You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI



TAARIFA KWA UMMA KUHUSU ZOEZI LA USAILI WA NAFASI YA MKAGUZI MSAIDIZI
WA UHAMIAJI LILILOFANYWA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KATIKA
UWANJA MPYA WA TAIFA TAREHE 13 JUNI, 2014
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imebaini taarifa mbalimbali zinazozungumzwa na
ambazo zimetolewa katika baadhi ya vyombo vya habari kuhusu zoezi la usaili wa
nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji lililofanywa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi tarehe 13 katika Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam.
Wizara ingependa kutoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya tuhuma zilizotolewa na baadhi ya
wadau kama ifuatavyo:
1. RUSHWA
Tuhuma za rushwa zinazoambatanishwa na zoezi hili ni hisia tu za wahusika
kwani, kwanza hazina ushahidi, na pia usaili ulifanywa kufuatana na kanuni na
sheria zinazosimamia ajira za watumishi wa Umma.

2. ULINZI
Katika Uwanja wa Taifa kulikuwa na Maafisa mbalimbali toka Taasisi za Wizara
ya Mambo ya Ndani ya nchi ambao walikuwepo kuhakikisha kuwa zoezi hilo
linafanyika kwa usalama.

3. WINGI WA WASAILIWA
Nafasi za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji zilitangazwa katika magazeti na Tovuti
ya Wizara na Idara ya Uhamiaji kufuatana na taratibu Serikali zinazosimamia
ujazaji wa nafasi za kazi katika utumishi wa umma kwa lengo la kuiweka wazi
kwa umma wa Watanzania na matokeo yake wahitimu zaidi ya 20,000 walitumia
haki yao ya msingi kuomba nafasi hizo.
Kufuatana na wingi wa waombaji, Wizara ilifanya zoezi la mchujo wa awali
ambao hatimaye ulibakiza kiasi cha maombi 10,000 yenye waombaji wenye sifa
zinazohitajika.
Aidha kutokana na wingi huo, na haki ya kila muombaji ya kupatiwa nafasi ya
kushindania nafasi hizo, ilibidi Wizara ifanye utaratibu wa kutafuta eneo lenye
nafasi ya kutosha ya kuweza kuwapokea wasailiwa, ambalo hatimaye ilionekana
iwe Uwanja mpya wa Taifa.
Wingi wa wasailiwa ni matokeo ya kidemokrasia ya kutoa nafasi kwa kila raia
kushindania nafasi za ajira zinazotolewa nchini ili mradi awe na sifa.

4. BAADHI YA WASAILIWA KUTOKUWA NA KALAMU
Maandalizi ya usaili ni pamoja na kuwa na vifaa vya kawaida vya kushiriki usaili
hivyo msailiwa aliyefika katika eneo la usaili akiwa mikono mitupu ni yule ambaye
hakujiandaa, wala kuwa na kalamu haihitaji kutangaziwa.

5. UFINYU WA ENEO
Uwanja mpya wa Taifa Dar es Salaam una uwezo wa kukaliwa na watu 60,000
hivyo idadi ya wasailiwa 10,000 waliokuwapo uwanjani hapo haikuwa tishio kwa
usalama wao.

MWISHO
Nia ya Wizara haikuwa kuleta usumbufu kwa mtu yeyote ila kutoa nafasi sawa
kwa walioleta maombi kushindania nafasi zilizotangazwa.

Imetolewa na:
Sgn
Isaac J. Nantanga
MSEMAJI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
14 JUNI, 2014

You might also like