Sample Transcript - Eunice PHD Study
Sample Transcript - Eunice PHD Study
1
1 Interviewer: sasa unaweza kuniambia ni nini umesikia kuhusu,
2 umesikia hio initiative ya serekali mahali mtu akikuja hospitali vile
3 umekuja leo, daktari anakushauri ukuje upimwe, umesikia kuhusu hayo
4 ama umesikia leo?
24 P17: wow. Mimi naweza sema hii ni ndoa yangu ya pili, kwa sababu my
25 first husband passed away in 1997, so katika ile hali ya kwenda kwa
26 wachungaji – mimi ni mhuduma, mimi nimeokoka na nampenda Yesu.
27 mimi ni mchungaji, mimi ni mevanjelisti, mimi ni mwalimu wa neno,
28 hizo zote, lakini officiator, hakujali mimi ni mchungaji ama mimi ni
29 mevanjelisti, alinituma lazima niende nipimwe. Na tukaenda
30 tukapimwe na mume ule alikuwa ananioa. Na tukakuta tuko sawa.
31 Lakini hata hivyo inabidi twende mara mingi, kendelea na kuendelea,
32 sasa ile imefanya nikuje huku, ni, nimekuwa ward, nimedischargiwa
33 last Saturday..
2
2 R17Pr150710 – Original P17
3
35 P17: Mbagathi. So, I miscarriage. So terms za daktari vile nilianza
36 kubleed, waliandika ati am suffering from incomplete abortion, so mimi
37 nilishtuka. Nikawaambia mimi sija abort. So wakaniambia hapana, hio
38 ni term ya daktari. Sasa ndio nikaelewa, lakini kwanza nilishtuka.
39 Nikafikiria nikimwambia bwana yangu ati ni incomplete abortion,
40 atafikiria nimemeza matembe ili nitoe mtoto na sio hivyo, so akaniamia
41 ni term ya daktari. So nikalazwa huko for four days na nikaoshwa,
42 nikadischargiwa on Saturday, nikaambiwa kwa sababu naishi
43 kawangware, nije huku nisaidiwe, na ndio nikatumwa kwa container ili
44 nimrudishie hio card.
4
3 R17Pr150710 – Original P17
5
65 P17: hawajitolei kwa sababu wengi watakuambia mimi sijalala na
66 mwanaume, lakini kulingana na vile nimepitia mikononi mwa
67 madaktari wengi, mara mingi tunasafiri, magari zinapata accident,
68 hata mimi nimekuwa kwa ma accident mingi, alafu daktari
69 anakwambia si lazima ukuwe umefanya ngono na mwanaume,
70 unaweza kuwa labda umekaa na mtu, ajali imefanyika ameumia, labda
71 alikuwa na virusi, inapita through. So unaweza pata na ushangae mimi
72 sijalala na mwanaume, sasa nimepata aje? Hio ndio inafanya sana
73 sana niende. Mwingine akaniambia hizi machoo sisi huenda za kukalia,
74 unaweza kwenda na upate ule mtu alikuwa hapo amewacha zile vitu
75 bado ziko fresh, alafu wewe unaenda unakaa hapo, unadhani hio choo
76 ni clean kumbe si clean so unapata umepata mahumbukizi. Vitu kama
77 hizo zinanitia moyo kwenda kupimwa kwa sababu ya daktari, ni kwa
78 sababu yangu.
82 P17: wa tatu. Anyway kile kilifanya, huyo mzee ni mchungaji pia, yeye
83 pia mke wake alikufa. He was a widower, I was a widow. Sasa
84 tulikutana uwanjani, so challenge ilikuwa mimi niachwa na watoto na
85 yeye hakuachwa na watoto. Alikaa na mke for 26 years bila mtoto.
86 sasa unaona mzee anakubali kukoa na watoto angalau kama uko na…
87 unaona angalau alee wake moja aone. Kwa sababu amependa wale
88 watoto, sasa ukimkazia unaona,hata mbele ya mungu, si unaona
89 unamkosea? Sasa ndio nilitamani hata kama ni mmoja.
6
4 R17Pr150710 – Original P17
7
98 P17: Enywewe.
101 P17: sijui sana lakini mtu husema heri nisijue kwa sababu nikijua…
102 kuna mtu mmoja niliongea naye aka sema unakaa mjinga. Kwa nini
103 unaenda kupimwa pimwa? Unaonekana wewe ni mtu wa kuhanya
104 hanya sana. Nikamwambia sihivyo. Unaona mimi ni mhubiri, nimelea
105 wengi wenye roho tofauti tofauti na wale wenye majibu. Hata kwa
106 kanisa. Unawatumikia lakini unaona wanakushusha. So mimi nimesha
107 zoea. So wana sema mimi sitaki kujua kwa sababu nikijua hio
108 itanisumbua. So nikikumbuka nilikuwa na girlfriend Fulani pahali
109 tukawachan, nilikuwa na boyfriend Fulani mahali tukawachana, sasa
110 akafa ama nikasikia fununu, …sana sana ni uwoga, sababu sijaongea
111 na wengi ni huyo moja tu.yeye ilikuwa uwonga tu. Just fear. Sasa
112 nikipatikana, what next? Kwa sababu kuna mwingine alipatikana nayo,
113 lakini yake haikuwa imeenda sana, yeye angesaidika, mimi naona
114 angepona. Lakini kwa sababu ya hasira alipopewa dawa, alikunywa
115 mara moja alafu akajidaisha, akatoka kwenye boma na akaenda mbali
116 kufanya vituko huko. Sasa unajua iliendelea? Wakati alirudi, alirudi
117 akiwa hali mbaya. Hakukaa. Alifariki. Sasa unaona huyo ni victim
118 number two. Hao wengine siwezi jua, isipokuwa huyo mmoja
119 aliniambia ni uwoga, hii kitu inaogopesha, ati niko na virusi. Sasa what
120 next nikiambiwa niko na virusi? Sasa afadhali nisijue. Ati hata kama
121 ziko, wacha ziwe lakini asijue ziko. Aendelee kuishi lakini asijue ziko.
122 Sasa hivyo ndio alinijibu. Sasa wengine sijui.
123
126 P17: kama mimi nina penda kujua kuwa afya yangu iko mzuri, sina
127 virusi, niko sawa yaani. Mtu anataka kujijua. Nivizuri kujijua. Hata Yesu
128 alikuwa anauliza wanafunzi wake, unadhani watu wanasema mimi ni
129 nani? Vitu kama hivyo. Mimi ni nani? Kule alikuwa alikenda, galilaya
130 wapi wapi, akiponya watu, alikuwa anauliza wanafunzi now what do
131 you think people are saying about me? Huyo ni Yesu. Si ati alikuwa na
8
5 R17Pr150710 – Original P17
9
132 virusi ama nini. Ah ahh (hapana) alikuwa anataka kujua watu
133 wanamsema nini. Sasa kwa nini hata mimi nisijijue niko aje? Kwa
134 sababu hii AIDS ilianza tu from nowhere. Watu wakaanza kushindwa
135 virusi na hii AIDS ni vitu gani. Na ikawa ni kweli na inaua watu. Sasa si
136 ni lazima ni jue? Sasa hata kuna wengine wanapuuza ati AIDS ni
137 ugonjwa kama TB ama malaria. Kwanza men. At least ladies wanaweza
138 kukusikiz hata kama hawataki, unaona hawataki lakini wanakusikiza.
139 Lakini men…watakuuliza si ata watu walikufa na bomb. Kweli walikufa
140 na ukimwi? Si ukuta iliangukia watu town? Si kifo ni kifo tu? Si lazima
141 nikufe na AIDS. Sijui sana kile kinaencourage watu wapimwe AIDS,
142 lakini watu wanataka wajue their own status.
143 Interviewer: ukicompare vile umesema unaenda Kenyatta and you get
144 tested, that is VCT and today you have come here and the doctor has
145 told you to get a test. How can you compare the two?
146 P17: me I can say they are just the same. Si ni kuhusu milii yetu? Mimi
147 nasema ni just the same.
150 Interviewer: in the communities, how do people treat people with HIV?
151 What do people say about it?
152 P17: Mara mingi, …mimi nimekaa Nairobi. Lakini huko mashinani it
153 depends. Unajua kuna community watu wengi wameokoka, wanamjua
154 Mungu. Wanamtreat huyo mtu with love, lakini kuna pahali pengine
155 watu bado wanaogopa, unaona mtu ametengwa, mpaka unaona mtu
156 anakuja kwa wachungaji anajisema vile hata kwa boma ametengwa,
157 unaona hata mahali pa kazi akiingia kwa ofisi na watu walikuwa
158 wanacheka, wanakimya so ana feel neglected. Lakini wengi wale wako
159 kwenye jamii kama vile mama, baba wanamjua Mungu, wanatreatiwa
160 vizuri. Hata ukienda huko huwezi jua. Nilikuwa na victim moja hapo
161 Riruta Satellite, mama mmoja niliendakuona alikuwa na mtoto ambaye
162 ni wa shemeji wake, mama na baba walikufa na AIDS, na watu katika
163 boma yao Ujaluoni walimkataa. Lakini huyu mama kwa sababu alikuwa
164 ameokoka, alikubali kuchuka huyu mtoto akiwa mdogo. Hata ukiingia
165 kwa hiyo nyumba huwezi jua kuwa akonazo kwa sababu aliachwa na
10
6 R17Pr150710 – Original P17
11
166 wazazi wake. Unajua akona watoto wake wako boarding wote na vile
167 anatreat huyu na si wake ilinivutia. Anamnunulia ile UHT ya box kwa
168 sababu akona virusi akunywe shule. Watoto wake anaweza wafanyia
169 shopping kidogo lakini huyu anamfanyia shopping nzito kwa sababu
170 huyu ana need special care asiwe affected akiwa shuleni. He is so
171 delicate lakini akiwa na watoto wengine huwezi jua mpaka
172 umkumbushe. Sasa nilikuwa naenda huko kwa sababu ya kushare na
173 kuomba pamoja. Sasa naenda na natoka very late nasikia akisema
174 “clara, umefanya hivyo?”nikataka kujua kufanya hivyo ni nini? Sasa
175 ndio akanieleza ati anamkumbusha kunywa hizo dawa. Sasa anasema
176 sijafanya hivyo alafu anakimbia bedroom kumeza dawa. Sasa
177 nikafurahia huyo mama nikampenda tu. Sasa huyu msichana anajua
178 hata kama mama na baba waloikufa, na niko na AIDS, na hata shuleni
179 walimu wanajua, ukiona huyo mtoto ako sawa. Mpaka nikaomba si
180 Mungu tu amponye? So unaona it depends? Huyu anamtreat vizuri na
181 yeye mahali ameolewa walimkataa. Sasa ni yeye tu alikubali
182 kumchukua. Wengine walimkataa hata cucu yake – mama aliyezaa
183 mama yake. Lakini ni yeye tu alikubali. Anamlea kama mtoto..huwa
184 nanamwita mtoto wake. So mimi naona inadepend. Naweza sema 50
185 50. Kuna wale wanatreat vizuri na kuna wale wantreat vibaya. Kuna
186 wale wanatupa kabisa, vitu kama hizo sasa inategemea.
187 Interviewer: do you think its normally because watu hufikiria ukiwa na
188 HIV ulikuwa unazururazurura. Do you think vile watu huwa
189 wanawaogopa wanawaneglect?
190 P17: mara ya kwanza ilikuwa kitu kama hio. Ukipata walikuja
191 kugundua, unaona kama huyo msichana aliumbukizwa na wazazi wake
192 hakuzurura? Wakati alitoka tu kwa tumbo alikuwa nazo sasa watu
193 alipokuja kujua hivyo, hizo mawazo zilianza kuwatoka. Sasa kama mimi
194 tuseme nipate AIDS kutoka kwa accident, nilizurura wapi? Sikuzurura.
195 Sasa unaona mwana damu anaona njia kubwa ni usherati. Watu
196 wanafaa kufunzwa wajue. Unajua hata kwa Bibilia inasema my people
197 die because of lack of knowledte. Sasa kitu mimi hunibore ni kuwa
198 watu wanasoma part A na hawasomi part B. Marifa iko lakini hawataki.
199 Wanakosea kwasababu hawapati maarifa na maarifa yako. Sasa mimi
200 huona si ati hawafundishwi. Si ati mtu tu amefanya usherati.
201 Nimezingushwa na injili Kenya hii, karibu Kenya yote, sasa unaona
12
7 R17Pr150710 – Original P17
13
202 unakutana na watu tofauti tofauti. Sasa ukiwa kwa pulpit, mtu
203 anakukujia anakuja na issue Fulani and you just feel. unasikia mtu
204 aliolewa wakati ma officiators hawakuwa concerned na status, so
205 unakuta huyo mzee aliokoka akiwa na virusi na amemuambukiza, alafu
206 anaenda kupimwa anaambiwa akonazo. Anashtuka kwa sababu
207 amejitunza. Anakiwambia aliokoka akiwa form two mpaka university na
208 niko kanisani na nikapata kijana kanisani. Sasa anauliza why. Hii kitu
209 unaona, inaumiza. Sasa mimi huona ni ile ukumpavu watu huwa nayo
210 wacha ni seme hivyo. How can you can assume umehanywa? Sasa
211 unajua tangu bwana yangu akufe ni 12 years. Sasa being a widow hio
212 hali ni chungu sana but I stayed. Sasa iko wakati niligonjeka na
213 nikapelekwa hospitali mpaka my own pastor akatumwa akujue anone
214 kama niko na AIDS. Sasa mimi sijahanya na ninajua sijalala na
215 mwanaume yeyote. Lakini nikomgonjwa kabisa ni kama nitakufa the
216 next minute. Sasa nilienda mimi mwenyewe nikawapelekea makaratasi
217 waconfirm ni AIDS. Sasa ilikuwa malaria kwa sababu nilikuwa
218 nimeenda Busia na unajua Busia nikujoto na Butere ni kucool kidogo so
219 ile kuchanganya. Na nilipona. Lakini vile sina bwana walisema labda
220 vile hana bwana amehanya hanya. Unaona hio ni wrong. Sikuhanya.
221 Na sina AIDS. Niko na malaria. So sijue na weza sema vipi. It is very
222 hard to explain. Mimi nasema Mungu atusaidie, because people can
223 talk anything, hurting, bitter words, mpaka zikikugonga kama huna
224 neema, unaweza react, but God is our witness. I say kama nimelala na
225 mtu mwingine God is my witness na kama sijalala na mtu Mungu ndiye
226 anajua so sijui kwa nini sisi hufikiria tu hivyo ati mtu ni kuhanya hanya
227 tu. Si kila mtu uhanya. Kuonao uhanya. Na sometimes wale uhanya
228 hawana. Na wanahanya 24 hours. Wewe umetunza ndoa yako,
229 unapimwa alafu unaambiwa uko nayo, unashindwa ulipata wapi. Sasa
230 si ati kwa sababu ya kuhanya. Ata watu wameogopa. Mtu akitaka
231 kuhanya anajipanga so sijui, ni vile tu ameona nikwa kulala tu. Hawajui
232 kunajia zingine.
233 Interviewer: do you think kwa sababu kuna alot of information about
234 AIDS kuna advertisements kwa radio kwote. Si information iko? Na
235 watu wanajua all this things vile wanaweza kupata HIV from many
236 ways. Kwa nini watu basi hawasikii hio information?
14
8 R17Pr150710 – Original P17
15
238 Interviewer: unakubali information iko?
239 P17: information iko hata kwa magazeti. Hata Yule hata tv anasikia
240 kwa radio. Mwenye hana radio anasikia kwa hospitali kama hapa. Sasa
241 mtu anaweza sema sina tv, sina radio, sina gazeti lakini sinimekuja
242 hapa? Sinipatana na wewe na umeniambia? Kwa maoni yangu watu
243 wengi wanapenda kupuuza vitu. Kwa mfano, unakumbuka ile trailer ya
244 mafuta ilichoma watu kule kunaitwa aje….
246 P17:…si uliona kweli ilikuwa sad surely. That’s why nakuambia
247 Kenyans tunapuuza. Watu wakashuhudia vifo hata makaburi iko na
248 watu hawakua wanajulikana walikuwa wanakaa aje. Tuwazike tu wote,
249 but still ingine ilianguka na wakakimbia? So mimi nikaona Kenyans
250 tunapenda kupuuza. Tukona spirit ya kupuuza.
252 P17: mimi ningekuwa na uwezo ningeenda kwa kila mtu ni waambie tu
253 wapimwe, na pia wafunzwe kwa sababu wameona tu kupata AIDS ni
254 through kuhanyana. Na kama ni lazima, tumia makinga, lakini kuna
255 wengine wana damu zinachemka in seconds, sasa kama uko na hiyo
256 basi tumia kinga. Unajua sijakufunga na kamba, sasa kwa sababu
257 sitakufunga na nakujali, so utumie tu kinga, tumia condoms, ujikinge
258 tu. Ongea na huyo mtu kama anakujali atatumia kinga. Lakini ukona
259 ule hataki, hajali. Kwa nini? Ati kwa nini nivae hizi masoaks? Lakini
260 mwenye anakujali, mtaongea na atakubali. Mimi hucounsel wasichana
261 kanisani na ningekuwa na uwezo ningewachapa viboko lakini kwa
262 sababu nawajali…unaongea sahii wanalia, lakini ukisikia mareporti ya
263 kesho utashangaa. Sasa kwa sababu sitawaweza, ni Mungu tu. Ukona
264 umeenda, jikinge tu. Kwa sababu utaona mwenye anaimba mpaka…
265 unasikia baada ya miezi ako na mimba. Na huyo msichana umeongea
266 na yeye mpaka akalia. So its very hard uwakataze na wasikie. Ni kama
267 their blood…sijui wanakula nini. Damu inawaka waka tu wanataka
268 waende na hawajui wanaenda na nani. Lakini naweza encourage watu
269 wajichunge tu. Watumie tu kinga. Kwa sababu mtu atasema nitameza
270 tembe ili nisipate mimba, na wengine wanaenda wakiwa young,
271 wanameza hizo dawa, sisemi ni mbaya, lakini kujaza madawa kwa
16
9 R17Pr150710 – Original P17
17
272 tumbo…wakitaka watoto wanakuta zimeharibu. Zinaharibungi si ni
273 kweli. Zinaharibu. Mtu akienda kudungwa sindano ya 5 years akiwa 20
274 years au 17 years, alafu atakuja kuolewa akiwa 35 years, si unaona
275 atakuwa ametumia sana? Sasa mimi nadiscourage hio, iko siku
276 utahitaji mtoto…so lazima tujichunge. Mimi husema I will not die I will
277 spread the word of God. So mimi bado nitaishi miaka mingi. So lazima
278 nijijue, lazima nipimwe, watu wanauliza kwa nini nipimwe na
279 nimeolewa na mchungaji.sifikiri ati mume wangu anahanya hanya. I
280 respect my husband kwa sababu si mtu wa kuhanya hanya. Kama
281 angekuwa wakuhanya hanya angefanya hivyo kitambo.
282 Kamahakujaribu ni sahii atajaribu akiwa 45 years? So ni vile tu watu
283 huwa hawaelewi. Hio pepo ikiwatoka, Kenyans are good people.
18