You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
Simu Na: +255 (026) 2963630 Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Nukushi: +255 (026) 2963629 na Utawala Bora,
Barua Pepe: ps@utumishi.go.tz Jengo la Taaluma Na. 1,
Tovuti:http://www.utumishi.go.tz Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
18 Barabara ya Mkalama,
S.L.P. 670,
40404 DODOMA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAFANYA UFUATILIAJI WA UTEKELEZAJI WA WARAKA
WA MAVAZI KWA WATUMISHI WAKE
Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora kwa kushirikiana na Kamati ya Uadilifu ya ofisi hiyo, imefanya ufuatiliaji wa
Utekelezaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 kwa watumishi wa ofisi hiyo
kwa lengo la kujiridhisha na kiwango cha utekelezaji wake, ikiwa ni pamoja na kuhimiza
watumishi wa umma nchini kuzingatia waraka huo mahala pa kazi.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ukuzaji Maadili, Sehemu ya
Ufuatiliaji Uzingatiaji wa Maadili, Bibi Janeth Mishinga mara baada ya kukamilika kwa
zoezi la ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Waraka huo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambao unawaelekeza watumishi
wa umma aina ya mavazi wanayostahili kuyavaa mahala pa kazi.
Bibi Mishinga amesema, Ofisi ya Rais-Utumishi ni msimamizi wa miongozo mbalimbali
ya kiutumishi ikiwemo Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma ambapo
kanuni ya kwanza inaelekeza utoaji wa huduma bora na kuongeza kuwa moja ya kigezo
cha watumishi wa umma kutoa huduma bora ni pamoja na kuvaa mavazi yenye staha.
Bibi Mishinga amefafanua kuwa, zoezi hilo la ukaguzi katika ofisi ya Rais-Utumishi
limebaini kuwa asilimia 95 ya watumishi wameonekana kutekeleza vema waraka huo wa
mavazi ikiwemo kuwahi kazini na asilimia tano ya watumishi waliobainika kutotekeleza
waraka huo wamekumbushwa kuuzingatia.
Aidha, Bibi Mishinga ametoa wito kwa wasimamizi wa taasisi zote za umma nchini
kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa waraka huo na kuwahimiza watumishi walio chini
yao kuwahi kazini kwa ili kutoa huduma bora na kwa wakati kama ambavyo Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anavyohimiza.
Bibi Mishinga amesisitiza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora ikiwa ndio msimamizi wa waraka huo wa mavazi itaendelea kufanya
ukaguzi na ufuatiliaji katika taasisi zote za umma nchini na haitosita kuwachukulia hatua
za kinidhamu watumishi wote wa umma watakaobainika kuukiuka.

IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 07 FEBRUARI, 2019

You might also like