You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA

TAHADHARI Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inawatahadharisha wananchi wote, ndani na nje ya nchi kujihadhari na watu wanaotumia jina la Utumishi kuwaibia fedha na kupoteza muda wao kufuatilia jambo ambalo halipo. Watu hao wanatumia majina yafuatayo katika mitandao; Saving Foundation Loans na Jakaya Foundation kwa anuani http://savingfoundation.wapka.mobi/index.xhtml na kuelekeza kuwa Makao Makuu yapo kwenye jengo la UTUMISHI. Namba za simu zifuatazo zimekuwa zikitumika kuwatapeli wananchi watume fedha; 0715-373307, 0656-037520 na 0762-269376. Wananchi epukeni kurubuniwa na watu hao kwani Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma haijishughulishi na kutoa mikopo ya aina yoyote kwa wananchi. Tangazo limetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma. 2 Aprili, 2014 Mawasiliano: permsec@utumishi.go.tz, S.L.P 2483 Dar es Salaam,Simu: + (255) 22 2118531-4

You might also like