Professional Documents
Culture Documents
ANNUUR 1171a
ANNUUR 1171a
com
Sauti ya Waislamu
ISSN 0856 - 3861 Na. 1171 JAMADIUL AKHER 1436, IJUMAA , APRILI 3 - 9, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=
Siasa za mabeberu
Iraq na Yemen
Mashabiki wa Abu Baghdad mnasimama wapi!
Kama Iraq ni tatizo la Shia kuzuiya Khilafah
Yemen napo Waarabu wanachopigania nini?
Soma Uk. 10
Lipo Jinamizi
PICHANI juu ni siasa za Zanzibar wakijeruhiana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili
ya mambo ya kisiasa. Picha chini mitutu ya vifaru vya Saudi Arabia vikielekezwa
Yemen. Nchi zote hizo za Kiarabu.
Soma Uk.7
Soma Uk. 2
Tahariri
AN-NUUR
TAMAA ya Waislamu
kwamba siku moja
wanaweza kuwa na
Mahakama yao ya Kadhi
nchini, chombo ambacho
kingekuwa suluhu ya
hitilafu nyingi katika
kutekeleza majukumu
yao ya msingi ya kiibada
na kimaadili, sasa ifikie
kikomo.
Pamoja na kwamba
wapo watu ambao bado
wanadhani kwamba
masu al a au matatizo
ya Waislamu yanaweza
k u t a t u l i wa n d a n i ya
mfumo wa sasa wa serikali
yetu na vyombo vyake
vya kimamlaka, lakini
ukweli ni kwamba historia
inadhihirisha kwamba
katu haiwezekani jamii
ya Waislamu kutimiziwa
au kukubaliwa haja zao za
kiimani ndani ya himaya
ya watu waliofura chuki,
ambao wengi wao ndio
waliopo katika nafasi nyeti
za maamuzi.
Mwandishi mashuhuri
wa makala, Mzee wetu
Bw. Shaaban Khalid
Mtwangi, siku za nyuma
aliwahi kuandika makala
yake kuhusu Mahakama
ya Kadhi katika gazeti hili,
akisema katu haiwezekani
M a h a k a m a ya K a d h i
ikaanzishwa nchini kwa
k u wa , i l i M a h a k a m a
hiyo iweze kupata
uhalali wa kuanzishwa
na kutambuliwa na
sheria ya nchi (katiba), ni
lazima kwanza muswada
wa kuanzishwa kwake
upelekwe Bungeni na
kuridhiwa na wabunge
walio wengi.
Kwa msingi huo, Bw.
Mtwangi alisema kwa
namna ambavyo sura
ya Bunge letu ilivyo,
akimaanisha kujaa
wabunge wengi wa
imani ya Kikristo, na kwa
kuzingatia ukweli kwamba
kuna chuki kubwa ya
kiimani iliyojificha ndani
ya mioyo yao, kamwe
hawawezi kukubali
kuupitisha muswada huo
hata utakapofikishwa
mbele yao.
Mzee Mtwangi
alihitimisha kwa kusema,
Waislamu wanapoteza
muda wao kudai
mahakama hiyo ndani
ya mfuno wa sasa wa
kimamlaka na kidola
n a a k a o n a Wa i s l a m u
kuendelea kupambana
katika mazingira haya
kudumu katika matumaini
kuwa watakubaliwa kuwa
na chombo chao hicho
kikatiba, ni kupoteza muda
na nguvu za kufanya
m a m b o m e n g i n e k wa
maslahi ya Waislamu.
Yeye alishauri kwamba
kwanza uwepo mkakati
wa kuhakikisha kwamba
jamii ya Waislamu, nao
wanakuwepo kwa namba
inayoridhisha katika
vyombo vya kidola
na kimamlaka hasa
Bunge. Hapo wanaweza
kupambana uso kwa uso
kusimamia heshima na
maslahi yao ya kiibada.
Tukitizama kwa kina
alichokuwa akikieleza
M z e e M t wa n g i n d a n i
ya makala yake hiyo,
utagundua kwamba suala
la kuanzisha Mahakama
ya Kadhi nchini, ni mchezo
wa kisiasa na hadaa tupu
dhidi ya jamii ya Kiislamu
nchini lakini ukweli
wake ni kwamba haiwezi
kukubaliwa iwepo.
Suala hili limekuwa
likipigiwa kelele kwa
muda mrefu, limewahi
hata kuingizwa katika Ilani
ya CCM ya mwaka 2005.
Waziri Mkuu Mizengo
Kayanza Pinda, ambaye
ndiye hasa aliyepewa
jukumu la kusimamia
mchakato wa kuanzishwa
mahakama hii kwa upande
wa serikali, pamoja na
kujaribu kuanzisha
mchakato huo kwa kuunda
K a m a t i ya Pa m o j a ya
Viongozi wa Jumuia za
Kiislamu na serikali, bado
yalifanyika madudu kwa
kuanzisha Mahakama ya
Kadhi ya Bakwata kule
Dodoma.
Makadhi ambao
hawafahamiki kisheria
(kikatiba), ambao
walipatikana bila utaratibu
wa Kiislamu na kibaya
zaidi, yote hayo yalifanyika
bila kuwepo mawasiliano
na Kamati ya Pamoja
iliyojumuisha serikali chini
ya Waziri Mkuu, ambayo
kimsingi ndicho chombo
halali kichokubalika na
Wa i s l a m u n a s e r i k a l i
kushughulikia suala hilo
kiutaratibu.
Tu n a a m i n i k wa m b a
hadaa hii dhidi ya Waislamu
AN-NUUR
3
Na Salma Alghaythiyah
H A L I i n a z i d i k u wa
tete Zanzibar ambapo
sasa watu wanatishiana
kusomeana Albadiri.
Hayo yalijiri katika
kikao cha Baraza la
Wa wa k i l i s h i a m b a p o
ilipelekwa hoja binafsi juu
ya baadhi ya Wazanzibari
kunyimwa vitambulisho
vya Ukaazi.
Alikuwa Mjumbe
mmoja baada ya kuona
wenzake wa CCM
wanakuja juu kupinga
hoja madai ya baadhi
ya wanachama wa CUF
kunyimwa vitambulisho
aliposema kuwa
anakusudia kuita watoto
wa m a d r a s a k u s o m a
Albadiri kuwashitaki
CCM kwa Mungu.
Hiyo ilikuwa baada
ya k u t o k e a m v u t a n o
mkali ndani ya
Baraza la Wawakilishi
kuhusiana na hoja binafsi
iliyowasilishwa na
Mwakilishi wa Ole (CUF)
Hamad Masoud Hamad
ya kuitaka serikali ichukue
hatua za kuhakikisha
Wa z a n z i b a r i a m b a o
hawana vitambulisho vya
Mzanzibari na wana sifa,
wapewe vitambulisho
kabla ya uchaguzi mkuu.
Mvutano huo ulianza
baada ya Mwakilishi wa
Jimbo la Kwahani Hamza
Hassan Juma (CCM)
kuuchana waraka wa
hoja hiyo iliyowasilishwa
na wapinzani ambapo
baadhi ya Wawakilishi
walikasirishwa na
kitendo hicho na kuanza
kusimama na kutaka
kupigana kutokana na
kitendo cha Mwakilishi
huyo.
Kufuatia taharuki
hiyo, Spika wa Baraza
hilo Pandu Ameir Kificho,
alilazimika kusitisha
shughuli za Baraza kwa
muda wa zaidi ya saa moja
na baada kurudi tena,
hakukuwa na maafikiano
ambapo kila upande
ukivutia upande wake
wa p i n z a n i wa k i s e m a
wanadhulumiwa
huku upande wa CCM
wakisema sheria zipo
wazi wenye kutaka
vitambulisho wafuate
sheria.
Kabla ya kuahirishwa
kwa kikao hicho, mjumbe
wa Baraza hilo kutoka
CCM , Issa Haji Gavu
ambae pia ni Naibu
Wizara wa Miundombinu
Habari
AN-NUUR
Wawakilishi Zanzibar
watishiana Albadiri
na Mawasiliano na
Mjumbe wa Baraza hilo
kutoka CUF Hassan
Hamad kutaka kupigana
katika kikao hicho na
kurushiana maneno ya
jazba na kudharauliana.
Wakati Gavu akitaka
kushikana shati na Hassan
huku Hamza aliyechana
waraka huo alishikana
kwa maneno makali na
Mnadhimu na Baraza hilo
kwa upande wa upinzani
Abdallah Juma Abdallah.
Baada ya nusu saa,
suluhu iliweza kupatikana
na wajumbe wote wa
Baraza hilo kurejea na
Spika kuendeleza kikao
huku Spika akisema
kuwa hajafurahishwa
hata kidogo kutokana
na kitendo kilichotokea
katika Baraza hilo.
Kitendo hiki kwa kweli
hakikuwa cha kupendeza
na kimeleta taswira
mbaya kwa wananchi
wanaotuangalia, alisema
Kificho.
Aidha Kificho aliwataka
wajumbe wa baraza hilo
kuwa na uvumilivu
wa kisiasa, kuacha
kutukanana na kutoleana
maneno ya kashfa, kwani
wana dhamana kubwa
kwa wananchi.
Chanzo cha ugomvi
na malumbano hayo ni
pale wajumbe wa Baraza
hilo wakati wakichangia
hoja hiyo kwa jazba na
baadhi yao kuchangia
michango hiyo kutoka nje
ya mada ambapo baadhi
yao walionekana kukerwa
na dhulma inayoendelea
k wa k u n y i m wa wa t u
vitambulisho huku
baadhi yao wakiwapeleka
viongozi kuwashitaki
mbele ya Allah.
Bi Ashura Sharif Ali
kutoka nafasi za wanawake
(CUF)aliwataka viongozi
kuziheshimu nafasi
zao na kujua kwamba
wana dhamana kubwa
waliopewa na Allah na
ipo siku watarudi kwa
Mwen ye enzi Mung u
na wanayoyatenda yote
wataulizwa.
N a p e n d a
kuwakumbusha kwamba
hapa duniani tumekuja
kuishi kama wapita njia
tu, bado kuna maisha
mengine ya milele, sasa
viongozi mnaopewa
hizi dhamana mjue haya
mnayoyatenda mtakuja
kuulizwa na kuhukumiwa
mbele ya Allah, alisema
kwa uchungu Bi Ashura.
Akichangia hoja hiyo Bi
Kadija Khamis Kona wa
(CUF) alisema kwa kuwa
hatua zote wameshapitia
za kuomba vitambulisho
hivyo lakini mamlaka
zinazohusika zinafanya
kusudi kuwakatalia, basi
anasubiri kumaliza vikao
vya Baraza arudi nyumbani
kwake na kuitisha kisomo
cha watoto wa chuoni
kumshitakia Mwenyeenzi
Mungu juu ya dhulma
hiyo.
Nitawakusanya
watoto wa chuoni tusome
halalbadri kwa sababu
anayepaswa kuombwa
na kutegemewa ni yeye
Mwenyeenzi Mungu tu,
alisema Mwakilishi huyo.
Wa k i c h a n g i a h o j a
hiyo, baadhi ya wajumbe
walisema Mwenyeenzi
Mungu ni wa watu wote
na baadhi yao walionesha
kubeza visomo hivyo
kuwa hata wao wanaweza
kusoma kwa kuwa ni
miongoni mwa wacha
Mungu.
Mwakilishi wa Viti
Maalum (CCM), Wanu
Hafidh Ameri alisema
hao wenye kumuelekea
Mwenye enzi Mungu, pia
nao wana mabaya yao na
hawezi kuiunga mkono
hoja hiyo kwa sababu
Baraza la Wawakilishi
halina uwezo wa kuangalia
utaratibu wa kisheria ila
Baraza kufuata utaratibu
wa kisheria na sio kutoa
maamuzi na masharti
ya kupata vitambulisho
kwani suala la kupata
vitambulisho hivyo lipo
kisheria.
Alisema, suala la
kupata kitambulisho cha
Mzanzibari Mkaazi, ni haki
ya kikatiba na masharti
ya kupata kitambulisho
hicho yameeleza vizuri
katika ibara ya sita ya
katiba ya Zanzibar na
ibara hiyo inaeleza
kama mtu hajaridhika
katika upatikanaji wa
vitambulisho hivyo
kwenda Mahakama Kuu
na sio katika Baraza la
Wawakilishi.
Aliyewasilisha hoja hii
kama anahisi wanaotoa
vitambulisho hivi kuwa
hawawajibiki na haki
haitendeki, basi aende
mahakamani na hakuna
haja ya kuishurutisha
serikali, alisema Wanu.
Alimtaka mjumbe huyo
aliewasilisha hoja hiyo ni
vyema kuwashajihisha
wananchi kufuata
utaratibu wa upatikanaji
wa vitambulisho hivyo ili
kuweza kupatia haki hiyo.
Mohammed Aboud
Mohammed ni Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamo wa
Pili wa Rais, aliwaomba
Wawakilishi wasifikishane
kwa Mungu kwa kuwa
mambo ya kupatikana
vitambulisho yana taratibu
zake na kuwataka wajumbe
wafuate taratibu, kauli
ambayo ilidharauliwa na
wapinzani kwa kuwa suala
hilo serikali imeshindwa
kulisimamia huku ofisi
yake ikishutumiwa kutoa
muongozo kwa masheha
wasitoe vitambulisho.
Mwakilishi wa Jimbo
Micheweni (CUF) Subeti
Khamis Faki Abdallah
Hamad ameunga mkono
h oja hi yo na k ui t a k a
serikali kuwachukulia
hatua za kisheria
wahusika wa utoaji wa
vitambulisho hivyo ambao
wanawanyima haki yao
hiyo baadhi ya wananchi
kwa sababu zisizo na
msingi.
Alisema, suala la
kuwanyima wananchi
vitambulisho hivyo
ni mtaji wa chama cha
mapinduzi na suala hilo
limeingizwa kisiasa zaidi.
Alisema suala
h i l o l a k u wa k o s e s h a
vitambulisho wananchi
ni njama ya CCM kuweza
k u n g a n g a n i a k u k a a
madarakani na kuweza
kupata ushindi katika
uchaguzi mkuu kwa kuwa
asie na kitambulisho hicho
hatoweza kupiga kura.
Aidha, Wawakilishi
wa C U F wa l i wa t u p i a
l a wa m a m a s h e h a wa
shehia (viongozi wa mitaa)
kutokana na kuwanyima
b a a d h i ya wa n a n c h i
vitambulisho hivyo kwa
makusudi kutokana na
itikadi za kisiasa.
Mwakilishi wa
viti maalum Salma
Mohammed Ali alisema
masheha wamepewa agizo
maalum la kuwakosesha
wananchi vitambulisho
hasa wale wenye msimamo
tofauti na Chama Cha
Mapinduzi ambapo
alisema hana imani na
Masheha kwa kuwa wao
ndio chanzo cha wananchi
kunyimwa haki zao.
Awali akizungumzia
suala hilo Waziri wa Sheria
na Katiba, Abubakar
Khamis Bakari alisema
sio kwamba wananchi
hawawezi kwenda
mahakamani, lakini tatizo
liliopo wananchi hawawezi
kufika mahakamani
kutokana na vikwazo
vingi wanavyowekewa na
suala la kuambiwa sheria
inasema hivi ni mambo
ya k u h a n g a i s h wa t u
wananchi.
Waziri wa Nchi ofisi
ya Rais, Idara Maalum,
Ta wa l a z a M i k o a n a
Vikosi vya SMZ, Haji
Omar Kheir amekanusha
kauli za baadhi ya
wajumbe wa Baraza la
Wa wa k l i s h i wa l i o d a i
kuwa vitambullisho
vya Mzanzibari Mkaazi
vinatolewa kwa sababu
ya siasa.
Huku akijisifu kuwa
yeye pia ni mcha Mungu
na amekuwa akitoa sadaka
n a z a k a k i l a m wa k a
pamoja na kwenda Hijja
ambapo alisema mwaka
huu anatarajia kwenda
tena kuhiji na umra kwake
yeye ni jambo la kawaida.
Kheri alisema
vitambulisho hivyo
vinatolewa kwa mujibu wa
sheria na kama wajumbe
hao wanaona kuwa sheria
hiyo ina mapungufu, basi
waifanyie marekebisho.
Waziri huyo alisema
kama kuna mtu
ananyimwa haki hiyo
ya kupata vitambulisho,
afuate taratibu za kisheria
ili kuweza kupata haki
yake hiyo.
4
Na Khalid Gwiji
Makala
AN-NUUR
wa Zanzibar na wa
Wa z a n z i b a r i k w a
k u t u m i k a k wa n j i a
y o y o t e i n a y o we z a
kuhujumu mshikamano,
umoja, mapenzi,
udugu na uvumilivu
baina yetu, uliojengeka
tokea kuasisiwa kwa
KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) akimjulia hali mmoja wa majeruhi
aliyeshambulia katika mkutano wa Chama hicho Unguja hivi karibuni.
wanaamini kuwa bila
ya migogoro - hawana
biashara.
N i
b u s a r a
tukakumbuka na
kuzingatia eneo la
mafanikio la Serikali ya
Umoja wa Kitaifa na kwa
pamoja tukaiendeleza
kutokana na ukweli
kwamba imekuwa na
maslahi mapana kwa
wote na ni vile vile ni
muakilishi na mtetezi
wa makundi yote.
Serikali ya Umoja
wa Kitaifa kimsingi
n i n ye n z o m u h i m u
sana katika ujenzi
wa Zanzibar mpya.
Imekuja kuzika siasa
za chuki, uhasama,
vurugu zilizolenga
kufukua makaburi
na visasi na badala
yake kuleta mfumo
mpya wa mahusiano
mema miongoni mwa
Wananchi, viongozi
na Serikali yao kwa
kuyawekea maua
makaburi. Serikali hii ya
pamoja ina eneo kubwa
la Mafanikio ambayo
ni pamoja na: Kwanza,
imeleta mshikamano
miongoni mwa
wananchi kwa kuzizika
siasa za chuki na
uhasama. Pili, ilianzisha
u s t a a r a b u m p ya n a
wenye ukomavu
wa kisiasa katika
uendeshaji wa siasa za
vyama. Matumizi ya
kuendeleza na
kusimamia amani na
utulivu. Saba, SUK
imesaidia kuengeza
wigo wa uvumilivu
wa kisiasa. Nane,
GNU ilisaidia serikali
kutotumia nguvu ya dola
dhidi ya wananchi kama
ambavyo pia ilisaidia
wananchi kutotumia
nguvu ya umma dhidi
ya serikali. Ilijaribu kuja
katika mrengo wa kati na
kati wa mazungumzo.
Muhimu zaidi, Serikali
ya Umoja wa Kitaifa
inahitaji kuendelezwa
kwa vile hatujawa na
demokrasia tulivu
(stable democracy)
ye n ye k u a m i n i j u u
ya m m o j a a t o k e n a
m we n g i n e a i n g i e demokrasia tulivu ya
kupokezana madaraka
na mamlaka kwa njia za
amani na ustaarabu.
Wito wetu kwa
Wazanzibari, ni muhimu
sana kuimarisha Umoja
wetu wa Pamoja,
kudumisha amani na
utulivu ndani ya nchi
yetu na kwamba harakati
zote za kuwatafuta na
kuwabaini walio nyuma
ya uovu huu ziendelee
na kuendelezwa na
Wazanzibari wote kwa
ajili ya kuthamini haki
na utu wa wenzetu
hawa.
Aidha, tusikubali
kutumiliwa na maadui
Maridhiano na Serikali
ya Umoja wa Kitaifa
(SUK) na kuipa nchi yetu
sifa njema na umaarufu
duniani.
Tusitumikie ajenda
potofu za baadhi ya
wanasiasa na watendaji
waliomo ndani ya
SUK ambao kwa wao
siasa ni biashara - na
ambao wanaamini kuwa
maslahi ya chama ni
makubwa zaidi kuliko
maslahi ya nchi na taifa
na wako tayari kuyabeza
maslahi ya nchi pale
yanapopingana na yake
ya vyama vyao.
Wengi wa wanasiasa
wa aina hii ni wakongwe
walioshindwa kufahamu
maana na umuhimu wa
SUK. Wao wamezoea
siasa za kimapinduzi
na/au ile za mfumo wa
chama kimoja. Mwisho,
t u n a t o a m k o n o wa
pole kwa wananchi
wenzetu wazalendo
waliojeruhiwa, kwa
familia, wafuasi na
wapenzi wao na
tunawaombea wapone
haraka, insha'Allah.
Mungu ibariki
Zanzibar.
Mungu wabariki
Wazanzibari.
Mungu wabariki
Watanzania
Habari za Kimataifa
AN-NUUR
College London.
Utafiti umeonesha
kwamba japokuwa
k i wa n g o c h a wa t o t o
walioambukizwa ni
kidogo kuliko watu
wazima, watoto na watoto
wachanga ambao walipata
ugonjwa huo walikuwa
na nafasi ndogo sana ya
kupona.
Virusi
hivyo
vinavyosababisha homa
kali na kutokwa damu
ndani na nje ya mwili,
vinaua asilimia 90 ya
watoto wachanga katika
mlipuko wa sasa.
Utafiti umebainisha
zaidi kuwa karibu asilimia
80 ya watoto wa umri
kati ya mwaka mmoja
na miaka mine, hufa
kama walivyogundua
wanasayansi.
Zaidi ya watu 23,000
waliambukizwa virusi vya
ebola na zaidi ya 10,000
walifariki dunia.(VOA).
M S E M A J I wa R a i s
Vl a d m i r P u t i n w a
Urusi, Dmitry Peskov,
amesema kuwa hakuna
kizuizi chochote cha
kisheria kitakachoizuia
serikali ya Urusi
kupeleka silaha na zana
za kijeshi nchini Syria.
Bw. Peskov, amesisitiza
kuwa hakuna kizuizi
chochote kitakachoweza
k u z u i a k u we p o p i a
mashirikiano ya kijeshi
na kiufundi kati ya
serikali za Moscow na
Damascus.
H a y o ya n a e l e z wa
katika hali ambapo
nchi za Marekani na
utawala wa Kizayuni
wa Israel, zimeingiwa
na hofu kutokana na
kuwepo uwezekano
mkubwa wa serikali ya
Urusi kupeleka nchini
Syria mfumo wa kuzuia
makombora S-300.
Msemaji huyo wa Rais
wa Urusi alisisitiza kuwa,
Moscow haijakiuka
sheria za kimataifa kwa
kuipelekea serikali ya
Syria silaha za kujihami
na kujilinda.
Hivi karibuni Rais
Bashar Assad wa Syria,
alivieleza vyombo vya
habari kwamba kuna
makubaliano mapya
ya silaha na zana za
kijeshi yaliyofikiwa kati
ya serikali yake na Urusi
na kusisitiza kwamba,
makubaliano hayo
yako katika hatua ya
utekelezaji. (irib).
na mazoezi ya kijeshi
yanayoendelea kufanywa
na majeshi ya shirika
la NATO huko Ulaya
Mashariki.
Inaonekana kuwa kwa
majaribio ya kombora hilo
la nyuklia, jeshi la Anga
la Marekani linafuatilia
malengo kadhaa.
Wachambuzi wanaeleza
kuwa Marekani inataka
kuonesha misuli na uwezo
wake wa silaha za nyuklia
k wa wa p i n z a n i wa k e
wakubwa hususan Urusi.
Katika kipindi cha miaka
kama miwili iliyopita
jeshi la Urusi lilifanya
majaribio ya makombora
yanayoweza kuvuka
mabara (Intercontinental
Ballistic Missile au IBM) na
hata kurusha makombora
kama hayo kwa kutumia
nyambizi. Kwa msingi
huo Marekani ilikuwa
i k i n ye m e l e a f u r s a ya
kukabiliana na majaribio
hayo ya silaha za nyuklia
ya Urusi.
Imefahamishwa
kwamba kichocheo cha
pili cha majaribia hayo ni
kukithiri mivutano baina
ya Urusi na NATO huko
Ulaya Mashariki, ambako
kumezifanya pande hizo
mbili kujizatiti kwenye
m e d a n i ya s i l a h a n a
majeshi katika eneo hilo
na katika Bahari Nyeusi.
Hivyo inaonekana
kuwa Marekani inataka
kumuonesha adui yake
mkubwa kijeshi, yaani
Urusi, kwamba iwapo
mgogoro huo utaendelea
inaweza kutumia silaha
zake za nyuklia.
Marekani ni miongoni
mwa wamiliki wakubwa
zaidi wa silaha za nyuklia
duniani na ndiyo nchi
pekee ambayo hadi sasa
imetumia silaha hizo kuua
watu wa taifa jingine.
Nchi hiyo kinyume na
ahadi zake za kupunguza
maghala yake ya silaha za
nyuklia, bado inaonekana
kustawisha na kupanua
zaidi silaha hizo na
kuzifanyia majaribio.
Pia
inadaiwa
kuziboresha zaidi
silaha zake za zamani
za nyuklia licha ya
harakati za kimataifa za
kupunguza silaha hizo,
husuan mkataba wa NPT
unaosisitiza kupunguzwa
na hatimaye kuangamizwa
kabisa silaha hizo.
Washington imetenga
bajeti ya dola bilioni
355 ambazo zitatumika
kuboresha mitambo yake
ya silaha na kuinua juu
kiwango cha majaribio ya
silaha za nyuklia.
Aidha Marekani
imechukua hatua za
kuboresha silaha na
maghala yake ya zana
za nyuklia barani Ulaya,
yakiwemo mabomu ya
nyuklia ya B-61.
K wa u t a r a t i b u h u o
Washington, kinyume na
mikataba ya kimataifa
ya k u z u i a u z a l i s h a j i
wa silaha za nyuklia,
inaendelea kuzalisha na
kufanyia majaribio silaha
za aina hiyo, suala ambalo
linakiuka mkataba wa
NPT na wakati huo huo
kutolalamikiwa na yeyote.
Wa k a t i M a r e k a n i
ikionyesha uwezo wake
wa silaha za nyuklia,
Tauifa hilo limekuwa
kinara wa kushinikiza
mataifa mengine, hasa
ya Mashariki ya Kati
kuachana kabisa na
mpango huo.
Wiki iliyopita
mazungumzo ya Iran
na kundi la 5+1 kuhusu
miradi ya nyuklia yenye
malengo ya amani ya
Iran, yalisimama mjini
Lausanne, Uswisi
kufuatia tofauti na hitilafu
zilizopo kati ya pande za
mazungumzo hayo.
Mazungumzo hayo
yamesimama baada ya
wawakilishi wa kundi la
5+1 kushindwa kuchukua
maamuzi magumu juu
ya kuondolewa vikwazo
dhidi ya Tehran. Licha ya
Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran kutekeleza masharti ya
makubaliano yaliyofikiwa
mjini Geneva miaka miwili
iliyopita, bado upande
wa p i l i u m e s h i n d wa
kutekeleza ahadi zake,
suala ambalo limeendelea
kuleta mvutano katika
mazungumzo hayo.
Kwa mufa mrefu Iran,
nchi ambayo imeonekana
kupiga hatua za haraka za
maendeleo ya teknolojia
n a k i j e s h i , i m e k u wa
ikiwekewa vikwazo
vya kiuchumi kufuatia
mpango wake kuzalisha
nishati ya nyklia na ajili
ya matumizi salama na
maendeleo ya Iran.
Makala
AN-NUUR
Na Mohammed Ghassany
MIONGONI mwa majeruhi wa mkasa wa kushambuliwa na watu wasiojuilikana wakati wakirudi mkutano
wa CUF, Makunduchi, tarehe 29 Machi 2015.
anarudi kugombea
uwakilishi kwa tiketi
ya CUF katika jimbo la
Kiembesamaki. Mansoor
alikuwa mwakilishi wa
jimbo hilo hapo kabla
kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), kabla
ya kufukuzwa kutokana na
msimamo wake kuelekea
Muungano wa Tanzania
na nafasi ya Zanzibar
kwenye Muungano huo.
Kwenye mkutano huo
kulizungumziwa kuwepo
kwa njama za kuiingiza
Zanzibar katika machafuko
kabla ya kura ya maoni ya
Aprili 30 mwaka huu na
kuelekea uchaguzi mkuu
wa Oktoba 25. Wito wa
wazungumzaji wa CUF
kwenye mkutano huo
ilikuwa kutochokozeka
na kutoondoshwa
kwenye mstari.
Mkutano huo nao
ulitanguliwa na mkutano
wa wazee wa CUF kwenye
ukumbi wa Salama, Hoteli
ya Bwawani Zanzibar,
ambako pamoja na mengine
mengi, Maalim Seif naye
alizungumzia mipango
hiyo ya fujo zinazopangwa
na zilizokwishafanywa
huko nyuma. Na yeye
akasogea mbele zaidi
kwa kurejelea tamko la
kutofukua makaburi lau
chama chake kitachukuwa
madaraka kamili baada
ya uchaguzi wa Oktoba.
Kwa hakika, aliwakemea
wote waliomo kwenye
chama chake, ambao
7
Na Omar Msangi
The Boogeyman ni filamu
ya kutisha ya Kimarekani
(American supernatural
slasher horror film)
iliyotolewa mwaka 1980.
Ikiongozwa na Ulli Lommel.
Wachezaji wakuu (stars)
walikuwa Suzanna Love,
John Carradine na Ron
James.
Filamu iliwahusu watoto
wawili, Willy na Lacey
a m b a o wa k i s h i r i k i a n a ,
walimuuwa rafiki wa kiume
wa mama yao. Willy alinyata
na kuingia chumbani kwa
mama yake ambapo alikuwa
akifanya mapenzi na rafikiye
haramu (kwa maana sio
mume wake wala baba wa
watoto wake). Kwa kutumia
kisu akamuuwa rafiki huyo
wa mama yake. Wakati hayo
yakifanyika, Lacey alikuwa
akitizama kupitia kiyoo.
Miaka 20 baadae, mpenzi
huyo wa mama yao anakuja
kulipiza kisasi katika namna
ya jinamizi, lililowahangaisha
sana watoto hao Lacey na
Willy, wakati huo wakiwa
wa t u wa z i m a . I l i k u wa
kila siku Lacey na Willy,
wanaweweseka kwa kujiwa
na mtu kama yule mpenzi
wa mama yao akiwa
na kisu mkononi akitaka
kuwashambulia. Majinamizi
kama haya (Bogeyman au
monsters), inakuwa tabu
sana kupambana nayo na
kuyashinda kwa sababu moja
tu muhimu: Sio viumbe halisi.
Inayodaiwa kuwa vita
dhidi ya ugaidi, imejaa
ma-bogey men, wengi iwe
kwa jina la Boko Haram,
Al-Shabaab, IS, Alqaidah,
Abubakar Shekau, Abu
Baghdad n.k. na kwa maana
hiyo, si vita inayotarajiwa
kumalizika kwa kutumia
polisi, makachero au
jeshi. Itamalizika tu kwa
wanaounda majinamizi haya
kuacha mchezo wao. Watu
hao kila kukicha, wanabuni
mbinu mpya ama za kubuni
majinamizi mapya au kuyapa
uhai na kuyadumisha
yaliyopo.
Oktoba 2008 ilichapishwa
habari moja katika vyombo
vya habari iliyopewa kichwa
cha habari: Beware the
Bogey Man: A new low, even
for McCain and his ignorant
supporters!
Chini ya kichwa hicho
likaelezwa tukio moja katika
mkutano wa hadhara wa
kampeni kule Minneapolis,
ambapo John McCain
alikuwa katika kampeni za
kuwania Urais wa Marekani.
Ilikuwa ni katika mkutano
h u o m wa n a m k e m m o j a
alieleza wasiwasi wake juu ya
Barack Obama akisema kuwa
hamwamini kwa sababu
amewahi kusoma mahali
kuwa Obama ni Mwarabu.
"I don't trust Obama. I have
read about him. He's an Arab."
Alisema mwanamke huyo
katika jitihada za kuonyesha
kuwa huenda John McCain
akawa Rais bora kuliko
Obama.
Katika kujibu swali la
mama huyo, John McCain
a l i p i g i l i a m s u m a r i wa
ubaguzi na kitisho cha
Muarabu na Muislamu.
Alisema:
No, maam. Hes a decent,
family man, [a] citizen that I just
happen to have disagreements
with on fundamental issues and
Makala
AN-NUUR
Lipo Jinamizi
Khadija Abubakar Abdulkadir, Maryam Said Aboud na Ummul Khayr Sadir Abdulla.
that's what this campaign is all
about."
Katika namna nyingine ni
sawa na kusema: Dont worry,
maam, Barack Obama is NOT
an Arab. Unlike Arabs, hes a
decent, family man.
Ukitizama namna zote
mbili, hapa John McCain
anachofanya ni kushindilia
tu msumari wa ubaguzi
na kitisho cha Uarabu
na Uislamu. Anamtoa
hofu muuliza swali kwa
kusema kuwa Obama ni
mtu mstaarabu, sio kama
Waarabu/Waislamu.
Kinachoelezwa na swali
la mama muuliza swali ni
kuwa jamii ya Kimarekani
imejengwa kuogopa kitisho
cha Waarabu na Waislamu,
na pengine John McCain
angeweza kusema lolote
k u s a h i h i s h a k u wa i w e
Muarabu, Mzungu, wote
ni raia wa Marekani bila
kujali asili zao. Au katika
muktadha wa dunia, kuwa
wote ni binadamu, watu
wasipimwe kutokana na
asili yao. Lakini hakufanya
hivyo. Akamwacha mama
huyo na wasilikizaji
wengine katika mkutano
huo wakibaki na ujinga wao
wa kuogopa kitisho bandia
cha Uislamu/Waislamu na
hivyo kuendeleza agenda
ya ubaguzi na vita dhidi ya
ugaidi.
Taarifa kuu na muhimu
kabisa wiki hii katika eneo letu
hili la Afrika Mashariki kwa
wiki hii, pengine zitakuwa ni
zile za kukamatwa wasichana
watatu, wakidaiwa kutaka
kuvuka mpaka kwenda
Somalia kujiunga na AlShabaab. Vyombo vya habari
vikasherehesha vikidai kuwa
wa s i c h a n a h a o K h a d i j a
Abubakar Abdulkadir,
Maryam Said Aboud na
Ummul Khayr Sadir Abdulla
waliokamatwa katika mji wa
El Wak ilikuwa wakaolewe na
Mujahidina wa Al-Shabaab
na IS. Kati ya wasichana hao,
mmoja ni kutoka Zanzibar
akitajwa kwa jina la Ummul
Khair Sadri Abdallah.
Taarifa zaidi zikafahamisha
kuwa wasichana hao
walijikuta katika mtego
wa k we n d a S o m a l i a - A l
Shabaab na kisha IS, kupitia
mawasiliano waliyokuwa
wakifanya na mwanamke
mmoja wa Syria, aliye katika
IS.
Katika jambo hili, upo
uwezekano wa namna mbili.
Moja ni kuwa inawezekana
kweli wasichana hao
walishawishiwa wakafikia
k i wa n g o c h a k u k u b a l i
kwenda kujiunga na AlShabaab. Nasema hivyo kwa
sababu ipo mifano mingi ya
watoto wa Kiislamu kuacha
shule na hata walio Vyuo
Vikuu baada ya kughilibiwa
kuwa kusoma ni kupoteza
muda, bali kinachotakiwa
ni kwenda Jihad. Lakini
hata kama itakuwa hivyo,
bado waliofanya kazi hiyo
watabaki kuwa mawakala wa
mabeberu walioandaliwa na
mabeberu kuwafanyia kazi.
Uwezekano wa pili ni
kuwa wasichana hao wapo
katika mtego alionasa Sami
Osmakac. Wakati mwingine
mawakala wanaofanya kazi
hii, ikionekana kasi yao
ndogo, makachero huingia
moja kwa moja na kuwatia
walengwa katika uhalifu
kisha kuwakamata na
kuwasukumizia tuhuma za
ugaidi. Ndiyo yaliyomkuta
Sami Osmakac ambaye hivi
sasa anatumikia kifungo cha
miaka 40 kule Marekani.
Hivi sasa kuna mikakati
ya kuhakikisha kuwa haya
mazimwi (bogey men)
yanahuishwa na namna ya
kuhuishwa ni kama hivi
kupatikana kwa watu
kama hao wakidaiwa
kwenda kujiunga na AlShabaab au IS. Namna
nyingine ni kupatikana kwa
mashambulizi ya kupanga
au kutolewa mara kwa mara
kwa tahadhari za vitisho
kama zile za wiki mbili
zilizopita kwamba magaidi
wa IS watapiga Mwanza,
Dar es Salaam, Nairobi na
Kampala.
Katika matoleo yetu
ya hivi karibuni, tuliwahi
kueleza kukamatwa watu
kule Uturuki ambao hufanya
kazi ya kunasa watu na
kuwapelekwa kwa IS na
kwamba mawakala hao
hufanya kazi kwa kutumwa
na chini ya uangalizi wa
v y o m b o v ya k i k a c h e r o
vya Magharibi na hupewa
fedha nyingi kwa kila mtu
wanayemnasa. Lengo ni
kuzidi kukoleza kitisho cha
bogey man IS.
Katika kadhia ya Sami
Osmakac, makachero wa
FBI waliunda mtego ambapo
walimnasisha kijana huyo
asiye na hatia, na kisha
kumtangazia ugaidi ambao
lau wasingekuwa wao FBI,
kijana huyo asingefanya yote
hayo aliyokuja kusingiziwa
kufanya.
Inawezekana pia kwa hawa
wasichana wakapatikana
makachero mawakala wa
mabeberu wakawachezea
akili zao na kuwanasisha
kama alivyonasa Sami
Osmakac kisha wakaibuka
na taarifa kuwa wanakwenda
Somalia kuolewa na AlShabaab.
Joseph Kibwetere
wa Uganda, aliweza
kuwaaminisha watu wake
kuwa wakijitia katika tanuri
la moto Kwa jina la Yesu,
wanaibukia upande wa pili
wakiwa Mbinguni (Peponi).
Mamia ya watu wakajitosa
wakafa. Sasa yaweza
v i j a n a wa k a t i wa i m a n i
hizi za Joseph Kibwetere
wakawaona wazazi wao
Wa i s l a m u n i m a k a f i r i
wakahiyari wakaolewe na AlShabaab, bila ya Walii maana
walii (mzazi) ashakuwa
kafiri!
Kwa
vyovyote
itakavyokuwa, kama nchi,
tunatakiwa tulitizame jambo
hili kwamba kwa asili yake,
sio la Waislamu wala AlShabaab. Ni mitengo na
mikakati ya mabeberu katika
kujihakikishia utawala na
udhibiti wa kidunia- US
World Hegemony. Kupitia
vita dhidi ya ugaidi,
kinapatikana kisingizio cha
kuingia popote kwa hoja
ya kuwafuata magaidi au
kusaidia nchi inayolengwa
kupambana na magaidi.
Tukilitizama kwa makengeza
kwamba ni tatizo la Ummul
Khair, tunajizamisha
wenyewe katika tope mithili
ya Boko Haram, ambalo
hatutaweza kutoka hata
tukitamani.
Imani yangu ni kuwa tuna
akili pevu za kuyatizama
mambo ya dunia hii kwa
mtizamo sahihi. Na niseme
hapa kuwa katika hili, akina
Makala
AN-NUUR
a l i ye t e r e m s h i wa h u o
ukumbusho kati yetu
sote? Bali huyu ni mwongo
mwenye kiburi! Kesho
watajua ni nani huyo
mwongo mwenye kiburi.
(Al-Qamar : 23-26)
Kama kweli y eye ni
Makala
AN-NUUR
Inaendelea Uk. 12
10
Makala
AN-NUUR
WA K AT I M a r e k a n i
ilipotangaza kuwa
inawashambulia ISIS,
b a a d h i ya wa s o m a j i
wetu walituandama kwa
maneno makali wakidai
kuwa kile tulichokuwa
tukisema juu ya uhusiano
wa Abu Baghdad (ISIS)
na Marekani, ilikuwa
uwongo mtupu. Msingi
wa shutuma zao ni kuwa
wakati sisi tukijenga
hoja kuwa ISIS ni
mawakala wa mabeberu
wakitumika katika proxy
war ya kuisambaratisha
Syria, Iraq na Mashariki
ya Kati kwa ujumla, wapo
Wa i s l a m u wa l i k u wa
wakiamini kuwa ISIS
walikuwa katika Jihad
ya kusimamisha Dola
ya Kiislamu/Khilafah
(Islamic State). Sasa
i l i p o k u wa M a r e k a n i
inawashambulia ISIS,
wakaja na hoja kuwa
kama IS wangekuwa
mawakala, mamluki na
vibaraka wa Marekani,
basi isingekuwa tena
Marekani iwashambulie
IS. Baadhi ya wasomaji
hao wakaenda mbali kwa
kuja na kashfa na matusi
wakisema kuwa sisi ni
Mashia na kwamba kwa
vile jeshi la Iraq na serikali
ya Iraq inadhibitiwa na
Mashia, basi Marekani
inashirikiana na
i n a wa s a i d i a M a s h i a
kuzuia Dola ya Kiislamu
kusimama Syria na Iraq.
Sisi tulisema kuwa
mashambulizi ya Marekani
hayalengi kuwamaliza
IS, wala Marekani
haiwashambulii IS, bali
inachofanya Marekani ni
kutumia kisingizio cha
kuwashambulia IS kupiga
na kuharibu miundo
mbinu na viwanda vya
Syria, kama mkakati
wa kumdhoofisha na
hatimaye kumngoa
Bashar Assad. Lakini pia
IS kuingia Iraq, ni namna
ya kukuza mgogoro wa
Shia na Sunni (Waislamu)
n a k u a c h a wa u wa n e
wenyewe kwa wenyewe.
IS kuwepo Iraq na tangazo
na Marekani kuwa
inapeleka jeshi kuwapiga,
ni kisingizio tu cha
kurejesha na kubakisha
jeshi la Marekani katika
nchi hiyo ikizingatiwa
kuwa ilishatangaza
kuondoka. Na hadi sasa
wakati Marekani ikidai
kuwa inawapiga IS, bado
likisaidiwa na Marekani
kuzuiya Dola ya Kiislamu,
Iraq na Syria, walibaki na
msimamo wao wakisubiri
Dola ya Kiislamu
kusimama Iraq na Syria
chini ya ISIS.
Katika Yemen, kundi
linalojulikana kwa jina la
Ansar Allah (anr allh
- "Supporters of God"),
m a a r u f u k wa j i n a l a
Houthis (al-thiyyn),
likitokana na jina la
kiongozi wao wa awali
Hussein Badreddin alHouthi,
ambao ni
Mashia wa dhehebu la
Zaidi Shia, wamemtimua
madarakani Rais wa nchi
hiyo Abdrabbuh Mansour
Hadi.
Labda tuulize,
k wa wa l e wa l i o k u wa
wakisema kuwa Marekani
inawasaidia Mashia
kuzuiya kusimama Dola ya
Kiislamu ya Abu Baghdad,
katika mgogoro huu wa
Ye m e n wa p o u p a n d e
gani. Je, wapo upande wa
Saudia Arabia na Israel
wanaowapiga Houthi au
wapo upande wa Houthi.
Na je, wanachotafuta
Israel, Marekani na Saudia
Arabia, ni kuzuia Ushia
kusimama Yemen? Kama
utasema ni kuzuiya Ushia
kuchukua madaraka
Yemen, mbona katika Iraq
ni Mashia na Marekani
wa n a o wa p i g a I S . N a
je, mbona katika Syria
ni Masuni walioungana
na Marekani na Israel
kuwapiga Mashia?
Hivi sasa Saudi Arabia
ikisaidiana na Israel
(Israeli Fighter Jets Join
Saudi Arabia in War on
Yemen), inawashambulia
wapiganaji wa Houthi.
Lakini kwa upande
mwingine pia Marekani
japo haijapeleka jeshi,
lakini imetangaza kuwa
inaisaidia Saudia Arabia na
muungano unaoundwa na
nchi za Kiarabu kuwapiga
Mashia wa Houthi. Jingine
ni kuwa wakati Marekani
i n a e n d e l e a k u wa p i g a
Masuni wanaodaiwa
kuwa ni Al-Qaidah,
haiwapigi Houthi. Lakini la
ziada ambalo limejitokeza
ni kuwa wakati Marekani
inasaidiana na Israel, Saudi
Arabia na muungano wa
nchi za Kiarabu kuwapiga
H o u t h i , k wa m l a n g o
wa n y u m a i n a t a f u t a
kuwasiliana na Houthi
waliomtimua Rais wa
Yemen na kuwahakikishia
Inaendelea Uk. 11
11
AN-NUUR
Makala
na washirika wao,
aliongeza mpiganaji
huyo. Kundi jingine la
Kishia ambalo linajiandaa
kuingia Yemen ni lile la
Badr Organization.
Katika Iraq, wapiganaji
12
MAKALA
SHAIRI LA BABA
Mimi nina sikitiko, limenijaa moyoni,
Nimepata fadhaiko, wa kufariji nani,
Juhudi zangu ni mwiko, wana hawazithamini,
Baba nae ni mzazi sifa anastahiki.
Kila nikijitahidi, sifa sipewi kwa nini,
Mbona hamna miadi,nyinyi ni watoto gani,
Au mwafanya kusudi, mnitoe duniani,
Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.
Zote mwelekeza sifa kwa mama mzazi,
Baba mi mmenibeza, hamjali yangu kazi,
Leo nawabembeleza, au niachie ngazi,
Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.
Mimi kwenu kama baba, nawajibika kwa mengi,
Jukumu langu ni kubwa, na tena ni la msingi,
Si tu kuleta ubwabwa, mkafaidi mitungi,
Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.
Mtume katuhimiza, kuwashukuru wazazi,
Hakuna alo m-beza, na kuweka pingamizi,
Japo mama ni wa kwanza, ila baba ni farazi,
Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.
Shime tuwapeni sifa, mababa zetu jamani,
Wamelijenga taifa, malipo yao kwa nani,
Tusisubiri wakafa, wakaenda kuzimuni,
Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.
Hayo tukiyatimiza, tutapunguza majonzi,
Nyoyo tutazisuuza, na kuondosha simanzi,
Mababa watatutunza, na kuboresha malezi,
Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.
Sasa ninahitimisha, wasia wangu jamani,
Yatosha nilokumbusha, wanangu tekelezeni,
Dharau kutozidisha, wazee tutaabani,
Baba nae ni mzazi, sifa anastahiki.
Zainab Mtima,
Mbweni- Zanzibar.
0717 165 602
AN-NUUR
Inatoka Uk. 9
Wa a r a b u wa l i u n d a
utamaduni wenye undani wa
elimu na kuonyesha njia ya
kuvumiliana, unaojumuisha
watu wa mataifa mbalimbali,
imani na lugha -hivyo kutoa
msukumo wa maendeleo
ya kila kitu kutoka hisabati
na unajimu, sayansi ya tiba,
ushairi na mawazo ya hali
ya baadaye ya ustaarabu
duniani, elimu, sheria na
haki, ubunifu majengo
unaostahimili nguvu
ya uvutano, hadi kufikia
maktaba ya kisayansi na
mengi zaidi.
Dunia ya Kiarabu na
Kiislamu ilishindwa kutoa
kiongozi yeyote mwenye
upeo na uadilifu kifikra
ili kuendana na hali
inayobadilika duniani
na masuala magumu ya
kimataifa karne ya 21.
Wakati Waarabu wakiwa
wanaongoza katika Imani
('Emaan') na maadili ya
kibinadamu, waliinua
utamaduni wa aina yake
unaokubali tofauti za
kiimani na tamaduni tofauti
za kijamii na kujenga kupitia
msingi wa umoja wa imani ya
Kiislamu kustawisha kuishi
kwa amani na maendeleo ya
binadamu. Ukiorodhesha
uvumbuzi na michango
ya wasomi wa Kiislamu,
hayahesabiki. Je, unajua
wanasayansi wengine au
wanazuoni ambao michango
yao ilitumika katika vitabu
vya kufundishia kwa
karne sita katika vyuo vya
tiba barani Ulaya? Fikiria
Muhammad Hussein bin
Ali Sina na Kanuni za
Msingi za Tiba. Wazungu
walibadili jina lake kuwa
Avicenna hivyo hakuna mtu
angejua kwamba alikuwa
mwanazuoni wa Kiislamu.
Inasemekana Ibn Sina pekee
aligundua na kuwezesha
kuthibitishwa dawa za aina
36 zinazoendelea kutumika
hadi sasa. (Angalia tungo ya
Marai Rosa Menocal - Enzi
Kuu ya Kuvumiliana: Pambo
la Dunia: Jinsi Waislamu,
Wa ya h u d i n a Wa k r i s t o
Walivyounda Utamaduni
wa Kuvumiliana katika
Hispania ya Kimwinyi,
iliyochapishwa 2003).
Anaeleza kuwa "mafunzo ya
historia, kama mafunzo ya
dini, mara nyingi hupuuza
mifano ya kuvumiliana.
USAJILI
S.2401
KWA WASICHANA TU
MASOMO
USAJILI
S.4384
KWA WAVULANA TU
13
Na Khamis Haji (OMKR)
K AT I B U M k u u wa
C UF, Mhe. Maalim
Seif Sharif Hamad,
amehudhuria mazishi
ya Hemed Salum Hemed
(38) aliyefariki katika
ajali ya barabarani
iliyotokea wakati
akirudi katika mkutano
wa hadhara wa chama
hicho uliofanyika
Makunduchi Wilaya ya
Kusini Unguja.
Marehemu ambaye
ni mkaazi wa Kinuni,
Wilaya ya Magharibi
Unguja aliswaliwa
katika Msikiti Ngamia,
Kilimahewa na kuzikwa
Kianga, mkoa wa Mjini
Magharibi Unguja.
Aidha, Maalim Seif
aliwatembelea na
kuwawafariji baadhi ya
wafuasi wa chama hicho
waliojeruhiwa na watu
wasiojulikana wakati
walipokuwa wakirudi
katika mkutano huo
walipofika eneo la Fuoni.
Tukio la kujeruhiwa
wafuasi 24 wa chama
cha CUF waliokuwa
wakitokea katika
mkutano wa hadhara
huko Makunduchi,
ambao wengi wao
walikuwa ni vijana,
lilitokea hivi karibuni
kufuatia vijana
waliokuwa katika gari
eneo la Fuoni Taveta
wakiwa na mapanga,
nondo na mawe
kuwarushia mawe
Kwa mujibu wa Naibu
Mkurugenzi wa Haki
za Binadamu wa CUF
Bi. Pavu Juma, alisema
baadhi ya majeruhi
hao walipata majeraha
makubwa na wamelazwa
k a t i k a h o s p i t a l i ya
Mnazimmoja na wengine
wamesafirishwa hadi
D a r e s S a l a a m k wa
matibabu zaidi.
M a p e m a
akiwatembelea baadhi
ya majeruhi huko
Mwembemakumbi,
Katibu Mkuu huyo
wa CUF, Mhe.
Maalim Seif Sharif
Hamad, alisema watu
waliowajeruhi wafuasi
wa CUF wamefanya
hivyo baada ya chama
chao kukosa sera za
kuwaeleza Wananchi
n a s a s a wa m e a m u a
kufanya hujuma
ambazo amesema
hazitowasaidia.
HABARI
AN-NUUR
KATIBU Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (wa tatu kutoka kulia),
akihudhuria mazishi ya Hemed Salum Hemed (38) aliyefariki katika ajali ya
barabarani iliyotokea wakati akirudi katika mkutano wa hadhara wa chama hicho
uliofanyika Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja hivi karibuni.
rasilimali zilizopo.
Zanzibar inazo
rasilimali na fursa
nyingi za kiuchumi
lakini bado hazijatumika
ipasavyo kuwanufaisha
wananchi wa kipato
cha chini, endapo CUF
kitashika hatamu za
dola, kitaziibua fursa
h i z o n a k u wa f a n ya
vijana wengi kuweza
kupata ajira katika sekta
mbalimbali zikiwemo
kilimo, uvuvi, biashara,
utalii na viwanda vidogo
vidogo. Alifafanua
Katibu Mkuu huyo.
Kuhusu katiba
inayopendekezwa,
Maalim Seif ambaye pia
ni Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar
alisema Serikali bado
haijawahi kukaa na
kutoa msimamo juu
ya k a t i b a h i y o , n a
kufafanua kuwa hakuna
msimamo wa serikali
juu ya jambo hilo.
Alisema mawazo
yanayoendelea
kutolewa kuhusiana na
katiba hiyo, yanabakia
kuwa misimamo ya
vyama na siyo msimamo
wa serikali kama
inavyodaiwa na baadhi
ya viongozi wa kisiasa.
Mimi nikiwa
Makamu wa Kwanza
wa Rais, kama Serikali
hatujawahi kukaa
kwenye Baraza la
Mapinduzi wala kikao
chochote cha kiserikali
kujadili au kutoa
msimamo kuhusu katiba
inayopendekezwa, sasa
i n a k u wa j e we n g i n e
wanasema msimamo wa
serikali ni huu, alihoji
Maalim Seif.
Kwa upande wake
Naibu Katibu Mkuu
wa CUF Zanzibar,
Nassor Ahmed Mazrui,
alisema mwaka 2015
ni mwaka wa wana
CUF kufanya maamuzi
ya kukiweka chama
hicho madarakani kwa
kukiwezesha kupata
ushindi mkubwa katika
uchaguzi mkuu ujao.
Katika mkutano
huo, wazee wa
CUF Makunduchi
walimkabidhi Maalim
Seif, ufunguo maalum
kwa ajili ya kuifungua
Zanzibar ambayo
wamedai kuwa
imekwama kwa zaidi
ya nusu karne sasa.
Kabla ya kuhutubia
mkutano huo, Katibu
Mkuu huyo alifanya
ziara ya kutembelea
barza na matawi ya
CUF na kupata fursa
ya kuzindua na kuweka
mawe ya msingi katika
matawi na barza hizo,
zikiwemo mbili za
akinamama.
Katika ziara hiyo,
Maalim Seif ambaye
aliambana na Naibu
Katibu Mkuu wa CUF
Zanzibar, aliwahimiza
wanachama wa barza
hizo kuanzisha matawi
kamili kutoka na idadi
kubwa ya wanachama
waliyonayo.
Miongoni mwa
barza na matawi
ya l i y o z i n d u l i wa n a
kuwekewa mawe ya
msingi ni pamoja na
Barza ya Kizimkazi
D i m b a n i , B a r z a ya
Ukawa ya Nganani,
Barza ya Ismail Jussa ya
Kitundani, Fatma Ferej
Madete Barza na Tawi
la CUF Shakani.
Wanachama wapya
waliojiunga na CUF
kutoka CCM ni pamoja
na aliyekuwa mjumbe
wa Baraza la Wazazi
Wilaya ya Kusini Bw.
Yahya Mkongoa Ali na
aliyekuwa mhamasishaji
wa CCM katika eneo
hilo Bi. Kihamba Ali
Ronge.
14
Makala
AN-NUUR
Na Ben Rijal
Na Ben Rijal
MAKALA hii itamuangalia
Mwanasayansi, mjuzi wa
elimu ya nyota na hesabati
Al-Sabi Thabit ibn Qurra
al-Harrani alioishi kutika
mwaka wa 826 hadi 901.
Thabit ibn Qurra alikuwa
akifahamu lugha ya
Kiyunani vilivyo na ufahamu
wake huo ulimuwezesha
kuzitafsiri kazi mbalimbali
zilizoandikwa na Wayunani.
Thabit ibn Qurra alikuwa
ni mjuzi wa hesabati na elimu
ya nyota. Aidha akiheshimika
na uelewa wa taaluma ya
utibabu. Thabit ibn Qurra
alizaliwa katika mji wa
Harran uliokuwa ukijulikana
kwa jina la Carrhae katika
nchi ya Uturuki, anatokana
na kizazi cha waliokuwa
wakiabudu nyota katika dini
ya Sabian.
Kutokana na uelewa wake
wa lugha ya Kiarabu na
Kiyunani, Thabit Ibn Qurra
aliheshimika pakubwa
h a s a k a t i k a u wa n j a wa
wana taaluma. Alikuwa
Muhammad ibn Musa ibn
Shakir baada ya kutambua
kipawa alichokuwa nacho
Thabit Ibn Qurra alimtaka
ahamie mji wa Baghdad nchini
Iraq kwani hapo kulikuwa
ndio kiringe kikuu cha wana
taaluma wa zama hizo.
Inafahamika kuwa msomi
huyu alijishughulisha katika
maisha yake yote kujifunza
hesabati, kutizamia, elimu
ya nyota, uchawi, somo la
makenika, utibabu na falsafa.
Thabit aliishi katika uongozi
wa A b a s s i a n a a l i k u wa
mwenzani mkuu wa kiongozi
al-Mutadid alioishi kutoka
mwaka wa 899-902.
Ramani iliopo hapo
j u u i n a o n ye s h a v i g o g o
vya Kiislamu waliofanya
kazi kubwa katika midani
ya hesabati inakadiriwa
kufikisha miaka 600 tangu
ilivyochorwa.
Katika kazi za kisomi
ambazo
zilikuwa
hazifahamiki nje ya Uyunani,
ziliweza kujulikana kutokana
na Thabit Ibn Qurra, kwani
uwezo wake wa kuelewa
lugha ya Kiyunani na
Kiarabu ulikuwa mkubwa,
aliyafanyia tafsiri maandiko
ya Hellenistic na Kiyunani
na kuyaandika kwa lugha
ya Kiarabu. Utastaajabu kwa
wakati huo mtu kama yeye
kuwa na nyezo haba akiweza
kuandika miswada na tafsiri
mbalimbali za kitaaluma,
wengine walimvulia kofia
kutokana na kuweza kutafsiri
maandiko ya kale na kuyapa
ufafanuzi.
Suala la kuwa na siku
sawa katika mwaka yaani
kwenye mwaka miongo
huwa haipishani kinyume
na maeneo mengine ambayo
miongo hupishana, kiangazi
huwa mchana mrefu na usiku
mfupi wakati wa Kipupwe
huwa mchana mfupi na usiku
mrefu, Thabit Ibn Qurra
alizama kutaka kujuwa
kile kinachofanyika katika
mzunguko wa dunia kuwa
katika baadhi ya maeneo
ni kitu gani huwa miongo
haibadiliki (Equinox). Kazi
yake hio kubwa ilikuja
kuheshimika kwani katika
nyakati hizo wasomi
walikuwa wakibishana na
kuhangaika na kila mmoja
wao kuja na dhana yake,
lakini Tahbit Ibn Qurra
maandiko yake yalikuja
kukubalika katika uga wa
kitaaluma.
Thabit Ibn Qurra alifanya
utafiti wa kujua katika mwaka
kwa kufwata kalenda ya jua
mwaka unakuwaje uwe na
siku 365, kwani kuna miezi
huwa na siku 30 na miezi
kuwa na siku 31, kinyume
na mwaka unaofwata
mwezi ikiwa miezi kuwa na
Inaendelea Uk. 18
15
Makala
AN-NUUR
k i l i c h o k u b a l i wa k a t i k a
itifaki ya Kyoto na vikao
mbalimbali vilivyofanyika
kutokea CopenheganDenmark, Cancun-Mexico,
Durban-Afrikak ya Kusini,
Doha-Qatar, Warsaw-Poland
na Lima-Peru na k ik ao
kijacho kitakuweko Paris
Ufaransa kuangalia namna
walimwengu watafikia vipi
upunguzaji wa hewa ukaa
na namna ya kusaidiwa nchi
zinazoendelea kupambana
na athari zitokanazo na
mabadiliko ya tabianchi.
Yanayoendelea juu ya
mpango wa MKUHUMI na
mafanikio yake :
Jee Suala la MKUHUMI
ina faida kwa Wananchi?
Hadi sasa tunaambiwa kuwa
unapopandisha miti ya misitu
unapunguza gesi ya hewa
ukaa kwahio kuna kipimo
maalumu kimeandaliwa
amabacho kitakuwezesha
kuuza gesi ukaa (Carbon
credit), mafanikio katika
uzaji wa gesi ukaa ni pale
wananchi watapokuja na
kupanda misitu ya kuwa ya
jamii, kwahio uuzaji wa gesi
ukaa utakuwa mkubwa.
Uislamu na upandaji wa miti
Imepokewa na Sahaba
Anas r.a anaeleza kuwa
Mtume SAW anasema Ikiwa
Qiyama kimewadia na moja
wenu amekuwa na mche
wa mtende basi ahakikishe
anatumia wakati huo uliobaki
kwa kupanda mti (Al-Albani)
Imepokewa kutokana na
Sahaba Anas kutoka kwa
Mtume SAW hadithi isemayo
Ikiwa Muislamu amepanda
mti au ameweka mbegu
ardhini baadaye ndege, watu
au wanyama wakafaidika
kutokana na mti ule hio huwa
ni sadaka (Bukhari)
Hadithi mbili hizi kama
Wa i s l a m u w a n g e k u w a
wamezizingatia, basi
MKUHUMI ungekuwa
umepamba moto kwa karne
katika nchi za Kislamu.
Inasikitisha leo kusikia
Muislamu tangu anazaliwa
hadi anafika kufa kuwa
hajawahi kupanda hata mti
mmoja. Waislamu katika
Misikiti, katika Maskuli
lazima wawe na mipango
maalumu ya upandaji wa
miti, ikiwa Misikiti yetu
tunaosali sala za Jamaa kuna
watu 50 tu na kila mtu kwa
mwezi anapanda miti 5
kutakuwa tumepanda miti
250 kwa mwaka miti 3,000
tuchukue kwa idadi hio hio
Misikiti 10 itapatikana miti
30,000 kwa hio waumini
tunaweza kuuza hewa ukaa
kama tutajipanga na kuitikia
wito wa Mtume SAW. Faida
tutapata ya kujipatia fedha za
halali hapa duniani na akhera
tutapata malipo tulioahidiwa.
16
Makala
AN-NUUR
(Kumbukumbu la Torati
16:2).
"Usimchinje Pasaka ndani
ya malango yako yote akupayo
BWANA, Mungu wako,
ila mahali atakapochagua
BWANA, Mungu wako,
apakalishe jina lake, ndipo
mtakapomchinja Pasaka
jioni, katika machweo ya jua,
kwa wakati kama uliotoka
Misri". (Kumbukumbu la
Torati 16:5-6).
Kulingana na maandiko
hayo juu, tunaona Biblia
inafundisha wazi kuwa
Pasaka ni kondoo au
ng'ombe ambaye Mungu
aliwaamuru wana wa Israeli
wamchinje kisha wamle.
Aidha, maandiko hayo
yanaonyesha wazi pia kuwa
amri hiyo (ya kuchinja na
kumla Pasaka) haikuwahusu
watu wa mataifa mengine
isipokuwa Waisraeli.
Pa m o j a n a wa n a wa
Israeli kuamriwa na Mungu
kumchinja Pasaka, Mungu
pia aliwawekea utaratibu
(sheria) wa kumla (Pasaka)
kama tunavyosoma katika
maandiko yafuatayo:
"BWANA akamwambia
Musa na Haruni, Amri ya
Pasaka ni hii; mtu mgeni
asimle; lakini mtumishi
wa mtu awaye yote
aliyenunuliwa kwa fedha,
ukiisha kumtahiri, ndipo
hapo atamla Pasaka. Akaaye
kwenu hali ya ugeni, na
m t u m i s h i a l i y e a j i r i wa ,
wasimle Pasaka. Na aliwe
ndani ya nyumba moja;
usiichukue nje ya nyumba
nyama yake yoyote; wala
msivunje mfupa wake uwao
wote. Na wafanye jambo hili
mkutano wa Israeli wote. Na
mgeni atakapoketi pamoja
nawe, na kupenda kumfanyia
BWANA Pasaka, waume
wake wote na watahiriwe,
ndipo hapo akaribie
na kufanya Pasaka, naye
atakuwa mfano mmoja na mtu
aliyezaliwa katika nchi; lakini
mtu yeyote asiyetahiriwa
asimle. Sheria ni hiyo
moja kwa mtu aliyezaliwa
k w e n u , n a k wa m g e n i
akaaye kati yenu ugenini.
Ndivyo walivyofanya wana
wa I s r a e l i w o t e ; k a m a
B WA N A a l i v y o wa a g i z a
Musa na Haruni; ndivyo
walivyofanya". (Kutoka
12:43-50)
"BWANA akanena na
Musa, akamwambia, mtu
wa kwenu, au vizazi vyenu,
yeyote atakayekuwa na
unajisi kwa ajili ya maiti,
au akiwako mbali katika
safari, na haya yote, ataishika
Pasaka kwa BWANA; mwezi
wa pili, siku ya kumi na nne
ya mwezi, wakati wa jioni,
wataishika watamla pamoja
na mikate isiyotiwa chachu na
mboga za uchungu; wasisaze
kitu chake chochote hata
asubuhi, wala wasimvunje
mfupa wake, kama hiyo
sheria yote ya Pasaka ilivyo
ndivyo watakavyoishika.
Lakini mtu aliyesafi, wala
hakuwa katika safari, naye
amekosa kuishika Pasaka,
mtu huyo atakataliwa
mbali na watu wake; kwa
sababu hakumtolea BWANA
matoleo kwa wakati wake
u l i o a m r i wa , m t u h u y o
PAPA Francis.
atachukua dhambi yake. Na
kama mgeni akiketi kati yenu
ugenini, naye ataka kuishika
Pasaka kwa BWANA; kama
hiyo sheria ya Pasaka ilivyo,
na kama amri yake ilivyo,
n d i v y o a t a k a v y o f a n ya ;
mtakuwa na sheria moja,
kwa huyo aliye mgeni, na
kwa huyo aliyezaliwa katika
nchi". (Hisabu 9:9-14).
Kwa kifupi, kama
maandiko hayo yanavyoeleza,
huo ndio ulikuwa utaratibu
wa Pasaka, ambao Mungu
aliwawekea wana wa Israeli.
Aidha tumeona maandiko
hayo nayo pia bado
yanatuonyesha kuwa Pasaka
ni mnyama ambaye Mungu
aliwaamuru wana wa Israeli
(peke yao) wamchinje kisha
wamle.
Pamoja na Mungu
kuwatajia wana wa Israeli
watu wanaoruhusiwa
kumla Pasaka (kama
tulivyoona katika maandiko
yaliyotangulia), tunaona
Mungu pia aliwapangia
siku na muda maalum wa
kuchinja na kumla Pasaka,
kama maandiko yafuatayo
yanavyoeleza:
"Kisha BWANA akanena
na Musa katika bara la
Sinai, mwezi wa kwanza
wa mwaka wa pili baada ya
kutoka kwao katika nchi ya
Misri, akamwambia, Tena
wana wa Israeli na washike
sikukuu ya Pasaka kwa
wakati wake ulioagizwa.
Siku ya kumi na nne kwa
mwezi huu, wakati wa jioni,
mtaishika kwa wakati wake
ulioagizwa; kwa amri zake
zote, na kama hukumu
zake zote zilivyo, ndivyo
mtakavyoishika. Kisha Musa
akawaambia wana wa Israeli
kwamba waishike sikukuu
ya Pasaka. Nao wakaishika
Pasaka katika mwezi wa
kwanza, siku ya kumi na nne
ya mwezi, wakati wa jioni,
katika bara ya Sinai, vile vile
kama haya yote BWANA
aliyomwagiza Musa, ndivyo
wa l i v y o f a n ya wa n a wa
Israeli".
(Hesabu 9:1-5)
U k a w e k wa m s i s i t i z o
"Tena, mwezi wa kwanza, siku
16:1-3).
Kwa maandiko hayo,
tunaona kuwa lengo la
Mungu kuweka sikukuu
hiyo ya Pasaka, ilikuwa ni
kwa ajili ya kukumbuka siku
aliyowakomboa Waisrael
kuwatoa Misri chini ya
utawala ya Farao (Firauni).
Ambapo maandiko ya
Biblia yamearifu kuwa wana
wa Israeli walikaa nchini
Misri katika hali ya utumwa
kwa muda usiopungua miaka
430 (tazama Kutoka 12:40-42).
Aidha, maandiko hayo
yanaonyesha lengo lingine la
Mungu kuwawekea wana wa
Israeli sikukuu hiyo (Pasaka)
ilikuwa kama desturi yake
kujenga uhusiano mzuri
baina yake na wanaadamu
endapo watatii amri zake.
Kama tulivyoona shuhuda
nyingi za maandiko ya Biblia,
jambo la kusisitiza hapa ni
kwamba, sikukuu ya Pasaka
iliwekwa na Mungu kwa
ajili ya kumbukumbu ya
kukombolewa wana wa
Israeli kutoka nchi ya Misri.
Dhana ya kufa na kufufuka
k wa Ye s u , ya we z e k a n a
kumenasibishwa tu Pasaka
kupitia mafundisho au
taratibu za kibinadamu
ambazo wamejipanga
wenyewe kwa jinsi
wanavyoona inafaa katika
imani.
Haya ni mambo ambayo
M u i s l a m u a m b a ye k wa
namna moja au nyingine
anashiriki ibada ya pasaka,
anatakiwa kuyafahamu na
kuyafanyia uchunguzi wa
kina kabla ya kujitosa.
Ama kwa Mkristo, ana
hiari ya kutekeleza ibada
hiyo ya Pasaka kwa namna
anavyoona ni sahihi kwa
kuwa huo ni utaratibu wa
kiibada uliopo ndani ya
imani yake.
Tu s e m e t u k w a m b a
umefika wakati wa
wanaadamu kujiepusha
na kuamini bila kuwa na
ujuzi wa kimantiki wa kile
unachokiamini (ububusa),
vinginevyo mtu anaweza
kuingia katika shirki kubwa.
Quran inatuambia, "Nani
dhalimu mkubwa kuliko
yule anaye mzulia uwongo
Mwenyezi Mungu, au anaye
sema: Mimi nimeletewa
wahyi; na hali hakuletewa
wahyi wowote. Na yule anaye
sema: Nitateremsha kama
alivyo teremsha Mwenyezi
Mungu. Na lau ungeli waona
madhaalimu wanavyo
kuwa katika mahangaiko
ya mauti, na Malaika
wamewanyooshea mikono
wakiwambia: Zitoeni roho
zenu! Leo mtalipwa adhabu
ya fedheha kwa sababu ya
mliyokuwa mkiyasema juu
ya Mwenyezi Mungu yasiyo
ya haki, na mlivyo kuwa
mkizifanyia kiburi Ishara
zake." Al -An'am 6.93.
"Hawakumwua wala
hawakumsulubu." (Qur.
4:158).
17
TANGAZO
AN-NUUR
Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:
KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL
SAME KILIMANJARO
NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL
MWANZA
UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOO L
DAR ES SALAAM
Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu.
Shule hizi ni za bweni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana .
Zipo tahasusi za masomo (Subject Combinations) ya SAYANSI, ARTSnaBIASHARA.
Wanafunzi wote wanafundishwa Islamic Knowledge,Introduction to Arabic na matumizi ya compyuta pamoja na kutumia mtandao
(internet) katika kujifunza.
Muombaji anatakiwa awe na sifa za kujiunga na kidato cha tano ziolizotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi amabazo ni :
Ufaulu wa masomo matatu (3) kwa kiwango cha Credit(yaani A,B+,B au C0 katika mtihani wa Kidato cha Nne, ns
Ufaulu usiopungua Daraja la Credit au GPA ya 1.6 katika Mtihani wa Kidato cha Nne, na
Ufaulu usiopungua Gredi D kwenye masomo yote ya tahasusi (combination).
AU
Ufaulu wa masomo matatu (3) ya tahasusi kwa kiwango cha Credit bila kujali daraja alilopata mtahiniwa
kwenye matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne.
Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.
Mwsho wa kurudisha fomu ni tarehe 15 Aprili, 2015.
Arusha
- Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni : 0783552414/0762817640.
18
VIONGOZI wa makabila
katika maeneo tofauti
nchini Yemen wametoa
tangazo rasmi la vita
dhidi ya Saudia kufuatia
mashambulizi yake
yaliyosababisha zaidi ya
watu 100 kuuawa hadi
sasa. Viongozi hao kutoka
madhehebu tofauti ya
K i i s l a m u wa k i we m o
Waislamu wa Suni, alHuthi, Shia Ithnaasharia
na wengine wamewataka
vijana wao kubeba
silaha kukabiliana na
chokochoko za Saudia
dhidi yao.
Viongozi wa makabila
ya Hashid, Bakil, Khulan,
a l - Twa y ya l , A m i r ,
Hamadan, Mudh'hij,
Qahtwan na kwa pamoja
wamelitaka jeshi la Yemen
kushambulia maeneo ya
kijeshi ya Saudia ukiwemo
mji mkuu wa nchi hiyo
Riyadh na ule wa Jeddah
ikiwa ni katika kujibu kile
kilichoitwa kuwa ni jinai
za utawala wa Aal Saud.
Ta a r i f a z i n a e l e z a
kuwa jeshi la Yemen
k wa k u s h i r i k i a n a n a
Wa n a h a r a k a t i wa
Answarullah, tayari
wameweka makombora
yake ya Scud ili kujibu
hujuma hiyo.
Awali baada ya Saudia
kuanza mashambulizi
dhidi ya Yemen, Balozi wa
Saudia nchini Marekani
Adel al Jubeir, alisema
kuwa mashambulizi hayo
yanafanyika ili kuilinda
serikali aliyodai halali ya
Rais aliyejiuzulu, Abdu
Rabu Mansour Hadi huko
Yemen.
Ndege za Kikosi cha
Anga cha Ufalme wa Saudi
Arabia zilishambulia
maeneo ya Ansarullah
k a t i k a m j i m k u u wa
Yemen, San'aa mapema
siku ya Alhamisi.
Televisheni ya al Alam
iliripoti kuwa, ndege moja
ya Saudia ilitunguliwa
na jeshi la anga la Yemen
na ripoti zilionyesha
hasara kwa raia katika
mashambulizi hayo.
Balozi huyo wa
Saudi Arabia nchini
Marekani alidai pia kuwa
mashambulizi hayo
yataendelea na kwamba,
mbali na kupata baraka
kamili za Marekani,
Riyadh inashirikiana na
nchi nyingine 10 katika
operesheni hizo.
Kwa mujibu wa
balozi huyo, alisema
kuwa mashambulizi
ya Saudia dhidi ya
Ye m e n , y a n a f a n y i k a
kwa ushirikiano na nchi
kadhaa za Kiarabu. Kauli
ya balozi huyo imedaiw
akuwa inathibitisha njama
chafu dhidi ya taifa la
Yemen na eneo zima la
Masharikiya Kati kwa
ujumla.
Shirika la Habari
la Saudi Arabia (SPA)
liliripoti kuwa ukitoa
Makala/Habari
AN-NUUR
Na Mwandishi Wetu
KESI ya Waislamu 23
wanao tuhumiwa
kwa ugaidi akiwemo
Sheikh Farid Had na
Sheikh Mselem Ali,
imeahirishwa tena hadi
Apili 13 mwaka huu.
Kesi hiyo inayo sikilizwa
k a t i k a M a h a k a m a ya
Hakimu Mkazi Kisutu
Jijini Dar es Salaam,
iliahirishwa Jumatano
wiki hii, Mahakamani
hapo, kwa maelezo kuwa
kesi hiyo imekatiwa rufaa
Mahakama Kuu.
Waendesha Mashitaka
walisema shauri lipo katika
hatua ya Rufaa kwa hiyo
waliomba siku nyingine,
hivyo imepangwa kurudi
April 13, 2015 kwa ajili
ya kutajwa. Imeelezwa
Mahakamani hapo.
Kutokana na hali hiyo,
Hakimu anaye sikiliza
kesi hiyo Mhe. Janet
Kaluyenda alilazimika
kuahirisha kesi hiyo hadi
Apili 13 mwaka huu.
A wa l i , k e s i h i y o
ambayo iliahirishwa
katika siku zilizopita
kufuatia upande wa
mashitaka ukiongozwa
na Wakili Pita Njike,
ulipoarifu Mahakama
kuwa, kesi hiyo ipo
Mahakama ya Rufaa na
wanasubiri kupangiwa
siku ya kusikilizwa.
N a y e Wa k i l i w a
u p a n d e wa u t e t e z i
Abdulfattah Abdallah,
akizungumza na
Wandishi wa habari
Mahakamani hapo
alisema, leo (Jumatano
wiki hii) Kesi hiyo
ilifikishwa hapo (Kisutu)
kwa ajili ya kutajwa
na washitak iwa wote
walikuwepo Mahakamani
hapo.
Wa k i l i A b d a l a h
alisema, kinachosubiriwa
Mahakama Kuu ni
mwenendo wa kesi na
wapo katika mchakato wa
kuhimiza suala hilo liende
haraka ukizingatia wateja
wao wapo ndani hawako
huru.
19
Makala ya Mtangazaji
AN-NUUR
Over 30 detained
in Jerusalem in
last 3 days
RAMALLAH, (WAFA)
- PLO Executive
Committee Member and
Head of the International
Criminal Court (ICC)
Higher National
Committee Saeb Erekat
said the occasion serves
as a reminder to the
international community
of its responsibilities
under international law,
in order to achieve a just
and lasting peace, and put
an end to the prolonged
Israeli Occupation.
In a press statement
on Palestine's official
accession to the ICC,
Erekat explained that
on the Palestinian level
the membership reflects
Palestine's commitment to
justice, international law,
and human rights.
Our determination
to protect our people
against the injustice of
those responsible for war
crimes is underscored
by our nation's accession
to the Rome Statute and
submission to the ICC's
jurisdiction.
Describing the
membership as historic,
Erekat called upon the
international community
to support the inalienable
rights of Palestinians,
including the right to
self-determination, by
supporting the peaceful
movement to end decades
of impunity, occupation,
and exile.
He renewed the
Palestinian authoritys
calls upon all nations of
conscience to recognize
the State of Palestine on
the 1967 border, with East
Jerusalem as its capital.
In a closed and special
ceremony, the ICC
officially accepted the
membership of the State
of Palestine accession to
the international legal
body making it the 123
of ICC's state parties.
However, Palestinians
might have to wait years
before actually opening a
full investigation against
Israel.
BETHLEHEM, (WAFA)
A number of Palestinian
students Tuesday suffered
suffocation by tear gas as
Israeli soldiers assualted
them while they were
heading to their schools in
the town of Taqou to the East
of Bethlehem, according to
security sources.
Sources told WAFA that
Israeli forces intercepted
students while they were
heading to their schools in
the early morning hours,
firing tear gas canisters and
stun grenades toward them,
causing many to suffer from
tear gas suffocation.
Israeli army previously
carried out numerous
attacks, with the deliberate
and reckless use of force,
against schools and
governmental institution
working for women's and
children's rights stated in a
press release issued in July
2014 that, Children have the
right to life and survival, nondiscrimination, education,
recreation, and safety.
In the meantime, a special
report issued by Al-Mizan
Center for Human Rights
said that Israel deliberately
targeted intellectual property
during its recent onslaught
on Gaza in the summer of
2014. Jean Gough, UNICEFoPt Special Representative
said that, Every child has
the right to learn and grow
in an environment where
their health and safety are
paramount.
RAMALLAH, (WAFA)
The Palestinian cabinet, in
its weekly session Tuesday,
rejected Israels unilateral
decision to transfer the
Palestinian Authoritys tax
revenues after deducting
almost 300 million shekels
($75 million).
The cabinet reiterated
its utmost rejection to
Israels repeated act
of withholding PAs tax
revenues and deducting 300
million shekels, describing
it as a premeditated crime,
a collective punishment
against Palestinians, and
a blatant violation of
previously agreed upon
agreements and international
resolutions.
It urged the international
community to pressure Israel
to release the entire sum, and
to put an end to this illegal
action.
Israels decision to deduct
millions of shekels from
Palestinians came under
AN-NUUR
20
MAKALA
20
Na Mwandishi Wetu
MAKAMU wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar,
Maalim Seif Sharif
Hamad, amemtembelea
kijana Shamsi Ali
Khamis nyumbani kwao
Mwembemakumbi.
Shamis ni mmoja kati
ya watu waliojeruhiwa
wakati msafara wao ukiwa
njiani kutoka mkutano
wa Chama cha Wananchi
(CUF) katika jimbo la
Makunduchi, Unguja
Kusini.
K i j a n a
h u y o
aliyejeruhiwa jicho la kulia,
alitarajiwa kusafirishwa
juzi kuelekea Dar es
Salaam kwa matibabu
zaidi.
Watu
kadhaa
walijeruhiwa baada ya
msafara wa wanachama
wa CUF waliokuwa
wakitoka katika mkutano
kushambuliwa na watu
wasio julikana.
Shambulio hilo linakuja
wakati siku zikiyoyoma
kuelekea uchaguzi mkuu
hali inayoleta wasiwasi
kuwa huenda hali isiwe
MAHAKAMA Kuu ya
Ta n z a n i a , i m e m t a k a
Mwanasheria wa
Serikali kujibu haraka
hoja za Masheikh walio
fungua kesi kupinga
m p a n g o wa S e r i k a l i
kuipa BAKWATA uwezo
kisheria kusimamia
mambo ya Waislamu.
Amri hiyo imekuja baada
ya Mwanasheria huyo
kuiomba Mahakama Jijini
Dar es Salaam, Jumanne
wiki hii wapewe muda
wa siku 14, ili waweze
kujibu hoja za Masheikh
h a o wa l i z o wa s i l i s h a
Mahakamani hapo,
mapema wiki iliyopita.
Upande wa Jamhuri
ukiongozwa na Wakili
Malata, uliomba wapewe
KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) akimjulia hali mmoja
wa majeruhi aliyeshambulia katika mkutano wa Chama hicho Unguja hivi karibuni.
shwari huko mbeleni.
Hii ni hali iliyokuwa
ikijiri huko nyuma kila
unapokaribia uchaguzi
mkuu hadi kupatikana
matokeo na hata
AN-NUUR
Mahakama ilikubalina
nao, lakini iliwaambia
kwa sababu hii Kesi ina
umuhimu mzito ingefaa
wajibu kabla ya siku hizo
14, sasa kwa maelezo
hayo ya Mahakama
wanatakiwa wajibu April
2 ,2015 siku ya Alhamisi
(jana) na sisi tutachukua
hayo majibu yao April
8, hivyo tutaanza kuja
kuanza kusikiliza Kesi
rasmi, utaratibu ni huo.
Alisema Wakili Nasoro.
Sheikh Rajabu Katimba,
n a w e n z a k e wa t a t u ,
mapema wiki iliyopita
walifungua kesi namba 17
ya 2015, katika Mahakama
Kuu ya Tanzania, kupinga
m p a n g o wa S e r i k a l i
kupitia hoja ya kuipa
BAKWATA uwezo rasmi
wa Kisheria kusimamia
mambo ya Waislamu na
kuteua Makadhi nchini.
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.