You are on page 1of 12

MKRISTO NA POMBE

By Zakaria Ngereja on Wednesday, 6 July 2011 at 06:13 ·

"Hii Ni tafsiri isiyo rasmi (unofficial translation) ambayo nimeifanya kutoka kwenye mada
ya Kiingereza Kama ilivyochapishwa kwenye kijarida cha Inside Magazine cha shirika la
Amazingfacts, Inc."

Mkristo Na pombe 

Na Doug Batchelor

Ukweli WA kushangza: Vipimo vinaonyesha kwamba mara baada ya kunywa chupa tatu
za BIA, kuna wastani wa kupoteza kumbukumbu kwa asilimia 13 kwa kunywa kiasi
kidogo tu cha alkoholi, wapiga chapa (typists) waliofunzwa vyema walijaribiwa, na makosa
ya uchapaji wao yaliongezeka kwa asilimia 40. Mililita moja tu ya alkoholi inaongeza kwa
asilimia 10 muda unaohitajika kwa mtu kufanya uamuzi juu ya jambo lolote, inazuia
uitikio wa misuli mwilini kwa asilimia 17, inaongeza makosa kwa kutokuwa makini kwa
asilimia 35 na asilimia 60 kwa misuli kukosa ushirikiano – Paul Itawey.

Je, inaruhusiwa kibiblia Kwa mkristo kunywa pombe?

Ikiwa ndivyo, Kwa kiasi gani? Mada hii yenye utata imezua maoni mengi miongoni mwa
wakristo. Kwa nini? Je neno la Mungu (Biblia) liko kimya au halieleweki Kwa maana
iwayo yote kuhusu pombe?

Ninawasilisha hoja hapa. Biblia si isiyoeleweka au yenye utata inapozungumzia juu ya


pombe Na uhusiano wake Kwa wafuasi WA Mungu.

Kambi mbili zinazokinzana


 

Kuna kambi kuu mbili zenye fikra tofauti katika mada hii nyeti. Kundi la kwanza lina hoja
kwamba Yesu mwenyewe alikunywa mvingo (wine), Na Kwa kuwa mkristo Ni mfuasi WA
Yesu, pombe inawezaje kuzuiliwa? Na Kwa ujumla, wanaongeza hewa kidogo; ikiwa hivyo
ndivyo, “kunywa pombe kidogo tu na usilewe”.

Kuna kambi nyingine: Pombe Ni kilevi Na Ni dawa angamivu ambayo mkristo hapaswi
kutumia Kwa kiwango chochote kile.

Naam, kati ya kambi hizi zinazokinzana, kuna tofauiti nyingi tu za maoni, katika muda
huu mfupi, sitoweza kuelezea mpambanuo WA mawazo Kwa kutumia maandiko Na akili
ya kuzaliwa, nitajaribu kubakia katika kanuni muhimu.

Kwa uwazi, nitaeleza kuanzia mwanzo kwamba niko katika kambi ile ya pili! Ninaamini
kwamba rejea ya maandiko Kwa Yesu kutumia divai (mvinyo) Ni ile divai isiyotiwa chachu
yaani juisi ya zabibu (grape juice). Unapaswa pia unielewe, ninatoka katika upande
mwingine ambapo nilikulia katika mazingira ambayo mara Kwa mara nilikuwa nikinywa
mvinyo au BIA wakati WA chakula, wakati Fulani nilitengeneza pombe yangu mimi
mwenyewe.  Lakini sijawahi kuwa mlevi.

Alkoholi (kilevi katika pombe) ni nini?

Tuanze Kwa kutoa tafsiri. Kuna aina nyingi za mchanganyiko unaoitwa alkoholi
(alcohol).   Hata hivyo, si makosa kwamba yote hii imewekwa kwenye kundi la sumu Kwa
mwili WA binadamu.  Kilevi kinachopatikana kwenye vinywaji Kama BIA, mvinyo Na
Brandi (brandy) inaitwa kitaalam ethanol (C2H50H), kimiminika chenye kiwango
kikubwa cha mlipuko (highly flarmable liquid) Na tabia Na harufu ya ethanol.

Kinatokea nini unapokunywa aina hii ya kilevi? Kifo mara nyingi hutokea pale
msongamano WA ethanol kwenye mfumo WA damu inapozidi asilimia tano.  Hata Kwa
wale wasiotumia mara Kwa mara, badiliko la ghafla la kitabia hutokea, uwezo WA kuona
Na kufanya maamuzi, Na kutojitambua hutokea Kwa msongamano mdogo tu mwilini.

 
Hili Ni jambo la kustaabisha, siyo? Kwa hakika hii Ni athali ile ile ambayo madawa
haramu Kama heroin Na bangi, huleta Kwa watumiaji.  Nina shaka Kama kuna kanisa la
kikristo ambalo litaruhusu utumiaji WA madawa ya kulevya hata katika matukio ya
kijamii ya kufurahia.  Je, kuna sababu yoyote ya kuzuia pombe isijumuishwe katika
orodha ya madawa ya kuepukwa?

Aina mbili za mvinyo zinazozungumzwa kibiblia

Neno “mvinyo” katika nyakati za zamani za Biblia inamaana ya “mpya”, “njema”,


“nzuri”, juisi ya zabibu.  Katika nyakati zingine limetumika kumaanisha “iliyochoka” au
zao lililochacha lenye dawa ya alkoholi.  Watafsiri hawakuwahi kutumia neno “juisi ya
zabibu” katika maandishi ya kiebrania, waandishi hutumia maneno tofauti kutofautisha
aina hizi mbili. Neno la kiebrania “tyayin” lilitumika kuelezea mvinyo usiotiwa chachu, Na
yayin lilitumika Kwa mvinyo uliochachushwa, lakini kuna upekee WA aina Fulani (Isaya
16:10).  Hata hivyo, katika Agano Jipya, neno moja tu la kigriki linatumika kueleza aina
zote mbili iliyochachushwa Na juisi ya zabibu. Nalo Ni Oinis.  Lakini, hili lisiwe tatizo Kwa
kuelewa muktadha WA paragrafu, maana halisi itatokea. Mpaka hapo maandiko
yatakeposema “ya zamani” au “divai mpya” (Kama ilivyo katika Luka 5:37 –39),
muktadha utatuelezea aina ya divai inayoelezwa.

Mfano mmoja unatokea katika Marko 2:22 “wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika
viriba vikukuu, ikiwa atatia, ile divai mpya itavipasua viriba vile, divai ikamwagika, vile
viriba vikaharibika.  Bali hutia divai mpya katika viriba vipya”. Bila shaka, divai mpya
ndiyo aina isiyotiwa chachu.

Kwa kuongezea, kutoka katika Agano la kale, Isaya 65:8 tunasoma, “Bwana asema hivi,
Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, Na mtu mmoja husema, usikiharibu
Kwa maana mna Baraka ndani yake; ndivyo nitakavyotenda Kwa ajili ya watumishi
wangu, Ili nisiwaharibu wote”.

Sababu hafifu, maamuzi yasiyosahihi 

Maandiko yote yako wazi Na yako kinyume Na utumiaji WA kilevi, lakini asili ya
binadamu Ni kutafuta andiko lenye utata Kama “upenyo” WA kutetea unywaji WA
pombe.

 
Mfano WA sababu Kama hizi Ni harusi ya kana, pale Yesu alipobadili maji kuwa divai. 
Wanaounga mkono unywaji WA pombe wanasema hapa Yesu alitengeneza pombe, hii
ilikuwa harusi, Na kila harusi lazima pawe Na pombe; Lakini hapa tutulie tuone matokeo.
Kulikuwa Na mitungi sita ya kujazwa maji Na kila moja ingechukua galoni 20 hadi 30. 
Hiyo Ni Kama galoni 180 za kinywaji.

Je, tuamini kwamba Yesu alitengeneza galoni 180 za madawa angamivu ambayo
yangetosha kumfanya kila mnywaji katika harusi ile alewe Na kuvuruga harusi ile?
Hakika, angekuwa kinyume Na maneno yake mwenyewe (Habakuki 2:15, Luka 12:45,
waefeso 5:18)! Tukiliangalia andiko hili Ni lazima tufikie hitimisho kwamba Yesu
alitengeneza divai isiyotiwa chachu (juisi ya zabibu) Na mwendesha sherehe aliisifia Kwa
ubora wake (Yohan 2:4-10).

Vipi kuhusu chakula cha jioni?

Wengine wanadai kwamba Kama Yesu alikunywa mvinyo wakati WA chakula cha jioni,
Na hata kuitumia Kama ishara ya damu yake iliyotakaswa, sasa iweje kunywa mvinyo
hata kidogo iwe kosa? Hakuna mjadala kwamba Yesu alitumia mvinyo au divai wakati
WA chakula cha jioni, lakini Ni makosa kudhania kwamba mvinyo ule ulikuwa
uliochachushwa (pombe); Lakini fungu katika Mathayo liko wazi kabisa.

“Kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo Kwa ajili ya wengi kwa ondoleo
la dhambi.  Lakini nawaambieni, sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu WA mzabibu,
hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme WA Baba yangu”
(Mathayo 26:28-29). Kwa hakika, hapa Yesu ametumia divai mpya Kama kielelezo cha
angao lake jipya Kwa watu wake.  Yesu pia anaiita divai “tunda la mzabibu”.  Hata hivyo,
divai ikiisha pita mchakakato WA kuchachushwa (fermentation), si tena tunda la mzabibu
Kama maziwa ya mgando yalivyo zao la ng’ombe.

Zaidi Sana, tunatambua kwamba Pasaka haikupaswa kuwa Na aina yoyote ya chachu
(Kutoka 12:19). Uchachushwaji (fermentation) Ni mchakato sawa Na chachu! Ikiwa mkate
haukupashwa kutiwa chachu, ambayo Ni dhambi hivyo basi, twaweza kuwa Na hakika
kwamba mvinyo, kielezo cha damu ya Yesu, iliyotumika kwenye chakula cha jioni
isingekuwa Na sumu za pombe (Alcohol).  Kamilifu, damu ya Yesu isiyokuwa Na hatia
isinge wakilishwa Kwa njia ya uozo Na kutakasa mvinyo wa zamani (pombe).

Yesu alilinganisha mafundisho yake Safi Na ujumla wa divai mpya (Mathayo 9:17). Hivyo
basi, mafundisho yote ya uoza yamefananishwa Na mvinyo uliotiwa chachu WA Babeli! 
Babeli ilitambuliwa kama mahala “ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao
katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake” (Ufunuo 17:2).

Mfano mwingine “lakini Daniel aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa
chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa”(Daniel 1:8).

Ukweli wa kushangaza: mwaka 1869, Dr. Thomas Bramwell Welch, tabibu na daktari
bingwa wa meno, alifanikiwa kutengeneza mvinyo usiotiwa chachu kwa kuchemcha juisi
ya zabibu (pasturised concord grape joice) kwa ajili ya wana-parish wa kanisa lake la
Vineland, New Jersey.  Alivuviwa kufanya hivyo baada ya mgeni kulewa baada tu ya
kupata komunio ambayo mvinyo uliochachushwa ulitumiwa.  Tangu kale, pamekuwepo Na
njia nyingi za kuzuia mvinyo usichache, lakini pia ilipoteza ladha.  Mchakato WA Dr.
Welch ulitunza yote.  Leo hii, juice ya zababu ya Welch imekuwa Kampuni ya chakula ya
kimataifa.

Je Yesu alikuwa mlevi?

Mara Kwa mara mafarisayo walimshutumu Yesu Kwa kuwa mlevi na mlafi.  Walisema pia
alikuwa Na shetani Na alimkufuru Mungu, miongoni mwa mambo mengi.  Tunaelewa
Yesu hakuwa mlafi au mwenye pepo, wala mkufuru, sasa ikiwa mambo haya si ya kweli,
Kwa nini tudhanie Bwana wetu alikuwa mnywaji wa pombe kama walivyodai mafarisayo,
kundi la wapinzani wa Yesu walijulikana sana kwa uaminifu wao wa shutuma?

Walikuwa wakilinganisha maisha yake na ya Yohana mbatizaji mnazareti aliyejitenga


mbali na matumizi ya kila mvinyo na alikula nzige na asali ya mwituni (Hesabu 6:3;
Mathayo 3:4; Marko 2:7; Luka 7.33-34, 1:15; Yohana 8:48-52).

Yesu alipoangikwa msalabani, askari WA kiruni walimletea mvinyo ulichanganywa na


nyongo. Lakini, mara moja Yesu alipoonja ladha yake Na kutambua kuwa ilikuwa imetiwa
chachu, aliikataa.  Ikiwa Yesu alikataa kinywaji hiki licha ya kuwa mwili wake ulikuwa
umeteseka Sana Kwa kiu isiyokuwa ya kawaida, Kwa nini hakunywa mvinyo (Mathayo
27:34)?

Na tukienda kwenye mada yetu Kwa nini sisi tunywe?


Pombe (Alcohol): Aibu ya Biblia isiyokubalika 

Habari za mwanzo kuhusu mvinyo tunazipata katika kitabu cha Mwanzo wakati Nuhu,
baada ya gharika, alipotengeneza mvinyo uliutiwa chachu (fermented grape juice).
“Akanywa divai, akalewa, akawa uchi katika hema yake” (Mwanzo 9:21) kumbukumbu
mbaya ni kwamba Nuhu alilewa na kuzunguka akiwa uchi na kwa aibu akajionyesha kwa
watoto wake wa kiume.  Jaribio hili la kwanza la dawa mpya lilipelekea laana Kwa
mafanikio ya Nuhu.

Lutu naye alilewa, Kwa urahihi kabisa akafanya zinaa Na binti zake. “Wakamnywesha
baba Yao mvinyo usiku ule akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari
alipolala wala alipoondoka (Mwanzo 19:33) watoto waliozaliwa kutokana na mahusiano
haya haramu wakawa taifa la wamoabu na waamon, maadui wa watu wa Mungu. Leo
hakuna ukosefu WA ushahidi kwamba pombe huongoza katika uvunjaji WA maadili ya
kingono, Kama vile uzinzi, uasherati, ubakaji na umaarimu (uhusiano wa kingono baina ya
watu wa damu moja).

Pia kuna uzoefu mwingine wakatai wana WA Israel walipokunywa pombe, walivua nguo
wakabaki uchi Na wakaabudu ndama WA dhahabu (Kutoka 32:6, 25).

Amon, mnywaji mwingine Na mwana WA Daud alimbaka dada yake Tamar. Kutokana Na
tukio hili alipoteza maisha yake mikononi mwa kaka yake alipowekewa sumu (2Samweli
13:28).

Tunayo mifano michache. Kwa kweli unapotazama kumbukumbu za kibiblia kuhusiana na


kinywaji kilichotiwa chachu, unapaswa ufikirie kwa nini mkristo wa kweli hatatetea
unywaji wa pombe.

Mvinyo uliochachushwa huleta ole (majuto)

Neno ole (woe) halitumiki Sana katika lugha za kawaida.  Neno hili humaanisha majuto,
mfadhaiko, huzuni.  Biblia inalitumia katika sehemu mbalimbali, haishangazi, matumizi ya
pombe ndio sababu ya neon hili kutomika.
 “ole wao waamkao asubuhi mapema, wapate kufuata kileo, wakishinda sana hata
usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao” (Isaya 5.11)
 “Ni nani apigaye, yowe, nani aliaye, ole?

Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno?

Ni nani aliye Na jeraha zisizo Na sababu?

Ni nani aliye Na macho mekundu?

Ni wale wakaao Sana kwenye mvinyo; waendao kutafuta divai iliyochanganyika” (Mithali
23:29-30)

 “ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia,
ili kuutazama uchi wao” (Habakuki 2:15)

Je, Mkristo anahitaji laana zaidi ya unywaji WA pombe kuliko hii?

Suala la afya 

“Maana mlinunuliwa kwa thamani.  Sasa basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu”
(Wakorintho 6:20). Kuanzia magonjwa ya ini, vidonda vya tumbo nk, orodha ndefu ya
matatizo ya kiafya imehusishwa na unywaji wa pombe.

Kilevi kilichomo katka pombe (alcohol) ni sumu ambayo huathiri sana mfumo wa fahamu
inapotumiwa. Mtu akiweka kiwango kidogo tu cha pombe ya whiskey mdomoni bila
kuimeza kwa dakika 10 tu, sehemu kadhaa ndani ya kinywa zitaanza kutetemeka.
Ukimfunika usoni, na kisha umwambie aonje aina nyingine ya kinywaji kama maji,
maziwa au soda, utagundua kwamba hataweza kutofausisha nini ni nini.  Jaribio hili
linathibitisha ukweli pombe si tu ni kichochezi, bali ni dawa yenye sumu (narcotic).

Ninafikiri hata watumiaji sana wa pombe watakubaliana nami kwa uaminifu kabisa
kwamba utumiaji wake haumtukuzi Mungu katika miili yao; badala yake, taratibu-
inaharibu mwili na akili, ambayo ni ukiukwaji mkubwa wa amri ya sita ya Mungu kama
ilivyo uvutaji wa sigara ambao ni kujiua mwenyewe (suicide), ndivyo ilivyo pombe ambayo
ni mvuaji mkubwa nchini Marekani.

Fikiria pia, kuna vinywaji vingi unavyoweza kuchagua vinavyoujenga mwili Na akili.  Kwa
nini waktristo watake kucheza Na hatari hii kwenye afya zao, familia zao Na uzima WA
milele Kwa kutetea maada hii haribifu (destructive substance). Kanuni salama Na rahisi
Kwa mambo haya ni hii: ukiwa na mashaka acha!

 
 

Ukweli wa kushangaza: Alexander mkuu alikuwa mtawala wa Makedonia akiwa na umri


wa miaka 16, jenerali mshindi wa miaka 18, mfalme akiwa na miaka 20, alikufa kutokana
na ulevi kabla hajatimiza miaka 33.  Kisa: Baada ya Alexander kuanza usiku WA pili wa
utawala wake mjini Babeli akiwa na wageni 20, alikunywa kwa ajili ya kila mgeni
aliyekuwa mezani.  Aliita kikombe kilichokuwa kimejazwa Sana, akanywa yote.
Alipamaliza tu akaanguka sakafuni, Na siku chache baadaye akafa.  Aliushinda ulimwengu
WA wakati huo, lakini akajishindwa yeye mwenyewe.

Maada inayo uwa sana hapa duniani

Abraham Lincoln alisema “Unywaji Ni saratani katika jamii ya wanadamu, hutafutana


viungo muhimu vya maisha na kuhatarisha uangamivu wake”.  Uharibifu mkubwa
husababishwa na pombe katika jamii yetu, barabarani, nyumbani, kwamba hili ni tamko
la kushangza.  Hata kama Biblia ingekuwa kumya kuhusiana na hili, funzo la uharibifu
kuanzia miaka mingi ya histoira bado lingekuwa wazi.  Lakini maandiko husema mengi.

“Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; itiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu,
mwisho wake huuma kama nyoka, huchoma kama fira.   Macho yako yataona mambo
mageni; na moyo wako utaona yaliyopotoka.  Naam, utakuwa Kama alalaye katikati ya
bahari, au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.  Utasema, wamenichapa wala sikuumia,
wamenipiga wala sina habari, nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena” (Mithali 23:31-35).

Na Yeremia alisema Mungu angetengeneza “chupa ya divai” ipatikanayo bure


kuliangamiza taifa (Yeremia 13:12-15).  Hii Ni kweli kiasi gani katika nchi yetu wenyewe,
matangazo yapi yameelekezwa Kwa vijana Na raia ambao wako katika hatari ya
kuathirika!

Inashangaza kuona taifa limejazwa matangazo ya uongo ya pombe, yanahamasisha


unywaji hata kwa vijana na watoto, kuna ushahidi wa kutosha unaohusisha unywaji wa
pombe na ongezeko la uharifu unaofanyiwa na vijana pamoja na watoto.  Mika pia alionya
kuhusiana na uongo na manabii wa uongo wanao shabikia mvinyo na kiywaji kikali (Mika
2:11). Leo, wanafundisha kiasi na pombe, lakini historia inaonyesha kwamba “kiasi”
kwenye madawa ya kulevya ni jambo lisilowezekana.
Suala la upendo 

“Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lolote ambalo kwa hilo
ndugu yako hukwazwa”.  (Warumi 14:21).  Mmoja kati ya watu saba wanaokunywa
mvinyo/pombe, watakuwa na matitizo ya ulevi, iweje mkristo akubaliane na chombo
kinachohamasisha watu wengi wawe waathirika badala ya utu unavyofaa.

Ikiwa kweli tunampenda Mungu wetu twawezaje kutetea unywaji wa pombe kwa kiwango
chochote kile? Paulo alisema kamwe hatakula nyama wala kunywa mvinyo au kutenda
jambo lolote litakalosababisha kumkwaza mwingine.  Wako watu wengi wanaohangaika
katia matatizo yaliyotokana Na ulevi hebu tusiwafanye wakarejea tena katika matatizo
haya.

Kukaribisha majaribu 

“Basi mtiini Mungu.  Mpingeni shetani, naye atawakimbia” (Yakobo 4:7).   Ni jambo
dhahiri lililodhinirishwa katika kumbukumbu kwamba unywaji wa kiwango kidogo tu
huharibu miitikio ya mwili.  Inapunguza msimamo WA mkristo kukutaa majaribu.  Kwa
nini mkristo awaye yote atake kufanya shetani amwingie kirahisi?

Waume na wanawake wengi wamejikuta kwa usiku mmoja tu wakibatizwa kwa glasi
chache tu za mvinyo ua chupa ya bia kabla hawajagundua kwamba, wamemeikosea amri
ya Mungu na maisha yao yameharibika pamoja na hadhi zao kupungua.

Ndio maana Petro anatuagiza “muwe na kiasi” na kukesha kwa kuwa mshitaki wenu
ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze” (1Petro
5:8).

Shetani amejitaiarisha kutukamata, hebu tusiifanye njia kuwa rahisi kwake Kwa
kutuhafisha Kwa pombe na ukinzani ambao Mungu ametupatia ili tuweze kumshinda.

Kumbuka, hata Yesu alipokuwa ametundikwa msalabani akiwa Na kiu kali, alikataa
kunywa mvinyo waliomletea (Mathayo 27:3).

 
Shuhuda zilizohafifishwa

Tabibu WA Canada Sir, William Osler alikuwa akitoa mhadhara kuhusu pombe “je ni
kweli” aliuliza mwanafunzi, “pombe humfanya mtu kutenda mambo mazuri zaidi?
“Hapana”, alijibu Sir William “huwafanaya kutoona aibu ya kutenda mambo vibaya
Sana”.

Wakristo wanaokunywa pombe wamehafifisha shuhuda zao katika ulimwengu


unaowazunguka Na wale walioko kanisani.  Na wale wanoumizwa zaidi na shuhuda hizi ni
watoto wadogo.

Kwa hakika, inachanganya Kwa watoto kuwaona mama au baba zao wakisali Na kisha
wanakunywa bia.  Yesu alilaani unafiki WA jinsi hii Kwa kauli kali “bali atakayemkosea
mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la
kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari” (Mathayo 18:6).

Baba mwenye shauku alimwendea mchungaji akasema, “Mhubiri, zungumza na kijana


wangu kuhusu unywaji wa pombe.  Alikuja nyumbani usiku WA Jana, akaanguka Na
kugalagal sakafuni akiwa amelewa Sana kuweza kuamka. Mama Yake alilia sana usiku
wote”. “Kwa nini usizungumze na mtoto wako wewe mwenyewe? Mhubiri aliuliza.

Lakini Baba WA mtoto alisema “mchungaji, siwezi kuongea naye kuhusu sula hili, maana
Mimi ndiye wa kulaumiwa. Nilitaka awe mwanaume, Kwa hiyo nilimpatia glas moja ya
pombe. Sikutegemea kwamba angekuwa mlevi.  Tafadhali ongea Na kijana wangu. Siwezi
kuzungumza naye.

Ni ukweli WA kushangaza, akina baba Na mama wengi wanajutia makosa Kama haya.
Tumeagizwa “Tokeni kati Yao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu
kilichokichafu, nami nitawakaribisha (2 Wakorintho 6:17).  Lakini, wakristo wanapoanza
kunywa pombe, wanaonyesha ya kwamba hawajitengi Na vitu vya kiulimwengu.

Mvinyo na Roho
 

Siku ya Pentekoste, wanafunzi alijazwa na Roho Mtakatifu, watazamaji walisema


“wamelewa kwa mvinyo mpya” (Matendo 2:13). Neno la kigriki Ni gleukos iliyomaanisha
isiyotiwa chachu au ‘lazima’ iliyo tamu, juisi ya zabibu iliyochemshwa isiyo na kilevi cha
alcohol, watazamaji hawa waliwapigia kilele wanafunzi kwa kusema “wemelewa juisi ya
zabibu hii inadhihirisha kwamba wanafunzi wa Yesu walifahamika kwa kutokutumia
pombe. Kwa nini basi tusifuate mfano wao?

Paulo pia anamwambia Timotheo “Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo
Kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara” (Timotheo 5:23). Ni
lazima Timotheo alikuwa akiishi Nazareti, kunywa tu maji Paulo alikuwa akimwambia
atumie juisi ya mzabibu, ambayo inaleta hali nzuri kwenye mwili, ikionyesha kwamba
Timotheo hakutumia mvinyo uliotiwa chachu Na alitakiwa ashauriwe kunywa mvinyo
mpya (usiotiwa chachu).

Kunywa mvinyo uliotiwa chachu huchangia mtu kupata vidonda vya tumbo.  Paulo
asingeshauri matumizi ya mvinyo WA zamani (uliotiwa chachu) Kwa tiba ya tumbo.

Paulo anaposema “tena msilewe Kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi, bali mjazwe na Roho”
(waefeso 5:18). Wengine wamefikiria fungu hili lina maana ya kunywa kidogo tu ILA
usilewe. La hasha! Hiyo siyo maana yake.  Tumeitwa kuwa meli takatifu iliyojazwa Na
Roho WA Mungu.

Muhutasari

Inasikitisha kutambua kwamba hata mika 4,300 baadaye, dhambi ya Nuhu bado
inasambaratisha familia hata Leo.  Je, tumejifunza kitu? Kunywa kidogo sio jibu la Mungu
la kuacha.  Kila mwathirika WA ulevi alianza kidogo.  Kanisa halipaswi kuruhusu unywaji
Kwa kuwafundisha watu wanywe pombe kidogo Tu.  Badala yake, linapaswa kushikilia
msimamo WA neno la Mungu, Kwa kutambua kwamba Yesu Ni mwanadamu aliyefanywa
mwanadamu akaja kuishi kati yetu.

Suala la pombe Kwa Mungu ni wazi, na imekuwa hivyo sikuzote. Pombe si takatifu na ni
chafu. Kutumia kinywaji hiki cha kidunia ni kuhafifisha viwango vya juu vya Mungu.

 
Ikiwa una tatizo la unywaji pombe, unakaribishwa kuwasiliana na Amazing facts na
utapatiwa masomo ya bure yahusuyo pombe na mkristo.  Tumeshuhudia maelfu
wakiwekwa huru kutoka katika pombe na madawa mengine ya kulevya kwa uwezo wa
Mungu.

“Ikiwa Bwana anaukuweka huru utakuwa huru kweli kweli (Yohana 8:36)

Mungu akubariki Sana ndugu msomaji.

=====

Imetafsiriwa Kwa Kiswahili Na: Zakaria Ngereja

Makala halisi ya Kiingereza inapatikana katika wavuti:


http://www.amazingfacts.org/Publications/InsideReport/tabid/123/articleType/
ArticleView/articleId/331/Christian-Alcohol.aspx

You might also like