You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
Simu Na: +255 (026) 2963630 Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Nukushi: +255 (026) 2963629 na Utawala Bora,
Barua Pepe: ps@utumishi.go.tz Jengo la Taaluma Na. 1,
Tovuti:http://www.utumishi.go.tz Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
18 Barabara ya Mkalama,
S.L.P. 670,
40404 DODOMA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YASAINI MKATABA NA WAKALA WA


MAJENGO TANZANIA KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA
SERIKALI JIJINI DODOMA

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora


imesaini Mkataba na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wa kuanza rasmi
ujenzi wa ofisi katika mji wa serikali, Ihumwa jijini Dodoma.

Mkataba huo umesainiwa ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya
kuhamishia shughuli za serikali Makao Makuu ya Nchi.

Kabla ya kusaini mkataba huo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya


Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro, amesema ujenzi wa ofisi
hiyo ni hatua muhimu ya kutimiza mpango wa serikali na maelekezo ya
Mhe. Dkt. Magufuli ya kuhamia Dodoma kwa lengo la kusogeza huduma
karibu na wananchi.

Dkt. Ndumbaro ameitaka TBA kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa ofisi


hiyo kwa wakati na kwa kiwango bora ili kuwawezesha watumishi wa ofisi
yake kutoa huduma kwa wananchi katika mazingira mazuri.

Kwa Upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Arch.


Elius Mwakalinga ameishukuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora kwa kuiamini ofisi yake na kuwapa kazi ya ujenzi
wa ofisi hiyo.

1
Arch. Mwakalinga ameahidi kufanya kazi ya ujenzi huo kwa weledi mkubwa
kwani wana vitendea kazi vya kisasa vinavyojitosheleza ikiwa ni pamoja na
wataalam wa kutosha watakaowezesha kukamilisha jengo hilo kwa
kiwango bora na kwa wakati.

Aidha, Arch. Mwakalinga ametoa wito kwa wakuu wa taasisi nyingine


kuitumia Wakala wa Majengo Tanzania katika ujenzi wa majengo
mbalimbali kwani wako tayari muda wote kutoa huduma kwa kiwango bora.

Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na


Utawala Bora katika mji wa serikali, Ihumwa ni sehemu ya mwendelezo wa
utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhamishia shughuli za serikali jijini
Dodoma aliyoyatoa tarehe 25 Julai, 2016 wakati wa maadhimisho ya
Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa.

IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 22 NOVEMBA, 2018

You might also like