuke makundi rika yaliyo maovu na makundi mabaya yenye tabia mbaya na hatarishi
katika mienendo yake.
 Ajilinde na vitu vinavyosababisha ama kuleta hisia za kimapenzi mfano sinema,
tamthiliya, programu za TV za mapenzi, majarida na vitabu vya mapenzi.
 Aepuke kutembelea mazingira yenye ushawishi mkubwa wa kubadili hisia zako na
kutamani kufanya mapenzi.
 Atenge muda mwingi kwa ajili ya kujifunza neno la Mungu kwa kusoma Biblia na
kushiriki ibada na programu mbalimbali za kanisa.
 Apambane kwa kila namna ili kuzidi kuwa safi, na kupambana huko kusiwe kwa uwezo
wake pekee bali ajikabidhi kwa Yesu Kristo aliye mshindi wa dhambi na hutushindia
pia.
 Achunge mdomo wake katika mazungumzo na aina ya mavazi anayovaa maana kwayo
huashiria urahisi na husadifu tabia ya mtu.
 Aachane na tabia ya kuangalia picha na mikanda ya watu walio uchi au nusu uchi
maana huathiri ubongo na hisia pia.

Frank Philemon Karoli


13
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Madhara ya Kuharakisha Ngono Kabla ya Ndoa


Mtumishi wa Mungu Gibsoni Ezekieli yeye anasema “vijana wote wa kike na
wakiume yawapasa kujua kuwa hakuna mstari unaotenganisha kutoka ujana kwenda utu
uzima. Namna unavyofanya mambo yako ukiwa kijana huathiri utu uzima wako. Tabia
unazoendekeza wakati wa ujana zitakufuata utakapokuwa mtu mzima. Vijana wengi
wamekuwa na tabia ya kuwa na mazoea mabaya, hususani juu ya kutoheshimu na kutilia
umakini suala la tendo la ndoa. Mazoea ya kubadirisha wasichana na wavulana kama nguo
kwa kujiaminisha kuwa wataacha kufanya hivyo endapo wataoa au kuolewa na kuwa katika
ndoa zao”.
Anaendelea kusema kuwa “Mazoea mabaya ni muuaji anayeonekana hana hatia
mwanzoni, na vijana hujifariji nitakapooa au kuolewa kwa sababu nitakuwa na mtu wa
kunipoza haja zangu nitaacha uzinzi na uasherati. Hawajui ya kuwa utegemezi au uraibu
(addiction) humfanya aliyezoea kuhitaji kufanya hivyo mara kwa mara. Pia husababisha kitu
ambacho wataalam wa saikolojia hukiita Objectification of women and men, yaaani
mwanamke au mwanamume anakuwa kama ni kitu tu cha kumridhisha mwanamume au
mwanamke. Mwanamke au mwanamume anakuwa si mtu bali kitu cha kutuliza haja za
kingono katika maisha”.
Kama tulivyoona katika nukuu ya maelezo ya mtumishi wa Mungu Gibson Ezekiel;
hivyo basi, mazoea ya ngono kabla ya ndoa kwa wasichana na wavulana huleta athari badaye
katika nyanja zifuatazo:
1. Kutokana na mazoea ya kubadirisha badirisha au kufanya ngono mara nyingi na
kwa hali ya juu kabla ya ndoa, mwanamke au mwanamume huonekana kama “sex machine”
katika ndoa kwa sababu tendo hilo limejengeka katika mawazo na fikra kama starehe na haja
ya msingi kila wakati. Inapoonekana mke au mume hawezi kuwa tayari muda wote kutenda
tendo la ndoa kwa mara nyingi inavyotakiwa kufanya kama miongoni mwa mmoja wa
wanandoa kama alivyozoea kufanya mara kwa mara hapo kabla ya ndoa, mmoja hutoka nje
ya ndoa ili kukidhi haja yake ya tendo la ndoa.
2. Yawezakuwa mke au mume huyo aliyepatikana kuwa tofauti na wale aliowazoea
kushiriki nao ngono hapo awali. Kwa ufupi unaweza ukaoa au kuolewa; mkeo au mumeo
asikupe ushirikiano kama ilivyotazamiwa kutokana na mazoea. Uhitaji mwingi kati ya mmoja
wa wanandoa itapelekea kuchepuka kwa sababu ya kushindwa kuvumilia hisia endapo mwezi
ameonekana kulegalega na kutokukidhi haja ya tendo la ndoa aidha, kwa sababu ya
majukumu na uchovu wa kazi au ugonjwa au ujauzito kwa mwanamke. Ndiyo maana
wanandoa wengi huendeleza tabia zilezile za kuwa na wenzi wengine wengi hata baada ya
kuoa au kuolewa, kwani hitaji lake lipo juu sana. Kwa sababu hiyo, tabia ya uzinzi hujitokeza
kwa wanandoa walio wengi.
Jambo la kuzingatia: Imeandikwa kuwa mume au mke kwa pamoja wasinyimane,
tena mume ana mamlaka juu ya mwili wa mkewe na mke ana mamlaka juu ya mwili wa
mumewe. Lakini Paulo akaonya ya kwamba, wanandoa wafanye tendo la ndoa kwa kiasi ili
wasije wakajaribiwa na Shetani katika hilo na kutenda dhambi (1Wakorintho 7:1-5).
Imeandikwa “....kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati” (1Wathesalonike 4:3) .

Frank Philemon Karoli


14
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 02 =

MAMBO YA KUTAMBUA NA KUZINGATIA KWA MCHUMBA


ANAYEPASWA KUWA MWENZI WA MAISHA

“Mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake; Hulisha kundi lake penye


nyinyoro. Hata jua lipunge, na vivuli vikimbie, Unigeukie, mpendwa wangu,
Nawe uwe kama paa, au ayala, Juu ya milima ya Betheri”

Wimbo Ulio Bora 2:16-17

Kumekuwapo na changamoto nyingi sana za ndoa, na hizo changamoto


zimesababishwa na kufanya makosa kwa wanandoa hapo awali katika suala nzima la
uchaguzi wa wenzi au wachumba wao katika hatua za uchumba kabla ya ndoa kuja.
Changamoto mojawapo katika ndoa imesababishwa na mitazamo tofauti na utashi binafsi wa
watu katika kuingia kwenye ndoa.
Kutokufahamu umuhimu wa ndoa kwa Wakristo baadhi kumepelekea kuvunjika kwa
ndoa baadhi, maana wanandoa hao wameoana kwa kuangalia vitu, kazi, mali, sura, kipaji,
mvuto, umaarufu au cho chote kutoka kwa mchumba kama kigezo cha kumvuta na kuiingia
katika mahusiano ya uchumba ili kuifikia hatua na adhima ya ndoa.
Ndoa (kama tasisi) ni takatifu, na Mungu aliasisi ndoa kwa makusudi matakatifu.
Ndoa ya kwanza iliasisiwa na Mungu mwenyewe katika bustani ya Edeni kati ya Adamu na
Hawa (mume mmoja na mke mmoja). Hivyo basi, mchakato mzima wa kumpata mwenzi wa
maisha kunahitaji kumshirikisha Mungu ili akupatie mwenzi mwema wa maisha wa kufanana
nawe. Vijana wa kike na wa kiume wanaotegemea kuingia katika ndoa, wanatakiwa wajue
kuwa, kunahitajika uangalifu mkubwa sana ili kumpata mchumba na mwenzi sahihi wa ndoa.

„A‟ Hadi „Z‟ kwa Mchumba Anayestahili kuwa Mwenzi wa Maisha


Ni vyema kutambua ni kipi cha kuzingatia ili kumpata mchumba anayefaa kuwa mke
au mume mwema katika maisha ya ndoa. Mithali 2:11 inatuambia kuwa: “Busara itakulinda;
Ufahamu utakuhifadhi”. Vipengele vifuatavyo („A‟ hadi „Z‟) vitatoa elimu, busara na
ufahamu ambao vijana wa kike na wa kiume utawahifadhi kwa kufuata hatua zitakazokuwa
za msingi katika kujipatia mwenzi anayestahili kwa ajili ya ndoa yenye furaha, amani na
upendo daima:
Azima ya Kuingia Kwenye Ndoa Itambulike
Azima na nia ya kuingia kwenye ndoa yampasa mtu aitambue. Jambo la kuwa katika
ndoa halikwepeki, muda ukifika wakufanya hivyo yampasa mtu kuazimia kwa dhati kabisa.
Biblia inasema kwenye kitabu cha Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake na wakati

Frank Philemon Karoli


15
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

kwa kila kusudi chini ya mbingu”. Kunuia kwa mtu na kuwa tayari kutamwandaa kisaikolojia
pamoja na kujipanga kwa ajili ya azima hiyo. Kwa namna nyingine, kuingia kwenye ndoa sio
suala la kuigiza wala kujaribu, bali kunahitaji azima ya kuingia kwenye ndoa moja kwa moja.

Bidii ya Kazi
Mchumba anayefaa ni yule mwenye bidii katika kazi na siyo alichonacho, mali
alizonazo, kazi aliyonayo nk. Mtu mwenye bidii katika kutafuta anauhakika wa kufanikiwa,
hivyo mchumba huangaliwa katika kufanya kazi kwa bidii na mipango thabiti kwa ajili ya
kuyatafuta mafanikio kwa njia halali. Mithali 10:4 na Mithali 12:27; mafungu haya
yamesadiki juu ya bidii katika kazi. Kulingana na mfumo wetu wa elimu (miaka 16 na zaidi
hutumika kwa ajili ya elimu toka chekechea hadi chuo kikuu). Kumpata kijana aliyefanikiwa
kuwa na funguo tatu yaani nyumba, ofisi na gari ni nadra sana. Mara nyi watu hupata funguo
tatu uzeeni na umri wa kuoa unakuwa umepita. Hivyo, angalia mchumba aliye na bidii katika
kazi, ili muyatafute maendeleo katika ndoa kwa pamoja.
Hivyo kwa wale wanaotafuta wenzi wenye funguo tatu hasa kwa kijana, yampasa
amtafute mtu mzee, mtu aliyefiwa na mwenzi wake au kwa binti aingie katika ndoa ya
mitara. Mchumba mvivu na tepetevu na asiyejibidisha hafai kuwa mke au mume kwani dunia
ya sasa inahitaji kusaidiana katika kutafuta ili kuyafikia malengo mapema. Huu ni ushauri
wangu mwenyewe, maana uzoefu unaonesha madhara yake. Mfano baba ambaye ni mtafutaji
pindi anapofariki au kupata ulemavu wa kudumu au ugonjwa wa kudumu, familia huyumba
na kusambaratika. Hili jambo lipo hata kwa upande wa wanaume, maana wapo wasiotafuta
wala kujibidisha katika kutafuta hivyo kutegemea mahitaji yaliyo mengi kutoka kwa wake
zao (ambapo sio salama pia).
Chunguza Tabia
Kipengele hiki ni nyeti sana maana ndipo kiini cha mchumba anayefaa kuwa mke au
mume. Kipengele hiki kinabeba muktadha mzima wa mchumba mwema atokaye kwa
Mungu. kupitia tabia ndipo unaweza kupata mke mwema. Wasifu wa nje wa mtu kuutambua
ni rahisi sana kuliko wasifu wa ndani wa mtu; vivyohivyo tabia za ndani na tabia za nje kwa
mchumba. Ukikosea kuchunguza tabia ya mchumba katika kipindi cha urafiki, ni vigumu
kuzibaini tabia katika uchumba maana atazificha ili kulifikia lengo la kuolewa au kuoa.
Tabia ni sawa na ngozi, kuibadirisha ni vigumu sana (Yeremia 13:23). Usijipe moyo
kwa kusema na kufikiri “ngoja anioe au nimuoe kisha nitambadirisha tabia yake”. Japo pia
mwenye uwezo wa kumbadirisha mtu tabia ni Mungu, hivyo itahitaji maombi mengi na ya
dhati kwa kumuombea mchumba au mume au mke. Mafungu yaliyo katika Mithali 7:10-12,
Mithali 11:16 na Mithali 12:4 yanaeleza juu ya tabia bainishi zinazofaa na zisizofaa kwa mtu
anayemwabudu na kumcha Mungu wa mbinguni. Kuna aina kuu mbili za tabia na mfano
wake ni:
1. Tabia zinazojipambanua kwa nje: Tabia za nje zinajipambanua katika matumizi ya
ulimi wakati wa kuongea, mitindo au aina za mavazi anazo pendelea kuvaa (Mwanzo 3:7,
Kumb 22:5, 1pet 3:1-6), kujipamba kwake kwa sura au mwili na manukato (Hosea 2:13,
Wimbo 1:3, Ezekiel 23:40), vyakula na vinywaji apendeleavyo (Mithali 23:20-21). Tabia zote
za nje kuzibaini hazihitaji muda mrefu sana, mfano, si vigumu kumbaini mtu mchafu au
msafi.

Frank Philemon Karoli


16
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

2. Tabia zinazojipambanua kwa ndani: Tabia hizi hazionekani kwa urahisi maana ni
za ndani mno; mfano wa hizo ni wivu, upole, uchoyo, kutojali, dharau, mtazamo kwa kutaja
baadhi. Tabia za ndani huchunguzwa kwa muda mrefu sambamba na matendo ya huyo mtu.
Warumi 3:12 imezungumzia tabia njema zinatakiwa kuwa hata za moyoni. Ubainishaji wa
tabia hizi juu ya mtu, kunahitaji kiwango na ujuzi mzuri wa saikoloji. Kubadilika kwa tabia
hizi za ndani kunahitaji uwezo wa Roho Mtakatifu na utayari wa mtu baada ya kugundua
udhaifu na mapungufu yake.
Dini au Dhehebu
Dini au dhehebu katika mahusiano ni kipengele cha kuzingatia na kutilia maanani
zaidi. Inapendekezwa kuwa, wale wanaotarajia kuwa wenzi ni vyema ukawepo ufanano wa
dini au dhehebu. Kila dini na dhehebu kuna mafundisho yake (doctrines) ambayo
yanapishana kutoka dhehebu au dini moja kwenda dhehebu au dini nyingine. 1Wakorintho
1:10 na 1Wakorintho 1:12; aya hizi zinatoa umuhimu na faida za wanandoa kuwa wenye dini
au dhehebu moja, maana hawatapishana katika misingi ya mafundisho bila kuwagawanya
watoto katika imani za mafundisho. Ukitaka familia iwe chini ya kiwango katika mambo ya
kiroho, jaribu kuchanganya dini mbili tofauti miongoni mwa wanandoa katika ndoa.

Elimu
Kuna elimu ya kweli ambayo inahusu uelewa na maarifa juu ya Mungu wa kweli wa
mbinguni na elimu ya kidunia ambayo tunaipata shuleni kupitia mitaala ya masomo
mbalimbali. Nitazungumzia juu ya elimu ya kidunia ambayo inaweza ikaleta utofauti kwa
wachumba watakapo kuwa katika maisha ya ndoa. Inashauriwa kuwa wachumba
wanaotarajia kuoana wasipishane sana viwango vya elimu au walingane viwango vya elimu
ili kuleta uwiano katika mitazamo, uelewa na tafakari.
Sanjali na viwango vya elimu kuwiana au kutotofautiana, kigezo cha elimu lazima
kipewe nafasi ili kila mmoja kati ya wachumba kuridhia wao kwa wao, endapo mmoja hajui
kusoma wala kuandika au hajaenda vidato katika elimu. Suala la elimu pia laweza kutatuliwa
kwa wenzi kukubaliana katika kuendelezana katika masuala ya elimu. Mafungu yafuatayo
yanaelezea juu ya elimu ya kweli na elimu dunia: Mithali 4:13, Waefeso 5:22 na Esta 1:22.

Familia Atokayo (Historia yake)


Suala la ufahamu wa historia na familia anayotoka mchumba ni vyema kuifahamu
bayana na kujiridhisha kwayo. Kuifahamu familia anayotoka mchumba ni jambo jema sana,
kwani itasaidia kujua endapo kuna magonjwa ya kurithi, malezi mabaya na tabia mbaya za
wazazi au walezi wa mchumba ama sivyo. Mara nyingi tabia ya wazazi au mzazi (walezi au
mlezi) hubainisha tabia ya mchumba, hususani binti kama anavyoelezwa katika Ezekieli
16:44.
Mafungu mengine yanayoelezea juu ya umuhimu wa kuijua historia ya familia
anayotoka mchumba ni Hosea 2:4-5 na 2Samweli 13:8-12. Yapo matendo yaliyofanywa na
wazazi na kupelekea matokeo yake kuendelea kuandama vizazi vinavyofuata (Kutoka 20:5)
hivyo ni bora kujiridhisha kabla ya kuoa au kuolewa.

Frank Philemon Karoli


17
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Gharama ya Mahali kwa Mchumba


Kila jambo halikosi kuwa na gharama aidha muda au pesa. Zipo gharama kwa
mchumba, hivyo ni vyema (kijana wa kiume) akazitambua ili kujua endapo atazimudu ama
sivyo. Ipo gharama kubwa ambayo huwa inawakabili vijana wa kiume ni lazima aipitie ili
kuifikia hatua ya kumuoa mchumba aliyempata.
Gharama hiyo huhusisha mahali pamoja na viambata vya zawadi (Mwanzo 24:48-53).
Suala la mahali linatofautiana tamaduni na tamaduni, sehemu na sehemu, imani moja kwenda
imani nyingine.
Nionavyo mimi: ifike wakati Wakristo tuachanane na suala la mahali ili tuepukane na
tamaduni katika mchakato wa ndoa. Mahali sio kitu kizuli maana taratibu zake zimejaa
upagani mwingi. Suala la mahali kuwa ghali, limekuwa kikwazo kikubwa katika jamii ya
Wikristo hususani kwa kusababisha vijana wasioane; hivyo, vijana kuoana bila kufuata
taratibu za Kibiblia, mabinti kutoolewa na mwisho wa siku kuzaa watoto nje ya ndoa aidha
wakiwa bado nyumbani kwa wazazi wao.
Aidha, kwa upande wa kijana wa kiume lazima aangalie gharama za maisha ya binti
kulingana na familia anayotoka ili kujua kama ataweza kumhudumia katika ndoa. Zipo
familia ambazo zipo vizuri kimaisha (kiuchumi), hivyo kunamaisha ya hali ya juu ambayo
mtoto wa kike amekuwa akiyaishi na kila alichohitaji alikipata. Kijana anaetarajia kuoa binti
atokaye katika familia tajiri lazima ajiandae kumhudumia kama alivyokuwa akiishi nyumbani
kwao. Kwa mtazamo wangu, pesa sio tiba ya kuleta upendo bali upendo wa dhati unatoka
moyoni mwa mtu husika. Soma Mithali15:16-17.

Hiari ya Mchumba Kuishi Naye


Upendo wa kweli hauhitaji shuruti wala kulazimisha, bali upendo huandamana na hiari
juu kuridhia toka moyoni. Hivyo, mchumba ni vyema akakubali yeye mwenyewe ili kuingia
ndani ya ndoa. Uhuru katika kukubari hakuleti majuto hapo baadae ndani ya ndoa, maana
mtu ameamua mwenyewe. Sio salama sana kutumia ushawishi wa kipesa, mali au misaada yo
yote ili kutengeneza mazingira ya mchumba kukubali, kwa sababu vitu au pesa vyaweza
kuwa mvuto bandia badala ya upendo wa kweli kutoka moyoni.
Rushwa yenye ushawishi katika uchumba si jambo jema, maana hapo baadae kwa
wenzi, kunaweza kukatokea upungufu au ukosefu wa upendo wa dhati ndani ya ndoa.
Kunajambo zuri la kujifunza katika Mwanzo 24:54 ambapo Rebeka alihiali yeye mwenye
kwenda kuungana na mume wake baada ya kutolewa zawadi na mahali.

Imani
Kipengele hiki ni sawa na kile kipengele cha dini au dhebu, lakini kinautofauti kidogo.
Suala la imani nalo ni jambo nyeti sana sawa sawa na kile kipengele cha dhehebu au dini juu
ya umuhimu wa wachumba kufanana kwa dhehebu au dini kabla ya kuoana. Yapendeza
wachumba wanaotaka kuoana wawe wa imani moja, maana kutofautiana imani huzaa
migogoro katika ndoa.
Zipo imani ambazo huruhusu kula vyakula vyote, kuoa na kuacha (kutalakiana),
kunywa pombe, kuoa wake wengi na kuvuta sigara, hivyo mwingine akiwa na masharti
katika hivyo vipengele, kutaleta migogoro mikubwa ndani ya ndoa. Sambamba na hayo, hata

Frank Philemon Karoli


18
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

taratibu za ibada kupisha kati ya imani moja na nyingine kwa wenza husababisha makwazano
miongo mwa wanandoa.
Suala lingine la msingi katika imani ni juu ya kiwango cha kiroho cha mchumba.
Inapotokea wachumba ni wa imani moja, suala la kiwango cha kiroho (imani) kwa mchumba
lafaa kuzingatiwa pia ili hapo baadaye wachumba hao watakapooana waweze kuwa na
familia yenye kiwango kizuri cha kiroho pamoja na malezi mazuri ya kiroho kwa watoto
wao.
Sio salama pia kutumia silaha ya kumtangazia mtu (mchumba) kuwa nitaolewa au
nitakuoa wewe endapo utabadiri imani yako na kuja kwenye imani yangu; kwa sababu
mchumba aweza kukubali kubadiri imani yake ili aolewe au kuoa kwa sababu ya kukidhi
hitaji lake na siyo kwa kuikiri imani.
Kitabu cha 1 Wafalme 11:4 kinasema hivi: “Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee,
wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa
mkamilifu kwa BWANA Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.” Ni vyema
wachumba wanaotarajia kuoana wawaze pamoja, wanuie pamoja, watende pamoja, waamini
pamoja katika imani ili kuondoa mpasuko hapo badae wawapo kwenye ndoa yao.

Julisha Wazazi
Uchumba wa Yusufu na Mariam ulitambulika nyumbani kwao na jamii
inayowazunguka. Wakati mwingine hata urafiki utambulike kwa wazazi ili wazazi nao
wapime uaminifu wa rafiki huyo kama ilivyotokea kwa Musa (Kutoka 2:16-21). Wachumba
wanaotarajia kuoana ni vyema wakazijulisha pande zote mbili za wazazi wao ili kuweka
uwazi na kulinda uchumba wao ili kuepuka usaliti kama ambavyo wangekuwa wawili kwa
uchumba wa siri.
Huwa ni moja ya heshima kubwa sana kwa wazazi kujulishwa juu ya uchumba wa
binti au kijana wao endapo amefikisha umri wa kufanya hivyo ili nao wapate ya kushauri au
kutoa baraka zao kwa ajili ya hatua nyingine kuelekea katika ndoa.

Kasoro Alizonazo Mchumba Zibaini Mapema


Kubaini kasoro alizonazo mchumba ni vyema na ni vizuri ili kujipima kama zitaweza
kuvumilika au kubadirika kama ni za kufanyiwa mabadiriko haraka kabla ya kuamua kuingia
kwenye ndoa. Biblia inamzungumzia Lea kasoro yake ya kuwa na makengeza lakini Yakobo
alimkubali kwa kasoro yake hiyo (Mwanzo 29:17). Lea huyo huyo mwenye kasoro na
asiyependwa alibarikiwa kupata mtoto mapema kuliko “Raheli”. (Mwanzo 29:31).
Hakuna mtu ambaye hakosi kasoro, labda awe malaika. Lakini, ni vyema kufahamu
kuwa; kasoro ambazo sio za kimaumbile bali ni za kitabia huachwa na si za kuvumiliwa.
Ukizibaini kasoro zako pia yakupasa kuziacha.

Linganisha Umri Wenu


Nionavyo mimi: jambo la msingi kutambua katika umri; wanawake hukomaa kiakili
mapema, kuliko wanaume; lakini pia wanawake hukua kiumbo haraka, lakini hawazeheki
mapema, bali wanaume hawakui haraka ila huzeeka mapema. Hivyo basi ni vyema
mwanamke awe chini kidogo ya umri wa mwanamume kutokana na kukua kwao haraka.

Frank Philemon Karoli


19
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Ulinganifu wa kiumri ni mzuri ili kubaini umri sahihi wa kuzaa pamoja na kuweza
kusimamia majukumu ya kifamilia. Kiafya inashauriwa kuwa, mwanamke asiendelee kuzaa
afikishapo umri kati ya miaka 34 hadi 36, hivyo ili mwanamke aweze kuzaa watoto watatu
wenye kutofautiana miaka mitatu; akichelewa sana mwanamke aanze kuzaa akiwa na umri
wa miaka 25 hadi 26 ili ukijumlisha miaka tisa ya tofauti ya watoto watatu, hivyo atakoma
kuzaa akiwa au kabla ya miaka 36. Jambo la kusisitiza ni kuwa si wote wanaoweza
kutendewa miujiza kama Sara alivyo zaa katika umri wa uzee (Mwanzo 17:17).
Sio vizuri pia kwa mwanamume kuchelewa kuoa, maana haipendezi kulea watoto
katika umri wa uzee, hivyo angalau mtu akichelewa sana miaka 32 awe ameoa. Sanjali na
hayo, kwa mtazamo wangu: umri wa miaka 18 hadi 25 kwa wanawake huwa ni umri wa
mabadiriko makubwa ya kimaumbile, na wengi wao hunenepa kutoka umbo la awali kwa
sababu ya mabadiliko ya kihomoni na maumbile. Umri wa miaka 25 na kuendele ndio umri
sahihi wa kutambua umbo la mwanamke maana atakuwa amepitia hatua zote za mabadiriko
ya kimakuzi.
Miliki Alizonazo Mchumba Zitambulike
Vijana wengi huwa hawana mali kwani huwa katika hatua za utafutaji wa mali.
Endapo kuna mali au miliki aidha za kurithi au kupewa na ndugu au jamaa; kunatakiwa
kuwepo ukweli na uwazi kwa wachumba juu ya mali na miliki walizonazo kwa kila mmoja
kabla ya kuoana.
Kukosekana kwa uwazi juu ya miliki au mali alizonazo mchumba kwa weza sababisha
kutoaminiana endapo siku moja miongoni mwao katika ndoa atabaini kuwa hakuwekwa
wazi. Kumficha mchumba juu ya miliki na mali hupelekea kupotea endapo mmoja atafariki
ghafla wakati wawapo katika ndoa. Uwazi wa miliki utawaweka huru wachumba wote
wanaotaka kuoana hapo baadae ili kurahisisha mipango ya maendeleo yao mapema.
Wakati mwingine mali alizonazo mchumba hujulikana bila hata kumuuliza mhusika,
kama ilivyokatika kisa cha kitabu cha Ruthu, ambapo Ruthu alitambua mali za Boazi kwa
kumuona katika usimamizi wa hiyo miliki yake (Ruthu2:3-4). Jua kuwa: Boazi alikuwa mzee
katika umri, hivyo mali zake alikuwa amezitafuta tangu enzi za ujana wake, hivyo ni tofauti
na vijana wengi ambao huwa hawana mali, kwani huwa katika mchakato wa kutafuta mali.

Ndoto za Mchumba Katika Maisha Yake


Kila mwanadamu aliye na akili timamu na mwenye uwezo wa kufikiria japo hata
kidogo huwa hakosi kuwa na ndoto za maisha anazotarajia kuzitimiza katika kipindi cha
muda fulani ndani ya maisha yake. Ni vyema ndoto za wachumba zibainike kwa kila mmoja,
ili waweze kuona namna na jinsi yakuweza kuzitimiza aidha ndani ya ndoa au kabla ya ndoa.
Aidha, mmoja wao kati ya wachumba anaweza akawa na mpango wa kufikia kiwango
fulani cha elimu, mfano shahada ya kwanza katika taaluma fulani ndipo aoelewe, hivyo ni
vyema mwingine kuvuta subira ili lengo la mchumba wake litimie katika ndoto ya maisha
yake. Endapo itakuwa ni vigumu kusubiri, basi huyo asiyeweza kusubiria amuache mchumba
wake na awe huru kutafuta mwingine aliyetayari kuingia katika ndoa bila kupoteza muda
mwingi.
Onesha Hali Halisi ya Maisha Yako
Kitendo cha kuonesha hali halisi ya maisha hata kabla ya uchumba na ndani ya
uchumba ni jambo jema na salama sana. Inawapasa wachumba kuepuka maisha ya kuigiza

Frank Philemon Karoli


20
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

tofauti na jinsi walivyo, maana ni mojawapo ya udanganyifu na huleta migogoro hapo


baadaye katika ndoa. Unakuta kijana anaazima gari, nguo ili aonekane ni wa maisha ya juu
sana na kushawishi wale wa karibu yake waone kuwa ni mtu wa maisha mazuri.
Ukiazima gari, eleza kuwa umeazima na kuazima nguo kumepitwa na wakati na
hakufai kabisa. Kitendo cha kuigiza hali ya maisha yasiyo Ruthu alikishinda, zaidi alionesha
hali ya maisha yake jinsi yalivyo toka moyoni hadi nje ya maisha aliyokuwa akiyaishi;
angalia Ruthu 1:16-17, Ruthu 3:10. Esta naye katika nchi ya ugenini pia naye alifanya vivyo
hivyo hadi kupata fursa ya kuolewa na mfalme, maana mabinti wengi walienda kwa
kujipamba, kuvaa vito na mavazi ya thamani sana wakati siyo hali ya maisha yao; Esta yeye
alienda jinsi alivyo (Esta 2: 15-17).
Tabia ni uchaguzi mtu anaweza akaibadirisha endapo akinuia kufanya hivyo kwa
dhati. Vijana wa kiume na wakike yawapasa kuishi katika kweli na ukweli mtupu ili ukweli
uwaweke huru. Katika uchumba wamo matapeli wengi sana, ndiyo maana wengi huumizwa
sana punde ibainikapo kuwa mchumba huyo sivyo alivyokuwa akimdhania na kujitumainisha
kwake.
Pima Uaminifu wa Mchumba
Uaminifu hauwezi ukaondolewa na mazingira, sababu fulani wala changamoto
inayomkabiri mchumba. Kuanza uhusiano (kuoa na kuolewa) na mtu ambaye
hujajihakikishia upendo na uaminifu wake juu yako ni kujipalia moto hapo badae; maana
wapo ambao huanzisha mahusiano na mtu fulani kwa kutimiza haja zao za matamanio au
kuchuma kitu fulani kwa huyo mtu.
Kwa wale wanaoelekea katika safari ya maisha ya ndoa na ambao bado wanatafuta;
kipindi salama cha kumchuguza tabia mtu, ni kipindi cha urafiki na kidogo kipindi cha
uchumba. Kijana wa kiume akimtamkia binti kuwa anataka kumuoa (yaani awe mchumba),
matarajio ni kuwa, huyo binti ataficha tabia ake mbaya alizonazo ili aolewe. Vivyo hivyo
kwa binti anapomkubalia kijana wa kiume kuingia naye uchumba, ategemee pia kijana huyo
atazificha tabia zake mbaya ili aweze kufanikisha kumuoa. Wote hao; kijana wa kie na wa
kiume wakifika kwenye ndoa hujibainisha tabia zao zote mbaya, ambapo kuzirekebisha
kunahitajika hekima ya kimbingu ya wanandoa na Mungu aingilie kati.

Ruhusa ya Wazazi
Ruhusa toka kwa wazazi huwa ni jambo la msingi sana kwa wachumba ili kuweza
kuoana. Mbaraka wa wazazi ni bora na mhimu kwa wachumba katika safari ya kuoana na
kuanzisha familia. Tena ni vyema pande zote za wazazi zikaridhia ili wachumba kuendelea
na mchakato wa kufanikisha ndoa. Kuridhia kwa wazazi hutengeneza upendo kila upande wa
wazazi wa wanandoa katika familia (soma Mwanzo 29:21-23).
Japo kunawakati pia wazazi hupinga kulingana na mila, wakati mwingine utashi wao
au imani, hivyo mtii baba na mama katika misingi ya Kibiblia na sio misingi iliyo nje na neno
la Mungu. Hekima ya wachumba katika kushauri itumike pale inapoonekana kuwa wazazi
hawako sahihi kwa yale wanayolazimisha kulingana na neno la Mungu linavyo elekeza, na
pia mazuri yaliyo mema ya wazazi wachumba wayafuate na kuyatii.
Samsoni mnadhiri wa Mungu alipingwa na wazazi wake kwa jambo jema kabisa; yeye
mwenyewe alikengeuka kwa utashi wake mwenyewe. Ukisoma Waamuzi 14:1-4 inaonesha
kuwa wazazi wake Samsoni walimpinga kwa ombi lake baya. Maamuzi yake Samsoni

Frank Philemon Karoli


21
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

yalikuwa kinyume na imani kama mnadhiri wa Mungu hivyo ilimgharimu mateso na hadi
kifo akiwa mateka katika himaya ya Wafilisti waabudu miungu.

Sura na Umbo la Mchumba


Ni vyema kuchagua mchumba utakayempenda daima wakati wote wa maisha ya ndoa
kwa kuzingatia uzuri wa tabia kwanza na uzuri wa umbo. Kila mtu ni mzuri kwa asili yake,
kulingana na muonekano wa nje au tabia za ndani. Biblia inazungumzia sana uzuri wa asili na
uzuri wa tabia na sio uzuri wa kununua au mapambo ya gharama na vito vya thamani. Katika
lugha yetu ya Kiswahili ni vyema ukatofautisha uzuri na urembo au ulimbwende.
Uzuri ni wa asili, urembo au ulimbwende ni mapambo na muonekano wa mavazi
katika mwili. Japo uzuri na urembo huenda pamoja na huwezi ukautofautisha kwa uharaka;
maana wapo wazuri kwa sababu ya mapambo na mavazi, na wapo wabaya kwa sababu ya
kukosa mapambo na mavazi nadhifu.
Soma mafungu yafuatayo: Esta 1:19 inazungumzia ukarimu, Mwanzo 26:7
inazungumzia uzuri wa Rebeka, Wimbo 2:14 inazungumzia uzuri wa umbo na sauti,
Wimbo1:15 inahusu uzuri wa mwanmke, Wimbo 5:10 inasifu rangi na umashuhuri na Esta
2:7 inasadiki uzuri wa sura na tabia njema.

Tamaduni Zisitofautiane Sana


Suala la tamaduni huleta changamoto na tofauti nyingi sana na hupelekea kutokea kwa
migogoro katika ndoa; hivyo ni vyema pia kwa wachumba kabla hawajaoana lazima
waliangalie hili ili lisije likawa changamoto aidha wao kwa wao au kutoka kwa ndugu zao
(angalia Mwanzo 28:2 na Waamzi 14:1-3). Kwenye Biblia hasa agano la kale, suala la
utamaduni limejitokeza katika mgongo wa imani kama inavyotanabaishwa katika mafungu
tajwa hapo juu. Agano jipya halitilii sana mkazo wa tamaduni bali imani.
Endapo Imani ni moja, suala la utamaduni halipo. Hakuna tamaduni iliyobora kuliko
nyingine, isipokuwa ni mitindo tu ya maisha ndiyo huleta tofauti ya tamaduni moja na
nyingine. Watu wa imani moja si sawa kulishupalia suala la utamaduni maana huleta
utengano na ubaguzi. Kwa sasa kutokana na kuingiliana, kuoleana na msingi wa utamaduni
wetu upo juu ya tabia ya Yesu Kristo; tamaduni zetu hazina nafasi tena, bali hoja ya msingi ni
imani hazitakiwi kutofautiana kama ilivyonenwa katika Mwanzo 24:3-4.

Ukarimu na Uvumilivu wa Mchumba


Kipengele hiki kitamhusu sana mwanamke na kiasi mwanamume, maana mwanamke
ndio muhimili mkuu wa familia japo baba ndiye kichwa cha familia. Mwangalie mchumba
wako Je, anaweza kuvumilia katika shida bila kusaliti anapoishiwa? Mwanamke katika ndoa
na familia yake, awe na moyo wa ukalimu, huruma, kutoa na kusaidia wengine walio wahitaji
(soma Mithali 31:20). Baadhi ya wanawake wana roho mbaya na hawana hata tone moja la
ukalimu na moyo wa kusaidia wengine; wakati mwingine huwabagua wale wasio wa upande
wa familia yake (suala hili lipo hata kwa wanaume pia).
Mwanamke anayemcha Mungu ni sehemu ya kimbilio na msaada kwa jamii na
wanafamilia wanaomzunguka. Moyo wa kutoa, kusaidia wahitaji na masikini pamoja na
kuwakalimu wageni ndizo funguo za baraka ya familia. Roho mbaya na ukali hukimbiza
wageni katika familia, na kupelekea kufunga milango yote ya baraka kutoka kwa Baba wa

Frank Philemon Karoli


22
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Mianga. Mwanamke mwanandoa mtarajiwa lazima ajenge tabia ya kuvaa viatu vya matatizo
ya wengine, ahurumie na kukumbuka kuwaombea walio katika shida na changamoto.
Mwanamke ambae ni mke mtarajiwa yampasa kuwa mwangalifu ili kujipatia mume
mwenye tabia njema. Katika 1Samweli 25:1-42, mtumishi wa Mungu Daudi alipanga
kumwangamiza Nabali kwa sababu ya kukosa hekima ya maneno na fadhira juu ya yale
Daudi aliyomtendea katika kumlindia mifugo yake, lakini Abigaeli mkewe Nabali
alijishusha kwa Daudi; kwa kutumia hekima na maneno mazuri alifanikisha kumuepushia
mumewe na upanga wa Daudi.

Vumilia Mapungufu Aliyonayo Mchumba Ikiwezekana


Kama tulivyoona kwenye kipengele cha kubaini kasoro za mchumba, kuwa hakuna
mwanadamu aliyekamilika asilimia mia. Ukimpata asiyekuwa na kasoro au hana mapungufu,
tegemea malaika pekee na ambapo hapa duniani hayupo. Yapo mapungufu mengi ambayo
yanaweza kujipambanua kutokana na silika ya dhambi kwa mwanadamu. Mapungufu hayo
yanaweza kuwa yaliyo katika nyanja kuu mbili, yaani mapungufu yatokanayo na wasifu wa
nje (mapungufu ya kimaumbile) na mapungu yatokanayo na wasifu wa ndani (matendo ya
kiroho zaidi, mfano uchoyo, hasira, kiburi n.k).
Suala la kumvumilia mchumba kutokana na mapungufu yake ni kanuni ya kimbingu
kama jinsi Mungu anavyotuvumilia kwa hali ya juu. Kuvumilia pekee hakutoshi, bali
muombee, mwelekeze kwa upole na kumfundisha kwa moyo wa upendo. Kwa mtazamo
wangu; tabia ni uchaguzi tofauti na kalama ambapo Mungu humpatia mtu.
Mungu anasehemu kubwa sana ya kutubadirisha kuliko tunavyoweza kufikiri na
kufanya kwa uwezo wetu. Tukimshirikisha Yeye aweza kutubadirisha na kuwa nuru au
chumvi ya ulimwengu. Mungu alimbadirisha Petro, Paulo; hivyo tukimwomba kwa nia ya
dhati atatubadirisha au kubadirisha tabia ya mchumba usiyoipenda.

Wasilianeni Mara kwa Mara


Kuwasiliana ni mojawapo ya kanuni inayoweza kufanikisha kudumu kwa uchumba
endapo wawili miongoni mwa wachumba wako mbali kimazingira. Kuwasiliana mara kwa
mara kunasaidia kujenga uhusiano na kutambuana mapungufu au matatizo, hata kukuza
upendo wa wachumba. Uchumba waweza vunjika kwa sababu ya kukosekana kwa
mawasiliano ya karibu na ya mara kwa mara.
Bila mawasiliano kutokana na umbali, mchumba anaweza kumsahau yule wa mbali
endapo atajitokeza anayeonesha kujari kwa ukaribu na kumjulia hali au kuzungumza naye
mara kwa mara. Zipo njia nyingi za kuwasiliana kwa ulimwengu wa sasa; kuwasiliana kwa
weza kuwa katika kuombeana, kuwasiliana kwa kutumia simu, barua kwa njia ya posta, barua
pepe na mitandao ya kijamii.
Mfumo wa maisha wa sasa haulingani na mfumo wa maisha ya babu zetu wa zamani,
vivyo hivyo uvumilivu na uaminifu bila kuvunja uchumba kwa hivi sasa hauwezekani kwa
sababu ya kukosa mawasiliano kwa dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia. Kuwasiliana
kunakumbusha kutunza ahadi ya wachumba ili kulifikia lengo lao la kuoana. Kuwasiliana pia
kunaonesha upendo katika kumjali mchumba ili aonekane kuwa ni wa thamani, pamoja na
kutiana moyo ili kuvishinda vishawishi.

Frank Philemon Karoli


23
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Yakinisha Pendo la Mchumba


Kwa mujibu wa 1Wakorintho 13:4-13; upendo ni uwazi, upendo ni uvumilivu, upendo
hauchoshi, upendo huwafanya wapendanao kubebeana matatizo na shida, upendo ni furaha,
hivyo upendo haujifichi. Ni vyema mchumba akaangalia nakuchunguza kweli ya upendo wa
mchumba wake. Mchumba aliye na upendo wa kweli, atamuweka mchumba wake kama
muhuri moyoni mwake. Katika kitabu cha
Waamuzi sura ya 16, upendo wa Delila kwa Samsoni haukuyakinisha upendo wa
kweli ukiachana na suala la uzinzi na uasherati kabla ya ndoa. Upendo wa Adamu kwa Hawa
ni upendo wa kuigwa kwa wachumba (ila si kwa kumuasi Mungu kama alivyofanya Adamu).
Kisa hiki cha Hawa na Adamu wengi hukichukulia juu juu; unajua haikuwa rahisi sana kwa
Adamu kufanya kosa la kula tunda alipoletewa na Hawa. Adamu alikubali kula tunda kwa
sababu ya upendo kwa mke wake, kuwa asiangamie peke yake (Mwanzo 3:6).
Tufanye nini maana Yesu ameturejeshea kile tulichokipoteza kutoka kwa wazazi wetu
kwenye bustani ya Edeni maana ni upendo mwingine waajabu wa agape, Yesu kukiacha kiti
chake cha enzi ili atufie siye tusiostahili. Hivyo, upendo ulilipwa kwa upendo wa juu zaidi.
Naamini kuwa; kuoa au kuolewa na mtu usiyempenda kwa dhati toka moyoni hupelekea
migogoro katika ndoa na kuingia katika dhambi ya kuchukiana na kuishi kwa kuvumiliana.

Zuia Kufanya Ngono Kabla ya Ndoa


Uchumba wa Yusufu na Mariamu ulikuwa katika kanuni ya kujizuia kufanya ngono
hadi ndoa itakapofungwa. Mariamu alikuwa bikira safi hakuwa ameguswa na mwanamume,
na Yusufu alijua kanuni ya uchumba kuwa kufanya ngono nje ya ndoa ni kujichumia dhambi
ya uzinzi (Mathayo 1:18-24 inaleza kisa chote). Kumekuwepo na ushawishi mkubwa wa
utandawazi na makundi rika yanayoharibu maana ya uchumba, kwa kusababisha vijanawengi
kufanya ngono kabla ya ndoa, hivyo kushiriki dhambi ya uzinzi.
Mwonja asali haonji mara moja, akionja huchonga mzinga daima. Samson alionja
mara moja na ikabidi ajenge mzinga (Waamuzi 16:1, na Waamzi 14:7). Thamani ya
mwanamume au mwanamke hupotea kwa mchumba wake endapo wachumba hao watakutana
kimwili kabla ya ndoa. Kuruhusu ngono kabla ya ndoa husababisha uchumba kuvunjika,
maana ile shauku ya kuoana hupotea kwa sababu wachumba wameshajuana tayari, hivyo
hufanyika mchakato wa kutafuta mchumba mpya.
Ngono kabla ya ndoa husababisha maambukizi ya magonjwa ya zinaa, mimba za nje
ya ndoa, au kuwa na watoto wengi kwa baba au mama tofauti. Nivyema wachumba wakawa
waaminifu hadi ndoa ifungwe ili washiriki zawadi yao kwa uhuru.
Wataalamu wa mahusiano katika misingi ya Kibiblia, hawashauri uchumba uzidi
mwaka mmoja kama hakuna kipingamizi kwa wachumba kuoana. Uchumba wa muda mrefu
mara nyingi huvunjika, au husababisha wachumba kufanya ngono babla ya ndoa. Jambo hilo
husababisha upendo kupungua au kutoweka kwa sababu Shetani anakuwa ameweka himaya
yake, na kupelekea uchumba uvunjike.
Ndoa ni takatifu, ndoa ni kielelezo cha uhusiano wa mwanadamu na Mungu, au
Mungu na kanisa, hivyo ndoa iheshimiwe na watu wote. Shetani huharibu utukufu wandoa ili
afanikishe kuharibu familia, kanisa na jamii kwa ujumla; hivyo, yawapasa wachumba kuwa

Frank Philemon Karoli


24
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

waangalifu daima katika hatua zao za uchumba, na haina haja ya kuchelewa kuoana kama
hakuna kipingamizi cha kuwachelewesha.

Sababu Zipelekeazo Vijana Kuangukia Katika Uchaguzi Mbaya wa Wenzi


Kufanya uchaguzi mbaya ni jambo ambalo halitokei ghafla au kwa bahati mbaya. Ni
jambo la mchakato mrefu na sio suala la usiku mmoja. Zifuatazo ni hatua ambazo vijana
huzipitia kisha kuingia katika matatizo ya kujipatia mwezi asiye mwema na asiye bora:
1. Kuwa katika makundi yasiyofaa yenye ushauri mabaya (Zaburi 1:1 na 1Wakorintho
15:33): Kwa kijana ye yote wa kike au wa kiume hawezi kujipatia mwenzi anayefaa kama
ushauri wa kuchagua mwenzi anaoupata unatoka kwa kundi baya lisilokuwa na mwelekeo
mzuri hivyo kijana ataangukia katika uchaguzi wa mwenzi asiyefaa.
2. Kukosa msimamo wa kifikra na hekima itokayo kwa Mungu (Mithali 1:7): Kijana
hawezi kujipatia mwenzi mwema endapo hekima na maagizo ya Mungu atayaweka kando.
Moyo wa mwanadamu ni mdanganyifu bali hekima za BWANA ni adiri kwa mwanadamu,
hivyo kijana atumiaye utashi wake bila kumshirikisha Mungu, ataangukia katika uchaguzi wa
mwenzi asiyefaa.
3. Kumtafuta mwenzi katika mazingira yasiyo sahihi (Mithali 7:8): Kosa kubwa
lingine wanalofanya vijana ni kumtafuta mwenzi wa maisha katika mazingira yasiyo sahihi.
Huwezi ukajipatia mwenzi mwema katika mazingira ya disko, baa na kwenye madanguro na
ukajisifia kuwa umepata mke mwema kutoka kwa BWANA.
4. Kumtafuta mwenzi wa maisha katia muda usio sahihi bila kujali maelekezo (Mithali
7:9): Si salama kujipatia mwenzi aliyemzururaji wa usiku, maana tambua hata malezi ya
kwao anapoishi hayako vizuri kwani mzazi aliyemcha Mungu hawezi kumruhusu mwanae
atembee hadi usiku wa manane. Kijana yampasa kujua kuwa ni wakati upi anapomtafuta
mwenza wake wa maisha, hasa kwa kuzingatia wakati, muda, mazingira, hali na utashi.
5. Kutojua viashiria vya mke au mume mwema na mbaya (Mithali 7:10): Kuna msemo
maarufu wa Kiswahili siku hizi unaoonesha mshangao kuwa: “hivi kweli kusoma hujui hata
picha kutazama napo huoni!”. Mwenzi aliye mwema na mcha Mungu au anayejiheshimu
utamtambua kutokana na kauli katika mazungumzo na mavazi au jinsi anayopendelea kuvaa.
Si salama kujipatia mwenzi anayevaa mlegezo masaa yote au anayevaa nguo zinazoonesha
maungo yake yote ya mwili; maana uvaaji huo unasadifu jinsi alivyo na hatakuwa mlezi
mzuri wa watoto katika misingi ya maadili mema.
6. Kujitafutia mwenzi pale adui-Shetani ameshajiwekea mitego yake (Mithali 7:13-15,
Mathayo 24:4, Mathayo 11:24): Sio salama kujipatia mwenzi ambapo Shetani ameshaweka
mizizi. Usitegeme kupata mwenzi mwema katika ndoa endapo mtu huyo ni mshirikina,
muasherati, mdanganyifu, mwizi, jambazi na anayekushawishi mzini kabla ya ndoa.
7. Kuvutiwa na vitu na siyo pendo lenye wema (Mithali 7:16-18): Vijana wengi
wanajikuta wamekosea kuchagua wenzi kwa sababu wanahadaika na sura, umbo, kujipamba
na mali au vitu alivyonavyo mtu. Vijana wengi wamehadaika na kudanganyika kwa sababu
ya vizawadi na misaada wanayopewa kisha kukubali kuingia kwenye ndoa kwa tamaa na
kudanganywa kwao na sasa wanalia na kusaga meno na majonzi kwao hayakomi.
8. Kuhararisha dhambi (Mithali 7:19-20): Vijana wanakosea kujipatia wenzi wema
kwa sababu ya kuipamba dhambi ili ionekane kuwa siyo dhambi. Kuongoa kwa kuoa
wakisema wanafanya uinjilisti na kuzini kabla ya ndoa wakisema wasije wakauziwa mbuzi

Frank Philemon Karoli


25
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

kwenye gunia. Vijana wanajiaminisha kuwa upendo wa kweli huja pale wanapovuliana nguo
na kuzini. Dhambi ni dhambi hata kama itapakwa rangi au kupuliziwa pafyumu iliyokali kiasi
gani.
9.Upofu unaopelekea kutorudi nyuma wala kujitambua (Mithali 7:21-22): Kijana
anaweza kuwa ameshauriwa na viongozi wa dini, wazazi hata watu wengine wa karibu yake
juu ya mtu anayetaka kumuoa au kuolewa naye, kuwa hafai lakini kijana hasikii wala haelewi
chochote maana amekuwa kipofu wa utambuzi, hivyo, mwisho wa siku anaangukia katika
mwenzi asiyestahili.
10. Hujiaminisha kuwa watawabadirisha tabia (Mithali 7:23): Vijana hujiaminisha
kuwa watawabadirisha tabia wenzi wao wa wapo ndani ya ndoa. Kuingia na mtu katika ndoa
asiye mwenzi mwema kunaleta maumivu katika mioyo ya wanandoa, maana siyo rahisi
mwanadamu kumbadirisha mwanadamu mwenzie bali ni Roho wa Mungu na kwa msaada wa
Yesu Kristo pekee ndiye anaweza kuibadirisha tabia na mienendo ya mwanadamu.

Njia Zisizo Sahihi za Kujipatia Mwenzi wa Maisha.


Suala la kujipatia mwenzi wa maisha ni jambo nyeti sana na wala sio jambo la mzaha.
Ukikosea mtu wa kuoa au kuolewa naye hupelekea furaha kutoweka daima katika uhai wa
maisha yote katika ndoa. Vijana wa kiume na wa kike (wachache) waliowateule wa Mungu
humtanguliza Mungu mbele katika jambo la kujipatia wenzi wa maisha wanaowafaa.
Vijana na watu wengi wamekuwa wakitumia hila au njia zisizo sahihi katika kujipatia
wenzi wao wa maisha. Zifuatazo ni baadhi ya njia zisizo sahihi katika kujipatia mwenzi wa
maisha:
1. Vijana wengi wanajitafutia wenzi wa maisha kwa kuangalia miongoni mwa
wanaomiliki funguo tatu; yaani awe na funguo za ofisi, funguo za nyumba na funguo za gari.
Mithali 15: 16-17 inaelezea kuwa mapenzi ya kweli siyo yatokanayo na mali au fedha bali
upendo wa kweli hauangalii mali na vitu.
2. Njia nyingine ni vijana wanaoa au kuolewa kwa sababu ya kutoa msaada au
kumuonea huruma mtu. Kumuoa au kuolewa na mtu kwa kumuonea huruma siyo njia salama
ya kujipatia mwenzi mwema maana hiyo huruma na msaada vyaweza kuwa kilio cha milele
katika ndoa.
3. Wasichana kutaka kuwa huru kutoka kwenye mikono ya wazazi wao. Wasichana
baadhi wanakimbilia kuolewa na watu hata walio na wake au wazee kwa sababu ya kutaka
kuwa huru kutoka kwenye mikono ya wazazi pamoja na kupata mteremko wa maisha yao.
Njia hii siyo sahihi kutumika ili kujipatia mwenzi wa maisha maana itakuwa ni kutatua tatizo
kwa kuongeza tatizo jingine hapo baadae.
4. Vijana wengi wanaoa au kuolewa kwa sababu tu wamepewa ujauzito au kumpa
ujauzito binti. Katika familia hii, mtoto atakuwa ndiye kiunganishi na siyo azima ya
wanandoa, hivyo huoana ili wafanikishe kumlea mtoto wao. Uzoefu na tafiti pia zinaonesha,
wengi wa vijana hubebeshana mimba ili kuifikia adhia ya kuoana endapo watakuwa
wamekubariana. Jambo lingine baya kabisa, ni pale mwanamke anapomuegeshea (wakati wa
kuzini) mimba (muda mfupi karibia na siku zake) mwanamume bila makubaliano ili ateke
upendo na kuolewa naye, kwa kumzalia mtoto; ndipo hutokea mambo mengine ya kukataa

Frank Philemon Karoli


26
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

mimba na kukataana pia. Njia hizo zote, siyo salama na ni dhambi kushiriki ngono kabla ya
ndoa.
5. Pia vijana hutumia njia ya kufanya ngono kwanza kama zawadi au kigezo cha
kufanikisha azima yao ya kuoana hapo baadae. Wanatumia kushiriki tendo la ndoa kama
sehemu ya kuthibitisha na kutakiana upendo. Mithali 6:32-33 inasema aziniye hana akili,
hivyo ni dhambi kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa kwa makusudi ya kumshawishi mtu
akupende kwa kumvulia nguo.
6. Njia nyingine isiyo salama inayotumiwa na vijana kujipatia wenzi ni kwa kutoa
rushwa, hususani zawadi (Mithali 18:16) ya kushawishi upendo. Rushwa au zawadi
itolewayo ili kuteka upendo wa mwingine inajumuisha kutoa pesa, vitu, tendo la ndoa na
kubeba mimba (kwa upande wa mabinti) ili kuteka upendo wa mwingine. Mambo ya Nyakati
16:19 imekataza maana hizo rushwa hupofusha macho.
7. Msukumo wa nje nao una nguvu kubwa unaotengeneza njia za kujipatia wenzi wa
maisha kwa vijana. Kijana anapendekezewa na kushawishiwa na marafiki zake juu ya mtu
fulani kuwa mwenzi. Njia hii imekuwa ikitumika hata kwa wazazi kuwachagulia wenzi wa
maisha watoto wao. Pia sio njia sahihi ya kujipatia mwenzi maana sio msukumo wa ndani wa
Roho mtakatifu.

Frank Philemon Karoli


27
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 03 =

HATIMA YA UCHUMBA NA MAAMUZI YA KUOA AU KUOLEWA

“Wewe ndiwe chemchemi ya bustani yangu, Kisima cha maji yaliyo hai, Vijito
vya Lebanoni viendavyo kasi”
Wimbo Ulio Bora 4:15

“Wakristo wote wenye shauku ya kuwa na nyumba bora ya Kikristo lazima watambue
kuwa, katika maisha ya kiulimwengu, thamani ya mtu inapimwa kwa mali aliyonayo. Lakini
vitabu vya mbinguni vinaandika thamani ya mtu inatokana na uwiano wa mema
aliyoyakamilisha kwa kutumia mali alizokabidhiwa na Mungu” [E. G. White 2 Selected
Message Vol.2, 193].
Suala la kuoa au kuolewa ni suala linalohitaji uangalifu katika kufanya maamuzi ya
kukubari kuingia katika ndoa. Siyo salama kukubari kuingia kwenye ndoa ingawa
kunamambo unayaona kwa mchumba wako hayako sawa. Katika hatua ya uchumba huwa
kuna maamuzi makuu mawili; uamuzi wa kuvunja uchumba au uamuzi wa kuendelea na
hatua za kufunga ndoa. Katika sura hii tutaona sababu zinazopelekea kuvunjika kwa
uchumba pamoja na utayari wa kuingia katika ndoa.

Sababu za Uchumba Kuvunjika


Uwezo wetu wa kumpenda mtu – na kuufrahia upendo wa mtu huyo integemea na
uzoefu wetu wa upendo wa Mungu (1Wakorintho 13:1; 1Yohana 4:8). Hivyo, ili umpende
mwenzi wako katika ndoa, upendo wako lazima uaksi upendo wa Agape. Zipo sababu nyingi
zinazopelekea kuvunjika kwa uchumba. Katika kitabu hiki zifuatazo ni baadhi ya sababu
chache miongoni mwa nyingi:

Msukumo usio sahihi wa kumpenda mchumba (Wimbo 8:6-7): Kukosekana kwa


msukumo sahihi wa kuingia kwenye uchumba na mtu au msukumo usio sahihi wa kumpenda
mchumba, hivyo uchumba ulioanzishwa kwa misukumo isiyo sahihi huvunjika kitambo tu
baada ya kuanzishwa. Misukumo binafsi kama talanta, tamaa ya macho na hisia juu ya
mwonekano wa sura au umbo pamoja na msukumo wa watu wengine katika kumpenda
mchumba husababisha kutokudumu kwa uchumba miongoni mwa wale waliouanzisha.
Kupenda kipawa au karama badala ya mtu (1wakorintho 12:1): Kupenda kipawa
alichonacho mtu ili kuanzisha uchumba naye sio upendo wa dhati katika yote aliyonayo
mchumba huyo, mwisho wa siku ukimzoea, akiacha kipawa chake au kugundua
anamapungufu lazima uchumba utavunjika maana hapakuwa na kilichovutia tofauti na
kipawa.
Kufanya uzinzi au uasherati kabla ya ndoa (1Wakorintho 6:16; 2Samweli 13:15 na
Mithali 6:32): Kufanya ngono kabla ya ndoa husababisha uchumba kuvunjika maana

Frank Philemon Karoli


28
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

kunakuwa na hatia ndani ya hao wachumba kwa sababu ya kuwa wamevunja sheria ya
Mungu tayari. Kushiriki tendo la ndoa kwa wachumba husababisha kuchukiana na ule
upendo wa kweli wa awali hupotea, maana panakuwa hakuna wanachokitumainia kukipata
hpo baadaye katika ndoa yao.
Kutokudumu kuomba ili kuifikia adhima ya kufunga ndoa (2Wakorintho 11:14):
Maombi pekee yaweza kuvunja uchumba kama mchumba aliyepatikana siye sahihi kuoana
naye, maana Mungu huwaepushia changamoto wale wanaomtumainia. Wakati mwingine siyo
salama kutodumu kuuombea uchumba maana maadui na mawakala wa Shetani hawakosi
kuushambulia uchumba ili uvunjike kwani nguvu za giza pia hutawala pasi na maombi ya
dhati, hivyo uchumba unaweza ukavunjika kwa sababu ya kukosa maombi ya dhati miongoni
mwa wachumba ili kuifikia ndoa.
Kutolipa umuhimu wa kutosha suala la ndoa: Kuna watu huanzisha uchumba
ingawa hawana dira yo yote katika kuifikia ndoa kama ilivyo azima ya kuuanzisha uchumba.
Panapoanzishwa uchumba bila malengo yo yote kwa wachumba, safari ya uchumba huwa
siyo ndefu kwa sababu uchumba huo huwa hauna madhumuni yo yote ya kuifikia ndoa.
Elimu inapaswa kutolewa kwa vijana wa Kikristo ili wajue madhumuni makuu ya kuanzisha
uchumba ni yapi.
Usiri wa uchumba na kukosa washauri sahihi (Mithali 12:15): Uchumba wa kificho
bila pande mbili za wazazi kujua au mashemasi wa kanisa kujua, uchumba huo hauwezi
kuwa na washauri wa maana ili kuwepo na mwelekeo mzuri wa wachumba kuifikia ndoa.
Uchumba wa kificho huishia katika kupotezeana muda kwa wachumba kisha kuachana.
Uchumba wa namna hii ulio wa giza au wa vichakani na vichocholoni si salama na wala sio
aina ya uchumba unaofaa, maana si wawazi.
Kuamini maneno ya watu bila kutafiti (Mithali 18:21): Kushikiwa akili na mtu juu
ya kutoa taarifa sahihi bila kufanya utafiti na kujiridhisha juu ya mwenendo mzima na tabia
ya mchumba nalo ni tatizo maana si wote wanaotoa taarifa wanania njema juu ya ustawi wa
uchumba unaoendelea. Mara nyingi si kila neno linalokuja kutoka kwa watu juu ya mchumba
linaweza kupokelewe zima zima bali mhusika kulichuja na kujiridhisha mwenyewe.
Uchumba waweza kuvunjika pale tu wachumba wanapokuwa na masikio yanayosikiliza
maneno kutoka kwa watu juu ya uchumba wao.
Wachumba kukosa muda wa kuwasiliana au kuzungumza kwa pamoja:
Kukosekana muda wa mazungumzo na mawasiliano ya uhakika kwa wachumba hujenga
uchumba usiokuwa na mikakati, kukumbushana na ari ya kuifikia ndoa. Wakati mwingine
kukosekana kwa mazungumzo na mawasiliano ya karibu husababisha upendo kuchuja
miongoni mwa wachumba, kisha uchumba waweza huvunjika.
Mazoea na tabia ya kuacha au kuachwa na wachumba: Tabia iliyojengeka katika
mazoea ya kuacha au kuachwa na wachumba husababisha kujenga hali ya mazoe ya kuachwa
au kuacha. Kuizoea hiyo tabia huleta mazoea hivyo kila uchumba unaoanzishwa huvunjika
kwa sababu ya kutoona madhara au maumivu wala cha kupoteza katika kuvunja uchumba.
Kutokuwa na kazi au chanzo sahihi cha uchumi (Mwanzo 2:15): Vijana baadhi wa
kiume walio Wakristo huvunja uchumba kwa sababu ya kutokuwa na kazi itakayoweza
kuleta pesa kwa ajili ya kufanikisha kupatikana kwa mahitaji ya msingi ya kifamilia katika
ndoa. Vijana wa kike wao huvunja uchumba kwa sababu wachumba wao hawana chanzo

Frank Philemon Karoli


29
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

sahihi cha uchumi, bila kujua kuwa mafanikio na maendeleo ya uchumi katika ndoa ni
kusaidizana wote wawili.

Mambo ya Kutafakari ili Kufanya Maamuzi ya Kuoa au Kuolewa


Kama unahitaji upendo wa kudumu wenye mafanikio, ndoa yenye furaha, inakupasa
uwe na vitu vinne katika upendo wako: uwe na hakiba ya upendo uliojikita mizizi katika
urafiki, uwe na wa upendo wa eros wenye mvuto baina ya wewe na mwenzi wako, uwe na
upendo wa phileo wa kuishi na mwenzi wako kama mtu na ndugu yake, na uhitaji upendo wa
Agape upendo wa Mungu usio na ubinafsi, ambao ndiyo msingi wa upendo wa aina zote.
Upendo ni maamuzi ya kila siku ya mmoja kujiweka pembeni katika mahitaji yake na
kuangalia mahitaji ya mwenzi wake.
Upendo ili udumu, lazima pasiwepo na ubinafsi, lakini kwa siku za sasa umimi
kwanza umetawala katika ndoa. Upendo ni kukubaliana na kupendana kila mmoja bila
mashariti (1Wakorintho 13:4-8), hupendo hauna majivuno, kujitazama mwenyewe wala
mashindano bali unyenyekevu (Wafilipi 2:3-4). Uwezo na matamanio ya kutoonesha ubinafsi
huwa ni jaribu kwa wenzi katika maisha yao ya kila siku wanapohusiana. Kuoa au kuolewa
kunahitaji utayari au kukusudia, hivyo kunahitajika kukubaliana na mambo yafuatayo kabla
ya kuridhia kuoa au kuolewa kwa kijana ye yote:
Tambua kuwa kuoa au kuolewa kunabadirisha ukaribu au uhusiano wako na
wazazi wako: Ye yote aliyejiandaa kuingia katika ndoa ajue kuwa kutakuwepo na utengano
wa ukaribu uliozoeleka baina yake na wazazi. Mwanzo 2:24 Mungu anasema, “Kwa hiyo
mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao
watakuwa mwili moja”.
Ye yote ajue kuwa anaenda kuunganishwa na familia nyingine: Kijana ye yote
anapoamua kuoa au kuolewa, afahamu ya kwamba hiyo ndoa inamuunganisha au kumuingiza
katika familia nyingine. Ni jambo la kujiandaa kisaikolojia ili kukabiliana na hali hiyo ya
mwingiliano.
Jipange kukabiliana na hali ya kutoshuka kiroho: Ukiamua kuoa au kuolewa,
wakati mwingine hali ya kiimani (kiroho) inaweza ikabadilika. Hali hii sana sana
huwakumba wale ambao wameoa au kuolewa na mtu ambaye hakuwa vizuri kiroho toka
awali au asiye wa imani moja. Kitabu cha 1Wafalme 11:4 kinasema kuwa: “Maana ikawa,
Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala
moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba
yake”. Kabla ya mtu kuingia kwenye ndoa lazima aweke mikakati ya kutoshuka kiroho.
Warumi 8:37; inatia moyo endapo Mungu atakuwa kimbilio, inasema: “Lakini katika mambo
hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda”.
Jiandae kwa ajili ya kuwajibika zaidi: Uamuzi wa kuoa au kuolewa ni muhimu, mtu
awe muangalifu kwa sababu kutamfanya awajibike zaidi aidha kuihudumia familia au kazi za
nyumbani. 1Timotheo 5:8 inasema kuwa “Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani,
wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiye amini”.
Tito 2:3-5 inasema “Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu, wasiwe
wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo mwingi, bali wafundishao mema, ili wawatie
wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao, na kuwa wenye

Frank Philemon Karoli


30
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

kiasi, na kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe,
ili neno la Mungu lisitukanwe”.
Tambua kuwa uamuzi wa kuoa au kuolewa, unaweza ukabadilisha
utumishi au wito wako kwa Mungu: Wakati mwingine ndoa inaweza ikabadirisha uelekeo
wa mtu kwa kazi aliyoitiwa na Bwana hususani kama mmoja wa wanandoa hajui umuhimu
wa kumtumikia Bwana kama moja wapo ya wito mkuu. Kitabu cha Waamuzi.16:21 (japo
siyo mfano sahihi wa aina ya ndoa) ni kisa kinachomwelezea Samsoni kutojikita katika wito
wake kwa sababu ya kuingia kwenye mahusiano na mwanamke asiye wa imani yake na
mwishowe adui wakamkamata. Fungu hilo linasema: “Wafilisti wakamkamata wakamng’oa
macho, wakateremka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba naye alikuwa
akisaga ngano katika gereza”
Jua ya kuwa utaongeza marafiki au madui: Uamuzi wa kuoa au kuolewa unaweza
wakati mwingine kukuletea marafiki au maadui maana ni muunganiko wa watu wawili.
Hesabu.12:1-2 inaonesha wazi kabisa ya kwamba uoaji wa Musa ulileta mgogoro katikati
yake na ndugu zake (Miriamu na Haruni). Cha kuzingati endapo umeamua kuingi katika ndoa
jiandae vyema kuwapenda maadui na marafiki watakao kuzunguka katika familia na ndoa
kama lilivyo agizo la Biblia usiwalipe baya kwa baya bali lipa jema kwa kila baya na jema.
Jihoji kama upo tayari kuzaa, kulea na kuhudumia watoto: Je nipo tayari kuzaa,
kutunza na kulea watoto? Ni swali la msingi kujiuliza kabla ya kufanya maamuzi ya kuingia
katika ndoa. Kuwahudumia watoto na kuwalea vyema ni jambo lisilohitaji mjadala kwa
wanandoa. Lakini pia tambua kuwa kupata watoto ni mapenzi ya Mungu na siyo mapenzi ya
mwanadamu hivyo mtegemee Mungu akupatie watoto kwa uzuri wake uutakao.

Zingatia: Baada ya kufanya maamuzi sahihi ya kuingia katika ndoa jitahidi katika
kumtii BWANA (mfanye kuwa wa kwanza) na muombe akupe maisha marefu na huyo
mwenzi wako huku mkizingatia kanuni za afya katika kweli yote ya maisha yenu ya ndoa.

Fundisho Kutoka Kwenye Kitabu cha Ruthu Juu Uchumba na Hatima ya Ndoa
Ruthu alikuwa ni binti wa Kimoabu aliyeolewa katika familia ya Kiebrania. Kitabu
cha Ruthu kinatoa dondoo nyingi za kujenga katika ufahamu mpana wa mahusiano ya
uchumba na ndoa kwa Wakristo. Kitabu hicho kimejengwa na wahusika wakuu watatu yaani
Ruthu, Naomi na Bozi.
Sura ya kwanza ya kitabu cha Ruthu inaelezea uaminifu na utiifu wa Ruthu kwa
Naomi; sura ya pili inaelezea jinsi Ruthu alivyoweza kufahamiana na Boazi; sura ya tatu
inamhusu Naomi katika kumtia moyo na kumhamasisha Ruthu kuolewa na Boazi na ile sura
ya nne, Ruthu na Boazi wanaoana na kuzaa mtoto wa kiume aliyeitwa\ Obedi babu yake na
Daudi ukoo aliozaliwa Masihi Yesu Kristo.
Ndani ya kitabu cha Ruthu, yamo mambo mengi ya kuwafunza wachumba na
wanandoa kama muhtasari wa sura hii ya kitabu; hususani juu ya mambo machache
yafuatayo:
Mchumba mwema ni yule mwenye tabia ya kutii na kufuata maelekezo ya wazazi
yaliyo na tija (Ruthu 3:1-12).
Mchumba wa kweli lazima aoneshe nia ya kuoa au kuolewa naye huyo mchumba
(Ruthu 3:8-9).

Frank Philemon Karoli


31
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Mchumba mwema ni yule mwenye kuonesha tabia ya kujali watu wengine (Ruthu
2:5).
Mchumba mwema ni yule mwenye tabia ya kuhurumia na kusaidia wengine (Ruthu
2:8).
Mchumba yampasa awe na tabia ya kuheshimu na kuonesha unyenyekevu (Ruthu
2:10).
Mchumba mwema ni yule mwenye tabia ya ukarimu (Ruthu 2:14, 16).
Mchumba mwema ni mwenye kumtumainia Mungu kwa kila jambo katika maisha
yake (Ruthu 2:20).
Mchumba mzuri ni yule aliye msafi na nadhifu na sio kwa sababu ya mapambo (Ruthu
3:3).
Mchumba mzuri ni yule mwenye washauri wema ili kufanikisha uchumba na siyo
kuubomoa (Ruthu 3:1-2).
Uchumba wa kweli hauhusishi ngono kabla ya ndoa (Ruthu 3:7-9).
Mchumba mwema ni yule aliye mwaminifu na watu wamshuhudie hivyo pia (Ruthu
3:11).
Uchumba wa kweli hauangalii vitu, talanta ama mali bali upendo ulio wa dhati (Ruthu
3:10).
Uchumba lazima uwe wa wazi kwa ndugu, jamaa na marafiki (Ruthu 4:9-11).
Uchumba wa kweli wenye uaminifu, huzaa ndoa yenye mibaraka (Ruthu 4:13).

Frank Philemon Karoli


32
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 04 =

MPANGO NA MAKUSUDI YA MUNGU KUASISI NDOA KWA


WANADAMU

“Mimi ni wake mpendwa wangu, Na shauku yake ni juu yangu”

Wimbo Ulio Bora 7:10

Ndoa ni agano kati ya mwanamke na mwanamume waliokusudia kwa dhati


kuungana na kuwa mume na mke kwa ajili ya maisha yao yote ya hapa duniani. Taasisi ya
ndoa ilianzishwa na Mungu katika juma la uumbaji siku ya sita (Mwanzo 1:27 na Mwanzo
2:18). Uhakika wake ulithibitishwa na Yesu alipokuwa hapa duniani (Mathayo 19:3-12).
Teolojia ya ndoa aliifundisha Mtume Paulo kwa upana zaidi katika Waefeso 5:22-
6:9. Hivyo basi, ndoa ni maisha ya familia yaliyojengwa katika misingi ya kiroho na
utakatifu au utukufu wa Mungu. Kusudi la Mungu kuasisi ndoa linajibu swali la msingi la
kuwa “kwa nini mwanamke na mwanamume waoane?”. Ni makusudi na mpango wa
Mungu na siyo mwanadamu kuhusu mwanamke na mwanamume kuoana. Yapo makusudi
makubwa manne:

1. Wanandoa kusaidiana (Mwanzo 2:28).


2. Kwa ajili ya wanandoa kuongeza uzao au kushiriki na kuendeleza uumbaji wa
Mungu(Mwanzo 1:28).
3. Wanandoa kushiriki tendo la ndoa (1Wakorintho 7:1-5) na kuwa wamoja.
4. Kukamilisha agano la kuwa mwili mmoja (Mwanzo 2:24), kwani kiuumbwaji
mwanamke ametokana na mwili (ubavu) wa wa mwanamume (Mwanzo 2:21- 23;
Mwanzo 5:2. Husianisha na Ezekieli 16:8).

Agizo la Kibiblia Juu ya Ndoa


Mungu ametoa maelekezo juu ya jinsi mwanadamu aoeje au aoleweje na afanyeje
sherehe za ndoa kwa kuzingatia misingi na taratibu za Kibiblia. Yafuatayo ni maelekezo
badhi ya Kibiblia juu ya namna ndoa iliyoasisiwa na Mungu iwe:
Ndoa iwe ya mke mmoja na mume mmoja: Mafungu yafuatayo yanathibitisha hilo:
Mwanzo 2:18-23, Mathayo 19:4-5, 1Wakorinto na 7:2-4. Mungu hakuruhusu ndoa za mitala
maana haukuwa mpango wake (angalia: 1Timotheo 3:2, na Kumbukumbu la Torati 17:17).
Ndoa ni kati ya mwanamke na mwanamume: Ndoa ni muunganiko wa
mwanamume na mwanamke na si vinginevyo. Ndoa haikuanzishwa kwa ajili ya kuoana watu
wenye jinsia moja yaani mwanamke kwa mwanamke au mwanamume kwa mwanamume
(yaani gays and lesbians). Anagalia: Warumi 1:26-27, na Mambo ya Walawi 18:22-23,
20:13.

Frank Philemon Karoli


33
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Ndoa inahusisha wanandoa kujitegemea: Wanandoa waliooana lazima wawaache


wazazi wao na kwenda kujitegemea katika kuanzisha familia zao. Mathayo 19:5, Mwanzo
2:24 na Waefeso 5:31.
Wanandoa washikamane na wala wasiachane: Wanandoa waliooana
wameunganishwa pamoja na kuwa mwili mmoja. Wanandoa wanapaswa kuthaminiana na
hayupo au wasiruhusu mtu kuwatenganisha au kuwaingilia katika ndoa yao. Wamekuwa
mwili mmoja kwa kufanya mambo na vitu kwa pamoja na kwa umoja kama mwili mmoja.

Hata tendo la ndoa ni la wanandoa wawili pekee na asihusishwe mwingine (angalia


katika Mithali 5:15-19). Hivyo basi, ndoa ni mshikamano wa kudumu daima hadi kifo
kitenganishe: ndoa iliyoasisiwa na Mungu, kuachana hakupo kutokana na maelekezo ya
Biblia (Mathayo 19:8-9 na 1Wakorintho 7:10-11).

Mambo ya Kuzingatia katika Muunganiko wa Ndoa ya Watu Wawili


Ndoa ya kwanza kabisa iliyoasisiwa na Mungu katika bustani ya Edeni (ya mume
mmoja na mke mmoja) ilihusisha kwa sehemu kubwa uwepo wa Mungu kwanza kabla ya
wanandoa wenyewe kuunganika. Kwa kuthibitisha hilo, neno Edeni linatokana na lugha ya
Kiebrania lenye maana ya uwepo wa Mungu. Kwa hiyo, bustani ya Edeni humanisha bustani
ya uwepo wa Mungu ambapo Adamu na Hawa waliweza kuungania katika ndoa yao.
Jua na tambua kuwa, mwanamke na mwanamume watawaacha wazazi wao
(watajitegemea bila kutegemea wazazi) na kuwa mwili mmoja (Mwanzo 2:24). Hivyo basi,
panapokuwepo na uwepo wa Mungu kwanza katika ndoa ya watu wawili (mke na mume),
wanandoa wanapaswa kufanya na kuzingatia mambo yafuatayo:
Wanandoa wajitoe kikamilifu kwa Mungu: Kwa wote wawili wamfanye Yesu ndiye
Mfalme na Bwana katika kila kitu katika muunganiko wao maana Yeye ndie kichwa kwao
wote.
Wasameheane wao kwa wao: Wanandoa wajenge tabia na moyo wa kusameheana
wao kwa wao. Rejea Waefeso 4:32, na Wakolosai 3:13.
Wavumiliane na kubebeana mizigo: Wanandoa ni lazima wajenge moyo wa
kubebeana mizigo yao wao kwa wao huku wakimtwisha mizigo na fadhaha zao Yesu Kristo.
Angalia Waefeso 4:2, na Wakolosai 3:13.
Kumheshimu na kumtii Mungu: Wanandoa na familia wampe nafasi ya kwanza
Mungu kisha wao na watoto au ndugu wafuate. Yote watendayo watende kwa utukufu wa
Mungu kama ilivyoelezwa katika 1Wakorintho 10:31 na 1Wakorintho 3:17 kuwa, kila
litendwalo katika familia litendwe kwa utukufu wa Mungu.
Uhuru wa kushirikishana, kuwasiliana na kuelewana: Wanandoa ni lazima
kuwekeana uhuru wa kushirikiana, kuwasliana na kuelewana ili kujenga ukaribu, upendo na
ushirikiano mzuri (Waefeso 5:19, 2Wafalme 4:8-10).
Uwazi, uaminifu na ukweli: Wanandoa lazima wawe wawazi, waaminifu na
wakweli kwa kila mmoja ili kuondoa kutiliana mashaka (Mwanzo 2:25).
Kuhudumiana na kujaliana: Wagalatia 5:13 inaeleza kuhudumiana kwa upendo
miongoni mwa wanandoa wao kwa wao kabla ya kuangalia mtu wa tatu.
Kuombeana na kuhurumiana: Miongoni mwa wanandoa wajengeane tabia ya
kuombeana kwa Mungu pamoja na kuhurumiana katika changamoto au adha ambazo mmoja
wa wanandoa atazipitia (Waefeso 6:18).

Frank Philemon Karoli


34
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Kutiana moyo na kuonyana kwa upole: Kutiana moyo, kuonyana kwa upole
miongoni mwa wanandoa ni suala la msingi katika kunyanyuana na kuelekezana (Mathayo
27:19, 24, 2Wafalme 4:8-11).
Kulindana: Wanandoa walindane katika uaminifu, kufichiana mapungufu na
kujaliana wao kwa wao (Yeremia 31:22).
Uwepo wa utii na upendo kwa wanandoa: Wanandoa wafuate kanuni rahisi ya
kibiblia inayohusu kutii na kupenda ili kuepuka vishawishi na kudumisha amani ya ndoa.
Waefeso 5:22-25.
Uhusiano wao ujengwe katika unyenyekevu unaopatikana kwa kuongozwa na
Roho Mtakatifu: Roho mtakatifu akitamalaki katika familiya, familia itakuwa mbingu ndogo
maana Roho mtakatifu hakai katika machafuko hivyo wanandoa waombe uwepo wake Roho
Mtakatifu. Tazamama Mithali 29:23; Isaya 57:15; Wafilipi 2:1-8.

Dhana ya Mahusiano Katika Jinsi na Jinsia


Jinsi ni hali ya kimaumbile inayomtofautisha au kubainisha utofauti uliopo kati ya
mwanamke na mwanamume. Jinsia ni mahusiano ya kijamii, kijinsi, kindoa au kiutamaduni
yanayozingatia mgawanyo wa majukumu kwa kuangalia jinsi (ya mwanamke na
mwanamume).
Jinsi na jinsia huzaa mgawanyo katika kazi, majukumu na mahusiano baina ya mtu
mwanamke na mtu mwanamume. Mahusiano katika muktadha wa dhana nzima ya kitabu
hiki ni uhusiano wa kijinsia kati ya mwanamke na mwanamume hususani kihisia. Mahusiano
ya kijinsia yapo katika makundi makuu manne:
Kundi la watu ambao hawajaingia katika mahusiano kabisa bali wapo katika hali ya
urafiki. Kundi hili linaweza kupelekea hatua ya pili kutokea (uchumba) baada ya marafiki wa
jinsia tofauti kuchunguzana na kuona kuwa wanaendana.
Kundi la watu ambalo linaanza kujiingiza katika mahusiano kutoka kwenye urafiki
na kuelekea kwenye uchumba. Katika kundi hili, huwa kunakuwa na muda wa matazamio
miongoni mwa wachumba kisha hatua zingine zinaweza kufuata kama uchumba
hautavunjika.
Kundi la watu walio katika mahusiano ya uchumba kwa kipindi fulani na huelekea
kutimiza adhima ya kuoana. Katika hatua hii, huwa panakuwa pamefayika makubaliano kwa
upande wa msichana na mvulana (mwanamke na mwanamume) ili kuifikia adhima ya
kuingia katika ndoa.
Kundi la watu ambao tayari wameoana na wako kwenye ndoa. Kundi hili lipo
katika mipango na majukumu ya kifamilia miongoni mwa wanandoa wanaoishi kama mwili
mmoja.
Mtazamo wa Kibiblia Juu ya Jinsi na Jinsia
Ujinsi na ujinsia ni mpango wa Mungu wala haikutokea kwa bahati mbaya au
kimakosa maana Yeye ndiye aliyeumba mtu mwanamume na mtu mwanamke (Mwanzo
2:18-25). Hivyo basi, jinsi na jinsia zimo ndani ya makusudi ya uumbaji wa Mungu katika
kumuumba mwanadamu. Makusudi ya Mungu kuweka jinsi kwa mwanadamu ni kama
yafuatayo: Kwa ajili ya kuzaa na kuongezeka (Mwanzo 1:28); Kukidhi hisia na umoja
(Mwanzo 4:1; Mathayo 19:5) na Kupata furaha, burudani au starehe (Mithali 5:15-19;
Mwanzo 18:12; Kumbukumbu 24:5).

Frank Philemon Karoli


35
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Uhusiano Mzuri wa Kijinsi na Kijinsia Katika Ndoa


Uhusiano mzuri wa kijinsi na jinsia katika ndoa unajipambanua katika mambo
yafuatayo (zingatia pia Waefeso 5:25-33):
o Mwanamke au mwanamme afanye majukumu yake kikamilifu kama Mungu
alivyopanga kulingana na jinsia au hali ya kibaiolojia na maumbile.

o Huzuni au furaha katika familia hutegemeana na wanandoa wenyewe kwa


namna wanavyoishi na kujihusisha na maisha yao na Mungu.

o Kila mmoja katika ndoa ajue ya kuwa hakuna aliyemkamilifu kama malaika,
bali wote wameathiriwa na dhambi na pambano kuu bado linaendelea hivyo,
wote ni wadhaifu.

o Wanandoa, hawatakiwi kuwa na hasira na kulaumiana juu ya njambo ambalo


hawakuwahi kulizungumzia, bali washirikishane kwa mambo vyote.

o Wanandoa wasimshirikishe mtu ye yote nje ya ndoa mambo yao ya siri yaliyo
ndani ya ndoa, hususani yale yanayoonesha udhaifu wa mwingine maana
itakuwa ni kumwaibisha na kujiaibisha pia kwa anayevujisha siri.

o Kila mwanandoa afikirie katika mtazamo chanya juu ya mwenzi wake. Mara
zote imeoneka wanamume huwafikiria hasi wanawake katika ndoa; ubaguzi huu
haufai katika familia ya Mkristo.

o Yawapasa wanandoa kuvaa mavazi yanayostiri mwili vyema ili wote wawe
mfano bora kuanzia kwa watoto wao na jamii nzima inayowazunguka.

Umuhimu na Haki ya Tendo la Ndoa kwa Wanandoa


Yafuatayo ni madhumuni makuu ya kuwekwa kwa tendo la ndoa kwa wanadamu
wanandoa:
 Kwa ajili ya kuzaa na kuongeza vizazi (Mwanzo 1:28, 38:8-10).
 Kuleta muunganiko wa wanandoa kuwa kitu kimoja (Mwanzo 2:24, 4:1 na 1Samweli
1:19).
 Kwa ajili ya starehe (Torati 24:5, Mwanzo 18:12, Mithali 5:15-19 na Mhubiri 9:9).
 Kuepuka kushiriki uzinzi (1Wakorintho 7:2).
 Ni haki na wajibiu wa wanandoa (1Wakorintho 7:3).
 Ni kielelezo cha wanandoa kujitoa kwa wenzi wao (1Wakorintho 7:4).
 Ni kielelezo cha wanandoa kukubaliana (1Wakorintho 7:5).
 Ni kielelezo cha usafi na utakatifu (Waebrania 13:4).

Frank Philemon Karoli


36
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Wanandoa Wanapaswa Kuzingatia Yafuatayo Juu ya Tendo la Ndoa


“Kuwa mwili mmoja” kwa muktadha wa Mwanzo 2:24, hakumanishi tu tendo la
ndoa, bali kumjua na kujuana, kupenda na kupendwa, kuumia wakati mwingine anapokuwa
ameumizwa, na kufurahi mwingine akifurahi pia. Kuwa mwili mmoja ni mshikamano,
kuongeza nguvu katika uwajibikaji na kuukuza kwa kina urafiki.
Wenzi mbao wapo tayari kuianzisha safari ya kuwa mwili mmoja wataupata uzoefu
wa lengo la Mungu la mpango wa ndoa. Kwa hiyo, wanandoa wanapaswa kuzingatia
yafuatayo juu ya tendo la ndoa:
 Tendo la ndoa ni kwa ajili ya waliooana na si vinginevyo (1Wakorintho 7:2).
 Tendo la ndoa litendwe kwa utukufu wa Mungu. Wanandoa waombe kwa ajili ya
tendo la ndoa kabla ya kushiriki (1Wakorintho 10:31, Wakolosai 3:17).
 Tendo la ndoa lifanyike kwa makubaliano ili pawepo ushirikiano na furaha ya tendo
hilo (1Wakorintho 7:5).
 Tendo la ndoa lifanywe kwa kiasi ili shetani asije akawajaribu wanandoa
(1Wakorintho 7:5).
 Tendo la ndoa lifanywe na kila mwanandoa alifurahie (Mithali 5:15-19, Kumbukumbu
24:5 na Mhubiri 9:9).
 Wanandoa wazingatie usafi na utakatifu wa tendo la ndoa (Waebrania 13:4).

Wakati Usiofaa Kufanya Tendo la Ndoa


Urafiki katika ndoa hutoa nafasi kwa wenzi kuwa wawazi, kujalianana kuonesha
hisia zao kwa ukaribu. Katika ndoa, urafiki hutoa uzoefu wa kuwa mwili mmoja wakati
ambapo mume na mke hushiriki hisia na fikra za ndani, shauku, ndoto, matamanio, furaha na
manbo yote yanayokatisha tamaa wawapo katika mazingira salama ya umoja wa ndoa.
Umoja huu ndiyo Mungu alioukusudia katika mpango wa kuasisi ndoa, na ndicho kinacho
wasukuma wenzi kuoana. Hivyo basi, wanandoa katika umoja wao wanaweza
wakasikilizana na kukubalia katika nyakati zisizofaa kushiriki tendo la ndoa kama zifuatazo:
 Mwanamke (mke) anapokuwa katika mzunguko wa siku zake.
 Mmoja au wote miongoni mwa wanandoa akiwa anaumwa na hali yake ya kiafya
haiko vizuri.
 Wakati ambapo mmoja baina ya wanandoa hajisikii kushiriki kwa sababu yo yote ile.

Vikwazo Katika Tendo la Ndoa kwa Wanandoa


Wataalamu wa mahusiano wamejaribu kuainisha vikwazo vifuatavyo katika tendo la
ndoa:
 Imebainika kuwa, wanawake wengi hawahitaji tendo la ndoa kwa sababu hawafurahii
tendo la ndoa au tu kwa kuwa sio hitaji lao mahususi kama wanaume;
 Mahusiano mabovu baina ya wanandoa ambayo yamepelekea kutokuwepo kwa
mvuto wa tendo la ndoa;
 Uchovu kutokana na kazi nzito wanazofanya wanandoa hivyo kukwamisha ushiriki
sahihi katika tendo la ndoa;
 Na afya duni miongoni mwa wanandoa nacho ni kikwazo katika ufanyikaji wa tendo
la ndoa.

Frank Philemon Karoli


37
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 05 =

UASI KATIKA NDOA NA FAMILIA YA KWANZA

“Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono


wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti…..”

Wimbo Ulio Bora 8:6

Shetani amekuwa na anazidi kushambulia tasisi takatifu ya ndoa, maana anajua kuwa
akiharibu ndoa atakuwa amefanikisha kuuharibu ulimwengu wote na kuweza kuwafanya
wanadamu wengi kuanguka na kufia dhambini na kuukosa ufalme wa milele.
Ndoa ya Hawa na Adamu (mke mmoja na mume mmoja) iliyoasisiwa na Mungu
mwenyewe katika bustani ya Edeni (Mwanzo 2:18-19) iliingia hitirafu kutokana na Shetani
kuweza kuwashawishi wanadoa hao kuasi maagizo ya Mungu juu ya kutokula matunda ya
mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambao Mungu aliwakataza wasiule (Mwanzo 2:16 -17).
Shetani alifanikisha adhima yake ya kuwaangusha wanandoa hao wa awali (Mwanzo
3:1-6) na hapo ndipo dhambi ikaingia katika ulimwengu na utukufu wa mwanadamu
ukatoweka, maisha ya umilele ya kapotea, shida, mateso na majanga ya kaanza kwa sababu
ya wanandoa hao kuasi maagizo ya Mungu.
Ndoa na familia zetu zaweza kuchangia kwa sehemu kubwa kuiharibu jamii, taifa na
ulimwengu au kuuletea amani pia. Hivyo, kama mzazi fanya sehemu yako katika kulea
watoto katika misingi ya wema na utii kwa Mungu ili hata kama watoto watakengeuka
ukubwani huko baadaye utakuwa umenawa mikono na upotevu wa roho zao Mungu
hatakudai maana ulifanya sehemu yako kama mzazi.
Mtoto aliyelelewa katika kweli yote ya Mungu kisha akakengeuka katika kuitii kweli
na maagizo ya Mungu hayuko katika familia za sasa tu bali palitokea hata katika familia ya
Hawa na Adamu hapo mwanzo kabisa. Kwa kuwa Shetani ambaye ni simba aungurumaye
hutafuta kuwapoteza wengi (1Petro 5:8) yumkini hata walio wateule ndivyo ilivyotokea
katika familia ya awali.
Chukulia kama jambo la kujifunza katika familia ya Adamu na Hawa; walizaa watoto
wawili wakiume nje ya bustani ya Edeni kama ilivyotajwa na Biblia. Swali la kujiuliza “kwa
nini familia hiyo yenye malezi katika misingi ya Mungu, Kaini aasi na Habili atii taratibu
zote za imani na ibaada?” Jua kuwa, Shetani hakomei kuwavuruga wanandoa pekee bali hata
wanafamilia yumkini hasa watoto.

Mambo ya Kujifunza Kutoka Katika Familia ya Adamu na Hawa


Watoto wawili wanazaliwa yaani „Kaini, na Habili‟ (Mwanzo 4:1). Kaini mtoto wa
kwanza (Mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani) na mkulima. Habili mtoto wa pili na mfugaji
wa kondoo. Habili kama mtoto wa pili ametajwa tu kwa makusudi makuu kama mfia dini.

Frank Philemon Karoli


38
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Mwanzo 4:3-5 inaonesha kuwa, katika hawa watoto wawili panajitokeza mgawanyiko wa
makundi mawili ya ibada; yaani ibada ya kweli (ya Mungu kutoka kwa Habili) na ibada ya
uongo (ya Shetani kutoka kwa Kaini).
Kutokana na ukengeufu wake Kaini, Mungu anamuonya Kaini kutokana na uasi wa
taratibu za ibada alizoziweka Yeye Mwenyewe (Mwanzo 4:6-7). Wivu wa Kaini juu ya
Mungu kupokea ibada ya Habili; Kaini anaamua kumuua mdogo wake (Mwanzo 4:8).
Shetani akamshupaza shingo Kaini na akawa hamsikilizi Mungu maana alimwona si cho
chote kwake tena ambapo Kaini anakuwa jeuri hata katika majibu yake kwa Mungu
Muumbaji (Mwanzo 4:9).
Mungu anampatia Kaini laana na kumtenga ili kuwa mbali na uzao wa familia ya
watakatifu (Mwanzo 4:10-16). Tukio la Kaini kuasi; Adamu na Hawa hawakuwa na hatia
kwa Mungu maana walitekeleza malezi mpaka watoto wao walipoanza kujitegemea kwa
mambo mengi; hasa ibada, na uzalishaji. Kwa sababu hiyo Adamu au Hawa walifanya
sehemu yao mpaka walipojitambua. Ili kujua kuwa Kaini na Habili walifundishwa vyema,
wanaonekana katika ufanano ufuatao: Wote walifundishwa na wazazi wao jinsi ya utoaji wa
sadaka ya kuteketeza katika ibada zao kwa Mungu.
Wote walitengeneza madhabahu kwa ajili ya kutoa sadaka zao kwa Mungu. Wote
walisimama kama wafanya ibada mbele za Mungu wa Mbinguni. Lakini utofauti wa Kaini na
Habili unajipambanua katika mambo yafuatayo: Kaini alikengeuka na kufanya matakwa yake
badala ya maelekezo ya Mungu katika ibada. Habili alienenda katika taratibu na sheria za
Mungu katika ibada na utoaji wa sadaka ya kuteketeza. Hivyo basi, Kaini anawakilisha
kanisa au mtu asiyefuata taratibu alizoziweka Mungu. Habili anasimama kama kanisa au mtu
ambaye ni mtiifu na mfuata taratibu na sheria za Mungu.
Funzo kutoka kwa Habili na Kaini watoto wa Adamu na Hawa ni katika mambo
yafuatayo: Habili ni mfano wa wafia dini katika familia au kanisa la Mungu bali Kaini ni
muasi wa sheria katika familia na kanisa la Mungu. Wanandoa wajue ya kuwa Mungu
haangalii matukio au matendo yetu ya nyuma ili atuhesabie haki na kufuta makosa yetu ya
hivi karibuni (kama Kaini alikengeuka mwishoni na ya nyuma yote Mungu hakuyatazama
maana alijua anajua na alimuonya pia).
Watoto katika familia wafundishwe kuwa, Mungu anaangalia katika utii wa kufuata
taratibu na maagizo yake pekee. Watoto wajuzwe kwamba Mungu anapokea ibada zetu,
endapo tutaenenda kwa utaratibu na utii juu Yake Yeye pekee. Wanafamilia ambao ndio
sehemu ya kanisa wajue ya kuwa dini, madhehebu na watu watungao ibada zao wenyewe
zisizompendeza Mungu au yasiyo maagizo ya Mungu; Mungu hazipokei wala kuzitambua
hivyo, wafanya ibada bure na yaweza kuwa wanamwabudu Shetani na siyo Mungu.
Watoto wafundishwe kuwa kabla ya kumwendea Mungu, yawapasa kujua kuwa ni
kitu gani kitasababisha ibada au maombi yao yasipokelewe na Mungu. Watoto wajuzwe pia
kuwa, katika ibada Mungu aweza asijibu maombi yao kwa sababu ibada zao haziko katika
usahihi au utaratibu wa Mungu. Wanadoa na watoto wajue kuwa haiwapasi kushupaza shingo
kama Kaini ili wasije wakapotea na kupelekea kutourithi uzima wa milele.
Siku zote wanafamilia au wanandoa na watoto wao yawapasa kujitahidi kadri ya
uwezo wa Roho Mtakatifu kufanya toba wanapokosea au kutenda dhambi ili ibada zao
zipokelewe na Mungu sawasawa na mapenzi Yake. Mwisho kabisa, wanandoa na watoto wao

Frank Philemon Karoli


39
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

watambue ya kuwa, yule asiyetii juu ya sheria na maonyo, ajue Mungu huongeza laana
badala ya baraka, hivyo mkono wa Mungu huondoka juu yake.

Uasi wa Kaini na Matokeo ya Gharika


Hawa na Adamu wanapoteza watoto wao wote wawili; mmoja kuwa mtangatangaji na
mwingine kwa kufa kifo. Hivyo, hapakuwa na ye yote aliyemrithi wa haki ipatikanayo kwa
imani. Kumbuka hata Abeli kutajwa katika Biblia ni kwa sababu ya kuifia dini. Kaini alikuwa
anamke toka mwanzo hata kabla ya kulaaniwa. Na kipindi hicho walikuwa wakioana ndugu
kwa ndugu (hivyo Kaini alikuwa ameoa dada yake, maana kwa kipindi hicho hapakuwa na
jamii nyingine tofauti na jamii ya familia ya Hawa na Adamu).
Mtoto wa kwanza wa Kaini ni Henoko (Mwanzo 4:17). Adamu na Hawa nao walizaa
watoto wengine tofauti ya wale wawili. Uzao wa Kaini na uzao wa Adamu ulitengeneza
makundi mawili: Uzao au ukoo mtakatifu ambaye mrithi wake ni Sethi na uzao au ukoo wa
wana wa wanadamu ambaye mrithi wake ni Henoko. Jua kuwa, kuna Henoko pia kutoka
ukoo mtakatifu tofauti na yule mtoto wa Kaini (Mwanzo 5:18) na huyo ndiye alitwaliwa na
Mungu (Mwanzo 5:24).
Henoko huyo kabla ya kutwaliwa, alimzaa Methusela aliyeishi miaka 969. Methusela
alimzaa Lameki (yupo Lameki upande wa Kaini pia ambaye ndiye mwanzilishi wa kuoa
wake wengi; Mwanzo 4:19) na Lameki aliyezaliwa na Methusela kutoka ukoo mtakatifu,
alimzaa Nuhu.
Changamano na mwingiliano kati ya wana wa Mungu na wana wa wanadamu uliathiri
sana mwenendo mzima wa ulimwengu wa wakati huo na kusababisha kuongezeka kwa
maovu kwa kasi kubwa kwa pande zote. Kwa sehemu kubwa ya Mwanzo sura ya sita (6)
inazungumzia ongezeko la watu ulimwenguni kwa kipindi hicho. Mwingiliano uliotokana na
kuoleana kwa pande mbili hizo kulisababisha kuongezeka kwa maovu, hivyo, uovu
uliongezeka sana.
Upande wa wana wa wanadamu walizaliwa watoto wengi bila mpangilio na wengi
wakiwa watoto wa kike. Pia upande huu palikuwa na kuoana katika umri mdogo pamoja na
uoanaji usiokuwa na mpangilio hasa kuoa wanawake wengi. Upande wa wana wa wanadamu
palizaliwa pia watoto waliokuwa wazuri wa sura hivyo, kuvutia kwao, kulipelekea watoto
wa kiume kutoka upande wa wana wa Mungu au ukoo mtakatifu kwenda kuoa mabinti
kutoka upande wa wana wa wanadamu (Mwanzo 6:1-2).
Maovu yalipoenea kutokana na kuingiliana kwa pande zote mbili, Mungu alipanga
mpango wa wokovu kwa wanadamu, na kwa kipindi hicho Nuhu ndiye aliyepata neema
machoni pa Mungu (Mwanzo 6:5-8). Kutokana na maovu ya wanadamu kuongezeka katika
uso wa dunia, Mungu akatoa rehema ya miaka 120 (Mwanzo 6:3). Katika hiyo miaka 120 ya
rehema, Nuhu alikuwa akijenga Safina kwa ajili ya wokovu wa wanadamu pale dunia itakapo
gharikishwa na waovu wote ambao hawakutii kuingia katiaka Safina kuangamizwa.
Maovu yote yaliyosababisha Mungu kuigharikisha dunia, yamechangiwa sehemu
kubwa na uasi wa Kaini na uzao wake kuichafua dunia nzima. Kwa habari hiyo ya Kaini;
jambo la msingi ambalo wazazi ni vyema wakalifahamu ni kuwa watoto ni mali na zawadi
kutoka kwa Mungu (Zaburi 127:3) hivyo, wazazi wasipozingatia katika kuwapa malezi
sahihi yenye adiri na uelekevu kwa Mungu na wakipotea hatia ipo juu ya wazazi maana Yesu
atamuuliza kila mmoja “lipi kundi jema nililo kukabidhi?”.

Frank Philemon Karoli


40
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Shetani anajua kuwa, mtoto mmoja akimwasi Mungu, hapo baadaye atakuwa na jeshi
kubwa kama alivyofanya kwa Kaini, ambapo vizazi vyake vilileta maafa kwa ulimwengu
hadi kipindi cha Nuhu. Uasi wo wote wa mwanadamu juu ya sheria na taratibu za Mungu
hufika kikomo na wamchao hupata neema Yake kama ilivyokuwa kipindi cha Nuhu
“BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. BWANA
akasema, nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na
mnyama, na kitaambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi kwamba nimewafanya.
Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana” (Mwanzo 6:6-8).

Kilichotokea Edeni na Fundisho kwa Wanandoa wa Sasa


Adamu na Hawa walikuwa ni wanadamu wa kwanza walioumbwa na Mungu wakiwa
hawana dhambi. Dhambi iliingia duniani pale tu Adamu na Hawa waliposhindwa kutii
maelekezo ya Mungu. Katika maelezo ya Mwanzo 3:1, yanamuonesha Shetani pale
alipoanza na swali la mtego lenye kupima uelewa wa Hawa kwa kusema, “Ati! Hivi ndivyo
alivyosema Mungu, msile matunda ya miti yote ya bustani?”.
Swali hilo lilifungua mazungumzo baina ya Shetani na Hawa. Mwanzo 3:2, 3
inamuonesha Hawa alivyojibu vyema swali la Shetani na kunukuu maelezo ya Mungu juu ya
kuruhusu kula matunda yote katika bustani, isipokuwa matunda ya mti ulio katikati ya
bustani. Shetani aliongea uongo na ukweli katika majibishano yake na Hawa ili kumpotosha
kuhusu maelekezo ya Mungu (Mwanzo 3: 4-5).
Shauku ya Hawa ya kujua maarifa (mema na mabaya) pamoja nakuutamani mti
kutokana na matamanio ya macho; Hawa anachukua jukumu la kuchuma matunda katika ule
mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kisha anakula na kumpelekea Adamu mumewe (Mwanzo
3:6). Kwa makosa waliyotenda; Hawa na Adamu wanajificha ili Mungu asiwaone (Mwazo
3:8). Lawama: Adamu anamtupia lawama Hawa na Hawa naye anamtupia lawama nyoka
(Mwanzo 3:12).
Mungu mwenye huruma anapanga mpango wa wokovu katika anguko la mwanadamu
(Mwanzo 3:15). Kwa mara ya kwanza mnyama anachinjwa ili kupata ngozi itakayoweza
kustiri miili yao (Mwanzo 3:21). Mungu anawafukuza Hawa na Adamu kutoka nje ya bustani
ya Edeni ili kuepusha kula tena matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya wasije kuishi
milele katika dhambi (Mwanzo 3:22-24).
Ukisoma kwa udadisi na kwa kutafakari vizuri Mwanzo 3:1-20 ambapo aya hizo
zinaelezea anguko la mwanadamu kwa kutenda dhambi katika bustani ya Edeni. Anguko la
wanandoa hao katika bustani ya Edeni ni onyo kwa wanandoa wa sasa kuwa: wachukue
tahadhari zifuatazo kama fundisho kwao kwa hali iliyotokea katika ndoa ya awali na
hatimaye anguko la mwanadamu:
Wanandoa wasitengane:
Mwanya wa Shetani kuingiza udanganyifu ni pale tu kosa lilipofanyika kwa wanandoa
kutengana. Hawa alipoondoka hakumuaga Adamu (maana Biblia haionyeshi kuwa Adamu
alijua wapi Hawa mkewe alipo) na Adamu hakumtafuta Hawa kuwa yuko wapi. Shetani
alitumia fursa hiyo ya utengano wa Hawa na Adamu kufanya udanganyifu kwa Hawa. Ni
vyema wanandoa kuagana po pote pale mmoja anapotaka kuelekea ili kuonesha uwazi na
kujali; na kama mmoja hatajua mwenzi wake yupo wapi, yampasa kujishughulisha kujua
wapi mwenzie alipo na anachangamoto gani inayomkabili.

Frank Philemon Karoli


41
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Mungu kwanza kisha mwenzi:


Kosa alilolifanya Adamu ni kumpenda sana mkewe na sio Mungu au yaweza
kuelezeka kuwa Adamu alimtii sana Hawa kuliko Mungu. Mwanzo 3:6 inaonesha kuwa
Hawa ndiye aliyempelekea mumewe tunda la ujuzi wa mema na mabaya, hivyo, Adamu
alikuwa na uwezo wa kukataa ili kuepusha anguko la ulimwengu. Sheria ya Mungu
imenyooka na haipindi katika kusimamia haki; maana yatupasa kuwa waaminifu mpaka kufa.
Mheshimu Mungu kwanza kisha mwenzi, yaani upendo ukiwa madhubuti kwa Mungu, kwa
mwezi utakuwa imara pia. Dhambi ya Hawa ilikuwa ni dhambi ya hatia yake, lakini dhambi
ya Adamu ilikuwa ni dhambi ya ulimwengu mzima (Warumi 5:12).

Wanandoa wasimruhusu Shetani kuwa karibu yao:


Kosa alilofanya Hawa ni kuruhusu mazungumzo na Shetani; mazungumzo yaliyotoa
mwanya wa Hawa kushawishika. Hivyo, tamaa itokanayo na ushawishi pamoja na udadisi
ilimwingia Hawa na hatimaye akachuma na kula. Katika hili, wanandoa yawapasa kuyaepuka
mazingira ya aina yo yote yanayoweza kuwasababishia kutenda dhambi, hususani usaliti wa
ndoa au taratibu na sheria za Mungu. Ni vyema muda mwingi ukatumika kumtafakari Yesu
ili kukuza mambo ya kiroho kupitia nyimbo, tenzi kama anavyoshauri Mtume Paulo katika
Waefeso 5:21.

Wanandoa waepuke dhambi hata kama inaushawishi kiasi gani:


Wanandoa yawapasa kutambua kuwa dhambi inakuja kwa sura nyingi na aina zake.
Dhambi huja katika sura zifuatazo: 1. Dhambi huwa ni yenye kukidhi haja ya mwili na hakili,
2. Dhambi huwa ni yenye kuvutia machoni katika kutamanika na 3. Dhambi huwa yenye
kutimiza au kuhitaji maarifa, ujuzi na uelewa. Katika sura hizo tatu za dhambi ndivyo
alivyoliona tunda Hawa katika sura zake tatu (Mwanzo 3:6).
Vyakula au vinywaji, maarifa mapya na mitindo fulani yenye ubunifu na kuvutia
vimeharibu mwenendo mzima wa uwajibikaji, afya, maadili na mambo ya kiroho kwa familia
na jamii ambapo hata za Wakristo nazo zimekengeuka vibaya. Mivuto ya dhambi
inasambaratisha au imeacha nyufa katika ndoa aidha, kwa kukosa uaminifu katika familia au
kukosekana kwa amani na maadili katika familia. Ushindi wa dhambi kwa wanandoa ni Yesu
Kristo pekee na kwa kumruhusu Roho Mtakatifu kuongoza maisha yao.

Wanandoa kutokukubali makosa waliyotenda ingawa yanajulikana:


Wakiwa ndani ya bustani ya Edeni, Adamu na Hawa hawakukubali makosa yao na
hivyo kuweka visingizio na kulaumu (Mwanzo 11:13) pale Mungu alipokuwa anawauliza
wakati wakiwa katika maficho yao. Wakati wa hali ngumu au changamoto zozote katika ndoa
siyo wakati wa kulaumiana na kusingiziana, bali ni wakati muafaka wa kutuliza mihemko na
akili ili shetani asipitie katika udhaifu huo na hatimae ndoa kuwa katika mgogoro mkubwa
zaidi.
Utulivu wakati wa changamoto hutoa suluhisho na jibu sahihi kwa wakati sahihi.
Kujificha kwa Hawa na Adamu hapakuwa na tija ili kumkwepa Mungu bali walijiona wapo
uchi kwa sababu ya dhambi, hivyo, utukufu uliondoka kwao na kushindwa kumkabili Mungu
uso kwa uso. Dhambi yo yote ya siri inapofanywa miongoni mwa mmoja wa wanandoa

Frank Philemon Karoli


42
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

ikigundulika huwa ni aibu ya wote (wanandoa) na wanandoa huona haya na aibu machoni pa
watu maana ni aibu kwao na wamemuaibisha Mungu.

Ndoa Kama Kielelezo cha Kiroho na Wokovu


Mungu kuanzisha ndoa ni kwa makusudi matakatifu kwa wanadamu. Ndoa ni
kielelezo cha kimbingu kinachohusisha utakatifu wa Mungu katika mambo ya kiroho. Mungu
huwa na wivu sana pale anapoona mwanadamu anafanya ibada katika miungu mingine
badala ya kumwabudu Yeye (Kutoka 20:3-5). Kitendo cha mwanadamu kufanya utii wa
kiibada kwa vitu vingine badala ya Yeye, Mungu anakiita ni uzinzi.
Uzinzi wa kuabudu miungu mingine ni uzinzi wa kiroho kama ilivyoelezwa katika
Ezekieli16:24-63. Jinsi mwanandoa anapomsaliti mwenzie na jinsi anavyoumia, Mungu
huumia sana maana agano la ndoa linaarifiwa katika kutolichafua na kutolivunja kwa kufanya
uzinzi. Mungu hapendi kuchanganywa kama ilivyo mwanandoa asivyopenda kuchanganywa
na wale wa nje wasio katika agano. Mungu hupenda kuabudiwa peke yake katika uaminifu
bila kushirikisha ibada za sanamu kama ilivyo kwenye ndoa ya kuwa mke mmoja na mume
mmoja wale wa ziada ni kufanya uzinzi ambapo ni dhambi pia.
Upendo wa kibinadamu (eros) ambao Adamu aliouonesha kwa Hawa mkewe na
kushiriki dhambi iliyoleta anguko la dunia ni upendo wa mke na mume, hivyo palitakiwa
upendo wa hali ya juu ili mwanadamu akombolewe kutoka dhambini. Pendo pekee
lililopaswa kutumika ni lile pendo la pekee la Mungu juu ya wanadamu ambalo ni pendo
lililojikita katika makusudi ya Mungu kumuumba mwanadamu hapo Mwanzo (Mwanzo
1:26).
Hivyo, pendo pekee lililotakiwa ni pendo la aina ya “agape” ambalo alishiriki Mwana
wa Mungu ambaye aliona hakuna haja ya kushikamana na enzi ya mbinguni pamoja na
Babaye, akazaliwa katika mwili ili awe Adamu wa pili katika upendo wa hali ya juu ili
awakomboe wanadamu. Dhambi ya Hawa ilikuwa ni dhambi ya hatia yake, lakini dhambi ya
Adamu ilikuwa ni dhambi ya ulimwengu mzima (Warumi 5:12). Yesu akazaliwa, akafanya
huduma na kisha kafara yake msalabani iliyotokana na mateso mengi pamoja na maumivu
makali, ndilo lilokuwa pendo la ajabu ambalo mwanadamu hawezi kufa kwa niaba ya
wanadamu ili awaondolee dhambi.
Anguko la wanandoa wa awali (Adamu na Hawa) lilipelekea kuwekwa bayana kwa
mpango wa ukombozi kwa mwanadamu. Mungu akasema kwa wanandoa hao wa kwanza,
kuwa, uzao wa mwanamke utamponda kichwa Ibilisi (Mwanzo 3:15). Mpango huu ulitimia
kwa kuzaliwa kwa Yesu; Mwana wa Mungu; Mungu pamoja nasi (Emmanueli) kupitia kwa
mwanamke bikira aitwaye Mariamu (Mathayo 1:18-25).
Suala la ndoa pia ni kielelezo cha Yesu Kristo na kanisa kama ilivyo mume na mke
katika ndoa. Mwanamume ni kichwa cha mkewe kama ilivyo Kristo kichwa cha kanisa.
Kanisa ni mwili wenye viungo vingi vinavyojenga mwili wa Kristo kadhalika, mwanamke ni
mwili katika ndoa katika kujenga mwili wa mumewe kama jinsi Hawa alivyopatikana kutoka
kwenye mwili wa Adamu. Pamoja na hayo yote, bado Kristo ndiye kiongozi kwa wanandoa
wanaolijenga kanisa lake.
Mungu ni kichwa cha Kristo, Kristo ni kichwa cha mwanamume na mwanamume ni
kichwa cha mkewe (1Wakorintho 11:3). Katika ndoa kunamshikamano wa ajabu sana ambao
hauwezi kuelezeka kwa namna ya kibinadamu pekee. Ni jambo baya sana wanadamu

Frank Philemon Karoli


43
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

kucheza na ndoa, tasisi aliyoiweka Mungu ili tuujue upendo wake na sisi wanadamu tutii
kwake kama ilivyo mwanamume hupenda na mwanamke hutii katika upendo wa mumewe.
Yesu alilipenda kanisa hivyo waume nao wawapende wake zao ili kanisa la Mungu liwe
takatifu na safi.
Katika jambo la kiroho, Yesu Kristo anasimama kama Bwana harusi na kanisa (na
watu wake) ni bibi harusi. Hivyo ndoa zetu zikiwa takatifu tutazalisha kanisa safi na takatifu,
na Yesu ajapo alitwae kanisa la Mungu lililo katika Ufunuo 12:1-6, ambalo ni kanisa safi na
bikira maana mafundisho yake ni safi, bali lile la Ufunuo 17:1-18 ni kanisa katika mtazamo
wa mwanamke kahaba asiye bikira maana halijatunza usafi wa mafundisho kwani limefanya
uzinzi wa kiroho.
Yesu anabisha ili aingie katika kanisa lake na ndoa zetu (Ufunuo 3:20-21) hivyo,
tumpokee ili tukaketi naye tukiwa washindi wa dhambi ndani ya kanisa ambalo ni bibi harusi
safi likifanya hukumu kwa mika 1000 na Bwana wake huko mbinguni na washiriki wake
wakiwa wamekula ule mti wa uzima na kubadirishwa tayari (Ufunuo 22:2).

Frank Philemon Karoli


44
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 06 =

CHANGAMOTO KATIKA BAADHI YA FAMILIA ZA KIKRISTO

“Ndoa yenye mafanikio, inaupendo usiokoma kwa mwenzi yule yule kila
siku. Ndoa yenye upendo hakuna kinachoharibika”
Frank P. Karoli

Hakuna umoja katika ndoa unaopatikana bila jitihada za wanandoa kuupalilia umoja
huo. Umoja katika ndoa ni safari ambayo kila mwanandoa lazima awe na shauku na utayari
wa kuhusika. Umoja huo kwa wanandoa lazima uwe wenyekutoa nafasi ya kumilikiana wao
kwa wao, ukaribu na muunganiko wa kimapezi. Ukweli ni kwamba, ndoa siyo tu nini
tunaweza kukipata na kunufaika nacho, bali utayari wa kutoa pia. Wakati ambapo kila
mwenzi anapotoa upendo wake kwa mwenzie na mtazamo wa furaha yake kwa mwingine,
lazima patokee matunda mema ya umoja katika ustawi wa ndoa.
Familia baadhi za Kikristo zipo katika changamoto na mitikisiko mikubwa ya kila
aina, hivyo, zinahitaji msaada wa hali ya juu kutoka kwa viongozi wa kanisa na watumishi
wa Mungu walio kielelezo chema na mfano mwema kwa jamii na kanisa kwa ujumla. Kanisa
na viongozi wake wanapaswa kutambua kuwa ndoa baadhi za washiriki zipo katika
changamoto nyingi sana. Zifuatazo ni baadhi miongoni mwa changamoto nyingi zilizo katika
familia baadhi za Kikristo:
 Zipo familia zimepungua katika mambo ya kiroho (imani kwa Mungu).
 Zipo familia za Kikristo zimepungua katika kusoma neno la Mungu ipaswavyo.
 Katika familia baadhi, elimu ya kidunia imepewa kipaumbele kuliko ya Mungu.
 Zipo familia ambazo uaminifu umepungua miongoni mwa wanandoa.
 Zipo familia zimeathiliwa sana na maendeleo ya utandawazi na teknolojia.
 Zipo baadhi zimeugeukia ulimwengu katika mitindo na mienendo ya maisha.
 Zipo ambazo kazi imekuwa kikwazo cha kutii na kutunza amri na sheria za Mungu.
 Zipo familia baadhi zimo katika migogoro inayotishia ustawi wa ndoa.
 Zipo familia ambazo wanandoa wanaishi kwa kuvumiliana si kwa upendo.
 Familia baadhi za Kikristo zimevunjika na kuhatarisha malezi ya watoto.

Hivyo basi, kanisa na viongozi wake wafanye mambo yafuatayo ili kuzinusuru familia za
wakristo:
1. Kanisa lifundishe mafundisho mengi na nyeti juu ya kaya na familia ili kuzinusuru
ndoa na familia za Kikristo. Hivyo, Makanisa yajenge tabia za kutoa semina mara kwa mara
kwa wanandoa.
2. Programu na mafundisho maalumu juu ya mambo ya kimahusiano yatolewe
ipaswavyo kwa vijana walioko ndani ya kanisa.

Frank Philemon Karoli


45
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

3. Pawepo na patolewe ushauri na semina endelevu kwa wachumba kabla ya ndoa na


siyo semina za siku moja au mbili pekee.
4. Mafundisho ya matendo mema ya Mkristo yatolewe kwa kushiriki au kutenda ili
kuongeza viwango vya kiroho kwa washiriki ambao ndani yake wamo wanandoa pia.
5. Semina nyingi zitolewe kwa wazazi juu ya kuwaandaa vijana katika maisha yao ya
badaye na siyo kanisa pekee kubeba mzigo wote ambapo haliwezi kuufikia utoshelevu.
6. Wanandoa waelimishwe ili wajue nini cha kufanya pale wanapokuwa nje au mbali na
familia zao ili kutoathiri mahusiano yao ya kindoa, familia na malezi ya watoto wao pia.

Aina za Migogoro Ndani ya Familia za Kikristo


Tamaduni zetu zimekuwa zikitudanganya ya kuwa, upendo ni hisia ambazo wenzi
wanahuska kwazo. Kwa hakika, upendo siyo hisia bali maamuzi yatokanayo na wanandoa
husika. Wanandoa wanakuwa wamoja wakati wanapokuwa tayari kustawi pamoja. Umoja wa
wanando upo katika nyanja kuu nne (4): 1. Umoja wa wanandoa katika hisia, 2. Umoja wa
wanandoa katika akili au mitazamo, 3. Umoja wa wanandoa katika mambo ya kiroho na 4.
Umoja wa wanandoa katika mapenzi au tendo la ndoa. Makundi hayo tajwa ya umoja, ndiyo
huzaa migogoro endapo wanandoa hawatayazingati katika kuyadumisha katika umoja wa
mwili mmoja.
Ipo aina nyingi ya migogoro inayoweza kuibuka katika ngazi ya familia ambayo
kwayo inahitaji utatuzi ili kutosababisha madhara makubwa katika familia. Kwa kutaja,
migogoro katika familia hujumuisha jumla ya aina zifuatazo: Wazazi kwa wazazi
(wanandoa); Wazazi kwa watoto (wazazi na watoto wao); Watoto kwa watoto (watoto wa
baba na mama mmoja); Wazazi kwa watoto wanaoishi nao wasio watoto wao; Watoto wa
nyumbani na watoto wanaoishi nyumbani ambapo siyo kwao na wazazi na jamaa za mzazi
mwingine (mfano; wifi, shemeji, shangazi n.k).

Talaka (Kuachana) Katika Ndoa za Kikristo


Neno talaka limetokana na neno la lugha ya Kiyunani (Kigiriki) “Poluo” lenye maana
ya “kuacha huru” “uhuru wa kitu kwenda” au “kutofungamanisha”. Katika Mathayo 19:6-
9, inaelezea kwa kina juu ya suala la talaka, na kwa kuwa ndoa ni agano hivyo
alichokiunganisha Mungu (kuwa mke na mume) mwanadamu hawezi kukitenganisha. Yesu
anasema kwa msisitizo ya kuwa Musa aliruhusu talaka kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya
wanadamu. Katika kitabu cha Malaki 2:16, Mungu anasema “anakuchukia kuachana”.

Mtume Paulo naye katika 1Wakorintho 7:10 anasisitiza kuwa waliooana wasitengane
na kama watakosana wasameheane wao kwa wao na kupatana. Marko naye anasema kuwa
kilichounganishwa na Mungu, mwanadamu hawezi kukitenganisha (Marko 10:9). Katika
Mathayo 19:9 Yesu anakataza kuachana, tena kwa habari ya uasherati wanandoa wanaweza
wakaachana, lakini asioe wala kuolewa miongoni mwa waliotalakiana. Kwa misingi hiyo
basi, kuachana siyo jambo rahisi maana walioachana hawaruhusiwi kuoa wala kuolewa.
Pamoja na habari ya uasherati inatoa nafasi ya kuachana kwa wanandoa lakini
panaweza kuwepo na mashauri, uvumilivu na kuonyana ili kuiponya ndoa katika kuachana.
Hivyo, talaka au kuvunja ndoa sio jambo jepesi zaidi sana ni kusameheana na kuvumiliana

Frank Philemon Karoli


46
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

pamoja na kuruhusu hekima ya kimbingu itawale. Biblia inabainisha sababu kuu tatu (3) za
wanandoa kuachana au kukoma kwa ndoa: 1. Kifo (Warumi 7:2-3), 2. Imani (1Wakorintho
7:15) na 3. Uasherati (Mathayo 19:9).

Sababu Zinazotoa Nafasi kwa Wanandoa Kuweza Kuachana


Kuachana kwa wanandoa huwa ni mchakato wa muda mrefu ambao huzaa mwanya
huo. Zipo sababu kadha wa kadha kati ya nyingi zinazotoa mwanya na kusababisha ongezeko
la ndoa nyingi kuvunjika hususani zinazosababisha usaliti kwa wanandoa:
1. Wanandoa kukaa mbalimbali aidha kwa sababu za kikazi au majukumu ya
kimasomo. Wanandoa kukaa mbalimbali husababisha kutoa mwanya kwa wanandoa
kusalitiana na ikigundulika kuacha matokeo yanayopelekea kuvunjika kwa ndoa, endapo
haitatumika hekima ya kimbingu katika kuzungumza na hatimae kusameheana.
2. Kukosekana kwa mawasiliano ya karibu katika masuala mazima ya kimahusiano na
tendo la ndoa kwa wanandoa; aidha, kwa sababu ya migogoro au kukosekana kwa ukaribu na
uwazi ambapo huweza kupelekea miongoni mwa wanandoa kutoka nje ya ndo na pindi inapo
bainika ndoa yaweza huvunjika.
3. Kukosekana kwa uaminifu juu ya mambo ya pesa au mali. Unapokosekana uamifu
juu ya mali au fedha miongoni mwa wanandoa husababisha kutokuwa na mshikamano au
kupanga mipango ya pamoja, hivyo kila mmoja huficha au huhamisha mali au fedha nje ya
mfumo mzima wa family. Hali hii mwishowe hupelekea ndoa kuvunjika kwa sababu kila
mmoja hupunguza uaminifu kwa mwenzie au kutoona umuhimu wake.
4. Wazazi wa wanandoa (wakwe) wanapoingilia mambo na maamuzi ya wanandoa
kwa nia ya kuwatenganisha. Mmojawapo au wote miongoni mwa wanandoa, endapo
atakubali kupokea msukumo wa nje kutoka kwa wazazi juu ya hamasa ya kuvunja ndoa; ndoa
inaweza ikavunjika endao hakutatumika busara ya kuwaunganisha. Hivyo, wazazi wa
wanandoa huwa ni sababu mojawapo ya ndoa nyingi kuvunjika. Wakati mwingine huwa siyo
wazazi pekee bali hata ndugu wengine na marafiki wanaweza kuwa sehemu ya
kuwachonganisha wanandoa kisha kuchochea migogoro na hatimaye ndoa inaweza
ikavunjika.
5. Migogoro ya kimajukumu katika mambo ya familia. Endapo mmoja miongoni mwa
wanandoa hatimizi au hatekelezi wajibu, hupelekea migogoro ambayo hutoa ufa unaoweza
kusababisa ndoa kuvunjika. Endapo mama au baba wa familia hatatimizi majukumu yake
ipasavyo kulingana na mfumo wa kindoa, mfano baba hahudumii familia ilivyo, au mama
hatekelezi majukumu yake ya nyumbani husababisha mitafaruku ya kimajukumu katika ndoa,
hatimae ndoa yaweza vunjika.
6. Wivu mbaya na kukosa kutendeana mema miongoni mwa wanandoa, husababisha
kuzaliwa kwa migogoro ambayo hupelekea ndoa kuvunjika. Wivu wenye kutiliana mashaka
juu ya uaminifu kwa wanandoa bila ushahidi au uhakika wa jambo husababisha tahaluki.
Tahaluki hizo husababisha wanandoa kutotendeana wema ndani ya ndoa hivyo hupelekea
kulipizana visasi na chuki ya kudumu miongoni mwa wanandoa. Hali hii humpa nafasi
Shetani kuisambaratisha ndoa hivyo, ndoa kuvunjika endapo itakosekana hekima ya
kimbingu.

Frank Philemon Karoli


47
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Madhara Yanayoletwa na Migogoro Pamoja na Kuachana kwa Wanandoa:


1. Kwa watu wa Mungu huwa ni aibu na fedheha katika macho ya jamii
inayowazunguka hivyo, heshima hupungua juu yao.
2. Husababisha magonjwa kutokana na maumivu ya moyo ya ndani hasa kwa
aliyekuwa mwaminifu miongoni mwa wanandoa kutokana na kutoitegemea hali hiyo
kutokea.
3. Husababisha matatizo ya kisaikolojia, kihisia, kiuchumi na kijamii kwa watoto
wanaoachwa upande wa mzazi mmoja baada ya ndoa kuvunjika. Maumivu na matatizo
yatokanayo na ndoa kuvuvunjika huacha majeraha yasiyofutika kwa watoto ambayo
yanaweza kuwaathiri hata kipindi cha utu uzima wao.
4. Huchangia mmomonyoko wa maadili pale watoto wanapokosa malezi na upendo
kutoka kwa wazazi wote wawili. Wakati mwingine watoto huiga matendo yasiyofaa ya
wazazi wao mfano kupigana, kutamkiana maneno mabaya mbele yao.
5. Watoto huchukia na kuliasi kanisa na huwachukia wazazi pia maana huona
wanachofundishwa na kinachotokea kwa wazazi wao walio sehemu ya familia hakiendani,
hivyo, kanisa na wazazi kuonekana kama siyo sehemu ya kujifunza jambo jema na zaidi
huuelekea ulimwengu.
6. Mabinti na vijana wa kiume watokao katika familia zilizovunjika huogopa au hukata
tamaa ya kuolewa au kuoa kwa kuogopa kuyapata yale yaliyotokea kwa baba na mama zao,
hivyo, huwa na mahusiano yasiyo salama au yale ya muda mfupi bila kupanga kushikamana
kama wanandoa.
7. Matokeo ya familia kuvunjika husababisha kanisa au jamii kuharibika kimaadili,
hivyo, husababisha ongezeko la mmonyoko wa maadili kutokana na vijana waliopatikana
ambao ni matokeo ya familia zilizovunjika.

Jinsi ya Kuepuka Kuachana (Kutalakiana) Kwa Wanandoa


Baada ya anguko la mwanadamu, imekuwepo changamoto kwa wanandoa
kuudumisha umoja wao (rejea Mwanzo 3:6-13). Kumezidi kuwepo na kizingiti, utengo, hofu,
uoga, visingizio, ubinafsi miongoni mwa wanandoa. Baada ya dhambi, wanandoa wamezidi
kuwa mbali wao kwa wao na wao na Mungu pia. Zifuatazo ni njia ambazo wanandoa
wanaweza kuzitumia ili kudumisha umoja wao na wasitengane:
 Wanandoa wanaooana, waoane wakiwa wa imani moja katika Kristo.
 Familia ziwe na ibada zenye maana kila siku ili Roho awe katika familia hiyo.
 Moyo na roho ya uvumilivu na misamaha iwe sehemu ya maisha ya wanandoa.
 Wanandoa wahakikishe kuwepo uaminifu miongoni mwao katika ndoa, hususani
kuaminiana wao kwa wao kwa kila mazingira ya uhusiano wao.
 Wanandoa waheshimiane, kusikilizana na kutatua matatizo yao wao wenyewe badala
ya kusikiliza na kuhusisha upande wa tatu usiojua ukina wa mgogoro. Wanandoa
wajifunze mbinu za kuwasiliana, kukubaliana na kushirikiana wao kwa wao.
 Pawepo uwazi, kushirikishana na uhuru katika kuwasiliana miongoni mwa wanandoa
ili kujenga hali ya uwazi na ukweli katika kila jambo.

Frank Philemon Karoli


48
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

 Yaepukwe manyanyaso na masimango miongoni mwa wanandoa ili kuondoa mianya


inayoweza kusababisha mmoja wa wanandoa kujitenga au kutojiona kuwa ni sehemu
ya ndoa au familia.
 Kila mmoja miongoni mwa wanandoa awajibike vyema katika majukumu yake ya
kifamilia ili kuepuka lawama au kulaumiana.
 Wazazi wa pande zote za wanandoa wahudumiwe kwa usawa bila upendeleo, lakini
pia wawekewe mipaka katika kutoa maamuzi kwenye familia ya wanandoa ambao ni
watoto wao.
 Wanandoa wajihusishe na kazi ya Mungu ili kuruhusu amani, upendo, furaha, ulinzi
na hekima itokayo kwa Mungu.
 Kuwepo na upatikanaji na kufikika miongoni mwa wanandoa katika nyanja zote ili
kutoa utayari wa kusikilizana, kushiriki furaha na maumivu kwa pamoja.

Jinsi ya Kufanya ili Kanisa Liepushe Ongezeko la Kuachana kwa Wanandoa:


 Zitolewe semina madhubuti za masuala ya kaya na familia ndani ya kanisa.
 Viongozi wa kanisa wahakikishe panafanyika ushauri, nasaha na semina kwa muda
wa kutosha kwa wachumba wanao talajia kuoana.
 Wanandoa wayatende kwa vitendo mafundisho wanayojifunza juu ya maisha ya
Ukristo na Kristo awe kielelezo kwao.
 Huduma na programu za mambo ya kaya na familia zielekezwe pia kwa vijana ili
kuwajengea uwezo na kujiandaa kisaikolojia juu ya majukumu na maisha ya ndoa
hapo baadaye.

Jinsi ya Kuponya Ndoa ili Kuepusha Kuachana kwa Wanandoa.


Ili kutengeneza ndoa yenye ustawi mzuri, yawapasa wanandoa kuwa na uwezo
mkubwa wa kuzikabili changamoto zinazojitokeza katika ndoa zao. Yawapasa pia wanandoa
kujua kuwa, ndani ya ndoa, kupishana mitazamo huwa kupo hata kama wanandoa
wanapendana kiasi gani. Hii ni kwa sababu ya kuwa, ndoa imeundwa na watu ambao siyo
malaika na sio wakamilifu kwa sehemu kubwa, hivyo kutofautiana kutakuwepo tu, na
kutakwisha endapapo uongozi wa Mungu utapewa kipa umbele.
Wanandoa ni vyema wakajua ya kuwa, ndoa (si zote ni baadhi) haikosi migogoro hata
ile midogo ya kiwango cha kawaida; makosa yanayopelekea kupitia hali na wakati mgumu.
Vyanzo vya migogoro vyaweza kusababishwa na mwanandoa mmoja au wote kwa sababu ya
ugomvi au kuhitilafiana na kufanyiana visasi pale mmoja anapokosewa au kukosea.
Kuhitilafiana katika ndoa hakujalishi kuwa ni kwa kiasi gani; wanandoa waweza kuwa
wanapendana lakini hapawezi kukosa migongano angalau hata kwa asilimia moja. Suala la
msingi huwa ni hekima au jinsi ya kuitatua hiyo mingongano ili kuinusuru ndoa. Baadhi ya
wanandoa hawajui cha kufanya pale wanapokuwa katika hitilafu na wenzi wao, hivyo,

Frank Philemon Karoli


49
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

huanza kujitangamanisha wao kwa wao bila kutatua hizo hitilafu kana kwamba
hawajakoseana chocho bali hukaa na jambo au mambo moyoni bila kuyatagfutia suluhu.
Ni kosa kubwa kwa wanandoa kuchukulia kuwa hawajakoseana na kukaa bila kutafuta
suluhu. Hali hii huwa ni hatari sana katika ustawi mzima wa ndoa, kwani huacha mioyo
ikiwa na utungu wa muda mrefu. Kila tatizo liletalo maumivu ya kihisia litatuliwe haraka na
kufutwa makosa kisha maisha ya amani na upendo katika Kristo yaendelee kama hapo awali.
Njia salama ya kuondoa hitilafu kwa wanandoa ni pale wanandoa wanapokubali kuwa:
kukoseana huwepo, hivyo, wajue kusameheana ili wapate kibali mbele za Mungu badala ya
dhambi kuzidi kuotea (Mwanzo 4:7).
Ndoa yo yote iliyojengwa katika kumtumainia Mungu na kuipa kipaumbele mipango
ya Mungu, hapawezi kuwa na migogoro ya mara kwa mara, bali amani itatawala daima
kwani wanandoa hao watakuwa wanaujua vyema upendo wa Kristo na wataudumisha
vivyohivyo katika ndoa yao (Yohana 13:17) katika kusameheana na kufutiana makosa yote.

Vikwazo Vinavyosababisha Wanandoa Wasiweze Kusameheana Wao kwa Wao:


1. Kutoishinda roho au hali ya kujivuna inayoondoa ubinadamu (Mithali 16:18),
2. Uzembe unaopelekea kutojali au kuhusika na mambo, hisia au changamoto za
mwingine (Mithali 24:30-34) miongoni mwa wanandoa,
3. Uoga wenye mazoea ya kutokukabiliana na jambo lenye kuleta madhara (hofu ya
kuogopa kukataliwa kwa msamaha, hofu ya kuogopa kushindwa, hofu ya kuogopa kuingia
katika mgogoro mkubwa zaidi),
4. Kuona aibu au haya kwa jambo lililofanyika na kuzaa mgogoro (2Wakorintho 12:9,
Yohana 1:11-13, na Wakolosai 3:12),
5. Na wwisho kabisa, wanandoa kuepuka kuonekana wenye hatia (2Wakorintho 7:10)
hivyo, kukaa na jambo bila kutafutiwa ufumbuzi wa namna ya kulitatua.

Kielelezo Kutoka Familia ya Ibrahimu


Mwanzo sura ya 16, 17 na 21, ni sura ambazo zina kisa kilichozoeleka sana kwa
Wakristo walio wengi. Sura hizo zinatoa taswira nzima juu ya familia ya Abramu (Ibrahimu)
na mkewe Sarai (Sara). Familia ya Abramu na Sarai ilikuwa na mjakazi aitwaye Hajiri
ambaye ni Mmisiri.
Familia hii ya Abramu na Sarai haikuwa na mtoto kwa muda mrefu (miaka mingi)
toka wameoana. Miaka iliposonga sana, Sarai alimshauri Abramu mumewe azae na kijakazi
aitwaye Hajiri ili kujipatia uzao (Mwanzo 16:2-4). Baada ya Ibrahimu kumjua Hajiri kama
alivyoshauliwa na mkewe. Hajiri alipata ujauzito na kujifungua mtoto wa kiume aliyeitwa
Ishimaeli (Mwanzo 16:11).
Ingawa Sarai alimruhusu mumewe kuzaa na kijakazi; matokeo hayo hakuyakubari na
alimtesa sana Hajiri baada ya kuonekana kuwa na kiburi juu yake: Mwanzo 16:6; “Naye
Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema
machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake”.
Baada ya Mungu kufanya agano na Ibrahimu; Mungu alimpatia mbaraka wa mtoto
aitwaye Isaka kupitia kwa mkewe Sara (Mwanzo 21:1-3). Isaka alizaliwa wakati ambapo
Ibrahimu alikuwa na miaka 100 na Sara alikuwa mwenye umri wa miaka 90. Hivyo, baada ya

Frank Philemon Karoli


50
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Sara kuzaa, familia ikawa na watoto wawili ambao ni Ishimaeli kutoka tumbo la Hajiri
(mjakazi) na Isaka kutoka tumbo la Sara mke halali wa Ibrahimu.
Watoto hawa ndio chanzo kikubwa cha mgogoro uliowatenganisha makazi baina ya
Hajiri na Sara (Mwanzo 21:8-10). Hivyo basi, kupitia familia ya Ibrahimu na Sara,
kunamambo machache ya kujifunza kama wanandoa na wale wanao tazamia kuingia katika
tasisi takatifu ya ndoa:
1. Abramu ni mfano wa mwanamume mwenye kusikiliza ushauli kutoka kwa mkewe
(Mwazo 16:2-3) na mwenye kusimamia haki (Mwanzo 16:6, 21:10-11). Wakati mwingine
imeonekana kuwa mwanamke hana wazo au neno lolote lenye tija linaloweza kujenga katika
ndoa. Kwa Ibrahimu haikuwa hivyo kwa mkewe; ndivyo yawapasa wanaume kuwa katika
ndoa zao. Ikumbukwe pia kuwa, kabla ya dhambi kuingia, mwanamke na mwanamume
walikuwa wenye daraja sawa na wote waliitwa Adamu baada ya kuumbwa ili kudhihilisha
kuwa mwanamke ametokana na ubavu wa mwanamume, hivyo ni mwili mmoja (Mwanzo
5:2); bali baada ya dhambi kuingia mwanamume alipewa mamlaka ya kumtawala mwanamke
(Mwanzo 3:16), .
2. Sarai ni mfano wa mwanamke mwenye kigeugeu juu ya maamuzi yake, (Mwanzo
16:5); mwenye jeuri na asiye na subira juu ya changamoto zinazojitokeza juu yake (Mwanzo
21:8-10). Mara nyingi imezoeleka kuwa, mwanamke hufanya maamuzi ya ghafla na
kutokuwa na subira juu ya changamoto fulani. Jambo hilo si jema kwa Mkristo, hekima na
subira hutakiwa ili kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi ili kutoleta madhara yenye
athari kubwa hapo baadaye katika ustawi wa ndoa. Kuwa na subira na kutoa maamuzi sahihi
bila harara haimuhusu mwanamke pekee, bali hata mwanamume pia katika ndoa yampasa
kuzingatia hilo.
3. Mara zote, Mungu hamuachi mtu anayeonewa pasipo kutendewa haki (Mwanzo
16:6-15). Mungu hakumuacha Hajiri pekee katika majonzi na utungu baada ya kukimbia
mateso ya Sara. Kilio cha cha Hajiri kilisikika kwa Mungu na Mungu akamtuma malaika
kumpa habari njema Hajiri. Yatupasa kujua kuwa, Mungu ni mwaminifu na hakawii
kututimizia hitaji na haja zetu wakati tunapomuhitaji au kuwa katika changamoto (Mwanzo
21:15-20). Sara aliamini kuwa anamkomesha Hajiri, kumbe anamtengenezea mazingira ya
kubarikiwa uzao wa tumbo lake. Hivyo, mwanandoa usilipe baya kwa adui yako bali lipa
jema na Mungu atakuwa nawe.
4. Mungu ndiye mwenye uweza wa kuwapa watoto hata walio vikongwe endapo
tumaini la mtu lipo juu ya Mungu (Mwanzo 17:15-17). Fikara za mwanadamu hukoma, lakini
Mungu Yeye ni muweza wa yote. Mungu hutupatia hitaji zetu pale tunapokuwa tumeshindwa
katika kutumia maarifa, nguvu na uweza wetu binafsi ili tu utukufu tumulejeshee Yeye.
Mtoaji wa watoto kwa wanandoa ni Mungu na si vinginevyo. Pale wanandoa wanapokosa
mbaraka wa watoto, wavumilie na wadumu katika kumuomba Mungu. Wasitumie njia
mbadala kama kwenda kwa mganga wa kienyeji, kuzaa nje ya ndoa, kuoa mke mwingine au
wanandoa kutalakiana.
5. Japo ni mara moja Ibrahimu alifuata matakwa ya mkewe na kuacha kumtii Mungu
katika kumjua Hajiri. Haidhuru, Ibrahimu bado ni kielelezo cha baba wa familia anayefuata
maelekezo ya Mungu nje ya utashi wake binafsi (Mwanzo 21:10-12). Mungu ni wa kwanza
katika kumtii kisha wanadamu na utashi wetu hufuatia. Wakati wote yatupasa kumtii Mungu
kwanza hata kama tupo katika mazingira magumu na nyakati hatarishi. Haikuwa rahisi

Frank Philemon Karoli


51
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Ibrahimu kumfukuza Hajiri na mwanae Ishimaeli kwa sababu ya msukumo wa Sara mkewe,
bali aliitii sauti ya Mungu bila kujali maumivu na uchungu wa moyo kwa mtoto wake
anayepaswa kutengana naye.
6. Heshima ya mama wa familia hushuka pale jukumu lake kwa mumewe
linapochukuliwa na mfanyakazi au kijakazi (Mwanzo 16:4). Kwa taswira ya sasa,
mfanyakazi wa ndani anapokabidhiwa majukumu hata yale yanayomhusu kuyatenda mama
wa familia, kutegemewe kupotea kwa heshima ya mama wa familia. Itegemewe kuwa,
ahsante zote za baba wa familia juu ya chakula, maji ya kuoga, kunyoshewa nguo,
kupokelewa mzigo, kufuliwa nguo, usafi wa nyumba na uangalizi wa watoto zitamwendea
mfanyakazi wa ndani ambapo ni halali ya mama wa familia kutoka kwa mumewe.
Udhaifu wa wazi wa mama wa familia katika kutotimiza majukumu yake kwa
mumewe au familia yake yanapotambuliwa na dada wa kazi, moja kwa moja dada wa kazi
hatakuwa na heshima au utii kwa mama wa familia; maana majukumu mazima ya familia
yapo katika uangalizi wake na ndiye msimamizi mkuu.
7. Uadui wa wazazi huhamia kwa watoto pia kwani chuki hupandikizwa juu yao
watoto (Mwanzo 21:9). Ni vibaya sana kuwashirikisha watoto uadui au chuki juu ya watu
wengine. Mazungumzo na masengenyo yo yote yasiwahusishe watoto, maana nao wanaweza
kutengeneza chuki ya moja kwa moja juu ya watu wanaosadikika kuwa ni maadui wa wazazi
wao. Ni vyema wtoto wakaambiwa kupisha pale panapooneka kuwepo kwa mazungumzo
yasiyofaa kwa watoto. Dhihaka ya Hajiri juu ya Sara ilionekana kwa Ishimaeli juu Isaka siku
ya karamu ya kuachishwa kunyonya kwa Isaka (Mwanzo 21:9). Dhambi ya chuki
iliyopandikizwa kwa watoto kutoka kwa wazazi huleta matokeo yenye madhara makubwa
miongoni mwa familia na jamii.
8. Mama (mzazi) mwenye upendo hawezi kuvumilia kumuona mtoto wake akifa huku
akiona kwa macho yake (Mwanzo 21:15-16). Ilikuwa ni vigumu kwa Hajiri kudumu
kumuona mbashara mwanae anavyopoteza uhai kwa kukosa maji ya kunywa alipokuwa
jangwani. Ndivyo ilivyo kwa mzazi ye yote mwenye mapenzi mema kwa mtoto wake
aliyemzaa; hawezi akawatelekeza au kutowapatia mahitaji ya msingi yaliyo chini ya uwezo
wake. Ndivyo pia Mungu anavyotupenda na hakutaka tuangamie dhambini, hivyo,
alitukomboa kwa damu ya thamani. Ifahamike kuwa: jambo la upendo na malezi ya watoto
linamahusiano makubwa sana na mambo ya kiroho juu ya mwanadamu na Mungu.
9. Si mpango wala maelekezo ya Mungu kwa mwanadamu kuwa na ndoa za mitala
(mke zaidi ya mmoja); bali ni maamuzi au utashi na tamaa za wananadamu. “Sarai
akamwambia Abramu, Basi BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu,
labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai” (Mwanzo16:2). Watoto
wanaozaliwa katika ndoa za mitala huwa hawaelewani kama ilivyo kwa wake wenza. Hivyo,
ni vigumu kujenga ndoa na familia yenye furaha na amani katika ndoa za mitala.
Hata hivyo, ili kupata maelezo ya kiteolojia zaidi juu ya familia ya Ibrahimu, waweza
soma Wagalatia 4:21-31, ukioanisha na Wagalatia sura ya tatu na sura ya nne yote.

Frank Philemon Karoli


52
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 07 =

JINSI YA KUWA MKE AU MUME MWEMA KATIKA NDOA NA


FAMILIA YA KIKRISTO

“Kinywa chake kimejaa maneno matamu, Ndiye mzuri sana pia pia. Ni
huyu mpendwa, ni huyu rafiki yangu…..”

Wimbo Ulio Bora 5:16

“Familia ambazo baba na mama wamemweka Mungu kuwa wa kwanza nyumbani


mwao, na kuwafundisha watoto wao kutambua kuwa kumcha BWANA ni chanzo wa
hekima; wanatengeneza familia zenye utaratibu bora na zenye nidhamu. Kristo siyo mgeni
nyumbani kwao – Jina lake ni jina la nyumbani, linaloheshimika na kutukuzwa. Malaika
wanafurahishwa na nyumba ambako Mungu ni mtawala mkuu na watoto wameelekezwa
kuheshimu dini, Biblia na Muumbaji wao” [E. G. White, The Adventist Home, uk. 27].
Yampasa Mkristo kujua kuwa kalama ni kipawa au zawadi atoayo Mungu, bali tabia ni
uchaguzi wa mtu mwenyewe. Sura hii ya kitabu inatoa muelekeo sahihi kwa wanandoa na
vijana ambao bado hawajaoa wala kuolewa ili kuwa wenzi wema katika ndoa na familia zao.

Mume Mwema Katika Ndoa na Familia


Katika sababu zifuatazo zitamuongoza mwanandoa mume kujua wapi amepungua na
arekebishe kwa kumshirikisha Yesu ili amsaidie kuwa mume mwema mwenye kufaa. Mume
mwema yampasa awe na sifa zifuatazo:
Mume mwema ni yule anayempenda mkewe kuliko kazi, vitu na watu wengine: Mke
hufuatia baada ya Mungu na nafasi ya tatu ni watoto, ya nne ni wazazi wa pande zote, na ya
tano ni kanisa, kazi nakuendelea.
Mume mwema hupanga mambo ya familia akiwa na mke wake: Huomba ushauri,
nasaha, maoni na mapendekezo kutoka kwa mkewe na kisha humwelekeza mke nini cha
kufanya katika mipango na makubaliano.
Mume mwema huwasiliana na mke wake katika kila jambo: Katika ndoa kila jambo
mume lazima amjulishe au kuwasiliana na mke wake kabla ya kutenda au kulifanya.
Mume mwema humsaidia na humtia moyo mke wake: Ni vyema mume akamsaidia
na kumtia moyo mkewe pale anapokuwa ametingwa na mambo au majukumu katika familia.
Mume mwema humsoma na kumwelewa mke wake: Mwanamume ni vyema akajua
udhaifu wa mke wake, uimara wake, umahili wake, na wapi, nini hushindwa na kwa sababu
gani. Nini na kipi, na wakati gani cha kuongea naye ili kumsaidia, kumtia moyo na
kubebeana naye madhaifu katika maisha ya ndoa.

Frank Philemon Karoli


53
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Mume mwema humheshimu mke wake: Mume ya mpasa kumheshimu mke wake.
Katika mambo mazuri, au mabaya mume lazima atumie lugha sahihi na iliyo ya staha katika
kufikisha ujumbe kwa mke wake wakati awapo peke yake au awapo mbele za watu.
Mume mwema ni mwaminifu kwa mke wake katika kila kitu: Hasa katika mambo ya
ndoa na mambo ya fedha au mali. Mwanamume yampasa kuwa wazi bila kificho wala
kudanganya juu ya matumizi na kile anachomiliki kwa mke wake wa ndoa.
Mume mwema huvaa vyema na nadhifu: Mwanamume aliye katika ndoa ni vyema
akawa safi na nadhifu katika kuvaa awapo mbele za Mungu, familia (watoto) na katika
shughuli zake za kazi au ofisini kama siyo ya kuchakalika.
Mume mwema ni yule anayeheshimu ndugu na wazazi wa mke wake na
kuwahudumia bila kuwabagua: Mwanamume aliyemume mwema asiwaongee vibaya,
kuwachukia au kuwabagua ndugu wa mke wake wa ndoa.
Mume mwema huhudumia na kutoa mahitaji yote kwa familia yake: Mume mwema
yampasa kuhudumia familia ipasavyo mfano tiba, chakula, malazi, elimu, na mengine
yaliyochini ya uwezo wake na yanayotekelezeka kulingana na uwezo wake wa kiuchumi.
Mume mwema ni yule ambaye hutenga muda wa kuwa na familiya yake:
Mwanamume katika ndoa lazima atenge muda wa kutosha wa kuwa na mkewe pamoja na
watoto ili ashiriki furaha, maumivu, majonzi, mafanikio, kushindwa, mipango na mawazo juu
ya ndoa na familia yake.
Mume mwema ni yule aliyempokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wake: Sio wote
wanaosali wapo karibu na Mungu. mume mwema lazima amuishi Yesu na kutembea katika
njia zake. Ajue kuwa popote alipo, aendapo, atendacho Mungu anamwona maana kwake
hapana kificho.
Namna ya Kuwa Mke Mwema Katika Ndoa
Biblia inasema kuwa mke mwema hutoka kwa Bwana; ili mwanandoa awe mke
mwema yampasa kuwa mwenye sifa na tabia zifuatazo katika ndoa:
Mke mwema awe mnyenyekevu daima kwa mume wake: Awe mwenye hekima na
mwenye kumjibu vizuri kwa adiri mumewe. Kulingana na hurka ya wanaume si salama
mwanamke akampandishia sauti mmumewe, maana tabia hiyo huwa haitatui chochote au
kumjenga mwanamume (Mithali 15:1).
Mke mwenye hekima hatoi siri za ndani za udhaifu wa mumewe kwa watu
wengine: Mwanamke kutoa siri za ndani zenye kuhusu udhaifu wa mume wake haimuaibishi
mume pekee bali hata yeye mwanamke anayetoa hizo siri. Kutoa siri za ndani ya ndoa
huondoa maana kamili ya kuwa, wanandoa ni mwili mmoja katika kubebeana madhaifu
(Waefeso5:12).
Mke mwema hamfananishi mume wake na wanaume wengine: Kufanya hivyo ni
kumpunguzia nafasi yake ya upekee kwako maana wanadamu wote hawafanani hivyo ni
ishara ya kutompenda au kutobebeana naye mapungufu yake, ispokuwa ni salama sana
kumwelekeza kwa upendo pale jambo au suala fulani halipendezi huku ukizidi kumuombea
ili abadirike kwa uwezo wa Mungu anayemjua zaidi.
Mke mwema huwapenda marafiki na ndugu za mume wake: Mke mwema haimpasi
kugombana au kugombezana na watu hususani ndugu na marafiki wa mume wake; ni vyema
na kupendeza mke akawaacha waamue mambo na mume wake ili asionekane kutenda vibaya

Frank Philemon Karoli


54
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

juu yao. Inapotokea mwanamke amekwazwa na jamaa za karibu wa mumewe, ajitahidi


kusema nao kwa upole na hekima.
Kutukanana au kugombezana nao kwa kujibishana maneno yasiyofaa au lugha zenye
kuudhi mwanamke (mke) ataonekana kuwa hana akili wala hekima mdomoni mwake kwa
yale anayoyatamka (Mithali 15:2, 13). Hivyo basi, mwanamke yampasa kuwa na hekima na
mkarimu kwa watu wote wanaomzunguka nje hata ya ndugu za mume wake.
Mke mwema yampasa kufanya majukumu yake vyema juu ya mume wake: Haifai na
haipendezi kila jambo au jukumu mke kumuachia mfanyakazi wa ndani alitekeleze maana
kufanya hivyo kutapunguza ukaribu na upendo kwa mumewe. Kwa maana hiyo, ikibainika
kuna mambo mazuri anayo yatenda mfanyakazi wa ndani, mume atamsifia ilihali ilimpasa
amsifie mke wake. Haimpasi mwanamke kumpa majukumu mtu mwingine hususani yale
yanayompasa ayatende yeye kama yeye kwa mumewe (Mwanzo 2:24, Waefeso 5:33).
Mke mwema ni yule anayemtia moyoni mumewe pale anapoonekana kutofanikiwa:
Ni kosa kubwa sana kwa mwanamke kumlaumu mumewe kwa sababu ameshindwa
kufanikiwa au amerudi nyumbani mikono mitupu. Mwanamke aliye mwema yampasa
kumtia moyo mume wake ili kutomkatisha tamaa katika kufanya mihangaiko ya kutafuta
maana ipo siku Mungu atambariki na atapata (Kumbukumbu la Torati 3:28).
Mke mwema hutumia pesa na mali vizuri: Mke mwema ni yule anayetumia pesa na
mali vizuri waliyoitafuta yeye na mume wake, maana jasho lao ni la thamani sana hivyo
halitakiwi kupotea bila utaratibu wenye tija. Mwanamke awe na nidhamu nzuri juu ya mali
na pesa ili kuyafanikisha maendeleo ya familia kama walivyojipangia yeye na mumewe.
Mke mwema ni yule asiyemjibu vibaya mume wake mbele za watu: Majibu
yasiyokuwa na hekima si vyema mwanamke kumjibu mumewe mbele za watu kama vile
watoto, wageni, au umati wa watu. Mwanamke mwenye hekima atamsubiria mumewe hadi
afike nyumbani hususani chumbani (au kumwita faragha) ndipo atumie fursa hiyo kutatua
matatizo yake na mumewe kwa hekima, adili na upendo (Mithali 13:3).
Mke mwema ni yule mwenye kujali usafi na kujitunza katika unadhifu: Mwanamke
mwema yampasa kuwa msafi daima hususani katika nyanja zote na mwenye kujitunza katika
unadhifu wake ulio wa asili bila kutumia vipodozi vyenye kemikali kali inayochubua au
kuharibu ngozi (Yeremia 13:23). Yampasa mwanamke kuvaa mavazi safi ya heshima yanayo
stili maungo ya mwili vyema. Usafi na unadhifu ni kitu cha msingi sana kwa mwanamke ili
kudumisha upendo kwa mume wake maana atakuwa ni mwenye kupendeza na kumvutia
mumewe kila siku na kila wakati.
Mke mwema ni yule anayempenda mume wake kwa hali zote: Upendo wa kweli
hauna mazingira, muda wala umri, hivyo mwanamke ya mpasa kumpenda mumewe katika
kila hali na namna. Si salama upendo wa mwanamke kwa mumewe ukawa tu pale
anapokuwa na kitu la hasha, upendo wa kweli hauna mafanikio wala shida au uwepo wa
chochote kile (1Wakorintho 13:4-7).
Mke mwema anatenga muda wa kutosha wa kuwa na mume wake: Haijalishi kuwa
mwanamke ana majukumu kiasi gani, yampasa kutenga muda wa kuwa na mumewe ili
kupalilia na kudumisha upendo. Kwa wanandoa, ni vyema pasikosekane matembezi na safari
za pamoja kati ya mke na mume, hivyo, shughuli zote zinazomfanya mwanamke kukosa
muda kwa ajili ya mumewe, lazima aziweke kando katika muda unaompasa kuwa na
mumewe.

Frank Philemon Karoli


55
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Mke mwema ni mbunifu kwa mume wake: Mwanamke yampasa kuwa mbunifu
kulingana na mazingira na wakati. Mfano vile vitu anavyovipenda mumewe yampasa
avifanye kwa ubunifu mkubwa na avikuze siku kwa siku na asivyovipenda mumewe aviache
mara moja ili kutomkwaza. Ubunifu waweza kuwa katika upambaji wa ndani ya nyumba,
biashara, mitindo ya mavazi ya heshima yenye kuvutia n.k. ili kuleta ustawi, mvuto na
maendeleo yenye tija katika familia.
Mke mwema aepuke tamaa ya vitu vya gharama vilivyo nje ya uwezo wa kipato:
Tamaa ya vitu vya gharama vilivyo juu ya uwezo wa kipato cha wanandoa, mwanamke
mwema huviepuka kwani anajua mazingira na hali ya kipato cha ndoa yao, na haombi vitu
vya gharama kuzidi uwezo wa kipato alicho nacho mumewe.
Mke mwema hana marafiki wasio wema: Mwanamke anayejitambua hana makundi
au marafiki wasio wema katika tabia na matendo, hivyo, huwaepuka marafiki wote wenye
mawazo hasi na mitazamo na tabia mbaya zisizofaa katika kuigwa. Upendo na ukarimu wake
uwe kwa watu wote lakini si kwa kushikamana na kufanya urafiki nao wale wote wenye
mienendo na tabia mbaya zisiyofaa katika maisha ya Mkristo.
Awapende na kuwalea vyema watoto wake: Mwanamke aliye mke mwema
huwapenda na kuwalea watoto wake katika matendo mema ili wasipotee maana uzao wa
tumbo lake ni baraka kutoka kwa Mungu, hivyo hata watakapo kuwa wazee hawataicha njia
ya kweli (Mithali 22:5).

Kanuni Nane (8) Za Msingi Kwa Wanandoa


Kila ndoa au wanandoa huwa wanakanuni zao zinazotengeneza falsafa ambayo
hutofautisha ndoa au familia moja na nyingine. Kanuni zifuatazo ni mhimu kwa wanandoa
wakazizingatia ili kuleta ustawi mzuri wa ndoa na familia zao:
Upendo na mahaba: Mahaba ni hisia, tendo au matendo yanayodhihirisha upendo
kwa mwenzi (soma Mwanzo 26:8). Mahaba ni zao la upendo na hudhihirisha upendo kwa
wenzi kuwa wapendanao. Mwanandoa ye yote asimpende mtu mwingine tofauti na mwenzi
wake wa ndoa.
Uaminifu: Mwanandoa asifanye uzinzi nje ya ndoa, wala kufanya usaliti wa aina yo
yote juu ya ndoa yake.
Sitaha mbele za watu: Mwanandoa yampasa kuongea kwa uangalifu, heshima,
nidhamu kwa mwenzi wake awapo mbele za watu au watoto.
Kuhifadhi kumbukumbu: Mwanandoa akumbuke kuhifadhi na kukumbuka siku na
tarehe muhimu katika maisha ya mwenzi wake. Mfano tarehe ya kuzaliwa, ndoa, kuhitimu
masomo n.k.
Heshima: Mwanandoa awahesimu wazazi na ndugu wa pande zote na wala
asiwaseme kwa mabaya na maovu yao kwa mwenzi wake wa ndoa.
Kujali: Mwanandoa amuelekeze mwenzi wake kwa upendo na upole pale anapokosea
na wala sio kumtukana, kumkosoa vibaya na kumtuhumu vikali kutokana na mapungufu au
madhaifu yake.
Uwazi: Mwanandoa asimdanganye mwenzi wake, bali awe muwazi na mkweli katika
mamboyake yote ili kujenga mshikamano na ushirikiano.

Frank Philemon Karoli


56
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Shirika na Ushirikiano: Wanandoa wamiliki vitu kwa pamoja na shirika maana


kwenye ndoa, vitu vyote ni vya wote na hakuna aliye na chake. Kama mmoja wa wanandoa
anakitu chake, basi hiyo ndoa itakuwa ina changamoto.

Frank Philemon Karoli


57
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 08 =

FUNZO KUTOKA „MITHALI 31:11-3‟ KWA WANAWAKE WALIO


KATIKA NDOA

“Mwanamke mwema ni taji ya mumewe; Bali aaibishaye ni kama kuoza


mifupani mwake”.

Mithali 12:4

Mithali 31:11-31 inatoa somo na mchango wa kuibadirisha jamii ya kinamama walio


katika ndoa zao aidha, kwa muda mrefu au muda mfupi, pamoja na wale wanaotarajia
kuingia katika tasisi hiyo takatifu ya ndoa. Kwa hiyo, wanawake walio katika ndoa kuna
mambo ya kujifunza mengi yenye kujenga ndani ya kitabu cha tano cha Mithali za Mfalme
Sulemani. Ni nukuu ya maneno ya Mfalme Lemueli; Muasia kama alivyofundishwa na mama
yake ambayo Sulemani aliyaandika katika kitabu cha Mithali.
Mafundisho hayo ni ya msingi kwa kiasi kikubwa kwa mwanamke aliye katika ndoa
au nje ya ndoa. Pitia kwa umakini ili kuona mambo mazuzuri na bora ya kujifunza na yenye
kujenga ustawi mzuri wa ndoa na familia:

Mwanamke katika ndoa yake, anamchango mkubwa wa kuleta mafanikio, hivyo


mume yampasa kuweka imani kubwa juu ya uwezo wa mkewe katika kuleta mafanikio
ya familia. Mithali 31:11 inasema: “Moyo wa mumewe humwamini, wala hatakosa kupata
mapato”. Kiasi kikubwa cha maendeleo ya familia kwa wanandoa huchochewa na
mwanamke. Mwanamke ni katibu na mtendaji kazi mkuu wa familia. Mwanamke
asiposimama imara katika familia, basi mambo mengi yatayumba katika familia au kwa
wanandoa. Kwa dunia ya sasa siungi hoja wala mtazamo juu ya mwanamke kuwa tegemzi
kwa kila kitu, maana dunia ya sasa ni kusaidiana katika kulisukuma guludumu la maendeleo
na mafanikio ya familia. Gharama za maisha zimepanda na mahitaji pia yameongezeka katika
kulea na kutunza watoto pamoja na kuishi kwa ujumla.
Kuna haja ya mwanamume kumwamini mkewe kuwa ana sehemu kubwa ya
kuchangia maendeleo, siyo kila mara atakapo kununua kitu aombe kwa mumewe pesa.
Mwanamke kuwa tegemezi kwa mume kwa kila kitu, ni kuandaa janga kubwa hapo badae;
maana mwanamume huyo abebaye jukumu lote la kuhudumia kuna kufariki, kufukuzwa kazi,
kuugua kwa muda mrefu, au kufungwa jela; na hapo yaweza kuwa ndiyo mwisho wa watoto
kusoma shule zenye ubora, na mambo mengine kupwaya.
Endapo mwanamke atapewa nafasi na kuaminiwa katika michakato ya kutafuta,
kujishughulisha katika njia zisizoharamu, basi mume aamini ya kuwa familia yake haitalala
njaa, au kuombwa pesa mara kwa mara toka ukweni. Mwanamke mvivu, asiejishughulisha ni

Frank Philemon Karoli


58
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

mzigo kwa mumewe, anakwamisha maendeleo ya familia na hafai kuwa mama wa kuigwa
isipokuwa kwa kukatazwa na mumewe tu.

Mwanamke katika ndoa yake daima atende mema kwa mume wake pasipo
kikomo. Mithali 31:12 inasema: “Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha
yake”. Mwanamke mwenye hekima anayemtumainia Mungu, hapaswi kumtendea mabaya
mumewe siku zote za maisha ya ndoa. Si vyema mwanamke kumsema vibaya mume wake,
kutoa siri, mapungufu na udhaifu wa mme wake kwa watu wengine. Sio sawa kumuwazia
mabaya mume wake, wala kutomthamini wala kutomjali, au kumdharau, kumsaliti na
kumjibu kwa jeuli mume wake. Mke amtendee mema na mazuri mume wake. Pale mwana
mume anapokosea mwanamke anene naye kwa adabu na hekima.
Nashauri kwamba: Ikitokea mume wako amekukosea, jitahidi kumsamehe na
umuombee badala ya kumjengea chuki au kumuwekea kisilani na kumnunia. Epuka kuwa na
hasira juu ya mume wako. Daima tambua kuwa, wewe na mume wako ni mwili mmoja, hivyo
mnene na mnuie mamoja ili kustawisha familia yenu. Na kamwe upendo wako usipungue juu
ya mumeo. Upendo wako udumu bila kujali muda, wakati, mazingira, sehemu na hali ya
kimaisha; upendo wako juu yake utamalaki daima.

Mwanamke katika ndoa yampasa afanye kazi zake kwa moyo na bidii. Mithali
31:13 inasema: “Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo”.
Mwanamke mwenye kumtumainia BWANA, ni mwenye bidii katika kufanya kazi na
kutafuta. Hufanya kazi za nyumbani na za kiuchumi kwa moyo wa bidii, na hakomi kuonesha
bidii katika kutafuta, ilimradi yote hayo anatenda kwa sababu ya ustawi wa familia yake.
Wakati mwingine, haina haja ya mfanyakazi wa ndani endapo sehemu ya majukumu
yanayomhusu mwanamke atamtendea mume wake na familia kwa ujumla. Mwanamke
atawaliwapo na moyo wa upendo wa kimbingu, hana sababu ya kujivuna, kujiona na
kujikweza katika suala zima la majukumu ya kifamilia, na yale yote yanayohusu ustawi na
afya ya familia yake.

Mwanamke katika ndoa anatakiwa kuwa mtafutaji na awe na moyo wa


kujituma hata kwenda maeneo ya mbali. Mithali 31:14 inasema “afanana na merikebu za
biashara; huleta chakula chake kutoka mbali”. Kunawakati mwingine baba wa familia
kukwama na hutingwa na majukumu kadhaa, mwanamke mwanandoa humpasa kuchukua
sehemu ya majukumu ya mumewe katika kusimamia na kumsaidia majukumu mumewe;
Mathalani masuala ya shamba, miradi, kupeleka na kuona watoto shuleni au kufuatilia
maendeleo ya watoto ya kishule hata kama ni mbali kiasi gani bali ni kuonesha kuijali familia
yake.
Jambo la msingi lingine, mwanamke awe radhi kutembea umbali mkubwa ili kutafuta
au kuvuna chakula kwa ajili ya familia yake. Wapo baadhi ya wanawake katika wanandoa
hawawezi kwenda kisimani kuchota maji, kwenda shambani kuvuna mazao, kwenda kwenye
mradi kusimamia kisa tu pako mbali na nyumbani. Aina ya wanawake hao ni wavivu wa
kutupwa na hawana moyo wa kufanya jambo ili kuhudumia na kustawisha familia zao. Wapo
radhi kulaza (au kuzishindisha) njaa familia kwa sababu ya umbali tu wa shamba, kisima,
soko n.k.

Frank Philemon Karoli


59
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Mwanamke katika ndoa anatakiwa kuamka mapema ili kupangilia na kuandaa


chakula cha familia yake. Mithali 31:15 inasema: “Tena huamka kabla haujaisha usiku;
huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi sehemu zao”. Uhai wa familia
katika ndoa upo mikononi mwa mwanamke. Katika masuala juu ya nini kipikwe, nini kiliwe
na kwa kiasi gani na kwa wakati gani ni jukumu la kifamilia ambalo lipo chini na mamlaka
ya mwanamke. Tena yampasa mwanamke kuamka asubuhi ya mapema kuhakikisha uhakika
na upatikanaji wa chakula kwa wanafamilia wote. Haina haja ya kubagua katika utoaji wa
huduma ya chakula, wote wapatiwe hata kwa wale wasio wanafamilia ilimradi tu wapo
malango mwa familia maana huo ndio ukarimu.
Jambo la kuamka mapema asubuhi na kuandaa chakula cha familia, ni jambo la
msingi kwa mwanamke katika ndoa. Watoto waendapo shule waondoke wamekula
(wamepata kifungua kinywa); baba wa familia aendapo kazini, aondoke nae akiwa amekula
chakula. Kula kwa pamoja asubuhi kunaepusha gharama za maisha katika kufanya
mgawanyo wa pesa na matumizi. Haipo sababu ya baba, mama na watoto wa shule kutumia
pesa ili kupata kifungua kinywa migahawani wakati upo uwezekano wa mama kuamka
mapema asubuhi na kuandaa chakula cha asubuhi kisha wanaoenda kazini waende na
wanaoenda shuleni waende.

Mwanamke yampasa kutafuta mapato, mali au kuanzisha miradi


itakayonyanyua uchumi wa familia yake. Mithali 31:16 inasema: “Huangalia shamba,
akalinunua; Kwa mapato yake hupanda mizabibu”. Wapo wanandoa (wanawake) wengi
huwekeza pesa zao katika nguo, kula, mapambo, vipodozi na mambo mengine ya anasa.
Mwanamke mwenye akili hutafuta mali na kuweka kwa ajili ya manufaa ya badae ya watoto
katika familia. Mwanamke yampasa kujitahidi kubana matumizi na kutumia pesa palipo na
jambo la msingi.
Endapo mama wa familia anapesa kiasi chochote na inaweza kutumika kuwekeza
kwenye mradi au shughuli yoyote; huo mradi au shughuli iliyowekezwa yaweza kusaidia
watoto au kuinua uchumi wafamilia hapo mbeleni. Mwanamke mwenye kuipenda familia
yake, huwekeza kwa ajili ya familia aipendayo, ili siku za usoni papatikane manufaa; hivyo,
mwanamke awekeze hata kwenye elimu ya watoto pia.

Mwanamke ya mpasa awe shupavu na imara katika suala la kujituma na


kuchapa kazi. Mithali 31:17 inasema: “Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi: Huitia
mikono yake nguvu”. Mwanamke akiwa mlegevu na mtepetevu kwa kila jambo, basi hapana
asubuhi katika kufanikisha kuinyanyua familia yake. Hataweza kuwajenga watoto wake
katika moyo wa kupenda kazi maana yeye pia hawezi kufanya hivyo. Mwanamke
akijikomboa kifikra katika kupenda kutenda kazi, amekomboa familia na sehemu taifa pia.
Kwenye ndoa mara azote ni wakati wa kupambana ili kuboresha uchumi pamoja na
mafanikio au maendeleo ya familia.
Miaka ya nyuma kidogo, jamii nyingi upande wa Tanzania katika ziwa Victoria
iliangalia sifa kuu ya mwanamke kuolewa ni uchapa kazi wake, maana ilikuwa ni aibu
familia kukosa chakula ili hali kwamba shamba lipo na nguvu kazi ipo (bibi na bwana).
Familia nyingi zilijengwa katika uchapa kazi na asilimia kubwa hazikuwa zinashambuliwa na

Frank Philemon Karoli


60
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

baa la njaa maana zilifanikiwa kuwa na chakula cha kutosha, hivyo, zilisonga mbele
kimaisha.

Mwanamke aweke akiba ya mapato yake ili asipungukiwe katika familia yake.
Mithali 31:18 inasema “Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku”.
Mwanamke laziwa awe mwanauchumi; ajitahidi kuhifadhi faida iliyotokana na nguvu kazi
yake. Lakini pia, yampasa afanye mahesabu mazuri kwa kile anachotaka kuwekeza (katika
mali au bidhaa) na kufanya, na awe na uhakika ya kuwa kitamletea faida hapo badae na sio
hasara. Taa (mtaji) yake idumu kuwaka ikiwa na mafuta tele. Yaani mtaji wake uzidi
kuongezeka kila siku bila kukata. Hivyo basi, mwanamke mwenye fikra pevu, huwekeza
kwenye mambo yaletayo faida na sio yatoayo au kuleta hasara.

Mwanamke katika ndoa, mikono yake iwe shupavu katika kutenda na kufanya
kazi. Mithali 31:19 inasema kuwa: “Hutia mikono yake katika kusokota; na mikono yake
huishika pia”. Hakuna kitu kizuri kama kuona manufaa na mafanikio yatokanayo na kazi ya
miko yako. Vivyohivyo kwamwanamke kutia mkono katika kujenga maendeleo ya famila
yake huleta furaha isiyo na kifani.
Mwanamke atakuwa na amani ya umiliki na amri juu ya mali au mapato ya familia
yake maana akili na mkono wake utakuwa umechangia kuyatafuta. Mwanamke aliye katika
ndoa apende kujishughulisha kwa kutumia uwezo wa akili na mikono yake ili kufanikisha
ustawi na ukuaji wa maendeleo ya familia yake. Si vyema mke akamuachia mume wake
jukumu lote la ufanikishaji mzima wa maendeleo ya familia.

Mwanamke katika ndoa yake, awe na moyo wa ukalimu, huruma na katika


kusaidia wengine (wahitaji) Mithali 31:20 inasema hivi: “Huwakunjulia masikini mikono
yake; Naam, Huwanyoshea wahitaji mikono yake”. Mwanamke anaemcha Mungu ni sehemu
ya kisima cha busara na msaada wa mawazo kwa jamii na wanafamilia wanaomzunguka.
Roho ya kutoa au kusaidia wahitaji pamoja na kukalimu wageni hufungua mibaraka ya
Mungu kwa familia.
Roho au tabia ya uchoyo na ukali mwingi hukimbiza wageni katika familia. Tabia
hiyo, hupelekea kufunga mibaraka kutoka kwa Baba wa Mianga. Mwanamke mwanandoa
yampasa kuwa na tabia ya kuvaa viatu vya matatizo ya wengine (aweza kuwa mumewe),
hurumia na kukumbuka kuwaombea walio katika shida na uhitaji. Kufanikiwa kusiwe
sehemu ya kuwanyanyasa na kuwatesa wengine, bali kuwe ni mbaraka na watu wamuone
Kristo juu ya mafanikio hayo.

Mwanamke ahakikishe usalama wa afya ya familia yake. Mithali 31:21 inaelezea


kuwa: “Hawahofii theluji watu wa nyumani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake
huwavika nguo nyekundu”. Kuwavika nguo nzito wanafamilia wakati wa baridi kali, ni moja
ya jambo linaloelezea kitendo na hari ya ujalifu (kujali) kwa mwanamke miongoni mwa
wanafamilia wake. Ni jukumu la mwanamke kujali au kuzingatia suala la usalama wa kiafya
la wanafamilia wote; Mfano kunywa maji safi na salama, mtoto yupi amechemka kwa sababu
ya homa na tiba ipi au chanjo inatakiwa, pamoja na kutekeleza utaratibu wa lishe au mlo
kamili kwa wanafamilia wote. Kwa hiyo, sehemu kubwa mwanamke ndiye mwangalizi na

Frank Philemon Karoli


61
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

mfuatiliaji wa mambo mengi ya kifamilia kuliko baba wa familia. Hivyo basi, uhai na
usalama wa kiafya upo kwa mama wa familia hata kama kuna kunamfanyakazi wa ndani.

Mwanamke katika ndoa yake awe hodari katika ubunifu na unadhifu katika
mavazi yake. Mithali 31:22 inaelezea kuwa: “Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake
ni kitani safi na urujuani”. Mambo ya upambaji, usafi wa nyumba na vyombo, mpangilio wa
vitu ndani, na utunzaji wa mali za ndani; ni sehemu ya jukumu la mama wa familia. Ubunifu
wa mapambo ya ndani, mfano kusuka na kufuma vitambaa, kudalizi mashuka n.k. ni jukumu
linalosimamiwa na mama wa nyumba pia.
Mama wa familia lazima ajijali katika usafi wa mwili na mavazi pia. Avae mavazi
nadhifu yenye kuvutia hata kama sio ya bei kubwa, bali mpangilio na usafi pekee ndio
kinachotakiwa. Kuolewa kwa mwanamke sio kuwa ndiyo kikomo cha kujiweka safi katika
hali ya unadhifu. Haipendezi kwa mwanamke kuvaa nguo zinazoshusha heshima, bali
yampasa avae nguo zinazostili mwili vyema. Kuvaa nguo zisizo za heshima na za kuaibisha,
ni kujiaibisha au kujidhalilisha, kujipunguzia heshima na kumdhalilisha mume na watoto pia.

Mwanamke katika ndoa amletee na kumjengea heshima mumewe. Mithali 31:23


inasema: “Mume wake hujulikana malangano; Aketipo pamoja na wazee wa nchi”. Mke
mwenye uchaji wa Mungu ni yule asiyeuaibisha ubavu wake, yaani mme bali huuletea
heshima kwa jamii inayomzunguka kutokana na matendo yake mema na mazuri. Sifa njema
za mwanamke ni fahari kwa mume wake, na tabia mbaya nia aibu kwa mumewe pia. Tabia
mbaya kama usengenyaji, uchonganishi, uvivu, kiburi, matukano, wizi, utapeli, ulevi,
umalaya, uasherati, utumiaji wa madawa ya kulevya kwa mwanamke, yote humchafua
mumewe na aibu humjaa mume na asiwe na jambo la kujivuni juu ya mke wake.
Tabia njema kama ukarimu, hekima, busara, uchapa kazi, matumizi mazuri ya lugha,
heshima n.k. ni sifa njema kwa mwanamke katika jamii na mume wake au familia pia.
Mwanamke mwanandoa ni vyema kuepuka kumuaibisha mume wake kwa mienendo na tabia
mbaya. Mwanamke kuwa na matendo au tabia mbaya, yaweza pelekea mume wake asiweze
hata kuongozana naye njiani au kufurahia kumtambulisha kwa jamaa na rafiki zake.

Mwanamke katika ndoa ajitahidi na yeye kujishughulisha ili asiwe mzigo na


tegemezi kwa mume wake. Mithali 31:24 insema: “Hufanya nguo za kitani na kuziuza;
Huwapa wafanya biashara mishipi”. Mwanamke kujishughulisha ili asiwe mzigo kwa jamii
na mume wake, nimelizungumzia kwa kina katika aya zilizopia huko juu. Nashauri kuwa, si
vyema mwanamke akawa tegemezi, japo mwanamume ananafasi ya msingi katika
kumhudumia familia.

Mwanamke mwenye hadhi na atendae kazi kwa nguvu, asiwaze juu ya jinsi gani
aishi kesho, bali huufurahia wakati ujao maana anajiamini katika kutafuta. Mithali
31:25 inasema: “Nguvu na hadhi, ndiyo ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao”.
Mwanamke mchapa kazi ana amani na matumaini juu ya kesho yake na familia yake.
Kutokana na uchapa kazi, hana wasiwasi na maisha maana ana moyo wa bidii ambapo ana
amini haishi kwa kubahatisha wala hawezi kumtegemea mume wake na kukaa akiwaza juu
ya kukosa na kufanikiwa kwa mmewe. Mwanamke anayetegemea mafanikio ya mume wake,

Frank Philemon Karoli


62
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

hana matumaini kwa sababu uhakika wa kupata ama kukosa mkate wa familia upo juu ya
kupata au kukosa kwa mumewe.

Mwanamke katika ndoa ajitahidi kuwa mwema na mwenye hekima. Mithali


31:26 inaeleza kuwa: “Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema katika
ulimi wake”. Ina aminika kuwa, asilimia kubwa ya wanamke ni waongeaji sana kuliko
wanaume. Kubarikiwa kuongea sana kwa mwanamke sio kigezo cha kinywa chake kukosa
hekima na kunena yaliyomema. Mwanamke mwenye hekima hatumii ulimi wake vibaya ili
kuleta magonvi ndani ya ndoa yake. Matusi au kauli mbaya pamoja na kutumia lugha
isiyokuwa na staha, si vyema yakatumiwa na mwanamke aliye katika ndoa juu ya mumewe,
watoto au watu wengine.
Majibu ya ovyo na matusi, mara nyingi huchochea hasira kwa wale wagombanao kwa
maneno. Mwanamke mwenye hekima hunyamaza kimya, na hujibu kwa ustarabu na hekima
pale mumewe ajapo juu na akiwa amepandwa na hasira. Mwanamke mwanandoa, atambue
hekima haiji bila kuiomba kwa Mungu. Chanzo cha hekima ni kumcha Mungu, maana kwa
Mungu ndiko kuliko na kisima cha hekima alikozitoa mfalme sulemani. Hekima zitokanazo
na Mungu zitamuongoza mwanamke katika ndoa kujua maneno gani ya kutumia na wakati
gani wa kujibu, kunyamaza, kunyenyekea au kujishusha juu ya mume wake (au mtu
mwingine) unapokuwa amemuudhi au kashikwa hasira.

Mwanamke katika ndoa afuatilie kwa ukaribu tabia na mienendo ya watu wa


familia. Mithali 31:27 inasema: “Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; wala
hali chakula cha uvivu”. Mwanamke katika ndoa ndiye aliye katika mstari wa mbele katika
kufuatilia kwa ukaribu mienendo na tabia za watoto pamoja na wanafamilia wote. Mara zote
wanaume huwa ni wavivu wa kufuatilia mienendo na tabia za watoto na wanafamilia
wengine, lazima mama wa familia ajue kila kitu na kisha amjulishe baba wa familia.
Mwanamke ni zaidi ya mwandishi wa habari katika uwezo wa kufuatilia vitu vingi kwa
wakati mmoja, na hiyo ndiyo sifa kuu ya pekee ya mwanamke tofauti na mwanamme.
Si kila jambo mke amfikishie mumewe, mengine yampasa kuyamaliza yeye
mwenyewe kwa kutumia hekima na atatoa mrejesho kwa mume wake. Endapo tatizo likiwa
kubwa sana anaweza akaliwasilisha kwa mumewe pia ili wajadiliane kwa pamoja na hatimae
walipatie ufumbuzi. Mwanamke kufuatilia njia za watu wa familia ni jukumu lake la msingi;
kwa maana nyingine, ndiye katibu au mtendaji mkuu wa familia, hivyo ni lazima awe makini
kwa kila jambo juu ya wanafamilia wake.

Mwanamke katika ndoa ahakikishe familia yake inamfurahia kujivunia na


kumsifia kwa mazuri na mema. Mithali 31:28 inasema: “Wanawe huondoka na humwita
heri; Mumewe naye humsifu…”. Sifa njema ya mama wa familia ni yule mwenye uwezo wa
kuifanya familia kuwa na upendo, mshikamano, furaha na amani. Mama mwenye kuonya,
kushauri, kukemea na kufundisha kwa lugha ya upole na upendo ni mama mzuri na ana
hekima ya Mungu, hivyo kwa mazuri yote ayatendayo kwa mumewe na watoto wake hakika
hawana budi kujivunia, kumfurahia, kumpenda na kumsifia.
Mama wa familia apendae magomvi na hatangulizi upendo kama ngao ya kuleta
amani katika familia, hawezi akasifiwa na mumewe wala watoto wake, maana yeye kila
kukicha ni siku ya magonvi kwa kukuza mambo hata kama sio makubwa. Mwanamke

Frank Philemon Karoli


63
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

amchae Mungu na mwenye hekima, hutumia upendo kama siraha ya kurejesha amani, umoja
na mshikamano katika familia yake.

Mwanamke katika ndoa awe mfano wa kuigwa kutokana na mazuri yake. Mithali
31:29 [Mume humsifu na kusema] “Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe
umewapita wote”. Mwanamke mwenye kujua majukumu na kuisimamia familia yake, jina
lake kutajwa na kutamkwa kwa mema na mazuri, kuanzia ngazi ya familiya hadi jamii
inayomzunguka. Kwa mazuri yake, jamii imzungukayo imtolee mfano wa kuigwa; hivyo
atakuwa barua njema kwa wengine.

Mwanamke mwenye kutenda mema na mengi yaliyo mazuri, mume wake hujivunia na
hana budi kumsifia maana jina lake jema linasomeka vyema kwa familia na jamii yote
inayomzunguka. Kama mama wa familia hasomeki vizuri katika mienendo na tabia yake,
hawezi akarithisha mambo mazuri kwa watoto (binti zake), hivyo, binti zake waweza kukaa
bila kuchumbiwa au kuolewa maana tabia ya mama yao sio nzuri.

Mwanamke katika ndoa; wanafamilia na jamii imsifie kwa ucha Mungu na sio
uzuri wake. Mithali 31:30 inasema: “Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali
mwanamke amchae BWANA, ndiye atakayesifiwa”. Baadhi ya wanawake walio katika ndoa
huwa na mikogo, ujivuni au kujisikia na kujiona ya kwa kuwa ni wazuri wa sura na umbo,
hivyo, hawawezi kuheshimu, kunyenyekea kwa waume zao. Mara zote uzuri wa sura
hudanganya, hivyo huharibu tabia na matendo ya mtu. Mwanamke amtumainie na kumcha
Bwana, ndiye apatae sifa maana upendo na uzuri wa moyo watoka kwa Mungu.
Mara nyingi wanawake walio wazuri wa sura ndiyo wanaoongoza kwa roho mbaya na
matendo mabaya pia na ndiyo wanaoongoza kuleta migogoro na kuvunja ndoa, maana
anaamini kwa uzuri wake atapata mwingine. Mama mwanandoa si vyema akatumia uzuri
wake kama fimbo ya kumnyanyasa mume wake. Heri uzuri wa moyo wenye kujenga, kuliko
uzuri wa sura udanganyao na wenye kubomoa.

Mwanamke mwanandoa, hata akipatiwa mapato ya mikono yake hatabadirika


na kuiacha tabia yake njema. Mithali 31:31 inaeleza kuwa: “Mpe mapato ya mikono yake,
Na matendo yake ya msifu malangoni”. Kuna baadhi ya wanawake katika ndoa hubadirika
tabia wanapomiliki vipato vikubwa au kuwa na mali nyingi. Tabia hii imepelekea wanaume
wengine kuwazuia wake zao kufanya kazi au biashara ili kujiingizia vipato vyao binafsi na
hivyo, kuwafanya kuwa mama wa nyumbani wakiwategemea waume zao kwa kila hitaji.
Mwanamke amchae Mungu, habadiliki tabia na habadirika katika kiwango cha upendo
eti kwa sababu ya mali, kazi, elimu au chochote kinachompatia kipato. Upendo wa kweli na
tabia njema ya mwanamke kwa mume wake haujalishi kiasi gani cha pesa au mali alizonazo.
Hivyo basi, mwanamke mwenye upendo wa kweli na tabia isiyobadirika kwa sababu ya pesa;
mumewe hawezi kujizuia kumpatia mali, wala kumzuia kuhusika katika utafutaji wa kipato
chake binafsi. Si vyema na salama pia, mwanamke akamsaliti mume wake kwa sababu au
tamaa ya pesa.

Frank Philemon Karoli


64
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 09 =

UFAHAMU NA MAARIFA KATIKA NDOA YA KIKRISTO

“Mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie


mashauri yenye njia”

Mithali 1:5

Waebrania 13:4 inaelezea kuwa ndoa na iheshimiwe na watu wote; hivyo ndoa ni
takatifu lazima iheshimiwe na watu wote. Kuchezea chezea ndoa nikosa na nikumkosea
Mungu aliyemwasisi wa taasisi hiyo. Ni jambo nyeti na la msingi pia kufahamu juu
mahusiano na maarifa katika ndoa.
Maarifa na ufahamu katika ndoa yapo kwenye uwepo wa Mungu katika ndoa. Maarifa
na ufahamu huo ni juu ya magomvi katika ndoa, pesa na mali katika ndoa, kusaidia ndugu
katika ndoa, afya katika ndoa, elimu katika ndoa, kanuni kuu ya maisha katika ndoa na kazi
katika ndoa.
Uwepo wa Mungu Katika Ndoa
Ndoa iliyofuata hatua zote na ikafungwa katika taratibu za Kikristo ni ndoa iliyohalali
na imekubarika mbele za Mungu kwa kuwa ndoa ni muunganiko wa mke, mume na Mungu
(Mithali 4:12). Yafuatayo ni mambo matano ya kufanya kwa wanandoa ili Mungu awepo
katika ndoa na familia yao:
Kuthamini mambo ya ibada
Wanandoa wathamini na kufanya ibada za kicho katika familia yao pamoja na
kuhudhuria na kushiriki ibada za maombi kanisani ili Mungu azidi kutamalaki na kuwepo
katika ndoa na familia yao (Waebrania 10:25).

Kuwa wasomaji wa neno la Mungu


Kuwepo na usomaji wa neno la Mungu kwa wanandoa ili kuutafakari ukuu wa Mungu
na kumruhusu Roho Mtakatifu aingie ndani ya maisha yao na kuwaongoza katika kutenda
yaliyo mapenzi yake Mungu daima. Familia inayosoma neno la Mungu na kuritafakari vyema
hukuza kiwango cha kiroho (Mithal 119:11; Mathayo 22:29; Mathayo 7 sura yote).

Kuwa watu wa maombi


Wanafamilia wawe watu wa maombi maana maombi mengi huleta nguvu nyingi za
kiroho. Maombi ni silaha, maombi ni ulinzi na maombi huruhusu uwepo wa Mungu na Roho
Mtakatifu katika ndoa na familia (Waefeso 6:18-20, Zaaburi 69:13).

Frank Philemon Karoli


65
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Kushiriki katika kufanya kazi ya Mungu na huduma za kijamii


Ili Mungu awepo katika ndoa na familia ya wanandoa, wanandoa yawapasa kujitahidi
kwa kushiriki kwa moyo wote katika kufanya kazi ya Mungu pamoja na kushiriki katika
kufanya huduma za jamii (matendo ya huruma) kwa kushirikiana na kanisa. Kufanya kazi ya
ushuhudiaji, uinjilisti na kushiriki matendo ya huruma katika jamii, Mungu hawezi kuwa
mbali na ndoa au familia hiyo (Yohana 14:12, Mathayo 24:13).

Kuwa waaminifu wa kumrudishia Mungu zaka na sadaka


Wanandoa wawe waaminifu katika kumrudishia Mungu zaka na sadaka maana Mungu
hakai katika nyumba ya wezi ambao wanamwibia. Mahusiano yanapoharibika kati ya
wanandoa na Mungu hata mahusiano ya wanandoa huharibika pia, hivyo, wanandoa
wajitahidi kuwa waaminifu katika kumrejeshea kilicho chake Mungu ili awe katikati ya ndoa
yao (Malaki 3:8-9).
Magomvi Katika Ndoa
Kulingana na pambano kuu kuendelea kuwepo pamoja na silka ya mwanadamu
itokanayo na dhambi, magomvi hujitokeza katika baadhi ya ndoa za Wakristo. Mada hii
imejadiliwa katika sura za nyuma, hivyo machache tu tutayaangalia kulingana na muktadha
wa kipengele hiki namba mbili.
Vyanzo vya magonvi katika ndoa ni: Miongoni au wanandoa wote kutojali wajibu
wao katika ndoa, usiri wa mambo ya pesa na mali kwa wanandoa, upendeleo wa ndugu wa
upande mmoja miongoni mwa wanandoa, kuingilia mazungumzo ya mmoja wa wanandoa,
uvivu wa kazi, uchafu, kuchelewa kupata mtoto, maisha ya kulipizana visasi, tabia ya
kukasirika kasirika haraka miongoni mwa wanandoa, kutokukubari makosa miongoni mwa
wanandoa au wote (Mithali 17:3), kutoa majibu kabla ya kuelewa swali, upendeleo wa
watoto na majibu mabaya.
Aina za magomvi katika ndoa ni: Kupigana, Maneno ya kashifa, Vitendo bila kusema
au vitendo vya kimya kimya, Vitisho na Kunyimana tendo la ndoa; haya ndiyo baadhi ya
magomvi yaliyo katika ndoa na familia za Kikristo ambayo huzisumbua. Magomvi katika
ndoa huzalisha madhara mengi katika ndoa na familia za Kikristo. Madhara ya magonvi ni:
hufukuza uwepo wa Mungu katika ndoa na familia, hushusha heshima ya wanandoa katika
jamii na kanisa, husababisha magonjwa kwa wanandoa na katika ndoa, husababisha vifo na
husababisha utengano baina ya wanandoa.

Fedha Katika Ndoa


Suala la fedha katika ndoa ni jambo ambalo linaleta changamoto katika baadhi ya ndoa
na familia za Kikristo. Ili kuziepuka changamoto zitokanazo na pesa katika ndoa na familia,
wanandoa inawapasa kuzingatia mambo yafuatayo: pesa zote zinazopatikana zimilikiwe
kwa pamoja, kila mwanandoa awe muwazi kwenye mapato yake yote, asiwepo wa kutumia
au kuchukua pesa bila taarifa kwa mwenzi wake, wanandoa wapange pamoja namna ya
kutumia pesa, kila mmoja amjulishe mwenzake akaunti (account) zake za benki, wanandoa
waepuke kushindana na watu wengine katika matumizi ya pesa, wanandoa waepuke maisha
ya kukopakopa, wanandoa waweke akiba ya pesa (Mithali 6:6-8, Mithali 24:27), na ni
vyema wakapanga mahitaji au bajeti (budget) wakati ambapo hakuna pesa.

Frank Philemon Karoli


66
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Watoto
Jambo la kuzaa watoto linahitaji maombi ya kina juu ya mtoto anayezaliwa awe ni
mpango wa Mungu ili Mungu aanze kumwandaa toka kutungwa kwa mimba na kukua kwake
tumboni (Yeremia 1:5). Maisha ya ndoa huanza yakiwa na watu wawili pasi na watoto;
watoto huja badae katika maisha ya ndoa ukiwa kama mbaraka kutoka kwa Mungu maana sio
kwa uwezo wao wanandoa kuwapata watoto, hivyo, yaweza kuchukua muda kwa wanandoa
kupata watoto au kuwahi. Maamuzi ya kuzaa watoto wangapi na kwa kipindi gani huwa ni
makubaliano ya wanandoa wao wenyewe na si jambo la mmoja miongoni mwa wanandoa.
Wanapopatikana watoto au wanandoa wanapowazaa watoto wao yawapasa
kuwahudumia kwa pamoja bila kuwabagua, hata katika kuwapatia elimu ili kujenga
ushirikiano na umoja katika familia na miongoni mwa watoto.

Kusaidia Ndugu
Kusaidia wengine ni moja ya jambo la kiroho kwa ye yote aliye Mkristo na mcha
Mungu, maana hufungua mibaraka. Kusaidia ndugu katika familia ya wanandoa kusiwe kwa
kupendelea upande mmoja wa ndugu miongoni mwa wanandoa. Wanandoa wawasaidie
walio na uhitaji ili nao waweze kujikwamua kimaisha. Wawatendee mema wale walio ndani
ya uwezo wao, ikiwezekana wawape mtaji au kianzio (ndoano) ili nao waweze kujitafutia
riziki (samaki) zao wenyewe na sio kuwazoeza kuwapa samaki kisha wakimaliza waombe
samaki tena.
Afya Katika Ndoa
Katika kitabu cha 3Yohana 1:2, Yohana anazungumzia juu ya kufanikiwa katika afya
na roho. Afya ni jambo la msingi kwa wanandoa, hivyo, walizingatie na kulitilia mkazo hata
kwa watoto wao. Ndani ya familia, wanandoa wahakikishe kufuata kanuni zote za afya
hususani kwa kuzingatia ulaji wa vyakula vya asili vyenye ubora na vitamini na siyo vyakula
vya kutoka viwandani. Ikiwezekana, wanando wasikoboe nafaka zinazopaswa kuliwa bila
kukobolewa.
Wanandoa wazingatie mazoezi na ulaji wa mpango kwa kuwa na kiasi ili kuepuka
unene na uzito kupita kiasi; pawepo na uwiano wa urefu wa mwili na uzito wa mwili pia.
Hivyo, wanandoa wazingatie kanuni kumi na mbili za afya (yaani CELEBRATIONS;
ikimanisha SHEREHE) ambapo hapo awali zilikuwa kanuni nane za afya (yaani
NEWSTART; ikimanisha MWANZO MPYA):

MWANZO MPYA (NEWSTART):

1. N = Nutrition (Lishe)
2. E = Exercise (Mazoezi)
3. W = Water (Maji)
4. S = Sleep (Kulala)
5. T = Trust in God (Kumwamini Mungu)
6. A = Air (Hewa Safi)
7. R = Rest (Kupumzika)
8. T = Temperance (Kuwa na kiasi)

Frank Philemon Karoli


67
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

SHEREHE (CELEBRATIONS):

1. C = Choices (Chaguwa afya njema)


2. E = Exercise (Mazoezi)
3. L = Liquid (Tumia viminika safi)
4. E = Environment (Mazingira salama)
5. B = Belief (Imani kwa Mungu)
6. R = Rest (Pumziko)
7. A = Air (Hewa safi)
8. T = Temperance (Kiasi)
9. I = Intergrity (Uaminifu)
10. O = Optiminism (Mtazamo chanya)
11. N = Nutrition (Lishe)
12. S = Social support & service (Kutoa huduma na
msaada kwa jamii)

Elimu Katika Maisha ya Ndoa


Wanandoa wasichoke katika kujielimisha katika mambo mbalimbali yaliyo na tija
katika ustawi wa maendeleo ya ndoa na familia yao maana elimu ni uzima, mafundisho na
maarifa (Mithali 4:13). Elimu yaweza husisha kwenda darasani au pasi na kwenda darasani
ili mradi njia yo yote na mfumo wo wote waweza kutumika ili kujiongezea maarifa na
uelewa (Mithali 12:1, Mithali 18:1).
Aidha, pawepo na makubaliano ya wanandoa katika kujiendeleza kielimu ili
kujiongezea maarifa na ufanisi katika kazi au shughuli wazifanyazo katika kuwaingizia
kipato cha familia yao; yaweza kuwa ujuzi, ufundi, fani, maarifa au taaluma yo yote
kulingana na mahitaji miongoni mwa wanandoa au wanafamilia.

Kanuni Kuu ya Maisha ya Ndoa


Kanuni kuu ya maisha ya ndoa ni mmoja kutii na mmoja kupenda kama tulivyoona
katika sura zingine za kitabu hiki hususani katika fungu lililo zoeleka la Waefeso 5:22-23.
Mwanandoa inampasa kumtii mwenzi wake tu endapo havunji mapenzi ya Mungu (Matendo
5:29), hivyo wanaume wawapende wake zao na kujitoa kwao kama Kristo alivyolipenda
kanisa na kujitoa kufa kwaajili yake (Waefeso 5:24-25).

Kazi Katika Ndoa


Suala la kazi katika ndoa na familia limejadiliwa kwa kina katika sura inayojitegemea
juu ya umuhimu wa kazi katika ndoa na familia. Wanandoa wapende kufanya kazi na
wawafundishe watoto wao nao kujua, kufanya na kupenda kazi kama lilivyo agizo la Mungu
katika Biblia. Kufanya kazi na mwili ukatoa jasho kisha ukachoka ni alama ya ukumbusho
wa kuumbwa kwa mwanadamu na anguko lake (Mwanzo 2:15).
Hivyo basi; kufanya kazi kisha kutoa jasho na kuchoka mwili ni kutukumbusha kuwa
tulitenda dhambi na tukakombolewa kwa damu ya thamani ya Yesu Kristo pale msalabani ili

Frank Philemon Karoli


68
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

tuupate wokovu na uzima wa milele; tuonapo hali hiyo basi tuzidi kujikabidhi na
kujinyenyekeza kwake aliyetukomboa ili tusipotee milele.
Kufanya kazi kwa wanandoa kunafaida zifuatazo: huleta heshima katika jamii
inayowazunguka, ni kumbukumbu ya sabato, kuepuka kutenda dhambi ya wizi na kutamani
vitu na mali za wengine, huleta furaha maishani daima, hujenga afya maana ni sehemu ya
mazoezi, hujenga ushupavu na uwezo wa akili katika kufanya maamuzi na kufikiria mambo,
kazi inaongeza urefu wa maisha kwani hupunguza mawazo yasiyokuwa na tija na kazi yo
yote ile inafaida (Mithali 14:23 na Mithali 31:10).
Kutofanya kazi kunaleta umasikini katika familia; Mambo yanayoleta umasikin
katika familia au ndoa ni: kutomrudishia BWANA kile alichowapatia wanandoa katika
mapato yao (Mithali 10:7), uvivu uliopitiliza (Mithal 10:4), usingizi uliopitiliza (Mithali
20:13), anasa kama ulevi na urafi (Mithali 21:17, Mithali 23:20-21), kufuata mambo yo yote
ya upuuzi na yasiyofaa (Mithali 28:19), kuzurura au kutumia muda mwingi kusafiri
kutembelea ndugu bila kufanya kazi (Mithali 25:17).

Frank Philemon Karoli


69
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 10 =

FAMILIA YA KIKRISTO ILIYO YA KIROHO NA YENYE FURAHA

“Kuwa na mali chache pamoja na kumcha BWANA; Ni bora kuliko mali


nyingi pamoja na taabu. Chakula cha mbogamboga penye mapendano; Ni
bora kuliko ng‟ombe aliyenona pamoja na kuchukiana”

Mithali 15:16-17

Msingi bora wa familia yenye afya ya kiroho ni familia yenye msingi


imara wa kroho. Familia ya kiroho ni familia yenye furaha maana ni familia iliyo na
matumaini daima; tumaini la kweli katika familia ya kiroho ni lile litokalo kwa Yesu Kristo
aliye mwamba na mwokozi wa maisha ya wanadamu wote wanao mkimbilia na kumkabidhi
fadhaa zao. Wanandoa walioijenga ndoa yao katika misingi mizuri ya kiroho, familia yao
huwa haiteteleki hata panapokuwepo changamoto maana tumaini lao ni Yesu na yote
yanayotokea humkabidhi yeye ili atende sawasawa na mapenzi yake.

Familia Yenye Furaha


Familia yenye furaha ya kweli ina viashiria vifuatavyo: ni yenye mawasiliano mazuri,
ni yenye kuhudumiana katika familia, hufanya na kuheshimu ibada, Yesu huheshimiwa na
kila mwana familia, Huombana Msamaha, wanandoa husahihishana kwa upole pale
wanapokoseana, kila mwana familia ni sehemu ya furaha ya familia, huwa inapata muda wa
kutosha katika kukaa pamoja, wanafamilia huthaminiana au kujaliana, kila mmoja huhusika
katika kila jambo la familia, hakuna wivu wala usiri miongoni mwa wanandoa, siri za familia
hubakia kama za familia ili kutovunja umoja wa familia, hushirikiana katika mambo ya
maendeleo, hufungamana na kushiriki kazi ya Mungu (kujitoa kikamilifu katika mambo ya
fedha au kushiriki moja kwa moja) na watoto huwa na nidhamu ya hali ya juu.

Familia ya Kiroho
Familia ya kiroho ni familia ambayo inaishi na kutembea katika heshima na utukufu
wa Mungu chini ya mwanaye mpendwa Yesu Kristo na imejawa na Roho Mtakatifu. Ili
kutengeneza au kuunda familia ya kiroho, wanandoa wafanye mambo yafuatayo:

Wampokee Yesu kama Bwana na Mwokozi wao: Familia ya kiroho ni ile


iliyompokea Yesu kama Bwana na mwokozi wao (Yohana 1:11-13); kumpokea Yesu ni
kuipokea injili ya kweli au ujumbe wa wokovu uliohubiriwa na wajumbe wa Mungu kutoka
kwenye Biblia (1Wakorintho 1:18, 15:13, 1Thesalonike 1:5-10, Warumi 10: 9-17).
Wanandoa na Wanafamilia Waishi na Kufuata Kweli Yote ya Yesu: Kila siku na
mara zote wanafamilia wa familia ya kiroho huishi na kutembea katika kweli yote ya Yesu

Frank Philemon Karoli


70
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Kristo (Wakolosai 2:6); kwa kusoma Biblia na uthubutu wa kulitafakari neno lake (Zaburi
119:1, Wakolosai 3:16, Matendo 17:11, 1Petro 2:2).
Wanafamilia Wapate Muda wa Kutosha Katika Kuomba: Familia ya kiroho hutenga
muda wa kutosha kwa ajili ya maombi; familia ya kiroho haifanyi maombi ya yasiyokuwa na
kicho au ya harakahara. Kila mwanafamilia katika familia yampasa kupata nafasi binafsi ya
kufanya maombi (Luka 18:1, Wafilipi 4:6, 1Wathesalonike 55:17, Waefeso 6:18).
Washiriki Imani Yao na Watu Wengine: Familia ya kiroho hushiriki imani yao na
watu wengine. Wanafamilia wanaposhuhudia watu wengine imani yao juu ya Yesu kwa dhati
huwa na nguvu nyingi za kiroho, hivyo, kiwango cha kiroho hupanda kila mara wanapo
zididi kutenda hivyo (Matendo 2:42).
Wanafamilia Washiriki Shughuli na Huduma Mbalimbali za Kanisa: Familia
inayohitaji kukua kiroho, haikwepi wala haiachi kushiriki huduma na shughuli za kanisa.
Shughuli na huduma za kanisa kama vile: huduma za jamii, ushuhudiaji, kujiunga na kwaya,
kuchangia pesa katika huduma za kueneza injili pamoja na kufanya kazi za mikono
zinazohusu kanisa huvutia uwepo wa Roho Mtakatifu miongoni mwa wanafamilia kwa
sababu ya kuwa mawakili waaminifu kwa Mungu.
Wanafamilia Waepuke Dhambi: Familia inayotaka kuwa familia ya kiroho ni lazima
iepuke kutenda au kushiriki dhambi ili waishi katika kweli yote na imani ya Yesu kristo
(Warumi 22:21, Wafilipi 1:270).
Wanafamilia Huliheshimu na Kulisoma Neno la Mungu: Familia inayotaka kuwa
familia ya kiroho ni lazima ilisome na kuliheshimu Neno la Mungu pamoja na kulifanyia kazi
na kuliishi. Familia ya kiroho itafundishana, kusoma kwa sauti na kulijadili neno la Mungu
(Kumbukumbu la Torati 6:7)

Jinsi Familia ya Kiroho Ilivyo kwa Muktadha wa Waefeso 5:21 Hadi 6:9:
 Wanafamilia wote ni Wakristo katika imani moja.
 Familia imeundwa na baba, mama, watoto, wazazi wa wanandoa, na wafanya kazi
(extended family).
 Familia ina utii na upendo kwa kila mmoja. Mwanamke anamtii mumewe na mume
anampenda mkewe.
 Watoto wanawaheshimu wazazi maana wanawalea katika nidhamu na utii kwa Mungu.
 Wafanyakazi wanawahudumia mabwana zao bila jicho la uangalizi; mabwana nao
wanawaonesha wafanyakazi usawa kama alivyo Bwana Yesu kwa wote.
 Familia hii inamwabudu Yesu maana yeye ni kichwa cha familia na wanafamilia wote.

Uendeshaji wa Ibada Katika Familia ya Kiroho


Familia ya kiroho ina mfumo na utaratibu mzuri wa ibada. Hivyo, familia inayotaka
kuwa familia ya kiroho iendeshe ibada zake kwa mfumo au mtindo ufuatao:
 Ipange ratiba ya kumwabudu Mungu kila siku hususani asubuhi na jioni.
 Ratiba ya ibada ioneshe namna au utaratibu wa kuendesha ibada na nani atahusika juu
ya nini katika ibada pamoja na nini cha kuombea.

Frank Philemon Karoli


71
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

 Iheshimu ratiba (muda) ya ibada na vitu vinavyoingilia ratiba hiyo viepukwe au


kuondolewa kabisa ikiwezekana.
 Ibada iwe yenye kicho mbele za Mungu; simu, radio na tv zizimwe wakati wa ibada.
Watoto wazoezwe kupiga magoti ili kujenga unyenyekevu kwa Mungu.
 Ibada iwe yenye programu za kuvutia ili isichoshe na kukinai.
 Ibada iwe fupi na yenye maombi mafupi; pasiwe na mafundisho au masomo marefu au
maombi marefu hususani kutowachosha watoto au ibada kuwakinai endapo kuna
watoto wadogo. Hivyo maombi na masomo yaguse vipengele vya za msingi tu.
 Baba au mama ahakikishe kila mwanafamilia anahusika na kushiriki kikamilifu na
kama umri wa baba na mama umesonga sana, huduma za ibada wakabidhiwe watoto
na wazazi wawe washauri na wachangiaji ili kusahihisha na kuongezea katika maelezo.
 Ndugu au wageni waliotembelea familia wasipewe nafasi ya kuharibu au kukwamisha
ratiba ya ibada.
 Baada ya ibada, wanafamilia waagane kwa kushikana mikono na kutakiana usiku
mwema, siku njema, masomo mema au kazi njema n.k.

Hofu Katika Familia


Kutia hofu na mashaka familia ni moja wapo ya mambo ambayo Shetani huyatumia
katika kuharibu familia. Marko 4:19 inaeleze hofu zitokanazo na kupenda mambo ya kidunia
ambayo wanafamilia huwachukulia muda mwingi badala ya yale ya Mungu. Miongoni mwa
familia za Kikristo zinahofu ya mambo yafuatayo:
o Hofu ya afya zenye mashaka kwa sababu ya kutojali kanuni za afya.
o Hofu ya kujihisi kutokuwepo na ulinzi hivyo, kuhita kinga za wanadamu.
o Hofu ya kukosekana kwa uhakika wa chakula na mahitaji mengine kunakopelekea
kutumia njia zisizofaa ili kujipatia pesa zinazoweza kukidhi mahitaji kwa familia.
o Hofu itokanayo na ukosefu wa uaminifu kwenye ndoa.
o Hofu ya elimu, hivyo, wanandoa kutumia muda mwingi kutafuta elimu ya dunia,
hivyo kuwa mbali na familia zao na Mungu pia.
o Hofu ya kazi au biashara na uzalishaji ambazo kwazo wanandoa huziabudu na
kuzifanya mungu kwao kwa kuvunja sheria na taratibu za Mungu.

Madhara ya Hofu Katika Familia:


 Wanafamilia wanaweza wakashindwa kufikiria vyema maana mtu ye yote aliye na
hofu hawezi kufikiria sawasawa.

Frank Philemon Karoli


72
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

 Hofu katika familia husababisha magonjwa ya kisaikolojia na moyo pamoja na


magonjwa mengine yanayotokana na msongo ya mawazo.
 Hofu huua mambo yote ya kiroho maana wanafamilia hukosa tumaini sahihi katika
maisha yao.
 Mwanafamilia mwenye hofu, huhisi kuwa Mungu hayupo kwa yale yanayomtokea,
hivyo, hupelekea kutenda dhambi ya kukufuru au kumlaumu Mungu kwa sababu
hampiganii au hajibu maombi yake.
 Mwananfamilia mwenye hofu, kila kitu kwake ni hasi, hivyo, huwa ni mtu mwenye
mashaka na mwenye kulalamika kutotendewa sawa katika kila kitu.
 Mwanafamilia mwenye hofu, hawezi akatekeleza mipango na mikakati yake vyema ili
aweze kuyafikia mafanikio katika malengo aliyojiwekea.

Jinsi ya Kuiondoa Hofu na Kudumisha Amani katika Ndoa:


 Kuzidi kudumu na kuwa na imani katika Mungu pekee (Waefeso 6:16; Hesabu 6:26;
Isaya 26:3-4; Ayubu 22:21).
 Kutambua uwezo, nguvu na neema ya Mungu iletayo amani katika dhoruba yo yote
ile (2Wakorintho 12:9; Wafilipi 4:13; Marko 4:37).
 Kuwa na moyo wa shukrani daima kwa Mungu kwa kila jambo linapotokea, aidha
zuri au baya (Mithali 17:22; Wafilipi 4:6).
 Kujitahidi kufanya toba ili kuwa mwenye haki (1Yohana 1:9; 32:17) itokayo kwenye
imani, kisha kuipata amani kwa njia ya Yesu Kristo(Warumi 5:1).
 Kujiepusha kuitafuta amani kutoka katika mambo ya kiulimwengu, bali kuitafuta
amani ya kweli kutoka kwa Yesu Kristo pekee (Yohana 14:27; Wafilipi 4:7).
 Kuepuka kutenda dhambi kwa kuvunja sheria na amri za Mungu (Isaya 48:18,22;
 Kujitahidi kuwa mwenye furaha na kufanya mazoezi ili kuimarisha afya (Waefeso
6:10) .
Namna ya Kudumisha Umoja Katika Familia
Kwa kuwa familia ni zaidi ya baba na mama, hivyo, kunaongezeko la watoto na watu
wengine wa karibu na familia; familia pia imezungukwa na jamii au majirani. Kuna mambo
mengi ya kuzingatia ili kuleta amani katika ndoa na familia. Kupalilia umoja wa familia
panahitajika mambo yafuatayo:

Kuwe na mahusiano mema miongoni mwa wanafamilia


Inafahamika kuwa adui wa mtu ni wale wa nyumbani kwake (Mathayo 10:36) hivyo,
lazima kuwe na mahusiano mema miongoni mwa wanafamilia yaliyojengeka katika Kristo
huku wakitafuta kuwa na amani na watu wote wanaowazunguka (Waebrania 12:4).

Frank Philemon Karoli


73
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Mwenzi ajue kipato cha mwenzi wake


Kila mmoja miongoni mwa wanandoa ni vyema akajua kipato cha mwenzie ili
kuondoa sintofahamu na mashaka miongoni mwao juu ya matumizi yao ya pesa. Ikiwezekana
wanandoa pia wa washirikishe watoto wao katika mipango ya familia endapo watakuwa
wamepevuka kiakili.

Kuwe na furaha miongoni mwa wanandoa na wanafamilia


Katika familia viepukwe visasi, visa, visirani, chuki na uhasama miongoni mwa
wanandoa au wanafamilia ili kujenga familia yenye upendo na mshikamano imara (Mhubiri
9:9).
Kutembea, kusafiri na kucheza pamoja
Wanafamilia wajenge mazoea ya kucheza au kushiriki michezo mbalimbali pamoja,
kusafiri pamoja kwa ajili ya matembezi ili kujenga mshikamano na ukaribu miongoni mwa
wanafamilia (Mwanzo 26:8).

Kuwe na mawasiliano mazuri ya karibu na yenye kufuata ngazi


Uhuru na uwazi katika kuwasiliana miongoni mwa wanafamilia kunajenga familia
yenye umoja na amani. Katika kuleta mawasiliano mazuri kwenye familia, patolewe majibu
sahihi yanayoeleweka au wazi kwa kuelekezana na kushirikishana hatua kwa hatua na ngazi
kwa ngazi (Yakobo 3:1-2; Mithali 20:19; Mithal 21:23; 1Wakorintho 15:33).

Kuheshimiana katika mazungumzo na kujariana katika hisia


Kuwepo uungwana, kuheshimiana na kujaliana katika kila hisia za mwanafamilia ili
kujenga ukaribu wa kubebeana matatizo. Patumike lugha zenye maneno ya sitaha na
kuheshimiana bila kukwazana au kuumiza hisia za mwingine (Mithali 1:21; Yakobo 1:19;
Mithali 10:14; Mithali 10:19).
Kuwe na usafi thabiti
Katika familia, pazingatiwe usafi kwa kila nyanja na kwa kila mwanafamilia ili
kuepusha makwazo na kero na malalamiko juu ya uchafu. Usafi wa mazingira, ndani ya
nyumba, mavazi na mwili uzingatiwe na kila mmoja aliye katika familia ili kutochokana au
kukwazana kwa namna moja au nyingine (Ruth 3:3).

Kushirikishana na uaminifu
Wanafamilia wawe wawazi kila mmoja na kushirikishana kila jambo ili kuwepo
kuombeana. Kuwepo na kushirikishana katika mikakati ya maisha na maendeleo ya familia
juu ya elimu, mahali pa kujenga na vitu vya kununua, hivyo basi kushirikisha kwa
wanafamilia kutawajengea uaminifu wao kwa wao. Pia siyo salama amana ya familia
ikauzwa bila kuwasiliana au kuzungumza miongoni mwa wanafamilia (Mithali 23:20-21).

Kusameheana na kufutiana makosa


Wanafamilia wawe na tabia ya kusameheana, na wanaposameheana wafutiane
makosa waliyotendeana. Tabia ya kusameheana huwasaidia wanafamilia kutovunja uhusiano

Frank Philemon Karoli


74
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

wa wao kwa wao maana hawawekeani chuki za kudumu juu yao bali huyatatua matatizo yao
kwa upole na kwa hekima ya kimbingu (Luka 11:4; Mithali 15:1).

Kuomba na kuombeana misamaha kwa Mungu


Wanandoa na wanafamilia wajenge tabia ya kuomba kuondolewa mazaifu yao na
kuombeana msamaha kwa Mungu juu ya yale waliyotendeana; yawapasa kujua kuwa
kukosana kwao ni kwa sababu ya dhambi na mashambulizi ya Shetani, hivyo, yaweza kuwa
hawajui wanayotendeana wakati mwingine. Kuombeana kwa wanafamilia ni sehemu ya
kubebeana mizigo na mazaifu ili Mungu ayaondoe juu yao (Mwanzo 25:21).

Kuomba na kufunga kwa ajili ya ndoa na ustawi wa familia


Maombi katika familia hufanya pawe kituo cha malaika au Mungu mwenyewe;
wanandoa au wanafamilia itafana sana iwapo watatenge muda wa kufunga na kuomba kwa
ajili ya amani na ustawi wa ndoa na familia kwa ujumla (Mithali 10:22).

Kudumisha uaminifu kwa kuepuka uzinzi


Amani ya familia itatawala na itakuwepo endapo tu wanandoa watakuwa waaminifu
katika kuiepuka zinaa na uzinzi kwa kuzisaliti ndoa zao. Usaliti au uzinzi nje huleta mpasuko
katika familia kwa asilimia kubwa kuliko matatizo mengine, hivyo, uzinzi na uasherati
ukiepukwa, ndoa na familia zitakuwa katika amani na furaha (Mithali 6:32; Ayubu 31:1;
Wakolosai 3:9).

Wanandoa wawe na uvumilivu katika kustahimili majaribu


Migogoro ya familia na ndoa hujitokeza kwa sababu wanafamilia huwa si wazuri
katika kukabiliana na majaribu au changamoto zinazojitokeza juu yao na familia. Wanandoa
yawapasa kuwa wavumilivu katika kuyastahimili majaribu yanayokuja au kuwaandama huku
wakidumu kuomba kwa kumkabidhi Mungu ili awashindie. Kwa kufanya hivyo, wataweza
kumpinga Shetani na atakimbia kwa kuwa mkono wa BWANA utakuwa pamoja nao (Yakobo
1:12; Yakobo 2:14).

Frank Philemon Karoli


75
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 11=

MALEZI BORA YA KIKRISTO KWA WATOTO

“Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa


mzee”

Mithali 22:6

Ipo changamoto inayojitokeza katika malezi ya watoto katika familia za Kikristo.


Kwa sababu ya utandawazi, miongoni mwa wazazi wameshindwa kuwalea watoto wao katika
misingi mizuri ya Kikristo kwa sababu ya kuuelekea ulimwengu bila kujua kuwa
wanawapoteza watoto wao katika kuupata wokovu na uzima wa milele. Kila mzazi aliye
Mkristo yampasa atambue kuwa: watoto ni mbaraka na zawadi pekee itokayo kwa Mungu
(Zaburi 127:3-4). Mungu huwaandaa watoto toka tumboni mwa mama zao (Waamuzi 13:4-
14), bali wazazi huwa na sehemu kubwa ya kuwaharibu pale wanapokuwa wamezaliwa
hususani kwa kuwapatia malezi mabaya yasiyofaa.
Kabla wanandoa hawajapanga kuzaa yawapasa wamwombe Mungu kwanza, pia
wajiandae katika utayari wa kumlea mtoto huyo ipaswavyo tangu akiwa tumboni. Mama
mjamzito aepuke vyakula, vinywaji au vileo vyenye kuleta madhara pamoja na vitu vyote
vinavyoweza kutishia uhai na makuzi mazuri ya mtoto awapo tumboni. Aidha, pasiwepo na
magomvi, utengano, makwazo, bali pawepo na amani na umoja katika kuilea mimba huku
mama mjamzito akizingatia ulaji wa vyakula vya asili, mazoezi, kuwa na amani itawaliwayo
na furaha, upendo, ibada, kusoma neno la Mungu, kuimba nyimbo katika kumcha BWANA.

Siri ya Malezi Bora Yenye Mafanikio


Kupanga na kujiandaa kutoa malezi mazuri kwa watoto ni jambo la kwanza na la
msingi kwa wanandoa (wazazi) kabla ya kuwazaa na wanapowazaa. Wazazi wengi
wanakwepa wajibu wao katika kuwalea watoto wao waliowaleta hapa duniani kwa kupatiwa
mbaraka na Mungu, na matokeo yake ndiyo tunayoyapata katika dunia ya sasa juu ya uasi na
uhalifu kwa kiasi kikubwa.
Wapo wazazi wengi walio waaminifu na wanaojaribu kufanya majukumu yao vizuri
kwa kuwalea watoto katika njia iwapasayo lakini hukwamishwa na changamoto za kiuchumi,
utandawazi na hitaji la wazazi kujiendeleza kielimu hivyo kuwa mbali na watoto wao. Hivyo,
wazazi watumie kanuni zifuatazo ili kutoa malezi yenye tija kwa watoto wao:
Wampende Mungu: Wampende Mungu kwa hali ya juu ndani ya mioyo yao ili wawe
tayali kuyafanya mapenzi yake kwa kuwalea watoto katika misingi ya kibiblia na si
vinginevyo ili watoto wampendeze Mungu na wanadamu pia.

Frank Philemon Karoli


76
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Biblia iwe mwongozo wao: Wazazi waikubali Biblia kama ndiyo njia pekee inayo
waongoza katika kutoa maelekezo ya malezi mema kwa watoto wao walio wazaa na mengine
yaliyo nje ya biblia yatumike kutokana na hekima za kimbingu baada ya kupimwa kuwa
yanafaa.
Wanandoa wapendane: Wanandoa wapendane kwanza wao kwa wao ili watoto
wajue kuwa wazazi wao wanapendana. Upendo wa wazazi utaleta picha nzuri kwa watoto ili
wayarithi na kuyaishi yale yote wanayowafundisha na kuwaonesha kwa vitendo. Wanandoa
wasineneane mabaya bali waungane katika kuleta nidhamu na maadili yaliyo mema ya
watoto kwa pamoja.
Wazazi wawapende watoto: Wazazi wawapende watoto wao kwelikweli ili waweze
kuwaonya katika adiri na wasipotee katika ukengeufu kwa kuielekea dunia.
Wazazi wawe na muda na watoto wao: Wazazi watenge muda wa kutosha wa kuwa
karibu na watoto wao ili waweze kuwalea kwa ukaribu huku wakionesha hali ya kuwajali na
kushirikiana kwa kila namna iliyo nzuri kadri iwezekanavyo.
Wazazi wa warudi watoto wao katika upendo: Wazazi wawaongoze watoto katika
njia ya kurejesha nidhamu yao kwa kutumia upendo kadri iwezekanavyo na siyo nguvu kwa
sehemu kubwa bali mara chache wawarudi kwa mapigo ili kutojenga usugu na chuki ndani
yao.
Wawatie moyo watoto: Wazazi wawasifie (commend) na kuwatia moyo (motivate
and reinforce) watoto wao pale wanapotenda mazuri na si kuwakatisha tamaa ili kuwajengea
moyo wa ubunifu na kujituma katika kutenda kwa hiari yale yote yaliyo mema na mazuri.
Wazazi wawe mfano mwema: Wazazi wajitahidi kuwa mfano mwema (role model)
kwa watoto wao ili watoto nao waishi kwa kuyaiga mambo na tabia njema za wazazi wao
badala ya kutafuta mifano toka nje ya familia ambapo yaweza kuwa siyo myema.
Wazazi wawalee watoto kulingana na falsafa ya kanisa: Watoto walelewe kulingana
na mafundisho na misingi ya kanisa ili wasipotoshwe na mafundisho yasiyofaa ya kidunia
huku wakiwaongoza kumkubali na kumpokea Yesu katika hatua za awali na hatua za makuzi
yao yote.
Wazazi wawe wanawaombea watoto wao: Maombi ya faragha yafanywe na wazazi ili
kuwaombea watoto wao kama alivyo fanya Ayubu (Ayubu 1:5) kwani huenda wakawa
wametenda dhambi pasipo wazazi kujua.
Wawafundishe nidhamu iliyobora: Watoto wafundishwe tabia ya kuwaheshimu watu
wote, kutii na kufuata mapenzi ya Mungu, kuheshimu Ibada pamoja na vitu vingine vilivyo
vitakatifu.
Baada ya kuona kanuni ambazo wazazi yawapasa kuzitumia ili kuleta malezi bora na
yenye tija kwa watoto wao, yapo pia mambo machache yanayowapasa wazazi kuyazingatia
katika kuwalea watoto wao ipasavyo:
Kazi isiwafanye wazazi kukosa muda wa kuwa na watoto wao kwa kumwamini
mfanya kazi wa ndani katika kuwalelea watoto wao.
Wazazi wajue kuwa, watoto ni mali ya Mungu siyo mali yao, hivyo, wakipotea
watadaiwa maana watoto ni kondoo wa kwanza wanaotakiwa kuokolewa kisha wengine
walio nje ya familia (zizi).

Frank Philemon Karoli


77
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Wazazi wajue ya kwamba nidhamu mbovu ya watoto huanzia nyumbani huko nje
huwa ni nyongeza, hivyo, ni vyema matatizo ya watoto yakatatuliwa nyumbani na siyo
wayatatue watu wengine walio nje ya familia.
Wazazi watambue ya kwamba malezi ya watoto ni wajibu wake na siyo jukumu la
serikali, kanisa, ndugu au jamii maana ndiye aliyewazaa.
Wazazi wajue ya kuwa watoto anaowazaa siyo kizazi alichozaliwa yeye, hivyo,
changamoto kwa watoto zinaongezeka.
Wazazi wajuwe kuwa anazaa watoto wasiofanana katika mazuri yao na mabaya yao
hivyo wajitahidi kupalilia mazuri ya kila mtoto. Mahitaji na malezi ya watoto hutofautiana
kulingana na jinsia, vipaji, vipawa na kalama hivyo tabia zile mbaya ziondolewe na nzuri
zipaliliwe.
Wazazi wafahamu ya kuwa wasipowafundisha watoto yawapasayo, ulimwengu
utamfundisha yale yawapasayo kiulimwengu na wazazi wasiwalaumu watoto bali awarejeshe
kwa upendo.
Wazazi watambue ya kuwa uwezo wa watoto kiakili haulingani kwa kila mtoto,
hivyo, si vyema kumfananinisha au kumlinganisha mtoto wako kwa mtoto wa mwingine bali
fanya sehemu yako kupalilia na kuamusha uwezo wa mtoto wa kiaklili.
Mzazi atambue kuwa ni kawaida watoto kuomba kitu mpaka cha ziada, hivyo, kama
unajadiliana naye (mtoto) kuwa ukipata utampatia. Mtoto asipokuwa huru kwa wazazi wake
hususani katika kuwaomba mahitaji yake anaweza akajenga tabia ya udokozi au wizi.

Namna ya Kumrudi Mtoto ili Awe na Nidhamu iliyo Njema


Katika kitabu cha Mithali (Mithali 13:24; 22:15; 23:13-14 na 29:15, 17) aya tajwa
kwenye mabano ni miongoni mwa nyingi zinazoelezea juu ya kuwarudi watoto ili wawe
katika nidhamu kama lilivyo agizo la kimbingu (maana hata Mungu huwa anawarudi
wanadamu), hivyo, wazazi wanaotambua wajibu wao lazima wafanye hivyo. Kutomwadhibu
mtoto ili kumrudi katika njia impasayo tutawakosesha mbingu pamoja na wazazi nao kuikosa
mbingu (1Samweli 3:12-14); katika namna ya kumrudi mtoto pazingatiwe mambo yafuatayo:
Mzazi amwadhibu mtoto pale anapokuwa na uhakika kuwa mtoto katenda kosa tena
kwa kukusudia au imekuwa nimazoea.
Mzazi asimwadhibu mtoto wakati akiwa na hasira maana wakati mwingine mzazi
anaweza akamalizia hasira zake kwa mtoto na kusababisha madhara kwa kumjeruhi au
kusababisha kifo mtroto.
Mzazi asimwadhibu mtoto mbele ya watoto wenzake maana hata wao hujihisi
kuzalilishwa na wanaweza kuwa wanamtania na kusababisha matatizo ya kisaikolojia kwa
mtoto.
Mzazi asitumie mbinu ya aina moja katika kumwadhibu mtoto ili kuepusha usugu kwa
mtoto kutokana na kuizoea aina hiyo ya adhabu. Aidha, adhabu ya kumnyima mtoto chakula
sio adhabu sahihi hata kidogo kumpatia mtoto.
Fimbo itumike kama hatua ya mwisho baada ya njia zingine kushindikana.
Ikumbukwe pia, fimbo, kufinya na makofi huwa yana kikomo cha umri fulani kwa watoto
hasa akiwa mkubwa kiumri.
Mzazi aepuke kutumia maneno ya kashifa na ya kumdhalilisha mtoto wake mfano
matusi ya nguoni, kumtukania baba au mama maana hujihisi kama wazazi walikosea kumzaa.

Frank Philemon Karoli


78
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Baada ya kumrudi au kumwadhibu mtoto, mzazi ajitahidi kurejesha na kuonesha


upendo kwa mtoto kama hapo awali na siyo kumchukia daima kwa kuwa tu amemkosea.

Matarajio Ambayo Watoto Hutegemea Kutoka kwa Wazazi Wao


Mara zote watoto wote hutegemea mambo mema na mazuri kutoka kwa wazazi wao
maana ndilo tumaini lao badala ya Mungu hapa duniani. Watoto hutegemea mambo
yafuatayo kutoka kwa wazazi wao: wazazi wao kupendana (wao kwa wao), wazazi
kuwapenda watoto kwa upendo usio na masharti, wazazi kushughulikia haja na mahitaji yao,
wazazi kuwa mfano bora kwao kwa mambo yote, wazazi kuwa na muda wa kuzungumza na
kufurahi nao, wazazi kuwa na ujasiri wa kuwakataza mambo mabaya na kuwaunga mkono
mambo mazuri wayatendayo, wazazi kuwafundisha watoto mambo yote mema na yenye tija
wanayopaswa kuyajua na kuyafahamu, wazazi wawe wakristo kweli kweli na wauishi
Ukristo na wazazi kuwatia moyo na kuwaombea kwa Mungu kila wakati.

Athari za Mazingira (Nurture) na Asiri (Nature) kwa Watoto


Mazingira yanayotuzunguka (nurture) na kurithi kutoka kwa wazazi (nature) ni vitu
viwili vinavyo athiri (kihasi au kichanya) ubora, uwezo, tabia, umbo, afya na muonekano na
mwenendo wa mtoto. Mtoto anaweza akarithi mambo mazuri au mabaya kutoka kwa wazazi
wake au tabia na makuzi yake yakaathiriwa na mazingira anayoyakulia mtoto.
Mzazi yampasa pia kuwa mwangalifu juu ya asili “nature” na mazingira “nurture”
katika makuzi na malezi ya mtoto. Jambo la kurithi hilo huwa ni jambo la kibailojia zaidi,
hivyo, huwapasa wazazi kulijua aidha kwa kupima afya zao au kumuomba Mungu endapo
tatizo hawakuligundua mapema katika hatua za uchumba (rejea sura ya pili juu ya A hadi Z
za uchumba), lakini suala la mazingira ndilo huwa linahitaji uangalifu kutoka kwa wazazi au
walezi maana ubora na uzuri wa mtoto aliozaliwa nao waweza kuongezewa au kuharibiwa na
mazingira anayokulia mtoto.
Tabia mbaya aliyojifunza mtoto kutoka kwa wazazi yaweza pia kurekebishika (kama
siyo ugonjwa) kulingana na mazingira ambayo wazazi wanamkuzia kwayo pamoja na
udhibiti wa mwingiliano na watoto wengine katika jamii inayomzunguka. Hivyo, basi asili
(nature) yaweza kurekebishika kwa mtoto endapo wazazi watakuwa makini katika kumlea
vyema maana madhaifu ya kitabia yanaweza kuondolewa kwa mtoto na kuingiziwa tabia
njema ambayo wazazi wanazitaka awenazo mtoto wao.
Anaweza akazaliwa mtoto ni muongeaji sana kutokana na kurithi kutoka kwa mzazi
mmoja au wote, lakini mazingira ya kumlelea mtoto huyo yakizingatiwa yanaweza
kuirekebisha tabia hiyo ya uongeaji kutoka kwa mtoto. Wapo watoto ambao wanaweza
kuzaliwa wakiwa au wanauwezo mzuri wa kiakili lakini wazazi wanaweza wakachangia
kuuharibu uwezo wao wa kiakili kwa kuwapatia vyakula visivyofaa na malezi mabaya
yasiyowapatia watoto nafasi ya kujifunza zaidi ili kuongeza uwezo wao wa kiakili.
Mazingira yanayoambatana na aina ya watoto anao cheza nao mtoto katika jamii
inayomzunguka yaweza kumwathiri kichanya au kihasi mtoto katika makuzi yake. Makundi
rika pia yanaweza yakaathiri tabia na uwezo wa mtoto kutokana na uchaguzi wa aina ya
marafiki. Wakati mwingine mazingira ya kumfungia mtoto ndani ya geti ili asichafuke au
asichangamane na watoto wengine kwa weza kuleta madhara katika makuzi yake maana
mtoto anaweza asiwe na uwezo mzuri wa kushirikiana na wengine, kuzizoea changamoto, na

Frank Philemon Karoli


79
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

kuwa mbunifu kulingana na fursa anazoweza kuzipata mtoto kutokana na kuchangamana na


watoto wengine.
Kuchangamana kunamsaidia mtoto kukuza uwezo wa kuongea maana anakuwa
akiongeza misamiati pale anapokuwa akiongea na wenzie pamoja na kukomaa kwa mifupa
katika mwili wake pale anapokuwa akicheza michezo mbalimbali na watoto wengine tofauti
na anapokuwa na wazazi au mfanyakazi wa nyumbani. Kutokana na sehemu kubwa
inayochangiwa na mazingira (nurture), hivyo, mazingira yana sehemu kubwa sana ya
kubadiri tabia na mienendo ya mtoto (kihasi au kichanya) hususani kupitia, kusikia, kuona,
kujaribu, kuhisi, kuonja n.k. katika sehemu zote tano za fahamu.
Kwa sababu ya mazingira na mambo yanayotendeka ndani yake katika mienendo na
mitindo ya kimaisha inapoteza na kuharibu watoto endapo wazazi hawatakuwa makini.
Niseme tu kuwa: kulea watoto ni kazi ngumu maana ni kazi inayowahitaji wazazi kuwa
waangalifu, wafuatiliaji wa karibu na warekebishaji wa kile kisichofaa kwa watoto kulingana
na mazingira yanayowazunguka pamoja na jamii wanayoishi.

Tabia Nne za Makundi ya Watoto


Watoto hutofautiana katika tabia kati ya mtoto mmoja na mtoto mwingine. Kulinga na
kuzaliwa kwao watoto, kuna makundi makuu manne ya aina za watoto:

Wenye silka ya kuhurumiwa


Watoto wa aina hii wapo wazi sana na hupenda sana kueleza hisi zao na mara nyingi
mazingira wanayoyaishi na kukulia kwayo huwa yanawagusa sana katika maisha yao ya kila
siku. Huwasilisha mambo yao kwa hisia ya hali ya juu (hata kwa kutia chumvi ili jambo lao
lisikilizwe na kufanyiwa kazi). Wanatabia ya ulalamishi, hivyo, wanapenda kuhurumiwa na
kutiwa moyo na kufarijiwa kwa hali ya juu pale wanapoleta malalamishi yao ya kuonewa au
kutotendewa vyema.
Hujisikia vizuri pale hisia zao zinapoguswa hususani kwa kusaidiwa katika uhitaji na
msaada wautakao. Watoto hawa mara nyingi hawaoni mambo kwa mtazamo chanya na ndiyo
maana hulalamika na kupenda kushitaki kwa wazazi wao. Aina ya watoto wa namna hii
hawatengenezi urafiki kwa haraka na wanapotengeneza urafiki ni kwa wale tu wanaowagusa
hisi zao na wenye tabia ya kuchukuliana matatizo.Mzazi mwenye mtoto wa silka hii asipende
kuacha kumsikiliza au kutomjali pale anapoleta malalamishi yake, tena ajitahidi kuwa na
mtazamo chanya huku akimtatulia matatizo yake kwa upole aidha, kwa kumfariji au kumtia
moyo na kumpa pole.
Watoto hawa wakilelewa vyema na kuwa watu wazima huwa ni wazuri katika suala
zima la kufikiria mambo makubwa, huwa wenye huruma na wenye kuguswa na matatizo ya
wengine haraka, hivyo, ni wepesi kusaidia na kutoa misaada, ni wabunifu kwa sababu ya
tabia yao iliyojengeka katika hisia za ndani zaidi. Kutokana na tabia yao ya kupenda kuguswa
na matatizo ya watu wengine, huwa wapo vizuri katika nyanja ya huduma za wateja, masoko
na mawasiliano pale wanapokuwa watu wazima na wenye taaluma zao.

Wenye silka ya utendaji


Watoto katika kundi hili ni watoto wenye purukushani nyingi sana na wanapenda
kutambuliwa, hivyo, hufanya jitihada ili waonekane kuwa wapo. Wanamaswali mengi sana

Frank Philemon Karoli


80
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

na niwadadisi na watafiti wa vitu. Wanatabia ya kutenda mambo bila kusukumwa kwani


wanauwezo mkubwa wakujisimamia na kufanya mambo bila msukumo wa nje tofauti na
msukumo wa ndani walionao. Watoto walio katika aina ya kundi hili wanapenda kusifiwa na
kupewa hongera kwa kile kizuri au mafanikio wanayoyafikia, aidha, katika ufaulu wao wa
masomo, kubuni jambo au kutengeneza kitu. Kwa chochote kile wanacho tenda wanapenda
mchango wao utambulike katika familia.
Wazazi wenye watoto wa namna hii wajitahidi kuwatia moyo watoto na
wasiwakatishe tamaa ili wasije kuua ari yao ya ubunifu bali watambue michango yao katika
utendaji na ubunifu; sanjali na hilo, wazazi wajitahidi kuwapongeza na kuwaambia waongeze
juhudi zaidi ya hapo. Watoto walio katika aina hii wakilelewa vyema na kukua, wengi wao
huwa ni wabunifu, wachunguzi, mafundi stadi na wasanifu wa mambo; niwazuri katika
kuongoza na kusimamia mipango maana wananidhamu ya kujisimamia na kusimamia jambo
hadi hatua ya mwisho. Wanauwezo mkubwa wa kiupelelezi, kisaikolojia, kiutafiti kutokana
na udadisi mkubwa walionao; ni wanamipango, waandishi na wachambuzi wa mambo
wazuri.
Wenye silka ya ucheshi
Watoto walio katika kundi la silka hii ni wachangamfu na wenye furaha ya hali ya juu
na pia ni wepesi wakutengeneza urafiki mapema na watoto wenzao au watu wazima.
Wanapendwa na kila mtu maana hawana makuu hata wanapokuwa wamekosewa. Watoto wa
aina hii huwa ni wenye kuleta uchangamfu na furaha katika familia maana ni wacheshi sana.
Hisia zao hazifichiki kwani zipo wazi; lo lote linalowatokea liwe gumu kiasi gani furaha yao
hurudi pale linapopita.
Wazazi wenye watoto wa silka hii ni vyema wakajitahidi kudumisha furaha yao katika
kuwa karibu na kufurahi nao na wawasimamie vyema katika kujali mambo kutokana na
hurka yao ya kutochukuli mambo kwa uzito. Watoto wa aina hii wakikua, wengi wao
wanafaa sana kwenye kuhamasisha au kushawishi, kuburudisha na kutengeneza urafiki kwa
haraka na watu wengine. Wanaweza sana kazi zinazohusu kuingliana na watu kwa sehemu
kubwa. Wanauwezo mkubwa pia wakuchekesha, hivyo, wanauwezo mkubwa katika sanaa ya
uchekeshaji kwa sababu ya uwezo wao mkubwa wa kuwafanya watu wachangamke na
kufurahi.
Wenye silka ya upokeaji
Watoto wenye silka ya upokeaji huwa ni kundi la watoto ambao hawapendi
kujishughulisha katika kutenda jambo kwa kubuni bali hupokea na kutenda. Mara zote
wanapenda kupokea amri ya kutenda kutokana na tabia yao ya kutojituma na uvivu.
Wanapenda kutendewa na sio kuwatendea wengine kutokana na tabia yao ya kutegea kwa
sehemu kubwa. Watoto wa aina hii sio wabunifu bali ni wapokeaji na wanapopokea ndipo
hutekeleza katika kutenda.
Watoto katika kundi hili, pale wanapohitaji kufanya jambo hufanya polepole. Watoto
hawa wana tabia ya ubinafsi na kujirimbikizia vitu kutokana na hali yao ya upokeaji iliyo
ndani yao. Wazazi wenye watoto wa aina hii wajitahidi kuwalea katika kuwapangia
majukumu ili kuwaondolea tabia ya uvivu na utegeaji; tabia yao ya ubinafsi, wazazi
wajitahidi kuwaondolea tabia ya upokeaji ili kuua tabia ya ubinafsi. Watoto wa aina hii
wanapokuwa wakubwa huwa ni wazuri katika kuwa viongozi; hufanya kazi vizuri iliyo na
masirahi kwao na katika kutekeleza kazi ambazo zimeshafanywa na wengine.

Frank Philemon Karoli


81
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Ngazi Nne Katika Makuzi ya Watoto na Maswali Yake:


Katika makuzi ya watoto na ufahamu wa kiakili, watoto hupitia hatua kuu nne za umri
katika mpangilio wa miaka kama ifuatavyo:

Mwaka 0-5 mtoto huwa anamaswali ya “Hiki ni nini?”


Katika umri huu wa mtoto anapozaliwa huwa hana kitu chochote kwenye ubongo
wake. Ubongo wake huwa wazi bila kitu chochote ndani yake (blank slate or empty mind),
hivyo, mtoto huwa anahitaji kujifunza kila kitu ili kujaza ubongo wake uliowazi. Katika
hatua hii watoto huwa wanauliza kila kitu kuwa “hiki ni nini?” na wakati mwingi huwa
mpaka wakiguse hicho kitu; umri huu ni wakati ambapo mzazi anatakiwa kuingiza vitu au
mambo ayatakayo kwenye ubongo wa mtoto kabla hajaingiza mambo mengine yasiyofaa.
Ndicho kipindi cha kumbadirisha mtoto na kumtawala.

Miaka 6-9 mtoto huwa anamaswali ya “Inakuwaje?”


Kipindi hiki huhitaji mahusiano ya karibu sana kati ya mtoto na wazazi wake ili
kujenga msingi wa mahusiano mazuri baina ya mtoto na wazazi. Hapa ndipo penye kuondoa
tabia mbaya za watoto zilizoingia kipindi cha kwanza cha miaka 0-5 maana katika hatua hii
watoto hutaka kujua kitu au jambo likoje. Ndani ya hatua hii inawapasa wazazi kutenga muda
wa kutosha wa kuwa karibu na watoto wao ili kuwaweka sawa na kujibu maswali yao.

Miaka 10-14 mtoto huwa anamaswali ya “Kwa nini?”


Katika hatua hii ya makuzi ya watoto, misuli ya kichwa na ubongo wa mtoto huwa
umeanza kukomaa, hivyo, uwezo wa mtoto kifikra na kiakili huwa umepevuka. Watoto
katika umri huu huwa wako makini sana katika kufikiri na kudadisi ili kujua na kutambua
mambo. Hatua hii mzazi humpasa awe na uwezo wa kumkataza jambo mtoto na amwambie
kwa nini anamkataza au kumruhusu kwa maelezo toshelevu maana ni umri ambao mtoto
anahitaji majibu yenye hoja za msingi na siyo majibu yenye maelezo ya juujuu tu.

Miaka 15-17 mtoto huwa anamaswali ya “hiki nini, naweza kujaribu?”


Umri katika hatua hii huathiriwa na hatua zote tatu za awali na maisha ya mtoto katika
umri huu huwa anakuwa na msimamo wake mwenyewe kutokana na nini alikipata katika
hatua tatu za makuzi yake. Umri huu, kila unachomkataza mtoto ni kama unamchochea
kutenda maana yawezakuwa wazazi walichelewa kumwekea misingi katika miaka ya hatua
tajwa tatu katika makuzi yake. Kipindi hiki mtoto hutaka kujaribu kila kitu kwa vitendo hata
yale mambo mabaya, mfano; sigara, pombe, madawa ya kulevya na ngono.

Namna ya Kuzikabili Changamoto za Watoto


Mzazi ni vyema awe tayali kuzikubali na kuzikabili changamoto za watoto kwa zile
zenye mwelekeo mwema kwao. Zifuatazo ni baadhi ya changamoto kutoka kwa watoto:
o Mtoto hawezi kujua kusamehe endapo hasamehewi pale anapokosea katika
mazingira ya nyumbani kwao.
o Mtoto hawezi kujifunza uvumilivu kama kila kitu anapata au kupatiwa na mzazi
kwa wakati.

Frank Philemon Karoli


82
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

o Mtoto hawezi kujenga kiwango cha kurizika kama hakosi wala kupungukiwa na
cho chote.
o Mtoto hawezi kujua kuwa hawezi endapo kama wote waliomzunguka ni
wakamilifu, hivyo, mtoto aachwe acheze na watoto wenzie ili kujua wapi hawezi
ili kujifunza.
o Mtoto hawezi kujifunza ubunifu kama kila kitu anakatazwa kufanya kisa
atajichafua au kuumia.
o Mtoto hawezi kujifunza ushirikiano kama kilakitu kwake anafanya peke yake bila
kushirikiana na wengine.
o Mtoto hawezi kujifunza ujasiri kama hakutani na mambo yenye kuhitaji ujasiri.
o Mtoto hawezi kujenga uking‟ang‟anizi au ukamiaji wa jambo kama kila kitu
achofanya kwake ni kirahisi tu.
o Mtoto hawezi kujiamini, kujirekebisha, na kuwa mbunifu kama hajui kushindwa.
o Watoto hawawezi kuwa na uwezo wa kujitawala wenyewe kama hawakai
wakakubaliana na wakubwa zao.

Mambo Mema ya Kuwajenga Watoto


Malezi ya watoto yanahusisha mambo ambayo wazazi wanatakiwa kuwafundisha
watoto wao. Katika malezi ya watoto, wazazi wa wahusishe watoto katika mambo yafuatayo:
Kuwashirikisha katika mipango ya familia. Wazazi wanapaswa kuwashirikisha watoto
wao mipango ya familia.
Watoto wafundishwe kufanya maombi na ibada ili kuwa madhubuti katika mambo ya
kiroho (Luka 2:45, Walawi 14:3, 1Sam 2:2).
Watoto wafundishwe juu ya kuheshimu vitu vitakatifu yaani ndoa, sabato, zaka na
vyombo vya Meza Bwana pamoja na huduma zote za ibada kanisani.
Watoto wafundiswe kumtumikia Mungu ili kulitimiza agizo la Yesu la kuihubili injili
ulimwenguni (Warumi 14:18).
Watoto wajue hali halisi ya maisha ya wazazi wao katika nyanja ya uchumi na mambo
mengine ili waweze kuishi kulingana na hali halisi ya uchumi wa familia yao.
Watoto wafundishwe juu ya umiliki wa mali ili kuwajengea misingi mizuri hapo badae
katika familia zao (Mwanzo 1:29).
Watoto wafundishwe maadili na mahusiano mema katika misingi ya Kikristo ili wawe
watu wema katika utu uzima wao.
Watoto wafundishwe namna ya kuongea na kuepuka matumizi mabaya ya ulimi katika
maneno.
Watoto wafundishwe namna ya kuheshimu wengine ili nao waheshimiwe vivyohivyo.
Watoto wafundishwe namna ya kuchagua marafiki ili wasije wakapotea kwa kufunga
nira na watu wasioamini.
Watoto wafundishwe namna ya kushukuru kwa kila jema watendewalo aidha na
Mungu au mwanadamu.
Wafundishwe juu ya umuhimu wa kufanya kazi pamoja na uchaguzi wa kazi ya maisha
Wafundishwe kutunza vitu na kumbukumbu ili wawe mawakili wazuri katika kupanga
na kutenda.

Frank Philemon Karoli


83
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Wafundishwe kuvaa mavazi ya heshima ili wasifanane na watu wa mataifa jinsi


wavaavyo (Mwanzo 4:2).
Wafundishwe uongozi kwa ajili ya manufaa yao hapo badae wajapo kupata majukumu
ya kifamilia na ya kikazi (1Sam 2:11).

Makosa ya Eli-Kuhani (1Samweli 2:12-36) na Fundisho kwa Wazazi.


Eli alitenda makosa ambayo wazazi wa Kikristo wa dunia hii ya sasa yawapasa
kujifunza ili kuyaepuka. Makosa aliyoyatenda Eli katika kuwalea watoto wake kama mzazi ni
yafuatayo: Eli alipaswa kuwaadhibu watoto wake ila hakufanya hivyo; Eli kama baba
alikuwa chini ya watoto hivyo, watoto walimtawala; Eli aliwaheshimu au kuwaogopa watoto
wake badala ya Mungu; Alikuwa ni baba mwenye kudekeza watoto hivyo, hakuwakaripia;
Japo aliteuliwa kuwa kiongozi, hakuweza kuiongoza familia yake vyema na Eli hakuwakanya
wanawe katika kuviheshimu vitu vitakatifu.

Kuwaombea Watoto
Hakuna mwanadamu aliye salama kwa siku bila maombi (Pambano Kuu uk 530).
Kila siku wazazi wanawafanyia watoto wao mambo mengi – ili kuonesha kuwa
wanawapenda na kuwajali, kuwafundisha, kuwaelekeza, kuwasaidia, kuwaongoza,
kuwawezesha, kuwatia moyo kuwalina na mengine mengi. Wazazi hutumia nyakati zao
njema ili kuwezesha maisha ya watoto wao, kuwasaidia kazi za shuleni na kuwaongoza
katika kutenda kazi. Wazazi hutumia pesa nyingi ili kufanikisha michezo ya watoto wao,
kuwapatia elimu bora ili wakue na kuwa jinsi wazazi wapendavyo, huwapatia watoto wao
misaada, fursa ili kuyafikia matamanio yao katika dunia hii.
Lakini katika nyakati za mchakaliko wa kazi nyingi katika maisha ya ulimwengu
huuu huwa tunakumbuka kuwaombea watoto wetu? Sirejerei yale maombi ya haraharaka ya
kwenda kulala au wakati wa kuagana nao asubuhi wakienda shuleni na wazazi wakienda
kazini ambayo yanaumaana kiasi kidogo tu juu yao watoto. Namanisha maombi mahususi ya
kina, yenye nguvu, yakuomba utimizwaji wa ahadi zilizoahidiwa na Mungu, pamoja na
maombi ya uvuvio wa watumaini kwa watoto. Kila mzazi hufurahia tabia njema ya watoto
wake pale wanapozidi kutembea katika kweli ya mungu. “Sina furaha iliyo kuu kuliko hii,
kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli” 3Yohana 1:4.
Hivyo, maombi yetu kwa watoto wetu hayaendi hivihivi wala kuptea bure na kufa,
bali huishi milele katika maisha ya watoto. Uhusiano wao na Yesu ni kitu pekee
kitakachowapeleka Mbinguni, na kwa hili lazima tuwaombee watoto wetu. Waombee tabia
zao, wokovu wao, ulinzi na hatima ya maisha yao ya baadaye. Marazote, mzazi naombeapo
watoto wake lazima azidai ahadi za Mungu kwa niaba yao. Hakuna kitu chenye nguvu kama
maombi ya kimyakimya ya wazazi wanapokuwa wamepiga magoti kwa unyenyekevu na
wakiwawasilisha watoto wao mbele za Mungu. Maombi yananguvu kwa sababu tunaye
Mungu ambeye hutenda hata katika mambo yasiyowezekana wakati tukimuomba (rejea
kujibiwa kwa ombi la Hana katika 1Samweli 1:27).
“Nguvu ya maombi ya mama anayeomba hayawezi kukisiwa. Anapopiga magoti
pembeni ya mtoto wake wa kiume au wa kike tangu utoto hadi ujana, madhara ya maombi
hayo hayawezi bainika mpaka wakati wa hukumu, kuwa maombi hayo yalikuwa na msaada
kwa watoto wake. Kama imani ya mama itaunganishwa na Mwana wa Mungu, maombi yake

Frank Philemon Karoli


84
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

yatamsaidia mtoto wa kiume kurejeshwa kutoka katika nguvu ya majaribu, yanaweza


yakamkinga binti kuzama katika tamaa ya dhambi” (tafsiri isiyo rasimi kutoka The Adventist
Home uk 266). Maeneo muhimu ya kuwaombea watoto ni kama yafuatayo:
1. Wokovu: Mzazi aombee wokovu wa watoto wake kwa siku nzima. Waombee
watoto wapate uzoefu wa wokovu kama Mtume Paulo (Wafilipi 3:10-11). Uombeapo watoto
wako, dai ahadi zilizo katika Warumi 10:9,13; Warumi 5:5; Isaya45:8; Tito 2:10; 2Timotheo
2:10.
2. Tabia: Tamanio la mzazi kwa watoto, tabia zao kuwa kama za Kristo
(1Wakorintho 11:1; Mathayo 5:16). Maombi yetu kwa tabia za watoto wetu ya daia ahadi
katika mafungu yafuatayo: Waefeso 4:32; Isaya 1:17; 1Samweli 12:24 na Mathayo 5:16.
3. Uhusiano: Maombi ya wazazi kwa watoto wao lazima ya jikite katika kutengeneza
uhusiano mzuri na Mungu kwa kuzipita njia sahihi katika mapenzi yake Mungu (Zaburi
23:3), pamoja na kuwaongoza katika uchaguzi mzuri wa marafiki na wenzi wao wa baadaye.
Mzazi ombea watoto kuwa na mahusiano chanya na kuwaongoza kwa Yesu. Ombea kila siku
waepukane na misukumo ya kutenda maovu (zaburi 1:1,2). Omba kuwa, Mungu
awaondolee watoto wako tabia zote mbaya za marafiki zao. Katika kuomba dai ahadi ya
Mungu kutoka 2Wakorintho 6:14.
4. Furaha: Kwa kuwa tamanio la kila mzazi ni kuona watoto wao wakiwa na furaha,
basi wasikome kuwaombea furaha watoto wao kama Mfalme Daudi asemavyo katika Zaburi
16:11 . Neno furaha katika Biblia limeandikwa mara 200 zaidi. Wazazi wawaombee watoto
wao furaha ya kimbingu na siyo ya kiulimwengu (Wafilipi 4:12-13). Mzazi anapoombea
watoto wake adai ahadi kutoka katika Nehemia 8:10; Wakolosai 13:5; Waebrania 13:5;
1Wathesalonike 1:6; Zaburi 92:4.
5. Ulinzi: Omba Zaburi 91:1-7 kwa niaba ya watoto wako sambamba na Waefeso
6:10-13. Moja ya siraha yenye nguvu kwa mzazi wa Kikristo aliyonayo ni uwezo wa kuomba
kila siku ili kuwe na ulinzi kwa watoto wao (2Wathesalonike 3:3). Uwe mahususi katika
kuzidai ahadi za Mungu katika kuwaombea watoto wako sambamba na Warumi 6:14;
Kumbukumbu la Torati 31:6; Waebrania 13:5. Hivyo, omba Zaburi 4:8; Hesabu 6:24-26;
2Wathesalonike 3:3.
6. Maisha ya baadae: Ombea watoto kuwa waaminifu na watii kuazia sasa na hata
milele kwa Mungu kama Henoko (Mwanzo 5:24) na pia, Yesu awe rafiki wa milele na
mwokozi wao.
7. Uaminifu: Tamanio lingine la wazazi katika kuwaombea watoto wao ni kuwa
waaminifu katika vitu vidogo na vikubwa maishani mwao (Luka 16:10). Ombea watoto
wawe waaminifu kwa Mungu, wenzi wao, watoto wao, kazi, fedha na kanisa. Kanisa la
awali lilikuwa na uaminifu (Matendo 2:26) , hata watoto wetu wawe waaminifu vivyohivyo.
Katika nyakati ngumu, ombea wasimame imara kama wale rafiki watatu wa Danieli –
shadraka, Meshaki na Abedinego (Danieli 3:16-18). Maombi yako kwa watoto yadai ahadi
kupitia mafungu yafuatayo: Joshua 24:15; Danieli 6:10-16; 2Timotheo 1:7; Joshua 1:9;
Waebrania 4:12; Waebrania 12:1-2; 1Wakorintho 13:4-8; Mithali 3:3; Mithali 14:22.
8. Maombi mengine ya msingi ya kuwaombea watoto ni: Kukua katika neema
(2Petro3:18); Upendo (Wagalatia 5:25; Waefeso 5:2); uaminifu na uadilifu (Zaburi 25:21;
Mithali 10:9); Kumtegemea Mungu (Mithali 3:5; Zaburi 3:5); Kulipenda Neno la Mungu
(Zaburi 19:10); Rehema (Luka 6:36; Luka 1:50); Heshima (wao wenyewe, wengine na

Frank Philemon Karoli


85
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

mamlaka: 1Petro 2:17; Waefeso 2:10 ); Ujasiri (Kumbukumbu la Torati 31:6); Usafi wa
moyo (Zaburi 51:10); Wema (1Wathesalonike 5:15); Ukarimu (1Timotheo 6:18-19); Amani
(Warumi 14:19; Isaya 26:3); Uvumilivu (Waebrania 12:1; 1Wakorintho 15:58);
Unyenyekevu (Tito 3:2; Mithali 22:4); Huruma (Wakolosai 3:12; Zaburi 145:9); Wajibu
(Wagalatia 6:5; Wakolosai 3:23); Kuridhika (Wafilipi 4:12-13; 1Timotheo 6:6); Imani (Luka
17:5-6; Waebrania 11:1-40); Moyo wa utumishi (Waefeso 6:7; Warumi 12:11); Tumaini
(Warumi 15:13); Hekima (Yakobo 1:5); Shauku juu ya Mungu (Zaburi 63:8; Zaburi 42:1;
Maombolezo 3:25); Wawe waombaji (1Wathesalonike 15:17); Shukrani (Waefeso 5:20;
Wakolosai 2:7; Zaburi 107:8); Utii (Matendo 5:29) na Kuwaombe msamaha au toba kwa
Mungu (Ayubu 1:5).

Frank Philemon Karoli


86
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 12 =

SAIKOLOJIA YA TABIA NA HISIA ZA MAKUNDI YA WATU

“Moyo wa mtu huifikiria njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake.
Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia
za mauti”

Mithali 16:9, 25

Kujifunza saikolojia ya tabia na hisia za wanadamu ni muhimu sana kwa wanandoa


na wachumba ili kuweza kuchukuliana na kutafuta namna ya kuweza kushabiina wao kwa
wao. Katika sura hii ya kitabu, inatoa upembuzi yakinifu juu aina za tabia za watu pamoja na
ubora na mapungufu kwa kila kundi la tabia, hivyo, soma kwa makini na kuelewa ili
kuyafanyia kazi katika kuepuka migogoro katika safari nzima ya ndoa au uchumba.
Neno linaloelezea mgawanyo wa tabia za watu (temperament) ligunduliwa na kuanza
kutumiwa kati ya mwaka wa 1640 na 1650 AD. Kabla ya neno “temperament” kuanza
kutumika, hapo awali neno “humour” lenye asili kutoka lugha ya Kilatini lenye maana ya
kimiminika (liquid) lilikuwa likitumika kuanzia mwaka wa 1000 AD; ikifikirika kuwa ndani
ya mwili wa binadamu kuna hali ya kiminika inayotembea inayoweza kusababisha
kubadirika badirika kwa tabia ya mwanadamu.
Kwa hiyo, neno humour lilitumika kwa kipindi kirefu cha zaidi ya miaka 600 ya neno
temperament kuanza kutumika likiwa linaelezea hisia zinazojenga tabia ya mtu.
Temperament ni neno katika lugha ya Kingereza lililotoholewa linaloelezea aina ya tabia,
hisia au mtazamo unaojenga tabia inayoathiri jumla ya tabia ya binadamu. Awali kabisa,
makundi ya tabia za wanadamu yalikuwa katika makundi makubwa mawili (2) kabla ya
kugawanywa kuwa makundi manne (4). Makundi hayo mawili ni yafuatayo:
Watu wenye hisia za nje au wazi (Extroverts): Hujumuisha kundi la watu walio
imara katika kuweka hisia zao wazi, watu wenye furaha, wacheshi, waongeaji na wenye
kuonesha hisia zao wazi pale wanapoguswa na jambo au kukwazwa. Watu walio katika kundi
hili ni wepesi wa kuunda urafiki na watu wengine, hawakai na jambo bila kuliweka wazi
maana siyo wavumilivu wa kukaa na mambo moyoni.
Watu wenye hisia za ndani au za uficho (Introverts): Kundi la watu hawa huwa ni
wasiri na wakimya sana. Hujitahidi kuficha hisia zao ili zisiweze kujulikana kirahisi. Wengi
wao wanaaibu sana na wenye haya na ni wagumu katika kutengeneza urafiki na watu kwa
haraka. Hawapendi kuweka wazi mambo yao, kwani hawapendi watu wengine wayajue
mambo yao hasa yalio ya sirini.

Frank Philemon Karoli


87
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Tabia za Makundi Manne (4) ya Matu


Makundi makuu mawili ya tabia za watu yaliweza kugawanywa na kupatikana
makundi mengine manne ya tabia za watu. Makundi hayo manne (4) ndiyo hutengeneza aina
nne za tabia yaani temperaments kwa wanadamu. Neno temperament lilitokana na neno la
Kilatini ambalo ni “temperare” linalomanisha mchanganyiko (mixture). Wanasaikolojia
wanadai kuwa: tabia hizi kwa binadamu huanza kujibainisha na kuweka mizizi kuanzia umri
wa miaka 6 hadi miaka 14.

Watu walio wacheshi (Sanguine)


Hawa ni watu wenye furaha, wachangamfu, wenye matumaini na mara nyingi
wanamitazamo chanya. Neno Sanguine limetokana na neno la Kilatini ambalo ni “Sanguis”
linalomanisha damu (blood) au uhusiano wa karibu.

Uimara wao watu wenye tabia hii:


 Husimulia visa vizuri.
 Waongeaji na wacheshi.
 Wanapenda kuchombeza katika mazungumzo au jambo.
 Wepesi wa kukumbuka rangi.
 Ni wawazi kwani ni “extrovat” asilimia mia.
 Ni wepesi wakutoa habari au kufichua siri.
 Wepesi wa kutoa faraja au kufariji wengine.
 Wapekuzi na wadadisi wa mambo au vitu.
 Ni wepesi kubadirika kitabia zao.
 Hawatunzi hasira wala chuki hivyo, hawana kinyongo.
 Ni rafiki wa watoto maana wanapenda kucheza na watoto.
 Wepesi wa kuanzisha urafiki hivyo, wanamarafiki wengi.
 Huungama na kukiri makosa yao haraka.
 Hupenda kuwa mashuhuri hivyo kufanya kila jitihadi waonekane.
 Hupenda kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.
 Wanajitolea sana kutenda mambo kadri ya jinsi wanavyoweza.

Udhaifu wa watu walio katika kundi hili:


 Watiaji wa chumvi kati simulizi, habari au maelezo wayatowayo.
 Wasahaulifu na vigeugeu, hivyo hawana msimamo wao binafsi.
 Hupenda kurudiarudia simulizi walizowahi kuzisimulia maana ni wepesi wa kusahau.
 Ni wachangiaji wazuri katika mazungumzo.
 Wakati mwingine hufanya mambo mengine yasiyokuwa na tija.
 Wanafuraha zilizopitiliza na mzaha au utani mwingi sana.
 Si wepesi wa kukumbuka majina ya watu.
 Walalamishi sana lakini pia ni wenye kujigamba (kujisifia) sana.
 Wanapenda kuonekana wako juu na hawapendi kushushwa daima.
 Wepesi wa kukasilika haraka.
 Huonekana kama hawajapevuka maana wanatabia ya utoto daima.

Frank Philemon Karoli


88
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

 Hawasikilizi jambo hadi mwisho hivyo hurukia habari na kutawala mazungumzo.


 Hupenda kupongezwa, hivyo, hufanya mambo yao ili kupata sifa.
 Hawana mpangilio wa mambo yao, maana hufanya mambo mengi kwa wakati
mmoja.
 Wengi wao wanatabia ya uchoyo na wivu kwa wengine.
 Hawajali katika utunzaji wa muda na vitu.

Kazi wawezazo watu wa tabia hii:


 Kukaribisha wageni.
 Utangazaji.
 Uhamasishaji.
 Kuhubiri (wengi wao ni wahubiri wazuri).
 Uigizaji (katika kipengele cha uchekeshaji au komedi)
 Uafisa masoko na biashara kwa kutaja baadhi.

Watu wasiokuwa na harara (Phlegmatic)


Watu katika kundi hili wana hisia za ndani, hivyo, ni wasiri na wavumilivu sana.
Huwa wanajitahidi kutafuta ukimya na utulivu wa maisha. Ni matajiri wa kutunza vitu ndani
ya mioyo yao. Hawana tabia ya papara wala harara (haraka) na hawatekelezi mambo kwa
wakati. Wanatabia ya kujali sana na hujiamini wao tu.
Watu wa aina hii, hotuba zao au mazungumzo yao pia huwa ni ya polepole, taratibu na
kustasta au kuzunguka. Si wepesi wa kukasirika haraka pale wanapo kwazwa au kutendewa
sivyo. Phlegmatic ni neno la Kigiriki (Kiyunani) ambalo ni “Phlegein” lenye maana sawa na
kuunguza. Watu walio katika kundi hili huhusishwa na tabia ya maji maana kutenda kwao
jambo haraka mpaka kuwepo msukumo wa nje.

Ubora wa watu walio katika kundi hili:


 Si wepesi wa kukasilika haraka.
 Wanapenda kuonesha haiba zao (personalities).
 Hufanya kazi polepole lakini kwa uhakika.
 Hawana wasiwasi wala papala kwani ni wavumilivu na watulivu.
 Wakimya na wenye kutumia akili sana katika kutenda jambo.
 Ni wachaguzi wa maneno katika kuzungumza.
 Ni wenye huruma na wakarimu pia
 Hufikisha hisia zao kwa namna walivyo na katika kuongea.
 Wanauwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto ziwaandamazo.
 Hupenda maridhiano hivyo, hawapendi migogoro. Pia ni watatuzi wazuri wa
migogoro.
 Huandaa na kujiandaa kwa jambo kwa uhakika endapo watapewa taarifa mapema.

Udhaifu wa watu walio katika kundi hili:


 Hawana bidii katika kazi.
 Wazito wa kufanya maamuzi.

Frank Philemon Karoli


89
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

 Wengi wao ni wategemezi kwa sehemu kubwa.


 Wanajilinda na kujiamini wao tu; ila ni wepesi wa kutekwa na mitazamo ya watu
wengine endapo wataikubali na kuiamini.
 Kwa sehemu kubwa hukwepa majukumu.
 Ni wenye haya na hufanya mambo yao kwa usiri sana.
 Hupenda kujihesabia haki binafsi.
 Waoga na wenye wasiwasi katika kuthubutu.
 Wengi wao ni wabinafsi.
 Si wepesi wa kuvutiwa na kubadirika tabia zao mpaka pale wanapokuwa
wamejiridhisha.
 Hufanya kazi zao polepole na kwa vituo.

Kazi zinazowafaa kufanya:


 Ualimu.
 Uhasibu.
 Ubunifu na usanifu.
 Diplomasia.
 Upatanishi.
 Jeshi.
 Ushauli, kwa kutaja baadhi.

Watu wenye silka ya hasira (Choleric)


Watu walio katika kundi hili ni watu wenye tabia inayohusishwa na tabia ya moto,
kwa sababu ya kuwa na hasira pa moja na mihemko iliyopitiliza. Wanatabia ya kuwa wazi na
hufikisha ujumbe ukiwa mkavu (bila kupunguza ukali wake) katika kuonesha hisia zao.
Hawana uwezo wa kutulia au kuvumilia katika kukaa na jambo. Choleric ni neno lililotokana
na lugha ya Kilatini “Cholera” lenye maana sawa na “Jaundice” likimanisha ngozi yenye
rangi ya njano.

Uimara wa watu katika kundi hili:


 Wanatabia ya uongozi (wanaweza kuongoza).
 Wanapenda kuleta mabadiliko kutokana na uhitaji.
 Wananguvu na uimara wa maamuzi.
 Hupenda kusahihisha makosa ili yasijirudie.
 Hujitegemea na kujitosheleza.
 Huwa si wachangiaji sana kwenye mapungufu.
 Ni watu wenye malengo na mikakati.
 Ni ving‟ang‟anizi wa kufanya jambo ili lifanikiwe.
 Wazuri katika mipango na kuitekeleza.
 Wazuri katika kutatua mambo hata yale yaliyomagumu.
 Ni watu wa vitendo na sio wapangaji wa midomoni.
 Wanajiamini sana kwani ni madhubuti na si wepesi wa kuteteleka.

Frank Philemon Karoli


90
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Udhaifu wa watu walio katika kundi hili:


 Wengi wao wanatabia ya ubinafsi.
 Ni watu wenye hasira kali (bad tempered). Wepesi sana kukasirika na hawawezi
kutuliza hasira zao.
 Hupenda sana kuwa mabosi, kwani upenda kutawala kila jambo.
 Hawana subira na uvumilivu. Kwa namna nyingine ni walazimishaji hata pasipo na
uwezekano.
 Hawawezi kupumuzika au kutulia (hawana mapumziko).
 Hawakubali pale wanapoonekana kushindwa.
 Hawapendi watu wanaolialia na kulalamika.
 Hawana huruma maana huchukulia hari ya huzuni kama hali ya kawaida.
 Wanajiamini kupita kiasi, hivyo, wakati mwinginge hufanya yasipendeza kwa watu.
 Wanapenda kupewa heshima na kutambuliwa kwa kile wanachokifanya.
 Wanapenda kazi zao zifanyike kwa uhakika na ubora.

Kazi wanazoweza kufanya:


 Utawala au uongozi.
 Usanifu na ufundi.
 Uzalishaji, kwa kutaja baadhi.
 Mipango na maendeleo n.k.

Watu walio na silka ya usiri (Melancholic)


Tabia za watu walio katika kundi hili huhusishwa na tabia za element za duni (earth
element). Kundi la watu hawa hujumuisha watu wenye tabia ya ubinafsi, usiri (introvert) na
wenye mashaka na kila mtu au kila jambo. Watu walio katika kundi hili wanapenda sana
kufanya kazi peke yao ili kufikia viwango wanavyovitaka wao wenyewe. Melancholic ni
neno la Kiyunani (Kigiriki) ambalo ni “Melankhoha” lenye maana sawa na “Nyongo
nyeusi” (Black bile).

Ubora wa watu katika kundi hili:


 Wachambuzi na watafiti wa mambo maana wapo makini na kila kitu.
 Wengi wao ni waaminifu maana waoga wa aibu, lawama na fadhaha.
 Hupenda kujitoa sana maana wanapenda ukamilifu wa jambo.
 Wanauelekeo wa kuwa wanafalsafa kwa sababu ya kujitegemea kwao kwa fikra na
mitizamo.
 Hutoa maamuzi (misimamo) yao kwa umakini sana.
 Wengi wao wanavipaji maalumu kwa sababu ya umakini wao.

Udhaifu wa watu walio katika kundi hili:


 Wana wana hisia kali za ndani (deep feelings).
 Hukumbuka matatizo yao mara kwa mara kutokana na ugumu wa kusahau pale
walipoumizwa katika hisia zao.

Frank Philemon Karoli


91
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

 Wanapenda kujiamini wao pekee yao, hivyo ni watu wenye mashaka na kila mtu au
jambo.
 Mitazamo yao siyo chanya mara zote.
 Wapo kinadharia na siyo kivitendo zaidi.
 Hawana tabia ya kuchangamana na watu, hivyo, si wepesi wa kujenga ursfiki haraka.
 Wanamisimamo ya kutokubadirika daima.
 Hukera kwa sababu ni wadadisi sana hata vitu ambavyo havina maana.

Kazi zinazowafaa kufanya:


 Uwanafalsafa.
 Sanaa mfano mziki na uandishi.
 Uvumbuzi.
 Uprofesa.
 Usanifu, kwa kutaja baadhi.

Aina za Watu katika Mawasiliano


Kwa kuwa binadamu tunahusiana na wengine kwa kufanya mawasiliano katika
maisha yetu ya kilasiku, yatupasa kufahamu aina za watu tunaofanya nao mawasiliano ya
majibizano (dailojia) kupitia mazungumzo yetu na wao. Yapo makundi manne ya watu
yanayojipambanua katika wawasiliano:
01. Majaji: Hawa huamini kuwa wapo sahihi kilakitu. Wanamasikio lakini hawasikii.
Watu wa namna hii mara zote huwa na mitazamo hasi na watu wa kukosoa kila kitu. Fikra
zao wamezifanya kuwa hivyo tayafri ili kuona hakuna faida katika kuwasikiliza wengine.
02. Washauri: Hawa wanauwezo wa kusikiliza watu kwa kwa makini na kwa muda
mrefu na kufanya tathimini ya haraka na kisha kuchukua hatua au kutoa majibu juu ya nini
cha kufanya. Watu hawa wametawaliwa na utashi wa kufanyia tathimini maelezo ya mtu na
kisha kutoa ushauri wakati mwingine bila kuombwa kufanya hivyo. Na huwashambulia wale
wasiopenda kusikiliza. Soma Mithali 18:13.
03. Waulizaji (wanaohoji): Ni watu wanaoamini kwamba njia nzuri ya kusikiliza ni
kuuliza maswali kwa muwasilishaji wa mada. Tabia ya watu hawa ya kuuliza maswali ni kitu
ambacho cha weza kuwa ni cha kukera, kuchosha au kuonesha kama kumshambulia
mtu.Watu hawa pia ni mabingwa wa kuingilia au kumkatisha mzungumzaji ili kuuliza swali
au maswali. Ni sawa, kuuliza maswali ni njia nzuri inayomfanya muulizaji kuelewa vyema,
ila watu hawa huzidi mno.
04. Wasikilizaji: Watu hawa hujitoa sana kusikiliza kwa ukaribu na hufuatilia
mazungumzo vyema kwa kuzingatia lugha ya picha, ishara, viungo vya mwili na tamathali za
semi. Watu hawa si watoa maamuzi au majibu kwa kile kilicho waslishwa katika
mazungumzo, bali tamanio lao ni ni kuelewa kisha kutoa majibu yakinifu. Angalia Yakobo
1:19.

Umhuhimu wa Kutambua Tabia na Hisia za Makundi ya Watu kwa Wanandoa na


Wachumba:
1. Itawasaidia wanandoa na wachumba kubebeana matatizo na kuvumiliana pia.

Frank Philemon Karoli


92
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

2. Itawasaidi kutambuwana tabia ili kurekebisha kwa upendo kwakila tabia zisizopendeza
miongoni mwa wachumba au wanandoa.
3. Itawasaidia wanandoa na wachumba kuombeana madhaifu na hulka walizonazo ili
Yesu aziondoe.
4. Itawasaidia kujuana umadhubuti wa kila mmoja hivyo kupanga namna ya kuzitumia ili
kuleta ustawi wa ndoa zao.
5. Itawasaidia wachumba kujiandaa kisaikolojia namna ya kuweza kuendana na mchumba
wake watakapokuwa katika ndoa.
6. Itawasaidia kuyakuza yale yaliyo mazuri kulingana na kundi la mtu miongoni mwa
wachumba au wanandoa ili kuleta ustawi mzu kwa familia au ndoa.

Frank Philemon Karoli


93
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 13 =

TOFAUTI ILIYOPO KATI YA MWANAMKE NA MWANAMUME

“Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia
msaidizi wa kufafana naye”
Mwanzo 2:18

Mwanamume na mwanamke wote waliumbwa na Mungu. Mwanamume aliumbwa


kwa mavumbi ya ardhi (udongo) na mwanamke aliumbwa kutokana na ubavu wa
mwanamume (Mwanzo 2:21-23). Mwanamke aliumbwa ili kumsaidia mwanamume
majukumu aliyokuwa amekabidhiwa na Mungu. Kusudi lingine la kuumbwa kwa mwanamke
lilikuwa ni kumwondolea mwanamume upweke aliokuwa nao. Mwanzo 2:18 inaeleza kusudi
hilo la kuumbwa kwa mwanamke “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke
yake, nitamfanyia msaidizi wa kufafana naye”.
Mwanamke na mwanamume wapo tofauti, lakini wapo sawa kihadhi mbele za Mungu
tangu kuumbwa kwao. Mwanzo 5: 2 inaeleza kuwa “mwanamume na mwanamke [Mungu]
aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa”. Utofauti uliopo
baina ya mwanamke na mwanamume hauelezei ubaya wala uzuri kwa kubeza upande
mwingine. Jambo la pekee linaloweka ufanano kati ya mwanamume na mwanamke ni kuwa
wote waliumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26-27).
Utofauti unaojitokeza baina ya mwanamke na mwanamume unachukua nyanja pana
sana. Mfano, wanawake huwaona wanaume kama watu wenye udhaifu wa kutowajali,
kutowasikiliza, siwaongeaji, hawajitoi sana katika kuwaonesha upendo, hawawajibiki katika
masuala mazima ya mahusiano na familia, wanapenda sana tendo la ndoa kuliko kusitawisha
upendo n.k. Sambamba na madhaifu yawanaume kama yanavyoelezewa na wanawake wengi;
wanaume nao hutoa madhaifu kwa upande wa wawanawake kuwa niwaongeaji sana,
hawaoneshi msukumo wa uhitaji wa tendo la ndoa, hawako makini, nidhaifu na wanapenda
kujidekeza.
Hivyo basi, wanawake na wanaume hufikiria mambo tofauti tofauti, huamini mambo
tofauti tofauti, uhitaji wao ni tofauti, mitazamo na tabia zao pia zipo tofauti. Tofauti hii ni
kutokana na kulelewa kwao, kufundishwa kwao, tofauti zao za homoni, tofauti zao za
kibaiolojia, tofauti zao za kimaumbile, tofauti zao za kimfumo wa ubongo ambazo hupelekea
utofauti katika majukumu, mitazamo, tabia na vipaumbele. Mwanamume na mwanamke
wapo tofati pia hata kibaumbile ya mwili na kibaiolojia pamoja na mfumo mzima wa bongo
zao.
Miongoni mwa tabia zetu na vipaumbele vyetu vya kijinsi na kijinsia vinatokana na
mfumo mzima wa jamii zetu tutokazo, mazingira tunayokulia, malezi na kile tufundishwacho

Frank Philemon Karoli


94
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

na walimu mashuleni. Sisi sote ni zao la kibaiolojia, utashi wa jamii zetu pamoja na
migawanyo ya majukumu kuendana na jinsi na jinsia zetu. Wanawake wanauwezo mkubwa
wa kuona kwa macho mambo mengi kwa upana. Pia, mwanamke anahisia za ndani za
kuweza kujua hisia za watoto na rafiki zao, matumaini yao, ndoto zao, hofu iliyofichika juu
ya nini wanachofikiria na kuhisi pia.
Kiwango cha kuona baina ya mwanamke na mwanamume kipo tofauti. Wanawake
wanauwezo mkubwa wa kuona pembeni (kulia na kushoto) kuliko mbele na nyuma.
Wanaume wanauwezo wa kuona vyema mbele na nyuma kuliko kiupana (upande wa kulia na
kushoto). Hivyo basi, mwanamke anauwezo wa kuona mambo mengi kwa upana kwa wakati
mmoja kuliko mwanamume. Tafiti za ajari za magari zinaonesha kuwa, kwa asilimia kubwa
wanawake hupata ajali za kugongwa au kugonga mbele au nyuma na wanaume kwa asilimia
kubwa hupata ajali za kugongwa au kugonga pembeni (upande ubavuni) wawapo katika
magari yao.
Inashauriwa kuwa, katika safari ya umbali mrefu, yampasa mwanamume aendeshe
hasa wakati wa usiku na wakati wa mchana mwanamke aendeshe gari, kwa sababu
mwanamume anaweza akatambua miondoko na aina za magari mengine yaliyo katika
barabara kwa mbele na nyuma yake. Itambulike kuwa hii ni kwa sababu jicho la
mwanamume limeumbwa na uwezo wa kuona mbali na jicho la mwanamke huona vyema
karibu na kwa upana mkubwa.
Mwanamke husikia vyema kuliko mwanamume na anauwezo mzuri wakutofautisha
sauti inapopanda na kushuka na sauti hiyo nini inaashiria. Wanawake pia wanauwezo
mkubwa wa kusikiliza na kuelewa lugha ya viongo vya mwili. Hivyo, ni vigumu sana kwa
mwanamume kumdanganya mwanamke wakiwa wanatazamana uso kwa uso. Kwa namna
hiyo, wanaume wanapohitaji kuwadanganya wake zao hutumia simu au barua wakiwa mbali,
ama taa zikiwa zimezimwa. Wanaume hutumia ubongo wa kulia tu wanapokuwa
wanasikiliza na wanawake hutumia ubongo wa kulia na kushoto kwa pamoja wakati
wanapokuwa wanasikiliza.
Mtoto wa kike mwenye umri wa wiki moja, anaweza akaitambua sauti ya mama yake
miongoni mwa sauti za wanawake wengine, ambapo mtoto wa kiume hawezi. Ubongo wa
mwanamke unauwezo wa kutenganisha na kutambua sauti na kisha kufanya maamuzi kwa
kila sauti tofauti na ubongo wa mwanamume. Mwanamume hupata shida au ugumu katika
kusikiliza mazungumzo wakati pakiwa na makelele.
Mwanamke anauwezo wa kutambua mabadiliko ya hisia ya mtu kutokana na sauti
yake ya mazungumzo, hasa kwa watoto wanapozungumza na watu wazima. Wanaume ni
wazuri kwa kuona kuliko kusikia. Wataalamu wa saikolojia wanadai kuwa, wanawake
huondokewa na misongo pale tu wanapotambua matatizo yanayowakabili. Na wakati
mwingine hupata ahuweni ya misongo pale wanapokumbatiwa na wale wanaowatia moyo.
Ngozi ya mwanamke inakiwango kikubwa cha hisia mara kumi zaidi ya ngozi ya
mwanamume. Ngozi ya mwanamke ni nyembamba sana kuliko ya mwanamume. Wanawake
hufurahia kuguswaguswa ngozi zao kuliko wanaume. Wataalamu wa tiba itokanayo na
kukumbatia (pet-patting therapy) wamethibitisha kuwa kukumbatia ni tendo la thamani
linalomsaidia mtu (hasa mwanamke) kuepuka huzuni na mtatizo mengine ya kisaikolojia.

Frank Philemon Karoli


95
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Wanawake hupenda kugusanagusana wao kwao pale wanapokuwa katika


mazungumzo yao kuliko wanaume. Kumvutia mwanamke yampasa mwanamume atumie
muda mwingi kumgusagusa. Wakati mwanamke anapokuwa na hasira ama amechukizwa na
mwanamume huwa hataki kuguswa. Lakini pia, ili kumpatia mtoto afya njema ya kiakili
anahitaji kukumbatiwa kwa wingi sana kwa sababu, watoto huzaliwa wakiwa hawana
chochote kwenye bongo zao, hivyo wazazi, walimu na mazingira huwajaza mitazamo, na
uchaguzi.
Mwaka 1999, palifanywa tafiti na Chuo Kikuu cha Mcgill katika jopo la watafiti
lililoongozwa na Meaney. Tafiti hii ilionesha kuwa watoto wa panya waliojaliwa na wazazi
wao ubongo wao ulikuwa vyema na watoto hao walikuwa na akili sana kuliko watoto wa
panya ambao wazazi wao hawakuwajali. Wanaume wengi hawaguswi au huguswa kidogo
katika hisia zao na anayehisi au kuugulia maumivu ama hajisikii vyema.
Wanawake wanauwezo mkubwa wa kutambua au kuhisi radha pamoja na harufu.
Wanaume wengi hupeda vyakula na vinywaji vyenye radha chungu kuliko wanawake.
Wanawake wengi hupenda vyakula na vinywaji vyenye radha tamu.
Ubongo wa mwanamume ni mkubwa kuliko wa mwanamke. Ubongo wa mwanaume
unaseli bilioni nne zaidi ya ubongo wa mwanamke. Sehemu kubwa ya ubongo wa
mwanamume umekaliwa na uhitaji wa tendo la ndoa (sex), lakini ubongo wa mwanamke
sehemu kubwa umetawaliwa na kujitolea au kuwajibika na kazi nyingi. Ubongo wa
mwanaume anasehemu maalumu inayowezesha kutambua uelekeo, lakini ubongo wa
mwanamke unasehemu maalumu inayomwezesha kuongea.
Tafiti pia zinaonesha kuwa, upande wa kulia wa ubongo wa mtoto wa kike hukua kwa
haraka zaidi kuliko wa mtoto wa kiume, ikimanisha kuwa mtoto wa kike atawahi kuongea
mapema kuliko mtoto wa kiume na atasoma, kujifunza na kuelewa lugha ngeni (mpya) kwa
haraka sana kuliko mtoto wa kiume. Ubongo wa kulia na kushoto wa mwanamke
umeunganishwa na nyuzi nene (kuliko ubongo wa mwanamume) iitwayo “corpus callosum”
ambayo husaidi mawasiliano na kubadilishana taarifa baina ya ubongo wa kulia na kushoto.
Ubongo wa kulia wa mtoto wa kiume huongezeka na kukua haraka kuliku ubongo wa
kushoto, na sehemu mbili hizo huwa na muunganiko mdogo sana. Kwa mtoto wa kike,
sehemu zote za ubongo hukua kwa uwiano sawa na kumpa uwezo mkubwa kuliko mtoto wa
kiume. Watoto wa kiume hupenda vitu bali watoto wa kike hupenda watu kwa sababu
ubongo wa mtoto wa kike umeunganishwa maalumu kupenda watu, bali ubongo wa mtoto wa
kiume ni kwa ajili ya kupenda vitu na maumbo yake.
Mwanamke na mwanamume hutumia sehemu tofauti ya ubongo wakati wakifanya
kazi ya aina moja. Wanawake wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi nyingi zisizofanana kwa
wakati mmoja kuliko mwanamume, kwa sababu mwanamke hutumia ubongo wa kushoto na
kulia kwa wakati mmoja, ambapo mwanamume hutumia ubongo wa kulia tu. Sehemu ya
ubongo wa kulia huhusika na ubunifu, mazungumzo, hoja ama fikara, maamuzi na kumudu
upande wa kulia wa mwili, wakati ubongo wa kushoto unahusika zaidi na lugha, misamiati,
hususani kwa wanaume.
Wanaume huongea ndani kwa ndani (kimya kimya), kwa sababu si wajuzi na hawana
uwezo mkubwa wa kimazungumzo kama walivyo wanawake ambapo wao wanao uwezo wa

Frank Philemon Karoli


96
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

kuzungumza nje kwa kutoa sauti. Sentensi za wanaume huwa fupi fupi sana na zenye
mpangilio kuliko za wanawake. Kwa wanandoa au wachumba, wakati mwanamume
anapokuwa amenyamaza kimya, ni rahisi kwa mwanamke kujihisi kuwa hapendwi.
Wanawake huongea huku wakisikiliza kwa wakati mmoja, lakini mwanamume
hawezi kusikiliza na kuongea kwa wakati mmoja. Kanuni ya msingi ya kuzingatia kwa
wanawake ni kwamba, wakati anapozungumza na mwanamume, aongee sentensi rahisi
zinazoeleweka na ajitahidi kumpa nafasi ya kuwa anafikiria kwa jambo moja baada ya
jingine. Sambamba na hilo, mwanamume hapendi kukatishwa wakati anapokuwa
anazungumza, ambambo ni ngumu kwa wanawake kufanya hivo.
Ubongo wa mwanamke umejengwa katika uchakatuaji (process-oriented) na ndiyo
maana wanawake wengi hupenda na kufurahia mchakato wa mazungumzo katika
mawasiliano. Sentensi zote zilizo katika hali au kauli ya taarifa hujenga mazingira rafiki kwa
wanawake pale wanapokuwa wanawasiliana wao kwa wao, ila hazifanyi kazi kwa wanaume,
kwa sababu, mwanamume hupenda sentensi zenye kauli ya moja kwa moja. Sentensi nyingi
za wanaume katika mazungumzo huwa ni za moja kwa moja na zimejikita katika kutoa
suluhisho au utatuzi wa tatizo zinapokuwa zinahitimishwa au kufika mwisho.
Ili kupata nafasi ya mwanamume kukusikiliza vyema yakupasa mtu ampe taarifa
kabla, mahali patakapofanyikia mazungumzo na mada husika itakayo tawala mjadala.
Ikitokea mwanamke anapenda kuongea sana na mtu fulani hasa jinsia ya kiume, jua ya kuwa
anamfurahia, na kama haongei naye jua yupo katika tatizo naye. Kuelezea na kutoa maana ya
neno kwa mwanamke si jambo la msingi kwake, maana yeye anajikita na sauti pamoja na
namna sauti inavyopanda na kushuka kulingana na hisia ya mzungumzaji sambamba na lugha
ya viungo vya mwili.
Mwanamke husoma kile kilichosemwa kutokana na sauti ya mzungumzaji, hivyo,
sura ya mwanamke huendana na hisia za msimuliaji au tukio husika linalotendeka kwa
wakati huo. Ili mwanamume kuuteka usikivu wa mwanamke yampasa sura yake na lugha ya
mwili kuendana na kile anachokizungumza au kusilikiliza. Tofauti na wanaume, wanawake
huwa na muonekano wa aina sita hadi saba katikanyuso zao wanapokuwa wakitazama au
kusiliza: sura ya huzuni, furaha, kuchukia, hofu, shauku, hasira, kushangaa na kurudia au
kusisitiza kile alichokiona au kukisikia.
Wanawake hupenda urafiki na kushirikiana, wanaume hupenda mamlaka na hadhi.
Wanaume hushindana, wanawake hushirikiana. Wanawake hupenda kuongelea chakula,
mavazi, urafiki, ndoa, watoto, haiba na matendo ya watu wengine. Wanaume hupenda
kuzungumzia michezo, kazi zao, habari na matukio, ujuzi na teknolojia. Jedwali lifuatalo
linaonesha tafiti iliyofanywa juu ya asilimia ya mazungumzo baina ya wanawake na
wanawake na wanaume kwa wanaume kwa njia ya simu katika kampuni moja ya simu huko
Uingereza mwaka 1999 kwa watumiaji wa simu 1, 000:
Aina ya mazungumzo Wanaume Wanawake
Marafiki 30% 53%
Mapenzi/mahusiano 18% 22%
Kazi 25% 11%
Michezo 16% 2%

Frank Philemon Karoli


97
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Mengineyo 11% 12%

Tafiti hiyo ilionesha pia, moja ya tatu ya wanawake wote mawasiliano yao yalidumu
angalau kwa dakika 15 na nusu ya wanaume mawasiliano yao yalidumu chini ya dakika 5.
Hivyo basi, wanawake huthamini mahusiano, wanaume huthamini vitu na kazi.
Mwanamke anaweza akamuacha mwenzi wake si tu kwa sababu hampatihii mahitaji
bali kwa sababu mwenzi huyo hatimizi hitaji la hisia kwa mke wake. Na mwanamume
anaweza akamuacha mwenzi wake kwa sababu ya kuona mwenzi huyo hana furaha kwa
sababu ya mahitaji anayotoa. Mwanamke anahitaji upendo, mahaba na mazungumzo. Hivyo,
mwanamume inampasa kuonesha mahaba, upendo na kumsikiliza mwenzi wake pale
anapokuwa anaelezea hisia zake badala ya kukimbilia kutuo suluhisho.
Mwanamume hapendi kukosolewa au kuonekana amekosea kwa sababu hujihisi kuwa
hajafanya jukumu lake impasavyo. Na hii ndiyo sababu ambayo humfanya mwanamume
kuwa mgumu kusema „samahani‟. Mwanamume huona kuwa anajihukumu moja kwa moja
kuwa anamakosa na ameshindwa. Ili kukabiliana na tatizo hilo, mwanamke inampasa
kutomfanya mwanamume kujihisi mkosaji anapojadili matatizo na yeye. Jambo hili kwa
wanaume huenda mbali sana, hata kwa kumpatia msaada mwanamume hujihisi ama
kutafasiri kuwa hayuko vyema sana au hajiwezi.
Mwanamume anachukulia kukosolewa, na ndio maana hupenda kuoa wanawake
ambao wanawazidi umri au ambao hawako juu yao kiuwezo aidha wa kielimu na kipato.
Wanaume hawapendi kujisalimisha kwa wenzi wao kuwa wameshindwa maana huhisi
wanaweza wasipendwe, lakini kiuhalisia mwanamke humpenda mwanamume ambaye
husema pale anaposhindwa. Mwanamume huficha hisia zake akimanisha kutoonesha wazi
wazi udhaifu wake. Kiasili mwanamume ni mtu mwenye mashaka, ushindani, kujihami na
anayejaribu kuzificha hisia zake.
Kwa mwanamume kuonesha hisia zake wazi wazi, hujiona kama ameshindwa
kujimudu. Tabia hii kuwa imejengeka tangu utoto wake kwa sababu ya maneno aliyokuwa
akiambiwa “wanaume hawalii”, “onesha sura ya kiume”, “kuwa na sura ya kazi”. Kwa
mwanamke, ubongo wake umeunganishwa kwa kuwa wazi, kuamini, kushirikiana, kuonesha
hisia. Kwa hoja hii, wanawake na wanaume hukutwa na changamoto kwa pamoja hasa kwa
kila mmoja kuchanganywa na mwenzake juu ya kutoelewa hali na hisia ya mwenzake.
Changamoto nyingine kwa wanaume ni kutokubali ama kuchukia kupewa ushauri. Hii
ni kwa sababu, mwanamume hujihisi kuwa anauwezo wa kutatua matatizo na kuona kuwa,
kuyajadili matatizo yake na wengine ni kuwaongezea mzigo wengine, labda huyo mtu awe na
jibu zuri zaidi. Kwa mwanamke kuweka wazi matatizo yao hujihisi kuwa na ahueni kutoka
kwenye msongo. Wanawake hawahitaji utatuzi wa matatizo yao, bali wanahitaji kuongea
matatizo yao na kusikilizwa tu. Mwanamke kushiriki tatizo lake na mtu mwingine ni
kuonesha ishara ya uaminifu katika urafiki au uhusiano wao.
Tofauti na mwanamke, mwanamume anapokuwa na msongo hawezi akaongea.
Wanaume huongea kwa ndani kwa sababu ubongo wao (wa kulia) hauna sehemu imara ya
mazungumzo kama ilivyo kwa wanawake. Kwa sababu hiyo, mwanamume hawezi akawa
anatatua tatizo huku anaongea. Kwa utofauti huo: mwanamke ni mwongeaji na mwanamume

Frank Philemon Karoli


98
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

ni mfikiriaji. Mwanamume anapokuwa anachangamoto, hutafuta jambo au kazi ya kufanya,


na anapokuwa anafanya ndivyo anavyokuwa anajaribu kutatua tatizo linalomkabili.
Wazazi wa kike hulalamika sana juu ya watoto wao wa kiume kuwa hawaongei nao.
Ifahamike kuwa, ili mzazi wa kike aweze kuongea na mtoto wake wa kiume lazima
ajihusishe na kazi anayofanya mwanae na ataweza kuongea nae wakati wafanyapo kazi hiyo.
Wakati wa hasira, wanawake huongea bila kufikiria na wanaume hufanya maamuzi bila
kufikiria, na ndiyo maana asilimia tisini (90%) waliopo gerezani ni wanaume. Mwanamume
yampasa kujua kuwa, wakati mwanamke anapokuwa katika changamoto huhitaji kuongea, na
kulia na jambo la msingi ni kumsikiliza na kumjali.
Wanawake hulia zaidi kuliko wanaume, kwa sababu ubongo wa wanawake
umeunganisha na hisia za ubongo mwingine. Mwanamke anaweza akalia wahati anapokuwa
ameonewa ama kutukanwa, lakini mwanamume hawezi akalia kwa sababu kihisia kwake
haimanishi cho chote. Katika nyakati ngumu, mwanamke anahitaji kutiwa moyo, kupewa
pole na katika jambo jema na zuri apewe hongera, sifa, ukaribu, pongezi kwa maelezo
toshelevu na siyo kwa majibu ya mkato. Hivyo basi, ndoa hutufundisha uaminifu, uvumilivu,
kujikana nafsi kwa kutaja baadhi – yawapasa wanandoa kuvumilia.
Wanandoa (wanawake na wanaume) watambue kuwa, hakuna aliyebora kuliko
mwingine mbele za Mungu, kama Wagalatia 3:28 inavyosema “Hapana Myahudi wala
Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote
mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu”. Kwa sababu hiyo yatupasa kuchukuliana, kutendeana
mema na kutobaguana kwa muktadha wa kijinsi na jinsia. Waefeso 2:10 inakazia pia
kuwa “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo
mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo” . Wote bila
kujali tofauti zetu za kibaiolojia, tupendane kama Yohana 13:34 inavyosema
“Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyo wapenda ninyi, nanyi
mpendane vivyo hivyo”.
Katika kuhitimisha sura hii, yatupasa kufahamu matamanio tofauti baina
ya mke na mume katika ndoa. Mwanamke katika ndoa hutamani mumewe awe
myenye kumthamini, mwenye akili mwenyemahaba, mcheshi, mzungumzaji,
msikilizaji, anayefikika, mwaminifu, muwazi, anayetoa mahitaji ya familia,
mwenyekuwa na muda na familia. Kwa upande wa mwanamume atika ndoa,
hupendezwa na mkemwenye kumridhisha, mwenye kumfanya kuwa na furaha,
kumvutia, mwenye kuleta amani nyumbani (Mithali 21:19; 27:15), mwenye
kumsifia na kumheshimu (Waefeso 5:33) na mwenye kujali usafi.

Frank Philemon Karoli


99
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 14 =

UMUHIMU WA KUSAMEHEANA MIONGONI MWA WANANDOA AU


WANAFAMILIA

“Mtu shujaa na imara ni yule anayesamehe kwani ni mwenye uwezo mkubwa


wa kuzimudu hisia zake, bali asiye samehe ni mwoga na dhaifu katika
kupambana na hisia zake”

Msamaha ni kumfungulia mwingine kutoka katika hukumu kwa sababu Kristo


ametufungulia kutoka katika hukumu yake. Kusamehe, ni kufuta kosa kabisa na
kutolikumbuka tena hata kama litakuja kosa lingine kutoka kwa mtu (mkosaji) yule yule.
Pakishatolewa msamaha juu ya kosa alilotenda mtu ama kumtendea mtu mwingine, haipaswi
kukumbushiwa au kukumbukwa na kuongezwa katika makosa au kosa lingine lililo jipya.
Kwa hiyo, kusamehe kuliko sahihi ni lazima mtu kufuta kosa na kulisahau kama jinsi Mungu
afanyavyo juu ya wanadamu katika kuwasamehe dhambi zao. Kusamehe kisha ukabaki
unakumbuka kosa la mtu alivyokutendea, utakuwa hujasamehe kwa maana ya kusamehe
kuliko sahihi.
Hivyo basi, kusamehe kuliko kwa kweli, ni kule kusiko na mashariti yo yote au
namna ya vigezo fulani vifikiwe, bali kusamehe ni kujua mtu alichokukosea na ukaendelea
kumsamehe, kutoweka kumbukumbu yo yote ya kosa (1Wakorintho), kutotoa adhabu ya
aina yo yote, kutokumbushia kosa, kuwa na rehema (Mathayo 5:7) na kuacha kosa hilo kuwa
limepita na kwenda zake.
Mwanandoa aliyemkristo wa kweli na msafiri anaye tazamia kuurithi uzima wa
milele ni lazima ajitahidi kuwa na kiwango cha juu cha kusamehe na kusahau anapokuwa
amekosewa au kutendewa baya ama na mwenzi wake au watu wengine. Kusamehe ni moja
wapo ya suala la msingi katika kujenga ndoa yenye ustawi mzuri. Mwanandoa kabla
hajaomba kusamehewa na Mungu, yampasa asamehe wengine kwanza (akiwemo mwenzi
wake) ili maombi yake yapate kibali kwa Mungu.
Katika injili ya Marko 11:25-26, kusameheana kumeelezewa kwa msisitizo kama
ifuatavyo: “Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili Baba
yenu aliyembinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehi, wala
Baba yenu aliye Mbinguni hatawasemehe ninyi makosa yenu”
Ukiisoma vyema pia Mathayo sura ya 5, 6 na ile sura 7 (hubiri la mlimani), ambayo ni
maneno ya Yesu mwenyewe, alisema mengi juu ya kusamehe; sio tu kwa wale walio wa
imani moja au walio ndani ya ndoa au familia moja, bali hata wale watu baki, msamaha
unawahusu pia. Ni vyema wanandoa wakapatana wao kwa wao pamoja na maadui zao kabla
ya kufanya ibada, kutoa sadaka na kuomba toba kwa Mungu aliye Muumba wao.

Frank Philemon Karoli


100
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Umuhimu wa Kusamehe kwa Wanandoa


Kushindwa kumsamehe mtu fulani ambaye ametukosea, hata kama hastahili msamaha,
kunaweza kutudhuru hata sisi wenyewe kuliko mtu huyo. Kama mtu fulani amekosea na
maumivu yanachoma kwa ndani kwa sababu unashindwa kusamehe, unaruhusu yakudhuru
hata zaidi. Maumivu ambayo hayajafanyiwa ufumbuzi miongoni mwa wanandoa huharibu
umoja wao. Mwanandoa amchae Mungu, hubeba tabia zote za Mungu, hivyo, kunasababu
nyingi za kusamehe na kusameheana, na baadhi ya sababu hizo ni zifuatazo:

Kusamehe ni tabia ya Mungu, na mwadamu ni mfano wa Mungu:


Mwanadamu mwanandoa ameumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26).
Mwanadamu amchae Mungu kwa kweli na dhati yote, lazima awe na tabia ya Mungu kwa
maana Mungu ni kielelezo cha kwanza kwa mwanadamu (Isaya 43:25. Isaya 1:18, 1Yohana
1:9).
Kusamehe ni hali ya Upendo:
Kama ilivyo tunda la roho ni upendo, vivyo hivyo kusamehe ni tunda la upendo
(1Wakorintho 13:4-7). Haina haja wala sababu ya mwanandoa mwenye roho ya upendo
kumuwazia mwenzi wake au mtu ye yote vibaya na kumchukia kwa sababu amemkosea na
kumtendea vibaya. Tabia ya mtu amchae Mungu ni upendo kwa wengine hata kama
atakwazwa.
Kwa kuwa Mungu ni pendo, mwanadamu pia yampasa awe na upendo utokanao na
Mungu. Kusamehe ni ishara na kielelezo cha upendo, kwa hiyo, mtu anayesamehe
anakiwango kikubwa cha upendo hivyo, wanandoa yawapasa kuiga na kujifunza upendo wa
Mungu ili amani itawale katika familia zao (Yohana 3:16. 1Yohana 4:8. Yeremia 29:11).

Ni kufanya kama Mungu anavyowasamehe wanandoa:


Kama Mungu anavyomsamehe mwanadamu (mtu mmoja miongoni mwa wanandoa au
wote) bila kuchoka, mwanandoa pia yampasa kusamehe wengine akiwemo mwanandoa
mwenzie vivyohivyo (Yohana 1:12-13. 1Petro 1:4).

Hakuna mwanadamu aliyemkamilifu asilimia mia:


Ye yote miongoni mwa wanandoa akijua kuwa hakuna aliyemkamilifu asilimia zote,
basi atakuwa anajua nini maana ya kutoa msamaha kwa mwenzi wake. Mwanadamu ye yote
hukosea na kukosewa pia. Haina maana wala haja kwa wanandoa kutazama mazuri pekee na
kuyafurahia, bali yale mabaya yasiweze kusameheka! Sio vizuri mwanandoa kujihesabia haki
kuliko mwingine; maana hata yeye akikosea ana hitaji kusamehewa pia. (Warumi 3:10.
Warumi 3:23. Marko 11:25-26).

Kusamehe kunaepusha kujengeka kwa mawazo ya kulipiza kisasi:


Mwanandoa asipojenga tabia ya kusamehe, hujenga mawazo ya kisasi pale anapozidi
kumchukia mwenzi wake. Kufikiria, kutosamehe na kuwaza jambo baya juu ya mtu
mwingine ni sawa na yule aliyetenda kwa vitendo. Kuendelea kumchukia mtu ni kutotoa
nafasi ya kumsamehe huyo mtu, hivyo dhambi yake ni sawa na aliyeua. Kutomsamehe

Frank Philemon Karoli


101
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

mwenzi katika ndoa kunajenga hali ya kulipa kisasi, maana kisasi ni kulipa baya kwa jinsi yo
yote ile kwa mtu aliyekukosea (Warumi 12:19; Yakobo 4: 12).

Kuepuka magonjwa ya kisaikolojia:


Kusameheana miongoni mwa wanandoa, kunasaidia kuepuka magonjwa ya
kisaikolojia kwa sababu ya hisia na mtazamo mbaya juu ya mwingine; maana kuweka jambo
moyoni bila kulifuta hujenga chuki ya moja kwa moja, hivyo, kunaweza kusababisha
misongo ya mawazo, kichwa kuuma, magonjwa ya moyo, presha pamoja na magonjwa
mengine.

Ili kuepuka kutenda dhambi:


Kutomsamehe mtu ni kujichumia dhambi itokanayo na kumuwazia vibaya, hivyo
wanandoa kuchukiana bila kutoa fursa ya kusamehe ni kujichumia dhambi ya maauji maana
kuuwa huanzia katika fikra na hatimae kutenda huwa ni utekelezaji tu. Kusameheana
miongoni mwa wanandoa kunaweza kukawauepusha katika kujichumia dhambi, hivyo,
kutompa nafasi Shetani kuweka makazi katika familia au ndoa.

Ni kuonesha hali ya unyenyekevu:


Tabia ya kusameheana kwa wanandoa ni kiwango kikubwa cha kiroho hususani
kuonesha hali ya unyenyekevu. Mtu asiyesamehe hukosa tabia ya Kristo ile ya kuwa
mnyenyekevu kwa wengine, hivyo, wanandoa yawapasa kuivaa tabia ya Kristo ya
unyenyekevu (Sefania 2:3; Waefeso 4:2-3; Wafilipi 2:3; Mithali 16:19 na Mithali 22:4).

Hurejesha mahusiano mema:


Kusameheana hurejesha mahusiano mema yaliyokuwa yamevunjiaka miongoni mwa
wanandoa. Tendo la kusameheana pia linamanufaa hata kwa watu wengine walio nje ya
familia endapo wanandoa waliokosana na watu wengine walio nje ya familia yao.

Madhara ya Kutosamehe Yanayoweza Kuwapata Wanandoa na Watu Baki.


Tabia ya kutoweza kusameheana au kutokukubali kusamehe kwa wanandoa wanaweza
wakapatwa na madhara yafuatayo:
Kutokusamehe Kunapelekea Kujitenga na Uwepo wa Mungu: Roho Mtakatifu
hawezi kukaa mahali palipo na machafuko au Mungu hawezi akashikamana na mdhambi
ambaye anawaza maovu bila kutubu. Kutosameheana kwa wanandoa huondoa uwepo wa
Mungu katika ndoa na familia (Warumi 12:17, 21).
Kutokusamehe Husababisha Kutokea kwa Majaribu Mengine Zaidi: Mtu
asiyesamehe hufungua njia ya majaribu mengine kumwandama, maana mkono wa Mungu
unapotoweka sheteni huweka makazi ili kuzidi kumpoteza huyo mtu. Kwa wanandoa
kutosameheana kwa kunaweza kukasababisha kujeruhiana kwa kupigana, kulipizana visasi au
kutengana kwa kuvunja ndoa (Mithali 17:13).
Kutokusamehe Hupelekea Kutenda Dhambi ya Mauaji: Kumuwazia mabaya
miongoni mwa wanandoa, hujenga hali ya kisasi hivyo, husababsha kutenda dhambi ya
mauaji maana dhambi hutendeka katika fikra au moyoni. Kwa hiyo, kufikiria ni sehemu tu ya
mpango wa kutenda. Wanandoa kuchukiana bila kusameheana ni kuvunja amri ya Mungu

Frank Philemon Karoli


102
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

inayokataza kuua hivyo hutenda dhambi (1Yohana 3:15, 1Yohana 3:11-12, Mathayo 5:21-
22.)
Kutosamehe Huongeza Maadui na Uadui: Kutosamehe kunakopelekea kulipa kisasi
huongeza maaudui na uadui miongoni mwa wanandoa pamoja na watu baki. Kulipa baya kwa
baya huwa hakuleti suluhu juu ya migogoro katika ndoa au jamii, bali huongeza uadui na
maadui kwa sababu ya kukosekana kwa upande au mtu anaye weza kujishusha katika, hivyo,
kulipizana mabaya hufanyika kwa ushindani wa kila upande.

Uhitaji na Umuhimu wa Wanandoa Kusameheana


Tunaweza kupatanishwa na mtu mtu fulani ambaye ametukosea, kwa vile Kristo
alitupatanisha Kwake Mwenyewe tulipomkosea. Tunaweza kusamehe kwa sababu
tumesamehewa. Tunaweza kupenda kwa sababu tumependwa. Msamaha ni uchaguzi.
Tunaweza kuchagua kusamehe licha ya matendo au mienendo ya mtu mwingine.
Kusameheana miongoni mwa wanandoa ni muhimu na inawezekana kama wanandoa
watakuwa wamekuwa kiroho (kukua katika Kristo). Ili kusameheana kuwe rahisi miongoni
mwa wanandoa yampasa wajue, kufuata, kufanya na kuyaishi mambo yafuatayo:
Wjue kuwa wao ni watoto wa Mungu, hivyo, yawapasa kusameheana na kufuta
makosa kama Mungu anavyowasmehe wanadamu na kufuta makosa yao (1Petro 1:18-19).
Wajitahidi kuwaombea mema na kuwapenda maadui zao siku zote na siyo kuwalipa
baya kwa baya (Mathayo 5:44-45), hivyo wawazie mema maadui zao siku zote (Warumi
12:20-21).
Watambue ya kuwa, wao siyo wenye kujipigania, bali Mungu ndiye huwapigania
walio wake. Hivyo, vita si vyao bali ni vya Mungu mwenyewe na mwanadamu yampasa
kumkabidhi Mungu vita yake (Ayubu 19:25, 2Nyakati 20:15).
Mwanandoa atambue kuwa, vita vyake si juu ya damu na nyama, bali vita yake ni ya
kiroho zaidi maana pambano kuu bado linaendelea kati ya wema na ubaya yaani vita kati ya
Shetani na Kristo (Waebrania 12:2-3, Wagalatia 4:7). Hivyo,wajue kuwa, si mtu amkoseae
bali ni Shetani anamtumia mwanadamu (mwenzi) kutenda yaliyo maudhi juu yake.

Jinsi ya Kufanya Ili Kuleta Amani (Kupatana) kwa Wanandoa.


Kukosana, kukwazana na kutendeana mabaya huzaa migogoro na chuki. Kukosana
kwa wanandoa kupo katika namna ya makundi yafuatayo: 1. Mtenda kosa hajui na mtendewa
kosa hajui (japo ipo siku mmoja au wote watakuja kujua kuwa alitenda au alitendewa kosa);
2. Mkosaji anajua kuwa ametenda kosa halafu mkosewaji hajui kuwa amekosewa; 3. Mkosaji
(mtenda kosa) hajui kuwa ametenda kosa bali mkosewaji (aliyetendewa kosa) anajua kuwa
amekosewa na 4. mwisho kabisa, Mtenda kosa anajua kuwa ametenda kosa na mtendewa
kosa anajua kuwa ametendewa kosa.
Zipo sababu nyingi zinazosababisha kutokea kwa migogoro na kutengeneza uadui
miongoni mwa wanandoa. Yapo makundi yanayosababisha kutokea kwa migogoro izalishayo
uadui, nayo ni 1. Migogoro ya kiuchumi katika ndoa na familia, 2. Migogoro ya kiutawala
katika ndoa na familia, 3. Migogoro ya kiimani (kutokana na utofauti wa imani au dhehebu)
katika ndoa na familia, 4. Migogoro ya kimitazamo au fikira katika ndoa na familia 5.
Migogoro ya kimahusiano (hasa yanapokuwa siyo mazuri) miongoni mwa wanandoa na

Frank Philemon Karoli


103
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

familia, na 6. Migogoro ya kimila na destu ri miongoni mwa wanandoa na familia (kama


hawatafuata mila na desturi ya Kristo).
Katika kanuni ya kutafuta amani ni mchakato ambao unahitaji kupatana au kutoa
suluhu ili amani ipatikane miongoni mwa pande mbili (wanandoa). Kanuni na taratibu za
kutafuta amani, zinahusisha kuonana ana kwa ana kwa pande mbili ili kupatana na kurejesha
amani iliyokuwa imepotea. Kama aliyefuatwa atakataa kupatana hatua zingine zitafuata kama
ilivyoelekezwa katika Mathayo 18:15-20.

Je, ni nani wa kumfuata mwingine ili kupatana na kurejesha amani na upendo?


Ni ye yote yule miongoni mwa wanandoa atakayekuwa wa kwanza kufahamu kuwa
amemkosea au amekosewa. Aidha, wakati huohuo au baadae kwa muda kitambo, basi
aliyewahi kugundua kabla ya mwenzake, yampasa aende kumuona aliyemkosea bila kujali
nani mkosaji au mkosewaji.
Zipo nyakati ambapo jitihada zote za kusuluhisha tatizo hazifanyi kazi. Katika hali
hii, Yesu anatuelekeza kuleta suala hilo kanisani (baraza la kanisa) endapo hatua mbili za
kwanza za Mathayo 18 hazijasaidia kupatanisha pande hizo mbili, japo kusudi ni lile lile la
kuleta mafanikio na sikuegemea upande wo wote.
“Usiruhusu uchungu ukomae na kuwa nia mbaya ya kudhuru. Usilipatie nafasi jeraha
litunge usaha na kupasuka katika maeneo yenye sumu, yanayochafua akili za wale
wanaosikia. Usiruhusu mawazo ya uchungu yaendelee kujaza akili yako na yake kukusiana
na suala hilo”. – Ellen G. White, Gospel Workers, uk 499.

Frank Philemon Karoli


104
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

= SURA YA 15 =

UWAKILI WA MUDA KATIKA NDOA NA FAMILIA YA KIKRISTO.

“Nitayakumbuka matendo ya BWANA; Naam, nitakumbuka maajabu yako


ya kale. Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako.

Zaburi 77:11-12

Jambo lingine la kutambua na kuliishi miongoni mwa wanandoa ni juu ya kuwa


mawakili au watumiaji wazuri wa muda wa Mungu. Uwakili wa muda ni miongo mwa aina
sita za uwakili ambazo ni: 1. Uwakili wa mwili (1Wakorintho 3:16-17), 2. Uwakili wa talanta
(Mathayo 25:14-29), 3. Uwakili wa wakati (1Petro 1:17), 4. Uwakili wa mali (Zaburi 24:1),
5. Uwakili wa mvuto (Warumi 14:21) na 6. Uwakili wa kujali au kuhusika (Luka 10:33).
Wanandoa yawapasa kumpatia Mungu muda wa kutosha katika kuwa nae kwa namna
au jinsi yo yote kama Paulo anavyoelezea katika Waefeso 5:15-21 kuwa: “Basi angalieni
sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
mkiukomboa wakati kwa maana zama hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali
mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya bwana. Tena msilewe Kwa mvinyo, ambamo mnaufisadi;
Bali mjazwe Roho; mkisemezana Kwa zaburi Na tenzi na nyimo za rohoni, huku mkiimba na
kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo
yote, katika jina lake Bwana Yesu Kristo; hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.
Pia kwaya ya “Ambassador of Christ” kutoka Rwanda (mjini Kigali) wao nao
wameusisitizia ulimwengu katika kutenga muda kwa ajili ya kumuomba BWANA katika
wimbo wao waliouimba ambao ni miongoni mwa Nyimbo za Kristo (Kesheni Kaombeni
(Watch For The Time is Short)) kilicho na beti zifuatazo:

1. Kesha ukaombe panapo nafasi; Wakati si mwingi. Kwa vile ukeshe,


Mwili ni dhaifu adui hodari karibu atakuja, Bwana wa arusi.

Kesha, Omba, Kesha, Omba,


Kesha Kaombe gizani, Mchana,
Daima Kesha.

2. Fukuza usingizi, fukuza mashaka; Ahadi ni yako, raha ya milele,


Bwana alikesha kwa ajili yako; Jasho yake ikawa matone ya damu.

3. Yesu umkubali awe nguvu zako; silaha uzivae; adui karibu,


Sasa nafasi iko, isipite bure; Bila kukawia masihiya kesha.

Frank Philemon Karoli


105
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Muktadha mkuu wa Waefeso 5:15-21 ni juu ya kuukomboa wakati kwa ajili ya


Mungu. Mtume Paulo anawaandikia Waefeso (Wakristo) juu ya kuukomboa wakati, akijua
ya kuwa hata yeye alikuwa mhanga katika kuupoteza muda wake huko mwanzo kwa kutenda
yasiyofaa mbele za Mungu. Hivyo, anasisitiza sana juu ya kuukomboa wakati katika wokovu
wa Mkristo kwani Wenye hekima huukomboa wakati kwa kutenda mema, bali wajinga na
wapumbavu hutenda maovu.
Wenye hekima walio na akili hutenga muda wao kwa ajili ya kumtukuza Mungu hasa
katika kuimba, kusemezana kwa zaburi, tenzi, nyimbo za rohoni, kumshukuru Mungu,
Kumshangilia Bwana moyoni mwao na kunyenyekeana wao kwa wao katika Kristo ili
wajazwe Roho Mtakatifu. Lakini waovu na wapumbavu hulewa mvinyo (aidha, mafundisho
mapotofu na mienendo mibaya ya dunia), kufanya kila aina ya ufisadi na ufusika; ni msisitizo
wa Paulo kwa Wakristo wote na si kwa Waefeso pekee.
Baada ya Mungu kuumba dunia alianza na muda kabla ya kuendelea na hatua zingine
za uumbaji katika siku zake zote za uumbaji (Mwanzo 1:3-4) ili kufanikisha uwekaji wa
nyakati au majira kwa ajili kumuwekea kumbukumbu sahihi mwanadamu hapo badae. Hivyo,
wanadamu hatuwezi kuutenganisha muda na uumbaji pamoja na ibada zetu kwa Mungu
aliyetuumba (wakiwemo gwanandoa). Katika nuru, yaani mwanga ambao hufanya mchana
pamoja na giza ambalo hufanya usiku uliwapatia fursa wanadamu kujua kuhesabu masaa,
siku, majuma, miezi na miaka.
Biblia ambamo limo neno lake Mungu, limeandikwa kwa kuzingatia wakati aidha,
jambo lilitokea, limetimia na litatokea. Muda wote ni wa Mungu, hivyo, Mungu kutupatia
muda (wakati), alikuwa na makusudi makubwa juu ya mwanadamu kuweza kuutunza muda
kwa kumwabudu na kumtukuza Yeye; kwa makusu hayo, kila mwanadamu akiwemo na
mwanando ni wakili wa muda wa Mungu.
Maswali mawili ya kujiuliza kwa wanandoa: Je, ni mawakili waaminifu wa muda wa
Mungu aliowapatia? Je, wanandoa hamtendi dhambi kwa kuiba muda wa Mungu?
Wanandoa kuhodhi muda wote wa Mungu kwa kufanya mambo yao binafsi pekee ni
kinyume na uanzishwaji wa muda kama yalivyokuwa na yalivyo makusudi ya Mungu. Ni
vyema wanando wakatenga muda maalumu kwa ajili ya kumwabudu, kumtukuza na
kumtumikia Mungu. Hivyo basi, wanandoa yawapasa kumpa Mungu muda wa kutosha katika
kufanya ibada, kushiriki kueneza injili na kuwashuhudia wengine ukuu wa Mungu.

Muda katika Mambo ya Kiroho


Muda ni miongoni mwa aina sita za uwakili kama tulivyoona hapo awali. Muda
unasehemu kubwa katika wokovu wetu, maana unaashiria mambo yafuatayo:
a) Wakati unaweka bayana kukombolewa kwetu katika dhambi.
b) Wakati unaonesha kikomo chetu cha rehema.
c) Wakati unabainisha kutumika kwetu kwa Mungu.
d) Wakati unapima ukomavu na ukuaji wetu wa kiroho.
e) Unatuelekeza kutimiliza mpangilio wa maagizo ya Mungu,
f) Wakati unatudhihirishia nini tufanye na kipi tusifanye katika wakati mahususi unaofaa
na usiofaa.

Frank Philemon Karoli


106
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

g) Wakati unatutanabaisha mambo yaliyopita katika yanayotufunza, yaliyopo na yajayo


ili yatimie katika unabii.
h) Wakati ni kumbukumbu kwenye hatima ya hukumu; maana kila jambo na kila tendo
kwa wakati lilipotendeka litaletwa hukumuni.

Wanandoa Kuwanaye Bwana Kila Muda


Muda kwa wanandoa ni zawadi ya thamani sana ambayo Mungu amewapatia kwa
makusudi ya kumsifu, kumtukuza na kumtumainia Yeye. Muda ni mali, muda sio rafiki
unapochelewa kutimiliza jambo, muda ni mstari hivyo wanandoa ni vyema kuwa nao
makini sana kwa ajili ya wokovu wao.
Mwanandoa Mkristo asiyetunza au kuutumia vizuri muda katika kuweka mahusiano
yake vyema na Mungu anajitengenezea mazingira ya kutokuwa wakili mwaminifu kwa
kumwibia Mungu muda Wake.

Madhumuni ya Mungu Kumpatia Muda Mwanadamu:


Ili Kila Mwanadamu Awajibike Kwake Yeye: Waefeso 5:16 “mkiukomboa wakati
kwa maana zama hizi ni za uovu”
Tuyafuate Maelekezo Yake Mungu: Waefeso 5:8 “Kwa maana zamani ninyi mlikuwa
giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru”
Tupange Ratiba kwa Ajili Yake Mungu: Zaburi 55:16-17 “Nami nitamwita Mungu,
Na Bwana ataniokoa; Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye atasikia sauti
yangu”
Tuwe Katika Utaratibu Sahihi: Kutoka 40:1-16 “…...16Musa akafanya hayo yote;
kama yote Bwana aliyoagiza ndivyo alivyofanya”
Tujikite Katika Hekima Yake: Zaburi 90:12 “Basi utujulishe kuzihesabu siku zetu,
Tujipatie moyo wa hekima”
Tuutafute Ufalme Wake: Mathew 25:34-35 “Kisha Mfalme atawambia wale walioko
mkono wake wa kuume, Njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa
tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa
na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha”
Atuponye na Maovu Katika Nyakati Zote: Zaburi 31:15 “Nyakati zangu zimo
mikononi mwako; Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia”
Kuwashuhudia na Kuwahubiri Wasio Mjua: Yohana 9:4 “Imetupasa kuzifanya kazi
zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana; usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi”.
Tuyajue Mazingira na Hari Yake: Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake,
na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu” (waweza soma hadi fungu la 8).
Tukumbuke Kuzishika Amri Zake: Mungu ameweka agano lake na wanadamu
ambazo ndizo sharia zake zinazomuongoza binadamu kuwa mwenye haki (Soma Kutoka
20:8-11; Kutoka 20:12).
Tuepuke Kufikiwa na Kikomo cha Rehema: Mhubiri 12:1-2 “Mkumbuke Mungu
wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala hazijakaribia miaka
utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo. Kabla jua, Na nuru, Na mwezi, Na nyota,
havijatiwa Giza; ………”

Frank Philemon Karoli


107
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

Namna ambavyo Wanandoa Wanamwibia Muda Mungu:


Kwa kufanya mambo maovu na uasi wa sheria: 1Yohana 3:4 “Kila atendaye
dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi”
Kwa kutumia muda mwingi kujiwekea akiba duniani: Mathayo 6:19-21
“Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; Bali
jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji
wala hawaibi; Kwa kuwa hazina ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako”.
Kutokufanya kazi yake Mungu ya utume: Mathayo 28:19-20 “Basi, enendeni,
mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na
Roho Mtakatifu; Na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi
nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa hadari”.
Kuwa na kiburi cha uzima na matumaini binafsi: Yakobo 4:13-14 “Haya basi, ninyi
msemao, leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya
biashara na kupata faida; Walakini hamjui yatakayokuwako kesho”.

Namna Nzuri Ambayo Wanandoa Wanaweza Wakautunza Muda wa Mungu:


Wayape kipaumbele yaliyo maagizo ya Mungu: Zaburi119:6 “Ndipo mimi sitaaibika,
Nikiyaangalia maagizo yako yote”.
Muda wa ibada na huduma uwe kipaumbele kwao: Isaya 55:6 “Mtafute Bwana,
Maadam anapatikana, Mwiteni, maadam yu karibu”
Watumie muda wao wa starehe na burudani kwa ajili mambo ya kiroho zaidi: Luka
4:4 “Yesu akamjibu, imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu”
Waandae, kutambua na kufuata ratiba yao kwa ajili ya Mungu: Kutoka 34:21
“Utafanya kazi siku sita, lakini katika siku ya saba utapumuzika; wakati wa kulima
mashamba, na wakati wa kuvuna pia, utapumzika”, Warumi 13:11 “Naam, tukiujua wakati,
kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u-
karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini”

Jambo la msingi: Wanandoa watumie kanuni ya GA-PA-E-TU-FA-FU-VI pale


wanapoona ratiba au muda wao na Mungu hawautekelezi kama ilivyo bainishwa kwenye
hatua zifuatazo:

Frank Philemon Karoli


108
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

GA = Gawanya na anza kufanya kile unachopaswa


kukifanya kwa kila muda/siku.
PA = Panga vitu vyako kwa jinsi utakavyovifanya kwa siku
nzima.
E = Epuka mwingiliano wa mambo katika ratiba yako kati
ya wewe na Mungu.
TU = Tumia muda katika ratiba yako kwa kujifunza na
kumtafakari Mungu peke yako.
FA = Fanya sasa, na sio kesho kwa kuitii ratiba yako
pamoja na Mungu.
FU = Fursa inapojitokeza tumia kama mojawapo ya faida
ya kuwa karibu na Mungu
VI = Vijue vitu au mambo yanayo kuchukulia muda wako
na Mungu ili uviepuke daima.

Mtumishi wa Mungu, Daudi alijua makusudi ya Mungu kuweka muda na katika


Zaburi 90:12 anasema: “Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima”
na katika Zaburi 39:4 Daudi anasihi: “BWANA, unijulishe mwisho wangu, na kiasi cha siku
zangu ni kiasi gani ..........”.
Mungu alipanga mpango wa wokovu, na wakati ulipotimia ikawa: Wagalatia 4:4
inasema: “Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma mwanawe ambaye
amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa
wana”. Hivyo basi, baada ya muda mfupi Yesu kufa msalabani:
Sadaka ya kuteketeza kwa ajili ya ondoleo la dhambi ikakoma maana Yesu
alisimama badala yake).
Sadaka ya upatanisho kwa ajili ya kulejesha amani ikakoma, Yesu akawa mbadala
maana ndiye mpatanishi katia dhambi za wanadamu.
Pasaka ya ukombozi wa Israeli toka utumwani ikakoma; meza ya Bwana ikaanza
kama pasaka ya kukumbuka kifo chake Yesu Kristo pale msalabani katika kumkombozi
mwanadamu.
Huduma ya upatanisho katika hekalu la duniani ikakoma maana huduma ya
ukuhani duniani ilikoma; Yesu akaendelea nayo huko mbinguni kama kuhani mkuu
akituombe na akifanya upatanisho kati ya mwanadamu na Mungu.
Sabato (masabato) na miandamo ya miezi iliyotumika kama kumbukumbu za
kuwakumbusha wanadamu katika kumcha Mungu na kutenda mambo mema
ikakomeshwa maana sasa yupo Roho Mtakatifu anayewakumbusha wanadamu kutenda
mema na haki yote ya Mungu.

Frank Philemon Karoli


109
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

HITIMISHO

“Neno linenwalo wakati wa kufaa. Ni kama machungwa katika


vyano vya fedha”

Mithali 25:11
Ndoa ni sawa na maisha, ambayo hutupa changamoto ili kupima ujasiri wetu na
utayari wetu wa kubadilika. Katika muda huo, hakuna nafasi ya kujifanya kwamba hakuna
linalotokea au kusema kuwa hauko tayari kuipokea hiyo changamoto; maana changamoto za
ndoa hazisubiri utayari wa mwanandoa. Ndoa ni maisha uliyoyaanza ambayo hayaangalii
nyuma, ni kama sheria mpya inayotungwa juu ya jambo fulani, huwa inaanzia pale
iliposainiwa.
Ili uwe huru pale unapoamua kuingia katika kifungo cha ndoa, lazima ujifunze
kusamehe na kusahau na kuacha mambo mengine yapite. Acha kuhusika na mambo
madogomadogo katika maisha ya ndoa bali acha yaende kwa kusamehe na kusahau. Tupa
woga unapoamua kuzikabili changamoto za ndoa, acha kuzisumbukia kumbukumbu za
nyuma juu ya nini kilitokea katika magumu ya ndoa. Kubali kuanza upya ili kuijenga
thamani ya ndoa aliyokupatia Mungu.
Kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa. Kanuni ya mafanikio katika maisha ya
ndoa ni sawa na jambo lo lote binadamu afanyalo ambalo huwa ni kuwa na mpango thabiti
unaoelekeza ni wapi mwanandoa anataka kufika na kwa kiwango gani. Mipango ya
mafanikio yetu katika ndoa hupangwa na vichwa vyetu pamoja na fikra tulivu zinazotawala
mioyo yetu huku tukiomba msaada toka kwa Mungu. Tukiwa na mipango, kinachofuatia ni
mikakati; hii huwa ni njia ya utekelezaji wa mipango yetu ndani ya ndoa.
Ukijua uendako katika ndoa ni rahisi sana kupata njia sahihi ya kukufikisha; hata kama
utachelewa kiasi gani, lakini uhakika wa kufika unao. Yaweza kuwa ulichelewa sana katika
kumpata mwenzi sahihi au kuingia katika ndoa, bali, jua ya kuwa, nafasi ya kuyafikia
malengo uwapo ndani ya ndoa bado unayo maana maisha ya ndoa hayakuhitaji uwe na elimu
kubwa sana ili ufanikiwe, bali kinachotakiwa ni kujitambua, kuweka mipango iliyo na
mikakati mizuri yenye vipaumbele, kujiamini na kusimamia unayo yaamini sambamba na
mapenzi ya Mungu.
Uwapo katika ndoa, kumbuka kuwahudumia na kuwalisha watoto wote bila ubaguzi
maana wote ni watoto wako na wana haki sawa katika kuyapata mahitaji yao. Kumjua mtu au
kutokumjua hakukupi sababu ya kumdharau au japo kumuamini sana; hivyo, watoto ambao
BWANA atakupatia uwapo katika ndoa jitahidi kuwafundisha kuto wadharau watu juu ya
kile wazazi au wao walichonacho ambacho huyo mtu hana, bali wajue kuwa kila mtu ni
muhimu kwao na ni muda tu haujafika au Mungu hajapanga wala hawajamkosea.
Ukiwa na Yesu utayaweza mambo yote yaliyo katika ndoa bila kujali kuwa umetoka
kwenye familia ya aina gani na wala haijalishi maisha yako ya zamani yalikuwaje kabla ya
sasa (soma Wafilipi 4:13). Uamuzi wako utakaoufanya sasa juu ya nini unataka kukitilia
mkazo na nini maana ya vitu fulani kwako katika ndoa, aina ya mafanikio uyatakayo na jinsi

Frank Philemon Karoli


110
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

ambavyo utafanya ili kuyafikia ndicho kitakachokupa mwanga wa mtu wa aina gani utakuwa
hapo badaye katika ndoa na familia yako.
Kila kitu duniani chenye mafanikio kilianzishwa na mtu fulani, ndivyo hata katika
familia, wazo laweza kuwa kichwani mwa mmoja wa wanandoa na yeye atakapomshirikisha
mwenzi wake atahesabika kuwa yeye ndiye aliyeleta jambo hilo japo ustawi wa familia
utakaopatikana ni manufaa ya wote katika ndoa. Kila mtu mwenye mafanikio alikuwa na
ndoto kabla, akazichambua ndoto zake na kuziishi huku akifanya kila njia kuzileta kwenye
uhalisia kwa kushirikisha wengine, hivyo, mwanandoa mmoja mmoja ananafasi ya kuifikisha
familia yake pale atakapo kama wote wawili watamshirikisha Mungu kwa kila hitaji na lengo
lao.
Kifo ni hatua ya mwisho ya muda wa binadamu katika dunia; haijarishi ni muda gani
utachukua kuwa hapa duniani ila jua tu kwamba ipo siku na wewe utakufa. Cha kujiuliza ni
kitu gani katika maisha ya uhai kitakacho kutambulisha baada ya kifo chako. Ni kitu gani
kitakufanya usimame ukiwa mwenye haki mbele za Muumba wako utakapokuwa ukifanyiwa
hesabu ya matendo yako ya imani katika siku ya hukumu? Hivyo, kufa hakuhitaji uwe
mgonjwa au upate ajali, ili ufe inahitajika siku yako iwe imefika.
Watu waliofanikiwa zaidi katika ndoa zao ni wale walioyajua matatizo, waliozijua
harakati za maisha na ndoa zao, waliokumbana na misukosuko na taabu, waliokutana na
majaribu bila kukata tamaa, lakini mwisho wa siku waliyakabili na kusonga mbele. Lo lote
ambalo haliwezekani leo, unaweza kulifanya liwezekane kesho, kama tu utaamua juu ya
mustakabali wa njia uipitayo huku ukimwalika Yesu atembee katika ustawi wa familia yako.
Umaskini wa fikra ni mbaya zaidi kuliko umasikini wa kipato. Fikra sahihi kwa wakati
sahihi ndio njia ya kupata suluhu ya kila limfikalo mwanandoa. Hekima ya kweli ni kumjua
Mungu ili uwe mwenye haki mbele zake; lakini upumbavu ni kuyajua yote ya dunia na raha
zake za kitambo kisha mwisho wa ulimwengu unadharauliwa milele huku ukilipwa ujira
wako sambamba na uliyo yatenda. Walee watoto katika hekima ya kumjua Mungu na siyo
hekima za kiduni ambazo haziwavushi ng‟ambo ya kaburi. Fanya sehemu yako kama mzazi
ili usije ukadaiwa kondoo wa nyumbani mwako ambao BWANA alikupatia nafasi ya
kuwalea na kuwatunza katika misingi inayostahili ili waurithi uzima wa milele.
Si vyema ukajisahau na kurizika kama bado hujafanikiwa kuurithi uzima wa milele.
Pamoja na familia yako, panga namna ya kuyakabili mashambulizi ya Shetani kwa kuwa
yeye ameshapanga namna ya kukukabili toka mwanzo wa uasi wake. Jiulize, kwa nini
unahali ile ile ya kiroho iliyo chini ya kiwango. Jiulize ulivyokuwa mwaka jana na ulivyo
mwaka huu upo sawa, au umepungua zaidi kwa sababu ya kuheshimu sanamu za maisha
kuliko Mungu. Je, kwanini hakuna tofauti ya mafanikio yako ya kiroho japo kuna ongezeko
la umri katika ndoa? Gundua kipaji chako, taranta na karama (kipawa chako) yako na uitumie
kwa ajili ya kazi ya Mungu. Elimu yako si kitu pia kama haina mchango katika kazi ya
BWANA hapa duniani.
Upendo wetu juu ya wengine hutufumba macho na kutufanya tusahau kuwa tuna
jukumu la kujitazama wenyewe pia, pale wengine wanaposhindwa kujali hisia na majonzi
yetu. Bwana atutie nguvu, hekima, uwezo, maarifa na upendo uliojengwa kuto kwake. Yesu
aponye ndoa zetu ili ziwe mbingu ndogo hapa duniani. Yesu atamalaki na kuzulu familia zetu
huku akizilinda na kuziepusha na mishale ya Shetani mwenye uhitaji wa ajabu katika
kuiangamiza tasisi ya ndoa.

Frank Philemon Karoli


111
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

REJEA

Adei, S: (2003). A Desertation about African Traditional Marriage and Biblical


Patterns the Case of Ashantis Of Ghana: University Of South Africa.

Andrews, S,. & Little, B: (2000). Anatomy of Desire: The Science and Psychology of
Sex, Love and Marriage.

Allen, L.S., Richey, MF., Chai, Y.M. & Gorski, R.A: (1991). Sex differences in the
corpus callosum of the living human being, Journal of Neurosdence 11, 933-942.

Beatty, W.W: (1988). „A Fargo Map Test: A Standardized Method for Assessing
Remote Memory for Visuospatial Information’ Journal of Clinic Psychology 44, 61-
67.

Bailey, J.M. & Bell, A.P: (1995). Familiality of Female and Male: Cambrigde
University Press.

Daniel, G: (2000). Change Your Brain, Change Your Life: The Breakthrough
Program for Conquering Anxiety, Depression, Obsessiveness, Anger and
Implsiveness. Times Book.

DeAngelis, B: (1997). Sectrets About Men Every Women Should Know. New York:
Norton

Karoli, F. P: (2018). Urafiki na Uchumba Katika misingi ya Kikristo. Pita Njia


Salama Kuielekea Ndoa Yako. Dar es Salaam: Zedco Branding Centre.

Pease, A. & and Pease, B: (2001). Why Men Don’t Listen and Women Can’t Read
Maps: Great Britain. Orion Publishing Group.

United Bible Societies (1952). The Holy Bible Version in Kiswahili. Union Version:
Published as Biblia Mandiko Matakatifu. Dodoma: The Bible Society of Tanzania.

S.D.A: (2004). Nyimbo Za Kristo: Kitabu Kidogo. Morogoro: Tanzania Adventst


Press.

Vishala, M: (2006). Guidance and Counseling: For Techers, Parents and Students.
New Delhi: Schand & Company Ltd.

White, E. G: (2002). Kuchagua Mchumba. Morogoro: Tanzania Adventist Press.

White, E. G: (1980). The Adventist Home. Tailend and UK: The Estnaborougs Press
Ltd.

Frank Philemon Karoli


112
Uchumba na Ndoa Katika Misingi ya Kikristo

White, E. G: (1983). Letter To Young Lovers. E.Publication: Ellen G. White Estate


Inc.

White, E. G: (1970). Conflict and Courage. E. Publication: Ellen G. White Estate Inc.

White, E. G: (1913). Counsels To Parents, Teachers and Students. E.Publication:


Ellen G. White Estate Inc.

White, E. G: (1940). Councels On Stewardship. E. Publication: Ellen G. White Estate


Inc.

White, E. G: (1953). Child Guidance. E. Publication: Ellen G. White Estate Inc.

White, E. G: (1922). Christian Experience and Teachings Of Ellen G White.


E.Publication: Ellen G. White Estate Inc.

White, E. G: (1981). Peter’s Councel To Parents. Online Book Collection: Ellen G.


White Estate Inc.

White, E. G: (1989). Testimonies On Sexual Behavior, Adultery And Divorce. Online


Book Collection: Ellen G. White Estate Inc.

Frank Philemon Karoli


113

You might also like