You are on page 1of 10

Ifahamu ibada ya funga.

(MM Kiza 0714459591)

MAANA YA FUNGA AINA ZAKE,


HUKUMU YAKE NA FADHILA ZAKE.
Maana ya funga.
Kilugha: Funga (swaum) ni kujizuia kufanya jambo lolote ambalo
umezoea kulifanya katika maisha yako ya kila siku, kama vile
kula, kutembea, kufanya mazoezi au kuzungumza, maana hii
inathhibitishwa na kauli ya Allah alipoelezea tukio la Bi Mariyam
kupata mtoto kabla ya ndoa, jambo ambalo lilikua sio la kawaida
katika jamii yake, Allah akampa maelekezo kwa kumwambia

“Basi ule na unywe na litue jicho lako, na kama ukimuona mtu yoyote
(akakuuliza habari za mtoto huyu) sema “hakika nimeweka nadhiri kwa
mwingi wa rehma ya kufunga (swaumu) kwa hiyo sitaongea na (mtu) yeyote”
(Maryam :26)
Aya hii inathibitisha kua funga aliyoifunga Bi Maryam ilikua sio
ya kuacha kula na kunywa, bali ilikua ni ya kuacha kuzungumza
na watu, jambo ambalo alikua akilifanya katika maisha yake ya
kila siku.
Ama kisheria: Funga (swaum) ni kujizuia na mambo yote
yanayoharibu swaum kuanzia kuchomoza kwa alfajiri mpaka
kuzama jua huku ukiwa na nia ya funga.

1
Ifahamu ibada ya funga. (MM Kiza 0714459591)
Aina za funga (swaum).
Funga imegawanywa katika mafungu makubwa mawili
Aina ya kwanza: Funga za lazima (faradhi), hizi ni funga
ambazo mwislam analazimika kuzifunga na anapoacha kuzifunga
hupata dhambi, funga hizi ni pamoja na ;
A: Funga ya ramadhani ambayo ni wajibu mwislam kuifunga kila
mwaka kwa muda wa siku ishirini na tisa au thelathini
B: Funga za kafara, hizi ni funga ambazo hupatikana baada ya
mwislam kufanya kosa fulani, funga za kafara zinazo fahamika
kwa mujibu wa sharia ni hizi zifuatazo.
i. Kufunga miezi miwili mfululizo kwa aliefanya tendo la ndoa
mchana wa mwezi wa ramadhani.
ii. Kufunga miezi miwili mfululizo kwa alie mfananisha mke na
mama yake mzazi.
iii. Kufunga miezi miwili mfululizo kwa alie muua mwislamu
kwa bahati mbaya.
iv. Kufunga siku tatu kwa ajili ya kuvunja kiapo.
C: Funga za nadhiri, hizi ni funga ambazo zinapatikana kwa
mwislam kujiwajibishia yeye mwenyewe kwa kuchukua ahadi
mbele ya Allah, mfano mtu kusema Allah akinijaalia kupata
mtoto wa kiume nitafunga siku tatu, basi Allah akimjaalia kupata
mtoto huyo atawajibika kutekeleza ahadi yake ya kufunga siku
tatu, mwislamu aliyeweka nadhiri ya kufunga iwapo ikatokea

2
Ifahamu ibada ya funga. (MM Kiza 0714459591)
akafa bila ya kuifunga warithi wake watawajibika kuifunga kwa
niaba yake.
Aina ya pili: Funga za sunna, hizi ni funga ambazo mwislam
huzifunga kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allah, mfano wa funga
hizi ni
i. Kufunga siku sita katika mwezi wa shawwal, amesema
mtume swalla llahu alaihi wasallama “atakaefunga ramadhani
kisha akafuatisha na siku sita za shawwal atakua ni kama kafunga
mwaka mzima (Muslim)
ii. Kufunga siku ya arafa kwa asie kuwapo katika viwanja vya
hajj, aliulizwa mtume swalla llahu ‘alaihi wasallama kuhusu
funga ya arafa akasema “hufuta dhambi za mwaka uliopita na
uliobaki” (Muslim)
iii. Kufunga siku ya ashura, amesimulila ibn Abbas radhi za
Allah ziwe juu yao, kuwa mtume swalla llahu „alaihi wasallama
laifunga siku ya ashura na akaamuru watu waifunge” (Muttafaqun)
iv. Kufunga siku tatu kila mwezi, amesema mtume swalla llahu
„alaihi wasallama unapofunga siku tatu kila mwezi basi funga (siku ya
) kumi na tatu, kumi nan ne na kumi na tano (Tirmidh)
v. Kufunga siku za juma tatu na alkhamisi, amesimulia Aisha
radhi za Allah ziwe juu yao, mtume swalla llahu „alaihi wasallama
alikuwa akikusudia kwa hima kufunga siku ya juma tatu na alkhamis
(Tirmidh)

3
Ifahamu ibada ya funga. (MM Kiza 0714459591)
vi. Kufunga funga ya nabii daud, unafunga siku moja na
kufungua siku moja.
vii. Kufunga sana katika mwezi wa shabani, amesimulia Aisha
radhi za Allah ziwe juu yake, mtume swalla llahu „alaihi
wasallama hakuwa akifunga katika mwezi wowote kwa wingi kama
mwezi wa sha‟abani” (muttafaqun)
viii. Kufunga miezi mitukufu, amesema mtume swalla llahu
‘alaihi wasallama “funga bora baada ya funga ya ramadhani (ni
funga ya) mwezi wa Allah wa Muharram, na swala bora zaidi baada ya
swala za faradhi ni swala za usiku”(Muslim)
Hukmu ya funga ramadhani.
Kufunga mwezi wa ramadhani ni lazima kwa kila mwislamu
aliekutwa na mwezi huo iwapo atakua amekamilisha vigezo
vinavyo mlazimisha kufunga, na hili ni kwa mujibu wa dalili
kutoka katika qur an sunna na ijmai.
Ama dalili kutoka ndani ya qur an, ni kaluli Allah sub-haanahu
wa ta’ala.

“Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga kama walivyo lazimishwa kufunga


walio kabla yenu, ili mpate kua wachaMungu” (Al-baqarah 2:183)

4
Ifahamu ibada ya funga. (MM Kiza 0714459591)
Mwezi wa ramadhani ambao imeteremshwa ndani yake qura ani, ili iwe
muongozo kwa watu na hoja zilizowazi na uongozi na upambanuzi (wa haki
na batili) basi atakae kua katika mji katika huu mwezi (wa ramadhani) basi
na afunge” (Al-baqarah 2:185)
Ama dalili kutoka katika sunna za mtume swalla llahu alaihi
wasallama ni kauli zake zifuatazo.
Mtu mmoja alimuuliza mtume wa Allah, Nieleze yale ambayo Allah
aliyo nifaradhishia katika funga” (mtume) akamjibu “(kufunga) mwezi wa
ramadhani” akauliza tena,” je kuna (swaum) nyingine? Akamjibu “hapana,
isipokua za sunna…”(Muttafaqun alayhi)
Pia imesimuliwa na Abdillahi bin Umar, kua mtume swalla llahu
‘alaihi wasallam amesema “Uislam umejengwa juu ya nguzo tano,
kushuhudia kua hakuna anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokua Allah
(peke yake), na kushuhudia kua Muhammad ni mtume wake, kusimamisha
swala, kutoa zaka, kuhiji na kufunga ramadhani (Bukharin a muslim)
Na dalili katika ijmai ni kua wamekubaliana wanazuoni wote wa
kislamu kwamba funga ya ramadhani ni lazima kwa kila
mwislamu, na ni katika moja ya misingi ya dini, na mwislamu
yeyote atakae pinga ulazima wa funga ya ramadhani atakua
ameritadi (ametoka katika uislam)
Fadhila za mwezi wa ramadhani.

5
Ifahamu ibada ya funga. (MM Kiza 0714459591)
Funga ya mwezi wa ramadhani ina fadhila nyingi kwa mfungaji
hapa duniani na kesho siku ya kiama kwa mujibu wa dalili
zifuatazo kutoka katika qur an na hadithi za mtume wa Allah.
1: Funga ni kafara ya makosa, yaani ni kifutio cha dhambi
alizofanya, maadamu mja muda wa maisha yake atakuwa
anajitahidi kujiepusha na kufanya dhambi kubwa, amesema
mtume swalla llahu ‘alaihi wasallama “Swala tano, ijumaa mpaka
ijumaa, na ramadhani mpaka ramadhani, ni kafara ya makosa yanapo
epukwa madhambi makubwa” (Muslim).
2: Allah ameichagua funga kua ndio nyenzo pekee muhimu ya
kumfikisha mwislamu katika uchamungu, amesema Allah
tabaaraka wa ta’ala.

Enyimlio amini mmefaradhishiwa kufunga kama walivyo faradhisiwa


waliokua kabla yenu ili muwe wachamungu” (Al-baqarah:183)
3: Dua ya mfungaji hupokelewa na Allah, amesema mtume swalla
llahu alaihi wasallama
“Watu wa aina tatu dua zao ni zenye kujibiwa, kiongozi muadilifu, mfungaji
anapo fungua, na alie dhulumiwa”(
4: Mfungaji hupata furaha mbili moja duniani na ya pili siku ya
kukutana na Allah, amesema mtume swalla llahu ‘alaihi
wasallama

6
Ifahamu ibada ya funga. (MM Kiza 0714459591)
“Mfungaji anafuraha mbili, anapo futuru na siku ya kukutana na mola wake”
(Muslim)
5: Funga ni katika amali zitakazo muombea mwislamu siku ya
kiyama, amesema mtume swalla llahu ‘alaihi wasallama
“Funga itaomba kumuombea mfungaji siku ya kiyama( kwa kusema) Ee
Allah nilimzuia (mfungaji huyu) na chakula na matamanio yake, kwa hio
naomba nimuombee” (Ahad )
6: Funga ni kinga itakayo mzuia mwislamu kuingia motoni,
amesema mtume swalla llahu ‘alaihi wasallama
“Atakaefunga siku moja kwa ajili ya Allah, Allah atauepusha uso wake
umbali wa miaka sabini kutoka moto (ulipo) (Muslim)
7: Mtu akifa hali ya kua amefunga ni sababu ya kuingia peponi,
amesema mtume swalla llahu ‘alaihi wasallama.
“Yeyote atakaefunga siku moja kwa ajili ya Allah, na siku hiyo ndiyo ikawa
siku yake ya mwisho (kuishi) ataingia peponi” (Ahmad )
8: Ndani ya ramadhani kuna usiku ambao ni bora kuliko miezi
elfu moja, amesema mtume swalla llahu ‘alaihi wasallama.
“ ………. Ndani yake upo usiku wenye cheo ambao ni bora kuliko miezi elfu
moja, atakae utukuza atatukuzwa” (Ahmad, Annisaa na Bayhaqi)
9: Ndani ya mwezi wa ramadhani milango ya pepo hufunguliwa,
moto hufungwa na shetani hufungwa

7
Ifahamu ibada ya funga. (MM Kiza 0714459591)
“ Ulipofika mwezi wa ramadhani, mtume swalla llahu „alaihi wasallama
alisema “umekufikieni mwezi wenye baraka, amefaradhisha Allah juu yenu
kufunga,(katika mwezi huo) hufunguliwa milango ya pepo na kufungwa
mashetani, ndani yake upo usiku wenye cheo ambao ni bora kuliko miezi elfu
moja, atakae utukuza atatukuzwa (Ahamd, Annisaa na Bayhaqi)
10: Wafungaji husamehewa dhambi zilizo tangulia, amesema
mtume swalla llahu alaihi wasallama. “Atakaefunga ramadhani kwa
imani na kutarajia malipo kutoka kwa Allah, atasamehewa madhambi aliyo
yatanguliza” (Muttafaqun alaihi)
Faida za funga ya ramadhani.
Funga ya ramadhani ni miongoni mwa ibada zenye faida nyingi
kwa mwislam binafsi na hata jamii inayo mzunguka, zifuatazo ni
miongoni mwa faida ambazo anazopata mfungaji.
1: Funga inazidishia mfungaji imani na utiifu wa kwa mola wake,
upo ushahidi mwingi unaothibitisha namna ambavyo waislam
wamekua wakishindana katika kumtii Allah tabaaraka wata’ala
wakati wakiwa katika funga ya ramadhani, waswaliji
huongezeka, swadaka huongezeka watu hushindana katika
kusaidiana, yote haya watu hufanya ili kujikurubisha kwa mola
wao, na hiki ni kipimo cha kuongezeka kwa imani ya waislam.
2: Funga hua inamjengea mwislam uwezo wa kutekeleza amri na
kuacha makatazo ya Allah, mtume swalla llahu ‘alaihi wasallama
amesema “Ramadhani inapoingia mashetani hufungwa..” moja ya

8
Ifahamu ibada ya funga. (MM Kiza 0714459591)
mambo ambayo humpelekea mtu kuacha kutekeleza amri na
kufanya maasi yaliyokatazwa ni vishawishi vya mashetani wa
kijini na wa kibinaadamu, ndani ya mwezi wa ramadhani idadi ya
wanaofanya maasi hupungua, na wapo wengi ambao hutumia
ibada hii ya funga kama zoezi la kuacha maasi katika ramadhani
na kudumu nalo katika maisha yao yote, kwahiyo kupitia ibada
ya funga mwislamu hua anaimarisha mahusiano yake na mola
wake kwa kufanya amri na kuacha makatazo.
3: Pia funga hua inamsaidia mfungaji kuondokana mambo ya
kipuuzi aliyoyazoea, ibada ya funga imekusudia kumuandaa
mfungaji kua mchamungu na katika sifa za wachamungu ni kuwa
hawashughuliki na mambo ya kipuuzi, kupitia funga ya
ramadhani kila mwislamu anavyo ongeza juhudi ya kufanya ibada
kama vile kufanya dhikri za asubuhi na jioni, kusoma quran,
kuhudhuria darsa, hujikuta anapunguza wa kufanya mambo ya
kipuuzi, zoezi hili la kiibada akidumu nalo kwa muda wa mwezi
mzima litamsaidia kuachana na mambo ya kipuuzi ambayo
amedumu nayo kwa muda mrefu.
4: Funga ina imarisha afya ya mfungaji kwa kupumzisha viungo
vya mwili, katika kipindi hiki cha funga mwili wa mwislamu
hupata fursa ya kutoa baadhi ya sumu zilizotokana na akiba ya
chakula alichokua akitumia kwa muda mrefu, hivyo uzito wa
mwili hupungua, kinga za mwili huimarika, chembechembe hai
za mwili huimarika, mfumo wa hewa huimarika na hivyo kuupa
mwili fursa ya kujiimarisha upya na mwislamu kua na afya bora.

9
Ifahamu ibada ya funga. (MM Kiza 0714459591)
5: Funga huuzoesha moyo kufanya ibada kwa lengo la kutarajia
malipo kutoka kwa Allah tu, amesema Allah tabaaraka wa ta’ala
“Na hawakuamrishwa isipokua kumuabudu Allah kwa kumtakasia dini..”
(Al bayyina 98:5)
Mfungaji anapofunga huingia moja kwa moja kwenye zoezi hili la
kuuzoesha moyo wake kufanya ibada kwa ajili ya Allah peke
yake, mambo mengi ambayo nafsi yake hua inatamani kufanya
kama vile kula na kunywa, lakini kwa ajili ya kutarajia radhi za
Allah hauacha kufanya, zoezi hili la kujizuia kufanya vitu
ambavyo vipo ndani ya uwezo wako kwa ajili ya kutarajia radhi
za Allah, akilizingatia kwa undani linamjengea uwezo mkubwa
wa kufanya yale anayoyaridhia Allah peke yake katika maisha
yake ya kila siku hata baada ya funga ya ramadhani.

10

You might also like