You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA


Ufafanuzi Kuhusu Kuuzwa kwa Hisa za Kampuni ya
TanzaniteOne.
Gazeti la Raia Mwema la Desemba 10, 2014 liliandika habari
iliyodai kwamba mmoja wa Wafanyabishara maarufu wa mjini
Arusha alishirikiana na mtoto wa kiongozi wa juu wa Serikali na
vigogo wa Wizara ya Nishati na Madini kufanikisha uuzwaji wa
asilimia 50 ya hisa za Kampuni ya Richland Resources katika
Kampuni ya TanzaniteOne inayochimba madini ya Tanzanite
katika eneo la Merelani Wilayani Simanjiro.
Aidha, taarifa hiyo ilidai kuwa licha ya hisa hizo kuuzwa kwa
mamilioni ya Dola, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TanzaniteOne
ametoa taarifa kuwa hisa hizo zimeuzwa kwa kiwango cha Dola
za Kimarekani 5.1milioni (sawa na shilingi bilioni 8.8 za
Kitanzania) ili kukwepa kodi. Vilevile, taarifa hiyo imeeleza kuwa
Wizara ina ukiritimba wa kuwawezesha watanzania kumiliki
rasilimali na kwamba leseni ya TanzaniteOne ilitolewa kimakosa
na hivyo si halali.
Wizara

inapenda

kutoa

maelezo

yafuatayo

kuhusu

hoja

zilizotolewa:
Suala la Uuzaji wa Hisa za TanzaniteOne
Kampuni ya TanzaniteOne imeijulisha Wizara kuhusu kusudio la
kuuza hisa zake asilimia 50 kwa Kampuni ya Sky Associate
Group Limited. Kampuni ya TanzaniteOne haijaomba rasmi

Wizara iridhie uuzaji wa hisa zinazokusudiwa kuuzwa. Mara


Kampuni hiyo itakapowasilisha taarifa kamili za kuuza hisa zake
ikiambatana na maombi ya kupata ridhaa ya kuhamisha umiliki
wa hisa hizo kwa Kampuni ya Sky Associates Group Limited,
Wizara itafanya uchunguzi wa kina na kuona kama utaratibu
umefuatwa wakati wa kuuza hisa hizo.
Uhalali wa Leseni ya TanzaniteOne/STAMICO
Kampuni ya TanzaniteOne imekuwa ikimiliki leseni ya uchimbaji
mkubwa wa madini-Special Mining Licence (SML 8/92) kwa
asilimia 100 katika eneo la Kitalu C Merelani iliyotolewa mwaka
1992. Leseni hiyo ilikuwa inafikia ukomo wake tarehe 9 Julai,
2012. Tarehe 25 Januari, 2011 Kampuni ya TanzaniteOne
iliwasilisha ombi la kuhuisha leseni hiyo kwa lengo la kuendelea
kuchimba madini katika eneo hilo la Kitalu C.
Wizara ilielekeza Kampuni ya TanzaniteOne irekebishe ombi la
tarehe 25 Januari 2011 kwa mujibu wa Kifungu cha 116 cha
Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Kifungu hicho kinaruhusu
kufanyika marekebisho mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha leseni
zilizotolewa chini ya Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 kuhamia
kwenye Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Marekebisho kama
hayo yamefanywa kwa maombi ya leseni za utafutaji mkubwa wa
awali wa madini (PLR) na leseni za uchimbaji madini ya vito
(GML) ambazo hazitolewi tena chini ya Sheria ya Madini ya
Mwaka 2010.
kwa kuwa Kampuni ya TanzaniteOne ilikwishamilikishwa leseni
katika eneo hilo kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka
1998, uhuishaji wa leseni Na. SML/8/92 na marekebisho
yaliyofanyika haukufanywa kwa mujibu wa Kifungu cha 8 cha
Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, bali chini ya kifungu cha 116
kama ilivyoelezwa awali.
Kwa

kuwa

maombi

ya

Kampuni

ya

TanzaniteOne

yalishughulikiwa katika mazingira ya kufanya marekebisho

(modification) ya leseni kutoka Sheria ya Madini ya Mwaka 1998


kwenda katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, leseni mpya
(ML 490/2013 )ilitolewa kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya
Tanzanite, tsavorite, graphite

na madini mengine yanayoweza

kupatikana. Leseni hiyo ina ukubwa wa kilomita za mraba 7.6.


Kihistoria uchimbaji katika kitalu C umekuwa ukihusisha
madini hayo yaliyoainishwa katika leseni hiyo.
Katika miaka ya 1970, TGI walijihusisha zaidi na uchimbaji wa
madini ya vito. Baadaye miaka ya 1990, Kampuni ya Graphtan
Ltd

ilijihusisha zaidi na uchimbaji wa graphite katika eneo la

kitalu C, huku madini ya vito (Tanzanite) yakiwa ni by-product.


Kwa kuzingatia matakwa ya Sera ya Madini ya Mwaka 2009
yanayohusu ushiriki wa Serikali kimkakati katika miradi ya
madini,

Serikali

ilifanya

majadiliano

na

Kampuni

ya

TanzaniteOne yaliyowezesha STAMICO kumiliki asilimia 50 ya


hisa katika mgodi huo wa Tanzanite. Kutokana na makubaliano
hayo Kampuni ya TanzaniteOne ilifanyia marekebisho ombi lake
la leseni ya uchimbaji madini na kuingiza STAMICO ambayo
inamiliki asilimia 50 katika leseni ya uchimbaji madini eneo la
Kitalu C.
Uwezeshaji wa Wazawa katika Sekta ya Madini
Katika taarifa ya gazeti hilo la Raia Mwema ilidaiwa kuwa Wizara
ya Nishati na Madini ina ukiritimba uliokithiri na viongozi wake
hawatoi fursa kiuwezeshaji kwa wazawa katika sekta ya madini.
Madai hayo ni kupotosha ukweli kwamba Wizara imepiga hatua
kubwa katika urasimishaji leseni kwa watanzania na katika
uwezeshaji wa wachimbaji wadogo. Hadi sasa kati ya leseni za
madini zipatazo 45,000, Watanzania wanamiliki asilimia 75 ya
leseni zote, na wageni wanamiliki asilimia 25. Aidha, katika
kipindi cha kuanzia mwaka 2011/12 hadi sasa Wizara imetenga
maeneo 33 kwa ajili ya uchimbaji mdogo; pamoja na kutenga

takriban shilingi bilioni 8 kwa ajili ya uwezeshaji wa wachimbaji


wadogo kupitia Benki ya Maendeleo ya TIB.
Imetolewa na,
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
11 Desemba, 2014

You might also like